Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 279 | 280 | (Page 281) | 282 | 283 | .... | 1898 | newer

  0 0

  DSC_0053
  Afisa Mipango Kitengo cha Mawasiliano, Habari na Tehama UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, akiwasilisha mada kuhusu mchango wa uhuru wa vyombo vya habari katika utawala bora, kukuza uwezo na kupunguza umaskini kongamano la waandishi wa habari lilioandaliwa kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yanayofanyika jijini Arusha.

  “Kwa sasa tasnia hii iko kwenye wakati mgumu sana kwani hata marais wa nchi mbalimbali mfano Uganda, Kenya hata Marekani wanakinzana na vyombo vya habari kwa madai kuwa kauli zao zinapotoshwa, laikini ukweli ni kwamba ni vyema kauli hizo za viongozi zikachunguzwa kwa undani zaidi ili kuelewa iwapo zina uwajibikaji ndani yake,” alisema Kibanda.

  Kibanda aliongeza kuwa wakati umefika sasa kwa waandishi kutambua kuwa kuna ajenda za siri zilizojificha dhidi ya uteswaji wa waandhishi wa habari hivyo yasidharauliwe, yafanyiwe kazi kwa kina ili kuelewa kiini cha tatizo kwa kupata ufumbuzi.
  Kwa upande wake mwandishi mkongwe na aliyetunukiwa tuzo ya maisha mwaka 2012 na Baraza la Habari Hamza Kasongo alisema vyombo vya habari vina nguvu kubwa katika kushawishi hivyo vitumie nguvu hiyo kama muhimili wa nne wa nchi katika kuzikabili changamoto zilizopo.

  “Kuwe na mtandao unaoeleweka wa mawasaliano kati ya waandishi wa habari nchini ili kuhakikisha kuwa matatizo yaliyopo yanatatuliwa bila woga na kwa ujasiri kwa lengo la kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa,” alisema Kasongo.
  DSC_0060
  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kitivo cha Sheria , Bw. James Jesse, akitoa mada kuhusu umuhimu wa sheria katika kulinda haki ya uhuru wa kujieleza kwa kila mtu wakati wa kongamano la waandishi wa habari lilioandaliwa kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani yanayofikia kilele leo jijini Arusha.

  Mwanahabari mwingine mkongwe Dokta Samwilu Mwaffisi aliyetoa mada ya Maadili ya Uandishi wa Habari alisema kuwa kuna haja ya waandishi kuzingatia uhuru wa habari walionao kwa kuzingatia maadili yanayowaongoza ili kuboresha heshima waliyonayo katika jamii kwa kuandika ukweli na uhakika, bila upendeleo, kutoa fursa ya kujitetea na kukubali kuomba radhi pale unapokosea.

  “Kuandika habari zenye kuzingatia maadili kunapunguza manung’uniko, mashauri na kuongeza heshima ya chombo cha habari na mwanahabari mwenyewe,”
  Akizungumzia suala la ufanisi, Rais wa Vilabu vya Waandishi wa Habari, Kenneth Simbaya, aliwaasa waandishi wa habari kusimamia ukweli katika kazi zao na kuacha kufanya kazi kwa mazoea jambo ambalo litakawaweka huru zaidi katika utekelezaji wa shughuli zao za uandishi wa habari.

  Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na umoja wa asasi mbalimbali chini ya uenyekiti wa MISA TANZANIA unafikia kilele chake tarehe 3 Mei kwa kuzindua majarida mbalimbali, matamko kutoka asasi mbalimbali na kuhitimishwa kwa tafrija ya chakula cha jioni chini ya mgeni rasmi Jaji Mstaafu Mheshimiwa Mark Bomani.
  DSC_0341
  Mwanahabari Mkongwe kutoka Chuo Kikuu Huria, Dokta Samwilu Mwaffisi (kulia) akiwasilisha mada ya Maadili ya Uandishi wa Habari kwenye kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha. Kushoto ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Iringa, Bw. Simon Berege.
  DSC_0311
  Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda, akitoa maoni yake wakati wa kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
  DSC_0079
  Pichani juu na chini ni baadhi ya waandishi wa habari wakongwe, mabalozi na wanahabari washiriki katika kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.


  DSC_0028
  DSC_0283
  DSC_0371
  Mwandishi wa Habari Chokonozi, Bw. Fredrick Katulanda, akielezea madhila mbalimbali yaliyomsibu katika utekelezaji wake wa kuandika habari za uchambuzi.
  DSC_0119
  Mwanahabari Mkongwe Bi. Leila Sheikh akichangia mada ya Mchango wa Uhuru Wa Vyombo Vya Habari Katika Utawala Bora, Kukuza Uwezo Na Kupunguza Umaskini wakati wa kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
  DSC_0348
  Mmiliki wa Gazeti tando la Mjengwa na Kituo cha Redio Kwanza Jamii, Bw. Maggid Mjengwa akielezea jinsi Intaneti inavyoweza kuunganisha mtandao wa Redio.
  DSC_0339
  Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA) na Mkurugenzi wa kituo cha mawasiliano Sengerema, Bw. Felician Ncheye akichangia mada.
  DSC_0386
  Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Mama Rose Haji Mwalimu, (kushoto) akiwa na baadhi ya washiriki wa Kongamamo hilo.
  DSC_0310
  Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Kenneth Simbaya, akishiriki kwenye kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
  DSC_0281
  Picha juu na chini Baadhi ya washiriki wakichangia maoni yao kwenye kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
  DSC_0322
  DSC_0214
  Kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 likiendelea.
  DSC_0164
  Mwanakamati wa maandilizi ya maadhimisho ya Kongamano la Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014, Usia Nkhoma Ledama wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda nje ya ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa AICC jijini Arusha.
  DSC_0017
  Baadhi ya waandishi wa habari na wadau kutoka asasi mbalimbali nchini wakifanya usajili kwenye kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.(Picha na Zainul Mzige).
  Na Waandishi Wetu, Arusha
  Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda ametoa wito kwa waandishi wa habari nchini kuyapa uzito matukio yanayowatokea waandishi wa habari na kuyapigia kelele kwa nguvu zote ili kuyakomesha.
  Kibanda aliyasema hayo jana mjini Arusha katika kongamano lililoandaliwa kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani na kuongeza kwamba wakati umefika kwa waandishi wa habari kuondoa tofauti zao na kuungana pamoja kuongeza nguvu waliyonayo kukabiliana na ukatili unaoendelea dhidi ya waandishi wa habari katika miaka ya hivi karibuni.
  “Baadhi ya wahariri huwa hawayaandiki madhila yanayowasibu waandishi wa habari na kuyapa uzito unaostahili aidha kwa huyapuuzia au kudharau kwa kuwa hayawahusu moja kwa moja,” alisema Kibanda.
  Aliongeza kwa kusema kuwa vyombo vya habari mara nyingi vimekuwa vikinyooshewa vidole na kulaumiwa kwa kutokufanya kazi kwa uadilifu jambo ambalo linatafsiriwa kuwa ni la uonevu, vinatumiwa vibaya na hakuna anayesimama kuvitetea kutokana na mchango wake mkubwa katika jamii.

  0 0

  Profesa Boas akiwa na Cheif wa swahilivilla Abou Shatry baada ya Mahojiano siku ya Ijumaa Mei 2, 2014 Maryland Nchini Marekani.   Sikiliza Audio ya Mahojiano kuhusu Muungano na Profesa Boas ambaye ni Mwalimu wa Mawasiliano na Sera (Communication and Public Policy) University of Maryland University College Washington DC

  0 0

  Ndani ya Kijiji cha Maisha Plus/ Mama Shujaa wa chakula kila siku ya Alhamisi huwa panafanyika uchaguzi wa kumpata Rais mpya ambaye anachaguliwa na Washiriki wenyewe wa Kijiji cha Maisha Plus ambapo kati ya hao mmoja hupatikana na  Marais  waliopita hawapatiwi nafasi ya kugombea tena, na kwamba mama yake na Rais huteuliwa moja kwa moja kuwa Markia wa Kijiji hicho.
  Markia Mpya wa Kijiji cha Maisha Plus Elizabeth Masha kutoka Morogoro Tanzania.
  Rais Mpya wa Kijiji cha Maisha Plus Mary Masha kutoka Nchini Kenya
  Kazi ya uchaguzi ilianza Kijijini hapo ambapo idadi ya washiriki 36 wakiwemo vijana 16 na kinamama 20 Kila siku ya Alhamisi ni siku ya uchaguzi wa Rais wa kijiji cha Maisha Plus  ambaye husimamia shughuli zote zinazofanyika katika kijji hicho. 

  Wiki hii washiriki 10 waliteuliwa kugombea nafasi ya urais ambapo 7 ndiyo waliopigiwa kura ya siri na kupata mshindi. Washiriki wawili kati yao hawakuweza kugombea nafasi ya hiyo kutokana na utaratibu uliopo kwamba aliyewahi kushika wadhifa huo kwa muhula uliopita hataweza kugombea tena. 

  Marais hao wa mihula uliyopita ni Bonifas Mang’anyi na Bakari Khalid wote watanzania. Abdul Karim kutoka Burundi alijitoa kwa kuwa hakuwa tayari kushika wadhifa huo kwa sasa.

