Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

Wanafunzi Dar Waadhimisha Valentine Day kwa Mtazamo wa Kijinsia

$
0
0
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Sinza Tower wakifanya maigizo kuonesha madhara ya wanafunzi kujihusisha na mapenzi wawapo shuleni.
Msimulizi wa Hadithi za fasihi, Rupal Ganatra (kulia) akitoa simulizi kwa wanafunzi walioshiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Wapendao kwa Mrengo wa Kijinsia katika bustani ya SOMA.

Meneja wa Idara ya Habari na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi (katikati) akifuatilia maigizo ya wanafunzi katika hafla hiyo.


 Na Thehabari.com

WANAFUNZI mbalimbali kutoka katika baadhi ya shule za Sekondari jijini Dar es Salaam leo wameadhimisha Siku Kuu ya Wapendanao (Valentine Day) kwa mtanzamo wa Kijinsia ikiwa ni
kushinikiza jamii kuadhimisha sherehe hiyo kwa mtazamo tofauti na mazoea kwa siku hiyo.

Wakizungumza katika maadhimisho hayo wengi waliitaka jamii kubadili mtazamo wa maadhimisho ya Valentine na kuijali jamii zaidi isiojiweza kwa kuisaidia kuonesha upendo na kuacha kuegemea katika mapenzi ambayo yamekuwa yakiipotosha jamii.

Mwanafunzi Grace David kutoka Shule ya Sekondari Loyola alisema mapenzi ya kweli hayawezi kuoneshwa kwa mtu kwa siku moja pekee, bali hali hiyo inapaswa kuwepo siku zote tofauti na mtazamo ya vijana wengi wanavyoichukulia 'Valentine Day'.

Naye Meneja wa Idara ya Habari na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi akizungumza na wanafunzi alisema siku ya Valentine hivi sasa imegeuzwa kibiashara zaidi na jamii kiasi cha kuyaathiri makundi mengine ya jamii kwa namna mbalimbali.

Alisema takwimu zinaonesha kuwa kadi za ujumbe wa mapenzi zinauzwa kwa kiasi kikubwa siku hiyo ukilinganisha na sikuu kuu zingine, huku biashara nyingine za starehe zikifanywa kiasi kikubwa.

Alisema jamii ina kila sababu ya kuanza kubadilika na kuadhimisha siku hiyo kwa kujitolea kwa makundi yasiojiweza kama watoto yatima, wazee na wajane ambao wanaishi katika mazingira magumu.

Hata hivyo alisema ukatili wa kijinsia na mapenzi umekuwa ukiibuka kwa kasi katika siku kuu hiyo; kama wapenzi (katika ndoa) kuwasaliti wapendwa wao, ukatili wa kimapenzi, vipingo na starehe zisizo na tija jambo ambalo linafanya makundi yasio na uwezo kutengwa.

Aidha aliongeza kuwa wanafunzi nao wamekuwa wakijikuta wakitoka katika maadili yao na kujiingiza katika mapenzi na ngono zembe jambo ambalo limekuwa likiwaathiri kwa kiasi kikubwa.

"Valentine ni maadhimisho ya kumbukumbu ya mwanaharakati aliyekuwa mtetezi wa haki za makundi ya vijana katika jamii ya Ki-nubi ambao walinyimwa haki zao katika masuala ya mahusiano, sasa tunaisherekea kimapenzi zaidi...," alisema Bi. Liundi.

Makundi hayo ya wanafunzi kutoka shule za Sekondari Yusuf Makamba, Loyola (Loyola High School), Mabibo, Perfect Vision na Sinza Tower yamekutanishwa na TGNP kwa kushirikiana na Taasisi ya Soma Book Cafe ya jijini Dar es Salaam.

*Imeandaliwa na www.thehabari.com


Meneja wa Habari TGNP, Lilian Liundi (aliyeshika kipaza sauti) akiimba na wanafunzi (hawapo pichani) pamoja na wageni waalikwa walioshiriki Siku ya Wapendanao kwa Mrengo wa Kijinsia Dar es Salaam.


Meneja wa Habari TGNP, Lilian Liundi (kulia) akizungumza na wanafunzi anuai waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Valentine kwa Mrengo wa Kijinsia.


Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Yusuf Makamba wakiwasilisha igizo lao katika hafla hiyo. Pichani aliyepiga magoti ni msichana aliyejiingiza kwenye mapenzi shuleni na kujikuta akipata ujauzito ambao ulikataliwa na aliyempa ujauzito huo (kijana anayeonekana kumuomba)-hili ni igizo tu.


Meneja wa Habari TGNP, Lilian Liundi akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho hayo.


Vikundi vya wanafunzi wakiwa katika majadiliano na tafakari baada ya kuwasilishwa kwa mada mbalimbali katika hafla hiyo.


Vikundi vya wanafunzi wakiwa katika majadiliano na tafakari baada ya kuwasilishwa kwa mada mbalimbali katika hafla hiyo.


Vikundi vya wanafunzi wakiwa katika majadiliano na tafakari baada ya kuwasilishwa kwa mada mbalimbali katika hafla hiyo.


Kutoka kushoto ni Lilian K, Lilian Liundi na Deo Temba wote kutoka Idara ya Habari ya Mtandao wa Jinsia Tanzaniua (TGNP) wakijadiliana jambo kwenye maadhimisho ya Siku ya Wapendanao kwa Mrengo wa Kijinsia.


Wanafunzi wakiwa katika majadiliano kwenye vikundi. Wa pili kutoka kulia ni Meneja wa Habari TGNP, Lilian Liundi akiwasikiliza.




Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Ambassador Khamis Kagasheki Meets with tourism stakeholders in Arusha

$
0
0
Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Ambassador Khamis Kagasheki (with mic) addressing tourism stakeholders in Arusha.
Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Ambassador Khamis Kagasheki (with mic) addressing tourism stakeholders in Arusha.
TANAPA representatives at the stakeholders meeting.
Tourism Stakeholders in the country listening attentively to the Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Ambassador Khamis Kagasheki.

Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Ambassador Khamis Kagasheki (left) greets the former government minister Basil Mramba during the meeting.
Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Ambassador Khamis Kagasheki (left) greets the former government minister Basil Mramba during the meeting.Director of Tanzania Tourist Board Dr. Aloyce Nzuki (right) paying attention to some of the tourism stakeholders during the meeting.
Director of Tanzania Tourist Board Dr. Aloyce Nzuki (right) paying attention to some of the tourism stakeholders during the meeting
Former Minister Basil Mramba talking to TANAPA officials Dr. Ezekiel Dembe, Acting Director of Touris_ (second left)_ Johnson Manase, Tourism Manager and Alphonce Akarrow, CIA(1)
Former Minister Basil Mramba talking to TANAPA officials Dr. Ezekiel Dembe, Acting Director of Touris; (second left); Johnson Manase, Tourism Manager and Alphonce Akarrow, CIA
Minister for Natural Resources Hon. Ambassador Khamis Kagasheki in a jovial mood with the CEO of Leopard Tours Mr. Fazal
Minister for Natural Resources Hon. Ambassador Khamis Kagasheki in a jovial mood with the CEO of Leopard Tours Mr. Fazal.
NCAA Public Relations Manager Adam Akyoo (right) talking to Paul Srakikya (middle) who is the Assistant Director of Ant poaching in the Ministry.
NCAA Public Relations Manager Adam Akyoo (right) talking to Paul Srakikya (middle) who is the Assistant Director of Ant poaching in the MinistryTTB Managing Director Dr. Aloyce Nzuki and Kibo Palace Hotel Marketing Manager Charity Githinji were also there to attend Tourism Stakeholders meeting.
TTB Managing Director Dr. Aloyce Nzuki and Kibo Palace Hotel Marketing Manager Charity Githinji were also there to attend Tourism Stakeholders meeting.

TAARIFA KUHUSU UZINDUZI WA KITABU KUHUSU USAGAJI NA UKIMWI..

$
0
0

RafikiElimu  Foundation  ni    Taasisi  isiyokuwa  ya  kiserikali  (  NGO )  inayo  jihusisha  na  Maendeleo  ya  Jamii  nchini  Tanzania.  Taasisi  kupitia  mradi  wake  “ Wanawake  na  Ukimwi “  inapenda  kuwaalika  watu  wote  kwenye  uzinduzi  wa  kitabu .

“  MAAMBUKIZI  YA  V.V.U  MIONGONI  MWA  WANAWAKE  WANAO  JAMIIANA  NA  WANAWAKE  WENZAO  NCHINI  TANZANIA  “.

KUHUSU  MRADI :  Mradi  wa  “  WANAWAKE  SALAMA  PROJECT “    (   SAFE   WOMEN  PROJECT )  ni  mradi  unao  ratibiwa  na  Taasisi  ya  RafikiElimu  Foundation  kwa  kushirikiana  na  mashirika  rafiki.

LENGO  LA  MRADI  :  
i.                       Kutoa  elimu  ya  mapambano   ya  ukimwi  kwa   wanawake  wanao  toka  katika  jamii    zinazo  shikilia  mila  na  desturi  hatarishi  kwa    maambukizi  ya  v.v.u  kama  vile; mila  ya  ukeketaji  watoto  wa  kike,  mila  ya  kurithi  wajane, mila  ya  kutakasa  wajane,  mila  ya  nyumba  nthobhu, mila  ya  kuoza  watoto  wadogo  na  mila  ya   kuoa  wanawake  wengi.
  
ii.                     Kutoa  elimu  ya  mapambano  ya  ukimwi  kwa  wanawake    walio  katika  hali  zinazo  waweka  katika  hatari  ya  kupatwa  na  maambukizi  ya  v.v.u. Mfano  wanawake  walemavu  kama  vile  walemavu  wa  akili, walemavu  wa  ngozi  ( albino ), walemavu  wa  macho, walemavu  wa  kuona,  walemavu  wa  kusikia, walemavu  wa  viungo  na  wenye  ulemavu  zaidi  ya  mmoja  mfano   kuona  na  kusikia.


iii.                  Kutoa  elimu  ya  mapambano  ya  ukimwi  kwa  wanawake  wanao  jishughulisha  na  tabia  za  kingono  ambazo  ni  hatarishi  kwa  maambukizi  ya  v.v.u  kama  vile  wanawake  wanao  jamiiana  kinyume  na  maumbile, wanawake  wanao  fanya  bishara  ya  kuuza  miili   yao  pamoja  na  wanawake  wanao  jamiiana  na  wanawake  wenzao. 


KUHUSU  KITABU  :   Kitabu  “  MAAMBUKIZI  YA  V.V.U  MIONGONI  MWA  WANAWAKE  WANAO  JAMIIANA  NA  WANAWAKE  WENZAO  NCHINI  TANZANIA  “  kinaelezea  kwa  kina  chanzo  na  sababu  zinazo  wafanya  wanawake  kuingia  katika  mahusiano  ya  jinsi  moja,   athari  wanazo zipata   kama  vile kupatwa  na  maambukizi  ya  magonjwa  mbalimbali  ya  zinaa  na  ukimwi,  pamoja  na  kupendekeza   suluhisho  sahihi  la  tatizo  hili. 

·         Ndani  ya  kitabu  hiki, kuna  shuhuda  mbalimbali  kutoka  kwa  wanawake  mbalimbali  wa  kitanzania  waliopata  maambukizi  ya  v.v.u  kwa  kujamiiana  na  wanawake  wenzao  nchini.

