Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 292 | 293 | (Page 294) | 295 | 296 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Dk. Eng. Binilithi Satano Mahenge wa pili (kulia), akiwa katika ziara yake ya kukagua mazingira ya Kiwanda cha bia (TBL) kilichopo kata ya Pasiasi wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, na wa pili (kushoto) ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Angelina Madete,wakati maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani yakiendelea jijini Mwanza.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais -Mazingira, Mh. Dk. Eng. Binilithi Satano Mahenge wa tatu (kulia)akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda cha bia bw. Said Lwambo wa kwanza (kushoto) juu ya jinsi mashine za Majitaka za kiwanda cha TBL kinavyofanya kazi na kulinda Mazingira.
  Mh. waziri wa Nchi Ofisi ya makamu wa Rais -Mazingira,Dk. Eng. Binilithi Satano Mahenge wa kwanza (kulia), Naibu Waziri Mh. Ummy Mwalimu wa kwanza (kushoto)na Mkuu wa Mkoa Eng. Everist Ndikilo wa pili (kulia) wakizungumza na mmiliki wa Kiwanda cha Coca Cola (Nyanza bottling) Bw. Christopher Mwita Chuma baada ya kuwasili ofisini kwake leo jijini Mwanza.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Ummy Mwalimu wa kwanza (kushoto)akiwa anafanya usafi eneo la mtaa wa Pamba A jijini Mwanza stendi ya zamani.

  0 0


  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Dkt. Elifatio Towo (Katikati) akieleza umuhimu wa vitamini A, Kushoto ni Afisa Lishe Mwandamizi Bi. Neema Joshua na kulia ni Afisa Mtafiti wa Sayansi ya Chakula Bi. Wessy Meghji.

  Afisa Mtafiti wa Sayansi ya Chakula na Lishe Wessy Meghji akionesha aina ya vyakula ambavyo vinaongeza vitamini A, kushoto ni Elifatio Towo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe

  TAASISI YA CHAKULA NA LISHE TANZANIA

  PROGRAM YA UTOAJI MATONE YA VITAMINI A KWA WATOTO WALIO KATIKA UMRI WA MIEZI 6 HADI MIAKA MITANO
  Upungufu wa vitamini na madini ni mojawapo ya matatizo makubwa ya kilishe yanayowaathiri hasa watoto na wanawake walio katika umri wa kuzaa hapa Tanzania. Takwimu za kitaifa juu ya demografia na afya ya jamii (Demographic and Health Survey) za mwaka 2010 zinaonesha kuwa hapa Tanzania upungufu wa vitamini A unaathiri asilimia 33 au theluthi moja ya watoto walio chini ya miaka mitano na asilimia 37 au zaidi ya theluthi moja ya wanawake walio katika umri wa kuzaa. 
  Upungufu wa madini chuma unaathiri asilimia 59 au zaidi ya nusu ya watoto wadogo na karibu asilimia 41 au karibu ya nusu ya akina mama wajawazito, na pia upungufu wa madini joto unakadiriwa kuathiri asilimia 7 ya Watanzania. Njia mojawapo ambayo inatumika kupunguza tatizo

  Kwa kuanzia tuangalie upungufu wa vitamini A

  •      Vitamini A ni mojawapo ya vitamini isiyotengenezwa na mwili na hivyo ni lazima itokane na vyakula

  •      Vyakula vywenye vit A kwa wingi

  –     Mboga na matunda hasa yenye rangi ya kijani na njano

  –     Samaki hasa dagaa

  –     Mafuta ya mawese

  –     Maini

  –     Viazi lishe

  Sababu za Upungufu

  •              Ulaji duni usiokidhi mahitaji ya Vit A mwilini

  •              Unyonyeshaji watoto maziwa ya mama usiofuata kanuni (Sub optimal breastfeeding)

  •              Magonjwa ya mara kwa mara

  •              Utunzaji duni wa makundi husika

  •              Mgawanyo mbaya wa rasilimali

  Waathirika wakuu:

  •      Watoto walio katika umri wa chini ya miaka mitano

  •      Wanawake walio katika umri wa uzazi.

  •      Asilimia 33 ya watoto walio katika umri wa chini ya miaka 5 wana upungufu wa vitamini A

  •      Asilimia 37 ya akina mama walio katika umri wa kuzaa wana upungufu wa vitamini A

  Madhara ya Upungufu wa vitamini A

  •      Kutokuona vizuri kwenye mwanga hafifu

  •      Upofu

  •      Maradhi ya mara kwa mara kutokana na kupungua kwa kinga ya mwili

  •      Vifo hasa vya watoto

  •      Kushuka kwa elimu

  •      Kupungua kwa tija

  Njia zinazotumika kupambana na tatizo

  •      Unyonyeshaji sahihi wa watoto

  •      Ulaji wa vyakula vyenye virutubishi hasa vya vitamin A kwa wingi na vya mchanganyiko

  •      Ulaji wa matunda na mboga za majani kwa wingi (Hasa vile vyenye rangi ya kijani kibichi na njano)

  •      Uongezaji virutubishi vya vitamini A kwenye vyakula (mafuta ya kula)

  •      Kutoa nyongeza ya matone ya vitamini A kwa watoto walio katika umri wa miezi 6 hadi miaka mitano
  Utoaji wa matone ya vitamin A

  Matone ya vitamini A hutolewa  kwa watoto walio katika umri wa miezi 6 hadi miaka mitano mara mbili kwa mwaka (June na December)
  Watoto wa umri wa miezi 6 hadi miezi 11 hupewa kidonge chenye IU 100,000
  Watoto wa umri wa mwaka mmoja hadi miaka mitano hupewa kidonge chenye IU 200,000
  Matone yanatolewa katika vituo vya afya na vituo vya muda hususani kwa kazi hiyo ili kuwafikia watoto wengi zaidi nia ikiwa ni kuwafikia wote.
  Kwa Tanzania zoezi limekuwa likiwafikia watoto zaidi ya asilimia 80.

