Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 30 | 31 | (Page 32) | 33 | 34 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Meneja Masoko na Mauzo wa kampuni ya Push Media Mobile, Rodney Rugambo akisisitiza jambo baada ya kupatikana kwa washindi wa ‘Valentine Campaign’ ambapo Mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Makongo, Mudhir Ndonya alishinda gari aina ya Vitz lenye thamani y ash milioni 8. 

  =======  ======  =======
  MWANAFUZI wa  shule ya Sekondari ya Makongo, Mudhir Ndonya (20) ameshinda zawadi ya gari aina ya Vitz kufuatia shindano la siku ya wapendanao (Valentine campaign) lililomalizika Februari 14.


  Mbali ya droo ya Vitz lenye thamani ya sh Milioni 8, pia washindi mbali mbali walipatikana katika siku ya mwisho wa shindano hilo lililofanyika kwenye ofisi za African Media Group (AMG). Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Push Media Mobile Rodney Rugambo alisema kuwa Ndonya ameibuka mshindi  baada ya namba yake kuibuka ya kwanza katika shindano hilo lililodumu kwa takribani miazi mitatu na kutumia zaidi ya sh milioni 30.


  Rugambo alisema kuwa wahsindi wengine katika droo hiyo ni Daudi Samson (22) ambaye pia ni mwanafunzi aliyejishindia Ipad, Tabia Lihonde (44) ambaye ni nesi anayefanya kazi Mtwara na kuibuka mshindi wa simu ya mkononi aina ya blackberry na Emmanuel Sanga aliyeshinda home theare.


  Akizungumza kwa baada ya ushindi huo, Ndonya alisema kuwa amefurahi sana kwani ndoto yake ya kushinda gari imetimia. “Nilishiriki katika shindano kama washindani wengine, ndoto yangu ilikuwa ni kushinda, nashukuru nimeshinda na ushindi huu ni chachu ya kuendelea kushiriki katika mashindano mengine yajayo, ” alisema  Ndonya. Mbali ya Push Media Mobile, droo hiyo pia iliendeshwa na kituo cha televisheni cha Channel Ten na Radio ya Magic FM na kudhaminiwa na Alliance Insurance.  0 0  0 0
  Mstahiki Meya wa manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Mh. Jerry Silaa akizungumza na wananchi wa Kata yake ya Gongo la Mboto ambapo amewasihi viongozi wa CCM ngazi za Chini kuhakikisha wanafuatilia na kutafutia ufumbuzi kero zinazo wakabili watu wanaowazunguka.

  Mstahiki Meya ametumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi na wana CCM kwa ujumla kufuatia kuteuliwa na Mh.rais kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na kusema ofisi za chama zinatakiwa kuwa wazi kuanzia ngazi ya kata mpaka mkoa ili wananchi waweze kufika kutoa kero zao. Aidha amewataka viongozi wenzake kufanyakazi kwa ushirikiano na uadilifu, na kuwa wale viongozi wachache wasio waadilifu watashughulikiwa kikamilifu ili kuleta ufanisi ndani ya chama.
  Jerry Silaa akivishwa lubega ya kimasai baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana Gongo la Mboto jijini Dar.

  Baadhi ya wananchi wa Gongo la Mboto wakichukua taswira ya Diwani wao Jerry Silaa wakati wa mkutano wa hadhara.
  Mmoja wachekeshaji katika mikutano ya CCM wanaofahamika kama Aki na Ukwa akimwombea Dua Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa mara baada ya kuzungumza na wana CCM wa Gongo la Mboto.
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa akisalimiana na wananchi wa Gongo la Mboto mara baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara.
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa akisalimiana na mmoja wa watoto waliohudhuria kwenye mkutano wa hadhara.
  "Asante kwa kuonyesha upendo...Mume wa mtu mie" ndivyo anavyoonekana kusema Mh. Jerry Silaa akimwambia mwana CCM mkereketwa aliyekwenda kumfuta jasho kwa kutumia Khanga yake.


  Baadhi ya kinamama wa Gongo la Mboto ambao ni wananchama wa CCM wakiwasili kwenye Uwanja uliopo karibu na reli Gongo la Mboto katika mkutano wa hadhara wa kumpongeza Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Jerry Silaa baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa. (Picha na Zainul Mzige wa Mo Blog).

  Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmshauri Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akisalimiana na waendesha Boda boda wa Gongo la Mboto waliofika kumlaki akitokea mjini Dodoma.
  Msafara wa waendesha Boda boda ukimsindikiza Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa kwenye viwanja vya Gongo la Mboto alipoandaliwa sherehe ya kumpongeza iliyoenda sambamba na mkutano wa hadhara.
  Watoto waliokuwa pembezoni mwa barabara wakimpungua kwa furaha Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa alipokuwa akipita na msafara wake.
  Pichani Juu na Chini ni baadhi ya viongozi wa CCM wakimlaki Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa katika Ofisi za CCM kata ya Gongo la Mboto alipopita kutia baraka ofisi hizo akielekea kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa kwa ajili ya kumpongeza.
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmshauri Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa akitia saini kitabu cha wageni cha Ofisi za CCM kata ya Gongo la Mboto.
  Waendesha boda boda wa Gongo la Mboto wakitia mbwembwe katika mkutano wa hadhara ulioenda sambamba na sherehe za kumpongeza Jerry Silaa aliyeteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
  Msafara wa Jerry Silaa ukiwasili uwanjani hapo kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Gongo la Mboto.
  Mjumbe wa kamati kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa akipunga mkono kwa wananchi, WanaCCM waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara ulioenda sambamba na sherehe za kumpongeza kuchaguliwa nafasi nyeti ya Chama cha Mapinduzi.
  Mjumbe wa Kamati kuu na Halmashauri kuu ya CCM taifa Jerry Silaa akivishwa skafu ya chama mara baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Gongo la Mboto.

  Pichani juu na chini ni Baadhi WanaCCM wa kata ya Gongo la Mboto wakimpongeza Jerry Silaa baada ya kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati kuu na Halmashauri kuu ya CCM Taifa wakati wa mkutano wa hadhara ulioenda sambamba na sherehe za kumpongeza katika viwanja vya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya umati wa wakazi wa Gongo la Mboto wakubwa kwa wadogo waliohudhuria mkutano wa hadhara ulioenda sambamba na sherehe za kumpongeza Jerry Silaa.
  Wanenguaji wa Mashujaa Band wakicheza staili ya Boda boda na Wana CCM wa Gongo la Mboto wakati wa mkutano wa hadhara.
  "UTU UZIMA DAWA KWA RAHA ZETU"...Rappa wa Bendi ya Mashujaa akicheza sambamba na kinamama wa Kata ya Gongo la Mboto wakati wa sherehe za kumpongeza Jerry Silaa zilizoenda sambamba na mkutano wa hadhara.
  Jukwaa kuu la viongozi mbalimbali wa chama cha Mapinduzi (CCM) walioshiriki katika mkutano wa hadhara uliofanyika mwishoni mwa wiki Gongo la Mboto jijini Dar.
  Katibu Mwenezi wa CCM Mtwara Bw. Haroun Maarifa akitoa salamu kwa wana CCM wa Gongo la Mboto wakati wa mkutano wa hadhara ulioenda sambamba na sherehe za kumpongeza Jerry Silaa.
  Wana CCM wa Gongo la Mboto wakitia manjonjo kwenye mkutano huo.
  Mbunge wa Ukonga Mh. Eugene Mwaiposi akizungumza na wananchi wa Gongo la Mboto wakati wa mkutano wa hadhara ulioenda sambamba na sherehe za kumpongeza Jerry Silaa ambapo amezungumzia mambo mbalimbali ya maendeleo ya Wakazi wa jimbo lake yanayopangwa kufanywa na Serikali kwa manufaa ya wakazi wa maeneo hayo.
  Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Abillahi Mlewa akizungumza machache na wananchi wa kata ya Gongo la Mboto kabla ya kumkaribisha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa kuhutubia wananchi katika mkutano huo.
  Mjumbe wa kamati kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa Jerry Silaa akisindikizwa Jukwaani kwa staili ya aina yake ya kufagiliwa njia na WanaCCM waliokuwa wakibiringika mpaka kwenye ngazi za jukwaa. Anayemsindikiza ni Diwani wa Kata ya Tabata Hajati Mtumwa Mohamedi.
  "Karibuni kwenye Chama chenye mshikamano na Sera za Ukweli" ndiyo maneno ya Mjumbe wa kamati kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa wakati akigawa kadi kwa Wanachama wapya wa Gongo la Mboto walipoamua kujiunga baada ya kukolewa na sera za CCM wakati wa mkutano huo.
  Zoezi la ugawaji kadi kwa wanachama wapya likiendelea. Kulia ni Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Abillahi Mlewa.
  Pichani juu na chini ni Wanachama wapya wa CCM wakila kiapo mbele ya Mjumbe wa kamati kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa na viongozi mbalimbali wa Chama wakati wa mkutano wa hadhara ulioenda sambamba na sherehe za kumpongeza Jerry Silaa.

