Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live

UTENGENEZAJI WA VIDEO YA WIMBO WA KIPI SIJASIKIA WA PROF JAY NA DIAMOND UNAENDELEA CHINI YA NEXT LEVEL

$
0
0
IMG_0217
Msanii mkongwe kwenye game la Bongo Fleva anajulikana kwa jina la Prof Jay leo mchana alikuwa akishoot video yake mpya aliyomshirikisha Diamond inaitwa KIPI SIJASIKIA. Video hiyo iliyokuwa ikishutiwa pale Sinza Makaburini ilipo Mahakama. Video imesimamiwa wa Dir Adam Juma kutoka Next Level
Prof Jay akiwa na Prod P Funk Majani,
DJ Choka akiingia mahakamani

Jini Kabula & DJ Choka
 Credit:Dj Choka

MKE WA MBUNGE WA CHALINZE AGAWA MISAADA KWA FAMILIA ZENYE MAHITAJI MUHIMU CHALINZE

$
0
0
1
Mke wa Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete,Bi. Arafa Mohammed (kushoto) akimkabidhi zawadi ya Vyombo vya ndani na Tende mzee Said Khamis Mnyika wa kijiji cha Changarikwa kata ya Mbwewe kama zawadi ya mbunge huyo katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan kwa familia zenye mahitaji muhimu kutokana na kuishi katika mazingira magumu.ambapo vifaa vya ndani pamoja na Tende zitatolewa kwa familia zipatazo 600 katika kata zote za jimbo hilo.

Huu ni mwendelezo wa shughuli za mbunge huyo katika kuwatumikia wapiga kura wake na kuboresha maisha yao ikiwa ni mikakati yake ya kufikia malengo aliyojipangia kwa kushirikiana na wananchi wa jimbo la Chalinze, Kulia ni Mzee Ahmad Ramadhan mmoja wa wazee wa kijiji cha Changarikwa akingoja kukabidhiwa zawadi zake .(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MBWEWE-CHALINZE)
2
Arafa Mohammed Mke wa Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete(kushoto) akimkabidhi zawadi ya vyombo vya ndani na Tende Mzee Ahmad Ramadhan mmoja wa wazee wa kijiji cha Changarikwa wakati alipotoa zawadi hizo kwa familia zenye mahitaji muhimu katika kata ya Mbwewe jana.
3
Arafa Mohammed Mke wa Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akimkabidhi zawadi hizo Bi.Halima Hassan katika kijiji cha Changarikwa jana.
4
Arafa Mohammed Mke wa Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wazee wa kijiji cha Kwaruhombo Kata ya Mbwewe jana baada ya kuwakabidhi zawadi ya Tende,Wa pili kutoka kushoto ni rehema Zando Diwani viti maalum Bagamoyo.

.
6
Arafa Mohammed Mke wa Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi aliowakabidhi zawadi hizo, baadhi ni viongozi wa kata hiyo na wilaya ya Bagamoyo.
8
Mzee Said Khamis Mnyika kushoto na Mzee Ahmad Ramadhan wa kijiji cha Changarikwa wakiwa na zawadi zao mara baada ya kupokea kutoka kwa Arafa Mohammed Mke wa Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete jana.
9
Arafa Mohammed Mke wa Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akipanga vifaa mbalimbali kwenye ofisi ya CCM kata ya Mbwewe kabla ya kuvikabidhi kwa familia za watu wenye mahitaji muhimu jana.
10
Arafa Mohammed Mke wa Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akimkabidhi zawadi ya vyombo vya ndani na Tende Bw. Abdulrahman Juma wa Mbwewe.
11
Arafa Mohammed Mke wa Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akimkabidhi zawadi hizo Mlemavu Halia Saleh.
13
Baadhi ya akina mama wakiwa na zawadi zao mara baada ya kukabidhiwa
14
Arafa Mohammed Mke wa Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi aliowakabidhi zawadi, wengine ni baadhi ya viongozi wa kata hiyo na wilaya ya Bagamoyo.
16
Arafa Mohammed Mke wa Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akimsikiliza mmoja wa akina mama waliopokea zawadi hizo wakati alipokuwa akitoa shukurani zake kwa Mh. Mbunge Ridhiwani Kikwete.
17
Arafa Mohammed Mke wa Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akihojiwa na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya kukamilisha kazi ya kugawa zawadi hizo kwa baadhi ya familia zinazoisi katika mazingira magumu.

WAZIRI MKUU: KONGAMANO LA DIASPORA KUFANYIKA AGOSTI

$
0
0
 WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali inaandaa kongamano la siku mbili litakalojadili mustakabali wa wana diaspora wa Tanzania kutoka nchi zote duniani ikiwa ni pamoja na kuwakutanisha na makampuni na wafanyabishara mbalimbali.

Ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati alipokutana na Watanzania wanaoishi Uingereza kwenye mkutano uliofanyika ubalozi wa Tanzania jijini London.

Waziri Mkuu alisema kongamano hilo ambalo limepangwa kufanyika Agosti 14-15, mwaka huu, linalenga kuitambulisha rasmi diaspora ama jamii ya Watanzania inayoishi ughaibuni kama wadau muhimu katika kuleta maendeleo nchini Tanzania."Lengo letu hasa ni kutaka jamii ya Watanzania ielewe kwamba tunao Watanzania walioko nje ya nchi kwa maelfu na kuna sehemu mnaweza kuchangia katika maendeleo ya nchi," alisema.

Mbali na hilo, Waziri Mkuu alisema, katika kuitambua rasmi jamii ya wanadiaspora, Serikali itapenda kujua wako, ni wangapi na wanafanya nini ambacho kama Serikali itahitaji ujuzi/utaalamu wao, inaweza kuwapata wapi.

Alisema kongamano hilo limeandaliwa kwa ushirikiano baina ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa pamoja na Umoja wa Wanadiaspora waliorudi nchini waitwao Tanzania Diaspora Initiative (TDI).

“Kongamano hilo litasaidia wanadiaspora kuweza kuona fursa mbalimbali zilizopo nchini, kuvutia wawekezaji wageni kuwekeza Tanzania, kukuza utalii nchini, kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa Diaspora pamoja na kuunganisha wawekezaji wa Tanzania na wawekezaji walioko nje ya nchi.”

Mada kuu ya kongamano hilo ni “Connect, Engage, Inform and Invest” na kaulimbiu yake ni “Nyumbani ni Nyumbani”. Aliwataka wajitokeze kwa wingi kushiriki kongamano hilo ambalo alisema limeandaliwa mahsusi kwa ajili yao na wasipojitokeza kwa wingi halitakuwa na maana.

Akifafanua zaidi kuhusu taswira nzima ya Diaspora, Waziri Mkuu alisema: "Sensa ya mwaka 2012 inaonyesha katika kaya zote zilizohesabiwa Tanzania Bara kuna mtu mmoja au zaidi ambaye yuko nje ya nchi. Hii ni sawa na asilimia 1.2. Kwa upande wa Zanzibar, hali iko tofauti sana. Wao ni mara mbili zaidi yaani kila kaya moja ina watu wawili na zaidi ambao wako nje ya nchi".

Alisema katika matokeo hayo ya sensa, ilibainika kwamba wanadiaspora wanaotoka kwenye kaya za mikoa ya Tanzania Bara wako 116,670 wakati wanatoka Zanzibar wanafikia 304,786. “Idadi ya Watanzania walioko Diaspora ni 421,456 ni karibu sawa na nusu milioni. Idadi hii si ndogo, ni kubwa. Na kama kundi hili lingetumika vizuri, fedha  waliyonayo ambayo wanaituma kutoka nje, ingesaidia sana kuendeleza Taifa letu,” alisema Waziri Mkuu.
                        
