Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

NGUMI ZILIVYOPIGWA JUMAMOSI MANZESE MASHABIKI WASHANGILIA MWANZO MWISHO

0
0
Bondia Hassana Mlutu akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Iddi Mustafa wakati wa mpamnano wao Mlutu alishinda kwa point mpambano huo.
WACHEZAJI WA NGUMI WA KAMBI YA SINZA MAKABURINI WAKIMPIGA TAFU MWENZAO MORO BEST KUSHOTO NI SHEDRACK IGNAS NA WA PILI KUSHOTO BONDIA MUSTAFA DOTO
Bondia Sako Mwaisege kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Hussein Gobiso wakati wa mchezo wao uliomalizika kwa droo ya kufungana kwa point .
Bondia Hassani Mandula kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Karim Migea wakati wa mpambano wao Mandula alishinda kwa k,o ya raundi ya pili .
Bondia Deo Samweli kushoto akipambana na Mann Issa wakati wa mpambano wao Samweeli alishinda kwa point
Msanii wa muziki wa hipop Karama Masoud 'Kala Pina'  akitumbuiza katika onesho lake lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita lililoandaliwa na kikosi cha mizinga entertainment

Na Mwandishi Wetu

Mpambano wa masumbwi uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita ulioandaliwa na Kikosi cha Mizinga Entertainment ya jijini Dar es salaam

imeleta chachu kwa mabondia mbalimbali baada ya wengi wao kuikubali kampuni hiyo na kuiunga mkono kwa kila hali .Mmoja wa wasisi wa kampuni hi ambaye ni Msanii wa muziki wa hipop Karama Masoud 'Kala Pina'  na Sempai Gola  wameahidi kuwa bega kwa bega na mabondia mbalimbali kwa ajili ya kushiriki katika ngumi zitakazo pangwa tena hivi karibuni

katika mchezo huo bondia Salum Msabaha alimsambalatisha Shabani Hamisi, na George Epson akipewa kichapo na Mohamed Kambuluta na Mwinyi Mzee akitoa droo na Ismail Ndende ,Rashid Mohamed alimshinda Sadiki Nuru kwa point,Hassani Mandula akimsambalatisha bila huruma bondia Karim Migea kwa K,O ya raundi ya pili na Julias Kisalawe akitoa droo na Hassan Kiwale

mpambano huo uliohudhuliwa na mashabiki lukuki ambao awajakaa kwenye viti vyao kwa ajili ya kushangilia mwanzo wa mchezo mpaka mwisho ambapo kila mmoja alifuraia kuona mchezo huo wa masumbwi kwa kushiliki vijana chipkizi wengi na wenye kuelewa nchezo wa ngumi

MBUNGE JOSHUA NASSARI AUAGA UKAPERA,AFUNGA NDOA NAA ANANDE NNKO KANISA LA PENTEKOSTE KILINGA,MERU

0
0
"Mmetuona "ni kama ndio maneno yaliyokuwa vichwani mwao maharusi,Joshua Nassari na Anande Nnko wakionesa vyeti vyao vya ndoa.
Maharusi wakiwasalimia waumini waliohudhuria ibada ya ndoa yao (hawapo pichani).
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Mh. Joshua Nassari na Mai Waifu wake Anande Nnko wakishangiliwa kwa shangwe mara baada ya kumeremeta kwao kwenye kanisa la Kipentekoste la Kilinga,Meru jijini Arusha.



MUIGIZAJI MKONGWE MZEE SMALL AFARIKI DUNIA

0
0
MUIGIZAJI MKONGWE HAPA NCHINI,SAID NGAMBA MAARUFU KWA JILA LA MZEE SMALL AMEFARIKI DUNIA USIKU WA LEO KATIKA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI ALIKOKUWA AMELAZWA AKIPATIWA MATIBABU.

AKITHIBITISHA TAARIFA YA KIFO CHA MZEE SMALL,MWANAE AITWAE MAHMOUD AMESEMA MZEE WAKE AMEFIKWA NA MAUTI HAYO MAJIRA YA SAA NNE USIKU WAKATI AKIWA HOSPITALINI HAPO AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU.

MIPANGO INAFANYIKA NYUMBANI KWAO TABATA NA KADRI TAARIFA ZITAKAVYOKUWA ZIKITUFIKIA TUTAENDELEA KUJULISHANA.

NI PIGO LINGINE TENA KWENYE TASNIA YA SANAA BAADA YA KUONDOKEWA NA WASANII KADHAA MAJUMA YALIYOPITA.

GLOBU YA JAMII IMEPOKEA TAARIFA HII KWA MASIKITIKO MAKUBWA,NA INAMUOMBEA KWA MWENYEZIMUNGU AIWEKE ROHO YAKE MAHALA PEMA PEPONI.

-AMIN.

