Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

MIKUTANO YA HADHARA YA WAZIRI WA UJENZI NA MBUNGE WA CHATO DKT. JOHN MBUNGE KATIKA KATA MBALIMBALI.

$
0
0
 Mbunge wa Jimbo la Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Wanachama wapya wa Chama cha Mapinduzi (CCM) walioamua kujiunga na chama hicho mara baada ya Mbunge huyo kufanya Mkutano mkubwa wa hadhara katika kijiji cha Nyabugela, kata ya Mganza katika Wilaya ya Chato leo.
 Mbunge wa Jimbo la Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli kihutubia mamia ya wakazi wa kata ya Mganza katika Wilaya ya Chato leo
 Wananchi wa Kata ya Mganza wakimfurahia Mbunge wa Jimbo lao la Chato Mheshimiwa Dkt. John Magufuli wakati akiwahutubia na kuwasisitiza wafanye kazi kwa bidii ili waweze kujiletea Maendeleo
 Mbunge wa Jimbo la Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akiwapokea wanachama wapya zaidi ya 100  walioamua kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM mara baada ya mbunge huyo kumaliza hotuba yake
Wanachama wapya wa Chama cha Mapinduzi kata ya Mganza wakila kiapo mbele ya Mbunge wao Mheshimiwa Dkt.John Magufuli ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi baada ya kukabidhiwa kadi za uanachama hivi leo

KAMPUNI YA ORIFLAME YATAMBULISHA BIDHAA ZAKE KWENYE SOKO LA TANZANIA

$
0
0
Kampuni ya Vipozi vya aina mbalimbali vya urembo OriFlame wamefanya maonesho ya Bidhaa zao Tarehe 2.07.2014 katika ukumbi wa Zanzibar katika Hotel ya Hyatt Regency(The Kilimanjaro Hotel).
Kampuni hiyo yenye wigo mpana wa kibiashara ambayo ina matawi zaidi ya nchi 20 duniani na pia Katika Mabara manne ya Duniani wametambulisha bidhaa zao mpya kwenye soko la Tanzania ambazo ni marashi ya kike na kiume pamoja na vipodozi mbalimbali,
Juu Pichani ni  Maznat Yusuph Sinare kutoka saloon ya Maznat Bridal mtaalamu wa kuchanganya Vipodozi akimremba mwanadada Janeci Maluli ili kuonyesha aina tofauti za vipodozi vya Kampuni hiyo.
 Maza Yusuph Sinare  akimpaka wanja wa nyusi Mwanamitindo Janeci Maluli kwenye  sherehe za uzinduzi wa bidhaa mpya za kampuni ya ORIFLAME iliyofanyika kwenye ukumbi wa Zanzibar katika Hotel ya Hyatt Regency(The Kilimanjaro Hotel).
Mwanadada Janeci Maluli akiwa kwenye pozi baada ya kumaliza kurembwa kwa  kutumia Vipodozi vya kampuni ya ORIFLAME
Waandishi wa habari wakipata maelekezo kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya ORIFLAME  Fortunata Nkya
Fredrick Njoka akizungumza jambo na mkuu wa masoko wa kampuni ya Vipodozi ya ORIFLAME, Harry Nyagi katika sherehe ya uzinduzi wa vipodozi vipya kwenye ukumbi wa Zanziba Hotel ya Hyatt Regency(The Kilimanjaro Hotel).
Mkurugenzi mkuu wa ORIFLAME katika upande wa Afrika ya Mashariki bwana Klas Kronaas (kushoto) akizungumza jambo na mkuu wa masoko wa kampuni ya Vipodozi ya ORIFLAME, Harry Nyagi (katikati) na kuliani mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo Bi. Fortunata Nkya.
 
 Fortunata Nkya akizungumza na waandishi wa habari kwenye sherehe ya utambulisho wa bidhaa za ORIFLAME  katika soko la Tanzania
Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya ORIFLAME katika upande wa Afrika ya Mashariki bwana Klas Kronaas akielezea namna bidhaa zao zinavyotengenezwa kwenye kwenye sherehe ya utambulisho wa bidhaa zao katika soko la Tanzania
Bi. Maznat Yusuph Sinare akieleza namna bidhaa na vipodozi mbalimbali vilivyokuwa na ubora wa kimataifa kwenye uzinduzi wa vipodozi vipya vya kampuni ya ORIFLAME kwenye ukumbi wa
 Maznat Yusuph Sinare akimpaka meck up mmoja wa warembo kwenye uzinduzi wa bidhaa mpya ya kampuni ya ORIFLAME
Mwanamitindo Neema Mbuya akipita jukwaani kuonesha moja ya Ripstick kwenye sherehe ya uzinduzi wa bidhaa mpya za kampuni ya ORIFLAME nchini Tanzania
 Mwanamitindo Annie Moses akiweka pozi la nguvu wakati akionesha Lipstick Ya kupaka mdomoni kwenye uzinduzi wa Bidhaa za kampuni ya ORIFLAME
Mwanamitindo Janeci Maluli alipita jukwaani akionesha moja  ya Ripstick kwenye sherehe ya uzinduzi wa bidhaa mpya ya kampuni ya ORIFLAME
Mkuu wa masoko wa kampuni ya Vipodozi ya ORIFLAME, Harry Nyagi akizungumza  jambo kwenye sherehe ya uzindizi wa bidhaa mpya za kampuni ya ORIFLAME
Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya ORIFLAME katika upande wa Afrika ya Mashariki bwana Klas Kronaas akifanya uzinduzi rasmi kwa kufungua bango lililokuwa linaonesha bidhaa zao mpya
Mwonekano wa bidhaa zilizozinduliwa na kampuni ya ORIFLAME nchini Tanzania
Wageni walioalikwa kushuhudia uzinduzi huo wakijadiliana jambo kuhusiana na Bidhaa za kampuni ya ORIFLAME

Baadhi ya wadau waliofika kwenye uzinduzi huo wakifuatilia kwa makini maelekezo ya bidhaa za kampuni ya ORIFLAME

WATANGAZAJI WA CLOUDS FM WAZICHAPA KAVU KAVU STUDIONI,WAWAOMBA RADHI WASIKILIZAJI WAO.

$
0
0

Redio ya Clouds FM 88.5 ya Mikocheni jijini Dar es salaam leo imetoa ya mwaka wakati DJ Fetty na Dj Adam Mchomvu waliposikika wakizichapa live wakati kipindi kipo hewani. Juhudi za kuupata uongozi wa Clouds FM zinaendelea kutaka kujua mustakabali wa watangazaji hao maarufu nchini. Hebu sikiliza mambo yalivyokuwa. Bofya mshale mwekundu hapo..

