Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

MSIKILIZE ALIYEKUWA MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA JOSEPH WARIOBA ALIPOONGEA NA ITV KATIKA DAKIKA 45


MWENDELEZO WA TAMASHA LA PASAKA;MWANAMUZIKI REBECCA MALOPE KUTUMBUIZA MEI 4 JIJINI MWANZA

$
0
0


MALKIA wa muziki wa Injili nchini Afrika Kusini, Rebecca Malope anatarajiwa kutua kwenye jiji la Mwanza a.k.a ROCKY CITY  Mei 4,ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa Tamasha la Pasaka 2014

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama amesema kuwa Nyota huyo wa muziki wa nyimbo za Kiroho,ni miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza kwenye Tamasha hilo,ameeleza kuwa msanii huyo alipata kura nyingi kutoka kwa mashabiki waliompendekeza kutumbuiza jijini humo.

“Tunashukuru kwamba baada ya mapendekezo ya mashabiki tuliwasiliana na Rebecca ambaye ameonesha uungwana wa hali ya juu na kutukubalia ombi letu. 

“Lakini pamoja na kukubali ana ratiba ya maonesho sehemu nyingine huko kwao, hivyo ametuambia hatatumbuiza katika mikoa yote ambayo tamasha litafanyika mwaka huu, hivyo tutaangalia wapi tumpangie kulingana na ratiba yake. 

“Lakini niwahakikishie mashabiki wetu kwamba msanii huyo tutakuwa naye na sasa ni suala la Kamati ya Maandalizi kuona ratiba yake ilivyo na kisha nasi tumuweke kwenye ratiba yetu ili mashabiki wafurahi,” alisema Msama. 

Rebecca amewahi kutamba na albamu za Saturday Nite (aliyoitoa Januari 1, 2009), Hlala Nami (Novemba 11, 2003), Siyabonga (Desemba 21, 2000), Free at Last (Novemba 18, 1997), African Classics (Mei 5, 2009) na Greatest Hits (Januari 10, 2006).
Wasanii wengine watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo ambao tayari wameshathibitisha ni Upendo Nkone, John Lissu, Upendo Kilahiro, Rose Muhando na waimbaji wengine ambao inaelezwa watatajwa hapo baadae.

SHEREHE ZA MEI MOSI ZAFANA JIJINI MWANZA

$
0
0
 Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa wakipita ya mgeni wa heshima Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng.Evarist Welle Ndikilo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi mkoa wa Mwanza ,matembezi hayo yalihitimishwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
 Wafanyakazi wa Mkemia Mkuu wa Serikali wakiingia uwanjani CCM Kirumba Mwanza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi mkoa wa Mwanza .
 Wafanyakazi wa Idara ya Maliasili wakiingia uwanjani CCM Kirumba katika kuhitimisha siku ya wafanyakazi..
 Mahakama ya Tanzania wakiingia uwanja wa CCM Kirumba huku wakitanguliza ujumbe mzito.
 Kibanda cha Veta kilikuwa moja ya vibanda vilivyovutia kwenye maonyesho ya Siku ya Wafanyakazi zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza.
 Wafanyakazi wa Hospitali ya Bugando wakielekea kuingia kwenye matembezi ya mshikamano katika kusheherekea siku ya Wafanyakazi kwenye Viwanja vya CCM Kirumba.
Wafanyakazi wa Halmashauri ya Jiji Mwanza wakipita ya mgeni wa heshima Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng.Evarist Welle Ndikilo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi mkoa wa Mwanza ,matembezi hayo yalihitimishwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

PPF ILIVYOADHIMISHA SIKU YA WAFANYAKAZI LEO,RAIS KIKWETE AMKABIDHI ZAWADI MFANYAKAZI BORA WA PPF

$
0
0
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 5, Herman Kachima, ambaye ni Msimamizi wa huduma kwa wateja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa NSSF, Dkt. Mohammed Dau (Wapili kulia), akiteta jambo na mkurugenzi mkuu wa PPF, William Erio, na mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya udhibiti wa mifuko ya hifadhi ya jamii, (SSRA), Irine Isaka (Kushoto), na mwenyekitinwa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida (Juu), wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete, akimsalimia mjumbe wa bodi ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mbaraka Igangula, wakati akiwasili kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo.
Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakipita kwenye maandamano mbele ya mgeni rasmi, rais Jakaya Kikwete (Hayupo pichani) kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio (Kushoto), akimsikiliza kwa makini, Naibu Katibu mMkuu wa Wizara ya Habari, Vijana na Michezo, Profesa Ole Gabriel, wakati wa maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo. 

JHIKOMAN & AFRIKABISA BAND LIVE ON SAUTI ZA BUSARA 2014

$
0
0
Mwanamuziki Mkongwe wa Reggae Tanzania. Jhikoman & Afrikabisa Band Live on Sauti Za Busara Festival 2014. Huyu ni Mmoja kati ya wanamuziki wakubwa wa Muziki wa Reggae hapa nyumbani Tanzania pamoja na Afrika Mashariki. Kwa sasa Jhikoman yupo katika Ziara yake ya Ulaya kufanya Maonyesho katika Nchi za mbali mbali.

Taswira za Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Jumuiya ya afrika mashariki jijini Arusha

$
0
0
 Wakuu wa Mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakizindua kitabu rasmi cha Muongozo wa Majaji wa Jumuiya hiyo kwenye Mkutano wa 12 wa siku moja wa Jumuiya hiyo uliofanyika ukumbi wa Kimataifa wa Arusha.  Rais Uhuru Kenyata wa Kenya ambae ndie Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni pamoja na Mwenyeji wa Mkutano huo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. Wengine ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Burundi Bwana Bazombasa, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyemuwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohd Sheni pamoja na Waziri Mkuu wa Rwanda Bwana Pierre Damieni Habumuryemi.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa niaba yaRais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Sheni akipokea kitabu wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mkoani Arusha.
 Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania waliohudhuria Mkutano wa 12 wa Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki huko Arusha. Wa mwanzo kutoka kushoto ni Waziri wa Ardhi wa SMZ Mh. Ramadhan Abdulla Shaaban, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Mh. Benard Membe na Waziri wa Afrika Mashariki Mh. Joh Samuel Sitta. 

MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI YAFANYIKA ZANZIBAR.

$
0
0
DSC_0025Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein kushoto anaepunga mkono akiyapokea maandamano ya Wafanyakazi wa Sekta mbalimbali katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (May Day) yaliofanyika Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar.DSC_0033DSC_0034Mashirika mbalimbali yakipita mbele ya Mgeni Rasmi hayupo pichani katika Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani (May Day) yaliofanyika Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar.DSC_0076Baadhi ya Mawaziri pamoja na Wananchi waliohudhuria katika Maadhimishi ya siku ya Wafanyakazi Duniani(May Day)wakiwa ndani ya Ukumbi wa Salama Holl Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar.
DSC_0097Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein watatu kulia akishikana mikono pamoja na Viongozi mbalimbali wakiimba wimbo wa Mshikamano kwa wafanyakazi ndani ya Ukumbi wa Salama Holl Bwawani Hotel mjini Zanzibar ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (May Day). 
PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR

MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI MKOANI RUKWA KATIKA UWANJA WA NELSON MANDELA MJINI SUMBAWANGA

$
0
0
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mkoani Rukwa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Methew Sedoyyeka (katikati) akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiimba kwa pamoja wimbo maarufu wa Wafanyakazi wa "Solidarity Forever" na wafanyakazi walioshiriki maadhimisho hayo katika uwanja wa Nelson Mandela Mjini Sumbawanga.
Baadhi ya viongozi wa vyama vya wafanyakazi Mkoa wa Rukwa wakiwaongoza wafanyakazi kuimba wimbo wa uishirikiano baina yao "Solidarity Forever" katika kuadhimisha Siku ya wafanyakazi duniani ambayo Kimkoa imefanyika mjini Sumbawanga katika uwanja wa Nelson Mandela.
Maandamano katika kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani Mkoani Rukwa katika uwanja wa Nelson Mandela Mjini Sumbawanga.
Wafanyakazi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa.


Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo.
Chuo cha Ufundi Stadi VETA Katandala.
Idara ya Maji Sumbawanga (RUKWA) wakifanya vitu vyao.
NMB Sumbawanga.
SIDO Rukwa.
Chuo Kikuu Huria tawi la Rukwa.
Onyesho lililohusisha watoto wachanga mapacha katika kuonyesha utoaji huduma kwa mama wajawazito na watoto wachanga katika Hospitali Kuu ya Rufaa ya Mkoa wa Rukwa.
Onyesho la uharibifu wa mazingira kwa uchomaji misitu na ukataji miti ambalo hupelekea nchi kuwa jangwa na kuua vyanzo vya maji. Onyesho hili liliandaliwa na Idara ya Maji Rukwa.
Kikundi cha Ngoma za asili cha Kanondo kikiburudisha katika maadhimisho hayo.
Kikundi cha Waalimu kikiimba wimbo wa kutetea haki za wafanyakazi.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, AWASILI MJINI BUKOBA MKOA WA KAGERA JIONI HII KUWASHA MWENGE WA UHURU KESHO

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara, mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa mjini Bukoba jioni hii kwa ajili ya kuwasha Mwenge wa Uhuru kesho katika hafla itakayofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, Mkoa wa Kagera 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akivishwa Skafu na Vijana wa 'Scout' wa mkoa wa Kagera, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa mjini Bukoba jioni hii kwa ajili ya kuwasha Mwenge wa Uhuru kesho katika hafla itakayofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, Mkoa wa Kagera. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi, waliompokea kwenye uwanja wa Ndege wa mjini Bukoba leo jioni.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhingo Rweyemamu, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa mjini Bukoba jioni hii kwa ajili ya kuwasha Mwenge wa Uhuru kesho katika hafla itakayofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, Mkoa wa Kagera.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Zakhia Bilal, wakifurahia ngoma ya asili ya kabila ya Wahaya baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa mjini Bukoba jioni hii kwa ajili ya kuwasha Mwenge wa Uhuru kesho katika hafla itakayofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, Mkoa wa Kagera. 
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu, Fabian Masawe, akisoma Taarifa ya Mkoa mbele ya Makamu wa Rais Dkt. Bilal.Picha na OMR

BAJETI KUU YA SERIKALI: takribani Sh. Tril. 19. 7 zatarajiwa kutumika mwaka 2014/2015.

$
0
0

Spika wa Bunge la Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akiwaasa wabunge wote kushiriki kikamilifu katika kamati zao kizalendo kwa kujali nchi yao ili ipatikane bajeti yenye tija kwa taifa leo (jana) wakati wa kupokea taarifa ya Wizara ya fedha jijini Dar es salaam.

Waziri wa Fedha Saada Mkuya  Salum akiwasilisha taarifa ya sura ya Bajeti kuu ya Serikali kwa wabunge leo (jana) jijini Dar es salaam inayotarajia kuanza kutumika kwa mwaka wa fedha unaoanza Julai 2014/2015.

Waziri Mkuu wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda  akizungumza na wabunge wakati wa kupokea taarifa ya Wizara ya fedha jijini Dar es salaam.

Waziri wa Fedha Saada Mkuya (kulia) akiteta jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Dkt.Mary Nagu (kushoto) kabla ya kupokea taarifa ya bajeti ya Wizara ya fedha jijini Dar es salaam.  

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servarcius Likwelile (wa kwanza kulia) akimsikiliza Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum  (hayupo pichani) wakati akiwasilisha taarifa ya sura ya Bajeti kuu ya Serikali kwa wabunge leo (jana)  jijini Dar es salaam.

