Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

HACKERS WAIBA AKAUNTI YA FACEBOOK YA MEYA WA ILALA JERRY SILAA

$
0
0
Napenda kuwajulisha marafiki zangu wote kwamba akaunti yangu ya facebook ime-hackiwa na kuanza kutuma ujumbe kwa marafiki zangu kuwataka waingie kwenye link kwani nina maongezi ya siri.

Tafadhali puuzia ujumbe huo kwani utasababisha akaunti yako nayo ku-hackiwa.
Tafadhali sambaza ujumbe huu, wakati tunaendelea kujaribu kuiokoa. Nawaomba radhi wote walopatwa na usumbufu huu.
Jerry Silaa

UNICEF Tanzania yawateua AY na Faraja K. Nyalandu kama Mabalozi wao wa kuhamasisha umma juu ya ukatili dhidi ya watoto

$
0
0
Halmashauri ya Wilaya ya Hai yazindua kituo cha huduma jumuishi cha kushughulikia ukatili wa wanawake na watoto.UNICEF Tanzania yawateua AY na Faraja K. Nyalandu kama Mabalozi wao wakuhamasisha umma juu ya ukatili dhidi ya watoto

Hai, 16 June, 2014 –Katika kusherehekea siku ya Mtoto wa Afrika tarehe 16 Juni, Halmashauri ya Wilaya ya Hai, ikishirikiana na viongozi wa serikali, UNICEF na Save the Children, imezindua Kituo cha Huduma Jumuishi, kitakachowasaidia wanawake na watoto ambao wameathiriwa na ukatili.

“Katika kituo hiki, huduma za kuwasaidia wahanga wa ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto ikiwa ni pamoja na huduma za afya, msaada wa kisaikolojia, ulinzi/usalama na msaada wa kisheria vinaweza kutolewa hapo katika eneo moja ndani ya kituo cha afya zikiwa zimeratibiwa vizuri Zaidi,” alisema  Charles Pallangyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. 

Aliongeza, “kituo hiki kitasaidia kupunguza madhara zaidi ya ukatili kwa sababu wahanga wa ukatili wataweza kupata huduma zote muhimu katika eneo moja na hawatakuwa na sababu ya kurudiarudia kuwaeleza watoa huduma mbalimbali walio katika maeneo tofauti yale mambo mabaya waliyoyapitia, au kutakiwa kwenda na kurudi kutokana na ukosefu wa uratibu na uwezo wa watendaji wa sekta mbalimbali katika kuwahudumia wahanga wa ukatili kwa ukamilifu.”

Mwakilishi wa UNICEF Tanzania, Dk. Jama Gulaid, anaamini kuwa kama tukifanya kazi kwa ushirikiano na serikali na wadau wengine, tunaweza kupata suluhu katika kumaliza ukatili dhidi ya watoto. “Ukatili dhidi ya watoto uko kila mahali na hatuwezi kuendelea kuufumbia macho. Watoto wote hapa Tanzania wanahaki ya kuishi na kukua katika mazingira yasiyo na ukatili. Kama sisi sote tukifanya kazi kwa kushirikiana pamoja, sina shaka tutaweza kumaliza ukatili dhidi ya watoto.”

Katika tukio hili huko Hai, UNICEF Tanzania imemteua msanii mahiri wa bongo flava Ambwene Yessyah, anayejulikana zaidi kama AY, pamoja na aliyewahi kuwa Miss Tanzania, Faraja Kotta Nyalandu kama Mabalozi wao katika ‘Kampeni ya Tokomeza Ukatili Dhidi ya Watoto.’ Wote wameahidi kusaidia kampeni ya ‘Kampeni ya Tokomeza Ukatili Dhidi ya Watoto’ na wameonyesha kuhamasishwa na heshima hii waliyopewa kutoa sauti zao kutetea ulinzi wa mtoto.

“Nimepewa heshima kubwa kwa kuteuliwa kwangu kuwa Balozi wa UNICEF Tanzania na nitajitoa katika kutumia sauti yangu na umaarufu wangu kusaidia kutokomeza ukatili dhidi ya watoto hapa Tanzania,” alisema AY alipokuwa akikubali wadhifa huo. 

Kwa kuwateua AY na Faraja Kotta Nyalandu kama Mabalozi wa UNICEF Tanzania wa kampeni ya ‘Kampeni ya Tokomeza Ukatili Dhidi ya Watoto’, UNICEF inategemea kuongeza uzito na muonekano zaidi wa suala la ulinzi wa mtoto katika mijadala inayoendelea kuhusu ukatili dhidi ya watoto na kuonyesha kuwa kuna suluhisho la tatizo hili. Kama mwazo wa kazi yao katika shughuli za UNICEF Tanzania, AY na Faraja Kotta Nyalandu walitembelea Dawati la Jinsia na Watoto katika kituo cha Polisi cha Hai kuona wenyewe kazi inayofanywa kusaidia wanawake na watoto waliofanyiwa au kuathiriwa na ukatili. 

Utafiti juu ya Ukatili Dhidi ya Watoto, uliozinduliwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto mwaka 2011, unaonyesha mambo yanayopelekea uhatarishi wa watoto kwenye ukatili kimwili na kingono hapa Tanzania – wastani wa msichana 1 kati ya 3 na mvulana 1 kati ya 7 wamefanyiwa vitendo vya ukatili wa kingono, na zaidi ya asilimia 70 ya wasichana na wavulana wamefanyiwa vitendo vya ukatili wa kimwili kabla hawajafikia umri wa miaka 18. Hata hivyo, wahanga wengi hawajamwambia mtu yeyote ukatili waliofanyiwa na ni kesi chache sana zimefikishwa polisi.

Kumekuwa na maendeleo katika kuboresha hali hii. UNICEF inasaidia serikali ya Tanzania kupitia Idara ya Ustawi wa Jamii kuanzisha na kuboresha ‘mifumo ya Ulinzi wa Mtoto’  katika halmashauri 13. Katika halmashauri hizi, afya, ustawi wa jamii, polisi, sekta za elimu na mahakama, magereza, wanasheria, asasi za kiraia pamoja na mifumo ya kijamii isiyo rasmi wanaunda Timu ya Halmashauri ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto na wanashirikiana kuhakikisha kuwa kesi za ukatili wa watoto zinashughulikiwa vyema na pia wanazuia ukatili kwa kuongeza uelewa wa jamii juu ya ukatili dhidi ya watoto. Lengo la Idara ya Ustawi wa Jamii ni kupanua utaratibu wa mfumo huu katika halmashauri 30 ifikapo mwaka 2016.

MUCOBA FC MABINGWA MUUNGANO CUP

$
0
0
 Kikosi cha Mucoba Fc kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wa fainali na Mbaspo Academy na kufanikiwa kunyakua kikombe cha Muungano katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Igowole. 
 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Leonard Thadeo akimkabidhi kikombe cha ubingwa nahodha wa timu ya Mucoba Fc Emanuel Sabinus baada ya kuwafunga Mbaspo academy kwa mikwaju ya penati 7-5 katika mchezo uliochezwa uwanja wa shule ya msingi Igowole wilayani Mufindi.
 Nahodha wa timu ya Mucoba Fc Emanuel Sabinus akinyanyua juu kombe la ubingwa wa Muungano Cup mara baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Leonard Thadeo.
=======  ===== =======
Na Denis Mlowe,Mufindi

FAINALI za 18 za mashindano ya kugombea kombe la Muungano  zilimalizika juzi kwa timu ya Mucoba Fc ya wilayani Mufindi mkoani Iringa kunyakua taji hilo kwa kuwafunga mabingwa watetetezi Mbaspo Academy ya mkoani Mbeya kwa mikwaju ya penati 7-5 katika mchezo mkali uliofanyika uwanja wa shule ya Msingi Igowole Mafinga.
 
Katika mchezo huo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Leonard Thadeo alishuhudia kila timu ilianza kwa kumsoma mpinzani wake kutokana na kujuana walikuwa Mucoba Fc walioanza kutawala katika dakika ishirini za mwanzo na kumweka katika wakati mgumu golikipa wa Mbaspo kwa mashuti ya kushtukiza, kosa kosa ziliandelea hivyo hadi kipindi cha kwanza kinamalizika hakuna timu iliyoona lango la mwenzake.
 
Kipindi cha pili kilianza kwa kusomana kama ilivyokuwa kipindi cha kwanza na ndipo katika dk ya 70 mshambuliaji hatari wa Mucoba Fc David Mhanga aliwapatia goli timu yake baada ya ushirikiano mzuri na kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Hussein na dk ya 75 David Mhanga aliongeza goli la pili kwa upande wa Mucoba FC.
 
