Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) yaendesha warsha ya uandishi bora wa tafiti kwa wataalamu wake

$
0
0
_1055413.JPG-3 Research methodology
Aziz Kilonge Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa kufunga warsha ya mafunzo ya uandishi bora wa tafiti ili kukidhi hitaji la msingi la kuhitimu taaluma ya ununuzi na ugavi iliyoratibiwa na kuendeshwa na Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) kuazia tarehe 21 julai mpaka 25 julai 2014. 

kwenye ukumbi wa baraza la maaskofu TEC-Kurasini jijini Dar es salaam akiwa katika [icha ya pamoja na wakufunzi, washiriki pamoja na baadhi ya wakuu wa taasisi hiyo .kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa PSPTB Dr. Clemence Tesha, kutoka kushoto ni Dr. E. Tumsifu-mwezeshaji wa washa na Ally Songoro Mkurugenzi wa Mafunzopamoja na washiriki wa warsha hiyo.
_1055431.JPG-1 research methodology
Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa (PSPTB) Dr. Clemence Tesha, kutoka kushoto ni Dr. E. Tumsifu-mwezeshaji wa washa na Ally Songoro Mkurugenzi wa Mafunzopamoja na washiriki wa warsha hiyo pamoja na wanawarsha.
_1015339.JPG-2-research methodology
Picha ya pamoja ya washiriki na baadhi ya viongozi wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) kwa maelezo zaidi kuhusu taarifa mbalimbali za bodi wataalamu wa Ununuzi na Ugavi kwa kubofywa hapa www. psptb.go.tz

MASHINDANO YA VIJANA YA AIRTEL RISING STAR YAZINDULIWA JIJINI DAR

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Saidi Meck Sadiki akisalimiana na wachezaji wa timu za Ilala wakati akizindua rasmi mashindano ya vijana ya Airtel Rising Star kwa mkoa wa Dar es Salaam jana.
 Mshambuliaji wa timu ya Ilala, Rashid Mohamed (kulia) akimtoka beki wa timu ya Buguruni Youth Center, Khamis Mohamed katika mashindano ya vijana ya Airtel Rising Star kwa mkoa wa Dar es Salaam jana.
 Mshambuliaji wa timu ya Ilala, Edwin Francis (kushoto) akituliza mpira mbele ya  beki wa timu ya Buguruni Youth Center, Salum Abdallah katika mashindano ya vijana ya Airtel Rising Star kwa mkoa wa Dar es Salaam jana.
 Mshambuliaji wa timu ya Ilala, Rajabu Ally (kushoto) akimtoka beki wa timu ya Buguruni Youth Center, Hassan Omari  katika mashindano ya vijana ya Airtel Rising Star kwa mkoa wa Dar es Salaam jana.
 Mshambuliaji wa timu ya Ilala, Francis Edwin (kushoto) akiwania mpira na beki wa timu ya Buguruni Youth Center, Hassan Juma katika mashindano ya vijana ya Airtel Rising Star kwa mkoa wa Dar es Salaam jana.

SHIRIKA LA NYUMBA NHC LAENDELEA KUONGEZA AJIRA KWA VIJANA

$
0
0
1
Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa Bi Rachel Kasanda akikabidhi mashine za kufyatulia matofali kwa Hassan Soud Katibu wa kikundi cha Changamoto kwa niaba ya vikundi vingine vya wilaya ya Ilala ambazo zimetolewa na shirika la Nyumba nchini NHC jana wakati wa mpokezi ya Mwenge wa Uhuru Ilala Boma mara baada ya Meneja wa Shirika hilo wilaya ya Ilala Bw. Jackson Maagi kumkabidhi kiongozi huyo wa mbio za mwenge ikiwa ni juhudi za shirika hilo kusaidia kupunguza uhaba wa ajira kwa vijana ili waweze kujiajiri kwa kuyatua matofali na kuuza.
3
Askari wa Kikosi cha FFU wakiulinda mwenge mara baada ya kuwasili Ilala Boma mahali ambapo ndiyo kituo ulipolala mwenge huo.
4
Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Jackson Maagi wa pili kutoka kushoto akiwa pamoja na wafanyakazi wnzake kabla ya kukabidhi mashinne hizo jana.
2
Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Jackson Maagi akizungumza wakati wa kukabidhi mashine hizo jana.
 
