Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

hili nalo ni gogolo lingine la Kitaifa..!

$
0
0
Shule ya Sekondari ya Mount Zion ina jumla ya vyumba 7 vya madarasa ambavyo ilisajiliwa navyo kuhudumia wanafunzi 160, madarasa yakibaki idadi hiyo, wanafunzi wameongezeka na kuwa 515 hali inayosababisha msongamano mkubwa wa wanafunzi darasani kiasi cha madarasa mengine kuwa na wanafunzi hadi 119 nao wanafunzi wengine wakilazimika kutumia ndoo kama viti kutokana na uhaba wa mkubwa wa madawati.PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

TIGO TANZANIA MIONGONI MWA KAMPUNI BORA ZAIDI DUNIANI YENYE MAHUSIANO YA KARIBU NA WATEJA KWENYE KURASA ZA FACEBOOK

$
0
0


Meneja wa Tigo Bw. William Mpinga akielezea jinsi kampuni ya tigo ilivyoshinda nafasi ya nane duniani kwenye kutoa huduma kwa Wateja


TIGO TANZANIA MIONGONI MWA KAMPUNI BORA ZAIDI DUNIANI YENYE MAHUSIANO YA KARIBU NA WATEJA KWENYE KURASA ZA FACEBOOK


Tigo Tanzania imetajwa kuwa miongoni mwa makampuni bora zaidi duniani yenye mahusiano ya karibu na wateja wake kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook. Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika la SocialBokers tarehe 7 February, 2013  ambalo lilifanya utafiti wa makampuni 10 bora zaidi duniani yenye uhusiano wa karibu na wateja kwenye mitandao ya jamii kwenye kipindi cha robo ya mwisho wa mwaka 2012. Tigo Tanzania ndiyo shirika pekee la simu kutoka kanda ya Kati, Mashariki na Kusini mwa bara la Afrika lililofikia viwango hivyo vilivyojumuisha makampuni yote bora duniani.

Mitandao ya kijamii inajitokeza kuwa njia rahisi zaidi kwa wateja mbali mbali kupata taarifa, kuomba misaada na kuelimishwa  kuhusu bidhaa mbalimbali, na makampuni yaliyo na uhusiano bora na wateja wao na yenye uwezo mkubwa yamechukua fursa hii kuboresha  mahusiano na kuwa karibu na wateja wao.  Mitandao hii mikubwa ya kijamii duniani kama vile Facebook, hutoa njia m-badala na iliyo bora kwa mashirika yaliyozidiwa ki-huduma na hivyo kutoa fursa kwa watu wa tamaduni mbali mbali kushirikishana kujadili na kueleweshana.


" Tigo Tanzania imeibuka kuwa namba 8 duniani kote kwenye tafiti hizi kutokana na kujikita vilivyo kwenye kuhakikisha kuwa inatoa huduma bora na za kujitosheleza kwa  wateja wake.Tunathamini sana wateja wetu na tunahakikisha kuwa tuko pamoja nao wakati wote kila wanapotuhijati. Maendeleo ya kiteknolojia na dijitali yamewezesha kuwepo kwa mijadala mingi kila wakati kwenye mitandao ya kijamii. Tigo kama  Kinara wa uvumbuzi wa bidhaa za  mawasiliano inatazama changamoto hii kama fursa ya kujiweka karibu zaidi na wateja na kushirikiana nao kwa ukaribu zaidi. Kila tunachofanya Tigo ni kwa ajili ya wateja wetu, hivyo  kutambuliwa huku ki-dunia ni fahari kubwa sana kwetu" alisema  Ndg. William Mpinga Manager brand ya Tigo.


Kwa mujibu wa shirika la SocialBoker, utafiti wa  mashirika yanayojituma zaidi kijamii kwa kipindi cha mwezi Oktoba na Desemba, 2012, umeonyesha kuwa mashirika  huwajibika na kujibu hoja kutoka kwa wateja wao haraka zaidi kwenye kurasa za Facebook. Hoja iliyokuwa inajibiwa kwa wastani wa   masaa 21 miezi ya nyuma sasa makampuni yanaweza kujibu kwa kipindi cha masaa 19.5 tu kuelekea mwishoni mwa 2012. Shirika la simu la Tigo Tanzania limepata asilimia 87.30% kwa kujibu hoja ndani ya masaa 28.