                                   KUHUSU   UZINDUZI  WA  KITABU  HIKI

Katika  uzinduzi  wa  kitabu  hiki, kutakuwa  na  matukio  mbalimbali  kama  ifuatavyo:

1.        PRESENTATIONS  :  Watafiti  Fina  Maziku, Mariam  Simba,  Nabwike  Mwakatika,  Naetwe  Kilango  na    Neema  Tido  kutoka  taasisi  ya  RafikiElimu   Foundation  wata presents  sura  mbalimbali  zilizomo  ndani  ya  kitabu  hiki.

2.       SHUHUDA  :  Kutakuwa  na  shuhuda  mbalimbali  kutoka  kwa  wanawake  mbalimbali  wa  kitanzania  walio  pata  maambukizi  ya  v.v.u  kwa  kujamiiana  na  wanawake  wenzao.

3.       MENGINEYO:  Kutakuwa  na  shughuli  nyinginezo  nyingi  kama  vile   maswali  na  majibu, mahojiano  nakadhalika.

LINI  :  Uzinduzi  wa  kitabu  hiki, utafanyika  siku  ya  Jumamosi  ya  tarehe  23   FEBRUARI  2013  katika  ukumbi  wa  hoteli  ya  NEW  HOLLIDAY  INN  HOTEL  uliopo  katikati  ya  jiji  la  Dar Es  salaam.

MUDA  :  Kuanzia  saa  8 kamili  mchana  hadi  saa  kumi  na  moja  kamili  jioni.

KUSHIRIKI  KATIKA  UZINDUZI  HUU :  Tiketi  za  kushiriki  katika  uzinduzi  huu  zinapatikana  kwa  gharama  ya  shilingi  Elfu  25  tu.  Piga  :  0652567932   au   0756606085  au    0782405936.

Kwa  maelezo  zaidi, tembelea  :  WWW.RAFIKIELIMU.BLOGSPOT.COM  

Rais Kikwete na Maaskofu wa KKKT jijini Arusha

$
0
0
Rais Dkt. Jakaya Mrisho kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu wa Kanisa la kiinjilki la Kilutheri Tanzania (KKKT) muda mfupi baada ya kumalizika kwa ibada ya Mazishi ya Marehemu Askofu Dkt.Thomas Laizer iliyofanyika katika usharika wa mjini Kati jana jioni.(picha na Freddy Maro).

Maneno mazito kabisa haya.. si ya kupuuzwa hata kidogo.

$
0
0

Pichani ni baadhi ya maneno yaliyozungumzwa na baadhi ya vingozi wa siasa hapa nchini wakatii wa kutoa heshima za mwisho na kuaga mwili wa Askofu Thomas Laizer jijini Arusha mwishoni mwa wiki,ambapo walizungumza maneno mazito kwa mustakabali wa mwenendo wa nchi yetu na yanayozidi kujiri hivi sasa kwa baadhi ya sehemu ya nchi.Pata Muda bofya na uyasikilize na kuyatafakari kwa umakini.
Mh Reginald Mengi

 

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASIMAMIA ZOEZI LA UTEKETEZAJI SILAHA HARAMU JIJINI DAR

$
0
0

Sehemu ya Silaha hizo zikianza kuteketea kwa moto baada ya Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kufyatua waya maalumu wa kuwasha moto huo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akivuta waya kuashiria kufyatua mtego wa kuwasha moto wa kuteketeza Silaha haramu, wakati alipokuwa mgeni rasmi katika zoezi hilo la uteketezaji wa silaha haramu, Lililofanyika katika Kambi ya Magereza jijini Dar es Salaam, Jumamosi Feb 16, 2013. Kushoto kwake ni Kamishna msaidizi wa Jeshi la Polisi Tanzania, Simon Siro na wa pili kulia kwake ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Perera Ame Silima na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kmataifa, Benard Membe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi, baada ya kusimamia zaoezi la uteketezaji wa Silaha haramu, lililofanyika Ukonga jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Simon Siro, wakati wakipita kukagua sihala hizo haramu kabla ya kuanza kwa zoezi la uteketezaji wa silaha hizo haramu lililofanyika Ukonga jijini Dar es Salaam.
Silaha haramu zilizoteketezwa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa zoezi la uteketezaji wa Silaha Haramu, lililofanyika Ukonga Jijini Dar es Salaam.
Wimbo wa Taifa, kabla ya kuanza kwa zoezi hilo. 

RAIS KIKWETE AZIFARIJI FAMILIA ZA WALIOKUFA KATIKA AJALI YA GARI UBENA ZOMOZI

$
0
0


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa mkono wa pole na kuwafariji ndugu, jamaa na marafiki wa familia zilizoondokewa na watoto na wazazi wao kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea maeneo ya kijiji cha Kibiki, Ubena Zomozi katika mkoa wa Pwani Februari 11, 2013 iliyoua hapohapo watu wanane wakiwemo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chalinze baada ya gari dogo aina ya Toyota Mark II lililokuwa limebeba abiria wanane kugongana uso kwa uso na roli.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia moja ya picha za ajali hiyo alizopewa na wanafamilia walioondokewa na watoto na wazazi wao kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea maeneo ya kijiji cha Kibiki, Ubena Zomozi katika mkoa wa Pwani Februari 11, 2013 iliyoua hapohapo watu wanane wakiwemo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chalinze baada ya gari dogo aina ya Toyota Mark II lililokuwa limebeba abiria wanane kugongana uso kwa uso na roli.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifariji ndugu, jamaa na marafiki wa familia zilizoondokewa na watoto na wazazi wao kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea maeneo ya kijiji cha Kibiki, Ubena Zomozi katika mkoa wa Pwani Februari 11, 2013 iliyoua hapohapo watu wanane wakiwemo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chalinze baada ya gari dogo aina ya Toyota Mark II lililokuwa limebeba abiria wanane kugongana uso kwa uso na roli.
Haya ndio magari yaliyopata ajali hiyo na kupelekea vifo vya watu wanane wakiwemo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chalinze.PICHA NA IKULU.

