Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live

ALIYEKUWA NA SAKATA LA NYOKA AINA YA CHATU JIJIINI ARUSHA,AWEKA MAMBO HADHARANI,ADAI NI MPANGO ULIOSUKWA KUMCHAFUA

$
0
0
 Pichani ni Bw.Joseph Magessa aliyetuhumiwa hivi karibuni na tukio la Nyoka aina ya Chatu.
 
SAKATA la kukutwa na chatu  eneo la sakina katika nyumba ya Joseph Magessa limechukua sura mpya baada ya  mhusika kuhojiwa na mtandao wa jamiiblog huu kuhusiana na tukio hilo.
 
Aidha chatu huyo ambaye alikutwa  nyumbani kwa mmiliki huyo hivi karibuni imeelezwa tuhuma hizo sio za kweli bali ni njama za kumuharibia tu na tukio hilo ni la kutengenezwa na watu kwa lengo la kumchafulia jina lake.
 
Magessa alisema kuwa ,ameshangazwa sana na tukio hilo kwani lilipotokea alikuwa safarini yeye na mke wake , ndipo alipopigiwa simu kuhusiana na tukio hilo na kuwataarifu  huyo chatu auawe.
.
Pia, amedai kuwa hizo zinaweza kuwa njama za watu  zilizolenga kumchafua na kwamba, suala hilo amemwachia Mungu kwani ndiye ajuaye ukweli.

Aliongeza kuwa, yeye hajawahi kuwa mshirikina wala mke wake bali wanachojua wao ni kuwa wanamtumikia Mungu na yeye pekee ndiye ajuaye kila jambo na kuwa mambo yote hayo yaliyotokea amemwachia Mungu ndiye atakayejibu.

Magessa alifafanua kuwa, ameshangazwa sana na taarifa mbalimbali ambazo zimekuwa zikizushwa kwenye vyombo vya habari pamoja na mitandao juu ya tukio hilo ila yeye amenyamaza kimya na amemwachia Mungu kwani ndiye ajuaye kila kitu.

KUHUSU KUTENGWA KWAKE  KANISANI .

Aidha akizungumzia kuhusiana na swala la kutengwa kwake na Kanisa katoliki alisema kuwa huo ni uongo na uzushi hakuna kitu kama hicho kwani wanamwelewa vizuri sana tabia yake na kuwa hana tabia ya ushirikina.

‘Tena waumini wa kanisa katoliki watakuja kufanya jumuiya nyumbani kwangu na tayari kuna masalaba pale kama kweli ningekuwa nimefanya hivyo leo hii wangefuata nini hapa kanisani’alisema Magessa.

 Naye mkewe Selina Magessa , akizungumza na jamiiblog kuhusiana na tukio hilo alisema kuwa.tangu ameanza kuishi na mumewe miaka mingi hadi sasa hivi ,hajawahi kusikia wala kuona
vitendo vya ushirikina.

“Niko na mume wangu miaka mingi, sijawahi kusikia kuwa anafuga nyoka ndani wala sijafiwa na mtoto yeyote, wote watatu wapo ila nashangaa kusikia kauli kwamba mume wangu aliagiza nyoka asiuawe kwa kuwa ni mtoto wake ama mama yake mzazi,” alisema Selina.

Alisema kuwa , kwa sasa hivi ni muda wao kupumzika na kutafakari mambo yao sio wakati wa kuzungumzia swala hilo tena kwani wamechishwa na maneno kila mahali ili wanachofanya ni kumwachia mungu pekee ndiye ajuaye.

Hata hivyo ,Magessa anapenda kuwaelezea watanzania kwamba huyo chatu sio wa kweli ni wa kurushwa kwenye fensi yake ili amchafulie  kwani chatu wa ukweli asingeweza kuburuzwa hadi kanisani kwani kila mtu anamwelewa mnyama huyo jinsi alivyo mkali ,kwa hiyo hizo ni njama tu za kuharibiana kwenye maisha .


Hivyo alisema kuwa, kusisitiza kuwa anaombwa watanzania wamwelewe kwani chatu wa ukweli wanafahamika.

ATOA RAI KWA VYOMBO VYA HABARI.

Aidha alivitaka vyombo hivyo kuelimisha jamii badala ya kupotosha ukweli wa jambo kama ambavyo sakata hilo limezua sura tofauti kwa watanzania .

‘mnajua nyie ndio vyombo tunavyovitegemea kwa jamii ,sasa mkiandika vitu ambavyo hamna uhakika navyo mnategemea italeta picha gani kwa jamii ya watanzania ‘alisema Magessa.(CHANZO Pamela Mollel jamiiblog)

SEMINA YA MAKATIBU WA MIKOA NA MAKATIBU WASAIDIZI WA TUICO YAFANYIKA MJNI MOROGORO.

$
0
0
 Katibu wa TUICO mkoa wa Pwani Kassim Matewele akitoa hoja katika semina ya makatibu wa mikoa na makatibu wasaidizi wa tuico mkoani morogoro.
 Nyuso za furaha, baadhi ya makatibu wasaidizi wa TUICO wakiwa katika semina hiyo.
 Katibu wa TUICO kanda ya kaskazini Hussen Ngowi akitoa hoja katika semina hiyo.
 Baadhi ya makatibu wasaidizi wa TUICO wakiwa katika semina inayofanyika katika hotel ya New Savoy mjini Morogoro.
Makatibu wakuu wa mikoa na wasaidizi wa TUICO wakiwa katika picha ya pamoja katika semina inayofanyika katika ukumbi wa New Savoy Hotel mjini Morogoro. (Picha zote na Denis Mlowe)

Sabasaba 2014 kuunganisha Uzalishaji na Masoko

$
0
0
Na Johary Kachwamba- MAELEZO.

Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam (38th DITF) yanatarajia kuanza tarehe  28 mwezi huu na kufikia kilele chake tarehe 8 Julai  2014 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya kilwa, jijini Dar-es-salaam.

Akitoa taarifa hiyo leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bibi. Jacqueline Mneney Maleko imeeleza kuwa maonesho  ya  mwaka huu yataongozwa na kauli mbiu isemayo “Tunaunganisha Uzalishaji na Masoko”

Amesema kuwa Kauli Mbiu hiyo imechaguliwa kutumika kuonesha uhusiano uliopo kati ya Uzalishaji na Masoko  na umuhimu wa mnyororo wa uzalishaji ambao ndio chimbuko la upatikanaji wa Bidhaa bora zenye ushindani katika soko. 

