Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 290 | 291 | (Page 292) | 293 | 294 | .... | 1897 | newer

  0 0

  MAREHEMU MAREHEMU NI MAURICE NOEL SINGANO

  Bibi Maria Singano wa Sahare Tanga anasikitika kutangaza kifo cha mume wake mpendwa Lt Col (Rtd)Maurice Noel Singano kilichotokea  Chennai India tarehe 31/05/2014.

  Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa mtoto wake Mikocheni B,Dar es salaam.

  Kutakuwa na Misa siku ya Alhamisi kanisa la Mt. Martha Mikocheni Dar es salaam.Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa tarehe 6/6/2014 Tanga.


  BLOG HII INATOA SALAM ZA POLE KWA FAMILIA NZIMA, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI WOTE 

  ...BWANA AMETOA NA BWANA AMETWA JINA LA BWANA LIBARIKIWE  

  0 0

  H.E. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a congratulatory message to H.E. Peter Mutharika President of the Republic of Malawi. 

   The message reads as follows;

  “H.E. Peter Mutharika,

   President of the Republic of Malawi,

   Lilongwe,

           MALAWI.


             Your Excellency,
  I have received with great pleasure, the news of your election as the new President of the Republic of Malawi following the general elections held on 20th May 2014. I would like, on behalf of the People and Government of the United Republic of Tanzania and on my own behalf, to extend to Your Excellency, our sincere congratulations on your impressive victory and that of your Party, the Democratic Progressive Party. 

   Your victory in these heavily contested elections is a clear testimony of the trust and confidence that the people of Malawi have bestowed on you and your exemplary leadership.

   I wish you every success as you take up the responsibilities and challenges of the leadership of your great nation. It is my hope that during your tenure of office, the people of Malawi will enjoy greater prosperity and development. It is equally my hope that under your able leadership, the excellent bilateral relations existing between our countries and their people will be strengthened further and taken to even higher heights.

  I look forward to working closely with Your Excellency not only in fostering our bilateral relations but also to concert our efforts in the cause for peace and stability in our region and the African Continent as a whole. 

   Please accept, Your Excellency, my best wishes for your personal good health and peace and prosperity for the people of Malawi. 

   Dr. Jakaya Mrisho Kikwete
  PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

   ISSUED BY THE MINISTRY OF FOREIGN 
  AFFAIRS AND INTERNATIONAL COOPERATION, DAR ES SALAAM. 

  31STMAY, 2014.


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akifungua rasmi Mkutano wa wadau wa Huduma ya Afya ya Msingi (PHC - Primary Health Care) kwa Wananchi Mkoani Rukwa tarehe 30 Mei 2014 katika ukumbi wa RDC mjini Sumbawanga. Katika kikao hicho mambo mbalimbali ya msingi kuhusu afya ya jamii yalijadiliwa na kuwekewa mpango kazi wa utekelezaji katika kuimarisha afya ya jamii Mkoani Rukwa. Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni pamoja na mkakati wa kupunguza vifo vya mama wajawazito, maendeleo ya shughuli za usafi wa mazingira, utekelezaji wa shughuli za chanjo ya magonjwa mbalimbali, utaratibu wa utoaji wa PF 3, hali ya homa ya Dengu na lishe. 

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Manyanya akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo. Katika salam zake za ufunguzi alisisitiza juu ya usafi wa mazingira ambao ndio kinga kuu ya magonjwa mbalimbali yakiwemo ya kuambukiza kama Dengu na magonjwa ya mlipuko. Aliupongeza mpango wa Sumbawanga Nga'ara ambao kwa kiwango kikubwa umeleta mabadiliko ya usafi katika mji wa Sumbawanga tofauti na siku za nyuma. Aliipongeza pia Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kwa hatua waliyofikia wa kuagiza magari mawili ya kubebea taka yatakasaidia katika kuimarisha mpango huo wa usafi katika Manispaa ya Sumbwanga na Mkoa wa Rukwa kwa ujumla.
  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha akiwasilisha mada ya hali ya huduma ya afya ya mama, baba na mtoto Mkoani Rukwa katika mkutano huo.
  Mwanasheria Mfawaidhi wa Serikali Mkoa wa Rukwa Msomi Prosper Rwegerera akiwasilisha mada ya utaratibu wa utoaji wa PF 3 kwa mtu alijeruhiwa. Alisema PF 3 ni muhimu katika ushahidi wa kimahakama pale mtu atakapokuwa anadai haki yake mahakamani kutokana na jeraha aliliopata na pia inakuwa ni kithibitisho cha kisheria kwa kilichotokea kwa majeruhi husika. Katikati ni Afsa Afya wa Mkoa wa Rukwa Ndugu Kenedy Kyauke.
  Sehemu ya wadau wa Mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa kwa umahiri mkubwa.
  Sehemu ya wadau wa mkutano huo.
  Sehemu ya wadau wa mkutano huo ulioshirikisha wajumbe mbalimbali kutoka katika sekta ya afya, asasi za kidini, viongozi wa Serikali na vyama vya siasa, watumishi wa Serikali na Sekta binafsi na wadau wengine waalikwa.- Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com

  0 0


  Shirika la  Hifadhi ya Jamii (NSSF), limeendesha  kambi za upimaji wa Afya Bure kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa kwa kipindi cha mwezi mmoja.

  Lengo la kambi hizi ni kuweza kutoa elimu na  kuwahamasisha wanachama wa NSSF na wananchi kwa ujumla waweze kujenga  tabia ya kupima afya zao mara kwa mara na kujiwekea mfumo bora wa maisha ili kuepukana na magonjwa sugu yasiyoambukiza.


  Zoezi hili litaanzia mkoa wa Mara, Manispaa ya Musoma  kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Mkendo, kuanzia tarehe 28/05/2014,  kwa siku tatu mfululizo, kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi na moja Jioni.  Baadae, Kambi hizi zitaendelea katika mikoa ya Shinyanga , Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Geita na  Mkoa wa Kagera.


  HUDUMA ZITAKAZOTOLEWA

  Huduma mbalimbali zitatolewa bure kwenye kambi hizi zikiwemo;


  Upimaji wa Shinikizo la damu
  Upimaji wa sukari kwenye damu- Kisukari

  Upimaji wa hali ya lishe (Uwiano wa Urefu kwa Unene)

  Utoaji wa dawa za Minyoo Ushauri wa kitaalam kwa watakaokutwa na Matatizo Ushauri nasaha  na upimaji hiari wa VVU (UKIMWI) Kutoa vipeperushi vya Maelezo ya uboreshaji wa Afya.

  Huduma  zote hizi zitatolewa na NSSF, BURE.


  NSSF inaendelea kuwasii na kuwahimiza wakazi wa kanda ya ziwa kuwa waendelee kujiandikisha kwenye NSSF HIARI Scheme. NSSF HIARI Scheme ni kwa ajili ya wajasiriamali wadogo, wachimbaji wadogo, Ushirika wa Bodaboda , Ushirika wa Wakulima pamoja na wanachama wa Mifuko mingine ya hifadhi ya jamii.