............................................................................................
HOTUBA FUPI YA MENEJA WA NHC ILALA KWA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA

Ndugu kiongozi wa Mbio za mwenge,Ninayo furaha kubwa sana kusimama mbele yenu na kuongea nanyi kama mwakilishi kutoka Shirika la Nyumba la Taifa.
Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge; Shirika la Nyumba la Taifa lina mpango mkakati wake wa miaka mitano ambao moja ya malengo yake sita makuu ni kuboresha taswira ya Shirika. 

 Katika utekelezaji wa lengo hili, Shirika lina sera ya huduma kwa jamii ambayo imejikita katika kusaidia vijana kujiajiri. Ili kuwezesha vijana kujiajiri, Shirika limeamua kuzisaidia Halmashauri za Miji na Wilaya kote nchini mashine za kuwezesha vikundi vya vijana kutengeneza matofali ya kujengea nyumba. Nchi yetu ina Halmashauri 160 na kila Halmashauri itapewa mashine 4 kwa ajili ya kusaidia vikundi vya vijana. Katika mpango huu jumla ya mashine 640 zitatolewa na Shirika na kugharimu shilingi 288,000,000/.

 Aidha, kila Halmashauri itapatiwa shilingi laki tano (500,000/=) kama mtaji kwa vijana kuanzia shughuli yao ya kutengeneza matofali. Kadhalika, Shirika limegharamia shilingi 800,000/= kwa kila Halmashauri kwa ajili ya kuwalipa wakufunzi kutoka VETA wanaotoa maelekezo kwa vijana namna ya kutumia mashine hizo.  

Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge,katika kutekeleza mradi huu jumla ya shilingi milioni mia saba (700,000,000/=) zitatumika. Aidha, tunatarajia kuwa ajira zaidi ya 8,000 za moja kwa moja na ajira nyingine zaidi ya 200,000 zisizo za moja kwa moja zitapatikana. Katika mpango huu kila Wilaya inatakiwa kuwa na vijana 40 watakaokuwa katika vikundi vya watu 10 kila kimoja. Msaada huu ni mkubwa lakini kutokana na ukubwa wa tatizo la ajira jitihada zaidi kutoka kwa wadau mbalimbali zinatakiwa. 

Ni matarajio yetu kuwa taasisi nyingine ama mtu mmoja mmoja atashiriki kukwamua vijana hawa. Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge, kupitia maadhimisho haya, Shirika linatoa mashine nne (4) kwa vikundi 4 vya vijana vilivyoundwa katika wilaya ya Ilala ambapo kila kikundi kina jumla ya vijana10 watakaotumia mashine moja. Hivyo jumla ya vijana 40 katika Wilaya hii watapata ajira kutokana na mashine hizi. Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge, mwisho Shirika linatoa rai kwa Taasisi za serikali, mashirika ya umma, binafsi na watu mbalimbali, kuunga mkono juhudi za Serikali za kupunguza tatizo la ajira kwa vijana. 

Ni matumaini yetu kuwa tutawaunga mkono kwa kununua matofali yao ama kusaidia upatikanaji wa mashine nyingine zaidi ili wengine ambao hawajafikiwa na mradi huu wafikiwe na wapate kufaidika. Kipekee tunaomba Serikali za Mitaa (kwa maana ya Halmashauri zetu za wilaya, miji, manispaa ama jiji) wawe ni wanunuzi wakuu wa matofali yatakayotengenezwa na vikundi hivi vya vijana ambayo ni ya gharama nafuu ili kusaidia miradi mbalimbali ya ujenzi na kuwaongezea kipato chao. Tunawaomba pia msaidie kusimamia mradi huu ili uweze kuwa endelevu.

EID MOSI -GROOVE 360' @ EAST 24/ARCADE!