Baada ya goli hizo mbili Mbaspo walikuja juu na ndipo katika dk ya 84 mchezaji aliyewateka mashabiki wa soka kwa kiwango chake Soud Mlindwa aliipatia bao timu yake na zikiwa zimesalia sekunde chache kumalizika kwa mpira na baadhi ya wachezaji wa Mucoba kuanza kushangilia ushindi Thabit Juma katika dk. 90 alisawazisha goli ndipo hatua ya kupigiana penati alipochukua hatamu.
 
 Timu ya Mbaspo waliweza kupata penati zao kwa kupitia Eliah Jimmy, Mpoki Mwansansu, Masoud Yusuph, Soud Mlindwa na Boaz Patson  waliokosa ni Thabit Juma na Michael Masinga.
  
Kwa upande wa Mucoba waliofunga penati zao ni Benjamin Mlowe, Ima Mwakajinga, Stanley Mwazangila, Elisha Mwasieni, Denis Lameck na Daud Mwanga aliyekosa ni Reward Abraham na katika mikwaju hiyo shujaa wa timu ya Mucoba alikuwa golikipa wake aliyeweza kupangua penati mbili.
 
Mara baada ya kumalizaka kwa mchezo huo Tanzania Daima lilizungumza kocha wa timu ya Mbaspo Academy Maka Mwarusye, aliwapongeza Mucoba kwa kuchukua ubingwa na kuahidi kwenda kujipanga upya kwa msimu ujao wa mashindano na kwa upande wa mchezo  ulikuwa mzuri kwa upande wa timu zote ila katika mchezo wa soka  kuna kushindwa na kushinda ua sare, hivyo hatua ya penati ni bahati nawapongeza mabingwa.
 
“Mashindano yalikuwa mazuri ingawa kulikuwa na changamoto zake na changamoto hizo ni viwanja kutokuwa na ubora na kuboresha waamuzi itasaidia sana nawapongeza sana Mucoba na vijana wangu kwa kufika fainali kwa mara ya pili” alisema Mwarusye.
 
Bingwa wa mashindano hayo timu ya Mucoba alijinyakulia shilingi milioni 3 na kombe lenye thamani ya shilingi milioni 1.2 na medali za dhahabu, mshindi wa pili timu ya Mbeya City iliondoka na kitita cha shilingi milioni 1.5.
 
Zawadi nyingine zilikwenda kwa mwamuzi bora wa mashindano hayo ambao Steven Makuka, Hashim Mgimba na Erasto Msalilwa waliojipatia sh. Elfu 50 kila mmoja, mchezaji bora wa mashindano hayo  golikipa wa Igowole Fc sh. Laki 2, Mfungaji bora Shadrack Tamimu sh. Laki 2 wa Mbeya City na timu yenye nidhamu Mbeya City sh. Laki 5 na kombe.
 
Mashindano ya Muungano yanayofanyika kila mwaka katika wilaya ya Mufindi na kuratibiwa na Daud Yasini yalidhaminiwa na  Chai Bora ,Asasi Limited, benki ya Mucoba ,na  PPF.

SAUTI SOL WATIKISA TAMASHA LA ZIFF 2014

$
0
0
Na MOblog, Zanzibar
MOJA ya vitu ambavyo wazanzibari watakumbuka ni jinsi kundi la Kenya ambalo hivi karibuni liliibuka kundi bora katika MTV Base lilivyovamia jukwaa na kuendesha shoo ya saa moja na nusu iliyokuwa na uhakika.
Kundi hilo lenye watu watano wakiongozwa na mtia sauti Bien Baraza liliwaacha hoi wazanzibari waliofurika katika ukumbi wa Mambo uliopo ndani ya Ngome Kongwe na muziki wenye mahadhi ya Afro Pop.
Muziki huo ambao uliwateka vijana kutokana na midundo yake na maneno ya kuchombeza ulionesha kwanini MTV Base walisema ni kundi bora.
DSC_0134
Wanamuziki wa Bendi ya Sauti Sol kutoka nchini Kenya likiwasha moto kwenye tamasha la ZIFF 2014 usiku wa kuamkia leo visiwani Zanzibar. Pichani ni Bien Baraza (vocalist) na Willis Austin Chimano (vocalist) wakifanya yao jukwaani. (Picha zote na Zainul Mzige wa Dewjiblog).
DSC_0163
Bien Baraza (kushoto) na Willis Austin Chimano (kulia) wakitoa burudani kwenye jukwaa la ZIFF 2014.
DSC_0193
Polycarp Otieno (Quitar & Vocalist) akifanya yake ndani ya ZIFF 2014.Sauti Sol watikisa tamasha la ZIFF 2014
DSC_0158
Mpiga kinanda wa bendi ya Sauti Sol akifanya yake jukwaani.
DSC_0136
Delvine Mudigi (vocals percussion & drums) akichapa drum kwa staili ya aina yake kwa wapenzi wa Live Music ndani ya ZIFF 2014.
DSC_0048
DSC_0121
Meneja wa Sauti Sol na mchumba wake wakifurahia kazi ya vijana wao ndani ya ZIFF 2014.


DSC_0084
DSC_0087
DSC_0089
Umati wa watu ulijitokeza kwenye tamasha la ZIFF 2014 linaloendelea visiwani Zanzibar, umekosekana wewe tu unayesoma post hii.
DSC_0271
Delvine Mudigi (vocals percussion & drums) wa Sauti Sol akiwapa raha wapenzi wa ZIFF 2014....Wadada walichizikaje sasa na ilende hivi ...Nakuomba Baby Unishike (Nishike)....Unishike Mpenzi (Nishike)...Unishike (Nishike)...No No No No No No No No (Nishike)...Until You Say aaaaaaaaai...Until You Say aaaaaaaaai.
DSC_0267
DSC_0090
Proud of my boys....!The manager him self....Sauti Sol Manager.
DSC_0286
Warembo wakijianda kuosherehesha jukwaa na bendi ya Sauti Sol.
DSC_0290
Willis Austin Chimano akiwatambulisha warembo kwa mashabiki kabla ya kuonyesha ufundi wao.
DSC_0296
Mwanadada akichizika jukwaani.
DSC_0307
Mtasha nae akasema hata mimi naweza nimejaaliwa kidogo...Mashalaah..!
DSC_0311
Twende sasa....mpaka chini ......!
DSC_0313
zunguka zunguka....!!
DSC_0102
DSC_0232
Ooooooiiiiii Oooooiii mzuka mzuka.....! Mashabiki wakichiziki kwa kelele na miruzi ndani ya tamasha la ZIFF 2014.
DSC_0235
Raia wa kigeni wakichizika na burudani ya bendi ya Sauti Sol ndani ya viunga vya Ngome Kongwe kwenye ukumbi wa Mambo Club.
DSC_0245
Mpiga kinanda wa Bendi ya Sauti Sol akifanya yake.
DSC_0184
Has T akichuka matukio ya tamasha la ZIFF 2014.
DSC_0220
Twende kazi...sasa...halali mtu hapa!
DSC_0249
Warembo na swaggaz...!!
DSC_0250
DSC_0320
Ikifika ule wakati wa Ukodak na mashabiki waliohudhuria tamasha la ZIFF 2014 linaloendelea kwenye viunga vya Ngome Kongwe visiwani Zanzibar. Pichani ni warembo wakipozi na Ukodak.
DSC_0040
Model Khalid Balala akiwa kwenye ukodak na Miss Zanzibar.
DSC_0322
Warembo wakipata Ukodak na wasanii wa Sauti Sol.
DSC_0326
DSC_0331
DSC_0349
Wadau waliopata tenda ya kutoa huduma za vinywaji vya aina zote ndani ya viunga vya Ngome Kongwe ukumbi wa Mambo Club wakipozi kwa UKODAK. Kutoka kushoto ni Joyce Joseph, Lucy Charles (Madam Boss Lady) na Winiefrida Nkwera.
DSC_0355
Edwin Fanuel a.k.a mtaalam wa Cocktail (katikati) Dida Shekha (kushoto) na Winiefrida Nkwera.
DSC_0020
Meneja wa Tamasha la ZIFF, Daniel Nyalusi "Dean" (kulia) akishow love na wadau kutoka DSM waliokuja kushuhudia performance ya bendi ya Sauti Sol.