MAMBO YAMEIVA NDANI YA BANDA LA MeTL GROUP KWENYE MAONYESHO YA SABASABA!

$
0
0
DSC_0004
Muonekano wa lango kuu la kuingia ndani ya banda la Makampuni ya MeTL Group kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yaliyozinduliwa rasmi jana kwa kupewa baraka na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Sefu Iddi katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
DSC_0008
Utajiuliza kwani LG wapo ndani ya Banda la MeTL Group kwenye maonyesho ya Sabasaba kwa sababu MeTL Group wamekuwa Mawakala waliothibitishwa Tanzania nzima (Authorized Dealers) kuuza vifaa vya LG nchini. USISAHAU KUJINADIKISHA KWA AJILI YA DROO YA BAHATI NASIBU ITAKAYOCHEZESHWA TAREHE 7 MWEZI HUU NDANI YA BANDA LETU...!
DSC_0120
Kampuni ya MeTL Group inahusika pia na masuala ya Vitenge, Khanga, Mashuka na n.k Njoo upendeze mwanamke na vitenge bora na imara kutoka MeTL Group.....Sikukuu ya Eid ilee na maandalizi yawe mapema kabisa...!
 
DSC_0125
Wakazi wa jiji la Dar wakivinjari ndani ya Banda la Mohammed Enterprises Tanzania Ltd. (MeTL Group) kujipatia mahitaji mbalimbali za bidhaa bora kabisa kwa bei nafuu msimu huu wa Sabasaba.
DSC_0151
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar wakiangalia na kupata maelezo ya bidhaa mbalimbali kama TV, Music System, Simu za mkononi za nyingine nyingi kutoka kampuni ya LG ambapo MeTL Group ndio Authorized Dealers pekee nchini Tanzania.
DSC_0124
Muonekano wa ndani wa Banda letu la MeTL Group ukiwa umenakshiwa kwa mabango pamoja na TV za LG zinazoonyesha matangazo mbalimbali ya bidhaa zetu.
DSC_0136
Mmoja wa wateja akipata maelezo kutoka kwa wataalamu wetu waliobobea wa vipozi kwenye banda letu la MeTL Group.
DSC_0117
Watu wanatakaje kupendeza.....!! bado wewe tu hujajipatia kitenge chako na Khanga....kwa bei nafuu kabisa katika msimu wa Sabasaba.
DSC_0360
Baadhi ya ushers wanaotohuduma kwa wateja ndani ya banda la MeTL GROUP wakipozi kwenye Big Screen ya LG inayoonyesha tangazo la bidhaa mpya ya "MO BEAUTY SOAP" ambapo Balozi wake ni mrembo aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania namba mbili JOKATE MWEGELO.
DSC_0238
Mmoja wa kikundi cha uhamasishaji kwenye banda la MeTL Group akikata kiu yake na kinywa chenye ladha tamu kabisa ambacho kitaingia sokoni hivi karibuni "MO Portello" kinachouzwa ndani ya banda hilo.
DSC_0240
Aaaah kinywaji safi kabisa...sasa nimekata kiu yangu...!! Unakaribishwa na wewe pia kukijaribu kinauzwa kwa bei nzuri kabisa ya offer katika msimu huu wa Sabasaba.
DSC_0242
Mimi napenda "MO Portello" wewe je....??
DSC_0292
AGRO MeTL wauzaji wa Mbolea na Matrekta ya kisasa ambayo ni imara na bora kwa mazingira yetu ya Tanzania yapo kwenye banda letu...Kilimo kwanza ndio mpango mzima...!!
DSC_0109
Mambo ya Katani yanahusika pia ndani ya banda la MeTL Group kwenye viwanja vya Sabasaba.
DSC_0131
Mambo ya Ugali, Maandazi na bidhaa mbalimbali za nafaka zinapatikana pia bila kusahau MO SEMBE..Unga safi kabisa wa kupikia.
DSC_0142
Mambo ya usafi pia yanahusika jamani eeeeh...Sabuni za kufulia za unga zenye kuondoa madoa sugu na uchafu wa aina zote zinapatikana pia wewe tu na pochi lako.
DSC_0224
Watoto wakipata maelezo kutoka kwa mhudumu wa vinywaji vya MeTL Group kwenye banda letu ndani ya maonyesho ya Sabasaba.
DSC_0236
Watoto wakipata Ukodak baada ya kuyakubali maji safi ya kunywa kwa gharama nafuu kabisa yanayotengenezwa na MeTL Group.
DSC_0253
Kata kiu yako kwa kujichagulia kinywaji ukipendacho hapa ndani ya banda la MeTL GROUP.
DSC_0345
Mmoja wa wateja akiangalia tangazo la bidhaa mpya ya MO BEAUTY SOAP ambapo Balozi wa sabuni hiyo ni mrembo aliyewahi kushitaji la Miss Tanzania namba mbili JOKATE MWEGELO.
DSC_0332
DSC_0113
Mfanyakazi wa MeTL Group akitoa maelezo ya ubora wa maji safi ya kunywa yenye viwango vya kimataifa. Unakaribishwa sana kuuliza maswali mbalimbali ndani ya banda letu.
DSC_0264
Kikundi cha NOMA SANA Group kikitoa burudani nje ya banda la MeTL Group kuwatumbuiza wakazi wa jiji wanaotembelea maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba yanayoendelea jijini.Kwa picha zaidi ingia hapa

TASAF YAWANOA MAKALI WATAALAMU WAELEKEZI WAKE .

$
0
0

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF umeajiri Wataalamu waelekezi ( TA) ambao watatoa huduma katika halmashauri mbalimbali nchini kwa lengo la kusimamia ipasavyo shughuli za Mpango wa kunusuru kaya masikini na zinazoishi kwenye mazingira hatarishi PSSN.Watalaam waelekezi hao wako katika mafunzo kwenye ukumbi wa CEEMI jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF ,Ladislaus Mwamanga (wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wataalam Waelekezi wapya (TA)ambao wako katika mafunzo ya namna ya utekeleza majukumu yao katika Mpango wa Kunusuru Kaya masikini PSSN ulioko chini ya TASAF awamu ya TATU. Walioketi ni baadhi ya wakurugenzi na mameneja wa TASAF.