MKUU WA WILAYA YA NKASI AZINDUA HUDUMA YA OPTION B PLUS MKOANI RUKWA

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi huduma ya Option B Plus Mkoani Rukwa jana tarehe 07 Juni, 2014 katika Kijiji cha Tamasenga Wilayani Sumbawanga. Huduma hiyo ina lengo la kutoa tiba ya kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto mchanga. Kaulimbiu ya huduma hiyo ikiwa "Amka Sasa Tokomeza VVU kwa Watoto, Kama mjamzito Pima VVU kwa maisha Bora, Tiba inapatikana"
Mkuu wa Wilaya Nkasi Iddi Hassan Kimanta (kulia) akipokea taarifa ya utaratibu maalum na tiba ya kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto mchanga kutoka kwa wataalamu wa tiba alipotembelea banda la Hospitali Kuu ya Rufaa ya Mkoa wa Rukwa muda mfupi kabla ya uzunduzi wa huduma hiyo katika viwanja vya Tamasenga Wilayani Sumbawanga. Katika salam zake Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wahudumu wa afya kuzingatia viapo vyao kwa kutunza siri za wagonjwa hususani walipomwa na kukutwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha akisoma risala kwa Mgeni Rasmi katika hafla hiyo ya uzinduzi wa huduma ya Option B Plus. Katika risala yake amesema maambukizi ya virusi vya Ukimwi Mkoani Rukwa yameongezeka ambapo sasa yapo kwa kiwango cha asilimia 6.2. Alisema mpaka sasa jumla ya watumishi 225 sawa na asilimia 75% wameshapatiwa mafunzo ya utoaji wa huduma hiyo ambapo matarajio ni kufikia watumishi 302. Alieleza kuwa mpaka sasa jumla ya vituo 116 vinatoa huduma hiyo sawa na asilimia 83% lengo likiwa kufikia vituo 139 hadi kufikia mwezi Septemba 2014.
Hafla hiyo ya uzinduzi ilipambwa na maandamano ya awali yaliyokuwa yakitoa ujumbe wa mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi kutoka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto mchanga. 
Meza kuu ikipokea maandamano hayo kwa kupiga makofi. Wakwanza kushoto ni Naibu Meya Manispaa ya Sumbawanga,  Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Erasmus Rugarabamu, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta na Mganga Mkuu Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha kushoto akiteta jambo na Mratibu wa Ukimwi Mkoa wa Rukwa Dkt. Hansi Ulaya muda mfupi kabla ya uzinduzi wa huduma hiyo.
Baadhi ya wadau wa huduma ya afya waliohidhuria katika hafla hiyo. 
- Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com

Sheria Ngowi Brand Proudly official designer of Diamond @MTV MAMA

0
0
sheriaDiamond
Diamond Platinumz and Wema Sepetu.
Being nominated in an internationally recognized award worldwide, is a sign of hardworking and thirst to achieve more.
You are really flying our Tanzanian flag globally and yet paved the way for international attention indeed.
Congratulations Diamond Platinumz, you have set a Benchmark. Keep up the good work.
Deogracious Kessy- Head of Marketing
#Sheria Ngowi Brand#

NAPE AKIZUNGUMZA NA WANACHAMA WA CCM SAUT MWANZA

0
0

MAZIWA YA ASAS DAIRIES LTD NDIO MAZIWA BORA TANZANIA YASHINDA TUZO YA UBORA KWA MIAKA MIWILI MFULULIZO ,MAKAMPUNI 30 YAACHWA MBALI

0
0
Afisa masoko wa kampuni ya maziwa ya Asas  Dairies Ltd ya mkoani Iringa Bw Jimy Kiwelu akishangilia baada ya  kampuni yake  kuwa ndio kampuni  bora ya uzalishaji maziwa nchini Tanzania katika mashindano yaliyofanyika mkoani mara
Watoto  wa mkoa wa Mara  wakishangaa ubora wa maziwa ya Asas kutoka Iringa
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dr. Titus Kamani kulia na  viongozi  wengine wakifuatilia maonyesho hayo huku  wakifurahia ubora wa maziwa ya Asas Dairies Ltd.
Picha zaidi BOFYA HAPA

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL MGENI RASMI KWENYE HAFLA YA KUCHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA MISITU YA MILIMA

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal akizungumza kwenye Hafla ya kuchangisha Fedha za kuwezesha Uhifadhi wa misitu ya milima ya Toa la mashariki kwenye hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilali akizindua Tovuti ya (EAMCEF)kwajili ya kuwezesha kuchangia kwa njia ya mtandao kwenye,Hafla ya kuchangisha Fedha za Uhifadhi wa Misitu ya Milima ya Toa ashariki iliyofanyika kwenye hotel ya Hyatt Regency, Jijini Dar es Salaam.
Makamu waRais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal akimkabidhi picha iliyopigwa mnada Bw Robert Vyampiga wa( DECO) Baada ya Kuinunua kwenye Harambe ya kuchangisha Fedha za Kuwezesha Uhifadhi wa Misitu ya Milima ya Toa la Mashariki iliyafanyika kwenye Hotel ya Hyalt Regency Jijini Dar es Salaam.(Picha OMR}

Article 4

0
0
Kikosi cha timu ya Kijitonyama Veterans, ambacho hii leo kimekubari kipigo cha mabao 3-1 bila shuruti kutoka kwa wapinzani wao, Waukae Veterans, katika mchezo wa kirafiki uliochezwa leo asubuhi katika Uwanja wa Kijitonyama. Mabao ya Waukae yamefungwa na Felix Kopou na mawili yakifungwa na Athuma Bamia, huku bao la kufutia machozi la Kijitonyama, likifungwa na Norbert.
Kikosi cha Waukae Veterans.
Wachezaji wa timu zote mbili wakishoo love kabla ya mchezo huo.
Mafoto akisubiri kuchukua nafasi..

RAIS KIKWETE AMEAMURU JESHI LA POLISI KUPELELEZA NA KISHA KUWACHUKULIA HATUA MARA MOJA WATU WOTE WANAOTUHUMIWA KWA WIZI NA UBADHILIFU KATIKA VYAMA VYA USHIRIKA MKOANI TABORA.