Bibi. Maleko amesema kuwa mwaka huu TanTrade imetenga eneo kubwa zaidi kwa ajili ya Wazalishaji wa ndani ya nchi na kubainisha maeneo yatakayotumiwa na wazalishaji hao kuwa ni jengo namba C.19 na eneo la wazi lililo nyuma ya ofisi za Mkurugenzi wa Utafiti, Mipango na Uwezeshaji kwa ajili ya bidhaa za kilimo na bidhaa zinazotengenezwa Tanzania.

Kuhusu ushiriki wa mataifa mengine katika maonesho hayo amefafanua kuwa tayari nchi 31 zimethibitisha kushiriki maonesho hayo zikiwemo Afrika Kusini,Czech Republic, China, Ghana, Indonesia, India, Iran, Finland, Ugiriki, Italia, Japan, Jordan, Kenya, Korea ya Kusini, Malaysia, Marekani, Misri, na Ujerumani.

Nchi zingine ni pamoja na Nigeria, Pakstani, Rwanda, Saudi Arabia, Singapore, Sudani, Syria, Uganda, Uingereza, Burundi, Sweden, Vietnam na Zimbabwe.

Aidha, amefafanua kuwa makampuni ya nje 490 yamethibitisha kushiriki katika maonesho hayo huku  Wizara na Taasisi za Serikali zilizothibitisha kushiriki maonesho hayo zikifikia 61. 

Kwa upande wa Mikoa amesema tayari mikoa 10 imethibitisha kushiriki ikiwemo, Mikoa ya Iringa, Ruvuma, Mbeya, Pwani, Kigoma, Kagera, Geita, Mara, Manyara na Ruvuma. Jumla ya Washiriki waliothibitisha kushiriki kutoka ndani ya nchi ni 1700.

Kuhusu  kiingilio wakati wa maonesho hayo amesema watu wazima walipia Shilingi 2,500 na watoto ni 500 kila siku kwa siku zote za maonesho isipokuwa tarehe 7 Julai,2014 ambapo ada itakuwa Shs. 3,000/= kwa watu wazima  na watoto ni Shs.1000/=

MARA BAADA YA SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) KUMALIZIKA KANDA YA PWANI, WATANZANIA SASA KUANZA KUWAPIGIA KURA WASHINDI

$
0
0
Na Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited - Dar es Salaam.

Safari ya Kutafuta vipaji katika Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) ilianzia Kanda ya Ziwa Mkoani Mwanza ambapo timu nzima ya TMT ilikuwa katika kanda hiyo kwaajili ya kusaka vipaji kupitia shindano hilo kubwa na la kwanza kufanyika Afrika Mashariki na Kati. 

Shindano la Tanzania Movie Talents ni shindano ambalo lilizunguka kanda zote sita za Tanzania na hatimaye kilele chake kilimalizika mnamo tarehe 18 Juni 2014 katika Ukumbi  wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam katika Ukanda wa Pwani na kupelekea washindi watano kupatikana na kukabidhiwa Shilingi laki tano kila Mmoja.

Mara baada ya kumalizika kwa hatua ya kwanza ya kutafuta washindi kutoka kanda zote sita sasa ni wakati wa washindi wa kanda hizo kuja jijini Dar es Salaam na Kukaa kambi moja huku wakipatiwa mafunzo kutoka kwa Walimu wa Sanaa kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na Chuo Cha Sanaa Bagamoyo lengo likiwa ni kuwapika kisanaa na kuanza kushindanishwa ili kuweza kupata Mshindi mmoja ambaye ataondoka na kitita cha Shilingi Milioni 50 katika fainali itakayofanyika mwisho wa Mwezi wa nane Jijini Dar Es Salaam.

Mara baada ya Fainali hiyo kumaliza washindi kumi watakaopatikana watakuwa chini ya Kampuni ya Proin Promotions na wataweza kutengeneza filamu ya Pamoja na hatimaye kuja kunufaika na filamu hiyo.

Shindano la TMT limekuwa ni shindano kubwa kabisa ambalo halijawahi kufanyika nchini na limekuwa likirusha vipindi vyake katika kituo cha Runinga cha ITV kuanzia mida ya Saa Nne Usiku siku ya Jumamosi na Marudio yake ni Kila Jumapili Saa 10 Jioni na Jumatano Saa 5 usiku huku Jumamosi ya tarehe 21 Juni 2014 kipindi cha Dar Es Salaam kitarushwa kupitia kituo hiko cha runinga na hatimaye Kazi ya Mchujo Kuanza Mara moja mara baada ya washindi wa kanda zote kuwasili Jijini Dar Es Salaam na kuanza kambi huku wananchi watakuwa wakiwapigia kura washiriki ambao wanawaona wenye uwezo.
 Wafanyakazi wa Kampuni ya Proin Promotions katika Mradi wa Kusaka vipaji vya Kuigiza Nchini TMT (Tanzania Movie Talents) wakishangilia kwa kufungua Mvinyo usio na kilevi mara baada ya kumaliza zoezi la Kuzunguka Katika Kanda Sita nchini kwa kusaka Vipaji vya kuigiza ambapo zoezi hilo lilimalizika katika Kanda ya Pwani, Mkoani Dar Es Salaam ambapo washindi watano kutoka kanda ya Pwani walipatikana na Kupewa zawadi zao za Shilingi laki Tano Kila Mmoja na Kushiriki katika fainali ya Kuwania Shilingi Milioni 50 za Kitanzania.
Mmoja wa Majaji katika Shindano la TMT Yvonne Cherry au Monalisa akifurahia kufungua Mvinyo huku wafanyakazi wa Proin wakifurahia pia kwa kukinga mvinyo huo mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kusaka vipaji vya kuigiza katika Kanda ya Pwani ambapo ndio imefunga zoezi hilo lililoanzia Kanda ya Ziwa, Kati, Nyanda za Juu Kusini, Kusini na Kaskazini.
Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin Group of Companies,Bw Johnson Lukaza akiongea na wafanyakazi wa Proin Promotions limited mara baada ya kumaliza vizuri kwa kazi za kutafuta vipaji katika Kanda Sita za Tanzania.Pamoja na kuongea na wafanyakazi hao aliweza kutoa neno la shukrani kwa kila mmoja kwa kutimiza wajibu wake na hatimaye kufanikisha zoezi hilo la hatua ya kwanza kumalizika vyema.