MAPOKEZI YA DIAMOND BAADA YA KUSHINDA TUZO YA MSANII BORA WA KIUME AFRIKA MASHARIKI

$
0
0




Picha kwa hisani ya Diamond Platinumz blog

Rais Kikwete aandaa futari kwa yatima, walemavu wa ngozi na watoto waishio kwenye mazingira magumu ikulu Dar es salaam

$
0
0
Rais Kikwete akipakua futari  Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni.
Yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakipakua futari waliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakipakua futari waliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakipakua futari waliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakipakua futari waliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa meza kuu  na viongozi wa vituo mbalimbali vya yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakati wa futari  aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakipakua futari waliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Vijana kutoka Chama cha Albino Wilaya ya Kinondoni wakimshukuru Mama Salma Kikwete kwa futari 
Vijana kutoka Chama cha Albino Wilaya ya Kinondoni wakipata picha ya pamoja na Mama Salma Kikwete baada ya  futari waliyoandaliwa na Rais Kikwete.

 

Rais Kikwete akipita meza moja baada ya ingine kuwasalimia yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakati wa futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Rais Kikwete akipita meza moja baada ya ingine kuwasalimia yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakati wa futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Rais Kikwete akipita meza moja baada ya ingine kuwasalimia yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakati wa futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwashukuru kwa kuja viongozi wa vituo mbalimbali vya yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu katika futari  aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Mama Salma Kikwete akitoa neno la shukurani kwa waalikwa kwenye futari hiyo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na mtoto Khaitham Jumbe Jumbe ambaye alimuandalia zawadi
Rais Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakipokea zawadi toka kwa mtoto Khaitham Jumbe Jumbe mwenye umri wa miaka saba na mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi ya Yemen iliyoko Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Rais Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakipokea zawadi toka kwa mtoto Khaitham Jumbe Jumbe mwenye umri wa miaka saba na mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi ya Yemen iliyoko Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Aliyeketi kushoto ni Bi. Mwajuma Hassan wa Chama cha Albino Wilaya ya Kinondoni.

Wageni waalikwa wakifurahia zawadi walizopewa kwenye futari hiyo
Yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakipakua futari waliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakipakua futari waliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakipakua futari waliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakiswali swala ya Magharibi wakati wa  futari waliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni.
PICHA NA IKULU

MBUNGEWA MOSHI VIJIJINI DKT CYRIL CHAMI ASIKITISHWA NA TAARIFA ZA KIZUSHI ZINAZOSAMBAZWA KWA BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI JUU YAKE.

$
0
0
Mimi Dr Cyril August Chami, Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM) napenda kueleza masikitiko yangu kwa taarifa za uzushi na za kutunga kuwa eti mke wangu asiye na jina amemuua mfanyakazi wetu Mwislamu kwa sababu "marehemu" alikataa kwenda kanisani.


Mimi sina mfanyakazi wa jina hilo la Mariamu. Wala sina mfanyakazi mwenye umri wa miaka 16. Hatuna tatizo lolote la mfanyakazi yeyote kupigwa, achilia mbali kuuawa. Lakini taarifa hizo ambazo ni za uongo mtupu zimewashtua wengi kwa sababu zimejengwa katika misingi ya chuki za kidini. Mwandishi alilenga kuifanya jamii iamini kwamba mke wangu ambaye ni Mkristo anawalazimisha wafanyakazi wetu wasio Wakristu waikane dini yao na kuwa Wakristo. Alilenga kuibua chuki dhidi ya Waislamu na familia yangu. 


Kwa hakika, mikakati hii ya kuichafua familia yangu inasababishwa na harakati za ubunge Moshi Vijijini 2015. Wapinzani wangu wanajua wazi kuwa hawana hoja ya msingi ya kuwafanya wapiga kura wasinirudishe kwenye nafasi ya ubunge. Kwenye jukwaa na hata kwenye medani ya maendeleo wanakwama. Kwa mfano, kabla ya barabara za lami kuanza kujengwa walisema mimi sina ushawishi wa kuifanya Serikali kuzijenga. Sasa zimejengwa na zinaendelea kujengwa wanajenga hoja kuwa sihusiki wala Serikali ya CCM haihusiki, bali ni Benki ya Dunia inajenga!!! Wananchi wanawauliza kwani kabla ya Dr Chami kuwa mbunge Benki ya Dunia haikuwepo? Wanakosa hoja! Hivyo hivyo kwa mashule, maji, vyuo vya ufundi nk.