TANGAZO LA MSIBA

$
0
0
FAMILIA YA GEORGE JOHNSON MPONDELA INATANGAZA KUWA MSIBA WA MZEE WAO MPENDWA GEORGE JOHNSON MPONDELA ALIYEFARIKI JUZI TAREHE 15/6/2014 KWA UGONJWA WA MOYO KATIKA  HOSPITAL YA TAIFA MUHIMBILI UTAKUWA NYUMBANI KWAKE KIGAMBONI MJI MWEMA.

 MAZISHI YATAKUWA SIKU YA ALHAMISI YA TAREHE 18/6/2014 SAA 10 JIONI MAKABURI YA KINONDONI DAR ES SALAAM,
IBADA YA MISA ITAFANYIKA KANISA LA KATOLIKI  MUHIMBILI SAA 7 MCHANA NA HESHIMA ZA MWISHO ZITATOLEWA HAPO.

KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA NAMBA 0658870106/0713508861

Mahojiano ya Kwanza Production na Fabian Lwamba wa Krystaal

$
0
0
Mubelwa Bandio wa Kwanza Production akimhoji Fabian Lwamba wa kundi la KRYSTAAL

Karibu kwenye mahojiano kati ya Kwanza Production na Fabian LwambaMmoja wa ndugu watatu wanaounda kundi la KRYSTAAL ambao walizaliwa kwenye familia iliyojiweza, lakini mgogoro wa kisiasa ukawafanya waikimbie Zaire na kutengana.
Lwamba Brothers

Walikuja kuungana Canada ambako kwa miaka 16 wamekuwa pamoja kama kundi la muziki wa injili.
Amezungumza pia mkanganyiko wa IMANI na TAMADUNI zetu.
Swali.... Ni upi muziki wa iNJILI?
Na yeye ambaye ni Mchungaji katika kanisa lao, anasemaje kuhusu TOFAUTI YA KUABUDU KATI YA AFRIKA NA MAGHARIBI
Mpaka sasa, Krystaal wametoa albamu 6 na kupata tuzo 26
Karibu uungane nasi

Kwa maoni ama ushauri usisite kuwasiliana nasi kupitia kwanzaproduction at gmail.com

KITABU : MWANAMKE MSAGAJI AMENIAMBUKIZA UKIMWI

$
0
0
Zuwena ( sio jina lake halisi ), ni mwanamke wa kitanzania mwenye umri wa miaka 43. Kwa sasa mwanadada huyu anaishi na virusi vya ukimwi. Mwanadada huyu anabainisha namna, alivyo pata maambukizi ya v.v.u kw kujamiiana na mwanamke mwenzake, ama kwa lugha nyingine, Zuwena anaeleza namna ambavyo mwanamke msagaji alimuambukiza v.v.u wakati wakiwa na uhusiano wa jinsi moja... Fuatilia kisa hiki cha kufundisha na kusikitisha.

Nakumbuka ilikuwa mwezi wa kumi na mbili mwaka 2007, nilipata tenda ya u MC katika sherehe ya kumuaga binti wa jirani yangu kule Buza Cape Town. Sherehe hiyo ilifanyika kwenye ukumbi wa Mihogoni Pub kulekule Buza.Saa moja usiku nilikuwa nimeshafika ukumbini na kutoa maelekezo kwa wageni waalikwa, watu walikuwa wengi kiasi ambacho hata mama mwenye sherehe alifurahi kwa jinsi watu walivyo muitikia. Kama kawaida niliendelea na matangazo ya hapa na pale, watu walicheza na kufurahi. Muda wa chakula ulipowadia nilikaa pembeni nikiwa naangalia watu wanavyo kwenda kuchukua chakula. 

Ghafla alitokea mama mmoja mtu mzima kwa kumkadiria alikuwa na miaka kama 48 – 50 hivi. Alinifata pale nilipokuwa nimesimama na kuanza kutoa sifa za hapa na pale mara umependeza , mara unaongea vizuri, mara vazi ulilovaa limekupendeza, mwisho aliniomba namba ya simu akaniambia kuwa ana sherehe ya kumuaga binti yake kwa hiyo angependa niwe MC katika shughuli yake. Kwa kweli mimi nilikuwa kazini, sikukataa kumpa namba yangu. Kesho yake alinipigia simu ya kunisalimia, kwa kuwa kiumri alinizidi nilimuamkia, ila nilichokisikia masikioni mwangu ni neno “ Ahsante baby “. Nilishituka lakini nikaona ni vitu vya kawaida , kadri siku zilivyokwenda tulizidi kufahamiana nilimwambia kuwa nina saluni yangu, alinitumia vocha na mwisho alliniambia anataka kuja kupajua ofisini kwangu, nilimuelekeza akawa anakuja kutengeneza nywele, akitoa 10,000/= nikimrudishia chenji ananiambia “ utakunywa soda “ , 

siku nyingine anafika ofisini kwangu ananipa hela anaondoka. Nikaanza kuwa na mawazo juu ya huyu mama lakini sikupata jibu. 11 Siku moja akanipigia simu akaniambia anataka kufungua saluni yake, kwa hiyo angeomba tukutane Cape Town Bar tuongee mimi na yeye. Ilikuwa siku ya Jumapili, wateja walikuwa wengi alinisubiri kama saa moja akanipigia kuniulizia nimekwama wapi? 

Nikamwambia bado nina wateja , akaniambia funga saluni njoo nikulipe hela ya siku hiyo yote. Nilifika pale akaniagizia kinywaji na baada ya hapo akatoa shilinge 50,000/= . Nilishindwa kumuelewa huyu mama akaanza kunihoji naishi na nani, nikamwambia naishi na watoto wangu watatu, baba yao baba yao amefariki miaka miwili iliyopita . Nikamuuliza saluni anataka kufungulia wapi? Akanijibu achana kwanza na mambo na mambo hayo tutaongea baadaye . 


Tuliendelea kunywa hadi saa mbili usiku nikamwambia nawawahi watoto wangu nyumbani akaniambia nitakupeleka na gari, kusema kweli sikuelewa nia yake ni nini hivyo hata nyumbani kwangu sikutaka apajue. Nilimuaga tena kwa mara ya pili akaniruhusu , kesho yake aliniletea viroba vya unga na mchele akavishusha saluni kwangu, akaniambia atanipigia simu , kesho yake aliniletea viroba vya unga na mchele akabishusha saluni kwangu , akaniambia atanipigia simu kesho yake kuna kitu anataka kunieleza. Nilianza kupata hofu, ilibidi niwaeleze rafiki zangu wa karibu , ushauri walionipa waliniambia usikubali kutoka naye kwenda popote mbali ya pale Buza kwa sababu nia yake hatueielewi.

Kesho yake akafika pale bar akanipigia simu, nikaenda ila nikapanga na rafiki yangu mmoja anifuate pale . Alipokuja nilitoa hela ili nimuagizie kinywaji, Yule mama alinizuia akatoa hela na kumuambia muhudumu alete kinywaji ila alimuomba Yule rafiki yangu akae meza nyingine. Kusema kweli alizidi kunichanganya, sikumuelewa. 12 Yule rafiki yangu alikunywa bia ya kwanza na ya pili na akaja kutuaga akaondoka. Nilimtumia meseji kuwa asicheze mbali. Baada ya kama lisaa limoja hivi alipigiwa simu, akaniaga akatoa Sh. 10,000/= akanibusu akaondoka. Yaani hapo ndio alinifanya niwe na mawazo sana, nikaenda kuwahadithia wenzangu wengine wakasema labda ni msagaji, wengine wakasema ametokea kukupenda tu au anataka kaka yake akuoe. Kesho yake akaja na dereva mwanamke, binti mdogo mwenye umri kati ya miaka 20 au 25, akaniambia nimsindikize mjini nikamchagulie nguo za biharusi mtarajiwa. Tukaondoka wote hadi Kariakoo, akamwambia Yule dada apaki gari pembeni ili akajisaidie, Yule binti akajitambulisha kwangu kuwa anaitwa Angel, akaniuliza huyu mama mmeanza kufahamiana toka lini, nakamwambia yapata mwezi mmoja sasa. Nikamuuliza mbona unaniuliza hivyo akaniambia nilikuwa nakuuliza tu. Akaniuliza unajishughulisha na nini , nikamwambia nina saluni na ni mc, akaniomba namba ya simu, Yule mama alipokuja akatuuliza mlikuwa mnaongea nini? Mimi nikamjibu kuwa dereva wako ananiuliza ile saluni ni yangu au nimeajiriwa ? Tukaja mpaka mtaa wa Tandamti akamwambia apaki gari atusubiri, tukaanza kuingia madukani, badala ya kutafuta nguo ya bi harusi akawa ananiambia mimi nichague nguo niliyo ipenda nikawa namkatalia , tukaja mpaka mtaa wa Agrrey kuna duka linauzwa nguo za kutokea usiku, tukaingia pale kuna nguo nzuri tuliikuta inauzwa 120,000/= akaniambia niichukue nikakataa, tulipotoka nje kuna kaka alikuwa anauza viatu simple akaniambia nichague nikaona nisimkatishe tama nikachagua naye akachagua , Mara ikaingia meseji kwenye simu yangu , meseji ilikuwa 13 inasema hivi “ Huyo mama unamtambua vizuri au haumtambui, ni msagaji mzuri poleAunty nakuhurumia, “ by Angel . 