"Tigo Tanzania mbali ya kujibu hoja za wateja kwenye mitandao ya kijamii inahakikisha kuwa  inafanya hivyo kwa ufanisi zaidi kila wakati. Kwa kuwa mstari wa mbele kwenye kutambua hilo tumefanikiwa kupata heshima hii kubwa. Tutazidi kuongeza ubunifu  ili kuboresha huduma na bidhaa zetu, na tunatambua kwamba, ili kutoa huduma stahili, ushiriki wa wateja wetu ni  nyenzo muhimu sana. Tumepata mafanikio makubwa tuliyonayo na kufika hapa tulipo leo kwa kuupa utoaji wa huduma bora kipaumbele, na kwa heshima hii kubwa, tunaahidi kuwa tutajikita kuhakikisha tunaendelea kutoa ufumbuzi wa mawasiliano uliobora zaidi jambo litakalomfanya kila mteja wetu kutabasamu." alihitimisha Ndg  Diego Gutierrez, Managa wa Tigo.

Socialboker ndilo shirika linaloongoza duniani miongoni mwa mashirika yanayofanya tafiti na kutoa takwimu kuhusu mitandao ya kijamii ya Facebook, Twitter, Google+, LinkedIn na You tube. Kwa njia hii inasaidia makampuni  uwezo wa kampeni za kijamii za makampuni yao. Tafiti za hivi karibuni zinajumuisha taarifa za Desemba 2012 za ‘Global Social Media Report’ ambapo utafiti mkubwa ulifanywa ukihusisha idadi ya kurasa za Facebook na watumiaji wake kidunia katika mataifa ya Marekani, Uingereza na Brazili. Mengine ni Azerbaijan, Serbia, Mexico, Poland na El Salvador- kwa kutaja machache.


Local EU Statement on Religious Intolerance

$
0
0


Local EU Statement on Religious Intolerance.
The European Union Delegation issues the following statement in agreement with the EU Heads of Mission in Tanzania

The EU Delegation condemns all recent acts of violence against religious leaders, and most recently the murder of Fr. Evarist Mushi on Sunday 17 February in Zanzibar. The EU Delegation offers its condolences to their families and all the religious communities who have been affected by recent acts of violence. 

The EU Delegation calls upon the authorities to undertake a full investigation into the killing of the Catholic priest and to continue their investigations into previous attacks on Muslim and Christian leaders and bring those responsible to account.

Freedom of religion or belief is a universal human right which needs to be protected everywhere and for everyone. Religious tolerance and peaceful co-existence have been a hallmark of Tanzanian society. The EU urges religious communities to make every effort to refrain from violence and to keep up the spirit of tolerance and respect of other people's beliefs and to resolve any differences through dialogue.

The EU Delegation calls upon the Government of Tanzania and the Government of Zanzibar and all stakeholders to support a process of open dialogue between Muslim and Christian communities, to take all necessary measures in order to prevent further incidents and to act against those who seek to spark violence, with full respect for
international human rights norms.

The Embassies of Norway and Switzerland associate themselves with this statement. 

In Dar es Salaam on 18 February 2013

tigo yampata MSHINDI WAke wa droo ya SMARTCARD.

$
0
0
Meneja wa Tigo bw. William Mpinga akimkabidhi bw.Julius Raphael Kanza ambaye ni mshindi wa smartcard droo mfano wa tiketi ya kwenda kushuhudia pambano la ligi kuu uhispania kati ya Real Madrid na Fc Barcelona mwezi machi.
====  ====== =====
Kampuni ya Tigo leo imemkabidhi mshindi wa smartcard droo bw. Julius Raphael Kanza Tiketi ya kwenda Uhispania kushuhudia pambano la ligi ya uhispania La Liga kati ya Real Madrid na Fc Barcelona mwezi machi.

Makabidhiano hayo yalifanywa na meneja wa chapa Tigo bw.William Mpinga leo kwenye ofisi za Tigo, ikiwa ni usafiri wa kwenda na kurudi, malazi na chakula vyote bure. Akizungumza bw. Kanza alisema hakutegemea kupata fursa hii ilikuwa ni kama ndoto, kwanza nilidhani ni utapeli kumbe si hivyo nawashukuru sana Tigo kwa kuniwezesha na nawashauri watumiaji waTigo wajiunge na huduma hii ya smartcard nao wabahatike.  Hizi ni droo za kila mwezi ambazo washindi wa zawadi tofauti kupatikana na droo kubwa ndio inamtoa mshindi wa mwaka.

Tuzo ya Wanawake Wenye Mafanikio Tanzania

FIFA YAZUIA UCHAGUZI MKUU TFF

$
0
0

Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limeahirisha uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na mkanganyiko uliojitokeza katika mchakato wa uchaguzi huo.

 Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ofisi za TFF jijini Dar es Salaam leo mchana (Februari 19 mwaka huu), Rais wa TFF, Leodegar Tenga amesema Fifa imetuma barua ikiagiza mchakato wa uchaguzi usimame baada ya kupata malalamiko.

 Amesema kutokana na mkanganyiko huo, Fifa katika barua yake ya leo (Februari 19) imeagiza mkutano wa uchaguzi wa TFF ambao awali ulipangwa kufanyika Februari 24 mwaka huu uahirishwe hadi hapo itakapotuma ujumbe wake nchini. Ujumbe huo wa FIFA unatarajiwa kufika nchini katikati ya mwezi ujao (Machi) ambapo utafanya tathimini ya hali hivyo, kutuma ripoti yake katika shirikisho hilo na baadaye kutoa mwongozo wa nini kifanyike.

Tenga amewaomba radhi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF kwa usumbufu uliojitokeza kutokana na uamuzi huo wa Fifa, hivyo kwa sasa hakutakuwa tena na mkutano huo mpaka hapo watakapopewa taarifa nyingi.

 “Nia yetu ni kuona watu wanatendewa haki, na nia ya Fifa ni kutafuta ukweli. Hivyo wahusika (waathirika) wajiandae, watumie wakati huu kuandaa hoja zao ili Fifa wakifika wawasikilize, wapate maelezo ya kina kuhusu utaratibu na malalamiko yaliyotolewa,” alisema Tenga.

Tenga amesema timu hiyo ya Fifa itakapofika yenyewe ndiyo itakayopanga izungumze na nani kwa wakati gani, hivyo ni vizuri waathirika na vyombo vyote vilivyohusika na mchakato wa uchaguzi wakajiandaa.

“Nataka tubakie kama tulivyokuwa. Malumbano yaishe. Pangeni hoja, wakija hao waheshimiwa (FIFA) muwaambie. FIFA ni chombo cha juu, nafurahi wamekubali kuingia katika hili, kwani wana shughuli nyingi wangeweza kukataa,” amesema.

Kuhusu fursa ya kufanya marejeo (review) kwenye Kamati ya Rufani ya Uchaguzi inayoongozwa na Idd Mtiginjola ambayo aliielezea Jumamosi, Rais Tenga amesema kwa vile hicho ndicho chombo cha mwisho nchini katika masuala ya uchaguzi alishauriwa kuwa kingeweza kufanya review.

“Kwa vile hakuna chombo kingine, nikashauriwa kuwa kinaweza kufanya review. Katika utaratibu wa kutoa haki, uamuzi ni lazima uwe wa wazi kwa kutoa sababu. Nilidhani hilo linawezekana, kwani Mahakama Kuu hufanya hivyo. Kwa hili uamuzi wa Mtiginjola ni sahihi,” amesema Rais Tenga.

Kamati ya Mtiginjola iliyokutana jana (Februari 18 mwaka huu) ilitupa maombi ya review yaliyowasilishwa mbele yake na waombaji uongozi watano kwa vile hakuna kipengele chochote kwenye Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi kinachotoa fursa hiyo. Waombaji hao walikuwa Jamal Emil Malinzi aliyeenguliwa kugombea urais wa TFF na Hamad Yahya aliyeondolewa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania uenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board).

 Wengine ni walioomba kuwania ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF na Kanda zao kwenye mabano; Eliud Peter Mvella (Iringa na Mbeya), Farid Salim Nahdi (Morogoro na Pwani) na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu).

RAIS KIWEKTE AKUTANA NA WANACHAMA WA SIMIYU COMMUNITY BANK LEO IKULU

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na  na ujumbe wa Benki ya Jamii ya Simiyu (Simiyu Community Bank) uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 19, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana  na ujumbe wa Benki ya Jamii ya Simiyu (Simiyu Community Bank) uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 19, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na ujumbe wa Benki ya Jamii ya Simiyu (Simiyu Community Bank) uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 19, 2013 kumwelezea mipango ya kufungua benki hiyo itayoshirikisha jamii katika mkoa huo mpya na ya jirani katika azma ya kumkomboa mjasiriamali na mkulima
mdogo.PICHA NA IKULU.

