Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 293 | 294 | (Page 295) | 296 | 297 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Baadhi ya Warembo wanaowania taji ya Ulimbwende la Jiji la Arusha,wakimsikiliza kwa makini Dr,Sober Mzighani wa Hospitali ya Maria Stopes ya jijini humo wakati wakipatia mafunzo mbali mbali yahusuyo maswala ya afya ya Binadamu.Hii ni sehemu ya maandalizi ya Onyesho hilo la Urembo ambalo linataraji kufanyika hivi karibuni.
  Warembo wanaowania taji ya Ulimbwende la Jiji la Arusha wakiwa katika picha ya pamoja.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Mwanza na wa Kiwada cha Cocacola, wakati alipowasili kwenye Kiwanda hicho kwa ajili ya kutembelea na kujionea mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika Kitaifa Mkoani Mwanza katika Viwanja vya Furahisha, jana Juni 5, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Msimamizi Mkuu wa ubora wa Mazingira na Usalama Kazini, Peter Simon, kuhusu jinsi wanavyo tunza mazingira kwa kutotupa maji machafu ambayo hutengenezwa na kuwa masafi na kutumika upya kwa baadhi ya shughuli za kiwandani hapo kama kumwagia bustani, kuoshea magari na n.k, wakati alipowasili kwenye Kiwanda hicho kwa ajili ya kutembelea na kujionea mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika Kitaifa Mkoani Mwanza katika Viwanja vya Furahisha, jana Juni 5, 2014.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Cocacola Mwanza, Christopher Gachuma, akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais Dkt. Bilal, kuzungumza na wafanyakazi wa kiwanda hicho, wakati alipowasili kwenye Kiwanda hicho kwa ajili ya kutembelea na kujionea mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika Kitaifa Mkoani Mwanza katika Viwanja vya Furahisha, jana Juni 5, 2014.
  Picha ya Pamoja na Wafanyakazi wa Kampuni hiyo.
  Makamu akiagana na wafanyakazi wa kiwanda hicho baada ya ziara yake.Picha na OMR.

  0 0

   Afisa mfuko wa pensheni wa pspf Hadji.H.Jamadary akizungumza namna yakuweza kufaidika na uchangiaji wa hiari katika mfuko wa pensheni wa PSS.
   Maofisa wa mfuko wa penshe wakitoa shukrani kwa wanachama walio weza kuhudhuria semina,kutoka kushoto ni Debora Danniel na kulia ni Hadji Jamadary.

  Picha ya pamoja baadhi ya wanahisa na maofisa wa mfuko wa pension PSPF

   Leo katika kuendelea kuchimba kwa mizizi kwa  kuwapa elimu wananchi mbalimbali mfuko wa pensheni wa Pspf katika mpango wa kuchangia kwa hiari Pss umeweza kuwafikia wananchi wa Tandika na mashirika mbalimbali wameweza kuhudhuria katika semina hiyo iliyo andaliwa na mfuko huo 

  semina hiyo ililenga katika wafanya biashari wa aina mbalimbali ambao hujulikana kama wajasiliamali ambapo kufuatiwa kwa wafanyabiashara hao kufika na kuweza kupata elimu nayo kampuni ya Tandika Grain Agents Plcambayo inajishughulika na uuzaji wa nafaka mbalimbali iliweza kufika na wanachama wake ili kupta elimu itakayo wasaidia katika kuendeleza biashara yao na maendeleo ya familia zao

  Akizungumza na wanachama walio hudhuria semina hiyo Afisa mufuko wa Pensheni wa PSPF Bw.Hadji Jamadary mbaye ndiye aliye kuwa akitoa maelezo katika semina hiyo alianza kwa kuwafahamisha mfuko wa pensheni wa PSPF ni nini na kuweza kuwapa utangulizi wa wa semin hiyo ambayo ilikuwa ikilenga uchangiaji wa hiari (PSS).

  Vilevile aliweza kutoa ufafanuzi wa namna ya kujiunga ,manufaa utakayo yapata endapo utajiunga na mfuko huu wa PSPF kwa mpango wa hiari PSS ambapo aliwaeleza kuna namna ya mafao ambayo unaweza ukachagua ili kuweza kuendelea kuchangia ambapo aliyataja mafao  hayo ambayo ni Fao la elimu, fao la ujasiriamali,fao la uzeeni,fao la kifo,fao la ugonjwa na fao la kujitoa aliweza kutoa ufafanuzi katika kila fao ambapo kwakuwa semina ilikuwa na wafanyabiashara aliweza kuwa fundisha kuhusu fao la ujasiliamali na faida zake .

