Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 277 | 278 | (Page 279) | 280 | 281 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Fatuma Machenga (GS) mfungaji bora katika Mpira wa Pete wa mashindano ya Mei Mosi 2014 akiwa na kikombe baada ya kutangazwa rasmi katika hafla fupi iliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuru mjini Morogoro.
  Baadhi ya wachezaji wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma (jezi za kijani) wakishangilia kwa kutawazwa mabingwa wapya wa Mpira wa Pete Mei Mosi 2014 kwa kuifunga timu ya Uchukuzi. Mashindano hayo yalimalizika jana jioni katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. 
  Baadhi ya wachezaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi Umma, pamoja na mashabiki wao wakipongezana baada ya kuibuka mabingwa wapya wa Mpira wa Pete kwa kuifunga Uchukuzi katika mashindano ya Mei Mosi 2014 yaliyomalizika katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
  Mabingwa wapya wa Mei Mosi 2014, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakiwa katika mazoezi mepesi kabla ya mchezo ambao waliifunga Uchukuzi na kunyaukua kombe la Mei Mosi 2014 iliyochezwa uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
  Mchezaji wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Sophia Komba akijiandaa kumdhibiti mchezaji wa Uchukuzi (C) (mwenye mpira) katika mechi ya fainali iliyochezwa katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
  Hekaheka ya kuwania mpira baina ya wachezaji wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma (jezi za kijani) na Uchukuzi (jezi za bluu) katika mechi ya fainali ya Mei Mosi 2014 iliyochezwa jana uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

  Na. James Katubuka

  Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma imetawazwa rasmi kuwa bingwa wa mpira wa Pete wa Mashindano ya Mei Mosi 2014.

  Utumishi imefanikiwa kuwa bingwa baada ya kuisambaratisha timu ya Wizara ya Uchukuzi kwa ushindi wa magoli 33 dhidi ya 21. Mchezo huo wa fainali ulifanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
  Katika mchezo huo mchezaji Fatuma Machenga (GS) wa Ofisi ya Rais Utumishi ndiye aliyekua tishio kwa kuongoza wachezaji wa timu yake kufanikisha ushindi huo. 

  Mchezaji Subira Jumanne (WA) wa Uchukuzi akizungumzia hali ya mchezo baada ya mpira kumalizika alisema kuwa mchezo ulikuwa mgumu na wapinzani wao walikua wamejiandaa vyema.
   “Naamini wakati wa mashindano mengine tutafanya vizuri kwa kujiandaa vyakutosha, asiyekubali kushindwa si mshindani” Subira alisema.

  Wakati huohuo, Fatuma Machenga (GS) wa Utumishi ameibuka kuwa mfungaji bora wa mpira wa Pete katika mashindano ya Mei Mosi 2014 kwa kufunga jumla ya magoli 136.
   “Tutahakikisha kuwa mwakani tunapambana zaidi kwa kufanya mazoezi ya kutosha ili kutetea ubingwa wetu” Machenga alisema.

  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma imenyakua kombe hilo lililokuwa likishikiliwa na timu ya Wizara ya Ulinzi iliyokuwa bingwa katika mashindano yaliyopita Mwaka 2013. 
  Mshindi wa Pili kwa mwaka 2014 ni Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Mashindano hayo yalimalizika jana katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

  0 0

  Mkurugenzi wa Tanzania Homes Expo, Zenno Ngowi  akizungumza na waandishi Dar es Salaam jana kuhusu Uzinduzi wa maonesho ya 4 ya Tanzania Homes Expo na EAG Group Ltd yatakayofanyika Dar es Salaam kuanzia Agosti 23-24 mwaka huu. Kushoto ni Meneja Biashara,Mathew Gugai. (Picha Francis Dande).

  0 0


  Ofisa muendeshaji wa Mfuko wa pensheni wa mashirika ya umma PSPF, Bw, Hadji Jamadary kushoto akimwelekeza kujaza fomu Shabani Maganga wakati wa mahadhimisho ya siku ya usalama na afya kazini yaliyofanyika viwanja vya mnazi mmoja Dar es salaam

  Afisa muendeshaji wa mfuko wa pensheni wa mashirika ya uma PSPF Bw, Lule Kasembwe kushoto akitoa maelekezo kwa wazee waliojitokeza 
  Ofisa muendeshaji wa PSPF Hadji Jamadary kushoto akiwapatia maelezo ya jinsi ya kujiunga na PSPF wakati wa mahadhimisho ya siku ya usalama na afya kazini yaliyofanyika viwanja vya mnazi mmoja Dar es salaam

  0 0


  Mwanamuziki mashuhuri wa reggae barani Afrika Jhikoman & Afrikabisa Band toka kule Bagamoyo,mkoani Pwani,Tanzania,anarajiwa kuwa miongoni mwa wasanii wakubwa watakao
  litingisha onyesho kubwa la 5 International African Festival-Tubingen litakalo fanyika mjini Tubingen, Ujerumani ya kusini kuanzia 17 Julai mpaka 20 Julai 2014.

