Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

AIRTEL YATOA MSAADA WA FUTARI JIJINI DAR

0
0
 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya (kulia) akikabidhi msaada wa vyakula mbalimbali vyenye thamani ya milioni 5/- kwa wawakilishi wa kituo cha kulelea watoto waliokatika mazingira magumu cha Irishad Madrasah cha Mbezi kwa Msuguri (kutoka kushoto), Mkurugenzi wa Kituo, Ustadhi Maulid Salim Kidebe, Ayoub Idrissa na Ramadhan Ayoub, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Airtel kupitia mpango wake wa huduma kwa jamii imeanza kutoa futari kwa vituo vitano vinavyolea watoto hao vya Sharif Saidi Al - Bath cha Mwanza, Al- Hidaya Children's Home cha Ilala, New Hope Family cha Mjimwema Kigamboni na Kiboa Orphanage Arusha.
 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya (kulia) akikabidhi msaada wa vyakula mbalimbali vyenye thamani ya milioni 5/- kwa wawakilishi wa kituo cha kulelea watoto waliokatika mazingira magumu cha New Hope Family cha Mjimwema Kigamboni (kutoka wa pili kushoto), Mlezi wa Kituo, Merry Stromberg, Victor Mshan, Anthony Mtatiro na Mwenyekiti wa kituo, Omari Kombe, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. 

Airtel kupitia mpango wake wa huduma kwa jamii imeanza kutoa futari kwa vituo vitano vinavyolea watoto hao vya Sharif Saidi Al - Bath cha Mwanza, Al- Hidaya Children's Home cha Ilala, Irishad Madrasah cha Mbezi kwa Msuguri na Kiboa Orphanage Arusha.

NYUMBA YATEKETEA KWA MOTO MWANANYAMALA JIJINI DAR LEO

0
0
Gari ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji likiwa eneo la Mwanyamala mapema leo mchana,ambapo moto mkubwa umezuka na kuteketeza nyumba nzima na  mali zilizokuwemo,ambazo thamani yake haikujulikana mapema,tukio hilo limetokea maeneo ya Mwananyamala jirani na hospitali ya Mwananyamala.
Baadhi ya watu wakishuhudia tukio la Moto lililotokea mapema leo mchana,ambapo moto huo umeteketeza nyumba nzima na mali zilizokuwemo,ambazo thamani yake mpaka Globu ya jamii inaondoka eneo la tukio haikufahamika.
Baadhi ya Askari  wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiendelea kuzima moto kwenye moja ya chumba cha nyumba hiyo,Mashuhuda waliokuweo kwenye tukio hilo wanaeleza kuwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme iliyokuwa imetokea kwenye moja ya chumba ndani ya nyumba hiyo.
Majirani walijitokeza kuzima moto kwa kutumia ndoo kama uonavyo pichani 
Mabati yaliyobahatika kutetekea kwa moto yakitolewa nje.
 Askari  wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiendelea kuzima moto.
baadhi ya raia wema pia walijitokeza kusaidia kuuzima moto huo.

ZIARA YA MAKAMU WA RAIS MKOANI KIGOMA

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mkuu wa Mkoa wa kigoma Mhe. Issa Machibya kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma baada ya kukamilisha ziara ya siku moja Mkoani humo leo. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Viongozi wa Dini na Viongozi wa Mkoa wa Kigoma wakati alipofanya ziara ya siku moja Mkoani humo leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na wananchi na Viongozi wa Mkoa wa kigoma kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma baada ya kukamilisha ziara ya siku moja Mkoani humo leo.(Picha na OMR)
 

MAALIM SEIF AKUTANA NA BALOZI MPYA WA TANZANIA NCHINI URUSI

0
0

 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na balozi mpya wa Tanzania nchini Urusi balozi Wynjones Kisamba, Ofisini kwake Migombani.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na balozi mpya wa Tanzania nchini Urusi balozi Wynjones Kisamba, Ofisini kwake Migombani. (Picha na Salmin Said, OMKR).

NCHI SABA ZATHIBITISHA KUSHIRIKI MASHINDANO YA SHULE ZA SEKONDARI AFRIKA MASHARIKI (FEASSA).

0
0
Jumla ya nchi saba zimethibitisha kushiriki katika mashindano ya shule za sekondari za Afrika Mashariki (Feasssa) yaliyopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam mwezi ujao.Nchi hizo ni  Rwanda, Kenya, Uganda, Burundi, Sudan Kusini, Zanzibar na wenyeji Tanzania Bara kwa mujibu wa mratibu wake, Laurence Madege.
 
Madenge alisema kuwa maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea vizuri na Tanzania Bara itashirikisha jumla ya wanamichezo 600 ambao watashiriki katika michezo mbali mbali. Alisema kuwa wanamichezo hao wamepatikana baada ya kufaya vyema katika mashindano ya Umiseta yaliyomalizika hivi karibuni Kibaha, Pwani.
 
Alisema kuwa  wawakilishi wa Tanzania Bara wanatarajia kuanza kambi mapema mwezi ujao kwa lengo la kushinda medali mbali mbali katika mashindano hayo yaliyopangwa kuanza Agosti  22mpaka 31.
 
“Tunatarajia kushirikisha jumla ya wanamichezo 2000 kutoka nchi mbali mbali, wanamichezo hao watashindana katika michezo 12 tofauti ambayo ni raga (kwa wavulana), netiboli (kwa wasichana) na michezo mengine, mpira wa wavu, magongo, mikoni, kuogolea, mpira wa meza, tenisi, mpira wa kikapu na soka.
 
Alisema kua uokiondoa raga na netiboli, michezo mingine yote itawashirikisha wasichana na wavulana. Hii ni mara ya pili kwa Tanzania kuandaa mashindano haya ambapo mwaka 2006, Makongo na Jitegemee ambazo ziliandaa kwa pamoja.

YANGA SC YAINGIA MAKUBALIANO YA KUNUNUA NYUMBA KWA AJILI YA WACHEZAJI WAKE NA NSSF

0
0
KLABU ya yanga imeingia makubaliano ya kununua nyumba kwa ajili ya wachezaji wake  na  Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) .

Akizungumza leo katika mkutano maalum na wachezaji hao Mkurugenzi wa  uendeshaji NSSF , Crecentius Magori amewaambia wachezaji hao kijana mjanja mjini ni yule ambaye ana miliki nyumba ama ardhi kuliko magari huku akiwahamasisha wachezaji wa Yanga kuchangamkia ununuzi wa nyumba hizo ambazo ziko katika mradi wa makao mapya katika kijiji cha
Dege Kigamboni jijini Dar es Salaam.

“Sisi tuko tayari kuwapa fomu  na kwenda kuwaonyesha nyumba hizo
ambazo zimejengwa kisasa zaidi hivyo ningependa kuwashauri  pindi
mnapopata fedha zenu za mikataba mkitoa kiasi ili kuweza kuwa kati ya
wamiliki wa nyumba hizo” alisema Magori.

“Endapo utaweza kumudu na kutoa kiasi cha sh. mil.8  taslimu  na
kulipa kwa miezi mitatu mfululizo unapewa NSSF wanamupa funguo  na
kuendelea kulipa kila mwisho wa mwezi hadi kwa miaka 15 unakuwa
mmiliki halali wa nyumba hiyo”alisema Magori.

Aidha aliongeza kwa kuwaambia wachezaji hao kwamba endapo utakufa
ndugu anaweza kurithi nyumba hiyo. Huku akiwasisitiza wachezaji ambao bado hawajajiunga na NSSF kufanya hivyo mara moja ili waweze kujivunia matunda ya uchezaji wa mpira hapo
baadaye.

Wakati huohuo  Katibu wa Yanga  Beno Njovu aliwaambia waandishi wa
habari kwamba hayo ni mawazo ya Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji
ambaye alizungumza na Mkurugenzi wa NSSF Ramadhan Dau ambapo wote kwa pamoja wameamua kuwawezesha wachezaji wa timu hiyo ili waweze kuwa na mali zao za kudumu hadi uzeeni.

