Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

Mahojiano ya Maggid Mjengwa na Kwanza Production

0
0
Maggid Mjengwa

Karibu katika mahojiano mwanahabari makini na wa muda mrefu ambaye pia ni mmiliki wa Kwanza Jamii, Maggid Mjengwa na Mubelwa Bandio wa Kwanza Production. Amegusia mambo mbalimbali kama masuala ya uandishi, siasa (kama mwenendo wa Bunge Maalum la Katiba) na mwenendo mzima wa nchi ya Tanzania.
Huu ni mfululizo wa mazungumzo na watu mbalimbali kuhusu masuala tofauti yaliyo muhimu kwa mustakabali wa nchi za Afrika Mashariki
Karibu
Kwa maoni, tafadhali wasiliana nasi kwa barua pepe kwanzaproduction at gmail dot com

NAPE AUNGURUMA MKOANI TABORA,AWAJIA JUU UKAWA.!

0
0

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KITUO CHA TIBA, UCHUNGUZI NA MAFUNZO YA MAGONJWA NA SARATANI ZA MATUMBO NA INI CHA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI, JIJINI DAR LEO.

0
0
1 (4) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) Mwakilishi wa Taasisi ya Else Kronner Fresenius Stiftung, Prof. Konrad Mebmer (wa tatu kushoto) Mwenyekiti wa Mfuko wa Magonjwa ya mfumo wa Chakula Munich nchini Ujerumani, Prof. Meinhard Classen (kulia) na Balozi mdogo wa Ujerumani nchini Tanzania, Hans Koeppel, kwa pamoja wakikata utepe kuashiria kufungua rasmi Jengo la Kituo cha Tiba, Uchunguzi na Mafunzo ya Magonjwa na Saratani za Matumbo na Ini cha Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati wa Hafla fupi ya ufunguzi huo iliyofanyika Hospitalini hapo jijini Dar es Salaam, leo Mei 30, 2014.
01 (3)Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa hafla ya ufunguzi wa Jengo la Kituo cha Tiba, Uchunguzi na Mafunzo ya Magonjwa na Saratani za Matumbo na Ini cha Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati wa Hafla fupi ya ufunguzi huo iliyofanyika Hospitalini hapo jijini Dar es Salaam, leo Mei 30, 2014. 
2 (4)Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Prof. Leonard Lema (wa pili kulia) kuhusu Mashine ya kuchunguza mfumo wa Hewa na Chakula, wakati Makamu alipokuwa akitembelea jengo jipya  la Kituo cha Tiba, Uchunguzi na Mafunzo ya Magonjwa na Saratani za Matumbo na Ini cha Hospitali ya Taifa Muhimbili na kujionea mashine hizo, leo Mei 30, 2014. (wa pili kushoto) ni Mtaalam wa mfumo wa chakula, Edwaldo Komba. 
4 (2)Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Muhimbili wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, alipokuwa akiwahutubia baada ya kufungua rasmi jingo hilo. Picha na OMR