   Kwa kawaida kila kijana huwa na mama katika kijiji cha Maisha Plus na endapo kijana atachaguliwa kuwa Rais mama yake huwa Malkia ambaye humshauri Rais na kufanya maamuzi katika kijiji hicho. 
   
  Uchaguzi ulifanyika kwa wagombea 7 akiwemo Shida Mganga, Seif Mohamed, Ally Thabiti, Mbonimpaye Nkoronko na Hyasinta Hokororo kutoka Tanzania, Ngabozinza Daniel kutoka Rwanda na Mary Masha kutoka Kenya. Uchaguzi wa Rais ulifanyika mara mbili kwa kuwa washindi walipata kura sawa iliyopelekea kurudia kupiga kura ili kupata mshindi mmoja. 

  Washindi waliopata kura sawa ni Mary Masha kutoka Kenya na Ally Thabit kutoka Tanzania ambapo Mary Masha aliibuka mshindi kwa kura 21 kwa 15. Hivyo Rais wa wiki hii ni Mary Masha na malkia Elizabeth Simon.

  Utaratibu wa kuchagua wagombea: Kila mshiriki hujaza fomu kuteua jina la atakayekuwa kuwa Rais wa wiki hiyo. Walioteuliwa hujinadi ili wapate kupigiwa kura na hatimaye kupata mshindi.

  0 0

  Mkurugenzi wa Shiriki la KIVULINI Bw Ramadhan Masele akisisitiza jambo wakati akifunga mafunzo maalum kwa wasichana 30 walio na umri kati ya miaka 18 mpaka 25 kutoka wilaya ya Ilemela na Nyamagana za jijini Mwanza hapo jana. Wasichana hao wamepewa mafunzo kuhusu ukatili wa kijinsia majumbani pamoja na Kingono lengo likiwa ni kuzalisha waelimisha rika wengi zaidi mitaani na kutengeneza jamii isiyokuwa na ukatili wa kijinsia na kingono kwa kwa watoto wa kike.
  Mkufunzi wa Masuala ya Kijinsia Bi. Tumaini Kyola akitoa mafunzo kwa kundi la Wasichana 30 ambao hawako mashuleni juu ya mbinu mbalimbali za kuelemisha jamii kuhusu masuala Ukatili wa Majumbani na wa kingono pia. Wasichana hawa wanategemewa kwenda kuwafundisha wasichana wenzao wa mitaani, kila mmoja amepewa lengo la kufikia wasichana 50. 
  Baadhi ya wasichana 30 wakiwa makini kufuatilia mafunzo waliokuwa wakipatiwa na mkufunzi wao (hayupo pichani), hili ni kundi la kwanza kwa wasichana waliokuwa nje ya shule ambapo mafunzo ya kundi la pili kwa wasichana waliopo mashuleni yanatarajiwa kuanza mwezi wa sita kwa kushirikisha shule zipatazo 40 toka wilaya za jiji la Mwanza.

  Wasichana thelathini pamoja na Mkufunzi wao na baadhi ya maafisa wa Kivulini wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mafunzo hayo ya siku tano hapo jana katika ukumbi wa VETA jijini Mwanza.


  Mkurugenzi wa shirika la kutetea Haki za Wanawake na Wasichana KIVULINI lenye makao yake makuu jijini Mwanza Bw. Ramadhan Masele amefunga rasmi mafunzo ya siku tano yanayolenga  kuwajengea wasichana uwezo wa kutoa elimu juu ya masuala ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia chini ya mradi wa kuwashirikisha vijana kuzui Ukatili wa majumbani ikiwa ni pamoja na ukatili wa  kingono kwa watoto wa kike na wasichana.  

  Akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo Bw. Masele aliwataka washiriki wote kutumia elimu hiyo muhimu waliyoipata kutoa elimu na kuongeza uwelewa zaidi kwa jamii yao kuanzia ngazi ya familia, marafiki na vikundi mbalimbali na kuwa chachu ya mabadiliko  juu ya kupigania haki za wanawake na wasichana wanaonyanyaswa kijinsia katika jamii zao.


  “Imani yangu ni kuwa semina hii itakuwa ni kiwanda kizuri cha kuwatengeneza nyinyi wote kuwa mabalozi wazuri katika jamii, baada ya mafunzo haya tunaamini kuwa mtakuwa chachu ya mabadiliko katika kutetea na kulinda haki za wanawake na wasichana kwa kukemea, Kupinga, kuripoti na kuzuia aina zote za ukatili wa majumbani na kingono kwa wasichana na wanawake na kutoa taarifa pindi vitendo hivi vinapotokea” alisema Bw. Masele


  “Kila mmoja aliyehudhuria mafunzo haya  kwa nafasi aliyonayo tunaamini anaweza kuwa chachu ya mabadiliko endapo atatimiza wajibu wake kwenye eneo analoishi. Hili suala la ukatili wa kijinsia si suala geni nchini hasa eneo hili la kanda ya ziwa hivyo kuna kila sababu ya kuzidisha mapambano dhidi yake, cha muhimu ni kuzingatia mafunzo mliyopewa na muwezeshaji wenu” aliongeza Bw. Masele.


  Mafunzo hayo yamefanyika kwa muda wa siku 5 kwa vijana 30 wa kike wenye umri kati ya miaka 18-24 kutoka wilaya mbili za Nyamagana na Ilemela jijini Mwanza. Lengo la Mafunzo ni kuwajengea vijana uwezo wao binafsi na uwezo wa kuelimisha jamii hasa Vijana wenzao  kupambana na kupinga Ukatili dhidi ya wanawake na wasichana katika maeneo wanayoishi.


  Mafunzo yalianza Jumatatu tarehe 28 Aprili, 2014 mpaka tarehe 2 Aprili, 2014 katika Ukumbi wa Chuo cha Ufundi Stadi, VETA kilichopo Nyakato nje kidogo ya jiji la Mwanza.


  Takwimu zinaonyesha bado jamii inakabiliwa na ukatili mkubwa wa kijinsia ambapo ubeberu wa wanaume pamoja na mila na desturi potofu zimeonekana kukandamiza jinsi ya kike zaidi kuliko jinsi ya kiume, ukatili huo ni wa kijamii, kiuchumi pamoja na kisaikolojia hivyo kunaitajika juhudi za dhati na makusudi kuweza kukabiliana na tatizo lilopo kwa jamii.


  Akimalizia mawaidha yake kwa washiriki Bw. Masele alisema lengo la mafunzo hayo ni kuona mabadiliko katika mfumo juu ya kujali na kuheshimu haki za mwanamke na wasichana, kwani jamii nyingi zinapambana na mifumo miwili mikubwa, ambayo ni mfumo dume ambao umekuwa ukiwakandamiza wanawake katika jamii na mfumo wa kitabaka unaoongeza nafasi kati ya matajiri na masikini.


  Shirika la KIVULINI kwa kushirikiana na Asasi ya Vijana  inayojulikana kama Wadada Centre for Solution Focus Approach ndio waandaji wa mafunzo hayo kupitia mradi wa kuwashirikisha vijana kuzui Ukatili majumbani na Ukatili wa Kingono chini ya ufadhili wa Shirika la terre des hommes ch (tdhschweiz) - Fursa kwa Vijana  la nchini Switzerland


  Kivulini ni shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na kutetea pamoja na kulinda Haki za Wanawake na Wasichana. Shiriki la Kivulini linahamasisha jamii (Wanawake, Wanaume na Vijana ) kulinda, kutetea Haki za Wanawake na Wasichana kwa kupinga vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia. Makao makuu ya shirika yapo jijini Mwanza, Wilaya ya Ilemela, Tanzania.


  0 0

  Postamasta mkuu na afisa mtendaji mkuu wa shirika la posta Tanzania Ndugu Deos Khamisi Mndeme(mwenye koti kushoto) akikabidhi cheti na hundi kwa mfanyakazi bora kitaifa kutoka wafanyakazi wasimamizi, Ndugu Michael Mhagama (kulia).
  Ndugu Deos Khamisi Mndeme akikabidhi cheti na hundi kwa mfanyakazi bora kutoka wafanyakazi watendaji Ndugu Joseph Kakokele.

  Mfanyakazi bora kutoka Divisheni ya Rasimali za Shirika, Fredrick Makundi, akipokea cheti na tuzo kutoka kwa Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakati wa hafla hiyo.
  Mfanyakazi bora kutoka Divisheni ya Rasimali za Shirika, Abdallah Waziri, akipokea cheti na tuzo kutoka kwa Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakati wa hafla hiyo.
  Mfanyakazi bora kutoka Ofisi ya Postamasta Mkuu, Mashala Lifunga, akipokea cheti na tuzo kutoka kwa Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakati wa hafla hiyo iliyofana kwa kiasi kikubwa.
  Mfanyakazi bora kutoka  Ofisi ya Postamasta Mkuu, Christopher Mjema, akipokea cheti na tuzo kutoka kwa Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), kwenye hafla hiyo.
   