TAARIFA YA AJALI MLIMA KILIMANJARO

0
0

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WASAANI NYOTA WA FILAMU NA MUZIKI KUTOKA NCHINI MAREKANI JIJINI DAR LEO

0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wasanii nyota wa filamu na muziki kutoka  Marekani walioko nchini kwa ziara ya kutoa mafunzo kwa wasanii wa Tanzania. Wasanii hao ni na  Terrence J. Jenkins, mwendeshaji wa kipindi cha muziki kwenye televisheni ya E! Entertainment (wa pili kulia) Chaka Zulu, Mtendaji wa Shughuli za Muziki kutoka Kampuni ya Disturbing The Peace Records (wa pili kushoto)  na Davis Banner, mwigizaji, mwanamuziki, mtunzi na msimamizi wa shughuli za muziki ambaye amepata kushinda tuzo maarufu ya Grammy.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitumia simu yake ya mkononi kuwaonesha vivutio vya kitalii wasanii nyota wa muziki na filamu wa Kimarekani walioko nchini kwa ziara ya kutoa mafunzo kwa wasanii wa Tanzania. Wasanii hao ni   Terrence J. (Jenkins), mwendeshaji wa kipindi cha muziki kwenye televisheni ya E! Entertainment, mwigizaji wa filamu na mtunzi wa vitabu na Revi Shelton, Mtendaji wa Shughuli za Muziki katika Kampuni ya Outlet Media Group. Wengine ni Chaka Zulu, Mtendaji wa Shughuli za Muziki kutoka Kampuni ya Disturbing The Peace Records na Davis Banner, mwigizaji, mwanamuziki, mtunzi na msimamizi wa shughuli za muziki ambaye amepata kushinda tuzo maarufu ya Grammy.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wasanii nyota wa muziki na filamu kutoka Marekani walioko nchini kwa ziara ya kutoa mafunzo kwa wasanii wa Tanzania. Wasanii hao ni   Terrence J. (Jenkins), mwendeshaji wa kipindi cha muziki kwenye televisheni ya E! Entertainment, mwigizaji wa filamu na mtunzi wa vitabu na Revi Shelton, Mtendaji wa Shughuli za Muziki katika Kampuni ya Outlet Media Group. Wengine ni Chaka Zulu, Mtendaji wa Shughuli za Muziki kutoka Kampuni ya Disturbing The Peace Records na Davis Banner, mwigizaji, mwanamuziki, mtunzi na msimamizi wa shughuli za muziki ambaye amepata kushinda tuzo maarufu ya Grammy.PICHA NA IKULU.
wakiwa katika picha ya Pamoja

MADUKA MATATU IKIWEMO NYUMBA VYATEKETEA KWA MOTO MWANANYAMALA KARIBIA NA HOSPITALI YA MWANANYAMALA LEO.

0
0

 Moto ukiwa umeanza kama utani, watu wakiwa wanaendelea na kazi kama kawaida.
 Moshi ukiwa unazidi katika eneo ambalo maduka matatu yameteketea kwa moto.
Gari likiwa linarudi nyuma lilipotokea baada ya kuona kuna moshi mkubwa mbele yao.
 Mashuhuda wakiwa wameanza kuelekea eneo la tukio
 Moto ukiwa unaanza kupamba moto, waya wa umeme unao onekana unashuka chini ndio umesababisha moto huo.
 Moto ukiwa unazidi pamba moto katika duka la kushonea nguo na kuuza vitambaa.
 Duka la nguo likiwa linapamba moto na maduka mengine yakiwa yameanza kupamba moto pamoja na nyumba ambayo ilikuwa imeungana na duka.
 Mmoja ya vijana akiwa anaanza kuokoa vitu vyake jirani na maduka yaliyokuwa yakiungua.
 Moto ukiwa unazidi
 Mamia ya watu wakiwa wamefika kushuhudia  tutuki la Moto
 Kazi za uokoaji zikiwa zimeanza huku wasamalia wema wakisaidia kuhamisha vitu
 Maduka mengine yakiwa yameanza kushika moto kwa kasi
 Baadhi ya vyombo na vifaa vya duka la kushonea nguo vikiwa vimeokolewa
 Kazi ya uokoaji ikiwa inaendelea
 Mashuhuda wakiwa wanaongezeka.


 Moshi Mkubwa uliowachanganya watu na kila mmoja kuanza kutaka kukimbia eneo la tukio
Vijana wasamalia wema wakiwa wameacha kazi zao za kutengeneza magari, kufyatua matofari na mambo mengine wakiwa wanafanya kazi ya kuanza kuuzima moto.
 Vijana wakiwa wameanza kufanya kazi ya kuzima moto baada ya Kikosi cha zima moto kuendelea kuchelewa kufika
Maduka yakizidi kwisha kwa kuteketea kwa moto, Huku wananchi wakipata tukio moja kwa moja
 Baadhi ya Vijana wasamalia mwema wakiwa wanaondoa mabati ili kuzuia moto usiendelee kuwaka zaidi
Sehemu ya nyaya za umeme uliosababisha moto huo.
 Upande mwengine wa mashuhuda
 Vijana wakiwa bize wanafanya kazi ya kuendelea kuzima moto kwa ushirikiano
 Vijana wakiwa wanashughulika kwa nguvu zote ili wapate kuzima moto mara moja
 Baadhi ya Mashuhuda wakimwagiwa maji kupisha njia ya waokoaji waliojitolea kuzima moto kupita
 Mmoja wa Mashuhuda akiwa anachukua tukio kwa umakini
 Kikosi cha zima moto wakiwa wakiwa wanawasili eneo la tukio, huku wananchi wakiwazuia wasifanye kazi kwa kuwa kazi wamekuta imeisha
 Kikosi cha zima moto wakiwa wameanza shuguli ya kumalizia kuzima moto
Maji ya kuwasha yakiwa yamefunguliwa ili kuwatawanya watu wakae mbele kupisha kazi ya kuzima moto na uharifu.
 Kikosi maalum cha kuzuia vurugu cha Jeshi la Polisi (FFU) wakiwa  wamefika eneo la  tukio kwa ajili ya kulinda usalama
 TANESCO wakiwa wamefika eneo la tukio
Vijana wakiwa wanalalamikia kikosi cha kuzuia moto kuwa wamechelewa kuzima moto.
 Watu wakiwa wanazidi kuzuiliwa kupisha kazi ya uokoaji.
 Kikosi Maalum cha kuzuia vurugu kutoka Jeshi la Polisi FFU wakiwa wanaongezeka kuongeza kuvu ya kuimarisha ulinzi
 Kazi ya uokoaji ukiwa unaishia
 Kikosi maalum cha zima moto wakiwa wanamalizia kazi ya kuzima moto kidogo uliobakia
 Kila mtu anajitahidi kupata tukio
 Kazi ikiwa inaelekea kumalizika
 Baadhi ya mabaki uya mabati.
Kazi ya kuzima moto ikiwa imeisha , mmoja ya wanakikosi cha wazima moto akiwa anafunga mtambo
 Hivi ndivyo maduka yalivyobakia pamoja na nyumba iliyo ungua
 Mabaki ya vitu katika duka la vitambaa ya nguo na ushonaji
 Mmoja ya wanakikosi cha zimamoto akiwa anaongea na wananchi
 Wananchi wa mwananyamala wakiwa wanasikika wakisema "Wamekuja zima moshi... wamekuja zima moshi..."
 Mmoja wa wazee wa Mwananyamala aliye vaa shati la Dhambalau akiwa anakanusha kuwa ni uongo kwamba Kikosi cha kuzima moto hakijafanya kazi bali wananchi ndio waliozima moto
 Mmoja wa mashuhuda akiwa anaelezea jinsi moto ulivyotokea na kushukuru wananchi na Kikosi cha kuzima moto kwa kazi kubwa iliyofanikisha zoezi ka kuzima moto.
 Kazi ikiwa imeisha hizi ndizo ndoo ambazo zilisaidia kwa kiasi kikubwa kuzima moto pamoja na baadhi ya vijana wachache walio saidia kuzima moto huo.