  Mwanamuziki huyo nyota Jhikoman kwa sasa anawashamoto katika majukwaa ya kimataifa huko ughaibuni ameanzia Finlan,na atakuwepo Norway na kwingineko.
  pata buradani kiduchu


  booking +358465919130

  0 0


  Berlin, Ujerumani

  Mchekeshaji maarufu   kutoka nchini Tanzania  Muarabu wa Dubai a.ka Mpoki ameondoka nchini Ujerumani kurudi nyumbani Tanzania baada ya ziara yake ya siku 4 kukamilika. Msanii huyo ambaye alifanya ziara nchini ujerumani baada ya kualikwa na Umoja wa wa Watanzania  Ujerumani (U T U) kwa ajili ya Sherehe za muungano wa Tanzania, zilizoambatana na kongamano la kibiashara pamoja na  Mkutano mkuu  wa uchaguzi wa 
         U T U.

  Mchekeshaji huyo maarufu kutoka kundi la Orijino Komedi  aliweza kuburudisha waliohudhuria katika sherehe hizo kubwa na za aina yake katika jiji La Berlin Ujerumani. 
  Kufuatia uchaguzi mkuu wa U T U.  Bw. Mfundo Peter Mfundo amepata ushindi  mkubwa wa % 98 na kuendelea kuwa Mwenyekiti wa U T U kwa kipindi kingine cha miaka 2.

  Nafasi ya makamo Mwenyekiti  ilinyakuliwa na Bw. Peter Kazaura nafasi ya Katibu imechukuliwa na Bi. LiLian Sorogo, nafasi ya  Muweka hazina  imechukuliwa na  Rajab Kaoneka.

  Wajumbe wa kamati ni. Zenat Jamal, Dr. Andreas Wesselmann, Julius Tsaxarra, Joyce Rupia, Vital kazimoto, na Fulgens Kisalya. Mutano huu wa Uchaguzi ulihudhuriwa na Mgeni Rasmi Mh. Naibu Balozi wa Tanzania nchini ujerumani Bw. Mvulla. Mwenyekiti wa U T U  Bw Mfundo Peter amesema timu yake mpya inategemea kubadilisha sura nzima na mwenendo wa Umoja  huu, ndani ya kipindi cha miezi 6 ya uongozi mpya. Chanzo cha habari kilinyetisha.

  Baada ya  mkutano  wa uchaguzi kumalizika mnamo saa 11:30 alasiri, Viongozi wa U T U na Wanachama  walijumuika na watanzania wengine katika tafrija ya chakula cha jioni katika Hotel ya MARITIM HOTEL Berlin.  ambayo iliandaliwa rasmi na Ubalozi wa Tanzania nchini ujerumani ili kuhitimisha sherehe za Muungano wa Tanzania katika Tafrija  hiyo kubwa  walihudhuria wageni mbali mbali, Diplomats, na burudani mbali mbali zilikuwepo zikiwemo ngoma  za asili kutoka Tanzania na Vichekesho kutoka kwa Mchekeshaji  MPOKI, pia kulikuwa na Muziki wa kunesanesa. Msanii wa Movie na mtayarishaji wa kipindi cha Beyond the Borders bi Devota Alfred aliweza kufanya mahojiano na wasanii pamoja na viongozi waliohudhuria sherehe hizi. naye mtangazaji wa Deutsche welle idhaa ya kiswahili Bw Sudi Mnete hakuwa mbali siku hii akirepoti kutoka katika eneo la tukio.


  0 0
 • 04/30/14--01:17: TAARIFA KWA UMMA
 • JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  WIZARA YA NISHATI NA MADINI

     Telegramu “NISHATI”                                                                         753/33 MTAA WA SAMORA,

  Simu: +255 22 2117156-9                                                                  S.L.P. 2000,

                    +255 22 2112793                                                                              DAR ES SALAAM.

  Nukshi:+255 22 2111749

  Barua pepe: ps@mem.go.tz


  TAARIFA KWA UMMA


  UTEUZI WA WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI

           YA WAKALA WA NISHATI VIJIJINI (REA).