Mkurugenzi  Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF ,Ladislaus Mwamanga (aliyesimama) akitoa hutuba ya ufunguzi wa mafunzi ya Wataalam Waelekezi (TA) walioajiriwa na TASAF kwa ajili ya kuhudumia Halmashauri za wilaya mbalimbali nchini (hawapo pichani)ikiwa ni mkakati wa kufanmikisha Mpango wa kunusuru kaya masikini nchini.
 Baadhi ya wataalamu Waelekezi TA wapya walioajiriwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF wakisikiliza hoyuba ya ufunguzi wa mafunzo yao katika ukumbi wa CEEMI ambayo ilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Ladislaus Mwamanga hayupo pichani  ambaye pamoja na mambo mengine alisistiza umuhimu wa wataalamu hao kufanya kmazi kwa uaminifu na kujituma na kushirikisha sekta nyingine kwenye halmashauri watakazopangiwa.
 Baadhi ya Wataalam waelekezi  wapya (TA ) watakaotoa huduma katika halmashauri mbalimbali nchini wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga hayupo pichani wakati alipofungua mafunzo elekezi ya namna ya kutekeleza majukumu yao kikamilifu kwa lengo la kufranikisha Mpango wa Kunusuru Kaya masikini nchini,PSSN.
 Meneja Rasilimali watu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF Bi Thecla  Makundi (aliyeshika tama)akimsikiliza kwa makini mmoja wa Wataalamu Waelekezi wapya alipokuwa akitoa maelezo katika mafunzo ya watalaam hao yanayofanyika kwenye ukumbi wa CEEMI jijini DSM.

TBL YATWAA TUZO YA UDHAMINI MAONESHO YA SABASABA DAR

$
0
0
Meneja wa Mawasiliano ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emma Oriyo , akifurahia tuzo ya udhamini kwa upande wa vinjwaji katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa baada kuipokea kutoka kwa  Makamu wa Pili wa  Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi, Seif Alli Idd Dar es Salaam.Katikati ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdalla Kigoda.

KAMATI YA BUNGE YA UCHUMI, VIWANDA NA BIASHARA YAIWAGIA SIFA MFUKO WA PENSHENI WA PPF KWA HUDUMA NZURI ZINAZOTOLEWA NA MFUKO HUO

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mh William Erio (wa kwanza Kushoto) akiongea na wabunge wa Kamati ya Uchumi, Viwanda na Biashara wakati wabunge hao walipotembelea Banda la PPF katika Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar Es Salaam yanayoendelea Kufanyika katika Viwanja Vya Sabasaba Jijini Dar Es Salaam.Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mh Luhoga J Mpina.
 Wabunge wa Kamati ya Uchumi, Viwanda na Biashara wakisikiliza maelezo kuhusiana na huduma mbalimbali zitolewazo na mfuko wa Pensheni wa PPF kutoka Kwa afisa uendeshaji wa Mfuko wa PPF kanda ya Ziwa, Bi Grace Balele (mwenye suti nyekundu) wakati walipotembelea banda la PPF kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar Es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba vilivyopo katika Barabara ya Kilwa Jijini Dar Es Salaam. Wa Kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mh William Erio.
 Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Mh William Erio (wa kwanza kushoto) akiwapatia maelezo ya ziada wabunge wa kamati ya Uchumi , Viwanda na Biashara wakati walipotembelea banda la PPF katika Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar Es Salaam yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar Es Salaam.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uchumi , Viwanda na Biashara, Mh Luhago Mpina (aliyenyoosha mkono) akiuliza swali kwa Mfanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakati walipotembelea banda la PPF katika maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar Es Salaam yanayoendelea kufanyika.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mh William Erio akiwaonyesha Wabunge wa kamati ya Uchumi, Viwanda na Biashara michoro ya Majengo inayoonekana kwenye runinga (haipo pichani) yanayotarajiwa kujengwa na PPF ikiwa njia mojawapo ya uwekazaji utakaofanywa na Mfuko Wa Pensheni wa PPF.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mh William Erio akiwaonyesha wabunge wa kamati ya Uchumi, Viwanda na Biashara miradi mbalimbali inayotarajiwa kuanza kutekelezwa na mfuko huo wakati wabunge hao walipotembelea banda la PPF katika Maonyesho ya Sabasaba aliyesimama ni Afisa Uwekezaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Anna Shayo.Picha Zote na Josephat Lukaza - Lukaza Blog

MJUE SuperModel wa Kibongo

$
0
0




Mfahamu mwanamitindo maarafu wa kiwango cha kimataifa Herieth Paul, ambaye ni raia wa Tanzania aneyeishi nchini Canada.  

Mwanamitindo huyu mwenye umri wa miaka 18 anafanya shughuli zake jijini New York Marekani, London Uingereza na Milan Italia. 

 Amesaini mkataba wa vipodozi na kampuni maarufu duniani ya Calvin Klein na ametokea katika kurasa mbele za majarida mashuhuri mbalimbali kama Elle Magazine, Teen Vogue na VogueItalia.  

Hivi karibuni pia mrembo huyu amekuwa miongoni mwa wanamitindo watatu waliochaguliwa katika kampeni ya kutangaza mavazi ya msimu wa spring ya mbunifu maarufu wa mavazi duniani, Tom Ford.

TWIGA BANCORP YAENDELEA KUTOA HUDUMA ZAKE NDANI YA VIWANJA VYA SABA SABA JIJINI DAR

$
0
0
 Katika kuboresha huduma za kibenki Twiga Bancorp,Afisa wa Benki hiyo,pichani kati Bi Tuddy Lutengano akimhudumia mteja pichani kulia katika banda lao lililopo kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwl.Julius Nyerere,Shoto ni Meneja wa Tawi lililopo ndani ya Maonyesho hayo,Bi. Upendo Tendewa akihakikisha huduma bora za kibenki zinafanyika na kukidhi haja kwa  wateja wao.
 Muonekano banda la Benki ya Twiga Bancorp lionekanavyo kwa nje ndani ya maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwl.Julius Nyerere,jijiniDar.
 Baadhi ya Wateja wakipata huduma za kibenki ndani ya Twiga Bancorp 
 Mmoja wa wateja wa Twiga Bancorp akipata maelezo kwa ufupi kuhusiana na huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo.
 Karibu:Baadhi ya Wafanyakazi wa Twiga Bancorp wakiwa nje ya banda lao kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwl.Julius Nyerere,jijini Dar.

Dk. Rehema Nchimbi afungua mkutano wa Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa,Dodoma

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi akifungua mkutano wa mwaka uliowakutanisha Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa mjini Dodoma leo.
Sehemu ya washiriki wa mkutano wa Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa wakimsikiliza mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi (hayupo pichani).
Sehemu ya Washiriki wa mkutano wa Wakuuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa hapa nchini wakipewa utaratibu wa siku ya kwanza.
Picha ya pamoja na waratibu wa mkutano wa Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa; Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. George D. Yambesi (watatu kutoka kushoto), akiwa na mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchini (wanne kutoka kushoto), na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (wa tano kushoto).