========  ====== ====== ======
Rais Jakaya Mrisho Kikwete Jumamosi hii ya Februari 16, 2015 amekwenda kuhani na kufariji ndugu, jamaa na marafiki wa familia zilizoondokewa na watoto na wazazi kufuatia ajali ya barabarani maeneo ya kijiji cha Kibiki, Ubena Zomozi katika mkoa wa Pwani iliyotokea Februari 11, 2013 na kupoteza hapohapo maisha ya watu nane wakiwemo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chalinze baada ya gari dogo aina ya Toyota Mark II lililokuwa limebeba abiria wanane kugongana uso kwa uso na roli la mizigo.

Familia alizokwenda kuhani na kuzifariji ni pamoja na za marehemu Hassan Erasto Kurunge (57), Maria Sadiki ((52) na mtoto wa mwaka mmoja Samweli Ismail wa kata ya Ubena.

Wengie ni marehemu Essau Enos Mwamgingo (16) , Stella Isaack Kazimoto (18), Bahati George Mbena (17) na Latifa Maneno (17).

Akiwa ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe Mwantumu Mahiza na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Ahmed Kipozi, Rais Kikwete alieleza kusikitishwa kwake kwa ajali hiyo, na kuwataka madereva wawe makini katika kuzingatia sheria za usalama barabarani.

Rais Kikwete alisikitishwa zaidi kwa taarifa kwamba gari hilo dogo lilikuwa limebeba abiria wanane, na kuwa dereva wake ambaye pia alipoteza maisha, hakuwa makini katika kuzingatia sheria za usalama barabarani.

PADRE APIGWA RISASI NA KUFA MAPEMA LEO ASUBUHI HUKO ZANZIBAR

$
0
0
TAARIFA ILIYOIFIKIA GLOBU YA JAMII HIVI PUNDE TOKA VISIWANI ZANZIBAR,INAELEZA KUWA PADRE  EVERIST MUSHI (PICHANI) WA KANISA KATOLIKI HUKO ZANZIBAR,AMEPIGWA RISASI YA KICHWA NA WATU WASIOJULIKANA NA KUFARIKI PAPO HAPO ASUBUHI YA LEO MNAMOA MAJIRA YA SAA MOJA UNUSU,WAKATI AKIELEKEA KWENYE IBADA KATIKA KANISA LA MTONI,ZANZIBAR.


SABABU ZA KUPIGWA RISASI KWA PADRE HUYO BADO HAZIJAFAHAMIKA MPAKA SASA. 


MASHUHUDA WA TUKIO HILO WANASEMA KUWA WATU HAO WALIOFANYA TUKIO HILO WALIKUWA NI WAWILI NA WALIKUWA WAMEPAKIZANA KWENYE PIKIPIKI AINA YA VESPA WAKATI PADRE HUYO ALIKUWA KWENYE GARI LAKE AMBALO BAADA YA KUTOKEA KWA TUKIO HILO NALO LILIACHA NJIA NA KWENDA KUGONGA NYUMBA MOJA ILIYOKUWA JIRANI NA KANISA HILO.. 


 GLOBU YA JAMII INAENDELEA KUFUATILIA TUKIO HILO NA TAARIFA KAMILI ITAWAJIA BAADAE 

MUNGU AILAZE ROHO YA MAEREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN.

Mbezi veterans yaingia mitini dhidi ya Kijitonyama Veterans

$
0
0

Mratibu wa timu ya Kijitonyama Veterans, Majuto Omary akimtoka mchezaji wa timu ya Kombaini ya Tabora, Ibrahim Masoud “Maestro” katika moja ya mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Kijitonyama. Timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 huku mabao yakifungwa na wachezaji hao wawili kwa upande wa timu zao.(picha; Mpigapicha wetu)
=======   ========  ======== =======
UONGOZI wa timu ya Kijitonyama Veterans umepitisha azimio la kutocheza mechi  yoyote ya kirafiki dhidi ya timu ya Mbezi Veterans  ya barabara ya Morogoro kutokana na kile ilichokiita ‘tabia si ya kiwanamichezo’.

Kauli hiyo ilitolewa na mratibu mkuu wa timu hiyo, Majuto Omary kufuatia kitendo cha timu hiyo kushindwa kutokea uwanjani katika mchezo wao maalum wa kirafiki uliopangwa kufanyika jana asubuhi kwenye uwanja wa  Kijitonyama.

Majuto alisema kuwa mechi hiyo iliombwa na timu hiyo ya Mbezi  na wao (Kijitonyama) kuwakubalia kutokana na ukweli kuwa michezo ni afya mbali ya kudumisha urafiki. Alisema kuwa  mechi hiyo ilipangwa kuanza saa 2.00 asubuhi, na timu hiyo ilithibitisha nusu saa kabla ya mechi hiyo kuwa wanakuja na wapo katika maandalizi.

Alifafanua kuwa baada ya hapo, viongozi wa timu hiyo hawakuonekana uwanjani na mbaya zaidi hawakupokea simu zao  walizokuwa wanapiga ili kujua wamefikia  wapi. “Kinanchosikitisha ni kwamba, walituweka hapo uwanjani na mbali ya kuwatumia ujumbe wa simu ya mkononi kuwa wamefika wapi au wamekwama, hawakujibu chochote, hii inaonekana kuwa ni makusudi,” alisema Majuto.

Majuto ambaye pia ni kiongozi wa timu ya waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa FC), alisema kuwa hiyo si mara ya kwanza kwa timu hiyo kushindwa kutokea uwanjani bila ya kutoa taarifa.