  Waziri wa nishati na madini Mheshimiwa Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo (Mb) ameteua wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kutoka Taasisi zisizo za kiserikali (NGO), Sekta Binafsi na washiriki wa Maendeleo kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 1 Aprili, 2014.


  Majina ya wajumbe walioteuliwa na Taasisi wanazoziwakilisha ni kama ifuatavyo:-


  i

  Bw. Edmund P. Mkwawa

          Tanzania Banker’s

          Association

  ii

  Bi Rehema Tukai

          Foundation for Civil

          Society

  iii

  Bi  Renatha J. Mwageni

          Tanzania Federation

          of Cooperation

  iv

  Bw. Innocent G. Luoga

          Wizara ya Nishati na

          Madini

   v

  Bw. Kalist Luanda

          Ofisi ya Waziri Mkuu –

          TAMISEMI

  vi

  Bw. Emmanuel M. Tutuba

          Wizara ya Fedha

  vii

  Dkt Gideon H. Kaunda

          Tanzania Private Sector

          Foundation

  vii

  Bi Stella Mandago (Observer)

  )       African Development

          Bank (AfDB)  Wakala wa Nishati Vijijini ulipitishwa kwa Sheria ya Bunge Na. 8 ya mwaka 2005 na uteuzi wa wajumbe hawa umezingatia Sifa muhimu   zinazotakiwa kwa wajumbe wa Bodi.  Kutokana na kukidhi sifa husika Mheshimiwa Prof. SospeterM. Muhongo(Mb) amemteua Bw. EdmundP.Mkwawa kuwa Mwenyekiti wa Wakurugenzi wa Bodi ya Nishati Vijijini  Imetolewa  KATIBU MKUU


  WIZARA YA NISHATI NA MADINI


  0 0

   Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi inayoundwa na wadau wa watoto jijini Mwanza Bw. Godfrey Salumu akifafanua utaratibu mzima wa utendaji kazi wa kamati ndogo ndogo zilizoundwa kwa wajumbe (hawapo pichani) ili kuweza kufanikisha maadhimisho hayo.
   Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya jiji la Mwanza Bi Eluminata Mwita akisikiliza jambo kwa makini toka kwa wajumbe (hawapo pichani).
   Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na Wasichana, KIVULINI Bw Ramadhani Masele (kushoto) ambae pia ni mjumbe wa kamati ya ndogo ya Uratibu, Mipango na Fedha akiteta jambo na mjumbe mwenzake wakati wa kikao hicho.

   Wajumbe wa Kikao cha kwanza cha maandalizi ya Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika itakayofanyika Juni 16 chini ya kauli mbiu ya “Kuondoa Mila Zenye Kuleta Madhara kwa Watoto ni Jukumu Letu Sote”.
    Uongozi wa kamati ya maandalizi ya sherehe ya siku ya Mtoto wa Afrika wilaya ya Nyamagana, Mwanza. Kulia ni Bw Godfrey Salumu ambae ni Mwenyekiti wa kamati, Bw. Devis Mrope (katikati) ambae na Katibu, kushoto ni Katibu Msaidizi Bi. Francisca Michael.
  =======  =======  ========
  HALMASHAURI NA WADAU WA JIJI LA MWANZA WAANZA MAANDALIZI YA SHEREHE ZA KUADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA ZITAKAZOFANYIKA JUNI 16.

  Halmashauri pamoja na wadau toka mashirika na taasisi za kutetea na kulinda haki za watoto jijini Mwanza wameanza rasmi vikao vya maandalizi ya kuadhimisha sherehe za siku ya mtoto wa Afrika inayoadhimishwa kila Mwaka Juni 16.

  Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri wa Jiji la Mwanza chini ya Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri hiyo Bi. Eluminatha Mwita wajumbe walikubaliana kuadhimisha siku hiyo katika Kata ya Buhongwa, kwa Wilaya ya Nyamagana.

  Siku ya mtoto wa Afrika huadhimishwa kimataifa kote duniani kwa lengo la kutambua thamani, utu, na umuhimu wa mtoto duniani. Maadhimisho haya hufanywa kila juni 16 tangu ilipotangazwa kuwa siku rasmi mwaka 1991 na jumuiya ya umoja wa Afrika.