Alitumia fursa hiyo kuwaelezea kuhusu mchakato wa katiba ulivyoenda na ulipofikia, maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na uchaguzi mkuu. “Kama Serikali tunajiandaa kwa lolote litakaloamuliwa na Bunge Maalum la Katiba. Kikubwa tunachoomba ni kuwa na mchakato wa amani hadi uchaguzi mkuu ufike,” aliongeza.

Aliwataka wanadiaspora waendelee kuiombea nchi ili ipate wagombea wenye kujali maendeleo ya watu kuliko kitu kingine chochote. “Endeleeni kuiombea nchi yetu ili tupate watu waadilifu, watu ambao wanajali watu wa hali ya chini na wenye kutaka maendeleo ya nchi kwanza kuliko vitu vingine (people who are for pro-poor development).

Endeleeni kuiombea nchi yetu amani, tuendelee kumuombea Rais Kikwete ili amalize kipindi chake vizuri na akabidhi kijiti kwa mwingine salama, alisema.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, JULAI 14, 2014.

WASHIRIKI WA TAMASHA LA USIKU WA MATUMAINI WATAMBIANA

$
0
0
Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo (katikati), ambaye kampuni yake inaandaa tamasha hilo, akizungumza kwenye mkutano huo.

WASHIRIKI wa ‘Tamasha la Usiku wa Matumaini’ leo wametambiana kwenye mkutano na vyombo vya habari uliofanyika Hoteli ya Atriums iliyopo Sinza, Afrika-Sana jijini Dar es Salaam.
Katika mkutano huo wa tamasha hilo la burudani mabondia, Mada Maugo na Thomas Mashali, kila mmoja amejitapa kumchakaza mwenzake katika pambano hilo huku Mbunge wa Nzega, Dkt. Hamis Kigwangala, aliyewawakilisha wabunge wa timu ya Simba alijitapa timu yake kuwamaliza Yanga.
Msanii wa Filamu za Maigizo, Issa Mussa 'Clouds 112' ambaye katika tamasha hilo atachapana makonde na Jacob Steven 'JB' katika mchezo wa 'boxing' wote wameahidi kutifuana 'kinomanoma'.
Rais na mwakilishi wa timu ya Bongo Muvi Unity, Steve Mengere 'Steve Nyerere',  alitamba timu yake kuigaragaza timu ya Bongo Fleva ambapo mwakilishi wake, Haruni Kahena 'Inspector Haruni',  alisema wao ndio watakaoibuka kidedea na kuwapiga Bongo Muvi Unity kwa mabao 7-1 kama walivyofanywa Wabrazil na Ujerumani wiki iliyopita kwenye nusu fainali za Kombe la Dunia.
Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika Agosti 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambapo huu utakuwa ni mwaka wa tatu mfululizo kufanyika likiandaliwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd.  
(HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS / GPL. )
Mkutano ukiendelea.
Sehemu ya mapaparazi waliofika kwenye tukio hilo.
Rais wa Chama cha Ngumi za Kulipwa nchini (T.P.B.O) Yasin Abdallah (katikati) ambao ndiyo wasimamizi wa pambano la Maugo na Mashali katika tamasha hilo,  akizungumzia pambano hilo.
Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (mwenye miwani) na Mkurugenzi Chuo cha Uandishi wa Habari, Biashara na Utawala cha Mlimani kilichopo Mbezi Kwa-Msuguri jijini Dar, Hassan Ngoma (kushoto kwa Mrisho), wakifuatilia kinachoendelea.

 
Khalid Chokoraa wa Bendi ya Mapacha Watatu akifuatilia kinachoendelea.
Mwakilishi na Rais wa Bongo Muvi Unity, Steve ‘Nyerere’, akielezea jinsi watakavyowagaragaza wasanii wa Bongo Fleva kwenye pambano la soka.
Mwakilishi wa timu ya Bongo Fleva, Inspector Haruni, akijibu mapigo kwa kueleza jinsi watakavyowararua Bongo Muvi Unity.  Kushoto ni mratibu wa tamasha hilo, Luqman Maloto, na Eric Shigongo.
Bondia Mada Maugo akijitapa kumchapa mpinzani wake, Thomas Mashali 'Simba Asiyefugika'.
Mashali akimjibu Maugo na kujitapa kuendeleza kichapo.
Mbunge Hamisi Kigwangala anayeiwakilisha timu ya wabunge wa Simba akieleza jinsi walivyojiandaa kuwaadabisha wabunge wa Yanga.
Msanii wa filamu, Jacob Steven 'JB', ambaye atachapana na msanii mwenzake, Issa Mussa 'Clouds 112', akichimba mkwara jinsi atakavyomkalisha msanii huyo.
Shigongo ‘akiwakutanisha’ mabondia wenye upinzani mkali, Mashali (kushoto) na Maugo (kulia).
Clouds 112 (kushoto) akimchimbia mkwara JB ambaye aliishia kumuangalia kidharau na kusema anasubiri siku ya Agosti 8 katika Uwanja wa Taifa.
Sehemu ya wanahabari wakipata maelezo. 

MKUU WA MKOA WA RUKWA ENG. STELLA MANYANYA AKUTANA NA WAFANYABIASHARA WA MNADANI MKOANI RUKWA LEO NA KUSIKILIZA KERO ZAO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (kulia) akizungumza na wafanyabiashara wa mnadani Mkoani Rukwa mapema leo tarehe 14/07/2014 katika uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga. Wafanyabiashara hao waliomba kuonana na Mkuu huyo wa Mkoa kumueleza kero zao ikiwemo tukio la hivi karibuni la tarehe 11/07/2014 la kuvamiwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi na kupelekea wafanyabiashara tisini (90) kuporwa simu na fedha katika njia ya Muze. Wafanyabishara hao wamemuomba Mkuu huyo wa Mkoa kuwasaidia katika ulinzi kwenye biashara zao kwani mitaji mingi waliyonayo ni fedha za kukopa ambazo zinahitaji marejesho.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya baada ya kupokea kero za wafanyabiashara hao wa mnadani (hawapo pichani) amelitaka jeshi la Polisi Mkoani Rukwa kuandaa utaratibu maalum wa kuwasaidia wafanyabiashara hao ikiwemo kuwapatia mafunzo maalumu ya mgambo ya kujilinda wao na mali zao. Amelitaka jeshi hilo kukaa na uongozi wa wafanyabiashara hao kuona ni jinsi gani watamaliza kero zilizopo ikiwepo tishio la majambazi na usumbufu wa kwenye malori. Pia amewataka wafanyabiashara hao kutojaza mizigo na abiria kupita kiasi kwenye malori jambo ambalo ni hatari kwa maisha yao. 
Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika wa Wafanyabiashara wa mnadani Mkoani Rukwa Ndugu E. Mazwile akizungumza katika kikao hicho ambapo amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwa kutenga muda wake na kamati yake ya ulinzi na usalama ya Mkoa kwa kufika na kukutana na wafanyabiashara hao na kusikiliza kero zao. 
Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Ndugu Symthies Pangisa (kushoto) akiwatambulisha viongozi mbalimbali walioambata na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa katika kikao hicho.
Sehemu ya wafanyabiashara hao wa mnadani.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com)

VIJANA WATAKIWA KUDUMISHA AMANI

$
0
0
 Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma akimvisha kofia ya ukamanda Profesa Peter Msolla baada ya kuteuliwa kuwa Kamanda wa UVCCM wilaya ya Kilolo sherehe zilizofanyika katika viwanja vya Kidabaga.