0
0
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Dkt. Joseph Komwihangiro, Mkurugenzi wa  Marie Stopes kwa kuwa mstari wa mbele katika huduma na elimu za mzazi wa mpango Jumamosi Mei 7, 2014 wakati akizindua  huduma za uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti Mkoani Tabora, katika uwanja wa Chipukizi mkoani humo.Wengine toka kushoto ni Mama Salma Kikwete, Mlezi wa MEWATA, Dkt. Serafina Mkuwa, Mwenyekiti wa MEWATA, Mhe. Kebwe Steven Kebwe (Mb.), Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, kulia kabisa ni Mbunge wa Tabora Mjini Mhe. Ismail Aden Ragge.
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea Jumamosi Mei 7, 2014 wakati akizindua  huduma za uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti Mkoani Tabora, katika uwanja wa Chipukizi mkoani humo.
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wanakwaya wa kambi ya Msange JKT ya Tabora  Jumamosi Mei 7, 2014 baada ya kuzindua  huduma za uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti Mkoani Tabora, katika uwanja wa Chipukizi mkoani humo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mbunge wa Tabora Mjini Mhe Ismail Aden Ragge   Jumamosi Mei 7, 2014 baada ya kuzindua  huduma za uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti Mkoani Tabora, katika uwanja wa Chipukizi mkoani humo.PICHA NA IKULU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ameamuru Jeshi la Polisi kupeleleza na kisha kuwachukulia hatua mara moja watu wote wanaotuhumiwa kwa wizi na ubadhilifu katika vyama vya ushirika mkoani Tabora. Rais Kikwete amesikitishwa sana na tuhuma hizo zilizosababisha kuwepo kwa tatizo la muda mrefu kwa wakulima wa tumbaku kwa kutokulipwa stahili zao na vyama vya ushirika kwa muda mrefu.

Alisema:  "Kwa upande wa tatizo la wakulima wa tumbaku kutokulipwa stahili zao na vyama vya ushirika nimeelezwa na kulielewa.  Kuna tuhuma za wizi na ubadhilifu.  

“Nimemuagiza Inspekta Jenerali wa Polisi atume watu wake wa upelelezi wa makosa ya Jinai waje wafanye uchunguzi ili wahusika wakamatwe na kufikishwa Mahakamani na kupewa adhabu zinazostahili. 

“Ameniahidi kuwa keshokutwa (Jumatatu)  watu hao watakuja.  Wapeni ushirikiano unaostahili ili tukomeshe uhalifu na dhuluma zinazofanywa na Maofisa wa Vyama vya Ushirika na taasisi za fedha kwa muda mrefu sasa".

Rais aliyasema hayo Jumamosi Mei 7, 2014 wakati akizindua  huduma za uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti Mkoani Tabora, katika uwanja wa Chipukizi mkoani humo.

Rais Kikwete alisisitiza kwamba zoezi la kuchukuliwa hatua watuhumiwa wa wizi na ubadhilifu katika vyama vya ushirika lisifanywe la kisiasa, na kwamba asiogopwe wala kuonewa haya mtu yeyote anayehusika hata awe nani.

MBUNGE MGIMWA AZINDUA VICOBA IHEMI

0
0
Mbunge  wa  jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa akizindua kikundi  cha VICOBA cha Igunga na Amkeni Group kata ya Ihemi
Mbunge  wa  jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa akikabidhi mchango  wake wa Tsh 700,000 kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za vicoba jimboni
……………………………………………………………………….. 
Na Francis Godwin Blog.

WANACHAMA  wa  vikundi  vya Vicoba  Igunga na Amkeni Group kata ya Mgama katika Halmashauri ya  Iringa   wamempongeza mbunge  wa  jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa  kwa  kuviwezesha  vikundi  hivyo mtaji  kwa ajili ya kuwawezesha  wanachama  hao kukopeshana  zaidi.

Mratibu  wa  Vicoba mkoa wa  Iringa Thisiana Kikoti alitoa  pongezi hizo leo  wakati uzinduzi  wa Vicoba katika kijiji  cha Ihemi  .
Kikoti  alisema  kuwa uanzishwaji wa vikundi  hivyo ni  jitihada za aliyekuwa mbunge wa  jimbo la Iringa mjini Monica Mbega ambae  alihamasisha  kuanzishwa kwa  VICOBA mkoani Iringa na katika  jimbo la Kalenga hamasa ya kuanzishwa kwa  vikundi  hivyo  imefanywa na aliyekuwa mbunge wa  jimbo hilo marehemu Dr Wiliam Mgimwa na sasa jitihada  zinazofanywa na mbunge  wa  sasa Godfrey Mgimwa ni  wazi zitafanikisha kukua kiuchumi kwa  wananchi  wa  jimbo hilo.

Alisema  kuwa  lengo  ni kuona  inaanzishwa bendi  ya  VICOBA kwa  ajili ya  kuwawezesha  wananchi zaidi  kiuchumi. Huku  kwa  upande  wake  mbunge Mgimwa  mbali ya  kuchingia  kiasi  cha Tsh 700,000 pia  alisema  kuwa  ndoto ya  mbunge aliyefariki wa  jimbo hilo ilikuwa ni kuanzisha  benki ya maendeleo katika  jimbo la kalenga  na kuwa tayari  alianza  kuandika andiko na suala hilo ataliendeleza .
wakati  huo  huo  mbunge  huyo  ameahidi  kuchangia  kiasi  cha shilingi 700,000 kwa  vikundi vya Ihekima ,tugele na Imani vyenye  wanachama 80 kwa  ajili  ya  kuviwezesha  zaidi
vikundi  hivyo vina akiba  ya shilingi milioni 8 toka vilipoanmzishwa  mapema  mwaka  huu.