NICE & LOVELY MISS TANGA 2014 WAKABIDHI MSAADA WA VYAKULA KITUO CHA WATOTO YATIMA TANGA

$
0
0
MSAADA 1MSAADA 2Warembo wa Miss Tanga wakiwa wamebeba msaada wa vyakula walivyopeleka kituo hapo.
MSAADA 3Warembo wa Miss Tanga wakiwa wamewabeba watoto hao na kuzungumza nao.
MSAADA 4Mwakilishi wa kampuni ya Loriel watengenezaji wa mafuta ya Nice & Lovely, Donata Mallya akimkabidhi msimamizi mkuu wa kituo hicho, Josephine Lyimo moja ya misaada waliyoipeleka kituoni hapo.
Washiriki wanaowania shindano la kumtafuta mrembo wa mkoa wa Tanga, Nice & Lovely Miss Tanga 2014 jana wametembelea kituo cha kulelea watoto yatima cha Association Cassa Familia kilichopo eneo la Raskazone jijini Tanga na kutoa msaada wa vyakula na sabuni za kuogea na kufulia.
Washiriki hao ambao watapanda jukwaani kesho jumamosi 21/06/2014 Mkonge Hotel kuwania taji la Miss Tanga 2014, waliwakabidhi watoto hao mchele kilo 50, unga wa ugali kilo 50, mafuta ya kupikia lita 20, sabuni za kufulia na kupikia pamoja na mafuta ya kujipaka naya nywele ya Nice & Lovelly.
 
Akiongea wakati wa kukabidhi msaada huo, mwakilishi wa kampuni ya Loriel ambao ndio wadhamini wakuu wa shindano hilo, Donata Mallya amesema wameamua kutoa msaada huo kama sehemu ya kuwajali na kuwathamini watoto hao.
Nice & Lovelly Miss Tanga 2014 linafanyika kesho Mkonge Hotel kuanzia saa moja usiku na burudani itatolewa na Malkia wa taarabu nchini, Hadija Omary Kopa.
 
Shindano hilo limedhaminiwa na Nice & Lovelly, Redd’s, EATV, Breeze Fm, CXC Africa, Rweyunga Blog na Mwambao Fm.

WAZIRI MKUU MHE. PINDA AKIWA BUNGENI MJINI DODOMA

$
0
0
PG4A2995Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Wazee Mohammed Cheupe (katikati) na Seif Membe (kulia)  kutoka Jimbo la   Ruangwa ambao walitembela bunge mjini Dodoma Juni 20, 2014, kwa mwaliko wa mbunge wao Kassim Majaliwa ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PG4A3018Mbunge wa  Rungwe Magharibi, Profesa David Mwakyusa   (kushoto) akiteta na Mbunge wa Viti Maalum, Rukia Kassim Ahmed, Bungeni mjini Dodoma Juni 20, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAADHIMISHO YA SIKU YA SIKO SELI DUANIANI YAFANYIKA DAR KWA UZINDUZI WA KILINIKI YA WATOTO.

$
0
0
  Mkurugenzi wa Idara ya Uboreshaji Afya wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Dk Sarah Maongezi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kliniki ya watoto wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sikoseli Duniani yalifanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam jana. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Idara ya Maabara, Dk. Alex Magesa, Mwenyekiti wa Mfuko wa Sikoseli Tanzania, Grace Rubambey na Mkurugenzi waTiba wa Hospitali ya Muhimbili, Dk Hedwiga Swai na kulia ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tiba Muhimbili (MUHAS), Profesa Eligius Lyamuya..
 Mkurugenzi wa Idara ya Uboreshaji Afya wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Dk Sarah Maongezi akihutubia wakati wa maadhimisho hayo jijini Dar es Salaam jana.
 Mwenyekiti wa Mfuko wa Sikoseli Tanzania (TSCF), Grace Rubambey akitoa takwimu kuhusu hali ya ugonjwa nchini. Tanzania ni nchi ya tano kuwa na wagonjwa wengi duniani ambao karibu watoto 11,000 huzaliwa na sikoseli kila mwaka.


 Mmoja wa wasichana wanaougua sikoseli, Hafsa Omari akitoa ushuhuda wa maisha yake na ni jinsi gani mtu anayeugua ugonjwa huo anaweza kuishi maisha salama.
  Mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Sikoseli Duniani, Dk. Sarah Maongezi (katikati) pamoja na wageni wengine wakipata maelezo kuhusu kliniki ya watoto kutoka kwa Dk. Elisha Osati muda mfupi baada ya uzinduzi rasmi wa kliniki hiyo.
  Mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Sikoseli Duniani, Dk. Sarah Maongezi (katikati) pamoja na wageni wakipata maelezo kuhusu kliniki ya watoto kutoka kwa Dk. Elisha Osati muda mfupi baada ya uzinduzi rasmi wa kliniki hiyo.
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Sikoseli Duniani, Dk. Sarah Maongezi (katikati, mstari wa mbele) pamoja na wageni wengine wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maadhimisho hayo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam jana.
  Baadhi ya watoto wanaougua sikoseli wakiwa na wazazi na wanafamilia wengine wakati wa maadhimisho hayo.
 Msanii wa muziki wa kufokafoka, Hudu Juma Mpili ambaye pia anaugua sikoseli akitoa burudani wakati wa maadhimisho hayo.
Wageni waalikwa wakifuatilia hotuba mbalimbali wakati wa maadhimisho.

MEYA WA ILALA MH JERRY SILAA ATEMBELEA NA KUKAGUA BARABARA YA TABATA-ST MARY'S YENYE MGOGORO BAINA YA MKANDARASI NA DAWASA

$
0
0
Meya wa Ilala Mh Jerry Silaa Akiongea na vyombo vya habari kutoa ufafanuzi wa nini kitafanyika ili kutatua mgogoro huo.
Diwani wa Kata ya Tabata -St Mary Bi Mtumwa Mohammed Akielezea ni jinsi gani wanainchi wa eneo hilo wanapata tabu baada ya barabara hiyo kuchimbwa hivyo kufanya upitaji wa magari kusitishwa kwa mda eneo hilo
Mkandarasi wa barabara ya Tabata_St Marys Bwana George Lupia akiongea na vyombo vya habari kuelezea ni ugumu gani anakumbana nao katika utekelezaji wa ujenzi wa barabara hiyo,kutokana na mabomba ya Dawasco kupita katikati ya barabara Hiyo
 Hiki ndio kipande cha barabara ya Tabata-St Marys ambacho  kinashindwa kuendelea na matengenezo kutokana na Mabomba ya Dawasa kupita kati kati ya barabara na pembezoni,hivyo kumpa hali ngumu mkandarasi kuchimba eneo hilo ili ajaze kifusi.
Pembenini maji yaliyotuama baada ya Bomba la Dawasa kupasuka Hivyo kuleta usumbufu kwa mkandarasi kukamilisha ujenzi wa eneo hilo.