Baadhi ya wabunge wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Dkt.Mary Nagu(aliyevaa blauzi nyeupe) kabla ya kupokea taarifa ya bajeti ya Wizara ya fedha jijini Dar es salaam.  Wa kwanza aliyesimama mstari wa nyuma ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Stephen Wasira na mbunge wa Vunjo Augustino Mrema (aliyevaa barghashia). 

(Picha zote na  Eleuteri mangi)


Na Eleuteri Mangi
Serikali imepanga kutumia jumla ya sh.19, 653.31 ambayo ndiyo sura ya bajeti katika mwaka wa fedha 2014/2015 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na ya maendeleo ya nchi na watu wake.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum alipokuwa akiwasilisha taarifa ya sura ya Bajeti kuu ya Serikali inayotarajia kuanza kutumika mwaka wa fedha unaoanza Julai 2014/2015 leo (jana) jijini Dar es salaam.

Waziri Saada alisema kuwa mfumo wa bajeti kwa mwaka wa fedha unaoanza unazingatia sera za bajeti kwa mwaka 2014/2015 ambazo zitazingatia vipaumbele vya mpango wa Maendeleo wa Taifa  na malengo ya utekelezaji wa mkakati wa matokeo makubwa sasa (BRN).

Kwa upande wa matumizi ya kawaida Serikali inatrajia kutumia jumla ya sh.trilioni 14, 208. 21 ambayo inajumuisha mfuko mkuu wa serikali, mishahara ya watumishi wa Serikali, wizara, mikoa, halmashauri, taasisi na wakala za Serikali.

Aidha, kwa matumizi mengine yatakuwa ni kwa ajili ya maendeleo kwa mwaka wa fedha unaotarrajiwa kuanza Julai mwaka huu ambapo kiasi cha 5, 445.10 ambazo ni sawa na asilimia 27.7 zimepangwa kutumika kwa kuhusisha fedha za ndani na za nje ya nchi.

Waziri Saada akiwasilisha taarifa yake kwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wabunge hao waliipokea Taarifa ya Serikali kuhusu Makadirio ya Bajeti katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam ambayo inatarajiwa kuongeza wigo wa wabunge kuijadili bajeti hiyo kabla ya kusomwa bungeni mjini Dodoma.

Shabaha ya bajeti ya mwaka ujao wa fedha ni kuhakikisha pato la taifa litakuwa kwa asilimia 7.2 mwaka 2014, asilimia 7.4 mwaka 2015, asilimia 7.7 mwaka 2016 na kuendelea kuongezeka hadi kufikia asilimias 8.0 ifikapo mwaka 2017.

Misingi ya bajeti ya Serikali kwa kipindi cha mwaka 2014/2015 ni pamoja na kuendelea kuwepo na kuimarishwa amani, usalama, utulivu na utengamano misingi ambayo itasaidia kupatikana kwa katiba mpya kwa wakati kama ilivyopangwa.

Kwa upande wake Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu Stephen Wasira akiwasilisha rasimu ya mpango wa maendeleo wa taifa katika bunge likikaa kama kamati alisema kuwa maeneo ya  vipaumbele yanalenga miradi ya kitaifa ya kimkakati inayolenga kutanzua vikwazo vikuu vya kiuchumi inajumuisha miundombinu ya uasfirishaji kama reli, barabara, bandari, na usafiri wa anga.

Vipaumbele vingine ni nishati, huduma ya maji mijini na vijijini, kilimo, viwanda, maendeleo ya rasilimali watu na huduma za kiuchumi kama fedha, biashsra na utalii.

Naye Spika wa Bunge  la Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda amewaasa wabunge wote washiriki kikamilifu katika kamati pamoja na serikali ili ipatikane bajeti yenye tija kwa taifa na wabunge waikamilishe kizalendo kwa kujali nchi yao.

Kikao cha Bunge la bajeti kinatanguliwa na kamati mbalimbali zitakutana ambapo vikao vilianza Aprili 27, 2014 kwa wajumbe kuwasili jijini Dar es salaam na kuhitimishwa Mei 4, 2014 na wabunge kuanza safari kwenda Dodoma tayari kwa kuanza kikao chake kama ilivyopangwa.

Kamati ya bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira wakati wa Bunge la bajeti, kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, kamati ya Nishati na Madini, kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali (PAC) kujadili hesabu zilizokaguliwa za Serikali kuu na mashirika ya umma, kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje na  Ushirikiano wa Kimataifa.

Na nyingine ni kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,  kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba,  Sheria na Utawala, kamati ya kudumu ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara,  kamati ya kudumu ya Bunge ya masuala ya UKIMWI, kamati ya LAAC Dar es salaam na kamati ya kudumu ya bunge ya maendeleo ya jamii.

RAIS KIKWETE ONGOZA MAADHIMISHO YA MEI MOSI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipungia mkono waandamanaji aliowapokea katika kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani (MEI MOSI) leo Mei 1, 2014 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
 Akiwa mwingi wa furaha, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea  waandamanaji  katika kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani (MEI MOSI) leo Mei 1, 2014 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kashikana mikono na viongozi wa serikali na wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA)  huku wakiimba wimbo wa wafanyakazi  katika kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani (MEI MOSI) leo Mei 1, 2014 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipungia mkono maandamano ya magari  aliyoyapokea katika kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani (MEI MOSI) leo Mei 1, 2014 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Wafantakazi Bora kutoka idara na taasisi mbalimbali wakimsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia  katika kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani (MEI MOSI) leo Mei 1, 2014 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia  katika kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani (MEI MOSI) leo Mei 1, 2014 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.PICHA NA IKULU