…………………………………………………………………………………………………….
TAREHE 30 MEI, 2014
Mhe. Dkt. Kebwe Steven Kebwe
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii;
Dkt. Gabriel Upunda
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, Hospitali ya Taifa Muhimbili;
Dkt. Rufaro Chatara
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO)
Prof. H.C. Konrad Meßmer (MESSMER);
 Mwakilishi wa Else Kroner – Fresenius Stiftung ya Ujerumani;
Prof. Meinhard Classen;
Mwenyekiti, Munich Society of Gastroenterology;
Waheshimiwa Mabalozi;
Dkt. Marina Njelekela
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili;
Prof. Ephata Kaaya
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha  Afya na Sayansi za Tiba Muhimbili;
Prof. Msemo Diwani
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji, Taasisi ya Saratani Ocean Road;
Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Napenda kuchukua nafasi hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa uongozi mzima wa Wizara ya afya kwa kunialika kushirikiana nanyi katika tukio hili. Kwa namna ya pekee nikupongezeni kwa maandalizi mazuri na kwa kuwa na wazo la kuanzisha kituo hiki ambacho kinaongeza nguvu katika utoaji huduma za afya hapa Tanzania. Kituo hiki ni cha kwanza katika nchi za Afrika Mashariki na kitatoa huduma za tiba, uchunguzi na mafunzo kwa kutumia Hadubini. Ni wazi kuwa kituo hiki kitasaidia wananchi wetu kupata huduma hapa nchini na kitawapunguzia gharama zilizotokana na wao kwenda nje kutafuta tiba ya magonjwa haya.
Mabibi na Mabwana;
Ninafahamu kuwa ujenzi wa Kituo hiki umewezekana kutokana na ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania na Chama cha Magonjwa ya Tumbo cha Munich. Serikali ya Tanzania imechangia shilingi Milioni Mia Nane na Chama cha Magonjwa ya Tumbo cha Munich kupitia msaada kutoka ELSE KRONER FRESENIUS STIFTUNG ya Ujerumani, imechangia zaidi ya shilingi za kitanzania Bilioni Moja kwa ajili ya ununuzi wa vifaa. Huu ni uwekezaji mkubwa sana na naomba kutumia nafasi hii kukuombeni wenzetu wa Hospitali ya Muhimbili kuhakikisha kuwa mnakitumia kituo hiki ipasavyo huku pia mkivitunza vifaa vilivyopo.
Mabibi na Mabwana;
Magonjwa ya mfumo wa chakula na ini ni  miongoni mwa  matatizo makubwa ya kiafya yanayoikabili dunia nzima kwa sasa. Kumbukumbu za magonjwa ya Saratani duniani zilizotolewa mwaka 2008 zinaonyesha kuwa, jumla ya wagonjwa wapya takribani milioni tatu na laki tano, waliugua saratani za mfumo wa chakula na ini.  Kati ya hao asilimia 65% walitoka katika nchi maskini, ikiwemo Tanzania.
Saratani ya koo la chakula na ini, ndizo zinazoongoza katika nchi maskini ukilinganisha na nchi zilizoendelea, zikifuatiwa na saratani ya tumbo. Hapa kwetu Tanzania, wastani wa watu 30 hadi 35 kwa kila wananchi 100,000 hufariki dunia kila mwaka kwa saratani ya koo la chakula.
Sababu kubwa za maradhi haya ni za mtindo wa maisha kama unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara. Pia, magonjwa ya kuambukiza kama homa ya ini na bakteria aina ya Helikobakta, ni sababu mojawapo ya mtu kupata saratani za mfumo wa chakula na ini.
Mabibi na Mabwana;
Ninaelewa kuwa hatuna wataalamu wa kutosha katika huduma hii ya afya wakiwemo madaktari, wauguzi na wataalamu wengine ili kufanikisha kuendesha kituo hiki vizuri. Mmenitaarifu kuwa kuna Mabingwa wa Hadubini wanane (8) hapa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa sasa, pamoja na wauguzi watano tu ambao ni wachache sana.
Katika kusaidia kukabiliana na upungufu huu, serikali yetu itasaidia katika kufanikisha mafunzo kwa wataalamu zaidi ndani na nje ya nchi katika maeneo haya ili walau tuwe na idadi inayohitajika.
Nitumie nafasi hii pia kuwaomba wenzetu wa Taasisi za Hospitali ya Taifa Muhimbili, Chuo Kikuu cha Afya na Sayanzi za Tiba Muhimbili na Taasisi ya Saratani Ocean Road, kupanua huduma zenu na kutoa huduma za kitaalamu zaidi kama vile upandikizaji wa figo na nyinginezo. Pale mnapohitaji msaada kutoka serikalini, msisite kufanya hivyo kwani suala la afya linagusa maisha ya kila mwananchi wetu.
Mabibi na Mabwana;
Pamoja na mikakati ya kutoa huduma za tiba, nakisihi kituo hiki pamoja na taasisi wadau kufikiria namna ya kuanzisha kinga ambayo inajumuisha chanjo kwa magonjwa kama hepatitis B na C ambayo yanachangia kwa kiasi kikubwa magonjwa ya tumbo na ini (hepatology) ikiwemo saratani ya ini. Ninaelewa kuwa katika mpango wa chanjo (Expanded Program of Immunisation) chanjo ya Hepatitis B inatolewa kwa watoto.
Hata hivyo, jitihada zinatakiwa kuendelea ili kujumuisha watu wazima ambao hawajapata chanjo hiyo. Zaidi ya hayo, tafiti zinazohusu maeneo ya Afrika ni muhimu sana kwani zitatuonesha mwelekeo na kutusaidia katika kubuni jitihada mbalimbali za kukabiliana na matatizo ya kiafya yanayokabili nchi zetu.
Ndugu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili; 
Katika hotuba yako umetaja upungufu mkubwa wa wafanyakazi kama moja ya changamoto. Ni kweli changamoto hii ipo katika kila sekta, ikiwemo sekta ya afya. Hata hivyo, serikali yetu inafanya kazi kwa bidii kukabiliana nayo ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya wanafunzi wanaosomea shahada ya uzamili katika tiba na uuguzi.
Mabibi na Mabwana;
Sekta ya afya ni moja  ya sekta zinazoathiriwa sana na tatizo la wataalamu kuondoka kwa ajili ya kupata maslahi bora zaidi nje ya nchi. Naelewa kuwa kwa maendeleo ya utandawazi tuliyonayo, mtu yeyote angependa kupata maslahi bora zaidi. Serikali yetu imekuwa ikijitahidi na inaendelea kujitahidi kuhakikisha kuwa wataalamu wetu wanapata maslahi bora kadiri ambavyo tunamudu.
Bajeti ni ndogo, lakini naelewa kuwa Hospitali ya Taifa ina huduma ya wagonjwa binafsi yaani “Intramural Private Practice (IPPM)” ambayo si kwa wagonjwa binafsi tu bali pia mifuko mbalimbali ya bima ya afya kama vile Mfuko wa Taifa wa Bima  ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Afya ya Jamii. Hivyo mnaweza kabisa kutumia mapato yanayopatikana kutokana na huduma hii katika kuboresha vipato vya wataalamu wenu. Ninaamini kuwa kama ikitumika vizuri, maslahi bora yanayosemwa hayatakuwa popote zaidi ya hapa hapa Hospitali ya Taifa Muhimbili
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Muhimbili, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi za Tiba Muhimbili na Wakurugenzi Watendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road,
Kuhusiana na kudumu kwa kituo hiki, ninafahamu kuwa marafiki zetu wa Gastroenterology Foundation of Munich na Else Kroner Fresenius Stiftung hawataendelea kutusaidia milele. Ni wakati muafaka sasa kwa kituo kupitia Hospitali ya Taifa Muhimbili kuwa na bajeti yake inayojitegemea kila mwaka ambayo itajumuishwa katika bajeti yote ya mwaka bila kutegemea bajeti ya jumla ya Hospitali.
Zaidi ya hayo, kupitia huduma ya IPPM, kituo kifanye kazi kama kitengo kinachotengeneza mapato yaani kwa lugha ya kigeni “business unit” ili kutengeneza mapato yake.  Mapato hayo yatumike kununua mahitaji ya kitengo kama vile vifaa tiba kuepuka kushindwa kutoa huduma kutokana na ukosefu wa vifaa. Hii itakihakikishia kitengo kufanya kazi vizuri muda wote na huduma zake zitakuwa endelevu.
Mabibi na Mabwana;
Nitakuwa sijatenda haki kama sitatoa shukrani za dhati kwa “Gastroenterology Foundation of Munich” na “Else Kronner Fresenius Stiftung” chini ya usimamizi wa Prof. Meinhard Classen kwa jitihada zake katika kuanzishwa kwa kituo hiki na kuifanya siku ya leo kuwa ya kukumbukwa. Ni ukweli usiopingika kuwa, ufadhili wa fedha uliofanywa na Else Kronner- Fresenius Stiftung ambaye Mwakilishi wake Prof. Dr. H.C. Konrad Meßmer (MESSMER) ambaye yupo hapa pamoja na kazi ya usimamizi wa mradi huu uliofanywa na Prof. Classen binafsi kupitia Gastroenterology Foundation of Munich, haukuwa rahisi wala nafuu.
Hawa ni watu wenye upendo wa dhati na wenye kujali wagonjwa na zaidi wenye mapenzi na Afrika ndio wanaweza kufanya kazi kubwa kama hii. Hivyo kwa niaba ya Serikali ya Tanzania nasema asante sana kwako Prof. Classen pamoja na rafiki zako wa Ujerumani ambao wachache wako hapa na wale wote waliochangia katika kufanikisha kituo hiki.  
Mabibi na Mabwana;
Ningependa kuchukua nafasi hii kuishukuru Serikali ya Ujerumani kwa misaada mbalimbali iliyokwishatoa kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa watanzania. Mmekuwa pamoja nasi mara zote siyo tu katika sekta ya afya bali pia katika sekta nyingine, ikiwemo uongozi bora. Kama watanzania, tunathamini ushirikiano huu na tunaamini kuwa utadumu kadiri nchi zetu mbili zitakavyodumu.
Nashukuru tena kwa kunikaribisha hapa na sasa natamka kwamba Kituo hiki cha TIBA, UCHUNGUZI NA MAFUNZO YA MAGONJWA NA SARATANI ZA MATUMBO NA INI CHA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI kimezinduliwa rasmi.
Asanteni kwa kunisikiliza