  Baada ya kutoa maelekezo hayo wafayabiashara waliruhusiwa kuuliza maswali na kuweza kuchagua na kujiunga na mpango huo wa hiari .

  Nao wafanya biashara hususani katika kampuni ya Tandika Grain Agents Plc Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Bw.Hassani Matibula aliweza kuwashukuru waelimishaji na waandaaji wa semina hiyo hususani  mfuko wa PSPF kuweza kuwafikia sehemu waliko na kuwafungu kwakuwa hawakuweza kupata watu watakao kuja na kuwapa elimu ya kuwajenga katika biashara zao alitoa wito kwa wafanya biashara wenzake waweze kujiunga ili waweze kupata manufaa na kuhifadhi sehemu salama kw fedha zao.

  Mpango huu umeanzishwa na PSPF kwaajiri ya kupanua wigo wa uanachama kwa kuandikasha wananchi waliojiajiri au kuajiriwa katika sekta rasimi na zisizo rasmi.


   Debora Danniel afisa masoko PSPF ambaye alikuwa akifanya zoezi la kusajiri wanahisa wa kikundi cha Tandika Grain Agents Company PLC baada ya semina
   Mmoja wa wanachama akifuatilia kwa makini maelezo ya majibu baada ya kuuliza swali ambalo lilijibiwa na maofisa wa mfuko wa pensheni kuhusu uchangiaji wa hiari Bw.Rashidi Iloko
   Bw.Hemed Abdullah akiwa makini kufuatilia
   Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Tandika Grain Agents plc Bw.Hassani Abdallah Matimbula
   Afisa masoko PSPF Debora Danniel akiwagawia vipeperushi vikiwa vina elezea PSS mfuko wa hiari
   Afisa masoko Akiwa katika usajiri wa wanachama walio weza kujiunga na mfuko wa hiari
  Zoezi la upigaji picha likiwa linaendelea kwa walio jaza fomu za kujiunga na mfuko wa huari PSS
   baadhi  ya wanahisa wa chama cha Tandika Grain agents comany plc

  0 0

  Hatimaye Video ya Haina Noma Ya - Julio Batalia ambaye alikuwa mshiriki wa shindano la BIGBROTHER AFRICA SEASON 7 (StarGame) mwaka 2012 imeshakwisha na video hiyo imekabidhiwa rasmi na director mkubwa wa kampuni ya NEXTLEVEL -Adam Juma (AJ) Akiwa na camera yenye vigezo vikubwa duniani REDCAMERA. 

   Video hii ambayo wameshirikishwa wasanii wakubwa wawili CHEGE CHIGUNDA kutoka TMK wanaume family na Madee ali Raisi wa Manzese kutoka TIPTOP Connection imeandaliwa katika location ya CLUB 601, Uzinduzi rasmi unafanyika leo tarehe 06/06/2014 - FNL East africa TV,nakuonyeshwa kwenye vituo mbali mbali kama Star tv,TBC,Clouds TV.. NK...

  0 0

   Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akiongea na Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali wakati wa Semina ya Mafunzo iliyoandaliwa na Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel na Kulia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Innocent Mungy
   Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel wakati wa Semina ya Mafunzo iliyoandaliwa na Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Leo Jijini Dar es Salaam.

   Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Sylvia Lupembe akitoa neno la shukrani kwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga, wakati wa Semina ya Mafunzo iliyoandaliwa na Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Leo Jijini Dar es Salaam.

   -Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel  akiwasilisha mada kuhusu huduma kwa mteja kwa Maafisa Habari na Mawasiliano wakati wa Semina ya Mafunzo iliyoandaliwa na Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Leo Jijini Dar es Salaam.

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel  akifurahia jambo na Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Innocent Mungy, Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Sylvia Lupembe na Katibu Mwenezi wa Chama hicho Bw. Abel Ngapemba.


  0 0

   Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Stephen Masele (aliyekaa ktikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa yote ya Tanzania Bara, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wenyeviti wa Halmashauri, Viongozi wa Dini na baadhi ya Watendaji wa Wizara, mara baada ya kufungua mkutano  uliojadili utekelezaji wa Sheria ya Madini uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. 

  Kutoka kushoto (waliokaa) ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Said Meck Sadik, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mwantumu Mahiza, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Abbas Kandoro ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa, Katibu Mkuu   Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, Deodatus Mtesiwa.

     Baadhi ya Wakuu wa Mikoa wakifuatilia kwa ukaribu mkutano uliokuwa ukiendelea ambapo wamepata nafasi ya kujadili namna bora ya kutekeleza sheria ya madini, changamoto na ushauri mbalimbali umetolewa ili kuwezesha sekta hiyo kuendelea  kuchangia kwa kiasi kikubwa zaidi  katika uchumi wan chi.