Swissport yapata ongezeko la faida kwa asilimia 17

$
0
0
 Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Swissport Tanzania Bw Gaudence Kilasara Temu akizungumza na wanahisa wa kampuni hiyo wakati wa mkutano wao Mkuu wa Mwaka uliyofanyika jijini Dar es Salaam Jumatano jioni.
 Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni ya Swissport Tanzania Jeroen de Clercqakizungumza na wanahisa wa kampuni hiyo wakati wa mkutano wao Mkuu wa Mwaka uliyofanyika jijini Dar es Salaam Jumatano jioni. Wapili kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya hiyo Bw Gaudence Kilasara Temu akifuatiwa na mmoja wa wakurugenzi wa bodi Bw. George Fumbuka. 
 Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Swissport Tanzania Bw. Gaudence Kilasara Temu akizungumza na waandishi wa habari nje ya mkutano mkuu wa mwaka wa kampuni yake uliyofanyika Jumatano jioni jijini Dar es Salaam. 
 Afisa Fedha Mkuu wa kampuni ya Swissport Tanzania Mrisho Yassin akiwaongoza wanahisa kupitia ripoti ya mahesabu ya fedha ya mwaka 2013, wakati wa Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa kampuni hiyo uliyofanyika jijini Dar es Salaam Jumatano jioni. Wapili kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya hiyo Bw Gaudence Kilasara Temu akifuatiwa na mmoja wa wakurugenzi wa bodi Bw. George Fumbuka na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bw. Jeroen de Clercq.   
Mmoja wa wanahisa wa kampuni ya Swissport Tanzania akichangia mada wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa wanahisa wa kampuni hiyo uliyofanyika jijini Dar es Salaam Jumatano jioni.


Swissport yapata ongezeko la faida kwa asilimia 17
·        Pato la kila hisa lapanda kwa asilimia 11.5
·        Yatenga Dola milioni 6.3 kujenga gala ya kisasa ya mizigo uwanja wa JNIA

Kampuni ya Swissport Tanzania Plc imepata ongezeko la faida ya kabla ya kodi la asilimia 17 la shilingi milioni 11,387 ikilinganishwa na shilingi milioni 9,723 zilizopatikana katika mwaka wa fedha wa 2012, mafanikio hayo yakitokana na maendeleo makubwa ya sekta ya usafiri wa anga Tanzania.

Ongezeko hilo la faida katika kampuni limewezesha pato la kila hisa kuongezeka mpaka shilingi 208.22 ukilinganisha na shilingi 186.75 iliyoripotiwa mwaka 2012, ikiwapatia wanahisa kila sababu za kutabasam baada ya kupata ongezeko la asilimia 11.5 la hisa zao.

Haya yalithibitishwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Swissport Tanzania Plc Bw. Gaudence Kilasara Temu katika taarifa yake kwa wanahisa wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka uliofanyika Jumatano jijini Dar es Salaam.   

Bw. Temu alisema kuwa ukuaji wa huduma za Fastjet, mwaka mzima wa uendeshwaji wa shirika la Kenya Airways, uanzishwaji wa safari za ndege kubwa kama Turkish Airlines na Qatar Airways katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro; na ongezeko la idadi za safari na mabadiliko makubwa yaliyofanywa na Emirates, KLM, Ethiopian Airways, Qatar Airways, South African Airways, Egypt Air na Rwanda Air yamesaidia kampuni ya Swissport kufanya vizuri.

“Huu ulikuwa mwaka wa mafanikio ambapo tumeweza kutanua shughuli zetu katika viwanja vya ndege vya Mtwara na Songwe. Tumewekeza kikamilifu katika vituo hivi vipya na tumeweza kufanikiwa. Vituo hivi viwili vinaumuhimu mkubwa kutokana na kuwa katika maeneo mazuri kijeografia,” alisema Temu. 

Alisema kwa mwaka 2013 kampuni iliweza kusimamia jumla ya safari 13,098 za ndege ikiwa ni ongezeko la asilimia 13 uklilinganisha na safari 11,590 zilizosimamiwa na kampuni hiyo kwa mwaka 2012.
Abiria waliohudumiwa na kampuni hiyo kwa mwaka 2013 walikuwa 905,347 ikilinganishwa na abiria 657,072 waliohudumiwa kwa mwaka 2012, ambalo ni ongezeko la asilimia 38 ikilinganishwa na mwaka 2012.

Mizigo iliyosimamiwa kwa mwaka 2013 ilikuwa ni tani 25,126 ikiwa ni ongezeko la asilimia 11 ikilinganishwa na tani 28,354 zilizosimamiwa mwaka 2012. 

“Ongezeko kubwa la safari zilizosimamiwa katika mwaka linaonyesha ukuaji wa pato kwa asilimia 25 mpaka shilingi milioni 23,214 ikilinganishwa na shilingi milioni 18,551 iliyopatikana mwaka jana. Pato litokanalo na mizigo nalo limekuwa kwa asilimia 9.3 mpaka shilingi milioni 12,900 ikilinganishwa na shilingi milioni 11,802 zilizopatikana mwaka 2012,” alisema.

Ofisa Mtendaji Mkuu huyo aliongeza kuwa pato la jumla la kiuendeshaji la kampuni kwa mwaka huo limeongezeka kwa asilimia 19 mpaka shilingi milioni 36,115 ikilinganishwa na shilingi milion 30,353 zilizopatikana katika mwaka 2012.

Alibainisha kuwa gharama za jumla za kiuendeshaji za kampuni kwa mwaka zilikuwa ni shilingi milioni 24,811 ambalo ni ongezeko la asilimia 20 ikilinganishwa na shilingi milioni 20,683 zilizoripotiwa katika mwaka 2012.

“Kwa upande mwingine mapato ya kabla ya riba, kodi, uchakavu na marejesho ya kampuni yalikuwa ni shilingi milioni 13,677 ikilinganishwa na shilingi milioni 11,598 iliyoripotiwa mwaka 2012, hii ikiwakilisha ongezeko la asilimia 18. Mali za jumla za kampuni nazo zimekuwa kwa asilimia 18.4 kutoka shilingi 18,490 milioni katika 2012 mpaka shilingi 21, 895 milioni kwa mwishoni mwa mwaka 2013,” alisema.