kumekucha WOMEN CELEBRATIONS 2013

$
0
0
HAYA WANAWAKE TIKETI YA SHUGHULI YETU SASA ZIKO MTAANI NA KWA WALE MLIOKUWA MMEBOOK MEZA, NI NYIE KUSEMA MKO TAYARI ILI TUWEZE KUWALETEA TIKETI ZETU (RESERVED)
NA KAMA UNAHITAJI MEZA YA WATU KUMI 
SHOSTISTO TABLE  300,000/=
PIGA NAMBA
0784 418941 AU 0755  551077 (ULETEWE TIKETI)
KWA TIKETI ZA MOJA MOJA ZITAPATIKANA
SHEAR ILLUSIONS (MLIMANI CITY)
8020 FASHIONS (SINZA MAPAMBANO)
SILVER BOUTIQUE (POSTA AZAM)
VIATUZI (SEA VIEW UPANGA)
ROZELLA FASHIONS (KINONDONI)
MAZNAT BRIDAL SALOON ( MIKOCHENI )
JACKZ COSMETICS( KINONDONI TX MARKET)UTAPATA NA ZAWADI
FABAK FASHIONS (MIKOCHENI KWA WARIOBA) AMAYA BEAUTY SALOON & SPA (POSTA) ANGALIZOTIKETI HAZITOUZWA MLANGONI
                                                                       TIKETI HIZI HAPA

JIPATIE NAKALA YAKO YA KITABU CHA ERIC SHIGONGO

$
0
0
KITABU CHA ERIC SHIGONGO KIITWACHO 'KIFO NI HAKI YANGU' KWA SASA KIPO TAYARI NA KITAANZA KUPATIKANA MACHI 25 2013. JIPATIE NAKALA YAKO! UNAPONUNUA KITABU HIKI UNAKUWA MZALENDO KWA KUMUUNGA MKONO MTUNZI PAMOJA NA NCHI YETU YA TANZANIA.Visit Global Publishers at: http://www.globalpublishers.info/?xg_source=msg_mes_network

WENGI WAMUAGA MAREHEMU GRACE CHAO JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0


Hatimaye Ndugu Jamaa na Marafiki waishio Jijini Dar es Salaam pamoja na Wafanyakazi wenzake na Marehemu Grace Mathew Chao leo wametoa heshima za Mwisho kwa Mwili wa Marehemu Mpendwa wao Grace katika zoezi lililofanyika Katika Hospitali ya Aga Khan Jijini Dar es Salaam ambako mauti yalimkuta Februari 17, 2013. Grace Chao alizaliwa Desemba 13, 1985.

Mwili wa Grace ulisafirishwa kuelekea Mazimbu Mkoani Morogoro ili kuwapa fursa wana jamii ya Mazimbu na Mzumbe ambako marehemu alizaliwa na kuishi zoezi ambalo litafanyika kesho Jumatano kabla ya Msafara kuelekea Marangu kwa mazishi. Ungana na Father Kidevu Blog katika tukio hilo.

 Vijana mbalimbali wa Kundi la Home Sweet Home – Kimzumbe Mzumbe waishio jijini Dar es Salaam kwa shughuli za kazi na masomo walijitokeza kuuaga mwili wa Mwana Mzumbe mwenzao.
 Mama wa Marehemu Grace (kushoto) akiwa na mwana familia mwingine wakati wa zoezi hilo leo.


Ilikuwa ni majonzi sana katika tukio hili, kwa Vijana mbalimbali wa Kundi la Home Sweet Home – Kimzumbe Mzumbe waishio jijini Dar es Salaam walijitokeza kuuaga mwili wa Mwana Mzumbe mwenzao.

 Wafanyakazi wa CRDB Bank waliita kutoa heshima kwa Mwili wa Mfanyakazi mwenzao.


 Vijana wa Mzumbe Wengi sana walijitokeza kumuaga Grace katika safari yake hiyo ya Mwisho.
Marafiki na vijana wa Mzumbe wakimfariji kaka wa Marehemu Edwin Ndesamburo Chao (kulia) kufuatia msiba wa dada yake.

kaazi kweli kweli..!

$
0
0

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Joyce Ndalichako akionesha karatasi ya majibu ya mmoja wa watahiniwa wa mtihani wa kidato cha nne wa mwaka 2012, Dar es Salaam jana. Picha na Edwin Mjwahuzi.

wanachama wapya CCM tawi la Napoli 2013

$
0
0
 Mwenyekiti wa tawi la Napoli ndugu Abdulrahamani A.Alli amewatangazia  wote waliojaza fomu za kujiunga na Chama cha Mapinduzi tawi la Napoli kuwa watafahamishwa baada ya kikao cha Halmashauri kuu ya tawi. Kagutta N.M
 Mwenyekiti akitoa maelezo mafupi kwa mwanachama mpya wa CCM wakati wa kukabidhi kadi ya uanachama

Mwenyekiti wa tawi la Chama Cha Mapinduzi ndugu Abdulrahamani A.Alli  akiwa na Katibu uenezi na Siasa wa tawi wakati wa kumuapisha mwanachama mpya wa CCM.

kinywaji cha kiasili cha Nzagamba chazinduliwa jijini Mwanza

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng.Evarist Ndfikilo Kulia alipo tembelea kiwanda hicho katikati .

