Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YAANZA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KWA MFUMO MPYA WA (BVR

$
0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi hapa nchini Jaji Mstaafu Damian Lubuva (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jana, kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Liana Hassan na kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Joseph Mchina.


Na Hillary Shoo, SINGIDA.

TUME ya Taifa ya Uchaguzi imeanza mchakato wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura,kwa kuwashirikisha kwa karibu waandishi wa habari hapa nchini.


Lengo la kuwashirikisha waandishi wa habari ni kutokana na uwezo na hekima katika kupeleka taarifa na kuhamasisha jamii na wananchi kwa ujumla kupitia vyombo vya habari.


Hayo yamebainisha jana mjini hapa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva wakati  akifungua mkutano na waandishi wa habari wa Mkoa wa Singida.


Jaji Lubuva alisema lengo ni kuhakikisha kuwa wale wote wenye sifa za kuwa wapiga kura wanajitokeza kwa wingi katika vituo vya kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.


Aidha alisema kuwa Tume inatarajia kufanaya uboreshaji wa Daftari la Kudumu wa Wapiga kura kwa awamu ya kwanza hivi karibuni kwa kutumia Teknolojia mpya ya Biometric Vote Regstration ( BVR).


Alisema mfumo huo mpya ni wa kuchukua au kupima taarifa za mtu za kibaiolojia au tabia ya mwanadamu na kuhifadhi katika kanzi data kwa ajili ya utambuzi.


“Mfumo huu hutumika katika kumtambua mtu na kumtofautisha na mwingine, ingawa tabia hizo za binadamu ziko nyingi, lakini kwa ajili ya kuandikisha wapiga kura alama za vidole kumi vya mikono, picha na saini ndizo zitachukuliwa na kuhifadhiwa kwenye Kanzi Data (Database) ya wapiga kura.” Alisisitiza Jaji Lubuva.



Hata hivyo alisema kwa kutumia mfumo huu wa (BVR), wananchi wote wenye sifa za kuwa wapiga kura na wale walio na kadi za mpiga kura watatakiwa kuandikishwa upya.


Jaji Lubuva alisema mafunzo kwa Watendaji yanatarajiwa kufanyika muda kuanzia Mwezi Julai mwaka hauu kabla ya zoezi la uboreshaji wa Daftari kufanyiaka.


Mwenyekiti huyo alibainisha kwamba uhakiki wa vituo vya kuandikisha wapiga kura umeshafanyika na kwa sasa uandikishaji utafanyika katika vituo vilivyo katika ngazi ya vitongoji, Vijiji na Mitaa. Kutokana na utaratibu huu wa sasa vituo vya kujiandikisha vimeongezeka kutoka 24,919 hadi kufikia vituo 40,015 ambavyo vimewekwa katika ngazi za Vitongoji, Vijiji na Mitaa’. Alisema na kuongeza


 “Ili kuwezesha kuwa karibu zaidi na wanancahi na hivyo kupunguza malalamiko ya auambali wa vituo vya kujiandikisha na kuaongeza mwamko wa kujiandikishwa na kupiga kura.” Alifafanua Jaji Lubuva.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Joseph Mchina, alisema maandalizi yote muhimu kwa ajili ya zoezi hilo katika Manispaa yake yamekamilika na hivyo kuwa na vituo 154 badala ya 84 vya awali.



BABA MBASHA: FLORA ALICHOKA KUISHI NA MWANANGU

NHIF ilivyonyakua kombe la ushindi Wiki ya Utumishi wa Umma

$
0
0
 Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akisaini kitabu cha wageni katika banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya katika Maonesho ya wiki ya Utumishi wa Umma aliyoyafunga jana.

 Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alitumia fursa hiyo pia kupima afya yake katika banda la upimaji afya la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF, Raphael Mwamoto akipokea cheti cha ushindi wa banda bora katika maonesho hayo.

  Ofisa Masoko na Elimu kwa Umma, Grace Michael akionesha kombe lililokabidhiwa kwa NHIF na Balozi Ombeni Sefue baada ya kuwa washindi.

 Maofisa wa NHIF wakifurahia ushindi

 Furaha iliendelea ndani ya banda

 Meneja wa NHIF, Mkoa wa Temeke, Ellentruda Mbogoro kushoto, Grace Michael (Katikati) na Meneja Masoko na Elimu kwa Umma, Anjela Mziray wakifurahia ushindi.

 Wananchi wakiendelea kupata huduma katika banda la NHIF.

REDD'S MISS CHANG'OMBE ZAWADI ZA WASHINDI ZATANGAZWA

$
0
0
 Mratibu wa Shindano la kumtafuta mrembo wa Redd's Miss Chang'ombe, Tom Chilala (katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo wakati wa kuitangaza zawadi za washindi. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Marie Stopes, Dk. Jophn Bosco na Ofisa Uhusiano  wa TV1, Mponjoli Katule. 
 Warembo wa shindano la Redd's Miss Chang'ombe wakiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa shindano hilo, wasanii watakaotoa burudani siku ya fainali. 
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Marie Stopes, Dk. Jophn Bosco akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Marie Stopes, Dk. Jophn Bosco akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo.
 Ofisa Uhusiano  wa TV1, Mponjoli Katule (wa tatu kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu udhamini wa TV1 katika shindano la Redd's Miss Chang'ombe.
Rapa wa bendi ya Ruvu Stars, Msafiri Diouf 'Sokoine' akighani wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
Warembo wakiwa wamepozi kwa picha.

