Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live

Wastaafu Loan Yazinduliwa jijini Dar

0
0
Katibu Mkuu Kionmgozi (Mstaafu), Philemon Luhanjo (Wapili kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayigu(Wapili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, (TPB), Sabasaba Moshingi), Wakwanza kulia) na Mstaafu Eunice Temu, wakiwa wamenyanyua juu mikono kuashiria uzinduzi wa mpango wa mfuko huo kuwakopesha wastaafu amabao ni wanachama wake kupitia benki ya Posta "Wastaafu Loan",. Hafla ya uzinduzi huo ulifantyika jijini Dar es Salaam jana.
Katibu Mkuu Kiongozi (Mstaafu), Philemon Luhanjo, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo, akitoa hotuba yake. 
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akitoa hotuba kuelezea huduma hiyo mpya ya "Wastaafu Loan"
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi, akitoa hotuba yake.  
Katibu Mkuu Kiongozi (Mstaafu), Philemon Luhanjo (Kulia), akiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu (Kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, mara baada ya kumalizika kwa hafla ya uzinduzi wa huduma ya "Wastaafu Loan" jijini Dar es Salaam Juni 20, 2014.
Msanii Mrisho Mpoto naye alikuwepo.
Baadhi ya maafisa wa benki ya posta Tanzania (TPB) na wenzao wa PSPF, wakifuatilia magtukio yaliyokuwa yakitokea kwenye uzinduzi huo.
Mstaafu na Mwanachama wa PSPF, Eunice Temu, akitoa hotuba ya shukrani

Wizara ya Viwanda na Biashara ilivyoshiriki katika maonyesho ya Wiki ya Utuimshi wa Umma

0
0
Ofisa Mkuu wa Wakala wa Vipimo, Zainabu Kafungo akielezea jinsi baadhi ya wafanyabiashara wanavyoiba kupitia mizani wakati wa maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika Banda la Wizara ya Viwanda na Biashara.

 Maofisa wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Huzaina Mushin na Kamala Gombe, wakitoa Elimu kwa wageni waliotembelea banda la Wizara hiyo katika maonyesho ya  wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnaza Mmoja,Dar es Salaam
 Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Viwanda na Biashara, Mary Mwangisa akiongoza  watumishi wa Wizara yake kutoa huduma katika Banda la Wizara hiyo katika maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma
 Kaimu Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Nicodemus  Mushi akihojiwa na vyombo vya habari.

WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI WAPONGEZWA KWA KUOKOA MABILIONI

0
0
 Afisa Habari wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini nchini (TMAA), Mhandisi Yesambi Shiwa (Kulia) akitoa maelezo juu ya utendaji kazi wa TMAA kwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Hab Mkwizu (Kushoto) wakati alipotembelea kwenye Banda la TMAA wakati wa Maadhimisho ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
 Mashine ya kisasa ya kupimia ubora wa sampuli za madini ikioneshwa kwenye Banda la TMAA wakati wa Maadhimisho ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Hab Mkwizu (Kushoto) akizungumza na watumishi wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) alipowatembelea kwenye Banda lao. Wanaomsikiliza ni Afisa Habari, Mhandisi Yesambi Shiwa (Kulia) na Afisa Utumishi, Bibi Fatma Chondo (Katikati).
 Makaa ya mawe yakioneshwa kwenye Banda la TMAA wakati wa Maadhimisho ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya sampuli za madini yapatikanayo nchini yakioneshwa kwenye Banda la TMAA wakati wa Maadhimisho ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Hab Mkwizu (Kushoto) akihimiza kufanya kazi kwa uzalendo kwa watumishi wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) alipowatembelea kwenye Banda lao. Picha zote na:Saidi Mkabakuli  

Na Saidi Mkabakuli.

Serikali imeupongeza Wakala wa ukaguzi wa madini nchini (TMAA) kwa kufanikiwa kuokoa kiasi kikubwa cha madini yaliyokuwa yakitoroshwa kinyemela katika viwanja vya ndege nchini hivyo kuokoa zaidi ya bilioni 15 zilizolipwa kama mrahaba tangu ilipoanzisha ukaguzi maalum kwa wasafiri waendao nje ya nchi.

Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Hab Mkwizu alipokuwa akikagua utendaji kazi wa Wakala katika maonesho ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.  Bw. Mkwizu alisema kuwa kwa muda mrefu sasa wafanyabiashara wasio waaminifu wamekuwa wakiitia hasara Serikali kwa kukwepa ulipaji wa kodi wa madini yaendayo nje ya Tanzania kinyume na utaratibu uliowekwa.

“Hongereni sana kwa kuweza kuokoa kiasi kikubwa cha madini yaliyokuwa yakisafirishwa bila kufuata taratibu zetu za usafirishaji wa madini yaendayo nje ya Tanzania,” alisema Bw. Mkwizu. Naibu Katibu Mkuu Mkwizu aliwasihi viongozi na watumishi wa Wakala kuongeza uchapaji kazi na uzalendo ili kuweza kukomesha kabisa tabia ya wafanyabiashara hao wasio waaminifu.

Akikaribishwa kwenye banda la Wakala kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja na Afisa Habari wa Wakala hiyo, Mhandisi Yisambi Shiwa, Bw. Mkwizu alijulishwa kuwa moja kati ya mafanikio yaliyofikiwa na Wakala mara baada ya ukaguzi wa ziada kwa wasafiri waendao nje ya Tanzania, ni pamoja na kubainika mamia ya wafanyabiashara wa madini ambao wamekuwa wakitorosha kinyemela madini ya thamani kubwa ya fedha bila kufuata taratibu.

