More Channels
Showcase
Articles on this Page
(showing articles 561 to 580 of 37937)
- 02/12/13--12:30: _MKURUGENZI MKUU WA ...
- 02/12/13--12:48: _WAZIRI HUVISA TEREZ...
- 02/12/13--12:57: _WAZIRI MKUU MIZENGO...
- 02/12/13--13:01: _MASHALI VS CHEKA WA...
- 02/12/13--13:18: _4th Edition Interna...
- 02/12/13--18:52: _makamu wa pili wa r...
- 02/12/13--20:51: _Rais Kikwete afungu...
- 02/12/13--22:13: _Wallet imepatikana.
- 02/12/13--22:58: _Mwei yazidi kunufai...
- 02/13/13--20:36: _3rd Wedding Anniver...
- 02/13/13--20:47: _KIGOMA ALL STARS - ...
- 02/13/13--20:54: _Watanzania wahudhur...
- 02/14/13--02:24: _WAPENZI WA KINYWAJI...
- 02/14/13--03:26: _Warsha ya Maafisa w...
- 02/14/13--03:39: _SWAHILI FASHION WEEK
- 02/14/13--07:00: _montage charity bal...
- 02/14/13--07:05: _mkutano wa tatu wa ...
- 02/14/13--07:14: _Ongea na Janeth yas...
- 02/14/13--07:30: _fLAVANITe iNadondos...
- 02/14/13--09:26: _MAMA SALMA kikwete ...
(showing articles 561 to 580 of 37937)
Channel Description:
Karibuni Jamvini Wanajamii
UONGOZI WA HOTELI YA JB BELMONT YA JIJINI DAR ES SALAAM ,UNASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MKURUGENZI MKUU WA HOTELI HIYO,NDG. JUSTICE BAGUMA (PICHANI) ALIEFARIKI ASUBUHI YA LEO WAKATI AKIWAHISHWA HOSPITALI KWA MATIBABU YA UGONJWA WA SHAMBULIO LA MOYO ULIOKUWA UKIMSUMBUA.
GLOBU YA JAMII IMEPOKEA KWA MASIKITIKO MAKUBWA TAARIFA HIYO,NA INAUNGANA NA WAOMBOLEZAJI WENGINE KWENYE MSIBA HUO MKUBWA.
TAARIFA KAMILI ITAFUATA BAADAE JUU YA TARATIBU YA MSIBA HUO.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Terezya Huvisa akimsikiliza Operesheni Meneja wa Kiwanda cha Bia cha Serengeti Shekhor Mokosare, Waziri alifanya Ziara ya kukagua na kuangalia Uchafuzi wa Mazingira Unaodaiwa kufanywa na Kiwanda cha Bia cha Serengeti cha Jijini Dar es Salaam [Picha na Ali Meja].
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk Terezya Huvisa akimsikiliza Bi Mwaka Washokela kuhusu Malalamiko ya Umwangaji wa Maji Machafu ya Kiwanda cha Bia cha Serengeti katika Mtaa wa Chamwenyewe, Chang'ombe Jijini Dar es Salaam.
-Wazir wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk Terezya Huvisa akionyeshwa Mfumo wa Maji Taka na Meneja Mazingira Bw Dominick Mariki wakati Waziri alipofanya Ziara ya Kutembelea Kiwanda cha Bia cha Serengeti (SBL) cha Jijini Dar es Salaam ambacho Wananchi wanakilalamikia kinawamwagia Maji Machafu katika Mtaa wa Chamwenyewe Chang'ombe.
0 |
|
0 |
|
Waziri mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (katikati) akiwaonyesha wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa jengo jipya la kuwahudumia wagonjwa wa kansa katika Hospitali ya Kansa Ocean Road kitabu cha Mkakati wa Kitaifa wa Kudhibiti na kupambana na Kansa nchini.
Waziri mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (katikati) akikata utepe kwa kushirikiana na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kimataifa la nguvu za Atomiki Duniani Yukiya Amano (wa pili kutoka kushoto) kuashiria uzinduzi rasmi wa jengo jipya lenye vifaa vya kisasa kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wa kansa katika Taasisi ya Kansa leo Ocean Road jijini Dar es salaam. Wengine ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto), Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kansa Ocen Road Prof. Twalib Ngoma (wa tatu kutoka kushoto) na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Seif Rashid.