Kwa kweli nilishtuka nikahisi nazimia , akaniambia mbona umesoma sms ukaonekana umeshtuka . Nikamwambia kaka yangu amenitumia sms mtoto wake anaumwa sana.Akaniambia twende nikupeleke , akili yangu ilishahama, nilimuambia tu hapana acha niende nikapande daladala niwahi hospitali. Alitoa shilingi 10,000/= akanipa kama nauli,  nilitoka speed mithili ya mshale, nilivuka mtaa wa uhuru, nusu nigongwe na gari, sikuamini macho yangu, nilifungua tena ile sms nikaisoma , ghafla akanitumia vocha ya sh. 5000/= na ujumbe uliosema “ I love you baby “ Nilipofika nyumbani nikawapigia rafiki zangu simu nikawaeleza, walishtuka sana, wengine waliniambia namsingizia . 

Rafiki yangu Hawa akanishauri nibadilishe laini siku hiyo hiyo na pale saluni nisikae. Nikanunua laini mpya , nikaenda kutafuta kazi ya saluni Yombo pale kwangu nikaweka msichana. Nikamwambia mtu yoyote akiniuliza amwambie nimesafiri na simu sina. Na kweli huyo mama alikuwa anakuja mara kwa mara saluni kwangu kuniulizia , lakini hakupata mafanikio yoyote. Matokeo yake niliamua kuhama nikapangisha nyumba yangu nikahamia Tandika nyumbani kwetu. Nilicho hofia ni kwamba kwa sababu nilishakula pesa yake nyingi, angefikia kunitaka kimapenzi, matokeo yake ningemkatalia angeweza kunifanyia chochote..

JE  KITU  GANI  KILITOKEA ? ILIKUA  KUWAJE  HADI  ZUWENA  AKAAMBUKIZWA  UKIMWI  NA  MWANAMKE  MSAGAJI ?

PATA  NAKALA  YA  KITABU  CHAKO  “ Mwanamke  Msagaji  Ameniambukiza  Ukimwi “.

Andika  barua  pepe  :  restitutamashauri@gmail.com

AU  WASILIANA  NA  WASAMBAZAJI  WA  KITABU  HIKI  KWA  SIMU

0766101669

MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZNAIA AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA NCHI ZA G77+CHINA NCHINI BOLIVIA

$
0
0
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza katika mkutano wa maadhimisho ya miaka 50 ya nchi za G77 na China, uliofanyika jijini Santa Cruz, Bolivia jana Juni 15, 2014. Picha na OMR. 
  Sehemu ya washiriki na wawakilishi wa viongozi wa mataifa mbalimbali katika mkutano huo. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa pili kushoto mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wenzake waliohudhuria na kuzungumza katika mkutano huo wa sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya nchi za G77 na China uliofanyika jana Juni 15, 2014, jijini Santa Cruz, Bolivia. Picha na OMR
baadhi ya Viongozi kutoka mataifa mbalimbali wakati wa ufunguzi wa maadhimisho hayo yaliyofanyika juzi usiku Juni 14, jijini Santa Cruz, Bolivia.

JUNI 15, 2014: ST CRUZ DE SIERRA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ameiwakilisha Tanzania katika maadhimisho ya miaka 50 ya nchi za G77+China yaliyofanyika katika jiji la St Cruz de Sierra nchini Bolivia. Mara baada ya kuwasili nchini hapa, ujumbe wa Mheshimiwa Makamu wa Rais ambao pia umeambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mahadhi Juma Maalim na Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi ulipokelewa na Meya wa jiji la St Cruz de la Sierra Percy Fernandez.

Maadhimisho haya yanafanyika hapa St Cruz mji wa Kibiashara nchini Bolivia ikiwa ni kutokana na nchi hii kukatia kiti cha Uenyekiti wa nchi za G77 kuanzia Januari 2014 nafasi ambayo watadumu nayo kwa mwaka mmoja kabla ya kuchukuliwa na Afrika Kusini. 

Sherehe hizi za kundi hili kubwa la wanachama ndani ya Umoja wa Mataifa zinahudhuriwa na zaidi ya wakuu wa nchi 20 sambamba na viongozi wa juu wa nchi hizo, huku zikiwa na lengo la kuendeleza msimamo wa pamoja kuhusu tathmini ya Malengo ya Milenia ambayo yanafikia kikomo mwakani. Pia mkutano huu una shabaha ya kubuni malengo mapya ambayo yatasaidia wananchi wa nchi hizi ambazo nyingi  ni zile zinazoendelea pamoja na zile zilizo na uchumi wa chini duniani kuhakikisha kuwa Malengo ya Milenia baada ya mwaka 2015 yanaangaza uhalisia wa maisha ya wananchi wa nchi hizi na kuwasaidia kukabiliana na umaskini na kuwa na maendeleo endelevu.

Akizungumza katika sherehe za ufunguzi wa maadhimisho haya, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon alizitaka nchi hizi kujivunia hatua waliyofikia na akaeleza kuwa, kupitia umoja huu familia ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa imefanikiwa kufanikisha agenda zake nyingi zinazolenga kuwasaidia maskini na kwamba kupitia umoja huu Umoja wa Mataifa umeweza kufanya kazi kirahisi kwa kuzingatia uhalisia baina ya wanachama wake. Pia alisisitiza kuwa G77+China ni sauti ya wanyonge katika dunia na kama utaendelea kudumishwa basi wananchi maskini wataendelea kupata sehemu ya kutolea kilio chao.

Kwa upande wake Rais wa sasa wa Baraza la 68 la Umoja wa Mataifa, John Ashe alisema maadhimisho haya ya miaka 50 ni ishara kuwa nchi hizi zimetoka mbali na bado zina mengi zinazohitaji kuyaona yakifanyika na ili kurahisisha mafanikio ipo haja kwa nchi za kundi hili kutanua masoko na mitaji ili kukabiliana na changamoto mpya zikiwemo za mabadiliko ya tabia nchi, umaskini na kuondosha migogoro duniani.

Akifungua maadhimisho haya Rais wa Bolivia Evo Morales alizungumzia ukandamizaji baina ya nchi tajiri dhidi ya maskini na akafafanua kuhusu minyororo ya ubepari inavyokwamisha maendleo ya nchi maskini huku akizitaka nchi za kundi hili kushirikiana kwa dhati katika kukabiliana na changamoto zinazozikabili sambamba na kuwa na mipango endelevu yenye kulenga kuleta tija kwa wananchi wa nchi hizo. 

Rais huyo pia alitumia nafasi hiyo kushukuru viongozi mbalimbali waliohudhuria maadhimisho haya na kueleza kuwa, nchi yake imefurahi kupata heshima ya kuwa mwenyeji wa maadhimisho haya huku akieleza pia kuwa, Bolivia itabakia mwananchama mtiifu wa kundi hili na itashiriki kikamilifu katika kupigania haki za G77+China ndani ya Umoja wa Mataifa na nje ya umoja huo.

Umoja wa nchi za G77 na China ulianzishwa mwaka 1964, na unajumuisha nchi nyingi zaidi katika wanachama wa Umoja wa Mataifa. Ndani ya Umoja huu kuna nchi zilizoendelea na zinazoendelea lakini zinabaki kuwa katika G77+China kufuatia kuwa na mahusiano na changamoto zinazofanana katika siasa ya dunia, sambamba na kuwa na mtazamo unaokaribiana na urafiki wa karibu wa kihistoria baina ya nchi hizi.
 