  Wakati wa zoezi la utoaji wa matone ya vitamini A watoto wote wenye umri wa mwaka 1 hadi miaka 5 hupatiwa pia dawa ya kutibu minyoo

  Changamoto Ambazo Zinafanyiwa Kazi

  Baadhi ya changamoto zilizopo ni pamoja na: Mfumo wa usambazaji matone ya vitamini A ili kuhakikisha walengwa wanavipata kwa wakati.

  Ukusanyaji wa takwimu za kiwango kilichofikiwa na kuwasilisha taarifa kwa wakati

  Kuweza kuwafikia walengwa wote hasa maeneo ambayo ni korofi

  Wazazi na walezi wanapaswa kufahamu nini? Ujumbe muhimu

  Kila mzazi / mlezi wa mtoto mdogo anapaswa kufahamu umuhimu wa vitamini A kwa ukuaji, maendeleo mazuri, afya na uhai wa mtoto.Vile vile vyakula tunavyokula havikidhi mahitaji ya vitamini A kwa watoto kwani hula kiasi kidogo wakati mahitaji yao ni makubwa na hivyo ni muhimu wapatiwe matone ya vitamini A mara mbili kila mwaka. Pia wanapaswa kufahamu wakati na mahali ambapo zoezi la utoaji wa matone ya vitamini A hufanyika ili waweze kuwapeleka watoto wao kila baada ya miezi sita

  Kwa mwaka huu 2014 matone ya vitamin A na dawa za minyoo zinatolewa lini

  Mwaka huu wa 2014 matone ya vitamini A na dawa za kutibu minyoo zitatolewa kwa awamu kama ifuatavyo

  Awamu ya kwanza matone ya vitamini A na dawa za kutibu minyoo zitatolewa katika halmashauri zote za Tanzania Bara katika kipindi chote cha mwezi ujao wa Juni 2014 kwa watoto wote wenye umri wa miezi 6 – 59 (vitamini A) na watoto wote wa umri wa mwaka 1 – 5 (dawa za kutibu minyoo).

  Awamu pili matone ya vitamini A na dawa za kutibu minyoo zitatolewa katika halmashauri zote za Tanzania Bara katika kipindi chote cha mwezi wa Disemba 2014 kwa watoto wote  wenye umri wa miezi 6 – 59 (vitamini A) na watoto wote wa umri wa mwaka 1 – 5 (dawa za kutibu minyoo).

  Wazazi na walezi wapelekeni watoto wakapate matone ya vitamini A na dawa zaminyoo kwa ajili ya kuboresha afya na ukuaji wao kwani ni haki yao.

  Wanahabari hamasisheni jamii kuwapeleka watoto walengwa wakapate matone ya vitamini A na dawa za kutibu minyoo kwa kuwafikishia ujumbe sahihi.

  0 0


  Sehemu ya Wacheza Filamu nchini waliokuwa wamebeba Jeneza lenye Mwili wa Marehemu George Otieno Okomu (George Tyson) wakijipanga tayari kwa akili ya kuongoza shughuli ya Kuga mwili iliyofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.Mwili huo umesafirishwa kupelekwa nchini Kenya ambako ni nyumbani kwao na Marehemu kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika Jumamosi ijayo baada ya kukamiliza kwa mipango yote.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Saddick akiwaongoza waombolezaji mbali mbali kwenye shughuli ya kuaga mwili wa Marehemu George Otieno Okomu (George Tyson) waliofika kwa wingi kwenye viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.

  Mkurugenzi Mkuu wa Kipindi cha The Mboni Show,Mboni Massimba (kulia) akiwa ni mwenye huzuni sana kwa kuondokewa na Mwaznilishi mwenza kwa Kipindi chake hicho ambaye alifariki Dunia katika ajali ya Gari huko Mkoani Morogoro wakati wakitokea Mkoani Dodoma kukabidhi msaada wa Madawati katika moja ya shule za msingi zilizopo mkoani humo ikiwa ni maadhimisho ya Miaka miwili ya kipindi hicho.

  Aliekuwa Mke wa Marehemu George Otieno Okomu (George Tyson),Yvone Chelly (Monalisa) na Mwanae Sonia wakiwa ni mwenye Majonzi makubwa kwa kuondokewa na mpendwa wao.Kushoto ni Mama wa Monalisa,Bi. Natasha.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Saddick akitoa nasaha zake wakati wa msiba huo.


  0 0


  0 0

   Mchora katuni, Nathan Mpangala (mwenye sanigogozi) akisikiliza simulizi toka kwa wenyeji wa Kitongoji cha Masakasa Mpala, Kilwa Masoko, Lindi hivi karibuni. Mzee Hamis Sumri (aliyetinga kitu cha Arsenal) anasema, sifa moja ya kitongoji chao ni hii; kiliwatoa Salum Chanza, Ali Juma, Idd Hamis na Mzee Juma kwenda kushiriki vita ya pili ya dunia kati ya Mjerumani na Mwingereza na walirudi salama salimini.
   Mchora vibonzo Nathan Mpangala, akipapasa mzinga ulio nje ya Boma la Wajerumani, Kilwa Kivinje, Lindi. Mtambo huu ambao kiukweli unaonekana kama hauna mwenyewe, yaani upo upo tu, ulitumika ‘kuwanyooshea’ watu waliokuwa wakipinga utawala wa mkoloni huyo.
   Ona hii. Fulu vichaka, mamlaka zinazohusika wamepasusa kabisaaaa!!! Hapa (Kilwa Kivinje, Lindi) ndipo walipolazwa Wajerumani waliodunguliwa katika vita ya Majimani, 1905 – 1907. Muongoza wageni, Bw. Samuel akimwonesha mchora vibonzo, Nathan Mpangala moja ya makaburi hayo. Picha ndogo ni maelezo ya kaburi hilo. Kama Kijerumani kinapanda tutafasirie, pliizi.
   Mnara wa kwa Bi. Adha, Kilwa Kivinje, Lindi. Kumbukumbu ya Wajerumani wawili waliuawa na wenyeji mwaka 1888 kwa imani kuwa walikwenda eneza dini ya Kikristo. Picha ndogo ni maelezo ya mnara huo.
   Mchora vibonzo, Nathan Mpangala (kulia), akistaajabu gofu ya iliyokuwa Ngome ya Kilwa, lililopo Kilwa Kisiwani, Lindi. Kwa mujibu wa muongoza wageni Bw. Samuel, anasema mjengo huo ambao ulikuwa mahsusi kwa ajili ya kulinda kisiwa, ulijengwa karne ya 16 na Wareno. Ilipofika karne ya 19 Waarabu wakaunakshi nakshi zaidi.
   Hili gofu laitwa Makutano Palace, limejaa tele Kilwa Kisiwani, Lindi. Moja ya kumbukumbu zake inadaiwa katika karne ya 18, Sultan wa Oman, Bw. Ibrahim alilitumia kuingia mkataba wa kumpa watumwa (babu zetu na bibi zetu), mfanyabiashara wa Kifaransa Bw. Moris. Uliopumzika ardhini ni mabaki ya mzinga uliotumika kusasambulia ‘maadui’.
   Mchora vibonzo, Nathan Mpangala akiwa mbele ya gofu la Makutano Palace lililo Kilwa Kisiwani, Lindi hivi karibuni. Hakika Tanzania ni zaidi ya tuijuavyo!