Naye, mwenyekiti wa Bodi ya Swissport, Juan José Andrés Alvez alibainisha kwa wanahisa kuwa mwishoni mwa mwaka wa fedha 2013, kampuni ilianza ujenzi wa gala la mizigo la kisasa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), ambao utagharimu zaidi ya Dola za kimarekani milioni 6.3.

“Gala hili jipya la mizigo ya kutoka nje linategemea kuanza kufanyakazi ifikapo mwishoni mwa mwezi Oktoba 2014 baada ya hapo gala la zamani litabadilishwa na kuwa eneo la mizigo inayokwenda nje, likiwa na kituo cha kuhifathi bidhaa zinazoharibika kwa haraka likiwa na majokofu na friji ili kuhifadhi bidhaa aina tofauti kama samaki, nyama, mbogamboga, maua na madawa. 

Eneo hili jipya la bidhaa ziendazo nje linategemewa kurahisisha usafirishwaji wa bidhaa nje ya nchi hususani bidhaa za jamii ya maua, nyama na samaki,” alisema.

Mwenyekiti aliongeza kuwa ikiwa ni kama mkakati wa kuboresha utoaji huduma kwa wateja wao, shilingi 3,165 milioni ziliwekezwa kwa mwaka 2013 ukilinganisha na shilingi 2,434 milioni zilizowekezwa katika mwaka 2012.  

“Sehemu kubwa ya uwekezaji ilielekezwa katika vifaa vinavyosaidia shughuli za ubebaji mizigo za ardhini ili kuwahudumia vizuri wateja wetu ambao ni mashirika tofauti ya ndege,” alisema Bw. Alvez.

Bayport Yazindua Bima Ya Elimu

$
0
0

Bayport yazindua Bima Ya Elimu,Kwenye hafla ndogo kwenye ofisi ya Wizara ya   Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto. Kuanzia mkono wa kushoto katika picha ni Mhe. Sophia Simba (Waziri) akifutiwa na wawakilishi wa Bayport Financial    Services Maneja Masoko Ngula Cheyo na Matthew Mbaga, Meneja wa Bima.


======  ======  =======


Bayport Financial Services, ambayo ni moja kati ya wakopeshaji akubwa kwa ajili ya wafanyakazi imezindua mpango wa bima kwa ajili ya elimu. 

Mfumo huo wa bima ni kwa ajili ya kuendeleza elimu kwa watoto pale ambapo wazazi wao wanafariki. Kwa kiwango cha chini cha TZS 2,500 kwa mwezi, bima hii ni nafuu kwa wafanyakazi wenye kipato cha chini na inamhakikishia mwanafunzi kupata mahitaji yake ya msingi katika elimu.


Akiongea katika ufunguzi wa huduma hii mpya jana, Meneja Masoko wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo aliwaeleza waandishi wa habari kwamba lengo la kubuni huduma hii ni kutokana na kuwepo kwa pengo kwenye soko la huduma ambayo inakidhi watu wenye kipato kidogo. ‘Kuwepo kwetu hapa Tanzania kwa muda mrefu kumetupa fursa ya kutambua kuwa huduma ya bima haiwafikii watu wengi na huduma hii ingewanufaisha watanzania wengi ambao wanajali watoto wao’, alisema Ngula.


Katika uzinduzi huo uliofanyika ofisini kwake, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, jinsia na Watoto, Meshimiwa Sophia Simba, aliisifu kampuni ya Bayport Financial Services kwa kuzindua huduma hii ambayo itasaidia kupunguza mzigo kwa ndugu wa mfiwa na kuhakikisha motto anaendelea na elimu yake. ‘Elimu ni haki ya kila mtoto na huduma hii itapunguza wanafunzi ambao wanaacha shule kwa sababu ya kushindwa kulipa ada pindi wazazi au walezi wao kufariki. Elimu inasaidia watanzania wengi kujikomoa na umasikini na kusiwe na pingamizi yoyote kwa mtoto kutoipata,’ alisema Mheshimiwa Simba.


 Wazazi na walezi wanauwezo wakuchagua jinsi ya kulipa na idadi ya wanafunzi wanaotaka kuwalipia bima hii. Bima hii inapatikana katika matawi yote ya Bayport ambayo yamesambaa katika mikoa yote hapa nchini. Matthew Mbaga ambaye ni Meneja wa Bima pia alieleza waandishi pia umuhimu na manufaa ya bima hii katika uzinduzi huo.

Mfumo wa kielektroniki waongeza mapato manispaa ya kinondoni

$
0
0
 Afisa Uhusiano wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Bw. Sebastian Mhowera akieleza kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mfumo mpya wa kielektroniki wa ukusanyaji  mapato unatumiwa na manispaa hiyo,wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari(MAELEZO) Fatma Salum.

Mchambuzi wa Mifumo ya Komputa Bw. Jackson Kiema akiwaonyesha waandishi wa habari(hawapo pichani) mashine ya kielektroniki inayotumika katika ukusanyaji wa mapato na kuhifadhi taarifa za mapato, wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Afisa Uhusiano wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Bw. Sebastian Mhowera. PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO.
======  ====== =====
MFUMO MPYA WA UKUSANYAJI WA MAPATO


Kutokana na kukua kwa sekta ya mawasiliano nchini, Manispaa ya Kinondoni imeanzisha utaratibu wa ulipaji wa kodi kwa kutumia huduma ya simu za mkononi na Max-malipo.


Huduma hiyo mpya inayotolewa kupitia mfumo unaojulikana kama “e–payment system”,humwezesha mwananchi kulipa kodi yake muda wowote, kwa haraka na urahisi na mahali popote.


Huduma hii inatolewa na Manispaa kwa kushirikiana na wakala anayetambulika kama “Max-malipo” ambaye kupitia huduma zake mitaa 171 iliyopo katika Kata 34 imeunganishwa katika mifumo hiyo ya ulipaji kodi.