  Jiunge na NSSF HIARI Scheme ili uweze kujipatia mafao bora ya NSSF yakiwemo Bima ya Afya BURE kwa familia nzima (SHIB), mikopo nafuu ya SACCOS,  pamoja na Mafao bora mengineyo.


  Wananchi wa kanda ya ziwa wanakumbushwa na kuhimizwa kujitokeza kwa wingi ili kupimwa na kupewa ushauri wa afya zao Bure.

  NSSF INAJENGA MAISHA YAKO YA SASA NA YA BAADAE.
   Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Jackson Msome ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa Kambi ya Upimaji Afya Bure Mkoani Mara akifafanua jambo mara baada ya kutembelea banda NSSF ambapo zoezi la upimaji afya lilikuwa likiendeshwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF). Watu 1080 walipima maambukizi ya  virusi vya ukimwi na watu 2020 walipima magonjwa ya kawaida. Kulia ni Meneja wa Mafao ya Matibabu NSSF, Ali Mtulia.
  Wakazi wa Mkoa wa Mara wakisubiri kumuona daktari kupata ushauri.
   Daktari wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Lucy Simbila (kulia), akimpima shinikizo la damu mmoja  ya  watu waliojitokeza  kupima afya mkoani Mara juzi, katika kambi ya Upimaji Afya Bure inayoendeshwa na NSSF katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. 
   Wakazi wa Mkoa wa mara wakiwa kwenye foleni ya kuelekea kwenye vipimo wakati wa zoezi hilo.
   Wakazi wa Mkoa wa mara wakiwa kwenye foleni ya kuelekea kwenye vipimo wakati wa zoezi hilo.
   Baadhi ya watu waliojitokeza katika zoezi hilo wakiwa kwenye foleni kuelekea kwenye vipimo wakati wa zoezi hilo.
   Madaktari wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), wakimpa ushauri mmoja wa watu waliofika kupima afya.
  Madaktari na Maofisa wa NSSF walioendesha kambi ya upimaji wa afya mkoani mara wakiwa katika picha ya pamoja.

  0 0

  NGOMA AFRICA BAND AKA FFU KUTUMBUIZA SIKU YA CAMEROON CHALLENGE ,DORTMUND UJERUMANI SIKU YA JUMAMOSI 7.JUNI 2014

  WAKAMERUNI ZAIDI YA 20,000 USO KWA USO NA FFU-UGHAIBUNI !

  Dortmund,Ujeruni,

  Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka "FFU-Ughaibuni, 
  ukipenda waite viumbe wa ajabu "Anunnaki" au " watoto wa mb..wa" yenye makao kule 
  ujerumani, bendi hiyo inatarajiwa kutumbuiza katika siku maalumu ya taifa ya kameruni, 
  katika onyesho la "Cameroon Challenge" siku ya jumamosi kuanzia saa 11 jioni, mjini 
  Dortumund,Ujerumani.

  Ngoma Africa band imealikwa na umoja wa wakameruni ughaibuni,ambao ndio wandaaji 
  wa onyesho hilo la wazi, wakameruni takribani 20,000 waishio ujerumani watachanganyikana wadau wa mataifa mengine kusakata muziki wa Ngoma Africa band,muziki ambao 
  wapenzi wa bendi hiyo wanaufananisha sawa na gwaride la FFU.
  wasilike FFU Ughaibuni at www.ngoma-africa.com au http://www.ngoma-africa.com

  0 0


  Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe, (Wakwanza kushoto), baba yake mzazi Zuberi Kabwe (Wakwanza kulia) na waombolezaji wengine, wakiomba dua kwenye msikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es Salaam huku picha ya chini, waombolezaji wakiingiza jeneza lenye mwilki za Saida Salum, mama mzazi wa Zitto, Jumapili Juni 1, 2014. Mama yake Zitto, alifariki mapema saa 5 asubuhi, akiwa na umri wa miaka 64, kwenye hospitali ya AMI, Msasani jijini Dar es Salaam, alikokuwa akipatiwa matibabu ya kansa ya kizazi.

  Kwa mujibu wa Zitto, Saida ambaye hadi umauti unamkuta, alikuwa mwenyekiti wa Chama cah Walemavu nchini, mjumbe wa bunge maalum la katiba na mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA, atazikwa Jumatatu Juni 2, huko Mwanga-Kisangani baada ya sala ya mchana (Adhuhuri). Ameacha mume, na watoto 10, wanaume 6 na wakike wanne. alisema Zitto.
  Picha zote kwa hisani ya Khalfan Said  0 0

  Zitto kabwe akiwa na Prof  Ibrahimu Lipumba wakati wa kuuaga Mwili wa mama yake kipenzi Bi Shida Salumu aliyefariki leo kabla ya kusafirishwa kwenda Kigoma kwa mazishi.
  Ndege Ikiandaliwa Ili kuweza Kuingiza Mwili wa Marehemu Mama yake Zitto Kabwe
  Waheshimiwa Wabunge na Baadhi ya Viongozi wakibeba Jeneza lililobeba Mwili wa Marehemu Mama Yake Zitto Kabwe Bi Shida Salum  kuingiza kwenye ndege Tayari kwa safari ya kwenda Kigoma Kwenye mazishi
  Prof Ibrahimu Lipumba akijadili jambo na Mwezie baada ya kupakia mwili wa marehemu kwenye ndege kuelekea kigoma Kwenye maziko


  Rais wa TASWA Juma Pinto akiwa VIP ya Terminal 1 JKN Airport alipokutana na Cardinal Pengo wakati wa kuaga mwili wa Mama yake Zitto Kabwe

  0 0

  Wananchi wa Kijiji cha Kitwai A wakiwa wamenyoosha mikono juu,kwenye mkutano wa hadhara,wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akimuunga mkono jambo Mbunge wa jimbo la Simanjiro,Mh Christopher Ole Sendeka,katika suala zima la Utekelezaji wa Ilani ya CCM .
  Baadhi ya Wanahabari pichani kati Kulia ni Mwinshehe kutoka gazeti la Jamboleo na Mary kutoka Gazeti la Nipashe wakiwa sambamba na wafuasi wa chama cha CCM,wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kitwai A,wilayani Simanjiro mkoani Manyara
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua gari la mradi wa Kukodisha la Kikunndi cha Vicoba Mkombozi chenye wanachama wapatao 30,mjini Orkesument,Wilayani Simanjiro mkoani Manayara.

  Kinana ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,wako moani Manyara kwa ziara ya siku saba ya Kukagua kuhimiza na kusukuma miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Chama,kukagua maandalizi ya uchaguzi ya serikali za mitaa,kusikiliza kero za wananchi na kuzitafututia ufumbuzi.