“Waliwahi kuomba kucheza na Taswa FC pale Leaders Club, tukawakubalia, lakini hawakutokea uwanjani na hata simu zetu wakawa hawapokei wala kujibu ujumbe kusema kuwa wameshindwa kuja, walituacha uwanjani na kupoteza muda, hii ni tabia yao,” alisema.

Alisema kuwa haya maamuzi ni ya kudumu na watajaribu kuzitahadharisha na timu nyingine kuhusiana na vitendo vya timu hiyo  kwani  ni vya kupotezea muda wanamichezo.

KUMBUKUMBU-SALAMU KWA BABA YETU KIPENZI.

$
0
0

Kazi ya Mungu haina makosa, lakini kwetu ni majonzi makubwa.

Kama binadamu tungekuwa na uwezo wa kukata rufaa ya kifo, hakika nasi tungekata rufaa mbele ya Mungu ili turudishiwe  baba yetu kipenzi, Geoffrey Nkurlu, na kuendelea kuishi pamoja nae hapa duniani.

Hakika,tunajikuta tukiandika barua hii kwa uchungu mkubwa, maana familia yako inaadhimisha miaka 12 ya kukukosa kwako, tangu  hapo tarehe kama ya leo 17/2/2001 ulipotutoka na kuwa mbali na sisi.

Baba mpendwa, watoto wako wote bado tumeshikamana  kwa pamoja kama jinsi wewe ulivyotulea na kutusisitiza  tuwe wamoja. Tuko pamoja katika dhiki na faraja,hakika tunaendelea kukuwaza, kukukumbuka, kukuenzi na kuishi katika maadili bora  ambayo ulitufunza.Kwa kweli tunakulilia miaka yote, maana mchango wako ni mkubwa katika kuilea familia yako, ambayo leo hii imeweza kusimama imara kutokana na malezi mema na  mapenzi yako.

Baba mpendwa, sisi watoto  wako, wakati mwingine kila tunapokufikiria, hakika mioyo yetu inashindwa kuamini kama ni kweli haupo pamoja nasi. Tangu kuzaliwa kwetu, umeweza kutulea, kutusumbukia na kutusomesha kwa kidogo chako ulichokuwa unakipata. Kitendo kama hicho ni cha kipekee. Nani kama wewe? Maisha yetu bila wewe, yangekuwaje katika kipindi cha maisha yetu, tangu kuzaliwa kwetu, kukua na kufikia katika kila kipindi kigumu ambacho daima ni picha kamili ya maisha yetu.

Ingawa tupo mbali na wewe, lakini  umetutoka kimwili tu, kiroho tuko na wewe. Bado tunakumbuka kauli zako, ushauri wako katika familia yako uliyoiacha katika wasiwasi mkubwa. Tumelia sana. Tumeumia sana.Na tuonapo baba wa wenzetu wakifurahia na kupata hata mawaidha, nasi huwa tunaukumbuka uwepo wako. Picha na mtiririko wa maisha yako ni ushahidi kuwa wewe ulikuwa baba bora kwetu, huku tukiamini Mungu muweza na muumba wa yote ataitumia fursa hiyo kama sehemu ya kukulaza mahali pema kwa unyenyekevu wako.

Suala zima la kifo, linaashiria kuwa ni sehemu ya mpito katika maisha ya duniani. Vitabu vyote vya dini vimekitaja kifo kuwa hakuna kiumbe ambaye anaweza kuvuka bila kupitia katika hatua hiyo, hivyo tunatumia nafasi hii kukuombea mwanga wa milele ukuangazie.

Baba mpendwa, wakati tunaendelea kuyakumbuka mazuri yako katika familia hii uliyoiacha hali ya kuwa bado inakuhitaji, macho yetu yanashindwa kuhimili mtiririko wa machozi katika mboni zetu, yakiwa ni mapenzi makubwa baina yako na yetu. Kazi ya Mungu haina makosa, lakini kwa upande wako ni ngumu mno kukubali matokeo na kujua kweli hatutakuwa wote katika kipindi cha maisha ya duniani. Umetangulia baba. Jina la bwana libarikiwe,sisi tunaendelea kukulilia miaka yote.



Tusingeweza na hatukuwa na sababu ya kuzuia hitaji la Mungu. Ingawa sisi tulikupenda na kukuhitaji sana, lakini Mungu alikupenda zaidi na aliona muda wako wa kuishi duniani umekoma na hakika ulistahili kwenda kwake kwa mapenzi yake, kwa vile kifo ni njia yetu sote na  kila nafsi itaonja mauti. Dunia tunapita.

Sisi watoto wako,Masala,Matina,Nzigia,Amani,Angaza na Atuza.
Tunakulilia na kukuombea daima.

Chadema yalaani Mauji yanayoendelea kutokea hapa nchini

$
0
0
 Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Freeman Mbowe akiwa anaongea na viongozi wa chama kutoka katika mikoa ya kanda ya kaskazini ambayo ni arusha ,kilimanjaro ,manyara pamoja na tanga kuhusiana na sera ya majimbo leo jijini Arusha
 Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema Freeman Mbowe akiwasili katika ukumbi wa bugaloo kwa ajili ya kuongea na viongozi wa vyama mbambali kwa jili ya kupanga mkakati wa chama chao
 mwenyekiti wa  muda wa  chama cha demokrasia na maendeleo Chadema kanda ya kaskazini ambaye pia ni mbunge wa karatu akiwakaribisha viongozi mbalimbali wa kanda ya kaskazini katika kikao cha viongozi wa chama hicho kanda  kikao ambacho kinajadili seraya majimbo
 picha juu na chini wajumbe ambao ni viongozi walioudhuria mkutano huo
KATIKA hali isiyokuwa ya Kawaida mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA),Freeman Mbowe amesema kuwa mauji ya Viongozi wa dini ambayo yametokea,katika mkoa wa Geita, na Zanzibar ni matokeo ya CCM,na hivyo kama wataandelea kuendesha nchi kwa msingi hiyo bado nchi itakabiliwa na mauji makubwa sana