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana (kushoto) akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar,Ndg. Vuai Ali Vuai wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Pemba,Mchana wa leo tayari kwa Mkutano wa Hadhara wa CCM kwa Mikoa Miwili ya Pemba.wengine pichani ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba, Ndg. Mzee Mbelwa (kulia) akifUatiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba,Abdallah Mshindo.
   Naibu Katibu Mkuu wa CCM - Zanzibar,Ndg. Vuai Ali Vuai (katikati) akifurahia jambo na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye wakati akimkaribisha Kisiwani Pemba leo.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana (kushoto) akizungumza jambo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar,Ndg. Vuai Ali Vuai mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Pemba,mchana huu.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana (kushoto) na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye wakisalimiana na baadhi ya wanaCCM wa Kisiwani Pemba waliofika uwanjani hapo kuwapokea.
   Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana ukitokea kwenye Uwanja wa Ndege wa Pemba kuelekea Ofisi Kuu ya CCM Pemba.   0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhi hundi ya jumla ya Shilingi Milioni miamoja na Hamsini 150m/- kwa wawakilishi wa kituo cha kulea watoto yatima cha Moyo wa Huruma kilichopo mkoa wa Geita.

  Fedha hizo si sehemu ya shilingi milioni mia saba(700m/-) alizokabidhi Rais Kikwete jana usiku kwa taasisi mbalimbali zinazojishughulisha na mapambano dhidi ya ukimwi Tanzania.Fedha hizo zinatokana na kampeni ya kukusanya fedha kwa njia ya kupanda mlima Kilimanjaro kila mwaka ambapo wafadhili mbalimbali huchangia watoto na watu wengine.

  Pichani watoto wawili watakaopanda mlima Kilimanjaro Jacob Musa(watatu kushoto) na Julitha Sylvester(wapili kulia) wanaofadhiliwa na kituo cha Moyo wa huruma wakipokea hundi ya kituo chao.

  Wengine katika picha kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dr.Florence Turuka,Mkurugenzi Mkuu wa TACAIDS Bi Fatma Mrisho,Mkurugenzi Mtendaji wa Geita Gold Mines Bwana Michael Van Anen(watano kushoto),Naibu Waziri wa Afya Dr.Steven Kebwe, na kulia ni msimamizi wa kituo cha kulelea watot yatima cha Moyo wa Huruma Sista Adalbera Mukure.

  Katika hafla ya jana ya kuchangia kampeni hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam zaidi ya shilingi milioni mia tisa 900m/- zilikusanywa. (picha na Freddy Maro) 

  0 0


  Na Woinde Shizza,Arusha.

  Jaji mstaafu  Mark Bomani jana (leo )amezindua rasmi video  ya wimbo
  wa waandishi wa habari ujulikanayo kwa jina la Uhuru wangu  pamoja na
  albamu mpya ya msanii wa mziki wa nyimbo za asili Mrisho Mpoto
  ijulikanayo kwa jina la Waite katika kilele cha maathimisho ya uhuru
  wa vyombo vya habari duniani.

  Uhuru wangu uko wapi mwanahabari mie,kalamu yangu,sauti yangu kamera  yangu leo ndio kaburi langu mie.Huo ndio wimbo wa kundi la  Mrisho Mpoto Band ambalo ulikuwa  ukiwaburudisha wanahabari katika uzinduzi wa albamu Mrisho Mpoto  Band,unaoelezea mambo mbalimbali wanayokumbana nayo wanahabari wa  vyombo mbalimbali vya habari.  Akighani mashairi ya wimbo huo katika uzinduzialisema poleni sana misa
  Tanzania,TMF,MOAT,UTPC ,TCRA kama mtu ile timu ya watu watano
  tuyioituma Ujerumani ,Norway,Sweden ipo wapi ripoti yake
  Akiongea wakati wa uzinduzi wa albamu hiyo pamoja na wimbo huo wa
  wanahabari msanii mrisho mpoto alisema kuwa yeye alifarijika sana pale
  alivyofatwa na wanahabari  na kumuomba awatungie wimbo  ambao
  unawahusu wanahabari pamoja mambo ambayo yanawakabili.

  Alisema kuwa wamekaa wakashauriana na timu yake na bendi yake  kuwa   watu wasanii wengi wamekuwa wakizindua albamu kwa kuweka  viingilio  vikubwa kualika watu wengi lakini yeye binafsi ameamua kuzindua albamu   hii  katika siku hii ya waandishi wa habari kwa kuwa wamemtoa mbali na   anakitu cha kuwapa zaidi ya kuwapa  zawadi hii ya kuzindua  albamu  yake mbele yao.  Alibainisha kuwa  mbali nakuzindua albamu hiyo pia kwa kuwa waandishi     wamempa hadhi ya kuwatungia wimbo pia anajitolea kuweka wimbo huu wa  waandishi wa habari   ndani ya   albamu yake ili kila mtanzania na   mshabiki wake ambaye atanunua albamu yake  aukute wimbo ndani ya    albamu yake.  "Hii albamu yangu itakuwa na nyimbo zangu zote ikiwa na wimbo wa
  nikipata nauli adi nyimbo zake zote ambazo zinajulikana na kiukweli
  najisikia kulia sana kupewa heshima hii nzito ya kuzindua albamu yangu
  na ata jana nilivyokuwa nakuja uku nilikuwa na zunguma na mh bomani
  kuwa hii kwangu itakuwa ni historia  katika maisha yake"alisema mpoto
  Katika wakati wimbo huu ukiendelea  wanahabari walionekana wakitoa
  machozi kwa kuuzunishwa na tenzi zilizopo katika wimbo huu kwani
  msanii huu ameuimba kiualisiazaidi.

  0 0


  0 0

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema shule za msingi hapa nchini zinakabiliwa na upungufu wa madawati karibu milioni moja na nusu ameitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ijifunge mkanda na kulipa kipaumbele suala la kupunguza tatizo hilo.

  Ametoa agizo hilo leo mchana (Jumamosi, Mei 3, 2014) wakati akiwahutubia mamia ya wakazi wa Mkoa wa Dodoma ambao walihudhuria uzinduzi wa Wiki ya Elimu Tanzania kwenye uwanja wa Jamhuri.

  “Takwimu nilizonazo zinaonyesha kuwa Tanzania ina mahitaji ya madawati 3,302,678 wakati madawati yaliyopo ni 1,837,783 kwa hiyo tuna upungufu wa madawati 1,464,895 katika shule zetu za msingi,”  alisema Waziri Mkuu.

  Kutokana na mahitaji hayo, Waziri Mkuu alisema endapo Serikali itaamua kutengeneza madawati 100,000 kwa mwaka kwa gharama ya sh. bilioni 12/-, itachukua miaka 15 kumaliza tatizo hilo ili kuziba pengo lililopo sasa.

  “Nimepita kwenye banda la Taasisi ya Maajar Trust na pale wameniambia kuwa wameshatengeneza madawati 12,000 na kuyagawa katika mikoa sita. Wastani wa kila dawati ni sh. 120,000/- lakini inategemea na upatikanaji wa mbao pamoja na gharama za ufundi.”

  “Tukichukua gharama zao, tukaamua kutengeneza madawati 200,000 kwa mwaka, itatugharimu sh. bilioni 24 na itachukua miaka saba kumaliza tatizo hilo wakati tukiamua kutengeneza madawati 300,000 kwa mwaka, itatugharimu sh. bilioni 36 na itachukua miaka mitano kumaliza tatizo hilo,” alifafanua Waziri Mkuu.

  Alisema ni lazima hatua madhubuti zichukuliwe kumaliza tatizo hilo kwani inatia aibu na hakuna sababu ya kuendelea kuona wanafunzi wakisoma huku wamekaa chini.

  “Waziri wa Elimu na watu wako ni lazima mjifunge mkanda na kipaumbele chenu kiwe ni kupunguza tatizo la madawati katika muda mfupi sana; na itakuwa vema kama mtajipanga haraka ili mje na suluhisho ndani ya wiki hii kabla Mheshimiwa Rais hajaja kufunga maonyesho haya,” aliongeza.

  "Kaeni na watu wa Taasisi ya Maajar Trust muone ni kwa njia gani mnaweza kutatua tatizo hili… kama ni kuandaa chakula cha hisani ili kuchangia madawati fanyeni hivyo ili tatizo hili liishe. Wako Watanzania wanaweza kuchangia dawati moja, mawili, matatu au zaidi na tukajikuta tumemaliza tatizo hili,” alisema.

  “Na ninyi wa TAMISEMI kaeni na kuandaa utaratibu wa kuondoa tatizo hili. Kila Halmashauri kwa nafasi yake iwe ya mjini au ya vijijini ina uwezo wa kupunguza tatizo kulingana na fursa ilizonazo. Nasisitiza jambo hili liwe ni ajenda ya kudumu,” aliongeza.

  Wakati huohuo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Profesa Idris Kikula, akitoa shukrani kwa niaba ya wadau wa elimu alisema anaunga mkono hoja ya uchangiaji wa madawati na kusisitiza kuwa kuna haja ya watu kubadili mtazamo walionao kuhusu suala la uchangiaji wa huduma za kijamii.

  “Kuna watu ukiwaambia kuchangia madawati wanakataa lakini wako waliopokea kadi nyingi za michango ya harusi na wako tayari kuzichangia kwa sababu wanajua huko kuna kula na kunywa. Niwasihi wananchi tubadilishe mtazamo wetu na tuisaidie Serikali katika suala hili la madawati kwa watoto wetu,” alisema.