*******
Moto mkubwa uliosababishwa na hitirafu ya umeme  umewaka eneo la Mwananyamala Jirani na Hospitali ya Mwananyamala na kusababisha kuungua kwa Maduka matatu pamoja na nyumba moja ambayo ilikuwa imeungana na duka moja wapo ambamo walikuwa wanauza vitambaa na kushona nguo.

Moto huo ulichukua zaidi ya masaa mawili ambapo wakazi wa eneo hilo ndio waliosaidia kwa kiasi kikubwa kuzima moto huo mpaka kuumaliza na baadae Kikosi cha kuzima moto kufika na kukuta moto ndio unaishia na kuendelea kumalizia kushirikiana na wananchi wengine kuzima moto huo.

Katika tukio la Moto huo hakuna mtu ambaye amedhuriwa ingawa katima maduka yote matatu walifanikiwa kuokoa baadhi ya vitu huku vilivyobakia kuteketea vibaya kwa moto huo.


Picha zote na Dar es salaam yetu Blog


ZIARA YA MKUU WA MKOA WA RUKWA ENG. STELLA MANYANYA KATIKA KUHAMASISHA MPANGO WA MATOKEO MAKUBWA SASA (BRN) KATIKA SEKTA YA ELIMU MKOANI HUMO

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza kwa hisia kubwa na wanafunzi wa shule ya Sekondari Itwelele iliyopo Manispaa ya Sumbawanga leo tarehe 15/07/2014 ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya kuhamasisha mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) kwa shule za Msingi na Sekondari Mkoani Rukwa. 

Katika ziara yake hii amepata fursa ya kuonana na wanafunzi na wadau wa elimu zikiwemo kamati za shule mbalimbali katika kata za Manispaa ya Sumbawanga na viongozi katika kujadili na kuweka mkakati wa kufanikisha mpango huo. Katika kuhakikisha BRN inafanikiwa ametoa maagizo kadhaa kwa viongozi husika ikiwemo kila shule ya msingi kuhakikisha kuwa na darasa la awali, kila shule ya sekondari kuwa na maabara ya sayansi, kila shule kutengeneza matofali 150, 000 na kila mzazi au mwananchi wa kata husika kutoa mchango wa Tsh. 10,000/= kusaidia ujenzi wa maabara hizo na madarasa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (kushoto) akizungumza na viongozi wa Manispaa ya Sumbawanga wakati akikagua moja ya maabara iliyokwishajengwa katika shule ya Sekondari Itwelele.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (kulia) akizungumza na wananchi wa kata ya Pito wakiwa katika zoezi la kufyatua matofali kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na maabara katika shule za kata hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akikagua sehemu ya mahindi yaliyozalishwa katika shamba la shule ya Sekondari Itwelele ikiwa ni matunda ya mpango ulioanzishwa na Serikali ya Mkoa wa Rukwa wa kugawa ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa shule zote Mkoani Rukwa ambazo zilitakiwa kulima shamba lisilopungua ekari tano litakalotumika kama shamba darasa na kusaidia upatikanaji wa chakula kwa shule husika. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na wadau wa elimu katika kata za Katandala, Izia na Majengo jana tarehe 14/07/2014 katika shule ya Sekondari Mazwi mjini Sumbawanga. 
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Sumbawanga akifafanua moja ya jambo katika kikao hicho. Alieleza kuwa kero inayowakabili wananchi na wanafunzi wa shule iliyokaribu na Dampo la Jangwani inakaribia kuisha kutokana na ujio wa magari mawili mapya ya kubebea taka yanayotegemewa kuwasili wiki hii mjini Sumbawanga.
Baadhi ya wadau wa elimu kutoka kata za Katandala, Izia na Majengo Mjini Sumbawanga wakiwa katika kikao cha kujadili mkakati wa kufanikisha mpango wa Matokeo Makubwa sasa (Big Result Now) kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (hayuko pichani).
- Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com.

WAZEE WA KIMILA NA WAKIDINI WAASWA KUKAA NA VIJANA KUEPUKA VIOVU

0
0
a.KATIBU mkuu wa umoja wa vijana ccm (UVCCM) Taifa , Sixtus Mapunda wa pili kulia akiwa anatoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya ziara yake katika mkoa wa Arusha
b.
Waandishi wa habari wakiwa kazini

KATIBU mkuu wa umoja wa vijana ccm (UVCCM) Taifa , Sixtus Mapunda amewataka wazee wa kimila (malwaigwanan), viongozi wa dini pamoja na wazazi kutumia muda wa ziada  kukaa na vijana wao na kukemea kuacha mara moja kutumiwa katika vitendo viovu vinavyoendelea mkoani hapa.

Alisema kuwa , vijana wengi  wamekuwa wakituhumiwa kufanya  uhalifu  wa  ulipuaji wa mabomu jijini hapa ambapo wengi wao ni vijana kuanzia umri wa miaka 18 hadi 25.

Aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na wananchi pamoja na vijana katika wilaya ya Arusha na Meru wakati alipotembelea  maeneo hayo kwa lengo la kujionea hali halisi ya vijana na kuzungumza nao.

Alisema kuwa, mkoa  wa Arusha hivi sasa unakabiliwa na wakati mgumu sana kutokana na uvunjifu wa amani unaofanywa na vijana kwa kutumiwa na baadhi ya watu kwa lengo ya kuvuruga amani ya mkoa wa Arusha na kwa nchi kwa ujumla.

Mapunda alisema kuwa, wazee wa kimila pamoja na viongozi wa dini wana mchango mkubwa sana katika jamii inayowazunguka hivyo wakiweza kuwakutanisha vijana na kuzungumza nao kuhusiana na kutokukubali kutumiwa katika uvunjifu wa amani badala yake wawe walinzi wa nchi yao na kuwa mstari wa mbele kuwafichua wahalifu.

‘jamani mkoa wa Arusha una vivutio vingi sana vya watalii ambavyo kwa ujumla vimekuwa vikiingizia mkoa wa Arusha fedha nyingi pamoja na taifa kwa ujumla , na pia kupitia vivutio hivyo vijana wengi wameweza kupata ajira na hata wengine kujiajiri sasa tunapofikia hatua ya kujiingiza kwenye uvunjifu wa amani ,hata uchumi unayumba kwani hakuna atakayependa kutembelea Arusha tena’.alisema Mapunda.

Alifafanua zaidi kuwa,ni vizuri vijana wakawa mstari wa mbele kuwafichua wale wahalifu wanaovunja amani badala ya kuwakumbatia na kuwapa ushirikiano  hali ambayo inachangia uchumi wa nchi kuyumba kwa ujumla.

Mapunda  aliwataka wadau mbalimbali nchini kushirikiana na  kuwa walinzi  katika maeneo yao ikiwemo kutoa ushirikiano wa kutosha kwa maeneo husika pale watakapowabaini wahalifu mahali popote ili tuweze kuinusuru nchi yetu badala ya kuachia swala la ulinzi kwa jeshi la polisi peke yake.

Naye Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha,Robinson Meitinyiku alisema kuwa,kutokana na matukio ya uhalifu wa mabomu yanayoendelea jijini hapa seriakli itaendelea kuchukua wajibu wake na kuhakikisha kuwa amani inadumushwa.

