Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

MACHOZI KISIMANI SHORT FILM -FILMED BY IN FOCUS FILMS


INTRODUCING NEW SONG-MY SHITOBE BY Y-TOWN.

MTOTO ANATAFUTWA NA WAZAZI WAKE

$
0
0
Mimi Reppyson Ishababaki na mke wangu Elida Fundi. Tunapenda kutoa taarifa ya kupotea kwa mtoto wetu kipenzi Meryline Reppyson. Ameibiwa jana jioni na mtu tusiyemfahamu na hatujampata mpaka sasa hivi.

 Tunawaomba Watanzania na watu wote mtusaidie kumtafuta mtoto wetu. Maneno yanayosemwa kwamba kachukuliwa na baba yake si ya kweli kwani mimi ndiye baba yake mzazi na tunaishi pamoja na mke wangu. 

Asanteni sana kwa msaada wenu na Mungu awabariki.

UFUNGUZI WA MAONESHO YA ZANA ZA KIJESHI ZA NCHI KAVU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk. Hussein Mwinyi akihutubia wakati alipokuwa akiyafungua maonesho ya zana za kivita za nchi kavu ya Afrika Mashariki 2014, Mlimani City, Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davies Mwamunyange.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk. Hussein Mwinyi (katikati), akipiga picha ya pamoja na baadhi ya wakuu na viongozi wa majeshi ya Afrika Mashariki, mara baada ya kuyafungua maonesho ya zana za kivita za nchi kavu ya Afrika Mashariki 2014, Mlimani City, jijini Dar es Salaam leo. Watatu kulia ni Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davies Mwamunyange.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk. Hussein Mwinyi (katikati), akipiga picha ya pamoja na baadhi ya wakuu na viongozi wa majeshi ya Afrika Mashariki pamoja na baadhi ya Maofisa wa Kijeshi wa nchi mbalimbali za nje, walioshiriki katika maonesho hayo, mara baada ya kuyafungua, Mlimani City, jijini Dar es Salaam leo. Watatu kulia ni Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davies Mwamunyange.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk. Hussein Mwinyi (katikati), akipiga picha ya pamoja na baadhi ya wakuu na viongozi wa majeshi ya Afrika Mashariki pamoja na baadhi ya Maofisa wa Kijeshi wa nchi mbalimbali za nje na Kampuni zinazotengeneza zana na silaha za kivita, walioshiriki katika maonesho hayo, mara baada ya kuyafungua, Mlimani City, jijini Dar es Salaam leo. Watatu kulia ni Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davies Mwamunyange.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk. Hussein Mwinyi akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya zana za kivita za nchi kavu ya Afrika Mashariki 2014, Mlimani City, Dar es Salaam leo.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk. Hussein Mwinyi akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya hayo, Mlimani City, Dar es Salaam leo.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk. Hussein Mwinyi akitembelea banda la Afrika Kusini mara baada ya kuyafungua maonesho ya zana za kivita za nchi kavu ya Afrika Mashariki 2014, Mlimani City, Dar es Salaam leo.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk. Hussein Mwinyi akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa viongozi wa banda la Afrika Kusini mara baada ya kuyafungua maonesho ya zana za kivita za nchi kavu ya Afrika Mashariki 2014, Mlimani City, Dar es Salaam leo.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk. Hussein Mwinyi akioneshwa zawadi ambayo alikabidhiwa kwenye banda hilo la Afrika Kusini.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk. Hussein Mwinyi akipatiwa maelezo na Meneja Mkuu wa Masoko na Ukuzaji Biashara wa Kampuni ya ARMSCOR, Lulu Mzili, watengenezaji wa zana za kijeshi ya Afrika Kusini.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, akiangalia kifaru kilichotengenezwa na Kiwanda cha Nyumbu cha Tanzania. Kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda hicho, Kanali John Nchimbi.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, akiangalia gari la Kijeshi lililotengenezwa na Kiwanda cha Nyumbu cha Tanzania. Kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda hicho, Kanali John Nchimbi.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha kutengeneza zana za Kijeshi cha Nyumbu cha Tanzania, Kanali John Nchimbi, alipokuwa akiangalia zana mbalimbali za Kijeshi, mara baada ya kuyafungua maonesho ya zana za kivita za nchi kavu ya Afrika Mashariki 2014, Mlimani City, Dar es Salaam leo.
Katibu Msaidizi wa Ubalozi wa Uturuki nchini, Berat Colak (kulia), akisalimiana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi.
Katibu Msaidizi wa Ubalozi wa Uturuki nchini, Berat Colak (kulia), akiwaleza jambo Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi (katikati) na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davies Mwamunyange (kushoto), wakati waziri alipokuwa akiangalia zana za Kijeshi, zilizotengenezwa na Kiwanda cha Nyumbu cha Tanzania.
Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davies Mwamunyange (kushoto), akimweleza jambo Katibu Msaidizi wa Ubalozi wa Uturuki nchini, Berat Colak (kulia), wakati alipokuwa akizungumza na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi (katikati), wakati waziri alipokuwa akiangalia zana za Kijeshi, zilizotengenezwa na Kiwanda cha Nyumbu cha Tanzania.

Kikosi cha Bendi cha Jeshi la Wananchi (JWTZ), kikitumbuiza katika maonesho hayo.
Kifaru cha Tanzania, kilichotengenezwa na Kampuni ya Nyumbu inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kikiwa kwenye maonesho hayo.