Na Mwandidhi Wetu




MNYANGE atakayevishwa taji la Redds Miss Temeke  2014 linalotarajia kufanyika Juni 27 mwaka huu katika  ukumbi wa TTC Chang'ombe anatarajia kujinyakuria  kitita cha sh. laki tano. 

Mshindi wa pili atajinyakulia laki tatu, mshindi wa tatu  laki mbili na washiriki wengine watapata kifuta jasho cha sh. 65,000.

 Mratibu wa shindano hilo Tom Chilala, alisema katika  shindano hilo anatarajia kumtoa mrembo atakafanikiwa  kutwaa taji la misi Tanzania mwaka huu hapo baadaye.



"Mwaka huu nina warembo wazuri na wenye vigezo vyote, naamini mwaka huu nitarudisha heshima yangu ya  kufanikiwa kutoa warembo kutoka Redd's Miss Temeke hadi Redd's Miss Tanzania," alisema.


 Alisema mwaka 2010 alifanikiwa kumtoa Genevieve Emmanuel, kutoka miss Temeke hadi miss Tanzania,  hivyo na kwa mwaka huu anaamini itakuwa hivyo kutokana na warembo alionao. 

Aidha shindano hilo litakarokuwa na washereheshaji kutoka bendi ya Ruvu Stars, Mchekeshaji Kitale pamoja na msanii anayetamba na kibao cha Basi Nenda Moshi Katena na wengine. Kiingilio katika shindano hilo kitakuwa ni sh. 20,000 kwa VIP na Elfu 10000 kawaida. 

Naye Mkurugenzi wa Marie Stoper John Bosco ambao ni wadhamini wa shindano hilo alisema wameamua kudhamini mashindano hayo kwa lengo la kuwaelimisha vijana kuhusiana na uzazi wa mpango.




Alisema hawataishia hapo wanaendelea kudhamini hadi miss Tanzania kutokana na kuona vijana hao wanaweza kuliwakilisha taifa."Katika sensa viijana ndio wameonekana kuwa na asilimia kubwa hivyo ni vizuri kuwa dhamini ili kuweza kujenga kizazi ambacho kimewezeshwa ambacho hakitaweza kuwa taifa tegemezi," alisema.

CHADEMA KWAWAKA, WAJUMBE WAKE WA BARAZA KUU NA WANACHAMA WATINGA KWA MSAJILI WA VYAMA NA KWA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI KUOMBA MBOWE NA SLAA WADHIBITIWE KWA UFISADI.

$
0
0
 Mjumbe wa Baraza Kuu Chadema ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Temeke Joseph Yona (kushoto) akiongoza wenzake kuingia Ofisi ya Msajili wa Vyama leo kuwashitaki viongozi wa ngazi ya juu wa chama hicho kwa kudaiwa kutotekeleza Demokrasia na kufuata Katiba ndani ya Chama.
 Wanachama na Viongozi wa Chadema wakiwemo wa Baraza Kuu la chama hicho, wakipiga kwata kuelekea Ofisi za Msajili wa Vyama vya Siasa, jijini Dar es Salaam, leo, kupeleka barua ya kumuomba Msajili huyo wa vyama, kuwataka viongozi wa ngazi ya juu wa Chadema kuzingatia Katiba ikiwemo kuitisha kikao cha Baraza Kuu na kuzingatia matumizi bora ya fedha za Chama.
 Yona akisaini kitabu cha wageni kwenye kwenye mapokezi ya Ofisi ya Msajili wa Vyama Jijini Dar es Salaam, alipowasili ya ujumbe wake. Kulia kwa Yona ni Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Kaliua mkoani Tabora ambaye ni Mjumbe wa  Baraza Kuu na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Chadema, Jorum Mbogo
 Naibu Msajili wa vyama vya Siasa Nchini akimkaribisha Yona na msafara wake.
 Wanachama waliofuatana na wajumbe wa Baraza Kuu Chadema wakisubiri kuwasisha barua yao kwa Mkuu wa Masijala wa Ofisi ya Msajili wa vyama.
 Yona akionyesha abarua ambayo baadaye aliikabidhi masijala kwa ajili ya kumfikia Msajili wa vyama
 Yona akikabidhi barua yao, kwa Mtunza kumbukumbu Mkuu wa Ofisi ya Msajili wa vyama, Jihadhari Saidi.
 Yona akizungumza nje ya Ofisi ya Msajili baada ya kuacha barua yao kwa Msajili wa Vyama
  Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Kaliua mkoani Tabora ambaye ni Mjumbe wa  Baraza Kuu na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Chadema, Jorum Mbogo akisoma taarifa yao kabla ya kwenda kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali baadaya ya kutoka kwa Msajili ya vyama.