 Hilo shimo hapo ni bomba amabalo limepita katikati ya barabara
 Mmiliki wa gari hii ndogo Toyota Premio alipatwa na hasira baada ya Gari yake kushindwa kupanda ili atokee upande wa pili ikambidi kushuka
 Wakiendelea kutazama gari yao kwa umakini
Akaamua kupanda kwa kasi baaada ya vizuizi kutolewa na yeye mwenyewe.
 Meya Wa Manispaa ya Ilala Mh Jery Silaa Wa Kwanza kulia  akifika eneo la  Tabata St Marrys kukagua kipande cha barabara huyo ambacho kimezua mgogoro baina na Manispaa na Shirika la maji safi na salama DAWASA.
 Mwenyekiti wa Serikali za Mitaaa Bwana Hassan Chambuso akimuongoza Mh Meya wa manispaa ya Ilala Jery Silaa kwenda kujionea eneo la kipande cha barabara ya St Marys Tabata ambacho kinaleta shida baina ya Mkandarasi na Dawasa
Mkandarasi wa barabara ya Tabata-St Mary Bwana  George Lupia wa pili kutoka kushoto akitoa ufafanuzi kwa Meya Wa Ilala Mh Jery Silaa kuhusu kukwama kwake kuendelea na Ujenzi kutokana na Mabomba ya Dawasa kupita Katikati ya barabara Hiyo.
Meya wa Ilala Mh Jery Silaa akifafanua Jambo kwa Mwenyekiti wa mitaa ya Tabata Bwana Chambuso kuhusu yeye Kulifuatilia Swala hilo kwenye mamlaka husika haraka iwezekanavyo,Pembeni yake ni Diwani wa Kata ya  Tabata St Marys Bi Mtumwa Mohamed mwenye Dira.
Mkandarasi Geoge Lupia Akimwelezea Meya wa Ilala Mh Jery Silaa kwamba wametumia pesa nyingi katika kuchimba eneo hilo na kupata usawa wa Barabara lakini kikwazo kimekuja baada ya kukuta mabomba ya Dawasa ambayo yamekatiza katikati ya barabara na pembeni Hivyo kuleta ugumu katika kufanikisha Umaliziaji wake.
Mkandarasi wa Manispaaa ya Ilala Bwana Kassim Muhinda Akimwelezea Meya Jerry Silaa kwamba washaongea na Dawasa lakini hawapewi ushirikiano wa kutosha na wa haraka katika kushughulikia utoaji wa Mabomba hayo
Mkandarasi wa Manispaaa ya Ilala Bwana Kassim Muhinda akiendelea kufafanua jambo kwa Mh Meya wa Ilala Jerry Silaa
Meya wa Manispaaa ya Ilala Mh Jerry Silaa ametembelea eneo la Tabata-St Marys kujionea maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo na pia kuweza kuona mabomba ambayo yanaleta mgogoro baina ya mkandarasi na Manispaaa na Dawasa,Akiwa eneo hilo la St Marys Mh Jerry Silaa ameweza kujionea namna mabomba ya Dawasa ambavyo yamepita katikati ya barabara na pembezoni yakiwa katika kima kifupi hivyo kumzuia mkandarasi kuendelea na ujenzi wake.

Akiongea na vyombo vya habari Mh Meya Amesema kuwa barabara hiyo imetumia gharama za takribani bilioni 1 lakini imeshindwa kumalizika kwa wakati kwa sababu ndogo ya Dawasa kutokushirikiana nao ili kuweza kumpa mkandarasi ramani kamili ya bara bara hiyo,Meya Silaa akaongeza kuwa wameshawasiliana na wenzao wa Dawasa kuhusu tatizo hilo lakina wamekuwa hawapewi majibu kwa wakati na ya kuridhisha.

Naye mkandarasi wa eneo hilo Bwana George Lupia amesema kuwa alipewa ramani na manispaa ambayo haikuonysha kama kuna mabomba ambayo yamepita hapo,lakini wakati ameanza kuchimba barabara hiyo ndio akakutana na mabomba hayo,Mkandarasi huyo akaongezea kwamba alishawasiliana na Dawasa kitambo sana lakini hapewi majibu ya kuridhisha kuhusu kushirikiana nao kuhamisha bomba hizo. 

Naye Diwani wa kata Hiyo Bibi  Mtumwa Mohhamed amesema wanainchi wa eneo hilo wanapata tabu sana kwa kuwa magari yao hayawezi kutoka ndani wala kuingia kwa kuwa barabara imechimbwa kwa kina kirefu sana,hivyo amewaahidi wanainchi wa eneo Hilo kwamba wanaendelea kulitatua tatizo hilo na wenzao wa dawasco ili kuweza kuhamisha mabomba ya eneo hilo. PICHA NA HABARI NA DJ SEK BLOG

RAIS KIKWETE ATOA MHADHARA KATIKA CHUO CHA ULINZI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo amekumbuka enzi za kuwa mwalimu katika Chuo cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania cha Monduli, Arusha, alipotoa  mhadhara  kuhusu Fursa (A lecture of Opportunity) katika Chuo cha Taifa cha ulinzi (National Defence College -NDC- ) kilichopo Kunduchi  jijini Dar es salaam ambako aliahidi kwamba baada ya kustaafu Urais mwakani atakuwa mwalimu chuoni hapo. Pichani anaonekana  Rais Kikwete akisikiliza swali kutoka kwa mmoja wanafunzi hao baada ya mhadhara wake.
  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo amekumbuka enzi za kuwa mwalimu katika Chuo cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania cha Monduli, Arusha, alipotoa  mhadhara  kuhusu Fursa (A lecture of Opportunity) katika Chuo cha Taifa cha ulinzi (National Defence College -NDC- ) kilichopo Kunduchi  jijini Dar es salaam ambako aliahidi kwamba baada ya kustaafu Urais mwakani atakuwa mwalimu chuoni hapo. Pichani anaonekana  Rais Kikwete akisikiliza swali kutoka kwa mmoja wanafunzi hao baada ya mhadhara wake. Pichani Rais Kikwete akijibu maswali kutoka kwa wanafunzi baada ya mhadhara wake
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Wahadhiri na wanafunzi wa  Chuo cha Taifa cha ulinzi (National Defence College -NDC- ) kilichopo Kunduchi  jijini Dar es salaam ambako aliahidi kwamba baada ya kustaafu Urais mwakani atakuwa mwalimu chuoni hapo.
(PICHA NA IKULU)

