Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | 2 | (Page 3) | 4 | 5 | .... | 1897 | newer

  0 0


   Waziri wa Ajira na Kazi, Gaudensia Kabaka (kushoto), akitembelea moja ya miradi mikubwa ya ujenzi wa shule inayotekelezwa na mgodi wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold (ABG) wakati wa ziara yake kwenye mgodi huo uliopo wilaya ya Tarime mkoa wa Mara hivi karibuni. Kushoto kwa waziri ni Mkurugenzi wa ABG wa Mahusiano na Serikali, Bw. Emmanuel ole Naiko.
   Waziri wa Ajira na Kazi, Gaudensia Kabaka (katikati), akitembelea moja ya miradi mikubwa ya ujenzi wa shule inayotekelezwa na mgodi wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold (ABG) wakati wa ziara yake kwenye mgodi huo uliopo wilaya ya Tarime mkoa wa Mara hivi karibuni. Kulia  ni Mkurugenzi wa ABG wa Mahusiano na Serikali, Bw. Emmanuel ole Naiko.
  Waziri wa Ajira na Kazi, Gaudensia Kabaka (kulia), akitembelea kituo cha afya cha Nyangoto kilichopo wilaya ya Tarime, mkoa wa Mara, ambacho kimepata ufadhili mkubwa wa ukarabati na vifaa kutoka kwa mgodi wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold (ABG). Pembeni ya waziri ni Mkurugenzi wa ABG wa Mahusiano na Serikali, Bw. Emmanuel ole Naiko.

  =======   =======   =======  =====

  Serikali yaahidi kumaliza tatizo la fao la kujitoa

  MWANDISHI WETU

  Tarime

  SERIKALI imewataka wafanyakazi wa sekta ya madini kuwa watulivu wakati inafanyia kazi malalamiko yao kuhusu fao la kujitoa katika mifuko ya hifadhi ya jamii, ambapo amesema inaandaa utaratibu maalumu utakaowawezesha wanachama wa mfuko husika kunufaika nao wakiwa kazini ama baada ya kumaliza utumishi wao.

  Serikali imewasisitizia wafanyakazi nchini kuwa suala hilo limepewa kipaumbele ili kupatiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

  Ari hiyo ilitolewa hivi karibuni na Waziri wa Ajira na Kazi, Gaudensia Kabaka, wakati akizungumza na wafanyakazi wa mgodi wa dhahabu wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold (ABG) wakati wa ziara yake kwenye mgodi huo uliopo wilaya ya Tarime, mkoa wa Mara.

  Waziri huyo aliwasihi wafanyakazi wenye mawazo ya kuacha kazi ili tu wachukue mafao yao ya kujitoa kuachana na fikra hizo potofu ambazo alisema zitaleta athari kwa familia zao.

  Bi.Kabaka amesema serikali imesikia kilio cha wafanyakazi we sekta ya madini na wengine na kwamba kwa pamoja na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), wako katika jitihada za kuangalia jinsi ambavyo wanachama walioandikishwa kwenye pensheni kama wanaweza kuanzishiwa utaratibu wa kuweka na kukopa yaani "supplementary scheme."

  "Serikali haijafikia uamuzi wakati wowote wa kufanya kuhusiana na mtu ama watu wanaotaka kujitoa katika fao hilo ndio maana niko hapa," alisema. Alitangaza kuwa serikali itakutana na SSRA na watu wa sekta ya madini jijini Dar es Salaam tarehe 7 Januari, kwa ajili ya kupata mawazo yao juu ya suala la mafao ambapo wafanyakazi wa Migodini watawakilishwa na wawakilishi  wao amabo ni chama cha wafanyakazi.

  Alisema kuwa serikali haina haraka juu ya suala hilo kwa kuwa inataka kusikiliza mawazo ya wananchama wote, Watanzania, wabunge na wadau mbalimbali ili kupata maoni ambayo yatatafsiriwa kisheria. Alisema serikali itawasikiliza Watanzania ili kujua ni nini wanapenda kiwepo katika masuala ya hifadhi ya jamii kwa sababu sheria na sera siyo msahafu hivyo inaweza kubadilika kila mara kutokana na mahitaji ya wakati husika.