  Mchora vibonzo, Nathan Mpangala akiwa makaburi ya Familia ya Sultani wa Kilwa, Al Hassan Bin Suleiman, Kilwa Kisiwani, Lindi hivi karibuni. Makaburi haya yanayodaiwa ya karne ya 16 yana alama ambazo ni rahisi kugundua lipi la mwanaume na lipi la mwanamke.

  0 0

  Kaimu Meneja wa Mafao ya Matibabu Dk. Lucy Simbila akizungumza kabla hajamkaribisha Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga afungue Kambi ya Upimaji Afya.
  Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dk. Charles Rweikiza akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kambi ya Upimaji Afya Wilaya ya Kahama. Kushoto ni Dk.Mzige, wa tatu kutoka kushoto ni  Kaimu Meneja wa NSSF Kahama , Salum Salahange, Kaimu Meneja wa Mafao ya Matibabu Dk.Lucy Simbila na Ofisa Uhusiano NSSF, Jumanne Mbepo. 
  Dk.Mzige Akitoa Ushauri kwa mmoja wa wakazi wa Kahama aliyejitokeza kupima.
  Dk.Kika akiwapima wakazi wa Kahama  Kisukari kwenye  kambi ya Upimaji Bure wilayani Kahama.
  Dk. Duma wa NSSF akipima uzito na urefu watu waliojitokeza kupima afya zao.
  Wakazi wa Kahama wakiwa kwenye foleni ya kujiandikisha ili waweze kupima afya zao.
  Wakazi wa kahama wakiwa kwenye foleni ya kwenda kumuona Daktari.
  Wakazi wa Kahama wakisubiria kwenda kuwaona madaktari wanaoendesha zoezi la upimaji Bure.
  Dk. Lucy  Simbila akishuhudia Dk. Ali Mzige akimpima Shinikizo la Damu Dk.Charles Rweikiza kuashiria kuanza kwa kambi ya upimaji Afya.
  Bw. Kika akipima sukari baadhi ya watu waliofika kwenye zoezi la upimaji Afya bure.
  Madaktari wakiwapa ushauri watu waliofika kupima afya zao.
  Katikati Afisa uhusiano wa NSSF Jumanne Mbepo akimkabidhi fulana mmoja wa watu waliopima afya.
  Wakazi wa shinyanga wakisubiri kwenda pima.


  Na Mwandishi Wetu

  Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), linaendesha  kambi za upimaji wa Afya bure kwa wakazi wa kanda ya ziwa kwa kipindi cha mwezi mmoja.  Lengo la kambi hizi ni kuweza kutoa elimu na  kuwahamasisha wanachama wa NSSF na wananchi kwa ujumla waweze kujenga  tabia ya kupima afya zao mara kwa mara na kujiwekea mfumo bora wa maisha ili kuepukana na magonjwa sugu yasiyoambukiza.  Zoezi ambalo lilianzia mkoa wa Mara na kupata mwitiko mkubwa wa wakazi wa Mara kwa kupima watu 1582 ambao watu waliopima VVU ni 1380, linaendelea mkoa wa Shinyanga , Wilaya ya Kahama, kwenye Viwanja vya Barcelona, kuanzia tarehe 04/06/2014, 

   kwa siku mbili mfululizo, kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi na moja Jioni.  Baadae, Kambi hizi zitaendelea katika Mkoa wa Geita na  Mkoa wa Kagera.


  HUDUMA ZITAKAZOTOLEWA

  Huduma mbalimbali zitatolewa  kwenye kambi hizi zikiwemo;

  ·         Upimaji wa Shinikizo la damu

  ·         Upimaji wa sukari kwenye damu- Kisukari

  ·         Upimaji wa hali ya lishe (Uwiano wa Urefu kwa Unene)

  ·         Utoaji wa dawa za Minyoo

  ·         Ushauri wa kitaalam kwa watakaokutwa na Matatizo

  ·         Ushauri nasaha  na upimaji hiari wa VVU (UKIMWI)

  ·         Kutoa vipeperushi vya Maelezo ya uboreshaji wa Afya.


  Huduma  zote hizi zitatolewa na NSSF, BURE.

  NSSF inaendelea kuwasii na kuwahimiza wakazi wa kanda ya ziwa kuwa waendelee kujiandikisha kwenye NSSF HIARI Scheme. NSSF HIARI Scheme ni kwa ajili ya wajasiriamali wadogo, wachimbaji wadogo, Ushirika wa Bodaboda , Ushirika wa Wakulima pamoja na wanachama wa Mifuko mingine ya hifadhi ya jamii.  Jiunge na NSSF HIARI Scheme ili uweze kujipatia mafao bora ya NSSF yakiwemo Bima ya Afya BURE kwa familia nzima (SHIB), mikopo nafuu ya SACCOS,  pamoja na Mafao bora mengineyo.  Wananchi wa kanda ya ziwa wanakumbushwa na kuhimizwa kujitokeza kwa wingi ili kupimwa na kupewa ushauri wa afya zao Bure.  NSSF INAJENGA MAISHA YAKO YA SASA NA YA BAADAE.

