Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel

Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels

Showcase

Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 329 | 330 | (Page 331) | 332 | 333 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Mkufuzi wa mafunzo ya waamuzi wa mchezo wa masumbwi Ally Bakari 'Champion' kushoto akiwaelekeza baadhi ya marefarii waliojitokeza katika mafunzo hayo yaliyo andaliwa na chama cha ngumi za kulipwa TPBC yaliyoanza Ilala CCM Dar es salaam juzi na kumalizika jumamosi  hii .
  Mkufuzi wa mafunzo ya waamuzi wa mchezo wa masumbwi Ally Bakari 'Champion' kulia akisisitiza jambo kwa wakati wa mafunzo hayo uku marefarii waliojitokeza wakimsikiliza kwa makini kutoka kushoto ni Kondo Nassoro, Sako Mtlya na Buchato Michael .
  Mkufuzi wa mafunzo ya waamuzi wa mchezo wa masumbwi Ally Bakari 'Champion' akitoa maelekezo kwa mabondia na marefarii kabla ya kupigana wakati wa mafunzo kwa vitendo ya urefarii wa mchezo huo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

  BAADHI YA MAREFARII WALIOSHILIKI KATIKA KOZI HIYO KUTOKA KUSHOTO NI BUCHATO MICHAEL,PEMBE NDAVA,HAMISI KIMANGA,RAJABU MHAMILA 'SUPER D' ALLY BAKARI,Ayubu Tezikoma NA SAKO MTLYA

  0 0

     Mkurugenzi wa mfuko wa pesheni kwa watumishi wa umma'PSPF' Adam Mayingu kushoto akisalimiana na msanii Rose Ndauka wakati wa semina iliyoandaliwa na mfuko huo kwa ajili ya kutoa elimu na kujiunga katika mfuko huo Dar es salaam juzi kulia ni msanii Ester Kiama picha na mpiga picha wetu
   Baadhi ya wasanii wakijadiliana jinsi ya kujaza fomu za kujiunga na mfuko wa wa pesheni kwa watumishi wa umma'PSPF'
   Mwigizaji na Mchekeshaji ambaye ni Mwenyekiti wa Kundi la Bongo Movie Unity, Steven Mengere a.k.a 'Steve Nyerere' kushoto akizungumza wakati wa semina kwa ajili ya wasanii iliyoandaliwa na mfuko wa pesheni kwa watumishi wa umma'PSPF' juzi makao makuu ya mfuko huo Dar es salaam juzi picha na mpiga picha wetu
  Mkurugenzi wa mfuko wa pesheni kwa watumishi wa umma'PSPF' Adam Mayingu kushoto akizungumza na wasanii Rose Ndauka wakati wa semina iliyoandaliwa na mfuko huo kwa ajili ya kutoa elimu na kujiunga katika mfuko huo Dar es salaam juzi kulia ni msanii Ester Kiama.

   Mkurugenzi wa mfuko wa pesheni kwa watumishi wa umma'PSPF' Adam Mayingu wa pili kushoto akizungumza na wasanii baada ya kufungua semina kwa ajili ya wasanii mbalimbali .
   
   Mkurugenzi wa mfuko wa pesheni kwa watumishi wa umma'PSPF' Adam Mayingu kushoto akisalimiana na kocha wa timu ya simba msimu uliopita Jamuhuri Kiweru 
  wakati wa semina iliyoandaliwa na mfuko huo kwa ajili ya kutoa elimu na kujiunga katika mfuko huo Dar es salaam juzi katikati ni Afisa Masoko wa mfuko huo Rahma Ngassa picha na mpigapicha wetu
  BAADHI YA WATU WALIOHUDHULIA SEMINA HIYO

  0 0

  We are taking this opportunity to thank our entire fans around the globe for your support to this band. It is your support that makes the Ngoma Africa band prosper, without you there will be no success!

  Please, we ask you again to keep on supporting and let the band be on the top most position in every event, festival, media etc.

  Let others around you join the band at www.ngoma-africa.com, here they will have the opportunity to enjoy music at www.ngoma-africa.com  or http://www.ngoma-africa.com
  Yours Sincerely

  0 0

  0 0

   Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Kanali James Ruzibiza Stashahada ya Usalama na Stratejia (Diploma in Security and Strategic Studies) katika mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014. Kanali Ruzibiza, ambaye anatokea Rwanda, ni mmoja wa washiriki tisa wa kozi waliotoka nchi za nje. Washiriki wengine kutoka nje y nchi walitoka Kenya, Malawi, Namibia, Nigeria, Uganda, zambia na Zimbabwe. Jumla ya wahitimu 30, wakiwemo maafisa wandamizi katika utumishi wa umma, ambapo 11 wametoka JWTZ na 10 kutoka vyombo vingine vya usalama na idara mbalimbali. 

   Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Luteni Jenerali C.L. Makakala Shahada ya Uzamili ya Falsafa ya Usalama na Stratejia katika mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014. Luteni jenerali Makakala, ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi wa kwanza, amekuwa mtunukiwa wa kwanza wa Shahada hiyo hapo chuoni.
   Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia baada ya kutunuku shahada katika  mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014.Jumla ya wahitimu 30 wamehudhuria kozi hiyo wakiwemo maafisa wandamizi katika utumishi wa umma, ambapo 11 wametoka JWTZ na 10 kutoka vyombo vingine vya usalama na idara mbalimbali. Washiriki wengine tisa wametoka  nchi za nje ambazo ni Kenya, Malawi, Namibia, Nigeria, Rwanda Uganda, Zambia na Zimbabwe.
   Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwaambia kuwa sasa ni zamu yao kupiga picha ya kumbukumbu bila yeye wahitimu wa Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014.
  Picha ya Pamoja.PICHA NA IKULU

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhad Mussa Salum alipowasili kwenye makaazi ya Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda (nyuma yao) Oysterbay jijini Dar es salaam kwa ajili ya Futari leo Jumamosi Julai 26, 2013. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na wa pili kulia ni Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi ya Dar es salaam Kamishna Suleiman Kova
   Rais Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali wakijumuika na waumini wengine katika Swala ya Magharibi katika  makaazi ya Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda Oysterbay jijini Dar es salaam alikoandaa Futari leo Jumamosi Julai 26, 2013
   Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiongea na baadhi ya waalikwa kwenye futari aliyoandaa, wakiwemo waigizaji Mpoki wa Ze Komedy, Stephen JB, na watangazaji wa redio

   Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda, Jaji Mkuu Mhe Mohamed Chande Othman na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Ndg Ramadhani Madabida wakipakua futari
   Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba akijumuika na waalikwa wengine kupakua futari
   Mawaziri wakuu Wastaafu Mzee Cleopa Msuya na Jaji Joseph Sinde Warioba wakiwa wameketi pamoja na Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu (kulia, mwenye baraghashia) na Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio
    Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi ya Dar es salaam Kamishna Suleiman Kova (kushoto) akiwa na viongozi wa dini Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) la Ubungo jijini Dar, Lusekelo Antony 'Mzee wa Upako' (wa pili kushoto),  Rais wa shirika la kidini la Wapo Mission International Bishop Sylvester Gamanywa (kulia) na mashehe 
   Meza kuu ikifurahia jambo baada ya futari
   Meya wa jiji la Dar es salaam Dkt Didas Masaburi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi ya Chama Cha mapinduzi CCM (Taifa) Bw. Abdallah Bulembo wakiwa na waalikwa wenzao kwenye futari hiyo
   Sehemu ya waalikwa
   Wazee Mashuhuri wa mkoa wa Dar es salaam mezani pao
   Mufti wa Tanzania Sheikh Shaaban Issa Simba akiongoza dua baada ya futari
   Sehemu  ya waalikwa kwenye futari hiyo
   Rais Kikwete akiagana na mmoja wa wazee mashuhuri wa Mkowa wa Dar es salaam
   Rais Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakisalimiana na waalikwa baada ya kufuturu pamoja
   Rais Kikwetena  Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal wakisalimiana na waalikwa 
   Rais Kikwetena Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakisalimiana na waalikwa baada ya futari
   Rais Kikwete akisalimiana na mchora katuni maarufu Ali Masoud 'Kipanya' huku Mrisho Mpoto akisubiri zamu yale
   Rais Kikwete akifurahi pamoja na waalikwa wenzie
   Rais Kikwete akisalimiana na mmoja wa wazee mashuhuri wa Dar es salaam
   Rais Kikwete akisalimiana na mwanamuziki Christian Bella
   Rais Kikwete akisalimiana na mwanahabari mkongwe Bw. Mwondosha Mfanga
   Rais Kikwete akisalimiana na mwanamuziki nyota wa kizazi kipya, Ommy Dimpoz

   Rais Kikwete akiongea na Mwana FA
   Rais Kikwete akisalimiana na mtayarishaji, Muongozaji na mwigizaji nyota wa filamu Kulwa Kikumba 'Dude
  Rais Kikwete akiendelea kusalimiana na waalikwa wenzie

  Mkono wa mwisho ni wa mtoto huyu aliyepata bahati ya kuagana na Rais Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali baada ya futari

  0 0

    Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiweka sawa  kanzu ya Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda kabla ya kushiriki katika futari waliyoandaliwa na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali katika makazi yake Oysterbay jijini Dar es salaam Ijumaa jioni Julai 25, 2014
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman wakiwasili kushiriki katika futari waliyoandAaliwa na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali katika makazi yake Oysterbay jijini Dar es salaam Ijumaa jioni Julai 25, 2014.PICHA NA IKULU

  0 0

   Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Deus Kibamba (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, wakati akitoa tamko kuhusu Bunge la Katiba litakaloanza Agosti 5, 2014 ambapo walishauri Bunge hilo likae wiki mbili badala ya miezi miwili kama ilivyopangwa ili kupunguza matumizi makubwa ya fedha za Umma. Kutoka kushoto ni Mjumbe wa Kamati na Uongozi Jukata Omar Ali Omar,  Meneja Habari na Mawasiliano wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Kenny Ngomuo, Makamu Mwenyekiti wa Jukata, Hebron Mwakagenda na  Mratibu wa Jukata, Diana Kidara.
   Makamu Mwenyekiti wa Jukata, Hebron Mwakagenda, akisoma tamko hilo.
   Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.