Kwa hiyo kwa upeo wao wanaona silaha pekee waliyo nayo ni kuzua kashfa dhidi yangu. Miezi michache iliyopita walizua nimeuza shamba la KNCU kwa shilingi bilioni 4 wakati mimi sina wadhifa wowote KNCU. Eti nimeuza nyumba mbili za Coffee Curing Moshi wakati mimi sina wadhifa wowote Coffee Curing. Walipoona tuhuma hizo za kutunga hazijakubalika masikioni mwa wapiga kura wa Moshi Vijijini,  sasa wamezua hili la mke wangu kuua ili Waislamu wa Moshi Vijijini wanione mtu nisiyefaa.

Sasa mimi napenda kuwauliza maswali haya:
Huyo mke wangu muuaji anaitwa nani? Inaingia akilini kweli kwamba mke huyo muuaji hafahamiki jina kwa hao "majirani" wetu wa kufikirika? Binti Mariamu kauawa mji upi? Kwa nini majirani hao wenye uchungu hawajatoa taarifa kwa RPC wa mkoa au kanda husika? Maiti kahifadhiwa hospitali ipi? Au "mke" wangu amekaa naye ndani baada ya kumuua na majirani wamekaa kimya tu?

Kwa desturi za dini ya Kiislamu binti huyo angeshazikwa sasa maana kwa mujibu wa habari hiyo ya kizushi, "aliuawa" usiku wa kuamkia jana. Je, kazikwa makaburi yapi na yako mji gani? Nani kahudhuria hayo mazishi? Kwa nini vyombo vya habari visituonyeshe hayo mazishi? Kwa nini RPC mhusika asimkamate huyo mke wa mbunge fedhuli namna hiyo na muuaji asiyevumilika?

Kwa nini polisi hawajaniita mimi Dr Chami kunihoji kuhusu huyo "mke" wangu? Si wanajua niko jimboni Moshi Vijijini na RPC Boaz wa Kilimanjaro anafahamu niko jimboni, tena jana nimeutembelea msikiti mmoja kwa minajili ya kuutafutia umeme na maji? Sote tunafahamu kuwa kuna mkuu mmoja wa mkoa alimuua mtu kwa kumpiga risasi na alikamatwa akapelekwa mahabusu. Huyo mke wa Dr Chami ni maarufu kuliko Mkuu wa Mkoa?  Kwa nini asikamatwe tuione sura yake magazetini?


Majibu ya maswali haya HAYAPO kwa sababu kila kitu kimetungwa kwa kujenga chuki tu. Hakuna Mariamu, hakuna kipigo, hakuna kifo. Ila kuna UBUNGE WA MOSHI VIJIJINI. Ndio unaopiganiwa, hamna kingine.  Napenda kuwaasa wanasiasa wenzangu kuwa Watanzania wa leo si wa jana. Si jambo rahisi kuwaghilibu kwa staili hii. Waende kwa wananchi wachape kazi. Wasipofanya hayo wakadhani uongo wa mitandao utawapa ubunge watashangazwa mwaka kesho 2015.


Mimi naendelea kuwaahidi wapiga kura wangu utumishi wa dhati. Nawapa pole ndugu zangu wa Kiislamu kwa usumbufu walioupata. Waislamu wa Moshi Vijijini wananifahamu kama kiongozi nisiyewabagua kwa sababu ya dini yao. Wanafahamu kuwa nawapenda na nafahamu kuwa wananipenda sana. Ndiyo maana wengi wamejiuliza iweje tena mke wangu amwage damu ya Mwislamu kwa sababu iliyotajwa. Naendelea kuwaahidi Waislamu wote upendo na ushirikiano siku zangu zote za kuwatumikia.

Wasalaam
Dr Chami.

AJALI HAINA KINGA,MADEREVA TUWE MAKINI BARABARANI,HII IMETOKEA JIJINI MBEYA LEO.