 Baadhi ya wanachama wanaodaiwa kuwa wa Chadema wakiwa na mabango nje ya Ofisi ya Msajili wa vyama
 Mamilioni ya ruzuku yanayeyukia wapi? Bango linauliza
 Eti Bora Chadema ife kuliko Mbowe kutapeli?
 Chadema wakiomba msaada kwa Msajili wa vyama
 Ujumbe mzito kwa Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe
   Wanachama na Viongozi wa Chadema wakiwemo wa Baraza Kuu la chama hicho, wakiwa nje ya Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali leo kupeleka maombi ya kutaka Mkaguzi huyo wa Hesabu za serikali kufanya ukaguzi wa hesabu wa Chadema kwa madai kwamba viongozi wa ngazi za juu wanazitafuna.KWA HISANI KUBWA YA KAMANDA WA MATUKIO BLOG.


TAARIFA YA KANUSHO LA KUFARIKI KWA MBUNGE SHUKURU KAWAMBWA

$
0
0
Ndg Watanzania,WanaBagamoyo na wapenda maendeleo, kwa niaba ya CCM-Bagamoyo na Ofisi ya Mbunge-Jimbo la Bagamoyo napenda kuleta kwenu Masikitiko yetu kwa niaba ya Chama na Familia ya Mheshimiwa Mbunge Shukuru Jumanne Kawambwa kutokana na Usumbufu ambao umesababishwa na habari zinazoenezwa Mitandaoni kwamba Mheshimiwa Kawambwa amekumbwa na Umauti akiwa njiani anaelekea Mwanza.


UKWELI
Mheshimiwa Shukuru Jumanne Kawambwa yupo Nchini Canada Akitimiza majukumu yake. Hivyo Watanzania na wana Bagamoyo mnaombwa radhi kwa usumbufu uliotokea na kwamba Mheshimiwa Mbunge yuko na Afya njema na utekelezaji wa Majukumu unaendelea kama kawaida.


Ndg.Ridhiwani Kikwete (Mnec)
Mbunge -Chalinze 

KARIBU JAMVINI MDAU WA THE HARUSI BLOG

$
0
0
Habari Wadau,
The Harusi Blog ni blog mpya inayojikita kwenye suala Zima la harusi na matukio muhimu yanayoambatana nayo, Hapa tunaelimishana, kukumbushana mambo muhimu lakini pia kuburudika ila zaidi ya yote inaruhusu kila mtu kutuma picha zake za harusi na ku share na ndugu jamaa marafiki n.k

Kimsingi mambo yoote kuhusu harusi utayapata hapa.
Naomba support kutoka kwenu kwa kushirikisha wengine na kunipa links kwenye blog/website zenu pia kuitabulisha.
Asante sana
 
Jackson
The Harusi Admin

MIFUKO YA HIFADHI ZA JAMII YATOA SEMINA KWA ASKARI POLISI MJINI MOSHI.

$
0
0
Ofisa mnadhimu namba moja wa jeshi la polisi mkao wa Kilimanjaro SSP Koka Moita akichangia jambo wakati wa semina juu ya mifuko ya hifadhi ya jamii iliyotolewa kwa maofisa wa jeshi hilo wa ngazi mbalimbali.
Kamanda wa polisi wa wilaya ya Moshi,OCD Deusdedit Kasindo akizungumza jambo wakati wa semina hiyo.
Viongozi wa ngazi ya juu wa jeshi la polisi mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia maelezo juu ya mifuko ya hifadhi ya jamii.
Baadhi ya askari polisi wa wilaya ya Moshi wakifuatilia maelezo juu ya mifuko ya hifadhi za jamii.
PICHA ZAIDI YA TUKIO HILI BOFYA HAPA

BONDIA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' AWASHUKURU VIONGOZI WA NGUMI NCHINI

$
0
0
BONDIA Ibrahimu Class 'King Class Mawe' amewashukuru viongozi wa ngumi nchini kwa sapoti yao wanayo mpa tangu ahanze ngumi mpaka sasa kwani yeye malengo yake ni kufika mbali zaidi baada ya kunyakuwa mkanda wa ubingwa unaotambuliwa na WPBF Africa Welterweight Title 

Aliyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa DDC Keko kulipokuwa na mkutano mkuu wa chama cha ngumi za kulipwa nchini cha TPBC, ambapo alikutana na viongozi mbalimbali na kupongezwa kwa kunyakuwa mkanda huo wa ubingwa alioupata Zambia kwa kumpiga bondia Mwansa Kabinga kwa TKO ya raundi ya tisa katika uwanja wa Arthur Davies Stadium, Kitwe, Zambia

bondia huyo mwenye ndoto za kuwa mmoja wa mabondia watakotamba duniani ambapo mwanzoni mwa mwaka huu aliteuliwa kuwa bondia bora wa mwaka 2013 katika uzito wake tuzo zilizoanza kufanyika mwaka huu

fikra zake kwa sasa ni kuwa bingwa wa mikanda mbalimbali inayotambulika Duniani katika uzito wake fikra zake siku moja ni kupambana katika mapambano makubwa zaidi hususani katika ukumbi wa MGM Gland nchini Marekani.

