Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 291 | 292 | (Page 293) | 294 | 295 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiwa na Rais mpya wa Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika wakiwa katika picha ya pamoja baada ya rais mpya wa Malawi kukabidhiwa madaraka leo jijini Brantyre kwenye hoteli Sunbird. Baada ya kukutana viongozi hao walipata fursa ya kuzungumzia masuala la kidiplomasia baina ya nchi hizi mbili na kukubaliana kuendelea kuwa na mahusiano mema kama nchi zinazoishi ndugu na jirani. Picha kwa Hisani ya Ikulu ya Malawi

  0 0   Taasisi ya faridas foundation inatarajia kufanya uzinduzi wake rasmi siku ya tar 28/6/2014 siku ya jumamosi katika ukumbi wa crystal hall, blue pearl hotel, ubungo plaza kuanzia saa 6-12 jioni. 

  Katika siku hyo taasisi itatoa misaada mbali mbali kwa walemavu ikiwemo baiskeli za walemavu, vyerehani, vifaa vya shule na vifaa vingine muhimu kwa walemavu ukiwa kama mdau au mtanzania unayeguswa na walemavu na ungependa kuhudhuria siku hyo maalumu kadi zinapatikana kwa mchango wa shilingi laki moja na kuendelea hii ikiambatana na chakula cha mchana vinywaji na burudani mbalimbali pia utakuwa umesaidia kuongeza idadi ya vifaa vitakavyotelewa kwa walemavu mbali mbali. 

  Kutoa ni moyo sio utajiri. Endapo una kampuni au ungependa kushiriki kama kampuni au taasisi kwa kudhamini pia nafasi bado zipo wazi wasiliana nasi kupitia +255715186262 au email faridasfoundation@gmail.com

  0 0

   Hivi ndivyo kituo cha Daladala cha Mwenge kilivyo bomolewa asubuhi ya leo.
   Hiki kilikuwa Choo cha kulipia kilichokuwa Mwenge nacho kikiwa kimebomolewa
   Ulinzi ukiwa umeimarishwa
   Kazi ya Kubomoa na kuondoa vibanda ikiwa inaendelea Mwenge
   Askari wa FFU akiwa anazuia watu wasipite eneo ambalo kulikuwa na kazi ya Bomoa bomoa ikiendelea.


   Mashuhuda wakiwa wanashuhudia ubomoaji ukiendelea
   Hili lilikuwa eneo la kupumzikia zamani la Abiria kungoja usafiri nacho kikiwa kimebomolewa
   Mabaki ya Vibanda
   Mmoja wa Mgambo akiwa amebeba Meza kupeleka eneo husika Tayari kwa kuzikusanya kuzipeleka eneo husika
   Kazi ya Ubebaji Meza na Mabaki ya Vibanda ikiendelea
   Mashuhuda wakiongezeka
   Moja ya eneo ndani ya Mwenge walipo hifadhi baadhi ya Meza za Biashara

   Bomoa Bomoa ikiendelea upande wa Juu Mwenge
   Hapa walikuwa wanabomoa Sehemu zote za vibanda zilivyo zidi mbele
   Mgambo anafanya kazi bila Air Mask wakati kazi inaendelea ya Bomoa bomoa

   Mashuhuda upande wa Juu Mwenge
   Ulinzi ukiwa umeimarishwa kila sehemu
   Hapa ilitaka kutokea Shoti ya Umeme Baada ya gari la kubomoa kupita sehemu ambayo kuna waya wa umeme, TANESCO hawajazima umeme eneo hilo jambo ambalo ni Hatarishi.
  Hali Halisi baada ya eneo hilo kubomolewa

  Picha na Dar es salaam yetu Blog

  0 0


  0 0

   Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Hussen Mwinyi (katikati), akikata utepe kuzindua rasmi kiwanda cha kutengezea vifaa vya ujenzi cha Uturuki STONE BLOCK BUILDING. Jun 2,2014.kilichopo Kawe Mbezi Beach jijini Dar es Salaam (wakwanza kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki,  Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Ali Davutoglu na maofisa wa Uturuki.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki wakijadiliana jambo na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Ali Davutoglu, wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho.
    Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Hussen Mwinyi (kushoto), akijadiliana jambo na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Ali Davutoglu,wengine ni maofisa kutoka Uturuki.
  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Hussen Mwinyi,akiwa na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Ali Davutoglu wakiwa wameambatana maofisa wengine wa Uturuki wakikagua kiwanda hicho.
   Wageni waalikwa wakiangalia burudani.
   Vijana wa kabila la Kimasai wakitoa burudani.
   Deus Kamwela, kutoka kikundi cha sanaa KCC akionyesha umahiri wake wa viongo.
   Wafanyakazi wa kiwanda hicho.


  0 0

  MWIMBAJI wa muziki wa kizazi kipya, Mbwana Mohamed, Mb Dog, amesema mashabiki wake wataanza kuona video ya wimbo wake wa Mbona Umenuna katika vituo vya luninga ndani ya wiki hii.
  Mb Dog, pichani.
  Video hiyo iliyoandaliwa kwa kiwango cha juu iliingizwa katika mitandao ya kijamii, huku kwenye luninga ikianza kusambazwa wiki hii ili kuwapa burudani mashabiki wake.

  Akizungumza leo mchana, Mb Dog alisema kwamba alianza kwanza kuingiza kwenye mitandao ya internet ili kuwapa nafasi watu wote, wakiwamo wan je ya nchi kuitazama video hiyo.

  “Hii ni video nzuri ambayo iliingia kwanza kwenye mtandao na kuwapa fursa watu kuitazama, ambapo natarajia mashabiki wengine wataanza kuangalia luningani wiki hii.