Serikali yapokea msaada wa Dola za Kimarekani elfu 93 kusaidia Timu za Taifa zinazoshiriki mashindano ya Jumiya ya Madola

$
0
0
 Kulia Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Juma Suleiman Nkamia akipeana mkono na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Bakhresa Group Said Muhammad Said Abeid mara baada ya kumkabithi Hundi yenye thamani ya Dola za Kimarekani 93,000 kutoka kwa Kampuni ya Bakhresa Group kwa ajili ya kusaidi timu za wanamichezo wanaoshiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola jijini Glasgow Scotland.Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Habari leo  jijini Dar es Salaam .
 Kutoka kulia Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Juma Suleiman Nkami,Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel, Meneja Chapa wa Kampuni ya Bakhresa Group, Katibu wa Naibu Waziri Bw. Francis Songoro na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Bakhresa Bw.Said Muhammad Said Abeid wakifurahia mara baada ya makabidhiano ya hudi yenye thamani ya Dola za Kimarekani 93,000/= ikiwa ni msaada wa kampuni hiyo kwa wanamichezo wanaoshiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola nchini Scotland.
 Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Juma Suleiman Nkamia akizunguza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kupokea msaada wa Hundi yenye thamani ya Dollar za Kimarekani 93,000 kutoka kwa Kampuni ya Bakhresa Group kwa ajili ya kusaidi timu za wanamichezo wanaoshiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola jijini Glasgow Scotland jijini Dar es Salaam leo, katikiti ni Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo Said Muhammad Said Abeid na Meneja Chapa wa Kampuni hiyo Bw. Abubaker S.A.

Baadhi ya waandishi wa habari wakishuhudia makabidhiano ya hundi ya mfano kutoka kwa wawakilishi wa Bakhresa Group katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo leo jijini Dar es Salaam.Kampuni hiyo imetoa msaada wa Dola za Kimarekani 93,000 ili kusaidia timu za wanamichezo wanaoshiriki Mashindano ya Jumuiya ya Madola yanayotaraji kuanza rasmi tarehe 23 mwezi huu huko mjini Glasgow Scotland.

Picha na Frank Shija
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini., WHVUM

RAIS KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM LEO

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM jijini Dar es salaam leo. PICHA NA IKULU

KITABU CHA "HISTORIA YA KLABU YA SIMBA"KILICHOANDIKWA NA MWINA KADUGUDA CHAZINDULIWA RASMI LEO

$
0
0
 Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia Akijiandaa kukata utepe ili kuweza kuzindua rasmi kitabu hicho cha historia ya Simba,Wanaoshuhudia kulia ni mtunzi wa kitabu hicho Mwina Kaduguda akifuatiwa na Bwana Mkuki Bgoya mkurugenzi wa Mkuki na Nyota Ambao ndio wachapishaji wa kitabu hicho.
 Mwina Kaduguda Mtunzi wa kitabu cha "HISTORIA YA SIMBA" akielezea kwa kina Magumu gani amepitia wakati anaanza kuandaa kitabu hicho,Wa kwanza Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia na Katikati ni Mkurugenzi wa Mkuki na Nyota Bwana Mkuki Bgoya ambao ndio wachapishaji wa kitabu hicho.Akielezea kwa ufupi Mwina Kaduguda amesema kwamba Dhumuni kubwa la Kutunga kitabu hicho ni kutaka kutunza historia ya soka ya Timu hiyo isipoteee ili iweze kusomwa kizazi na kizazi.

Mkurugenzi wa Mkuki na Nyota Bwana Mkuki Bgoya  Akielezea namna walivyochapa kitabu hicho na ubora wake .
 Mjumbe wa kamati ya Utendaji Klabu ya Simba Bwana Collin Frisch akiongea kwa niaba ya Rais wa Simba,ambapo amempongeza sana Mwina Kaduguda na kusema ameiweka Klabu ya Simba kwenye Kumbukumbu muhimu sana kwenye soka la Tanzania hivyo inatakiwa aungwe mkono kwa nguvu zote.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia akitoa neno kumpongeza Mwina Kaduguda  kwa kufikiria mbali sana kwa kuweka soka la Tanzania kwenye maandishi namna klabu ya simba ilivyoanza,Akaongeza kuwa Klabu za soka Tanzania zinatakiwa kuwa na watu kama Mwina Kaduguda ili kuleta maendeleo ya soka.Naibu waziri pia akasisitiza ni wakati wa kila mwanachama kujituma kwa bidii na kuacha kukaaa kwenye korido za Klabu na kupiga Zoga.
Mwina kaduguda Mtunzi wa Kitabu cha "HISTORIA YA SIMBA" Akimkabidhi  Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia Zawadi ya Kitabu ambayo ameomba apelekewe Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

MATOKEO YA KIDATO CHA SITA YATANGAZWA, KUONA BOFYA LINK HAPO CHINI


RAIS KIKWETE AANDAA FUTARI KWA VIONGOZI WA DINI YA KIISLAMU IKULU, DAR ES SALAAM

$
0
0

Kadhi Mkuu wa Tanzania Sheikh Abdullah Yusuf bin Ali bin Yusuf ash-Shirazi Mnyasi (mwenye kipaaza sauti) akiongoza dua katika futari aliyoandaa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa viongozi wa madhehebu mbalimbali wa dini ya Kiislamu Ikulu jijini Dar es salaam jioni ya Julai 16, 2014
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum (aliyesimama kushoto), akitoa neno la Shukurani baada ya futari aliyoandaa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa viongozi wa madhehebu mbalimbali wa dini ya Kiislamu Ikulu jijini Dar es salaam jioni ya Julai 16, 2014
Jk4: Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwashukuru viongozi wa madhehebu mbalimbali wa dini ya Kiislamu kwa kuhudhuria katika furari aliyowaandalia kulu jijini Dar es salaam jioni ya Julai 16, 2014
Sehemu ya waliohudhuria katika futari aliyoandaa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa viongozi wa madhehebu mbalimbali wa dini ya Kiislamu Ikulu jijini Dar es salaam jioni ya Julai 16, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiungana na viongozi wa madhehebu mbalimbali wa dini ya Kiislamu katika furari aliyowaandalia kulu jijini Dar es salaam jioni ya Julai 16, 2014.
PICHA NA IKULU