  0 0

  Ndugu Fredricky Kajiru Mroki wa Kipera-Kinyenze Morogoro, anasikitika kutangaza kifo cha mtoto wake Eliewaha Kajiru (Pichani) kilichotokea alfajiri ya leo Nyumbani kwake Kipera. 


  Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa Bibi yake Kinyenze, Mvomero Morogoro. Habari ziwafikie, Baba Mkubwa wa Marehemu, Lloyd Atenaka wa Kibaha Block B, Baba wadogo wa Marehemu, Dossa Mroki, Onesmo Nathan, Thomas Nathan, Daniel Nathan, Kyase Nathan na Mroki Mroki. Shangazi wa Marehemu, Stella Kaluse na Namche Mroki wa Dar es Salaam. Pia habari ziwafikie Babu wa Marehemu Agustino Shogholo Mgonja wa Pugu Kajiungeni na ukoo wote wa Kajiru, Mroki, na Shogholo popote pale walipo. 


  BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.

  0 0

  Promoter DMK,Diamond Platnumz,Kevin Liles,Raisi Kikwete.
  Hivi Majuzi wakati Tour ya Diamond ilipokuwa New York,Ma Promoter wake pamoja na Yeye mwenyewe walikaribishwa na Mheshimiwa Raisi ambapo mbali na mambo mengine Mheshimiwa alimpongeza Diamond katika mafanikio yake ikiwa nipamoja na Kuchaguliwa kuwania tuzo za BET hapa nchini Marekani.

  Rais hakuwahi kupata nafasi ya kumpongeza kijana huyo kwani wakatimatangazo yalipotoka Diamond alikuwa nje ya nchi.Mheshimiwa pia alimkutanisha Diamond na aliyekuwa Raisi wa Def Jam Record/Warner Bros Music group Mr Kevin Liles ambaye alionyesha nia ya kufanya mambo makubwa na Diamond.

  Kevin ni Multi Millionare mwenye utajiri wa zaidi ya Dollar Milioni 60 ambaye kwa sasa ni manager wa wanamuziki Trey Song,Big Sean,Ty Dolla Sign,Kuna uwezekano mwanamuziki Diamond akawajoin Hao hivi karibuni..waingereza wanasema(hard work pays)Congratulation to Diamond for hard work and Thank you Mr President for Supporting your Youths.
  Kuna jambo liliwafurahisha kutoka kwenye video za Diamond
                                          Je wataka kujua Nini hapa kilikuwa kikizungumziwa?
                                                         
  Kevin akiangalia Video ya Diamond akiwa Congo kwenye simu yake.

  0 0

  Karibu katika mahojiano ya Kwanza Production na Dekula Kahanga "Vumbi" Vumbi ambaye anamiliki Dekula Band nchini Sweden
  Amezungumzia mambo mengi ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa albamu yake mpya ya Shujaa Mamadou Ndala iliyozinduliwa Aprili 23 na 24 huko Sweden.
  Pia, ametoa ushauri kwa wasanii wa Afrika Mashariki wanaotaka kufanya muziki nchi za Scandinavia
  KARIBU UUNGANE NASI
  Kwa maoni na ama ushauri usisite kuwasiliana nasi kupitia kwanzaproduction at gmail.com

  0 0

  *Geneviveve Nnaji na John Dumelo nao ndani
  *Habib Koite, Didier Awadi kuburudisha
  *Filamu ya Mandela kufungua pazia
  DSC_0021
  Mkurugenzi Mkuu wa ZIFF, Profesa Martin Mhando (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuzindua rasmi Tamasha la Filamu la nchi za Majahazi la 17 maarufu kama Zanzibar International Film Festival (ZIFF). Kulia Msaidizi wa Kitengo cha habari ZIFF, Lara Prieston, Kushoto ni Meneja wa Tamasha la ZIFF, Daniel Nyalusi (Dean), Afisa Mawasiliano wa ZIFF, Hassan Musa "Has T" (wa pili kushoto) na Music Coordinator wa ZIFF, Edward Lusala (katikati). Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog

  Na Andrew Chale
  DUNIA inatarajia kushuhudia tukio kubwa na la kihistoria ndani ya viunga vya Ngome Kongwe ndani Mji Mkongwe wa Stone Town, Unguja, kwa watu wa mataifa yote watakapoungana na kushuhudia ‘Hatma ya Pamoja’ (A common Destiny) Juni 14 hadi 22, 2014, katika Tamasha la Kimataifa la filamu la Zanzibar (ZIFF).

  Tamasha hilo maarufu kama filamu la nchi za Majahazi ZIFF, kwa mwaka huu linatarajiwa kufanyika kwa mara ya 17, tokea kuanzishwa kwake.
  Akizungumza mapema leo jijini Dar es Salaam, kwenye halfa maalum ya uzinduzi wa tamasha hilo la 17, kwa wandishi wa habari iliyofanyika Goethe Institut kituo cha utamaduni, Mkurugenzi Mkuu wa tamasha hilo, Profesa Martin Mhando, alisema tamasha hilo msimu wa mwaka huu linatarajiwa kuwa moto kwani linakuja na mambo mbalimbali yenye kuleta mabadiliko ya hali ya juu.

  Ni kutokana na mabadiliko hayo, Profesa Mhando anasema tasnia ya filamu kwa Tanzania inahitaji kubadilika ikiwemo wasanii wenyewe kujituma na hata kuingia darasani ili kufanya kazi zenye uhakika. Akimaanisha kila msanii wa filamu aweze kufikia malengo yake, hana budi kujifunza na kushirikisha wale waliotangulia katika tasnia hiyo. Anazungumziaje kaulimbiu ya ‘A Common Destiny’.

  Prof. Mhando amesema kauli mbiu ya mwaka huu yenye kusema Hatma ya pamoja yenye maana ya ‘A common Destiny’, ina lengo la kuwakutanisha watu wa mataifa mbalimbali kuwa kitu kimoja na kufurahia kwa pamoja ikiwemo kubadilishana mawazo kwa pamoja kwa tasnia ya filamu, muziki, kwa mlengo ya kujenga.