  Mbunge wa jimbo la Simanjiro,Mh Christopher Ole Sendeka,akiwahutubia baadhi ya  Wananchi wa Kijiji cha Kitwai A,akiwa ameambatana na msafar wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,Katika kijiji hicho Ndugu Kinana alizindua Ofisi ya Mtendaji Kata ya CCM Kitwai A,na kuahidi kujenga shule ya Sekondari kwa ajili wananchi hao ambao hapo awali walikuwa na shule za msingi tu.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo mafupi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Simanjiro,Mh.Ole Sendeka wakati akiangalia josho la ng'ombe la Orkirung'rung ambapo  kuna mradi wa ufugaji wa ng'ombe chotara ambao ni ufugaji wenye tija na unasaidia sana kuongeza thamani mifugo.
  Mbunge wa Jimbo la Simanjiro,Mh.Ole Sendeka akifafanua jambo Kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (hayupo pichani),kuhuasiana na Mradi huo wa ufugaji wa ng'ombe wa kisasa (Nyama na Maziwa),wakati akiangalia josho la ng'ombe la Orkirung'rung ambapo  kuna mradi wa ufugaji wa ng'ombe chotara,ufugaji wenye tija na unaosaidia kuongeza thamani mifugo.
  Pichani mbele ye bango kulia ni jengo la Mama na Mtoto la kituo cha Afya Orkesument,Wilayani Simanjiro,ambalo pia Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alikagua.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akimsikiliza Dkt.Juma Nahonyo wakati wa ukaguzi wa jengo litakalokuwa bohari ya Dawa katika kituo cha Afya cha Orkesument,kulia ni Mbunge wa jimbo la Simanjiro,Mh Christopher Ole Sendeka 
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua mradi wa Kikundi cha Mazingira kilichopo mjini Orkesument,Wilayani Simanjiro mkoani Manayara.Kikundi hicho kitatumika kueleimisha wananchi wa mji huo katika masuala ya usafi na kulinda mazingira,kuwaelimisha wananchi kuhusiana na mambo ya maambukizi ya UKIMWI,masuala ya Rushwa na mengineyo. 
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia Wananchi wa Orkesument kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mjini humo wilayani Simanjiro,Kinana aliwaeleza wananchi hao kuwa ahadi za Rais zilizoahidiwa 2010 zitatekelezwa kwa zilivyoahidiwa kwa wananchi wa Simanjiro,pia aliwasisitizia wananchi hao kutochagua viongozi wa vijiji wa hovyo ambao mwisho wa siku ndio wanaoleta mikorogo na migongano kwa wananchi kwa kuuza ardhi,hali inayoleta migogolo isiyokwisha kila siku.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana wakielekea kukagua jengo la Ofisi ya Mtendaji Kata ya CCM Kitwai A,wilayani Simanjiro
   Mbunge wa jimbo la Simanjiro,Mh Christopher Ole Sendeka akitetea jambo na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye katika kijiji cha Kitwai A,Simanjiro mkoani Manyara.
  Mdau akifuatilia jambo
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipokelewa na Mwenyekiti wa CCM,wilayani ya Simanjiro,Ndugu Brown Ole Suya pamoja na  Mbunge wa jimbo la Simanjiro,Mh Christopher Ole Sendeka .
  Jengo la Ofisi ya Mtendaji Kata ya CCM Kitwai A,wilayani Simanjiro lililozinduliwa na Katibu Mkuu wa CCM,Ndug Kinana

  0 0

  Flashback: Hayati Baba wa Taifa enzi za uhai wake akiingia katika kanisa la Mtakatifu Peter la Oysterbay jijini Dar es salaam. Alifanya hivyo kila siku asubuhi

   Baadhi ya Watanzania wakati Rais wa Uganda, Mhe Yoweri Kaguta Museveni akiwatubia mamia ya wananchi waliohudhuria misa ya kuombea mchakato wa kumfanya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kutangazwa Mwenyeheri na hatimaye mtakatifu
   Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akiwatubia mamia ya wananchi waliohudhuria misa ya kuombea mchakato wa kumfanya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kutangazwa Mwenyeheri na hatimaye mtakatifu
   Baadhi ya watu waliohudhuria walikwenda kumpa mkono Mama Maria Nyerere
  Flashback: January 21, 2006 - Bodi ya Dayosisi ya iliyoundwa kuanza mchakato wa mwalimu Nyerere kutangazwa Mwenyeheri na hatimaye mtakatifu.
  ========  ======  =======

  Na Paul Mallimbo, Kampala, Uganda
  Rais Yoweri Museveni, amesema kiongozi bora ni yule anayefuata maagizo ya Mungu na kuwatumikia binadamu wote kwa usawa na haki. Rais Museveni aliyasema hayo (Juni mosi) wakati ibada ya kuombea mchakato wa kumfanya Marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kuwa mwenyeheri na hatimaye kutangazwa mtakatifu. 

  Alisema hata kwenye maandiko matakatifu ya Biblia kuna mistari inayomtaka binadamu ampende binadamu mwenzake kama anavyojipenda yeye;“Kwenye biblia kuna sehemu inauliza kuwa utampendaje Mungu ambaye hujawahi kumuona, na ushindwe kumpenda binadamu mwenzako,” Alisema kwa sababu aliwahi kufanya kazi na mwalimu, anaweza kutoa ushahidi kwamba mwalimu alifanya yote mawili, kumtii Mungu na kuwatumikia binadamu. 

  Alisema mojawapo ya sababu iliyomfanya Marehemu Papa Paulo II kutangazwa mtakatifu kuisaidia Ulaya Mashariki, ambayo wananchi wake walikuwa hawamwamini Mungu. “Marehemu Papa Paulo II alisaidia kuikomboa Ulaya Mashariki kutoka kwenye ukomunisti, wananchi walikuwa hawaamini kuna mungu, lakini kwa juhudi zake aliwafanya wamwamini na kumpenda Mungu,”alisema. 

  Rais Museveni alisema anatarajia kupeleka ushahidi kwa Papa Benedict kwamba Mwalimu anasifa za kutangazwa kuwa mtakatifu kwa sababu alimtii Mungu na kuwatumikia binadamu. “Mimi nitapeleka ushahidi kwa Papa, kwamba mbali na mwalimu kumtii Mungu na kuwpenda binadamu wote, pia aliwakomboa Waafrika kutoka Ruvuma mpaka Capetown, huu ni ukweli siyo hadithi,alisisitiza Rais Museveni. 

  Kufuatia hatua hiyo ya kwenda Roma kutoa ushahidi, Rais Museveni amesema katika maadhimisho ya kuombea mchakato wa Mwalimu kuwa Mtakatifu yatakayofanyika mwakani, ameahidi kuwaita maraisi wote waliowahi kufanya kazi na Mwalimu Nyerere ili kuuthibitishia ulimwengu kuwa Marehemu Baba wa Taifa ameweza kuwaunganisha Waafrika. 
  Alifafanua kuwa Mwalimu ametoa mchango mkubwa wa ukombozi kwa nchi za Msumbiji, Zambia, Zimbabwe, Namibia, Angola, Afrika Kusini, Uganda na Tanzania yenyewe. Hivyo kuja kwa viongozi hao kushiriki ibada hii itakuwa Baraka kubwa. 