Bondia huyo mwenye rekodi ya kushinda mapambano 11 na kupoteza mpambano mmoja wakati ananza mchezo huo.bondia huyo anawashukurujopo la makocha wake wa kambi ya ilala linalo ongozwa na kocha mkongwe wa mchezo huo Habibi Kinyogoli 'Masta',kondo Nassoro,Sakwe Mtulya na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kwa kumsimamia na kumpa ushari anapokuwa ulingoni akipambana

bila kuwasahau mashabiki wake waliojaa kila kona ya jiji la Dar es salaam na Tanzania nzima kwa ujumla

TBL KUWAJENGEA KISIMA CHA MAJI CHA SH MIL. 29 WANANCHI WA SARANGA, DAR

$
0
0
 Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu akimkabidhi Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa King'ongo, Benetris Mapesi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil 29  za msaada wa ujenzi wa kisima cha maji katika mtaa huo uliopo Kata ya Saranga, Kinondoni Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika katika mtaa huo mwishoni mwa wiki.Wanaoshuhudia makabidhiano hayo ni Mkandarasi wa kisima hicho, Onesmo Sigala (wa pili kulia) wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MO Resources Limited,na Mjumbe wa Kamati ya Maji ya Mtaa wa King'ongo, Anna Kibwana ( wa pili kushoto).
Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ukandarasi ya MO Resources Limited, Onesmo Sigala (kulia) mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil 29  za msaada wa ujenzi wa kisima cha maji katika mtaa huo uliopo Kata ya Saranga, Kinondoni Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika katika mtaa huo mwishoni mwa wiki.Wanaoshuhudia makabidhiano hayo ni Mjumbe wa Kamati ya Maji ya Mtaa wa King'ongo, Anna Kibwana (wa pili kushoto),Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa King'ongo, Benetris Mapesi.

KUPANGA MIJI SIO KUKATA VIWANJA,AFAGILIA UTENDAJI KAZI WA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA-PROF.TIBAIJUKA

$
0
0
 Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mh.Prof Anna Tibaijuka akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wadau mbalimbali kwenye jukwaa la Uwekezaji katika Sekta ya Nyumba.Prof.Tibaijuka alisema kuwa Serikali inaridhishwa na utendaji unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Alisema katika kipindi kifupi Shirika limefanya mageuzi makubwa kwenye sekta ya makazi na kwamba miradi hiyo itakapokamilika,itaifanya miji hiyo kuwa ya kisasa.Prof.Tibaijuka alisema kuwa kampuni za uwekezaji kwenye sekta ya nyumba ni muhimu na hunyanyua uchumi wa nchi,alisema kuwa ili Taifa liweze kuendelea ni lazima liwe na mipango miji na kwamba kupanga miji sio kukata viwanja bali ni kunahitaji mambo mengi.Prof Tibaijuka amewataka wananchi kuwa tayari katika suala la kupanga miji,na maeneo yote yatakayopangwa ni lazima yafidiwe.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC,Nehemia Mchechu akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wadau mbalimbali kwenye jukwaa la Uwekezaji wa sekta ya nyumba lililofanyika jijini Dar.Bwa.Mchechu alisema kuwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),limedhamiria kuyabadilisha maeneo ya jiji la Dar na mikoa mingine nchini baada ya kuzindua ujenzi wa miji midogo.

Alisema kuwa Miradi hiyo itakapokamilika itabadilisha mandhari ya maeneo mbalimbali nchini na kuyafanya kuwa ya kisasa,Mchechu alisema kuwa wataanza na miradi mitatu ikiwemo miji midogo katika majiji ya Dar es salaam na Arusha na kuendeleza nyumba zao zilizobomolewa.

Alisema kuwa katika jiji la Dar,watakuwa na mradi wa salama Kigamboni na Kawe mbayo italifanya jiji hilo kubadilika kuwa la kisasa,aliongea kuwa katika miradi hiyo,kutajengwa nyumba nyingi za kuishi, biashara na sehemu za huduma muhimu .

Mchechu amesema kuwa mradi mwingine utakaotekelezwa ni wa Usa River Safari City utakaojengwa jijini Arusha,ambao utalenga kulibadilisha jiji hilo na kuwa la kisasa,aliongeza kusema kuwa mradi huo utagharimu dola za Kimarekani bilioni mbili (zaidi ya shilingi bilioni 3.4) na itakamilika kati ya kipindi cha miaka saba mpaka 12.Bwa.alisema kuwa miradi mingine ambayo itatekelezwa ni pamoja na  Bagamoyo,Dodoma,Mbeya,Mtwara,Lindi,Mwanza na maeneo Mengine.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),Bi.Zakhia Meghi akizungumza kwa ufupi mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wadau mbalimbali kwenye jukwaa la Uwekezaji wa sekta ya nyumba.

Sehemu ya meza kuu ikifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye jukwaa hilo la uwekezaji wa sekta ya Nyumba,lililofanyika jijini Dar

Wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye kwenye jukwaa la Uwekezaji wa sekta ya nyumba.