THT YAANDAA HAFLA YA KUMUAGA MSANII LINAH,AZINDUA VIDEO MPYA MBELE YA MASUPASTAA KIBAO JIJINI DAR

$
0
0
  Mkurugenzi wa Tanzania House Of Talent (THT) Ruge Mutahaba akifafanua jambo mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo  wanahabari,wadau na wasanii wa filamu na muziki,katika hafla ya kumuaga msanii Linah jana Julai 16, 2014 kutoka kwao na kuelekea kampuni ya No Fake Zone (NFZ) ambao ndiyo wanaanza kumsimamia msanii huyo pamoja na kazi zake.Linah pia alizindua video yake mpya chini ya kampuni NFZ iitwayo OLe Themba.
MKurugenzi wa Kampuni ya NO FAKE ZONE,Abby akizungumza jambo mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo wanahabari,wadau na wasanii wa filamu na muziki,katika hafla ya kumuaga msanii Linah jana Julai 16, 2014  ambaye anahamia hiyo,itakayokuwa ikisimamia kazi zake za msanii huyo.Linah pia alizindua video yake mpya chini ya kampuni NFZ iitwayo OLe Themba.
Msanii Linah akizungumza na kutoa shukurani mbalimbali kwa wadau wa muziki walioshiriki kwa namna moja ama nyingine kumpa sapoti katika anga ya muziki wa kizazi kipya.
 Mkurugenzi wa Tanzania House Of Talent (THT) Ruge Mutahaba akimkabidhi cheti cha heshima msanii wa kizazi kipya,Mwasiti kwa kuwa msanii mwenye nidhamu kubwa kutoka chuo cha kipaji cha THT kwa muda mrefu.
Wasanii na Wadau wa muziki wakifuatilia uzinduzi wa video mpya ya Msanii Linah 
Wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi wa vido mya ya Linah iitwayo OLe Themba
Msanii Linah akiwa amepozi kwenye bango lake linaloelezea ujio wa video yake mpya ya Ole Themba pamoja na jina la kampuni anayohamia
Wadau wa Muziki sambambana Wanamuziki walikuwepo kushuhudia tukio hilo likiwemo la uzinduZi wa video mpya ya msanii Linah
Baadhi ya wanahabari waliokuwa wakirekodi tukio hilo adhimu .

FAIDIKA yawezesha wajasiriamali baada ya mafunzo ya biashara

$
0
0
 Mkurugenzi wa viwanda vidogo na biashara ndogo ndogo na za kati kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Consolata Ishebabiakizungumuza na wajasiriamali kutoka mikoa ya Mbeya, Arusha na Dar es Salaam waliopata mafunzo juu ya uendeshaji biashara, kabla ya kupata fedha kwa ajili ya mitaji kutoka taasisi ya kifedha ya FAIDIKA. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa FAIDIKA Marion Moore na kulia ni Mwalimu wa wajasiriamali Bi. MariamTambwe.
 Mkurugenzi wa viwanda vidogo na biashara ndogo ndogo na za kati kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Consolata Ishebabiakimkabidhi zawadi Bi. Joan Kitembe kutoka Mkoa wa Arusha, baada ya kuibuka mshindi wa kanza kimkoa katika mashindano ya kuandika mchanganuo wa biashara ulioandaliwa na taasisi ya kifedha ya FAIDIKA. Wapili kushato ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa FAIDIKA Marion Moore na kulia ni Mwalimu wa wajasiriamali Bi. MariamTambwe.
 Mkurugenzi wa viwanda vidogo na biashara ndogo ndogo na za kati kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Consolata Ishebabiakimkabidhi zawadi Bi. Bahati Bukubilo kutoka Mbeya, baada ya kuibuka mshindi wa kanza kimkoa katika mashindano ya kuandika mchanganuo wa biashara ulioandaliwa na taasisi ya kifedha ya FAIDIKA. Wapili kushato ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa FAIDIKA Marion Moore na kulia ni Mwalimu wa wajasiriamali Bi. MariamTambwe.
 Mkurugenzi wa viwanda vidogo na biashara ndogo ndogo na za kati kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Consolata Ishebabiakimkabidhi zawadi Bw. Linus Mwangoya kutoka Mbeya, baada ya kuibuka mshindi wa pili kimkoa katika mashindano ya kuandika mchanganuo wa biashara ulioandaliwa na taasisi ya kifedha ya FAIDIKA. Wapili kushato ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa FAIDIKA Marion Moore na kulia ni Mwalimu wa wajasiriamali Bi. MariamTambwe.
 Mkurugenzi wa viwanda vidogo na biashara ndogo ndogo na za kati kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Consolata Ishebabiakimkabidhi zawadi Bw. Bakari Khamisi kutoka Mbeya, baada ya kuibuka mshindi wa tatu kimkoa katika mashindano ya kuandika mchanganuo wa biashara ulioandaliwa na taasisi ya kifedha ya FAIDIKA. Wapili kushato ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa FAIDIKA Marion Moore na kulia ni Mwalimu wa wajasiriamali Bi. MariamTambwe.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa FAIDIKA Marion Moore (wa nane kulia kwa waliosimama) pamoja na Mkurugenzi wa viwanda vidogo na biashara ndogo ndogo na za kati kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Consolata Ishebabi (kushoto kwa Marion) wakiwa katika picha ya pamoja na wajasiriamali kutoka mikoa ya Mbeya, Arusha na Dar es Salaam waliopata mafunzo juu ya uendeshaji biashara, kabla ya kupata fedha kwa ajili ya mitaji kutoka taasisi ya kifedha ya FAIDIKA.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa FAIDIKA Marion Moore akizungumuza na wajasiriamali kutoka mikoa ya Mbeya, Arusha na Dar es Salaam waliopata mafunzo juu ya uendeshaji biashara, kabla ya kupata fedha kwa ajili ya mitaji kutoka taasisi ya kifedha ya FAIDIKA. Kushoto ni Mkurugenzi wa viwanda vidogo na biashara ndogo ndogo na za kati kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Consolata Ishebabi na kulia ni Mwalimu wa wajasiriamali Bi. MariamTambwe


