Afisa Fedha Mkuu wa Benki ya Exim, Bw. Selemani Ponda (Katikati) akizungumza na waandishi (hawapo pichani) juu ya utendaji wa kifedha wa benki hiyo katika robo ya kwanza ya mwaka ambapo faida ya benki ya kabla ya kodi imekua kwa asilimia 42 mpaka shilingi bilioni 6.4 ikilinganishwa na kipindi hicho mwaka jana. Kushoto ni Mkuu wa Hazina wa Benki ya Exim Bw. George Shumbusho na kulia Meneja Fedha Mwandamizi Bw. Issa Hamisi.
Afisa Fedha Mkuu wa Benki ya Exim, Bw. Selemani Ponda (wapili kulia) akizungumza na waandishi (hawapo pichani) juu ya utendaji wa kifedha wa benki hiyo katika robo ya kwanza ya mwaka ambapo faida ya benki ya kabla ya kodi imekua kwa asilimia 42 mpaka shilingi bilioni 6.4 ikilinganishwa na kipindi hicho mwaka jana. Wa kwanza kushoto ni Meneja Msaidizi Masoko wa Benki ya Exim Bi. Anita Goshashy, Mkuu wa Hazina wa Benki hiyo Bw. George Shumbusho (wapili kushoto) na kulia ni Meneja Fedha Mwandamizi Bw. Issa Hamisi.
======== ======= =======
BENKI ya Exim imepata faida ya shilingi bilioni 6.8 kabla ya kodi katika robo ya kwanza ya mwaka wake wa fedha, ambayo ni ongezeko la asilimia 42 ukilinganisha na mahesabu ya mapato ya mwaka jana kipidi kama hiki.
“Tunayofuraha yakuripoti matokeo mazuri katika mwanzo huu wa mwaka,” alisema Ponda, Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Exim. “Kukua huku kwa mapato kunaonyesha mafanikio ya hali ya juu ya benki katika vyanzo mbali mbali vya mapato. Tutaendelea kuboresha utendaji wetu ili kufikia matakwa ya wateja wetu. Benki yetu inaendelea kwenda katika mwelekeo nzuri. Tunazidi kupiga hatua katika kufikia malengo yetu. Matokeo tuliyoyapata ya kifedha katika robo hii ya kwanza ya mwaka yanatupa matumaini makubwa,” aliongeza Ponda.
Pato la jumla limeweza kukua hadi shilingi bilioni 12.5 ambayo ni ongezeko kwa asilimia 27 ukilinganisha na kipindi sawa na hichi mwaka 2013. Pato litokanalo na tozo na kamisheni limeweza kukua hadi shilingi bilioni 8, ambayo ni ukuwaji kwa asilimia 37 ukilinganisha na robo ya mwaka jana, hali iliyosababishwa na kutanuka kwa biashara ya fedha za kigeni.
“Matumizi ya uendeshaji wa benki yalidhibitiwa na kupanda kidogo kwa asilimia 11.6 mpaka shilingi bilioni 13, yakitokana na uanzishwaji wa gharama za matawi mapya na motisha za wafanyakazi zikiwa ni jitihada za kuongeza upatikanaji wa benki kijeografia na kuimarisha shughuli zake. Kwa hivyo, uwiano wa gharama na mapato umeshuka kwa kiasi kikubwa kutoka asilimia 75 iliyopatikana katika robo ya mwaka uliopita mpaka asilimia 64, "aliongeza.
Amana za wateja zimebaki palepale shilingi bilioni 747 ukilinganisha na robo ya mwaka uliopita. Jalada la mikopo limerekodi kupanda kwa asilimia 22 ukilinganisha na robo ya mwaka jana mpaka shilingi bilioni 538 pamoja na mizania ya benki kukua kwa asilimia 10 mpaka shilingi tilioni 1.1.
“Kipaumbele kikubwa kwetu bado kipo katika jitihada za kuimarisha nafasi yetu katika soko na kuboresha huduma ili kufikia matakwa ya wateja wetu kupitia uboreshaji wa shughuli zetu. Mwenendo mzuri wa kuwatosheleza wateja ni ishara nzuri inayoonyesha kuwa tutafikia malengo yetu kwa mwaka huu,” alisema Afisa huyo mkuu wa fedha.
Katika mchakato wa kurahisisha utoaji huduma bora kwa wateja, baadhi ya shughuli kama vile za kufungua akaunti na uanzishaji zimeweza kuboreshwa zaidi. Uanzishwaji wa “operesheni ya pamoja” umelenga katika kuongeza msukumo na motisha katika michakato yote ya kazi ili kuongeza ufanisi zaidi na kuhakikisha matakwa ya wateja yanafikiwa kikamilifu,” alisema Bw. Ponda.
Katika jitihada za kupambana na mabadiliko ya mahitaji ya wateja, Benki imeweza kuliunda tawi lake la Kariakoo kwa namna ya kuwahudumia wateja ambaowanafanya shughuli zao zaidi ya masaa ya kawaida ya benki na kuruhusiwa kupata huduma za kibenki kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa mbili usiku. Pia,"Barua pepe na SMS" zinatoa ujumbe wa papo kwa wateja kuwajulisha mihamala mbali mbali inayofanyika katika akaunti zao.
Benki pia imeendelea na jitihada zake za kutanua huduma zake. Benki hivi karibuni imefungua tawi jipya katika kisiwa cha Anjouni mjini Domoni. Kituo cha biashara cha kipekee mkoani Arusha, cha tatu katika jiji na cha 26 nchini kilizinduliwa rasmi katika robo hii. Benki pia inampango wa kufungua tawi jipya mkoani Tabora ambalo litafanya jumla ya matawi kuwa 32 nchi nzima. Kulingana na utendaji mzuri katika robo hii ya kwanza na fursa zilizopo katika uchumi, Benki ya inalenga kuboresha zaidi utendaji katika robo ikijikita zaidi katikakampeni za kimauzo na kuongeza ufanisi zaidi.