“Katika kuboresha utendaji kazi wa Wakala, tulitambulisha mpangokazi mpya wa ukaguzi wa ziada katika viwanja vyetu vya ndege vikubwa vya Dar es Salaam, Kilimanjaro na kile cha Mwanza lengo ni kubaini wafanyabiashara wasio waaminifu na ndipo tulipobaini wizi huu,” alisema Mhandisi Shiwa. Akizungumzia thamani ya madini hayo, Mhandisi Shiwa alisema kuwa kufuatia ukaguzi huu, mpaka sasa Wakala imeweza kuokoa madini yenye thamani ya zaidi ya shilingi za kitanzania bilioni 15. “Ukaguzi huu umesaidia kuokoa kiasi kikubwa cha madini yenye thamani ya shilingi bilioni 15.3 hadi kufikia mwaka na hivyo kuiongezea serikali yetu mapato ambayo yalikuwa yatoroshwe na wafanyabiashara hao wasio waaminifu,” aliongeza.

Kwa mujibu wa Mhandisi Shiwa, kiasi hiki cha fedha ni sehemu ya mrahaba wa kisheria unaostahili kuchangiwa na wafanyabiashara hao kwa umiliki wao wa madini hayo kabla ya kusafirisha nje ya nchi.
Mhandisi Shiwa aliongeza kuwa katika kuendelea kudhibiti tabia hizi, Wakala kwa kushirikiana na taasisi nyingine za serikali imekuwa ikishikilia na kutaifisha madini yanayotiliwa shaka ama kumilikiwa isivyo halali yanayopatikana katika viwanja hivyo.

Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania ni Wakala wa Serikali ulioanzishwa tarehe 2 Novemba, 2009 chini ya Sheria ya Wakala wa Serikali, Sura ya 245. Tamko la Waziri la kuanzisha Wakala lilichapishwa kwenye Gazeti la Serikali Namba 362 la tarehe 6 Novemba, 2009.

Lengo la Wakala ni kuhakikisha kwamba, Serikali inapata mapato stahiki kutoka kwenye shughuli za uzalishaji na biashara ya madini nchini kupitia usimamizi na ukaguzi makini wa shughuli za uchimbaji, na kuhakikisha kuwa shughuli hizo zinafanyika kwa kuzingatia uhifadhi na utunzaji thabiti wa mazingira katika maeneo ya migodi.

KAMANDA KOVA AZINDUA PIKIPIKI YA HERO DAWN 125 CC

0
0
  Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova (katikati), na  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya  Astarc Motors Tanzania Ltd, Sameer Musale (kushoto), akifungua kitmbaa kuashiria
uzinduzi wa pikipiki mpya aina ya Hero Dawn 125cc katika hafla yailiyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
  Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akijaribu moja ya pikipiki mpya aina ya Hero Dawn 125cc katika hafla ya uzinduzi wa pikipiki hiyo jijini Dar es Salaam jana. Wa tatu
kushoto ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya  Astarc Motors Tanzania Ltd, Sameer Musale na  wawakilishi kutoka Astarc.
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova (kulia), akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya  Astarc Motors Tanzania Ltd, Sameer Musale (kushoto) katka hafla hiyo.
  Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda ya Dar es Salaam Kamishna Msaidizi wa Polisi, Amiri Konja (kulia) akitoa rai kwa waendesha bodaboda kutii sheria za barabarani ili klupunguza ajali ambazo tawimu zinaonyesha kuongezeka. Kulia kwake ni  Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova (katikati), na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya  Astarc Motors Tanzania Ltd, Sameer Musale.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Roma Mkatoliki akitoa burudani katika hafla ua uzinduzi wa pikipiki aina ya Hero Dawn 125cc jijini Dar es Salaam jana.

Kampeni ya Uchangiaji damu iliyoendeshwa na Diwani wa Kipawa,Mh. Bonna Kaluwa yafikia tamati leo

0
0
Meya wa Ilala, Jerry Silaa akifungua rasmi tamasha la kuchangia damu katika viwanja vya Stakishari, Majumbasita, Dar es Salaam leo. Kampeni hiyo ya siku 10 iliratibiwa na Diwani wa Kipawa Bonnah Kaluwa (CCM).
Meya Silaa akipata maelezo kutoka kwa maofisa wa Damu Salama kabla ya kuchangia damu ili kuwaokoa wagonjwa wakiwemo wakina mama wajawazito katika viwanja vya Sitakishari Majumbasita, Dar es Salaam.
Meya Silaa na Diwani Bonnah wakiendelea kusikiliza maelezo kutoka kwa maofisa wa damu salama kabla ya kuchangia damu ili kuwaokoa wagonjwa wanaoteseka mahospitali kwa kukosa damu.
Meya wa Ilala, Jerry Silaa akiugulia maumivu ya sindano wakati akitoa damu ili kuwaokoa wagonjwa wanaohitaji damu katika hospitali mbalimbali wakiwemo wajawazito bila kuwasahau madereva na abiria wa bodaboda wanaoandamwa na ajali.
Diwani wa Kipawa, Bonnah Kaluwa naye akidhihirisha azma yake ya kuchangia damu kwa vitendo katika kilele cha kampeni yake ya kuchangia damu jana katika viwanja vya Sitakishari, Majumbasita ambapo mamia ya wakazi wa Dar es Salaam walijitokeza.
Mwakilishi wa Chuo cha Diplomasia, Kennedy Ndosi (katikati) aliyewahamasisha wanafunzi wa Chuo hicho waliofika kuchangia damu akiwasikiliza Meya Silaa na Diwani Bonnah wakati wa tamasha hilo.