Taasisi ya kifedha ya FAIDIKA, inayoshughulika na utoaji mikopo hapa nchini, imewawezesha wajasiriamali kutoka mikoa ya Mbeya, Arusha na Dar es Salaam baada ya kuwapa mafunzo ya njia bora ya ufanyaji biashara. 

Wajasiriamali hao ni miongoni mwa wale 300 waliopata mafunzo na baadae kuingizwa katika mashindano ya kuandika mchanganuo wa biashara, kisha kuwapata washindi watatu katika kila mkoa. 

Akizungumuzia mashindano hayo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa FAIDIKA Marion Moore alisema washindi watano katika kila mkoa walipatikana baada ya kuwasilisha maandiko ya mchanganuo wa biashara ambazo zilionekana kukidhi vigezo vilivyowekwa na walimu wa wajasiriamali hao.

“Leo FAIDIKA inatimiza ahadi yake ya kuwapa wajasiriamali ambao michanganuo yao ya biashara imeonekana kuwa bora zaidi. Katika kila mkoa, mshindi wa kwanza amepata Tsh milioni 1.2, mshindi wa pili Tsh 800,000, watatu 500,000, wanne Tsh 300,000 na wa tano kupata 200,000.

“FAIDIKA ilifanya mashindano haya baada ya mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 300 kutoka katika mkoa wa Dar es Salaam, Mbeya na Arusha, ikilenga jumla ya makundi matatu: Wanawake wa Tanzania asilimia 34, watu wenye ulemavu asilimia 32 na watu wa kawaida mitaani asilimia 34," alisema.

Awali, mgeni rasmi katika hafla hiyo ya utoaji zawadi kwa washindi, iliyofanyika Jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa viwanda vidogo na biashara ndogo ndogo na za kati kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Consolata Ishebabi aliwataka wafanyabiashara ndogo ndogo kurasimisha biashara zao ili kuepuka usumbufu wanaopata wa kupoteza mali zao na mitaji ya biashara wakati wa oparesheni ya safisha mji.

Bi. Ishebabi alisema biashara zilizorasimishwa na kupewa leseni, hupangiwa utaratibu mzuri wa kufanyia shughuli za biashara, hivyo kumfanya mjasiriamali awe na nafasi ya kutumia biashara yake kukopa mikopo katika taasisi mbali mAbali za kifedha.

“Wafanyabiashara ndogo ndogo wakijisajili katika mfumo rasmi, inakuwa rahisi hata kwa taasisi zinazotoa mikopo kuwaamini na kuwapa mikopo na kuweza kutanua mitaji yao. Bila kuwa rasmi, ni vigumu kuaminika. Kwa biashara zilizorasimishwa, oparesheni ya safisha mji haiwaathiri kwani watakuwa katika maeneo maalum waliopangiwa kufanya shughuli zao,” alisema Bi. Ishebabi.

Alipongeza uongozi wa FAIDIKA kwa kuja na utaratibu wa kuwafuatilia wajasiriamali ili kuhakikisha kuwa wanazingatia biashara walizoombea hela na kuwaonyesha njia bora ya kuboresha biashara zao, na kuzitaka taasisi zingine zinazotoa mikopo kuiga mfano huo, mbali na kujali tu kama mkopaji anarejesha mkopo.

MBUNGE JOSHUA NASSARI ASHIRIKI MDAHALO WA VIONGOZI WADOGO BARANI AFRIKA NCHINI MAREKANI

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari akizungumza wakati wa mdahalo wa viongozi wadogo wanaoshiriki programu ya rais Obama kwa viongozi wadogo wanaoonyesha dira .Mdahalo huo umefanyika katika chuo kikuu cha Arkansas ambacho Rais Mstaafu wa Marekani  Bill Clinton na mkewe Hillary walianzia kazi ya kufundisha Sheria.
Baadhi ya washiriki katika mdahalo huo ambamo miongoni mwa waalikwa walikuwa ni watanzania waishio Arkansas.
Mkurugenzi wa program ya Rais Obama ya "Young African Leaders initiative "(YALI) Dr, Leyah akizungumza katika mdahalo huo uliobeba kichwa cha "BRINGNG THE GAP BETWEEN THE DIASPORA AND OUR HOME COUNTRIES".
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari akizungumza muda mfupi baada ya kutembelea makao makuu ya shirika la Heifer International ambalo limetoa ahadi ya kuendelea kusaidia jamii hususani katika elimu na mitaji huku likitoa mradi wa Ng'ombe wa maziwa kutoka kwa jimbo la Arumeru Masharik