Mfumo huu wa ukusanyaji wa kodi ndani ya Manispaa ni hatua ya utekelezaji unaozingatia maelekezo ya waraka wa Serikali Na. 5 wa mwaka 2009 unaohamasisha matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa lengo la kurahisisha utoaji wa huduma kwa Umma, kwa ufanisi na kwa wakati.


Kimsingi hatua hii inahamasisha ushirikishwaji wa wananchi katika utoaji wa maamuzi yanayohusu mambo yao na kuwezesha uwepo wa Serikali iliyo wazi, inayowajibika na makini katika kutekeleza majukumu yake kwa Taifa.


Hivyo basi kutokana na malengo na umuhimu wa kuwarahisishia wananchi, Manispaa iliona ni vema ikaingia haraka ndani ya utaratibu huu ili Mwananchi aweze kulipia kodi popote kwa kutumia Max-malipo au wakala wa simu za mkononi yaani Tigo pesaNa.212888 na M-Pesa Na. 212888.


MAFANIKIO YALIYOPATIKANA.


Katika kipindi kifupi cha muda wa miezi 3, tangu mfumo huu mpya ulipoanzishwa rasmi kumekuwa na mafanikio makubwa kama ifuatavyo:-


·        Mapato yameongezeka kwa kiwango kikubwa mfano; ada ya kuchangia huduma za Afya (Cost sharing) imeongezeka kutoka Tshs. 45,000,000/= kwa wiki hadi kufikia Tshs. 65,000,000/= kwa wiki, sawa na ongezeko LA 69%


·        Chanzo cha kodi ya majengo hadi mwishoni mwa Machi tulikusanya Tshs. 339,000,000/= tofauti na awali ambapo hadi kipindi kama mwaka 2013 tulikusanya sawa na ongezeko la asilimia 269 hiki Tshs. 126,000,000/=


·        Maeneo mengine ongezeko la mapato limezidi bajeti ya mwaka iliyotakiwa kukusanywa. Kwa mfano katika ushuru wa huduma za jiji (City Service Kavy) ambapo tumezidi kwa 18%


·        Ushuru wa Masoko umeongezeka kwa wastani wa asilimia 20 ya lengo la kila mwezi.


·        Lesseni za biashara hadi Machi tumekusanya Tshs. 2.4 Bilioni sawa na 93% ya bajeti ya Manispaa ya chanzo hiki ya Tshs. 2.6 Bilioni kwa mwaka.


Napenda kuwahakikishia wananchi wa Kinondoni kuwa Manispaa ya Kinondoni itazidi kuboresha huduma zake ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa na kuwawezesha kuwa na maisha bora kutokana na mafanikio haya, lipa.


Lipa kodi kwa maendeleo ya Manispaa yako.


IMETOLEWA NA



SEBASTIAN MODESTUS MHOWERA

AFISA UHUSIANO WA MANISPAA

HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI

SIMU NA:0754-227024

CLOUDS MEDIA YAPATA LESENI YA URUSHAJI WA MATANGAZO KATIKA NCHI ZA FALME ZA KIARABU.

$
0
0

Kampuni ya Clouds Media International leo imetangaza kuwa imepewa leseni ya kurusha  matangazo  katika nchi za umoja wa falme za kiarabu (UAE).  Akielezea kuhusu leseni hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni  hiyo Bwana Joseph Kusaga, amesema  sasa kituo cha  Clouds TV kimataifa kitakuwa kikishuhudiwa na watu wa mataifa mbalimbali.

Clouds TV kimataifa ni mwendelezo wa televisheni maarufu sana kwa vijana  nchini Tanzania,  hata hivyo sehemu kubwa ya maudhui yatakayokuwemo kwenye Clouds TV kimataifa itakuwa na mpangilio mpana wa vipindi kwa watazamaji vitakavyorushwa kwa  lugha za Kiingereza na Kifaransa. Akieleza zaidi Kusaga amesema "Leo ni siku ya  kihistoria na alama ya hatua moja katika mpango wetu wa kina wa kupeleka maudhui ya Clouds TV kimataifa kupitia  matangazo kwa njia ya  mitandao’’.

Clouds TV kimataifa  haitotoa tu burudani, lakini pia itakuwa kiunganishi kwa waafrika waishio katika umoja wa nchi za falme za kiarabu pamoja na kuwapa fursa za kutangaza bidhaa zao na kuimarisha uhusiano baina yao.


Vituo vya televisheni katika Umoja wa falme za kiarabu vipo vingi na vyenye ushindani mkubwa, lakini Clouds TV kimataifa imebahatika kupata nafasi ya kurusha matangazo yatakayowafikia walengwa katika chaneli yenye uwezo wa kuwahudumia zaidi ya watazamaji  takribani milioni 3.5 kutoka katika nchi za Afrika. Kwa sasa hakuna kituo kinachotoa huduma hii na hivyo kuwa fursa muhimu kwa watazamaji.


Clouds TV kimataifa itarusha vipindi vya burudani, tamthilia, maigizo, ucheshi, na muziki, vyote vitakavyo kuwa vimeandaliwa kutoka nchi za mashariki, magharibi na kusini mwa bara la afrika na itapatikana kwa watazamaji walio katika Umoja wa falme za kiarabu kupitia huduma ya IPTV inayotolewa  na Etisalat na Du.


Clouds TV kimataifa itarushwa kupitia mamlaka ya Abu Dhabi ijulikanayo kama twofour54, ikiungana na vituo kama FOX na CNN. Clouds TV kimataifa itaanza kurusha matangazo ya  majaribio katika wiki chache zijazo kabla ya tarehe 15 mwezi June mwaka huu.