 Mbunge wa jimbo la Kilolo,Profesa Peter Msola akila kiapo cha kuwa kamanda wa UVccm mbele ya Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma.
 Mbunge wa jimbo la Kilolo,Prof Peter Msola akiwaapisha makamanda wa vijana ccm katika wilaya ya Kilolo sherehezz ilizofanyika katika uwanja wa Kidabaga.

Na Denis Mlowe,Kilolo

MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana  Chama  cha Mapinduzi (CCM)  Taifa, Sadifa Juma Hamis ametoa rai kwa   vijana kuepuka kutumika katika kuvuruga amani na utulivu uliopo nchini Tanzania kwa kutumika na baadhi ya vyama vya siasa na kuhatarisha amani  ya Taifa.
 
Sadifa alitoa rai hiyo mwishoni mwa wiki katika  viwanja  vya Kidabaga wakati akiwahutubia wananchi  wa Kidabaga kata ya Bomalang’ombe wilayani Kilolo wakati wa kusimikwa kwa mbunge wa jimbo la Kilolo Prof. Peter Msola kuwa kamanda wa umoja wa vijana CCM wa wilaya ya hiyo.
Alisema kuwa amani  ambayo tunajivunia  ipo  siku  itatoweka  na iwapo  vyama  vya siasa  vitaacha kufanya kazi yake ya  kisiasa kwa kunadi  sera  za vyama  vyao na kueneza  chuki  dhidi ya  serikali kama ilivyo  hivi  sasa kwa baadhi ya  vyama kuendesha siasa  za  chuki na  kuwatumia vijana kuvuruga amani yetu.
 
" Nawaombeni  sana vijana  wa   kuendelea   kuonyesha mfano  kwa  vijana  bora katika kudumisha amani iliyopo na kamwe msije iga siasa vya vyama  vya upinzani siasa ya  kufanya  vurugu ..... hiyo ni siasa mbaya  sana na itakuja  kuliweka Taifa katika umwagaji damu ambao hakika itakuwa ngumu sana kuweza kuishi tena kama mwanzo” alisemaSadifa
 
Alitoa mfano kuwa kuna ushahidi kwa nchi jirani unaonesha madhara ya kuichezea amani na kuongeza kuwa ni rahisi sana kupoteza amani na umoja lakini ni vigumu sana kuirejesha na kuwataka vijana kuacha kuandamana kwa kuiga tu kwa kuwa umeambiwa fanya jambo hilo
 
Mbali ya kuwataka  vijana kuacha kutumiwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa Sadifa aliwataka viongozi  wa vyama  vya siasa kutowatumia vijana hao  katika kuvuruga amani pia aliwataka vijana kutokubali siasa  chafu zenye chembe ya vurugu kwa watanzania na kuongeza kuwa sehemu yoyote yenye amani na utulivu, yapo maendeleo kwa sababu wananchi wanafanya shughuli za maendeleo kwa uhuru
 
 Kwa upande wake Kamanda mpya wa umoja wa vijana Ccm wilaya ya Kilolo, Prof Peter Msola aliwataka vijana kufanya kazi kwa bidii kwa lengo la kuondokana na umaskini katika wilaya hiyo na kuwataka kushirikiana katika kudumisha amani iliyopo nchini Tanzania.
 
Alisema moja changamoto kubwa inayowakabili vijana na ambayo kwa kushirikiana nao atahakikisha inafanyiwa kazi kwa kutumia fursa mbalimbali zinazowazunguka ni ajira kwa kuwa fursa hizo zinaweza kuwa  katika sekta ya biashara, kilimo na ushauri kwa kupitia vikundi vya maendeleo.
 
Alisema ardhi na hali ya hewa nzuri ya wilaya ya Kilolo inaweza kuwaongezea fursa ya ajira vijana wa wilaya hiyo.

Naibu Waziri wa Uchukuzi atembelea Shirka la Ndege Tanzania (ATCL)

$
0
0
 Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba (kulia), akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Mr. Salim Msoma wakati alipotembelea shirika hilo mwishoni mwa wiki kuongea na Bodi, Menejiment na wafanyakazi wa Shirika hilo. Nyuma ya Mr Msoma ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo, Kapteni Milton Lazaro.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati wa kikao chake na wajumbe wa bodi na menejiment ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), wakati alipoongea nao mwishoni mwa wiki katika ofisi za Makao ya Shirika hilo.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba, akisisitiza jambo wakati alipoongea na Bodi, Menejimenti na wafanyakazi wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Naibu Waziri aliwasisitiza watumishi hao kufanya kazi kwa bidii na kurudisha sifa ya shirika hilo. Picha na kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi

AIRTEL YATOA FUTARI KWA WATOTO YATIMA MKOANI MWANZA

$
0
0

Meneja  Biashara Kanda ya Ziwa Raphael Daudi (wa tatu kutoka kulia) akiwa na Meneja wa Masoko Kanda Emanuel Raphael (wa kwanza kulia) pamoja na  Meneja wa Airtel mkoa wa Mwanza David Wankulu wakikabidhi msaada wa chakula cha kufuturisha katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani  kwa Katibu mkuu wa Jumuiya ya Kuendeleza Quran na Suna Tanzania (JUQUSUTA)  Twaha bin Bakari Utari (wa tano kutoka kulia) akiwa katika picha na wadau wengine wa Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza.
Vijana wa Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza wakishusha vyakula toka katika gari la wadau wa Airtel ambao wamedhuru katika kituo hicho kwaajili ya kusababisha tabasamu kwa watoto hao kwa kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani..
Upakuaji ukiendelea.
Ni sukari, chumvi, majani ya chai, mchele, sabuni, mafuta, unga wa sembe, unga wa ngano, juice za matunda na vinginevyo kama sehemu ya msaada wa chakula toka Airtel Tanzania kwa Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza. 

SERA YA DIASPORA IKO MBIONI KUKAMILIKA - PINDA

$
0
0
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema rasimu ya Sera ya Diaspora iko kwenye hatua za mwisho za maandalizi na muda si mrefu itaingizwa kwenye utaratibu wa Kiserikali ili hatimaye iweze kuwasilishwa kwenye Baraza la Mawaziri.

Akizungumza na Watanzania wanaoishi Uingereza kwenye mkutano uliofanyika ubalozi wa Tanzania jijini London, mwishoni mwa wiki, Waziri Mkuu alisema mchakato wa kuandaa rasimu hiyo ulihusisha wadau wengi kwa kadri ilivyowezekana ili kupata wigo mpana wa suala zima la diaspora.

“Katika hatua za awali, mbali ya ofisi yangu na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, tuliwashirikisha kwa karibu Umoja wa Wanadiaspora waliorudi Tanzania (Tanzania Diaspora Initiative) na wanadiaspora kutoka Uingereza, Marekani, China, Oman, India na Afrika Kusini ili kupata uzoefu wao kutokea huko waliko,” alisema na kuongeza:

“Baadaye tukawapelekea wataalamu ambao ni Profesa Samuel Wangwe wa REPOA, Profesa Joseph Semboja wa Uongozi Institute na Profesa Faustine Kamuzora wa Chuo Kikuu cha Mzumbe kila mmoja kwa wakati wake na kuwaambia waichanechane kadri wawezavyo na kisha watupe mrejesho wao.”

Aliwataja wadau wenginu muhimu waliohusishwa kwenye kuichambua rasimu hiyo kuwa ni Shirika la Kimataifa linaloshughulika na Wahamiaji (International Organisation for Migration –IOM) ambao wamebobea katika masuala ya wahamiaji katika nchi mbalimbali duniani. 