Alisema kuwa, wao kama uvccm mkoa wa Arusha wamekuwa wakiwaomba wazee wa kimila pamoja na viongozi mbalimbali kukaa na vijana na kuweza kuwasihi kutokubali kutumiwa katika uhalifu huo.(Pamela Mollel wa jamiiblog)

MTOTO WA RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI AJUMUIKA NA WADAU WA BENKI YA FNB KUPATA IFTARI YA PAMOJA JIJINI DAR

0
0
Pichani kulia ni Mgeni rasmi,Mtoto wa Rais Mstaafu awamu ya pili,Mh,Ali Hassan Mwinyi,Abdallah Ali Hassan Mwinyi kwenye hafla ya Iftari ilioandaliwa na benki ya FNB,na kufanyika kwenye bustani ya Serena Hotel jijini Dar hapo jana,anaefuatia kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa benki ya FNB,Ndugu Dave Aitken akiwa na baadhi ya wageni waalikwa wengine.
Mgeni rasmi Abdallah Ali Hassan Mwinyi sambamba na Mkurugenzi Mkuu wa benki ya FNB,Ndugu Dave Aitken wakijumuika pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo wakiwa pia na baadhi ya wateja wa benki ya FNB waliolikwa kwenye hafla ya Iftari ilioandaliwa na benki hiyo jana jioni katika bustani ya Serena Hotel jijini Dar hapo jana.

 Baadhi ya Wadau wa benki ya FNB wakiwa kwenye hafla ya Iftari
Baadhi ya wadau wa FNB Benki wakijadiliana jambo huku wakipata Iftari iliyoandaliwa na benki hiyo maalum kwa wateja wao katika bustani ya Serena hotel hapo jana.
Pichani kulia ni Mgeni rasmi,Mtoto wa Rais Mstaafu awamu ya pili,Mh.Ali Hassan Mwinyi,Bwa. Abdallah Ali Hassan Mwinyi akiongoza wageni waalikwa kupata Iftari ya pamoja ilioandaliwa na benki ya FNB,kwenye bustani ya Serena Hotel jijini Dar hapo jana.
Wageni walikwa na wadau wakubwa wa benki ya FNB wakiendelea kupata Iftari.
Mambo ya kupata Iftari ya pamoja ilioandaliwa na benki ya FNB.

Naibu Waziri wa Uchukuzi atemebelea chuo cha bahari dar es Salaam (DMI)

0
0
 Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), mara baaada ya kuwasili chuoni hapo kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na chuo hicho na kuongea na wafanyakazi wa Chuo hicho, mwanzoni mwa wiki. Kulia kwake anaemtazama ni Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Kapteni Yasin Songoro.
 Mkufunzi wa Chuo cha Bahari  Dar es Salaam (DMI), akimpa maelezo ya namna ambavyo wahandisi wanaofanya kazi ndani ya chumba cha injini ndani ya Meli wanavyoendesha mitambo hiyo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba, wakati alipotembea chuoni hapo mwanzoni mwa wiki kuongea na wafanyakazi wa chuo hicho.
 Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba, akimsikilza Kapteni Jumanne Karume, alipokuwa akimpa maelezo ya namna nahodha anavyoendesha Meli, wakati alipotembelea Chuo Cha Bahari Dar es Salaam(DMI), mwanzoni mwa wiki. Kushoto kwa Dk Tizeba ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Kapteni Yasin Songoro.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba (aliyeweka mikono mfukoni), akimsikiliza Kapteni Peter Mkunja wakati akimpa maelezo ya namna vyombo vya kujiokoa vinavyotumika endapo meli itazama ama kupata hitilafu yoyote, wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea Chuo hicho Mwanzoni mwa wiki.
 Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Bahari Dar es Salaam (DMI), Kapteni Yasin Songoro, akitoa maelezo ya namna ambavyo mashine inayotengeneza vipuri vinayoharibika ndani ya meli inavyofanya kazi kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba, alipotembelea Chuoni hapo Mwanzoni mwa wiki hii.
Sehemu ya Menejimenti na wafanyakazi wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba (Hayupo Pichani), wakati alipoongea nao mwanzoni mwa wiki.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)

WAZIRI LAZARO NYALANDU ASHIRIKI HAFLA YA KUCHANGIA USTAWI WA MISITU KAMA VYANZO MUHIMU VYA MAJI BARANI AFRIKA JIJINI PENNSYLVANIA MAREKAN

0
0
1
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (MB) akizungumza katika halfa maalum ya kuchangia ustawi wa misitu kama vyanzo muhimu vya maji barani Afrika iliyoandaliwa na Taasisi ya Africa 6000 International jana mjini Erie, Pennsylvania, Marekani
2
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Africa 6000 International Bi. Teresa Murtland akizungumza katika halfa maalum ya kuchangia ustawi wa misitu kama vyanzo muhimu vya maji barani Afrika iliyoandaliwa na Taasisi ya Africa 6000 International jana mjini Erie, Pennsylvania, Marekani.
3
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (MB) (kati) akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Africa 6000 International Bi. Teresa Murtland (kulia) na Bw. John Bongiorno ambaye ni mdau katika sekta ya maji aliyeshiriki katika hafla hiyo
4
Sehemu ya waalikwa waliohudhuria halfa maalum ya kuchangia ustawi wa misitu kama vyanzo muhimu vya maji barani Afrika iliyoandaliwa na Taasisi ya Africa 6000 International jana mjini Erie, Pennsylvania, Marekani

WAFUASI WA CCM,CHADEMA NUSURA WAZITWANGE MKUTANO WA NAIBU WAZIRI WA MAJI

0
0
 Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azzan wa CCM (KULIA), akiamulia ugomvi wa Diwani wa Kimara, Pascal Manota wa Chadema (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge waliotaka kuzichapa ulipotokea mzozo katika mkutano wa hadhara wa Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla katika Uwanja wa Shule ya Mavurunza, Kata ya Salanga, Jimbo la Ubungo, Dar es Salaam jana.
 Wafuasi wa CCM na Chadema wakitaka kuzipiga kavu kavu baada ya kutokea mzozo ambapo wanaCCM walikuwa wakimzomea Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Mhe John Mnyika  akihutubia na WanaChadema wakimzomea Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla  akihutubia katika mkutano huo.
 Polisi wakiwatuliza wafuasi wa Chadema waliokuwa wakipinga Mbunge wao John Mnyika asijibu swali lililoulizwa na Mkazi wa Kibamba, Jordan Balindo aliyemtaka Mnyika aeleze ni jitihada gani amezifanya binafsi kama mbunge kutatua changamoto ya ukosefu wa maji katika jimbo la Ubungo.

MBUNGE KABATI ATEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO

0
0
 Daktari wa Mifugo wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Augustino Nyenza akimwelekeza Mbunge wa viti maalum Lita Kabati mradi wa machinjia ya kisasa yaliyoko Ngelewala yaliyopo katika kata ya Isakalilo.
 Mganga Mfawishi wa Hospitali ya wilaya ya Frelimo Dk. Hassan Mtani akitoa taarifa kuhusu hospitali hiyo mbele ya mbunge wa Viti maalum CCm Lita Kabati
 Baadhi ya wahudumu wa hospitali ya Frelimo
 Mbunge wa viti maalum CCM Lita Kabati akimpa pole mama aliyejifungua hospitalini hapo.
 Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Iringa kwa tiketi ya chama cha mapinduzi(CCM), Lita Kabati akikagua mradi wa barabara kiwango cha lami katika eneo la Ngome
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Iringa kwa tiketi ya chama cha mapinduzi(CCM), Lita Kabati akishiriki katika ujenzi wa mitaro ya maji katika barabara ya ngome. (Picha zote na Denis Mlowe)
 
Na Denis Mlowe,Iringa

MKOA wa Iringa umeanza kutekeleza mkakati wa serikali wa Matokeo Makubwa Sasa ili kuwaletea wananchi maendeleo ya haraka katika sekta za Kilimo, Maji, Elimu, Uchukuzi, Nishati na Madini, na Uwezeshaji wa wananchi kupitia miradi ambayo imetekelezwa kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2013/2014.

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Iringa kwa tiketi ya chama cha mapinduzi(CCM), Lita Kabati ametembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya mkakati wa matokeo makubwa sasa ili kujua maendeleo yake pamoja na changamoto zilizopo. Moja ya mradi aliotembelea ni mradi wa ujenzi wa barabara kiwango cha lami katika eneo la Mkimbizi, Kihesa hadi Tumaini uliogharimu sh. bilioni 1.8 wenye km 2.5

Mradi mwingine uliotembelewa ni mradi wa ujenzi wa machinjio ya kisasa yaliyoko Ngelewala yaliyopo katika kata ya Isakalilo yaliyogharimu sh. Bilioni 1.4 na hadi sasa matengenezo yake  yakiwa yamegharimu nusu ya fedha hizo na ujenzi unaendelea mradi uliopangwa kutekelezwa kwa awamu tano.