  (mwisho)

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 980,
  DODOMA.
  JUMAMOSI, MEI 4, 2014

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Askofu Mteule, Alen Legeza Siso, baada ya kumkabidhi Katiba na Kanuni za Kanisa la Methodist Tanzania, wakati wa Ibada Maalum ya Kuwekwa Wakfu (kusimikwa) askofu huyo, iliyofanyika kwenye Kanisa la Imanueli dhehebu la Methodox, Jimbo teule la Pwani na Mashariki lililopo Bunju Jijini Dar es Salaam, leo Mei 3, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia Waumini wa dini ya Kikristo wa Kanisa la Methodist Tanzania, wakati wa Ibada Maalum ya Kusimikwa Askofu Mteule Alen Legeza Siso, iliyofanyika kwenye Kanisa la Imanueli, Jimbo teule la Pwani na Mashariki lililopo Bunju Jijini Dar es Salaam, leo Mei 3, 2014. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Askofu Mkuu wa Kanisa la Methidist Tanzania, Dkt. Mathew Byamungu, baada ya Ibada maalum ya kusimikwa Askofu Mteule, Alen Legeza Siso, (kulia) kuwa Askofu wa Jimbo la Mashariki na Pwani iliyofanyika kwenye Kanisa la Imanueli, Jimbo hilo lililopo Bunju Jijini Dar es Salaam, leo Mei 3, 2014.
   Askofu Mkuu wa Kanisa la Methidist Tanzania, Mathew Byamungu, akimsimika Askofu Alen Legeza Siso, kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo la Mashariki na Pwani, Makanisa ya Methodist Tanzania, wakati wa Ibada Maalum ya kuwekwa Wakfu Askofu huyo iliyofanyika leo Mei 3, 2014, kwenye Kanisa la Emanueli lililopo Bunju jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimina na baadhi ya wachungaji wa Kanisa la Emanueli, Jimbo la Mashariki na Pwani, wakati alipowasili jimboni hapo kwa ajili ya kuhudhuria Ibada maalum ya Kusimikwa, Askofu Mteule, Alen Legeza Siso, jijini Dar es Salaam, leo Mei 3, 2014.
   Baadhi ya Waumini wa Kanisa hilo waliohudhuria Ibada hiyo maalum ya kumsimika Askofu Mteule, Alen Siso.  Makamu wa Rais wa Jamhiri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Askofu Mkuu wa Kanisa la  Methodist  Tanzania, Dkt. Mathew Byamungu, Askofu Mteule wa Jimbo la Mashariki na Pwani, aliyesimikwa, Alen Siso na baadhi ya wachungaji wa Kanisa la Emanuel, baada ya ibada maalum ya kusimikwa Askofu, Alen, leo Mei 3, 2014. 
  Kikundi cha Kwaya cha Msasani, kikitoa burudani wakati wa Ibada hiyo.
  Askofu Mkuu wa Kanisa la  Methodist  Tanzania, Dkt. Mathew Byamungu, akimvisha pete Askofu Alen Legeza Siso, ya kuashiria kuwa Askofo wa Kanisa hilo, baada ya kusimikwa rasmi wakati wa Ibada maalum iliyofanyika Kanisa la Emanueli lililopo Bunju jijini Dar Es Salaam, leo Mei 3, 2014. Picha na OMR

  ======  =======
  HOTUBA YA  MHESHIMIWA  DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL, MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KATIKA IBADA YA KUSIMIKWA ASKOFU  MTEULE ALEN SISO WA KANISA LA METHODIST TANZANIA- JIMBO TEULE LA MASHARIKI NA PWANI, DAR ES SALAAM, TAREHE 3.5.2014
  Mhe. Said Meck Sadiki, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam;
  Baba Dkt. Mathew Byamungu , Askofu Mkuu wa Kanisa la  Methodist  Tanzania ;
  Alen Siso, Askofu wa Jimbo Teule la Mashariki na Pwani;
  Mhe. Jordan Rugimbana, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni;
  Maaskofu na Wakuu wa Madhehebu mbalimbali  mliopo;
  Viongozi wa Serikali na Vyama vya Siasa mliopo hapa;
  Wawakilishi wa Mashirika na Wahisani mbalimbali;
  Ndugu Waandishi wa Habari;
  Waumini  wote mliohudhuria;
  Wageni Waalikwa;
  Mabibi na Mabwana;