DIAMOND PLATNUMZ ALIVYOWARUSHA WADAU NDANI YA YA JIJI LA BRUSSEL

0
0
 Diamond Platnumz akifanya mavituzz ukumbini na wacheza show wake wakiwa wanaendeleza manjonjo
 Waaaawwwoohh..ni umati haswaaa..kweli Diamond anapedwa
 Diamond Platnuz kijana mdogo mwenye mafanikio katika mziki na kimaisha akiimba wimbo wa nimpende nani
 V.I.P. table ilijumlishwa na viongozi mbalimbali,pichani ni mke wa Mh: wa Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi bwana Kamala aliyevalia nguo ya mizungo miyeusi na miyeupe
 Hapo sasa..Diamond Plutnumz akiendelea kukonga nyoyo za waliofika kumshughudia show yake
 Sema naeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee..!! warembo toka Tz wakishangilia show ya Diamond ikiendelea.
                                                              OOOooyoooooooooooh
 Ooooooiiihhh!!! Ni peace n' Love toka kwa watoto wa nyumbani
 Umati wa watu wakiendelea kupata burudani ya muziki toka kwa msanii Diamond Platnumz
Ngololo aai ngololo mama  ngololo...... and show me how they do ngololo ngololo ni Saidi Biboze na dada yake Zuhra Biboze wakijiachia kwa raha zao.
 (Picha zote na Maganga One Blogger)


 (Picha zote na Maganga One Blogger)

Profesa Mchome azindua ofisi za NACTE mikoani

0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akimkabidhi Edward  Mneda nyaraka za utendaji kazi kufuatia kuteuliwa kuwa Mkuu wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Kanda ya Kati. Kushoto ni Mkuu wa Kanda Msaidizi wa Kanda ya Ziwa Beatrice Mpanda. Baraza hilo limefungua ofisi katika kanda tano Dodoma, Arusha, Zanzibar, Mbeya na Mwanza kurahisisha utekelezaji wa majukumu yake.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akimkabidhi Rainey Mwinuka nyaraka za utendaji kazi kufuatia kuteuliwa kuwa Mkuu wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Kanda ya Ziwa. Katikati ni Katibu Mtendaji wa NACTE Dk. Primus Nkwera na kushoto ni Mkuu wa Kanda Msaidizi Beatrice Mpanda. Baraza hilo limefungua ofisi katika kanda tano Dodoma, Arusha, Zanzibar, Mbeya na Mwanza kurahisisha utekelezaji wa majukumu yake. 
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji mbalimbali wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) wakiwemo Wakuu Wapya wa Kanda Tano za Baraza hilo muda mfupi baada ya kuzindua rasmi kanda hizo jijini Dar es salaam. Wa tatu kushoto ni Katibu Mtendaji wa NACTE Dk. Primus Nkwera. Ofisi za kanda zilizozinduliwa ni Arusha (Kaskazini), Dodoma (Kati), Mwanza (Ziwa), Mbeya (Kusini) na Zanzibar
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome (kushoto) akibadilishana mawazo na mafias wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) wakati wa hafla ya uzinduzi wa ofisi tano za kanda za baraza hilo kwa lengo la kuharisisha utoaji huduma na usimamizi wa vyuo vya ufundi nchini. Kanda hizo ni Kaskazini (Arusha), Kati (Dodoma), Ziwa (Mwanza), Kusini (Mbeya) na Zanzibar

Mamlaka za Usafiri wa Anga zashiriki kikamilifu katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma

0
0
 Mwenye Koti jeusi katikati Mkurugenzi Mkuu wa Viwanja vya Ndege Nchini Suleiman S. Suleiman  akiangalia mfano wa jengo la Tatu (Termina III) ),alipotembelea banda la Taasisi yake wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika viwanja vya Mnazi Mmoja jana jijini Dar es Salaam. Jengo hilo linalojengwa katika eneo la Kipawa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) na linatarijiwa kutumiwa na Wasafiri wa Kigeni pindi litakapokamiilka.Mwenye kilemba kichwani ni Afisa Rasilimali Watu Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Bibi. Fatma Mtimba, anayemfuatia ni Meneja Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Bw. Mohamed Ally na anayeelezea mfano wa Jengo hilo ni Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta Bw. Geofrey Youze..
  Kushoto Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini Suleiman S. Suleiman akifurahia jambo na baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka hiyo alipotembelea Maonyesho ya Wiki wa Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa TAA Bw. Laurent Mwigune, Afisa Habari Mwandamizi Bi. Frida Nkondokaya na Afisa Sheria na Mahusiano Bi. Nuru Nyoni.

 Afisa Habari wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA) Bw. Ally Z. Changwila akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa mwananchi aliyetembelea banda la Taasisi yao wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

 Katikati Afisa Vibali wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA) Bw. Christopher Peter Sabuni akielezea program yaKusaidi Wanafunzi wanaosomea masomo ya Urubani inayotolewa na Taasisi hiyo, kulia ni Afisa Habari wa Mamlaka hiyo Bw. Ally Z. Changwila. TCAA mpaka sasa imekwisha saidi jumla ya wanafunzi watano walioenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya masomo ya Urubani na Uinjinia wa Ndege. Picha na Frank Shija, WHVUM


MAKAMU WA RAIS WA CHINA AWASILI NCHINI TANZANIA LEO JUMAPILI

0
0

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Li Yuanchao (kushoto) akiwa na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Gharib Bilal akikagua gwaride mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere leo 22 Juni, 2014. 
 Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Gharib Bilal (kushoto) akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Li Yuanchao (kulia) alipowasili leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere leo 22 Juni, 2014.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Li Yuanchao akipungia mkono viongozi pamoja na baadhi ya watu waliokuja kumpokea (hawako pichani) wakati akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere leo 22 Juni, 2014.

