Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live

MH. LOWASSA AZUNGUMZIA VURUGU ZA BUSERERE,MKOANI GEITA

0
0
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mchungaji Trafaina Aseri Nkya ambaye pia ni msaidizi wa Askofu Mteule wa Dayosisi ya Kusini Mashariki mwa Ziwa Victoria na ujumbe wake walipofika nyumbani kwake eneo la Ngarashi kijijini kwake Monduli, kumshukuru kwa harambee ya ujenzi wa kanisa lao aliyoiendesha Januari mwaka jana na kupatikana kiasi cha shilingi millioni 200 zikiwa ni fedha tasilimu pamoja na ahadi.
ujumbe wa kamati ya ujenzi wa kanisa hilo ukimsikiliza Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (hayupo pichani).
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwasindikizawajumbe hao.
======  ==========  ===
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa, amewataka viongozi wa dini nchini, kusaidia na kurejesha hali ya amani kati ya wasilam na wakiristo ambayo inaonekana inaanza kupotea.

Akizungumza hayo nyumbani kwake Monduli, wakati alipokuwa akipokea ujumbe kutoka kanisa la KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki mwa Ziwa Victoria, Lowassa amesema vurugu na mauaji yaliyotokea huko Buserere, yanasikitisha sana na kuongeza kuwa ni dalili mbaya ya kutoweka kwa amani ya Tanzania.

``Rais ameelezea masikitiko yake, kwa kweli inasikitisha sana, mimi nawaomba viongozi wa dini na madhehubu yote wasimamie na kuzuia mambo haya, nawaomba watanzania wenzangu tusali kwa imani zetu kuomba amani yetu isipotee`` alisema Lowassa kwa masikitikiko makubwa.

Katika fujo hizo za Buserere,mchungaji mmoja wa kanisa la sabato aliuwawa baada ya kuzuka kwa mapigano kati ya waislam na wakristo.Chanzo cha mapigano hayo kilikuwa ni wakristo kuamua kuchinja ng'ombe na kuuza kwenye bucha lao, hatua iliyopingwa na wananchi wa dini ya kiislam kwenye eneo hilo.

Ujumbe huo uliyofika nyumbani kwa Mh Lowassa ukiongozwa na msaidizi wa askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya kusini mashariki mwa ziwa victoria, ulifika kumshukuru kutokana na kusimamia na kuendesha harambee ya ujenzi wa kanisa kuu la Shinyanga January mwaka jana ambapo zaidi ya shillingi millioni 200 zikiwa ni fedha tasilimu pamoja na ahadi zilipatikana.

mbunge amos makalla atembelea jimboni mwake na kutoa msaada.

0
0

 Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla ( kushoto) akiwakabidhi bati 24 kwa viongozi wa CCM Tawi la Kwa Mayambi, kata ya Sungaji ili kuezekea jengo la Ofisi.
 Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla ( kushoto) akikabidhi viti 45 kwa uongizo wa CCM Kata ya Sungaji ili vitumike wakati wa mikutano ya Chama
 Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla ( kulia) akimkabidhi kitabu cha somo la sayansi ikiwa ni sehemu ya vitabu 121 kwa Mkuu wa Sekondari Adrian Mkoba ,Harold Mhando

 Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla ( kati kati) akiwa na baadhi ya viongozi wa kitiuo cha kulea watoto yatima cha Mzumbe pamoja na Diwani wa Kata ya Mzumbe akipotembelea Kituo hicho na kutoa misaada mbalimbali
 Mbunge Amos Makalla akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto yatima wa kituo cha CDTFN kilichopo Kata ya Mzumbe, wilayani Mvomero.
 Baadhi ya walimu wa sekondari Adrian Mkoba pamoja na wanafunzi wa shule hiyo wakimsikiliza Mbunge wao Amos Makalla aliyeteembelea Shule hiyo na kutoa msaada wa vitabu vya masomo mbalimbali , jezi na mipira.
 Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla ( kulia) akimkabidhi fedha sh.360,000 Katibu wa kikundi cha vijana 100 wa Kijiji cha Msufini, Kata ya Hembeti,Victor Thobias, ili kununua mbegu za vitunguu.
 Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla ( wapili kutoka nyuma) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Habari, vijana, Utamaduni na Michezo akiongozana na baadhi ya viongozi wa Kijiji cha Mlaguzi kukagua ujenzi wa Zahanati.

Rais Kikwete ashiriki ibada ya Mazishi ya Marehemu Askofu Mstaafu Jimbo Katoliki Moshi Mhashamu Amedeus Msarikie

0
0


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la Askofu Mstaafu jimbo Katoloki la Moshi Marehemu Mhashamu Amedeus Msarikie wakati wa ibada ya mazishi Iliyofanyika katika Kanisa la Kristu Mfalme mjni Moshi leo. Picha na Freddy Maro wa Ikulu.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Askofu Mstaafu Jimbo katoliki la Moshi,Marehemu Mhashamu Amedeus Msarikie wakati wa ibada ya mazishi Iliyofanyika katika Kanisa la Kristu Mfalme mjni Moshi leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za Mwisho mbele ya jeneza la Askofu Mtsaafu jimbo Katoliki la Moshi Marehemu Mhashamu Amedeus Msarikie wakati wa misa ya Mazishi iliyofanyika katika kanisa na Kristu Mfalme, mjini Moshi leo.

======== ======= ====== =====
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Alhamisi, Februari 14, 2013 ameungana na mamia kwa mamia ya waumini wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Moshi na kutoka sehemu nyingine nchini, kumzika Askofu Mstahivu (Bishop Emeritus) Amedeus Peter Msarikie. 

 Rais Kikwete amewasili kwenye Kanisa Kuu la Kristo Mfalme mjini Moshi kiasi cha saa sita na dakika tano mchana kuungana na marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa na mamia kwa mamia wananchi kwa ajili ya mazishi ya Askofu Msarikie ambaye alifariki dunia Alhamisi iliyopita, Februari 7, 2013 kwa ugonjwa wa saratani katika hospitali moja mjini Nairobi, Kenya. 
 Mara baada ya kuwasili, Rais Kikwete ametia saini kwenye kitabu cha maombolezo na ikaanza ibada ya mazishi ilivyohudhuriwa na mamia kwa mamia ya wananchi wakiwamo maaskofu zaidi ya 20 kutoka majimbo mbali mbali ya Kanisa Katoliki nchini. 

 Mwili wa Marehemu Msarikie uliteremshwa kaburini kiasi cha saa saba na dakika 35 ndani ya Kanisa hilo na Rais Kikwete akaweka udogo kwenye kaburi na baadaye shada la maua.

 Akizungumza kwenye mazishi hayo, Rais Kikwete amemwelezea Askofu Msarikie ambaye alikuwa Askofu wa Jimbo la Moshi kwa miaka 26 kama “kiongozi shupavu wa kiroho ambaye aliwalea vyema kondoo wa bwana. Lakini pia alikuwa kiongozi hodari kwa maendeleo ya jamii yaliyowanufaisha waumini wake na hata wale wa madhehebu na dini nyingine.” 

 Amesisitiza Rais Kikwete: “Kwa kweli sote tumepoteza mtu muhimu. Tunamfahamu marehemu Baba Askofu Msarikie kwa mema mengi aliyowatendea watu wa jimbo lake, ya kiroho na ya maendeleo. Mimi binafsi, wana-moshi na Watanzania kwa ujumla tutamkumbuka na kumuenzi Baba Askofu Msarikie kwa mema mengi aliyowafanya wanadamu wenzake na nchi yetu.”