  “Tukiwa na haja moja, kuishi kwa amani na kuleta mapinduzi ya kiuchumi, kifikira na maendeleo kwa amani, ZIFF kwa kutumia dira hiyo hasa kupitia filamu zetu za ndani zenye mchanganyiko wa utamaduni na asili yetu.
  “Wazanzibari na hata wageni watakaoshuhudia filamu hizi wataweza kuchukua utamaduni huo na kuupeleka nje kwa furaha kubwa katika kufikia hatma ya pamoja” amesema Prof. Mhando.
  DSC_0082
  Music Coordinator wa ZIFF, Edward Lusala akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na wasanii watakaotoa burudani kwenye tamasha hilo.
  Lupita-Nyong-o-729-620x349
  Lupita Nyong’o, Genevieve ndani ya nyumba
  Tukio kubwa ambalo kwa sasa Tanzania hasa kwenye viunga vya Zanzibar na nchi nyingine duniani katika tamasha hilo la 17, ni ujio wa msanii wa Kenya na Mexico, Lupita Nyong’o, atakayeudhuria utoaji wa tuzo hizo za ZIFF mwaka huu.

  Lupita ambaye ametwaa tuzo za Oscar na nyingine nyingi na kupelekea kutikisa Hollywood kwa sasa ni miongoni mwa mastaa watakaokuwa kwenye tamasha hilo huku akitarajiwa kuambatana na wazazi wake wote wawili pamoja na wadogo zake.

  Prof. Mhando amesema tayari wazazi wote wawili wa Lupita akiwemo Dorothy na Peter Anyang’ Nyong’o, watakuwapo kwa siku zote 10 kwenye tamasha hilo huku Lupita mwenyewe akiahidi kuangalia uwezekano wa kuhudhuria japo katika utoaji wa tuzo kama ratiba za shughuli zake hazita mbana.

  Prof. Mhando alisema Lupita ni zao la ZIFF na ndiyo iliyomfungulia mwanya wa kujulikana na baadaye alienda kusoma zaidi masuala hayo ya filamu, ambapo alishiriki ZIFF 2007 kama Volunteer. Mara nyingi staa huyo amekua akihudhuria matamasha na halfa mbalimbali za utoaji wa tuzo na zawadi zingine huku akiwa ameambatana na wazazi wake wote wawili.

  Lupita mbali na tuzo hiyo ya Oscar, kupitia filamu ya ‘12 Years a Slave’ pia filamu hiyo imempatia tuzo mbalimbali zikiwemo: tuzo ya Steve McQueen kama mwigizaji mwenye mvuto, mwigizaji bora wa kike aliyeshirikishwa, ‘Academy Award’, ‘Screen Actors’ Guild Award’, ‘NAACP Image Award’, ‘Independent Spirit Award’, ‘Broadcast Film Critics Association Award’, na nyingine nyingi.
  Genevieve-Nnaji-Cover
  Genevieve Nnaji.
  Mbali na Lupita, katika kuongeza utamu wa tamasha hilo, mastaa wengine nguli wa Afrika kwa mwaka huu wanaotarajiwa kuwapo katika ushuhudiaji wa utoaji wa tuzo hizo ni pamoja na muigizaji na mwanamitindo nyota wa Nigeria, Genevieve Nnaji.

  Wengine ni Amr Waked (Misri), Faouzi Bensaidi (Morocco), Nadia Buari, Richard Mote Damijo ‘RMD’, John Dumelo, Desmond Eliot na Florence Masebe.


  DSC_0067
  Afisa Habari wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Fizza Moloo akizungumzia kuhusiana na Filamu iliyopewa jina la "Women with Altitude" iliyoandaliwa na WFP ambapo ndani yake imeshirikisha wanawake wa kitanzania watatu waliofanikiwa kufika kilele cha Mlima Kilimanjaro wakiwa wameambatana na wenzao nane kutoka Nepal na kuzungumzia changamoto mbalimbali wakati wa kupata elimu na maisha kwa ujumla itakayoonyeshwa kwenye tamasha hilo tarehe 17/6/2014 saa 19:15 jioni ukumbi wa Old Fort visiwani Zanzibar.

  Filamu ya Mandela kufungua pazia

  Jumla ya filamu 79, kutoka mataifa mbalimbali zinatarajiwa kuonyeshwa huku filamu iliyoingia kwenye tuzo za Oscar, ya Mandela: ‘A Long Walk to Freedom’ ndiyo itakayofungua pazia kwenye tamasha hilo, Juni 14.
  “Katika filamu hizo 79 za kimataifa zitaoneshwa ZIFF, nyingi zikiwa zinatoka katika nchi za Kiafrika na filamu ya Mandela imepata bahati ya kuwa ya ufunguzi”, amesema Profesa Mhando.