 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo akiwa pamoja na baadhi ya viongozi wengine wakati wa kumpokea Makamu wa Rais wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Li Yuanchao alipowasili leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere leo 22 Juni, 2014.

 Vikundi mbalimbali vya ngoma vikicheza mbele ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati alipowasili leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere leo 22 Juni, 2014.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.

========  ========  ======

MAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao, amewasili leo (Jumapili Juni 22, 2014)  nchini  kuanza ziara yake ya siku 5 ya Kiserikali hapa nchini.

Akiwa katika uwanja ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Mhe. Yuanchao amepokelewa na Mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mohammed Gharib Bilal na Viongozi mbalimbali wa Serikali.


Kwa Mujibu wa ratiba iliyotolewa leo Jumapili Juni 22, 2014 na Ofisi ya Intifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, katika siku yake ya pili ya ziara yake Jumatatu Juni 23, 2014, Mhe. Yuanchao anatarajia kukutana na Viongozi wa Serikali akiwemo Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Mkuu Mizengo Pinda Ikulu Jijini Dar Es Salaam.


Aidha mbali na kukutana na Viongozi hao, Mhe. Yuanchao akiwa na Mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mohammed Gharib Bilal pia anatarajia kufungua mkutano wa Jukwaa la Uwekezaji baina ya Tanzania na China katika  ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania.


Katika siku ya tatu ya ziara yake Jumanne (Juni 24, 2014), Mhe. Yuanchao, anatarajia kukutana na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM akiwemo Makamu Mwenyekiti, Bw, Philip Mangula katika hateli ya Serena na baadaye kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi Mpya za Ubalozi wa China hapa nchini.


Mhe. Yuanchao katika siku ya nne Jumatano (Juni, 25, 2014) ya Ziara yake anataraji kushiriki katika hafla ya ukataji utepe wa kuzinduliwa kwa vifaa vya kubebea mizigo mizito katika ofisi za Mamlaka ya Usafiri wa Reli wa Tanzania na Zambia (TAZARA) na baadae kusafiri na treni kutokea Kituo cha Tazara hadi Yombo akiongozana na Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Harrison Mwakyembe.


Aidha katika siku hiyo pia, Mhe. Yuanchao anatarajia kukutana na Wawekezaji kutoka China wanaofanya shughuli zao hapa nchini na baadaye kuelekea Zanzibar ambapo atakutana na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Madaktari kutoka China waliopo katika eneo la Vuga.


Aidha katika siku ya mwisho ya ziara yake hapa nchini Alhamisi (Juni 26, 2014), Mhe. Yuanchao akiwa Zanzibar anatajia kutembelea eneo la makumbusho la Stone Town na kujionea makumbusho mbalimbali ya kihistoria ikiwemo Soko la zamani la watumwa. Makamu huyo wa Rais kabla ya kumaliza ziara yake hapa nchini (Alhamisi Juni 26, 2014) anataraji kukabidhi gari la kurushia matangazo kwa Kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC) na baadaye jioni kupanda ndege kurejea nyumbani nchini China.

Na Ismail Ngayonga

MAELEZO

Dar es Salaam

22. Juni, 2014

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAGENI KUTOKA CHINA NA OMAN LEO

0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Dkt Anne Suk-Ching, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Chama Tawala cha Jamhuri ya Watu wa China baada ya kukutana naye  Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Dkt Anne Suk-Ching, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Chama Tawala cha Jamhuri ya Watu wa China aliyemtembelea  Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2014

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mhe Saoud Ali Mohamed Al Ruqaishi, Balozi wa Oman gapa nchini na Mjumbe Maalum wa Sultan Qaboos Bin Said wa Oman ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ujumbe kutoka kwa  Mhe Saoud Ali Mohamed Al Ruqaishi, Balozi wa Oman gapa nchini na Mjumbe Maalum wa Sultan Qaboos Bin Said wa Oman ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2014.picha na IKULU

NAPE: WASOMI CHANGIENI MAONI YENU KATIKA KUBORESHA SERA MBALI MBALI

0
0

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na wanachama wa CCM wa Tawi la STEMMUCO mkoani Mtwara wakati wa sherehe za kuwaaga wanachama wa CCM waliohitimu masomo yao katika Chuo cha SAUT ambapo aliwaambia wasomi washiriki katika kukisaidia chama hasa katika kuboresha sera mbali mbali.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara Ndugu Mohamed Sinani akizungumza wakati wa sherehe za kuwaaga wanachama wa CCM Tawi la STEMMUCO mkoani Mtwara ambao wamehitimu masomo katika Chuo cha SAUT ,Mwenyekiti aliwaeleza wanafunzi hao kuwa CCM ni chama pekee kinachoweza kuwavusha kutoka hapa walipo na kusonga mbele.
 Katibu wa CCM Mkoa wa Mtwara Ndugu Shaibu Akwilombe akizungumza wakati wa sherehe za kuwaaga wanachama wa CCM Tawi la STEMMUCO mkoani Mtwara ambao wamehitimu masomo katika Chuo cha SAUT ambapo alisisitiza wasomi kufanya tafiti zao kabla ya kuchagua chama gani cha siasa kinaweza kuwasaidia.