Askofu Amani: Tumeingiliwa na saratani ya uvunjifu wa amani

0
0

Askofu wa Jimbo la Moshi la Kanisa Katoliki Tanzania, Askofu Isaac Amani Massawe amesema kuwa Tanzania imeingiliwa na ugonjwa wa saratani wa kuvunja amani na utulivu na Watanzania wasipobalika na kukubatia amani watajuta.
Amesema kuwa baada ya miaka 50 ya Uhuru, Watanzania sasa wamefungua ukurasa mpya na nchi imeanza kupoteza sifa ya kuwa nchi ya amani na utulivu.
Aidha, amesema kuwa wajibu wa watu kuishi kwa amani siyo wajibu wa Serikali ama wa Dini ama wa Kanisa bali ni wa kila mtu kwa nafsi yake.
Askofu Amani ameyasema hayo leo, Alhamisi, Februari 14, 2013 wakati alipokuwa anatoa neno la shukurani baada ya kumalizika kwa Ibada ya Mazishi ya aliyekuwa Askofu Jimbo la Moshi, Askofu Mstahivu Amedeus Peter Msarikie katika Kanisa Kuu la Kristo Mfalme mjini Moshi.
Askofu amewaambia mamia kwa mamia ya waumini: “Tumefungua ukurasa mpya katika Tanzania. Baada ya miaka 50 ya amani na utulivu sasa tumebadilika. Tanzania ya leo siyo Tanzania ya zamani sasa tumeanza kuongozwa na misingi ya vurugu za kidini na vurugu za kifedha.”
Ameuliza Baba Askofu Amani: “Tumeelimika zaidi ama tumechoka amani? Tumeingiwa na saratani ya uvunjifu wa amani na migawanyiko kwa misingi ya kidini na kifedha na mingine ya aina mbali mbali. Njia nzuri ya kuagana na mzee wetu Askofu Msarikie ni kuishi maisha aliyoishi yeye- maisha ya amani na utulivu. Yeye alikuwa chombo cha amani na anapumzika kwa amani kwa sababu aliishi maisha ya amani.”
Ameongeza: “Kuishi kwa amani na utulivu siyo suala wala wajibu wa Serikali ama wa Kanisa ama wa Dini ni wajibu wa kila mtu kwa nafsi yake na kila mmojawetu anao wajibu wa kusali ili kuombea amani ambayo imedumu katika nchi yetu kwa miaka mingi sana – miaka 50 sasa lakini inaonyesha kila dalili ya kutoweka.”
Amesisitiza: “Ndugu zangu amani hairithishwi, amani hujengwa na hulindwa. Changamoto alichotuachia Askofu Msarikie ni kutafuta na kuilinda amani katika nchi yetu. Huwezi kuwa mtu wa vurugu na mvunja amani na bado ukapata starehe ya milele mbele ya Mwenyezi Mungu. Sasa ni wakati wa kulea taifa letu, kulitengeneza upya na tumwombe Mungu atusaidie katika safari hii ndefu.”  

Rais Kikwete asaini kitabu cha Maombolezo, Atoa heshima za Mwisho Kwa Marehemu Askofu Thomas Laizer

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitia saini kitabu cha maombolezo ya Askofu Thomas Laizer wa Dayosisi ya Kaskazini Kati la Kanisa la Kiinjili cha Kilutheri Tanzania (KKKT) leo, Alhamisi, kwenye Kanisa Kuu la KKKT mjini Arusha kabla ya kutoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa Askofu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa Askofu Thomas Laizer wa Dayosisi ya Kaskazini Kati la Kanisa la Kiinjili cha Kilutheri Tanzania (KKKT) leo, Alhamisi, kwenye Kanisa Kuu la KKKT mjini Arusha. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiifariji familia ya Askofu Thomas Laizer wa Dayosisi ya Kaskazini Kati nyumbani kwa Askofu mara baada ya kuwa ametoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu kwenye Kanisa Kuu la KKKT mjini Arusha leo, Alhamisi, Februari 14, 2013. (Picha zote na Fredy Maro wa Ikulu). 

kalunde band yasherehekea miaka yake saba tangu kuanzishwa kwake.

0
0

2
Mkurugenzi wa bendi ya Kalunde Deo Mwanambilimbi kushoto Debora Nyangi Meneja wa bendi hiyo pamoja na Mwapwani mwimbaji wa bendi ya Kalunde kwa pamoja wakikata keki kuashiria sherehe za kutimiza miaka saba toka bendi hiyo ianzishwe.
3
Meneja wa Bendi la Kalude Debora Nyangi akimlisha keki Mkurugenzi wa bendi hiyo Deo Mwanambilimbi katika onesho la Valentine na sherehe za utimiza miaka 7 ya kuanzishwa kwa bendi hiyo.

1Mkurugenzi wa Bendi ya Kalunde Deo Mwanambilimbi akiimba huku wacheza shoo wa bendi hiyo Kushoto ni Queen Vero na kulia ni Frola Bamboocha wakati wa onesho la Valentine lililofanyika kwenye ukumbi wa Trinit Oysterbay jijini Dar es salaam usiku huu, Katika Onesho hilo pia bendi ya Kalunde imetimiza miaka 7 toka ianzishwa na kusherehekea mwaka wake wa saba wa utendaji wa kazi.

15Bamboocha na Shabiki wake hapa ni Full Mzuka hebu wacheki.
4 
5Mkurugenzi wa bendi hiyo Deo Mwanambilimbi akimlisha keki Meneja wa Bendi la Kalude Debora Nyangi katika onesho la Valentine na sherehe za utimiza miaka 7 ya kuanzishwa kwa bendi hiyo.
6
Debora Nyangi akimlisha keki Shekh Mwakichui mwimbaji na mpiga kinanda wa bendi ya hiyo
7
Debora Nyangi akimlisha keki Bon Kamprobo mpiga gitaa la solo maarufu wa bendi hiyo


8
Debora Nyangi akimlisha keki Bob Ludala mmoja wa waimbaji maarufu na makini wa bendi ya Kalunde.
9
Debora Nyangi akimlisha keki Eric mmoja wa mashabiki na wadau muhimu wa bendi ya Kalunde.
10
Mkurugenzi wa bendi ya Kalunde Deo Mwanambilimbi akiwa katika picha ya pamoja na Debora Nyangi ambaye pia ni Meneja wa bendi ya Kalunde na pia wakiwa wanamuziki waanzilishi wa bendi wakiwa pamoja na Deo Mwanambilimbi mwenyewe.
11
Mashabiki wa bendi ya Kalunde wakijimwaga stejini wakati bendi hiyo ikitumbuiza kwenye ukumbi wa Trinit Oysterbay jijini Dar es salaam usiku huu.
12
Hapa ni Full Kushwangweka na Valentine kama wanavyoonekana katika picha mashabiki hawa wakiwa stejini.
13
Mnenguaji Frola Bamboocha akijimwaga na mmoja wa mashabiki wa bendi ya kalunde kwenye ukumbi wa Trinit Oysterbay usiku huu.
14
Hapa ni Burudani tu kama wanavyoonekana mashabiki hawa wa Kalunde Band.