Kamati Tendaji ya Taifa ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF, yazuru Kibaha, Pwani.

0
0
 Mkurugenzi Mtendaji waTASAF,LadislausMwamanga (aliyesimama)akitoa ufafanuzi juu ya utekelezaji waMpangowa KunusuruKaya MasikinikwawalengwawaMpangohuo(hawapo pichani).

 MkurugenziMtendajiwaHalmashauriyawilayayaKibahamkoaniPwaniTatu Seleman(mwenyemiwani) akiangaliamojayamikekailiyosukwana walengwawaMpangowaKunusuruKayamasikini,PSSN,katika kijijichaVikugekamanjiamojawapoyakukuzakipatochawananchi.

 WalengwawaMpangowakunusurukayamasikinikatikakijijichaVikugewilayayaKibahamkoaniPwani wakiwakatikamkutanouliohudhuriwapiana wajumbewakamatitendajiyaTASAF(hawapo pichani) iliyotembeleakijijihichokukaguashughulizaMpangohuozinavyoendelea.

 KaribuwagenihivindivyoanavyoelekeakusemaMkuuwamkoawaPwaniMwantumuMahiza(aliyeko mbeleya wajumbe)wakatialipowakaribishawajumbewakamatitendajiyaTASAFiliyomtembeleaofisini kwakekablayakutembeleavijijivyaVikugenaMisufinikukutanana walengwawaMpangowakunusuru kayamasikini,PSSN.

 KaimumwenyekitiwakamatitendajiyaTASAFAbbasKandoro(katikati)akisisitizajambombeleyaMkuu wamkoawaPwaniMwantumuMahiza(aliyevaakilemba)wakatiwajumbewakamatihiyo walipomtembeleamkuuhuyowamkoawaPwaniofisinikwakekablayakutembeleavijijivyaVikugena MisufinikatikawilayayaKibahakukaguwashughuliza walengwawaMpangowaKunusurukayamasikini unaoratibiwa naTASAF,kushotokwa KandoroniMkurugenziMtendajiwaTASAF, LadislausMwamanga



KamatiTendajiyaTaifayaMfukowaMaendeleoyaJamiiTASAF,yazuruKibaha, Pwani.



Wajumbewa kamatitendajiyaTaifayaMfukowaMaendeleoyaJamii,TASAFwamefanyaziarakatikavijiji vyaVikugenaMisufinikatikawilayayaKibahaMkoaniPwanikuonanamnawalengwawaMpangowa kunusurukayamasikininazinazoishikatikamazingirahatarishi,PSSN,wanavyonufaikanampangohuo.


Kablayakutembeleavijijihivyowajumbewa kamatihiyowalikutananamkuuwamkoawaPwani MwantumuMahizaambayealionyeshakuridhishwakwakenanamnaTASAFinavyochangiajitihadaza wakaziwamkoawakekupambananaumasikini.


MkuuhuyowamkoawaPwaniamesemamabadilikoyakujivuniayameanzakuonekanakatikanyanjaza elimu,afya,makazinahatauchumihususanikwenyemaeneoambayoTASAFinatekelezampangohuowa PSSN.


KatikavijijivyaVikuganaMisufiniwalengwawaMpangowa kunusurukayamasikiniwamebainishakuwa mpangohuoumesisimuakwakiwangokikubwashughulizamaendeleomiongonimwaohuku wakibainishakuwahatauwezowa kuwahudumiawatotokwendashulenakupatahudumazaafya umeongezeka.