Sherehe za maadhimisho ya miaka 50 zilipambwa na nyimbo za kuusifu umoja huu pamoja na makaribisho kwa washiriki nchini Bolivia, huku Rais Morales akitumia nafasi hiyo kuzungumza na kila kiongozi wa ujumbe kutoka kwa nchi wanbachama na kusisitiza kuhusu ushirikiano baina ya nchi hizi.

RAIS KIKWETE ATEMBELEWA NA VIONGOZI WA CCM WA LUDEWA LEO IKULU DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe 92  kutoka  jimbo la Ludewa mkoani Njombe  ambao ni  wenyeviti kata na makatibu kata wa CCM  kutoka kata zote 25  za  jimbo la  Ludewa na viongozi  wa  wilaya wa chama hicho ambao  leo Juni 16, 2014 wanahitimisha  ziara  ya  siku nne ya mafunzo mjini  Dodoma na Dar es Salaam. Wajumbe hao pamoja na Mbunge wa jimbo la Ludewa Mhe Deo Filikunjombe walifika Ikulu kumtembelea Rais. (Picha na Ikulu)

MISS IRINGA KUFANYIKA JUNI 20

$
0
0
10Redds Miss Iringa 2013 Neema Mality akiwaongoza washiriki wa 2014 katika mazoezi yanayofanyika katika hotel ya Gentle Hill.1Baadhi ya washiriki wa redds miss iringa wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mazoezi katika ukumbi wanakofanyia mazoezi hotel ya Gentle Hill iliyoko mkoani Iringa.
………………………………………………………
Na Denis Mlowe,Iringa
 
HATIMAYE kinyang’anyiro cha kumsaka Redds Miss Iringa kinatarajia kufanyika Juni 20 mwaka huu baada ya aliyekuwa mratibu wa kwanza Mohamed Mcholeka kutoweka katika mazingira ya kutatanisha na kushindwa kufanyika Juni 6 kama lilivyopangwa mwanzoni na Tanzania Daima kuwa la kwanza kuripoti kuhusiana kutoweka kwa shindano hilo.

 
Waandaji wa Redds Miss Tanzania chini ya Lino Agency Hashim Lundenga baaada ya kugundua hilo wamempatia kibali cha kuandaa shindano hilo ambalo lilikuwa linasubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa tasnia ya urembo na kwasasa Redds Miss Iringa imepata mratibu mwingine ambaye ni kutoka kampuni ya Chakudika Intertainment chini uongozi wake Victor Chakudika ambaye ni Meneja wa kituo cha radio ya Nuru Fm ya mjini Iringa.
 
Akizungumza na Tanzania Daima ofisini kwake jana Mkurugenz wa kampuni hiyo, Victor Chakudika alisema maamuzi ya kuandaa shindano la Redds Miss Iringa kwa lengo a kutopoteza vipaji vya mabinti waliokuwa tayari kushiriki shindano hilo na kuondoa aibu ya mkoa wa Iringa kutopelekwa mwakilishi katika shindano la Redds Nyanda za Juu ambako wamekuwa wakishiriki kila mwaka.
 
Alisema kuwa shindano la Redds Miss Iringa limekuwa chachu ya ajira kwa mabinti wengi mkoani hapa kwa kuweza kutangaza vipaji vya washiriki wanaojitokeza kushiriki kila mwaka.
 
Chakudika alisema shindano hilo linatarajia kuwa la kisasa kutokana na maandalizi yake kuendelea vyema na kuwataka wadau wa tasnia ya urembo ujitokeza kwa wingi katika ukumbi wa St. Dominic likalofanyika shindano hilo.
 
“Kwa kweli baada ya mratibu wa kwanza kukimbia kutokana na gharama za uandaaji niliamua kuchukua jukumu hilo kulikomboa shindano hilo lifanyike na warembo wengi wamejitokeza kushiriki miss iringa” alisema Chakudika.
 
Aliongeza kuwa hadi sasa warembo 12 wamejitokeza kushiriki shindano hilo na wanaendelea na mazoezi katika ukumbi wa Hotel ya Gentle hill ya mjini hapa.
 
Aidha msanii Mo Music anayetamba na wimbo wake wa ‘Basi Nenda’ anatarajia kutoa burudani kali katika shindano hilo ,wasanii wengine chupukizi wa mjini Iringa, vikundi vya sanaa, Wakali wa Kudance wa mjini Iringa.
Aliwataja wadhamini wa shindano hilo licha ya TBL kupitia kinywaji chake cha Redds, wengine ni Nuru Fm, kampuni mpya ya mabasi ya Sutco High Class, Gentle Hills na kuwataka wadau zaidi kujitokeza  kudhamini shindano hilo.

RAIS KIKWETE ATETA NA WASANII DODOMA

$
0
0
D92A1853
D92A1860
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana  na msanii wa kizazi kipya Nasib Abdul “Diamond”ikulu ndogo mjini Dodoma wakati chakula cha usiku alichowaandalia wasanii walioshiriki katika tamasha la Uzalendo na Uzinduzi wa Video ya wimbo maalum wa miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lililofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma jumamosi.Kulia ni mbunge wa Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete.
D92A1891
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza kwa makini mwanamuziki wa kizazi kipya Ommy Dimpoz wakati chakula cha usiku alichowaandalia wasanii walioshiriki katika tamasha la Uzalendo na Uzinduzi wa Video ya wimbo maalum wa miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lililofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma jumamosi iliyopita kulia ni Mh. Ridhiwani Kikwete Mbunge wa jimbo la Chalinze(picha na Freddy Maro).

GEITA GOLD MINE – KILIMANJARO CHALLENGE FLAG OFF

$
0
0
1
The Minister for Tourism and Natural Resources, Hon. Lazaro Samuel Nyalandu with the two children from Moyo wa Huruma Orphanage Centre who will join other climbers locally and internationally for the Kilimanjaro Challenge 2014 which has been sponsored by Geita Gold Mine (GGM) in partnership with Tanzania Commissions for AIDS (TACAIDS) joined by Mrs. Faraja Nyalandu, Dr. Fatma Mrisho, Executive Director of TACAIDS and the climbers at the Flag Off Ceremony in Moshi to raise funds to fight against HIV/AIDS in Tanzania.2Kili Challenge climbers as they hope to reach Uhuru Peak so as to raise funds to fight against HIV/AIDS in Tanzania.3Kili Challenge Ambassadors from Scotland Rugby team Mr. Rory Lawson and Mr. Dave Callam joined by Ms. Fatma Fernandes Managing Director of Abel & Fernandes Communications at the Flag Off Machame Gate in Moshi, Tanzania for the Kilimanjaro Challenge 2014 which has been sponsored by Geita Gold Mine (GGM) in partnership with Tanzania Commissions for AIDS (TACAIDS) to raise funds to fight against HIV/AIDS in Tanzania..
………………………………………………………………………
Geita Gold Mine (GGM) in partnership with Tanzania Commission for AIDS (TACAIDS) officiated yet another year of the Flag-Off of the Kilimanjaro Challenge at Machame Gate in Moshi. The Kili Challenge Flag-Off ceremony was officiated by Hon. Lazaro Samuel Nyalandu the Minister for Tourism and Natural Resources in the presence of Kilimanjaro Regional Commissioner Hon. Leonidas Gama and Moshi District Commissioner Hon. Dr. Ibrahim Msengi.
This year marks the 13th historic climb for this noble course with more than 500 individuals from all across the world participating in Kilimanjaro Challenge and its impact is tangibly seen amongst our communities. The Kilimanjaro Challenge is an annual activity that aims to raise funds from different partners through sponsorship of climbers to Mount Kilimanjaro and to distribute the funds to relevant charities fighting HIV/AIDS in Tanzania.
During his flag-off speech at Machame in Moshi, the Hon. Lazaro Samuel Nyalandu said, “This year’s climb began in Dar es Salaam in early May this year where our President H.E. Hon. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, officially launched the beginning of this great journey of which today we are witnessing. The biggest message we take from this climb today is determination, zeal and hope. 
These three can take us to a higher elevation in this fight. With the zeal, hope and determination you have shown us that Tanzania without HIV/AIDS is possible. The government would like to applaud this initiative by Geita Gold Mine (GGM) and Tanzania Commission for AIDS (TACAIDS) as the Kili HIV/AIDS Challenge has contributed towards raising awareness on the HIV/AIDS pandemic and is supporting the Tanzanian government’s national initiatives towards zero new infections, zero stigma incidences and zero mother to child infections so that as a country we meet the Millennium Development Goals.”
According to the Executive Director of TACAIDS Dr. Fatma Mrisho, “What our climbers will achieve in the next 7 days will be a monumental task in our national struggle to tame the deadly scourge. It is this kind of involvement to our society, youth in particular, and realization that HIV/AIDS can be mitigated that will take our country to an ultimate success of seeing Tanzania free of the HIV/AIDS Challenge. It can be done if each and every one of us plays our part. 
Approximately 1.6 million people in Tanzania are living with HIV/AIDS and about 86,000 new infections every year. This pandemic is mostly affecting the youth of Tanzania and the disease has orphaned 1.3 million children. We need to change this therefore TACAIDs in collaboration with Geita Gold Mine and other various stakeholders through Kilimanjaro Challenge, we will continue to provide financial support in order to fight against this pandemic.”  She continued to say, “We hope to build a national team spirit in the fight against this menace and I urge other stakeholders from local and international investors to come forward, join us and contribute to the Kilimanjaro Challenge fund so that we can meet our dream of having a zero free generation from HIV/AIDS.”
Speaking in regard to the flag-off ceremony, the Managing director for Geita Gold Mine Mr. Michael Van Anen said “GGM is proud to be part of this initiative where various companies which are working locally, could join forces and participate in this noble course. GGM leads this initiative by establishing relationships and mobilizing key likeminded partners to raise funds, sponsor individual climbers, or donate through an auction for this cause. Currently in its 13th year, the difference in life changing in the communities is enormous and we are looking forward for an HIV/AIDS zero Tanzania in the near future.” He continued to say, “I would like to urge anyone who would like to join us to visit www.geitakilichallenge.com and see how they can be part of this great initiative.”
AngloGold Ashanti Sustainability Vice President Mr. Simon Shayo said “More than 600 people from different parts of the world have participated to climb Mt. Kilimanjaro for the Kilimanjaro Challenge initiative which has raised in excess of US$500,000 per annum. For the 2014 our heroic determined climbers we say bravo to you all! We highly commend you for deciding to undertake this challenge for a good course and for fulfilling your dreams. 
You are set out to conquer the highest mountain in Africa, Mt. Kilimanjaro, not for fun but as a way demonstrate your solidarity with the rest of Tanzania and the World in responding to the challenge of HIV/AIDS, and in particular your devotion sends a message of care and love for those affected in one way of another by HIV/AIDS as well as reaffirming our duty and commitment to fight HIV/AIDS in Tanzania. In reality HIV/AIDS affect us all, it affects humanity in its entirety.”
Geita Gold Mine and TACAIDS using the umbrella of Kilimanjaro Challenge is playing a pioneering role in the awareness on the HIV/AIDS pandemic and look forward for the day when Tanzania will be declared Zero HIV and AIDS infection as it is reported that Tanzania’s prevalence rate has gone down from over 13% in 2000 to 7.8% by 2007 and as low as 5.1% today. Let us all rise up to join the fight against HIV/AIDS to get to Zero on HIV and AIDS: Zero New Infections, Zero Stigma and Zero AIDS related deaths.