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng.Evalist Ndikiro akiwasili katika  kiwanda cha kinywaji aina ya Nzagamba jijini Mwanza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng.Evalist Ndikiro akitembelea kiwanda cha kinywaji aina ya Nzagamba wa pili Kushoto ni Kilowi Suma Mkurugenzi wa tatu ni Nyamoronga John Meneja uzalishaji wa nne ni Ashraf Gugu meneja mauzo .
Kushoto ni Mkurugenzi wa kinywaji cha Nzagabwa Kiroi Suma akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng.Evarist Ndfikilo Kulia alipo tembelea kiwanda hicho katikati ni Mkuu wa kiwanda cha Nzagamba Bw.Patrick Phiri
Meneja masoko wa kampuni ya Bia nchini TBL Fimbo Butallah akishiriki kushika nyoka kwenye burudani ya uzinduzi wa kiwanda kipya cha bia ya Asili cha NZAGAMBA kilichopo mkoani Mwanza ambapo uzinduzi huo ulifanywa na mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo
Kikundi cha Burudani cha Bia ya Asili cha NZAGAMBA kilichopo mkoani Mwanza kikitoa burudani ya kipekeekwenye uzinduzi wa kiwanda kipya cha kutengeneza Bia ya Asli ambapo uzinduzi huo ulifanywa na mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo

===== ====== ===== ====

Na Mwandishi Wetu 

KIWANDA kipya cha kuzalisha bia ya asili ijulikanayo Nzagamba kimefunguliwa rasmi jana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evaristi Ndikilo. Kiwanda hicho ambacho kipo chini ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kitajihusisha na kutengeneza bia hiyo ya asili, ambayo tayari imeanza kupokelewa kwa shangwe na wenyeji wa Kanda ya Ziwa. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho, Mhandisi Ndikilo alisema, amefarijika mno kuona kimejengwa Mwanza, kwani kitachangia kwa kiasi kikubwa mapato ya mkoa huo.

 “Niwapongeze sana wenzetu wa Nzagamba kwa kuja na wazo zuri kama hili la kuanzisha bia ya asili, tena wakaipa jina lenye asili ya Kanda ya Ziwa hususani kabila la Wasukuma. 

 “Hii imenifurahisha. Lakini kikubwa zaidi ni uamuzi wa kukiweka kiwanda hiki hapa Mwanza, kwa sababu mlikuwa na uwezo wakuamua kujenga mkoa mwingine wowote ule lakini mkatoa upendeleo wa dhati kwa mkoa wetu. Kwa uamuzi huo tunashukuru sana,” alisema. 

 Aliwataka wananchi kuhakikisha wanaonyesha uzalendo wa dhati kwa kupenda kutumia vitu vya asili, huku akitolea mifano ya nchi za Zambia na Malawi, ambapo bia za asili zinapewa nafasi kubwa. 

 Mkurugenzi wa Kiwanda cha Nzagamba, Kirowi Suma naye alisema watahakikisha wanazalisha bidhaa bora zaidi na kuwataka Watanzania wapende vitu vya asili ili kuonyesha uzalendo wao. 

 “Kwetu Nzagamba tunaamini tutaendelea kupigania ubora wa bidhaa yetu na naomba Watanzania watuunge mkono kwa kuipa nafasi bia hii ya asili,” alisema Suma. Nzagamba tayari imeanza kusambazwa, huku ikipokelewa vizuri zaidi na watumiaji, kutokana na kuwekwa katika ubora unaotakiwa.