  Bwana Yesu asifiwe! 
  Aawali ya yote, tuna kila sababu kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema , kwa kutupa uzima na kutuwezesha kukusanyika hapa siku  leo. Tuliopata kibali hiki, ni upendeleo wa aina yake, wapo  wenzetu wengi, wameshindwa kuiona siku ya leo, wengine wamelala hospitalini wakipigania uhai. Sisi tuliopata nafasi hii, tuna kila sababu, kumrudishia Mungu sifa na utukufu.
  Baba Askofu Mkuu;
  Ndugu  Waumini;
  Kabla sijaendelea, napenda niseme neno moja; Nimekuwa na bahati kubwa kusimama chini ya dari ya Kanisa la Methodist Tanzania. Nakumbuka ni mwaka jana, Aprili 27, mlinialika  katika Harambe na Ibada  Maalumu ya kumshukuru Mungu, kwenye  Kanisa la Methodist Tanzania, pale Msasani. Leo hii mmenialika tena  katika tukio hili la kihistoria, la kusimikwa Askofu Mteule Alen Siso. Nawashukuru sana, kwa moyo wa upendo na heshima kubwa mnayonipa.  Sina maneno mazito ya kushukuru, zaidi ya kusema ; Bwana azidi kuwatunza na kuwapigania !
  Nichukue fursa hii  kipekee, kukushukuru wewe binafsi Baba Askofu Mkuu Dkt. Byamungu, Watendaji wa Jimbo  Teule la Mashariki na Pwani, na Uongozi mzima wa  Kanisa la Methodist Tanzania,  kwa  mwaliko wenu wa leo. Nimeupokea kwa moyo mweupe, na  mikono miwili. Asanteni sana.
  Baba Askofu Mkuu;
  Ndugu waumini;
  Napenda nitumie nafasi hii, kulipongeza Kanisa la Methodist Tanzania, chini ya uongozi wako Baba Askofu Mkuu, Dkt. Byamungu , kwa namna mnavyoendelea kupanuka, sambamba na kuunga mkono juhudi za Serikali, kuwaletea wananchi wake maendeleo.
  Kwa mujibu wa maelezo, Kanisa la Methodist Tanzania, lilianza kutoa huduma ya kiroho hapa nchini, Juni 12 mwaka 1991. Leo hii  lina miaka 23 tu, lakini tumeona namna lilivyopiga hatua kubwa, kuchangia nyanja mbalimbali za maendeleo ya jamii.
  Ujenzi wa hospitali tano mkoani Geita, shule mkoani Arusha, uchimbaji visima virefu kwa shule na magereza  katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, na ujenzi wa Chuo cha Theolojia  huko Dodoma na Arusha, ni baadhi tu ya mambo mengi mema, yanayofanywa na kanisa hili. Kwa niaba ya Serikali, nawapongeza  kwa kazi kubwa mnayofanya. Tutaendelea kuwa karibu nanyi,   kwa kila jambo mtakaloona tunapaswa kushirikiana.
  Wageni Waalikwa;
  Mabibi na Mabwana;
  Napenda nipongeze pia, mchango mkubwa unaotolewa na mashirika na taasisi mbalimbali za dini hapa nchini, kusaidia juhudi za Serikali kuwaletea wananchi wake maendeleo. Taasisi na mashirika ya dini, yamekuwa mstari wa  mbele kujenga  shule, vyuo, hospitali na huduma zingine mbalimbali za jamii. Serikali peke yake haiwezi kufanya miujiza.Tunathamini na kutambua  mchango mkubwa  unaotolewa na mashirika na taasisi zote za dini .  Nawahakikishia kwamba, Serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu na mashirika haya, kwa maslahi ya maendeleo ya nchi yetu.
  Wito wangu kwa mashirika na taasisi za dini; Fanyeni kila linalowezekana, kuboresha  zaidi huduma zenu,  ili ziendane na ushindani  wa zama hizi. Hakikisheni mnakuwa na shule bora za kisasa zenye vifaa vya kutosha kufundishia, kadhalika hospitali zenu ziwe za kisasa , hata visima mnavyochimba, viwe na ubora wa unaotakiwa. Nawatia shime;  Kazi mnayofanya ni nzuri, endeleeni na moyo huo,  na Bwana atazidi kubariki kazi za mikono yenu.
  Baba Askofu Mkuu;
  Ndugu Waumini;
  Mabibi na Mabwana;
  Napenda kutumia nafasi hii kuwaasa Watanzania kudumisha amani na mshikamano wetu, ambao umekuwa tunu kubwa tangu tulipopata Uhuru. Ni juzi tu tumeadhimisha Miaka 50 ya Muungano wetu huku nchi yetu ikiendelea kuwa kisiwa cha amani na utulivu.  Katika hili, nawakumbusha watu wa Mungu kukesha na kuliombea  Taifa  letu. Si  watu wote wanafurahia mafanikio haya. Wapo wanaotuombea mabaya usiku na mchana, wanataka waone  siku moja tumefarakana na kupoteza mwelekeo. Naamini watu wa Mungu mkisugua goti katika hili, kamwe Shetani hatapata nafasi ya kujiinua katika Taifa letu. 
  Sisi katika Serikali, tutaendelea kusimamia kwa nguvu zote,  dhamana kubwa mliyotupa, ya kudumisha  Umoja na Mshikamano wa nchi yetu. Naamini kwa kuwa hata  Mungu wetu hafurahii mafarakano na utengano, ataendelea kusimama upande wa haki kutupigania. Tutaendelea kusimamia misingi ya utawala wa bora  bila kujali rangi ya mtu kabila, dini, jinsia  wala eneo analotoka.
  Baba Askofu Mkuu;
  Ndugu Waumini;
  Upendo ni sharti  muhimu sana katika maisha ya kila siku ndani ya jamii. Nilipozungumza nanyi mwaka jana huko Msasani, nilizungumzia hili, Napenda kurudia tena katika hadhara hii. Nazungumzia hili kutokana na mazingira ya mpito ambayo Taifa letu,  linapita kwa sasa. 
  Baba Askofu Mkuu, ni vigumu nchi yetu kuendelea kuwa na amani kama watu wetu hawapendani. Ni vigumu watu wetu kuendelea kukaa  pamoja  kama hawavumiliani. Ni vigumu nchi yetu kuendelea kuwa ya amani  na utulivu, kama watu wetu hawaheshimiani.  Bila Upendo na Kuvumiliana, Taifa letu litasambaratika.
  Tupo katika mchakato wa kuandika Katiba Mpya. Tulianzisha mchakato huu kwa nia njema ya kuwawezesha Watanzania kupata Katiba, inayoendana na  mazingira ya sasa. Tofauti na ilivyotarajiwa, mchakato huu umeanza kugubikwa na malumbano huku baadhi ya Wabunge wa Bunge Maalumu la Katiba, wakitangaza  kususa vikao. Kukosekana Upendo, ni moja ya sababu  kuu ya kushindwa kuvumiliana, hata katika mijadala ya Bunge la Katiba.  
  Ndani ya Biblia takatifu,  Kitabu cha Wakorintho wa Kwanza, mlango wa 13, mstari wa 4  hadi 8, kimezungumza  vizuri sana kuhusu Upendo; nitanukuu:-“Upendo huvumilia, hufadhili, upendo hauhusudu, upendo hautakabari, haujivuni, haukosi kuwa na adabu, hautafuti mambo yake, hauoni uchungu,hauhesababu mabaya, haufurahii udhalimu bali hufurahi pamoja na kweli, huvumilia yote, hustahimili yote,  upendo haupungui neno wakati wowote… Ukiendelea mstari wa 13, unahitimisha kwa kusema:-  “Basi sasa inadumu imani, tumaini , upendo  haya matatu;  na katika hayo,  lililo kuu ni  UPENDO.”
  Pia Maandiko matakatifu katika Waraka wa Kwanza wa Petro Mtume, mlango wa 4, mstari wa 8  hadi 10, yanasema hivi; nitanukuu:-” Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana kwasababu upendano husitiri wingi wa dhambi. Mkaribishane ninyi kwa ninyi pasipo kunung’unika  kila mmoja kwa kadri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu.”
  Nawasihi waumini wa dini zote nchini, kuzidi kuombea jambo  hili , ili mchato huo, ufikie hatma njema kama ilivyokusudiwa. Nawakumbusha pia  Wabunge wa Bunge Maalumu la Katiba, watakaporejea Agosti mwaka huu, kujenga upendo miongoni mwao , wakumbuke kwamba wanawakilisha mamilioni ya Watanzania. Biblia imetuambia kuwa wakijenga upendo, Watavumiliana, hawatahesabiana mabaya,  hawatapenda udhalimu na wala hawatakoseana adabu.
  Baba Askofu Mkuu;
  Viongozi wa dini mbalimbali mliopo;
  Ndugu Waumini;
  Jukumu mlilotupa la kuongoza Watanzania,  haliwezi kuwa na tija, kama wananchi tunaowaongoza, hawatamjua  Mungu na kufuata mafundisho yake.  Watu wetu wakimjua Mungu hawatatoa wala kupokea rushwa, hawatauza wala kutumia dawa za kuleva, hawatajichukulia sheria mikononi, hawataiba wala kudhulumu, hawatajilimbikizia mali,  hawatatega kazini, watakaa mbali na uasherati  na maovu mengine yote. Taifa la wacha Mungu lina  amani , upendo, umoja na mshikamano. Hivyo lina nafasi  kubwa ya kusonga mbele. Lakini ni kazi ngumu sana kuongoza Taifa la watu waliotekwa na ibilisi.
  Natoa changamoto kwa viongozi wa dini zote nchini, kuhakikisha  mnawajengea waumini  wenu, misingi ya madili mema. Waumini wenu wakifuata mafundisho ya Mungu, Taifa litakuwa na raia wema, wachapakazi, maovu ndani ya jamii yatapungua sana kama si kumalizika kabisa.
  Vilevile nitumie nafasi hii, kuwakumbusha waumini wa dini zote nchini, kuendelea kuvumiliana, kuheshimiana na kupendana. Ni wajibu wa kila mmoja wetu, kuheshimu dini ya  mwenzake. Hakuna dini bora kuliko nyingine, dini zote ni sawa, tofauti yake, ni taratibu za namna ya kuabudu. Tofauti hizi haziondoi haki yetu ya kuwa watoto wa Baba mmoja Mungu,  walio katika nyumba moja ambayo ni Tanzania. Pendaneni, kwani maandiko matakatifu, yanatufundisha kuwapenda hata maadui wanaotuudhi.
  Kitabu cha Mathayo, mlango wa 5, mstari wa 43 hadi 45  unasema hivi,nanukuu;  “Mmesikia kwamba imenenwa umpende jirani yako, na umchukie adui yako, lakini mimi nawaambia, wapendeni adui zenu , waombeeni wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni, maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema , huwanyeshea mvua wenye haki na wasio na haki.”
  Baba Askofu Mkuu;
  Ndugu Waumini;
  Mabibi na Mabwana;
  Nitumie nafasi hii kukupongeza Baba Askofu Alen Siso, kwa namna Mungu alivyokuinua, hatimaye leo umesimikwa rasmi kuwa Askofu wa Jimbo Teule la Mashariki na Pwani. Naamini kuchaguliwa kwako, hakukuja kwa bahati bali “BWANA AMEKUCHAGUA, NA  ANA HAJA NAWE.”
  Baba Askofu Siso, tukio hili kwako, ni ile  sauti iliyoandikwa katika Kitabu cha nabiiIsaya mlango  6 mstari wa 8, ikisema kwamba, nanukuu; “ Kisha nikasikia sauti ya Bwana akisema, Nimtume nani, naye ni nani atakayekwenda kwa ajili yenu? Ndipo niliposema. Mimi hapa, nitume mimi.” 
  Ujumbe huu umeelezwa pia katika Injili ya  Luka , mlango wa 12,  mstari wa 42 hadi wa 43,  nanukuu; Bwana akasema, ni nani basi aliye  wakili mwaminifu, mwenye busara, ambaye Bwana wake atamweka juu ya utumishi wake wote, awape watu posho kwa wakati wake?
  Baba Askofu Siso, mistari niliyoisoma hapo juu ni ushahidi kwamba umepokea utumishi huu kwa Kuitwa na Kuitika. Sisi sote tuliokusanyika hapa leo, ni mashahidi.  Ifanye kazi ya Mungu kwa moyo mmoja. Naamini utakuwa mchungaji mwema, utakaowachunga kondoo wa Mungu, na kuwarudisha zizini wale waliopotea.
  Ndugu Waumini;
  Mabibi na Mabwana;
  Niwaombe viongozi wote wa kanisa hili, kuanzia wewe Baba Askofu Mkuu, Dkt. Byamungu, kuzidisha mshikamano miongoni mwenu, na kumsaidia Askofu wetu mpya, kufanya kazi hii takatifu kwa ufanisi.  Zingatieni  maneno ya Mungu kutoka Waraka wa Kwanza wa Petro Mtumemlango wa 5, mstari  wa 2 hadi wa 4, nanukuu ;“Lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa bali kwa hiyari, kama Mungu atakavyo,si kwa kutaka fedha ya aibu bali kwa moyo, wala si kama wajifanyao mabwana juu ya mitaa yao, bali kwa kujifanya vielelezo kwa lile kundi.”

  Baba Askofu Mkuu Byamungu;
  Askofu Siso;
  Ndugu Waumini;
  Mabibi na Mabwana;
  Kabla ya kuhitimisha hotuba yangu, napenda kuwahakikishia kuwa,  nimepokea changamoto zenu mbalimbali mlizosoma  kwenye risala yenu. Nimesikia matatizo yenu ya maeneo ya kujenga miradi. Serikali kupitia mamlaka zake, itafuatilia kwa karibu masuala hayo, kuangalia namna bora ya kuyapatia ufumbuzi.
  Baada ya kusema hayo, kwa mara nyingine, napenda kukushukuruni kwa kunialika mahali hapa siku ya leo. Nazidi kuwasihi sana watu wa Mungu, msichoke kuliombea Taifa letu, kwani kuna nguvu kubwa ndani  ya maombi. Kemeeni  njama zote zenye nia mbaya ya kuvuruga Amani, Umoja na Mshikamano wetu.  Daima, pendeni kusikiliza mema, msivutike kusikiliza maovu . Nawaachia ujumbe kutoka Kitabu cha Mithali,  mlango wa 11, mstari wa 31 hadi 32, unasema hivi; “ Kinywa cha mwenye haki hutoa hekima, bali ulimi wa ukaidi utakatiliwa mbali. Midomo ya mwenye haki huyajua yatakayokubaliwa, bali kinywa chao wasio haki hunena ukaidi.”
   Mungu awabariki sana.  Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.