  0 0

   Msimamizi wa Uchaguzi Bw. Alfred Kayombo (kulia) akimtangaza mshindi wa nafasi ya mwenyekiti Bw. Ibrahim Ngogo.
  Kwa mara ya kwanza katika historia, chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Makete mkoani Njombe kimefanya uchaguzi wa uongozi mbalimbali ambapo Bw. Ibrahim Ngogo amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa ngazi ya wilaya.

  Na Edwin Moshi, Makete
  Akitangaza matokeo msimamizi wa uchaguzi huo Bw. Alfred Kayombo amesema Bw. Ibrahim Ngogo amepata kura 25 akifuatiwa na Isaac Sanga aliyepata kura 6 na Shaaban Mkakanze aliyepata kura 1.

  Bw. Kayombo amesema kutokana na umuhimu wa demokrasia ndani ya chama hicho, wameamua kufanya uchaguzi huo kwa mara ya kwanza toka chadema iingie wilayani hapa, hivyo kuonesha kuwajali wanachama wake
  Mbali na viongozi hao wa juu wa chama pia Bw. Lazaro Chaula amechaguliwa kuwa katibu mwenezi wa Chadema wilaya ya Makete kwa kupata kura 30, Bi. Rose Mbilinyi amechaguliwa kuwa Mtunza hazina wa wilaya kwa kupata kura 26.

  Aidha Bw. Atukuzwe Mahenge amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa baraza la vijana (BAVICHA) wilaya na Bw. Shadraack Mwachota akichaguliwa kuwa katibu wake na wote wamepita bila kupingwa.

  Bi. Beatrice Kyando amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa baraza la wanawake wa chadema wilaya (BAWACHA), Bi Christina Timoth akichaguliwa kuwa katibu wa BAWACHA, na Bi. Mariam Asheli akichaguliwa kuwa Katibu wa uhamasishaji wa BAWACHA na wote wamepita bila kupingwa.

  katika uchaguzi huo pia Bw. Abiud Elia amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa baraza la wazee kwa kura 3, Abeli Juma Sanga akipata kura 1 na kuchaguliwa kuwa Makamu mwenyekiti, pamoja na Simon Nyasanga kuwa katibu wa baraza la wazee wilaya.

  Katika hatua nyingine wamechaguliwa wajumbe 4 waliochaguliwa kuingia kwenye kamati tendaji ambao ni John Sanga, Patison Pela,Orignal Sanga na Alafat Msigwa, huku Bw.Illomo Werner Naftal akichaguliwa kuwa mwakilishi wa wilaya kwenye mkutano mkuu taifa.

  Akiahirisha mkutano huo mwenyekiti wa Chadema wilaya Bw. Ibrahim Ngogo amewasihi wajumbe kuondoa makundi na kutokubali kutumia kwa ajili ya kukibomoa chama na badala yake washikamane wawe kitu kimoja kukijenga chama.

  "Makamanda uchaguuzi umeisha haitakiwi tuwe na makundi, tushikamane kukijenga chama chetu, hilo ndilo la msingi kwa sasa, sisi viongozi mtupe ushirikiano" amesema Ngogo  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Dr Joel Bendera Leo amewaongoza mamia ya wananchi wa mkoa wa Morogoro kumzika Mke wa Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini, Mh lnocenti Kalogeris. Watu mbali mbali wakiwemo wabunge,wakuu wa mikoa wastaafu na watu mashuhuri wamefurika nyumbani kwa mbunge huyo ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Morogoro 
   Mkuu wa mkoa akimpeleka Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mh  Innocent Kalogeris  kupokea mwili wa mpendwa mke wake,kulia ni dada wa mbunge huyo.
   Marehemu Elizabeth Kapoloma enzi za Uhai wake , Bi,Elizabeth Kapoloma alifariki Alhamisi Kwa Ugonjwa Moyo.
   Mwili wa marehemu ukiwasili nyumbani kwake kwajili ya Heshima za Mwisho na Ibada kabla ya Mazishi leo    

    Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mh Dk Joel Bendera akimbembeleza Mume wa marehemu Mhe lnocent Kalogeris