ALBINUS KUGOMBEA UBINGWA WA DUNIA WA IBF KWA VIJANA

$
0
0

Bondia kijana na anayeinukia kwa kasi Albinu Felesianu wa nchi ya Namibia amepewa ofa ya kugombea ubingwa wa dunia wa Featherweight kwa vijana walio chini ya miaka 25 unaotambuliwa na IBF. 
Albinus amezoea kupewa zawadi za Christmas na siku kuu yake ya kuzaliwa lakini hamna kilichomwandaa na mshtuko mkubwa ambao aliupata wakati IBF ilipotangaza hivi karibuni kuwa imempatia nafasi ya kugombea mkanda wa dunia kwa vijana walio chini ya miaka 25.
 Mtua ambaye anaweza kuiua furaha yake ni mmoja wa watoto wa Nkrumah, Mghana Ishmael Ayeetey ambaye amekulia katika moja ya viunga vinavyosifika kwa kutoa mabingwa wa ngumi wa dunia kama kina Azumah Nelson, Joseph Agbeko na Ike Quartey. 
Albinus Felesianu
Albinus Felesianu kulia akimrushia ngumi mpinzani wake kushoto

Mpambano huo utafanyika katika jiji la Windhoek nchini Namibia tarehe 29 March chini ya kampuni ya Kinda Boxing promotions ya bwana Kinda Nangolo!
 Hili litakuwa pambano la pili la ubingwa wa dunia kwa vijana baada ya bondia Ilunga Makabu wa Jamhuri ya Watu wa Kongo (DRC) kumtwanga bondia Gogito Gorgiladze wa Georgia jijini Johannesburg nchini Afrika ya Kusini jumamosi iliyopita.

ISSUED BY:

INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA

Dar yaibuka kidedea Tamasha la Pasaka

$
0
0

MKOA wa Dar es Salaam umeshinda katika mchakato wa kuchagua mkoa wa kwanza ambao Tamasha la Pasaka mwaka huu litaendeshwa.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema kamati yake ilikuwa ikiendesha kura za maoni kwa mashabiki wao wa eneo lipi tamasha hilo lifanyike.

“Tulifanya kura za maoni kwa njia ya simu za mkononi, pia tulikuwa na vipindi maalum kwenye baadhi  ya redio kwa mashabiki kutoa maoni yao. “Mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya, Dodoma na Mwanza ilikuwa ikichuana vikali katika kupata mahali ambapo tamasha litafanyika, maana tulikuwa bado hatujatangaza.

“Lakini leo (jana) tumechagua Dar es Salaam, ambapo zaidi ya mashabiki 15,000 walichagua tamasha lifanyike Dar es Salaam, mashabiki 13,000 walitaka lifanyike Mbeya, mashabiki 7,000 walitaka Mwanza na mashabiki 3,000 walitaka Dodoma,” alisema Msama.

Alieleza kuwa hivi sasa wanatazama mkoa upi lifanyike Jumatatu ya Pasaka na siku zingine zitakazofuata. “Siku yenyewe ya pasaka tushapata kwamba ni Dar es Salaam, sasa tunajipanga kwa siku zingine maana mwaka huu tunataka mikoa saba tufanye tamasha letu,” alisema Msama na kuongeza kuwa kwa Dar es Salaam litakuwa Machi 31 mwaka huu.

Pichani kati ni sehemu ya picha ya Mwanamuziki mahiri wa nyimbo za kiroho kutoka nchini Afrika Kusini,Rebecca Malope akiwa amemshika mwimbaji mwenzake kutoka nchini Tanzania,Rose Muhando,wakati wa Tamasha la pasaka lililofanyika kwenye Uwanja wa Taifa,Mwaka jana.

Pia alisema bado wanaendelea na mazungumzo na wasanii mbalimbali  kwa ajili ya kushiriki tamasha la mwaka huu. Baadhi ya wasanii walioshiriki tamasha la mwaka jana ni Rose Muhando,Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava, Ephraim Sekeleti na kundi la Glorious Celebration.

Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilikuwa miongoni mwa burudani zilizokuwepo siku hiyo.