LULU NA JOTI WAFUNGA NDOA KIMYA KIMYA, USIKOSE KUANGALIA NDOA YAO IFIKAPO SAA 4 USIKU ITV

$
0
0
Hatimaye Msanii Elizabeth Michael maarufu kama Lulu afunga Ndoa ya Kimya Kimya na Msanii wa Vichekesho Lucas Mhavile maarufu kama JOTI. Ndoa hiyo ya Kimya imefungwa siku chache zilizopita katika fukwe za Kiota cha Maraha cha Escape 1 Mikocheni.
Mchungaji akiwafungisha Ndoa hiyo ambae pia ana kipawa cha Uchekeshaji na MC aitwaye Mc Pilipili.
Lulu akiwa katika vazi la Harusi kabla hajafunga ndoa hiyo.Ndoa hiyo itarushwa leo Saa Nne usiku katika Kituo cha Runinga cha ITV na Marudio yake itakuwa ni Jumapili saa 10 Jioni na Jumatano saa 5 usiku.
Najua ungependa kujua Ndoa hiyo ya Lulu na kuona jinsi ilivyokuwa usikose leo Saa 4 usiku katika Runinga ya ITV. Picha Zote na Josephat Lukaza

WAANDISHI WA HABARI WA MKOA WA NJOMBE WAKABIDHIWA VYETI VYA USHIRIKI WA MAFUNZO YALIYOTOLEWA NA MCT

$
0
0
Katibu wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Njombe Hamis Kassapa akipokea cheti cha kushiriki mafunzo yaliyotolewa na baraza la habari Tanzania MCT kwa waandishi wa habari wa mkoa huo jana Juni 19, 2014
Mtangazaji wa Uplands Fm Zenobia Mtei akipokea cheti chake kutoka kwa wawakilishi wa MCT
David Jothamson kutoka Kings FM ya Njombe akipokea cheti chake cha kushiriki mafunzo.

Mtangazaji Veronica Mtauka wa redio Kitulo FM ya wilayani Makete mkoani Njombe akipokea kwa furaha cheti chake kama mshiriki wa mafunzo hayo
Mkurugenzi wa Ice FM ya Makambako mkoani Njombe MCDonald Mase akipokea cheti chake
 Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Njombe Mercy James akikabidhiwa cheti chake
 Meneja wa kitucha redio Uplands Fm, Novatus Lyaruu akipokea cheti chake kama mshiriki wa mafunzo hayo
Mwandishi wa habari wa gazeti la Majira na mtandao wa Habari Ludewa Blog NIckson Mahundi akikabidhiwa cheti chake
Mtangazaji wa Best FM ya Ludewa mkoani Njombe akipewa cheti chake cha ushiriki wa mafunzo hayo
Mmiliki wa Eddy Blog Edwin Moshi akipokea cheti cha mafunzo hayo ya siku nne yaliyoandaliwa na MCT.

Mafunzo hayo yaliandaliwa na baraza la habari Tanzania (MCT) kwa kushirikiana na chama cha waandishi wa habari mkoa wa Njombe (NPC) yenye lengo la kuwasaidia waandishi hao kuandika habari kwa kufuata weledi wa taaluma hiyoPICHA ZOTE NA EDWIN MOSHI

ADY BATISTA WA “THE THORN OF THE ROSE” AKONGA NYOYO ZA WAPENZI WA SINEMA TAMASHA LA ZIFF 2014

$
0
0
DSC_0128
ADY de Batista (30).
DSC_0154
ADY de Batista akisaidiwa kushuka kwenye gari na meneja wake Sholey Maqueta mara baada ya kuwasili kwenye viunga vya Ngome Kongwe visiwani Zanzibar. (Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).

Na Mwandishi wetu, Zanzibar
ADY de Batista alishuka taratibu katika gari la Noah, akiwa amevalia nguo nyeupe.Alisaidiwa kushuka kwenye gari na meneja wake Sholey Maqueta na kuingia katika ukumbi wa maonesho ya sinema wa wazi uliopo Ngome 

Kongwe kwa ajili ya sinema yake ya O Espinho Da Rosa.
Kutoka kwenye gari hadi alipopokewa na Mtendaji wa tamasha la Filamu la Kimataifa la Zanzibar (ZIFF) Profesa Martin Mhando,unamuona mdada anayejiamini, mwenye uzuri wa asili na weusi unaong'aa majira ya magharibi kabisa, kabla ya swala ya insha.
DSC_0157
ADY de Batista akiingia kwenye lango kuu la Ngome Kongwe.
Alikuwa anatembea taratibu kama malkia kushoto akiwawepo meneja Sholey na Kulia rafiki yake wa kiume Antoine Simonet.Nyuma alikuwapo mdogo wake Nautenle Batista.

Alipokewa na Mtendaji wa ZIFF Profesa Martin Mhando ambaye alizungumza kidogo kuhusu O Espinho Da Rosa (The Thorn Of The Rose) kabla ya kumkaribisha kuzungumza na wapenzi wa sinema waliokuwa wamejazana pomoni katika ukumbi wa sinema.
DSC_0181
ADY de Batista na Meneja wake wakielekea kwenye jukwaa la ZIFF 2014 kuhutubia. 

Kabla ya kuzungumza kuhusu filamu hiyo ambayo imechezwa na Júlio Mesquita, mwenyewe Ady Batista, Daniel Martinho, Ângelo Torres na Ciomara Morais, Ady alishukuru kuwepo Zanzibar na kusema kwamba ndoto yake imetimia, anashukuru sana.

Sinema hii ambayo ni saa moja na dakika 37, ni sinema yenye makali yote ya maisha, mashaka na pia imani zilizojikita vyema katika jamii ambayo imekuwa ikikabiliwa na matatizo mbalimbali.


