Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

NAFASI ZA MAFUNZO NA KAZI.

$
0
0

Taasisi  ya  RafikiElimu  Foundation  kupitia MRADI  WA  WANAWAKE  SALAMA  TANZANIA  inatangaza  nafasi  za  mafunzo  ya  UANDAAJI  NA  UTENGENEZAJI  WA  VYAKULA-LISHE MAALUMU KWA  WAGONJWA NA  WENYE MATATIZO  MBALIMBALI  YA KIAFYA.

Wahitimu  wa  mafunzo  haya  watapata  nafasi  ya  kufanya  kazi   kama  waandaji  na  watayarishaji  wa  Vyakula –Lishe  katika  MRADI  WA  WANAWAKE  SALAMA  TANZANIA.
Masomo  yatakayo  tolewa  ni pamoja na  UANDAAJI  WA VYAKULA-LISHE  MBALIMBALI  pamoja na   AFYA  YA UZAZI  KWA  WANAWAKE.

SIFA  ZA  MWOMBAJI  NAFASI.
1.          Awe  wa  jinsia  ya  kike.
2.          Awe  na  elimu  ya  kuanzia  kidato  cha  nne  na  kuendelea.
3.          Awe  anaishi  jijini  Dar  Es  salaam.
4.           Awe  tayari  kufanya  kazi kama  muandaaji  na  mtayarishaji  wa  vyakula-lishe  katika MRADI WA  WANAWAKE SALAMA TANZANIA.
5.          Awe  na  uwezo  wa  kusoma  na  kuelewa  mwenyewe   kwa  njia  ya  vitabu na   VIDEO  CD  bila  kuingia  darasani.

KUANZA  KWA  MAFUNZO : Mafunzo  haya  taanza tarehe 21   JULAI  2014.

MUDA  WA  MAFUNZO :
Mafunzo  haya  yatafanyika  kwa  muda  wa  mwezi  mmoja .

   ADA     YA   MAFUNZO  : 
Mafunzo  haya  yanatolewa  BURE  chini  ya  udhamini  wa  mashirika  hisani..

FOMU ZA   KUJIUNGA  NA  MAFUNZO :
Fomu  za  kujiunga  na  mafunzo  haya  zinapatikana  katika  ofisi  zetu  zilizopo  katika  eneo  la  CHANGANYIKENI  karibu  na   CHUO  CHA  TAKWIMU mbele  ya CHUO  KIKUU  CHA  DAR  ES  SALAAM.

JINSI  YA  KUFIKA  OFISINI  KWETU :
Panda  daladala  za  UBUNGO-CHANGANYIKENI  kasha  shuka  kituo  cha  TAKWIMU  halafu  tembea  hatua  ishirini  mbele  kasha  tazama  upande  wako wa  kulia  utaona  ofisi  imeandikwa  RAEFO  TANZANIA.

MWISHO  WA  KUCHUKUA  FOMU:
Mwisho  wa  kuchukua  fomu  za  kujiunga  na  mafunzo  haya  ni  tarehe  18  JULAI  2014  saa  sita  kamili  mchana.

KWA  MAELEZO  ZAIDI,WASILIANA  NASI  KWA  SIMU  NAMBA 0784406508
 Au  tuandikie  kupitia  barua  pepe  yetu  :


MAKAMU WA RAIS, DKT. BILAL AMKARIBISHA MAKAMU WA RAIS WA CHINA NA UJUMBE WAKE IKULU DAR LEO, WASAINI MIKATABA

$
0
0
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara (kulia) akisainiana mkataba na Naibu Waziri wa Wizara ya Biashara ya Wau wa China, Li Jinzao, wa Makabidhiano ya gari la matangazo la Shirika la Utangazaji la TBC, yaliyofanyika mapema mwaka huu. Shughuli hiyo ya kutiliana saini imefanyika leo Juni 23, 2014, Ikulu jijini Dar es Salaam, ikishuhudiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dorothy Mwanyika, (kulia) akisainiana mikataba miwili na Naibu Waziri wa Wizara ya Biashara ya Wau wa China, Li Jinzao, ya makubaliano ya ushirikiano wa Kitaalamu utakaoiwezesha China kuwapa mafunzo Wanariadha wa Tanzania nchini China na wa makubaliano ya awamu ya tatu ya Ushirikiano wa kiufundi baada ya China kusaidia na kukamilisha Ujenzi wa Uwanja wa Taifa. Shughuli hiyo ya kutiliana saini imefanyika leo Juni 23, 2014, Ikulu jijini Dar es Salaam, ikishuhudiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao, wakati alipowasili Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo June 23, 2014. Li Yuanchao, yupo nchini kwa ziara ya siku sita
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa pili kulia) na baadhi ya Mawaziri wake, akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao, aliyeongozana na ujumbe wake  wakati alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 23, 2014 kwa ajili ya mazungumzo.  Li Yuanchao, yupo nchini kwa ziara ya siku sita.
 Baadhi ya Mawaziri waliofika katika mazungumzo hayo Ikulu jijini Dar es Salaam, na baadhi kusaini mikataba na watu wa China.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao, wakati alipowasili Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo juni 23, 2014 akiongozana na Ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo.  Li Yuanchao, yupo nchini kwa ziara ya siku sita.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao, wakati alipowasili Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 23, 2014 akiongozana na Ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo.  Li Yuanchao, yupo nchini kwa ziara ya siku sita.  Wa pili (Kulia) ni Balozi wa Tanzania, nchini China, Luteni General Abraham Shimbo.