TPDC yaibuka kidedea kwenye maonesho ya Sabasaba

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Saif Ali Idd akifungua maonesho ya kimataifa ya Saba Saba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mtaalam kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Bi. Edith Simtengu akipokea kikombe cha ushindi kwa niaba ya washiriki wenzake.
Washiriki kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) wakiwa katika picha ya pamoja na kikombe cha ushindi mara baada ya kuibuka washindi wa kwanza katika kundi la makampuni ya mafuta na gesi katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
Mtaalam kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Bw. Emmanuel Gilbert akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda hilo kwenye maonesho ya kimataifa ya Saba Saba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.


Greyson Mwase na Malik Munisi.

Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) limeibuka kidedea na kukabidhiwa kikombe cha ushindi katika kundi la mashirika ya petroli na mafuta nchini baada ya kuyabwaga chini mashirika megine mengi yaliyokuwa yanawania kikombe hicho katika maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere vilivyopo jijini Dar es Salaam.

Kikombe hicho kilikabidhiwa na mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi ambapo aliyataka makampuni mengine kuiga mfano wa TPDC katika uwekezaji kwa maendeleo ya nchi.

Balozi Iddi alisema ili nchi yoyote iweze kukua kiuchumi haina budi kuwekeza kupitia viwada na kusema kuwa serikali imeweka mkakati wa kuhakikisha kuwa viwanda vinachangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kikombe hicho kwa niaba ya TPDC msemaji wa shirika hilo na msimamizi wa banda Bw. Sebastian Shana amesema kuwa ushindi huo ni faraja kuwa kwa shirika hilo na kuongeza kuwa shirika hilo litaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuchangia ukuaji wa uchumi kupitia sekta za gesi na mafuta.

Akizungumzia siri ya mafanikio ya ushindi kwa shirika la TPDC Bw. Shana alisema kuwa ni kuanza maandalizi mapema na kujituma zaidi hali iliyopelekea shirika hilo kufanya vizuri zaidi.

Akizungumzia mikakati ya shirika hilo Bw. Shana alisema kuwa shirika hilo limepanga kufanya utafiti zaidi wa gesi na mafuta kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha nchi inapiga hatua kubwa kiuchumi.

“ Unajua nia ya serikali ni kuhakikisha kuwa nchi inakuwa katika kipato cha kati ifikapo mwaka 2025, na katika kuhakikisha serikali inafikia lengo hilo, TPDC ipo tayari kushirikiana na wadau wa ndani na nje ya nchi katika kuendeleza sekta ya gesi na hivyo kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi.” Alisema Bw. Shana.

Bwana Shana aliendelea kusema kuwa gesi iliyogunduliwa inachangia kwa zaidi ya asilimia 50 katika umeme wa gridi ya taifa na kusisitiza kuwa kama shirika, wako tayari kuweka nguvu zaidi katika utafutaji na uzalishaji wa gesi ili iweze kuwa na mchango mkubwa zaidi katika uzalishaji wa umeme.

Bw. Shana alisema kuwa TPDC imekuwa ikishirikiana na wadau wakuu kama Wizara ya Nishati na Madini ambayo imelisaidia shirika hilo kupiga hatua kubwa katika uendelezaji wa shughuli za utafutaji wa gesi na mafuta.

Hii ni mara ya saba kwa shirika hilo kujinyakulia vikombe kwenye maonesho ya kimataifa ya Sabasaba tangu lilipoanza kushiriki.

UN YAZIDI KUNG'AA MAONYESHO YA SABASABA, YATWAA TUZO YA "MACHAPISHO KWA UMMA

$
0
0
DSC_0218
Wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wakiwa kwenye picha ya pamoja ndani ya banda lao na nyuso za bashasha baada ya kunyakua tuzo ya Machapisho kwa Umma (Mass Media na Publicity) kwa mara ya tatu mfululizo kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yaliyozinduliwa rasmi jana na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Sefu Iddi katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar. Kutoka kushoto ni Programme Coordination Specialist wa UNAIDS, Jimmy Mbazi, Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama, Programme Officer wa Shirika la Kimataifa linalohusika na uhamiaji (IOM), Charles Mkude na Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu.
DSC_0232
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akifafanua jambo kwa wageni waliofika kwenye banda la Umoja wa Mataifa lililopo ndani ya Karume Hall kwenye Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
DSC_0162
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama (wa tatu kushoto) akizungumza na mzazi aliyeambatana na watoto wake kwenye banda la Umoja wa Mataifa lililopo ndani ya Karume Hall kwa ajili ya kufahamu kazi mbalimbali zinazofanywa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini. Kushoto ni Amos Mtamba kijana mwenye fani ya uchoraji anayefadhiliwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) kupitia Mpango wa Kukuza Ajira kwa Vijana " Kazi Njenje" na anayefuatia ni Programme Coordination Specialist wa UNAIDS, Jimmy Mbazi.
DSC_0174
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akifafanua jambo kwa mzazi aliyeambatana na watoto kwenye banda la Umoja wa Mataifa kufahamu kazi mbalimbali zinazofanywa na Umoja wa Mataifa hapa nchini kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
DSC_0195
Amos Mtamba kijana mwenye fani ya uchoraji anayefadhiliwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) kupitia Mpango wa Kukuza Ajira kwa Vijana "Kazi Njenje" akieleza kwa mmoja wa wadau namna anavyofanya kazi zake za uchoraji ambapo UN imempa nafasi ya kuonyesha kuonyesha kazi zake za sanaa ya uchoraji kwenye banda hilo kwa ajili yakujitafutia soko na kuendeleza maisha yake.

MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AKUTANA NA MABALOZI WA OMAN NA SYRIA

$
0
0
Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi wa Syria nchini Tanzania, Abdulmonem Annan, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 3, 2014 kwa mazungumzo.
Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Syria nchini Tanzania, Abdulmonem Annan, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 3, 2014 kwa mazungumzo. 
Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi wa Oman nchini Tanzania, Saoud Ali Mohammed Al-Ruqaish, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 3, 2014 kwa mazungumzo.
Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Oman nchini Tanzania, Saoud Ali Mohammed Al-Ruqaish, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 3, 2014 kwa mazungumzo.Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal leo Alhamisi Julai 03, 2014 amekutana na Waheshimiwa Mabalozi wa nchi za Oman na Syria wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania. Mheshimiwa Makamu wa Rais amekutana na Mabalozi hao ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam.