Baadhi ya wataalam wa Taasisi ya Kansa ya Ocean Road wakiwa ndani ya moja ya chumba cha jengo jipya lililozinduliwa jijini Dar es salaam chenye moja ya mashine yenye uwezo wa kuwahudumia wagonjwa 1600 kwa mwaka. Mashine hiyo imetolewa na Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA)
Sehemu ya nje ya jengo jipya la Taasisi ya Kansa ya Ocean Road lenye vifaa vya kisasa lilozinduliwa leo jijini Dar es salaam. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kimataifa la nguvu za Atomiki Duniani Yukiya Amano akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es salaam mara baada ya kuzinduliwa kwa jengo jipya la Taasisi ya Kansa Ocean Road lililojengwa na serikali ya Tanzania huku shirika hilo likitoa msaada wa mashine mbili kwa za kutambua athari za ugonjwa wa kansa kwenye mwili wa binadamu.
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es salaam mara baada ya kuzindua jengo jipya la Taasisi ya Kansa Ocean Road lililojengwa na serikali ya Tanzania lenye uwezo wa kuhudumia wa 257 kwa gharama ya shilingi bilioni 7.2 huku Shirika la nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) likichangia mashine 2 za kutambua sehemu zilizoathiriwa na ugonjwa wa kansa katika mwili wa binadamu zenye uwezo wa kuhudumia wagonjwa 1600 kila moja kwa mwaka.
Mabondia Thomas Mashali kushoto akitia saini mkataba wa makubaliano wa kucheza mpambano na Fransic Cheka kulia katikati ni Promota wa mpambano huo Tanaka Adam . |
Promota wa Mpambano wa ubingwa wa IBF Tanaka Adam katikati akiwaelekeza mabondia Thomas Mashali kushoto na Fransic Cheka jinsi ya kusaini ya mkataba wa makubaliano wa mpambano wao utakaofanyika mei mosi mwaka huu picha na www.superdboxingcoach. |

0 |
|
0 |
|
![]() | ||
|
0 |
|
0 |
|
Mgeni Rasmi katika hafla ya Ufunguzi wa Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd akisoma hotuba yake wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) utakaoanza kufanyika kuanzia Februari 13,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka akisoma hotuba yake mbele ya wageni waalikwa mbalimbali usiku huu waliofika kwenye hafla ya Ufunguzi wa Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) utakaoanza kufanyika kuanzia Februari 13,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau akizungumza machache usiku huu wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) utakaoanza kufanyika kuanzia Februari 13,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
Mgeni Rasmi katika hafla ya Uzinduzi wa Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd akipongezwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NSSF,Ndg. Aboubakar Rajab mara baada ya kutoa hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) utakaoanza kufanyika kuanzia Februari 13,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crenscentius Magori akitangaza majina ya washindi wa tuzo mbali mbali za NSSF kutoka mashirika,makampuni pamoja na watu binafsi .
Zawadi ya kumbukumbu ya heshima pia ilikwenda kwa Mh. Waziri Kabaka.
Baadhi ya Washindi wa Tuzo mbali mbali za NSSF wakipokea tuzo zao kutoka kwa Mgeni Rasmi katika hafla ya Ufunguzi wa Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd.Aidha zilitolewa zawadi pia kwa makampuni kadhaa kutokana na vigezo vyao hasa kwenye sekta ya uajiri,ambapo kampuni ya Vodacom,Exim Bank,Ifakara Health Institute,chuo cha St.Augustine pamoja na TPA-Bandari walinyakuwa zawadi
Mgeni Rasmi katika hafla ya Ufunguzi wa Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau akiagana na Mke wa Makamu wa pili wa Zanzibar,Mama Asha Seif Idd.
Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka (kulia) akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Ajira,Ndg. Eric Shitindi (katikati) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NSSF,Ndg. Aboubakar Rajab.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF,William Erio (kulia) akimtambulisha Meneja Mahusiano wa PPF,Lulu Mengele kwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe.
Baadhi ya Wafanyakazi wa NSSF.
Wakurugenzi Wakuu wastaafu.
Mambo ya inua Kitambaa cheupee kuonesha ishara ya upendo.
Mgeni Rasmi katika hafla ya Ufunguzi wa Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd (wa tatu kulia) na Mkewe,Mama Asha Seif Idd (wa pili kushoto) wakiwasili kwenye hoteli ya Mount Meru,Jijini Arusha usiku huu tayari kwa ufunguzi wa Mkutano huo utakaoanza kufanyika kuanzia Februari 13,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.Wengine pichani ni Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka (katikati),Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Dkt. Makongoro Mahanga (wa pili kulia),Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NSSF,Ndg. Aboubakar Rajab (nyuma ya Waziri Kabaka) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau (kulia).Picha zaidi Bofya Hapa.