KaimuMwenyekitiwa kamatihiyotendajiyaTASAF,ABBASKANDOROakizungumzana walengwawa mpangohuoamewatakakutobwetekanamafanikiowaliyoanzakuyapatakutokananampangohuowa TASAFbaliwaendeleekuongezajuhudikatikauzalishajimaliilihatimayewawezekujikwamuakutoka katikadimbwilaumasikini.


NayeMkurugenziMtendajiwaTASAF, LadislausMwamangaamebainishakuwataratibuzinakamishwaili hatimayewatotowaliokokatikakayamasikiniambaowamefaulukujiunganamasomoyasekondari wawezekuhudumiwakupitiaMpangowa kunusurukayamasikinikuanziamweziJulaimwakahuu.


MwamangaamesemahalihiyoimetokananaMfukokubainikuwaidadikubwayakayamasikini zilizoingizwakwenyempangowa kunusurukayamasikiniwatotowaowameitikiawitowa kuhudhuria masomokamamojawapoyamashartinahivyowengiwaokufaulukujiunganamasomoyasekondari lakinichangamotoiliyokoniuwezomdogowa kayahusikakuwasomeshawatotohao katikangaziya sekondari.




Wajumbewa kamatitendajiyaTASAFchiniyamwenyekitiwake mpyaFlorensTuruka ambayepianikatibu MkuuOfisiyaWaziriMkuuleonakeshowanahudhuriakikao cha bodi hiyojijini Dar es  Salaam.

KATIBU MKUU KIONGOZI AKUTANA NA NCHI WASHIRIKA WA MAENDELEO JIJINI DAR ES SALAAM LEO

0
0
 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akibadilishana mawazo na mabalozi na wawakilishi wa nchi washirika wa maendeleo kabla ya  mkutano aliowaandalia leo Mei 30, 2014 katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro hotel jijini Dar es salaam kuzungumzia  michango katika Kapu la Afya (Health Basket Fund) pamoja na mpango wa serikali wa kuiingiza sekta ya afya katika  kutekeleza Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN)
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa saba kutoka kushoto) akiwa katika mazungumzo  na mabalozi na wawakilishi wan chi washirika wa maendeleo katika mkutano aliowaandalia leo Mei 30, 2014 katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro hotel jijini Dar es salaam kuzungumzia  michango katika Kapu la Afya (Health Basket Fund) pamoja na mpango wa serikali wa kuiingiza sekta ya afya katika  kutekeleza  Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN)

PICHA NA IKULU

KINANA AMALIZA ZIARA YAKE WILAYANI BABATI,KESHO KUUNGURUMA WILAYANI KITETO MKOANI MANYARA

0
0
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia Wananchi,katika mkutano wa hadhara wakati akihitimisha ziara yake katika wilaya ya Babati,mkoani Manyara. Mkutano huo umefanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa Kwaraa mjini Babati,ukihudhuriwa na maelfu ya Wananchi.Ndugu Kinana akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,kwenye ziara ya siku saba mkoani Manyara,ya Kukagua kuhimiza na kusukuma miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Chama,kukagua maandalizi ya uchaguzi ya serikali za mitaa,kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Maelfu ya Wananchi wa mjini Babati wakiwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Kwaraa,ambapo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana aliwahutubia Wananchi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wananchi jioni ya leo kwenye uwanja wa Kwarahaa,wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Babati .
 

 

Katibu wa CCM,Ndugu Kinana akisikiliza maelezo kutoka kwa Dkt.Daniel Mbwambo (wa pili pichani kulia),ambaye pia ni Meneja wa Maabara katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Manyara wakati alipotembelea hospitali hiyo na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010.Shoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Manyara,Injinia Omar Chambo
 Pichani Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Manyara,Injinia Omar Chambo,akizungumza  mbele ya katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pamoja na baadhi ya watumishi wa hospitali hiyo ,Katibu Tawala mkoa wa Manyara,Injinia Omar Chambo amesema kuwa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kwenye hospitali ya Kilutherii ya Haydom wilayani Mbulu imezaa Matunda,kufuatia Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii kumtaarifu kuwa anatakiwa kuwaajiri watumishi 93 wa hospital hiyo,ambao walikuwa wanahamia serikalini katika hospitali mbalimbal,hivyo wanaingizwa katika utaratibu wa ajira ya serilali na wanatakiwa kubaki hospitalini hapo kwa utumishi wao.

Aidha Serikali katika utaratibu wake wa ruzuku,imeiongezea ruzuku hospitali hiyo inayofadhiliwa  na nchi ya Sweden kwa miaka 50,kutoka shilingi milioni 200 mpaka milioni 320 kwa mwaka ili kuboresha zaidi huduma za hospitali hiyo,ambayo imekuwa ikihudumia zaidi ya mikoa sita ya kaskazini na kanda ya kati.

 katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na baadhi ya watumishi wa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Manyara jioni ya leo.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikagua madarasa ya shule ya sekondari ya Kamoto wilayani Babati mapema leo.
 Kinana akikagua moja ya nyumba ya waalimu shule ya sekondari ya Kamoto wilayani Babati.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya Maji mkazi wa Kijiji cha Himiti Kata ya Bonga, wilaya ya Babati mjini, Zena Rashid, baada ya kuzindua mradi wa maji wa kata hiyo leo akiwa katika katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua katika wilaya hiyo ya Babati mjini mkoani Manyara. 
 Wananchi wakishangilia jambo kwenye mkutano huo.
 Sehemu  ya Wananchi wakifautilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wa hadhara mjini Babati