$
0
0
Wasamalia wema wakijaribu kulinasua gari aina ya Toyota Corolla (namba zake za usajili hazikuweza fahamamika mara moja kutokana na kutokuwepo) lililoingia kwenye mtaro baada ya dereva wake kuzidiwa maarifa ya kiudereza na kujikuta akiingia mtaroni,katika eneo la Mafiat mkabala na kituo cha mafuta cha Oilcom jijini Mbeya asubuhi hii.Dereva wa Gari hilo pamoja na mtu mwingine mmoja wamejeruhiwa na kukimbizwa hospital kwa matibabu.Chanzo cha ajali hiyo inaelezwa ni mwendo kasi aliokuwa nao Dereva wa gari hilo.
Wasamalia wema hao wakiangalia namna ya kuweza kulichomoa gari hilo.
Hayaaaa..... Moja.... mbili.... tatuuu twendeeeeeeee......
Mara wakafanikiwa kulitoma kwenye mtaro huo.Picha na Fadhil Atick,Mbeya

Mdau Alamba Nondoooz

$
0
0
 Mdau Bryan Becon akiwa na mdogo wake Rodney Becon na mama yake Mrs Becon mara baada  ya kula nondoz ya degree ya Business Management kutoka chuo cha Aston University, Birmingham Uingereza 24 July 2014. Uongozi wa Giraffe Ocean View Hotel na Tanga Beach Resort unamtakia kila la kheri.

MTEMVU ATOA MKONO WA IDD WA VYOMBO NA SH. 10,000 KWA VIONGOZI 912 WA MATAWI YA CCM TEMEKE

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (kulia), akimkabidhi boksi la vyombo na zawadi ya sh. 10,000 mmoja wa viongozi 912 wa matawi wa ya CCM na jumuiya zake wa jimbo hilo, katika hafla ya kutoa mkono wa Idd el Fitr Dar es Salaam jana. Kila mmoja alipata zawadi kama hiyo. Katika boksi hilo kuna vikombe, birika, vijigo, sahani na chupa ya chai. Katikati ni mke wa mbunge huyo, Mariam Mtemvu. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Mtemvu akimkabidhi Mwenyekiti wa UWT CCM tawi la Mji Mpya Kata ya Buza, Temeke.

Baadhi ya viongozi wakiondoka na vyombo vyao huku wakiwa na sh. 10,000 kibindoni.
Shehena ya vyombo vilivyokuwa vinagawiwa
Sehemu ya umati wa viongozi wa CCM wa matawi waliofika kupata zawadi hizo. Wengi walimpongeza Mtemvu kwa moyo wake wa kujitolea.

 
Ni furaha tele kwa mama huyo

                          Mary wa Yombo Kilakala akifurahia zawadi yake na kitita cha sh. 10,000
Mwenyekiti wa CCM Tawi la Mlimani, Kata ya Kilakala, Temeke, Dar es Salaam, Omar Kichapwi huyoooo na vyombo vyake . ndani ya vyombo hivyo kuna vikombe, birika vijiko na chupa ya chai
Mke wa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Mariam Mtemvu akimkabidhi zawadi ya vyombo na sh. 10,000 mmoja wa viongozi wa CCM wa Jimbo hilo.
Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke,  akimkabidhi vyombo na sh. sh. 10,000 mmoja wa viongozi wa matawi wa CCM wa Jimbo hilo. Zawadi hizo zilitolewa na Mbunge wa Jimbo hilo, Abbas Mtemvu (kulia).
Wakifurahia kupata zawadi hizo



MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AAGANA NA BALOZI WA TZ NCHINI URUSI, NA WA UJERUMAN NCHINI TZ NA KUMKARIBISHA MPYA WA UJERUMAN

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi mpya wa Tanzania nchini Urusi, Luteni Generali Wyjones Matthew Kisamba, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 28, 2014 kwa ajili ya kumuaga akielekea kuanza kazi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi mpya wa Tanzania nchini Urusi, Luteni Generali Wyjones Matthew Kisamba, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 28, 2014 kwa ajili ya mazungumzo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi mpya wa Ujerumani nchini Tanzania, Balozi Egon Kochanke, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 28, 2014 kwa ajili ya kujitambulisha kuanza kazi. Kushoto ni aliyekuwa Kaimu Balozi wa Ujeruman Tanzania, aliyemaliza muda wake. Hans Koeppel.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi mpya wa Ujerumani nchini Tanzania, Balozi Egon Kochanke, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 28, 2014 kwa ajili ya kujitambulisha kuanza kazi. Kushoto ni aliyekuwa Kaimu Balozi wa Ujeruman Tanzania, aliyemaliza muda wake. Hans Koeppel.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na aliyekuwa Kaimu Balozi wa Ujeruman Tanzania, aliyemaliza muda wake, Hans Koeppel  wakati alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 28, 2014 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake. Kushoto ni Balozi mpya wa Ujerumani nchini Tanzania, Egon Kochanke, aliyefika kujitambulisha kuanza kazi. Picha na OMR