Mradi huo wa machinjio ulianzishwa baada ya Halmashauri kuona machinjio iliyopo haikidhi mahitaji ya uchinjaji kwa sasa ikiwemo kuchakaa kwa miundombinu,kuwa jirani na makazi ya watu,kuwa na eneo dogo la uchinjaji kutokana na ongezeko la hali ya uchinjaji.
Aidha mbunge Kabati alitembelea mradi wa hospitali ya wilaya ya Frelimo ambayo inafanya kazi na wagonjwa wameshaanza kuitumia baada ya kukamilika na moja ya hospitali zinaztoa huduma bora za meno

Akizungumza  katika mrejesho wa majumuisho ya ziara hiyo Lita Kabati alisema kuwa amelidhishwa na maendeleo yaliyopo kulingana na fedha iliyotumika katika kufanikisha miradi hiyo. Alisema mradi wa machinjio unatakiwa kupiganiwa zaidi ili uweze kukamilika kwani utasaidia kuwapatia ajira vijana zaidi ya 200 mara baada ya kukamilika kwake.

Mbali na hayo alisema kuwa wabunge wanapaswa kujua fedha  zinazoletwa kwa ajili ya miradi inaendana na mradi wenyewe  kutokana na kuwa fedha nyingi zimekuwa zikitumika tofauti na nyingine kupotea.

Kabati aliahidi kuwa atashirikiana na manispaa  kwa kuhakikisha wanafatilia miradi hiyo na kusaidia  changamoto ziweze kukabiliwa na kutimizwa kwa wakati.

Revisited And Re-Released: MwanaFA Feat.Jay Moe "IngeKuwa Vipi"

0
0
Ingekuwa Vipi-Revisited And Re-Released Ingekuwa Vipi-Revisited And Re-Released[/caption] MwanaFA [real name Hamis Mwinjuma] is, without a doubt, one of the most successfully and respected Bongo Hip-Hop artist in Tanzania, across East Africa and certainly beyond those borders. If that statement made your eyebrows tilt even a bit, I’d suggest you take one step back and think a little. 

His lyrics and songs have inspired new words, idioms etc into the street and classroom dictionaries and thesauruses of Swahili. The grandness of his lyrical abilities staggers even me who was once upon a time considered by my peers and schoolmates to be a walking Swahili dictionary. He can rhyme quickly, confidently and cleanly while making sense of every word that come out of his mouth. Recently I approached him with an idea I have wrestled with for a while. 

How about re-releasing some of the biggest hits from the time when Bongo Fleva/ Bongo Hip-Hop was starting to see the white-blue sky. The motivation is to flaunt the standards of the past and give today’s generation a renewed chance to hear not only the “old school” stuff all over again but to gain a hindsight of the stories behind. He didn’t hesitate even for a second. He agreed and here we are. Let’s Go!

RAIS KIKWETE AKABIDHI BENDERA TIMU YA TAIFA YA RIADHA ITAYOSHIRIKI MICHUANO YA JUMUIYA YA MADOLA HUKO GLASGOW, SCOTLAND

0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi bendera nahodha wa timu ya Taifa ya riadha inayoondoka kesho Julai 16, 2014 kwenda Glasgow, Scotland, kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola kwenye hafla fupi iliyofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kushuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernand Membe, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe Juma Nkamia na wadau wa michezo.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi bendera nahodha wa timu ya Taifa ya riadha inayoondoka kesho Julai 16, 2014 kwenda Glasgow, Scotland, kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola kwenye hafla fupi iliyofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kushuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernand Membe, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe Juma Nkamia na wadau wa michezo.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na wachezaji na viongozi wa timu ya Taifa ya riadha inayoondoka kesho Julai 16, 2014 kwenda Glasgow, Scotland, kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola kwenye hafla fupi iliyofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kushuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernand Membe, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe Juma Nkamia na wadau wa michezo.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana  na wachezaji na viongozi wa timu ya Taifa ya riadha inayoondoka kesho Julai 16, 2014 kwenda Glasgow, Scotland, kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola kwenye hafla fupi iliyofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kushuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernand Membe, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe Juma Nkamia na wadau wa michezo.
  Wakimsikiliza kwa makini Rais Kikwete ni wachezajina viongozi wa timu ya Taifa ya riadha inayoondoka kesho Julai 16, 2014 kwenda Glasgow, Scotland, kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola kwenye hafla fupi iliyofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kushuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernand Membe, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe Juma Nkamia na wadau wa michezo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wachezaji na viongozi wa timu ya Taifa ya riadha inayoondoka kesho Julai 16, 2014 kwenda Glasgow, Scotland, kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola kwenye hafla fupi ya kukabidhi bendera iliyofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kushuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernand Membe, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe Juma Nkamia na wadau wa michezo.PICHA NA IKULU.

SOMA VIPAUMBELE VYA DISMAS LYASSA, MGOMBEA URAIS TUCTA

0
0
 


Na Dismas Lyassa
Mgombea Urais wa TUCTA; Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi

Salaam
Wapendwa ndugu zangu wana habari…Asalam Aleikum…Tumsifu Yesu Kristo… Bwana Yesu Asifiwe…!
Shukrani
Ndugu wanahabari
Nawapenda kuwashukuru kwa ujio wenu. Nichukue fursa hii niwatambulishe walioko mbele yenu ili kufahamiana. Nianze kwa kujitambulisha mimi mwenyewe, naitwa Dismas Lyassa, ni mwandishi wa habari mwenzenu…nimekuwa katika hii kazi kwa miaka 20 sasa na nimewahi kufanyia kazi katika magazeti mbalimbali yakiwamo Alasiri, Financial Times, Leo ni Leo na tangu 2005 nimekuwa nikifanyia kazi katika gazeti la Mwananchi hadi sasa nikiwa mhariri anayeshughulikia masuala ya biashara na uchumi. Pia toka mwaka 2012 nilichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa COTWU tawi la Mwananchi Communications Limited, nafasi ambayo kisheria mtu anapaswa kudumu kwa miaka mitano, lakini akitaka anaweza kugombea.

Utambulisho
Ndugu wanahabari
Wengine niliombatana nao ni mke wangu Mchungaji Rightess Lyassa wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Kawe -Dar es Salaam, Mussa Mwakalinga Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Mawasiliano na Usafirishaji (COTWU) kanda ya Dar es Salaam, wakili wangu Jebra Kambole kutoka kampuni ya Uwakili ya Law Guards ya Jijini Dar es Salaam, na meneja kampeni Khamis Tembo.

Ndugu wanahabari

Lengo hasa la kuwaiteni mahali hapa ni kutoa taarifa kwenu kuwa ninagombea Urais wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania, uchaguzi ambao unatarajiwa kufanyika Agosti 4-5, Dodoma. 
 