Exim FC yaichapa PWC 5-2 mechi ya kirafiki

$
0
0
 Kiungo wa timu ya Exim Bank FC,Mustafa Juma (kulia) akikokota mpira wakati wa mechi ya kirafiki na timu ya PWC iliyochezwa katika uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Exim Bank FC ilishinda kwa magoli 5 – 2.
Mchezaji wa timu ya Exim Bank FC,Edwin Setebe akikokota mpira wakati wa mechi ya kirafiki na timu ya PWC iliyochezwa katika uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Exim Bank FC ilishinda kwa magoli 5 – 2.

TIMU ya Benki ya Exim maarufu kama 'Innovation Team’  imeichapa PWC mabao  5 - 2 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.


Wakati wa mechi hiyo iliyoshuhudiwa na watazamaji mbali mbali, timu ya Exim FC iliyoongoza kwa upande wa umilikaji mpira na kuweza kujipatia goli la kwanza katika dakika ya 20 shukrani zikimwendea mchezaji Lusajo Adam,  wakati katika dakika 22 kiungo Norbert Misana aliipatia timu hiyo goli la pili, mpaka kipindi cha kwanza kinaisha Exim FC ilikuwa ikiongoza kwa goli 2-0.

PWC walifanya mabadiliko katika kipindi cha pili yaliyowaletea matunda na kuweza kupata magoli katika dakika ya  47 na 54 ya mchezo baada ya kupata nafasi mbili za wazi kutokana mabeki wa timu ya Exim FC kushindwa kuwazuia washambuliaji wa PWC kuto funga magoli ya kusawazisha.

Exim FC kupitia mchezaji Norbert Misana aliweza kufunga mabao mengine mawili, goli la tatu likifungwa katika dakika ya 55 na goli la nne likipachikwa kimyani katika dakika ya 70 ya mchezo kabla ya Rogers Timoth kumalizia karamu ya mabao katika dakika ya 85 lililowawezesha Exim FC kuibuka na ushindi baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa.

Akizungumza muda mfupi baada ya kipenga cha mwisho cha mchezo kupulizwa, Norbert Misana ambaye aliibuka mchezaji bora wa mechi hiyo alisema mechi hiyo ilikuwa rahisi zaidi ikilinganishwa na mechi zao nyingine zilizopita.


"Tumecheza mchezo mzuri zaidi ukilinganisha na mpinzani wetu.  Leo timu yetu ilikuwa imejipanga vizuri zaidi hususani katika nafasi ya katikati, na ndiyo maana tuliweza kuudhibiti mchezo kapita vipindi vyote. Tumeweza kucheza kitimu  katika muda wote wa mchezo kitu ambacho kimetusaidia tuweze kutengeneza nafasi nyingi za magoli.


"Wapinzani wetu, PWC ni timu bora, lakini leo nadhani timu yetu, kila mchezaji amekuwa katika fomu kutokana na mazoezi  ya kutosha tuliyokuwanayo na tunaamini tukiendelea na hali hii, timu yetu itafika mbali kimchezo.


"Tumekuwa tukifanya mazoezi kila mwishoni mwa wiki. Hali hii ya mazoezi kwa wiki sio tu inatujenga kiuwezo ili kumfunga kila tunaekutana nae lakini pia yanatuweka imara kiafya na kiakili na hivyo kuweza kutekeleza majukumu yetu vizuri na kwa ufanisi kama wafanyakazi wa Benki ya Exim,” alisema Norbert Misana.

JUMA PINTO MGENI RASMI KATIKA BONANZA LA TASWA ARUSHA

$
0
0

  picha ikionyesha katibu wa chama cha waandishi wa habari  Mussa Juma  akiwa  na mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari za michezo, Arusha (TASWA) Jamila Omary wakiwa wana pokea cheki ya  shilingi   milioni moja na laki tano  kutoka kwa meneja masoko wa  Megatrade  Gudluck Kwayu katika ukumbi wa hoteli ya palace mkoani Arusha. 


katibu wa taswa wa kwanza  kushoto  Musa juma akiwa anaongea na waandishi wa habari kuhusiana na bonanza la taswa linalotarajiwa kufanyika jumamosi katika viwanja vya general trye jijini hapa wa katikati ni meneja matukio wa TBL Chris Salakana (picha zote na woinde shizza,Arusha.

Na Woinde Shizza,Arusha

 Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari za michezo nchini
(TASWA), Juma Pinto, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika bonanza la
vyombo vya habari kanda ya kaskazini, June 28 mwaka huu ambalo
limedhaminiwa na kampuni ya hia nchini (tbl)

Katibu wa TASWA mkoa wa Arusha, Mussa Juma akizungumza na waandishi wa   habari, palace hoteli katika kikao cha kutangaza zawadi na wadhamini wa bonanza hilo.alisema maandalizi ya bonanza hilo  ambalo wadhami  wakuu ni kampuni ya bia nchini (TBL) yamekamilika.



