Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

RAIS DR. JAKAYA KIKWETE AKAGUA MRADI UJENZI WA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU MKINGA MKOANI TANGA

$
0
0
DSC_9455
Rais Dr. Jakaya Kikwete akizindua mradi huo pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mh. George Simbachawene katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Felix Maagi na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh. Chiku Galawa
DSC_9456
Rais Dr. Jakaya Kikwete na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mh. George Simbachawene kulia na Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Felix Maagi kwa pamoja wakipiga makofi mara baada ya Rais kuzindua rasmi mradi huo uliopo wilayani Mkinga
DSC_9460
Rais Dr. Jakaya Kikwete akisikiliza kwa makini wakati akipata maelezo ya mradi huo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC Bw. elix Maagi.
DSC_9461
Rais Dr. Jakaya Kikwete na Mkuu wa mkoa wa Tanga Mh. Chiku Galawa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa shirika la Nyumba NHC Bw. Felix Maagi wakikata utepe kwa pamoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi huo.
DSC_9463
Rais Dr. Jakaya Kikwete na Mkuu wa mkoa wa Tanga Mh. Chiku Galawa wa pili kutoka kushoto , Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mh. George Simbachawene wa pili kutoka kulia na Kaimu Mkurugenzi wa shirika la Nyumba NHC Bw. Felix Maagi wakikata utepe kwa pamoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi huo.
DSC_9467
Rais jakaya Kikwete akikata utepe kabla ya kukabidhi Mashine za kufyatulia matofali kwa mkuu wa mkoa wa Tanga ambazo zitagawiwa kwa kila wilaya za mkoa wa Tanga mashine nne kulia ni mkuu wa mkoa wa Tanga Mh. Chiku Galawa.
DSC_9443
Rais Dr. Jakaya Kikwete akiwasili katika eneo la mradi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na Shirika la Nyumba (NHC) na kupokelewa na Ndg. Felix Maagi Kaimu Mkurungenzi Mkuu NHC na Mkurugenzi wa Fedha kulia wakati alipokagua mradi huo uliopo katika wilaya ya Mkinga mkoani Tanga akiwa katika ziara yake ya kikazi jana Rais Dr. Jakaya Kikwete anaendelea na ziara mkoani humo leo.
DSC_9451
Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na wafanyakazi mbalimbali wa shirika la Nyumba wakati alipowasili katika eneo la mradina kujionea shughuli za ujenzi katika mradi huo

DSC_9480
Rais Dr. Jakaya Kikwete akipata taarifa ya mradi huo wa nyumba za gharama nafuu kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa shirika la Nyumba NHC Bw. Felix Maagi.
DSC_9427
Baadhi ya nyumba zilizokamilika zinavyoonekana

MSHIRIKI WA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) AZIMIA JUKWAANI

$
0
0
Baadhi ya Washiriki wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) ambao wapo kwenye Maumivu ya kuchomwa na Jua la Utosi Wakimpa huduma ya Kwanza Mmoja wa Washiriki mwenzao ambae alipoteza fahamu jukwaani Hapo jana mara baada ya kuchomwa na Jua la Utosi na Kupelekea Kutolewa kwenye kinyanganyiro cha Kushindania Kitita cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania katika Fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) itakayofanyika Mwishoni mwa Mwezi wa nane.
 Baadhi ya wafanyakazi wa TMT wakimpepea mmoja wa washiriki wa TMT ambae aliaga mashindano hayo mara baada ya kupitiwa na Jua La Utosi na kupelekea kupoteza fahamu jukwaani wakati wa Onyesho la Mchujo wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) lililofanyika jana katika Ukumbi wa Uhuru uliopo makumbusho ya Taifa, Jijini Dar Es Salaam


Na Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited - Dar Es Salaam

Mara baada ya Safari ya Kuzisaka Nyota katika Kanda sita za Tanzania ambazo ni Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kati, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Kusini, Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Pwani sasa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) limeingia katika hatua nyingine ya Washiriki kuwa chini ya Jua la Utosi huku mshiriki Mmoja wa TMT Kutoka Kanda ya Ziwa kuzimia Jukwaani mara baada ya kuunguzwa na jua la utosi kwenye Kinyanganyiro  cha Kuwania Kitita cha Shilingi Milioni 50 katika Fainali itakayofanyika Mwishoni mwa Mwezi wa Nane.

Mara Baada ya Mshiriki Huyo kuunguzwa na Jua la Utosi na kupoteza fahamu Jukwaani show ilisimama takribani Kwa muda wa Dakika 20 ili kuweza kuruhusu Mshiriki huyo kurudi Jukwaani ili zoezi zima la mchujo liweze kuendelea.

Shindano la TMT limekuwa likiwavutia Wapenzi na Watazamaji wengi wa kila rika kutokana na Utofauti wake, ubora wake pamoja na vipaji vinavyoendelea kuonyeshwa na washiriki wake katika Shindano hilo Kubwa kabisa na La Kwanza Kufanyika Afrika Mashariki na Kati.