  0 0


   Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi uliofanyika jioni ya leo kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba.Katika hotuba yake,Ndg. Kinana amewataka Wananchi wa Kisiwani humo,kutohadaika na Wanasiasa wanapita kila mahali kwa lengo la kulipotosha Taifa,hasa juu ya swala la Muundo wa Serikali katika Mchakato wa Katiba Mpya.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akiendelea kuwahutubia wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi uliofanyika jioni ya leo kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba.
   Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar,Ndg. Vuai Ali Vuai akizungumza na wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi uliofanyika jioni ya leo kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba.
   Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye akiwapa somo wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi,uliofanyika jioni ya leo kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba.
   Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye akiendelea kuzungumza.
  Makamu Mwenyekiti UWT,Bi. Asha Bakari Makame akizungumza kwa msisitizo mkubwa na wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi,uliofanyika jioni ya leo kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba.

  Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar,Ndg. Shaka Hamdu Shaka akizungumza machache na wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi,uliofanyika jioni ya leo kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba.

  Vijana wa CCM, Fatma Juma Ramadhan (kushoto) na Halima Juma Hajj wakighani mashairi mazuri ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana (hayupo pichani).
  Sehemu ya picha mbali mbali za wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba wakifuatilia Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi,uliofanyika jioni ya leo kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba.


  Sehemu ya picha mbali mbali za wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba wakifuatilia Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi,uliofanyika jioni ya leo kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba.Picha zote na Othman Michuzi

  0 0

  Mwimbaji Mahiri wa muziki wa nyimbo za Kiroho a.k.a Injili,Rose Muhando akiimba wimbo wake mpya wa Facebook na Twitter mbele ya mashabiki wake,katika uwanja wa Kambarage mapema jioni ya leo mkoani Shinyanga,ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa tamasha la Pasaka.Tamasha hilo linaloandaliwa na Msama Promotions Ltd  kesho jumapili linaendelea katika uwanja wa CCM Kirumba jijiini Mwanza,ambapo Nyota wa Nyimbo za Injili kutoka nchini Afrika Kusini,Rebecca Malope atawatumbuiza wakazi wa jiji hilo sambamba na waimbaji wengine..
   Mwimbaji wa nyimbo za Injili,Upendo Kilahiro akiimba mbele ya wapenzi wa muziki wa injili ndani ya uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
    Sehemu ya wapenzi wa muziki wa injili wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo.

   Upendo Nkone,ambaye amejizolea sifa kubwa kwa kuimba nyimbo za kusifu na kuabudu,akiwaimbisha mashabiki ba wapenzi wa muziki wa injili ndani ya uwanja wa kambarage jioni ya leo.
   Pichani kulia ni Mwimbaji wa nyimbo za Injili,Upendo Kilahiro akiimba jukwaani huku akiungwa mkono na waimbaji wenzake wa muziki huo,anaefuta ni Tumaini Njole,Faraja Ntaboba kutoka nchini Congo DRC na Mess Chengula.
   Muziki wa Injili ulikuwa umekolea hapa.
  Mwimbaji wa nyimbo za injili, Faraja Ntaboba kutoka nchini Congo DRC akiimba kwa hisia kubwa mbele wakazi wa mji wa shinyanga waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo la muendelezo wa pasaka,ambapo leo Jumapili watatumbuiza kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. 
   Walioguswa na nyimbo za injili walinyoosha mikono hewani
   Mdauu akifurahia jambo huku akiendelea kuunza dvd za wasanii wa nyimbo za injili

  0 0

   Tingatinga la Mamraka ya ustawishaji makao makuu [CDA] likibomoa moja ya nyumba zilizopo katika hifadhi ya Barabara inayotarajiwa kuanza kujengwa havi karibuni, ambapo zaidi ya nyumba 65 zilibomolewa katika eneo hilo la mlamwa kusini.

   Wanawake wa mtaa wa Mlimwa wakimsaidia Mwenzao aiyezilai baada ya Tingatinga la CDA kufika kwa ajili ya kubomoa nyumba yake kwa ajili ya kupisha ujenzi wa Barabara, zoezi hilo lilifanyika Jana ambapo nyumba zaidi ya 65 zilibomolewa na kuacha familia zaidi ya 150 zikikosa makazi.
   Mwenyekiti wa mtaa huo Zubeda Haji akielekeza jambo wakati wa ubomoaji huo.
   Wananchi wa Mlimwa waking'oa mabati muda mfupi kabla ya Tinga tinga la CDA kufika na kuibomoa nyumba hiyo ili kupisha hifadhi ya Barabara
    Bibi huyu mkazi wa Mlimwa Kusini ambaye hakufahamika jina lake akiwa hajui la kufanya baada ya nyumba yake aliyokuwa akiishi iliyojengwa kwa mtindo wa Tembe huku akiachwa na vyombo vyake alivyoweka kwenye shamba la mahindi baada ya CDA kufanya uvunjaji huo kwa nyumba zote zilizopo katika hifadhi ya Barabara.
  Wananchi wa Mlimwa kusini wakiwa katika hekaheka ya kuhamisha mizigo yao na kukimbia nyumba zao baada ya kupata taarifa za ujio wa Tinga tinga la CDA kwa ajili ya kubomoa nyumba zao ili kupisha ujenzi wa barabara.

  PICHA NA JOHN BANDA WA PAMOJA BLOG


  0 0

   Wafanyakazi wa VETA Makete wakiwa katika picha na watoto yatima wa kituo cha Bulongwa.
   Mfanyakazi wa VETA Makete akiwa amembeba mtoto yatima anayelelewa kituoni hapo
   Sanga akiwa amembeba mtoto yatima anayelelewa katika kituo cha Bulongwa
   Wakifurahia pamoja na watoto hao kwa kuimba nyombo.
   Wakiwa katika picha ya pamoja nje ya kituo hicho.
   Methew Komba akiwa amembeba mtoto yatima
   watoto wakifurahia kutembelewa na wafanyakazi wa VETA Makete.
   Hapa mmoja wa wafanyakazi wa VETA Makete akicheza na watoto hao.
  ---------
  Kufuatia wilaya ya Makete mkoani Njombe kuwa miongoni mwa wilaya zenye watoto yatima, wafanyakazi wa chuo cha VETA Makete wametembelea kituo cha kulelea watoto yatima cha Bulongwa kilichopo wilayani hapa na kutoa misaada mbalimbali

  Akizungumza na mwandishi wetu kwa niaba ya wafanyakazi wenzake alioambatana nao Bw. Mathew Komba amesema wao kama VETA Makete wameguswa na namna watoto hao wanavyopata tabu kwani hawakupenda kuishi maisha hayo lakini kutokana na kufiwa na wazazi wao ndiyo maana wapo katika kituo hicho

  Amesema awali walikuwa wamepanga kuwatembelea watoto hao kabla ya pasaka lakini kutokana na sababu zisizoepukika walishindwa kufanya hivyo lakini walijipanga kama walivyokuwa wamedhamiria na jana walifika kituoni hapo kuwaona watoto hao na kuwapa msaada huo

  Bw. Komba amesema baadhi ya vitu walivyovikabidhi ni pamoja na mafuta ya kupikia, sukari, mchele, sabuni, juisi, dawa za meno na vingine vingi vyote vikiwa na thamani ya tsh. 329,000/=

  Amewaomba wadau wengine kuwaunga mkono kwa kwenda kuwasaidia watoto yatima kwani ni jukumu la jamii kwa ujumla kuhakikisha wanawatunza watoto hao licha ya kwamba wanalelewa kwenye vituo mbalimbali

  Kwa upande wake Bi Sekela Nkyami kutoka kituo hicho cha kulelea watoto yatima Bulongwa amesema ingawa kituo hicho kina vitega uchumi mbalimbali lakini bado kinategemea misaada kutoka kwa wafadhili mbalimbali wakiwemo wakazi wa Makete wenye moyo wa huruma kama walioufanya chuo cha VETA

  Amesema watoto hao waliopo katika kituo hicho si mali ya kituo pekee bali ni wa jamii yote kwa hiyo kuiomba jamii kushirikiana nao katika matunzo ili watoto hao wasijisikie wapweke kutokana na uyatima walio nao

  "Ni kweli uyatima unatesa, ila tunawaomba wananchi waje kutoa misaada mbalimbali kwa watoto hawa, kumekuwa na kasumba kuwa wakishaletwa hapa basi si wao tena bali ni wa kituo, hii sia sawa bali tunatakiwa tushirikiane kwa pamoja chochote kidogo utakachokipata kinatosha kutusaidia" amesema Bi. Nkyami