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Stephen Masele (katikati) akiwasili katika ukumbi wa mikutano Kilimanjaro Hotel (Hyatt) , kwa ajili ya kufungua rasmi mkutano huo. Wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava, Wa kwanza kulia ni Kamishna wa Madini Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Paul Masanja, wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruruma Mhe. Said Mwambungu.

  Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi (katikati) akiongea jambo na baadhi ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo.


  0 0

  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (kulia), Afisa Mtendaji Mkuu Zantel Bw. Pratap Ghose (kushoto) pamoja na viongozi kutoka Chama cha Ngumi Tanzania (BFT) wakiunganisha mikono kwa pamoja kuonyesha ushirikiano wakati wa makabidhiano ya hundi ya shilingi Milioni kumi kama msaada kutoka Zantel kwa Chama cha Ngumi Tanzania (BFT).
  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kupokea msaada wa hundi ya milioni kumi kutoka Zantel kwa ajili ya Chama cha Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) leo jijini Dar es Salaaam, kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu Zantel Bw. Pratap Ghose.
  Rais wa Chama cha Ngumi Tanzania Bw. Mutta Rwakatare akitoa shukrani kwa Zantel baada ya kukabidhiwa hundi ya shilingi milioni kumi kuinua mchezo wa ngumi, kushoto ni Katibu Chama cha Ngumi Tanzania Bw. Makole Mashaga na kulia ni Mjumbe wa Maendeleo ya Wanawake Bi. Aisha George Voniatis. Picha na Genofeva Matemu. 

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro akitoa hotuba yake wakati akifunga mafunzo kwa madereva bodaboda wilayani Makete. Mafunzo hayo yametolewa na shirika la APEC
   Madereva bodaboda wakifurahia kupatiwa vyeti vya mafunzo hayo.
   Bi Rehebian Mahenge ambaye alikuwa katibu katika mafunzo hayo akisoma risala mbele ya mgeni rasmi
   Bi Mahenge akimkabidhi risala mkuu wa wilaya ya Makete Mh Josephine Matiro ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika mafunzo hayo
  Mkuu wa polisi wilaya ya Makete Alfred Kasonde akitoa nasaha kwa wahitimu wa mafunzo hayo
   Mkuu wa wilaya akitoa hotuba yake
   Mkurugenzi wa APEC Bw. RespiciusTimanywa akitoa maelezo ya awali jinsi walivyoendesha mafunzo hayo na matarajio wanayoyategemea kutoka kwa wahitimu hao

   Miongoni mwa wahitimu wa mafunzo hayo ambaye pia ni askari polisi wilayaani Makete Afande Moses akipokea cheti chake
   Picha ya pamoja na mgeni rasmi
   Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Josephine Matiro akiteta jambo na Mkurugenzi wa APEC Bw. Respicius Timanywa mara baada ya kumaliza kufunga rasmi mafunzo hayo
   Baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Makete wakiwa kwenye picha ya pamoja
   wawezeshaji wa mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalam wilaya ya Makete

  0 0

   Kocha wa Tim ya Zanzibar Petroleum LTD Ali Hakiba Hassan alieshika kombe na kikosi kamili cha Zanzibar Petroleum kilicho twaa ubingwa wa Kombe la Mazingira kwaka 2014/2015.(Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar).
   Meneja wa Zanzibar Petroleum LTD Altaf Jiwan akionyesha furaha yake kwa kuletewa kombe (kulia) kocha wa tim hiyo Bwa. Ali Hakiba Hassan.
   Wachezaji wa Tim ya Zanzibar Petroleum LTD na wafanyakazi wa Kampuni hiyo katika picha ya pamoja.
  Meneja wa Zanzibar Petroleum LTD Altaf Jiwan akiwapongeza wachezaji wake kwa kuchukua ubingwa wa Kombe la Mazingira lililoandaliwa na Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar, kwa kuifunga tim ya Wizara ya Fedha kwa mikwaju ya penanti 4 kwa 3.Sherehe hizo ilifanyika Ofisini kwao Mtoni Zanzibar

  0 0

   Waziri wa Afya Zanzibar Juma Duni Haji akisoma Taarifa ya Uzinduzi wa Mpango mpya wa Ugawaji wa Vyandarua vyenye dawa ya Muda mrefu ikiwa ni mkakati wa kutokomeza Ugonjwa wa Maleria Zanzibar katika Ukumbi wa Kitengo cha kupambana na Maleria MwanaKwerekwe Zanzibar.
  Mfano wa Chandarua kinachotarajiwa kugawiwa Wananchi chenye dawa ya muda mrefu ili kujikinga na Ugonjwa wa Maleria. Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar.

  Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar      

  Wizara ya Afya Zanzibar imezindua Ugawaji wa Vyandarua Vyenye dawa ya muda mrefu ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha Ugonjwa wa Malaria unatokomezwa Zanzibar.

  Akizindua Mpango huo Waziri wa Wizara hiyo Juma Duni Haji amesema kukamilika kwa ugawaji wa vyandarua hivyo kunaweza kutokomeza moja kwa moja Ugonjwa wa Maleria ambao kwa sasa upo chini ya Asilimia moja.

  Amesema licha ya maambukizi kuwa chini ya Asilimia moja lakini Mikakati ya Wizara ni kuhakikisha ugonjwa huo unabaki historia katika Visiwa vya Zanzibar.
  “Kwa kweli hadi sasa maambukizi yapo Chini ya Asilimia 1 lakini mipango yetu ni kuhakikisha Maleria yanabaki kuwa historia Nchi hii ndio maana tunaandaa kila mkakati kufikia lengo hilo” Alisema Duni.

  Waziri Duni amefahamisha kuwa Jumla ya Vyandarua  315,465 vinatarajiwa kugawiwa kwa Wakazi wa Unguja na Pemba ambapo Unguja Watagawiwa Vyandarua 221,803 ambapo kwa Pemba watapata 78,637.

  Amewataja watakaonufaika na Vyandarua hivyo kuwa ni kinamama Wajawazito,Walemavu, Wajane na Waliofikwa na Majanga yanayopelekea kukosa Uwezo wa kununua Vyandarua.

  Kwa upande wake Msaidizi Meneja wa Kitengo cha kupambana na Malaria Zanzibar Mwinyi Mselem amesema pamoja na Kutoa Vyandarua hivyo Kitengo chake pia kinaendelea na Upigaji dawa kwa ajili ya kuulia mazalio ya Mmbu wa Maleria.

  Mkakati mwingine wanaoutumia kutokomeza Maleria ni kufuatilia hali ya Ugonjwa inavyoendelea ambapo amewaomba Wananchi kuchukua tahadhari ya kuweka Mazingira safi na kuripoti Vituo vya afya pindi wanapojiskia Vibaya.

  Kuhusu Ugawaji wa Vyandarua Mwinyi amesema Masheha wa Shehia ndio watakaohusika kutoa Kuponi kwa wale wanaostahiki kupewa Vyandarua ambapo amesisitiza kuwa Watajitahidi ili kila mwenye sifa za kupewa apate Vyandarua hivyo.

  “Ndugu waandishi tumewaelekeza vizuri Masheha wetu tunaamini watatenda haki lakini kama kuna Sheha ambaye ataenda kinyume na mkapata ushahidi basi musisite kumpripoti ila haki ipatikane kwa Walengwa” Alibainisha Mwinyi.

  Mradi huo Uliofadhiliwa na Mfuko wa Dunia(Global Fund),Mfuko wa Rais Bush wa kupambana na Maleria kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar utaanza siku ya Jumatatu ambapo Walengwa watapa Vyandarua hviyo Unguja na Pemba.
  IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR 

  0 0

  Moses Iriria, kutoka ANSAF (Mtafiti) akiwasilisha mada katika mjadala huo. Moses Iriria, kutoka ANSAF (Mtafiti) akiwasilisha mada katika mjadala huo.Mkurugenzi Mtendaji wa Sikika, Irenei Kiria akiwasilisha mada wa washiriki. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Sikika, Irenei Kiria akiwasilisha mada wa washirikiAliyekuwa Mkurugenzi wa TGNP Matandao, Bi. Usu Mallya akiendesha majadiliano kwa washiriki. 
  Aliyekuwa Mkurugenzi wa TGNP Matandao, Bi. Usu Mallya akiendesha majadiliano kwa washiriki.Ofisa Miradi wa TAWJA, Asha Komba ikiwasilisha mada yake katika mjadala wa wazi. 
  Ofisa Miradi wa TAWJA, Asha Komba ikiwasilisha mada yake katika mjadala wa waziBaadhi ya washiriki wa mjadala huo wa wazi. Baadhi ya washiriki wa mjadala huo wa wazi.Sehemu ya washiriki wa mjadala huo wa wazi. Sehemu ya washiriki wa mjadala huo wa waziPichani juu ni baadhi ya washiriki wa mjadala huo wakichangia mada anuai. Pichani juu ni baadhi ya washiriki wa mjadala huo wakichangia mada anuai.Pichani juu ni baadhi ya washiriki wa mjadala huo wakichangia mada anuai. 
  Pichani juu ni baadhi ya washiriki wa mjadala huo wakichangia mada anuai.Mwanaharakati Badi Darusi akiwasilisha mada yake.  
  Mwanaharakati Badi Darusi akiwasilisha mada yake. Baadhi ya washiriki wa mjadala huo wa wazi. Baadhi ya washiriki wa mjadala huo wa wazi.