“Kwa mtazamo wangu hii rasimu imekaa vizuri kwa sababu tumejitahidi kugusa kila eneo ambalo kwenu lilikuwa na umuhimu wa kipekee. Sasa hivi imeshawekwa vizuri kimfumo na inasubiri iingie katika utaratibu wa kiserikali,” alisema.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, JULAI 14, 2014.

TBC YAFANYA HAFLA YA KUHITIMISHA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA 2014, DAR

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Clement Mshana (kulia) akiwakaribisha wageni walioalikwa katika hafla ya kuhitimisha michuano ya kombe la dunia 2014 iliyofanyika jana Julai 12, 2014 katika ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante ole Gabriel, akiongea machache katika hafla ya kuhitimisha michuano ya kombe la dunia 2014 iliyofanyika jana Julai 12, 2014 katika ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante ole Gabriel, akimkaribisha Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe. Juma Nkamia ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuhitimisha michuano ya kombe la dunia 2014 iliyofanyika jana Julai 12, 2014 katika ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam. 
Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia akiongea akiongea katika hafla ya kuhitimisha michuano ya kombe la dunia 2014 iliyofanyika jana Julai 12, 2014 katika ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam. 


Mshehereshaji wa Hafla hiyo Elisha Elia akiongea machache.
Rais wa Bongo Movie, Steve Nyerere akitoa shukrani zake kwa niaba ya wasanii katika hafla ya kuhitimisha michuano ya kombe la dunia 2014 iliyofanyika jana Julai 12, 2014 katika ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Ommy Dimpoz akiongea machache hafla ya kuhitimisha michuano ya kombe la dunia 2014 iliyofanyika jana Julai 12, 2014 katika ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam. 

Kutoka kushoto ni Mboni Masimba, Mbunge wa Temeke Mh. Abbas Mtemvu pamoja na mchambuzi wa Mpira Manara katika hafla ya kuhitimisha michuano ya kombe la dunia 2014 iliyofanyika jana Julai 12, 2014 katika ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam. 
Wasanii walioalikwa wakipakua chakula (futari) iliyoandaliwa katika hafla hiyo.
Wasanii mbali mbali walioungana katika hafla hiyo wakipata futari.
Wafanyakazi wa TBC hawakuwa nyuma kujipongeza kwa kazi nzuri waliyoifanya.
Wasanii wakifurahia jambo na Mchambuzi wa Mpira, Mw. Kashasha.
Msanii JB akiongea na Mchambuzi wa Mpira wa Miguu, Mwl. Kashasha.
Wasanii wakijadili mambo.
Dokta Cheni akishow love.
Mw. Kashasha nae alikuwepo.
Meza kuu kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Clement Mshana, Mbunge wa Temeke Mhe. Abbas Mtemvu, Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia pamoja na Mdau mkubwa wa Michezo, Juma Kipingu wakifuatilia mpira wa fainali ya kombe la dunia 2014, kati ya Argentina na Ujerumani
Wasanii wakifuatilia kwa makini mpira huo.
Wafanyakazi wa TBC nao hawakuwa nyuma.
Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wakipongezwa kwa kazi waliyoifanya.
Picha ya pamoja ya viongozi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)  na wakurugenzi wa bodi. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.

SHULE YA ARUSHA MODERN YAADHIMISHA SIKU YA MICHEZO

$
0
0
Na.Ashura mohamed -arusha

Katika hali ya kukuza michezo mashuleni na kuinua vipaji vya wanafunzi shule ya Arusha Modern imeendesha mashindano maalum kwa wanafunzi wa shule hiyo kwa upande wa msingi na sekondari ikiwa ni kuadhimisha siku ya michezo shuleni.

Katika mashindano hayo yalihusisha makundi mbali mbali kutoka shule ya msingi na sekondari ya Arusha modern, ambapo kila kundi lilishiriki michezo mbalimbali ikiwemo Mpira wa miguu, mpira wa mikono, mpira  wa pete, riadha, kukimbia kwenye magunia huku wazazi na walimu kushindana kuvuta kamba.

Kwa upande wa wanafunzi wa shule za awali wakishindana kujaza maji kwenye chupa ya mililita 250, kupasua mapulizo sambamba na mashindano ya kuzunguka viti ambapo kila kundi  kupatiwa point za maksi walizopata.

Mashindano hayo yalihusisha kundi la Mandela team, Babro team, Nyerere team pamoja na Einstean team ambapo kundi la Mandela lilifanikiwa kuzibwaga makundi pinzani 3 kwa kunyakua point 173 ikifuatiwa na Babro ikinyakua point 171 huku akijipatia point 135 na kundi la Eistean ikijifuta machozi kwa point 110.

Akizungumzia mashindano hayo, mkuu wa shule ya Msingi Arusha Modern Philip Wasike alisema kuwa siku hii wameamua kuiadhimisha kwa mashindano hayo kutokana na kutambua umuhimu wa michezo hasa kwa mwanafunzi anaetumia muda mwingi kusoma hivyo ni lazima apate pia muda wa kupumzisha akili ili aweze kuelewa na kufaulu yale anayoyasoma.

Maadhimisho hayo yaliyokuwa na kauli mbiu “michezo ni ajira” Wasike Alisema kuwa mbali na hilo mashindano hayo wanakuwa wanaangalia vipaji vya wanafunzi wao ili kuweza kuunda timu za kichezo mbalimbali na kuzishindanisha na timu za michezo hiyo kutoka katika shule zingine za hapa jijini Arusha na mikoa mingine kwa ujumla.

“Kikubwa tunachokifanya hapa ni kuangalia vipaji vya wanafunzi wetu ili kuunda timu za mashindano na shule zingine ambapo tumeshapata baadhi ya majina ya wanafunzi wanaofaa katika michezo mbalimbali hivyo tunachokifanya sasa ni kupeleka barua za maombi katika shule zingine tuwe na mashindano ya hapa na pale angalau mara moja kwa wiki au mwezi” Alisema wasike.

Kwa upande wa wadhamini wakuu wa mashindano hayo, Ally Ramoudh kupitia kampuni ya Pepsi alisema kuwa kutokana na mvuto wa mashindano hayo na msisimko wake kwa wanafunzi na kuvuta umati mkubwa wa wakazi wa eneo hilo kampuni ya Pepsi itaendelea kudhamini siku hiyo ya michezo ili kufanikisha kukuza vipaji vya wanafunzi hao na kufananishwa na wachezaji maarufu kitaifa na kimataifa kwani shuleni ndio sehem ya nzuri ya kuonyesha kipaji na kukuzwa kwa urahisi.

KATIBU MKUU WA UVCCM AFANYA ZIARA MKOA WA ARUSHA

$
0
0

six14Katibu mkuu wa UVCCM Taifa na mjumbe wa baraza la katiba Sixtus Mapunda akiendelea na ujenzi katika uwanja wa michezo wa st.Benjamin uliopo Usa river kwa ufadhili wa edinburgh global partnerships na YES Tanzania katika ziara yake ya kwanza ya kikazi ya siku tatu katika Mkoa wa Arusha
six16Aliyevalia sweta ni mkuu wa Wilaya ya Arumeru Nyirembe Munasa akisalimiana na viongozi wa chama Wilayani hapo ambapo mradi huo umetekelezwa kulia ni Katibu mkuu UVCCM Sixtus Mapunda akifurahia jambo
six17Katibu mkuu wa UVCCM Taifa na mjumbe wa baraza la katiba Sixtus Mapunda akipokelewa na viongozi na wa chama hicho mapema kabla ya kutembelea miradi
 six12Katibu mkuu wa UVCCM Taifa na mjumbe wa baraza la katiba Sixtus Mapunda akimkabidhi cheti mmoja wa wa vijana waliojitolea katika mradi wa ujenzi wa kiwanja cha michezo
six11Hapa viongozi na wadau wakishuhudia jiwe la msingi katika kiwanja hicho cha michezo kilichozinduliwa rasmi na Katibu mkuu wa UVCCM Taifa na mjumbe wa baraza la katiba Sixtus Mapunda
six10Katibu mkuu wa UVCCM Taifa na mjumbe wa baraza la katiba Sixtus Mapunda akimkabidhi cheti mshindi wa mbio za pikipiki greengad maarufu kwa jina la Mjusi.
six9Katibu mkuu wa UVCCM Taifa na mjumbe wa baraza la katiba Sixtus Mapunda akizindua shina la Ngarasero