mkutano wa tatu wa Wadau wa NSSF WAMALIZIKA LEO JIJINI ARUSHA

0
0
Naibu Waziri wa kazi na Ajira,Dkt.Makongoro Mahanga akifunga mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),uliomalizika leo,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha,ambapo kauli mbiu yake kwa mwaka huu ilihusu "Sekta ya hifadhi ya Jamii Tanzania,Njia panda-Nini kifanyike".
wenyekiti wa bodi ya wadhamini wa NSSF,Aboubakar Rajab akizungumza machache kabla ya kufungwa kwa mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambao kilele chake kimekoma leo,ikiwa ni siku ya tatu,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha,ambapo kauli mbiu yake kwa mwaka huu ilihusu "Sekta ya hifadhi ya Jamii Tanzania,Njia panda-Nini kifanyike".
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau akitoa ufafanuzi wa jambo kabla ya kufungwa kwa mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambao kilele chake kimekoma leo,ikiwa ni siku ya tatu,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha,ambapo kauli mbiu yake kwa mwaka huu ilihusu "Sekta ya hifadhi ya Jamii Tanzania,Njia panda-Nini kifanyike".
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Emanuel Humba(pichani shoto) akiongoza mjadala wa mambo ya Afya,kwenye mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambao kilele chake kinakoma leo,ikiwa ni siku ya tatu,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha,ambapo kauli mbiu yake kwa mwaka huu ilihusu "Sekta ya hifadhi ya Jamii Tanzania,Njia panda-Nini kifanyike".Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau.
Mkurugenzi wa hospitali ya IMTU,ambaye pia ni mshauri wa mambo ya Afya kwa Jamii,Dkt.Ali Mzige akijibu mijadala ya maswali mbalimbali ,yaliyokuwa yakiulizwa na wadau mbalimbali kuhusiana na mada ya Afya,kwenye mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambao kilele chake kinakoma leo,ikiwa ni siku ya tatu,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha,ambapo kauli mbiu yake kwa mwaka huu ilihusu "Sekta ya hifadhi ya Jamii Tanzania,Njia panda-Nini kifanyike".


Mbunge wa Rombo, Mhe. Joseph Selasini (CHADEMA),akiuliza swali wakati wa mada ya Afya,kwenye mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambao kilele chake kinakoma leo,ikiwa ni siku ya tatu,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha,ambapo kauli mbiu yake kwa mwaka huu ilihusu "Sekta ya hifadhi ya Jamii Tanzania,Njia panda-Nini kifanyike".
Baadhi ya wadau zaidi ya 1000 waliohudhuria mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambao kilele chake kinakoma leo,ikiwa ni siku ya tatu,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha,ambapo kauli mbiu yake kwa mwaka huu ilihusu "Sekta ya hifadhi ya Jamii Tanzania,Njia panda-Nini kifanyike".

TAMKO LA JUKWAA LA WAHARIRI KUHUSU

0
0

TAMKO LA JUKWAA LA WAHARIRI KUHUSU
KUSUDIO LA KUZUIWA KWA MATANGAZO YA MOJA KWA MOJA KUTOKA BUNGENI - DODOMA

UTANGULIZI
1.   JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF) limepokea kwa masikitiko taarifa kwamba Bunge linaandaa utaratibu wa kuzuia vyombo vya habari kurusha moja kwa moja (live) matangazo ya Bunge.

2.   Taarifa ya Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah aliyoitoa juzi Jumatano, Februari 13, 2013 inasema kwamba eti ni kosa pia kwa wapigapicha kuwapiga picha wabunge wakiwa wamesinzia ndani ya ukumbi wa bunge.

3.   Kwamba baadhi ya wabunge wanazomoka kwa kujua kwamba michango yao inarushwa moja kwa moja hewani na hivyo kufanya vituko bungeni, kwahiyo kuzuia matangazo ya moja kwa moja ni kuwadhibiti wale wanaofanya fujo na vituko Bungeni.

4.   Dk. Kashililah anasema kwamba ofisi yake inaandaa mpango wa kurekodi vipindi hivyo na kuvirusha baadaye vikiwa vimehaririwa na kwamba ofisi yake inawasiliana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupata njia ya kurusha matangazo hayo ya Bunge yaliyohaririwa.

MAONI YA TEF
Hatua hii ya ofisi ya Bunge inatupa shaka na pengine ni ishara ya mwendelezo ya kile ambacho kinaonekana kama jitihada mpya za kuuminya uhuru wa habari nchini. Kwa maana hiyo;
   
1.   Tunashangaa Bunge la Tanzania limejifunza wapi siasa hizi za kufunika mambo yanayowahusu wananchi, huku likijua kwamba wanaofuatilia vikao hivyo ndio walipa kodi na wapiga kura wa wabunge ambao uongozi wa Bunge unataka kuwalinda?

2.   Ni kama Taifa letu linarudi katika enzi za giza la usiri ambao kimsingi hatupaswi kuurejea. Tangazo hili ni moja ya mambo ya bahati mbaya yanayoikuba nchi yetu kwa sasa, wakati ambao dunia inahimiza uwazi hasa katika vyombo vya uamuzi.

3.    Ikumbukwe kwamba Tanzania imetokea katika mfumo wa chama kimoja kilichoshika hatamu hadi 1992, ambao uliifanya Serikali, Bunge na Mahakama kuendeshwa kwa usiri wa hali ya juu.

4.   Mara zote, usiri ni chimbuko la matumizi mabaya ya madaraka ni kinyume na misingi ya utawala bora na usiri unatoa mamlaka yasiyositahiki kwa kikundi cha watu wachache wenye masilahi binafsi ya kufisadi nchi.

5.   Hali hii inatufanya tuwe na shaka iwapo serikali yetu ilifanya kwa dhati mambo yafuatayo:
(a)                Kuridhia Tamko la Haki za Binadamu, Desemba 10, 1948 ambapo Kifungu cha 19 cha tamko hili (Article 19) kinatoa uhuru wa mtu kutoa na kupokea mawazo bila kujali mipaka ya nchi na haki hii ya kutoa mawazo haipaswi kuingiliwa.

(b)                Kufanya mabadiliko ya 5 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1984 ambayo kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii, yaliliingiza tamko hili la Haki za Binadamu hivyo kuwezesha Ibara ya 18 ya katiba hiyo ya 1977 kuakisi Kifungu cha 19 cha tamko hiko kwa kutoa uhuru mawasiliano na haki ya kupewa taarifa.

(c)               Kutia saini Mpango wa Sherikali ya Uwazi (Open Government Partnership/Initiative) unaongozwa na Rais Barrack Obama wa Marekani mwaka 2010, ambapo tayari Wizara ya Katiba na Sheria imeanza mchakato wa kutunga Sheria ya Haki ya Kupata Habari, itakayoruhusu nyaraka zote muhimu za Serikali kuwekwa wazi kwa wananchi.


MSIMAMO WA TEF
1.   Tunautaka uongozi wa Bunge kuachana  na harakati hizo kwani hazitasaidia kukuza demokorasia au kuboresha maadili ya Bunge. Badala yake zitazidisha mashaka ya umma dhidi ya chombo hicho cha uwakilishi kwa wananchi kutaka kufanya kazi zao “gizani”.

2.   TEF tunamaani kwamba kazi ya utangazaji si kazi inayopaswa kusimamiwa na uongozi wa Bunge, wala hatuna kumbukumbu za matukio na hatua za namna hii katika miaka ya karibuni, hata katika nchi  nyingine.

3.   Ikumbukwe kuwa, kama si ufinyu wa nafasi na mfumo wa uwakilishi bungeni tunaoutumia, ilibidi wananchi wote waingie bungeni na kutoa mawazo yao. Kwa maana nyingine wabunge ni wawakilishi wa wananchi na hivyo ni dhambi kuweka usiri wa yale yanayozungumzwa au kuhariri alichozungumza mbunge aliyetumwa na wananchi.