SHIRIKA LA HUDUMA ZA AFYA LA MAREKANI (JHPIGO) LAONYESHA FILAMU KATIKA TAMASHA LA KIMATAIFA LA NCHI ZA JAHAZI ZIFF.

$
0
0
  Wananchi na waandaaji wa Filamu ya tohara kwa wanaume iliyotengenezwa na Lisa Russeli wakiangalia filamu hiyo katika Ukumbi wa Hoteli ya Double Tree.
 Wananchi na waandaaji wa filamu ya Tohara kwa wanaume wakiangalia filamu hiyo hapo jana.
 Mkurugenzi wa Shirika la Huduma za Afya la Marekani (JHPIEGO) Nchini Tanzania Hally Mahler akielezea umuhimu wa tohara kwa wanaume na sababu zilizopelekea kufadhili na kuandaa filamu hiyo.
 Mkuu wa Mpango wa Taifa wa kudhibiti maradhi ya ngono Dkt. Gissenge Lija akitoa maelezo ya Mpango huo baada ya maonyesho ya filamu ya umuhimu wa tohara kwa wanaume kwenye Tamasha la Kimataifa la Nchi za Jahazi (ZIFF).
 Msimulizi wa Filamu hiyo msanii Fareed Kubanda (Fid Q) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu madhara yanayowapata wanaume wasiofanyiwa  tohara hasa katika Mikoa ya Njombe  na Iringa Tanzania Bara.
Picha ya pamoja ya watengenezaji wa filamu ya umuhimu wa tohara kwa wanaume iliyowasilishwa kwenye Tamasha la Kimataifa la Nchi za Jahazi (ZIFF) katika Ukumbi wa Hoteli ya Double Tree Shangani Mjini Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

Rais Kikwete afungua Mkutano wa Wakaguzi wa Hesabu za Serikali Dar es Salaam

$
0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa wakaguzi wa Hesabu za Serikali uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo(pich na Freddy Maro) .
Baadhi ya wajumbe walioshiriki katika hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Mwaja wa wakaguzi wa Hesabu za Serikali uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere(JNICC) jijini Dar es Salaam leo.(picha na Freddy Maro).
 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali Bwana Ludovick  Utouh  akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Kikwete na kuwatambulisha baadhi ya wageni na viongozi waandamizi walioshiriki katika hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa wakaguzi wa Hesabu za Serikali uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere(JNICC) jijini Dar es Salaam leo.

Kutoka kushoto ni balozi wa Sweden Mh.Lennarth Hjelmaker, mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Sweden Bwana Jan Landahl, na watatu kutoka kushoto ni Bibi Lara Tayloir Pearce ambaye ni mdhibiti na mkaguzi mkuu wa Serikali ya Sierra leone.
  

Mb Dog akamilisha mbili mpya

$
0
0
Msanii Mb Dog pichani.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

MWIMBAJI wa muziki wa kizazi kipya, Mbwana Mohamed Mb Dog, amekamilisha nyimbo nyingine mbili mpya zinazojulikana kama Ya Moto na Demu Mwingine.

Kukamilika kwa nyimbo hizo ni mwendelezo wa mikakati ya msanii huyo kufanya kazi nzuri ili kumuweka katika kiwango cha juu katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya.

Akizungumza leo mchanaa jijini Dar es Salaam, Mb Dog alisema kwamba nyimbo hizo amezirekodi katika Studio yake ya Macoppa, zilizopo jijini Dar es Salaam. Alisema kuwa nyimbo hizo zinaungana na ile ‘Mbona Umenuna’ aliyoachia mapema mwezi uliopita na kupokewa kwa shangwe na wadau wa Bongo Fleva Tanzania.

“Hizi ni nyimbo mbili mpya na ambazo naamini zitapokewa kwa shangwe na wadau mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini. “Naamini kila kitu kitakwenda vizuri kuhakikisha kuwa mambo yanakuwa mazuri, ukizingatia kuwa mipango iliyopo mbele yangu ni kufanya kazi ya maana ili nionyeshe ukomavu wangu kisanaa,” alisema Mb Dog.