WAZIRI CHIKAWE AWAPA URAIA WA TANZANIA WAKIMBIZI WA KISOMALI 1,514 WA KAMBI YA CHOGO, HANDENI MKOANI TANGA

0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akimpa cheti cha uraia  wa Tanzania, Mkimbizi wa Kisomali mwenye asili ya Kibantu, Ramadhani Haji katika hafla iliyofanyika katika Kijiji cha Chogo, Wilaya ya Handeni mkoani Tanga. Waziri Chikawe alitoa vyeti vya uraia kwa wakimbizi 1,514 waliopo katika Makazi ya Chogo ambao waliomba kupewa uraia kwa mujibu wa Sheria ya Tanzania. 

Kulia kwa Waziri ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi nchini, Harrison Mseke. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na mamia ya wakimbizi wa Kisomali wenye asili ya Kibantu (hawapo pichani), baada ya kutoa vyeti vya uraia wa Tanzania kwa wakimbizi 1,514 waliopo katika Makazi ya Chogo, Wilaya ya Handeni mkoani Tanga. Katika hotuba yake, Waziri Chikawe aliwataka Wakimbizi hao ambao sasa ni raia halali wa Tanzania kudumisha amani kwa kufuata sheria za nchi ili waweze kuishi kwa amani. Kulia (Meza Kuu) ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Salum Chima. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (watatu kulia waliokaa), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke (kulia), Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Salum Chima (wapili kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakimbizi wa Kisomali wenye asili ya Kibantu baada ya kupewa vyeti vya uraia wa Tanzania.Waziri Chikawe alitoa vyeti vya uraia kwa wakimbizi 1,514 waliopo katika Makazi ya Chogo, Wilaya ya Handeni mkoani Tanga. Katika hotuba yake, Waziri Chikawe aliwataka Wakimbizi hao ambao sasa ni raia halali wa Tanzania kudumisha amani kwa kufuata sheria za nchi ili waweze kuishi kwa amani. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Sehemu ya Wakimbizi wa Kisomali wenye asili ya Kibantu wanaoishi katika Makazi ya Chogo, Handeni mkoani Tanga wakimshangilia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi (hayupo pichani) alipofika katika makazi yao ili kuwapa vyeti vya uraia wa Tanzania kwa wakimbizi 1,514 waliopo katika makazi hayo baada ya kuomba uraia kwa mujibu wa sheria ya Tanzania. Waziri Chikawe alitoa vyeti kwa wakimbizi hao na kuwataka kudumisha amani kwa kufuata sheria za nchi ili waweze kuishi kwa amani. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Michuzi TV IPO HEWANI...JIUNGE SASA - You'll love it!

0
0
NDUGU MDAU MICHUZI TV SASA IPO HEWANI. 
JIUNGE HARAKA UPATE MAMBO MOTOMTO!!
TUNAANZIA  NA WATEJA WA VODACOM, AMBAO WANAKARIBISHWA KUPIGA  *149*01#  KISHA CHAGUA NAMBA 4 SIMU.tv (MPYA) 
HALAFU NENDA  NAMBA 1. Habari (BURE), 
BAADA YA HAPO 
CHAGUA NAMBA 5 Michuzi TV (BURE) KISHA KUBALI...
UNAKUWA UMESHAJISAJILI KWA HUDUMA HII MPYA. 
LIBENEKE OYE!

Kuelekea Kombe la Dunia...Mahojiano na Halifa Ramadhan kutoka Brazil

0
0

Photo Credits: EyesOnNews.com 
Siku chache kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia la Soka huko Brazil, mambo mengi yamekuwa yakizungumzwa kuhusu maandalizi ya michuano hiyo.
Kuna malalamiko na maandamano nchini humo ambavyo kwa hakika vinaleta taswira isiyo njema kuhusu maandalizi ya michuano hiyo
Kutaka kujua mengi, Kwanza Production imefanya mahojiano na Halifa Ramadhan.
Mtanzania mwenye maskani yake nchini Brazil ambaye amezungumzia mengi kuhusu maandalizi ya fainali za kombe la dunia na pia maisha ya nchini humo kwa ujumla.
KARIBU UUNGANE NASI
Kwa maoni ama ushauri tuandikie kupitia kwanzaproduction at gmail.com

LT. COL. MSTAAFU MAURICE NOEL SINGANO AZIKWA MKOANI TANGA

0
0
 Marehemu Lt. Col. Mstaafu Maurice Noel Singano enzi ya uhai wake.
 Jeneza lenye mwili wa Marehemu, likiwa lemebebwa na askari wa JWTZ Kikosi cha 37, likiwasili katika makaburi ya Bombo mjini Tanga kwaajili ya mazishi.

 Shughuli za mazishi zikiendelea.
 Shughuli za uwekaji wa mashada ya maua zikiendelea. 
 Askari wa JWTZ  37KJ wakifanya mazishi ya kijeshi, ikiwa ni pamoja na kupiga risasi kadhaa hewani.