4.   Tunaamini kwamba jitihada zozote za kuwafungia wabunge ndani na kuhariri kazi wanazofanya na matamko wanayotoa, ni ishara kwamba Bunge linataka kuficha maovu au udhaifu wa mhimili huo au mihimili mingine inayowajibishwa na wabunge.

5.   Hatua hii ya kuzuia vikao vya Bunge kuonyeshwa moja kwa moja itakuwa inawachimbia kaburi la kisiasa wabunge kwani ndio wanaomulikwa kwa majibu ya maswali wanayoulizwa na hatua wanazochukua.

6.   Jukwaa la wahariri linaamini kwamba utaratibu huu unaoandaliwa sasa na Dk. Kashililah ni wa kidikteta na ni mbaya kuliko udikteta wowote uliowahi kutokea hapa nchini kwa miaka yote ya uhuru wa Tanzania.

7.   Kwa hatua hii uongozi wa Bunge utakuwa umedhihirisha udhaifu usiomithilika ambao uongozi wa Bunge uliopita uliuondoa kwa kuweka misingi na kanuni za uwazi na uwajibikaji. Ni kwa sura ya nje, harakati hizi za uongozi wa sasa wa Bunge zinaonekana kama hatua za kufuta yaliyofanywa na uongozi wa Bunge la tisa.

8.   Katika mazingira haya, tunaamini kwamba iwapo hili litatokea, jitihada ndogo za uwazi zilizokuwa zimefanywa na Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais Jakaya Kikwete, zitafutika na kiumfanya raia aonekane mbele ya jumuiya ya kimataifa kuwa kiongozi dhalimu na dikteta asiyevumilia kukosolewa.

9.   Na kwa kuwa hili linatokea kueleka mwisho wa uongozi wake, ni dhahiri litakuwa limefuta mema mengi aliyotenda na kujivunia katika misingi ya uwazi na uwajibikaji.

10.                Kwa ujumla hatua hii itavifanya serikali na Bunge visiaminike kwa umma na itasababisha zogo na vurugu zisizomithilika kwani waliojifungia ndani watatoka na kusema hadharani kwa jinsi watakavyoona inafaa hivyo kuharibu kabisa mfumo wa taarifa za chombo hicho.

11.                Jukwaa linaamini kwamba njia halisi ya kurejesha amani Bungeni ni uongozi wa Bunge kutenda haki wa wabunge wote; maana hata vikao vyao visiporushwa moja kwa moja, vurugu hazitaisha iwapo wahusika hawataamini kwamba wanatendewa haki.

12.                Kuhusu suala la wabunge kulala bungeni na wakapigwa picha, tunasema magazeti na televisheni zinazofanya hivyo zinastahili kupongezwa badala ya kulaumiwa. Bungeni si mahala pa kusinzia, ni mahala pa kuchapa kazi. Wabunge wanaotaka kulala usingizi wabaki hotelini na si kulala kwenye ukumbi wa bunge.

HITIMISHO
1.           Watanzania wamepata fursa ya kuwafahamu wabunge wao baada ya utaratibu wa kurusha moja kwa moja mijadala ya wabunge kuanza miaka ya 2000. Kwa maana hiyo jaribio lolote la kuzuia matangazo hayo ni kuturejesha enzi za Bunge mazongwe na kadhia  ya kuficha habari ambapo hata barua za mialiko ziligongwa mihuri ya siri.

2.           Ndiyo maana tumesema hatua hii inakiuka misingi ya uhuru, uwazi na uwajibikaji wa vyombo vya umma na viongozi wa serikali. Ni mpango unaoweza kusababisha vurugu zitokanazo na kiu ya wananchi kujua kinachoendelea na kutumia taarifa potofu watakazozipata popote wanapojua na kwa staili wanayojua.

3.           Iwapo kuna kasoro katika Kanuni za Bunge zinazotokana na Sheria ya Haki, Wajibu na Mamlaka ya Bunge ya Mwaka 1988, basi kasoro hizo zirekebishwe na kuwabana wabunge  wanaozikiuka. Lakini hatukubaliana na mpango wa Bunge kuwaadhibu wananchi wasione kinachoendelea bungeni eti kwa lengo la kuwalinda wabunge.

4.           Mwisho tunasema nia ya kudhibiti (censorship), kuhariri na au kuzuia baadhi ya habari kutoka bungeni, kamwe Jukwaa la Wahariri halikubalini nayo na litaendelea kuipiga hadi hatua ya mwisho. Tunawataka wananchi watuunge mkono katika msimamo huu na sisi kama wahariri tutahakikisha tunachapisha maoni yao kwa kina kupinga suala hili.


Absalom Kibanda,
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF)
Dar es Salaam
Februari 15, 2013

MKUU WA MKOA WA RUKWA AAHIDI KUWACHUKULIA HATUA KALI WALANGUZI WA NISHATI YA MAFUTA MKOANI HUMO

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza katika kikao cha baraza la ushauri la watumiaji wa nishati na maji nchini na wadau wake walipotembelea Mkoani Rukwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali za baraza hilo. Mkuu huyo wa Mkoa alitoa pongezi kwa kazi nzuri wanayofanya na kuahidi kuwachukulia hatua walanguzi wa nishati ya mafuta pamoja na wale wanasimamia kwa kushindwa kufanya kazi yao vizuri. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima.
Mwenyekiti wa baraza la ushauri watumiaji wa maji na nishati nchini Eng. Profesa Katima akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema kazi kubwa ya baraza hilo ni kutetea na kulinda haki za watumiaji wa maji na nishati ambayo ni maji safi na maji taka, umeme, petroli na gesi asilia.
Baadhi ya wadau wa mkutano huo ambao ni vyombo vya ulinzi na usalama, Tanesco, EWURA Mkoa wa Rukwa, wawakilishi wa sheli za mafuta na shirika la Maji safi na Maji taka Mkoa wa Rukwa (SUWASA) 
Wawakilishi wa baraza hilo Mkoani Rukwa.
Picha ya pamoja. (Na Hamza Temba -Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa - rukwareview.blogspot.com)

EAC KUONGOZA ZOEZI LA UTEKETEZAJI WA SILAHA NDOGO NDOGO UKONGA KESHO

0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) anaeshughulikia masuala ya Siasa, Dk. Julius Rotich (wapili kushoto) akizungumza leo katika Mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juu ya zoezi la Uteketezaji wa Silaha ndogo ndogo litakalo fanyika Ukonga chini ya usimamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania. Pamoja nae kutoka kushoto ni Mtaalam wa Masuala ya Amani wa EAC, Leonard Onyonyi, Mkuu wa Kitengo cha Silaha Ndogo ndogo wa Jeshi la Polisi Tanzania, SACP. Modest Mwauzi na Mtaalam wa Masuala ya Habari wa EAC, Sukhdev Chatbar.

Mbali na zoezi hilo la uteketezaji wa silaha pia kutakuwapo na Utilaji saini ya itifaki ya Ulinzi na Amani kwa nchi za Jumuia hiyo.Mgeni Rasmi anataraji kuwa Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal.(Picha na Mroki Mroki-FATHER KIDEVU BLOG)
 Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya ndani na nje ya Jumuia ya Afrika Mashariki wakifuatilia mkutano huo.
Mtaalam wa Masuala ya Amani wa EAC, Leonard Onyonyi, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusiana na zoezi hilo pamoja na kutiliana saini kwa Itifaki ya kufungwa kwa zoezi hilo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) anaeshughulikia masuala ya Siasa, Dk. Julius Rotich.