 
six8Mwenyekiti UVCCM Mkoa wa Arusha Robson Meitinyiku akiongea katika mkutano wa hadhara katika kata ya Leguruki Mkoani Arusha ambapo aliwahimiza vijana wadumishe upendo,Amani katika Nchi yao huku akiwataka kuepuka uvinjifu wa Amani
six6six5Katibu mkuu wa UVCCM Taifa na mjumbe wa baraza la katiba Sixtus Mapunda akimkabidhi cheti mmoja wa wadau waliodhamini maradi wa uwanja wa michezo kutoka kamapuni ya YES
sixx18Zaidi ya Wanachama wapya 27 kutoka chama cha demokrasia na maendeleo chadema waliochukua rasmi kadi za CCM wakionyasha kadi zao mara baada ya kukihama chama hicho
six20Umati wa wananchi waliojitokeza kumsikiliza Katibu mkuu wa UVCCM Taifa na mjumbe wa baraza la katiba Sixtus Mapunda
six21
six 19Katibu mkuu wa UVCCM Taifa na mjumbe wa baraza la katiba Sixtus Mapunda akimkabidhikadi mwanachama mpya kutoka chadema
six22six20
six4
six3Katibu mkuu wa UVCCM Taifa na mjumbe wa baraza la katiba Sixtus Mapunda akimkabidhicheti mkurugenzi wa YES Tanzania Samwel Mpenzu
six2
six1Katibu mkuu wa UVCCM Taifa na mjumbe wa baraza la katiba Sixtus Mapunda akiongea baada ya uzinduzi wa uwanja pamoja na mashina katika kata ya Ngarasero Mkoa Arusha katika ziara yake ya kwanza ya kikazi toka ateuliwe (Pamela Mollel jamiiblog)

Sekeleti kumbeba Rose Muhando

$
0
0

MWIMBAJI mahiri wa muziki wa Injili, Ephraim Sekeleti, atatumbuiza kwenye uzinduzi wa albamu ya Kamata Pindo la Yesu ya Rose Muhando Agosti 3, mwaka huu.

Taarifa kwa vyombo vya habari aliyoitoa Rose Muhando jana, ilieleza kuwa tayari Kampuni ya Msama Promotions inayodhamini uzinduzi wake imeshamalizana na mwimbaji huyo.

“Nashukuru sana Msama Promotions kwa udhamini wao, na jana (juzi) wamenihakikishia wameshamalizana na Sekeleti na amekubali kuja kuungana nami katika uzinduzi wangu.

“Ni msanii mwenye uwezo mkubwa, ambaye mashabiki wangu watapenda kuja kumuona jukwaani,” alisema mwimbaji huyo na kuzitaja baadhi ya nyimbo maarufu za Sekeleti kuwa ni Uniongoze na Kidonge cha Yesu.

Uzinduzi wa albamu hiyo utafanyika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam Agosti 3, mwaka huu na kisha Agosti 10 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.Waimbaji wengine ambao hadi sasa wameshathibitisha kushiriki uzinduzi huo ni Upendo Nkone, John Lissu na Bonny Mwaitege, huku wasanii wengine mahiri wakitarajiwa nao kuthibitisha ushiriki wao siku za usoni.

INTRODUCING Heri Muziki - Nakukumbukaga Video

MITUMBA GRADE ONE KUTOKA CANADA

$
0
0
Mwezi mtukufu wa Ramadhan, umebakiza takribani majuma mawili tu. Kwa maana hiyo, maandalizi ya sikukuu ya Eid-El-Fitri tayari yameshaanza. Eid huwa ni wakati wa furaha na mara nyingi huenda sambamba na kujumuika na ndugu,jamaa na marafiki kufurahi na kutukuza yale yote aliyotujalia Mwenyezi Mungu. 

 Palipo na mkusanyiko wa watu, huwa pia pana "mtoko". Kila binadamu hupenda kupendeza. Wenzetu wa jinsia ya kike,hupenda sio tu kupendeza bali pia kusifiwa kwamba "wamependeza". Kupendeza, kwa bahati mbaya, hakutokei kama ajali. Kunahitaji maandalizi. Sharti manunuzi yafanyike. Ili nisije onekana mwenye choyo, napenda kukushirikisha katika hili. Kuna punguzo maalumu kabisa kuelekea sikukuu ya Eid-El-Fitri. Punguzo la nini? Tizama hapa chini. Soma.Usiache kumwambia na mwenzio. Mitumba Bei Rahisi,Jumla na Rejareja Tanzania

WAZIRI LAZARO NYALANDU AKUTANA NA TAASISI ZA UHIFADHI WANYAMAPORI JIJINI NEW YORK

$
0
0
 Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Waandamizi wa Taasisi ya Vulcan ya nchini Marekani  Bw. Dave Stewart (kushoto) na Bi. Lauren Ryder, inayojihusisha na masuala ya kuidadi tembo katika nchi 18 barani Afrika ikiwemo Tanzania, baada ya kufanya mazungumzo maalum ya ushirikiano yaliyofanyika katika jiji la New York nchini Marekani jana.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu  akiagana na Bw. Dave Stewart kutoka Taasisi ya Vulcan inayojihusisha na masuala ya kuidadi tembo katika nchi 18 barani Afrika ikiwemo Tanzania mara baada ya kumaliza mazungumzo nao  jana jijini New York nchini Marekani.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu  (watatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Waandamizi wa Taasisi ya inaundwa na Wanajeshi Wastaafu wa jeshi la Marekani walioanzisha umoja wao ujulikanao kama (VETPAW)kwa ajili ya kusaidia Uhifadhi wa Wanyamapori barani Afrika mara baada ya kumaliza mazungumzo baina yao jana jijini New York, Marekani.  Kushoto ni Balozi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu  akizungumza na Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi  mara baada ya kukamilika kwa kikao jana baina ya Waziri Nyalandu na ujumbe wake pamoja na taasisi mbalimbali za uhifadhi jijini New York, Marekani. Kati ni Katibu wa Waziri Bw. Imani Nkuwi.

AJALI YA MAGARI MAWILI NA PIKIPIKI YAPOTEZA MAISHA YA WATU WAWILI

$
0
0
Gari aina ya Range Rover lenye likiwa limeharibika vibaya baada a kugongana uso kwa uso na gari dogo 
Gari dogo aina ya Toyota Corolla lilikiwa limeharibika vibaya baada ya kugongana uso kwa uso na Range Rover katika makutano ya barabara ya Arusha/Moshi jirani kabisa na kipita shoto(Keep left) cha Arusha

Mifuko maalumu ya kuzuia abiria asiumie wakati wa ajali ikiwa imefumuka baada ya ajali .
Pikipiki ikiwa chini ya gari aina ya Range Rover baada ya kugongwa.
Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo wakitizama pikipiki iliyokuwa chini ya gari hiyo
Hivi ndivyo pikipiki inavyoonekana ikiwa chini gari.
Askari polisi wa kikosi cha usalama barabarani wakichukua vipimo mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo ambayo watu wawili wanadaiwa kufariki dunia papo hapo huku wengine watatu wakijeruhiwa vibaya akiwemo dereva bodaboda aliyevunjika miguu.
Baadhi ya wanannchi wakitizama ajali iliyotokea katika makutano ya barabara kuu ya Moshi/Arusha na ile ya kuelekea ofisi za mkuuu wa wilaya ya Moshi.Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.