Mbunge jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nssari akila pozi la picha na mratibu wa kijiji cha Heifer ,Bi Hellen Brown .
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari pia alipata nafasi ya kushiriki mahojiano juu "vijana na mustakabali wa Afrika"katika kituo cha Luninga cha Umma kinachojulikana kama Fayetteville Public  Access Television.shoto ni mwandishi wa kituo hicho Dan,Prof Mitiku toka chuo kikuu cha Makelle nchini Ethiopia,wote hawa wanashiriki program ya Rais Obama ya viongozi wadogo wa kiafrika katika chuo kikuu cha Arkansas nchini Marekani.
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari akiwa na mshiriki mwenzake katika programu ya rais Obama ya viongozi wadogo wa kiafrika inayofanyika katika chuo kikuu cha Arkansas nchini Marekani ,Bi Clara toka nchini Nigeria ambaye pia ni balozi wa UN Charter nchini Nigeria.

WAZIRI MAKALLA ATOLEWA CHINI YA ULINZI WA POLISI BAADA YA MKUTANO WAKE KUFANYIWA VURUGU NA CHADEMA

$
0
0
 Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (katikati), akiongozwa polisi kuingia kwenye gari baada ya kutokea vurugu meza kuu, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Goba, Kinondoni Dar es Salaam, ambazo alidai zilipangwa kwa makusudi na viongozi wa Chadema kwa lengo la kumvulugia ziara yake ya kuwaelezea wananchi utekelezaji wa Ilani ya CCM katika suala la upatikanaji wa maji ya uhakika jijini Dar es Salaam ifikapo Septemba, mwakani.
 Gari lililombeba Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla, likilindwa na polisi lililopokuwa linaondoka baada mkutano wa hadhara kuvunjika kulikosababishwa na vurugu ambazo waziri alidai kuwa zilipangwa kwa makusudi na wafuasi pamoja na viongozi wa Chadema waliokuwa wakirumbana na viongozi wa CCM, katika Kata ya Goba, Kinondoni, Dar es Salaam. Makalla alikuwa katika ziara ya kukagua miradi ya maji katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
 Poilisi wakiwadhibiti baadhi ya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakisababisha vurugu katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Makongo. Kinondoni.
 Polisi wakimdhibiti mmoja wa viongozi wa Chadema wakati wa mzozo uliotokea jukwaa kuu katika mkutano wa Naibu Waziri wa Maji, Makalla na wananchi wa Kata ya Goba.
 Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (kulia), akimhoji mchezaji wa zamani wa Simba, Dua Said ambaye alikuwa miongoni mwa watu watano waliokamatwa kwa tuhuma za kujiunganishia maji isivyo halali  kutoka kwenye mabomba ya Mamlaka ya Maji Safi na Taka (Dawasa), kwenye nyumba zao zilizopo Bonde la Mto Msimbazi, Kigogo, Dar es Salaam. Makalla alikuwa kwenye ziara ya kukagua miradi ya maji Dar es Salaam.







 Makalla akijadiliana na maofisa wa CCM na Polisi kabla ya kwenda kupanda gari na kuondoka.
 Kiongozi wa cHADEMA AKIZOZANA NA WA ccm jukwaani katika mkutano wa Makongo Juu.
 Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee akizoza jukwaani katika mkutano uliofanyika katika Kata ya Goba na hatimaye kuvunjika
 Polisi wakimdhibiti mfuasi wa Chadema asiendelee kufanya fujo katika mkutano wa Waziri na Wananchi wa Kata ya Goba
 Askari wa FFU, akilinda doria wakati waziri Makalla akikagua nyumba ambazo watu wamejiunganishia isivyo halali eneo la Bonde la Msimbazi, Dar es Salaam.
 Makalla na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (kushoto) wakiangalia pampu zinazotumika kujazia maji kwenye malori yanayonyonywa kutoka kwenye mabomba ya Dawasa. Pampu hizo zilinaswa uani mwa nyumba katika eneo la Bonde la Mto Msimbazi Dar es Salam
 Waziri Makalla na viongozi wengini wakishanga kuona tanki kubwa la maji lililojengwa chini ya moja kati ya nyumba tano katika eneo hilo ambazo wamiliki wake wamejiunganishia maji ya Dawasa  isivyo halali
 Askari wakilinda doria katika eneo hilo
 Moja ya malori yanayojazwa maji katika eneo hilo. Nalo liko chini ya ulinzi
 Waziri Makalla akielezea athari zinazotokana na wizi huo wa maji ambapo alisema kuwa katika nyumba hizo tano kila siku wanaiba maji lita laki tatu, hivyo kila siku kuikoseasha serikali mapato ambapo kwa mwezi yanafikia sh. bil 1.4.
 Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika akielezea jinsi atakavyoshirikiana na Serikali katika mapambano dhidi ya ufisadi wa maji jijini na kwamba atakuwa bega kwa bega kuhakikisha mswada wa adhabu kubwa kwa wezi wa maji unapelekwa Bunge la Novemba mwaka huu.
 Mchaezaji wa zamani wa Simba, Dua Said akielezea kwa wanahabari na mbele ya Waziri Makalla, jinsi anavyoshirikiana na Shirika la Maji Safi na Taka Dar es Salaam (DAWASCO), katika biashara ya kuuza maji. Dua Said alikuwa ni miongoni mwa watu watano waliokamatwa kwa tuhuma za kujiunganishia maji ya Dawasco isivyo halali katika eneo la Bonde la Msimbazi
 Bomba jipya la maji likitandazwa eneo la Makongo tayari kwa maandalizi ya kusafirisha maji kutoka Mtambo wa Ruvu Chini ambao upanuzi wake umekamilika hivi karibuni.
 Makalla akiuliza swali kwa wakandarasi kuhusu utandazaji wa bomba hilo, wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maji Dar na Pwani.
 Waziri Makalla akiwa na Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee, Mwenyekiti wa CCM, Salum Madenge, (KUSHOTO)  Deusdedit Mtiro (kulia) walipokuwa wakimlaki alipowasili kwenye mkutano katika Kata ya Makongo.