Vipaumbele vyangu ni vyangu
Ndugu wanahabari
Nina malengo ya kuifufua na kuleta TUCTA yenye uhai na mabadiliko ya kweli kwa kufanya yafuatayo;

Ndugu wanahabari
1. Kupigania na kulinda haki za wafanyakazi;
Katika kipaumbele hili lengo hasa ni kuondoa matatizo sugu ya wafanyakazi yakiwamo-:
i.             Kulipwa ujira/mishahara duni isiyoendana na uhalisia wa maisha.
ii.           Ucheleweshaji wa upatikanaji wa ujira/mishahara
iii.          Ucheleweshaji fedha za kujikimu kwa waajiriwa wapya/ kiwango kidogo cha fedha za kujikimu
iv.          Uhaba au kutokuwepo kabisa makazi kwa wafanyakazi wapya
v.            Rushwa na kuajiri kwa misingi ya kujuana kwa mfano katika Halmashauri ya Siha, wilaya ambayo imegawanywa kutoka Hai, kuna pori kubwa la West Kilimanjaro mlimani kabisa, hakuna maendeleo…ni suala la kawaida kuona watu wakiongea kilugha ofisini kama lugha ya Taifa
vi.          Wakubwa yaani mabosi kujifanya Mungu kwa kuwaendesha wafanyakazi kwa kadri wanavyotaka wao, sivyo inavyosema sheria.
vii.         Uwepo wa mpangilio usio sawa wa ujira/mishahara.
viii.       Kutopewa posho au kupewa kidogo au kutopewa kwa wakati
ix.          Fedha za uhamisho na likizo; kwa mfano kuna walimu ambao wameanza kazi 2004 NIT Shule ya msingi Dar es Salaam wamelipwa fedha za likizo mara moja mwaka 2012, mfano halisi ni mwalimu Ruth Natumwa, huyo ni kati ya walimu hao. Matatizo ya walimu kimsingi ni janga la taifa, yapo Taifa zima, kwa mfano katika shule ya Sekondari Kizota, Dodoma kuna walimu wengi  wana madai yao dhidi ya Serikali, waliajiriwa mwaka jana Machi, wakaanza kupata mshahara mwenzi wa tisa…walilipwa mshahara wa mwezi wa tisa tu na kuendelea,  ile mingine wanaendelea kudai.
x.            Mazingira magumu ya kazi mijini na vijijini (tunapozungumzia mazingira magumu inahusisha kutokuwepo vitendea kazi au kuwa vichache, miundo mbinu duni nk).
xi.          Waajiri kutochangia mifuko ya jamii
xii.        Fedha za makato ya wafanyakazi kupitia mifuko ya jamii zimekuwa zikikopeshwa watu wengine wasio wanachama wakiwamo wanasiasa huku wafanyakazi wenyewe wakiendelea kuwa na maisha duni
xiii.       Kufanya kazi kama kibarua kwa miaka mingi jambo ambalo ni tofauti za sheria za kazi
xiv.       Huduma za kifedha kuwa mbali na maeneo ya kazi, hali inayosababisha wafanyakazi kutumia fedha nyingi kufuatilia mishahara kwa vile ni mbali na eneo wanalofanyia kazi.
xv.         Kutokuwa na mfumo unaoeleweka wa upandishaji vyeo na ujira/malipo kwa wafanyakazi/vibarua
xvi.       Waajiri hasa binafsi kufukuza wafanyakazi hovyo/no job security…kufanya kazi bila mikataba
xvii.      Kupambana na tatizo la kodi kubwa kwa mishahara (PAYE)
xviii.    Tatizo la mabosi kutoa upendeleo wa wazi kwa baadhi ya wafanyazi kwa sababu zisizo za kitaalamu; wakati mwingine ni kwa sababu ya ngono; kuwataka kimapenzi wafanyakazi ili waendelee kuwepo kazini au kupandishwa vyeo…tatizo hili linaonekana kuwa sugu, wanawake wengi maofisini hawako huru sana, wamekuwa wakitakwa kimapenzi mno na mabosi wao, wengi wanashindwa kujizuia, tunataka kuona kunakuwa na sheria kali dhidi ya mabosi wa aina hii kama ilivyo katika nchi nyingine.
 
Ndugu wanahabari
Tatizo la ajira kuporwa na wageni
 Ingawa sheria/sera za ajira zinaeleza wazi kwamba hairuhusiwi wageni kuingia nchini zaidi ya watano kwa kazi ziziso na ujuzi, baadhi ya makampuni yamekuwa yakiingiza wageni kwa kazi ambazo Watanzania wengi wanaweza kuzifanya.

Ndugu wanahabariNitahakikisha wazawa wanapewa fursa ya kufanya kazi nchini; hii ni pamoja na kuomba CV za wageni ili tuone kama ni kweli hakuna Watanzania wenye sifa za kufanya hiyo kazi hiyo.
        -: Kumekuwa na taarifa za uwepo wageni katika makampuni kadhaa yakiwamo mahoteli, migodi, viwanda vya sarufi nk ambao baadhi wanalipwa malipo makubwa tofauti na wazawa japo hawana elimu au ujuzi wa kuwazidi wazawa. Nitakuwa na kamati maalumu ya kufuatilia waajiriwa wote Tanzania hasa wageni ili kujua kama wanazo sifa za kufanya kazi au wanapora nafasi za Watanzania.

Ndugu wanahabari
Nitapigania kuhakikisha tabia ya waajiri kulazimisha waajiriwa lazima wawe na uzoefu mkubwa inapungua au kukoma kabisa
  Kigezo cha kupata ajira kiwe ni uwezo wa mtu wakati huo baada ya kufanyiwa usaili, siyo lazima awe na uzoefu  wa miaka mitatu au mitano kama ambavyo waajiri wengi wanalazimisha; tunahitaji kuona Serikali inasimamia hili. Kama hali ni hii, wahitimu wanawezaje kupata ajira? Ni suala ambalo nitakuwa mkali nalo mno kwa sababu lina athari kubwa kwa jamii ya Tanzania, limekuwa ni sababu ya rushwa ikiwamo ya ngono…walioko vyuoni wengi hawana uhakika wa ajira, kwa sababu ya tabia hii. Ni lazima tubadilike, watu waajiriwe kulingana na uwezo wao wa kazi, siyo uzoefu.

Ndugu wanahabari
Wanafunzi shule ya Msingi/Sekondari nk wapatiwe elimu ya kujiajiri.
Kwa nafasi nitakayokuwanayo nitaishawishi Serikali iingize elimu ya ufundi/utengenezaji bidhaa na ujasiriamali kama mojawapo ya masomo ya ziada kama njia ya kupambana na tatizo la ajira ambalo linaonekana kukua nchini. Kama ambavyo kumekuwa na masomo ya dini katika shule zenu, tuwe pia na masomo ya ujasiriamali. Nitaangalia namna ya kuzishawishi taasisi zingine za ndani na nje kuhakikisha hili linafanyika; lengo ni kuhakikisha hata mhitimu wa msingi au sekondari nk awe ana uwezo wa kufanya ujuzi anaotaka kama kujenga, kushona, kufuma, kufuga, kutengeneza batiki, vikoi, sabuni, mishumaa nk.

Ndugu wanahabari
Nitaanzisha idara mbili mpya na kuboresha zilizoko;
     i. Idara ya walemavu
Hii itahusika kuangalia hali ya maisha ya wafanyakazi walemavu nchini ikiwamo kuwasaidia kupata baiskeli na huduma zingine muhimu.Nitatumia uzoefu wangu kwa kushirikiana na rafiki zangu wa nje kuhakikisha hili linafanikiwa. Tutaangalia namna ya kushirikiana na mashirika mbalimbali yakiwamo Free Wheelchair Foundation www.wheelchairfoundation.org.

Ndugu wanahabari
Kutakuwa ni mikakati mbalimbali kuhusu wafanyakazi walemavu na wale wanaopata ulemavu wakiwa kazini, kwa mfano Mwenyekiti wa Wasioona mkoani Tanga amekuwa ni mtu ambaye ameumia kazini, lakini aliishia kulipwa Sh150,000 na bandari ambako alikuwa anafanya kazi kama kibarua.  Kitendo kitakuwa na jukumu la kufuatilia kwa ukaribu hali za wafanyakazi walemavu, kuangalia kama wanavyotoka vyuoni wanapewa ajira au wanaishia kunyanyapaliwa? Utafiti unaonyesha kuna wanafunzi wengi wanaohitimu masomo wakiwa na ulemavu, hata hivyo hawaonekani kwenye maofisi wakifanya kazi. Wanakwenda wapi? Litakuwa ni jukumu la hicho kitengo.