DSC_0194
ADY de Batista akizungumzia filamu yake.
Maneno ya ndoto kutimia yameonesha furaha aliyoiandika katika mtandao wa kijamii wa Facebook Mei mwaka huu baada ya kuambiwa kwamba filamu yake imeingia katika mashindano ZIFF.

Katika hiyo face book ya Mei mwaka huu aliandika: E nós fomos seleccionados! Júlio Mesquita Audilia Batista Daniel Martinho Daniel Martinho Angelo Torres Ciomara Morais Sonia Claudia Neves Eric Santos Eric Santos akimaananisha : Tumechaguliwa! akiwataarifu Júlio Mesquita Audilia Batista Daniel Martin Daniel Martin Angelo Torres Noelle Matthews Sonia Santos Santos Eric Eric Claudia Neves .
DSC_0186
Shangilio lililokuwa katika facebook ndilo hasa alilolionesha wakati akizungumzia sinema yake hiyo ambayo ilipigwa picha kwa siku 20 na kutoa matokeo kama sinema ya Hollywood kwa ubora.
Ikiwa inajulikana kama The Thorn of the Rose,kwa kingereza, filamu hii ambayo ilikuwa ya kwanza kwa mtengeneza sinema Filipe Henriques ipo katika maelezo ya ushindani ambayo yanatoa ubora wa picha na skripti yenyewe kwa namna ambavyo matukio yamefungwa pamoja na kuwa kama visa zaidi ya viwili katika filamu.
DSC_0207
Kiukweli wakati natazama sinema hii Ngome Kongwe na hata katika maonesho binafsi ya ndani ya ukumbi wa kujitegemea Double Tree Hotel, ina wakati inakuchanganya mwenendo ambao unatakiwa kuwa nao makini kwani kuna muda unajisikia kama kutapika kwa hasira wakati mtengeneza sinema alipokuwa akiiperemba jamii na makovu ya wanasiasa.
Unaweza kusema kwamba simulizi hili lina mashetani, lakini masimulzii yake yanakupa neno jema kabisa la kuzungumza wakati ukimaliza kuona sinema hii.
Mwendesha mashtaka David Lungha (Júlio Mesquita) katika filamu hii anakutana na binti mrembo ambaye uwepo na utokeaji wake ni wa 'utata' zaidi anayekwenda kwa jina la Rosa (Ady Batista).
Hawa wawili wanakutana katika baa ambapo watu walikuwa wanamsubiri kumpa hongera kwa ushindi wake mahakamani. Amabo anaukiri na kusema mapambano yanaendelea.
Akisema hivyo anakwenda kukaa katika kiti cha baa na pembeni mwake kuna askari polisi.
Akiketi pale mmoja wa wasaidizi wake anafika kwake akionekana wazi si tu kutoa hongera bali kumtaka kimapenzi na kumkataa, lakini akiondoka analetewa bahasha na mtandia , lakini kabla ya hapo anazungumza na polisi ambaye anamwambia hakuna ua waridi lisilokuwa na miba na ogopa unapopata ua waridi tatu.
Akaondoka akmfyonza lakini kweli aliona kuna ua waridi na maneno ya polisi yanaweza kuwa kweli.
DSC_0230
Muda mfupi tunasikia kishindo cha kiatu na anaingia binti wa kike ambaye mwendesha mashtaka anaingiwa na kwikwi na wanaanza mambo ambayo yanapeleka katika mtandao mkubwa zaidi wa uwongo, kusalitiana, mauaji na rushwa.
Ukiangalia sinema hii hata mwanzo unapata maswali mengi kama kweli Rosa ni mtu kweli au ni mawazo ya mwendesha mashtaka, ama ni mzimu ambao hauwezi kutulia kuzimu mpaka habari ya kifo chake ielezwe.
katika simulizi hili muigizaji kinara David Lungha ni mwanamume mwenye mvuto mkubwa wa kimapenzi lakini mtata; na mtu wetu wa leo katika sebule la sinema Ady Batista ni mdada mzuri, ambaye anaonekana kuchukua kiatu cha Rosa, kama asiyekuwa na raha huko aliko.
Ndani humu Eric Santos ni askari ambaye amekuwa polisi akiwa na siri nyingi mbaya za kwake.
Lakini msimuliaji wetu anataka kukueleza kwamba si sahihi kuacha kurekebisha mambo na wale waliokufa, kwani hutafuta njia ya kurudi na kurekebisha mambo yao, imani ambayo Waguinea wanayo sana.
Mapenzi ya mwendesha mashtaka David Lunga kwa Rosa kuna vuruga kila kitu na Lunga anajikuta akifanya vitu vingi kwanza kumaananisha kwamba hana kosa wala hana sababu ya kujuta.
DSC_0248
Filamu hii ambayo iliwapa shida watu wa sensa wa ZIFF ili iweze kuonwa na watu wengi ukumbi wa wazi, unazungumzia kwa namna ya pekee rushwa, ubakaji ambao unafanywa katika maisha ya binti, kifo chake na jinsi ambavyo anataka jumuiya ijue.
Pamoja na kwamba binti alikufa katika utata wa kutoa mimba alirejea duniani kutafuta msaada wa haki kutendeka na katika hili Polisi yule (askari wa zamani) aliwaua lakini akashindwa kummaliza moja kwa moja Lunga ambaye alimuua.
Kiukweli kuelekea mwisho wa sinema unaona matukio mengi na jinsi hali ilivyo ngumu na lazima aifanyie kazi.
Filipe Henriques ameifanyakazi kubwa sinema hii ambayo imejaa usaliti kuanzia wa kisiasa, kijamii hadi kimapenzi huku mazungumzo yakiwa mapenzi kwa watoto wadogo.
Lugha ya kireno ambayo imeambatana na lugha ya kiingereza katika maandishi yanayopita si nzuri kihivyo, lugha ina matusi mengi na isiyopendeza na kuna grafiki za mapenzi ya kulazimishwa katika hali isiyokubalika.
DSC_0249
ADY de Batista akiondoka mara baada ya kumalizika kwa filamu yake.
Mdada huyu ambaye katika mazungumzo alisema kwamba simulizi la sinema ile ni matukio ya kweli nyumbani kwao ambapo pia kuna imani kubwa kuhusu mizimu kurejea duniani pamoja na kuwapo dini ya Kikristo na Kiislamu,ametaka jamii kujipambanua na maradhi ya woga na kuchukua hatua kwanza binafsi na kisha kijamii dhidi ya maovu.
Mdada huyu ambaye hajaolewa lakini ana rafiki wa kiume, alikuwa Zanzibar na mdogo wake na Meneja wake.
Mdogo wake ndiye anayejua kiingereza kwa ufasaha zaidi huku yeye mwenyewe amebahatisha.
Nilipomuuliza kuhusu nguo yake nyeupe, kwani katika sinema kuna vazi la harusi, alisema rangi nyeupe ni alama ya matumaini.
DSC_0257
Kuendelea kusoma zaidi bofya hapa