  0 0

  Jaji Vyonne Cherry au Monalisa akitoa maoni kwa washiriki waliokuwa wameshiriki kwenye filamu fupi iliyochezwa na washiriki wa TMT
    Kundi la Kwanza la Washiriki wa TMT waliocheza filamu fupi iitwayo LUGHA GONGANA wakiwa mbele ya meza ya Pilato katika ukumbi wa makumbusho ya Taifa mwanzoni mwa wiki.
   Mshiriki wa TMT, Mwanaafa Mwinzago akifunika uso wake kwa kutoamini kuwa ameponea kwenye tundu la sindano kutokana na kuondolewa katika maumivu ya Jua la Utosi na kuendelea na mashindano hayo
   Mshiriki Wa TMT, Moses Obunde (Mwenye Suti) akimpongeza Mshiriki Mwenzie Mzee Kapalata Mtawa kwa kuweza kuondolewa Kwenye Jua la Utosi na Kupelekwa Kivulini katika Shindano la TMT linaloendelea.
   Washiriki walioingia kwenye Jua la Utosi wakiwa mbele ya Meza ya Pilato huku mshiriki mmoja kutoka kwa washiriki hao aliyaaga mashindano ya TMT.
   Simanzi Zikianzia hapo sasa mara baada ya Washiriki kupunguzwa ili apatikane mmoja wa kuondoka.
  Majaji wa shindano la TMT wakimsikiliza kwa makini Mshiriki wa TMT, Mwanaafa Mwinzago (anayeonekana kwenye runinga mbele) wakati akijielezea kabla ya filamu fupi aliyoshiriki kuonyeshwa ili majaji waweze kutoa hukumu kwa washiriki wa kundi hilo
   Majaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) katikati wakiwasikiliza washiriki wa kundi la kwanza wanavyojielezea kabla ya filamu fupi waliyochezwa kuonyeshwa katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa wiki iliyopita
   Majaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) wakiangalia filamu fupi iliyochezwa na washiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) katika ukumbi wa makumbusho kabla ya kuanza kutoa hukumu kwa washiriki ni nani anatoka na nani anabaki.
   Wakabaki wawili na hatimaye mmoja kati ya hao aliweza kuondolewa katika mashindano hayo
   Hatimaye Mshiriki Isalito Isaya Akaweza kurudi ndani ya Mjengo wa TMT kutokana na Kura zake kumzidi Mshiriki mwenzie Pendo ambaye aliweza kuaga mashindano hayo kutokana na kura kuwa chache
  Baadhi ya Washiriki wa TMT wakimuaga Mshiriki mwenzao Pendo Edward (Katikati) ambaye aliweza kutolewa kwenye mashindano kutokana na kura kuwa chache.Picha Zote na Josephat Lukaza
  Na Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited - Dar Es Salaam.
  Hatua ya mchujo katika Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) limeingia wiki ya tatu ya mchujo sasa mara baada ya mshiriki mmoja kuaga shindano hilo wiki hii. Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) limekuwa shindano bora ambalo kadri siku zinavyozidi kwenda linazidi kuteka nyoyo za watanzania wengi waliopo ndani na nje ya Nchi kutokana na utofauti wake na uzuri wake pia.
  Mshiriki mmoja ambaye ni Pendo Edward aliweza  kuchomwa na jua la utosi lililompelekea kutoka kwenye shindano hilo kubwa la Tanzania Movie Talents (TMT) ambapo mpaka sasa washiriki kumi na tano (15) ndio wamebaki katika nyumba ya TMT na hali ya simanzi bado inaendelea katika nyumba ya TMT kwa wiki hii ambapo mshiriki mwingine atatakiwa kutoka.
  Shindao la TMT limekuwa likivuta hisia za watanzania wengi waliopo ndani na Nje ya Tanzania kutokana na Utofauti wake na ubora wake na kupelekea watanzania wengi sana kufuatilia shindano hilo kwa ukaribu na umakini zaidi.
  Hatimaye wiki hii Tanzania Movie Talents iliamua kuzindua Zoezi la kuwapigia kura washiriki wake kupitia ukurasa wetu wa facebook ambapo sasa watanzania na wapenzi wa TMT ambao wanauwezo wa kupata na kutumia internet sasa wanaweza kuwapigia kura washiriki waliowavutia kupitia ukurasa wetu wa facebook na vilevile kuendelea kuwapigia kura washiriki kwa kutumia simu zao za mkononi.
  Jinsi ya Kumpigia kura Mshiriki umpendae kwa Kutumia Simu ya Mkononi Andika Neno "TMT" ikifuatiwa na namba ya ushiriki halafu tuma kwenda 15678. Mfano TMT 00 tuma kwenda 15678.
  Na Jinsi ya Kumpigia kura mshiriki kupitia ukurasa wetu wa facebook BOFYA HAPA  kwa kupata maelezo.