 Mwili wa Marehemu Luteni Kanali mstaafu, Maurice Noel Singano ukiwasili nyumbani kwa mtoto wake Mikocheni B jijini Dar es Salaam Alhamisi Juni 05.2014, kabla ya kusafirishwa kwenda mkoani Tanga kwa mazishi yaliyofanyika Ijumaa Juni 06.2014. Marehemu Mzee Singano alifariki Mei 31, mwaka huu huko katika Hospitali ya Appolo Chennai nchini India alikuwa akipatiwa matibabu baada ya kupata mshtuko.

  Waziri Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim akiwa na wafiwa alipokwenda kuhani msiba Mikocheni B jijini Dar.

 Waziri Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu wakati wa kuuaga Mikocheni B jijini Dar.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. John Haule akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu wakati wa kuuaga Mikocheni B jijini Dar.

 Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha siasa cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu wakati wa kuuaga Mikocheni B jijini Dar.

 ) Dada za Marehemu wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu wakati wa kuuaga Mikocheni B jijini Dar.

 Jeneza lenye mwili wa marehemu likiingizwa katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Martha lililopo Mikocheni B jijini Dar, kwaajili ya misa kabla ya kuanza safari ya kuelekea Tanga kwa mazishi.
 Maafisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kikosi cha 37 Tanga, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu wakati wa kuuaga nyumbani marehemu katika eneo la Sahare mkoani Tanga.

 Mjane wa Marehemu, Bi. Maria Singano akilia kwa uchungu wakati akiuaga mwili wa mpendwa  mume wake, nyumbani kwao katika eneo la Sahare mkoani Tanga.
 Mtoto wa Marehemu, ambaye ni Mkuu wa Mahusiano wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, Bi. Beatrice Singano akilia kwa uchungu wakati akiuaga mwili wa mpendwa baba yake, nyumbani kwao katika eneo la Sahare mkoani Tanga. 
 Jeneza lenye mwili wa Marehemu, likiwa lemebebwa na askari wa JWTZ Kikosi cha 37, likitolewa nyumbani katika eneo la Sahare mkoani Tanga kwaajili ya kwenda kanisani na baadaye mazishi katika makaburi ya Bombo mkoani humo. Aliyeshika Msalana ni mototo wa Marehemu, Bw. Billy. 
 Jeneza lenye mwili wa Marehemu, likiwa lemebebwa na askari wa JWTZ Kikosi cha 37, likiwasili katika Kanisa Katoliki la Mt. Mathias mjini Tanga kwaajili ya misa kabla ya mazishi.

 Padri wa Kanisa Katoliki la Mt. Mathias mjini Tanga akifanya sala kwa marehemu.

 Wombolezaji kanisani



CFAO YAANZISHA HUDUMA MPYA KWA WAMILIKI WA MALORI YA MERCEDES BENZ NCHINI

0
0
DSC_0426
Msimamizi wa ufundi wa Magari aina ya Mercedes Benz kutoka kampuni ya CFAO Motors Bw. Winner Mushi (wa tatu kushoto) akionyesha matumizi ya kifaa maalum cha ukaguzi wa Malori ya Mercedes Benz (Star Diagnosis Machine) kwa baadhi ya mafundi na wasimamizi wa ufundi wa magari ya kampuni ya Bakhresa Group.

Bakhresa Group ni mmoja wapo wa wateja wa CFAO Motors ambao wanamiliki malori ya Mercedes Benz. Bw. Heico Herzog Mtaalamu wa ufundi (Flying Doctor) kutoka Mercedes Benz Ujerumani,(wa tatu kulia) akisimamia shughuli hiyo iliyoendeshwa na Bw. Mushi.

Wengine ni Key Account Manager wa Mercedes Benz, Bw. George Washington (kulia), Meneja wa Usafirishaji kutoka kampuni ya Bakhresa Group, Bw. Abdallah Seif (kushoto), Jarangi Nyabagara ambaye ni fundi wa Mercedes Benz (wa pili kushoto), na aliyechuchumaa ni Mohammed Shariff Meneja wa Karakana ya Bakhresa Group.

Na Mwandishi Wetu,
KAMPUNI ya CFAO Motor Tanzania hivi karibuni imezindua huduma mpya ya “Service Camp” ambapo chini ya huduma hii wa wamiliki wa malori yanayotengenezwa na Mercedez Benz watapata huduma ya ukaguzi bure na mafunzo kwa madereva wao.

Akizungumza na mwandishi wetu, jijini Dar es Salaam Key Account Manager wa Mercedez Benz, Bw George Washington amesema kwamba wameamua kuanzisha huduma hiyo ili kuweza kuwahudumia wamilimi wa magari hayo kwa karibu zaidi.“Mpango huu utapeleka huduma karibu na wateja na kwa kuwa hapo mwanzo wamiliki wa malori walikuwa hawapati huduma za matengenezo vizuri barani Afrika,” amesema.