Awali alikuwa ni Balozi wa Oman, Mheshimiwa Saoud Ali Mohammed Al-Ruqaish aliyefika kukutana na Mheshimiwa Makamu na kufafanua kuwa uhusiano baina ya Tanzania na Oman unazidi kuimarika na kwamba wawekezaji kutoka Oman wamekuwa wakija kwa wingi kuwekeza Tanzania tofauti na siku za nyuma huku pia Tanzania ikionesha kufungua milango yake kwa uwekezaji mkubwa wa kati nchini Tanzania.

Kwa upande wa Balozi wa Syria Mheshimiwa Abdulmonem Annan yeye alimueleza Mheshimiwa Makamu wa Rais kuwa Syria iko katika kipindi kigumu na kwamba nchi hiyo kwa sasa inatafuta kila linalowezekana kurejesha amani. Balozi huyo alifafanua kuwa nchi yake inahitaji msaada wa nchi za Kimataifa ili kusaidia kuweka pande zote zinazokinzana mezani kwa lengo la kufikia maazimio yatakayoifanya nchi hiyo isiparanganyike.

Mheshimiwa Makamu wa Rais alimueleza Balozi za Syria kuwa, Tanzania inatamani sana kuona hali ya utulivu inarejea Syria na kwamba nchi hiyo inaendelea kujenga uchumi uliobomoka tayari. Pia alisema kuwa msimamo wa Tanzania unabakia katika kutaka pande zinazohusika katika mgogoro huo zinafuikia suluhu kwa amani ili wananchi wengi wasipoteze maisha.

Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Ikulu Dar es Salaam

WARSHA YA MUZIKI WA SAMBA REGGE NA SARAKASI KUHITIMISHWA KESHO KWENYE UWANJA WA KASULU, MBURAHATI KWA JONGO

$
0
0
 
 Mkufunzi wa Ngoma za Samba regge, Manni Spaniol akimwelekeza mmoja wa watoto wanaoshiriki warsha ya fit for life iliyoandaliwa na kituo cha Baba watoto cha Mburahati kwa Jongo, Jijini Dar es Salaam.
 Mkufunzi wa ndani, Mwajabu Omari akimwelekeza namna ya kufanya sarakasi mmoja wa watoto wanaoshirika kwenye warsha ya sarakasi na ngomba za samba regge iliyoandaiwa na kituo cha Baba Watoto
 Mafunzo ya Sarakasi

 Wanafunzi na wakufunzi wakifanya mazoezi ya kujiandaa na onyesho la muziki wa samba regge litakalofanyika kesho kwenye viwanja vya Kasulu, Mburahati kwa Jongo.

 

Watoto zaidi ya 80 kutoka kituo cha Baba Watoto kesho wanatarajiwa kupanda katika jukwaa moja kuonyesha ngoma za kibrazili na sarakasi ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha mafunzo ya wiki tatu ya michezo hiyo kupitia mradi wa fit for life yaliyokuwa yakifanyika Mburahati jijini Dar es Salaam.

Warsha hiyo ambayo imewashirikisha watoto walio kwenye mazingira magumu kati ya umri wa miaka 10 hadi 25 imefadhiliwa na umoja wa ulaya (EU) na kusimamiwa na kituo cha Utamaduni cha Ujerumani Goethe-Institut kwa ubia na Ufa-Fabrik ya Ujerumani na Parapanda Theatre.

Meneja mradi wa Fit for life, Habiba Issa amesema kuwa onyesho hilo linafanyika kesho Ijumaa kuanzia saa tisa mchana kwenye kiwanja cha Kasulu Mburahati kwa Jongo, ambapo watoto hao wataonyesha ustadi wa miruko ya sarakasi, trapezi na muziki wa samba regge kutoka nchini Brazil.

Alisema kuwa onyesho hilo litakuwa ndio hitimisha la warsha ya wiki tatu ambayo ililega kuwajengea uwezo watoto na vijana wa kufanya shughuli za sanaa ambazo ni pamoja na ushonaji wa maleba, muziki, ufundi seremala, ujengaji wa majukwaa makubwa na taa na utaalamu wa sauti ya jukwaani.

“Tunategemea vijana hawa watatumia ujuzi huu katika maisha yao ya kila siku maana mwaka jana waijifunza mengi na sasa tumewaongezea uwezo zaidi ili kuwawezesha kujitegemea na kuinua uchumi wao na kuwapa mbinu nyingi za kukabiliana na maisha” alisema Issa.

Akizungumzia maandalizi ya onyesho hilo Msimamizi wa wakufunzi wa ndani katika mafunzo hayo, Mkude Kilosa alisema kuwa vijana wako tayari kwa onyesho hilo na kwamba sasa wako katika hatua za mwisho za maandalizi hayo.

“Mafunzo yanaendelea vizuri na sasa tunajiandaa na onyesho letu la ijumaa ambapo wale waliojiunga nasi mapema wako katika hali nzuri na sasa tunashughulika na hawa wapya ili waweze pia kufanya onyesho siku hiyo” alisema Kilosa

Alisema kuwa mbali na kuwafundisha watoto hao namna ya kucheza sarakasi na muziki wa samba regge pia wanawaandaa kuwa walimu wa sanaa hizo ili waweze kuwafundisha wengine na kukuza vipaji vya watu wengi zaidi nchini
Alisema onyesho hilo linatarajiwa kuwa la kuvutia kutokana ujuzi waliopata watoto hao kutoka kwa wakufunzi wao kutoka Ujerumani, Ufaransa na Kambodia.

BENKI YA CRDB TAWI LA BABATI LAANZA KUTOA HUDUMA ZA KIBENKI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Elaston Mbwilo akiwa na wadau mbalimbali wa mkoa huo, wakiwa kwenye Tawi la Babati la Benki ya CRDB ambalo jana lilianza kutoa huduma ya fedha kwa wateja wake, kulia kwake ni Meneja wa CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa na kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa huo Omary Chambo na kushoto kwa RC Mbwilo ni DC wa Babati Khalid Juma Mandia na Katibu wa CCM wa Mkoa huo Ndeng'aso Ndekubali.  (PICHA
NA WOINDE SHIZZA,MANYARA.
Baadhi ya wadau walioshiriki ufunguzi wa huduma za fedha kwenye Benki
ya CRDB Tawi la Babati Mkoani Manyara, ambalo jana lilianza kutoa
huduma za fedha kwa wateja ikiemo kuweka akiba, kutoa fedha na
kuchukua mikopo, ambapo linatarajiwa kufanyiwa uzinduzi wake hivi
karibuni.
 Meneja wa Benki CRDB Tawi la Babati Mkoani Manyara, Ronald Paul
akizungumza na waandishi wa habari ambapo kwa mara ya kwanza Tawi hilo lilianza kutoa huduma ya fedha kwa wateja wake jana na linatarajia
kuzinduliwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda au Rais Jakaya Kikwete.
Baadhi ya Maofisa wa Jeshi la JWTZ wakipata maelezo mbalimbali kuhusiana na huduma za kibenki ndani ya Benki ya CRDB Tawi la Babati Mkoani Manyara, lilipoanza kutoa huduma ya fedha kwa wateja mbalimbali mkoani humo ikiwemo kuweka akiba, kutoa fedha na kutoa mikopo.