 Baadhi ya wanachama waliohitimu kutoka chuo cha SAUT wakifuatilia kwa makini hotuba kutoka kwa viongozi wao wakati wa sherehe za kuwaaga rasmi zilizofanyika kwenye ukumbi wa Pentecoste COCO Beach Mtwara
 Mwajuma Abas Nasombe na Zena Ibrahim wakiimba shairi maalum linalohusu CCM
 Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wakiimba nyimbo za hamasa.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akionyesha juu moja ya kadi za Chadema zilizorudishwa  kisha wanachama hao kujiunga na CCM

BONDIA KING CLASS MAWE AONESHA MKANDA WAKE WA WPBF KWA VIONGOZI WA NGUMI WA TPBC PAMOJA NA WADAU MBALIMBALI KWENYE MKUTANO

0
0

Mdau wa mchezo wa masumbwi nchini Ally Bakari 'Champion' kulia akimpongeza bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' ambaye ni bingwa wa Afrika anayetambuliwa na chama cha WPBF ambao aliupata ubingwa huo nchini Zambia hivi karibuni  katikati ni Bondia Kassimu Gamboo.

Mwenyekiti wa mda wa chama cha ngumi za kulipwa nchini TPBC Chaurembo Palasa akizungumza wakati wa kufungua mkutano kwa wadau wa mchezo wa ngumi uliofanyika jumapili katika ukumbi wa DDC Keko wengine kushoto ni Chuku Duso,Habibu Kinyogoli,Hamisi Kimanga na Buchato Michael picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com



















Mdau wa mchezo wa masumbwi nchini Ally Bakari 'Champion' kushoto akimpongeza bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' ambaye ni bingwa wa Afrika anayetambuliwa na chama cha WPBF ambao aliupata ubingwa huo nchini Zambia hivi karibuni  kulia ni Mwenyekiti wa TPBC Chaurembo Palasa  picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com.

Mjumbe Habibu Kinyogoli akizungumza wakati wa mkutano huo
wajumbe mblalimbali wakifatilia mkutano huo leo kutoka kushoto ni Aga Peter,Maneno Osward na Ernest Bujiku
Rais wa PST Emanuel Mlundwa akichangia moja ya mada za mkutano huo 
 Mjumbe Ally Bakari akichangia wakati wa mkutano huo




Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ' Super D' aliyekaa kulia akiwa na mabondia mbalimbali wakati wa mkutano mkuu wa TPBC

VIONGOZI WAKIPITIA MAKABRASHA MBALIMBALI
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' katikati akiwa na ubingwa wake wa chama cha WPBF Africa alioupata hivi karibuni nchini Zambia wengine kushoto ni Habibu Kinyogoli,Hamisi Kimanga,Chaurembo Palasa na Michael Buchato picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com



Mahojiano ya Kwanza Production na Haika Lawere. Mkurugenzi wa Mbezi Garden Hotel

0
0
Haika Lawere akizungumza na wanawake kwenye tukio la wanawake waTanzania Washington DC
Photo Credits: IskaJojo Studios 
Karibu katika mahojiano kati ya Kwanza Production na Haika Lawere.
Yeye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mbezi Garden Hotel ya Dar Es Salaam Tanzania.

Amezungumzia mengi kuhusu maisha yake, kazi yake, changamoto anazokumbana nazo katika kazi, ziaa yake hapa Marekani na hata ushauri wake kwa wasikilizaji.Amezungumza mengi mema
Karibu uungane nasi

Kwa maoni ama ushauri usisite kuwasiliana nasi kupitia kwanzaproduction at gmail dot com

NEHEMIA MCHECHU ATEULIWA KUWA MWENYEKITI MPYA WA BODI YA SERENGETI BREWERIES LTD (SBL).

0
0
Kampuni ya Serengeti Breweries Limited ( SBL ) leo inatangaza uteuzi wa Ndugu Nehemia Mchechu kama Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi ya SBL

Uteuzi wa Ndugu Mchechu unafuata ukamilisho wa umiliki wa Mhe. Jaji (mstaafu) Mark Bomani . Katika nafasi yake mpya , Bw Mchechu pia atakukwa memba wa bodi ya  kampuni ya bia ya East Africa.
Ndugu,Nehemia Mchechu kwa sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Nyumba la Taifa ( NHC) . Bw. Mchechu anauzoefu mkubwa katika masuala ya fedha na usimamizi. Hapo awali alishika  nafasi muhimu katika sekta ya benki , hasa kama Mkuu wa Masoko Kimataifa na mkurugenzi msaidizi benki ya Standard Chartered, na  kuwa Mkurugenzi Mtendaji  benki ya  Commercial Bank of Africa Tanzania (CBA) .
Bwa.Mchechu ana Shahada ya Biashara (Fedha) na Utawala ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Yeye pia ni Rais wa Umoja wa wanafunzi waliomaliza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kitivo cha Biashara na mwanachama wa ACI – Financial Market Association Tanzania.
Miongoni mwa nafasi nyingine muhimu, Bwa.Mchechu pia ni Mkurugenzi na mwanachama wa CEORT na  pia ni Mkurugenzii wa TIC.
SBL inachukua fursa hii kumkaribisha na kumpongeza Mwenyekiti wake mpya wa bodi na kuwashukuru mwenyekiti wa bodi Mheshimiwa Bomani kwa mchango wake bora na wa kipekee wakati wa uongozi wake.

TAARIFA YA MBUNGE WA JIMBO LA UBUNGO (CHADEMA),JOHN MNYIKA KWA DAWASA NA DAWASCO

0
0
Katika kutekeleza kazi ya mbunge ya kuisimamia Serikali itakumbukwa kwamba tarehe 12 Mei 2014 nilichukua hatua bungeni ya kutaka Serikali kutatua kwa dharura matatizo katika mtambo wa maji wa Ruvu Juu yenye kukosesha maji kwa wananchi wa Mkoa wa Dar Es Salaam na Pwani.