  0 0


  FAMILIA  ya Marehemu Mathew Ndesamburo Chao wa Mazimbu Morogoro, inasikitika kuwatangazia Msiba wa Binti yao Mpendwa Grace Chao kilichotokea leo asubuhi katika Hospitali ya Agha Khan jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa Matibabu.

  Mipango ya Mazishi kwa sasa inafanyika nyumbani kwa dada wa Marehemu Yombo kwa Abiola jijini Dar es Salaam na Maiti itasafirishwa kesho Jumaane kwenda Mazimbu Morogo na kutolewa heshima kwa ndugu jamaa na marafiki waishio Morogoro Mjini na Mzumbe.

  Jumatano Mwili wa Mpendwa wetu Grace Chao, utasafirishwa kutoka Mazimbu Morogoro kwenda Marangu Mamba kwa Makundi kwa mazishi.

  Mwana Mzumbe na Morogoro kwa Ujumla tunaombwa sana kushirikiana na Familia ya Marehemu katika kipindi hiki kigumu cha Maombolezo.

  Taarifa hii ni kwa Mujibu wa Kaka wa Marehemu, Edwin Chao.
              
  Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa Jina lake Lihimidiwe.

  0 0

   Mwandishi mkongwe wa Habari na pia ni mkufunzi wa waandishi wa Habari Salim Saidi Salim akiwajenga uwezo waandishi wa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar katika semina iliyo fanyika katika ukumbi wa Tume ya Utangazaji kikwajuni mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga Maelezo Zanzibar.
   -Mkurugenzi mipango sera na utafiti Mwita Masheko Hasan(wakushoto)akifungua semina ya siku 5 ya kuwajenga uwezo waandishi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar yaliyofadhiliwa na Shirika la UNESCO huko katika ukumbi wa Tume ya Utangazaji kikwajuni mjini Zanzibar. 

  -Baazi ya waandishi wa habari wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar wakimsikiliza kwa makini Mundishi mkongwe na pia ni mkufunzi wa wandishi wa Habari Salim Saidi Salim hayupo pichani katika Semina ya siku 5 ya kuwajenga uwezo waandishi wa Habari yaliyofadhiliwa na Shirika la UNESCO huko katika ukumbi wa Tume ya Utangazaji kikwajuni mjini Zanzibar.

  0 0

   Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa (MB) leo ametangaza rasmi matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Nne, maarifa na QT.

  Jumla ya watahiniwa waliofaulu kwa Mujibu wa Matokeo hayo ni 23520 kuanzia daraja la I hadi la IV huku katika mchakato huo wasichana waliofaulu katika mchakato huo ni 7178 na wavulana ni 16342.Aidha Waziri Kawambwa amesema kuwa waliofaulu kwa daraja la kwanza ni 1641, daraja la pili ni 6495 na daraja la tatu ni 15426 na walio feli ni 24903.

  Shule bora ni pamoja na St. Francis Girl ya Mbeya, Marian Boys ya Bagamoyo, Feza Boys Dar es Salaam, Marian Girls Bagamoyo na Simini,hizo ndizo zilizopo kwenye tano bora huku shule nyingine ni Kanosa, Jude, St. Mary.
    Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa (MB) akimuelekeza jambo Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo.Mh Philipo Augustino Mulugo kabla ya kuanza  kutangaza matokeo ya kidato cha nne mbele ya baadhi ya  wanahabari wa vyombo mbalimbali,kwenye makao makuu ya ofisi za wizara hiyo jijini Dar.
  Baaadhi ya  wanahabari kutoka vyombo mbalimbali,wakiwa ndani ya ofisi za makao makuu ya Wizara hiyo jijini Dar wakiwajibika.