 ===========  ========  =======

Na Woinde Shizza,Manyara.

Wananchi wa Mkoa wa Manyara, wametakiwa kutumia fursa ya kuwepo kwa huduma ya benki ya CRDB Tawi la Babati, kwa kujiwekea akiba na kuchukua mikopo kwa lengo la kujinufaisha kiuchumi na kuongeza pato la Taifa.

Mkuu wa mkoa wa Manyara, Elaston Mbwilo aliyasema hayo wakati wa zoezi la benki ya CRDB tawi la Babati, lilipoanza kutoa huduma ya fedha kwa wateja wake na yeye kuwa mtu wa kwanza kuweka fedha kwenye tawi hilo.

Mbwilo aliwataka wananchi wa mkoa huo kufungua akaunti za fedha kwenye benki tofauti ikiwemo CRDB, NMB, NBC, Posta na Exim, ambazo zipo mjini Babati, kuliko kuweka kwenye benki moja na kuitegemea yenyewe pekee.

"Waswahili wanasema usiweke mayai yote kwenye kapu moja, hivyo tutumie fursa hii kwa kuweka akiba katika benki tofauti tofauti, hapa unaweka sh200, kule sh300, pengine sh100 ndiyo nidhamu ya fedha ilivyo," alisema Mbwilo. Hata hivyo, alisema Waziri Mkuu Mizengo Pinda au Rais Jakaya Kikwete mmoja wao ndiye atakayekuja kulizindua rasmi Tawi hilo na alitoa wito kwa benki hiyo ya CRDB kuanzisha matawi mengine kwenye wilaya za mkoa wa Manyara.

"Siku za nyuma tulikuwa tunaona gari la benki linakuwa hapa kwa wiki mara moja ila sasa mmeweza kuweka Tawi hapa Babati, sambaeni na sehemu nyingine huko wilayani msogeze huduma hizi karibu na jamii," alisema Mbwilo. Naye, Meneja wa CRDB Tawi la Babati Ronald
Paul aliwataka wafanyabiashara, watumishi, wakulima na wafugaji wa
mkoa huo kutumia fursa ya kuwepo kwa benki hiyo kwa ajili ya kupata huduma za kifedha ikiwemo kuweka akiba.

"Jamii itumie nafasi hii kwa kuweka na kutoa fedha na pia hapa Babati ni kwenye barabara kuu hata viongozi wengi wanapita kuelekea Dodoma, hivyo watatumia fursa hii ya kuwepo kwa tawi letu kupata huduma ya fedha," alisema Paul.

UFUNGUZI WA WARSHAYA MAFUNZO YA MAFUNDI MAJOKOFU NA VIYOYOZI JIJINI ARUSHA LEO

$
0
0
Pichani kulia ni Mkurugenzi msaidizi Idara ya Mazingira kutoka ofisi ya makamu wa Rais Bi Magdalena Mtenga, akifafanua jambo katika ufunguzi wa warsha ya mafunzo ya mafundi majokofu na viyoyozi kuhusu teknolojia mbadala za upozaji na rafiki kwa tabaka la ozoni mjini Arusha leo.
 Sehemu ya washiriki katika warsha ya Mafunzo ya mafundi majokofu na viyoyozi mjini Arusha kuhusu Teknolojia Mbadala za upozaaji  na rafiki kwa tabaka la ozoni.
 Aliyesimama, Mkurugenzi wa idara ya Mazingira Ofisi ya makamu wa Rais dkt. Julius Ningu akizungumza  machache kwa wanawarsha na wataalam katika warsha ya mafunzo kuhusu teknolojia mbadala za upoozaji na rafiki kwatabaka la ozoni mjini Arusha leo.. Aliyekaa ni Mkuu wa Chuo cha VETA Moshi. Bw.Daniel Komba(Picha zote na Evelyn Mkokoi)

WANAHABARI WAPATIWA ELIMU YA MFUMO UTAKAOTUMIKA KUBORESHA DAFTARI LA KUDUMU LA KUPIGA KURA.

$
0
0
 Mjumbe wa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu John Mkwawa  wakati akisoma taarifa wakati   akifungua mkutano wa siku moja na waandishi wa habari wa Mkoa wa Iringa unaohusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya kwanza na matumizi ya Teknolojia mpya ya Biometric Voter Registration uliofanyika katika ukumbi wa ofisi za mkuu wa mkoa wa Iringa. 
 Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wa NEC kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya kwanza na matumizi ya Teknolojia mpya ya Biometric Voter Registration uliofanyika katika ukumbi wa ofisi za mkuu wa mkoa wa Iringa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mkoa wa Iringa. 
Mkurugenzi wa Idara ya habari na Elimu kwa Wapiga Kura Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Ruth Mashama akizungumza kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya kwanza na matumizi ya Teknolojia mpya ya Biometric Voter Registration uliofanyika katika ukumbi wa ofisi za mkuu wa mkoa wa Iringa


Na Denis Mlowe,Iringa

TUME ya Taifa ya Uchaguzi imetoa elimu kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Iringa kuhusu kusambaza elimu juu ya  mchakato wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa wananchi juu ya mfumo mpya utakaotumika kuandikisha wapiga kura wa mkoani hapa wa teknelojia ya kibailojia(BVR).

Tume inatarajia kufanya uboreshaji wa daftari la Kudumu wa Wapiga kura kwa awamu ya kwanza hivi karibuni kwa kutumia Teknolojia mpya ya Biometric Vote Regstration (BVR).

Hayo yamebainishwa juzi  mjini hapa na Mjumbe wa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu John Mkwawa  wakati  akifungua mkutano wa siku moja na waandishi wa habari wa Mkoa wa Iringa unaohusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya kwanza na matumizi ya Teknolojia mpya ya Biometric Voter Registration uliofanyika katika ukumbi wa ofisi za mkuu wa mkoa wa Iringa.