MRADI WA MIL 700/- WA MATUMIZI YA RASILIMALI ENDELEVU USAMBARA WAANZA

$
0
0
DSC_0008
Afisa Mradi wa uchumi wa kijani ndani ya hifadhi hai (GEBR) Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko, (kulia) akisalimiana na Mtendaji wa Kata ya Mnyuzi, Bw. Gosbert Ishengoma mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za kata hiyo wilayani Korogwe. Katikati ni Afisa Usafi na Mazingira wa Wilaya ya Korogwe, Bw. Frederick Linga.

==========  =======  ========

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limezindua mradi wa mamilioni katika eneo la hifadhi Usambara Mashariki, kwa mafunzo kwa wakazi waliomo na wanaozunguka hifadhi ya Usambara Mashariki.

Mradi huo ambao umelenga kuwainua wanavijiji kiuchumi huku wakitunza mazingira umepata fedha kutoka Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo la Kimataifa la Korea ( KOICA). Mradi huo unaotekelezwa katika vijiji 19 vinavyozunguka Hifadhi Hai ya usambara mashariki ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa uchumi wa kijani ndani ya hifadhi hai(GEBR).

Mradi huo utawawezesha wananchi kwenye vijiji hivyo kutumia raslimali zao kwa namna endelevu. Mradi huo unaojulikana kama “Green Economy in Biosphere Reserves (GEBR)”,wenye thamani ya shilingi milioni 700 utapunguza ukataji miti na kulinda hifadhi kwa kutumia raslimali kwa busara zaidi.

Mradi huo unatarajiwa kuwezesha wananchi wa maeneo hayo kupunguza umaskini kwa kutumia raslimali zilizopo kwa busara na wakati huo huo kuhifadhi mazingira.
DSC_0012
Afisa Mradi wa uchumi wa kijani ndani ya hifadhi hai (GEBR) Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko, akisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi za kata ya Mnyuzi mara baada ya kuwasili wilayani hapo kwa ajili ya kuzindua mradi wa mamilioni katika eneo la hifadhi Usambara Mashariki, na kuendesha mafunzo kwa wakazi waliomo na wanaozunguka hifadhi ya Usambara Mashariki.

Baadhi ya shughuli zitakazofanyika katika mradi huo ni mafunzo ya kuwawezesha wananchi kufanya shughuli za kiuchumi katika hifadhi ambayo yalifunguliwa leo na Mjumbe wa Kamati ya Hifadhi Hai Tanzania, Joseph Kigula. Mafunzo hayo kwa vijiji vitatu ambayo yanaendeshwa na EUBR na Wizara ya Mali Asili na Utalii wanavijiji watafunzwa masuala ya menejimenti ya biashara, soko, uhasibu, fedha, ujasiriamali mazingira na elimu ya hifadhi.

Elimu hiyo inatarajiwa kupanua uelewa wanakijiji kuhusu mahusiano ya biashara na hifadhi ya mazingira na kujenga uwezo wa ujasairiamali.

Mafunzo mengine mawili yanatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka.
Mmoja wa wajasirimali, Jason J Drew alisema kwamba mazingira yamekuwa yakiathirika sana katika shughuli za kiuchumi na watu kuachana na dhana ya hamsini kwa hamsini. UNESCO imesema ni matumaini yake kwamba katika mradi huu, mazingira ya maeneo hayo yataendelea kuneemeka huku wananchi wakifanya shughuli za kiuchumi.
DSC_0023
Baadhi ya wanakijiji wa kata ya Mnyuzi wakitoa burudani kabla ya ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo yaliyoanza jana kwenye hoteli ya SB Palace kata ya Mnyuzi wilayani Korogwe.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi huo, Mjumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Hifadhi Hai Tanzania, Bw. Joseph Kibula alisema kuwa mradi huo ambao unatekelezwa katika maeneo ya Usambara Mashariki hapa nchini utawezesha wananchi wanaoishi kwenye vijiji vinavyozunguka hifadhi kutunza mazingira lakini kujiendeleza kiuchumi.

Kibula alisema nia kubwa ya mradi ni kukuza uchumi wa wananchi kwa kupitia njia zilizoboreshwa ambazo haziathiri rasilimali za misitu sambamba na kuanzisha biashara za kijani kwa ajili maendeleo endelevu ya wakazi wa maeneo hayo.
 