King Majuto atoa msaada wa Steps Solar kwa kituo cha Polisi Mjimwema

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Kigamboni,Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akizungumza jambo wakati wa hafla ya kupokea Vifaa vya Solar kutoka kampuni ya Steps Solar kwa ajili ya Kituo cha Polisi cha Polisi cha Mjimwema,Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Steps Solar,Dilesh Solank. 
Mmoja wa Mabalozi wa Steps Solar,Jacob Stephen akiongea na wananchi wa Mjimwema.
Mabalozi wa Steps Solar Jacob Stephen (JB) na Amri Athuman (King Majuto) wakiwa kwenye hafla hiyo.
Mwigizaji mkongwe katika tasnia ya filamu nchini,Amri Athuman ‘King Majuto’ wiki iliyopita akiwa kama Balozi wa Steps Solar alitoa msaada wa kukifungukia Solar kituo cha Polisi cha Mjimwema, ikiwa ni katika kampeni za kuhakikisha kila mtanzania anafaidika na matumizi ya nishati ya umeme Nuru.

Akiongea na Waandishi wa habari katika hafla iliyoandaliwa na kampuni ya Steps Entertainment ambao ndio wafadhali wa msanii huyo, alisema kuwa kampuni hiyo imekuwa ikisambaza filamu zake lakini kuna utaratibu wa kutoa misaada kwa jamii, kwake yeye ameona tatizo linalowakabili watu wengi nje ya miji ni umeme.

“Nimeanza kampeni kama Balozi wa Steps Solar kuwasaidia wapenzi wa kazi zangu, ambazo ninaamini bila wao siwezi kabisa kuwa King, kama vile mnavyopenda kuniita, nimeanza katika kituo cha Polisi cha Mjimwema lakini nikiwa na wenzangu tutafika sehemu nyingi zaidi,”alisema King Majuto.

Afisa mahusiano wa kampuni hiyo Moses Mwanyilu amesema kuwa mradi huo ni endelevu ambapo wanatarajia kufunga Steps Solar katika Kituo cha Yatima Tuangoma, Mjimwema, vituo vya Polisi ni Mjimwema na Ferry, vituo vya afya ni Mjimwema, Ungindoni, Homboza Chanika na Tuangoma.

Msanii huyo aliambatana na wasanii wengine ambao pia ni mabalozi wa Steps Solar, ambao ni Jacob Stephen ‘JB’ na Salma Jabu ‘Nisha’ mgeni wa heshima katika hafla hizo alikuwa Mh. Dr. Faustine Ndugulile mbunge wa Kigamboni.

KUMBUKUMBU

$
0
0
MAREHEMU MZEE ANGELOUS DANIEL NGONYANI
 
NI MWAKA MMOJA SASA TANGU ULIPOTUTOKA GHAFLA TAREHE 01-05-2013
KATIKA HOSPITALI YA TUMAINI DAR ES SALAAM.

HAKIKA SIKU ILE ITABAKI KUWA KUMBUKUMBU KWETU
UNAKUMBUKWA NA MKE WAKO ADOLPHINA,WATOTO WAKO DANIEL, MELANIA, LAURENCIA NA DITRICK PAMOJA NA WAJUKUU WAKO LAURA,ALPHA NA ALVIN. UMETUACHIA FUMBO ZITO LAKINI KWA YOTE TUNAMSHUKURU MUNGU KWANI UMETUACHIA MENGI YA KUIGA, HEKIMA ZAKO, UPOLE, UPENDO, UVUMILIVU VIMEBAKI MIOYONI MWETU NA TUNAVIENZI DAIMA

RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA …NA MWANGA WA MILELE UMWANGAZIE
APUMZIKE KWA AMANI AMINA

TIMU YA NETIBOLI YA UTUMISHI YAPONGEZWA KWA KUNYAKUA UBINGWA MEIMEOSI 2014

$
0
0
 Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma  Mh. Celina O. Kombani (Mb) akikabidhiwa kombe la ubingwa wa mpira wa Pete la Mei Mosi 2014 kutoka kwa Kapteni wa timu Elizabeth Fusi katika hafla fupi aliyoiandaa kuwapongeza mabingwa hao iliyofanyika ofisini kwake mapema leo
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma  Bw. HAB Mkwizu akimkaribisha mgeni rasmi  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma  Mh. Celina O. Kombani (kushoto) kuongea na wachezaji wa ofisi yake na watumishi katika hafla fupi aliyoiandaa kuipongeza timu ya Utumishi kwa kuwa mabingwa wa Mpira wa Pete, Mei Mosi 2014 iliyofanyika ofisini kwake mapema leo 
 Wachezaji wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, pamoja na wafanyakazi wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, menejimenti ya Utumishi wa Umma  Mh. Celina O. Kombani (Mb), hayupo pichani katika hafla fupi ya kuipongeza timu ya Mpira wa Pete kwa kunyakua kombe la Mei Mosi 2014 iliyofanyika ofisini hapo mapema leo.
 Watumishi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma  wakisimama kwa dakika moja kumkumbuka mwenzao wa Ofisi ya Rais-Ikulu aliyepoteza maisha ghafla siku ya Mei Mosi 2014. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani (Mb)  (katikati)  akisimama pamoja na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu (kushoto ) na Mwenyekiti wa timu ya Mpira wa Pete ya Utumishi Bw. Lumuli  Mtaki  (kulia) kumkumbuka mtumishi wa Ofisi ya Rais-Ikulu aliyepoteza maisha ghafla siku ya Mei Mosi 2014.

Rais Mstaa awamu ya Tatu Mkapa kupitia taasisi yake akabidhi nyumba za afya Singida.

$
0
0
 Rais awamu ya tatu  Benjamen Mkapa (katikati) mkuu mkoa Singida Dk. Parseko Kone (kushoto) na mwakilishi wizara ya afya na ustawi wa jamii Dk. Catherine Joachim, akizindua nyumba ya watumishi wa afya vijijini, kati ya 30 zilizogharimu zaidi ya Sh. Bilioni 1.9 kupitia mfuko wa ‘Mkapa Foundation’ kwa wilaya za Mkalama, Iramba, Singida, Ikungi na Manyoni Mkoani Singida.