   Na Mwandishi Wetu, Dar es SalaamMTANDAO wa Jinsia nchini (TGNP Mtandao) umefanya mjadala wa wazi ulioshirikisha taasisi mbalimbali zisizo za Serikali (NGO's) pamoja na wadau wa masuala ya kijinsia juu ya uboreshaji wa uwajibikaji kwa kuzingatia mgawanyo wa rasilimali kijinsia kwa huduma bora za kijamii nchini Tanzania.  

  Mjadala huo wa wazi uliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika Hotel ya Blue Pearl, pamoja na mambo mengine lengo kuu ilikuwa ni kuimarisha sauti ya pamoja kudai uwajibikaji kwa watunga sera kwa kuzingatia mgawanyo wa rasilimali kijinsia, kupiga vita rushwa na kuboresha utoaji huduma za kijamii. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya kumalizika kwa mjadala huo, Kaimu Meneja wa Habari na Mawasiliano wa TGNP Mtandao, Bi. Kenny Ngomuo alisema malengo mahususi ya mjadala ni pamoja na kukuza uelewa wa muktadha wa kimataifa, kitaifa na kijamii na athari zake kwa maisha ya wanawake walioko pembezoni.

   Alisema lengo lingine ni kwa washiriki kubadilishana uzoefu na mafanikio ya harakati mbalimbali kuhusu uchambuzi wa bajeti na ufuatiliaji wa utendaji katika ngazi za jamii hadi taifa na pia kuweka mikakati ya kuendeleza mapambano zidi ya rushwa, kukuza utawala bora ili kuboresha utoaji wa huduma kwa jamii. "...Malengo mengine mahususi kwa washiriki wa mjadala huu ilikuwa kuweka kumbukumbu za mafanikio yanayohusiana na mapambano dhidi ya rushwa ikiwa ni pamoja na kupigania bajeti ya kijinsia na ufuatiliaji. 

  Kuimarisha mitandao na ujenzi wa nguvu za pamoja juu ya masuala ya bajeti ya kijinsia, vita dhidi ya rushwa na huduma bora kwa jamii," alisema Bi. Ngomuo. Kabla ya kuanza kwa mjadala huo mada mbalimbali ziliwasilishwa kwa washiriki, ambazo ziligusa maeneo anuai ya huduma za kijamii, rushwa na changamoto nyingine zinazoikabili jamii kabla ya wajumbe kupata fursa ya kujadiliana kwa pamoja. Takribani washiriki 130 kutoka Dar es Salaam na mikoa ya jirani ikiwemo Morogoro na Pwani wameshiriki mjadala huo.


  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakijumuika na waombolezaji wengine katika Kanisa la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Ernesti B. Ngereza, aliyekuwa mfanyakazi wa Ikulu aliyefariki dunia Mei 5, 2014, kabla ya mwili huo kusafirishwa kwenda nyumbani kwa marehemu Lushoto, Mkoani Tanga Ijumaa Mei 6, 2014.
                Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima zao za mwisho katika Kanisa la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Ernesti B. Ngereza, aliyekuwa mfanyakazi  wa Ikulu aliyefariki dunia Mei 5, 2014, kabla ya mwili huo kusafirishwa kwenda nyumbani kwa marehemu Lushoto, Mkoani Tanga Ijumaa Mei 6, 2014.

  PICHA NA IKULU


  0 0

   Redd's Miss Tabata 2014, Ambasia Maliy akitabasamu baada ya kutangazwa  rasmi kuwa Mrembo wa Kitongoji cha Tabata.
  Redd's Miss Tabata 2014, Ambasia Maliy akipunga mkono kwa mashabiki wake muda mfupi baada ya kutawazwa rasmi kuwa Mrembo wa Kitongoji cha Tabata, Shindano hilo lilifanyika kwenye Ukumbi wa Da'west Park,Tabata jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia jumamosi.Wengine pichani ni Mshindi wa Pili wa shindano hilo,  Faudhia Feka (kulia) pamoja na Mshindi wa Tatu, Ramta Mkadara .
   