 WAFUASI WA CHADEMA WAKISHANGILIA NA KUMTAKA WAZIRI AWAHAKIKISHIE UPATIKANAJI WA MAJI MAKONGO JUU
 Chadema na CCM wakishangilia katika mkutano huo
 Waziri Makalla akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Makongo
 Moja wa wananchi akilalamika mbele ya waziri kuhusu adha kubwa wanaipata ya maji eneo la Makongo juu
 Msafara wa viongozi wa Chadema na CCM ukielekea kwenye mkutano wa wananchi katika Kata ya Goba ambao hata hivyo ulivunjika baada ya kutokea vurugu
 WanaCCM wakimshangilia Waziri Makalla alipokuwa akihutubia wananchi katika Kata ya Makongo
 Chadema wakishangilia wakati Halima Mdee akihutubia Makongo Juu
 Mfuasi wa Chadema akilalama
 Mdee akizungumza na wanahabari baada ya mkutano wa Kata ya Goba kuvunjika
 Wana CCM WAKISEREBUKA
 MNYIKA AKIZUNGUMZA NA WAFUASI WA CcHADEMA BAADA YA MKUTANO KUVUNJIKA. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG.

TAARIFA KUTOKA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

$
0
0

Jana tarehe 16/07/2014 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ilifanya kikao cha kawaida cha siku moja mjini Dar es salaam. Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.

Pamoja na mambo mengine kikao hicho kilipokea taarifa ya mazungumzo yanayoendelea kati ya CCM kwa upande mmoja na CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi kwa upande wa pili.

Mazungumzo hayo yanayosimamiwa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi yana lengo la kuangalia kwa kina ni kwa nini baadhi ya wajumbe wachache wa Bunge Maalum la Katiba walisusia na kutoka nje katika awamu ya kwanza ya Bunge hilo, na kuangalia namna watakavyorudi ili kukamilisha mchakato wa mabadiliko ya Katiba nchini.

Kwa ujumla Kamati Kuu ya CCM imeridhishwa na mwenendo wa mazungumzo hayo na kupongeza juhudi hizo zilizofanywa na Msajili wa Vyama vya Siasa na Vyama husika. Kamati Kuu inapenda kueleza imani yake kuwa mazungumzo hayo yatazaa matunda kwa wajumbe wachache waliosusia Bunge Maalum la Katiba, kurejea Bungeni na kumalizia sehemu ya mchakato uliobakia. Kamati Kuu inayatakia kila la kheri mazungumzo hayo.

Kamati Kuu pia ilipokea taarifa za harakati za baadhi ya wanachama wa CCM walioonesha nia ya kuomba ridhaa ya CCM kugombea Urais. Baada ya kutafakari kwa kina, Kamati Kuu inapenda kuwakumbusha wote kuwa ili wasipoteze sifa za kugombea, ni muhimu wakazingatia Katiba, Kanuni na taratibu za Chama zinazosimamia masuala hayo.

Kuhusu wale waliopewa adhabu na Kamati Kuu kutokana na kukiuka baadhi ya taratibu za Chama kwa suala hili, Kamati ya Usalama na Maadili ya Chama itafanya mapitio ya mwenendo wao wa utekelezaji wa adhabu hiyo mwezi wa nane (Agosti 2014), na kama itabainika kuwa hawatekelezi ipasavyo masharti ya adhabu zao, itapendekeza kwa Kamati Kuu kuongezwa kwa adhabu kufuatana taratibu za Chama. 
Ni muhimu wanachama wote wakakumbuka kuwa Chama ni pamoja na Katiba, Kanuni na taratibu zake, hivyo kutoziheshimu na kuzifuata ni kukivuruga, jambo ambalo halivumiliki.

Nia ya CCM kusimamia haya ni kuhakikisha Chama kinakuwa na umoja na mshikamano ambao ni muhimu sana, hasa tunapoelekea kukamilisha kazi ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2010/2015 na Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.
Aidha, Kamati Kuu imewatakia kheri na fanaka Watanzania wote wakati huu wanapomalizia mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Imetolewa na:-

Nape M. Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
ITIKADI NA UENEZI
17/07/2014

Rais Kikwete apokea Hati za Utambulisho za Balozi wa New Zealand hapa nchini

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mhe. Richard Stuart Mann, Balozi wa New Zealand hapa nchini mwenye makazi yake Afrika Kusini. Hafla hiyo fupi ilifanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 15 Julai, 2014.
Balozi Mann akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) mara baada ya Balozi huyo kuwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Mhe. Rais Kikwete, wakwanza kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi maalum Mhe. Prof. Mark J. Mwandosya (Mb.)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mhe. Richard Stuart Mann
Balozi Richard Stuart Mann akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu.
Balozi Mann akisikiliza Wimbo wa Taifa lake ukipigwa kwa heshima yake mara baada ya kuwasili Ikulu. Kulia ni Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki, Balozi Mohammed Juma Maharage na wakwanza kushoto ni Mnikulu, Bw. Shaaban Gurumo.Picha na Reginald Philip.