Amesema kuwa kuna upungufu katika kuwahudumia wamiliki wa malori ya Mercedez Benz Afrika na hivyo wameona ni busara kuja na ‘Service Camp’ ili kuwapeleka wateja huduma za matengenezo na mafunzo kwa madereva wao huko walipo. Aliongeza kwamba huduma hiyo ya ‘Service Camp’ itakuwa ikitolewa kwa njia mbili tofauti ambazo ni kwenda kwa mteja na kukagua malori bila gharama yoyote.Amesema kwamba vile vile chini ya huduma hiyo watakuwa wakitoa mafunzo kwa madereva wa malori ili waweze kujajua vizuri magari hayo pindi wanapopata tatizo la kiufundi.
DSC_0448
Bw.Washighton aliongeza kwamba vile vile watakuwa wanawafundisha madereva jinsi vipuri vya Mercedez Benz vinavyopaswa kuwa ili kuweza kutambua vipuri bandia kwenye soko la nchini au karakana mbalimbali. “Tunawaonesha vipuri halisi na vipuri bandia kwa sababu kuna madhara katika kutumia vipuri bandia ambapo madhara yanaweza yasionekane katika muda wa siku chache bali huonekana baada ya muda mrefu,”

“Ukianza kuangalia gharama ya kutengeneza gari baada ya madhara kutokea unakuta gharama yake ni kubwa kuliko ambapo ungetumia vipuri halisi,” alieleza Bw Washington.

Alisisitiza kwamba kwamba hatua ya pili ni kuweka kambi barabarani ambapo malori mengi ya Mercedes Benz yanapita, hivyo kila ambaye anamiliki lori aina ya Mercedes Benz na anataka kufanyiwa ukaguzi, hupata huduma hiyo bila gharama, na hatimaye taarifa kamili zake za ukaguzi kurudishwa kwa mmiliki wake.

Washington amesema kwamba kampuni ya CFAO inataka kuwa karibu zaidi na wateja wake, kwani inataka wateja waone kwamba kuna watu wanaowajali ili kudumisha na kuimarisha uhusiano kati yao na wateja wao.


DSC_0392
Muuzaji wa vipuli vya magari ya Mercedes Benz nchini kutoka kampuni ya CFAO Motors, Emmanuel Sembua akimfafanulia jambo Meneja wa Usafirishaji kutoka kampuni ya Bakhresa Group, Bw. Abdallah Seif jinsi ya kutambua vifaa feki vya magari vya Mercedes Benz ili kujieupusha na matapeli ya vifaa hivyo.
“Tunataka wateja wetu waone kwamba iwapo magari yao yanapata matatizo, kuna watu ambao watawafuata na kuwahudumia kwa wakati unaofaa. Kama unavyojua haya ni malori kwa ajili ya transport business, hivyo hayapaswi kuwa mabovu kwa wakati mrefu kwa kuwa hiyo itawasababishia hasara wateja wetu. Wameyanunua ili wayatumie kwenye biashara na kazi zao, sasa, yakiwa out of service, hiyo ni hasara, na sisi hatutaki wateja wetu wapate hasara,” aliongeza Washington.
Alipoulizwa kuhusu upatikanaji wa huduma hiyo ya “Service Camp”, Washington amesema kwamba hii ni mara ya kwanza huduma hiyo kupatikana hapa nchini, ila kwa nchi jirani ya Kenya, huduma hiyo imeshapatikana mara tatu. Aliongeza kwamba huduma ya “Service Camp” itapatikana tena mwezi Novemba mwaka huu.
“Tutaitoa huduma hii kwa muda mfupi hapa Dar es Salaam kisha tutahamia mikoani na huu ni mpango endelevu, sio kitu cha mara moja,” alisisitiza.
Akizungumzia kuhusu huduma iliyotolewa kabla ya kuanzishwa kwa “Service Camp”, Washington amesema kwamba awali walikuwa na huduma inayoitwa “Technical Exchange”, ambayo ilikuwa na lengo ya kubadilishana uzoefu wa kiufundi kati ya wasimamizi wa karakana za wamiliki wa magari hayo na mafundi wa CFAO.
DSC_0403
Meneja wa Usafirishaji kutoka kampuni ya Bakhresa Group, Bw. Abdallah Seif na Meneja wa Karakana ya Bakhresa Group, Mohammed Shariff wakipewa maelezo na Muuzaji wa vipuli vya magari ya Mercedes Benz nchini kutoka kampuni ya CFAO Motors, Emmanuel Sembua (kulia) ya Battery zinazouzwa na kampuni ya CFAO Motors yenye garantii na uwezo mkubwa kwa malori.
“Tumegundua kwamba baada ya kuifanya hii technical exchange kumekuwa na mafanikio makubwa sana na tumeenda mbele na kuiboresha zaidi na tutafika wakati ambapo kutakuwa na washindi, kwani tumeona tuwashindanishe hawa mafundi wakuu kwa nia ya kuongeza ufanisi wao ili waweze kuyasimamia magari ya waajiri wao vizuri zaidi.
“Kutakuwa na washindi ambao tutawapeleka Ujerumani, kule kwenye kiwanda, ili waweze kuona jinsi ambavyo magari yanaundwa na kusimamiwa,
“kuanzia ubunifu hadi majaribio na mwisho kwenda kiwandani kwa ajili ya uundwaji. Huu ndio mpango ambao tunao hivi sasa na mpaka mwaka kesho tutakuwa tumempata mshindi ambaye tutampeleka Ujerumani ili atuwakilishe kule na kuona jinsi mambo yanavyoendesha. Kwa mantiki hii mpango huu nao pia ni mpango endelevu,” amesema Washington.
Washington alihitimisha na kusema kwamba mpango huu wa “Service Camp” unahusu magari ambayo ni malori pekee yaani Atos, Actros na Atego, na kwamba magari madogo hayatahusishwa na mpango huu.
DSC_0442
Picha ya pamoja baada ya zoezi hilo.
Amesema kwamba kwa sasa huduma hii inapatikana kwenye karakana zilizopo kwenye ofisi za CFAO zilizopo Barabara ya Nyerere na kwa upande wa Road Inspection, wamiliki wa malori ya Mercedes Benz watajulishwa mapema.
Aliongeza kwamba kuhusu mwezi Novemba, kituo kikuu cha kwanza nje ya Dar es Salaam kitakuwa Kibaha kwa kuwa barabara hiyo inatumiwa na magari mengi yanayokwenda mikoani.
Hatimaye, vituo vingine ambavyo vimepangwa vitatangazwa mapema iwezekanavyo ili wateja wa CFAO wapate muda wa kutosha kujiandaa.