Mb Dog ni mmoja wa wasanii wanaotambulika kwa umahiri wao katika tasnia ya Bongo Fleva, huku akikumbukwa kwa nyimbo zake, ukiwamo ule wa Latifa na nyinginezo.

xxxxxx Mb Dog akamilisha mbili mpya bomba balaa Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam MWIMBAJI wa muziki wa kizazi kipya, Mbwana Mohamed Mb Dog, amekamilisha nyimbo nyingine mbili mpya zinazojulikana kama Ya Moto na Demu Mwingine.

Manispaa ya Kinondoni Kujenga Daraja litakalounganisha Mabwepande na Kitongoji cha Kikwete Visheni

$
0
0
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda (katikati) akisaini mkataba wa Ujenzi wa daraja la Mabwepande kwenda Kitongoji cha Kikwete Vision Mji Mpya na Meja Jenerali Dk,Charles Muzanila (kulia) wa Shirika la Ujenzi la Mzinga na Diwani wa Kata ya Mabwepande,Clement Boko (kushoto) huku wadau wakishuhudia.Sherehe ya kusaini ilifanyika eneo la ujenzi.
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda (pili kulia) wakibadilishana nyaraka baada ya kutia saini ya ujenzi wa Daraja na Meja Jenerali Dk,Charles Muzanila (kulia) wa Shirika la Ujenzi la Mzinga na Diwani wa Kata ya Mabwepande,Clement Boko (kushoto) akishuhudia.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda (wa pili kushoto),Diwani wa Kata ya Mabwepande Clement Boko (kushoto) Naibu Meya Songoro Mnyonge (wa pili kulia) na Meja Jenerali Dk,Charles Muzanila (kulia) wa Shirika la Ujenzi la Mzinga,wadau wakiwa katika sherehe ya kusaini mkataba wa Ujenzi wa Daraja linalounganisha Mabwepande na Kitongoji cha Kikwete Visheni.
 Hili ndiyo eneo linalotarajiwa kujengwa Daraja Upande zinakoonekana nguzo za umeme Mabwepande na kwenye watoto ni Kitongoji cha Kikwete Visheni.
Eneo la bonde lenye mto litakapo pita Daraja.

Wabunge wapata semina ya Itifaki ya Umoja wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki

$
0
0
 Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwezeshaji wa Uchumi Dkt. Mary Nagu akifungua semina ya Wabunge kuhusu Itifaki ya Umoja wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki jana katika ukumbi wa Bunge wa Msekwa mjini Dodoma. Kulia ni Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum.

 Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akisisitiza umuhimu wa Itifaki ya Umoja wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Wabunge katika semina iliyofanyika jana ukumbi wa Bunge wa Msekwa mjini Dodoma.

 Mkurugenzi Msaidizi Sekta za Uzalishaji Wizara ya Afika Mashariki Dkt. Abdula Makame akiwaeleza Wabunge umuhimu wa Itifaki ya Umoja wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa semina iliyofanyika jana katika ukumbi wa Bunge wa Msekwa mjini Dodoma.

 Mkurugenzi  wa Masuala ya Utafiti wa Uchumi na Sera Benki Kuu ya Tanzania Dkt. Joseph Masawe akitoa mada juu ya Majukumu ya Benki Kuu ya Afrika Mashariki na Benki Kuu Wanachama  na Nchi wanachama walivyojifunza kutoka Umoja wa Ulaya wakati wa semina ya Wabunge iliyofanyika jana katika ukumbi wa Bunge wa Msekwa mjini Dodoma.

 Mchungaji Luckson Mwanjale, mbunge wa Mbeya Vijjini akichangia hoja juu ya Itifaki ya Umoja wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki jana mjini Dodoma.

Sara Msafiri (Viti Maalum) akichangia mada juu ya itifaki ya Umoja wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa semina ya Wabunge iliyofanyika jana katika ukumbi 

mahafali ya Wahitimu wa Uhifadhi wa wanyamapori jijini mwanza

$
0
0

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizindua maabara ya kompyuta katika  chuo cha Taasisi ya Taaluma ya wanyamapori Pasiansi Mwanza wakati wa mahafali ya 49 ya chuo hicho. Kulia ni Balozi wa Marekani Mark Childless.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na Balozi wa Marekani Mark Childless wakikagua gwaride la heshima la wahitimu wa chuo hicho.