Mara baada ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) kuingia katika Jua La Utosi, Washiriki tisa waliweza kuchomwa na Jua la Utosi na Kupelekea Washiriki wawili kuondolewa katika Shindano hilo huku mshiriki mmoja akizidiwa hadi kupoteza fahamu jukwaani.

Jumamosi ya Kesho Katika Kipindi cha TMT kupitia Kituo cha Runinga cha ITV Saa 4 Usiku washiriki tisa waliochomwa na jua la Utosi wataonyeshwa na hatimae watanzania, wapenzi na watazamaji wa Shindano hili kubwa Afrika Mashariki na Kati wataweza kujionea na kumfahamu mshiriki mmoja wapo kati ya wawili waliotolewa ambae alipoteza fahamu jukwaani kutokana na kuchomwa na Jua la Utosi na kupelekea Kutolewa kwenye kinyanganyiro hiko huku wengine Saba wakiponea Chupuchupu lakini hali zao zikiwa bado mbaya. 

Shindano la TMT limeanza kuvuta hisia za watanzania wengi waliopo ndani na Nje ya Nchini kutokana na uzuri wake pamoja na Ubora.

Ili Kuweza Kumnusuru Mshiriki wako kutoka kwenye Maumivu ya Kuchomwa na Jua la Utosi unachotakiwa kufanya ni Kumpigia kura. Jinsi ya Kumpigia Kura Mshiriki wako ili kuwezesha kutokumbwa na kuchomwa na Jua la Utosi au kumnusuru kutoka kwenye maumivu ya jua la Utosi unachotakiwa kufanya ni Kuandika neno "TMT" ikifuatiwa na namba ya Mshiriki halafu tuma Kwenda 15678 kupitia simu yako ya Mkononi. MFANO: TMT00 tuma Kwenda 15678

THOMAS MASHALI KUZIPIGA NA MADA MAUGO NANE NANE UWANJA WA TAIFA

$
0
0
Rais wa TPBO Yassin Abdallah 'Ostadhi' akiwainua mikono juu mabondia Mada Maugo kushoto na Thomas Mashali baada ya kusaini mkataba wa makubaliano wa kupambana Sikukuu ya Nanenane (8/8/2014) katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wakati wa tamasha la usiku wa matumaini lililoandaliwa na kampuni ya global publisher Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mabondia Mada Maugo na Thomas Mashali wakitunishiana misuli baada ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kupambana Agost 8 katika uwanja wa taifa Dar es salaam wakati wa tamasha la matumaini siku ya Sikukuu ya Nanenane lililoandaliwa na kampuni ya global publisher.

Rais wa TPBO Yassin Abdallah 'Ostadhi' kushoto akimkabidhi sehemu ya fedha kidogo bondia Mada Maugo  kwa ajili ya maandalizi ya mpambano wake na Thomas Mashali utakaofanyika  Agost 8 katika uwanja wa taifa Dar es salaam wakati wa tamasha la matumaini siku ya Sikukuu ya Nanenane lililoandaliwa na kampuni ya global publisher.
Rais wa TPBO Yassin Abdallah 'Ostadhi' kushoto akimkabidhi sehemu ya fedha kidogo bondia Thomas Mashali  kwa ajili ya maandalizi ya mpambano wake na Mada Maugo utakaofanyika
Agost 8 katika uwanja wa taifa Dar es salaam wakati wa tamasha la matumaini siku ya Sikukuu ya Nanenane lililoandaliwa na kampuni ya global publisher Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
 
Mabondia Mada Maugo na Thomas Mashali wakitunishiana misuli baada ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kupambana Agost 8 katika uwanja wa taifa Dar es salaam wakati wa tamasha la matumaini siku ya Sikukuu ya Nanenane lililoandaliwa na kampuni ya global publisher Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

MGOMBEA URAIS WA MSUMBIJI KWA TIKETI YA FRELIMO AKUTANA NA RAIS KIKWETE

$
0
0
 Mgombea Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya chama cha Ukombozi cha FRELIMO Filipe Nyusi akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, Ikulu Ndogo mjini Tanga, mgombea huyo alipokwenda kumsalimia na kuwa na mazungumzo na Rais leo.
Rais Kikwete na Mkewe Mama Salma, wakiwa katika picha ya kumbukumbu na mgombea huyo kwa tiketi ya FRELIMO Filipe Nyusi, Ikulu Ndogo mjini Tanga. Kushoto ni Mwenyeji wa Mgomba huyo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. Picha na Adam Mzee wa CCM Blog.