  0 0

  Principle Operation Officer wa NSSF, Joyce Mruma akigawa zawadi kwa wastaafu wa NSSF wakati wa hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na shirika hilo. 
  Ofisa Mwandamizi wa Operesheni wa NSSF, Lydia Ignace akitoa zawadi kwa wastaafu wa Shirika hilo waliohudhuria hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na NSSF kwa ajili ya wastaafu wa Mkoa wa Tanga.
  Principle Operation Officer wa NSSF, Joyce Mruma akitoa zawadi kwa mstaafu wa NSSF, Bella Antao wakati wa hafla ya kufuturisha wastaafu wa Shirika hilo.   Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Ummy Mwalimu akizungumza katika hafla hiyo.
  Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego akizungumza wakati wa hafla ya kufuturisha wastaafu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), iliyofanyika mkoani Tanga.
  Sheikh Mkuu Mkoa wa Tanga, Alhaji Juma Luhudu akizungumza wakati wa hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na NSSF kwa ajili ya wastaafu wa Mkoa wa Tanga pamoja na wadau wake.
  Kaimu Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mkoa wa Tanga, Emmanuel Masika akizungumza wakati wa hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa kwa ajili ya wastaafu wa Mkoa wa Tanga.
  Baadhi ya maofisa wa NSSF wakiwa katika picha ya pamoja.
  Wastaafu.
  Baadhi ya wastaafu wa NSSF Mkoa wa Tanga wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kufuturisha wastaafu hao iliyoandaliwa na NSSF.

  Mmoja wa wastaafu akitaka ufafanuzi kutika kwa viongozi wa shirika hilo kuhusu huduma za shirika hilo.
  Mstaafu wa NSSF, Edith Lumeya akiuliza swali kuhusu malipo ya wastaafu.
  Mstaafu wa NSSF, Muni Hussein Ally  akiuliza swali.
  Meneja wa Mafao wa NSSF, James Oigo akijibu maswali ya baadhi ya wastaafu waliotaka ufafanuzi kuhusu huduma mbalimbali za shirika hilo. 
  Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji, Maryam Muhaji hafla ya kufuturisha wastaafu iliyofanyika Mkoa wa Tanga. 
  Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Alhaji Juma Luwuchu akizungumza wakati wa hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na NSSF kwa ajili ya wastaafu wa Mkoa wa Tanga.
  Baadhi ya wastaafu wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego (katikati).
  Baadhi ya wastaafu wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego (katikati).
  Baadhi ya Maofisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego (katikati), wa pili kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Alhaji Juma Luwuchu, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Chiku Matesa (wa  tatu kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji, Maryam Muhaji.
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Ummy Mwalimu, (kushoto)  akishiriki futari.
  Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego (wa pili kushoto)  akiwaongoza akinamama kupata futari.
  Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego (wa tatu kushoto), akishiriki katika futari iliyoandaliwa na NSSF kwa ajili ya wastaafu wa Mkoa wa Tanga pamoja na wadau wake. Kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Ummy Mwalimu na wa pili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa NSSF, Chiku Matesa.
  Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego (kulia), akishiriki katika futari iliyoandaliwa na NSSF kwa ajili ya wastaafu wa Mkoa wa Tanga pamoja na wadau wake. Kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Ummy Mwalimu na Kaimu Mkurugenzi wa NSSF, Chiku Matesa.
  Wastaafu na wadau wa NSSF Mkoani Tanga wakijumuika katika futari.
  Waastaafu wa wadau wa NSSF Mkoani Tanga wakijumuika katika futari.
  Wastaafu na wadau wa NSSF Mkoani Tanga wakijumuika katika futari.
  Baaadhi ya wadau wa mfuko huo wakipata futari.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Chiku Matesa akiwashukuru Wastaafu na Wadau waliohudhulia futari iliyoandaliwaa na mfuko huo.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Chiku Matesa akiwashukuru Wastaafu na Wadau waliohudhulia futari iliyoandaliwaa na mfuko huo.
  Watoto wanaoishi katika Kituo cha Kulelea Watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Barabara ya 7 Mkoani Tanga wakiwa ni miongoni mwa wageni waalikwa katika futari iliyoandaliwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa ajili ya Wastaafu na Wadau wa Mfuko huo iliofanyika mkoani Tanga.

  Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Alhaji Juma Luwuchu akiomba dua.

  Na Elizabeth Kilindi, Tanga

  SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limejipanga kuhakikisha linaboresha mfuko huo kwa kuwafikia wakulima na wafugaji nchini kote ili kupanua wigo kwa wanachama wake.  Hayo yameelezwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Chiku Matesa, wakati akizungumza katika hafla ya kufuturisha wastaafu (PENSHENI) pamoja na wadau wa mfuko huo iliyofanyika katika hotel ya Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.

  Alisema kuwa  wakulima na wafugaji wamekuwa wakisaulika hivyo kama shirika limeona vema kuwafikia ikiwemo kuwapatia elimu ambayo itawasaidia kujiunga na mfuko huo.

  ‘Sisi  kama shirika tumeona itakuwa ni vizuri zaidi kuwafikia wakulima na wafugaji ili kuweza kujiunga na mfuko wetu ambao unamafao uzazi, kuumia kazini, Kustaafu na mengineyo'.

  Kaimu Mkurugenzi huyo alisema shirika limeanzisha mpango wa kutoa mikopo kwa wanachama wake kupitia Saccos ambapo utalenga kuwawezesha wanachama wa mfuko  huo kujikwamua kiuchumi.