Wahitimu wakionesha utaalamu wa Karate.
 Wahitimu wa Uhifadhi wa wanyamapori katika chuo cha Taasisi ya Taaluma ya wanyamapori Psiansi Mwanza wakionyesha ujuzi wa kutumia silaha wakati wa mahafali ya 49 ya chuo hicho juzi.
 Wahitimu wa Uhifadhi wa wanyamapori katika chuo Taasisi ya Taaluma ya wanyamapori Psiansi Mwanza wakicheza gwaride juzi, wakati wa  wa mahafali ya 49 ya chuo hicho juzi.


makamu wa rais wa china,Li Yuanchao afungua mkutano wa uwekezaji kati ya tanzania na china jijini Dar leo

$
0
0
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao wakitazama picha za ziara ya hayati Baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere kabla ya mgeni huyo kufungua mkutano wa Uwekezaji kati ya Tanzania na China kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es salaam  Juni 23, 3014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akimkabidhi zawadi ya kinyago, Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao  kabla ya mgeni huyo kufungua mkutano wa Uwekezaji kati ya Tanzania na China kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es salaam  Juni 23, 3014.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda   na  Makamu wa Rais wa China, Li  Yuanchao wakifungua  vitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la Kitegauchumi la Mfuko wa Mwalimu Nyerere mjini Dar es salaam Juni 23, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WWF's AFRICA VISION 2020 Document launch

$
0
0
 The Director General of World Wide Fund for Nature (WWF) International Dr. Marco Lambertini (Middle) cutting a ribbon to officially launch the Africa vision 2020 document. Left is Mr. Bell’Aube Houinato WWF Tanzania’s Country Director and right is Dr.Julius Ningu, Director of Environment – VPO witnessing in Dar es salaam on June 22nd  2014.
 The Director General of World Wide Fund for Nature (WWF) International Dr. Marco Lambertini (Middle) showing the  Africa vision 2020 document , left is Mr. Bell’Aube Houinato WWF Tanzania’s Country Director and right is Dr. Julius Ningu, Director of Environment during the launch ceremony in Dar es salaam on June 22, 2014.
 The Director General of World Wide Fund for Nature (WWF) International Dr. Marco Lambertini giving a speech during the Africa vision 2020 document launch in Dar es salaam on June 22nd, 2014. 
 WWF International Dr. Marco Lambertini in group photo with WWF Tanzania  employees at their Dar es salaam Country Office.

Rais kikwete akutana na Makamu wa Rais wa China pamoja na Mmiliki wa kampuni ya Dangote

$
0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati akizungumza na makamu wa Rais wa Jamhuri  ya Watu wa China Mh. Li Yuanchao ikulu jijini Dar es Salaam leo.
-Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na mmiliki wa kampuni kubwa ya kuzalisha saruji DANGOTE Industries Ltd Alhaji Aliko Dangote ikulu jijini Dar es Salaam leo  (picha na Freddy Maro)

MFUKO WA PSPF WAMALIZA WIKI YA UTUMISHI KWA MAFANIKIO MAKUBWA

$
0
0
Ofisa masoko wa mfuko wa pesheni kwa watumishi wa umma'PSPF' Bi, Rahma Ngassa kulia akimkaribishakatibu Mkuu Kiongozi  Balozi Ombeni Sefue katika banda la PSPF wakati wa maonesho ya wiki ya utumishi wa Umma yaliyomalizika jumatatu ya wiki hii.


Ofisa uhendeshaji wa mfuko wa pesheni kwa watumishi wa umma 'PSPF' Bw, Mohamed Masoud kulia akimpatia mahelezo katibu Mkuu Kiongozi  Balozi Ombeni Sefue alipotembeleabanda la PSPF wakati wa maonesho ya wiki ya utumishi wa Umma yaliyomalizika jumatatu ya wiki hii
Mkurugenzi wa mipango ya uwekezaji wa mfuko wa pesheni kwa watumishi wa umma 'PSPF' Bw, Gabriel Silayo katikati akiwa na baadhi ya maofisa wa PSPF wakati wa maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma
 Ofisa uhendeshaji wa mfuko wa pesheni kwa watumishi wa umma 'PSPF' Bw, Mohamed Masoud akimkaribisha Bi, Veronica Nyambajo wakati wa mahadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma yaliyomalizika jumatatu hii
 Ofisa uhendeshaji wa mfuko wa pesheni kwa watumishi wa umma 'PSPF' Bw, Mohamed Masoud aki muhakiki mteja Francisca Kwitende ambaye alitembelea banda hilo kwa ajili ya kupata mahelezo mbalimbali wakati wa mahadhimisho ya maadhimisho ya watumishi wa Umma
Afisa wa mfuko wa pesheni kwa watumishi wa umma Bi, Leila Laizer kulia akimpatia maelekezo Francisca Kwitende ambaye alitembelea banda hilo kwa ajili ya kupata mahelezo mbalimbali wakati wa mahadhimisho ya maadhimisho ya watumishi wa Umma.
BAADHI YA WANANCHI WALIOTEMBELEA BANDA LA PSPF WAKIPATIWA HUDUMA MBALIMBALI WAKATI WA  MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA.
Afisa uendeshaji wa mfuko wa pesheni kwa watumishi wa umma 'PSPF'  Bw,Hadji Jamadary kulia akitoa maelekezo mbalimbali jinsi ya kujiunga na mfuko huo

MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII,TASAF NA JITIHADA ZA KUPAMBANA NA UMASIKINI NCHINI.