   Redd's Miss Tabata aliemaliza muda wake, Doris Molel (alieketi) akisuburi kutangazwa kwa mrithi wake.
   Warembo walioingia hatua ya tano bora katika Shindano la Redd's Miss Tabata 2013
   Kumi Bora.
   Warembo wakitoa burudani.


   Bendi ya Twanga Pepeta ikitoa burudani kwenye shindano la miss Tabata lililofanyika kwenye usiku wa kuamkia leo
   Mshereheshaji akizungumza jambo
   Warembo wakiwa wamevaa vazi la ufukweni
   Warembo wakitoa burudani
   Majaji wakifanalaizi mambo.
   Jaji wa Missi Tabata 2014, Le Mutuzi akiwataja warmbo kumi bora na pia aliwataja tano bora
   Washindi wa Miss Ukonga nao walikuja kuonesha ya kwao
   Maswali yakiulizwa kwa Warembo
   Burudani ikiendelea
   Wadau waliokuwa kwenye miss Tabata
   Wakuu wa Kamati ya Miss Tanzania wakifuatilia kwa makini shindano la Miss Tabata. Miss Talent 2014 alichukua Faudhia Feka
  Miss Discipline alichukua, Nuru Omary
     Redd's Miss Tabata aliemaliza muda wake, Doris Molel (alieketi) akisuburi kutangazwa kwa mrithi wake.
  Aliyekuwa Redd's Miss Tabata 2013, Doris Molel akimvisha Sasha mshindi wa Miss Tabata 2014, Ambasia Maliy.
   Aliyekuwa Redd's Miss Tabata 2013, Doris Molel akimvisha taji mshindi wa Miss Tabata 2014, Ambasia Maliy.
  Wadau waliofika kutizama Redd's Miss Tabata 2014

  PICHA NA PAMOJA BLOG 

  0 0

   Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo  na Waziri Mwandamizi anayeshughulikia Mambo ya Nje na Ndani wa Jamhuri ya Singapore, Mhe. Masagos Zulkifli, Ikulu jijini Dar es salaam Mei 6, 2014. Waziri huyo na ujumbe wake yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tano. 
   Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na  Waziri Mwandamizi anayeshughulikia Mambo ya Nje na Ndani wa Jamhuri ya Singapore, Mhe. Masagos Zulkifli, na ujumbe wake  Ikulu jijini Dar es salaam Mei 6, 2014. Waziri huyo  yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tano. Wa pili kutoka kulia mstari wa mbele ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha, na kushoto kwake ni Balozi wa Tanzania nchini India anayewakilisha pia nchini Singapore, Mhe. John Kijazi 
  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameongozana na Waziri Mwandamizi anayeshughulikia Mambo ya Nje na Ndani wa Jamhuri ya Singapore, Mhe. Masagos Zulkifli, Ikulu jijini Dar es salaam Mei 6, 2014. Waziri huyo na ujumbe wake yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tano.

  0 0

   Wafanyakazi wa Benki ya Exim ya Tanzania Tawi la Shinyanga wakisafisha eneo la Soko Kuu mkoani humo katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani ambayo uadhimishwa kila ifikapo tarehe 5 mwezi wa 6 kila mwaka.

    

  0 0


  Promosheni ya Kwea Pipa na televisheni ya Taifa ya TBC  kwa kushirikiana na kampuni ya Push Mobile Media Limited imezidi kupamba moto baada ya mshindi mmoja zaidi kupatikana.

  Deocary Mkenda ambaye ni mkazi wa Sinza ameungana na wenzake wawili ambao wamekwisha zawadiwa tiketi zao na sasa kampuni ya Push Mobile Media Limited inawatafutia pasipoti kwa ajili ya kusafri na kuona mechi ya Brazil na Cameroon Juni 23 mjini Rio de Janeiro.

  Mkenda (35) ambaye ni Mhasibu katika kampuni ya Ernst & Young ya jijini anaungana na Donald Milinde Shija (34) mkazi wa Mabibo jijini ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya Davis and Shirtliff na mshindi mwingine ni Shaban Athumani Saidi (22) mkazi wa Banana-Kitunda. 

  Meneja kampeni wa promosheni hiyo ya Semu Bandora alisema kuwa bado tiketi mbili kwa ajili ya mashabiki wa soka nchini ili kujishindia tiketi kwa ajili ya kuona kombe hilo.

  Bandora alisema kuwa droo nyingine itafanyika wiki ijayo na lengo ni kuona mashabiki wanapata fursa hiyo ya kuona mashindano hayo makubwa kabisa ya soka duniani.