  Naye  Mkuu wa Wilaya Tanga Halima Dendego aliwataka  wafanyakazi waliojiajiri na walioajiriwa ikiwemo wa mashambani kujiunga na mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF ili kuweza kujiwekea akiba hasa ya uzeeni.
  “Nawaasa hawa wafanyakazi wajiunge na mfuko huu kwani unafaida kubwa hasa unapostaafu unakuwa na uhakika wa kuishi maisha bora yasiokuwa na wasiwasi’’alisema Dendego. 

  Principle Operation Officer wa NSSF, Joyce Mruma akigawa zawadi kwa wastaafu wa NSSF wakati wa hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na shirika hilo. 
  Ofisa Mwandamizi wa Operesheni wa NSSF, Lydia Ignace akitoa zawadi kwa wastaafu wa Shirika hilo waliohudhuria hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na NSSF kwa ajili ya wastaafu wa Mkoa wa Tanga.
  Principle Operation Officer wa NSSF, Joyce Mruma akitoa zawadi kwa mstaafu wa NSSF, Bella Antao wakati wa hafla ya kufuturisha wastaafu wa Shirika hilo.

  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Ummy Mwalimu akizungumza katika hafla hiyo.

  0 0  0 0

  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha akipimwa kabla ya kuchangia damu katika zoezi lilioendeshwa na Shrika la Red Cross katika kuchangia damu Mkoani Rukwa. Kumekuwepo na uhaba mkubwa wa damu katika Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa na vituo vingine uhaba ambao unafikia nusu kwa nusu ukilinganisha kiasi kinachopatikana na mahitaji yaliyopo. 

  Uhaba huo umesababishwa na muamko hafifu wa wananchi kuchangia damu kutokana na hofu inayosababishwa na dhana potofu kuwa uchangiaji damu una madhara kwa mchangiaji. Madaktari hao wa Hosptali Kuu ya Mkoa pamoja na watumishi wengine wa Serikali waliamua kujitolea ili kuonyesha mfano kwa wananchi waweze kuondokana na hofu hiyo waweze kujitokeza kuchangia damu kuokoa maisha ya watanzania wanaohitaji huduma hiyo muhimu.
  Baadhi ya madaktari wa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa wkichangia damu.
  Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Esther Kasegezya akichangia damu katika zoezi hilo.
  Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Rukwa Dkt. Samwel Marwa akipatiwa vipimo muda mfupi kabla ya kuchangia damu.
  Dkt. Marwa akichangia damu.
  Mchangiaji baada kutoa damu hupata viburudisho ikiwemo vinywaji baridi na biskuti maalum.
  Sehemu ya damu iliyokuwa imechangiwa katika zoezi hilo.
  (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa)

  0 0

   Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Janet Mbene akiangalia bidhaa wakati wa ufunguzi huo leo.

  Wafanyakazi wa Nakumatt Mlimani wakifurahia wakati wa sherehe za ufunguzi wa mall hiyo Mlimani City jijini Dar es salaam leo
  Furaha ya kuanza kazi Nakumatt Mlimani leo
  Mkurugenzi Mtendaji wa Nakumatt Holdings, Atul Shah akimuonesha baadhi ya bidhaa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Janet Mbene wakati wa ufunguzi huo leo

  KAMPUNI ya Nakumatt Holdings, imezindua rasmi tawi la kwanza kati ya matawi yake matatu makubwa nchini Tanzania ambayo awali yalimilikiwa na Kampuni ya Shoprite ya Afrika ya Kusini. 

  Ikiwa ni mpango wake mpya wa kuboresha zaidi huduma zake, Nakumatt holdings, imezindua tawi hilo kubwa ambalo litakuwa utambulisho muhimu wa huduma zake katika eneo la biashara la Mlimani City litakaloitwa Nakumatt Mlimani. 

  Tawi hilo la 48 la Nakumatt limepambwa kwa rangi na mwonekano wa alama za Nakumatt na kwa ubunifu wa hali ya juu. Pamoja na Nakumatt Mlimani, kampuni hiyo pia iko mbioni kuzindua tawi lengine kubwa litakalojulikana kama ‘Nakumatt Pugu Road’ jijini Dar es salaam ambako pia kutakuwa makao yake makuu. Pia itafungua Nakumatt Arusha siku zijazo. 

   Kwa kufungua matawi yake matatu moja baada ya jingine, Nakumatt pia itakuwa imefikisha matawi 50 katika mtandao wake wa huduma za uuzaji bidhaa na hivyo kutekeleza mkakati wake wa maendeleo ambao ulizinduliwa mwaka 2011.

   Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka lake la kwanza in Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Nakumatt Holdings, Atul Shah alisema kufunguliwa kwa matawi matatu mapya yaliogharimu takriban dola za Marekani milioni 3 ni sehemu ya mpango wa upanuzi wa huduma za uuzaji bidhaa katika kanda ya Afrika. Kutokana na uzinduzi wa Tawi la Nakumatt Mlimani, Shah alisema kuwa Nakumatt sasa ina maduka mawili makubwa yanayofanya kazi nchini Tanzania. 