  "Naamini mashabiki wangu wote watapata burudani ya kutosha, ukizingatia kuwa nimefanya video nzuri inayoonyesha umahiri wangu kisanaa,” alisema.

  Mb Dog ni miongoni mwa wasanii wa Bongo Fleva wenye uwezo wa juu wa kutunga na kuimba, ambapo wimbo wake wa kwanza uliomuibua ni Latifa na nyinginezo.


  0 0


  Wananchi wanne kati ya watano wanaamini kuwa mafuta na gesi yatawanufaisha wao, watoto wao na nchi yao kwa ujumla. Wakati huo huo, wananchi wanne kati ya kumi (37%) wanaamini kuwa viongozi wa Serikali na matajiri ndio wataofaidika zaidi. Pia, zaidi ya nusu (55%)  wangependa baadhi ya mapato ya mafuta na gesi wapewe wananchi moja kwa moja kama fedha taslimu.

  Matokeo haya yametolewa na Twaweza katika muhtasari wa utafiti wenye jina la Kusimamia Maliasili: Wananchi wanasemaje? Utafiti huu ulifanywa kwa kushirikiana na Benki ya Dunia na umetokana na takwimu za Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza Afrika kwa njia ya simu ya mkononi wenye uwakilishi wa kitaifa.

  Utafiti unaonesha kwamba matakwa ya wananchi ni kuwa, angalau kiasi cha mapato ya mafuta na gesi kipelekwe moja kwa moja kwa wananchi. Mwananchi mmoja kati ya watano (20%) angependelea kiasi kikubwa cha fedha kipelekwa moja kwa moja kwa wananchi; wakati wananchi asilimia 18 wangependelea kuwe na mgawo sawa wa mapato kati ya serikali na wananchi. Asilimia 17 wangependelea Serikali ipate asilimia kubwa zaidi ya mapato kwa ajili ya kuendeleza miundombinu na huduma za kijamii na wananchi wapewe kiasi kinachobaki.

  Hata hivyo, Watanzania walio wengi (43%)  wangependa mapato yote yaende Serikalini kwa ajili ya kugharamia huduma muhimu. Isitoshe, wananchi walipoulizwa namna wanavyoamini mapato ya rasilimali yanaweza kuleta manufaa kwa Watanzania, nusu yao (46%) walisema mapato yatumike katika kutoa huduma za afya na elimu, na wananchi wanne kati ya kumi (20%) walipendekeza yatumike kwenye miundombinu au kwenye mipango ya kupambana na umaskini (17%).

  Linapokuja suala la usimamizi wa maliasili, jambo la msingi ni kuhakikisha kuwa Tanzania haiangukii kwenye uhanga wa laana ya utajiri wa maliasili. Uzoefu kutoka nchi nyingine unaonyesha kuwepo kwa uwazi kuhusu mapato na mchakato kama kitu muhimu sana katika kuepuka laana hii, pamoja na ushiriki wa wananchi katika kufanya maamuzi yanayohusu namna mapato yanavyosimamiwa.

  Hivi sasa, ingawa Watanzania wengi (64%) wanafahamu ugunduzi wa mafuta na gesi, Utafiti wa Sauti za Wananchi ulibaini kuwa Watanzania wawili kati ya watatu (65%)  wangependa kupata taarifa zaidi. Pindi taarifa zinapokosekana, tetesi na uvumi mara nyingi huziba pengo hilo. Ingawa makadirio ya sasa yanasema kuwa uchimbaji mkubwa wa mafuta na gesi hautaleta faida katika kipindi cha miaka saba hadi kumi ijayo, mwananchi mmoja kati ya watatu (36%) anaamini kuwa makampuni ya mafuta na gesi tayari yameshaanza kupata fedha kutokana na ugunduzi huu. Isitoshe wananchi watatu kati ya kumi (28%) hawana uhakika kama tayari kuna mapato kutoka kwenye mafuta na gesi au la. Aina hii ya mapengo kati ya mitazamo na uhalisia, kama haitaangaliwa vizuri, inaweza kusababisha wananchi kutoridhishwa na usimamizi wa maliasili.

  Mjadala mwingine mkali umekuwa juu ya nafasi ya makampuni ya ndani na ya nje ya nchi katika kuchimba mafuta na gesi. Wafabiashara wengi wamedai kwa msisitizo upendeleo utolewe kwa makampuni ya Tanzania. Nusu ya Watanzania (52%) wangependa kunufaika na utaalamu wa makampuni ya kigeni katika sekta hii, lakini kwa kushirikiana na makampuni ya ndani ambayo yanapaswa kumiliki hisa kubwa zaidi katika ushirikiano wa kibiashara hio. Mwananchi mmoja kati ya watatu (35%) anaamini kuwa makampuni ya ndani yapewe kipaumbele kwenye zabuni za makubaliano. Aidha, Watanzania sita kati ya kumi (61%) wako tayari kuona mafuta na gesi yakiuzwa kimataifa kwenye nchi zote. Hata hivyo, wananchi watatu kati ya kumi (28%) wanafikiri gesi inapaswa kutumika nchini tu, na mwananchi mmoja tu kati ya ishirini (5%) anafikiri mauzo ya gesi yafanyike nchi za Afrika Mashariki pekee.

  Rakesh Rajani, Mkuu wa Twaweza, alisema "Kama tunataka watu wa Tanzania wanufaike na ugunduzi wa gesi, tunahitaji uongozi wa serikali ulio imara, wenye uwazi na ubunifu. Kuwepo kwa mfuko huru wa utajiri wa taifa ni sehemu moja muhimu ya ufumbuzi. Hata hivyo, tunahitaji kufikiria juu ya njia mbadala, kama vile kupeleka fedha moja kwa moja kwa watu. Jambo la msingi zaidi ni kuweka wazi taarifa, kusikiliza maoni ya wananchi na kuwasiliana ili kujenga imani ya wananchi kufahamu namna fedha za gesi inavyotumika."