KONGAMANO LA NNE LA MAKATIBU MUHTASI TANZANIA (TAPSEA) LAFUNGULIWA LEO JIJINI MWANZA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA),Mh. Dk. Mary Nagu akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la nne la Makatibu Muhtasi Tanzania,leo Julai 11,2013 jijini Mwanza.Mh. Nagu katika hotuba yake,amesema atawasimamia Makatibu hao na kuhakikisha wanaanzisha Benki yao ambayo itawawezesha kuweka abiba zao na kukopeshana pia.
Mgeni Rasmi katika Kongamano la Makatibu Muhtasi Tanzania na Mshauri wa Mambo ya Kisheria wa TAPSEA,Naibu Waziri wa Katiba na Sheria,Mh. Angela Kairuki akitoa hotuba yake katika ufunguzi wa Kongamano la nne la Makatibu Muhtasi Tanzania,leo Julai 11,2013 jijini Mwanza.Mh. Kairuki amewahimiza Makatibu Muhtasi hao kuhakikisha wanaudumisha na kuulinda umoja walionao,kwani umoja ndio msingi wa maendeo.
Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania,Bi. Pilli Mpenda akisoma hotuba yake kwenye ufunguzi wa Kongamano la nne la Makatibu Muhtasi Tanzania,leo Julai 11,2013 kwenye hoteli ya Malaika,jijini Mwanza.
Washiriki wa Kongamano la nne la Makatibu Muhtasi Tanzania kutoka maeneo mbali mbali wakifatilia mada mbali mbali.

KONGAMANO LA NNE LA MAKATIBU MUHTASI TANZANIA (TAPSEA) LAFUNGULIWA LEO JIJINI MWANZA

$
0
0

Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania,Bi. Pilli Mpenda akisoma hotuba yake kwenye ufunguzi wa Kongamano la nne la Makatibu Muhtasi Tanzania,leo Julai 11,2013 kwenye hoteli ya Malaika,jijini Mwanza.

MGOMBEA WA URAIS WA MSUMBIJI ATEMBELEA ZANZIBAR,AWEKA SHADA LA MAUA KWENYE KABULI LA KARUME

$
0
0
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai akimkaribisha Mheshimiwa Filipe Nyusi Mgombea wa nafasi ya Urais kutoka chama cha FRELIMO Msumbiji
 Wanachama wa FRELIMO wanaoishi Zanzibar wakimpokea Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia chama chao Mheshimiwa filipe Nyusi mara baada ya kuwasili Zanzibar.
Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwat iketi ya chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Nyusi akiweka Shada la Maua kwenye kaburi la Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar na Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Sheikh  Abeid Amani Karume

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimuonyesha Mgombea wa nafasi ya Urais nchini Msumbiji kwa tiketi ya chama cha FRELIMO Mh. Filipe Nyusi Kitabu cha Wageni ambacho kilisainiwa pia na Marehemu Samora Machel Rais wa Kwanza wa Msumbiji kwenye Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.

Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akimkaribisha Mgombea wa nafasi ya Urais nchini Msumbiji kwa tiketi ya chama cha FRELIMO Mh. Filipe Nyusi ,Ikulu ya Zanzibara ambapo walifanya mazungumzo.

Rais Kikwete ziarani Pangani mkoa wa Tanga

$
0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua bomba la maji wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji Bweni wilayani Pangani mkoa wa Tanga leo.
 ais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtwika ndoo ya maji mmoja wa wakazi wa Bweni Wilayani Pangani wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji huko Bweni Wilayani Pangani Mkoa wa Tanga leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na mbunge wa Pangani Mhe.Saleh Pamba wakifunua kitambaa katika jiwe la msingi kuzindua ujenzi wa maabara katika shule ya sekondari Kipumbwi huko Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia fukwe za mji wa Pangani wakati akivuka kwenda kata ya Bweni kwa kutumia kivuko kipya M.V.Pangani jana.Mji wa Pangani uko katika hatari ya kumezwa na bahari kutokana na kuongezeka kwa kina cha maji kulikosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mwenyeji wake mkuu wa mkoa wa Tanga Mhe.Chiku Galawa wakivuka mto Pangani kwa kutumia kivuko kipya M.V.Pangani kwenda kata ya Bweni ambapo alizindua mradi wa maji,maabara na kuhutubia mkutano wa hadhara. Picha na Freddy Maro.

JOPO LA WAHARIRI LATEMBELEA MIRADI YA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU WA NHC MTANDA, LINDI NA SHANGANI MTWARA