Mkuu wa Kitengo cha Silaha Ndogo ndogo wa Jeshi la Polisi Tanzania, SACP. Modest Mwauzi akitoa maelezo juu ya maandalizi ya zoezi hilo.

Naibu Katibu Mkuu wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) anaeshughulikia masuala ya Siasa, Dk. Julius Rotich (katikati) akizungumza leo katika Mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juu ya zoezi la Uteketezaji wa Silaha ndogo ndogo litakalo fanyika Ukonga chini ya usimamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania. Pamoja nae kutoka kushoto ni Mtaalam wa Masuala ya Amani wa EAC, Leonard Onyonyi, na Mkuu wa Kitengo cha Silaha Ndogo ndogo wa Jeshi la Polisi Tanzania, SACP. Modest Mwauzi.

NEEC na NDC wasaini makubaliano ya ushirikiano wa kuwawezesha wananchi kiuchumi.

0
0

Mkurugenzi wa Viwanda vya kuongeza Ubora wa Thamani kutoka Shirika la Taifa la Maendeleo Bw. Shannel Mvungi akibadilishana hati za makubaliano ya Ushirikiano wa Kuwawezesha wananchi Kiuchumi   na Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi Dkt. Anaclet Kashuliza (kulia) leo jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi wa Viwanda vya kuongeza Ubora wa Thamani kutoka Shirika la Taifa la Maendeleo Bw. Shannel Mvungi akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu namna makubaliano hayo ya uwezeshaji wananchi kiuchumi katika maeneo yenye miradi ya NDC yatakavyofanya kazi. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.   
============   =======  =======
   Na. Aron Msigwa - MAELEZO.
 15/2/2013, Dar Es Salaam.

Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi nchini (NEEC) na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) wameanzisha ushirikiano utakaowawezesha wananchi kunufaishwa kiuchumi na rasilimali zinazowazunguka katika maeneo ambayo  NDC ina miradi ya maendeleo.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wa pamoja wa utiaji saini wa makubaliano kuwawezesha wananchi kiuchumi kati NDC na NEEC  yenye lengo la kutoa fursa kubwa za ushiriki wa kiuchumi kwa wananchi wanaoishi kuzunguka maeneo yenye miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.

 Akizungumza mara baada ya utiaji saini wa makubaliano hayo kwa niaba ya Mkurugenzi wa NDC Bw. Shannel Mvungi amesema kuwa miradi watakayonufaika wananchi ni pamoja na uchimbaji wa Makaa ya Mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga Wilayani Ludewa unaotekelezwa na Kampuni ya ubia ya Tanzania China International Minerals Resources Limited ambao inayotarajia kutoa ajira za moja kwa moja zaidi ya 5000 kwa wananchi wa  Ludewa.


Amesema kuwa lengo kubwa la  NEEC na NDC ni kuwaendeleza na kuwawezesha wananchi kiuchumi hasa wale walio katika maeneo   ambayo tayari miradi imeanza kutekelezwa  kwa kutoa mafunzo ya ujengaji uwezo na ujuzi katika kutambua fursa zilizopo na jinsi ya kuzitumia, kuhamasisha fursa na miundo mbinu ya kiuchumi, kuwahamasisha wananchi kujiunga katika mitandao ya Vikundi na Masoko.

Fursa nyingine watakazopata wananchi ni pamoja na uwezeshwaji wa upatikanaji wa mitaji na kuunganishwa na Taasisi za Fedha, kuainisha na kuendeleza maeneo huru ya Kufanyia Biashara na kuhamasisha umuhimu wa wananchi kujiunga na Ushirika.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji wananchi kiuchumi Dkt. Anaclet Kashuliza amesema kuwa taasisi hizo zinatarajia kushirikiana vema katika  kuwaunganisha wadau mbali mbali wa maendeleo katika maeneo husika hususani wawekezaji wa sekta binafsi,mashirika yasiyo ya kiserikali,wadau wa maendeleo na serikali za mikoa na wilaya. 

" Ni matarajio ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kuona kuwa rasilimali asilia zikiwanufaisha wananchi katika maeneo yao kwa kuwawezesha kushiriki kwa kiasi kikubwa katika shughuli za kiuchumi na kubadili hali zao za maisha kupitia ongezeko la kipato na kuboreka kwa miundombinu" Amesema Dkt. Kashuliza. 

Akizungumzia kuhusu maendeleo ya taasisi hizo Dkt. Kashuliza  amesema kuwa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi hilolilianzishwa chini ya kifungu cha nne (4) cha Sheria ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na kazi rasmi mwaka 2005 likiwa ni chombo cha juu cha kusimamia utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi huku shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) linalomilikiwa  kwa asilimia 100 na Serikali liloanzishwa mwaka 1965 kwa lengo la kusimamia  maendeleo ya nchi kupitia viwanda katika sekta zote za uchumi.

SHIRIKA LA UNDER THE SAME SUN LATOA PONGEZI KWA UONGOZI WA MKOA WA RUKWA KWA KUFANIKIWA KUWAKAMATA WATUHUMIWA WALIOMKATA MKONO MLEMAVU WA NGOZI (ALBINO) NA KIZIBITI HICHO

0
0

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa shirika linalotetea haki za watu wenye ulemavu wa ngozi nchini (Albino) Vicky Mketema kulia na wajumbe wenzake wa shirika hilo watatu waliosimama nyuma. Kulia waliosimama ni katibu wa Mkuu huyo wa Mkoa Frank Mateni na kushoto aliyekaa ni Afsa maendeleo ya jamii Mkoa wa Rukwa Deonisya Njuyui.

Mama Maria Chambanenge mlemavu wa ngozi anayenyonyesha mtoto wa miezi mitano alikatwa mkono na watuhumiwa ambao wameshatiwa nguvuni na jeshi la polisi Mkoa wa Rukwa na Mkono wake uliokatwa umeshapatikana. Upelelezi bado unaendelea kuwapata watuhumiwa zaidi wanaohusika na vitendo hivyo.

Mkurugenzi wa shirika la under the same sun Vicky Mketema ametoa pongezi za dhati kwa uongozi wa Mkoa wa Rukwa kwa kushughulikia tatizo hilo kikamilifu na kwa haraka na kufanikiwa kupata kiungo hicho na watuhumiwa waliohusika kwa muda wa siku mbili. Alisema endapo mikoa yote ingekuwa inashughulikia matatizo kama hayo kwa muda mfupi kama huo basi uhalifu na namna hii ungekuwa umeshatoweka nchini.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ametoa onyo kali kwa wale wote watakaohusika na vitendo vya uvunjifu wa amani Mkoani humo ambapo amewataka wananchi kutoa taarifa mapema kwa vyombo vya ulinzi pale wanapowashuku wahalifu wa vitendo hivyo. Amewato hofu wananchi kwani vyombo vya ulinzi na usalama vipo kwa ajili yo. 

Muathirika huyo anaendelea kupata huduma za matibabu katika Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa na hali yake inaendelea vizuri. (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa -rukwareview.blogspot.com)

Rais Kikwete aongoza maelfu ya watu mazishi ya askofu thomas laizer jijini arusha leo.