  0 0  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Kiongozi wa Kanisa la Orthodox Pope Theodoros II (wapili kushoto) mara baada ya kufanya mazungumzo na kiongozi huyo ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Askofu wa Mwanza na Bukoba Askofu Jeronymos. Nyuma ya Rais mwenye tai nyekundu ni mwenyekiti wa Hellenic society of Tanganyika Dimitris Mantheakis, na kulia ni askofu mkuu wa Dar es Salaam na mashariki askofu Dimistrious.picha na Freddy Maro.


  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Kiongozi wa Kanisa la Orthodox Pope Theodoros II ikulu jijini Dar es Salaam.

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Kiongozi wa Kanisa la Orthodox Pope Theodoros II ikulu jijini Dar es Salaam leo.Kiongozi huyo wa Kanisa la Orthodox yupo hapa nchini kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine atatembelea miradi mbalimbali inayoendeshwa na kanisa hilo hapa nchini ikiwemo Zahanati na shule ya msingi Iringa pamoja na Hospitali ambayo inaendelea kujengwa huko Bukoba Mkoani Kagera.

  0 0


  0 0

  Meli ya kivita  ya kupambana na uharamia aina ya  Anti Submarine iitwayo  Marshal Shaposhnikov’,  ilipokuwa ikiingia na kasha baadae kutia nanga katika bandari ya Dar es Salaam, kwa ziara fupi yenye lengo la kuimarisha urafiki baina ya Jeshi la Wanamaji wa Tanzania na Urusi. Wakati nchi ya Somalia ikiendelea kuwa kitovu cha uharamia, jumuiya ya kimataifa ilikubaliana kudhamiria kupambana na vitendo hivyo viovu. Lakini hadi sasa, wakati nchi nyingine zikitumia mbinu mbalimbali katika mapambano hayo, ni nchi za Russia, India na China pekee zinazosindikiza meli zao za biashara na nyinginezo ili kuzilinda na uharamia. Meli hiyo imewasili siku ya Jumamosi na inategemea kuondoka kesho, Jumatano.
  Balozi wa  Urusi hapa nchini Mheshimiwa Alexander Rannikh  akiambatana na kiongozi wa wanajeshi waliofatana na meli hiyo Rear Admiral Vdovenko
  Kwa pamoja, Balozi Rannikh na wanajeshi wa Kirusi waliimba wimbo wao wataifa wakiwa katika meli.

  Balozi Rannikh akiwapongeza wanajeshi wake kwa kufika Dar es Salaam, Tanzania na kuwakaribisha nchi pia.
  Baada ya salamu hizo, Balozi Rannikh nae alikaribishwa keki na mmvinyo iliyoandaliwa na wanajeshi katika meli.
  Balozi wa  Urusi hapa nchini Mheshimiwa Alexander Rannikh akipokea salamu kutoka kwa  kiongozi mkuu Rear Admiral Vladimir Vdovenko wakati alipotembelea meli hiyo bandarini.

  Wanajeshi wa Kirusi wakionesha umahili wao wa ukakamavu 

  0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa amekabidhi pikipiki nne za miguu mitatu maarufu kama Bajaji ambazo ni maalum kwa kubebea mizigo zenye thamani ya kiasi cha shilingi millioni 50,kwa umoja wa vijana wilaya ya Monduli ili kuwasaidia vijana waliokuwa wakikakabiliwa na tatizo la Ajira.Pichani ni Mh. Lowassa akikabidhi funguo za pikipiki hizo kwa mmoja wa viongozi wa matawi ya vijana wilayani hapo,ambao walifika nyumbani kwake Ngarash Monduli kwa ajili ya kupokea pikipiki hizo.  0 0

  Umati wa wananchi wa Goba kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na CCM Mkoa wa Dar es salaam.

  Profesa Jumanne Maghembe akihutubia wakazi wa Goba na kutoa majibu ya kuridhisha kuhusu mikakati na mipango ya kuleta maji Goba.