$
0
0
2
Meneja wa Shirika la Nyumba Mtwara, Joseph John akizungumza na wahariri walipotembelea mradi wa nyumba za makazi za Shangani Mjini Mtwara leo jioni. Kutoka Kulia ni Theophi Makunga, Mhariri na Meneja Bishara wa Mwananchi Communications Limited, Jesse Kwayu Mhariri Mtendaji wa Nipashe na Bakari Machumu Mhariri Mtendaji wa Mwananchi Communications Limited. (Picha zote kwa hisani ya Shirika la Nyumba la Taifa)
3
4
Wahariri wakifuatilia maelezo ya Meneja wa mkoa wa Mtwara wa Shirika la Nyumba la Taifa, Joseph John (hayupo pichani) wakati Meneja huyo akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa mradi huo jana mbele ya Wahariri.
5
Wahariri wakifuatilia maelezo ya Meneja wa mkoa wa Mtwara wa Shirika la Nyumba la Taifa, Joseph John (hayupo pichani) wakati Meneja huyo akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa mradi huo jana mbele ya Wahariri.
6
Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakimsikiliza Meneja wa Shirika la Nyumba Mtwara, Joseph John walipotembelea mradi wa nyumba za makazi za Shangani Mjini Mtwara jana jioni. Kutoka kulia ni Jabir Idrisa, Mhariri wa Mwanahalisi, Salim Salim nguli wa Habari na Mwalimu kutoka Zanzibar, Joseph Kulangwa wa Uhuru Publications.
8
Mojawapo ya majengo ya majengo ya Mradi wa nyumba za makazi za Shangani kama linavyoonekana leo hii. Ni mojawapo kati ya majengo matatu yenye nyumba 10 kila moja na hivyo kufanya idadi kufikia 30.
9

Juzi, Alhamisi (Julai 10, 2014) na jana Ijumaa (Julai 11, 2014) jopo la Jukwaa la wahariri takriban 85 walitembelea kwenye miradi yetu miwili, mmoja wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu Mtanda mkoani Lindi na mwingine wa nyumba za makazi za kati na juu zilizopo eneo la Shangani Mtwara.

Jopo hilo likiongozwa na Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Absalom Kibanda na Katibu wa Jukwaa hilo, Neville Meena. Walisomewa taarifa fupi ya maendeleo ya ujenzi wa miradi ya Nyumba hizo zipatazo 30 Lindi ambazo sasa zimefikia kwenye hatua za mwisho tayari kwa kukabidhiwa kwa wamiliki wake kwani nyumba zote 30 tayari zilishanunuliwa na zile za Mtwara ambazo pia ni 30, 10 kati ya hizo zikiwa zimeshanunuliwa.

Miongoni mwa mambo makubwa yaliyozungumzwa na wahariri hao ni kuliomba kuendelea kusimamia azam yake ya kuwauzia nyumba Watanzania wa kipato cha chini, kwani kwa kufanya hivyo watanzania wa kawaida watakuwa na uwezo wa kumiliki nyumba na siyo kuendelea kuwa wapangaji wa shirika.

IPTL yatoa Tsh milioni 20 kwa RT kusaidia maandalizi ya mashindano ya riadha ya kitaifa

$
0
0
 Makamu wa Rais-Utawala wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) William Kallaghe (wapili kushoto) akipokea sehemu ya fedha taslim Tsh milioni 20 zilizotolewa na kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) kusaidia maandalizi ya mashindano ya mwaka huu ya Riadha ya Kitaifa yatakayoanza leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaaam. Kulia ni Katibu na Mwanasheria Mkuu wa IPTL/ Pan African Power Solutions (PAP), Bw. Joseph Makandege, akifuatiwa na Msaidizi wa kampuni hiyo Rajiv Bhesania na kushoto ni Katibu Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui.
 Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui (wapili kushoto) akipokea sehemu ya fedha taslim Tsh milioni 20 zilizotolewa na kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) kusaidia maandalizi ya mashindano ya mwaka huu ya Riadha ya Kitaifa yatakayoanza leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaaam. Kulia ni Katibu na Mwanasheria Mkuu wa IPTL/ Pan African Power Solutions (PAP), Bw. Joseph Makandege, akifuatiwa na Msaidizi wa kampuni hiyo Rajiv Bhesania na kushoto ni Makamu wa Raisi-Utawala wa RT, William Kallaghe.

==============  ==========  ===========
SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT) limepokea shilingi milioni 20 kutoka katika kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania (IPTL) kwa lengo la kusaidia uandaaji wa mashindano ya Riadha ya Kitaifa yanayoanza leo jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui aliwaeleza waandishi wa habari kuwa fedha hizo zilipokelewa zitasaidia katika maandalizi ya mbio hizo kubwa za kitaifa ambazo zitatumika katika kuwaandaa wanariadha watakaoiwakilisha nchi katika mashindano mbali mbali ya kimataifa.

Bw. Nyambui alisema kuwa zaidi ya wanariadha 400 wanatarajiwa kushiriki katika mbio hizo zitakazofanyika kwa siku mbili na zaidi ya waamuzi 200 watakuwa tayari kuhakikisha wanaofanya vizuri wanachaguliwa na kupewa mafunzo zaidi kwa ajili ya mashindano ya baadae.

Alibainisha kuwa ufadhili wa kampuni ya IPTL utasaidia kwa kiasi kikubwa kulipia gharama za maandalizi na uendshaji wa tukio hilo, na hivyo kuisaidia RT kufikia malengo yake katika mashindano ya mwaka huu ya kitaifa. 

"Mashindano ya mwaka huu ya riadha ya kitaifa yanaanza kesho (leo jumamosi) katika uwanja wa taifa wa Dar es Salaam, ambapo mikoa yote 30 nchini Tanzania inatarajiwa kushiriki.