$
0
0
Afisa kutoka TASAF makao makuu Bw. Geodfrey Nyamwihula akisisitiza jambo kwa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini katika shehia ya Bandamaji wilaya ya Kaskazini B Unguja wakati walengwa wa mpango huo walipopewa mafunzo ya namna ya kuibua miradi ya ujenzi PWP ambayo ni moja ya jitihada za serikali kupitia TASAF kuongeza pato la kaya husika .

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF umeanza zoezi la kuwashirikisha walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini kuibua miradi ya Ujenzi PWP ambayo kwa mujibu wa taratibu walengwa watatumia fursa ya kufanya kazi katika miradi watakayoibua kwenye maeneo yao na kisha kulipwa ujira ambao utasaidia kuwaongezea kipato.

Walengwa watafanya kazi hiyo kwa kipindi cha siku 15 katika mwezi na siku 60 kwa mwaka hususani wakati wa kipindi cha hari (kipindi kigumu).Chini ya utaratibu huo asilimia 75 ya fedha zitalipwa kwa walengwa na 25 zitatumika kununua vifaa vitakavyotumika kwenye mradi husika.
 Pichani walengwa wa PWP katika shehia ya Mpapa wakisikiliza maelezo kutoka kwa mwezeshaji (hayupo pichani) juu ya namna ya uibuaji wa miradi kwenye eneo lao.
  Afisa kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Ofisi ya Zanzibar,Bw. Abbas Salehe akitoa maelezo kwa walengwa wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini PSSN juu ya namna ya kuibua miradi ya PWP katika eneo la Shehia ya Mpapa wilaya ya Kati Unguja.
 Mmoja wa wawezeshaji wa Mpango wa kuwawezesha walengwa wa mpango wa PSSN katika kuibua miradi ya Ujenzi PWP katika shehia  ya Mpapa wilaya ya Kati Unguja akisikiliza maelezo kutoka kwa walengwa wa mpango huo.
 Hapa lazima ieleweke ndivyo anavyoelekea kusema Mwezeshaji wa PWP Rafii Fadhili Hasan alipotoa mafunzo kwa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini katika kuibua miradi ya ujenzi katika shehia ya Bandamaji wilaya ya Kaskazini B.
 Walengwa wa Mpango wa kunusuru Kaya masikini katika shehia ya Bandamaji wilaya ya Kaskazini B wakimsikiliza mwezashaji wa Mpango wa uibuaji wa miradi ya Ujenzi PWP ambayo ni moja ya jitihada za TASAF kuongeza kipato kwa walengwa ambao watapaswa kutumia nguvu kazi yao kuitekeleza miradi watakayoibua.
Baadhi ya walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya Masikini wakisikiliza maelezo ya utaratibu wa kuibua miradi ya Ujenzi PWP katika shehia ya Bandamaji ,Unguja , kutoka kwa mwezeshaji wa Mpango huo (hayupo pichani).
Mwezeshaji wa Mpango wa uibuaji miradi ya Ujenzi Issa Jabri akitoa maelezo ya namna ya kuibua miradi ya ujenzi PWP katika shehia ya Bandamaji wilaya ya Kaskazini B Unguja.

Mwezeshaji wa PWP katika shehia ya Kipange,huko Unguja Bi. Hidaya Mussa akitoa maelezo ya namna ya kuibua Miradi ya Ujenzi PWP kwa walengwa wa mpango huo .

BINTI SELITIAN NATA,MWENYE UVIMBE ANAOMBA MSAADA WA MATIBABU

$
0
0
Na John Gagarini, Bagamoyo.
 
MSICHANA Selitian Nata (25) mkazi wa Kijiji cha Kisogo kata ya Vigwaza Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani yuko kwenye hali mbaya ya kiafya baada ya kuvimba mguu na kuwa kwenye maumivu makali.Ugonjwa huo uvimbe huo ulianza kama kipele kidogo miaka zaidi ya 10  iliyopita lakini kadiri siku zilivyokuwa zikienda ndipo uvimbe huo ulizidi kuongezeka na kufikia usawa wa mbavu.
 