  0 0   Hatimaye Mtoto Nasra Mvungi aliyefariki Juni mosi mwaka huu kufuatia kuaishi katika matesa makubwa kutoka kwa mama yake mkubwa baada ya mama yake kufariki na kuishi katika boksi bila huduma muhimu anazostahili kupatiwa binadamu hasa mtoto mdogo mwenye umri wa mwaka mmoja amezikwa kwa heshima zote na wakazi wa Morogoro wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Joel Nkaya Bendera, Mbunge wa Morogoro mjini, Abdulaziz Abood na mfanyabiashara wa mabasi na vituo vya mafuta mkoani Morogoro Al Saed Omary. Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, ametaka vyombo vya sheria Mahaka, kutoa hukumu inayowastahili waliohusika kwa mateso na kupelekea kifo cha Nasra.
   Waombolezaji wakiwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, kuaga mwili wa mtoto Nasra Mvungi.

   Mfanyabiashara, Al Saed Omary aliyefanikisha kuleta mwili wa marehemu Nasra kutoka Dar es Salaam.
   Waombolezaji wakiingia katika mabasi ya Abood, kwenda katika maziko.
   Mazishi ya mtoto Nasra yaliendelea makaburi ya Kola mkoani Morogoro.
   Mbunge Abdulaziz Abood akiweka udongo katika kaburi la marehemu Nasra na kuahidi kumfanyia hitma baada ya siku 40 tangu kuzikwa kwake.
  Mfanyabiashara Al Saed Omar nae akiweka udongo katika kaburi la marehemu.

  Picha kwa Hisani ya Father Kidevu Blog

  0 0

   Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania Silas Mwakibinga akiwaonesha waandishi wa habari uthibitisho wa malipo ya shilingi milioni 400 ikiwa ni sehemu ya pili ya malipo kwa ajili ya Ligi Kuu.

   Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Azam Media Rhys Torrington (kulia) akimkabidhi  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania Silas Mwakibinga nakala ya uthibitisho wa malipo ya fedha kwa ajili ya Ligi Kuu ya Vodacom. 
  KAMPUNI ya Azam Media imetangaza kuwa tayari imeshatuma fedha kwa Bodi ya Ligi kwa ajili ya msimu wa ligi wa Vodacom kwa mwaka 2014/ 2015.
  Fedha hizo zimetolewa mapema zaidi kwa ajili ya kusaidia maandalizi mapema kwa timu kama ilivyokubaliwa kwenye mkataba wa miaka mitatu ya udhamini wao katika ligi hiyo.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi za Azam zilizopo Tazara, Dar es salaam, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Rhys Torrington, alisema kuwa kampuni hiyo inavutiwa na aina nzuri ya ushirikiano kati yake na bodi ya Ligi.

  Alisema kuwa kupitia bodi hiyo Azam imepiga hatua kubwa katika kufanikisha adhma yake ya kuifanya Ligi hiyo ya Vodacom kuwa ya kuvutia zaidi.
  “Ligi hii tunataka kuifanya kuwa ni moja kati ya ligi zinazovutia na kuonesha ushindani barani Afrika, ingawaje ninajua kuwa kuna mengi ambayo yanatakiwa kuendelea kufanywa ili kuipa nguvu zaidi ligi hii”alisema Torrington. Alisema kuwa kwa kutambua hilo ndio maana Azam Media imehakikisha kuwa klabu zote zinapata fedha mapema ili kusaidia suala zima la maandalizi.

  Akizungumzia mikakati ya baadae ya Azam Media alisema kuwa inatarajia kuanza kuonesha soka la mitaani (street soccer) mbalimbali moja kwa moja (live) itakayokuwa ikiendelea kwenye nchi za Kenya na Uganda.

  Alisema kuwa kwa sasa Azam Media imeanza kujikita katika nchi za Kenya, Uganda na Malawi ambapo itakuwa ikiuza ving’amuzi vyake katika nchi hizo. Aliongeza kuwa pia katika kuhakikisha kuwa inatoa mwanya zaidi wa vipindi vizuri na vya kuvutia inaendelea na vipindi vya michezo vya Morning Trumpet, sport@8 pamoja na Kwetu House.

  Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya ligi, Mr Silas Mwakibinga alisema kuwa kwa hatua hiyo ya Azam ya kuhakikisha upatikanaji wa fedha hizo kwa wakati ni nzuri na itasaidia kuzipatia timu muda mzuri wa kujiandaa. Alisema kuwa bodi yake inavutiwa sio tu na utangazaji wa vipindi unaofanywa na Azam bali pia hata nia yao ya kuendeleza soka la Tanzania.

  Azam Media ilisaini mkataba wa miaka mitatu na wenye thamani ya TSHS5,560,800,000 kuonesha mechi za live na za kurekodi mechi za Ligi Kuu na fedha hizo zinalipwa kwa awamu tatu.

  0 0

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda  amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi za kwanza katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kuingia kwenye ubia na sekta binafsi katika mradi mkubwa wa usafirishaji abiria.

  Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Juni 3, 2014) wakati akifungua Mkutano wa Majadiliano yenye lengo la kuutangaza mradi wa mabasi yaendayo kasi kwenye ukumbi wa Mlimani City. Mkutano huo wa siku mbili, utamalizika kesho (Jumatano, Juni 4, 2014).

  Waziri Mkuu amesema kutèkelezwa kwa mradi huo kutatoa fursa za ubunifu utakaowezesha kupatikana kwa suluhisho la usafiri mijini na hasa kwenye miji inakua kwa kasi barani Afrika.

  "Mbali ya kutoa huduma za hali ya juu, za haraka na ambazo siyo ghali kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, nia ya Serikali ni kuona mfumo mpya wa matumizi ya kadi kwenye mpango huu wa usafiri unatumika ipasavyo," alisema.