UN KUZINDUA MFUMO MPYA WA KUHABARISHA UMMA NDANI YA TAMASHA LA ZIFF 2014 JIONI HII

$
0
0
un1
Ofisa habari wa Kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vusso (kushoto) akionesha taarifa ya Umoja wa Mataifa ya utekelezaji wa mpango wa pamoja wa mashirika ya Umoja wa mataifa hapa nchini. Taarifa hiyo imo katika documentary (taarifa ambayo iko katika mfumo wa video) ya dakika saba inayoonyesha kazi mbalimbali Umoja wa Mataifa nchi itazinduliwa leo kwenye ukumbi wa Ngome Kongwe kuanzia saa moja jioni katika mpango wa Umoja wa Mataifa wa kutumia mitandao ya kijamii kuwafikia wadau wake wa maendeleo.(Picha na Zainul Mzige wa Mo Blog).
Un2
Mkuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini Anna Liboro Senga (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo kuhusu uzinduzi wa mfumo mpya wa utoaji wa taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa wadau wake.Mpango huo unazinduliwa leo jioni katika ukumbi wa wazi wa Ngome Kongwe. Kushoto ni Ofisa habari wa Kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vusso .(Picha na Zainul Mzige wa Mo Blog)

MKUU WA WILAYA YA MAKETE ATOA RAI KWA JAMII YA MAKETE KUSAIDIA WATOTO YATIMA NA WAISHIO KWENYE MAZINGIRA HATARISHI

$
0
0
 Mkuu wa wilaya ya Makete mwenye suti nyeusi (aliyesuka nywele) Mh. Josephine Matiro, mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu Helen Kijo Bisimba (kulia kwa mkuu wa wilaya) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto walioshiriki maadhimisho hayo.
 Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro(wa tatu kushoto walioketi) na Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu Helen Kijo Bisimba (wa pili walioketi kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa shirika la wasaidizi wa kisheria Makete
 Katika picha ya pamoja na wanafunzi wa sekondari ya Iwawa Makete ambao nao walishiriki
 Wanafunzi wa shule ya msingi Ndulamo wakiwa katika picha ya pamoja.(Picha/habari na Edwin Moshi na Conrad Mpila, Makete.)
Imeelezwa kuwa ni jukumu la kila mmoja kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi, na si kuiachia serikali ama mashirika yasiyo ya kiserikali peke yao kufanya kazi hiyo
Kauli hiyo imetolewa leo hii Juni 16 na mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika kitaifa (kwa asasi zisizo za kiserikali) katika viwanja vya mabehewani kata ya Iwawa wilayani Makete mkoani Njombe.
Hata hivyo mkuu wa wilaya hiyo amekiri kuwepo kwa changamoto ya watoto walio wengi Wilayani Makete ambao ni Yatima na waishio katika mazingira magumu ambao wanahitaji msaada wa kila mmoja

"Ni kweli wilaya ya Makete ina watoto ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi, wengine wanalelewa katika vituo maalum vilivyopo wilayani mwetu, hivyo ni jukumu letu kuwasaidia kila mtu kwa kadri ya uwezo wake, mwenye sabuni, kalamu, fedha ama chochote anaweza kufanya hivyo kwa wakati wake" amesema Matiro

Katika risala iliyosomwa na mwanafunzi Gaudencia Malangalila wa Shule ya msingi Ndulamo kwa niaba ya wanafunzi wenzake amesema Kuwa watoto walio wengi wanakabiliwa na unyanyasaji kwa kufanyishwa Kazi ngumu na hatarishi,kutopata haki katika huduma za matibabu,walezi kunyang'anya misaada wanayopewa na wadau mbalimbali

Naye Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) Bi. Helen Kijo Bisimba amesema Kuwa kwa Tafiti alizofanya amebaini Kuwa kuna watoto ambao waliondoka kwenda nje ya Makete kwa kufanya Kazi na hawarudi tena huku wazazi hawajui Kama wapo hai au la,kwani hata mawasiliano na wazazi ama walezi wao bado ni magumu.
Hivyo amewasihi wazazi/walezi Kuwa makini na watoto wao pindi wanapoitwa kwenda kufanya Kazi maeneo ya mbali kwani mara nyingi huko wanakokwenda wanakutana na mambo ambayo ni kinyume na walioyatarajia.

Katika maadhimisho hayo kikundi cha wazazi kutoka Kijiji cha Isapulano na Ndulamo Maarufu Kama mama mkubwa wamesema Kuwa vikundi hivyo vitaendelea Kulinda haki za watoto na kutoa ujumbe kwa jamii kwa njia ya sanaa  na kufanya uchunguzi dhidi ya watoto wanaofanyiwa unyanyasaji na watatoa taarifa katika ngazi husika na wakigundulikaa wahusika wachukuliwe hatua za kisheria
 Kauli mbiu ya mwaka huu ni "kila mtoto ana haki ya elimu bora bila vikwazo" 

PPF YATOA HUDUMA Wiki ya Utumishi Mnazi Mmoja Dar

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (Utawala Bora), George Mkuchika, akisalimiana na Meneja Kumbukumbu wa Mfuko wa Pesnheni wa PPF, Gladness Mteta, alipotembelea banda la PPF, kwenye maonyesho ya wiki ya Utumishi yaliyoanza jana kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika, akimsikiliza Meneja Kumbukumbu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Gladness Mteta (Wakwanza kushoto), alipotembelea bandfa la Mfuko huo kwenye ufunguzi wa Wiki ya Utumishi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Jumatatu Juni 16, 2014
Maafisa wa PPF wakihudumia wateja kwenye maonyesho ya wiki ya utumishi kwebnye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Maafisa wa Mfuko wa Pesnheni wa PPF, wakiongozwa na Meneja wa Kumbukumbu, Gladness Mteta (Wapili kushoto), Sereki Michael (Wakwanza kushoto), Paulina Msanga na Nelusigwa Mwalugaja, wakisubiri kuhudumia wateja kwenye banda lao wakati wa ufunguzi wa wiki ya Utumishi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Juni 16, 2014.