Ndugu wanahabari,
    Idara ya pili ni
Idara ya fursa/Career Development Department na Mafunzo
 Nimetembea katika nchi tofauti Duniani ikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Mauritius, India, Thailand, Sweden na Marekani…nimeona fursa kadhaa ambazo zimenishawishi kuanzisha idara maalum ya kusaidia wafanyakazi kufahamu fursa zinazoendelea Duniani na hapa nchini. Fursa hizo zitakuwa zinapatikana katika tovuti za TUCTA na ofisi za vyama vya wafanyakazi mikoani. Baadhi ya fursa ni namna gani mtu anaweza kusoma nje ya nchi bila kulipa ada kwa kozi za muda mrefu na mfupi, fursa ya mashirika ambayo yanatoa misaada kwenye sekta mbalimbali.
-Kwa mfano kuna mashirika kama www.nuffic.nl au vyuo ambavyo mtu anaweza kusoma bure bila kulipa chembe ya ada kama www.berea.edu  ya Marekani na fursa nyingine nyingi. Nimegundua Watanzania wengi hawanufaiki sana na fursa hizi. Ziko pia taasisi nyingine zinatoa.

Ndugu wanahabari
Idara hii itakuwa na majukumu ya kutoa elimu kwa wafanyakazi kuzifahamu sheria za kazi, hali kadhalika itakuwa inawasiliana na waajiri ili zaidi ya barua ya ajira au mkataba wanaompa mwajiriwa, ampe pia na  chapisho letu ambalo mwajiriwa anapaswa kupewa siku ya kuajiriwa kwake ili ajue kwa uhakika sheria za kazi zinasemaje; haki ya mwajiriwa kwa mwajiri au ipi na haki ya mwajiri kwa mwajiriwa ni ipi; tutashawishi hili liwe ni suala la lazima. Tutakuwa na vituo maalum vya msaada wa kisheria mikoani kote au kwenye kanda. Tutakuwa na vipindi kwenye televisheni angalau kila mwezi mara kuelezea masuala ya sheria za kazi. Tutaitumia tovuti ya TUCTA  kuwa ya kisasa zaidi.

Ndugu wanahabari
 Kulifufua gazeti la Mfanyakazi ndani ya siku 90 ili liwe sauti thabiti ya wafanyakazi
Haijalishi kama TUCTA itakuwa na fedha au la, nitahakikisha ndani ya siku 126  litakuwa mitaani likiandika habari mbalimbali hasa likitumika kama sauti ya wafanyakazi na yote ambayo yataonekana ni ya maana kwa ustawi wa taifa. Nina uzoefu zaidi ya miaka 20 katika sekya ya habari kama Mhariri, na hata sasa ni Mhariri wa Biashara gazeti la Mwananchi, nitahakikisha tunatafuta fedha ndani na nje ya TUCTA ikiwamo kuwatumia wafanyabiashara kwa kubadilishana msaada kwa matangazo kwa muda, ili hatimaye liweze kuwa mitaani. Ni aibu kubwa kuona nchi ina wafanyakazi wengi, lakini gazeti kama hili la wafanyakazi haliko mitaani.

Ndugu wanahabari
 Kuimarisha uhusiano wa vyama vya ndani na vyama vya nje
Nitahakikisha nafanya mawasiliano na mashirika mengine yakiwamo International Trade Union Confederation, Secretary General Sharan  Barrow na mashirika mengine ili kuona namna gani vyama vya wafanyakazi vya nchini vinanufaika na ushirikiano huo kwa kubadilishana uzoefu na kadhalika mara kwa mara kadri inavyowezekana.

Ndugu wanahabari
Nitatutumia uzoefu wangu wa shughuli za kuwasiliana na vyuo vya nje na uzoefu wangu wa kufanya kazi katika mashirika mbalimbali ya nje kama muwakilishi wao hapa nchini, na  kutembea nchi mbalimbali, kuviunganisha vyama vya ndani vya wafanyakazi, kuwa na ukaribu zaidi na vile vya nje, na pia kujenga uwezekano wa viongozi nchini kwenda nje kupitia ushirikiano huo.

Ndugu wanahabari
Hili linawezekana kwa njia mbili, kwanza kama washirika wetu kwa vile tutakuwa tuna mawasiliano ya karibu na aina ya chama ambacho mtu anatoka, kwa mfano kama COTWU, TTU, TALGWU, TUICO, TAMICO, TEWUTA, DOWUTA, TPAWU, RAAWU, TUGHE, CHODAWU, TRAWU. Nahitaji kuona ofisi za vyama vya wafanyakazi nchini zinakuwa za kuvutia kwa kuzipatia vitendea kazi, kuna mashirika nayafahamu, tunaweza kuyatumia kuwasiliana nayo yakatusaidia kama vile Computer Aid International la Uingereza ambalo hutoa misaada ya computer za aina mbalimbali kwa nchi maskini kama Tanzania (www.computeraid.org). Nje ya hiyo nitakuwa na vikao na viongozi wa chama kimoja badala ya kingine kuangalia namna gani tunaweza kuboresha shughuli za utendaji za ndani na nje hasa kuimarisha rasilimali watu na vifaa. Lengo kubwa la kuomba niwe Rais wa TUCTA ni kuangalia namna gani tunaweza kushirikiana na wafanyakazi na viongozi wa vyama katika kuimarisha wafanyakazi, kwani malalamiko ni mengi. Tutaendeleza mali za TUCTA zikiwamo Chuo cha Wafanyakazi Mbeya na maeneo mengine.
                                                                                          
Ndugu wanahabari
NAMNA GANI HAYA YATAWEZEKANA?
Mkakati wa kuondoa kero zote zilizoelezwa juu utafanikiwa kwa majadiliano yenye ukomo (deadline) na Serikali/waajiri, au kufanya chochote ambacho katiba inaruhusu. Sheria ziko wazi, nitahamasisha zifuatwe na zifahamike. Shida kubwa ninayoiona kwa sasa, wafanyakazi wengi hawajui haki zao pia msaada wa vyama katika kuwasaidia wafanyakazi ni mdogo.

Ndugu wanahabari
Hata hivyo mkakati hasa ni kuangalia TUCTA kwa kushirikiana na vyama shiriki vinafanya nini kuondoa changamoto ambazo sisi wenyewe tunaweza kuziondoa. Uongozi siyo kulalamika, bali kuthubutu kuchukua hatua zinazoweza kuondoa shida zilizoko. Tayari nimeanza kuwasiliana na vyama mbalimbali vya wafanyakazi katika mataifa ya nje ili kuangalia namna gani tunashirikiana kwa maana ya kubadilishana uzoefu nk.

Ndugu wanahabari
Ofisi nyingi za vyama vya wafanyakazi zimechakaa, naangalia uwezekano wa kushirikiana nao katika hili kwa njia ya kutafuta wafadhili wa nje au kubuni miradi itakayosaidia kuondoa hali hiyo; nataka pia maisha ya viongozi wa vyama vya wafanyakazi na wafanyakazi kwa ujumla yabadilike kwa kutumia jitihada hizo nilizozieleza juu, nafahamu vizuri namna ya kusaka wafadhili, kwani ni shughuli ambayo nimekuwa nikifanya kwa muda mrefu kupitia taasisi yangu ya Global Source Watch, niliyoianzisha toka mwaka 2001 ambayo imekuwa ikifanya kazi ya kuwaunganisha watu na vyuo zaidi ya 78 vya nje kama Marekani, Canada, Greece, India, Malaysia nk.

Ndugu wanahabari
Nafahamu kuna vyama vina miradi ya maendeleo, vinawasaidiaje wanachama wao? Nahitaji niwe Rais ili nishirikiane na vyama vya wafanyakazi na wafanyakazi kwa ujumla kuleta tija kwa Watanzania. Tusiwe watu wa kunyoosheana vidole…kila mtu awe chanzo cha mabadiliko anayotaka kuyaona Tanzania! Naamini kila mtu akifanya kazi zake vizuri…Tanzania itakuwa na maendeleo kwa kasi. Wafanyakazi wanahitaji mambo mengi zaidi ya kuhamasishwa migomo, lakini kama tutaamua kugoma, tunapaswa kugoma kwa kumaanisha, hatupaswi kuogopa kutekeleza yaliyo haki yetu.