  Alisema ni matumaini ya Serikali kwamba wadau kutoka sekta binafsi ambao ni wazawa na wa kutoka nje ya nchi watashiriki kwenye mradi huu ili uweze kuboresha matumizi ya kadi ambayo mtu hatatakiwa kulipia fedha taslimu akiwa ndani ya basi bali kutumia kadi anayoilipia kabla ya kuingia ndani ya basi husika.

  Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano huo, Waziri Mkuu alisema Serikali iliamua kuanzisha mradi huo ili kupunguza msongamano wa magari kwenye barabara za Jiji la Dar es Salaam.

  "Hii ni awamu ya kwanza ambayo inakaribia kukamilika na inaanzia Kimara hadi Kivukoni na itakuwa na matawi mawili ya Morocco na Karikoo. Mradi wote una awamu sita za ujenzi kuelekea maeneo tofauti ya Jiji," alisema.

  Mbali na mradi huo wa mabasi yaendayo kasi, Serikali inaangalia uwezekano wa kutumia usafiri wa majini kwa kutumia boti kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo kama njia mojawapo ya kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam.

  Vilevile tutaimarisha usafiri wa reli kama njia nyingie ya kupunguza tatizo hili. Dk. Mwakyembe (Waziri wa Uchukuzi) ameanza na sote tumeona ni jambo linalowezekana. Cha msingi ni kuimarisha tu usafiri huu, aliongeza Waziri Mkuu.

  Mapema, akiwakaribisha wajumbe wa mkutano huo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Bibi Hawa Ghasia alisema Serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa mradi huo unafanikiwa.

  Pia alitumia fursa hiyo kuishukuru Benki ya Dunia ambayo alisema imetoa kiasi cha dola za Marekani milioni 200 kwa ajili ya kufadhili mradi huo.

  Mkutano huo unawashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wa ndani na wa nje wanaotarajiwa kutoa huduma za mabasi makubwa na madogo, utoaji tiketi, ulinzi, usafi na huduma za maduka.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 3021,
  DAR ES SALAAM.
  JUMANNE, JUNI 3, 2014.

  0 0
  0 0


   Diwani wa kata ya Mgama Denis Lupala akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mgama wakati alipowatembelea na kula pamoja chakula cha mchana.
   Diwani wa kata ya Mgama Denis Lupala akizungumza na mwalimu mkuu wa shule hiyo Simeone Lihuluku. 
   Diwani wa kata ya Mgama, Denis Lupala akimpakulia chakula mmoja wa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mgama wakati alipowatembelea na kula pamoja chakula cha mchana
  baadhi ya wanafunzi shule ya sekondari ya Mgama wakiwa katika foleni ya chakula kilichoandaliwa na diwani wa kata ya Mgama Denis Lupala.


  Na Denis Mlowe,Iringa

  SHULE ya sekondari Mgama iliyoko katika kata ya Mgama jimbo la Kalenga wilaya ya Iringa Vijijini inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa matundu ya vyoo  30 yaliyopo 12 na miundo mbinu mibovu.
   
  Akizungumza na mwandishi wa habari hizi wakati wa hafla iliyoandaliwa na diwani wa kata hiyo Denis Lupala,Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Simeone Lihuluku alisema kuwa licha ya upungufu wa matundu ya choo shule hiyo inakabiliwa na ukosefu wa maktaba na maabara kwa wanafunzi wanaosoma shuleni hapo tangu kuanzishwa kwake miaka saba iliyopita.
   
  Luhuluku alisema  shule hiyo inakabiliwa na ukosefu wa mabweni ya wanafunzi na nyumba za kuishi walimu kitu kinachochangia wanafunzi kupanga mbali na maeneo ya shule changamoto inayosababisha ufaulu hafifu kutokana na utoro pamoja na upatikanaji wa mimba kwa watoto wa kike.

  Alisema mwaka huu tayari wanafunzi watatu wamekatisha masomo kutokana na kupata ujauzito huku nyumba za walimu zinazohitajika zikiwa 18 na zilizopo kwa sasa ni nyumba mbili za walimu.
   
  “Licha ya upungufu wa matundu ya vyoo vilevile tunakabiliwa na changamoto nyingi sana katika shule hii lakini kubwa zaidi ni ukosefu wa maabara na maktaba kwa ajili ya wanafunzi na tumekuwa tunatumia chumba kimoja cha darasa kama maabara kitu kinachosabisha wanafunzi kutosoma vizuri na kupunguza ufaulu naomba sana wadau waweze kuwasaidia kuondokana na changamoto hizi” alisema Lihuluku
   
  Aliongeza kuwa shule hiyo imekosa huduma ya umeme,vyanzo vya kuaminika vya maji safi na vifaa vya kufundishia pamoja na uchangiaji hafifu wa michango ya shule kwa wazazi.
   
  Kwa upande wao wanafunzi  wa shule hiyo wamemshukuru diwani huyo kwa kuwaandalia chakula huku wakimuomba kuwasaidia kutatua changamoto zinazowakabili katika shule yao kwa lengo la kuongeza ufaulu shuleni hapo.

  Shule ilianzishwa mwaka 2007 ikiwa inatoa elimu ya kidato cha kwanza hadi cha nne ikiwa na jumla ya wanafunzi 516 kati ya hao wavulana wakiwa 221 na wasichana 295 na walimu 20.