Waziri Mkuchika: Tanzania ni nchi ya pili Afrika Mashariki kwa Utawala Bora na Vita dhidi ya Rushwa

$
0
0
Mgeni Rasmi kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika akizungumza kuzindua Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salam.

Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma Hab Mkwizu akizungumza wakati akimkaribisha Mgeni Rasmi kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salam.
Baadhi ya watumishi wa Umma wakifuatilia Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyoanza leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salam.
Brass Band ya Jeshi la Polisi ikiongoza maandamano ya Maadhimishi ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salam.
Watumishi kutoka Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wakipita mbele ya meza Kuu wakati wa Maandamano Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyoanza leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salam.
Afisa Habari wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Robi Bwiru akimueleza jambo mmoja wa wananchi waliotembelea banda la Wizara hiyo wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salam.
Baadhi ya wananchi wakipata maelezo kuhusu shughuli zinazofanywa na Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki , wakati walipotembelea banda la Wizara hiyo. Picha na Hussein Makame-MAELEZO  .

=======  =======  =======
Hussein Makame-MAELEZO

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora, Kapteni Mstaafu George Mkuchika amesema kuwa Tanzania inashika nafasi ya pili kati ya nchi tano za Shirikisho la Afrika Mashariki katika suala la Utawala Bora na vita dhidi ya Rushwa.


Waziri Mkuchika amayasema hayo wakati akizindua Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.


Alisema kuwa tangu Serikali ya Awamu ya Kwanza, Serikali ya Tanzania ilitangaza vita dhidi ya Rushwa na imekuwa ikiimarisha mapambano dhidi ya adui huyo hadi katika Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais Jakaya Kikwete.


“Katika nchi za Afrika Mashariki suala la Utawala Bora na Vita dhidi ya Rushwa, Tanzania tunashika nafasi ya pili, Rwanda ni ya kwanza, ya tatu ni Uganda na ya nne ni Kenya” alisema Waziri Mkuchika. Waziri Mkuchika alikuwa akizungumzia madai yanayotolewa na baadhi ya watu hapa nchini kuwa Serikali ya Tanzania haina dhamira ya kupambana na Rushwa.

Alikanusha madai hayo na kusema kuwa Serikali ya Tanzania ina dhamira ya kupambana na Rushwa ndio maana imepitisha Sheria dhidi ya Rushwa,Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) ina matawi kila mkoa na kila wilaya.


Alisema  kiashiria kingine cha kuthibitisha kuwa Serikali ya Tanzania inapamabana na Rushwa ni kufikishwa mahakamani kwa watu wanaotuhumiwa na Rushwa. Hata hivyo, alibainisha kuwa mtumishi wa Takukuru hawezi kuwafikisha watu mahakamani bila ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi.

Hivyo aliwataka Watanzania wote kutambua kuwa wana wajibu wa kupambana na rushwa kwa kutoa taarifa kwa mamlaka husika ili kufanikisha vita hiyo dhidi ya Rushwa. Waziri Mkuchika aliwakumbusha Watanzania kuwa mtumishi yeyote wa umma kumhudumia mwananchi ni haki yake, hivyo mtumishi anayeomba Rushwa ili atoe huduma anashiriki katika tendo la Rushwa. Kutokana na hali hiyo, aliwaomba watumishi wajiepushe na Rushwa kwani Rushwa inawanyima watu haki, kukiwa na malalamiko anayepata haki ni yule anayetoa Rushwa.

Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ya mwaka huu inasema “Mkataba wa Misingi na Kanuni za Utumishi wa Umma Barani Afrika ni Chachu ya Kuimarisha Utawala Bora na Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazi”.

MSANII AY NA MREMBO FARAJA KOTTA NYALANDU WATEULIWA KUWA MABALOZI WA UNICEF.

$
0
0
Mrembo aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania ,Faraja Kotta Nyalandu akiwa na msanii wa muziki wa Bongo Fleva Ambwene Yesaya "AY"katika viwanja vya hosptali ya wilaya ya Hai.
Mwakilishi wa Unicef Tanzania Dk Jamal Gulaid akiwatangaza Mrembo aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania ,Faraja Kotta Nyalandu akiwa na msanii wa muziki wa Bongo Fleva Ambwene Yesaya "AY kuwa mabalozi wa UNICEF katika kampeni ya Tokomeza Ukatili dhidi ya watoto.
Mrembo aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania ,Faraja Kotta Nyalandu akiwa na msanii wa muziki wa Bongo Fleva Ambwene Yesaya "AY" wakati wa kutangazwa kuwa mabalozi wa UNICEF.
Mwakilishi wa Unicef Tanzania Dk Jamal Gulaid akimkabidhi barua ya uteuzi Mrembo aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania ,Faraja Kotta Nyalandu ya kuteuliwa kuwa balozi wa UNICEF katika kampeni ya Tokomeza Ukatili dhidi ya watoto.
Mwakilishi wa Unicef Tanzania Dk Jamal Gulaid akimkabidhi barua msanii wa muziki wa Bongo Fleva Ambwene Yesaya "AY" ya kuwa balozi wa UNICEF katika kampeni ya Tokomeza Ukatili dhidi ya watoto.
Mabalozi wa UNICEF ,Faraja Kotta Nyalandu na Ambwene Yesaya "AY wakijadiliana jambo muda mfupi baada ya kutangazwa kuwa mabalozi wa UNICEF katika kampeni ya Tokomeza Ukatili dhidi ya watoto.


Mrembo aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania ,Faraja Kotta Nyalandu akizungumza mara baada ya kuteuliwa balozi wa UNICEF katika kampeni ya Tokomeza Ukatili dhidi ya watoto.
Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Ambwene Yesaya ."AY" akizungumza mara baada ya kuteuliwa balozi wa UNICEF katika kampeni ya Tokomeza Ukatili dhidi ya watoto.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Hai,Clement Kwayu akiteta jambo na Mrembo aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania ,Fraja Kotta Nyalandu muda mfupi baada ya kutangazwa balozi wa UNICEF.
Msanii Oscar Peter maarufu kama Oscer Nyerere akitoa burudani kwa wananchi wa wilaya ya Hai(hawako pichani)wakati wa sherehe ya kutangazwa kwa mabalozi wa UNICEF.
Mrembo aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania ,Fraja Kotta Nyalandu akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa kupambana na ukatili wa wanawake na watoto.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Hai,Clement Kwayu akimzungumzia Mrembo aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania ,Fraja Kotta Nyalandu kuhusu kitabu chake alichozindua hivi karibuni.

Katika kusherehekea siku ya Mtoto wa Afrika tarehe 16 Juni, Halmashauri ya Wilaya ya Hai, ikishirikiana na viongozi wa serikali, UNICEF na Save the Children, imezindua Kituo cha Huduma Jumuishi, kitakachowasaidia wanawake na watoto ambao wameathiriwa na ukatili.


“Katika kituo hiki, huduma za kuwasaidia wahanga wa ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto ikiwa ni pamoja na huduma za afya, msaada wa kisaikolojia, ulinzi/usalama na msaada wa kisheria vinaweza kutolewa hapo katika eneo moja ndani ya kituo cha afya zikiwa zimeratibiwa vizuri Zaidi,” alisema Charles Pallangyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. 


Aliongeza, “kituo hiki kitasaidia kupunguza madhara zaidi ya ukatili kwa sababu wahanga wa ukatili wataweza kupata huduma zote muhimu katika eneo moja na hawatakuwa na sababu ya kurudiarudia kuwaeleza watoa huduma mbalimbali walio katika maeneo tofauti yale mambo mabaya waliyoyapitia, au kutakiwa kwenda na kurudi kutokana na ukosefu wa uratibu na uwezo wa watendaji wa sekta mbalimbali katika kuwahudumia wahanga wa ukatili kwa ukamilifu.”