 Mkuu Mkoa Singida Dk. Parseko Kone akimkabidhi hati ya nyumba mganga mkuu wa Wilaya Iramba Dk Japhet Simeo mara baada ya rais mstaafu Benjamen Mkapa kukabidhi nyumba za kisasa 30 kwa watumishi wa afya vijijini zilizojengwa na taasisi ya Mkapa foundation, kwa wilaya za Manyoni, Ikungi Mkalama, Singida na Iramba, makabidhiano yaliyofanyika kijiji cha Senenemfuru halmashauri ya wilaya Singida.
Rais awamu ya tatu, Benjamen Mkapa akikabidhiwa kibuyu na akina mama wa kijiji cha Senenemfuru Singida vijijini, kikiwa na maana ya upendo, kwenye hafla ya kukabidhi nyumba, kati ya 30 zilizojengwa na Mkapa foundation kwa halmashauri tano za mkoa wa Singida.
 Mwonekano wa nyumba iliyojengwa na taasisi ya Benjamen Mkapa katika kijiji cha Senenemfuru halmashauri ya wilaya Singida, kati ya 30 zilizojengwa katika wilaya tano mkoani Singida kwa ajili ya watumishi wa afya vijijini kwa gharama ya Sh.1,945,187,143.Picha na ELISANTE JOHN-Singida.   

Na Elisante John, Singida

RAIS mstaafu awamu ya tatu Benjamen W. Mkapa kupitia taasisi yake ‘Benjamen William Mkapa HIV/AIDS’ (BMAF), amekabidhi nyumba 30 zilizojengwa kwenye zahanati 13 na vituo vya afya viwili kwa zaidi ya Sh. Bilioni 1. 9, katika halmashauri tano za Wilaya Mkoani Singida.

Akikabidhi sehemu ya nyumba hizo jana kwenye hafla iliyofanyika kijiji cha Senenemfuru Singida vijijini, mzee Mkapa alishukuru wafadhili waliowezesha kazi hiyo, ukiwemo mfuko wa dunia wa kupambana na Ukimwi, kifua kikuu na malaria (Global fund), kwa kuonyesha imani na serikali ya Tanzania.

Nyumba hizo zimejengwa katika zahanati ya Misughaa na Mangonyi (Ikungi), Mkenge, Mpambaa na Senenemfuru (Singida), Ulemo Uwanza na kituo cha afya Ndago (Iramba), Kinyambuli na Dominiki (Mkalama), pia kituo cha afya Itigi, Idodyandole, Heka, Mpola na Chibumagwa (Manyoni).

maadhimisho ya Wiki ya Elimu Kufanyika kitaifa mkoani Dodoma

$
0
0
Msemaji wa Serikali Bw. Assah Mwambene akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu maadhimisho ya Wiki ya Elimu yatakayo fanyika kitaifa mkoani Dodoma. kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Magreth Kinabo.


=======
HASSAN SILAYO- MAELEZO

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda kesho atazindua maadhimisho wa Wiki ya Elimu Mjini Dodoma.


Akizungumza na waandishi wa Habari Msemaji wa Serikali Bw. Assah Mwambene alisema kuwa Maadhimisho hayo yatakwenda sambamba na Maafisa elimu wa Mikoa kutoa taarifa kwa wananchi kupitia vyombo vya habari kuhusu maendeleo ya sekta ya elimu katika mikoa yao.


“Maadhimisho ya wiki ya elimu yatakwenda sambamba kwa taarifa mbalimbali kuhusu mafanikio katika sekta ya elimu kutolewa na maafisa elimu wa mikoa ili kuwapa fursa wananchi kujua nini kimefanyika katika sekta ya elimu”. Alisema Mwambene.

Pia Bw. Mwambene aliongeza kuwa katika maadhimisho hayo shule mbalimbali za msingi na sekondari zilizofanya vizuri katika mitihani ya kitaifa zitapewa zawadi.

Aidha Mwambene aliongeza kuwa wanafunzi walioandika insha kuhusu Afrika Mashariki na SADC watapewa zawadi.


Maadhimisho hayo yatafungwa Tarehe kumi na Rais Jakaya Kikwete mkoani Dodoma.


KUJUA RATIBA BOFYA HAPO CHINI KUSOMA



RATIBA YA MIKUTANO YA WAANDISHI WA HABARI NA MAAFISA ELIMU WA MIKOA

S/N

TAREHE

MKOA

MHUSIKA

NAMBA YA SIMU

1

2/5/2014

DODOMA

BW.JUMA KAPONDA


0784 584863

MOROGORO

BIBI W. NKAYA


2

3/5/2014

DSM

BW. R. MAPUNDA

0754 744536

PWANI

BW. YUSUPH KIPENGELE


TANGA

BW. R. CHOMOLA


3

4/5/2014

KILIMANJARO

BIBI. LUCY MALISA


TABORA

BW. J. MABEYO


RUVUMA

BIBI. MAYASA HASHIM


4

5/5/2014

KATAVI

BW. ERNEST HINJU


RUKWA

BW. S. MGINA


LINDI

BW. GIFT ENOCK


MTWARA

BW. HIPSON KIPENYA


5

6/5/2014

MANYARA

BW. IBRAHIM MBANGO


NJOMBE

BW. SAID NYANSILO


MBEYA

BW. R. NTYAMA


ARUSHA

BW. NESTORY MLOKA


6

7/5/2014

MWANZA

BW. H. MAULID

0754 432691

MARA

BW. E. MPALILE


GEITA

BIBI. E. BUCHUMA


SIMIYU

BW. A. KAMAMBA

0764856644

7

8/5/2014

KIGOMA

BW. SALVATORY SHAURI

0754 361266

KAGERA



SHINYANGA

BIBI. EVA MLOPA


8

9/5/2014

IRINGA

BW. J. MNYIKAMBI


SINGIDA

BIBI. FATUMA KILIMIA



9


10/5/2014




Viewing all 46334 articles
Browse latest View live


Latest Images