Akizungumza na waandishiw ahabari ambao walimtembelea nyumbani kwao alisema kuwa uvimbe huo una ambatana na maumivu makali pamoja na homa kali hasa nyakati za usiku.
 
“Niko kwenye wakati mgumu kama mnavyoniona napata shida naomba nisaidiwe kwani nimekwenda hospitali toka kipindi hicho lakini sikupata matibabu zaidi ya kupewa vidonge tu ambavyo hupunguza maumivu lakini uvimbe uko pale pale,” alisema Nata.
 
Nata ambaye ana mtoto mmoja wa kike mwenye umri wa miaka (2) alisema kuwa wakati tatizo hilo linaanza alikwenda hospitali mbalimbali lakini hakuweza kupatiwa matibabu sahihi na kupelekea uvimbe huo kuongezeka hadi hapo ulipofikia na kumkosesha raha.
 
“Naomba wataalamu mbalimbali pamoja na wafadhili ili niweze kupata matibabu sahihi ambayo yataondoa uvimbe huu ili name niweze kuishi kwa raha kama wengine,” alisema Nata.
 
Kwa upande wa baba yake Nata Mumbi alisema kuwa alimpeleka mwanae kwenye hospitali mbalimbali kwa ajili ya matibabu lakini hakuna mafanikio yoyote.“Tatizo matibabu ambayo wanayompa si ya kina jambo ambalo linasababisha mwanangu asipate nafuu, lakini kupitia vyombo vya habari naomba wasamaria wema wamsaidie mwanangu ili aweze kupata matibabu sahihi,” alisema Mumbi.
 
Aidha alisema kuwa anashangaa kuona kila anapokwenda hospitali mwanae anapewa vidonge tu jambo ambalo linafanya wakate tamaa ya kumpatia matibabu. 

Rais Kikwete apewa Tuzo Ya Uongozi Bora nchini

$
0
0
 Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali Bwana Ludovick Utouh akikmabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Tuzo maalum kwa kutambua mchango wange kwa taasisi simamizi katika kuimarisha Uwazi,Uadilifu na uwajibikaji wakati wa hafla maalum ya chakula cha jioni iliyofanyika katika ukumbi wa  wa kimataifa wa  mikutano Julius Nyerere(JNICC) jijini Dar es Salaam leo jioni.

Bwana Utouh alikabidhi Tuzo hiyo kwa niaba ya taasisi sita ambazo niBodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi,TAKUKURU,Mamlaka ya Udhibiti na Ununuzi wa Umma,Mamlaka ya udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya jamii,Mkaguzi wa ndani Mkuu wa Serikali,na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa umma (picha na Freddy Maro).

KATIBU MKUU KIONGOZI AELIMISHWA KUHUSU UTHAMINI MADINI YA ALMAS

$
0
0
   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akimsikiliza Mtaalamu wa madini ya Vito vya Rangi na Almas Bibi Teddy Goliama kutoka Kitengo cha Uthamini Madini ya Almas na Vito (TANSORT), Wizara ya Nishati na Madini, akimweleza namna Idara hiyo inavyofanya shughuli za Uthamini wa Madini ya Almas. Kushoto kwa Katibu Mkuu Kiongozi ni Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Bw. Eliakim Maswi na anayefuatia ni mmoja wa wateja waliofika bandani hapo.
 Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini  Bw. Eliakim Maswi  (kushoto)akimweleza jambo mgeni aliyefika katika Banda la Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) aliyetaka kufahamu kuhusu Mradi wa Umeme Vijijini unaosimamiwa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA). Wa pili kulia anayesikiliza na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava na katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikali Wizara ya Nishati na Madini Bibi Badra Masoud.

 Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake wakiwa katika picha ya pamoja baada ya TANESCO kupata kombe la Ushindi katika kipengele cha Taasisi iliyotoa huduma Bora na Ubunifu wakati wa Maonesho hayo.
Mhandisi Mwandamizi Masoko na Huduma kwa Wateja, Juliana Pallangyo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) akimweleza Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue namna mashine ya Umeme Tayari (UMETA) “Ready Board” inavyofanya kazi. Anaesikiliza ni Katibu Mkuu Bw. Eliakim Maswi wa pili kushoto kwa Katibu Mkuu Kiongozi na anayefuatia ni mgeni aliyefika banda la Wizara.


·        TANESCO  Yaibuka Mtoaji Huduma Bora na Ubunifu
·        Wizara yaingia 10 Bora
Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam

Katibu Mkuu Kiongozi,  Balozi Ombeni Sefue ametembelea banda la Wizara ya Nishati na Madini wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma na kupata fursa ya kusikiliza maelezo kutoka kwa wataalam wa Wizara kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wizara ya Nishati na Madini.