  Akizungumza wakati wa kufungua kikao hicho Afisa Maendeleo Jamii wa Jiji la Mwanza Bi. Eluminatha Mwita alisema kuwa kauli Mbiu ya mwaka huu ni “Kuondoa Mila Zenye Kuleta Madhara kwa Watoto ni Jukumu Letu Sote” na kufafanua kuwa kauli hiyo inalenga kuwasisitiza wazazi na walezi kuacha mila potofu zenye kuleta madhara kwa watoto.

  Bi Eluminatha alisema kuwa “Kauli mbiu hiyo ina lenga kuangalia mila zote kandamizi na potofu zinazotokana na jamii husika katika malezi ya mtoto na kusababisha madhara mbalimbali ikiwemo kuongezeka kwa watoto wa mitaani, kubakwa kwa watoto, kukosa elimu, afya na malezi bora pamoja na vifo kwa watoto hawa”.

  Kikao hicho cha kwanza kiliweza kuchagua viongozi wa kamati hiyo ya maandalizi, mwenyekiti aliyechaguliwa ni Godfrey Salum huku katibu ni Devis Mrope na katibu msaidizi akichaguliwa Francisca Michael, baada ya kupata viongozi kamati nne ziliundwa na wajumbe, Kamati ya Uratibu, Mipango na Fedha, Kamati ya Usafiri na Ulinzi, Kamati ya Mapambo na Burudani pamoja na kamati ya Hotuba na Habari.

  Imeandaliwa na Afisa Habari wa Kamati ya Maandalizi
  Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika - Mwanza

  0 0
 • 04/30/14--01:28: TANGAZO
 • MABADILIKO YA ANUANI YA OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA

  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma inapenda kuwafahamisha wadau wake kuwa anuani yake imebadilika hivyo kuanzia sasa mawasiliano yafanyike kwa kutumia anuani ifuatayo;


  OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA

  UTUMISHI HOUSE

  8 BARABARA YA KIVUKONI

  11404 DAR ES SALAAM

  au

  PRESIDENT’S OFFICE, PUBLIC SERVICE MANAGEMENT

  UTUMISHI HOUSE

  8 KIVUKONI ROAD

  11404 DAR ES SALAAM


  Anuani hii inachukua nafasi ya Sanduku la Posta 2483, Dar es salaam. Hivyo, mawasiliano yote yazingatie anuani mpya.


  Limetolewa na

  Katibu Mkuu

  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma


  Barua pepe; permsec@utumishi.go.tz


  0 0

  Airtel Afisa mauzo wa kanda ya Pwani  William Mrocky akikabithi kwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi Chau Bwana Elvin Msangi msaada wa viti na meza kwaajili ya ofisi ya walimu wa shule ya msingi ya chau iliyoko Chalinze Mkoani Pwani.
  ======  =====  =====

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kupitia shughuli zake za huduma kwa jamii imetoa msaada vifaa kwa ajili ya ofisi ya  walimu kwa shule ya msingi ya Chau iliyoko Chalinze mkoani Pwani.

  Akiongea kwa niaba ya Airtel Afisa mauzo wa kanda ya Pwani  William Mrocky alisema” leo tunayofuraha kutoa msaada wa viti na meza kwaajili ya ofisi ya walimu shuleni hapa, msaada huu unalenga katika kuboresha mazingira ya ofisi  na kuwawezesha walimu kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi.

  Huu ni mwendelezo wetu wa huduma kwa jamii hususani katika sekta ya elimu ambapo kupitia mradi wetu wa “shule yetu” tumeziwezesha shule mbalimbali za sekondari kupata vitabu vya ada na kiada na kukabili changamoto za uhaba wa vitabu mashuleni. Sambamba na vitabu pia tunatoa msaada wa madawati na vifaa vya ofisi kama tunavyofanya leo katika shule hii ya msingi Chau.”Tunaamini msaada huu utaleta tija na kuboresha utendaji wa kazi kwa walimu shuleni hapa” aliongeza Mrocky.

  Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya msingi Chau bwana Elvin Msangi alisema” nashukuru sana Airtel kwa kutufikia shuleni hapa, hii ni mara yakwanza kupokea msada kama huu shuleni hapa hivyo tunajisikia faraja kuona kampuni kama ya Airtel inafanya kazi kubwa katika kusaidia sekta ya elimu. Tunayo mahitaji mengi hapa shuleni, Tunategemea huu ni mwanzo hivyo mtatumkumbuka katika program zetu itakayokuja  siku za usoni.