Article 0

JE UNAHITAJI WRISTBANDS

MKUTANO WA MAJADILIANO KUHUSU UFADHILI WA MIRADI YA MAENDELEO KATI YA SERIKALI YA TANZANIA NA JAPAN KWA MWAKA 2014/201

$
0
0
 Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip I. Mpango (wa pili kushoto) akifungua mkutano wa majadiliano baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Japan kuhusu ufadhili wa miradi ya maendeleo kwa mwaka 2014/15. Majadiliano hayo yalifanyika Julai 25, 2014 katika ukumbi  wa mikutano wa Wizara ya Fedha na yaliratibiwa na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Wajumbe wa mkutano uliohusisha Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wa Wizara, Wakurugenzi na Wataalam wa Sekta mbalimbali wakifuatilia kwa makini majadiliano yaliyokua yakiendelea.

Wajumbe wa mkutano wakimsiliza Mwenyekiti wa mjadala Dkt. Philip Mpango. Upande wa kulia ni wajumbe kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na upande wa kushoto ni wajumbe kutoka serikali ya Japan.Picha na: Thomas Nyindo, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
 Wajumbe kutoka Serikali ya Tanzania wakifuatilia michango mbalimbali kutoka kwa wajumbe wa mkutano huo. Miradi iliyowasilishwa ilihusisha Sekta za Kilimo, Viwanda, Usafirishaji, Nishati, Maji, na Afya.
 Baadhi ya wajumbe kutoka Tume ya Mipango, Klasta ya Biashara ya Kimataifa na Mahusiano ya Kiuchumi ambao walioshiriki kuratibu majadiliano hayo kutoka kulia Bw. Robert Senya na Bi. Sudah Lulandala wakifuatilia mjadala wakati wa mkutano huo.
 Wajumbe kutoka Serikali ya Japan wakichukua mambo ya muhimu wakati Mkutano wa Majadiliano ulipokuwa ukiendelea. Ujumbe huo uliongozwa na Balozi wa Japan nchini Tanzania Bw. Masaki Okada.

Obama kukutana leo viongozi wadogo walioonyesha dira toka nchi zote za Afrika jijini Washington DC

$
0
0
 Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe Joshua Nassari akiingia  kwenye ukumbi wa mkutano  wa Town Hall ambao baadaye yeye na viongozi vijana wenzie watakutana na Rais Barak Obama wa Marekani  atakapozungumza nao  jijini Washington DC.

Hii ni sehemu ya program ya mafunzo kwa viongozi wadogo walioonyesha dira toka nchi zote za Afrika (most promising young African leaders) . Program hii imeanzishwa na Rais Obama mwenyewe.
Miongoni mwa watanzania wachache waliopata fursa ya kuhudhuria ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Steven Masele na Mhe. Joshua Nassari. Watakutana pia na Waziri wa mambo ya nje wa marekani John Kerry na Mke wa Rais Obama Bi Michelle Obama Pamoja na maseneta, Magavana, wafanyabiashara wakubwa an watu wengine mashuhuri


Article 4

UTUPAJI TAKA HOVYO JIJINI DAR NI KERO KUBWA

$
0
0
 Uchafu uliotupwa jirani ya  makutano ya barabara ya Mogogoro, Uhuru na Lumumba jijini Dares Salaam na watu wasiojulikana wakati barabara hiyo ikiboreshwa kwa ajili ya mabasi yaendayo kasi ili kupunguza msomgamano wa magari huku eneo hilo likiwa si dampo la takataka.picha na Magreth Kinabo - Maelezo.