Jaji Mkwawa alisema lengo ni kuhakikisha kuwa wale wote wenye sifa za kuwa wapiga kura  waliofika umri wa miaka 18 na hawapo katika daftari la kudumu la kupiga kura,waliohama makazi yao ya awali walikojiandikisha na  wanajitokeza kwa wingi katika vituo vya kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.

Alisema mfumo huo mpya ni wa kuchukua au kupima taarifa za mtu za kibaiolojia au tabia ya mwanadamu na kuhifadhi katika kanzi data kwa ajili ya utambuzi na kutumia kitambulisho kipya cha kupiga kura.

“Mfumo huu hutumika katika kumtambua mtu na kumtofautisha na mwingine, ingawa tabia hizo za binadamu ziko nyingi, lakini kwa ajili ya kuandikisha wapiga kura watachukuliwa alama za vidole vyote kumi  vya mikono, picha na saini ndizo zitachukuliwa na kuhifadhiwa kwenye Kanzi Data (Database) ya wapiga kura” Alisema Jaji Mkwawa

Jaji Mkwawa alisema kupiga kura kwa Watanzania walio wengi sio lazima hivyo  hawaoni thamani ya kupiga kura, hivyo Vyombo vya Habari vinawajibu mkubwa wa kuelimisha umma juu ya  umuhimu wa kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura na ni tofauti na nchi ya Shelisheli ambayo kujiandikisha na kupiga kura ni lazima.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya habari na Elimu kwa Wapiga Kura Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Ruth Mashama akiwasilisha mada inayohusu maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura  kwa kutumia teknolojia ya Biometric Vote Registration (BVR) ameeleza kuwa Tume inatarajia kuboresha Daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya kwanza hivi karibuni na maandalizi yake tayari yamekamilika kwa sehemu kubwa na baadhi ya vifaa vimeanza kuwasili nchini Tanzania.

Alisema matumizi ya mfumo mpya utatumika katika zoezi la uandikishaji  pekee tofauti na nchi nyingine zilizotumia mfumo hadi katika kupiga kura na kugundua mafanikio yaliambatana na changamaoto mbalimbali za kiteknolojia na kimfumo.

Mashama alizitaja baadhi ya nchi za Kiafrika zilizokwisha tumia mfumo wa BVR kuwa ni Nigeria 2007,Ghana 2009,Liberia2005,Guinea 2005,Mali 2005, Uganda 2008,Kenya 2013,Zambia 2008, Afrika Kusini na Zanzibar 2009.

Rais Kikwete aonana na Mwana Mfalme wa Japan Prince Akishino na Mkewe Princess Kiko leo Ikulu, Dar

$
0
0
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki Mwana Mfalme wa Japan Prince Akishino alieambatana na Mkewe Princess Kiko walipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo July 3, 2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Mkurugenzi wa Idara ya Asia Bw. Mbelwa Kairuki kwa Mwana Mfalme wa Japan Prince Akishino na Mkewe Princess Kiko waliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo July 3, 2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazunzumzo na Mwana Mfalme wa Japan Prince Akishino na Mkewe Princess Kiko Ikulu jijini Dar es salaam leo July 3, 2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwatembeza Ikulu Mwana Mfalme wa Japan Prince Akishino na Mkewe Princess Kiko jijini Dar es salaam leo July 3, 2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mwana Mfalme wa Japan Prince Akishino na Mkewe Princess Kiko walipomtembelea jijini Dar es salaam leo July 3, 2014. Wengine ni WaZiri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe, Naibu WaZiri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Mahadhi, balozi wa Tanzania nchini japan Mhe Salome Sijaona na balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe Masaki Okada.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwaonesha Simba waliotengenezwa Mwana Mfalme wa Japan Prince Akishino na Mkewe Princess Kiko walipomtembelea jijini Dar es salaam leo July 3, 2014.

WAZIRI WA ARDHI PROFESA ANNA TIBAIJUKA ASIFU KAZI INAYOFANYWA NA SHIRIKA LA NYUMBA (NHC)

$
0
0
1Waziri wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi Mh. Prof. Anna Tibaijuka akipokewa na Felic Maagi Mkurugenzi wa Fedha wa NHC wakati alipowasili kwenye Banda la Shirika hilo kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa TANTRADE yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu J.K.Nyerere barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam leo. 2Waziri wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi Mh. Prof. Anna Tibaijuka akizungumza na baadhi ya viongozi wa shirika la nyumba nchini NHC baada ya kuwasili kwenye banda hilo tayari kwa kukagua shughuli zinazofaywa na shirika hilo, Kutoka kulia ni Muungano Saguya Meneja za Jamii NHC, Davidi Shambwe Mkurugenzi wa Biashara na Maendeleo wa NHC  na Felix Maagi Mkurugenzi wa Fedha NHC.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)3Waziri wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi Mh. Prof. Anna Tibaijjuka akipata maelezo kutoka kwa maofisa wa shirika hilo wakati alipotembele banda la NHC Kushoto ni Felix Maagi Mkurugenzi wa Fedha na kutoka kulia ni Elias Msese Meneja Miliki Uendeshaji Makao Mkuu na Edith Ngunwe Afisa Mawasiliano NHC.4Mmoja wa watu waliotembelea banda la NHC akipata maelezo kutoka kwa maofisa wa shirika hilo kutoka kulia ni Nalindwa Norbert, Rhobi Wambura na Wilson Sanane.5Davidi Shambwe Meneja Maoko wa NHC akitoa maelezo wa Waziri wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi Mh. Prof. Anna Tibaijuka wakati alipotembelea banda la shirika hilo kushoto ni Felix Maagi Mkurugenzi wa Fedha na Kutoka kulia ni Rhobi Wambura na Wilson Sanane maofisa wa NHC.6Waziri wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi Mh. Prof. Anna Tibaijuka akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika bana hilo.7 
Waziri wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi Mh. Prof. Anna Tibaijuka akzungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea banda hilo kushoto ni Bw. Felix Maagi Mkurugenzi wa Fedha NHC.
.......................................................................................
1.Nalipongeza Shirika la Nyumba la Taifa kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuwapatia wananchi makazi bora. Sisi upande wa Serikali tutaendelea kuwasaidia kisera ili waweze kutimiza wajibu wao vizuri zaidi. 