NORWAY NA ZANZIBAR ZATILIANA SAINI UJENGWAJI WA WODI MPYA YA WATOTO HOSPITAL YA MNAZI MMOJA

0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Mohammed Jidawi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo Kikuu cha Helse Bergen kiliopo Haukelang Norway Dkt. Stener Kvinnsland wakitia saini makubaliano ya ujenzi wa Wodi mpya ya watoto eneo la Mnazi mmoja wakishuhudiwa na Balozi wa Norway Nchini Tanzania Bi. Ingunn Klepsvik alieva miwani.
Balozi wa Norway Nchini Tanzania Bi. Ingunn Klepsvik akizungumza na viongozi wa Wizara ya Afya waliongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Mohammed Jidawi mara baada ya utiaji saini makubaliano ya ujenzi wa Wodi ya watoto eneo la Mnazi mmoja, utakaoghari bilioni moja na milioni miasita za kitanzania mpaka kumalizika kwake.
Balozi wa Norway Nchini Tanzania Bi. Ingunn Klepsvik wakiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Mohammed Jidawi mara baada ya utiaji saini makubaliano ya ujenzi wa Wodi mpya ya watoto Hospitali ya Mnazi mmoja.

MAMBO YA - RED CARPET -DIAMOND CONCERT HOUSTON TEXAS.....JUMAMOSI HII NEW NEW YORK NEW JERSEY!


MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA CHI ZA NJE WA UTURUKI.

0
0
 Makamu wa Rai wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Uturuki, Ahmet Dovutoglu, aliyeongozana na ujumbe wake wakati walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo leo, Mei 30, 2014.  Katika mazungumzo yao walisisitiza juu ya ushirikiano katika Nyanja mbalimbali baina nchi hizi mbili .  Waziri huyo yupo nchini kwa ziara ya Kiserikali iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Uturuki, Ahmet Dovutoglu, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo Mei 30, 2014. 

MWANAMITONDO AFARIKI DUNIA KUZIKWA MEI 31

0
0
Rodney enzi za uhai wake.

MBUNIFU na mwanamitindo (model) Rodrick Charles maarufu kwa jina la ‘Rodney de lativo’ amefariki dunia jana (Mei 30) baada ya kuugua kwa muda alipokuwa amelazwa Hospitali ya Jeshi, Lugalo.



Akizungumza na  Mtandao huu mapema leo kwa njia ya simu,  Rafiki wa karibu wa familia ya marehemu, David Msangi  alisema marehemu alipatwa na umauti alipokuwa akiendelea na matibabu katika Hospitali ya Lugalo, alipokuwa amelazwa na msiba huo hupo nyumbani kwa marehemu Tabata Bonyokwa, Dar.



“Tumempoteza mtu muhimu sana ambaye alikuwa na mawazo mengi ya kufikia mafanikio yake. Tutaendelea kumkumbuka.”  Alisema Msangi ambaye pia alikuwa mshahuri wa karibu wa marehemu", Msangi alisema.

Kwa mujibu wa familia ya marehemu, anatarajiwa kuzikwa  hiyo Jumamosi Mei 31huko huko kwenye makaburi ya Tabata Segerea.
Wakati wa uhai wake, marehemu alifanya kazi kwenye majukwaa mbalimbali na wabunifu na wanamitindo wakubwa wakiwemo wabunifu Ally Remtullah, Mustapha Hassanali, Asia Idarous. Wanamitindo Rio Poul, Martin Kadinda, Justine, Faustine Simon na wengine wengi.

Rodney mpaka anakutwa na umauti, alikuwa mshahuri na model  wa kampuni ya  Crisswelly African Fashion. Mareehemu alizaliwa Mei 26, 1994.  Elimu yake alisomea Magoze Sekondari  na kuhitimu 2011 na kuingia moja kwa moja kwenye  fani ya uwanamitindo na kuendelea hadi alipokutwa na umauti.

Aidha, kwa jamaa wa karibu na wabunifu na wanamitindo kwa watakaotaka maelezo ya kufika kwa marehemu wanaweza kuwasiliana na David Msangi kwa namba hii 0652901684


..Rest In Peace Rodney. I remember you forever.
Aidha kwa taarifa zaidi:
TAARIFA ZA FAMILIA NI KWAMBA MSIBA UPO BONYOKWA JIJINI DAR ES SALAAM. PANDA GARI YA TABATA SEGEREA SHUKA MWISHO WA GARI KISHA PANDA GARI ZA BONYOKWA SHUKA MWISHO NDIPO MSIBA ULIPO WA NDUGU YETU MPENDWA RODNEY TUTA MUHIFADHI KESHO SIKU YA JUMAMOSI SAA 9 ALASIRI  UKIWA NI MMOJA WAPO WA MDAU WA TANZANIA FASHION NA Crisswelly African International Fashion, MODEL AU DESIGNER NIVEMA KUJITIKEZA NA KUSHIRIKI KUMSINDIKIZA SAFARI YA MWISHO YA MPENDWA WETU RODNEY.  PIA WAWEZA KUTUMA MCHANGO WAKO KWA MAMA Asya Khamsin KWA TIGOPESA NO0713263363 
MUNGU AKUBARIKI TAFADHALI SHARE UJUMBE HUU KWA MARAFIKI ZAKO UTABARIKIWA AMEN!!!!!!!!!!!!!!
KWA MAELEZO WASILIANA NA #CRISSWELLY NO 0714802527

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS

0
0

GEORGE OTIENO TYSON AFARIKI DUNIA AJALINI MKOANI MOROGORO

0
0
TAARIFA ZILIZOIFIKIWA GLOBU YA JAMII USIKU HUU,ZINAELEZA KUWA ALIEKUWA MUONGOZAJI WA FILAMU NA VIPINDI MBALI MBALI VYA TELEVISHENI HAPA NCHINI,GEORGE TYSON (PICHANI), AMEFARIKI DUNIA.