  Pia Profesa Mhando amesema kuwa zitakuwepo filamu zinatoka katika nchi 35 zikiwemo filamu fupi 38, filamu ndefu za kuburudisha 24 na makala 17.
  DSC_0137
  Meneja wa Tamasha la ZIFF, Daniel Nyalusi "Dean" akionyesha kitabu chenye ratiba nzima ya tamasha hilo litakalorindima visiwani Zanzibar kuanzia Juni 14 hadi 22 mwaka huu.
  Burudani zitakazopamba
  Kwa upande wake, Edward Lusala anayeshughulikia muziki kwenye tamasha hilo la 17, anasema kuwa, wamejiandaa kutoa burudani ya aina yake ambayo itaacha historia kwa mwaka huu.
  Lusala amesema jumla ya makundi 18 yanatarajiwa kutumbuiza. Huku kwa wasanii gwiji wakiwemo pia Didier Awadi kutoka nchi ya Senegal na Habib Koite (Mali) wanatarajiwa kuja kuishika Zanzibar na viunga vyake.
  “Wasanii Koite na Didier ni miongoni mwa wasanii wakubwa sana na wenye heshima kubwa hasa kwa muziki wao kwani wanapiga kimataifa hasa katika matamasha makubwa na wamekuwa wakipiga miziki ya kipekee. Hivyo watu wote watafurahia” amefafanua Lusala.
  Ameongeza kuwa, wasanii wengine ni pamoja na Farid Kubanda ‘Fid Q’, Ambwene Yesaya ‘ Ay’, Sauti Soul, Mzungu Kichaa, Ras Inncent Nganyagwa, Grace Matata na wengine wengi ambao watatoka Tanzania.
  Na kuongeza kuwa kwa sasa AY yupo nchini Malawi akijifua na moja bendi maarufu ya muziki wa Live ambapo anatajiwa kukaa jukwaani kwa zaidi ya lisaa limoja na nusu huku akiimbaLIVE.
  Pia vikundi vya muziki nguli toka Tanzania, Egypt, Kenya, Uganda, Malawi na Afrika ya Kusini vitatumbuiza kila siku katika tamasha hilo.
  Aidha, Lusala amesema kuwa, kwa mwaka huu wanatarajia kufanya ‘surprise’ kwa kumleta msanii mkubwa ambaye bado wapo kwenye mazungumzo na msanii huyo kutoka Afrika kusini.
  Kwa upande wake Meneja wa tamasha hilo, Daniel Nyalusi amewataja wadhamini wa tamasha hilo ni pamoja mdhamini mkuu ZUKU Pay tv, huku wengine ni Ethiopian Airlines, Tanzania Media Fund TMF, ComNet, Cello, Air Uganda, Gina Din, FASTJET and United Petroleum. Wengine ni shirika la Rosa Luzemburg Foundation, Arterial Networking, Steps International, Azam marine, Prime Time Promotions, Goethe Institut na wengine wengi.
  ZIFF moja kati ya matamasha ya filamu makubwa duniani hukutanisha wadau katika tasnia ya filamu. Wakiwemo waigizaji wa siku nyingi na maarufu, waongozaji, waigizaji wachanga na wanafunzi kutoka ulimwenguni kote
  DSC_0119
  Meneja wa Biashara wa shirika la ndege la Fastjet, Jean Uku akizungumzia udhamini wao kwenye tamasha hilo ambapo wametoa tiketi za safari ya washiriki kutoka Afrika Kusini watakaoshiriki kwenye tamasha hilo.
  DSC_0084
  Msanii wa Hip Hop, Harry Kaale kutoka kundi la One "The Incredible" akielezea namna watakavyotoa burudani na elimu kwa vijana kwenye tamasha hilo.
  DSC_0105
  Msanii Mzungu Kichaa akiwashukuru ZIFF kwa kutoa nafasi kwa wazalendo kuonyesha vipaji vyao kwenye tamasha la ZIFF.
  DSC_0108
  DJ maarufu Kahlil Jacobs-Fantauzzi kutoka Puerto rico akisisitiza kutoa burudani ya aina yake kwenye tamasha hilo.

  0 0

  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mjumbe Maalumu wa Rais Jacob Zuma wa Afrika kusini ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mama Maite Nkoana-Mashabane Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 6, 2014.  Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernad Membe alikuwepo pia


  0 0

  Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wizara ya Uchukuzi, Bw. Issa Nchasi, akifanya usafi katika eneo la bandari ya Dar es Salaam kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani ambayo kwa mwaka huu kauli mbiu ni ‘Tunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi Tanzania’.
  Sehemu ya wafanyakazi wa Wizara ya Uchukuzi na taasisi zake wakiwa kwenye zoezi la usafi wa mazingira katika eneo la Bandari ya Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya Mazingiza Duniani.
  Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira wa Wizara ya Uchukuzi, Bi, Tumpe Mwaijande (kulia), akipanda mti katika eneo la bandari ya Dar es Salaam leo asubuhi, kama sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Mazingira. Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira yanafanyika kitaifa mkoani Mwanza ambapo kwa mwaka huu kauli mbiu ni ‘Tunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi Tanzania’. (Picha na kitengo cha mawasiliano Serikalini-Uchukuzi) 

  0 0

  Mratibu wa Mac D Promotions, waandaaji wa mashindano ya Nice & Lovely Miss Tanga 2014, Benson Jackson akiongea na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari katika hoteli ya Mkonge jijini Tanga, ambapo amesema mpaka sasa jumla ya washiriki 19 wamechukua na kurudisha fomu za kushiriki shindano hilo linalosubiriwa kwa hamu kubwa na wakazi wa jiji la Tanga, shindano ambalo litafanyika jumamosi ya tarehe 21/ 06/ 2014 Mkonge Hotel.
  Gari aina ya Toyota Vitz atakalokabidhiwa mshindi wa shindano hilo la Nice & Lovely Miss Tanga 2014 likiwa katika bustani ya Mkonge Hotel jijini Tanga. Shindano hilo limedhaminiwa na Nice & Lovely, EATV, Redd's, Tanga Beach Resort, Breeze Fm, CXC Africa, Rweyunga Blog na Mwambao Fm. 

  0 0

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya madini Mhe. Stephen Masele akifungua mafunzo ya wachimbaji wadogo yaliyofanyika Kibara, mkoani Mara. Pia semina hiyo ilishirikisha viongozi wa vijiji, vyama pamoja na madiwani lengo likiwa ni kuwapa uelewa wa sheria na kanuni za uchimbaji wa madini. Aliyekaa katikati ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara Mhe. Kangi Lugora. Kushoto ni Kamishna Msaidizi – Uendelezaji wa Uchimbaji Mdogo Mhandisi Fredy Mahobe.
  Mtalaamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Kungulu Kasongi akiwasilisha mada wakati wa semina hiyo.
  Mtaalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Kungulu Kasongi akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya madini Mhe. Stephen Masele akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachimbaji wadogo mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo.
  Sekretarieti ya maandalizi ya semina hiyo ikiwajibika.
  Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na mwezeshaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Kungulu Kasongi (hayupo pichani) 

  0 0

   Husna Ibrahim
   Evodia Mdemu
   Happiness Wilson
   Lightness Olomi
   Fatma Hussein
   Marium Shwaib
   Ramta Mkadara
   Angela Kashaga
   Ambasia Maliy
   10.Nuru Omary
   Mary Henry
   Najma Charles
   Faudhia Feka
   .Lydia Charle
   .Lydia Charle
  Mary Kazula

  0 0

  Wasilisha ombi la tiketi kabla ya Agosti 5 kwa safari za hadi Novemba 30, 2014  Shirika la Ndege la Emirates, linalosifika kwa kutoa huduma bora za usafiri wa anga kwa abiria kwa mataifa mbalimbali, limetangaza ofa maalumu kwa Watanzania watakaokwenda Chicago nchini Marekani, kupitia Dubai wakitokea Dar es Salaam. Punguzo hilo au ofa hiyo maalumu ni kwa madaraja ya abiria wa kawaida yaani Economy Class na daraja la wafanyabiashara ‘Business Class’.