   Rais Museveni ambaye alitumia muda mwingi wa hotuba yake kuzungumza Kiswahili, alisema baada ya jitihada za mwalimu kuikomboa Uganda, ndipo na wao walipoweza kuzisaidia nchi za Rwanda, Sudan Kusini na Congo kujikomboa na kuongeza kuwa kama si juhudi za mwalimu wasingekuwa na uwezo wa kuwasaidia wengine. 

  Aidha Rais huyo wa Uganda ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1986, alisema kuwa, kwa upande wa viongozi weusi, hakuna kiongozi ambaye ametoa mchango mkubwa kama Marehemu Mwalimu Nyerere. 
  “Hapa Duniani sidhani kama kuna mtu mweusi mwingine ambaye ametoa mchango kama mwalimu, na hili nimelishudia mwenyewe sikuambiwa na mtu, aliongeza kuwa, hata mzee wetu Nelson Mandela alifanya kazi kubwa Afrika ya Kusini lakini Mwalimu alifanya kazi kubwa zaidi ya ukombozi wa Afrika, Alisema. 

  Alisema Mwalimu aliikomboa Tanzania na kuwafundisha dini ya Kristu, kwa vitendo siyo kwa maneno. Aliongeza kuwa nchi nyingine za Afrika zimepatwa na machafuko ya ukabila na dini kutokana na msingi mbaya wa viongozi waliotangulia.  “Tanzania ni nchi ya Wakristo, Waislamu na wale wengine wanaoamini dini za kienyeji lakini mwalimu aliwafundisha Watanzania fikra za kizalendo za umoja,alisema . 

  Alisema Uganda haikupata elimu nzuri juu ya jambo hilo, viongozi wa kwanza wa taifa hilo waliwapandikiza wananchi chuki, kwamba dini ni kumchukia mwenzako, waumini wa dini moja kuwachukkia waumini ya dini dini nyingine na matokeo yake ni umwagaji wa damu.

   “Biblia inasema kile unachopanda ndicho unachovuna, kwa hiyo sisi hapa tulipanda mbegu mbaya na tukavuna umwagaji wa damu,” alisema na kuongeza kuwa Tanzania haijawahi kuona umwagaji mkubwa wa damu zaidi ya ajali za magari na ile ya kipindi kile wakati askari wa Tanzania walipokwenda Uganda kupigana na Idd Amin.
  Nadhani hii ndiyo damu pekee mmeona,” alisema.
   Alisema baadhi ya waasisi wa Uganda waliwafundisha kuwa wakristu kuwachukia Waislamu, matokeo yake nchi imekuwa katika umwagaji wa damu tangu ilipopata uhuru. Aliongeza kuwa mpaka 1986 wakati anaingia madarakani raia 800,000 wa Uganda walikuwa wamekufa kutokana na chuki za udini na ukabila. 

  “Uganda imeshuhudia umwagaji mkubwa sana wa damu, Congo wameona damu, Sudan, Somalia, Kenya, Rwanda na Burundi ni Tanzania pekee ambayo imekuwa kama kisiwa cha amani, hii yote ni kutokana na mchango wa mwalimu Nyerere ambaye alidumisha amani, umoja na maendeleo kwa watu wake.

   Alisisitiza kuwa, kwa sababu mojawapo ya sababu ya kumfanya mtu awe mtakatifu ni watu kutoa ushahidi wa matukio mbali mbali yaliyofanywa na mtu huyo wakati wa uhai wake, aliahidi kwenda Roma kutoa ushahidi kuhusu matendo ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. 

  “Nikienda kwa Baba Mtakatifu, Papa Benedict nitatoa ushahidi mzuri juu ya  marehemu Mwalimu Nyerere tena nitatoa kwa maandishi siyo kwa maneno pekee yake”alisisitiza. 

  Ibada ya kumuombea Baba wa Taifa ilifanyika katika Kanisa la Mashahidi wa Uganda, Namugongo, ambapo ibada hiyo iliendeshwa na Askofu Mkuu wa Jimbo la Kampala, Dk. Cyprian Kizito Lwanga, ambaye aliiomba serikali kusaidia kuboresha eneo la kanisa hilo ili liwe na miundombinu ya kisasa zaidi. 
  Hii ni mara ya nane ibada ya kuombea mchakato wa kumfanya baba wa Taifa kuwa Mwenyeheri na hatimye mtakatifu unafanyika katika kanisa hilo nchini Uganda. Mchakato huo ulianza mwaka 2006. 

   Katika ibada hiyo ambayo imehudhuria na maelfu ya Watanzania, pamoja na mataifa mbali mbali duniani, pia ilihudhuriwa na familia ya Marehemu Baba wa Taifa, Waziri Mkuu wa Uganda Amama Mbabazi mawaziri na wabunge kutoka Uganda, ambapo Tanzania iliwakilishwa na Balozi wa Tanzania nchini Uganda.


  0 0

  DSC_0540
  Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa mradi wa mafunzo ya bure kwa waandishi wa habari kwenye maeneo matano, sekta ya uchimbaji, unyanyasaji wa kjinsia, kupamba na biashara ya madawa ya kulevya na kuzuia utumiaji wa madawa ya Kulevya kwa waandishi wa habari na utayarishaji na utengenezaji wa vipindi vya luninga na wanawake watangazaji jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma. kushoto kwake ni Msaidizi wa Mwakilishi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya watu, Dorothy Temu –Usiri na Mkurugenzi wa Mfuko wa vyombo vya habari, Ernest Sungura.(Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).

  Na Damas Makangale, MOblog Tanzania
  WAANDISHI WA HABARI nchini wamehimizwa kushirikiana kwa karibu na Mfuko wa Vyombo vya Habari (TMF) ili kuacha kutegemea zaidi matangazo kwa sababu kuna weka taaluma yao rehani.

  Akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa mradi wa kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari jinsi ya kuripoti mambo ya sekta ya uchimbaji, unyanyasaji wa kijinsia, kupamba na biashara ya madawa ya kulevya na kuzuia utumiaji wa madawa ya Kulevyana watayarishaji wa vipindi vya luninga, Waziri wa kazi na Ajira, Mhe, Gaudensia Kabaka amesema kwamba vyombo vya habari lazima vishirikiane na mfuko huo ili kuwa huru wakati wa kuripoti.

  “kuendelea kutengemea matangazo kutoka kwenye makampuni mbalimbali ili kujiendesha kuna wafanya kutokuwa huru katika uandishi wetu na tasnia ya habari kwa ujumla,” amesema Kabaka.

  Amesema mradi huo wa mafunzo ya bure kwa waandishi ni muhimu kwa taifa kwa sababu tatizo kubwa la ajira hasa kwa vijana na wanawake linachangia kwa kiasi kikubwa vijana wengi kujiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya.
  DSC_0434
  Baadhi ya wadau na wageni waalikwa wakimsikiliza mgeni rasmi hayupo pichani.