  Waziri Kabaka pia alitembelea miradi mbalimbali ya jamii inayofadhiliwa na mgodi huo wa Barrick na kuisifu kampuni hiyo kwa kusaidia jamii. Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa shule mpya na ukarabati mkubwa wa kituo cha afya cha Nyangoto

  0 0

  Bondia Mada Maugo (Tanzania) akitangazwa mshindi baada ya kumtwanga bondia Yiga Juma (Uganda) kwa ‘Knock Out’ raundi ya kwanza.
  Bondia Mbwana Matumla (Tanzania) akitangazwa mshindi baada ya kumpa kichapo bondia David Charanga (Kenya).
  Mada Maugo (kushoto) akimshushia kichapo bondia Yiga Juma (Uganda) wakati wa mpambano wao.
  Bondia Mbwana Matumla (kulia) akitupiana makonde na bondia David Charanga kutoka Kenya.
  Bondia David Charanga kutoka Kenya (kulia) akienda chini baada ya kupokea konde kutoka kwa Mbwana Matumla.
  David Charanga kutoka Kenya (kulia) akimkabili bondia Mbwana Matumla wakati wa mpambano wao jana.
  --
  Mabondia wa Tanzania jana waling'ara katika mapambano yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala Zakhem. Bondia maarufu nchini, Mada Maugo alimchapa Yiga Juma kutoka Uganda raundi ya kwanza kwa ‘Knock Out’. Katika hali iliyoonesha kuwa siku ya vichapo kwa wageni, pambano lingine ambalo bondia Mbwana Matumla alipambana na bondia kutoka Kenya, David Charanga lililokuwa la raundi nane, Matumla aliibuka kidedea katika raundi zote nane na kumfanya aibuke na ushindi wa kishindo.
  (PICHA NA ISSA MNALLY NA RICHARD BUKOS / GPL)

  0 0


   Mgeni rasmi katika kampeni ya Mradi wa Upandaji Miti jijini Mwanza, Henry Mongi, akipanda mti  wakati wa kampeni hiyo katika moja ya mitaa ya jiji hilo.Anayeshudia kulia ni Afisa Ubora wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Caroline Muhonoli na wa pili kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Mkuyuni, Fasheni Lugo. Mradi huo umefadhiliwa na Kampuni ya Bia Tanzania.
   Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Steven Kilindo, akifukia udongo kwenye shimo alilopanda mti wakati wa kampeni ya upandaji miti jijini Mwanza mwishoni mwa wiki..Wanaoshuhudia katikati ni Meneja Ubora wa kampuni hiyo, Caroline Muhonoli na nyuma ya Kilindo ni Diwani wa Kata ya Mkuyunim, Lugo Fashen.TBL imetumia zaidi ya milioni 30 kupanda miti 7000 katika mikoa ya Mwanza,Kilimanjaro na Mbeya. Kwa Mkoa wa Mwanza pekee imetumia sh. mil. 10 kupanda miti 2600.
   Meneja wa TBL Mwanza, Richmondx Raymond akipanda mti katika uzinduzi wa mradi wa upandaji miti jijini Mwanza mwishoni mwa wiki, uliofanywa na kampuni hiyo kwa kupanda miti 2600 kando kando ya barabara za Balewa, Kenyatta, machemba na shule za sekondari Nyamaganana na Nyegezi na Kiwanda cha Bia cha kampuni hiyo. 

  0 0

  Rais Jakaya Kikwete akionesha mbwa mwitu(hawapo pichani) wanavyorejea katika hifadhi ya Serengeti mara baada ya kuachiwa kutoka katika banda maalum walilokuwa wamehifadhiwa ikiwa ni awamu ya pili ya kundi la mbwa hao chini ya Mradi wa Uhifadhi na Ulinzi wa wanyama hao walio katika hatari ya kutoweka. Vodacom Foundation hadi sasa imeshatumia zaidi ya Sh 450 Milioni kufadhili mradi huo kama sehemu ya kuchangia maendeleo ya sekta ya Utalii nchini. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Tifa - TANAPA Allan Kijazi, Meneja wa Mahusiano ya Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim na Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon.
  Rais Jakaya Kiwete Kikwete akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)katika eneo la Nyamuma ndani ya hifadhi ya taifa ya Serengeti mara baada ya kuongoza zoezi la kuwaruhusu mbwa mwitu kumi na watano kurejea hifadhini baada ya kuwa chini ya uangalizi maalum kupitia mradi wa Uhifadhi na Ulinzi wa Wanyama hao walio katika hatari ya kutoweka. Vodacom Foundation hadi sasa imeshatumia zaidi ya Sh 450 Milioni kufadhili mradi huo kama sehemu ya kuchangia maendeleo ya sekta ya Utalii nchini.


  0 0
  Afyacheck ni kipindi kipya cha tv ambacho kinakupa fursa ya kujua afya yako. pia utapata nafasi ya kuuliza maswali yakusu afya. na utajibiwa. kipindi hiki kitakua kinaruka kupitia Clouds tv. Hii link niya kipindi cha kwanza cha afyacheck inazungumziwa swala zima la afya ya uzazi tazama uone mtoto anavyo patikana kila hatua inaonekana mpaka mbegu zinavyo ungana.