"Tunategemea wanariadha wetu wa taifa kuonyesha uwezo wao kabla hawajasafiri kwenda Scotland kwa ajili ya mashindani ya Jumuiya ya Madola yaliyopangwa kufanyika mwezi wa Julai tarehe 23 mpaka Agosti tarehe 3,"alisema Nyambui.

Licha ya mashindano hayo ya kitaifa kutumiwa na RT  kama nafasi  ya kupasha misuli moto kwa wanariadha watakaoiwakilisha nchi kwa mashindano yajayo ya jumuiya ya madola, mashindano hayo yatawapatia wanariadha wanaochipukia nafasi ya kuonyesha ujuzi wao.

Aliongeza kuwa mbio hizo zitatumika katika kuchagua timu ya kitaifa ya wanariadha watakaoiwakilisha nchi katika mashindano mbali mbali ya kimataifa kama vile ya Ukanda wa Tano, Mashindano ya Dunia na Afrika yatakayofanyika baadae mwaka huu.

Kwa upande wake, Katibu na Mwanasheria Mkuu wa IPTL/ Pan African Power Solutions (PAP), Bw. Joseph Makandege alisema kuwa kampuni yake imekubali kudhamini mashindano hayo kama njia ya kuipa RT nafasi ya kutambua vipaji vipya na pia kuwaandaa wanariadha wa kitanzania kwa ajili ya mashindano ya kimataifa. 

"Riadha ni eneo mojawapo ambalo Tanzania inaweza kulitumia ili kujiweka katika ramani ya dunia ya michezo. Miaka iliyopita, wanariadha wetu walililetea heshima kubwa taifa hili. IPTL inaamini kuwa  bado kuna vipaji vingi vinavyoweza kuchukuliwa na kutumika katika kuipeperusha vyema  bendera yetu ya taifa katika mashindano mbali mbali ya kimataifa.

"Udhamini wetu pia unalenga katika kuwatengenezea nafasi za ajira vijana wa kitanzania. Tunajua kuwa vijana wetu wengi wana vipaji, ambavyo vinapotea tu. Kama RT watasaidiwa kuviinua vipaji hivi, vijana wengi watajipatia chanzo cha mapato yao kupitia riadha. Hili linaendana na sera yetu ya kurudisha kile tukipatacho kwa jamii ambayo pia imejikita katika kuiwezesha jamii inayotuzunguka kiuchumi," alisema.

Wakati huo huo, Makamu wa Rais- Utawala wa RT , William Kallaghe aliishukuru IPTL kwa msaada wake, huku akiongeza kuwa mashindano ya kitaifa ya riadha ya mwaka huu yatakuwa tofauti na yaliyopita,  kwa kuwa yatatumika kuiandaa timu ya taifa kwa ajili ya mashindano yajayo ya kimataifa ya mwakani au miaka miwili ijayo.

RAIS JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA MGOMBEA WA URAIS WA MSUMBIJI MKOANI TANGA

$
0
0
 Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Nyusi pamoja na mwenyeji wake Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakivishwa skafu baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege mkoani Tanga ambapo alikutana na Mwenyekiti wa CCM Taifa,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.
  Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Nyusi akishiriki kucheza ngoma na wenyeji wa Tanga waliojitokeza wakati wa mapokezi.
  Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Nyusi akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mheshimiwa Chiku Galawa mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Tanga.
Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Nyusi katika Ikulu ya Tanga ambapo walifanya mazungumzo.

Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia Chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Nyusi akimsalimia Mzee Said Mbaruku wa Tanga wakati alipomtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kwenye mazungumzo na Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia Chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Nyusi,Ikulu mjini Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa kwenye mazungumzo na Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia Chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Nyusi pamoja na Mbunge wa Tanga Mjini Mheshimiwa Omar Nundu nje ya Ikulu mjini Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete na Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia Chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Nyusi wakiwa kwenye picha ya pamoja Ikulu Ndogo mjini Tanga,wengine katika picha ni Komredi Oscar Monteiro,Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Mbunge wa tanga mjini Mh.Omar Nundu ,WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora, Kapteni Mstaafu George Mkuchika na Viongozi wengine kutoka Msumbiji
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia Chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Nyusi mara baada ya kumaliza mazungumzo Ikulu mkoani Tanga.(Picha na Adam Mzee).

BALOZI MERO AWAANDALIA FUTARI WATANZANIA GENEVA

$
0
0
Balozi wa Tanzania katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Geneva,  Mhe.  Modest Mero (kanzu jeupe) akila futari pamoja na wageni wake mbalimbali wakiwepo watanzania waishio Geneva katika futari maalum aliyowaandalia nyumbani kwake jana. 
wageni mbalimbali wakijipakulia futari hiyo katika makazi ya Balozi.