  Kabaka aliongeza kuwa mafunzo haya yatakayotolewa kwa ufadhili wa TMF ni muhimu ili kuelimisha jamii madhara ya kuuza na kusambaza dawa za kulevya na matumizi yake yanavyoathiri kizazi na kizazi.
  “kwa sasa nchi yetu ya Tanzania ni moja ya nchi zilizoathirika sana na matumizi ya dawa za kulevya na mbaya zaidi kutumika katika njia ya kusambaza madawa hayo hatari,”

  “kwa mujibu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii tuna jumla ya watu 20,626 walioathirika na dawa za kulevya na kwa sasa wanapatiwa matibabu,” alisisitiza Kabaka. Amesema nchini matumizi ya dawa za kulevya kwa zaidi ni Bangi, Heroin, Mirungi na Cocaine na cha kutisha matumizi haya yanaathiri pia wanafunzi wa sekondari na shule za msingi nchini.
  DSC_0515
  Msaidizi wa Mwakilishi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya watu(UNFPA), Dorothy Temu Usiri akitoa nasaha zake kwenye uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.

  Kwa upande wake, Msaidizi wa Mwakilishi Mkazi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya watu, Dorothy Temu-Usiri amesema kuwa kuongezeka kwa vitendo vya kikatili vya kijinsia na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi vimechochea kushirikiana na TMF kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari hapa nchini.

  “kwa kuanzisha mafunzo haya ya bure kutasaidia waandishi wa habari kuandika kwa kina juu ya madhara ya matumizi ya dawa za kulevya ambazo ndio kichocheo cha ukatili wa kijinsia hasa kwa Wanawake,” amesema Usiri.

  Usiri aliongeza kwamba nchini Tanzania idadi kubwa ya watu wenye nguvu ya kufanya kazi ni vijana kwahiyo ni muhimu jamii ya kimataifa kushirikiana na serikali na taasisi zingine ili kunusuru kundi hili muhimu kwenye nchi.
  DSC_0423
  Mkurugenzi wa TMF nchini, Ernest Sungura akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo wa mafunzo ya bure yanayofadhiliwa na mfuko wake ambapo amesema kwamba malipo madogo kwa wahariri na waandishi wa habari kunadidimiza taaluma ya uandishi wa habari pamoja na swala la kutokubobea katika sekta husika (Specialization).


  DSC_0490
  Wadau watakaoshiriki kwa ukaribu kwenye mradi huo wakitambulishwa kwa mgeni rasmi kutoka kushoto ni Dkt. Pilly Said kutoka kitengo cha madawa ya kulevya hospitali ya Mwananyamala, January Nzisi Mkuu wa Kitengo cha Mtandao Tume ya Kudhibiti Madawa ya kulevya, Geodfrey Nzowa, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi, kitengo cha Kupambana na Madawa ya Kulevya, Bi. Aida Teshe Kaimu Kamishina kutoka Tume ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya (DCC) na Florence Bahati Khambi Afisa Habari kutoka Tume ya Kudhibiti dawa za kulevya.
  DSC_0458
  Wadau mbalimbali na wageni waalikwa wakifuatilia yaliyojiri kwenye uzinduzi wa mradi wa mafunzo ya bure kwa waandishi wa habari kwenye maeneo matano, viwanda, jinsia, madawa ya kulevya, kuzuia madawa ya kulevya kwa waandishi wa habari na utayarishaji na utengenezaji wa vipindi vya luninga na wanawake watangazaji jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.
  DSC_0498
  Afisa Habari kutoka kitengo cha Umoja wa Mataifa cha Habari (UNIC), Stella Vuzo amesema kwamba mradi huo umekuja katika muda mwafaka kwa taifa la Tanzania kwa sababu takwimu za matumizi ya dawa za kulevya zinatisha kwa vijana ni lazima taasisi za ndani na jamii za kimataifa kushirikiana kupambana na janga hili.
  DSC_0405
  Pichani juu na chini ni sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo katika maeneo mbalimbali.
  DSC_0406
  DSC_0410
  DSC_0395
  DSC_0418
  Afisa Habari kutoka kitengo cha Umoja wa Mataifa cha Habari (UNIC), Stella Vuzo (kulia) pamoja na Bw. Phillip Musiba kutoka UNIC.
  DSC_0432
  Afisa mafunzo wa TMF, Bi. Raziah Mwawanga akinakili mambo muhimu yaliyokuwa yakijiri wakati wa uzinduzi huo.
  DSC_0414
  Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA(Mstaafu) Ananilea Nkya (kushoto) na Mwandishi wa Habari Mkongwe Mama Eda Sanga (katikati) ambaye ni miongoni mwa mentors kwenye mradi huo. Kulia Sawiche Wamunza kutoka UNFPA.Kwa matukio zaidi ingia humu

  0 0

   Abiria wakiwa wanashangaa Daladala zinapita Mwenge Bila kusimama
   Daladala zikiwa zinapita bila kusimama sehemu yoyote
   Kituo cha kwenda Tegeta , Kawe na Mbezi kikiwa Kitupu Muda huu
   Kituo cha Mabasi Mwenye Cheupe hakuna hata Daladala hata moja
   Bajaji ndizo zimegeuka kuwa daladala na ni Tsh 1000 tu kwa mtu mmoja mpaka Mwenge
   Eneo ambalo Daladala zilikuwa nyingi sasa hakuna tena mabasi hayo

   Bajaji zikiendelea na Kazi
   Upande wa Mwenge kwenda Morocco Pia hakuna mabasi hayasimami
   Hali ya utulivu Mwenge
   Peupe hakuna Mabasi
   Abiria wakingoja Magari
   Wafanya Biashara Wadogo wadogo wakiwa wanajikusanya kwa ajili ya kujadili jinsi ya kuanza Mgomo na kushinikiza waanze kuweka meza zao pia hawataki ushuru
   Wafanya Biashara wakiwa wanaendelea kukusanyika ili kuandaa Mgomo wao
   Kushoto ni Meza moja ya Biashara ikiwa imeinuliwa ishara ya kuweka Meza na Kuanza Mgomo rasmi na kushinikiza kuwa waanze Biashara zao hapo kama kawaida na kutotaka ushuru wa kulipia pesa nyingi.

  Endelea Kufuatilia hapa... Mpaka tunaondoka eneo la tukio Polisi walikuwa wamesha wasili kwa kuanza Doria  na kuangalia usalama.

  Picha na Dar es salaam yetu blog

  0 0

  Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania ‘Airtel Diva’, Amitin Mbamba (kulia), akikabidhi msaada wa machela za kisasa mbili, ‘wheel chair’ mbili na bidhaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya milioni 5/-, kwa Muuguzi Mkuu wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Mary Haule, kwaajili ya matumizi ya wagongwa katika taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni wanachama wa Airtel Diva.
  Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania ‘Airtel Diva’, Amitin Mbamba (kulia), akikabidhi msaada wa moja kati ya ‘wheel chair’ mbili, machela za kisasa mbili na bidhaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya milioni 5/-, kwa Muuguzi Mkuu wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Mary Haule, kwaajili ya matumizi ya wagongwa katika taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni wanachama wa Airtel Diva.
  Muuguzi Mkuu wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Mary Haule (kulia) akiwaongoza wanachama wa kikundi cha wafanyakazi wanawake wa Airtel Tanzania ‘Airtel Diva’, wakati walipotembelea wagonjwa wa taasisi hiyo, baada ya kukabidhi msaada wa machela za kisasa mbili, ‘wheel chair’ mbili na bidhaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya milioni 5/-, kwaajili ya matumizi ya wagongwa katika taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Wanachama wa kikundi cha wafanyakazi wanawake wa Airtel Tanzania ‘Airtel Diva’, wakiwa wamebeba bidhaa mbalimbali, walipotembelea wagonjwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) na kukabidhi msaada wa machela za kisasa mbili, wheel chair mbili vyenye thamani ya zaidi ya milioni 5/-, kwaajili ya matumizi ya wagongwa katika taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.