  0 0
 • 12/27/12--09:47: Barnaba na Suma Lee Video

 • 0 0
 • 12/27/12--10:04: DEATH ANNOUNCEMENT

 • THE FAMILY OF PROF. BRUNO J. NDUNGURU REGRET TO ANNOUNCE THE SAD DEATH OF THEIR BELOVED, PROF. BRUNO J. NDUNGURU WHO PASSED AWAYON WEDNESDAY 26TH DECEMBER AT AMI HOSPITAL IN DAR ES SALAAM.

  THE WAKE WILL BE HELD AT HIS RESIDENCE IN BOKO.

  HIS BURIAL WILL BE ON SATURDAY 29TH DECEMBER 2012 IN DAR ES SALAAM.

  WHAT GOD GIVES, GOD TAKES. MAY HIS SOUL REST IN ETERNAL PEACE.

  FOR MORE INFORMATION CALL: 0754 300408 - CORETHA

  0 0


  0 0


  Mbunge wa Rorya Lameck Airo akifanya uzinduzi rasmi wa shule ya msingi kata ya Kirogo yenye madarasa mawili tu huku mengine mapya yakiendelea kujengwa kwa nguvu ya wananchi pamoja na sapoti ya mbunge huyo kama sehemu ya kusapoti maendeleo ya elimu wilaya ya Rorya mkoani Mara. 


  Hatua yapili kuelekea kuona kibao cha uzinduzi. 


  Hatua hii nifaraja kwa wananchi wa kata ya Kirogo kwani ni safari kuelekea kuisaka elimu bora yenye manufaa kwa watoto waishio maeneo ya karibu katani humu.


  Jiwe la msingi la jengo hili limewekwa na Mhe. Lameck Airo Mbunge wa Wilaya ya Rorya tarehe 21/12/2012.

  Uhaba wa madawati katika shule nyingi za msingi na sekondari nchini umeendelea kuumiza vichwa vya wengi wapenda elimu pamoja na wazazi kwa ujumla hali iliyomlazimu mbunge Lameck Airo kujisukuma kuchangia madawati kama inavyoonekana pichani ndani ya moja ya madarasa haya.


  Mara baada ya kufanya ufunguzi kwa shule hiyo Mhe. Mbunge Lameck Airo alizungumza na wananchi wa kata hiyo kuweka msisitizo kwa masuala kadhaa ikiwemo matunzo ya majengo ya shule, ukarabati wa kila mara, kuhamasisha elimu na uboreshaji wa michezo.


  Wananchi wa kata ya kirogo wakimsikiliza kwa umakini Mbunge wao kwenye kusanyikohilo.


  Mzee kiongozi wa kata hiyo akimkabidhi Mhe. Mbunge Lameck Airo zawadi ya kuku dume (Jogoo) kuafiki mchango wake katika maendeleo ya kata ya Kirogo. 


  Mmoja wa akinamama wa kata ya Kirogo akijidai na vazi lake kusanyikoni.


  Katika kuchangia na kuendeleza michezo ndani ya kata ya Kirogo Mbunge wa Rorya Mhe. Lameck Airo aliikabidhi mipira kwa Captein wa timu ya Cheleche Fc George Fabian (kushoto) kama hamasa kwa timu hiyo iliyo moja ya timu zinazofanya vizuri katika uwakilishaji kata hiyo kwenye kandanda.


  0 0

   Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Mtwara Mjini wakiwa kwenye maandamano makubwa waliyoyafanya mapema leo kupinga gesi kusafirishwa kwenda Dar!
   Wakazi hao wakiwa na mabango yao yenye jumbe mbalimbali kama uonavyo pichani

   Waandamanaji wakiwa wamekusanyika kwenye moja ya uwanja mjni Mtwara mapema leo wakipinga gesi kusafirishwa kwenda jijini Dar! 

    Mmoja wa wakazi wa mji wa Mtwara mjini akiwa amebeba bango lake
  Baadhi ya askari wakiwa kwenye gari yao wakiangalia usalama wa hapa na pale kufuati maandamano makubwa yalliyofanya na wakazi wa Mkoa wa Mtwara, mapema leo wakipinga gesi kusafirishwa kwenda jijini Dar!

  0 0

   Heineken Tanzania Team in a group photo
   from Right: Uche Unigwe – Country Manager Tanzania, Elizabeth Buitendijk – PA to the Country Manager and Koen Morshuis – General Manager East Africa. 

  from left to right: Uche Unigwe-Tanzania Country Manager, Fey Gwendolene Bananuka – Hassan – Trade Marketing Consultant Tanzania and Koen Morshuis-General Manager East Africa.