  Msaada huu utawawezesha walimu kuwa na ofisi nzuri na kuwaboreshea mazingira yao ya kazi kuwa bora zaidi. Airtel kupitia mradi wake wa shule yetu unaziwezesha shule mbalimbali nchini kufaidia na vitabu, zaidi ya shule 900 nchini zimefaidika na mradi huu mpaka sasa.


  0 0

   Mwalimu mkuu shule ya sekondari Mwembetogwa Kelvin Mlengule akitoa maelezo kwa mkuu wa wilaya ya Kilolo Gerald Guninita kuhusiana na mabweni ya wasichana wa shule hiyo.
   Baadhi ya wahitimu wa shule ya sekondari Mwembetogwa
   Mwalimu mkuu shule ya sekondari Mwembetogwa Kelvin Mlengule akitoa taarifa ya shule kwa wazazi na wanafunzi wa shule ya sekondari Mwembetogwa katika mahafali ya 18 ya shule hiyo.
  Mkuu wa wilaya ya Kilolo Gerald Guninita akichangisha fedha kwa wazazi kwa ajili ya ununuzi wa vitanda vya mabweni ya wasichana wa shule ya sekondari Mwembetogwa. (picha zote na Denis Mlowe)

  Na Denis Mlowe,Iringa

  SHULE ya Sekondari ya Mwembetogwa iliyoko katika halmashauri ya Manispaa Iringa inakabiliwa na upungufu mkubwa wa vitanda 160 kwa wanafunzi wa kike wanaotakiwa kuishi katika mabweni yaliyokamilika katika shule hiyo.

  Akizungumza katika mahafali ya 18 ya kidato cha sita na harambee ya kuchangia ununuzi wa vitanda iliyofanyika jana katika ukumbi wa shule hiyo Mkuu wa shule,Kelvin Mlengule alisema upungufu wa madawati umesababisha wanafunzi wa kike wanaotakiwa kuishi shuleni hapo kulazimika kupanga katika nyumba za watu binafsi na kuwasababisha wengi wao kujiunga katika makundi hatarishi na kupata ujauzito.

  Mlengule alisema kwa sasa wapo kwenye mchakato wa kuhakikisha wanapata vitanda kwa ajili ya mabweni ya wasichana ambayo tayari yamekwishamilika huku wakiendelea na mpango wa kujenga mabweni mengine ya wavulana wa kidato cha tano na sita shuleni hapo.

  Alisema harambee iliyofanyika katika mahafali hayo wamepata mchango wa zaidi ya shilingi milioni 10 zikiwemo ahadi kutoka kwa wadau mbalimbali kati ya shilingi milioni 15 zinazohitajika kukamilisha upungufu wa vitanda na milango katika mabweni hayo.

  Kwa upande wake mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dk Christene Ishengoma (Mb), Mkuu wa wilaya ya Kilolo,Gerald Guninita amewataka wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya kuhitimu elimu ya kidato cha sita nchini kutumia muda uliobaki kwa ajili ya maandalizi ya mtihani wa kumaliza masomo yao kikamilifu.

  “Vijana wangu ni vyema mkatumia muda huu mchache ulibaki kwa ajili ya kujiandaa zaidi katika kukabiliana na mtihani wenu mnaotarajia kuanza kuufanya Mei 5nkwa  kuweza kufanya vizuri na kuepuka tabia hatarishi ambazo zinaweza kuwakosesha maisha mazuri hapo mbeleni “ alisema Guninita

  Guninita alisema maadili waliyofundishwa shuleni hapo ni vema wakayatumie vizuri kwa kuwa mabalozi katika jamii wanayoishi na kuepuka vishawishi na tama za kutaka vizuri kuliko uwezo wao na kuwataka kudumisha suala la nidhamu na kukataa kutumiwa na wanasiasa hususani katika suala hili linalo endelea sasa la mchakato wa kupata katiba mpya.
   
  Aidha Guninita ameongeza kuwa wapo wanasiasa watako fanya mikutano na maandamano kwa kuwashirikisha vijana na kuwapatia pesa ili kuleta vurugu kitendo ambacho kinaweza kuhatarisha amani na maisha yao,hivyo wahakikishe kuwa hawajihusishi kwa namna yeyote katika vitendo hivyo.
   
  Pia amewataka wazazi kushiriki kikamilifu katika kutoa michango mbalimbali ya maendeleo katika elimu,na kuacha kuchangia michango mingine isiyo na tija katika jamii zikiwemo harusi na vipaimara.
   
  Katika mahafari hayo kwa niaba ya mkuu wa mkoa Guninita aliahidi kutoa vitanda 40 vyenye thamani ya shilingi milioni 4.8 ikiwemo ahadi yake ya shilingi laki mbili na elfu arobaini kwa ajili kununulia vitanda viwili.