Rais wa zanzibar Dkt.shein atoa salamu za Mwisho kwa Padri Mushi

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akitoa salamu ya Mwisho kwa mwili wa Marehemu Padri Evarest Mushi,katika Kanisa la Minaramiwili Mjini Zanzibar, Padri Gabriel Mushi,aliyefariki kwa kupigwa risasi na watu wasijuilikanwa Jumapili iliyopita,na atazikwa leo Kijini Kitope Wilaya ya Kaskazini B Unguja,(katikati) Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar Augustino Shao.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein,akitia saini kitabu cha maombolezi ya Padri Evarist Gabriel Mushi,katika Kanisa la Minaramiwili MjiniZanzibar,ambapo alifika kutoa salamu ya mwisho kwa Padri huyo,aliyefariki kwa kupigwa risasi na watu wasijuilikanwa Jumapili iliyopita,na atazikwa leo Kijini Kitope Wilaya ya Kaskazini BUnguja,(kushoto)  Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar Augustino Shao.
Baadhi ya Waombolezaji wakiwa ndani ya Kanisa la Minaramiwili Mjini Zanzibar wakati wa kutoa salamu ya Mwisho kwa Padri Evarist Gabriel Mushi,aliyefariki kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana Jumapili iliyopita,na atazikwa leo Kijijini Kitope Wilaya ya Kaskazini B Unguja.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar Augustino Shao wakati alipofika katika Kanisa la Minaramiwili Mjini Zanzibar kutoa salamu ya Mwisho kwa Padri Evarist Gabriel  Mushi,aliyefariki kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana Jumapili iliyopita,na atazikwa leo Kijijini Kitope Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein,akiwasalimia wananchi wakati alipofika katika Kanisa la Minaramiwili Mjini Zanzibar kutoa salamu ya Mwishokwa Padri Evarist Gabriel Mushi,aliyefariki kwa kupigwa risasi na watu wasijuilikanwa Jumapili iliyopita,na atazikwa leo Kijini Kitope Wilaya ya Kaskazini B Unguja.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]

President Kikwete meets USAID administrator Dr.Rajiv Shah at Dar es Salaam State House

$
0
0
  President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete welcomes to the State House the USAID Administrator Dr.Rajiv Shah this morning. 
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with the USAID administrator Dr.Rajiv Shah at State House Dar es Salaam this morning.(photos by Freddy Maro)

habari za zilizowashtua wengi hivi karibuni.

Mablogger acheni uvivu na mjitume msisubiri kukopi na kupaste tu

$
0
0

Uongozi wa mtandao huu umesikitishwa na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wamiliki wa blogs, kuwa wakiiba kazi za watu katika blogs mbalimbali yaani ‘Kukopi na Kupaste’ kutoka katika blog Fulani na kuweka katika Blogs zao bila kujali haki miliki ya kazi ya mtu, wala kumpa haki yule aliyechukuliwa kazi yake kwa kuandika mahala ulipochukua kazi hiyo.


Kama inavyojulikana utafutaji wa habari si lelemama na ikumbukwe ili kupata habari iliyo bora na itakayowafurahisha wasomaji wako, kwenda na wakati ni lazima uihangaikie na katika kuihangaikia kuna gharama kibao zinazotumika, ikiwa ni pamoja na usafiri, pesa, na hata mafuta ya gari kutoka mahala Fulani kwenda sehemu nyingine, gharama za simu na hata kuwalipa wale unaowatuma ili kukufanyia kazi hiyo.


Kama umeweza kufanya mambo yote hayo kwa gharama unazozijua wewe uliyeweka stori, ama picha katika Blog yako, halafu watu wenye Blog Fulani wasio na uwezo wa kufanya kazi na kuchukua kazi yako kana kwamba ameokota tu jalalani na anaweka kwake ili wasomaji wake wasome, bila kuwajulisha kuwa kazi hiyo iliyomvutia imefanywa na mtandao Fulani kwa kweli inaumiza, inaudhi na inarudisha nyuma malengo hasa ya kuwa na mitandao hii, wote tutajaonekana wapuuzi.


Mtandao huu umewavumilia watu hawa kiasi cha kutosha lakini sasa imezidi kukithiri, kwani jamaa hawa wapo katika ukurasa wako kukusubiri kuona tu ulichoweka kwa wakati huo, ili wao wakopi na kupaste kwao, halafu tayari wamemaliza wala hawataki kujihangaisha kufanya kazi ili kuboresha mitandao yao na kuwavutia wasomaji wao.


‘Unapoamua kutangaza vita ujue tayari umeshajipanga kukabiliana na kila litakalotokea mbele yako, na pia umejipanga katika kutoka upinzani wa kweli ili watu waone na wakutambue, lakini sio kwa staili hii ya kuomba mtangaziwe blog zenu kupitia kwa wale walioanza mapema halafu kumbe kazi yenyewe ni kuchukua kazi za watu tu na si kufanya kazi’ yaani kukopi na kupaste,


Kuna msanii mmoja alichoshwa na wenzake wanaotamani kuingia kwenye gemu, lakini wanashindwa kuumiza vichwa kubuni ili kuweza kupata radha tofauti, na kuamua kuwafikishia ujumbe kwa kuwaimba kuwa ‘Si lazima wote tuimbe kuna michezo mingi hata kucheza bao kama huwezi kuimba, ikiwa kila wimbo unaotoka mpya umekopiwa, kama si mashahiri, basi ni Beat,