  0 0

  Gari ambalo atakabidhiwa mshindi wa shindano kubwa nala kipekee linalosubiriwa kwa hamu na wakazi wa mkoa wa Tanga, Nice & Lovely Miss Tanga 2014 tayari limepelekwa mkoani humo na sasa lipo katika maegesho ya magari katika hotel ya Mkonge.

  Mkurugenzi wa kampuni ya Mac D Promotion ambao ndio waandaaji wa shindano hilo, Irene Rweyunga amesema mwaka huu wampaniakuhakikisha wanapata washiriki wenye sifa na viwango lengo likiwa ni kuhakikisha mshindi anakuja kutwaa taji la Redds Miss Tanzania mwaka huu. 

  Irene amesema mwish wa kuchukua na kurudisha fomu za kuhiriki shindano hilo ni jumampili hii ya tarehe 08 June 2014, na kambi rasmi itaanza jumatatu ya tarehe 09 June 2014 katika hotel ya Tanga Beach Resort.

  Shindano la Nice & Lovely Miss Tanga litafanyika June 21' 2014 katika Hotel ya Mkonge. Wadamini waliodhamini shindano hili ni Nice & Lovely, Eatv, Redds, Breeze Fm, Tanga Beach Resort, Mwambao Fm na Rweyunga Blog

  0 0

   
   MWANAMITINDO wa kimataifa wa hapa nchini na Miss Tanzania 2001 anaefanya kazi yake hiyo nchini Marekani Millen Magese ameiomba serikali kumpatia eneo ambalo atalitumia kujenga hospitali maalum ya kushugulikia afya ya wanawake.

  Millen alitoa ombi hilo jana wakati akizungumza na watu mbalimbali waliohudhuria semina ya bure kuhusiana na hali ya Endometriosis inayowakabili wanawake wengi hapa nchini na Afrika kwa ujumla. Millen anakabiliwa na tatizo hilo la Endometriosis ambalo ni hali ya mwanamke kushindwa kupata siku zake za mwezi katika hali ya kawaida na yenye kuleta madhara kwa afya yake hususan kwenye uzazi.

  Millen alisema kuwa akiwa kama mwanamke maarufu na mwenye ushawishi katika jamii yake ameamua kutoa elimu ya tatizo hilo ili kusaidia kuongeza uwelewa wa suala hilo ili kuwasaidia wanawake wengine. 


  Alisema kuwa kwa kuwa suala hilo linahusiana na afya hivyo linahitaji msaada wa ukaribu zaidi kutoka kwa wataalamu wa afya kwa ajili ya kusaidia wasichana na wanawake wenye matatizo mengine ya kiafya pia. Alisema kuwa mwanamke anaekabiliwa na tatizo kama hilo anafikia wakati anakuwa akitakiwa kufanyiwa upasuaji na lakini kutokana na ugeni wa tatizo husika kwa hapa nchini hakuna vifaa vya kutambua na kufanyia upasuaji huo. Ambapo mpaka sasa ni KCMC pekee ndio wana kifaa cha kuweza kutambua tatizo hilo.

  Alisema kuwa ameshaanza kupata misaada kutoka kwa watu mbalimbali wa Marekani kama vile taasisi ya Swan Development LLC, Texas ambao wameahidi kumpatia mashine za za kutambua tatizo na upasuaji pamoja na dawa, ambapo angependa ziwekwe hospital ya Dar es salaam kulingana na mapendekezo ya wadau ingawa lengo lake la muda mrefu ni kufungua hospital itakayojihusisha na magonjwa ya wanawake na ndio maana anaomba msaada wa serikali na wananchi kwa ujumla ili kufanikisha lengo hilo.


  "Ningependa kama kufungua hiyo hospitali basi iwe ni Dodoma au Bagamoyo kwa kuwa ni rahisi zaidi kwa Dodoma watu mbalimbali kufika na kwa Bagamoyo inakuwa ni rahisi pia kuzifikisha mashine kutoka Bandarini"alisema Millen. Aliongeza kuwa kwa kuwa tatizo hilo linakuja kutokana na kushindwa kulishughulikia mapema hasa wakati msichana anapokuwa amevunja ungo na kuanza siku zake za hezi akiwa na maumivu makali.

  Aliwataka watoto kuwaambia wazazi pindi wanapokuwa wakipatwa na maumivu makali yaliyopitiliza wakati wakiwa kwenye siku zao za hezi na pia wazazi kujadiliana na watoto wao punde hali hiyo inapotokea na kuwawahisha hospital ili wapatiwe huduma sahihi.


  Katika tukio hilo la jana Millen aliambatana na madaktari bingwa wa wanawake wawili ambao ni daktari Fadhlun M. Alwy na daktari Belinda Ballandya wote kutoka chuo kikuu cha Afya Muhimbili ambao walitoa elimu ihusianayo na tatizo hilo na Endometriosis.  Watu wengi walijitokeza kupata somo hilo na kuzungumzia suala hilo wakiwemo, wanawake, wananume na watoto. 


     0 0
 • 06/02/14--07:24: SPORTS XTRA DAY -ARUSHA
 • Zenith Media Yatwaa Kombe la Sports Extra Day Bonanza kwa Jiji la Arusha.
  Timu ya Banana investiments ikisali kabla ya kuanza kwa mchezo.
  Huyu nae alikuwa aki #BRAZUCA katika mchezo wa Sports Xtra Day Jijini Arusha.
  Mbwiga mbwiguke the Captain wa Sports Xtra akiwapanga vijana wake.
  Huyu kijana nae alipata wasaa wa kuongea na Shaffih Dauda kuwa ana kipaji cha utangazaji wa mpira ,sasa atafikaje hapo yeye (shaffih) alipo?
  Super Striker Shaffih Dauda wa Sports Xtra akichomoka na mpira katika bonanza la Sports Xtra Day ndani ya Sheikh Amri Abeid ,Jijini Arusha.


  Captaiiiiiiiiin wa Sports Xtra Mbwiga Mbwiguke akielekea mapumziko na wenzake, pamoja na kucheza pia alitoa burudani sana kwa mashabiki na watazamaji wa Sports Xtra Day Bonanza.
  Hapa ni timu ya Mega Trade investments (K-Vant) wakicheza na Kitambi Noma.