0 |
|
0 |
|
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi muda mfupi baada ya kufungua mkutano wao wa Mwaka uliofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Dodoma jana Jioni,Kauli Mbiu ya mkutano Huo ni” Tujenge Uwezo wa Jamii na Polisi kukabiliana na Vurugu kwa Kuimarisha Utii wa Sheria Bila Shuruti,”.Walioketi Mbele ni.Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt.Emmanuel Nchimbi,Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi Saidi Mwema,Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda na Naibu Spika Johna Ndugai.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi ulifanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma jana.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt.Emmanuel Nchimbi pamoja na Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi Saidi Mwema muda mfupi baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Mjini Dodoma jana. Picha na Freddy Maro wa Ikulu
Kama nilivyokuambia mchana nimemfuatilia yule mtu aliyepiga simu chuo
kusema ana vitu vyangu. Nimekuta ni kijana aliyemaliza form four
anafanya kibarua Tanesco akingoja matokeo.
Amaniomba msamaha sana kwa
usumbufu nioupata kwani angetakiwa anitafute na kunirudishia mapema.
Kanirudishia wallet yangu na kila kitu isipokua fedha ambazo anasema
wenzake walizigombania mara tu walipoiokota pale petrol station.
Pia
anasema alichelewa kunitafuta kwa sababu wenzake walimshawishi kuwa
anaweza kujiingiza kwenye matatizo ya kudaiwa fedha nyingi iwapo
angejitokeza na kusema kuwa ni yeye kaikota.
Kwa mara nyingine nikushukuru sana wewe na wengine wote walionisaidia
kutangaza na kufuatilia upatikanaji wake. Mungu awabariki sana.
Mathew Mndeme
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo (aliyebeba mtoto) akiwa katika picha ya pamoja na wanakikundi cha Nguvu Kazi pamoja na maofisa wa Vodacom muda mfupi baada ya Mkuu huyo wa Wilaya kukabidhi mikopo nafuu isiyo na riba wala dhamana kwa vikundi kumi vya wanwake wajasiriamali wa kata ya Kwa mndolwa vyenye wanawake wajasriamali wadogowadogo zaidi ya 90. Mikopo hiyo imetolewa na Vodacom Foundation kupitia mradi wake wa Mwei.
Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon akiongea katika hafla ya kuwapatia mikopo ya Mwei wanawake wajasiriamali zaidi ya 90 wa Kijiji cha Kwa Mndolwa Wilayani Korogwe. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo na Meneja wa Uhusiano wa NJe wa Vodacom Salum Mwalim. Mikopo hiyo isiyo na riba wala dhamana imetolewa kwa wanawawake hao mwishoni mwa wiki kijijini hapo.
Akina mama wajasiriamali wa kata ya Kwa Mndolwa Wilayani Korogwe wakimtumbuiza Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo(hayupo pichani) muda mfupi baada ya Mkuu huyo wa Wilaya kuwasili katika kijiji cha Kwa Mndolwa mwishoni mwa wiki kuongoza hafka ya kukabidhi mikopo nafuu kwa wanawake zaidi ya 90 iliyotolewa na Vodacom Foundation kupitia mradi wake wa Mwei
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo akiongea katika hafla ya kuwapatia mikopo ya Mwei kutoka Vodacom Foundation wanawake wajasiriamali zaidi ya 90 wa Kijiji cha Kwa Mndolwa Wilayani Korogwe. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa NJe wa Vodacom Salum Mwalim na Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon (Kulia). Mikopo hiyo isiyo na riba wala dhamana imetolewa kwa wanawawake hao mwishoni mwa wiki kijijini hapo
Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo akimsikiliza Meneja Uhusiano wa nje wa Vodacom Salum Mwalim wakati wa hafla ya kuwapatia mikopo ya Mwei wanawake wajasiriamali zaidi ya 90 wa Kijiji cha Kwa Mndolwa Wilayani Korogwe.
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo akimkabidhi Hadija Tengeza wa kijiji cha Kwa Mndolwa mkopo wa Mwei kutoka Vodacom Foundation uliowanufaisha wanawake wajasariamali zaidi ya 90 wa kijijini hapo. Wengine picha kutoka kushoto ni Kaimu Katibu Tawala wa Korogwe Martha Munuo, Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim, Afisa wa Vodacom Foundation Ally Mbuyu na Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon(kulia).
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo (wa kwanza kushoto) na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim wakifuatilia maongezi na Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon(wa kwanza kulia) wakati Mkuu huyo na msafara wake ukiwasili katika kijiji cha Kwa Mndolwa kuongoza hafla ya utoaji mikopo ya Mwei mwishoni mwa wiki, Zaidi ya wanawake 90 wamenufaika na mikopo hiyo nafuu isiyo na riba wala dhamana.
Tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu Mwingi Wa Rehma kwa kutuwezesha
kufika tarehe 14 Februari ikiwa tumetimiza Miaka Mitatu Ya Ndoa Yetu
na kubarikiwa kupata Watoto Wawili yaani Lemmysa na Bahati.
Mimi
Bahati Singh nashukuru kwa Upendo na Mapenzi ya dhati aliyonayo Mke
Wangu Zeenat "Mama Iffe" yuko bega kwa bega nami wakati wote wa Tabu
na Raha Allah amuongoze na aweze kuzidisha Mapenzi, Upendo na Furaha
Kwangu na Familia kwa ujumla.. Zeenat is Strong Women, Full of Wisdom
na anaenilelea Wanangu Watano (Rahim, Joseph, Asha, Lemmysa na
Bahati).. I Love you Zeenat Miaka 100...
Asante.
Caroline Lupilli, aliyevaa koti nyekundu akiwa na dada yake Ellen Lupilli, mwenye kijaketi cha kijivu Mshindi kupitia Choice FM – Eric Massinda, mwenye T shirt ya njano na miwani, aliyeongozana na rafiki yake Alex Galinoma, mwenye T shirt ya njano.
Mshindi kupitia Castle Lite Facebook – Edger Marumbo, mwenye T shirt nyeusi akiwa na kaka yake Christopher marumbo mwenye t shirt ya blue ya mistari.
– Baadhi ya wateja wakipata ufafanuzi kuhusu kinywaji cha Baileys kutoka kwa mmoja wa mabalozi wa kinywaji hicho kinachosambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Diana Josephat (mwenye blauzi nyekundu)
Mmoja wa wapenzi wa kinywaji cha Baileys Bi. Pamela Nyambo akipokea zawadi ya glasi kutoka kwa mmoja wa mabalozi wa kinywaji hicho kinachosambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti.
Balozi wa kinywaji cha Baileys kutoka Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Erick Salva akimkabidhi zawadi ya “t-shirt” Tunu Jongolo ambaye alijishindia zawadi hiyo baada ya kununua chupa ya Baileys.
Gillian Mbori mmoja wa mabalozi wa kinywaji cha Baileys kutoka Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) akitoa ufafanuzi kwa wana habari kuhusu kinywaji cha Baileys akihusianisha na siku ya wapendao.
Mmoja wa washindi wa chakula cha jioni Bw. John Kyatika akipokea vocha ya kupata chakula cha jioni yeye pamoja na mwenzi wake leo katika siku ya wapendanao katika mgahawa wa Akemi uliopo jijini Dar es Salaam kutoka kwa mmoja wa mabalozi wa kinywaji cha Baileys Frank Kapama kutoka Kampuni ya bia ya Serengeti.
– Queen Ramson (mwenye blauzi ya kijani) akipokea zawadi ya chupa ya Baileys kutoka kwa balozi wa kinywaji hicho kinachosambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti .
0 |
|
0 |
|
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw Sazi Salula akiwa katika Picha ya Pamoja na Washiriki wa Warsha ya Maafisa wa Mazingira wa Majiji ya Mwanza,Arusha,Tangana Mbeya Warsha imefanyika kwenye Hotel ya Giraffe Jijini Dar es Salaam.
-Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Sazi Salula akifungua Warsha ya Maafisa Mazingira wa Majiji kuhusu kukuza uelewa wa kuandaa taarifa ya Hali ya Mazingira kwa Majiji ya Mwanza,Arusha, Mbeya na Tanga. Warsha hiyo iliyofanyika Giraffe Hotel, Dar es Salaam
Baadhi ya Maafisa Mazingira wa Majiji Wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais[pichani hayupo] alipokua anafungua Warsha ya Majiji kuhusu Kukuza Uelewa wa Kuandaa Tarifa ya Hali ya Mazingira ya Majiji iliiofanyika kwenye Hotel ya Giraffe Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Ofis ya Makamu wa Rais Sazi Salula akizungumza na Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Mazingia UNEP Bi Clara Makenya Mara baada ya Ufunguzi wa Warsha ya Maafisa wa Mazingira waMajiji.[Picha na Ali Meja]
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau akisisitiza jambo mbele ya Wadau zaidi ya 1000 kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania, kwenye mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaondelea hivi sasa ukiwa ni siku ya pili,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha,ambapo kauli mbiu yake kwa mwaka huu ni Sekta ya hifadhi ya Jamii Tanzania,Njia panda-Nini kifanyike.