GEORGE TYSON AMEFIKWA NA MAUTI HAYO USIKU HUU BAADA YA KUPATA AJALI MBAYA SANA BAADA YA  GARI WALIOLOKUWA WAKISAFIRIA KUTOKA MKOANI DODOMA KUJA DAR ES SALAAM, KUPINDUKA MARA KADHAA KUTOKANA NA KUPASUKA MATAIRI YA GARI HIYO AINA YA TOYOTA NOAH. 

AJALI HIYO IMETOKEA MAJIRA YA SAA MOJA JIONI,ENEO LA GAIRO MKOANI MOROGORO.WAALIKUWA WAKITOKEA KWENYE HAFLA YA KUADHIMISHA MIAKA MIWILI YA KIPINI CHA TELEVISHENI CHA THE MBONI SHOW.

NDANI YA GARI HILO KULIKUWA NA WATU WANANE AMBAO NAO HALI ZAO NI MBAYA KUTOKANA NA KUUMIA MAENEO MBALI MBALI YA MIILI YAO.  WOTE WALIKIMBIZWA  HOSPITALI YA RUFAA YA MOROGORO KWA MATIBABU.

MAREHEMU TYSON ATAKUMBUKWA KAMA MMOJA WA WATAALAMU WALIOLETA MABADILIKO MAKUBWA KATIKA  TASNIA YA FILAMU NA TV  NCHINI, AKIONGOZA FILAMU NA VIPINDI VINGI VILIVYOPATA MAFANIKIO MAKUBWA.  ALIKUWA MUME WA MSANII YVONNE CHERRY 'MONALISA' AMBAYE WALIPATA MTOTO WA KIKE, SONIA.

TUTAENDELEA KUPEANA TAARIFA KADRI ZITAKAVYOKUWA ZIKITUFIKIA.
GLOBU YA JAMII INAUNGANA NA NDUGU, JAMAA NA MARFIKI WA MAREHEMU GEORGE TYSON KATIKA KUOMBOLEZA MSIBA HUU.

MOLA NA AIWEKE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI
AMIN.

Kuona baadhi za habari  
enzi za uhai wa Tyson BOFYA HAPA

WAWILI WAPOTEZA MAISHA NA WENGINE TISA MAJERUHI KATIKA AJALI MBILI TOFAUTI MOJA IKIHUSISHA GARI LILILOBEBA WANAHABARI WA MBONI SHOW MKOANI DODOMA.

0
0
Na Sylvester Onesmo 
wa Jeshi la Polisi, Dodoma.

Watu wawili wamepoteza maisha kutokana na ajali mbili zilizotokea katika maeneo mawili tofauti na nyakati tofauti Mkoani Dodoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP (pichani) ameeleza kuwa, ajali ya kwanza ilitokea tarehe 30/05/2014 majira ya saa 18:30hrs katika kijiji cha Ipala Wilaya ya Dodoma ambapo gari lenye namba za usajili DFP 614 Toyota Land Cruiser mali ya chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo likitokea chuoni kuelekea Dodoma mjini likiendeshwa na ALFRED S/O MLIGO, MIAKA 35, MHEHE, liliacha njia na kupinduka na kusababisha kifo chake.  Pia watu watano walipata maumivu mbalimbali na walitibiwa na kuruhusiwa. 

Mwili wa marehemu upo katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma kusubiri taratibu nyingine.

Kamanda MISIME AMESEMA ajali ya pili imetokea majira ya saa 18:45hrs huko katika kijiji cha SILWA barabara ya Dodoma – Morogoro ambapo gari lenye namba za usajili T.150 CWA Toyota Granvia Station Wagon likiendeshwa na MGENI S/O SHEMAKAME, MBONDEI, MIAKA 29 MKAZI WA MBURAHATI DSM liliacha njia na kusababisha kifo cha GEORGE S/O TYSON, MIAKA 39, MWANAHABARI, Mkazi wa mbezi DSM.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Gairo ukisubiri taratibu za Polisi na wanandugu. 

Pia katika ajali hiyo wanahabari wanne (4) wa Mboni show walipata majeraha mbalimbali na kutibiwa na kuruhusiwa, ambao ni:-

1.   NIXON S/O KABUMBILE, MHAYA, MIAKA 31
2.   GRACE D/O MEENA, MCHAGA, MIAKA 28
3.   NTWA S/O KABOLE, MNYAKYUSA, MIAKA 33
4.   JUSTINE S/O BAYO, MIAKA 27, MMASAI

 Uchunguzi wa awali unaonyesha ajali zote mbili zimesababishwa na mwendokasi. Kamanda MISIME ametoa wito kwa madereva kuepuka mwendokasi na kuwa na udereva wa kujihami ambao unasaidia dereva kusimama bila kusababisha madhara linapotokea jambo lolote na hata kama ajali ikitokea madhara hayawezi kuwa makubwa kama yanavyokuwa anapokuwa kwenye mwendo wa kasi.