Alisema Pinto ambaye pia ni mjumbe wa Bodi ya  hifadhi ya Mamlaka ya
Ngorongoro, anatajiwa kutoa zawadi kwa washindi, ambapo bingwa anavuna    kikombe na fedha taslimi 200, 000.



Mshindi wa pili katika soka atavuna 100,000, mshindi mpira wa pete
atavuna 100,000 huku timu yenye nidhamu itapokea tsh 50, 000.

Awali Mwenyekiti wa Taswa mkoa wa Arusha, Jamila Omar alisema timu za   wanahabari na wadau wa habari, watachuana katika soka, mpira ya pete,  kuvuta kamba, kukimbiza kuku, mbio za magunia.



Aliwataja wadhamini wengine kuwa ni Mega trade, Mamlaka ya hifadhi
Ngorongoro, Kampuni ya Tanzanite forever,  TANAPA,Coca Cola, Pepsi
Arusha, Aicc na palace Hotel.

Timu ambazo zitashiriki ni Triple A, Sunrise radio, AJTC, Wazee Klabu,
Taswa Arusha, Radio 5, ,Arusha One, Mj radio, Radio ORS kutoka mkoa wa
Manyara na  NSSF.

Katika kikao hicho, ,Meneja masoko wa mega Trade alikabidhi the hundi
ya udhamini kiasi cha Tsh 1.5 milioni huku, Meneja matukio wa TBL
kanda kaskazini  Fred Sarakana akitangaza Tbl kuendelea kuwa wadhamini   wakuu wa bonanza hilo na kuwataka wanahabari kujitokeza kushiriki.

POLISI KILIMANJARO YABAINI MBINU MPYA INAYOTUMIKA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA .

$
0
0
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,SACP,Robert Boaz akitoa dawa za kulevya katika mikoba ya kike ambayo imekamatwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro KIA.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,SACP,Robert Boaz akiwaonesha waandishi wa habari(hawako pichani)moja ya mikoba iliyotumika kufichia dawa za kulevya kwa ustadi mkubwa.
Dawa za Kulevya ambazo hazijafahamika ni aina gani zikiwa katika mifuko maalumu.
Baadhi ya waandishi wa habari mkoa wa Kilimanjaro wakimsikiliza kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro wakati akitoa taarifa  juu ya kukamatwa kwa dawa za kulevya katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro KIA.

ROSE MUHANDO KUZINDUA ALBAMU YAKE YA FACEBOOK AGOSTI 3/2014 JIJINI DAR

$
0
0

TANGAZO LA KUPUNGUZA UZITO

$
0
0


CLEAN 9 ni nini na ina nini??

Ina mchanganyiko wa bidhaa nne (Alovera Gel chupa 3, Ultra Lite, Bee pollen na Garcinia. Pia ina tape measure pamoja na chupa ya kupimia)

Ina kitabu cha muongozo wa jinsi ya kutumia.
CLEAN 9 ni muhimu katika kupunguza mwili kwasababu inafanya kazi ya kusaidia mfumo wako wa mmeng'enyo wa chakula,kuondoa sumu mwilini,kuondoa mafuta yaliyozidi mwilini na kukupa mfumo bora wa ulaji chakula.

Matumizi yake ni rahisi sana. Tumia bidhaa kwa usahihi kisha utahitaji kufanya mazoezi walau dakika 20 (kutembea,kuruka kamba,kukimbia au gym ukipenda), Kunywa maji ya kutosha angalau lita tatu kwa siku pungza au acha kabisa ulaji wa vyakula vyenye sukari,wanga na mafuta.

Unatumia kwa siku tisa na itakusaidia kupungua kilo 3 mpaka 8 na kupungua zaidi utatumia Nutri lean ambayo ina bidhaa za mwezi mzima na una uwezo wa kupungua kilo 10 mpaka 15. Rahisi eeh??
Wasiliana nasi kwa kupiga au watsup kwa maelezo zaidi +255 713 418 475

Redd's Miss Sinza 2014 Kufanyika kesho Meeda Club Sinza

$
0
0
Mratibu wa shindano la Redd's miss Sinza 2014 Tinna Matutuna katikati akizungumza na waandishi wa Habari katika ukumbi wa mikutano wa Meeda Night Club sinza juu ya Shindano la Redd's Miss Sinza litakalofanyika kesho ijumaa katika ukumbi wa Meeda Night Club kwa kiingilio cha 5,000 kwa viti vya kawaida na 10,000 kwa Viti Maalum kushoto na kulia ni baadhi ya warembo wa shindano hilo.
=======  ====== =====
MNYANGE atakayefanikiwa kuibuka mrembo wa kitongoji cha Sinza ‘ Redds Miss Sinza  2014’ katika shindano litakalofamyika leo Ijumaa kwenye Ukumbi wa Meeda Night Club uliopo Sinza jijini Dar es Salaam atazawadiwa kitita cha Sh. 300,000.


 Akizungumza jana jijini, Mratibu wa shindano hilo, Tinna Makutika, alisema kuwa mshindi wa pili atajinyakulia Sh. 200,000, mshindi wa tatu  Sh. 100,000 huku warembo wengine waliobakia kila mmoja ataambulia zawadi ya kifuta jasho ya Sh. 50,000.