Mboye aliyasema hayo mapema leo wakati akizindua kanda ya kaskazini
kwa chama hicho ambayo itaweza kuhudumia mikoa ya kanda ya kaskazini
katika shuguli za kichama na za kijamii

Alisema kuwa hapo awali Chadema kilishasema kuwa CCM isipuuzie
matatizo ya ubaguaji wa dini lakini chama hicho hakikusikia na badala
yake kiliendelea kujiendesha kwa misingi ya kubaguana kidini hali
ambayo sasa inanyima watu uhuru wa kuabudu na kufanya mambo yao

Alisistiza kuwa kama CCM  bado iliendelea kufanya ubaguzo wa dini kwa
misingi kuwa inakomoa Chadema lakini hawakujua na kutambua kuwa hali
hiyo inafanya mauaji ya kila siku ambayo sasa yameanza Geita lakini
Leo yameelekea Zanzibar mara baada ya Padre kuuliwa wakati akielekea
Kanisani kusalisha misa


“Leo kila mahali unasikia mauji ya dini lakini mimi nilishawaambia CCM
kuwa hiii sio hali ya kuendelea kuangalia lakini walujua  kuwa ni
siasa na wao  walifanya hivi kwa malengo ya kuwa wanatukomoa sisi
Chadema kwa kugawa Taifa katika Imani ya kidini sasa wamelikoriga
wanatakiwa kulinywa’aliongeza Mbowe

Katika hatua Nyingine Mbowe alisema kuwa wao kama Chadema wanalaani
Mauji ambayo yanatokea kila siku ndani ya Tanzania na kwa hali hiyo
hawataweza kuwagawa wananchi  katika misingi ya kidini kwa kuwa wote
wapo sawa na kama Nchi itaendeshwa hivyo ni wazi kuwa damu ambazo
hazina hatia zitamwagika kila mara.

“Chadema tunaalani kwa kweli haya mauji na kwetu Muislamu, Mkristo
wote ni wa moja na kamwe kiongozi ambaye ataonesha ubaguzi dhidi ya
wakristo na waislamu ni wazi kuwa tutamkimbia hatuwezi kuingiza
jitiada za CCM ndani ya chama chetu,na kuweka utaratibu wa kumwaga
damu ambazo hazina hatia kabisa’aliongeza Mbowe

Akiongelea suala la kanda ya kaskazini ndani ya chama hicho alisema
kuwa hiyo ni moja ya mikakati ambayo imewekwa na mbali na hilo pia
kupitia viongozi wa kanda ya kaskazini wataweza kujiwekea nafasi nzuri
sana ya kuchukua Nchi ya Tanzania kwa kipindi cha mwaka 2015 hivyo
kufanya Nchi iwe huru zaidi kuliko  ilivyo kwa sasa

Mbowe aliongeza kuwa kanda ya kaskazini pia itaweza kuwa chachu ya
Maendeleo kwa kuwa itaweza kutatua kero mbalimbali za wananchi ambazo
zinawakabili kwa kuwa sasa kazi za maendeleo zitafanywa chini ya mikoa
minnne tofauti na hapo awali ambapo kila mkoa ulikuwa unajitegemea kwa
shuguli za kichama na za kichama.Habari picha na Woinde Shiza-Arusha.

Diamond alivyokinukisha kwenye kiota cha safari jijini arusha mwishoni mwa wiki

$
0
0
 Msanii wa kizazi kipya ajulikanaye kwa jina la Nasib Abudul(diamond Platinum)akiwapa burudani wa kazi wa jiji la Arusha katika shoo yake iliodhaminiwa na kituo cha radio 5 ndani ya  klabu ya safari iliopo ndani ya ukumbi wa jengo la sundown cornival lililopo nje kidogo ya jiji la Arusha
warembo wakichat wakati burudani ikiendelea.

 picha juu na  chini ni warembo wa  kituo cha radio 5 ambao ndio wathamini wa kuu wa show hiyo ya diamond plaatinum

 wadada nao wanajua kutunza, huyu mdada yeye alipenda wimbo wa kizai zai wa diamond akaamua kwenda kumtunza kabisa


 Msanii diamond akiwapagawisha mashabiki wa Arusha waliouthuria katika show
Mashabiki wa diamond wakitamani kupigwa ata Kiss na msanii huyo 
 Ma dance wanaotikisa Tanzania kutoka Arusha Contegeous waliokuwepo katika show hiyo wakiburudisha
 Baadhi ya wadada waliokuja kutazama show wakimfurahia msanii daimond
 Wakwanza kutoka kulia ni mkurugenzi wa mwandago investiment akifuatiwa na meneja masoko wa K-vant Gin Godluck kwayu,meneja wa sigara kanda ya kaskazini jina halijaweza fahamika mara moja akifuatiwa na meneja wa TBL nao waliudhuria katika show ya diamond platinum


Diamond Akicheza na mshabiki wake baada ya kushuka stage
 Hili ni jiko la kisasa la kuchoma nyama lililopo ndani ya hotel ya sundown conival

taarifa rasmi kutoka zanzibar kuhusiana na mauaji ya padre Evaristitus Mushi.

$
0
0

Padri Evaristitus Mushi wa kANISA LA katoliki,Parokia ya ST.Joseph,Shangani,Unguja ameuwawa leo mnamo saa moja asubuhi katika eneo la Beit-EL-Ras karibu na kanisa la Katoliki.
 
Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na Waziri wa nchi  Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Mohamed Aboud imeeleza kuwa kutokana na tukio hilo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeliagiza Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina ili kuwatambua wale wote waliohusika na tukio hilo kwa ajili ya kuwachukulia hatua zinazofaa kwa mujibu wa sheria.
 