“Matarajio ni kuzijengea uwezo jamii za vijiji zenye bidhii ya kuhifadhi bioanuwai na kupunguza athari dhidi ya rasilimali za misitu …ili ziweze kutafuta riziki kwa maendeleo endelevu”,alisema Kibula.
Kwa upande wake, Afisa Mradi Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko, alisema wanatarajia elimu hiyo ilete mabadiliko chanya kwa wananchi kaika kupunguza umaskini na kufanya biashara za kijani kwa maendeleo endelevu ya jamii wa Hifadhi Hai ya Usambara Mashariki.
Ko alisema kuwa kutokana na ushahidi wa huduma zitokanazo na bioanuwai,biashara ya kijani ni zana itakayowezesha kuhifadhi na kuleta maendeleo endelevu kupitia mgawanyo wa maslahi unaolingana.
DSC_0038
Afisa Mradi wa uchumi wa kijani ndani ya hifadhi hai (GEBR) Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko akijumuika na baadhi ya wanakijiji wa Mnyuzi kucheza ngoma ya asili aina ya Mdumange kabla ya kufungua mafunzo hayo.
“Mradi huu unatoa fursa kwa jamii zilizopo na zilizopakana na hifadhi hai nchini Tanzania katika njia ya mazingira rafiki na uchumi wenye neema hususan Hifadhi Hai ya Usambara Mashariki…tunaamini kwa kupitia mradi huu na elimu hii mtaweza kujipatia utajiri mkubwa kwa kupitia shughuli za kiuchumi mtakazozifanya”,alisisitiza Mwakilishi huyo wa Unesco na Koica.
Nao baadhi ya wananchi waliopewa elimu hiyo walishukuru na kusema kuwa itawasaidia kupata mbinu za kufanya shughuli za kiuchumi kwa kutumia rasilimali zinazowazunguka.
“Katika utunzaji na uhifadhi wa mazingira tunafanya shughuli mbalimbali ikiwemo ufugaji wa nyuki,vipepeo na hata shughuli za mikono kwa akina mama hivyo elimu hii ya ujasiriamali itatuwezesha sana kujiinua kiuchumi na kuondokana na umaskini”,alisema Ayubu Rashid mkazi wa Kijiji cha Mnyuzi.
DSC_0046
Mkurugenzi Msaidizi wa Mambo ya Kale Taifa, Bw. John Kimaro ( wa pili kushoto) akifurahi jambo na Afisa Mradi wa uchumi wa kijani ndani ya hifadhi hai (GEBR) Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko (kushoto) wakati wa burudani huku mgeni rasmi Mjumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Hifadhi Hai Tanzania,Bw. Joseph Kigula (wa tatu kushoto) akingalia taswira mbalimbali alizochukua kupitia "Tablet" yake.
Kwa mujibu wa UNESCO asilimia 38 ya ardhi ya tanzania imekaliwa na misitu ambayo ni muhimu kayika maisha ya wanadamu na viumbe hai.
Hata hivyo inaaminika kwamba asilimia 75 ya watanzania wanaishi vijijini wakitegemea zaidi maliasili na kilimo.
Wamesema utegemezi huo umekuwa kikwazo kikubwa katika hifadi ya misitu ambayo imekuwa ikivamiwa kwa ajili ya mahitaji ya nishati na mbao.
Mradi wa GEBR unagusa wilaya ya Muheza, Mkinga, na Korogwe .
DSC_0073
Mkuu wa msafara wa ugeni huo Mhifadhi Hifadhi ya Mazingira asili Amani, Bi. Mwanaidi Kijazi akitoa utambulisho wa meza kuu kwa washiriki wa mafunzo hayo kutoka vijiji 19 (hawapo pichani) watakaonufaika na mradi huo.
DSC_0111
Mgeni rasmi Mjumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Hifadhi Hai Tanzania, Bw. Joseph Kigula, akizungumza wakati akizindua rasmi mafunzo kwa washiriki kutoka vijiji 19 vinavyozunguka Hifadhi Hai ya usambara mashariki ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa uchumi wa kijani ndani ya hifadhi hai(GEBR) unaoratibiwa na UNESCO kwa ufadhili wa KOICA. Kulia ni Mwenyekiti wa Kata ya Mnyuzi, Bw. Juma Mkunguti, Kutoka Kushoto ni Afisa Mradi wa Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko, Mhifadhi Hifadhi ya Mazingira asili Amani, Bi. Mwanaidi Kijazi na Mkurugenzi Msaidizi wa Mambo ya Kale Taifa, Bw. John Kimaro.
DSC_0078
Afisa Mradi wa uchumi wa kijani ndani ya hifadhi hai (GEBR) Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko (wa pili kushoto) akizungumza na washiriki na kuelezea lengo la mradi huo ambapo amesema unalenga kuwakomboa kiuchumi na kupunguza umaskini kwenye jamii zao. Wa tatu kushoto ni Mkuu wa msafara wa ugeni huo Mhifadhi Hifadhi ya Mazingira asili Amani, Bi. Mwanaidi Kijazi akitafsiri kwa washiriki.
DSC_0213
Mkufunzi wa Ujasiriamali/Biashara wa Program ya anzisha na imarisha biashara yako (SIYB) iliyochini ya Shirika la Kazi Duniani (ILO), Bw. Mussa Mashishanga akitoa mada ya namna ya kutafuta masoko kwenye mafunzo ya kuzijengea uwezo jamii za vijiji zenye bidii ya kuhifadhi bioanuwai na kupunguza athari dhidi ya rasilimali za misitu ili ziweze kutafuta riziki kwa maendeleo endelevu yanayofanyika kwenye Hoteli ya BS Palace kata Mnyuzi wilayani Korogwe.
DSC_0149
Pichani juu na chini ni Sehemu ya washiriki kutoka vijiji 19 vinavyozunguka Hifadhi Hai ya Usambara mashariki ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa uchumi wa kijani ndani ya hifadhi hai(GEBR) wakifuatilia kwa umakini mafunzo hayo.
DSC_0128
DSC_0159
Mshauri na Mkufunzi wa Ujasiriamali/Biashara wa Program ya anzisha na imarisha biashara yako (SIYB) iliyochini ya Shirika la Kazi Duniani (ILO), Bw. Lawrence Ambokile akifafanua jambo kwa washiriki wakati wa mafunzo hayo.
DSC_0115
Mgeni rasmi Mjumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Hifadhi Hai Tanzania Joseph Kigula (walioketi wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wakufunzi pamoja na washiriki wa mafunzo hayo.
DSC_0114

NAIBU WAZIRI WA MAJI, MAKALLA AWANASA WEZI WA MAJI DAR NA KUTANGAZA KUFILISI MALI ZAO.

$
0
0

Meneja Mkuu wa Kampuni ya ufyatuaji matofali ya Ujenzi Solutions, ya Kimara kwa Msuguri, Dar es Salaam, Rahim Hamis na mfanyabiashara wa kampuni isiyo na jina, Credo Rajab (kulia) wakiwa chini ya uliznzi wa Polisi huku wakiwa wamevishwa pingu baada Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla kuamuru kuwakamata alipokagua viwanda vyao vya ufyatuaji na kugundulika kuwa wanatumia maji isivyo halali kwa kujiunganishia kwenye bomba kuu la Mamlaka ya Maji Safi na Taka Dar  ws Salaam (DAWASA).  Makalla ambaye alifanya ziara ya kukagua maendeleo ya upanuzi wa Matambo wa Maji wa Ruvu Juu, Mlandizi, mkoani Pwani , pia alifanya msako wa kushitukiza kwa kampuni hizo.
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (kulia) akijaribu kuendesha katapila la Kampuni ya Ujenzi ya VA Tech Wabag Ltd, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya upanuzi wa Mitambo ya Maji ya Ruvu Juu, Mlandizi, mkoani Pwani .Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa na Meneja Mradi wa kampuni hiyo, Pintu Dutta.
Askari wa FFU wakilinda doria katika kiwanda cha ufatuaji tofali cha Ujenzi Solutions, Kimara Dar es Salaam
Moja ya mabomba linalodaiwa kuunganishwa kiholela kwenye bomba kuu la Ruvu Juu linaloleta maji  mjini na kampuni ya Ujenzi Solutions eneo la Kimara
Makalla akizungumza mbele ya Lori la Maji lililokamatwa likijazwa maji yanayodaiwa kuwa ya Dawass, katika kiwanda cha matofali cha Ujenzi Solutions
Pumpu iliyonaswa na Dawasa ikinyonyonya maji kutoka bomba kuu la Ruvu Juu eneo la Ubungo, Dar es Salaam
Makalla akiondoka katika kiwanda cha matofali cha Moto ambacho alisitisha shguli zake baada ya kubainika wakiiba maji ya Dawasa eneo la Ubungo.
Ramani ya upanuzi wa Mtambo wa Maji wa Ruvu Juu, eneo la Mlandizi, Pwanik.
Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa akijaribu kuendesha katapila la Kampuni ya Wagani ambayo imepewa tenda ya upanuzi wa Mtambo wa Maji wa Ruvu Juu.
Makalla (wa pili kushoto) Mbunge wa Kihaha Vijijini, Hamoud Jumaa ( wa pili kulia) na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Halima Kihemba kulia, wakikagua ujenzi wa upanuzi wa mtambo huo. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG



 Na Richard Mwaikenda

NAIBU Waziri wa  Maji, Amos Makalla amezifungia kampuni tatu za ufyatuaji tofali kuendesha shughuli baada ya kubainika  kujiunganishia isivyo halali maji kutoka kwenye bomba kuu la Mamlaka ya Maji Safi na Taka (DAWASA), wakati wa ukaguzi wa kushitukiza alioufanya leo katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Makalla aliamuru viongozi wa kampuni  hizo wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa hatua zaidi, ambapo pia aliagiza mali zote za kampuni hizo zifilisiwe ili zitumike kulipa fidia kwa hasara kubwa iliyoingizia Serikali.

Akiwa katika ukaguzi huo, Makala aligundua madudu mengi yanayofanywa na kampuni hizo, ambazo zimejiunganishia maji kwa ajili ya kufyatulia matofali na kuuza kwa kutumia malori.

Kampuni alizozikagua leo na kukutwa na dhahama hiyo ni; Moto iliyopo mita chache kutoka Makao Makuu ya Wizara ya Maji, Ubungo Dar es Salaam, Ujenzi Solutions iliyopo Kimara kwa Msuguri pamoja na kampuni isiyo na jina iliyopo pia Kimara kwa Msuguri.