  “Tunawaomba mashabiki wa soka kuendelea kushiriki katika promosheni hii ili kupata nafasi ya kuwaona mastaa wa dunia kama akina Benoit Assou-Ekotto, Alex Song na Samuel Eto’o na yule wa Brazil kama vile Neymar da Silva Santos Júnior, Thiago Silva, Dan Alves na wengine wengi,” alisema Bandora.

  Alisema kuwa mbali ya tiketi za kombe la dunia, pia kuna zawadi za ving’amuzi zaidi ya 250, televisheni za flat screen sita na fedha taslimu ambazo zote zimeandaliwa kwa ajili ya kuwazawadia mashabiki wa soka.

  0 0

  Sehemu ya wachezaji mpira wa sasa na wazamani wakiwa wamesimama pembeni ya Jeneza lenye Mwili wa aliyekuwa Mchezaji wa Timu ya Simba miaka ya nyuma,Marehemu Gebbo Peter aliefariki jana kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.hapa wakiwa nyumbani kwake Vingunguti tayari kwa safari ya kwenda kwenye maziko yake Kigurunyembe mkoani Morogoro (Picha na Evance Ng'ingo)

  Wadau mbali mbali wa soka wakiwemo viongozi wa soka wakipita kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Marehemu Gebbo Peter,Nyumbani kwake Vingunguti,jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza safari ya kuelekea Kigurunyembe mkoani Morogoro kwa mazishi.
  Ibada ikifanyika.
  Mbunge wa Jimbo la Ilala,Mh. Mussa Azzan Zungu akitoa heshima za Mwisho.

  Mwili ukiwasili nyumbani.

  0 0

  WAZIRI MKUU ACHARUKA, AKATAA KUKAGUA JENGO LA ZAHANATI
  *Ni baada ya wataalam kukiuka maagizo yake aliyotoa Machi mwaka huu


  ILE HALI ya kufanya kazi kwa mazoea (business as usual)  iliyojengeka kwa baadhi ya watendaji wa Serikali leo imewatokea puani watendaji wa Manispaa ya Dodoma wakati Waziri Mkuu alipoamua kufanya ziara kukagua miradi ya maendeleo.

  Akiwa katika eneo la kwanza ambalo alipangiwa kukagua ujenzi wa kituo cha afya cha Mkonze leo asubuhi (Jumamosi, Juni 7, 2014) Waziri Mkuu alipokea taarifa ya ujenzi wa kituo na kubaini kuwa hawajafanya chochote ili kutekeleza maagizo yake aliyoyatoa Machi 22, 2014.

  Katika taarifa yake, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Mhandisi Lusako Kilembe alimweleza Waziri Mkuu kwamba walifanya tathmini ya ujenzi wa kituo hicho na kubaini kuwa zinahitajika sh. Milioni 24.15 na kwamba maombi ya matumizi hayo yamepangwa kujadiliwa kwenye kikao cha kamati ya fedha na uongozi kitakachofanyika Juni 10, mwaka huu.

  Akiwa katika maadhimisho ya kilele cha wiki ya maji ambayo Kitaifa yalifanyika mkoani Dodoma, Waziri Mkuu alizindua mradi wa maji jirani na kituo cha afya cha Mkonze na kubaini kuwa kuna hitilafu za ujenzi. Ndipo akaagiza kwamba ufanyike ukarabati na yeye akaahidi kuja kukagua ukarabati huo mwezi Juni, 2014.

  Mara baada ya kusomewa taarifa ya mradi, Waziri Mkuu akahoji ni kwa nini hawajafanya chochote tangu alipotoa maelekezo Machi, mwaka huu. Hakupata jibu la kueleweka kutoka kwa viongozi wa wilaya na mkoa.

  Waziri Mkuu aliwasalimia wananchi waliokuwepo kwenye eneo hilo na kuwaeleza kwamba hawezi kukagua kituo hicho ilhali hakuna kilichotekelezwa tangu afike hapo Machi mwaka huu.

  Alisema haiwezekani yeye atoe maagizo katika kipindi chote hicho halafu kisifanyike kitu chochote. Akaondoka na kuendelea na ziara hadi kijiji cha Manzase ambako alikagua mradi wa kisima cha maji.
  Mapema, katika taarifa yake, Mhandisi Kilembe alisema kituo hicho cha afya kilijengwa chini ya ufadhili wa ubalozi katika makubaliano yaliyofikiwa Novemba 11, 2009 kwamba ingetoa dola za marekani 84,307 sawa na sh. Milioni 152.86.

  Hata hivyo, mara baada ya ujenzi kukamilika Agosti 29, 2012, kituo hicho kilipata nyufa nyingi hali iliyosababisha kifungwe na wananchi walitoa malalamiko yao kwa Waziri Mkuu Machi mwaka huu wakati alipokwenda kuzindua mradi wa maji kwenye kijiji cha Mkonze jirani na kituo hicho.