Wakina mama nao wakila futari hiyo iliyoandaliwa na Balozi pamoja na familia yake katika makazi yao mjini Geneva.
Picha cha mbalimbali za kumbukumbu na wageni waalikwa katika futari hiyo zilipigwa. Picha ya Mwisho ni Balozi Mero akiwa na mkewe na binti yao ambao ndio walikuwa waandazi wa futari hiyo.

MSANII MWAJUMA JIMAMA AFUNGA NDOA NA MELELA

$
0
0



 Msanii wa filamu na unenguaji Mwajuma Thabiti 'Mwajuma Jimama' akiwa katika pozi na mume wake Melela Mussa baada ya kufunga ndoa hivi karibuni Ilala bungoni na kufuatia na sherehe kubwa bwana harusi ni mfanya bihashara na bi, ni msanii wa kujitegemea.

JHIKOMAN ATEMBELEA SHULE YA MUZIKI YA REUTLINGEN,UJERMANI

$
0
0
WANAFUNZI NA WAKUU WA SHULE WAHIDI KUTEMBELEA BAGAMOYO ! KILA WAKATI 

Tubingen,Ujerumani,
Mwanamuziki maarufu wa Reggae barani Afrika Jhikoman ambaye yupo katika ziara ya kikazi barani ulaya,juzi alitua katika mji wa Tubingen,Ujerumani kwa ajili ya kushiriki katika maonyeso makubwa 5th International African Festival Tubingen 2014,ambako amealikwa na shirika la Afrikaktiv Org. 
 
Jhikoman amelamba deal la mkataba wa kudumu wa kutumbuiza katika onyesho hilo,pia amepata nafasi za kualikwa na kutembelea miradi mbali mbali ya utamaduni nchini ujerumani zikiwemo shule na tahasisi za muziki,ambazo amekuwa kivutio kikubwa na taasisi hizo zimehaidi kwenda Bagamoyo kwa kupata ujuzi zaidi wa kimuziki na utamaduni .
 Darasa la muziki katika tahasisi ya shule ya muziki Reutlingen Jhikoman anakubalika kimataifa
 Jhikoman mwalimu mwalikwa katika shule ya muziki Reutlingen,Ujerumani
 Mwanamuziki Jhikoman akitoa somo ktk shule ya muziki ya Reutlingen kama mwalimu mwalikwa
 Mwanamuziki Jhikoman akiwapa somo wanafunzi wa shule ya muziki Reutlingen

RAIS JAKAYA KIKWETE NA MKEWE MAMA SALMA WAKATIZA MTAANI NA KUNUNUA NG'ONDA

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakinunua samaki katika kibanda huko Bweni Wilaya ya Pangani juzi wakati Rais alipokwenda kuzindua mradi wa maji na kuweka jiwe la msingi kwaajili ya ujenzi wa maabara shuke ya sekondari Kipumbwi. 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakinunua samaki katika kibanda huko Bweni Wilaya ya Pangani juzi wakati Rais alipokwenda kuzindua mradi wa maji na kuweka jiwe la msingi kwaajili ya ujenzi wa maabara shuke ya sekondari Kipumbwi.(picha na Freddy Maro)

MH: NAMELOK SOKOINE ATIMIZA AHADI YAKE KWA KIKUNDI CHA VIKOBA- ARUSHA

$
0
0
Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Arusha, Namelok Sokoine (kushoto), akikabidhi Shs. milioni 5 kwa Mwenyekiti wa Vikoba Kata ya Engutoto, Bilhuda Kisasa,  ikiwa ni sehemu ya mchango wake wa shs. milioni 10 alizoahidi kuwasaidia akinamama wa kata hiyo. (Na Mpiga Picha Wetu)
Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Arusha, Namelok Sokoine (kulia), akizindua katiba ya vikundi vya vikoba katika kata ya Engutoto Wilayani Monduli jana. Hafla hiyo ilikwenda sambamba na harambee ya kutunisha mfuko wa vikoba, ambapo katika harambee hiyo jumla ya shilingi milioni 12 zilipatikana. Kushoto ni Mwenyekiti wa vikoba kata ya Engutoto, Bilhuda Kisasa .
Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Arusha, Namelok Sokoine (kulia), akizindua katiba ya vikundi vya vikoba katika kata ya Engutoto Wilayani Monduli jana. Hafla hiyo ilikwenda sambamba na harambee ya kutunisha mfuko wa vikoba, ambapo katika harambee hiyo jumla ya shilingi milioni 12 zilipatikana. Kushoto ni Mwenyekiti wa vikoba kata ya Engutoto, Bilhuda Kisasa . 

NA  MWANDISHI  WETU,  ARUSHA

WANACHAMA wa vikundi vya kuweka na kukopa (VIKOBA) mkoani Arusha wametakiwa kutumia na kupanga vizuri matumizi ya fedha wanazokusanya ili ziwasaidie kutoka daraja mhadi jingine katika maisha yao.