SHIWATA YATOA VIWANJA BURE OFA YA MWENGE MKURANGA

$
0
0
WILAYA ya Mkuranga imepanga kupeleka Mwenge wa uhuru katika kijiji cha wasanii kilichopo MWANZEGA, Mkuranga Julai 22, mwaka huu.

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Cassim  Taalib alisema jana kuwa mwenge utapokelewa kutoka wilaya ya Rufiji katikia kijiji cha Kiparang’anda na baadaye utakwenda moja kwa moja katika kijiji cha wasanii na wanamichezo cha Mwanzega ambako utawasili saa 7 mchana.

Alisema kutokana na ujio wa ugeni huo mkubwa SHIWATA imetangaza ofa ya  siku kumi ambapo itapokea wanachama kwa punguzo la asilimia 50 na kugawa bure viwanja vya kujenga nyumba wasanii na wanamichezo ambao watapata nafasi ya kwenda katika sherehe na watakabidhiwa viwanja vyao.

Wasanii na wanamichezo zaidi ya 600 wanatarajiwa kuondoka makao makuu ya shiwata ilala bungoni saa 12 asubuhi Jumanne asubuhi kwenda mkuranga.

Katika sherehe hizo kiongozi wa mbio za Mwenge, ataweka jiwe la msingi katika kijiji cha wasanii kuzindua rasmi kijiji hicho ambacho kinatarajiwa kuwekwa umeme, barabara na miundombinu ya kisasa.

Taalib alisema katika sherehe hizo msanii  maarufu wa atavishwa joho ya kutawazwa kuwa balozi wa kwanza wa kijiji cha wasanii na wanamichezo hapa nchini.

SHIWATA pia inatoa pongezi kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mkuuu wa Wilaya ya Mkuranga, Viongozi wa Tarafa ya Shungubweni kata ya Mbezi,viongozi wa Mwanzega,Ngarambe.Alisema kutakuwa na mkutano wa wasanii.

RAIS KIKWETE AELEKEA MKOANI RUVUMA KWA ZIARA YA KIKAZI YA WIKI MOJA

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana  na Kamishna wa Polisi Msaidizi Mwandamizi (SACP) Mary Nzuki, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Julai 17, 2014  wakati akipanda ndege kuelekea mkoani  Ruvuma kuanza ziara ya Kikazi ya wiki moja ambapo atakagua na kuzindua miradi ya maendeleo na kuongea na wananchi. Kati kati ni Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)  Hamisi Selemani, Kamanda wa Polisi katika Uwanja huo wa ndege. PICHA NA IKULU

MKATABA WA GESI WA STATOIL NA TANZANIA

$
0
0
Swali kwa TPDC: Kwanini Makubaliano ni tofauti na Mkataba Elekezi (Model PSA)?
Baada ya kuvuja kwa Mkataba wa kutafuta na kuzalisha Gesi Asilia (PSA) kati ya Serikali kupitia TPDC na Kampuni ya Norway ya StatOil na baada ya baadhi ya wachambuzi kuhoji kuhusu mkataba huo, Shirika la TPDC limetoa maelezo yake. Sio mara moja, sasa ni mara ya tatu. Kimsingi TPDC wanasema wachambuzi waliochambua nyongeza hiyo ya Mkataba hawana uelewa wa mambo haya na wanaleta siasa. 
 
Nadhani ni muhimu TPDC wakajikita katika kueleza kwa lugha ambayo wananchi wa kawaida wataelewa badala ya kusingizia uelewa wa watu katika masuala haya. Wizara ya Nishati na Madini haina uelewa wa pekee wa masuala ya Mafuta na Gesi kama wanavyotaka umma uamini. Kuna watanzania wengi tu wenye kufuatilia mambo haya na wenye uwezo mpana hasa katika masuala ya kodi katika tasnia hii. Ni wajibu wa TPDC kutoa maelezo yasiyo changanya wananchi na bora zaidi waweke mikataba hii ya Gesi na Mafuta wazi. Maelezo yaliyotolewa na TPDC mpaka sasa hayaeleweki na yana lengo la kuwachanganya wananchi kama sio kuwaongopea.
 
Swali la Msingi
Serikali kupitia “Model PSA” imeweka viwango vya mgawanyo wa mapato kati ya Mwekezaji na nchi. Viwango hivi ni vya mgawo wa mafuta au gesi asilia yanayozalishwa kwa siku. Mkataba huu elekezi upo kwenye tovuti ya Shirika la TPDC na ndio mwongozo wa majadiliano kwa mikataba yote. Kwa mujibu wa Mkataba huu elekezi uzalishaji wa gesi asilia unapokuwa wa chini kabisa (0 –249.999 MMscf kwa siku) mgawo kati ya Tanzania na Mwekezaji unakuwa ni nusu kwa nusu (50 – 50 ) baada ya mwekezaji kuondoa gharama zake zote za uzalishaji. 
 
Iwapo uzalishaji umefikia hali ya juu kabisa ( 1500 MMscf na zaidi) mgawo wa Tanzania unakuwa asilimia 80 na Mwekezaji asilimia 20. Mwekezaji anaruhusiwa kuchukua mpaka asilimia 70 ya Gesi iliyozalishwa kufidia gharama za uzalishaji. Hivyo, kinachogawanywa ni asilimia 30 zinazobakia.
 