HARAMBEE YA KUMCHANGIA NDUGU ERICK BAHUNDE YAFANA DMV

0
0
Bwna Erick Elisha Bahunde picha akiwa hospitali wakati alipopatwa na ajaliPhoto Via Vijimambo
Na Abou Sharty Washington DC
Jumuiya ya waTanzani waishio DMV imeweza kushirikiana katika harambe ya kumchangia ndugu yetu, Erick Elisha Bahunde ambaye alipatwa na ajali mbaya wakati alipokuwa akiwajibika kazini na kukatika miguu yake yote miwili pamoja na mkono wa kushoto, mnamo February 2014. katika  Jimbo la Indiana nchini Marekani.

Harambe hiyo ulioyongozwa na wana jumuiya wa hapa DMV akiwemu MC Saidi Mwamende, Katibu wa Jumuiya ya waTanzania , Amos Cherehani, Mchungaji Malekela Ndugu Faraja Isingo, Mashaka Bilali pamoja na Rais wa Jumuiya ya waTanzania DMV Bwna Iddi Sandaly.
Watanzania mbali mbali walihudhuria katika harambe hiyo iliofunguliwa rasmi kwa dua iliyoombwa na Mchungaji Malekela, na pia kuwaasa watanzania kushirikiana kwa hali na mali pale mtu yoyote atakaefikwa na  misukosuko yoyote ile ambayo anastahili kusaidiwa asaidiwe. 

Mchungaji Malekela aliendelea kwa kusema kuwa ''Mungu amesema kwamba kama mwanaadamu anatafuta kuwa na dini safi basi dini safi ndio hii'' kwa kuweza kujitolea kuwahudumia Wajane, Masikini, Mayatima na wahitaji wasiyojiweza kama wagonjwa n.k, huku akikumbusha kwamba ''Mungu ataendelea kugusa watu'' na pia kuwataka waliohudhuria katika ukumbu huo  kuchochea gharama dhidi ya kumchangia mtarajiwa anaestahiki kuchangiwa.

Baada ya ufunguzi kwa maneno ya Mungu, waTanzani waliohudhuria katika harambee hiyo walianza kuchangia michango mbalimbali zikiwemo pesa taslim, cheki pamoja na vitu ama bidha mbalimbali vilizofikishwa ndani ya ukumbi huo, pia wale walioahidi kutoa michango na kuandika idadi ya kiwango cha pesa watakazozitoa walijumuika pamoja na kuaza kutoa michango hiyo, huku katibu wa jumuiya ya waTanzania DMV  Bwna Amos Cherehani  pamoja na Mashaka Bilal wakisherehesha shuhuli hiyo kwa  uuzaji wa kunadi bidhaa hizo zilizofikishwa katika harambee hiyo.

Kulikuwa na uzwaji wa bidhaa tofauti zilizoletwa na wana waTanzania waishio hapa DMV zikiwemo vitenge, kanga, gauni, saa za ukutani kopo za kahawa ya kinyumbani, vitu vyote hivyo viliuzwa na hakuna hata kimoja kilichobakia katika harambe hiyo na kutimiza kiwango cha $ 4.800 dhidi ya watu wachache waliohudhuria katika Harambee hiyo ilioandalidwa na Familia ya Erick Elisha pamoja na Jumuiya ya waTanzania DMV, Siku ya Jumapili June 8, ndani ya ukumbi wa Sligo Creek uliopo Silver Spring Maryland Nchini Marekani.

Aidhi Bwna Erick Elisha Bahunde  aliwashukuru wale wote waliotoa michango yao kwa hali na mali kwa kuweza kukamilisha harambee hiyo kwa upendo wao mkubwa na kujisikia furaha kwa michango hiyo aliyoipa kwa watanzania wenzake wanaoishi hapa Washington DC.

Msaada wa Matibabu kwa Mtoto Maimuna Yahaya (11)

0
0
 
 Pichani ni Mtoto Maimuna Yahaya
 Mtoto Maimuna Yahaya akiwa na Mama yake Mzazi  Tunu Juma
 **********************

Msaada wa Matibabu kwa mtoto Maimuna Yahaya Mtoto Maimuna Yahaya (11) anayesoma shule ya Msingi ya watoto wenye mahitaji maalum (wenye ulemavu) ya Irente Rainbow (Lushoto- Tanga) Darasa la pili, anasumbuliwa na tatizo la mifupa na ukubwa wa kichwa tangu kuzaliwa kwake, tatizo lililompelekea kuwa na ulemavu wa viungo na mtindio wa Ubongo.


Mama wa mtoto huyo, Bi. Tunu Juma Maziku amesema amekuwa akimpeleka mwanae huyo Maimuna katika hospitali ya KCMC kwa muda wa miaka 11. Hali ya mtoto inaendelea kuimarika, anaweza kukaa na anaweza kuongea.