Nilitaka kwa mujibu wa Kanuni ya 49 ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la mwaka 2013, Waziri wa Maji Prof Jumanne Maghembe atoe kauli bungeni juu ya matatizo ya maji katika maeneo yanayohudumiwa na mabomba kutoka katika mtambo kwa kuweka bayana iwapo kuna hujuma na kurejesha kwa haraka huduma kwa wananchi.


Kufuatia hatua hiyo hali ya upatikanaji wa maji iliongezeka katika maeneo machache ndani ya siku chache lakini kwa sasa katika maeneo mengi yanayohudumiwa na mabomba kutoka katika mtambo wa Ruvu Juu katika kata za Kwembe, Kibamba, Mbezi Lois, Msigani, Kimara, Saranga, Ubungo na Makuburi matatizo ya maji yamejirudia.


Katika kuendelea kutekeleza wajibu wa kibunge wa kuishauri na kuisimamia Serikali natoa mwito wa wazi kwa wenyeviti wa bodi za Wakurugenzi na Maafisa Watendaji Wakuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka  Dar Es Salaam (DAWASA) na Kampuni ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASCO) ndani ya siku tatu kusimamia kazi ya dharura kuhusu matatizo ya mtambo wa maji wa Ruvu Juu yanayoendelea mpaka hivi sasa.


Aidha, ndani ya siku hizo tatu wajitokeze mbele ya vyombo vya habari kutoa maelezo kwa umma kueleza kwanini mpaka sasa huduma ya maji katika maeneo mengi katika Jimbo la Ubungo na Jiji la Dar Es Salaam  kwa ujumla yanayohudumiwa na mabomba yanayotoka katika mtambo wa Ruvu Juu hayapati huduma ya maji inavyostahili na lini matatizo yaliyopo yatapatiwa ufumbuzi.


Kwa upande mwingine, ndani ya muda huo huo wa siku tatu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji ajitokeze mbele ya vyombo vya habari na kueleza umma matokeo ya uchunguzi uliopaswa kufanyika ndani ya mwezi mmoja kubaini kama matatizo ya mara kwa mara ya Mtambo wa maji wa Ruvu Juu yanatokana na masuala ya kiufundi, kiuendeshaji  au makosa mengine ya kibinadamu.


DAWASA, DAWASCO na Wizara ya Maji wasipojitokeza ndani ya siku tatu mbele ya vyombo vya habari kutoa maelezo kwa umma nitachukua hatua za kibunge nitakazoona zinafaa dhidi ya Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe kwa kulidanganya Bunge kupitia kauli ya Serikali aliyotoa Bungeni mwezi Mei 2014.


Ikumbukwe kwamba tarehe 12 Mei 2014 ikiwa ni sehemu ya kutimiza wajibu wa mbunge wa kuwawakilisha wananchi nilieleza Bunge kwamba matatizo katika mtambo wa Ruvu Juu yamekuwa yakijirudiarudia kwa nyakati mbalimbali kwa kipindi cha takribani miezi mitatu kati ya Januari mpaka Mei 2014 katika maeneo ambayo awali yalikuwa yakipata mgawo wa maji.


Nilichukua hatua hiyo kwa niaba ya wananchi  wanaohudumiwa na mtambo huo katika kata za Kwembe, Kibamba, Mbezi Lois, Msigani, Kimara, Saranga, Ubungo na Makuburi  kwenye Jimbo la Ubungo; na kata mbalimbali za majimbo ya Kibaha Mjini, Kibaha Vijijini, Segerea nk.


Kufuatia hatua hiyo, Mwezi Mei 2014 Waziri wa Maji Prof. Maghembe alitoa kauli ya Serikali ya kueleza matatizo yanayoukabili mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu Juu kwa ajili ya Jiji la Dar es salaam na maeneo ya DAWASA katika mkoa wa Pwani.

Katika kauli yake Waziri Maghembe alikiri kwamba kwa takribani siku 67 (kati ya tarehe 01.03.2014 na tarehe 06.05.2014) mtambo ulizalisha maji chini ya kiwango na kufikia kati ya lita milioni 8.2 na lita milioni 57.4 ikilinganishwa na lita milioni 82 kwa siku, ambazo ndio uwezo halisi wa mtambo huo.


Katika kauli yake bungeni, Waziri Maghembe aliorodhesha matatizo ya mtambo wa Ruvu Juu kuwa ni: Kuharibika kwa pampu mara kwa mara kunakosababishwa na uchakavu  unaosababishwa na umri kua mkubwa miaka (60), kukatika kwa Umeme mara kwa mara, maji kuwa na tope jingi sana (turbidity) wakati wa mvua na mafuriko hali inayopunguza uwezo wa pampu za kusukuma maji na husababisha kusagika kwa vifaa vya pampu na ugumu wa upatikanaji wa vipuri halisi (genuine parts). Hata hivyo, Waziri Maghembe hakukiri wala kukanusha juu ya madai ya kuwepo kwa udhaifu, uzembe, ufisadi na hujuma katika mitambo ya vyanzo vya maji na mitandao ya mabomba ya maji.

Waziri Maghembe alieleza Bunge kwamba Wizara imechukua hatua za kutatua matatizo yaiyopo kwa kuchonga vipuri na vifaa vya pampu katika karakana zilizopo hapa nchini kwa kuwatumia wataalamu wa jeshi, kuagiza vipuri nje ya nchi na kutoa matangazo kwa wananchi kuhusu upungufu wa maji pale uzalishaji unapopungua/kusimama.