  Emirates ilitangaza ofa hiyo mapema Februari mwaka huu na ndege zake zitakuwa zikitua kwenye Uwanja wa  Ndege wa Kimataifa wa Chicago O’Hare. Safari hizo za kila siku zitaanzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai, Terminal 5 ifikapo Agosti 5, 2014 na ndege ya Emirates itakayotumika ni aina ya Boeing 777-200 LR na hivyo kutoa fursa kwa Watanzania kutembelea jiji hilo la tatu kwa ukubwa nchini Marekani.

  Gharama za tiketi ni kuanzia dola za Marekani 1,309 4,285 kwa tiketi ya daraja la abiria wa kawaida kwenda na kurudi na kwa abiria wafanyabiashara gharama ya tiketi ni dola za Marekani 4,285.


  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Emirates maombi ya ununuzi wa tiketi yafanywe kabla ya Agosti 5 na ununuzi wa tiketi hizo za ofa utafanywa kati ya Agosti 5 hadi Novemba 30, 2014. Kwa habari zaidi kuhusu gharama za tiketi na masharti mengineyo, wateja wanaombwa kufuatilia katika tovuti: http://www.emirates.com/tz.

  Chicago iliyopewa hadhi ya jiji tangu mwaka 1837, ina idadi ya watu milioni 2.7na ni jiji linalosifika kwa mambo ya utamaduni na sanaa mbalimbali. Lakini pia jiji hilo linafahamika kwa kuwa bora katika michezo na hivyo hivyo kuwavutia watalii wengi kila mwaka. Inakadiriwa kuwa watalii wanaotembelea jiji hilo kila mwaka ni milioni 46.


  Shirika la Ndege Emirates linafanya safari mbalimbali nchini Marekani na baadhi ya miji ambayo Watanzania wengi wamefikishwa na shirika hilo ni pamoja na Boston, Dallas Fort Worth, Houston, Los Angeles, New York City, San Francisco, Seattle na Washington D.C.


  Abiria wa daraja la kawaida, pia wanaweza kununua tiketi kutoka Dar es Salaam kwenda Boston kwa dola za Marekani 1,534, kwenda Dallas Fort Worth 1,519, Houston 1,518, Los Angeles 1,854, New York City 1,533, San Francisco 1,854, Seattle 1,854 na Washington D.C dola 1,533. Gharama hizo ni kwenda na kurudi.


  Kwa abiria wanaotaka kusafiri kutoka Dar es Salaam kwa daraja la wafanyabiashara kwenda na kurudi katika miji ya Marekani, gaharama ya tiketi ni kama ifuatavyo. Kwenda Boston dola 5,170, Dallas Fort Worth dola 5,810, Houston dola 5,810.


  Kwenda Los Angeles ni dola 6,540, gharama ya New York ni dola 5,170 huku tiketi ya San Francisco ikiuzwa kuanzia dola 6,540 kwenda Seattle ni dola 6,540 na dola 5,170kwenda Washington D.C.


  Emirates ilianza kusafirisha abiria kila siku kwenda Marekani mwaka 2004 na safari zake ni za moja kutoka Dubai hadi New York JFK. Kwa sasa safari zake zimepanuka na kuifikia miji ya Washington, Houston, Dallas, Seattle, San Francisco, Los Angeles. Huduma za kuelekea Chicago zitazinduliwa Agosti. Wasafiri ni mashuhuda kuwa tuzo ya ubora wa huduma iliyopewa Emirates inadhihirishwa kwa ubora wa huduma na uzoefu kutoka kwa wafanyakazi kutoka nchi 120 mbalimbali.

  Abiria awapo safarini huburudishwa kwa aina tofauti za muziki wa kusikiliza na video. Mteja anaweza pia kuomba muziki autakao kulingana na matakwa yake. Ndege yenye namba EK 725 huondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa kila sikua kuanzia saa 04:50 asubuhi na hutua Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere saa 09:15 mchana. Ndege hiyo huruka kurejea Dubai saa 10:45 jioni na kuwasili saa 05:20 usiku.

  0 0

  TAMPRO inayofuraha kwa heshima na taadhima kukuarifu kufanyika kwa Kungamano la Sita la Kukaribisha Mwezi wa Ramadhan 1435H, Siku ya Jumapili Juni 22, 2014 Katika ukumbi wa Julias Nyerere International Convention Centre (JNICC) – Shaaban Robert Street,Dar es Salaam kuanzia saa 02:30 Asubuhi Mpaka Saa 10:30 Alasiri.

  TAMPRO ni Taasisi ya wanataaluma wa Kiislamu katika fani mbali mbali iliyosajiriwa Mwaka 1997 kwa lengo la kuwaleta pamoja wanataaluma wa kiislamu kulitumikia taifa huku wakiendelea kuimarisha misingi na thamani za matendo bora ya kiislamu.

  Wanachama wake hutokea katika taaluma mbali mbali zikiwemo za Afya, Uchumi, Uhandisi, Elimu, Sheria, Usimamizi wa Biashara pamoja na nyanja mbali mbali za Uongozi na sayansi za jamii.
  Kwa Miaka Sita Mfululizo, TAMPRO imejenga utamaduni wa kuwaalika Waislam Mbali mbali kujumuika pamoja katika Jumapili ya Mwisho ya Mwezi wa Shaaban katika kongamano la kuwaandaa na kukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan “Welcoming Ramadhan Conference” ili kufahamiana, kudumisha udugu, Kuwa Karibu na Wanazuoni wa Kiislam na kuonyesha uwepo wao katika Jamii.
  Katika Kongamano la Mwaka huu “The 6th Welcoming Ramadhan Conference 1434H” Anwani ya Mkutano itakuwa ni “Vijana Wetu, Hazina Yetu” ambapo mambo kadhaa yatajadiliwa ikiwa ni pamoja na Mafanikio na changamoto zinazowakabili Vijana katika jamii.