Kabla ya kufika katika kampuni hizo, ulinzi wa Polisi wenye silaha ulikuwa umeimarishwa, ambapo Makalla alitoa agizo kwamba wasiondoke katika maeneo hayo ili wahusika na wafanyakazi wao wasiendelee na kazi yoyote.

Katika kampuni ya Moto, ilikutwa pampu ikiendelea na kazi ya kuvuta maji ambapo Msimamizi wa kampuni hiyo, Frederick Tarimo alikana kuiba maji kwenye bomba la Dawasa na kudai kwamba maji hayo wanayatoa kutoka kwenye mto.

Tarimo alisema kuwa hutumia lita 3000 za maji kwa siku, ambapo hufyatua matofali kati ya 1500 na 2000 kwa siku. Pia huuza kwa siku kiasi cha matofali kama hayo. Kila tofari huuzwa kati ya sh. 800 na 1000. Alisema kuwa endapo hatofanya kazi kwa muda wa mwezi mmoja ataingia hasara ya sh. mil. 90, hivyo kila siku kupata hasara ya sh. mil. 3.

Naye Meneja wa kampuni ya Ujenzi Solutions, Rahim Hamis, alikana katakata kwamba maji wanayoyatumia wameunganisha kutoka kwenye bomba la Dawasa, bali wanatumia maji kutoka kwenye bwawa dogo lililopo jirani na kampuni yao. Pia katika eneo hilo lilikamatwa lori  aina ya Isuzu namba 957 AJK likijazwa maji.

Viongozi waliokamatwa ni Frederck Tarimo ambaye alijitaja kuwa msimamizi wa kampuni ya Moto, Meneja Mkuu wa kampuni ya Ujenzi Solutions, Rahim Hamis na Credo Rajab mmiliki wa kampuni aliyodai haina jina.

Makalla, alisema ili kupambana na wezi wa maji, haina budi sasa kupeleka mswada bungeni ili watungiwe sheria ya uhujumu uchumi pamoja na kutoa adhabu kali ikiwemo ya kutaifisha mali zao, tofauti na adhabu wanayopewa sasa ya kulipishwa faini ya sh, mil 2.

Katika ziara hiyo pia alifanya ukaguzi wa matanki ya kuhifadhia maji ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambapo alijionea jinsi maji yalivyopungua kwenye matanki hayo ambayo pia yapo kwenye maandalizi ya kufanyiwa ukarabati mkubwa ili yafae kwa ajili ya hifadhi ya maji kutoka bomba la Ruvu Chini ambalo upanuzi wake umekamilika.

Pia alitembelea kuona maendeleo ya upanuzi wa Mtambo wa Maji wa Ruvu Juu, Chalinze, Mkoa wa Pwani. kesho anaendelea tena na ziara kama hiyo katika Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.

MBUNGE GODFREY MGIMWA AKABIDHI MSAADA WA BATI KIJIJI CHA USENGERENDETI NA MAHANZI

$
0
0
Katibu  wa mbunge  wa jimbo la Kalenga  Bw  Martine Simangwa  kushoto akikabidhi msaada wa bati  100 kwa  uongozi wa kijiji cha Usengerendeti  kwa  ajili ya ujenzi wa nyumba ya wauguzi wa Zanahati ya  kijiji  .
Wananchi  wakishiriki kushusha  bati  hizo
Katibu  wa mbunge Mgimwa Bw Martine Simangwa akieleza kazi mbali mbali  zilizofanywa na mbunge Godfrey Mgimwa toka alipochaguliwa 
Katibu wa mbunge Mgimwa Bw Martine  Simangwa kushoto akikabidhi bati 80  kwa uongozi wa  serikali ya  kijiji  cha Mahanzi  kwa ajili ya ujenzi  wa vyumba vya madarasa katika  kijiji hicho kipya 
 Wananchi  wakimpongeza  katibu wa Mgimwa kwa niaba ya mbunge wao Godfrey Mgimwa 
.............................................................................................
Na Francis Godwin Blog.
MBUNGE  wa  jimbo la  Kalenga  Godfrey  Mgimwa ametoa  msaada wa  bati 180 zenye tahamani ya  zaidi ya Tsh milioni 1 kwa  kata ya  Wasa kwa  kama  sehemu ya  utekelezaji wa ahadi zake  katika kata  hiyo.

Akikabidhi msaada  huo   kwa niaba ya mbunge Mgimwa katibu  wake Martine Simangwa alisema  kuwa  bati  hizo  ni   sehemu ya jitihada za mbunge  huyo kuunga  mkono  harakati za wananchi  katika  kuibua miradi ya kimaendeleo katika maeneo yao.

Hata  hivyo  alisema kuwa bati hizo 100 ni kwa ajili ya  kijiji  cha Usengerendeti ambao  wapo katika  ujenzi wa nyumba  ya  waganga katika  Zahanati ya  kijiji na bati  80 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa  shule katika  kijiji kipya   cha Mahanzi .

Alisema kuwa moja kati  ya mambo ambayo mbunge  Mgimwa ameyawekea  kipaumbele zaidi ni pamoja na elimu pamoja na afya  na kuwa  jitihada za kuhakikisha  mambo  hayo yanashughulikiwa  zinafanyika .

Pia  alisema katika  kuhakikisha maendeleo ya  jimbo  hilo la Kalenga  yanaendelea  kusonga  mbele zaidi ni  vema  wananchi  wa  jimbo  hilo kuelekeza  nguvu zao katika maendeleo na kuachana na  baadhi ya  watu wanaopita katika  jimbo  hilo kwa ajili ya kuutaka ubunge mwaka 2015.

Kwani  kufanya hivyo ni kuendelea  kurudisha  nyuma maendeleo ya  jimbo  hilo na kuwataka  wanaofanya hivyo  kwa sasa  kusubiri  muda  ukifika ndipo  wananze  kujipitisha  na kuwa kimsingi katika nafasi ya  ubunge hakuna mbunge kivuli hivyo  kitendo cha  watu hao wanaojipitisha  kufanya hivyo kwa  sasa ni kuvuruga kasi ya maendeleo ya  jimbo  hilo.

Akizungumzia  kuhusu  suala la afya  katika  jimbo hilo alisema kuwa hali ya huduma ya afya  bado si mbaya  sana  japo kuna  changamoto mbali mbali ambazo  zinapaswa kushughulikiwa  ikiwemo ya dawa pamoja ,ukosefu wa  nyumba za  watumishi wa afya na baadhi ya maeneo  zahanati na  vituo hivyo vya afya  kukosa umeme.

Awali  wananchi  wa kata  hiyo ya   Wasa  walimpongeza  mbunge  huyo kwa  kuonyesha  uaminifu kwao na hata  kuanza  kutimiza ahadi  zake kwa wakati mfupi  zaidi  ukilinganisha na  wabunge  wengine  waliopata  kuongoza  jimbo  hilo ambao hadi  wameondoka madarakani  baadhi ya ahadi  hawajatekeleza kwa  wananchi.

Alisema Yohana Sanga  kuwa  jimbo la Kalenga kwa  muda  mrefu  limekuwa ni  jimbo linaloongoza kwa kubadili  wabunge kwa  kila kipindi  kimoja na ndi  sababu ya  jimbo  hilo  kuendelea  kuwa nyuma katika maendeleo  ukilinganisha na majimbo ambayo  wabunge wake wameongoza kwa  zaidi ya kipindi  kimoja na kuwa kwa  sasa wao  hawana haja ya  kubadili mbunge mwingine  zaidi ya Mgimwa .
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live




Latest Images