Mbunge wa jimbo la Perahamio-Songea,Mh Jenista Mhagama akiomba kupewa ufafanuzi kuhusiana na Sera na Sheria za fedha ziko salama kiasi gani katika mifuko ya hifadhi ya jamii,kwenye mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaondelea hivi sasa ukiwa ni siku ya pili,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha,ambapo kauli mbiu yake kwa mwaka huu ni Sekta ya hifadhi ya Jamii Tanzania,Njia panda-Nini kifanyike.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA),Irene Isaka,akifafanua kuhusiana na mambo mbalimbali yahusuyo mifuko ya hifadhi ya jamii,ikiwemo sambamba na namna gani inavyoweza kukuza uchumi na kuleta maendeleo makubwa ndani ya jamii.
Mchambuzi Mkuuwa masuala ya Kifedha kutoka Benki kuu ya Tanzania (BOT),Bi.Liku Katekamba akitoa ufafanuzi kuhusiana na usalama wa fedha ndani ya mifuko ya hifadhi ya jamii,na pia amewataka Wanachama kuwa na imani ya mifuko yao ya hifadhi ya jamii.
Mchambuzi Mkuuwa masuala ya Kifedha kutoka Benki kuu ya Tanzania (BOT),Bi.Liku Katekamba akitoa ufafanuzi kuhusiana na usalama wa fedha ndani ya mifuko ya hifadhi ya jamii,na pia amewataka Wanachama kuwa na imani ya mifuko yao ya hifadhi ya jamii.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crenscentius Magori akiteta jambo na Mkuu wa Kitengo cha mahusiano NSSF,Eunice Chiume wakati wa mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaondelea hivi sasa ukiwa ni siku ya pili,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha,ambapo kauli mbiu yake kwa mwaka huu ni Sekta ya hifadhi ya Jamii Tanzania,Njia panda-Nini kifanyike.

Pichani ni sehemu ya Wadau mbalimbali zaidi ya 1000 waliohudhuria Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaondelea hivi sasa ukiwa ni siku ya pili,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha,ambapo kauli mbiu yake kwa mwaka huu ni Sekta ya hifadhi ya Jamii Tanzania,Njia panda-Nini kifanyike.PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Mkurugenzi Mkuu wa kituo hicho akitambulisha wageni kwa watoto wanaolelewa kituoni hapo.
Mmoja wa watoto wanaolelewa na kituo hspo akitoa shukrani kwa Bi. Janeth Sostenese pamoja na Crew kwa kuonyesha upendo wa dhati kitu ambacho ni adimu kwao kutokana na mazingira waliyotoka.
Mtangazaji wa Kipindi cha Ongea na Janet akizungumza na watoto wa kituo cha Kiwohede ambapo amewataka kudumisha upendo baina yao na kujiona kama watu wengine, pia amewaasa kukazania elimu ambayo itawakomboa na kuweza kuwa kama yeye hapo baadae na amewaahidi kuendelea kuwa nao pamoja.
Janeth Sostenesi na Crew nzima ya Ongea na Janeth wakikabidhi msaada wa fedha taslim kwa mwakilishi wa watoto hao ikiwa ni upendo wake katika siku hii ya wapendanao.
Baadhi ya Watoto wa kituo cha Kiwohede wakifurahia msaada huo kutoka kwa kipindi cha Ongea na Janeth.
Crew nzima ya Ongea na Janeth katika picha ya pamoja na watoto wanaoishi katika mazingira magumu wa kituo cha Kiwohede.
Mwendeshaji wa Kipindi cha Ongea na Janeth kinachorusshwa na Clouds Tv na DStv Bi. Janeth Sostenesi akisaini daftari la wageni katika kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Kiwohede kilichopo Buguruni jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili kwa ajili kufurahi na watoto hao katika sikukuu ya wapendanao pamoja na kukabidhi msaada.
Bi. Janeth Sostenesi akijaribu moja ya bidhaa za mikono zinazotengenezwa na watoto wa kituo cha Kiwohede. Kushoto Mratibu Mipango wa Kituo hicho Bi. Stella Mwambenja.


Janeth Sostenesi akishow love na Mkurugenzi Mkuu wa shirikila lisilo la kiserikali la Kiwohede Bi. Justa Mwaituka.
0 |
|
0 |
|

Mama Salma Kikwete pichani kulia akimpa pole Mama Hawa Ghasia kutokana na msiba wa baba yake,Mzee Abdulrahman Ghasia, leo katika Kijiji cha Naumbu, Mtwara. (picha na Bashir Nkoromo).