  1. Sheikh, Mwanasayansi, Profesa Mohammed Badamana kutoka Chuo Kikuu Cha Nairobi atazungumza kuhusu “Changamoto za kuwalea vijana wa kiislam katika dunia ya sasa inayobadilika kwa haraka”
  2. Sheikh Mh. Amir Mussa Kundecha, Kutoka Baraka Kuu la Jumuia na Taasisi za Kiislam ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba atazungumza kuhusu “Qur an Tukufu, Katiba mpya ya nchi yetu na Mustakbali wa Vijana wa Kiislam”
  3. Ndugu Ali Masoud Maarufu Kama Masoud Kipanya atazungumza kuhusu “Vijana, Vyombo vya Habari na Utandawazi”
  Karibu Ujumuike na Waislamu Wanaataluma mbali mbali zaidi ya 600katika kusukuma mbele Uislamu kwa kujuana na kuongeza Mshikamano wa Wanazuoni Wetu Mbali Mbali. Mchango wa ushiriki na Maandalizi ya Kongamano ni TZS 30,000 kwa Mtu na TZS 50,000 kwa Mke na Mume. Mume mwenye Mke Zaidi ya Mmoja atapewa upendeleo Maalum.
  Tuna matumaini makubwa na kupata uwakilishi wako katika shughuli hii pamoja na kuwafikishia taarifa hii wanataaluma wengine watakaoweza kufika na kujumuika Pamoja.

  Kadi za Ushiriki zinapatikana Ofisi za TAMPRO Makao Makuu Magomeni Usalama karibu na Ofisi za Manispaa ya Kinondoni, Dar es salaam au Piga Simu namba hizi ili kuletewa au kuwekewa kadi yako:0688 130828.   0714151532 .   0767 151532
  In sha Allah Mwenyezi Mungu atufikishe salama na atufanyie wepesi kujumuika na kutimiza malengo ya mjumuiko huu.

  Maassalaam

  Mohamed,
  Mwenyekiti, Kamati ya Maandalizi
  +255787670714 or 0767565560.

  0 0
 • 06/06/14--00:40: Article 10

 • 0 0

  Katibu Bodi ya Filamu  Bibi Joyce Fisoo akisoma salamu za rambirambi wakati wa kuuaga mwili wa aliyekua mtayarishaji wa filamu nchini George Otieno Okumu “Tyson” katika viwanja vya Leaders’ Kinondoni. Tyson alifariki mwishoni mwa wiki iliyopita kwa ajali ya gari.  Ndugu zangu nashindwa hata niseme nini kutokana na mfululizo wa misiba ya wanatasnia wenzetu, nashindwa kueleza simanzi kubwa niliyonayo, nakosa la kuongea ninabaki kusema kazi ya Mungu haina makosa katika yeye tumeubwa na yote yanayotokea ni kwa mapenzi yake yeye aliye muumba.

  Bodi ya Filamu nchini inaungana na wadau wote wa filamu pamoja na familia kufuatia kifo cha ghafla cha mwongozaji mahiri wa filamu ndugu yetu George Otieno Okumu (Tyson) kilichotokea kwa ajali ya gari. Ninatambua wakati mgumu ambao familia yake unao, watoto wake, wanatasnia wote na wafanyakazi wenzake wa TV 1.


  Jina George Tyson lipo masikioni mwa watanzania tangu mwanzoni mwa mwaka 2000 na limetambulishwa na umahiri wa kazi alizoziongoza ikiwemo filamu iliyoitwa Girl friend ambayo ilitikisa soko la filamu. Tyson ni miongoni mwa wanatasnia waliotoa mchango mkubwa katika kuinua tasnia ya filamu hapa nchini na katika kuongoza vipindi mbalimbali vya runinga.


  Nyote mnakumbuka kundi la Mambo Hayo ambalo ndugu yetu Tyson alikuwa mmoja wa waasisi wakubwa. Wanatasnia wengi walio mahiri hapa nchini wamebahatika kupata fursa ya kufundishwa na Tyson.

  Tyson ameweza kutambulisha na kukuza vipaji vingi, kimsingi aliwekeza katika kufundisha makundi mbalimbali ya wanatasnia, alikua mahiri na kwa hakika amechangia katika kukua na kuendeleza tasnia ya filamu nchini.


  Ni ukweli usiopingika kuwa msisimko mkubwa miongoni mwa wafanyakazi wa tasnia ya filamu nchini uliongezwa na kazi alizofanya ndugu yetu Tyson. Kuondoka kwake ni pigo kubwa sana kwetu wanatasnia. Daima tutamkumbuka kwa mchango wake, katika kuendeleza juhudi zake nawasihi wanatasnia tuenzi yale yote mema aliyotuachia na tuyaendeleze.


  Narudia kutoa pole nyingi na Mungu atupe subira katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.


  Daima tumkumbuke na kumuenzi.

  MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU GEORGE OTIENO OKUMU (TYSON) MAHALI PEMA PEPONI AMENI.


  0 0

  NDUGU MDAU MICHUZI TV SASA IPO HEWANI. 
  JIUNGE HARAKA UPATE MAMBO MOTOMTO!!
  KWA KUANZIA WADAU WA VODACOM WANAKARIBISHWA KUPIGA
   *149*01#  KISHA CHAGUA NAMBA 4 SIMU.tv (MPYA) 
  HALAFU NENDA  NAMBA 1. Habari (BURE), 
  BAADA YA HAPO 
  CHAGUA NAMBA 5 Michuzi TV (BURE) 
  UNAKUWA UMESHAJISAJILI KWA HUDUMA HII MPYA. 
  LIBENEKE OYE!

older | 1 | .... | 292 | 293 | (Page 294) | 295 | 296 | .... | 1897 | newer