  ======     =======  ======

  Heineken rewards best performing employees


  Heineken celebrates end of the year party by rewarding best performing employees

    
  Heineken Tanzania has celebrated its end of the year party at Akemi restaurant in Dar es Salaam, by rewarding its best performing employees for the year 2012.


  The event gathered Heineken employees, customers, suppliers, community members and VIPs around a great atmosphere while enjoying the entertaining program and delicious food.


  Mr Uche Unigwe, Heineken Tanzania Country Manager, welcomed everyone and wished them a very festive 2013, mentioning Heineken achievements and expansion plans.


  “I am very pleased to tell you that Heineken has done exceptionally well in Tanzania for this year, and this is just the beginning as we have many amazing things in the horizon for 2013’ said Unigwe.


  Heineken has had an outstanding year in Tanzania as they have made major waves in the market when they launched the Heineken Champions Planet in Masaki.  Giving an exclusive location where football fans could watch most of the UEFA Champions Cup action on big screen TV’s while enjoying the Heineken brand with friends.  Heineken Champions planet was followed by an exclusive black carpet premier event at Century Cinemas that rewarded 300 loyal consumers and their partners as well as A list celebrities with a private premier of the latest James Bond movie, Skyfall, in Dar es Salaam one day before the movie premiered in London or Hollywood. 


  On the ground, HEINEKEN has partnered with key outlets in Dar es Salaam and have gone well beyond the usual activity of most beer brands which are notorious for limiting their support to placing signboards and posters, at Didi’s Pub in Dar, HEINEKEN invested in complete renovation of the Oyster Bay landmark. Some of the upgrades that HEINEKEN provided include new lighting, new seating, tiled flooring, and windows.


  It was this year again that Heineken also formalized their local operations and opened the HEINEKEN Tanzania Limited offices in Oyster Bay.  With these offices now open, HEINEKEN is relying upon their local team of majority Tanzanian’s to manage the everyday marketing of the brand, alongside with landing a new distribution partner, Maxam, who is slated with the task of ensuring that the Heineken brand is available everywhere in Tanzania thus tying up loopholes that previously existed within the distribution chain.


  HEINEKEN Country Manager, Mr. Uche Unigwe said that this year’s activities are just a beginning for the Heineken brand in Tanzania and East Africa as a whole. “We are here for the long haul and have some things in store for 2013 that will shake up the market” said Unigwe.


  “HEINEKEN has always been known for being a market leader in creativity and innovative ways to reach our target consumers, our events this year in Tanzania have proven that fact and in 2013 we intend to take the Heineken brand to the next level” added Unigwe.

  0 0


  Ile siku iliyosubiriwa na watanzania wengi kutaka kujua nani ataibuka mshindi wa shindano la kumsaka mwanamitindo wa mwaka mwenye sifa za pekee nchini Tanzania imewadia .Homa ya shindano imezidi kupanda ikiwa usiku wa leo atajulikana nani atavishwa taji la unque model of the year 2012 taji lenye heshima katika tasnia ya mitindo nchini Tanzania.

  Jumla ya washiriki kumi na mbili wanapanda kujwaani kuwania taji hilo ikiwa fainali zake zitafanyika katika ukumbi wa maraha New Maisha club uliopo Oysterbay jijini Dar. Wanaowania taji hilo ni Vestina Jax,Judith sangu,Amina Ayoub,Catherine Masumbigana,Elizabeth Pertty,Elizabeth Boniface,Vivian  Gilbert ,Darline Mmari , Zeenath   Habibb,Sandra Suleiman,Cecilia Emmanuel,Magreth Msafiri.

  Mratibu wa shindano hili Bwana Methusela Magese amewaomba watanzania wajitokeze kwa wingi siku ya kesho kwani kuna mambo mazuri ya kufurahisha ikiwemo burudani ya muziki wa bendi toka kwa mashujaa,ngoma za asili na bongo flava  kwa kiingilio cha Tshs 15,000/= tu.

  0 0
 • 12/27/12--20:57: gari lateketea kwa moto.

 • GARIMOTO1 GARIMOTO3 GARIMOTO2Baadhi ya vijana wa eneo hilo wakijaribu kukwapua baadhi ya spea za gari hilo wakati likiungua.

  GARI aina ya Toyota Starlet lenye namba za usajili T 382 BUN mali ya mwanamke mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake, limeteketea kwa moto nje kidogo ya ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam zilizopo Ilala – Boma. Kitendo cha ajabu ni kuona vijana waliokuwa eneo hilo baada ya kusaidia kuzima moto usiendelee kuliteketeza gari hilo, walionekana wakiwa ‘busy’ kung’oa baadhi ya spea za gari hilo. Picha kwa hisani ya William

  0 0

  So grab your swimsuits and come get WeTT @ thE Last " HOT & WET POOL & BeACH Xperience @ the most beautiful AZURA Beach (next 2 kawe bridge) From 11:30am-8pm!