  Mwenyekiti wa CCM ,Mkoa wa Dar es salaam akihutubia wananchi wa Goba katika mkutano wa hadhara uliofanyika 

  Mwenyekiti wa  CCM Kata ya Goba,Theresia Chihota akiukaribisha ugeni kutoka CCM Mkoa wa Dar es salaam na CCM Taifa ambao walifika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Goba

  Mtela Mwampamba akihutubia wananchi wa Goba sababu zilizomfanya ajiunge na chama cha CCM.

  Juliana Shonza aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA,akihutubia wakazi wa Goba 
  Sura za furaha zinazoashiria jimbo la Ubungo linarudi CCM

  Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi ,Nape Nnauye amekabidhi pikipiki kwa vijana wa Goba kwa shughuli za ujasiriamali,pia amewapa wakina mama wenye kikundi cha Vikoba shilingi milioni moja na pia ameahidi kuongeza pikipiki na jezi za timu ya mpira.

  Mkutano wa hadhara wa CCM, uliofanyika Goba umeongeza wananchama wapya 162, na wengine wanne kutoka chama cha upinzani,pichani mmoja wa aliyekuwa mwanachama wa Chadema akirudisha kadi yake na kujiunga na CCM.


  0 0  0 0


  0 0

  Mnenguaji Maarufu nchini Mwajuma Thabiti ' Mwajuma jimama' akifanya vitu vyake mbele ya mwimbaji wa bendi ya Mashauzi Classic, Isha Ramadhani wakati bendi hiyo ilipofanya onesho lake katika ukumbi wa TCC Chang'ombe Dar es salaam picha na www.burudan.blogspot.com

  0 0

    wawakilishi wa Tanzania katika timu ya ushangiliaji ya Afrika Filbert Nestory and Yahya Hamza wakiwa katika moja ya maeneo ya michezo nchini Afrika ya kusini wakati wakishiriki kwenye mjumuiko wa ushangiliaji kwenye mchezo baina ya bukinafaso na Nigeria
   Filbert Nestory.  hapa akionyesha umahiri wake kwenye ushangiliaji kwenye mjumuiko wa ushangiliaji kwenye mchezo baina ya bukinafaso na Nigeria


  wawakilishi wa kutoka nchi mbalimbali katika timu ya ushangiliaji ya Afrika wakiwa katika moja ya maeneo ya michezo nchini Afrika ya kusini wakati wakishiriki kwenye mjumuiko wa ushangiliaji kwenye mchezo baina ya bukinafaso na Nigeria.

  0 0
 • 02/19/13--00:49: kaazi kweli kweli


 • 0 0

   Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu Tanzania (TAS) "Tanzania Albino Society" ndugu Ernest Kimaya akizungumza kwa uchungu mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (Pichani chini) kuelezea juu ya tukio la kinyama alilofanyiwa Maria Chambanenge (39) la kukatwa mkono wake wa kushoto kwa kile kinachodaiwa kwa imani za kishirikina kuwa ni kupata utajiri. Watuhumiwa waliohusika na tukio hilo ambao pia yupo mume wake na muathirika wameshakamatwa na polisi na kuonyesha mkono huo, taratibu za mashitaka zinaendelea ili haki iweze kupatikana. Mwenyekiti huyo ameiomba Serikali kufkiria adhabu kali kwa watuhumiwa kama ho ikiwepo kunyongwa ili fundisho kwa wengine na Albino waweze kuishi katika nchi yao kwa amani. 
   Mwenyekiti wa TAS akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ofisini kwake. Kulia ni Katibu Mkuu wa chama hicho ndugu Mohammed Chanzi. 
   Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza kwa uchungu na kutoa onyo kali kuwa vitendo hivyo vya kinyama havitavumiliwa. Alitoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kutokomeza vitendo hivyo.
   Kabla ya kwenda kumtembelea mgongwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliandaa chakula kwa wageni wake. 
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na msafara wake pamoja na viongozi wa chama cha Albino Tanzania (TAS) wakimfariji Mama Maria Chambanenge walipomtembelea katika hospitali kuu ya Mkoa Rukwa ambapo hali yake kwa sasa inaendelea vizuri japo ameongezewa ulemavu mwingine wa viungo kwa kukatwa mkono wake wa kushoto.  
   Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu Tanzania (Albino) ndugu Ernest Kimaya akimfariji Mama Maria Chambanenge ambaye anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali kuu ya Mkoa Rukwa kufuatia kukatwa mkono wake wa kushoto na watu walioshirikiana na mume wake na ambao tayari wapo mikononi mwa polisi.