  Shule ya Sekondari  ya Mwembetogwa ni shule inayomilikiwa na wazazi ilianzishwa mwaka 1984 wakati huo ikiwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne pekee na wahitimu waliokabidhiwa vyeti walikuwa 122 kati ya 150 walitarajiwa kuhitimu kidato cha sita.

  0 0

   Tingatinga la Manispaa ya Ilala likibomoa vibanda vilivyojengwa maeneo yasiyoruhusiwa Kariakoo katika operesheni safisha jiji iliyofanyika Dar es Salaam, mitaa ya Aggrey na Livingstone.
   Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakiimarisha ulinzi wakati wa oparesheni hiyo.

  0 0

  Mama mzazi wa Mtangazaji wa Television ya Taifa (TBC1), Angella Michael Msangi, Marehemu Mama Misheli Singoye atazikwa leo Jumatano Aprili 30, 2014 ambapo ibada itaanza saa tatu asubuhi katika Kanisa la Pentekoste, Kigamboni na baada ya hapo safari ya kuelekea kwenye maziko Zinga kwa Awadhi, Bagamoyo Pwani.

  Marehemu Mama Misheli Singoye alifariki Aprili 26, 2014 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa.

  0 0

  Na Miza Kona Maelezo Zanzibar       
  TATIZO la Wananchi  kujichukulia hatua mikononi mwao na matumizi ya nguvu zisizo za lazima kwa baadhi ya vyombo vya dola ni changamoto kubwa inayodhoofisha utekelezaji wa haki za binadamu.
  Hayo yameelezwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria Zanzibar Harusi Miraji Mpatani kwenye  mafunzo ya Haki za Binadamu yaliyoandaliwa kwa ajili ya Waandishi wa habari katika  Ofisi ya Kituo hicho  Migombani Mjini Zanzibar.
  Amesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya watu kujichukulia sheria mikononi mwao  pale inapotokea tuhuma  inayopelekea kuwepo kwa uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu.
  Amesema licha ya juhudi zinazochukuliwa katika kuhakikisha kuwa sheria ya haki za binadamu zinafikiwa kwa jamii,  bado matukio ya uvunjwaji na ukiukwaji  wa Haki za binadamu yanaendelea kutokea nchini.
  “Watoto na walemavu wamekuwa ni wahanga wakubwa wa matukio ya unyanyasaji na udhalilishaji wa kingono, mbali na hali dhaifu ya kimaumbile waliyonayo bado jamii haijabadili mtazamo kuwa kundi hili linahitaji kulindwa kutokana na vitendo hivyo”, alifahamiisha Bi Harusi.
  Aidha ameeleza kuwa waandishi wa habari wanawajibu katika kusimamia haki hizo kwa kutoa taaluma juu ya haki za binadamu kwa jamii wanayoifanyia kazi kwa kutumia vyema kalamu zao ili kujiepusha kuandika habari zinapelekea uchochezi na kusababisha uvunjifu wa haki za binadamu.
  Amewataka Waandishi kufuatilia bila ya woga matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu ili kuweza kuibua matukio mbali mbali ili  sheria iweze kuzifanyia kazi na kuondosha matatizo hayo.
  Mada nane zinatarajiwa kujadiliwa katika mafunzo hayo zikiwemo Ufafanuzi wa katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Haki za Binadamu na nafasi ya Waandishi wa habari katika kusimamia Haki za Binadamu, Utawala bora pamoja na Utawala wa Sheria.
  Mafunzo hayo  ya siku mbili yametaarishwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar  na yanawashirikisha waandishi wa vyombo mbali mbali  vya Habari vya Serikali na biinafsi nchini.
         IMETOLEWA NA MEALEZO ZANZIBAR

  0 0

  Timu ya mpira wa wavu Mbozi akiwa katika picha kabla ya kupambana na wenzao MUst Mbeya. (picha zote na denis mlowe).

  Na Denis Mlowe, Iringa

  Makamu Mwenyekiti wa Idara ya michezo ya Halmashauri ya Manispaa Iringa, Kalulu Nsumba ameiomba Serekali pamoja na wadau wa Michezo kusaidia upatikanaji wa vifaa vya mchezo na viwanja bora  ili waweze kuuendeleza mchezo wa Volleball.
   