  Nakumatt Mlimani inaungana na duka jingine la la Nakumatt Moshi lililofunguliwa mwaka 2011 katika mji huo ambako kuna Mlima Kilimajaro. 
  ”Uzinduzi wa Nakumatt Mlimani ni ndoto ya muda mrefu ambayo sasa imekuwa kweli ambapo tumekuwa tukifikira mahali pa kuweka duka letu jijini Dar es salaam na maeneo mengine nchini Tanzania,” alisema Shah na kuongeza: “Uzinduzi huu pia ni hatua nzuri itakayopelekea uzinduzi mwingine wa duka letu la 50 katikati ya Agosti ambapo tutakuwa tumefanikiwa kufikia malengo yetu tuliyojiwekea kuyafikia Februari mwakani.” Maduka matatu ya Shoprite yalifungwa mwezi uliopita ili kufanikisha kazi ya kuyaboresha zaidi sambamba kwa kuzingatia viwango na uzoefu wa Nakumatt. 

  Pia Nakumatt inatarajia kufungua matawi mengine matatu ya biashara nchini Kenya kabla ya mwisho wa mwaka huu. Pia kampuni hiyo itakuwa na duka kubwa katika eneo kubwa la kifahari la Green Square mjini Kericho nchini Kenya. Shah alisema Nakumatt ina mkakati wa kukuza biashara wa kampuni ambao unategemea zaidi uwepo wa vitega uchumi ambapo kampuni inaweza kuendesha shughuli zake za maduka ya supermaketi. Shah aliongeza kwa kusema:

   “ Kwa sasa tunaendesha shughuli zetu katika nchi 12 na tunashirikiana na wamiliki wa maeneo ya biashara nchini Kenya ambao wanaweza kutoa huduma za kujenga maeneo ya maduka makubwa katika maeneo ya Machakos, Nyeri, Kajiado, Garissa, Embu, Naivasha,Narok Busia and Homabay.” 

  Ili kutimiza masharti ya Nakumatt, Shah aliwahimiza waendelezaji wa maeneo ya biashara na Mameneja wa Miradi kushauriana na wataalam wa Nakumatt kuhusu namna ya kuboresha uchoraji wa ramani na ujenzi wenye mvuto kwa wateja katika maduka ya kampuni hiyo.

  0 0

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Pwani Bi.Mwantumu Mahiza akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki leo Jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akitoa neno la shukrani kwa Mkuu wa Pwani Bi. Mwantumu Mahiza kwa Kuukabidhi mwenge wa Uhuru Salama Mkoani Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akitoa neno la shukrani kwa Mkuu wa Pwani Bi. Mwantumu Mahiza kwa Kuukabidhi mwenge wa Uhuru Salama Mkoani Dar es Salaam.
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akishika mwenge wa Uhuru ulipowasili mkoani Dar es Salaam.(Picha na Hassan silayo na Benjamin sawe).
   
   Kikundi cha vijana toka Halmashauri ya Manispaa ya Temeke wakisherehesha wakati wa kuwasili kwa mwenge wa Uhuru uliokabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik kutoka kwa mkuu wa Mkoa wa Pwani Bi. Mwantumu Mahiza Leo Jijini Dar es Salaam
   Kikundi cha vijana toka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala wakisherehesha wakati wa kuwasili kwa mwenge wa Uhuru uliokabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik kutoka kwa mkuu wa Mkoa wa Pwani Bi. Mwantumu Mahiza Leo Jijini Dar es Salaam
   Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa(mwenye miwani) akishiriki kucheza pamoja na Kikundi cha vijana toka Manispaa hiyo wakati wa kuwasili kwa mwenge wa Uhuru leo Jijini Dar es Salaam.
   Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana James Kajugusi(katikati) akiwaeleza jambo Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga(Kulia) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel wakati wa kuwasili kwa mwenge wa Uhuru leo Jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Wilaya ya Mafia Sauda Salum Mtondoo akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana James Kajugusi alipowasili wakati wa kuukabidhi mwenye wa uhuru kutoka wilaya yake.
   Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akisalimiana na Vijana wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa walipowasili kutoka Wilaya ya Mafia
   Mkuu wa Wilaya ya Mafia Sauda Salum Mtondoo akikimbiza Mwenge wa Uhuru kwa ajili ya kuukabidhi tayari kuanza ziara yake Mkoani Dar es Salaam.
   Mkuu wa Wilaya ya Mafia Sauda Salum Mtondoo (Mwenye T-shirt nyeupe) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Pwani Bi.Mwantumu Mahiza Leo Jijini Dar es Salaam
   Mkuu wa Mkoa wa Pwani Bi.Mwantumu Mahiza akikimbiza mwenge wa Uhuru Tayari kwa kuukabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadiki.
   Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkingaakisalimiana na Kiongozi wa mbio za Mwenge Taifa, Rachel Kasanda wakati wa kuwasili kwa mwenge wa uhuru leo Jijini Dar es Salaam.