Wafanyakazi wa Benki ya NBC waipiga jeki timu ya watoto wenye ulemavu wa akili Zanzibar

0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (kulia) akipokea  msaada wa sh milioni mbili kutoka kwa Meneja wa NBC tawi la Zanzibar, Rajab Maalim (kushoto) zilizochangwa na wafanyakazi wa benki hiyo kwa ajili ya timu ya watoto wenye  ulemavu wa akili watakaoshiriki michezo ya olimpiki maalumu inayotarajiwa kuanza Juni 6 mwaka huu Wilayani Kibaha katika Mkoa wa Pwani. makabidhiano yalifanyika kwenye ofisi za makamu wa rais, Vuga, Zanzibar jana
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, : Balozi Seif Ali Idd akikabidhi fedha zilizochangwa na wafanyakazi wa NBC nchini pamoja na yeye mwenyewe kwa  Makamu Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Olimpiki Zanzibar, Saada Hamad katika hafla hiyo mjini Zanzibar.
Baadhi ya watoto wenye ulemavu wa akili watakaoshiriki michuano hiyo  wakiwa katika hafla hiyo.

serengeti breweries yazindua kilaji kipya cha platinum

0
0

 Wadau wakifurahia uzinduzi wa kilaji kipya cha Serengeti Platinum katika kiota cha maraha cha Escape 1 Mikocheni Mlalakuwa jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo
 Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL),Ephraim Mafuru (kulia) akiungana na wadau kukaribisha kilaji hicho kipya
 Fashifashi za uzinduzi wa kilaji kipya. Chupa hiyo ilishushwa na helikopta 
 Vijana wa THT wakinogesha hafla hiyo
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL),Ephraim Mafuru na Meneja Masoko wa Kampuni hiyo  Allan Chonjo wakisherehekea ujio wa Platinum

UCHAGUZI WA AFRIKA KUSINI NA MALAWI ULIKUWA NA KASORO - JUKWAA LA KATIBA

0
0
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya Tamko kwa Vyombo vya Habari juu ya Chaguzi za Afrika Kusini na Malawi uliofanyika mapema huu. Mkutano huo wa waandishi wa habari ulifanyika mwishoni mwa wiki katika ofisi za Jukwaa La Katiba zilizopo Sinza Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba akitia msisitizo juu ya Tamko kwa Vyombo vya Habari juu ya Chaguzi za Afrika Kusini na Malawi uliofanyika hivi karibuni.
Hali ya uchaguzi ilivyokuwa nchini Africa Kusini na Malawi ni kama ifuatavyo;
Picha inaonyesha mwanachama aliyevaa flana yenye nembo ya chama cha ANC cha Afrika Kusini siku ya uchaguzi. Hii ni sawa na kupiga kampeini siku ya uchaguzi kitendo ambacho ni kinyume na sheria za
uchaguzi.
Picha inaonyesha wapiga kura nchini Malawi wakiwa kwenye foleni ya kupiga kura eneo la wazi ikimanisha jua na mvua vinaweza vikaathiri mchakato pia sehemu ya kupigia kura ipo kwenye ngazi kwahiyo siyo
mazingira rafiki kwa watu wenye ulemavu na wazee.

SERIKALI YATOA ZAIDI YA SHILINGI 6.7 BILIONI KUJENGA HOSPITALI YA RUFAA SINGIDA

0
0
DSC_0473
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahamani Kinana akiongozwa na Mkuu wa Moa wa Singida Dk, Parseko Kone, Katibu Tawala Lianna Hassan na viongozi wengine wa Mkoa wa Singida kukagua hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida, wakati Kinana alipokuwa Mkoani Singida kwa ziara ya kikazi ya siku saba.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).

Na Nathaniel Limu, Singida
MKUU wa Mkoa wa Singida,Dk.Parseko Vicent Kone amesema serikali imetoa zaidi ya shilingi 6.7 bilioni kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoani hapa iliyoko kijiji cha Madewa nje kidogo ya Singida mjini.
Dk.Kone amesema hospitali hiyo itakapokamilika,itahudumia wagonjwa kutoka mikoa yote ya kanda ya kati.

Mkuu huyo alitoa rai hiyo wakati akitoa akitoa taarifa yake kwa katibu mkuu CCM taifa,Abrahamani Kinana aliyetembelea hospitali hiyo hivi karibuni.

Amesema mkoa umetegewa eneo la ekari 283 kwa ajili ya uendelezaji wa mradi wa hospitali hiyo, ambayo itakuwa ya mfano hapa nchini.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Dorothy Gwajima amesema lengo la mradi huo ni kuimarisha huduma za afya mkoani pamoja na mikoa jirani.
DSC_0429
Katibu Mkuu wa CCM akiweka saini kwenye kitabu cha hospitali ya Rufaa huku Naibu Katibu Mkuu wake Mwigulu Nchemba na mkuu wa Mkoa wa Singida Kone wakishuhudia.

Dk.Gwajima amesema mradi huo utakapomalizika,utakuwa na majengo 29 yatakayotumika kutoa huduma mbali mbali. Mganga huyo mkuu,amesema changamoto inayowakabili ni pamoja na uhaba wa watumishi,nyumba za kuishi watumishi na ufinyu mdogo wa bajeti ya dawa kutoka bohari kuu ya madawa (MSD).

Kwa upande wake Kinana,alitumia fursa hiyo kumpongeza Dk.Kone kwa utendaji kazi wake ambao umesaidia kujengwa kwa hospitali hiyo.
DSC_0446
Mganga mkuu wa hospitali ya Mkoa wa Singida (RMO) Bi. Doroth Bwajima akisoma taarifa ya ujenzi wa hospitali hiyo.
Amesema baada ya mradi huo kukamilika mkoa wa Singida utaondokana na matatizo ya huduma za afya.