Mkataba uliovuja ( TPDC na StatOil hawajaukanusha) unaonyesha kuwa kiwango cha chini kabisa cha uzalishaji Serikali inapata asilimia 30 tu na Mwekezaji asilimia 70 licha ya kwamba tayari gharama zake keshajirudishia. Vile vile kiwango cha juu kabisa cha uzalishaji mgawo unakuwa sawa kwa sawa! Swali la msingi hapa ni, Kwanini makubaliano na kampuni hii ya StatOil yanaenda tofauti na Mkataba elekezi? Je, mikataba yote 26 imekwenda harijojo namna hii? Maswali haya bado hayajajibiwa na TPDC.
 
Tuelewe
Mkataba wa Gesi Asilia au Mafuta ni makubaliano ya kugawana mapato yanayotokana na kiwango kilichozalishwa. Katika maelezo yao TPDC wanaeleza kuhusu kodi ya mapato, mrahaba na kodi ya huduma. Kodi ya Mapato na kodi ya huduma ni kodi ambazo kila mfanyabiashara nchini anapaswa kulipa. Ikumbukwe kuwa imechukua miaka 20 na kelele nyingi sana mpaka kampuni za Madini kuanza kulipa kodi ya mapato na ushuru wa huduma. Mpaka leo hii bado Halmashauri za Geita na Kahama zinahangaika na kampuni za Madini kulipwa ushuru huu. 
 
Kampuni za Madini na za Mafuta hutumia mikakati ya kupanga kukwepa kodi (tax planning measures) kwa kutumia Tax Havens na Mikataba ya Double Taxation Treaties. Hivyo TPDC kusema tutegemee kodi ya Mapato ni sawa na kuimba kama kasuku na baada ya miaka 20 tutajikuta kwenye lawama zile zile za sekta ya Madini. Kwenye baadhi ya mikataba, kodi wanayolipa wawekezaji hukatwa kwenye mgawo wa TPDC na hivyo kodi hiyo hulipwa na TPDC na sio Mwekezaji kama tunavyoaminishwa na Serikali.
 
Kuhusu mrahaba wa asilimia 5 napo kuna tatizo kwani kwenye mikataba ya Gesi Asilia Mrahaba unalipwa na TPDC maana ndio mwenye leseni na sio Mwekezaji ambaye ni kandarasi tu. Mikataba kadhaa imeandikwa kwa namna ambayo Mwekezaji akilipa mrahaba, anajirudishia kwenye mapato ya Gesi kama gharama. Hivyo kimsingi mapato yetu ya uhakika ni kwenye mgawo wa uzalishaji. Ndio maana tunapiga kelele kuhusu mkataba huu wa StatOil kwenda kinyume na Mkataba mwelekezi wa Serikali.
 
Tutaambulia kiduchu sana
Kwa kuchambua Mkataba huu kati ya Tanzania na StatOil ya Norway hesabu zinaonyesha kuwa Nchi yetu itapata mgawo kiduchu sana. Chukulia uniti 1000 za gesi asilimia zimezalishwa kwa siku. Uniti 700 zinachukuliwa na Mwekezaji kufidia gharama za kuzalisha gesi hiyo na Uniti 300 zinazobakia Mwekezaji anachukua uniti 150 kama mgawo wake wa faida (profit gas). Hivyo Tanzania itabakia na uniti 150 tu kama mgawo wake, sawa na 15% tu ya Gesi Asilia yote iliyozalishwa katika siku hiyo. Iwapo Mkataba elekezi ungefuatwa Tanzania ingebakia na uniti 240 sawa na 24% ya gesi asilia iliyozalishwa.
 
Natoa rai kwa vyombo vya habari nchini kuandika masuala haya bila kuyumba maana yanahusu utajiri wa nchi yetu. Dhahabu imebakia mashimo kwa sababu Tanzania ililala na watawala kuandika mikataba ya hovyo. Tusilale kwenye Gesi Asilia. Wakati wa kutaka mikataba kuwa wazi ni sasa. Huu mmoja tu wa StatOil tunaweza kupoteza shilingi 1.6 trilioni, hiyo mingine 26 je? Nchi itabakia kweli? Tusikubali majibu mepesi. Tutake mikataba iwekwe wazi. Uwazi huleta uwajibikaji.
Zitto Kabwe, Mb
17 Julai, 2014

KUMBUKUMBU YA MWAKA MMOJA YA MZEE GODFREY MSEI

$
0
0
Marehemu Mzee Godfrey Daud Msei

Mpendwa Baba yetu, mpaka kufikia tarehe 15 Julai 2015 umetimiza mwaka mmoja tangu ulipoitwa na Bwana bila ya neno la kwaheri kwetu.Tunakukumbuka sana na tunakosa uwepo wako,upendo wako na ucheshi wako ila tunasema kiroho tuko pamoja nawe daima.

Unakumbukwa na Mkeo,Bi. Elizabert,Watoto zako Fabian Msei,Daud Msei ,Angella Msei,Jonathan (Gia) Msei,Rev. John Msei pamoja na James Msei,Wajukuu zako,Mama yako Mzazi Bi. Mboza,Dada zako,Shemeji zako,Kaka zako,ndugu,jamaa na Majirani.

Pengo lako halitazibika daima,tunamuoma Mungu aiweke roho yako mahala pema peponi.

-Amin.

Misa ya shukrani itafanyika katika kanisa la Anglikana,Mwenge/Kijitonyama jijini Dar es Saalam,siku ya jumamosi tarehe 19 Julai 2014.

Wote mnakaribishwa.

NAPE NNAUYE AZUNGUMZA NA WANAHABARI JIJINI DAR LEO

Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images