MSANII WA BONGO MOVIE ESTER KIAMA AFUTURISHA WASANII WENZAKE JIJINI DAR

$
0
0
Msanii chupukizi wa Bongo Movie, Ester Kiama leo alifuturisha wasanii, ndugu,jamaa na marafiki zake ikiwa ni ishara ya kumkumbuka marehemu mama yake mzazi ambaye alishatangulia mbele ya haki. Akitoa shukrani zake kwa waalikwa, alisema ameona vyema kuandaa chakula cha pamoja ili waweze kumuenzi mama yao mzazi kwa vile alipenda sana watu hasa kukutana na kupata chakula pamoja.
Msanii chupukizi wa Bongo Movie, Ester Kiama akiendelea kutoa shukrani zake za pekee.

Mjomba wa Msanii chipukizi wa Bongo Movie, Ester Kiama akitoa shukrani zake za pekee.
Wasanii, ndugu jamaa na marafiki waliofika wakipata futari.
Kila mmoja hakuwa nyuma kupata futari.

 
Huduma zikiendelea kutolewa.
Kumbu Kumbu.
Picha ya pamoja na wasanii wenzake mara baada ya kupata futari.
Msanii chupukizi wa Bongo Movie, Ester Kiama (kati) akiwa na Dada yake kushoto na mdogo wake wakipata ukodak.
Msanii chupukizi wa Bongo Movie, Ester Kiama akiwa na wajomba zake.


Msanii wa runinga, Michael Deodatus Sango ‘Mike’ akitoa shukrani kwa niaba ya rais wa Bongo Movie Steve Nyerere ambaye hakuweza kufika.

BENKI YA EXIM YAWAANDALIA FUTARI WATEJA WAKE ZANZIBAR

$
0
0
Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko wa Zanzibar, Mhe. Nassor Mazrui (kulia) akizungumza wakati wa Iftari iliyoandaliwa na Benki ya Exim Tanzania Tawi la Zanzibar kwa ajili ya wateja wake hivi karibuni. Wengine kulia kwake ni baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo na wateja walioalikwa katika tukio hilo. 
 Baadhi ya wafanyakazi na wateja wa Benki ya Exim Tanzania wakijumuika pamoja akatika Iftari iliyoandaliwa na benki hiyo Visiwani Zanzibar kwa ajili ya wateja wake.
 

RAIS BARACK OBAMA ASHIRIKI MKUTANO WA VIJANA WA AFRIKA

$
0
0


Rais wa Marekani ,Barack Obama akizungumza na Viongozi vijana toka nchi mbalimbali za Afrika waliokuwa wakipata mafunzo katika vyuo vikuu vya Arkansas na Florida.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry akitoa hotuba yake kwa Viongozi vijana toka barani Afrika waliokuwa wakishiriki mafunzo katika vyuo vikuu vya Arkansas na Florida nchini Marekani.
Rais Obama akiondoka Ukumbini mara baada ya kuzungumza na Viongozi vijana toka nchi mbalimbali za Afrika waliokuwa wakipata mafunzo katika vyuo vikuu vya Arkansas na Florida.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari ni miongoni mwa Vongozi vijana toka barani Afrika waliohudhuria mkutano huo na Rais Barack Obama .
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari ni miongoni mwa Vongozi vijana toka barani Afrika waliohudhuria mkutano huo na Rais Barack Obama hapa akifuatilia kwa makini Hotuba ya Rais Obama. .
Mbunge Joshua Nassari akiwa na Viongozi vijana wenzake walioshiriki mafunzo hayo nchini Marekani.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari  akionesha cheti chake cha kuhitimu mafunzo ya wiki tisa yaliyoshirikisha  Vongozi vijana toka barani Afrika .
Cheti cha kuhitimu Mafunzo ya wiki tisa alichotunukiwa Mbunge Joshua Nassari baada ya kuhitimu mafunzo ya wiki tisa yaliyoshirikisha Viongozi Vijana  nchini Marekani.


Ukumbi wa Regency Ballroom katika Hotel ya Omni Shoreham Washington DC ukiwa umepambwa kwa Bendera toka mataifa mbalimbali ikiwemo Tanzania.
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images