"Ili kumuunga mkono Dk.Kone kwa hili jambo nzuri la ujenzi wa hospitali ya rufaa ambayo itasaidia Watanzania wengi kupata huduma ya afya kwa kiwango kizuri,nitahakikisha nina muunganisha na baadhi ya marafiki zangu wa ndani na nje ya nchi ili waweze kusaidia kumalizika kwa ujenzi wa hospaitali hii inayovutia",amesema Kinana.
DSC_0453
Mganga mfwawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida, Dkt Joseph Malunda, akiwaonesha michoro ya hospitali hiyo viongozi walioambatana na Kinana.
DSC_0463
Viongozi mbalimbali wa mkoa huo wakimsikiliza Dkt Malunda.
DSC_0481
Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Pendael Maasai akisisitiza jambo kwa Kinana.
DSC_0499
Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Pendael Maasai akimwonyesha Katibu Mkuu kinana vifaa mbalimbali vilivyopo kwenye hospitali hiyo ya rufaa.
DSC_0506
Mbunge MO akiangalia mojawapo ya vifaa vya hospitali ya rufaa ya singida.
DSC_0496
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mohammed Dewji akisalimiana na Daktari bingwa wa magonjwa ya kina mama wa mkoa wa Singida Dkt, Seleman Mutani wakati wa ukaguzi wa hospitali hiyo.
DSC_0522
Katibu Mkuu wa CCM Taifa akiongozana na mkuu wa Mkoa Kone, Mbunge wa jimbo la Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji, wasaidizi wa Mbunge Duda Mugheny na David Mkufya wakimwongoza Kinana kutoka nje mara baada ya kukagua hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).

KINANA AMALIZA ZIARA YAKE WILAYANI KITETO,LEO AELEKEA WILAYANI SIMANJIRO MKOANI MANYARA.

0
0
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wajumbe wa kamati ya Siasa wilaya ya Kiteto na mkoa wa Manyara,katika kikao kilichofanyoka kwenye ukumbi wa CCM wilaya.
Wananchi jamii ya Kimasai wakiwa na bango lao wakisubiri kuwasiri kwa msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana katika kijiji cha Kimotorok wilayani Kiteto mkoani Manyara.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na wananchi jamii ya Kimasai katika Kijiji cha Kimotorok baada kumsimamisha na kumuelezea changamoto walizonazo,hasa mgogolo mkubwa wa ardhi kati yao na hifadhi.
Kinana akisalimiana na wananchi jamii ya Kimasai mara baada ya kuzungumza nao katika kijiji cha Kimotorok,wilayani Kiteto mkoani Manyara,ambako inaelezwa kuwa kuna mgogolo mkubwa wa ardhi,kati ya Wafugaji na wakulima,wafugaji na hifadhi,Kinana ameahidi kuyasikiliza matatizo hayo na kueleza kuwa atayafikisha katika ngazi ya juu na kuhakikisha ufumbuzi wa kina unafanyika na kupatikana kwa wakati.
Kinana akisalimiana na wazee wa kimila wa Kimasai
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akitazama sehemu maalum ya kunyweshea maji mifugo,ambayo yeye mwenyewe aliiizindua
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akimtwisha ndoo ya maji mama wa jamii ya kimasai,mara baada ya kuzindua mradi wa maji safi na salama wenye thamani ya shilingi bilioni mbili na zaidi katika kijiji cha Ilela kata ya Esekii wilayani Kiteto mkoani Manyara.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia waanchi wa kijiji cha Nalangton,Wilayani Kiteto mkoani Manyara.
Baadhi ya Vijana wa Boda boda akiwa na bango lao
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipanda mti kwenye moja ya shule ya msingi ya Laalakir,ilioko mjini Kibaya,Wilayani Kiteto,shule ya Wakulina na Wafugaji ambayo imekuwa ikifanya vizuri wilayani humo,mkoani Manyara.
Sehemu ya Umati wa wananchi wakimsikiliza katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa mpira mjini Kibaya,wilayani Kiteto mkoani Manyara
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia wananchi wa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mpira mjini Kibaya,wilayani Kiteto mkoani Manyara
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mpira mjini Kibaya,wilayani Kiteto mkoani Manyara.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Kiteto,Mh.Benedict Ole Nangoro katika kijiji cha  cha Irkiushbor,wilaya ya Kiteto mkoani Manyara.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwasalimia wananchi mara baada ya kupokelewa katika kijiji cha Irkiushbor,wilaya ya Kiteto mkoani Manyara.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata maelezo ya mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 200 na zaidi,katika  kijiji cha Ilela kata ya Esekii wilayani Kiteto mkoani Manyara. 

Mama Mzazi wa Mhe Zitto Kabwe Afariki dunia

0
0


Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe Zitto Kabwe akiwa na mama yake Mama  Bi. Shida Salum, enzi za uhai wake. Mhe. Zitto kupitia mtandao wa Twitter amearifu kuwa mama yake amefariki dunia leo.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Tanzania (CHAWATA).Bi Shida Salun,na Mjumbe wa kamati Kuu ya chama cha CHADEMA,aliyekuwa amelazwa chumba cha Wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU),katika Hospitali ya AMI,Masaki jijini Dar,ameaga Dunia.

MWILI WA GEORGE TYSON ULIPOWASILI JIJINI DAR

0
0

 Dada wa marehemu Tyson, Doreen akilia kwa simanzi baada ya mwili wa kaka yake kuwasili katika hospitali ya Kairuki Mikocheni jijini Dar es salaam jana jioni. 
 Jeneza lenye mwili wa George Tyson likiingizwa mochwari katika Hospitali ya Kairuki, Mikocheni jijini Dar.
Wadau wa tasnia ya filamu wakiwa na jeneza la Mwili wa Tyson ukiwa mochwari katika Hospitali ya Kairuki. PICHA NA GPL
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images