Na hata katika mablogger si lazima wote tuwe na Mablogger, kama huwezi kuumiza kichwa utoke vipi, basi kaa pembeni waachie wenye uwezo wa kufanya kazi hiyo, kukopi na kupaste hadi mitandao yote inakuwa sawa nini maana ya habari za haraka mtandaoni?,


Huoni kuwa mnawachosha wasomaji wenu, kwa kosoma habari na picha zinazofafa kwa wakati mmoja na katika mitandao yote?,


Tena msomaji wako wakiwa ni waelewa hawawezi kusoma tena mtandao wako kwani habari kama hiyo hiyo walikwishaiona katika mtandao Fulani muda mchache uliopita na dakika chache baadaye wanaikuta vile vile walivyoisoma kwingine ikiwa katika ukurasa wako, mara moja mara mbili msomaji huyo si umempoteza?’’.


Mablogger acheni uvivu na mjitume msisubiri kukopi na kupaste tu, na kama ukifanya hivyo basi jitahidi kumpa credit yule uliyemchukulia kazi yake.


VITU muhimu vy kuwa navyo ili kufanikisha kazi yako ya Blog, ni Laptop ‘Kompyuta mpakato’, ama Desk Top, Modem ‘Internet Wireless’, Kamera hata ndogo tu ya mkononi, na pia ujue maana ya kuanzisha hiyoBlog yako na malengo yako kwa jamii, kwani sidhani kama unaweza kuanzisha blog ili uwe ukisoma mwenyewe na naniliu wako tu.


Na kuwa na kamera si bora tu kuwa kamera pia ujue kuitumia ipasavyo ili kunasa picha nzuri uitakayo na itakayofikisha ujumbe kwa wasomaji wako hata kwa kuiangalia tu, kwa kile ulichokusudia kuwaarifu wasomaji wako.


Baadhi ya Blogs zenye tabia ya kukopi na kupaste orodha yake tayari tunayo na baada ya tangazo hili, zikiendelea tutaziweka hewani ili wasomaji wajue ni Blog ipi ya kweli na ipi ni mamluki.

MARY MWANJELWA atoa msaada wa mifuko ya saruji tani moja kuhamasisha ujenzi wa shule ya sekondari ya kata jijini mbeya

$
0
0

DR.MARY MWANJELWA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA AMBAYE PIA NI M-NEC TAIFA AMETOA ZAIDI YA TANI MOJA YA MIFUKO YA SARUJI NA KUHAMASISISHA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI KATA YA ITAGANO JIJINI MBEYA




DR.MARY MWANJELWA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA AMBAYE PIA NI M-NEC TAIFA AKIWEKA TOFARI KUHAMASISHA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI ITAGANO .
HAPA MWESHIMIWA DR. MARYA MWANJELWA AKIENDELEA NA UJENZI WA KUPANDISHA UKUTA WA DARASA MOJA

DR.MARY MWANJELWA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA AMBAYE PIA NI M-NEC TAIFA  AKIMKABIDHI MIFUKO YA SARUJI ZAIDI YA TANI MOJA MWESHIMIWA DIWANI KATA YA ITAGANO MBWIGA NDALAMA KWA AJILI YA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI ITAGANO
NAE MWESHIMIWA DIWANI WA KATA YA ITAGANO MBWIGA NDALAMA AKIMSHUKURU MWESHIMIWA MBUNGE DR.MARY MWANJELWA KWA KUTOA MSAADA HUO NA PIA KUWAHAMASISHA KATIKA UJENZI WA SHULE HIYO YA SEKONDARI ITAGANO DIWANI HUYO AMESEMA KUWA SHULE HIYO ITAKAPOKAMILIKA ITASAIDIA HATA WATOTO WA VIJIJI JIRANI NA KATA HIYO KUAPATA ELIMU YA SEKONDARI  PIA WAMEMWAHIDI MWESHIMIWA MBUGE KUWA MADARASA MATATU MPAKA KUFIKIA MWEZI WA SITA YATAKUWA YAMEKAMILIKA NA TAYARI KWA KUTUMIWA
HAPA MWESHIMIWA MBUNGE AKIPATA MAELEZO TOKA KWA MWESHIMIWA DIWANI WA KATA YA ITAGANO JINSI UJENZI WA MADARASA HAYO UTAKAVYOKAMILIKA MAPEMA MARA BAADA YA KUKABIDHIWA SARUJI.PICHA ZOTE KWA HISANI YA MBEYA YETU BLOG.
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images