Kauli hiyo ilitolewa jana wilayani hapa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Arusha Namelok Sokoine alipokuwa akiendesha utunishaji wa fedha kwa Umoja wa Wanavikoba wa Kata ya Engutoto yenye vikundi 20 na wanachama 600.

Katika utunishaji huo, Namelok alichangia Sh. Milioni 10 huku kiasi cha Sh. Milioni 12 kikipatikana katika shughuli hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Umoja wa Wanawake UTW wilayani Monduli.

Akizungumza na wanavikundi hao Mbunge Namelok aliwataka wanawake kujitokeza na kujiunga katika vikundi huku akiwataka kuacha kuogopa kufanya shughuli za ujasiriamali.

“Wanawake nawaomba sana muendelee kujitokeza na kujiunga katika Vikoba kwani huku ndipo eneo ambalo litatuwezesha tuwe na sauti ya kujitegemea kimapato.

“Lakini pia naomba niwakumbushe jambo muhimu hizi fedha tunazokusanya nawaomba sana muonyeshe mfano wa kuzitumia vizuri ili kesho zitusaidie kutoka daraja moja kwenda daraja jingine katika maisha yetu,” alisema Namelok.

Kwa upande wake Katibu wa UWT Kata ya Engutoto Glory Emmanuel alisema wana vikundi wengi waliopo kwenye vikoba wanakabiliwa na changamoto ya elimu ya ujasiriamali.

“Tunaomba suala la ofisi za vikoba uliangalie kwani vikundi havina ofisini.Pia wanachama hawana elimu hatua inayosababisha kukopa na kutumia sivyo kutokana na kutokuwa na elimu ndogo ya biashara,” alisema Glory.

Naye mwana kikundi Zaituni Mwishehe alibainisha jinsi alivyonufaika na kuwa katika vikundi hivyo vya kuweka na kukopa ambapo hadi sasa ameweza kujitegemea katika matumizi ya kawaida ndani ya nyumba.

“Sasa hivi naweza kulipia michango midogomidogo ya mwanangu shuleni. Lakini pia hata kutatua matatizo mengine ya kifamilia kupitia mikopo ninayochukua kwenye kikundi bila hata kumsubiria mume wangu,” alisema Zaituni.

NAIBU WAZIRI ANGELLAH JASMINI KAIRUKI ZIARANI DAR ES SALAAM KUANZIA KESHO JULAI 14-18, 2014

$
0
0
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Jasmine Kairuki (MB) anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya siku tano kuanzia Jumatatu, Julai 14  hadi Ijumaa 18, 2014 katika jiji la Dar Es Salaam akitembelea asasi mbalimbali zinazotoa huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi kwa lengo la kujionea huduma zinazotolewa na asasi hizi ikiwa ni pamoja na kukutana na wananchi wanaopata huduma hii. 

Pamoja na kujionea huduma hizi Mh. Naibu Waziri anatarajiwa kujionea ufanisi wa kazi zinazofanywa na asasi hizi, changamoto zinazowakabili pamoja na kupokea maoni, ushauri na kubadilishana mawazo ili kujua jinsi ambavyo serikali inaweza kuboresha utoaji wa huduma hii.

Katika ziara hiyo, Mhe. Kairuki anatarajia kutembelea jumla ya asasi 13 ikiwa ni pamoja na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Taasisi ya Haki za Binadamu na Mazingira (Envirocare), Kamati ya Msaada wa Kisheria ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Nyingine ni pamoja na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake (WLAC) na Kituo Kinachoshughulikia Maslahi ya Wanawake na Watoto (TWCWC).

Taasisi nyingine atazozitembelea ni Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wajane na Watoto  (CWCA), Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), Kituo cha Msaada wa Kisheria cha Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Nyumba ya Amani na Ofisi ya Mfuko wa Huduma za Kisheria (Legal Services Facility).

Mheshimiwa Kairuki anatarajia kumaliza ziara yake siku ya Ijumaa, Julai 18, 2014 kwa kutembelea Sekretariati ya Msaada wa Kisheria Tanzania ijnayoratibu shughuli za utaoji wa Msaada wa Kisheria Tanzania na kisha kufanya mkutano wa majumuisho na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria kuanzia saa 5:00 asubuhi.

Imetolewa na Wizara ya Katiba na Sheria,
Dar es Salaam,
Jumapili, Julai 13, 2014

WAZAZI WATAKIWA KUWEKEZA KATIKA ELIMU

$
0
0
 Mbunge wa jimbo la Kilolo Prof. Peter Msola akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwatasi katika kata ya Bomalang'ombe katika jimbo la Kilolo wilayani Kilolo Mkoani Iringa.
 baadhi ya wakazi wa kijiji cha Mwatasi waliohudhuria mkutano wa hadhara katika kiwanja cha shule ya msingi Mwatasi wakisikiliza hotuba ya mbunge wao Prof Peter Msola
 Mmoja wa wakazi wa jimbo la Kilolo, Ayubu Sanga akitoa taarifa ya kijiji cha Mwatasi mbele ya Mbunge wa jimbo hilo Prof. Peter Msola


 -============ 
Na Denis Mlowe, Kilolo
 
MBUNGE wa jimbo Kilolo, Profesa Peter Msola amewataka wananchi wa jimbo hilo kuwekeza katika elimu kwa kuwapeleka watoto wanaotakiwa kuanza shule na kuondokana na janga la kukosa elimu katika wilaya hiyo.
 