  0 0

  Fainali za Kombe la Dunia ni uwanja mpana. Ni mahali ambapo vipaji na vipaji vya wanasoka duniani huonekana. Madalali wa kuvumbua na kununua wachezaji [scouts] hufurika kwenye mashindano kama haya wakijua wazi kabisa kwamba pale ndipo watakapoona “lulu” kwa ajili ya vilabu vyao. Kwa maana hiyo kuna kila aina ya harakati za kimichezo na kuonyesha na kuonyeshana vipaji. Hii sio kumaanisha kwamba wachezaji wote mahiri hapa duniani walicheza katika fainali za Kombe la Dunia.La. Wapo wasakata kabumbu kadhaa ambao hawakuwahi kugusa fainali hizi.Mfano ni George Opong Weah na watu kama kina George West nk.

  Lakini wakati wengine wakionyesha vipaji ili wang’amuliwe na kubadilisha maisha yao ya kisoka,wapo wale ambao wanashuka dimbani tayari wakiwa na majina [superstars] na ambao dunia tayari inakuwa ikiwaangalia kwa makini kutaka kujua na kuona kile watakachokifanya. Kila timu huwa na mchezaji ambaye hutizamwa zaidi. Kwa umombo unaweza kumuita Key Player. Kila timu,kwa kupenda au kutopenda,huwa ina star player. Hii haimanishi kwamba katika timu hakuna wachezaji wengine wenye majina au wanaoweza pia kuwa stars.La. Ni sheria ya mmoja mmoja inayozingatiwa hapa.

  Kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali wa soka,wachezaji hawa 32 [mmoja kutoka katika kila timu inayoshiriki fainali za Kombe la Dunia mwaka huu] ndio watarajiwa kuchomoza zaidi huko Brazil. Mpangilio huu hapa ni kutokana na makundi ya FIFA World Cup 2014. NB: Orodha hii inaweza kubadilika kwani imeandikwa kabla timu zote hazijathibitisha wachezaji wake 23 iliyowachagua mwisho. Wengine wanaweza kuumia katika siku hizi za mwisho na hivyo kutokwenda Brazil.Zingatia.
  168820285RM00031_Brazil_v_ENeymar-Brazil.
  Hakuna ubishi kwamba Neymar anayechezea soka la kulipwa Barcelona nchini Spain ndio gumzo kubwa kwa timu ya Brazil. Anatarajiwa kuongoza mashambulizi ya The Kings Of Samba[Brazil]
  hi-res-160980702-oribe-peralta-of-mexico-shoots-the-ball-against-denmark_crop_exactOribe Peralta-Mexico
  Ingawa wachezaji wengine wa Mexico kama Chicharito na Giovani dos Santos wanatajwa kama ma-star,Oribe Peralta ambaye anacheza katika ligi ya nyumbani katika club ya Santos Laguna, ndiye anaaminika hivi sasa kuwa star zaidi
  croatia_modricLuka Modric-Croatia
  Hakuna shaka kwamba Luka Modric ndiye mchezaji star zaidi hivi sasa katika timu ya Croatia. Kiungo huyu ambaye hivi sasa anachezea timu ya Real Madrid nchini Spain ameonekana wazi kuwa tegemeo sio tu katika club bali nchi yake Croatia.
  Charles+Itandje+Tunisia+v+Cameroon+FIFA+2014+268_zMNMuiklCharles Itandje-Cameroon
  Ingawa ungetegemea mchezaji kama Samuel E’too kuendelea kuwa star na tegemeo zaidi katika timu ya Cameroon, golikipa Charles Itandje ndio tegemeo na ambaye wengi watapenda kumuona akiokoa mikwaji. Charles ambaye anachezea timu ya Konyaspor nchini Uturuki[kwa mkopo kutoka PAOK FC ya Ugiriki] aling’ara vilivyo katika mchezo dhidi ya Tunisia wakati wa kuwania nafasi ya kwenda Brazil.Google utaona alichofanya.
  Diego+Costa+Spain+v+Italy+YIz2iTWGapSlDiego Costa-Spain
  Ingawa bado kuna utata kuhusu hali yake na kama atakuwa fit kabla ya kuanza kwa fainali za Kombe la Dunia huko Brazil,Diego Costa mshambuliaji mahiri wa timu ya Atletico Madrid anatarajiwa kuwa nyota wa Spain. Lakini pia huenda akawa ndiye mchezaji atakayezomewa zaidi huko Brazil kwani Diego ni mzaliwa wa Brazil na angeweza kabisa kuchezea Brazil mwaka huu kama asingeamua kuchezea Spain[pia ni raia wa Spain].Wabrazil hawajaipenda hiyo.
  Arjen_RobbenArjen Robben-Holland[The Netherlands]
  Robben,mshambuliaji mahiri ambaye hivi sasa anaendelea kuwika na timu ya Bayern Munich nchini Ujerumani,ndiye mchezaji ambaye ni star zaidi na ambaye ameonyesha kuwa na kile kiwango kinachoitwa “cha dunia”. Ana miaka 30 hivi sasa.
  HABARI ZAIDI BOFYA LINK HIYO HAPO

  0 0

  Mkuu wa Mkoa Singida Dkt. Parseko V. Kone akizungumza na

  waandishi wa habari juu ya mbio za mwenge wa uhuru Mkoani Singida kulia
  kwake ni katibu Tawala Mkoa wa Singida Liana Hassan.

   Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Singida (wa
  kwanza ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Geofrey Kamwela)

  wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Parseko V. Kone muda mfupi
  kabla ya kuelekea kijiji cha Rungwa tayari kwa kuupokea Mwenge wa Uhuru
  Mkoani Singida.

    Wakimbiza Mwenge Mkoa wa Singida wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa
  wa Singida Dkt. Parseko V. Kone muda mfupi kabla ya kuelekea kijiji cha

  Rungwa tayari kwa kuupokea Mwenge wa Uhuru Mkoani Singida.

  ========  =========
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Parseko V. Kone  amewataka wananchi Mkoani  humo kushirikiana katika kusimamia miradi itakayowekewa mawe ya msingi na Mwenge wa Uhuru  ili thamani halisi ya fedha zitakazotumika iweze kupatikana na miradi hiyo kukamilika kwa wakati.