Waziri Maghembe alilieleza bunge kwamba baada ya hatua hizo uzalishaji wa Maji wa Mtambo wa Ruvu Juu unaendelea kurudi katika hali yake ya kawaida na kutoa mfano wa kwamba tarehe 17 Mei, 2014 uzalishaji wa maji ulikua lita milioni 80.3 kwa siku. Aidha, Waziri Maghembe alitoa kauli Bungeni kwamba Wizara ya Maji imeunda Kamati Maalum ambayo imeanza kufanya tathmini ya kina juu ya chanzo cha matatizo ya mara kwa mara katika mtambo wa kusafisha maji wa Ruvu Juu.

Waziri Maghembe alieleza kwamba kamati hiyo itafanya uchunguzi kubaini kama matatizo hayo yanatokana na masuala ya kiufundi, kiuendeshaji au makosa ya binadamu na kuahidi kwamba kamati itatoa taarifa yake katika kipindi cha mwezi mmoja. Mwezi mmoja umepita tangu nilipohoji bungeni tarehe 12 Mei 2014, hivyo ni wakati muafaka kwa mamlaka zote zinazohusika kuweza kutoa mrejesho juu ya uchunguzi huo na hatua nyingine za haraka za kuboresha upatikanaji wa maji safi kama nilivyozieleza katika hoja binafsi niliyoiwasilisha bungeni kwa niaba ya wananchi tarehe 4 Februari 2013.
Wenu katika uwakilishi wa wananchi,

John Mnyika (Mb)

TAARIFA TOKA MAMLAKA YA HALI YA HEWA: MWELEKEO WA HALI YA JOTO NA MVUA KATIKA KIPINDI CHA JUNI HADI AGOSTI 2014

0
0

WAZIRI MEMBE AZINDUA FILAMU MPYA YA 'I LOVE MWANZA' JIJINI MWANZA

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (wa pili kushoto), akisadiwa na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba, kukata utepe kuzindua filamu mpya iitwayo ‘I Love Mwanza’ iliyoandaliwa na Lake Zone Youth Empowerment Foundation kwa kushirikiana na Tropical Media Tanzania Ltd, katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza Jumamosi usiku. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (wa watatu kushoto), na Mwenyekiti wa Chama cha Sanaa za Maonyesho na Waigizaji Tanzania (TDFAA), Mkoani Mwanza, Anitha Kagemulo. PICHA ZOTE/ JOHN BADI WA Daily Mitikasi Blog
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (wa pili kushoto), akionyesha CD ya filamu mpya iitwayo ‘I Love Mwanza’, iliyoandaliwa na Lake Zone Youth Empowerment Foundation kwa kushirikiana na Tropical Media Tanzania Ltd, baada ya kuizindua katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza Jumamosi usiku. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (wa watatu kushoto), Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba (kushoto), na Mwenyekiti wa Chama cha Sanaa za Maonyesho na Waigizaji Tanzania (TDFAA), Mkoani Mwanza, Anitha Kagemulo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (kushoto), akinunua CD ya filamu mpya iitwayo ‘I Love Mwanza’, iliyoandaliwa na Lake Zone Youth Empowerment Foundation kwa kushirikiana na Tropical Media Tanzania Ltd, baada ya kuizindua katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza Jumamosi usiku. Waziri Membe aliwezesha filamu hiyo kununuliwa na wadau kwa zaidi ya Milioni 50/- katika hafla hiyo. Kulia ni Msanii wa Bongo Movies, Blandina Chagula ‘Johari’.

Broo Msaada BAGAMOYO HISTORICAL MARATHON 2014 YAWA KIVUTIO

0
0
 Wakimbiaji wakitimua vumbi katika mashindano ya Bagamoyo Historical Marathon, mjini Bagamoyo, Pwani  jana. Mashindano hayo yaliandaliwa na Kampuni ya 4Beli.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Juliana Yassoda (katikati) akihutubia wakati akifungunga mashindano ya Bagamoyo Marathon mjini Bagamoyo jana.
 
Washiriki wa Bagamoyo  Marathon 2014  mara baada ya kumaliza mbio hizo ambazo kwa wanariadha wengine walikuwa bado wanawasili.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Juliana Yassoda (katikati) akimpongeza mshindi wa mbio za kilomita 21 wanaume, Ismail Juma. Wengine ni baadhi ya washindi na viongozi wa Kampuni ya 4Beli iliyoratibu mashindano hayo ya Bagamoyo Marathon 2014. Chanzo : Matukio tz
 Mwakilishi wa Kampuni ya 4Beli akitoa zawadi kwa mmoja wa washiriki wa mashindano.
 Mwakilishi kutoka Benki ya Posta Tanzania (TPB) ambao walikuwa mmoja wa walidhamini wa mashindano hayo akitoa zawadi kwa washindi.Chanzo : Matukio tz
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Juliana Yassoda Akikabidhi Zawadi kwa Mshindi
Mwenyekiti wa zamani wa Baraza la Michezo la Taifa  Kanali mstaafu  Idd Kipingu akimpongeza Mshindi wa Bagamoyo
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Juliana Yassoda
Picha ya Pamoja ya Washiriki   Kutoka Kushoto Eligi Albert,Evance Mosha na Thomas Karia Mara baada ya Kumaliza Mbio za KM 10.Chanzo : Matukio tz

Production of gold at the Buckreef Gold Mine in Geita Region

0
0
Ndunguru 3
Acting (STAMICO) Managing Director Engineer Edwin Ngonyani Left and Director Of Finance and Corporate Affairs Mr Peter Gembe.
........................................................................................
By STAFF REPORTER

PRODUCTION of gold at the Buckreef Gold Mine in Geita Region in which the State Mining Corporation (Stamico) has 45 per cent stake is expected to kick-start in November this year, it has been learned. Stamico signed an agreement for development of the project in the year 2011 with Tanzania American International Development Corporation Limited (TANZAM 2000), a subsidiary of Canada's Tanzania Royalty Exploration Corporation. Tanzam 2000 is the majority shareholder with 55 per cent stake.