  Entry: 10,000 inclusive of Water! Barbecue, 2$ Cocktails, Music by Dj SuMMeR, HOTT People Getting WETT all day by the Pool or at the beach! Grab a friend n Come enjoy the Xperience! Oh yea..U can Bring UR Own BottLes! Can't Beat That!

  HaPPy New Year!
  DONT MISSSSSS!!!!

  0 0

   Washiriki wa Warsha ya Usimamizi wa mazao na bidhaa zitokanazo na bioteknolojia ya kisasa wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi (katikati) Mara baada ya kufungua warsha hiyo kwenye Hoteli ya La kairo Jiji Mwanza. 
    Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Ngosi Mwihava akisalimiana na Afisa Afya Mkoa wa Shinyanga Bw. Nyanza Masakilija mara Baada ya Ufunguzi wa Warsha ya Usimamizi wa Mazao na bidhaa zitokanazo na Bioteknolojia ya kisasa katika Hoteli ya La Kairo Jiji Mwanza
   Baadhi ya Washiriki wa Warsha ya Usimamizi wa mazao na bidhaa zitokanazo na bioteknolojia ya kisasa wakimsikiliza Mgeni Rasmi Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Ngosi Mwihava [pichani hayupo] kwenje Hoteli ya La kairo Jiji Mwanza [Picha na Ali Meja] 
   Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Ngosi Mwihava akifungua Warsha kwa maafisa wa mipakani kuhusu usimamizi wa mazao na bidhaa zitokanazo na Bioteknolojia ya kisasa. Kulia ni Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Julius Ningu na kushoto ni Afisa Mazingira Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Esta Makwaia. Warsha hii imefanyika leo kwenye Hotel ya La kairo jijini Mwanza.
  =======  =======  =====

  Lulu Mussa na Ali Meja

  Mwanza


  Imeelezwa kuwa Tanzania kama nchi nyingine haiwezi kukwepa maendeleo ya bioteknolojia kutokana na utandawazi na maendeleo dunia kote, kwa kuwa bioteknolojia ya kisasa ni nyenzo muhimu katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini, kuboresha kilimo, uzalishaji viwandani, afya na hifadhi ya mazingira.


  Hayo yamesemwa leo na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Ngosi Mwihava katika warsha ya siku moja kwa maafisa wa mipakani kutoka mikoa ya kanda ya ziwa, warsha iliyolenga kukuza uelewa kwa watendaji wanaosimamia mazao na bidhaa zitokanazo na bioteknolojia ya kisasa.


  Amesema, Serikali kwa kutambua mchango mkubwa unaoweza kupatikana kutokana na matumizi ya bioteknolojia ya kisasa katika sekta za afya, kilimo, viwanda na mazingira, imeridhia Itifaki ya Cartagena ya Mkataba wa Bioanuai mwaka 2003 kwa lengo la kuhifadhi mazingira kwa kuzingatia usalama katika usafirishaji,  kuunda na kupitisha mfumo wa kitaifa wa usimamizi wa matumizi salama ya Bioteknolojia mwaka 2007.


  Eng. Mwihava amewaasa watendaji katika maeneo ya mipakani kuwa na usimamizi madhubuti katika maeneo yao ya kazi kwa kuwa mipaka kati ya Tanzania na nchi nyingine ndiyo njia kuu za uingizaji wa mazao na bidhaa zitokazo nje.


  Pamoja na faida za bioteknolojia hiyo ya kisasa Eng. Mwihava amewataka watendaji hao kuwa makini na athari zinazoweza kutokana na matumizi ya teknolojia hiyo pale itakapotumiwa bila kufuata taratibu za usalama zilizowekwa.


  Warsha hii ya siku moja kwa imewashirikisha maafisa forodha, Maafisa Afya na watafiti wa Mazao kutoka Mikoa ya Mwanza, Mara na Kagera,  kutoka Idara , wakala za Serikali na sekta binafsi.


  0 0  THE FAMILY OF PROF. BRUNO J. NDUNGURU REGRETS TO ANNOUNCE THE SAD DEATH OF THEIR BELOVED, PROF. BRUNO J. NDUNGURU WHO PASSED AWAYON WEDNESDAY 26TH DECEMBER AT AMI HOSPITAL IN DAR ES SALAAM.

  THE WAKE WILL BE HELD AT HIS RESIDENCE IN BOKO.

  HIS BURIAL WILL BE ON SATURDAY 29TH DECEMBER 2012 AT KINONDONI CEMETERY IN DAR ES SALAAM.