 2. Pamoja na ujenzi wa nyumba wanaoufanya katika maeneo mbalimbali nchini na kwa watu wa vipato vya chini na watu wa vipato vya kati na juu, Serikali inaupongeza mpango wa Shirika waliouanza kwa kasi wa kujenga nyumba za gharama nafuu nchini, mpango unaoendeshwa kwa kaulimbiu ya “nyumba yangu, maisha yangu” 

3. Nyumba hizo sasa zimekamilika katika maeneo 14 ya Halmashauri za miji ikiwemo Mkinga(Tanga), Mvomero(Morogoro), Mnyakongo-Kongwa(Dodoma), Mkuzo (Songea), Mtanda(Lindi), Mrara(Babati), Unyankumi(Singida), Kibada na Mwongozo (Kigamboni), Bombambili(Geita), Ilembo na Inyonga(Katavi), Uyui(Tabora), Longido na Monduli(Arusha) na Mlole(Kigoma). Miradi mingine ya aina hii imeanza kutekelezwa katika Halmashauri mbalimbali za Miji na Wilaya hapa nchini, lengo likiwa ni kufikia Mikoa yote na ikibidi kila Halmashauri nchini. 

4. Ili kuufanya mpango huu mzuri wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu kuwa endelevu, mambo kadhaa ni lazima yafanyike:-Kwanza ni kwa Halmashauri kote nchini kuunga mkono kwa kulipatia Shirika maeneo ya kujenga nyumba hizo yasiyokuwa na masharti magumu. Ardhi isifanywe kitegauchumi na Halmashauri kwa kuiuza kwa gharama kubwa kwani kufanya hivyo kutafanya nyumba zinazojengwa kuwa aghali.Pili, Halmashauri na wananchi kwa ujumla wajitokeze kwa wingi kununua nyumba zinazojengwa na NHC ili mapato yatakayopatikana yawezeshe kujenga nyumba zingine kwa ajili ya wananchi. 

5 Zipo pia nyumba zinazojengwa katika miji mikubwa “satellite cities” zenye lengo la kuwapatia wananchi makazi na kuondoa msongamano wa magari mijini. Miji hiyo ni pamoja na Burka, Usar River na Mateves Arusha, Luguruni, Kunduchi Rifle Range, Uvumba na Kawe - Dar es salaam. Aidha, katika mikoa kadhaa hivi sasa majengo makubwa ya biashara yanajengwa ili kuipa sura mpya miji yetu na kukuza shughuli za kibiashara. 

6. Serikali inaitambua sekta ya nyumba kuwa ni sekta mtambuka kwa kuwa hukuza uchumi, huongeza ajira na kusaidia kudumisha amani ya nchi yetu. Hivyo, nalihimiza Shirika hili liendelee na mipango yake kabambe ya kujenga nyumba za gharama nafuu ili kuwawezesha wananchi wengi kumiliki nyumba. Wananchi wengi wakimiliki nyumba utakuwa mkakati mmojawapo wa kupunguza umaskini nchini maana wananchi hao wataweza kutumia nyumba zao kupata mikopo benki ya kuendeleza shughuli zao za kiuchumi. 

7. Nawasihi watanzania watembelee banda hili la NHC ili wapate taarifa za kina za namna ya kununua nyumba na mahali nyumba hizo zilipo.

MKOA WA DODOMA WASHEREHEKEA KUANZA KWA UJENZI WA MRADI WA BARABARA YA DODOMA (MAYAMAYA) - BABATI (BONGA)

$
0
0
  Mkuu wa  Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akimkabidhi Dereva Abuu Ally Funguo ya kuwashia mitambo ya kujengea barabara kuashiria kuanza rasmi kwa Ujenzi wa Barabara ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kwa kiwango cha lami wakati wa kuadhimisha sherehe za kuanza kwa ujenzi wa mradi huo zilizofanyika mapema Julai Mosi, 2014 kijijini Kolo Wilayani Kondoa, Kulia anayeshuhudia ni Mbunge wa Kondoa Kaskazini Mhe. Zabein Mhita.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (Katikati mwenye kilemba) na ujumbe alioambatana nao wakipatiwa maelezo ya mradi wa barabara kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kutoka kwa wakandarasi wa Kampuni inayojenga barabara hiyo ya China Railway Seventh Group wakati alipotembelea kambi ya kampuni hiyo  iliyopo kijiji cha Kolo Wilayani Kondoa mapema Julai Mosi, 2014
 Wakandarasi wa Kampuni ya China Railway Seventh Group inayojenga barabara ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kipande cha Bonga-Mela (88.8KM) kwa kiwango cha lami wakisikiliza salamu ya Mkuu wa Mkoa Dodoma (Hayupo pichani) wakati wa kuadhimisha sherehe za kuanza kwa ujenzi wa mradi huo zilizofanyika Julai Mosi, 2014 kwenye Kijiji cha Kolo Wilayani Kondoa.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, wadau, Mafundi na Wataalamu wa Kampuni ya China Railway Seventh Group inayojenga barabara ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kwa kiwango cha lami kipande cha Bonga-Mela (88.8KM) wakiwa kwenye picha ya pamoja muda mfupi baada ya kumalizika kwa sherehe za kuanza kwa ujenzi wa mradi huo wa barabara zilizofanyika Kijijini Kolo Wilayani Kondoa Mapema Julai Mosi, 2014.

 
Sehemu ya Wananchi wa Kijiji cha Kolo Wilayani Kondoa waliojitokeza kwa wingi kuadhimisha sherehe za kuanza kwa ujenzi wa mradi wa barabara ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kwa kiwango cha lami wakisikiliza salamu za Mkuu wa Mkoa Dodoma (Hayupo pichani), Sherehe hizo zilifanyika mapema Julai Mosi, 2014. Picha na John Banda wa Pamoja Blog.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchmbi (wa nne kutoka kushoto) akiwaongoza wadau waliofika kuadhimisha sherehe za kuanza kwa ujenzi wa mradi wa barabara ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kwa kiwango cha lami kuomba Dua ili mradi huo ukamilike kwa wakati bila kukwamishwa na changamoto mbalimbali. Sherehe hizo zilifanyika mapema Julai Mosi, 2014 kijijini Kolo Wilayani Kondoa.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (wa pili kushoto) na ujumbe alioambatana nao wakikagua magari yanayotumika kwenye ujenzi wa barabara ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kwa kiwango cha lami Mapema jana wakati wa maadhimisho ya kusherehekea kuanza kwa ujenzi wa mradi huo yaliyofanyika Kijiji cha Kolo Wilayani Kondoa, wengine pichani ni wakandarasi wa Kampuni ya China Railway Seventh Group inayojenga barabara hiyo kipande cha Bonga-Mela (88.8KM).
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images