  Dkt. Kone ametoa wito huo leo asubuhi katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa
  Mkoa wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya mbio za mwenge wa uhuru   kwa mwaka 2014 Mkoani Singida zitakazoanza rasmi kesho asubuhi.

  Amesema Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kupokelewa katika kijiji cha Rungwa  Tarafa ya Itigi Wilaya ya Manyoni ukitokea Mkoani Mbeya na utakimbizwa  katika halmashauri sita za Mkoa wa Singida kisha kukabidhiwa Mkoa wa Dodoma, Wilaya ya Chemba kijiji cha Kinyamshindo tarehe 10 Juni 2014.

  Dkt. Kone ameongeza kuwa Mwenge wa uhuru utazindua, kuweka mawe ya msingi na kutembelea miradi 60 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 5.9 katika sekta za afya, elimu, maji, barabara, kilimo,ufugaji, ushirika,
  misitu na sekta binafsi.

  Aidha amewasihi wananchi kufika katika maeneo ambapo salamu za Mwenge zitatolewa ili kupata na kuuzingatia ujumbe huo. Dkt. Kone ameongeza kuwa moja ya ujumbe wa mwenge ni suala la kukamilisha mchakato wa katiba mpya huku akisisitiza wananchi kutumia haki yao ya kidemokrasia ya kushiriki katika mchakato huo bila ya kuathiri umoja, amani na utulivu wa nchi yetu.

  Amesema mbio za Mwenge wa uhuru kwa mwaka 2014 zimebeba ujumbe usemao  “Katiba ni sheria kuu ya  Nchi” huku kauli mbiu ikiwa ni “Jitokeze kupiga kura ya maoni tupate Katiba Mpya” Pia ujumbe huo utaambatana na kauli za uhamasishaji jamii kupitia ujumbe wa kudumu wa Mwenge kuhusu mapambano dhidi ya Ukimwi yenye kauli mbiu  isemayo “Maambukizi mapya, unyanyapaa na vifo vitokanavyo na Ukimwi sifuri”.

  Mapambano dhidi ya rushwa yatahamasishwa kwa kauli mbiu isemayo “Palipo na rushwa hakuna maendeleo” wakati huohuo kauli mbiu ya mapambano dhidi ya dawa za kulevya itakuwa ni “Furahia afya yako sio dawa za kulevya”.

  0 0

         Pamona na show kuchelewa kuanza na club kufungwa mapema wakazi wa NY.NJ walipata show kali kutoka kwa mkali huyo wa Bongo Flava


           SECURITY WALIFANYA KAZI KUBWA KUWAZUIA WAKINA DADA WASIMPANDIE  pamoja nakazi nzuri ya Security Kinadada waliwezakuvamia Stage


  0 0

  Marehemu Dada, Fides Chale 
  Marehemu Dada, Fides Chale (1940 - 2014)

  TGNP Mtandao tumepata pigo kubwa kwa kumpoteza mwanaharakati na Mwenyekiti wa kwanza wa shirika, aliyefariki Juni 2, 2014 Ubungo Msewe Dar es Salaam. Fides Chale alikuwa ni mwalimu na kiongozi aliyegusa maisha ya wengi hapa Tanzania, Mwanaharakati mtetezi wa haki za wanawake, wasichana na makundi mengine yaliyoko pembezoni. 

   Dada Fides amekuwa mtu wa watu, mcheshi, mwenye upendo, utu, huruma, mpole, mwenye sura ya kutabasamu muda wote hata alipokuwa kwenye hali ya ugonjwa. Tunapoombeleza kumpoteza dada yetu Fides Chale, tunasheherekea maisha yake mchango wake mkubwa jinsi alivyojitolea kwa hali na mali kulilea shirika tangu lilipoanza hadi mauti yalipomfika. 

  Fides Chale alishika uongozi TGNP wakati shirika likiwa changa, kuliwekea misingi imara na endelevu wa kiuongozi, kiutawala, na mfumo mzuri wa kubadilishana uongozi unaoendelea hadi leo. Mipango ya mazishi inaendelea nyumbani Ubungo Msewe. Alhamis 05/06/2014 ibada itafanyika katika Kanisa Katoliki Mt. Petro Osterbay na kufuatiwa na mazishi katika makaburi ya Kinondoni. Imetolewa na; Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, TGNP Mtandao

  0 0

   Rais wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini T.P.B.O Yassin Abdalla 'Ostadhi' kushoto akimkabidhi leseni ya ngumi bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' ambayo anaweza kutumia Dunia nzima kwa ajili ya kutambulika kitaifa na kimataifa ambayo inaweka rekodi mbalimbali za bondia pindi anapocheza mchezo.
  Rais wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini T.P.B.O Yassin Abdalla 'Ostadhi' kushoto akimkabidhi leseni ya ngumi pamoja na kitambulisho na nyaraka mbalimbali za bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kwa ajili ya shughuli zake leseni hiyo inayotumika kitaifa na kimataifa kwa ajili ya kuhifadhia kumbukumbu mbalimbali za michezo aliyo shiriki. hafla ya makabidhiano hayo zimefanyika katika ofisi ya ngumi za kulipwa nchini jana  Picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
  Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto  akiwa na nyaraka mbalimbali alizo kabidhiwa na Rais wa TPBO Yassini Abdallah
  Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto  akiwa na nyaraka mbalimbali alizo kabidhiwa