Akiwa katika banda la Wizara, Balozi Sefue ameelimishwa namna Kitengo cha Uthamini Madini ya Almas na Vito (TANSORT) kinavyofanya shughuli za Uthamini madini ya Almas na namna kitengo hicho kinavyopata bei za madini katika soko la Kimataifa na namna kinavyowasiliana na wachimbaji kuwafahamisha kuhusu bei hizo katika soko la Kimataifa.

Aidha, Katibu Mkuu Kiongozi amefahamishwa kuhusu namna mashine ya Umeme Tayari (UMETA) “Ready Board” inavyofanya kazi. Akitoa maelezo namna kifaa hicho kinavyofanya kazi, Mhandisi  Mwandamizi  Masoko na Huduma kwa Wateja, Juliana Pallangyo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ameeleza kuwa, kifaa hicho kinatumika katika maeneo yasiyohitaji ‘wiring’ hasa vijijini na kinatolewa bure vijijini.

Katika hatua nyingine, TANESCO limeibuka na ushindi wa kuwa miongoni  mwa taasisi tatu bora zinazotoa huduma kwa ubunifu katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, ambapo Wizara ya Nishati na Madini imekuwa miongoni mwa taasisi  10  zenye mabanda bora katika maonesho hayo yaliyofikia kilele leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. 

Akifunga rasmi maonesho hayo, mgeni rasmi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesisitiza watumishi wa umma kuwatumikia wananchi kwa uadilifu, ukarimu, upendo, weledi na kwa wakati. 
   

Serikali ya Ujerumani Yaahidi Kutoa Msaada wa Euro Milioni Moja Kusaidia uhifadhi wa pori la akiba selous

Airtel yazindua michuano ya ARS 2014

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Sunil Colaso akiongea wakati wa uzinduzi rasmi ya Airtel Rising Stars 2014 jijini Dar es Salaam jana.

Mkuuu wa Idara ya Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya akiongea wakati wa uzinduzi rasmi ya Airtel Rising Stars 2014 jijini Dar es Salaam jana.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Jamal Malinzi akiongea wakati wa uzinduzi wa Airtel Rising Stars 2014 jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Sunil Colaso.

 Dar es Salaam, Jumatatu Juni 23, 2014…Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imezindua rasmi msimu wa nne wa mashindano ya soka kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars ambayo yataanza kutimua vumbi Julai 7 katika ngazi ya awali na kuhitimishwa kwa fainali za Kitaifa jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 3 hadi 10 mwaka huu.

Akiongea na waandishi wa habari kwenye hafla ya uzinduzi jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Sunil Colaso amesema kampuni ya Airtel Tanzania  ina nia thabiti ya kusaidia maendeleo ya mchezo wa mpira wa miguu hapa nchini na kujivunia mafanikio yaliyotokana na michuano hiyo kwa miaka mitatu iliyopita.

 “Tunaona fahari kwamba michuano ya Airtel Rising Stars imeweza kuibua vipaji vya wachezaji ambao baadhi yao wamechaguliwa kujiunga na timu za taifa za vijana chini ya umri wa miaka 20”, alisema Colaso. Kumbu kumbu za TFF zinaonyesha kwamba timu ya taifa ya wanawake imeundwa na wachezaji wengi kutoka Airtel Rising Stars ambayo madhumuni yake makubwa ni kuibua na kuendeleza vipaji vya soka kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17.

Huu ni mwaka wa nne mfululizo kwa michuano ya Airtel Rising Stars kufanyika hapa nchini Tanzania ambayo huanzia ngazi ya chini hadi Taifa. Mashindano ya taifa hutoa wachezaji nyota ambao huenda kupeperusha bendera ya Taifa kwenye michuano ya kimataifa ambayo hujumuisha wachezaji nyota kutoka pande zote za Afrika ambako ARS hufanyika.

Mwaka jana, michuano ya Airtel Rising Stars ya kimataifa ilifanyika nchini Nigeria ambapo Niger iliibuka bingwa kwa upande wa wavulana na Tanzania kutwaa taji la ubingwa kwa timu za wasichana. Mwaka huu michuano ya ARS itajumuisha mikoa ya Mwanza, Morogoro, Mbeya, Temeke, Ilala na Kinonondoni kwa upande wa wavulana na wasichana watawakilishwa na mikoa ya Mwanza, Zanzibar, Mbeya, Temeke, Ilala na Kinondoni.

Colaso pia aliipongeza Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF) pamoja na serikali kupitia Wizara ya Michezo kwa kuungana mkono  kwa dhati michuano ya Airtel Rising Stars tangu ilipoanzishwa nchini mwaka 2011.