  NA HAMZA TEMBA - OFISI YA MKUU WA MKOA RUKWA
  .........................................................................................................................................................
  Mwenyekiti wa chama watu wenye ulemavu wa ngozi Tanzania "Tanzania Albino Society" (TAS) ndugu Ernest Kimaya ameiomba serikali kupitia upya sheria ya haki ya kuishi kwa kuwapatia adhabu kali ya kifo wale wote wanaohusika kwa vitendo vya kinyama dhidi ya albino ikiwepo mauaji na ukataji wa viungo vyao wakiwa hai kwa kile kinachoaminika katika imani za kishirikina kuwa ni kujipatia utajiri.
  Aliyasema hayo jana akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya ofisini kwake alipomtembelea akiongozana na viongozi wengine wa chama hicho kumpa pongezi zake za dhati kwa kile alichosema ni mfano wa kuigwa kwani tangu vitendo hivyo vianze hapa nchini kwa muda wa miaka mitano iliyopita ni Mkoa wa Rukwa pekee umefanikiwa kuwakamata wahalifu wa namna hiyo pamoja na kiungo husika kwa muda mfupi usiozidi siku tatu.
  Amesema kuwa maalbino wamenyanyasika sana katika nchi yao kwa kukosa uhuru na amani kama watu wengine jambo ambalo ni kinyume na haki za binadam. "Watu waliokamatwa sio wa kuachiwa huru, wabanwe hata kuchomwa moto wataje wahusika wengine kwani mtandao wao ni mmoja na inatia uchungu sana kwa sisi maalbino" alisema mwenyekiti huyo.
  Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alimshukuru mwenyekiti wa chama hicho na viongozi wenzake kwa kufika Mkoani kwake kujionea hali halisi baada ya kuskika kwa matukio hayo ya kinyama kwa Albino wenzao na pia kuwashukuru wananchi na jeshi la Polisi kwa ushirikiano mzuri walioutoa kufanikisha watuhumiwa kutiwa mbaroni ili haki iweze kutendeka. Mkuu huyo wa Mkoa alisema vitendo kama hivo kaamwe havitaweza kuvumilika Mkoani kwake.
  Kumekuwepo na matukio ya kusikitisha hivi karibuni ya ukatili kwa Albino ambapo mama mlemavu wa ngozi Maria Chambanenge (39) mkazi wa kijiji cha kavifuli katika Wilaya ya Sumbawanga alivamiwa nyumbani kwake usiku wa manane na kukatwa mkono wake wa kushoto na watuhumiwa ambao wameshakamatwa na jeshi la polisi na taratibu za mashitaka yao zinaendelea.
  Vilevile katika bonde la ziwa Rukwa kata ya Milepa mtoto wa kiume mwenye ulemavu wa ngozi ‘albino” Mwigulu Matomange Magessa mwenye umri wa miaka saba ameshambuliwa na vijana watatu waliovaa kininja na kumkata mkono wake mmoja na kutokomea na kusikojulikana. Polisi wanaendelea na uchunguzi kuwabaini wahusika.
  Matukio yote hayo yanahusishwa na wahalifu kutoka Mkoa jirani wa Mbeya ambapo vitendo hivi vya imani za kishirikina vimeshamiri. 

  0 0  Matokeo yaKidato cha Nne ya namna hii (zaidi ya nusu ya wahitimu kupata sifuri) na takribani asilimia 90 kufeli kwa kupata daraja la nne na daraja la sifuri ni mwaka tatu sasa mfululizo. Matokeo yakitoka tunasema weeee mpaka povu linatoka. Baada ya wiki tumeshasahau na hakuna hatua yeyote. Lazima Uwajibikaji utokee.

  kwanza Waziri lazima awajibike na Naibu wake na Katibu Mkuu na Kamishna. Najua kuwa haina uhusiano wa moja kwa moja maana matatizo ya elimu ni makubwa sana nchini. Lakini ni lazima kitu fulani kitokee ili kufanya mabadiliko. Uwajibikaji ni njia mojawapo inayoleta nidhamu na 'urgency' katika utendaji kazi.