  Na Mwandishi Wetu

  BONDIA Ibrahimu Class 'King Class Mawe' amekabidhiwa leseni kwa ajili ya ngumi pamoja na kitambulisho na nyaraka mbalimbali za kumtambua kitaifa na kimataifa

  akizungumza wakati wa utoaji wa leseni kwa bondia huyo Rais wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini Yassini Abdalla 'Ostadhi' amesema leseni ni jambo la muhimu sana kuwa nayo bondia kitu ambacho kila bondia anatakiwa kuwa nayo ambapo ndio hinaweka kumbukumbu yako ya mapambano yako yote uliocheza ndani na nje ya nchi kitaifa na kimataifa

  hivyo ni kitu muhimu sana leo hii natoa leseni kwa bondia Class kwa kuwa natambua kazi yake na uwezo wake akiwa katika uringo ambapo itamsaidia kwa ajili ya kazi yake kumbuka hii ni ajira hapa kajiajiri mwenyewe' mtaji wa masikini nui nguvu zake mwenyewe'

  nae bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' alishukuru kwa kusema leseni itamuongezea chachu ya kupigana vizuri zaidi awapo uringoni kwani ngumi ndio mchezo anao upenda na ndio anaucheza hivyo atafanya jitiada ili aweze kufika mbali kupitia mchezo wa ngumi

  bondia huyo anaenolewa na jopo la makocha kutoka kambi ya Ilala likiongozwa na Habibu Kinyogoli 'Masta'  Kondo Nassoro, Sako Mtulya na Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye ana msimamia katika mapambano yake mbalimbali na kumpatia ushauri  wa jinsi gani ya kupigana na watu anaokabiliana nao awapo ulingoni

  0 0


  Na James Festo, Njombe.

  KATIKA kuelekea siku ya maadhisho ya mazingira  ambayo hufanyika june tano ya kila mwaka  huku Halmashauri ya mji wa Njombe ikiwa inaendelea kushika nafasi za juu kwa usafi   wananchi wake wameendelea kuitupia lawama za kushindwa kuzoa takataka  kwenye vizimba hali ambayo inaweza kusababisha  magonjwa ya mlipuko.

  Hali hiyo inakuja kufuatia kusuasua kwa uzoaji taka  katika vizimba vya takataka vikiwemo vilivyopo karibu na maeneo yanayotumika katika uuzaji wa vyakula  kitu ambacho kinaweza kusabisha madhara makubwa kwa wauzaji pamoja na wateja wao

  Mwandishi wa habari hii alitembelea na kujionea  vituo mbalimbali Ndani ya halmashauri ya Mji wa Njombe  hali mbaya ya takataka zilizofurika  nje ya vizimba  licha ya wananchi kuendelea na biashara  likiwemo eneo nyuma ya kituo cha mabasi mjini njombe.

  Wakizungumza na majira baadhi ya wafanyabiashara hao walisema kuwa tangu kusimama  kwa mawakala waliokuwa wakifanya kazi hiyo ya kuzoa takataka kwenye vizimba na Halmashuri kuvaa jukumu hilo  mwenendo umekuwa wa kusuasua na kueleza kushangazwa  kuona wakilipa ushuru kila uchao wakati taka hazizolewi kwa wakati.

   "   sasa hivi michango imesitishwa  ndio maana ya kwenye vizimba taka ni nyingi.... labda kila mwananchi awe anachangia  kila kaya ...tunataka tuchangie..... tukisema tufanye hivi hatufiki ...... wakala ameshindwa kufanya kazi kwa sababu  kipato anachopata halmashauri  ni kidogo "   walisema wafanyabiashara hao.

  Aidha Wafanyabiashara  hao waliiomba halmashuri kutumia  fedha zinazokusanywa katika ushuru wa soko kutumika katika kufanya usafi wa soko hilo na kuwasisitiza watumishi wa sekta hiyo kuacha uzembe wa kukaa ofisini.

  Andove Mgani ni mwenyekiti wa  soko la  wafanyabishara lililopo nyuma ya kituo cha mabasi cha Njombe alisema kuwa tangu Halmashuri ya Mji ianze kusimamia yenyewe  zoezi ya utoaji wa taka hizo imekuwa ikizidiwa na kusababisha  taka kukaa zaidi ya wiki  kitu ambacho ni hatari kwa wananchi  mjini hapa.

  "  ninachojua zamani taka taka na yule wakala alikuwa makini na kazi yake lakini baada ya kusimamiwa na halmashauri  vizimba vya hapa mjini vyote vinakaa na takataka muda wote  kama wafanyabiashara tungekuwa na uwezo wa kuamua  tungemuaomba arudi afanye kazi ya kuzoa takataka"   alisema Bw Ndonya.

  Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Bw. Venance Msungu alikiri kuwepo kwa tatizo hilo la uzoaji wa takataka  alisimama kutokana kiasi cha fedha aliyokuwa akilipwa huku mji wa Njombe ukiendeea kuongezeka kwa uchafu.

  Alisema kuwa katika kipindi cha miezi miwili baada ya wakala huyo Halmashauri hiyo imekuwa ikiendelea na zoezi hilo  huku wakisubiri mwezi julai mwaka huu wa kutangazwa kwa mzabuni ambaye ataanza kufanya kazi hiyo ambaye atakuwa na vifaa vya kutosha tofauti na Halmashauri  ambayo imekuwa ikitumia magari mawili pekee.

  "  hata waandishi wa habari inayostahili watu wanaongea kwamba uchafu bado tatizo jambo linaonyesha kukosa uelewa wa kulinganisha na sehemu zingine  hapa nchini....zabuni zitafunguliwa mwezi huu  wa sita  na inapoanza mwezi julai  tutakuwa na mzabini mwenye vifaa vya kutosha vya kutolea uchafu"   alisema bw Msungu.