Kwa upande wake, Rais wa TFF Jamal Malinzi aliipongeza Airtel Tanzania kwa kuwekeza kwenye soka la vijana. “Nawapongeza sana kampuni ya Airtel Tanzania kwa mpango wake huu wa kuwekeza kwenye soka la vijana ambayo kwa kweli ndio msingi wa maendeleo wa mpira wa miguu hapa Tanzania na duniani kote”, alisema.

Airtel ni kampuni ya simu za mkononi yenye matawi barani Afrika katika nchi za Burkina Fasso, Chad, Congo, Brazzaville, DRC, Gabon, Ghana, Kenye, Madagascar, Malawi, Niger, Nigeria, Rwanda, Selisheli, Sierra-Leone, Tanzania, Uganda na Zambia.
   

BODI MPYA YA KITUO CHA UWEKEZAJI NCHINI (TIC) YAZINDULIWA JIJINI DAR

$
0
0
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza jambo na Mwenyekiti mpya wa bodi ya Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Prof. Lucian Msambichaka (wa pili kushoto) wakati alipozindua bodi mpya ya kituo hicho Jumatatu wiki hii jijini Dar es Salaam. Wengine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu (kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Bi. Juliet kairuki (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Bw. Raymond Mushi (kushoto). 



Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya wakurugenzi ya Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Jumatatu wiki hii jijini Dar es Salaam.  kushoto ni Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo,  Prof. Lucian Msambichaka; Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu (nguo nyekundu), Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Bw. Raymond Mushi (kulia katikati) na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dk. Florens Turuka (kulia). 

 Mwenyekiti mpya wa bodi ya Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Prof. Lucian Msambichaka (kulia) akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Bi. Juliet Kairuki (kushoto) pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu (katikati) wakati wa uzinduzi rasmi wa bodi mpya ya kituo hicho Jumatatu wiki hii jijini Dar es Salaam uliofanywa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

WASHINDI WA TMT KUTOKA KANDA YA ZIWA NA NYANDA ZA JUU KUSINI WAWASILI DAR ES SALAAM TAYARI KWA SAFARI YA KUSHINDANIA MILIONI 50

$
0
0
 Washindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) kutoka Kanda ya Ziwa wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwl Nyerere, Jijini Dar Es Salaam jana kwaajili ya Kuingia kambini tayari kwa safari ya kushindania Milioni 50 katika fainali itakayofanyika Mwishoni mwa Mwezi wa Nane
 Washindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) kanda ya Nyanda za Kusini, Stephen Mapunda(mwenye kofia nyekundu) na Mtawa Kaparata (mwenye fimbo) wakiwasili katika uwanja wa Ndege wa Mwl Nyerere jana tayari kwa safari ya kushindania Shilingi Milioni 50 za Kitanzania
 Washindi wa Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu Kusini wakibadilishana Mawazo wakati walipowasili katika uwanja wa Ndege wa Mwl Nyerere, Jijini Dar Es Salaam jana.
 Washindi wa Tanzania Movie Talents (TMT) wakielekea kwenye basi la TMT tayari kwa kupelekwa kwenye Hoteli kwaajili ya Kupumzika mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwl Nyerere, Jijini Dar Es Salaam.  Picha zote na Josephat Lukaza.

Washindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) kutoka kanda zote za Tanzania wamewasili jijini Dar Es Salaam jana kwaajili ya kuingia kambini tayari kwa Kuanza safari ya kushindania kitita cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania katika Fainali ya Shindano la TMT itakayofanyika Mwishoni mwa Mwezi wa Nane.
Fainali hiyo ya aina yake inayotarajiwa kutoa Mshindi mmoja mkubwa ambae ataondoka na Kitita cha Shilingi Milioni 50 ambapo washindi wengine tisa wakiungana na mshindi mmoja watacheza filamu ya pamoja ambayo itauzwa na kusambazwa na Kampuni ya Proin Promotions na washiriki hao kuweza kunufaika na Mauzo ya filamu hiyo.
Mara baada ya washindi 20 kutoka kanda zote sita wataingia Kambini mara baada ya kutoka kupima afya zao na hatimaye mchakato wa kumpata mshindi mmoja wa Shilingi Milioni 50 kuanza. Katika hatua hii ya kuanza kumtafuta mshindi wa milioni 50, Majaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) watakuwa wamepunguziwa majukumu kwa asilimia 40 na kazi hiyo kuelekea kwa wananchi ambapo watawapigia kura washiriki ambao wanawaona Wana vipaji na uwezo wa kuigiza.
Zoezi hilo la Upigaji kura litaanza mara moja mara baada ya washindi hao kuingia rasmi kambini na kuanza kupewa shule ya Sanaa na Walimu kutoka Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam na Chuo Cha Sanaa Bagamoyo.
Wananchi watawapigia Kura kwa Kutuma Ujumbe Mfupi wa Maneno.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images