DAR LIVE INAKULETEA VUNJA JUNGU, JUMAMOSI JUNI 28, 2014

Rais Kikwete akusudia kushika chaki tena

Rais Kikwete afungua Semina ya Commodity Exchange Dodoma

$
0
0
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kiikwete akifungua Semina ya Africa Rural Commodity Exchange iliyofanyika katika ukumbi wa St.Gasper mjini Dodoma leo.Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na watatu kushoto ni Mtaalamu wa Masoko ya mitaji kutoka Ethiopia Dkt.Eleni Gabre Madhin.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina ya Africa Rural Commodity exchange iliyofanyika katika ukumbi wa St.Gasper mjini Dodoma leo, Semina hiyo yenye maudhui Toward a vibrant Tanzania Commodity Exchange ilihudhuriwa na Mawaziri na makatibu wakuu.Semina hiyo iliendeshwa na mtaalamu wa masoko ya mitaji kutoka Ethiopia Dr.Eleni Gabre Madhin.Kushoto ni Waziri mkuu Mizengo Pinda.Picha na Freddy Maro 

DKT BILAL AZINDUA MTAMBO WA MAJI TAKA WA KIWANDA CHA SERENGETI CHA MWANZA LEO

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal akikatautepe kuzindua mtambo wa Maji taka ya kiwanda cha Serengeti cha Mjini Mwanza kulia Mwenyekiti wa Bodi Nehemiah Mchechu kushoto Mkurugenzi Mtendaji Bw Steve Gannon.
 Makamu wa Rais wa jamhuri ya Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal akisalimia wananchi wakati wa uzinduzi wa Mtambo wa Maji taka wa Kiwanda cha Serengeticha mjini Mwanza
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal akiwa katika picha ya Pamoja na wafanyakazi wa kike wa Kiwanda cha Serengeti cha Jijini Mwanza.
 Makamu wa Rais wa jamhuri ya Tanzania Dkt Mohammed Gharib  Bilal akifungua kipazia kuzindua Mtambo wa Maji taka wa Kiwanda cha Serengeti cha Mjijini mwanza kushoto Mwenyekiti wa Bodi ya kiwanda cha Serengeti.
Makamu wa Rais wa jamhuri ya Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal akipata maelezo kwa Inspekta wa Mazingira Bi Anna Mangara  juu ya maji yaliyosafishwa kwenye Mtambo wakusafishia Maji taka kwenye kiwanda cha serengeti cha mjini mwanza.

Rais KIkwete- Vyama vingi vimepanua wigo wa kisiasa

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa mfumo wa vyama vingi vya siasa ni mzuri, umeleta matumaini kwa kupanua wigo na kufungua zaidi uwanja wa kisiasa pamoja na kuiwajibisha Serikali.

Hata hivyo, Rais Kikwete amesema kuwa ili mfumo huo uboreshwe zaidi na uweze kuimarisha misingi mikuu ya maendeleo ni lazima uendeshwa kwa watu kufuata sheria na wala siyo kuingiza matumizi ya nguvu ambayo yanaweza kuvuruga nchi.

Rais Kikwete ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama aliyasema hayo jana, Ijumaa, Juni 20, 2014, wakati alipotoa Mhadhara (Lecture) kuhusu Usalama wa taifa – The Security of a Nation- kwenye Chuo cha Taifa cha Ulinzi  - National Defence College (NDC) Kunduchi, mjini Dar Es Salaam.

Rais Kikwete alikuwa anajibu swali la mwanafunzi wa kozi ya pili kwenye chuo hicho kutoka Kenya ambaye alitaka kujua jinsi gani vyama vingi vya siasa vinavyoathiri umoja wa kitaifa na kuibadilishaTanzania kufuatia miaka zaidi ya 30 ya Tanzania kuwa nchi yenye kuleta matumaini kwa nchi nyingine za Afrika na Waafrika.

Rais kikwete alisema: “Vyama vingi ni vizuri. Mfumo wa vyama vingi unaleta matumaini kwa kupanua wigo wa kisiasa ambao haukuwa mpana kiasi hicho huko nyuma. Sasa mtu anaweza kuamua kujiunga na chama chochote cha siasa anachokipenda yeye.”

Aliongeza rais Kikwete: “Ni mfumo ambao unaiwajibisha Serikali. Ni mfumo mzuri kwa upanuzi wa demokrasia. Sasa watu wanaweza hata kuamua kupunguza bajeti ya safari za Rais nje ya nchi. Wanadhani kuwa Rais anaweza kufanikiwa zaidi na Tanzania kupita hatua za maendeleo haraka zaidi kama Rais atabakia amejifungia ndani ya nchi.”

Rais Kikwete alizidi kujibu swali hilo: “Jambo la maana ni kwamba tunahitaji aina mbali mbali ya mawazo. Mawazo ya namna hiyo hayaathiri demokrasia. Mawazo ya namna hiyo yanasaidia hata chama changu kuimarika zaidi.”

Hata hivyo, Rais Kikwete amesema kuwa mfumo huo utavurugika endapo baadhi ya watu wataendekeza matumizi ya nguvu na hoja za nguvu badala ya kupambana kwa hoja na nguvu ya hoja.
“Wasiwasi wangu ni kuingiza matumizi ya nguvu katika ujenzi wa demokrasia. Ni makosa kwa watu kukimbilia kutumia nguvu baada ya kushindwa kwenye hoja. Na hili halivumiliki na likitokea basi Serikali itaingilia kati kudumisha amani.”