0
0



Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za mwisho mara baada ya kuweka shada la maua kwenye Kaburi la aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Dayosisi ya Kaskazini na Kati,Marehemu Askofu Dk. Thomas Laizer aliyefariki Dunia Februari 7,2013 katika Hospitali ya Hospitali ya Selian,Jijini Arusha.Wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika jioni ya leo nje ya Kanisa hilo.
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili,Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mkewe Mama Sitti Mwinyi wakiweka shada la maua kwenye Kaburi la aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la  Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Dayosisi ya Kaskazini na Kati,Marehemu Askofu Dk. Thomas Laizer aliefariki Dunia Februari 7,2013 katika Hospitali ya Hospitali ya Selian,Jijini Arusha.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina Lowassa wakiweka shada la maua kwenye Kaburi la aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Dayosisi ya Kaskazini na Kati,Marehemu Askofu Dk. Thomas Laizer aliefariki Dunia Februari 7,2013 katika Hospitali ya Hospitali ya Selian,Jijini Arusha.
 Mwenyekiti wa makampuni ya IPP,Mh Reginard Mengi akiweka shada la maua kwenye Kaburi la aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Dayosisi ya Kaskazini na Kati,Marehemu Askofu Dk. Thomas Laizer aliefariki Dunia Februari 7,2013 katika Hospitali ya Hospitali ya Selian,Jijini Arusha. 
katibu Mkuu wa chama cha Mapinduzi (CCM),Ndugu Abdularhaman Kinana akiweka shada la maua kwenye Kaburi la aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Dayosisi ya Kaskazini na Kati,Marehemu Askofu Dk. Thomas Laizer aliefariki Dunia Februari 7,2013 katika Hospitali ya Hospitali ya Selian,Jijini Arusha.
 Sanduku lenye mwili wa merehemu aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la  Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Dayosisi ya Kaskazini na Kati,Marehemu Askofu Dk. Thomas Laizer aliefariki Dunia Februari 7,2013 katika Hospitali ya Hospitali ya Selian,Jijini Arusha,wakitoka nje ya kanisa na kuelekea sehemu iliyoandaliwa kwa ajili ya maziko nje kanisa hilo. 
Rais Kikwete akitoa salamu za rambi rambi mbele ya waombolezaji  (hawapo pichani) ndani ya kanisa kuu la KKKT,waliofika kushiriki mazishi ya aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Dayosisi ya Kaskazini na Kati,Marehemu Askofu Dk. Thomas Laizer aliefariki Dunia Februari 7,2013 katika Hospitali ya Hospitali ya Selian,Jijini Arusha.
Sehemu ya viongozi wakuu wa Serikali wakiongozwa na Rais Kikwete,wakati wa mazishi ya mazishi ya aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Dayosisi ya Kaskazini na Kati,Marehemu Askofu Dk. Thomas Laizer aliefariki Dunia Februari 7,2013 katika Hospitali ya Hospitali ya Selian,Jijini Arusha.
 sala ya mazishi ya aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Dayosisi ya Kaskazini na Kati,Marehemu Askofu Dk. Thomas Laizer aliefariki Dunia Februari 7,2013 katika Hospitali ya Hospitali ya Selian,Jijini Arusha 
 Askofu Mkuu wa kanisa la KKKT,Dkt Alex Malasusa akiongoza sala ya mazishi ya aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Dayosisi ya Kaskazini na Kati,Marehemu Askofu Dk. Thomas Laizer aliefariki Dunia Februari 7,2013 katika Hospitali ya Hospitali ya Selian,Jijini Arusha
 Baadhi ya Viongozi wa dini ya Kiislam wakiwasili kwenye Kanisa kuu la KKKT,kwa ajili ya kushiriki mazishi ya aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Dayosisi ya Kaskazini na Kati,Marehemu Askofu Dk. Thomas Laizer aliefariki Dunia Februari 7,2013 katika Hospitali ya Hospitali ya Selian,Jijini Arusha. 
Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA,Mh.Freeman Mbowe akizungumza machache mbele ya waombolezaji  (hawapo pichani) ndani ya kanisa kuu la KKKT,waliofika kushiriki mazishi ya aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Dayosisi ya Kaskazini na Kati,Marehemu Askofu Dk. Thomas Laizer aliefariki Dunia Februari 7,2013 katika Hospitali ya Hospitali ya Selian,Jijini Arusha.
Rais Kikwete akiwasalimia baadhi ya watu waliokuwa nje ya kanisa la KKKT,mapema leo mchana mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kushiriki mazishi ya aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la  Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Dayosisi ya Kaskazini na Kati,Marehemu Askofu Dk. Thomas Laizer aliefariki Dunia Februari 7,2013 katika Hospitali ya Hospitali ya Selian,Jijini Arusha. 
Rais Kikwete akiwaaga waombolezaji mbalimbali waliokuwa nje ya kanisa la KKKT,mapema leo mchana mara baada ya kushiriki mazishi ya aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la  Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Dayosisi ya Kaskazini na Kati,Marehemu Askofu Dk. Thomas Laizer aliefariki Dunia Februari 7,2013 katika Hospitali ya Hospitali ya Selian,Jijini Arusha.


 Pichani juu ni sehemu ya waombolezaji wakiwa ndani ya kanisa kuu la KKKT,wakisikiliza sala ya mazishi iliyokuwa ikisomwa.
 Watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini mbalimbali,Serikali wamehudhuria  mazishi hayo.
Mbunge wa jimbo la Simanjiro (CCM),Mh.Christopher Ole Sendeka akizungumza machache mbele ya waombolezaji  (hawapo pichani) ndani ya kanisa kuu la KKKT,waliofika kushiriki mazishi ya aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Dayosisi ya Kaskazini na Kati,Marehemu Askofu Dk. Thomas Laizer aliefariki Dunia Februari 7,2013 katika Hospitali ya Hospitali ya Selian,Jijini Arusha.
Mbunge wa NCCR-Mageuzi,Mh.James Mbatia akizungumza machache mbele ya waombolezaji  (hawapo pichani) ndani ya kanisa kuu la KKKT,waliofika kushiriki mazishi ya aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Dayosisi ya Kaskazini na Kati,Marehemu Askofu Dk. Thomas Laizer aliefariki Dunia Februari 7,2013 katika Hospitali ya Hospitali ya Selian,Jijini Arusha. 

mh mbowe afunguka kwenye mazishi ya askofu thomas leizer leo jijini arusha.

0
0

wizara ya afya na ustawi wa jamii yagawa vifaa vya watu wenye ulemavu

0
0


MSIMU WA VALENTINE NA BAILEYS WAFIKA TAMATI KWA MAFANIKIO

0
0


Richa Adhia akipokea zadi ya glasi kutoka kwa mmoja wa mabalozi wa
kinywaji cha Baileys kinachosambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti.
Miss Tanzania 2007 Richa Adhia aliyeshika chupa ya Baileys akiwa na
Gipson Godwin(kulia) na Scolastica Dotto ambaao ni mabalozi wa kinywaji
hicho kutoka Kampuni ya bia ya Serengeti.
====== ======  ======= ======

MSIMU WA VALENTINE NA KINYWAJI CHA BAILEYS WAFIKIA TAMATI KWA MAFANIKIO

Miss Tanzania 2007 Richa Adhia  amewataka watanzania kujenga utamaduni wa kuwakupenda  na kuwajali watu wengine wakiwemo wenye mahitaji maalum kama watoto na wazee  kwa kuwa wanahitaji faraja toka kwa jamii nzima nyakati zote badala ya kusubiri  maadhimisho ya sikukuu mbalimbali.