  WHAT GOD GIVES, GOD TAKES. MAY HIS SOUL REST IN ETERNAL PEACE.

  FOR MORE INFORMATION CALL: 0754 300408 - COLLETA


  0 0


  Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla akizungumza wakati wa Mkutano huo.
  ====== ===== =====
  Naibu Waziri, Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla akiwa na mwigizaji, Raymond Kindosi (Ray) muda mfupi baada ya kumalizika kwa Mkutano wa wasanii na wadau wa Tasnia ya muziki uliofanyika katika Ukumbi wa Wizara hiyo leo

  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla akiwa na baadhi ya wasanii muda mfupi baada ya kumalizia kwa Mkutano huo


  0 0

  Kikosi cha timu ya Chama Cha waandishi wa habari za Mizhezo TASWA FC kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa kirafiki kati yake na timu ya Bagamoyo Veteran uliofanyika kwenye uwanja wa Mawanakerenge Mjini Bagamoyo jioni ya leo, ambapo timu ya TASWA FC imechapwa magoli 4-0 na maveterani hao kutoka mjini Bagamoyo,
  Timu ya Waandishi wa habari ya TASWA FC imeshiriki katika mchezo huo ikiwa ni moja ya programu ya mkutano wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika kesho kwenye hoteli ya Kiromo View mjini Bagamoyo ambapo utafunguliwa na Ridhiwani Kikwete na Kufungwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ndugu Assah Mwambene PICHA NA FULLSHANGWEBLOG.
  Hiki ndiyo kikosi cha timu ya Bagamoyo Veteran kilichotoa kichapo kwa timu ya TASWA FC mjini Bagamoyo leo.
  Baadhi ya waandishi wa habari ambao ni mashabiki wa timu hiyo wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
  Mjumbe wa kamati ya utendaji wa klabu ya Simba Ibrahim Masoud katikati akizungumza na Mzee Willy Chiwango kutoka gazeti la This Day kulia na Beny Kisaka mkurugenzi mwanadamizi gazeti la Jambo Leo.
  Mkuu wa Wilala ya Bagamoyo Ahmed Kipozi wa pili kutoka kulia akizungumza na mwandishi mkongwe kutoka Zanzibar Said Salim huku wanahabari wengine wakifuatilia mazungumzo hayo.
  Mchezaji wa timu ya TASWA FC Juma Pinto akimiliki mpira mbele ya beki wa timu ya Bagamoyo Veterani katika mchezo huo uliofanyika kwenyeuwanja wa Mwanakerenge mjini Bagamoyo
  Mchezaji wa timu ya TASWA FC Shafii Dauda akimiliki mpirahuku beki wa timu ya Bagamoyo Veterani akiuwania katika mchezo huo, katikati ni mchezji wa timu ya TASWA FC Mohamed Akida.
  Mshauri wa timu ya TASWA FC Masoud Sanani akihimiza wachezaji wa TASWA FC kucheza kwa bidii baada ya kuchapwa magoli 4-0 huku wachezaji wa timu hiyo wakishangaa wasijue la kufanya wakati zikiwa zimesalia dakika za majeruhi.

  0 0

  Mwanamitindo bora wa mwaka 2012 Catherine Masumbiga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Unique Model Photogenic Elizabeth Pertty (kushoto) na Unique Model Talent Vestina Charles mara baada ya kutangazwa kwa mshindi.
  Mwanamitindo wa mwaka 2012 Catherine Masumbiga (katikati) amepatikana jana usiku kwenye shindano lililofanyika kwenye Klabu ya New Maisha jijini Dar es Salaam akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa pili Cesilia Michael (kushoto) na mshindi watatu Amina Ayubu.


  Washiriki waliongia tano bora.
  Washiriki waliongia tano bora.
  Majaji wa shindano hilo kutoka kushoto ni Gymkhana Hilal kutoka Paka Wear , Asia Idarous na Martine Kadinda.
  Unique Model Talent of the year 2012 Vestina Charles akionyesha uwezowake wa kucheza jukwaani.
  Wakitumbuiza mashabiki mapema kabla ya kuingia kuonyesha mavazi ya aina mbalimbali.
  Washiriki 12 wa shindano hilo wakiwa wamejipanga tayari kusubiri kutangazwa mshindi.