The gold mine has 2.4 million ounces of the precious mineral and exploration is still ongoing as the project has 19 prospecting licences at the area, according to Stamico's Drilling Manager Alex Rutagwelela. "We have already conducted the environmental and social impact assessment (ESIA) and has been sent to the National Environment Management Council (NEMC) for approval," Mr Rutagwelela noted.

This was revealed during a news conference held in Dar es Salaam on Wednesday presided by the newly appointed Acting Managing Director of Stamico Eng. Edwin Ngonyani. During the occasion, Eng. Ngonyani revealed on the other hand that Stamico expects to make a net profit of 7bn/- during the next two and half years from Biharamulo Gold Mine, formerly known as Tulawaka, which it acquired from African Barrick Gold (ABG), last year.
The medium-scale mine under the new management is expected to start production by August, this year. It will be managed by StamiGold, a subsidiary of Stamico.

There are proved deposits of 100,000 ounces of gold at the mine but prospects are higher for more discoveries, according to the Acting Stamico boss. “We will continue drilling in the area and surrounding areas in a distance of about four kilometres. Hopes are high that there could be between 150,000 and 200,000 ounces of the precious mineral,” Eng. Ngonyani explained.


Stamico acquired the mine in November, last year at 5 million US dollars (about 8bn/-) after ABG closed it in March 2013 citing high operation costs. The corporation is using the 11.6 million US dollars (about 18.56bn/-) rehabilitation fund it received from ABG for the closure of the mine, as part of capital to operate at the Biharamulo Gold Mine.

Eng. Ngonyani, who assumed the position on June 1, this year, said he is focused to turn around the corporation to ensure it generates money for the treasury coffers and on the other hand enable artisanal miners to employ advanced technology in their operations.“My focus is to turn around the corporation in shortest time possible, possibly within the next two or three years and start making contributions to the treasury and shun dependence on the state for funds,” he explained.

On the other hand, the Stamico boss said the exactly value of Kiwira Coal Mine will be known in one-month time as a time of experts has been sent there to assess projects ahead of envisaged investment. The coal mine has the capacity to generate 6MW of electricity but the intention is to boost power generation to 200MW to be injected to the national grid through a 100- km power transmission line.

Stamico’s Director of Finance and Administration Peter Gembe said Kiwira’s underground mine would be expanded to double its capacity to 300,000 tonnes from the current 150,000 tonnes of coal to be used in generating power. “There will be also an open cast mine that will be constructed with a capacity to produce 1.5 million tonnes of coal. Producing 200MW of power electricity requires this amount of coal,” Mr Gembe said.

The director hinted that several investors have expressed interests in the project, which was repossessed from Tanpower Resources last year, but stressed new investors will be picked through a competitive and transparent manner.Mr Gembe explained further that it is only after a technical report on financial requirements of the mine which has remained idle for some years that major decisions would be made.

Mama Maria Nyerere awaasa Wanawake Wajasiliamali kujiamini

0
0
 Mama Maria Nyerere akitoa nasaa wakati wa Ufunguzi wa Semina kwa Wanawake Wajasiliamali kutoka Mikoa yote ya Tanzania, akiwa ni Mwanamke Mjasiliamali pia, amewahakikishia wanawake mafanikio iwapo watajiamini na kumsirikisha Mungu katika kazi zao.
 Mwenyekiti wa EOTF Mama Anna Mkapa, akitoa utangulizi wa Mafunzo na ntambulisho wa Waalikwa, wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya siku tatu kwa Wanawake Wajasiliamali, kuanzia Juni 23-25/2014, kuanzia saa2  asubuhi  katika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mgulani jijini Dares Salaam.Picha na Maelezo. 
 Mkurugenzi  Mtendaji wa Mfuko wa Fursa Sawa Kwa Wote(EOTF), Ndugu, Stephen Emmanuel akimkaribisha Mwenyekiti wa EOTF, Mama Anna Mkapa (hayuko pichani) leo, tarehe 23/06/2014 wakati wa Ufunguzi wa Semina kwa Wanawake Wajasiliamali kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar. Mafunzo hayo yanalenga kumsaidia Mwanamke kukabiliana na changamoto za Ujasiliamali.
 
Wanawake kutoka Mikoa Mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar wakiwa katika Ufunguzi wa Semina ya Mafunzo ya Wajasilaimali, Mafunzo ni ya muda wa siku tatu kuanzia Juni 23-25/2014, kuanzia saa2  asubuhi  katika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mgulani jijini Dares Salaam.



Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa IPP, Dkt. Reginald Mengi (aliayevaa Suti) akiwasili katika Ufunguzi wa Semina ya Mafunzo kwa Wanawake Wajasiliamali, Mbele ya Msafara ni Mama Maria Nyerere na Mwenyekiti wa EOTF Mama Anna Mkapa. Semina kwa Wajasiliamali imeandaliwa na Mfuko wa Fursa Sawa Kwa wote(EOTF), Mafunzo ni ya muda wa siku tatu kuanzia Juni 23-25/2014, kuanzia saa2  asubuhi  katika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mgulani jijini Dares Salaam
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live




Latest Images