Bi. Tunu amekuwa akimpeleka mwanae huyu shule na kumsubiri hadi wamalizapo masomo ya siku na kumrejesha nyumbani kwa muda wa miaka miwili. Bi. Tunu Juma Maziku  anasema kwa sasa hali yake ya kiuchumi si nzuri, anashindwa kumpeleka mwanae kuhudhuria matibabu KCMC, hivyo anaomba msaada wa kifedha kwa wasamalia wema ili mtoto wake aendelee na matibabu.   Mahali wanapopatikana: Lushoto Mabwawani 

Mawasiliano: Namba ya simu ya mama mzazi: +255712504768 Namba ya Tigo Pesa mesajiliwa kwa Jina la Maimuna Yahaya +255655779345 na Namba ya Airtel Money ni 0787204160 imesajiliwa kwa jina la Tunu Juma.
 

Article 10

0
0

ZAIDI YA WANANCHI 50 WAHANGA WA MAFURIKO WAPATIWA MSAADA WA CHAKULA KIJIJI CHA THEMI YA SIMBA ARUSHA

0
0
Mzee wa kanisa la Waadventista wasabato  mtaa wa kijenge   Agrey Tumaini akigawa mahindi kwa wananchi wa kitongoji cha kitongoji  cha Nyamagana  kilichopo katika kijiji cha Themi ya simba wilayani Arumeru MKoani Arusha (picha na woinde shizza,Arusha
=========  ======  ======
Na Woinde shizza,Arusha

Zaidi ya wananchi  50  wa kitongoji  cha Nyamagana  kilichopo katika kijiji cha Themi ya simba wilayani Arumeru MKoani Arusha ambao waliathiriwa na mafuriko yaliotokea mwisho mwa mwezi wa nne mwaka huu wamepatiwa msaada wa chakula na nguo kijijini hapa.

 Akikabidhi chakula hicho mzee wa kanisa la Waadventista wasabato  mtaa wa kijenge   Agrey Tumaini alisema kuwa wameamua kuwasaidia wananchi hawa kutokana na janga ambalo liliwakuta la kuingiliwa na mafuriko ya maji  ambapo yaliwasababishia nyumba pamoja na mazao yao kuezuliwa na maji hayo

Alisema kuwa wao kama kikundi cha WAMO  kutoka katika kanisa hilo waliguswa sana na tatizo hili ambalo liliwatokea hivyo wakaamua kujichanga na kununua vyakula ivyo na nguo kwa ajili ya wahanga hao wa mafuriko.

Alisema kuwa wameweza kutoa gunia kumi za mahindi ,maharage kunia tatu,unga wa ugali pamoja na nguo kwa ajili ya watoto  wa wananchi ambao walikubwa na janga hilila mafuriko.

“sisi tumeguswa sana na tukio hili wenzetu kukubwa na  mafuriko kwa kweli wameadhirika vikubwa kwani wengine awana sehemu zakukaa wengine walikuwa wamelima mazao yao kama mahindi yaliezuliwa na mafuriko hayo yaani kiukweli hadi sasa kuna watu awajui wataishije kwa mwaka huu lakini tumeona sio vibaya iwapo tukiwasaidia ichi kidogo  tulichonacho maana ata neno la mungu linasema  katika mathayo uwa mlikuja na njaa nikawapa chakula,mlikuja uchi nikawavisha sasa na sisi tumeamua kuwapa ichi kidogona tunawaomba watu wengine waendelee kujitokeza kwa wingi kuwasaidia wananchi hawa kwani wapo katika mazingira magumu sana”alisema Tumaini.

Akipokwa msaada huo mmoja wa wananchi hao alietambulika kwa jina la  Gidion Maganga alisema kuwa anashukuru sana kanisa hili la wa sabato kwa kuja kuwasaidia kwani kuna baadhi yao walikuwa hawajui hatima ya maisha yao kwani ata chakula kwao kupata ni tabu .

Alisema kuwa pamoja kuwa kuna baadhi yaviongozi na taasisi ambazo zimewapelekea chakula kama maindi ,magodoro  pamoja na nguo lakini bado wanaitaji maada kwani mvua zile ziliwachukulia vitu vyao vingi ikiwemo mazao maindi waliokuwa wameyaifadhi ndani vyombo ,magodoro na sio ivyo tu lakini pia zileweza kumuua mwananchi mmoja.

Akizungumzia tukio hilo mwananchi mungine ambaye aliyejitaja kwa jina la Zainabu Minja alisema kuwa siku hiyo ya tukio lilitokea majira ya saa saba usiku wakati wamelala  huku mvua ikinyesha ndipo gafla waliona maji mengi yamekuja na kujaa ndani  ya nyumba  kitu ambacho kiliwaogopesha zaidi ni pa le maji yale yalivyoanza kusomba vitu.

“yaani ndugu muandishi usione apa yaani maji yalikuja na kasi unaona hii chuma ina uzitowa kilomia ndio niliichukuwa nikaishika na uyu ni mama yangu na unamuona alivyo mzee nilimwambia ashikilie iyo chuma akashika mwishowe mikono ikafa ganzi ndipo nikachukua kanga na kumfunga kiunoni nikaunganisha na chuma ili asipelekwe na maji ila nashukuru mungu alituona pamoja vitu vilizolewa lakini sisi ni wazima kwakweli”alisema bi Zainabu

Alitoa wito kwa wananchi serekali pamoja na taasisi mbalimbali kujitokeza kwa wingi kuwasiaidia kwani wapo katika halingumu sana  katika kipindi hichi.
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images