  Akiwa katika kijiji cha Manzase Waziri Mkuu aliridhishwa na ujenzi wa mradi wa maji kwa ajili ya wakazi 9,000 wa eneo ambapo alielezwa kwamba utakamilika Julai 16, 2014.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 980,
  DODOMA.
  JUMAMOSI, JUNI 7, 2014

  0 0

  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na wanachama wa CCM Tawi la SAUT Kambarage ambapo aliwaambia kuwa wasomi wa vyuo wanatakiwa kuchangia mawazo yao kwenye chama ambayo yatasaidia kuleta mabadiliko hasa ya kiuchumi ,alisema ni vyema kuja na mikakati ya kuonyesha uchumi umepanda kwa mwananchi kuliko huu wa sasa ambao unaonyesha uchumi umepanda lakini ni uchumi wa kwenye makaratasi.Uongozi Tawi la SAUT Kambarage ulimualika Katibu wa Itikadi na Uenezi kuja kushuhudia makabidhiano ya Uongozi na tathmini ya Tawi kwa miaka minane sasa.
   Aliyekuwa Rais wa Serikali ya Wanafunzi katika Chuo cha SAUT Mwanza Ndugu Dova Mcheshi akizungumza wakati wa shughuli ya kukabidhiana Uongozi wa Tawi la SAUT Kambarage ambapo aliwaambia wanachama wa CCM katika Chuo cha SAUT kuwa kuanzia sasa chama kinajiimarisha zaidi kwenye Chuo cha SAUT.Dova laiyekuwa CHADEMA lakini sasa amejiunga na CCM .
   Wadada wakiwa wamependeza na Sare yao ya Chama.
   Viongozi wa CCM mkoani Mwanza na Viongozi wa Serikali ya wanafunzi wakiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu Mwenezi wa CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye.
   Wanachama wa Tawi la CCM SAUT Kambarage,Mwanza.

  0 0

  Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Kanisa Katoliki, Muadhama Policarp Kadinali Pengo,akinzungumza wakati wa sherehe za siku ya wazazi ya shule ya sekondari ya wasichana, Marian, iliyoko Bagamoyo mkoani Pwani, Jumamosi Juni 7, 2014.
  Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Kanisa Katoliki, Muadhama Policarp Kadinali Pengo, akimshukuru Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, kutokana na Mfuko huo kudhamini sherehe za siku ya Wazazi ya sekondari za Marian, huko Bagamoyo, mkoani Pwani Jumamosi Juni 7, 2014.
  Eliamini Amon Urio, (Katikati), mzazi wa Eileen, ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari ya wasichana, Marian, iliyoko Bagamoyo  mkoani Pwani, akielezea jinsi fao la elimu litolewalo na Mfuko wa Pensheni wa PPF, linavyosadia kumsomesha mtoto wake, baada ya kumpoteza mumewe mwaka 2005. Aliyasma hayo wakati wa sherehe za siku ya wazazi ya shule hiyo, Jumamosi Juni 7, 2014. Kushoto ni Meneja Uhusiano na Masoko wa PPF, Lulu Mengele na kulia ni Afisa Michango wa PPF, Kanda ya Kinondoni, Kwame Temu.
  Joyce Nachenga, (Kusho), mwakilishi wa Mfuko wa PPF, Kanda ya Kinondoni  jijini Dar es Salaam, akiwaeleza wazazi wa wanafunzi wa shule ya sekondari Marian, faida za kujiunga na Mfuko huo, wakati wa sherehe za siku ya wazazi iliyofanyika shuleni hapo Jumamosi Juni 7, 2014.
  Mmoja wa wanafunzi wanaofaidika na fao la Elimu, litolewalo na Mfuko wa Pensheni wa PPF, Rosalia Faustin Madulu, (Kulia), akieleza jinsi yeye binafsi ambaye kwa sasa yuko kidato cha Kwanza shule ya sekondari Marian iliyoko Bagamoyo, jinsi anavyofaidika na fao hilo tangu apoteze mzazi wake miaka 9 iliyopita. Aliyasema hayo wakati wa siku ya wazazi ya sekondari hiyo, Jumamosi Juni 7, 2014.Wakwanza kushoto ni Meneja Uhusian na Masoko wa PPF, Lulu Mengele, na wengine ni wanafunzi wengine wa shule hiyo wanaofaidika la fao hilo, Deborah Kibona, (Wapili kushoto) na Eileen Amon Urio.

older | 1 | .... | 293 | 294 | (Page 295) | 296 | 297 | .... | 1897 | newer