Ndugu wanahabari
Kwa nafasi nitakayokuwa nayo nitaanzisha semina, makongamano, mijadara itakayokuwa ya wazi na kutoa elimu ya kutosha juu ya haki za wafanyakazi na wajibu wa waajiri kwa wafanyakazi. Hii itasaidia kupunguza migogoro na wafanyakazi watatambua haki zao.

Ndugu wanahabari
Tunatakiwa kuwa sauti ya wafanyakazi hapa Tanzania, TUCTA imelala, tunataka kuikimbiza mchakamchaka,, kuna mambo mengi yanatokea dhidi ya wafanyakazi hapa nchini lakini TUCTA haitoi hata matamko au kutetea wafanyakazi,


Ndugu wanahabari
Natambua changamoto za wafanyakazi, tunataka kuwa na
TUCTA Mpya
Nguvu Mpya
Uongozi Mpya
Sauti Mpya
Umoja Mpya
Maendeleo Mapya
Kwa pamoja tunaweza.

Mungu awabariki!
Dismas Lyassa
Mgombea nafasi ya Urais-TUCTAsimu 0754 49 89 72
 
HOTUBA FUPI KUTOKA KWA JEBRA KAMBOLE, Wakili wa Dismas Lyassa anayefanya Kampuni ya Uwakili ya Law Guards Advocates ya Jijini Dar-es-salaam kwa Waandishi wa Habari.
Ndugu waandishi wa Habari wa vyombo vyote vya Habari,
Ndugu watanzania wengine mliopo hapa,

Shukrani
Tunashukuru sana kwa kuitikia wito wetu, Mungu awabariki sana, Tunamshukuru mwenyezi mungu kwa kutupa afya na sia njema,

Ndugu waandishi wa Habari
Kuna mambo muhimu manne tunataka kuwaeleza watanzania wote, hasa wafanyakazi na viongozi wa vyama vyote vya wafanyakazi
Moja, Ndugu anatimu iliyojipanga makini kuhakikisha TUCTA inarejea na kuwa na Nguvu zaidi, Ni kijana makini mwenye malengo ya kuleta maendeleo ya haraka na kufufua uhai wa TUCTA.

Ndugu Waandishi wa Habari
Napenda kuchukua fursa hii kutoa onyo kwa wanaopanga kutoa rushwa kwenye huu uchaguzi wa TUCTA kuwa tuko makini na hili tumejipanga, tutachukua hatua za haraka za kisheria dhidi yao, ikiwa ni pamoja na kuwaripoti kwenye vyombo husika, Rushwa si kipaumbele utapinga kwa nguvu zetu zote.

Ndugu Waandishi wa Habari
Ndugu Dismas Lyasa pia atasaidia kuanzisha kituo au kushirikiana na mashirika mengine kutoa masaada wa kisheria kwa wafanyakazi wanaofukuzwa makazini kinyume cha sheria. Wafanyakazi wengi wakikumbwa na matatizo wafanyakazi wenzao wanawatenga, vyama vyao vinawatenga, Dismas atahakikisha kuwa TUCTA ni kimbilio lao.

Ndugu Waandishi wa Habari
Ndugu Dismas Lyasa atasaidia kutoa mafunzo ya kisheria kwa wafanyakazi ili waweze kutambua haki zao za msingi, kwa kuendesha semina, makongamano na mijadara itakayotoa elimu na kuibua mijadara kwa wafanyakazi.
CHAGUA DISMAS LYASA KWA TUCTA MPYA, Mabadiliko ni sasa,,,Asanteni

ANGALIZO KWA WATEJA WANAOFANYA MIAMALA YA BIASHARA KUPITIA MITANDAO

0
0
Huduma ya kufanya miamala ya kibiashara kupitia mtandao inafanya maisha ya leo kua rahisi zaidi kulinganisha na maisha ya awali. Hii ni kutokana na uwezekano wa kufanya miamala hiyo popote pale ilimradi tu uwe unamtandao.

 Hili lakua na mtandao kwa Tanzania limeendelea kuwa rahisi hasa baada ya mitandao ya simu kutoa huduma za wavuti inayo sababisha takriban watanzania walio wengi hasa waishio mijini kuweza kupata huduma za mitandao.

Kila teknolojia inachangamoto zake. Na hii ya kufanya miamala kwa msaada wa mtandao pia imekuja na changamoto kadhaa ambazo bado kuna tatizo kubwa la uelewa wa jinsi gani ya kua salama pale miamala ya kibiashara inapofanywa.

Muamala wa kibiashara unapofanyika vibaya unaweza kumgharimu sana mtumiaji  kwa kupoteza fedha na hata kupoteza utambulisho wake ( Hii ni pale taarifa zako kupatikana na wahalifu na kutumika vibaya baadae).

Swala la uhalifu mtandao unao athiri miamala ya kibiashara inayofanywa kwa msaada wa mitandao hapo awali ulikua maarufu sana katika nchi za afrika magharibi hasa Nchi kama Nigeria  na Ghana – Unaweza kusoma taarifa ya nchi hizo na hali ilivyo hadi sasa kupitia taarifa inayosomeka "HAPA"


Aidha Kwa afrika mashariki ikiwemo Tanzania, Hali Imebadilika na Hivi sasa uhalifu huu umeendelea kushika kasi sana ambapo wahalifu mtandao wamekua wakielekeza zaidi nguvu zao kuibia watu wafanyao miamala ya kibiashara kwa msaada wa Mitandao. Hivi karibuni nilipata kuandikia taarifa ya uhalifu mpya unaokua kwa kasi kama inavyosomeka "HAPA" nikifafanua hali halisi nchini hivi sasa kwenye hili.

Hivi karibuni Benki ya CRDB imewaonya wateja wake kuwa makini na baadhi ya mitandao inayoibuka na kulaghai kwa kuwataka wananchi,kutoa taarifa zao muhimu za kibenki,jambo ambalo linahatarisha usalama wa fedha zao zinazohifadhiwa na benki hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dr Charles Kimei alipolizungumzia hili jijini Dar es salaam alifafanua kuwa kumeibuka mchezo kwa baadhi ya mitandao ya kijamii,ikijaribu kuwalaghai wateja kwa kuwaomba taarifa za akaunti zao ili kufanya uhalifu.

Alisisitiza wananchi wanatakiwa kuwa makini na kundi hilo,wasikubali kudanganyika kwa kutoa taarifa zinazohusiana na nyaraka nyeti za benki zao na kusisitiza kuwa ni marufuku kutoa taarifa hizo kwa wafanyakazi wa benki.

Mkurugenzi huyo amesema pamoja na kwamba benki hiyo inawapigia simu wateja wao wakitaka kukamilisha usaili wao kuhusiana na kuingia katika mfumo wa uboreshaji wa huduma za benki hiyo kupitia simu za mkononi unaoitwa Simbaking  watambue kuwa hawataulizwa kutoa taarifa zozote za akaunti.

Kuhusu mbinu zinazotumiwa na wahalifu,Mkurugenzi wa Idara Hatarishi James Mabula amesema huwapigia simu wakijifanya kuwa wakurugenzi ama wafanyakazi wa benki hiyo na kisha kuwaghilibu kwa kutaka kupatiwa namba za siri za akaunti husika.

Kwa upande mwingine, Mitandao ya simu bado haijabaki salama – huduma za  miamala inayofanywa kwa msaada wa simu pia imeendelea kuathirika ambapo kila mara pameendelea kuripotiwa uhalifu katika maeneo hayo.

Nilipata kuandika mwishoni mwa mwaka jana Taarifa ya kingereza inayosomeka hapo chini kuonyesha hali halisi na makabiliano yanayoendelea kudhibiti uhalifu huu mtandao nchini Tanzania huku nikiambatanisha na mapendekezo ambapo juhudi za dhati kuyaendea zinaendela ili kupata taifa salama kimtandao.
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images