  Na Edwin Moshi, Makete

  0 0

  Marcos Maidana punches as Floyd Mayweather Jr. defends during their fight at MGM Grand.
  Bondia Floyd Myweathe kushoto akipangua ngumi ya Marcos Maidana wakati wa mpambano wao uliochezwa alfajili ya kuamkia leo point za majaji, Judge Michael Pernick scored it 114-114, a draw. Bert Clements had it 117-111 and Dave Moretti score it 116-112
  Floyd Mayweather Jr. punches Marcos Maidana during their fight at MGM Grand.
  Bondia Floyd Myweather kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Marcos Maidana wakati wa mpambano wao uliochezwa alfajili ya kuamkia leo point za majaji, Judge Michael Pernick scored it 114-114, a draw. Bert Clements had it 117-111 and Dave Moretti score it 116-112.
  Mabondia wa Tanzania Kalama Nyilawila kushoto,Rashidi Matumla na Fransic Cheka wakifatilia kwa makini mpambano huo uliochezwa alfajili ya leo katika ukumbi wa Igo Lounge sinza mapambano walipokuwa wakionesha live kupitia luninga kubwa kwa mashabiki wa mchezo huo
  Marcos Maidana defends against Floyd Mayweather Jr. during their fight at MGM Grand.
  Bondia Floyd Myweather kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Marcos Maidana wakati wa mpambano wao uliochezwa alfajili ya kuamkia leo point za majaji, Judge Michael Pernick scored it 114-114, a draw. Bert Clements had it 117-111 and Dave Moretti score it 116-112   TANGAZO LIKIONESSHA KUWEPO KWA NGUMI ZA LIVE KUPITIA LUNINGA
  Mabondia Rashid Matumla kushoto,Fransic Cheka na Kalama Nyilawila wakifatilia mpambano wa Myweather na Maidana kupitia luninga katika ukumbi wa Igo lounge sinza mapambano leo picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
  makamu wa rais Shirikisho la ngumi za ridhaa nchini (BFT)?  Anderson Lukelo, mabondia Rashid Matumla kushoto,Fransic Cheka na Kalama Nyilawila wakifatilia mpambano wa Myweather na Maidana kupitia luninga katika ukumbi wa Igo lounge sinza mapambano leo wakiwa na wadau mbalimbali wa masumbwi nchini picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
  mashabiki wakifurahia mchezo wa ngumi kupitia luninga
  MYWEATHE NA MAIDANA WAKIPAMBANA LIVE KATIKA LUNINGA
  Bondia Fransic Cheka akitoa tasmini ya mchezo ulivyokuwa baada ya myweathe kutangazwa mshindi
  Bondia Kalama Nyilawila akitoa tasmini ya mchezo ulivyokuwa baada ya myweathe kutangazwa mshindi
  wadau mbalimbali wakipiga picha na cheka picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com

  Na Mwandishi Wetu

  MABONDIA mbalimbali alfajili ya kuamkia leo wamejitokeza kuangalia mpambano uliokuwa ukifanyika Marekani kati ya bondia Floyd Myweather na Marcos Maidana  mpambano uliokuwa unafanyika katika ukumbi mkubwa kabisa wa ngumi duniani MGM grand

  ambapo hapa nchini mabondia Rashidi  Matumla, Kalama Nyilawila pamoja na Fransic Cheka namakamu wa rais Shirikisho la ngumi za ridhaa nchini (BFT)?  Anderson Lukelo pamoja na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' 

  walijumuika kwa pamoja kuangalia mpambano huo live katika ukumbi wa 
  Igo lounge uliopo  sinza mapambano

  mpambano huo ulikuwa mkali ambao dunia nzima ya wapenda mchezo wa ngumi walikuwa wakisubili kwa hamu kuangalia wakali hawo wa masumbwi wanavyo oneshana umwamba

  hata hivyo mpaka dakika ya mwisho ya mpambano huo ulisha kwa bondia Floyd Myweather kushinda kwa pointi za majaji wawili na mmoja wa majaji akitoa droo mpambano huo
  Michael Pernick scored, 114-114, a draw. Bert Clements , 117-111 and Dave Moretti , 116-112 

  wakizungumzia mpambano huo walio uona live kupitia luninga bondia Rashid Matumla alisema wenzetu wana uwezo mkubwa sana katika masumbwi ata katika kujaji maidana alikuwa anacheza fujo tu katika mchezo huu hivyo ndio kitu kilicho mnyima ushindi

  nae cheka aliongeza kwa kusema siku zote bingwa analindwa sana hivyo myweather ameweza kutetea taji lake vizuri

  nae kalama amesema mambo haya yanatokea kila siku mana nakumbuka zama za Tyson ndio watu walikuwa wanajazana namna hii kuamka alfajili kuangalia ngumi sasa myweather anatisha kachukua urithi wa Tyson huyu bondia ni mzuri kwa jkutembea awapo ulingoni kacheza vizuri nimemfurahia

  0 0

   The President of United Republic of Tanzania, Hon. Dr. Jakaya M. Kikwete with Ms. Fatma Fernandes, Managing Director of Abel & Fernandes Communications who bought the auctioned painting to show support at the Kilimanjaro Challenge Launch which has been sponsored by Geita Gold Mine (GGM) in partnership with Tanzania Commissions for AIDS (TACAIDS) to raise funds to fight against HIV/AIDS in Tanzania. 
  The President of United Republic of Tanzania, Hon. Dr. Jakaya M. Kikwete with the two children from Moyo wa Huruma Orphanage Centre who will join other climbers locally and internationally for the Kilimanjaro Challenge which has been sponsored by Geita Gold Mine (GGM) in partnership with Tanzania Commissions for AIDS (TACAIDS) to raise funds to fight against HIV/AIDS in Tanzania. 
    The team from Tanzania Commision for AIDS (TACAIDS) at the Kilimanjaro Challenge Launch which has been sponsored by Geita Gold Mine (GGM) in partnership with Tanzania Commissions for AIDS (TACAIDS) to raise funds to fight against HIV/AIDS in Tanzania.

  =====  ======  =====
  THE KILIMANJARO CHALLENGE AGAINST HIV and AIDS 2014


  Geita Gold Mine (GGM) in partnership with Tanzania Commission for AIDS (TACAIDS) officiated yet another year of Kilimanjaro Challenge at Hyatt Kilimanjaro Hotel in Dar es Salaam, Tanzania. The Kili Challenge was officiated by the President of the United Republic of Tanzania Hon. Dr. Jakaya M. Kikwete. The launch involved the naming and disbursing of funds to local organizations.


  The Kilimanjaro Challenge is an annual activity that aims to raise funds from different partners through sponsorship of climbers to Mount Kilimanjaro and to distribute the funds to relevant charities fighting HIV/AIDS in Tanzania. The annual climb was initiated in response to former President Benjamin Mkapa’s 1999 call to the entire nation, including the private sector, to commit itself to the fight against HIV/AIDS in Tanzania.


  During his opening speech at the launch of Kili Challenge 2014, the President Hon. Dr. Jakaya M. Kikwete said, “I am honored to officiate the launch of Kilimanjaro Challenge which will raise charity funds that have already continued to benefit both national and local level development initiatives focusing on HIV/AIDS treatment and prevention in Tanzania. 

  The government would like to applaud this initiative by Geita Gold Mine (GGM) and Tanzania Commission for AIDS (TACAIDS) as the Kili HIV/AIDS Challenge has contributed towards raising awareness on the HIV/AIDS pandemic and is supporting the Tanzanian government’s national initiatives towards zero new infections, zero stigma incidences and zero mother to child infections so that as a country we meet our Millennium Development Goals.”


  According to the Executive Director of TACAIDS Dr. Fatma Mrisho, “Approximately 1.6 million people in Tanzania are living with HIV and AIDS and about 86,000 new infections every year. This pandemic is mostly affecting the youth of Tanzania and the disease has orphaned 1.3 million children. We need to change this therefore TACAIDs in collaboration with GGM and other various stakeholders through Kilimanjaro Challenge, we will continue to provide financial support in order to fight against this pandemic.”  She continued to say, “We hope to build a national team spirit in the fight against this menace and I urge other stakeholders from local and international investors to come forward, join us and contribute to the Kilimanjaro Challenge fund so that we can meet our dream of having a zero free generation from HIV and AIDS.”


  Speaking in regard to the event, the Managing director for GGM Mr. Michael Van Anen said “GGM is proud to be part of this initiative where various companies which are working locally, could join forces and participate in this noble course. GGM leads this initiative by establishing relationships and mobilizing key likeminded partners to raise funds, sponsor individual climbers, or donate through an auction for this cause. 

  Currently in its 13th year, the difference in life changing in the communities is enormous and we are looking forward for an HIV/AIDS zero Tanzania in the near future.” He continued to say, “I would like to urge anyone who would like to join us to visit www.geitakilichallenge.com and see how they can be part of this great initiative.”


  AngloGold Ashanti Sustainability Vice President Mr. Simon Shayo said “Since Kilimanjaro Challenge initiative started 12 years ago, more than 600 people from different parts of the world have participated to climb Mt. Kilimanjaro for this noble cause which have raised in excess of US$500,000 per annum. 

  The fund have benefited over 30 NGO countrywide in order to fight against HIV and AIDS in Tanzania. Institutions which had no funds to operate get relieved with these funds from Kili Challenge; Children, who had lost their parents due to HIV and AIDS, are now finding care and love and can smile again. We would like to acknowledge some of our participating partners, including but not limited to CAPITAL DRILL, AKO, Wambi Oil, Mantrac, Prime Fuel, African Barrick Gold, Airtel, Southern Sun, ZARA, MACS, AUSDRILL and other valued supporters. It is because of you that this noble fight against HIV and AIDS continues hence ensuring the success and continuity of this annual event,” He concluded.