  0 0


  Mh zitto Kabwe
  Maandamano ya amani yaliyofanyika mjini Mtwara siku ya alhamis wiki hii yameibua hoja mbali mbali kutoka kwa viongozi, wananchi, vyombo vya habari na mjadala wa siku nzima kwenye mitandao ya kijamii hasa facebook, twitter na JamiiForums. Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ameita waandamanaji wapuuzi na Waziri wa Nishati na Madini amewaita watu hatari na wahaini. CHADEMA tumetoa kauli kupitia kwa Waziri Kivuli wa Nishati na Madini kwamba udhaifu wa utendaji serikalini ndio chanzo cha maandamano haya.
  Lakini kuna tatizo kubwa zaidi ambalo linaonekana siyo katika sekta hii tu bali pia katika sekta nyingine ambapo tunaona matokeo yake katika maisha ya watu wetu na naweza kusema ni dalili za kushindikana kwa sera za CCM. Sera hizi ndizo ambazo zimelifikisha taifa hili hadi hapa. Kama hadi wananchi wa Mtwara ambako kwa muda mrefu imekuwa ni ngombe ya CCM wanaanza kuhoji matokeo ya sera za chama tawala basi ni dalili kuwa Watanzania wamefungua macho yao na wanaona.
  Wanaona katika nishati, wanaona katika utawala bora, wanaona katia elimu (kuanzia ya msingi hadi ya juu kabisa!), wanaona katika afya, wanaona katika utendaji wa jeshi la polisi wanaona katika madini. Sera za CCM zimeshindwa. Zimeshindwa kuinua maisha yao na zinaonekana kuendelea kushindwa.
  Mtwara na Lindi wanataka nini?.
  Watu wa Mtwara wanataka gesi isiondoke Mtwara na badala yake viwanda na mitambo ijengwe Mtwara kisha kama ni umeme au mbolea isafirishwe kupelekwa sehemu nyingine ya nchi. Watu wa Mtwara hawasemi kwamba Gesi yote na mazao yake vibaki Mtwara na Lindi. Wanasema umeme uzalishwe Mtwara usambazwe nchi nzima. Mbolea izalishwe Mtwara na kusambazwa nchi nzima. Wanataka Bandari ya Mtwara iboreshwe na kuhudumia mikoa ya Kusini. Watu wa Mtwara hawasemi kwamba mapato yote ya Gesi yatumike Mtwara tu la hasha.
  Sio dhambi hata kidogo kwa watu wa Mtwara kudai masuala haya. Watu wa Mtwara wamefanya maandamano kwa amani kabisa bila kuharibu mali na kutoa maoni yao. Kwanini tuwasute na kuwasusubika kwa madai yao haya? Kwa nini tusiwasikilize? Kosa lao nini kudai viwanda ili wapate ajira? Tumesahau kuwa mikoa ya Lindi na Mtwara ni mikoa masikini kabisa nchini? 
  Tumesahau kuwa mikoa ya Lindi na Mtwara ilitumika kwa ukombozi wa kusini mwa Afrika kiasi cha kuwa katika hatari kabisa? Tumesahau ‘sacrifice’ ya watu wa Mtwara na Lindi dhidi ya usalama wa nchi yetu? Tumesahau kuwa Korosho imekuwa zao kubwa la biashara na linaloingiza mapato mengi sana ya Fedha za kigeni? Waziri Muhongo anasema Mtwara warudishe Fedha za Mkonge na Kahawa. Mbona hataji fedha za Korosho? Mwaka 2011 Korosho ilikuwa zao la pili kwa kuingiza fedha nyingi za kigeni baada ya Tumbaku.
  Lakini tujiulize, watu wa Mtwara na Lindi walifadi fedha za Mkonge? Walifaidi fedha za Kahawa? Wamefaidi fedha zao za Korosho? Tumesahau hata Reli iliyoachwa na Mkoloni ya Nachingwea – Mtwara iling’olewa na Serikali huru ya Tanzania?
  Tujiulize zaidi, hivi watu wa Nzega wamefaidika vipi na Mgodi wa Resolute pale Lusu? Mgodi umefungwa ukiwa umezalisha na kuuaza dhahabu ya thamani ya dola za marekani 3.3 bilioni. Hivi katika uhai wa mgodi huu Serikali Kuu imekusanya kodi kiasi gani? Halmashauri ya Wilaya ya Nzega imepata ushuru kiasi gani? Watu wa Mtwara wanayaona haya yaliyotokea Nzega na yanayotokea Tarime, Biharamulo, Kahama na Geita. Watu wa Mtwara wana Haki kuandamana kuzuia haya yaliyotokea wenzao yasiwatokee wao kwenye Gesi asilia.