Aboud amesema kuwa wakati uchunguzi huo unaendelea, Serikali inawaomba wananachi wote kuwa watulivu na kuliachia Jeshi hilo la Polisi kutekeleza wajibu wake .
 
Aidha Serikali imetoa mkono wa pole kwa familia na wanafamilia wa marehemu pamoja na waumini wa kanisa hilo kuwa wastahamilivu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.
 
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
178/2/2013

MAMA SALMA KIKWETE AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOANI LINDI

$
0
0
Mjumbe wa NEC, Mama Salma Kikwete akikagua bidhaa za wajasiriamali, alipotembelea eneo la Raha Leo, Lindi mjini leo Februari 17, 2013. akiwa katika ziara ya kukagua na kuimarisha uhai wa chama mkoani Lindi.
Mjumbe wa NEC, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimsalimia mkazi wa Raha Leo Lindi mjini, Bella Linje, aliyekuwa kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika katika eneo hilo, leo, Februari 17, 2013.
Mjumbe wa NEC, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika Kata ya Raha Leo,Lindi mjini.
Wanachama wapya wa CCM wakila kiapo baada ya kukabishiwa kadi zao na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mama Salma Kikwete, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo FEB 17, 2013 katika Kata ya Raha Leo Lindi mjini.
Baadhi ya wakazi wa kata ya Raha Leo mjini Lindi wakiuliza maswali mbali mbali kwa Mjumbe wa NEC, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kwenye mkutano huo.

WATATU WASHIkiLIKIWA NA POLISI KUFUATIA MAUAJI YA PADRI EVARIST MUSHI-ZANZIBAR


RAIS KIKWETE ALIPOKWENDA ZIFARIJI FAMILIA ZA WALIOKUFA KATIKA AJALI YA GARI UBENA ZOMOZI

Ziara ya Epiq BSS yawakuna wakazi wa Dodoma, wakazi wa Dar kaeni mkao wa kula

$
0
0

Mmoja wa Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya walioshiriki shindano la kuimba la Epiq Bongo Star Search pichani shoto,Walter akionesha umahiri wake wa kuimba akiwa sambamba na msanii mwingine wa bongofleva ajulikanae kwa jina la Ben Paul,kwenye onesho lao la pamoja lililofanyika mwishoni mwa wiki  katika ukumbi wa Club Maisha  mkoani Dodoma.
 Mmoja wa Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya walioshiriki shindano la kuimba la Epiq Bongo Star Search pichani shoto,Wababa akipongezwa na mmoja wa mashabiki waliofika kushuhudia onesho lao la pamoja lililofanyika mwishoni mwa wiki  kwenye ukumbi wa Club Maisha  mkoani Dodoma. 
 Mmoja wa Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya walioshiriki shindano la kuimba la Epiq Bongo Star Search pichani,Husna akiwapagawaisha mashabiki (hawapo pichani),kwenye onesho lao la pamoja lililofanyika mwishoni mwa wiki  kwenye ukumbi wa Club Maisha  mkoani Dodoma. 
 Mmoja wa wasanii mahiri wa bongofleva,Barnaba akiwaimbisha mashabiki wake( hawapo pichani) waliofika kushuhudia wakali wa Epiq Bongo Star Search walipofanya onesho lao  la pamoja lililofanyika mwishoni mwa wiki  kwenye ukumbi wa Club Maisha  mkoani Dodoma. 
Pichani ni baadhi ya mashabiki wakifurahia burudani nzuri iliyokuwa ikitolewa na wasanii walioshriki shindano la Epiq Bongo Star Search,lililofanyika mwishoni mwa wiki  kwenye ukumbi wa Club Maisha  mkoani Dodoma. 
========  ======= =====  ====
WASANII wa Muziki wa Kizazi Kipya walioshiriki shindano la kuimba la Epiq Bongo Star Search, Norman, Husna, Menina, Wababa, Geofrey na Walter jana walionyesha wao ni moto wa kuotea mbali baada ya kuwapagawisha mashabiki zaidi ya elfu tatu waliohudhuria katika ukumbi wa Club Maisha Dodoma. Show hiyo kali ilianza majira ya saa tano usiku, kwa mkali kutoka THT Ali Nipishe anayetamba na kibao chake cha ‘MY’, na baadaye kumtambulisha Norman Severino ambaye kwa mara ya kwanza alizindua wimbo wake wa ‘Si Wewe’.

Steji ilizidi kuwaka moto pale kijana tokea Dodoma, Godfrey Levis alipopanda kuimba wimbo wake wa ‘MAYA’ na kufuatiwa na malkia kutoka THT, Linah, aliyeimba nyimbo zake zote kali. Lakini alikuwa ni mwanadada, Nsami aliyeonyesha kwamba wanawake waliopo kwenye tasnia wajipange alipopanda kuimba wimbo wa ‘MUONGO’ na hatimaye mdada wa taarab, Husna akawamaliza wanadodoma kwa kuimba wimbo wake wa ‘Nawamimina’, huku akisifiwa na wengi kwa uwezo wake mkubwa wa kulimiliki jukwaa.

Kama hiyo haitoshi, mashabiki pia waliburudishwa vya kutosha na mwimbaji bora wa kiume wa mwaka, Barnaba, ambaye aliiimba nyimbo zake kama Magubegube na Sorry, ambao unafanya vizuri sana sasa hivi na kuwafanya mashabiki kupiga kelele kwa kumshangilia. Ukumbi ulizidi kulipuka kwa mayowe baada ya Barnaba kumtambulisha mwanadada mwingine, Menina, ambaye wimbo wake wa Dream tonight unafanya vizuri kwenye vyomba vya habari hapa nchini. Menina, ambaye alimsaidia Barnaba kuitikia wimbo wake wa Wrong Number, alionyesha uwezo mkubwa katika kumiliki jukwaa.