  Muonekano mzuri wa uwanja wa kumbu kumbu ya Sheikh Amri Abeid na mlima Meru.
  Wadhamini wa Sports Xtra Day ni Clouds Media Group, Mega Trade Investments (K -Vant), Banana Investments, SBC Company Limited (Pepsi) ,Zenith Media na Wazalendo 25 Blog.
  Timu ya Zenith Media wakipanga mashambulizi yao
  Mshindi wa pili ni Timu ya Makocha wa Arusha wakitoka na Kombe lao.
  Mkurugenzi wa mauzo na Masoko wa MegaTrade Investments (K -Vant) Bw. Good Luck Kway akiongea machache, pamoja na kuipongeza Clouds Media Group na kuitaka waongeze makampuni mengine na mashindano yawe ya siku tatu au hata wiki nzima.
  Mwakilishi toka Banana Investments akizungumza machache kuhusu shindano la Sports Xtra Day
  Mwakilishi wa Zenith Media akiwashukuru waandaji wa Sports Xtra Day na kufurahia kwa Ushindi walioupata.
  Cameraman toka Clouds Media Group Ezra Kaaya akifanya yake katika Sports Xtra Day ,jijini Arusha.
  Shaffih Dauda akipata picha na Shabiki wa Kitambi Noma
  Wazee wa Kitambiiiiiii Noooma.....wakifurahia kwa ushindi wa Raundi ya kwanza

  Mbwiga Mbwiguke the Captain akipata Picha na Mashabiki wa Kitambi Noma, Kulia mwenye Box Ya huduma ya kwanza ni Jimmy Chocolate 'Mukate'

  Mchzaji wa zamani wa AFC na Zingine Cheupe akisalimiana na Mbwiga Mbwiguke
  Mbwiga Mbwiguke na shabiki wa Kitambi Noma  Mchezaji Bora ni Abuu Juma wa Timu ya Makocha wa Arusha na anaichezea mtibwa ya Morogoro akipata chupa moja ya K- Vant toka Mega Trade Investment


  Na Gadiola Emanuel wa Wazalendo 25 Blog - Arusha  Timu ya Zenith Media imeibuka mshindi wa Sports Extra Day Bonanza kwa kuifunga timu ya Makocha wa Arusha kwa njia ya penati baada ya kutoka sare bila ya kufungana, iliyofanyika katika uwanja wa kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

  Michuano hiyo ilishirikisha timu nane na kupelekea timu ya Sports Extra kutolewa kwa hatua ya mtoano, huku nahodha wake Mbwiga Mbwiguke akishindwa kuendesha timu vema ila kuambulia kuleta burudani kwa mashabiki katika mchezo huo.

  Sports extra Day Bonanza ilishirikisha makampuni tofauti tofauti ya hapa jijini Arusha. Timu hizo ni clouds sports extra , Kitambi noma, Aqua Kings ,na SBC Company inayotengeneza kinywaji cha Pepsi.

  Pia zilikuwepo timu ya Zenith Media, Timu ya Makocha wa Arusha, Banana na Mega trade investment (K vant) , ambapo zilicheza kwa hatua ya mtoano, kwa hatua ya kwanza timu ya makocha ilicheza na Aqua kings  na timu ya maocha kuibuka na goli 1 -0 , kitambi noma na Pepsi na timu ya pepsi kuibuka na ushindi wa bao 1- 0, clouds fm na zenith media ambapo zilitoka suluhu bila kufungana, na  Mega Trade Investiments (K-Vant) na Banana pia zilitoka suluhu bila kufungana .

  Hatua ya pili ilicheza kitambi noma na K-vant  ambapo kitambi noma iliibuka na goli 1- 0 dhidi ya Mega trade investiment, zenith media ilicheza na timu ya makocha ambapo walitoka 1-1. pia clouds fm ikacheza na Aqua zilitoka suluhu bila kufungana huku pepsi ikiifunga timu ya Banana Investiment.

  Timu nne zilizoingia nusu fainali ni timu ya Makocha wa Arusha na kitambi noma ambapo kitambi noma ilibamizwa 2 -0 , huku Zenith Media ikiibamiza timu ya Pepsi kwa goli 1-0 na kutinga fainali. Timu ya Arusha na Zenith Media ziliiingia Fainali.

  Mwakilishi wa TFF kwa mkoa wa Arusha Bw. Omari Wali aliwapongeza Clouds Media Group kwa kuanzisha mashindano hayo ila ikawaasa washirikishe makampuni mengine yalipo hapa Arusha. Picha zote na Gadiola Emanuel wa Wazalendo 25 Blog

  0 0
 • 06/02/14--07:26: Article 2
 • MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI SHEREHE ZA MAKABIDHIANO YA URAIS NCHINI MALAWI
   Makamu  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DkT. Mohammed Gharib Bilal leo Jumatatu Juni 02, 2014 ameshiriki katika sherehe za kukabidhi madaraka kwa Rais mpya wa Malawi Profesa Arthur Peter Mutharika katika sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Kamuzu Banda jijini Blantyre. Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na Rais wa Botswana sambamba na wawakilishi wa nchi za Zimbabwe, Msumbiji, Afrika Kusini na nyinginezo.
  Akihutubia baada ya kukabidhiwa sime ambayo ni ishara ya kuwa kiongozi wa watu wa Malawi, Rais Mteule Mutharika alisisitiza kuwa, katika kipindi cha utawala wake atahakikisha kuwa anaifanyia makubwa Malawi sambamba na uhakikisha kuwa anaifanya Malawi itimize majukumu yake ya kimataifa kufuatia kutambua kuwa kujitenga kunaweza kuifanya Malawi kutonufaika na fursa zilizopo duniani.
  “Nchi hii ipo katika dunia na siyo rahisi tena kuwa na fikra kwamba Malawi inaweza kubaki peke yake kama kisiwa. Tunahitaji kuwa na wenzetu wa kusaidia maendeleo ya Malawi. Tunawahitaji wahisani toka Kusini ama Mashariki, tunayahitaji mataifa tajiri na mataifa yanayoendelea. Tutafanikiwa sana kama tutaendeleza urafiki kwa wote. Tufanye hivi bila kujali kuwa sisi ni taifa kwani hali ya sasa inahitaji kila mmoja wetu kushirikiana na mwenzake,” alisema.
  Katika hotuba hiyo pia amesisitiza kuwa kipindi chake cha utawala atajitahidi kukabiliana na rushwa na kwamba hatakuwa na mchezo kwa wala rushwa katika kipindi akiwa madarakani. Pia alisisitiza kuhusu umuhimu wa kuiunganisha Malawi kwa miundombinu bora ili kuboresha maisha ya wananchi sambamba na kusogeza huduma za wananchi karibu.
  Rais Mutharika aliapishwa juzi baada ya kuwashinda washindani wake akiwemo Rais aliyemaliza kipindi chake Joyce Banda ambaye hata hivyo hakuweza kutokea katika sherehe hizi za kukabidhi madaraka. Akizungumzia suala la kutohudhuria kwa Rais Banda, Rais Mteule Mutharika alisema alitegemea Rais Banda kuwepo lakini hakufika nay eye anatambua kuwa wakati wa uchaguzi kulikuwa na tofauti baina yao lakini kwa sasa uchaguzi umeisha na amesahau yaliyopita ili kuanza ukurasa mpya wa kuijenga Malawi. Katika shughuli hiyo pia Rais wa zamani wa Malawi Kamuzu Banda alihudhuria.
  Makamu wa Rais Dkt. Bilal na msafara wake walitarajiwa kurejea nyumbani leo hii Jumatatu mara tu baada ya kukamilika kwa kazi hii ya makabidhiano.
   
  Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
  Juni 02, 2014 Blantyre, Malawi

  0 0

  Mwili wa marehemu Shida Salum ukiandaliwa kwa ajili ya kuombewa.
  Mwili wa marehemu ulipowasili nyumbani.
  Mwili wa marehemu Shida Salum ukishushwa baada ya kuwasili nyumbani mchana wa leo.
  Mwili wa marehemu Shida Salum ukiandaliwa kwa ajili ya kuombewa.

  Mwili wa marehemu ulipowasili nyumbani.

  Viongozi mbalimbali wakishiriki kuombea mwili wa marehemu. 

  Zitto Kabwe akiungana na waombolezaji kuombea mwili wa mama yake.

  0 0

  Mchana wa June 02 ndiyo yamefanyika mazishi ya mama mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe Bi.Shida Salum ambaye alifariki jana Mei 01 Jijini Dar es salaam kisha akasafirishwa kwa ajili ya kwenda kuzikwa Kigoma.Mazishi yamefanyika saa 9 alasiri Huko Kigoma.

  0 0

  Viongozi wa Kampuni ya Bantu Sports And Fitness Enterprise, wakipanda mti wakati wa Uzinduzi wa Kampuni hiyo iliyoambatana na utoaji wa Msaada wa Vifaa vya Michezo na vya mafunzo ya kuepuka matumizi ya madawa ya kulevya pamoja na kutunza mazingra katika Shule ya Sekondari Miono na Kikaro zilizopo Chalinze Mkoa wa Pwani.
  Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kevin William na Alex Mode wa Shule ya Kikaro wakichuana kuwania mpira baada ya kupokea msaada wa Vifaa vya Michezo na vya mafunzo ya kuepuka matumizi ya madawa ya kulevya uliotolewa na Kampuni ya Bantu Sports And Fitness Enterprise.
  Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwamtumu Mahiza kulia akimkabidhi Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kikaro, Alex Mode, mbuzi aliyetolewa na Kampuni ya Bantu Sports And Fitness Enterprise inayotoa elimu ya kupambana na mazingira madawa ya kulevya na kuhamasisha michezo pia kampuni hiyo imetoa vifaa mbalimbali vya michezo katika shule mbili hizo. Miono Kikaro zilizopo Chalinze Mkoa wa Pwani.
  Wanafunzi wa Shule ya Sekondari, Kikaro wakiwa wamembeba juu juu mbuzi waliopewa na Kampuni ya Bantu Sports And Fitness Enterprise, inayotoa elimu ya kupambana na mazingira madawa ya kulevya na kuhamasisha michezo baada ya kuifunga timu ya Shule ya Sekondari Miono kampuni hiyo pia imetoa vifaa mbalimbali vya michezo katika shule mbili hizo.
  Mbia wa Kampuni ya Bantu Sports And Fitness Enterprise, inayotoa elimu ya kupambana na mazingira madawa ya kulevya na kuhamasisha michezo Mashuleni, Said Said kulia akimkabidhi msaada wa vifaa vya kuelimisha wanafunzi jinsi ya kuepukana na matumizi ya madawa ya kurevya Mwalimu wa Shule ya Sekondari Miono, Ally Miango shuleni hapo juzi.
  Mbia wa Kampuni ya Bantu Sports And Fitness Enterprise, inayotoa elimu ya kupambana na mazingira madawa ya kulevya na kuhamasisha michezo Mashuleni, Adam Kasale, kushoto akimkabidhi msaada wa vifaa vya michezo Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kikaro, Gabriel Dominc baada ya Kampuni hiyo kutoa msaada kwa shule hiyo na Miono zilizopo Chalinze Mkoa wa Pwani, katikati ni Mkuu wa Mkoa huo, Mwamtum Mahiza.

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akioneshwa vipande vya madini aina ya Tanzanite ,katika mgodi wa mchimbaji mzawa wa madini ya Tanzanite Bi.Suzie Didas Kennedy.Katibu Mkuu wa CCM alitembelea migodi ya wachimbaji wadogo wa Mererani na kuzungumza nao juu ya changamoto zinazowakabili na namna ya kuzitatua. Pichani kati anaeshuhudia ni Mbunge wa Jimbo la Simanjiro,Mh.Christopher Ole Sendeka.
   Moja ya jiwe lenye madini kabla ya kufanyiwa mchakato. 
     Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia namna wachimbaji wadogo wanavyotumia mashine kubebea mchanga kutoka kwenye mgodi wa mchimbaji mzawa wa madini ya Tanzanite Bi.Suzie Didas Kennedy.Katibu Mkuu wa CCM alitembelea migodi ya wachimbaji wadogo wa Mererani na kuzungumza nao juu ya changamoto zinazowakabili na namna ya kuzitatua. 
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mererani ambao aliwaambia vyama vya Upinzania ni sawa na Jogoo kwani hata awike vipi hawezi fungua mlango na kwa sababu vyama hivyo havipo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi basi vinaelekea kufa kwani havina sera mpya za kujinadi kwa wananchi. 
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mererani wilaya ya Simanjiro ambao wengi ni wachimbaj wa wadogo wadogo wa madini kwenye mkutano wake wa mwisho baada ya kumaliza ziara ya siku 26 ambapo alitembelea mikoa mitatu ya Tabora, Singida na Manyara.
   Jengo la Kituo cha Afya cha Endiamtu,Mererani Simanjiro,ambapo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alikwenda kukagua na kujionea ujenzi wake ulipofikia
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akitoka kukagua mradi wa ujenzi wa kituo cha afya cha Mama na Matoto cha Endiamtu,Mererani wilayani Simanjiro.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu abdulrahman Kinana akikagua mradi wa ujenzi wa tanki la maji litakaloweza kuhudumia watu 25,000 na kutoa  lita 36,000 kwa saa linalojengwa Naisinyai Mererani.
    Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha Landanai,Wilayani Simanjiro
     Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Landanai,Wilayani Simanjiro
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiri ujenzi wa Ofisi  ya tawi jipya la CCM la Kandasikira.
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipandisha bendera ya Chama Cha Mapinduzi baada ya kuzindua tawi jipya la CCM tawi la Kandasikira.
   Baadhi ya Wazee wa Kimasai wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipofanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kandasikira,Wilayani Simanjiro.
      Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Kandasikira,Wilayani Simanjiro.
      Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana  akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Kandasikira,Wilayani Simanjiro.

older | 1 | .... | 290 | 291 | (Page 292) | 293 | 294 | .... | 1897 | newer