  Nsumba ameyasema hayo katika Bonanza la Mchezo huo lililoandaliwa na na Iringa Manispaa Sport Club lilofanyika kwa siku mbili katika viwanja vya Shule ya sekondari Lugalo na kuzilikisha timu nane za mikoa ya Iringa,Njombe na Mbeya.
   
  Amesema mchezo wa volleyball umesaulika na lengo la kuandaa ni kukuza mchezo huo utambulike kama mpira wa miguu na kujenga ushirikiano miongoni mwa vijana wa Nyanda za juu Kusini.
   
   Ameongeza kuwa Nyanda za Juu Kusini kuna vipaji lukuki vya mchezo huo lakini kinachokosekana ni vifaa na viwanja vya mchezo huo na kuwataka wadau kujitokeza kudhamini na kusaida ujenzi wa viwaja bora na kuwataka vijana kujiunga na mchezo huo.
   
  Nsumba amedai kuwa kama kutakuwa na ushirikiano wa kutosha na kuwezeshwa kikamilifu mchezo huo kama ilivyo kwa mpira wa miguu anaamini kuwa Iringa na mikoa ya jirani inaweza kuwa na timu zinazoweza kufanya vizuri katika mashindano ya kitaifa na kimataifa.
   
  Alizitaja timu zilizoshiriki bonanza hilo kuwa ni Iringa Manispaa (IMC), Chuo Kikuu cha Iringa (Tumaini), Chuo Kikuu Kishirikishi cha Mkwawa, Must Mbeya, Mbozi Vollebal Club, Tukuyu Volleball Club, Njombe, Ruco na kuwashirikisha vijana zaidi ya 100.
   
  Aliwashukuru makampuni ya MT.Huwel, Assas, Meneja wa NBC mkoa wa Iringa na Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa Iringa na shule ya sekondari Lugalo kwa msaada waliotoa kufanikisha bonanza hilo linalotarajiwa kufanyika kila mwaka kwa mikoa ya Iringa, Mbeya na Njombe.

  0 0

  Serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imemaliza kupitia Rasimu ya Katiba ya Club ya Simba kwa ajili ya kuidhinisha katiba hiyo na kuifanya Club ya Simba kuendelea na taratibu za uchaguzi mkuu. 

  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Michezo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Leonard Thadeo alipokutana na waandishi wa habari kujibu hoja mbalimbali za waandishi leo jijini Dar es Salaam.

  Akijibu moja ya hoja iliyomtaka kufafanua Wizara imefikia wapi katika upatikanaji wa Katiba ya Club ya Simba Bw. Thadeo amesema kuwa upitiaji wa Katiba umemelizika na kuonekana kuwa na mapungufu machache yanayohitaji kurekebishwa ili Wizara iweze kuidhinisha katiba hiyo.


  “Mchakato wa upitiaji wa Katiba ya Club ya Simba umemalizika jana lakini kumekuwepo na mapungufu machache yanayohitaji kurekebishwa ili Wizara iweze kuidhinisha Katiba hiyo” amesema Bw. Thadeo.


  Akifafanua zaidi Bw. Thadeo amesema kuwa mapungufu hayo yanalenga zaidi upande wa kisheria ambapo mtu anaweza kutafsiri neno vibaya hivyo kupata maana tofauti na Katiba ilivyokusudia hivyo kuitaka Club hiyo kufanya marekebisho hayo mapema na kurejesha Katiba hiyo Wizarani kwa ajili ya kuidhinishwa.  Aidha Bw. Thadeo amewataka waandishi wa habari pamoja na wanachama wa Club ya Simba kuwa na subira ili waweze kupata Katiba itakayokidhi malengo ya Club yao kwani mchakato wa upitiaji wa Katiba ulihitaji umakini.


  Na: Genofeva Matemu – Afisa Mawasiliano Serikalini (WHVUM)

  30TH April, 2014.

  0 0


  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema bila uwekezaji nchi haiwezi kusonga mbele na akawataka watendaji serikalini kubadili mtazamo wao kuhusiana na suala zima la uwekezaji. 

  Ametoa kauli hiyo jana usiku (Jumanne, Aprili 29, 2014) wakati akizungumza na wafanyabiashara na wajasiriamali mbalimbali wa hapa nchini kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa Taasisi ya Mkoba Private Equity Fund inayojishughulisha na utoaji mitaji kwa wajasiriamali wadogo na wa kati. 

  "Bila uwekezaji tunajidanganya... ni ukweli usiopingika kwamba uwekezaji mkubwa unatoka kwenye sekta binafsi, kwa hiyo watendaji wetu serikalini wanapaswa kubadili mtazamo wanaposhughulikia masuala ya sekta binafsi," alisema. 