  Mtwara na Lindi wanakosea wapi?
  Madai yao halali na mimi binafsi na chama changu tunayaunga mkono. Lakini kuna mahala lazima waelimishwe.
  Watu wa Mtwara pia wanapaswa kuelewa kuwa juhudi zao zisiwatenganishe na Watanzania wengine kwani bado utajiri wa Taifa unafadisha kikundi cha Watanzania wachache sana. Watu wa Mtwara wanahitaji kuungana na watu wa Mara, watu wa Mwanza, watu wa Shinyanga na watu wa Kagera kudai utajiri wa nchi utumike kwa maendeleo ya watu badala ya kunufaisha kundi dogo la watu. Watu wa Mtwara wanapaswa kuunganisha nguvu na Watanzania wengine kuzuia uporaji wa rasilimali ya nchi dhidi ya kizazi kijacho. Watu wa Mtwara wasijitenge wakawa peke yao na Gesi yao. Nguvu ya mnyonge ni umoja.
  Serikali isiyosikia
  Serikali ina hoja kuhusu kujenga Bomba la Gesi kwa ajili ya kuzalisha umeme kwa gharama nafuu. Umeme unaotumiwa na asilimia 14 tu ya Watanzania. Kwa kuwa hii asilimia 14 ndio wenye sauti basi watu wa Mtwara wataonekana hawana hoja kabisa. Lakini Serikali imejiuliza mara mbilimbili kuhusu mradi huu wa Bomba? 
  Tunaambiwa na Wataalamu kwamba kuna uwezekano mkubwa mwakani gesi asilia ya kiasi cha futi za ujazo trillioni 20 itakuwa imegunduliwa katika Kitalu namba 7( block 7) ambacho kipo mkoani Dar es Salaam katika Wilaya ya Temeke. Iwapo gesi nyingi hivi itakuwa hapa Dar karibu kabisa na mitambo ya kuzalisha umeme, mradi huu wa Bomba unaojengwa kwa trillioni za shilingi utakuwa na maana tena? Huu mkopo utakuwa na tija?
  Serikali imewaambia watu wa Mtwara gharama za kuleta bomba Dar dhidi ya gharama za kujenga mtambo wa kuzalisha umeme Mtwara na kuusafirisha umeme kwenda maeneo mengine ya Tanzania? Serikali imeangalia faida ya kujenga gridi nyingine badala ya kuwa na gridi moja tu yenye kushikwa na bwawa la Mtera? Leo bwawa la Mtera lisipozalisha hata megawati moja hata Dar es Salaam izalishe megawati alfu kumi umeme hautakuwapo maana uti wa mgongo wa gridi ni Mtera! Kwa nini tusiwe na gridi nyingine yenye uti wa mgongo Lindi au Mtwara?
  Tuwasikilize watu wa Mtwara
  Watanzania sio mabwege tena. Kuwaita watu wa Mtwara ni wahaini, wapuuzi au watu hatari haisaidii kujenga Taifa moja lenye watu huru. Serikali na wadau wote wa sekta ya Gesi likiwemo Bunge washirikiane na watu wa Mtwara kuhusu miradi ya gesi asilia. Tuwe na Azimio la Mtwara, tamko la kuelekeza namna bora ya kutumia utajiri wetu wa Gesi bila kuathiri umoja wa Taifa letu.
  Ujio wa Sera, Maono na Uongozi Mbadala
  Sasa hivi wananchi wa Mtwara kama wananchi wa sehemu nyingine wanahitaji maono mbadala, uongozi mbadala, sera mbadala na mwelekeo mbadala wa kitaifa ambao utaangalia mahitaji yao, utazingatia raslimali zilizopo na utaunganisha utendaji wa sekta mbalimbali katika kutengeneza mfumo wa kiutawala na kiuchumi ambao utaliinua taifa zima.
  Ni kwa sababu hiyo naamini chama changu ni jibu sahihi kwa matamanio na kiu ya wananchi wa Mtwara na sehemu nyingine nchini. Ikumbukwe kuwa katika Ilani yetu ya Uchaguzi ya 2010 tulielewa haja ya kuangalia mikoa hii ya Kusini kwa namna ya pekee na kuipa mwelekeo wa kipekee katika sera.  Bado tuna makusudio hayo tunapoelekea 2015 na tukishika Dola wananchi wa Mtwara na sehemu nyingine zote zilizoachwa pembezoni mwa mafanikio wajue kuwa wamepata rafiki na mshirika wa karibu wa kushirikiana nao kuleta maendeleo.
  Siyo katika suala la gesi tu bali katika nishati, maji, elimu, miundombinu, kilimo, ufugaji, uvuvi, utalii. Mtwara kama ilivyo mikoa mingine ina raslimali za kutosha kuweza kuwainua wananchi wake kimaisha, na zaidi ya yote kutoa mchango mkubwa wa kiuchumi. Hili ambalo ni kweli kwa Mtwara ni kweli kwa mikoa mingine kama Kigoma, Manyara, Katavi, Lindi n.k.

older | 1 | 2 | (Page 3) | 4 | 5 | .... | 1897 | newer