Akizungumza wakati wa kilele cha msimu wa  siku ya wapenda nao ulioandalia na Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji cha Baileys katika viwanja vya shoppers jijini Dar es Salaam,  Richa alisema “siku ya wapendanao ikitumika  kuongeza ari ya kuwasaidia watu wenye mahitaji inakuwa na maana zaidi kuliko kuitumia siku  hiyo kwa mapenzi zaidi na sio vibaya kutumia siku ya wapendanao  kuanzisha mapenzi mapya au kuboresha mapenzi yaliyokuwepo lakini pia itumike kuwakumbuka wahitaji ambao ni wazee na watoto”.

Kwa upande wake Meneja Masoko wa vinywaji vikali kutoka Kampuni ya bia ya Serengeti Emilian Rwejuna amesema “ tumeamua kufanya kampeni hii ili kuamsha ari ya kuwajali na kuwapenda wengine ikiwemo kujenga utamaduni wa kuwanunulia zawadi kama tulivyofanya kwa wapenzi wa kinywaji cha Baileys na kwa kuwa zawadi zina mchango mkubwa katika maisha ya mahusiano hivyo mtoto anayempa zawadi mzazi wake hujiweka katika mazingira mazuri kimahusiano kuliko asiyefanya hivyo”.Pia alielezea kuwa Kampuni ya bia ya Serengeti imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuhamasisha na kutoa chachu na kuahidi itaendelea kuhamasisha mahusiano mema  miongoni mwa jamii.

Kampeni ya msimu wa valentine  iliyoandaliwa na Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha Baileys ilinza tarehe mosi mwenzi wa Februari kwa kupita katika maeneo mbalimbali ya manunuzi ili kuwahamasisha wananchi kujenga utamaduni wa kuwanunulia wenzi wao zawadi na kukamalika siku ya wapendanao Februari 14. Ambapo zawadi mbali mbali zilitolewa katika kampeni hiyo ikiwemo chupa ya Baileys, fulana, glasi, maua na kubwa zaidi pea nane zilipata bahati ya kupata chakula jioni katika mgahawa wa Akemi uliopo jijini Dar es Salaam.

BUNGE HALINA MPANGO WA KUSITISHA MATANGAZO YA BUNGE WALA KAMATI ZAKE-Kashililah

0
0



TAARIFA MAALUM KUHUSU BUNGE NA KAMATI

Ofisi ya Bunge imepokea kwa masikitiko taarifa kuhusu tafsiri ya kusitisha matangazo ya Shughuli za Bunge na Kamati, kinyume na jinsi ilivyoakisiwa katika mazungumzo ya pamoja kati ya Wanahabari na Katibu wa Bunge. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, Bunge la Jamhuri ya Muungano halina mpango wa kusitisha matangazo ya Bunge wala Kamati zake, ambazo kwa mahitaji ya sasa nazo zinapaswa kurushwa moja kwa moja kama sehemu ya mpango kabambe wa kuwapasha Wananchi yanayojiri katika Uendeshaji bora wa Shughuli za Bunge. Dhamira ya Bunge ni kuhakikisha kuwa mpango kabambe uliopo ni kumfikia kila Mtanzania alipo na kwa uwezo alionao aweze kupata na kushiriki katika uendeshaji wa shughuli za Bunge.

Hivyo Mpango mkakati uliopo utakuwa kuboresha mawasiliano ya kawaida kupitia Teknolojia ya Mawasiliano TEKNOHAMA, kwa wale watakaokuwa na uwezo wa kupata huduma za mtandao, na tayari tumeanza kurusha live video striping kupitia tovuti ya Bunge, na hata wale watakaopenda kujua zaidi, basi wanaweza kupitia majadiliano ya Bunge kwa nyakati tofauti. 

Aidha, kwa wale watakaokuwa na uwezo wa kushika mawimbi ya Radio, basi wataweza kufuatilia majadiliano ya Bunge katika Radio ya Bunge inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni katika masafa yanayoweza kupatikana nchi nzima, hii ikiwa ni jitihada za ziada kwa kuwa kuna Radio zinazotoa huduma hiyo ya moja kwa moja vizuri hadi sasa, kama vile RTD, BBC, STAR etc. Aidha, kwa wale watakaoweza kuwa na uwezo wa kumudu Luninga, basi Bunge limejipanga kuwapatia huduma hiyo moja kwamoja kupitia katika mtandao wake mpya utakaokuwa ukirushwa masaa 24, baada ya mitambo mipya ya kunakili majadiliano Bungeni na katika Kamati kusimikwa.

Hivyo basi utaratibu uliopo sasa utaendelea kutumika ambapo vituo vyote vya Television vitapewa fursa ya kurusha matangazo kwa utashi wao bila kuwekewa mipaka ya aina yoyote sambamba na matangazo yatakayotolewa na mitandao ya Bunge. Utaratibu huu unatokana na uamuzi wa pamoja kati ya Bunge na Tume ya Mawasiliano, ambapo vipindi vyote vya Bunge vitakuwa vinarushwa bila kudhaminiwa na taasisi yoyote zaidi ya mamlaka tajwa juu ya mawasiliano TCRA.

Hivyo basi kwa maelezo hayo ni dhahiri kuwa Bunge halina mpango wa kusitisha matangazo ya TV wala yale ya Radio au Teknohama, bali linatarajia kuboresha upatikanaji wa huduma kwa utaratibu ulio rahisi na unaoweza kusimamiwa na pande zote, yaani Bunge na Wananchi. Aidha, kwa utaratibu uliopo sasa,Bunge halirushi matangazo ya aina yoyote, bali hutoa nakala ya majadiliano hayo kwa mtu yeyote atakaye au TV na Radio yoyote kupitia katika mitambo yake. 

TV zote zinazorusha matangazo ya Bunge hupata feed toka katika mitambo ya Bunge, na pale wanapoona yafaa basi huomba kutumia mitambo yao na hivyo kutumia fursa hiyo kuingiza Camera na Wanahabari ndani ya ukumbi wa Bunge kwa minajiri hiyo. Kuzingatia mabadiliko tajwa, utaratibu huo umepewa ukomo, ili sasa hapatakuwa na fursa ya kuingiza Camera ndani ya Kumbi za Bunge, bali wote watakaotaka kurusha matangazo ya Bunge kwa utashi wao, watapata clear feed toka katika mitambo ya Bunge na hivyo kurusha live vipindi vyote vya Bunge bila kuhaririwa kama ilivyonakiliwa katika makala mbalimbali.

Hata hivyo utaratibu huu wa kutumia Camera katika Kumbi utaendelea katika Kamati za Bunge, hadi hapo mitambo mipya ya mawasiliano itakapofungwa katika Kumbi zote za Kamati. Hivyo basi, ili kwenda sawia na taratibu hizo, Bunge litaendesha zoezi la kuwatathmini Waandishi wote wa habari za Bunge na kuwasajili kwa vigezo vitakavyoafikiwa kati ya Baraza la Habari, Idara ya Habari na Bunge lenyewe. 

Aidha ili kulinda heshima na maadili ya utangazaji, Bunge litatoa utaratibu (Code of Conducts for Media broadcasting) wa namna ya kunakili na kurusha matangazo ya Bunge bila kujali yanarushwa kwa utaratibu upi. Hili litasaidia kuweka misingi bora ya mawasilaino na hivyo kuwapa fursa Wananchi kujua hali halisi ya matukio yote ndani ya Bunge na katika Kamati, bila kuegemea upande wowote (Non Partisan). 