Mwakilishi wa UNICEF Tanzania, Dk. Jama Gulaid, anaamini kuwa kama tukifanya kazi kwa ushirikiano na serikali na wadau wengine, tunaweza kupata suluhu katika kumaliza ukatili dhidi ya watoto. “Ukatili dhidi ya watoto uko kila mahali na hatuwezi kuendelea kuufumbia macho. Watoto wote hapa Tanzania wanahaki ya kuishi na kukua katika mazingira yasiyo na ukatili. Kama sisi sote tukifanya kazi kwa kushirikiana pamoja, sina shaka tutaweza kumaliza ukatili dhidi ya watoto.”


Katika tukio hili huko Hai, UNICEF Tanzania imemteua msanii mahiri wa bongo flava Ambwene Yessyah, anayejulikana zaidi kama AY, pamoja na aliyewahi kuwa Miss Tanzania, Faraja Kotta Nyalandu kama Mabalozi wao katika ‘Kampeni ya Tokomeza Ukatili Dhidi ya Watoto.’ Wote wameahidi kusaidia kampeni ya ‘Kampeni ya Tokomeza Ukatili Dhidi ya Watoto’ na wameonyesha kuhamasishwa na heshima hii waliyopewa kutoa sauti zao kutetea ulinzi wa mtoto.


“Nimepewa heshima kubwa kwa kuteuliwa kwangu kuwa Balozi wa UNICEF Tanzania na nitajitoa katika kutumia sauti yangu na umaarufu wangu kusaidia kutokomeza ukatili dhidi ya watoto hapa Tanzania,” alisema AY alipokuwa akikubali wadhifa huo. 


Kwa kuwateua AY na Faraja Kotta Nyalandu kama Mabalozi wa UNICEF Tanzania wa kampeni ya ‘Kampeni ya Tokomeza Ukatili Dhidi ya Watoto’, UNICEF inategemea kuongeza uzito na muonekano zaidi wa suala la ulinzi wa mtoto katika mijadala inayoendelea kuhusu ukatili dhidi ya watoto na kuonyesha kuwa kuna suluhisho la tatizo hili.

 Kama mwazo wa kazi yao katika shughuli za UNICEF Tanzania, AY na Faraja Kotta Nyalandu walitembelea Dawati la Jinsia na Watoto katika kituo cha Polisi cha Hai kuona wenyewe kazi inayofanywa kusaidia wanawake na watoto waliofanyiwa au kuathiriwa na ukatili. 


Utafiti juu ya Ukatili Dhidi ya Watoto, uliozinduliwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto mwaka 2011, unaonyesha mambo yanayopelekea uhatarishi wa watoto kwenye ukatili kimwili na kingono hapa Tanzania – wastani wa msichana 1 kati ya 3 na mvulana 1 kati ya 7 wamefanyiwa vitendo vya ukatili wa kingono, na zaidi ya asilimia 70 ya wasichana na wavulana wamefanyiwa vitendo vya ukatili wa kimwili kabla hawajafikia umri wa miaka 18. Hata hivyo, wahanga wengi hawajamwambia mtu yeyote ukatili waliofanyiwa na ni kesi chache sana zimefikishwa polisi.


Kumekuwa na maendeleo katika kuboresha hali hii. UNICEF inasaidia serikali ya Tanzania kupitia Idara ya Ustawi wa Jamii kuanzisha na kuboresha ‘mifumo ya Ulinzi wa Mtoto’ katika halmashauri 13. 

Katika halmashauri hizi, afya, ustawi wa jamii, polisi, sekta za elimu na mahakama, magereza, wanasheria, asasi za kiraia pamoja na mifumo ya kijamii isiyo rasmi wanaunda Timu ya Halmashauri ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto na wanashirikiana kuhakikisha kuwa kesi za ukatili wa watoto zinashughulikiwa vyema na pia wanazuia ukatili kwa kuongeza uelewa wa jamii juu ya ukatili dhidi ya watoto. 

Lengo la Idara ya Ustawi wa Jamii ni kupanua utaratibu wa mfumo huu katika halmashauri 30 ifikapo mwaka 2016.
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini

INNOCENT MELLECK ASIMIKWA KUWA NAIBU KAMANDA WA UVCCM WILAYA YA MOSHI VIJIJINI.

$
0
0
Innocent Melleck akikaribishwa na chipukizi katika uwanja wa Ghala -Himo wilaya ya Moshi vijijini kwa ajili ya kusimikwa kuwa naibu kamanda wa UVCCM katika wilaya hiyo.
Mbunge wa jimbo la Moshi vijijini Dk Cyril Chami(katikati)akiwa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Moshi vijijini Moris Makoi(shoto kwake)wakati wa shughuli ya kumsimika naibu kamanda wa UVCCM wilaya ya Moshi vijijini.
Mbunge wa jimbo la Moshi vijijini Dk Cyril Chami(katikati) Innocent Melleck ,Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Moshi vijijini Moris Makoi na viongozi wengine wa CCM wakipunga mkono kwa wananchi (hawapo pichani) wakati wa shughuli ya kumsimika naibu kamanda wa UVCCM wilaya ya Moshi vijijini.
Mbunge wa jimbo la Moshi vijijini Dk Cyril Chami akiteta jambo na Innocent Melleck wakati wa shughuli ya kumsimika ku wa naibu kamanda wa UVCCM wilaya ya Moshi vijijini.
Baadhi ya wananchi waliofika katika mkutano huo uliofanyika viwanja vya ghalani Himo.
Mbunge wa jimbo la Moshi vijijini na kamanda wa UVCCM wilaya ya Moshi vijijini Dk Cyril Chami akimvisha vazi maalumu Innocent Melleckak wakati akisimikwa kuwa Naibu kamanda wa UVCCM wa wilaya hiyo.
Mbunge wa jimbo la Moshi vijijini na kamanda wa UVCCM wilaya ya Moshi vijijini Dk Cyril Chami akimkabidhi Innocent Melleckak ngao na mkuki kuashiria kukabidhiwa majukumu ya kuwa Naibu kamanda wa UVCCM wa wilaya hiyo
Naibu kamanda wa UVCCM wilaya ya Moshi vijijini ,Innocent Melleck akiwa katika picha ya pamoja na vijana wa chipukizi muda mfupi baada ya kusimikwa kuwa naibu kamanda wa UVCCM wialaya ya Moshi vijijini.
Mbunge wa jimbo la Moshi vijijini na kamanda wa UVCCM wilaya ya Moshi vijijini Dk Cyril Chami akimuapisha  Innocent Melleckak kuwa Naibu kamanda wa UVCCM wa wilaya hiyo.

Naibu kamanda wa UVCCM wilaya ya Moshi vijijini Innocent Melleck akizungumza mara baada ya kusimikwa kushika nafasi hiyo. 
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.

Ziara ya NHC na wakurugenzi wa Bodi Singapore

$
0
0

PSPF KUENDELEA KUTOA ELIMU KWA UMMA JUU YA MAFAO WAYATOWAYO KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA

$
0
0


Afisa uendeshaji wa mfuko wa pesheni kwa watumishi wa umma 'PSPF'  Bw,Hadji Jamadary kulia  akimpatia maelezo Bw,Arbogast Nzeyimana wakati wa maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma
Afisa uendeshaji wa mfuko wa pesheni kwa watumishi wa umma 'PSPF'  Bw,Hadji Jamadary kulia na ofisa wa mfuko huo Bi, Leila Laizer wakimpatia maelezo Bw,Kambilo Crement wakati wa maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma


Ofisa masoko wa mfuko wa pesheni kwa watumishi wa umma'PSPF' Bi, Rahma Ngassa kulia akimpatia mahelezo mmoja ya wananchi waliofika kutembelea banda lake Bw.Ahmed Sendi wakati wa mahadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma inayoendelea katika viwanja vya mmnazi mmoja Dar es salaam Picha na mpiga picha wetu
--

Afisa wa mfuko wa pesheni kwa watumishi wa umma Bi, Leila Laizerkulia akisalimiana na mtumishi wa manspaa ya Temeke idara ya maendeleo ya jamii Bw.Emanuel Hinjo alipotembelea banda hilo katika mahazimisho ya wiki ya utumishi wa umma katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam

 maandamano
 wafanyakazi wa PSPF wakipita mbele ya mgeni rasmi
banda la PSPF  lilivyo katika viwanja vya mnazi mmoja

BAADHI YA MAOFISA KUTOKA MFUKO WA PESHENI KWA WATUMISHI WA Umma 'PSPF' WAKIWA TAYALI KUWASIKILIZA WATU MBALIMBALI KATIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA WAKATI WA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA.
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images