  0 0

   Mwakilishi wa Jimbo la Uzini(CCM) Mohamedraza Hassanal akizungumza na Waandishi wa habari katika ukumbi wa Hoteli ya Grand Palace mjini Zanzibar.Katika mazungumzo yake alisema ni Vyema Bunge la Katiba likaghairishwa ili kutoa fursa zaidi Watu wajihusishe na harakati za Uchaguzi Mkuu wa 2015 na Kupatikane Wasaa mpana wa kujadiliana kwa dhamira ya dhati ya kupata Katiba Bora inayoridhiwa na upande wa Bara na Visiwani.

  0 0

  *Awaasa wananchi wasikubali kugeuzwa mtaji na wagombea

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewaonya Watanzania kuwa makini na watu wanaotumia rushwa ili kupata nafasi za uongozi na hasa kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, 2015.

  Ametoa onyo hilo leo mchana (Jumapili, Julai 27, 2014) wakati akizungumza na mamia ya waumini na viongozi mbalimbali waliohudhuria ibada ya uzinduzi wa dayosisi mpya ya Ruvuma ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na kuwekwa wakfu Askofu Amon Mwenda aliyeteuliwa kuongoza dayosisi hiyo.

  “Ninawasihi wananchi wawe makini na viongozi wanaopenda kutoa rushwa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu. Kama mtu ana nia ya kweli ya kuongoza ni kwa nini atumie fedha ili kupata nafasi ya uongozi?,” alihoji.

  “Tatizo ni kwamba hata wananchi hivi sasa wanakubali kupokea kile kinachotolewa na wagombea. Atakuja huyu atakupa hiki na mwingine naye atakupa kile, lakini ujue akiingia madarakani anaanza kurudisha haraka vile alivyowagawia,” alisema.

  Aliwaonya wananchi kuwa makini ili wasije wakageuzwa mtaji wa kuwanufaisha watu binafsi. “Tukikubali kutumika ni sawa tutapata viongozi wakati wa uchaguzi, lakini watakuwa ni wale wasio na hofu ya Mungu, wenye kujali maslahi yao kuliko ya wananchi waliowachagua,” aliongeza.

  Aliwaomba viongozi wote wa dini waliohudhuria sherehe hizo pamoja na waumini wote waendelee kuliombea Taifa ili Mungu aliepushe na janga hilo la watu kupenda rushwa. Alitumia fursa hiyo pia kuwaomba wazidi kuuombea mchakato wa kupata Katiba mpya ili wabunge wote warejee ndani ya Bunge na kuikamilisha kazi waliyoianza.

  Alimuomba Askofu huyo mpya apokee jukumu hilo kwa mikono miwili na kumuahidi kuwa kama Serikali watakuwa naye bega kwa bega kuwaongoza Watanzania walioko kwenye dayosisi yake. Dayosisi hiyo mpya inahusisha mkoa wote wa Ruvuma na wilaya ya Ludewa eneo ambalo lina ukubwa wa kilometa za mraba 72,630. Kati ya hizo km. za mraba 64,233 ni za mkoa wa Ruvuma na km. za mraba 8,397 ni za wilaya ya Ludewa.

  Mapema, akitoa hotuba yake ya kwanza mara baada ya kusimikwa rasmi, Askofu Mwenda alisema dayosisi mpya ya Ruvuma imezaliwa katika kipindi chenye changamoto nyingi za kidunia na utandawazi ukiwemo mmomonyoko mkubwa wa maadili.

  Hata hivyo, akiainisha malengo ya dayosisi hiyo ambayo anakuwa Askofu wake wa kwanza, Askofu Mwenda alisema mbali ya kufundisha neno la Mungu, dayosisi hiyo itahimiza ufanyaji kazi ili wakazi wake wawe na akiba ya chakula cha kutosha.

  Alisema watashirikiana na Serikali na wadau wa ndani najje katika kutoa huduma za kijamii hasa elimu na afya. Aidha alisema atakabiliana na changamoto za sasa ambazo alizitaja kuwa ni mmomonyoko wa maadili, rushwa, mauaji ya albino, unajisi wa watoto na ubakaji wa wanawake.

  Akitoa shukrani kwa niaba ya waumini wa kanisa hilo, Askofu Mkuu wa KKKT, Dk. Alex Malasusa alisema Kanisa lingependa kupata viongozi ambao ni wacha Mungu. Akirejea mahubiri yake, Askofu Malasusa alisema inashangaza kuona kuna baadhi ya watu wanagombea nafasi za uongozi lakini hawana mapenzi na Mungu aliyewaumba watu anaotaka kuwaongoza.

  “Bila kujali imani ya mtu, tunatamani tungepata kiongozi ambaye anamcha Mungu. Awe anapenda kuhudhuria ibada. Awe anampenda Mungu ndipo atawapenda watu anaowaongoza,” alisisitiza.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMAPILI, JULAI 27, 2014

older | 1 | .... | 329 | 330 | (Page 331) | 332 | 333 | .... | 1898 | newer