  0 0

   Meneja wa Uhusiano Mambo ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania  (TBL), Emma Oriyo (kushoto) akishiriki na viongozi mbalimbali kufanya usafi, Ilala, Dar es Salaam juzi, katika  maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani Dar es Salaa
   Meneja wa Uhusiano Mambo ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania  (TBL), Emma Oriyo (kushoto) akishiriki na viongozi mbalimbali kufanya usafi, Ilala, Dar es Salaam juzi, katika  maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani Dar es Salaam.
   Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa,(wa pili kulia) akishiriki na viongozi mbalimbali  na wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kufanya usafi Ilala, Dar es Salaam, 
  katika  maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani.
   Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (katikati) akikabidhiwa vifaa vya usafi vyenye thamani ya sh.mil. 15 na Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu katika 
  hafla iliyofanyika, Ilala, Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani. Wafanyakazi wa TBL walishiriki kufanya usafi eneo la Karume, Ilala. Kushoto ni Meneja  
  Uhusiano wa TBL, Emma Oriyo.
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (katikati)akikabidhiwa vifaa vya usafi vyenye thamani ya sh.mil. 15 na Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu katika 
  hafla iliyofanyika, Ilala, Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani. Wafanyakazi wa TBL walishiriki kufanya usafi eneo la Karume, Ilala. Kushoto ni Meneja  
  Uhusiano wa TBL, Emma Oriyo.

  0 0

  DSC_0340
  Kamishina Mwandamizi wa Jeshi la Polisi nchini (SACP) Simon Sirro akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya wiki mbili kwa makamanda wa Jeshi hilo nchini, mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na UNDP yana lengo la kuwajengea uwezo makamanda jinsi ya kupambana na viashiria vya uvunjifu wa amani bila kuleta madhara makubwa kwa jamii. Kushoto ni Mtaalamu wa Uchaguzi kutoka UNDP, William Hogan na kulia ni wakufunzi kutoka Uingereza, Adrian Barnes (kulia) na Alan Binks (wa pili kulia).

  Na Mwandishi Wetu, MOblog Tanzania
  JESHI LA POLISI nchini limejisifu kwa kuzingatia weledi na maadili ya kazi yao kwa kuruhusu maandamano mengi kufanyika hapa nchini na ni maandamano machache tu yaliyowahi kupigwa marufuku. MOblog inaripoti.

  Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Dar es Salaam wakati akifungua mafunzo ya wiki mbili kwa maofisa 88 wa Jeshi la Polisi yanayofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Programu ya Maendeleo (UNDP) kupitia mradi wa Uwezeshaji Demokrasia (DEP), Kamishina Mwandamizi wa Jeshi la Polisi nchini (SACP), Simon Sirro amesema mafunzo hayo kwa makamanda ni kusaidia uelewa wao katika kupambana na maandamano au dalili za uvunjifu wa amani bila kuleta madhara makubwa kwa jamii.

  “mafunzo haya kwa makamanda wa Jeshi la Polisi nchini litasaidia kuongeza uelewa kuhusu haki za binadamu na utawala bora ili kudumisha amani na utulivu nyakati za uchaguzi,” amesema Sirro.
  DSC_0310
  Mtaalamu wa Uchaguzi kutoka UNDP, William Hogan akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo kwa makamanda wa Jeshi la Polisi nchini kuhusu mafunzo hayo na muhimu wake katika kudumisha amani na kusaidia uchaguzi kufanyika katika hali ya utulivu na kidemokrasia zaidi.

  Kamanda Sirro amesema kwamba mafunzo hayo yanalenga pia kusaidia uelewa makamanda jinsi ya kushughulika na wavunjifu wa amani kwa kuzingati weledi wa Jeshi la Polisi nchini. Amesema kuelekea katika uchaguzi mkuu mwakani 2015 mafunzo yamekuja wakati mwafaka kwa Jeshi la Polisi kupanua wigo wao katika maswala haya ya utawala bora na haki za binadamu nchini.

  “utafiti unaonyesha kwamba maandamano mengi yamewahi kuruhusiwa na Jeshi la Polisi kuzidi yale yaliyopigwa marufuku kwa hiyo yana ya kwamba jeshi linazuia haki za raia kukusanyika au kuandamana haipo isipokuwa kwa sababu za kiusalama tu,’ aliongeza Kamanda Sirro.

  Kwa upande wake, Mtaalamu wa Uchaguzi, kutoka UNDP, William Hogan amesema kuwa mafunzo hayo yanahusu kumudu kuleta utulivu wa umma na yanaendeshwa katika ukumbi wa maofisa wa Polisi wa Oysterbay na ukumbi wa maofisa w Polisi Zanzibar.
  DSC_0316
  DSC_0325
  Baadhi ya Maafisa wa Kikosi cha kutuliza ghasia nchini (FFU) nchini wakifuatilia hotuba za Kamanda Sirro wakati ufunguzi wa mkutano huo jijini Dar es Salaam. Amesema lengo la mafunzo hayo ni kujenga uwezo wa makamanda wa polisi wa kupanga, kumudu na kuratibu kwa ufanisi hatua za kipolisi za kushughulikia matukio yanayotishia utulivu katika jamii.

  “kupitia program hii ya mfululizo wa kozi nne zitakazodumu kwa majuma mawili kila moja, maofisa 88 ngazi za kati na juu kutoka kila mkoa katika nchini watafunzwa na wakufunzi waandamizi nane kutoka katika Chuo cha Mafunzo ya Polisi cha Uingereza,” amesema Hogan
  DSC_0317
  DSC_0361
  Mgeni Rasmi Kamishina Mwandamizi wa Jeshi la Polisi nchini (SACP), Simon Sirro aliyemwakilisha Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo.
  DSC_0355
  SACP Simon Sirro akiteta jambo na Mtaalamu wa Uchaguzi kutoka, UNDP, William Hogan baada ya picha ya pamoja.

older | 1 | .... | 291 | 292 | (Page 293) | 294 | 295 | .... | 1897 | newer