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM 

21 Juni, 2014

WARSHA YA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WA HABARI KUHUSU UANDISHI WA HABARI ZA KITAKWIMU YAFANYIKA MKOANI MOROGORO

$
0
0
Mkurugenzi wa Takwimu za Kijamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Morice Oyuke (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Morogoro leo wakati akifungua Warsha ya siku moja ya kuwajengea uwezo wanahabari kuhusu namna bora ya kuandika habari za kitakwimu. Kulia ni Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa, Daniel Masolwa.
Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa, Daniel Masolwa (kulia), akitoa mada katika warsha hiyo. Kushoto ni Watakwimu, Stephano Cosmas na Hashim Njowele.
Mkurugenzi wa Takwimu za Kijamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Morice Oyuke (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Morogoro leo wakati akifungua Warsha ya siku moja ya kuwajengea uwezo wanahabari kuhusu namna bora ya kuandika habari za kitakwimu. Kulia ni Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa, Daniel Masolwa.
Mtakwimu, Stephano Cosmas, akitoa mada katika warsha hiyo.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye warsha hiyo.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye warsha hiyo.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye warsha hiyo.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye warsha hiyo.
Maofisa wa Takwimu, Stephano Cosmas na Hashim NNjowele wakisubiri kutoa mada katika warsha hiyo.
Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa, Daniel Masolwa (kulia), akimkaribisha mgeni rasmiMkurugenzi wa Takwimu za Kijamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Morice Oyuke (kushoto), kufungua warsha hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk.Albina Chuwa.
Wanahabari wakiwa katika warsha hiyo.

Dotto Mwaibale, Morogoro

WAANDISHI wa Habari nchini wametakiwa kutumia taaluma yao kwa ajili ya kuhamasisha Umma kuhusu umuhimu wa Takwimu.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Takwimu za Kiuchumi Morice Oyuke kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa.mjini Morogoro leo asubuhi wakati akifungua Warsha ya siku moja ya kuwajengea uwezo wanahabari kuhusu namna bora ya kuandika habari za kitakwimu.

"Ninyi wanahabari ni muhimu katika masuala ya takwimu hivyo ni vizuri mjifunze jinsi takwimu zinavyoisaidia serikali, wadau wa maendeleo na wadau wa takwimu katika kupanga Sera na kufanya tathmini ya utekelezaji wa mipango mbalimbali ya kitaifa na kimataifa kama vile Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025 Tanzania Bara na mwaka 2020 Tanzania Zanzibar" alisema Oyuke.

Oyuke alitaja mambo mengine wanayopaswa kujifunza ni Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania Bara (Mkukuta) Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Zanzibar (Mkuza) na Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2010/11 mpaka 2015/16 na Malengo ya Melenia (MDGs).

Alisema eneo jingine watakalofundishwa ni kuhusu Pato la Taifa na jinsi linavyokokotolewa na bei za ajira, takwimu za jamii na umuhimu wake.
Dk.Chuwa alisema vyombo vya habari vinajukumu la kutoa taarifa sahihi zilizo rasmi ambazo zinazalishwa na tafiti mbalimbali nchini ili ziwafikie wadau wote nchini bila ya kupoteza maana.

Lameck Ditto introducing New Video "Tuongeze Bidii"

VIONGOZI WA KAMATI ZA AFYA ZA SHEHIYA WAPATIWA MAFUNZO JUU YA MIKAKATI YA AFYA YA JAMII ZANZIBAR

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Magharibi Hassan Mussa Takrima akitoa nasaha kwa washiri wa mafunzo ya siku tano juu ya mkakati wa Afya ya jamii kwa viongozi wa kamati za Afya za Shehiya, katika ukumbi wa Ofisi ya walemavu Kikwajuni weles Mjini Zanzibar.
 Afisa Mipango na Utumishi wa Wilaya ya Magharibi Unguja Bw. Ameir Ali Haji akitoa maelezo juu mafunzo ya siku tano kwa viongozi wa kamati za Afya za Shehiya tatu za Magharibi, (kulia) Mkuu wa Wilaya ya Magharibi Hassan Mussa Takrima ambae ni mgeni rasmin katika mafunzo hayo. Yaliofanyi ukumbi wa Ofisi ya walemavu Kikwajuni weles Mjini Zanzibar.

Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo.
 Muezeshaji kutoka kitengo cha elimu ya Afya ya jamii Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Amina Sleyum akitoa mafunzo juu ya elimu ya Afya kwa jamii.

 Washiriki wakifanya mtihani.
(Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar). 


MKUU wa Wilaya wa Magharibi, Hassan Mussa Takrima amewataka watendaji wa wizara ya afya kushirikiana na masheha katika kuelimisha wananchi juu ya utekelezaji wa mpango wa afya kwa jamii ili uweze kutatua changamoto za kifya nchini.

Amesema kuwa endapo mpango huo ukihamasishwa kwa jamii utaweza kuwasaidia wananchi katika kujikwamua na matatizo ya kujikinga na maradhi mbalimbali yanayojitokeza katika maeneo yao .
Akizungungumza katika ufunguzi wa mafunzo juu ya mkakati wa afya ya jamii kwa kamati kiongozi  za shehia za Magogoni,Meli nne na Chukwani zilizopo katika wilaya Magharibi ili ziweze kufanya kazi kwa ufanisi katika kupunmguza matatizo ya kifya yanayozikabili shehia hizo.
Alieleza kuwa serikali ya mapinduzi Zanzibar imeamua kutoa fursa kwa watendaji wa sekta ya afya waweze kufanya kazi kwa mashirikiano na viongozi kuanzia ngazi ya shehia kwa lengo la kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na afya bora.
“Tumieni mafunzo yenu vizuri kwa hekima na upole kwani nyinyi mnaenda kuielimisha jamii, na uko kuna makundi mbalimbali yanayotakiwa kupewa taaluma juu ya umuhimu wa kutunza afya na utekelezaji wa mpango huu kwa vitendo.”alisema Takrima.
Nae Afisa wa afya  wa wilaya hiyo, Abubakar Mohamed Ali ameeleza kuwa katika katika mafunzo hayo washiriki watafundishwa njia mbadala ya kuwawezesha masheha na viongozi wengine kutumia rasilimali zilizomo katika maeneo yao ili kutatua changamoto za kiafya bila kusubili utekelezaji kutoka  serikali kuu.
Kwa upande wake afisa mipango wa Wilaya hiyo Ameir Ali Haji alifamisha kuwa  lengo la mkakati huo ni kuimarisha mahusiano baina ya sekta ya afya na jamii ili kuinua huduma za afya zinazotolewa ziweze kuendana na viwango vilivyowekwa na serikali.
NA MAELEZO ZANZIBAR.
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live




Latest Images