 Mratibu wa shindano hilo alisema kuwa maandalizi ya kinyang’anyiro hicho yamekamilika na anaamini Sinza mwaka huu itafanikiwa kutwaa taji la taifa ambalo linashikiliwa na mrembo kutoka Dodoma.


Alisema kuwa warembo wake wamejiandaa kuonyesha ushindani na kila mmoja amejipanga kufanya vizuri ili kushinda taji la Sinza usiku wa leo.

"Mwaka huu nina warembo wazuri na wenye vigezo vyote, naamini mwaka huu nitarudisha heshima ya watu wa Sinza ya  kufanikiwa kutoa mshindi wa taji la Redd's Miss Kinondoni  na Redd's Miss Tanzania mwaka 2014”, alisema Tinna.


Aliongeza kuwa wamejipanga kuendeleza mazuri yaliyofanywa na Brigitte Alfred, ambaye alitwaa taji la taifa na kupata nafasi ya kuitangaza nchi kwenye mashindano ya dunia ya Miss World.Alisema pia shindano hilo linatarajiwa kuwa na burudani mbalimbali ikiwamo  bendi mahiri ya muziki wa dansi, FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ ambao wanatamba na Chuki ya Nini. Kiingilio cha juu katika shindano hilo ni Sh. 10,000 kwa viti maalum na vya kawaida ni Sh. 5,000.


Aliwataja warembo 12 watakaochuana ni Liliani Sandi,Priscar Sarakikya,Agnes Mwikombe,Esta Wilson,Rose Lucas,Zubeda Saburi,Tuku Harison,Dorine Benne,Farida Iddy,Qeenlatifa Hashim,Jane Masawe na Wahida Ahmed.


Naye Meneja wa kinywaji cha bia ya Redd’s Original, Victoria Kimaro, alisema ni muda muafaka kwa wapenzi wa tasnia ya urembo nchini wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kuhudhuria shindano hilo ili kushuhudia namna kitongoji cha Sinza kilivyo na bahati ya kutoa warembo wenye ushindani katika fainali za taifa.

Victoria alisema kuwa wadau wa sanaa ya urembo wanatakiwa kuona sanaa hiyo ni sehemu inayowapa nafasi wasichana kutimiza ndoto zao na hatimaye kujiendeleza kimaisha.

WASHIRIKI WA FAINALI YA SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) WATEMBELEA OFISI ZA GLOBAL PUBLISHERS LEO

$
0
0
 
Washiriki wa fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) ambao ni washindi wa TMT kutoka kanda sita za Tanzania wakisikiliza maelezo kwa makini kutoka kwa Mmoja wa Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers Limited (hayupo pichani)
 Mmoja wa washiriki wa fainali wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) ambae pia ni mshindi kutoka kanda ya Kati Mkoa wa Dodoma Mwinshehe Mohamed akijitambulisha mbele ya wafanyakazi wa Kampuni ya Kubwa ya Habari ya Global Publishers Limited ambao ndio watengenezaji wa Magazeti pendwa hapa Nchini wakati washiriki hao walipotembelea ofisi za Global Publishers zilizopo Bamaga Mwenge
 Baadhi ya wafanyakazi wa Global Publishers wakiwa katika majukumu yao ya kila siku


 Washiriki wa fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents wakipewa maelekezo ya jinsi magazeti ya kampuni hiyo yanavyoandaliwa hadi yanaponunuliwa na wadau wa habari
 Maelekezo yakiendelea kwa washiriki wa fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents
Washiriki wa Fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) wakiwa katika picha ya Pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publisher mara baada yakutembelea ofisi zao leo zilizopo 

Bamaga Mwenge Jijini Dar Es Salaam.
Na Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited - Dar Es Salaam
Washindi wa Kanda zote Sita za Tanzania wa Shindano la Tanzania Movie Talents ambao ni washiriki wa Fainali ya Shindano hilo kubwa kabisa nchini na Afrika Mashariki na Kati watembelea ofisi za Kampuni ya Uchapishaji wa Magazeti ya Risasi, Ijumaa, Uwazi nk ya Global Publishers limited kwaajili ya kujionea jinsi magazeti kutoka kampuni hiyo yanavyoandaliwa mpaka yanapowafikia wasomaji.

Washiriki hao pia waliweza kupata fursa ya kuuliza maswali kwa wafanyakazi hao wa Kampuni ya Global Publishers kwaajili yakufahamu mambo mbalimbali yanayohusu kampuni hiyo Kubwa kabisa Tanzania.
Washiriki wa Fainali ya shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) wanatarajia kuingia kambini leo tayari kwa mchakato wa kushindania shilingi Milioni 50 za Kitanzania kwa mshindi mmoja.

Huu ndio muda wa Watanzania kuweza kumchagua mshindi wa Milioni 50 kwa kumpigia kura mshiriki ambae ataonekana kukuna nyonga zao kwa kuonyesha kipaji cha kweli. Watanzania wataweza kuwapigia kura washiriki watakaoonekana kuwa na vipaji kwa kutuma namba za washiriki kwenda namba maalumu itakayotolewa.