  Geita Gold Mine and TACAIDS using the umbrella of Kilimanjaro Challenge is playing a pioneering role in the awareness on the HIV and AIDS pandemic and look forward for the day when Tanzania will be declared Zero HIV and AIDS infection as it is reported that Tanzania’s prevalence rate has gone down from over 13% in 2000 to 7.8% by 2007 and as low as 5.1% today.  0 0

  Mbunge wa jimbo la Nzega Mkoani Tabora kupitia CCM, Hamis Kigwangala, ametanabaisha kuwa anatafakari kama anaweza kugombea Urais kwenye uchaguzi mkuu ujao kupitia chama cha mapinduzi CCM.

  Akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua fununu zilizo enea kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii ambayo imekuwa ikiibua mijadala mara kwa mara inayomshawishi kugombea Urais mwaka 2015, Dk. Kigwangala amesema anatafakari jambo hilo zito na kuongeza kuwa muda utakapofika atayazingatia maoni ya wananchi.

  Akizungumzia maelezo kwamba haoni kama ni hatari kwake kutangazwa mapema kwamba anataka kuwa kugombea Urais ni kujipunguzia sifa katika chama chake, Dk. Kigwangala alisema yeye hajatangaza kama anataka Urais na wala hajamtuma mtu kuanza kumfanyia kampeni, kwani watanzania wanaongozwa na katiba yenye Uhuru wa kujieleza na kutoa maoni, hivyo hayo ni mawazo yao na wana haki ya kufanya hivyo na yeye binafsi hawezi kuwapinga.

  Hivi karibuni kumeibuka mijadala mizito kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya wanaharakati kutengeneza vuguvugu la kumshawishi Dk. Kigwangala kuchukua fomu ya kugombea Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ifikapo mwaka 2015.

  Mijadala hiyo mizito imeanzishwa katika mitandao ya Internet na simu za mkononi walio ipachika jina "Citizens for Kigwangala" ambapo katika mijadala hiyo wamekuwa wakishawishiana na kumwagia sifa Dk Kigwangala kwamba ndiye kiongozi pekee anayefaa kuwakilisha chama cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu ujao.

  Baadhi ya vijana wamekuwa wakijadili kuwa Dk Kigwangala ndiye anayeweza kuleta upinzani wa kweli kwa vyama vya upinzani, wakijenga hoja kuwa amekuwa na misimamo na uwezo wa kujieleza kwa ufasaha ndani ya vikao vya bunge.

  Dk Kigwangala ni mbunge wa jimbo la Nzega mkoani Tabora, mwenye taaluma ya udaktari wa tiba ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya tawala za mikoa na serikali za mitaa.

  0 0

   Mgeni ambaye ni mwenyekiti wa ccm mkoa wa Iringa  Jesca Msambatavangu akizungumza na wazazi na wanafunzi wa shule ya shule ya sekondari ya wasichana Iringa katika ukumbi wa shule hiyo hivi karibuni.
   Baadhi ya wahitimu wa kidato cha sita wa shule ya sekondari ya wasichana wakiwa katika mahafali yao
   Mwanafunzi bora wa kidato cha sita Asderia Sanga akikabidhiwa zawadi na mgeni rasmi Jesca Msambatavangu.

  ======  ======
  Na Denis Mlowe,Iringa
   
  WANAFUNZI wa kike wanaotarajiwa kuhitimu elimu ya kidato cha sita wameaswa kujiamini,kujitambua na kufahamu wajibu wao kwa jamii inayowazunguka kwa kutokukimbilia kuolewa kwa lengo la kujikomboa kifikra na kiuchumi na kutimiza ndoto za maisha yao.
   
  Ushauri huo ulitolewa mwishoni mwa wiki na mgeni rasmi Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa, Jesca Msambavangu,wakati wa harambee na mahafali ya 22 ya shule ya sekondari ya wasichana ya Iringa na kufanyika katika ukumbi wa shule hiyo mjini hapa.
   
  Msambavangu alisema imeibuka kasumba kwa wanaume wengi kukimbilia kwa wasichana wadogo na kuwaharibia maisha yao kabla hawajatimiza ndoto zao za maisha kutokana na kupewa ujauzito na wanaume wenye nia mbaya na maisha ya mabinti.
   
  Alisema ndoto nyingi za wasichana zinakatishwa na wanaume wakware na wasichana wengi wanamalengo ambayo wanataka kutimiza lakini kutokana na mabadiliko ya haraka kwa watoto wa kike yanaweza kukuletea madhara kuliko faida na kuwataka kukazania masomo.
   
  “Asilimia kubwa ya wazazi wanataka mtoto wao asome afikie ngazi kubwa kama baadhi ya viongozi wa kike waliomadarakani lakini kwa tamaa za chips kuku wengi wenu mmekuwa mkiishia njiani, nawaomba sana watoto wangu msiende njia ambayo wakware watawadanganya na kuzimisha ndoto zenu za kuwa madaktari, walimu na viongozi wa baadaye someni sana” aliwaasa Msambavangu.
   
  Amewataka wanafunzi hao kutambua thamani yao kuepuka kutumiwa vibaya na kushinda majaribu ya watu wanaotaka kuwavurugia safari ya maisha waliyoanza nayo tangu wakiwa wadogo kwa kuwakataa wanaume wenye fedha na wasiona fedha kwa kuongwa vitu vidogo vidogo vikiwemo simu na nguo.

  Aidha aliwataka kuacha tabia ya wanafunzi kuchukua muda wao mwingi kwenye mitandao ya kijamii kwa kufuatilia mambo yasiyo na msingi kwao na badala yake watumie mitandao hiyo kwa manufaa yao kielimu.
   
  Katika harambee ya kuchangia ununuzi wa gari la shule Msambatavangu alichangia shilingi milioni 1.5 na kiasi kilichopatikana kilikuwa shilingi milioni 4 .6 kati ya shilingi milioni 25 zinazohitajika.

  Awali mkuu wa shule hiyo Joyce Msigwa aliwashukuru wazazi wa wanafunzi kwa michango yao na kuongeza kuwa kuna changamoto kubwa ya usafiri wa wanafunzi katika shule hiyo na wanatarajia kukusanya fedha hiyo kuweza kuondokana na hali hiyo na kuwatakawadau kuwachangia kiasi cha fedha kilichobaki.
   
  Alisema kuwa wanafunzi wanakabiliwa na wakati mgumu inapojitokeza dharula katika kutekeleza majukumu ya shule na wanafunzi wanapohitaji gari wakipatwa na matatizo hususani katika kipindi cha ugonjwa.
   
  “Tunaomba wadau mbalimbali, wazazi na makampuni mbalimbali kutuchangia katika ununuzi wa gari la wanafunzi ambalo bei yake ni kubwa hivyo tunategemea sana misaada kutoka kwao na waandishi tunaomba sana mtusaidie kufikisha ujumbe kwa jamii kuweza kuwakomboa hawa mabinti wawe na usafiri wao yaliyokuwepo yote yameharibika” alisema Msigwa

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Unguja waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa hadhara wa Chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika jioni ya leo kwenye Uwanja wa Demokrasia uliopo eneo la Kibanda Maiti,Mjini Unguja Zanzibar.

  Maelfu ya  Wananchi wakishangilia huku wakionyesha ishara ya serikali mbili, wakati wa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwenye Viwanja vya Kibandamaiti mjini Zanzibar jioni ya leo.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd akiwasalimia wananchi wa Unguja waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa hadhara wa Chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika jioni ya leo kwenye Uwanja wa Demokrasia uliopo eneo la Kibanda Maiti,Mjini Unguja Zanzibar.
  Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar,Hayati Aman Karume,Mama Fatma Karume akiongea kwa msisitizo mkubwa huku akiwataka Wazanzibar kuacha kabisa kuuchezea Muungano kwa kuwafuata watu wanaoupotosha.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akimpongeza Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar,Hayati Aman Karume,Mama Fatma Karume mara baada ya kuzungumza na wazanzibar jioni ya leo waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Demokrasia ,Kibada Maiti mjini Unguja.

  Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye akiwaeleza wananchi wa Unguja kuhusu umoja ulioanzishwa wa baadhi ya vyama vya siasa na malengo ya umoja huo,wakati wa Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi,uliofanyika jioni ya leo kwenye Uwanja wa Demokrasia uliopo eneo la Kibanda Maiti,Mjini Unguja Zanzibar. 
  Mbunge wa Viti Maalum CCM,Mh. Ummy Mwalimu akiwahutubiwa wananchi wa Zanzibar kupitia Mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika kwenye Uwanja wa Demokrasia uliopo eneo la Kibanda Maiti,Mjini Unguja Zanzibar jioni ya leo,ambapo amewataka Wazanzibari kutohadaishwa na UKAWA kuhusu swala la muundo wa Serikali katika mchakato wa Katiba.
  Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini,Mh. Emmanuel Nchimbi akinukuu sehemu ya maandishi yaliopo kwenye kitabu cha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,Maalim Seif Sharif Hamad wakati wa Mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika jioni ya leo kwenye Uwanja wa Demokrasia uliopo eneo la Kibanda Maiti,Mjini Unguja Zanzibar.


older | 1 | .... | 279 | 280 | (Page 281) | 282 | 283 | .... | 1898 | newer