Profesa Msola aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kilolo katika kijiji cha Mwatasi kata ya Bomalang’ombe wakati wa ziara ya siku moja kwa wananchi wa jimbo hilo juzi na kusisitiza umuhimu wa wazazi kuwaelimisha na kuwapatia elimu watoto wao.
 
Msola alisema kuna wazazi ambao wanashindwa kuwekeza katika elimu na kuwafanya watoto wao kukimbilia mijini ambapo maisha ya huko ni magumu bila kuwa na elimu na kuwataka kukazania elimu kwa watoto wao kwanza.
 
Alisema kuwa  maendeleo miongoni mwa jamii yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na kiwango cha uwekezaji katika elimu, ni vema jamii iwekeze kwa kiwango kikubwa katika sekta ya elimu ili kujikwamua na umaskini uliopo na kupambana katika soko la ajira. 

“Tukumbuke kwamba kuwekeza katika elimu ni mkakati wa muda mrefu unaohitaji dhamira, subira na kwamba matokeo yake huonekana baada ya muda mrefu wa uwekezaji na faida kwa wazazi mara baada ya mtoto kusoma na kuweza kumsaidia pindi azeekapo” alisema Prof. Msola
 
Aidha Prof Msola alisema wilaya ya Kilolo ina rasilimali nyingi zinazohitaji viongozi wabunifu watakaohakikisha zinatumiwa vizuri kwa faida ya watu wote hivyo bila kuwekeza katika elimu rasimali hizo zitatumiwa vibaya na watu wasiojua faida ya elimu.
 
Aliongeza kuwa  katika mipango yake ya kuifikisha wilaya hiyo kwenye kilele cha mafanikio, atahakikisha barabara zinazotakiwa kuiunganisha wilaya hiyo na wilaya nyingine zaidi zinajengwa.
 
Alisema hatua hiyo itaongeza shughuli za uwekezaji, utalii, kilimo na biashara na hivyo kuwaongezea kipato wananchi wake.

RAIS KIKWETE MGENI RASMI SHEREHE ZA MIAKA 75 YA KANISA LA TAG JIJINI MBEYA LEO

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia maelfu ya wananchi kwenye  kilele cha Sherehe za Miaka 78 ya kanisa la Tanzania Assemblies of God  katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya leo Julai 13, 2014. 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua kitabu cha  Tanzania Assemblies of God (TAG) akiwa na  Askofu Mkuu wa TAG Dkt Barnabas Weston Mtokambali  wakati wa kilele cha Sherehe za Miaka 78 ya kanisa hilo katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya leo Julai 13, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhiwa tuzo na Askofu Mkuu wa Tanzania Assemblies of God (TAG) Dkt Barnabas Weston Mtokambali wakati wa kilele cha Sherehe za Miaka 78 ya kanisa hilo katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya leo Julai 13, 2014.PICHA NA IKULU

Mahojiano na washiriki wa maonyesho ya Utamaduni wa Kenya hapa Washington DC

$
0
0
Kati ya Juni 25 na Julai 6, jiji la Washington DC lilikuwa mwenyeji wa maonyesho ya kila mwaka ya yanayohusu maisha a watu na jamii mbalimbali.
Mwaka huu, nchi ya Kenya ilishirikishwa, wakionyesha utamaduni wao na changamoto za kuzidumisha katika zama hizi za sayansi na teknolojia.
Kwanza Production ilipata fursa ya kutembelea maonyesho hayo na kuzungumza na baadhi ya washiriki wa maonyesho hayo ambapo walieleza mengi ya kufurahisha.
KARIBU UUNGANE NASI

Zaidi ya washiriki 100 kutoka nchini Kenya waLIkuja hapa jijini kuonyesha mambo mbalimbali kama kutengeneza vyungu kwa ufinyanzi, uchongaji vinyago, mapambo ya shanga, useremala, nakshi za majengo, ujenzi wa majahazi, mapishi , muziki na mengine yanayotunza utamaduni wa nchi hiyo
Maelezo ya ujenzi na sehemu za JAHAZI (DHOW) toka kwa Ali Skanda aliyetoka Lamu Kenya
Na mtangazaji mkongwe abdushakur Aboud mbele ya Jahazi lililoletwa kwenye makumbusho ya hapa Washington DC kutoka Lamu nchini Kenya
Mtaalamu wa mapambo yatokanayo na shanga na usimamizi wa filamu nchini Kenya Emmah Irungu.
Mwandishi wa habari kutoka Kenya BMJ Mureithi
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images