  Tumwambie Rais aichukue Wizara ya Elimu, yaani Waziri wa Elimu awe yeye (kuwe na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Elimu). Tumwambie matokeo yakibaki hivi mwakani na yeye atatoka. Najua wa mwakani ndio wapo kidato cha nne sasa na wana msingi mbaya tayari lakini sio jukumu letu kujipa majibu bali ni jukumu letu kuiambia Serikali hapana.Tuwape Masharti. Vinginevyo haya yatakwisha na mwakani itakuja nk.

  Hawa watoto wanakwenda wapi? Mwaka jana tulisema mpango wa kujenga vyuo vya ufundi kila Halmashauri ya Wilaya uanze mara moja. Katika Bajeti Kivuli mwaka 2011 tulipiga hesabu kwamba tunahitaji tshs 720 bilioni katika kipindi cha miaka 5 ijayo kujenga vyuo vya ufundi vya VETA kila Wilaya. Tukawaambia badala ya kukopa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kulipana posho ni vema tukope kuwekeza kwenye elimu maana Elimu ni Hifadhi ya Jamii. Elimu yetu ya sasa inazalisha matabaka kwneye jamii na ni hatari sana kwa uhai wa Taifa.

  Tunaweza kujidai kujenga madaraja na miji mipya. Tunaweza kujidai kujenga mabomba ya gesi na kusambaza umeme kila kijiji mpaka kwenye vyoo. Kama hakuna Elimu haya yote ni bure kabisa. Hata kukosa uvumilivu wa kiimani sasa hali itakuwa mbaya zaidi unapokuwa na Taifa la mambumbumbu. Waziri Kawambwa na wenzake watoke. Watoke SASA

  0 0

  The Human Resource Manager of African Barrick Gold's (ABG) North Mara Gold Mine, Elias Kasitila (left), receives an award from Zanzibar Second Vice President Seif Iddi as a valued contributing employer in the mining sector for compliance and timely payment of members' contributions to the National Social Security Fund (NSSF).
  The Human Resource Manager of African Barrick Gold's (ABG) North Mara Gold Mine, Elias Kasitila (left), poses with an award from the National Social Security Fund (NSSF) for compliance and timely payment of members' contributions. Lookin on from right are Zanzibar Second Vice President Seif Iddi, Labour Minister Gaudensia Kabaka and NSSF Director General Dr Ramadhani Dau.

  0 0

  Mkuu wa Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule na Meneja biashara wa kitengo cha Mahusiano Vodacom Bi.Lilian Kisamba,wakimkabidhi kompyuta kati ya 10 zenye thamani yua shilingi Milioni 7,Mwl.Joyce Martin wa shule ya sekondari ya wasichana ya MT.Theresa wa Avila.Iliyopo Mkoa wa Shinyanga Wilaya ya Kahama.
  Mkuu wa Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule (kushoto)akimkabidhi Bi. Jacquline Augustine moja ya kompyuta kati ya 10 zenye thamani ya Milioni 7 zilizotolewa kwa msaada na Vodacom Foundation kwenye shule ya sekondari ya wasichana ya MT.Theresa wa Avila,anaeshuhudia kulia ni Meneja biashara wa kitengo cha Mahusiano Vodacom Bi.Lilian Kisamba.
  Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya MT.Theresa wa Avila.Iliyopo Mkoa wa Shinyanga Wilaya ya Kahama,wakifatilia kwa ukaribu makabidhiano ya kompyuta kati ya 10 zenye thamani ya Milioni 7 zilizotolewa msaada na Vodacom Foundation.
  Baadhi ya wananchi na wazazi wa wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya MT.Theresa wa Avila.Iliyopo Mkoa wa Shinyanga Wilaya ya Kahama,walifika kushuhudia makabidhiano ya ya kompyuta kati ya 10 zenye thamani ya Milioni 7 zilizotolewa na Vodacom Foundation mwishoni mwa wiki.

older | 1 | .... | 30 | 31 | (Page 32) | 33 | 34 | .... | 1897 | newer