Hivyo basi, wakati zoezi la maboresho hayo likiendelea, Wananchi watajulishwa kila hatua na matarajio tajwa na kwamba tunaendelea kusisitiza tena, Wananchi wasiwe na hofu juu ya taarifa zilizopewa uzito usio stahili za kusitisha matangazo ya Bunge, ambao hazikuwa sahihi na pia hazikuainisha zoezi zima la maboresho ya upatikanaji na usambazaji wa habari za Bunge. Tunasikitika kwa usumbufu uliowasibu wote walioakisiwa na taarifa hiyo.

Dr. Thomas D. Kashililah

KATIBU WA BUNGE

Mazungumzo yataepusha migogoro ya Kidini-UN

0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Jan Eliasson 
======  ======  ========
Na Mwandishi Maalum.


Wakati viongozi wakuu  mbalimbali nchini Tanzania  wakisisitiza haja na umuhimu wa viongozi wa madhebu ya dini kuwa na utaratibu wa kukutana mara kwa mara. Umoja wa Mataifa nao kwa upande wake  unaeleza kwamba ni kwa  njia ya  mazungumzo  migogoro ya dini inaweza kuepukika.


 Kauli hiyo ya Umoja wa Mataifa,  umetolewa na  Jan Eliasson,Nabu Katibu Mkuu wa  chombo hicho ya kimataifa ,  wakati wa  tukio maalum  la Muungano  kwaajili ya utamaduni wa Amani kwa njia ya  maelewano ya  madhehebu ya dini. Tukio ambalo limefanyika mwishoni mwa wiki hapa umoja wa mataifa likiwahusisha  wawakilishi kutoka  dini mbalimbali, vyama visivyo vya kiserikali na mabalozi.



“Migogoro mingi inayoendelea  hivi sasa duniani,  ni migogoro ya kidini. Mazungumzo baina ya imani mbalimbali yanaweza kusaidia kusuluhisha migogoro hii.  Tunaweza kupambana na chuki kwa njia ya mazungumzo   ili kujenga maelewano   na kujenga daraja la maisha bora kwa jamii zetu”.Akasema  Naibu Katibu Mkuu.



Na kuongeza kuwa, dini zote zimekuwa  mstari wa mbele katika juhudi si tu za kuhimiza amani na upendo, bali hata katika miradi ya  kuwasaidia watu maskini kwa kutoa huduma  kama vile za afya, na kuwasaidia vijana.

 Hata hivyo akaonya kwamba, siasa kali za  kidini zimekuwa chimbuko la uharibifu wa kudumu na  mateso  katika jamii.



Na kwa sababu hiyo akasisitiza kutoachiwa kwa vikundi vya dini vyenye misimamo mikali  kuharibu na kuvuruga amani  na maendeleo na kazi nzuri inayofanywa na madhehebu ya dini .  “Hatuwezi kuruhusu kundi dogo la watu wenye misimamo mikali  kuharibu kazi nzuri zinazofanywa na  jumuia za kidini kwa waumini wao duniani kote” akahimiza Bw. Eliasson.

Akaelezea  wasi wasi wake kuhusu vijana kutumiwa  na vikundi vyenye misimamo mikali kueneza  kampeni za chuki na  vurugu kwa ahadi za kupata dhawabu au wokovu ili wao watimize malengo yao. “Kwa kawaida  vijana wana nguvu.  Tunapashwa  kutafuta   njia nzuri na sahihi za kuwafanya wazitumie nvugu  zao kuboresha maisha yao” akasisitiza Naibu Katibu Mkuu.
Naye  Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Bw. Vuk Jeremic kwa  upande wake alisema  Umoja wa Mataifa unaweza  kufaidika sana  kama viongozi wote wa dini watajihusisha na kufanya kazi kwa moja ili kuleta amani. Huku akiutaka  Umoja huo kuogeza kasi ya kushirikiana na madhehebu ya dini.



“ Hebu basi  na turejee na kukumbatia wito unaotolewa na imani zetu, wito wa kuwasaidia watu wengine wenye matatizo, wito wa kuheshimiana wenyewe kwa  wenyewe,ikiwa  ni pamoja na  uhuru wa kuabudu wakati wowote na mahali popote bila ya kujali tofauti zetu za imani”.



Rais huyo wa Baraza Kuu akasema kila mtu anawajibu wa kuwasiliana na mwenzake na kusahau yaliyopitia na kuonya kwamba kama vyanzo vilivyopita  vya migogoro ya kidini vitaendelea kukumbushiwa mara kwa mara, kuna hatari kubwa ya kuitumbukiza dunia katika  machafuko ya kutisha.

ZIARA YA MAMA SALMA KIKWETE LINDI MJINI

0
0

  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM wilaya ya Lindi mjini, Mama Salma Kikwete mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nanyanje, wilaya ya Chikonje, wilaya ya Lindi mjini.

 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Kata ya Chikonje, wakimsikiliza Mama Salma Kikwete alipozungumza nao katika kikao cha ndani, kwenye Ofisi ya CCM ya Kata hiyo.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM wilaya ya Lindi mjini, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, akimsalimia mwananchi baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara aliohutubia katika kijiji cha Nanyanje, Kata ya Chikonje wilayani humo leo, akiwa katika ziara ya siku saba kukagua na kuimarisha uhai wa Chama na Utekelezaji wa ilani.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Mama Salma Kikwete akipokea kadi ya CUF kutoka kwa aliyekuwa mwanachama wa chama hicho, Salma Saidi (kushoto) baada ya kutangaza kuhamia CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Nanyanje, Kata ya Chikonje mkoani Lindi.





 Mama Salma Kikwete akishiriki kucheza ngoma ya zindiko ya wakazi wa Chikonje, iliyotumbuiza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika leo.
 Wasanii wa kundi la ngoma ya zindiko ya Chikonje wakionyesha umahiri wao katika mkutano huo.
 Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo wa kijiji cha Nanyanje kata ya Chikonje mkoani Lindi.
Wananchi wakiselebuka kwa nyimbo za CCM wakati wa mkutano huo.

ZIARA YA MAMA SALMA KIKWETE mkoani LINDI LEO.

0
0


 Mkazi wa Kijiji cha Ng'apa wilaya ya Lindi mjini, akionyesha kadi yake ya matibabu ya Huduma ya Kadi ulkiopo chini ya Bima ya Afya, wakati wa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete katika kijiji hicho, leo Feb 16, 2013. Mama Salma Kikwete alimpatia fursa ya kuzungumza wakati akihimiza umuhimu wa wananchi kujiunga na mpango huo wa matibabu.


 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Narunyu, Kata ya Tandangongoro, alipokwenda kuhutubia mkutano wa hadhara katika kijiji hicho leo, Feb 16, 2013.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasalimiana na watoto wa kijiji cha Narunyu, Kata ya Tandangongoro, alipokwenda kuhutubia mkutano wa hadhara katika kijiji hicho leo, Feb 16, 2013.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa amegoma kushuka katika gari lake, kukataa kwenda kwenye mkutano wa ndani wa Chama Kata ya Tandangongoro, uliokuwa umepangwa na viongozi wa kata hiyo kufanyika katika chumba cha darasa la shule ya msingi ya kijiji cha Ng'apa, mkoani Lindi, leo Februari 16, 2013. Hatua hiyo iliwalazimu viongozi kutafuta ukumbi mwingine wa dharura. Mama Salma alisema si sahihi mkutano wa ndani wa Chama cha siasa kufanyika katika chumba cha darasa la shule ya serikali
Umati wa wananchi wa Kijiji cha Ng'apa wakimsiliza Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akilipowahutubia mkutano wa hadhara leo, Feb 16, 2013. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO).
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live




Latest Images