Hadi wakati mshindi wa tatu wa shindano la EBSS, Wababa Mtuka anapanda jukwaani kuimba kibao chake cha ‘My Wife’ watu wa Dodoma walikuwa bado wakishangilia namna alivoonyesha uwezo katika kuimba. Wa mwisho kabla ya mshindi wa milioni hamsini kupanda alikuwa ni Ben Paul, ambaye aliwakonga nyoyo mashabiki wake kwa nyimbo zake kali kama Pete na Samboira kabla ya kumkaribisha jukwaani Walter.

Mashabiki hao waliokuwa wakimsubiri kwa hamu, walianza kupiga kelele Walter Walter, kabla ya kuwatuliza kwa kuimba wimbo wake mpya wa ‘Siachi’ akifuatiwa wimbo wake mwingine wa ‘Mamy Love’ ambao aliutoa kama zawadi kwa mashabiki zake wa Dodoma. Walter alipata wakati mgumu jukwaani ambapo mashabiki walimuomba azirudie nyimbo zake zaidi ya mara tatu hali iliyoonyesha kukubalika kwa hali ya juu.

Mashabiki wengi wakizungumza baada ya burudani hiyo walionyesha kuwakubali vilivyo wasanii wa EBSS, huku wakiwatabiria makubwa. ‘Hakika vijana wana vipaji na wanajua hasa kutoa burudani, wakipewa sapoti watafika mbali sana’ alisema Maliki Abdul mkazi wa Dodoma aliyehudhuria burudani hiyo. Ziara hiyo ya washindi wa Epiq BSS inaelekea Dar mwisho wa mwezi huu kabla ya kuelekea Mtwara.

gazeti lako la dira liko sokoni kwa sh 500/= tu

fastjet yatoa mafunzo kwa Mtanzania wa Kwanza Mmaasai kuongoza ndege aina ya Airbus

$
0
0

William Zelothe Stepehen ni Mtanzania wa Kwanza Mmaasai aliyepewa ithibati ya kuiongoza ndege aina ya Airbus A319 punde tu baada ya kupokea mafunzo ya urubani yaliyodhaminiwa na shirika la ndege la fastjet. Alipata mafunzo hayo nchini Uingereza kwa muda wa takriban miezi miwili na amerudi nchini Tanzania hivi karibuni. William alikulia Olosipe jijini Arusha ambapo ni nyumbani kwa wazazi wake.

William anafananisha anavyojihisi anapoiongoza ndege ya Airbus A319, na wakati akiwa katika nyumba nzuri ya kifahari na ya kisasa; anaielezea ndege ya Airbus A319 kama ndege iliyo imara na ambayo imewekewa mifumo mingi ya usalama. Kwa maneno yake mwenyewe, anasema “Ndege ya Airbus inakulinda kweli kweli, kama unaifahamu vyema”

William amewahi kusomea usimamizi wa wanyama pori; alipata mafunzo ya urubani kwa mara ya kwanza kule Florida Aviation Academy nchini Marekani mwaka 2006 ambapo alipata leseni yake ya usafirishaji kwa ndege. Ingawa ana umri mdogo, ana uzoefu wa masaa 3,053 ya kuongoza ndege.

Kumwajiri rubani huyu mtanzania mwenye miaka 28, ni mojawapo ya jitihada za fastjet za kuhakikisha kuwa kampuni hiyo inaajiri watendaji wazawa waliobobea katika fani hiyo hapa nchini. Mikakati yao ya kuajiri pia ni mojawapo ya wajibu wao mpana wa kuwekeza nchini Tanzania. Kwa kila rubani aliyepokea mafunzo, fastjet imetumia gharama inayokadiriwa shilingi 49,546,400 hela za kitanzania ambayo ni sawa na 31,027 dola za kimarekani.

fastjet ni shirika jipya la ndege la nauli nafuu Afrika ambalo lilipata umiliki wa FLY540 na kwa mantiki hiyo likazindua kampuni ya kwanza ya usafiri wa ndege ambalo linazingatia bajeti. Fastjet, ambayo inaungwa mkono na mwanzilishi wa Lonrho na easyGroup Bwana Stelios Haji Ioannou, imetambulisha nauli za kiwango cha chini hadi kiasi cha Tsh32,000 bila kujumlisha kodi ili kuwawezesha mamilioni  ya watu ambao walikuwa wameshindwa kusafiri kwa ndege, kuweza kusafiria ndege kwa mara ya kwanza na kuendelea kutumia ndege mara kwa mara. Tangu kuzinduliwa kwake mwezi Novemba 2012, shirika hili la fastjet limewasafirisha zaidi ya watu 70,000 na asilimia 99.7 ya safari za ndege zikisafiri katika muda uliopangwa.

Mama salma kikwete kuwa mgeni rasmi hafla ya Montage Charity Ball serena hotel jijini dar.

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage,Teddy Mapunda (katikati) akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitandaza kufanyika kwa tafrija maalum ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo ya afya hapa nchini kupitia mfuko wa Montage Charity Ball,itakayofanyika Februari 22 kwenye Hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam

Aidha Teddy ameeleza kuwa malengo hasa ni kukusanya kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Wanawake wenye matatizo mbali mbali.Mgeni rasmi katika Tafrija hiyo anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA),Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.Kulia ni Meneja Masoko na Mauzo wa Serena Hoteli,Seraphin Lusala na kushoto ni Mwenyekiti Kamati ya Maandlizi ya Tafrija hiyo,Barbara Hassan.
Meneja Masoko na Mauzo wa Serena Hoteli,Seraphin Lusala akifafanua jambo kwa wanahabari juu ya tafrija hiyo.
Mwenyekiti Kamati ya Maandalizi ya Tafrija hiyo,Barbara Hassan akizungumzia maandalizi yalivyofikia.Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Montage,Zainab Mkindi.
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live


Latest Images