Rais Kikwete ashiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Umoja wa Afrika,Mjini Malabo, Equatorial Guinea

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiambatana na ujumbe wa Tanzania kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika Mjini Malabo, Equatorial Guinea. Miongoni mwa masuala muhimu yanayotarajiwa kujadiliwa kwenye mkutano huu ni bajeti ya umoja huo na mkakati wa kukusanya maoni kutoka nchi wanachama kuhusu Afrika ifikapo mwaka 2063, ambapo umajo huu utafikisha miaka mia moja.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wajumbe wenzake wa kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika unaofanyika Mjini Malabo, Equatorial Guinea.
Viongozi wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika wakiwa kwenye picha ya Pamoja.Picha na IKULU.

FARIDA FOUNDATION YATOA MISAADA HOSPITALI YA PALESTINA SINZA NA KWA WALEMAVU ENEO LA UBUNGO DARAJANI

$
0
0
 Mkurugenzi wa Farida Foundation akikabidhi moja ya msaada kwa kaimu Mganga mkuu wa Hospitali ya Palestina Dk Hugoline Mselle,Huku wafanyakazi wengine wa Hospitali hiyo wakishuhudia.
 Bi Farida Abdul Akikabidhi bandeji kwa ajili ya kufungia wagonjwa kwa Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Palestina Dk Hugoline Mselle
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Palestina Dk Hugoline Mselle akipoke Ndoo zitakazotumika kwa ajili ya kuhifadhia uchafu katika Hospitali hiyo,ambazo zilitolewa kama Msaada na Farida Foundation
 Bi Farida Abdul akimuonyesha kaimu Mganga mkuu wa Hospitali ya Palestina Dk Hugoline Mselle Vifaa ambavyo vimeletwa kama msaada kwenye Hospitali hiyo.Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Viti vya magurudumu vitatu ambavyo vitasaidia kubebea wagonjwa,Bandeji za kufungia vidonda,Ndoo za kuwekea taka,na vinginevyo.
 Hivi ni viti Vitatu vya kubebea wagonjwa ambavyo vilitolewa kama msaada kwenye Hospitali ya Palestina(sinza) na Farida Foundation.


 Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Palestina Akimshukuru Bi Farida Abdul kwa kutoa msaada katika hospitali hiyo na akampongeza kwa moyo wake na kumsisitiza aendelee Kusaidia kila mara anapopata nafasi ili huduma zao ziwe bora zaidi kila siku.
 Mkurugenzi wa Farida Foundation Bi Farida Abdul akiongea na vyombo vya habari na kuelezea ni kwanini ameamua kutoa misaada hiyo katika hospitali ya Palestina,Amesema kwamba Serikali peke yake haiwezi kufika kwa kila mgonjwa na hospitali kwa wakati,kwa hiyo inatakiwa kujitoa kwa mashirika kusaidiana na Serikali ili Hospitalietu Ziweze kuwa na Huduma bora.
Kaimu mganga Mkuu wa Hospitali ya Palestina Dk Hugoline Mselle ameishukuru Taasisi ya Farida Foundation kwa misaada waliyotoa kwani itawasaidia sana kuboresha Huduma zao.

BAADA YA KUTOKA HOSPITALI YA PALESTINA SINZA FARIDA FOUNDATION WALIELEKEA UBUNGO DARAJANI KWA AJILI YA KUTOA MSAADA KWA MLEMAVU WA MIGUU,AMBAPO WALIMPATIA BAISKELI NA MTAJI WA VITU VYA BIASHARA
 Mkurugenzi wa Farida Foundation Bi Faridah Abdul akiongea na mlemavu wa miguu ndugu Marcerine Mayemba eneo la ubungo darajani kabla ya kumkabidhi msaada wa mtaji wa biashara pamoja na baiskeli atakayokuwa anaitumia.
 Bi Farida Abdul Akiwa na baiskeli ambayo aliikabidhi kwa mlemavu wa miguu bwana Marceline Mayemba,kwa ajili ya kumsaidia katika matumizi yake ya kila siku
 Mlemavu wa Miguu Bwana Marceline Mayemba Akipanda kwenye Baiskeli yake aliyokabidhhiwa na Farida Foundation
 Mlemavu wa Miguu Bwana Marceline Mayemba Akiendesha Baiskeli yake mara tu baada ya kukabidhiwa na Farida Foundation
 Bi Farida Abdul Akimkabidhi Mlemavu wa miguu bwana Marceline Mayemba Katoni ya Bidhaa ambazo ataanza nazo kama mtaji wa bishara,pia alikabidhiwa katoni tatu za maji,Katoni tatu za Juice na Katoni zingine Vifaa kama pipi,bigijii ili viwe kama kianzio kwa biashara yake.
Bi Farida Abdul Mkurugenzi wa Farida Foundation akikabidhi Mlemavu mwingine Chakula Pamoja na vinywaji.
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live


Latest Images