  Alisema watendaji serikalini wanapaswa kubadili mitazamo yao hasa wanapokuwa wanawasiliana na watu wa sekta binafsi kwa sababu kwa mfanyabiashara yeyote wakati ni mali. 

  "Tanzania imejipanga kuelekea kuwa Taifa lenye uchumi wa kati, kama kweli tunataka kufika huko mapema ni lazima tuwachukulie wadau wa sekta kwa mtazamo wa tofauti. Siyo anakuja kutaka taarifa unaanza kumzungusha bila sababu, anataka kusajili kampuni unamwambia unajua mafaili hayaonekani wakati hakuna cha mafaili wala nini bali unatafuta mwanya wa kudai chochote," alisema. 

  Akizungumzia kuhusu utoaji mikopo kwa ajili ya mitaji ya kibiashara, Waziri Mkuu aliitaka Taasisi ya Mkoba Equity Fund ihakikishe inajenga kwanza uwezo wa wahusika ili waweze kuzalisha mali kama ilivyokusudiwa. 

  Akitoa mfano wake binafsi, Waziri Mkuu alisema wakati anaanza biashara ya ufugaji nyuki miaka mitatu iliyopita, hakuwahi kuandaa mchanganuo wowote (write-up) wala hakuwahi kuandaa mpango wa biashara (business plan). Matokeo yake, alikuwa anatoa tu fedha mfukoni na kununua vifaa kadri mahitaji yalivyokuwa yakijitokeza, jambo ambalo alisema si sahihi. 

  "Ninawasihi sana viongozi wa Mkoba Equity Fund wasitoe mikopo kwa watu wanaotaka kufanya biashara kama nilivyoanza mimi. Wekezeni kwanza kwa kuwajengea uwezo wajasiriamali watakaoomba fedha za mitaji kutoka kwenye taasisi hii," alisisitiza. 

  Akitoa ushauri kwa wajasiriamali wadogo waliotoa shuhuda zao kuhusu changamoto walizokabiliana nazo wakati wakianzisha biashara zao, Waziri Mkuu aliwataka wasirudi nyuma wala wasikate tamaa. "Fursa ni nyingi sana na mnaweza kufanya mambo mengi. Kitu cha msingi ni kuwa na nia thabiti (determination). 

  Wajasiriamali walitoa shuhuda zao ni Mkurugenzi wa kampuni ya Montage, Bi. Teddy Mapunda; Mkurugenzi wa kampuni ya Go-Financing, Bw. Geoffrey Ndossi, Mkurugenzi wa kampuni ya SIGA Ltd, Bw. Marwa Busigara na Mkurugenzi wa kampuni ya WIA, Bw. Eric Mwenda. 

  IMETOLEWA NA: 
  OFISI YA WAZIRI MKUU, 
  S. L. P. 3021, 
  DAR ES SALAAM. 
  JUMATANO, APRILI 30, 2014

  0 0

  Shirikisho la ngumi Tanzania (BFT) linatoa pongezi za dhati kwa Waziri  wa Mambo ya Nchi za Nje Mh. Bernard Membe kwa hatua na jitihada alizozifanya  za kutafua na kufanikisha  kambi ya mazoezi kwa Timu ya Taifa ya ngumi  inayojiandaa kushiriki mashindano ya jumuiya ya madola yatakayofanyika July, 2014 Nchini Scotland.

  Kwa hakika ni mmoja wa watanzania ambae ameguswa na maandalizi ya Timu  yetu ya Taifa kwa kuitafatia  kambi ya mazoezi ya kimataifa Nchini Uturuki na Nchini China kwani timu yetu ilikuwa inafanya mazoezi katika hali duni  bila ya kuwa na vifaa vya kisasa kulingana na mabadiliko ya mchezo wa ngumi duniani.


  Kwa kufanya hivyo tunakuwa na uhakika mkubwa wa kupata medali katika mashindano hayo ya Jumuiya ya Madola na Tanzania kutangazika vema Kimataifa kupitia mchezo wa ngumi maana bado tunakumbuka historia nzuri ya ushiriki waTanzania katika mashindano ya Jumuiya ya madola kwani kwa mara ya kwanza Tanzania ilishiriki mwaka 1972 na Tanzania  kupata medali ya kwanza ya kimataifa baada ya   Tanzania kupata  uhuru, iliyoletwa na Bondia (LYTUS SIMBA) na baada ya hapo baadhi ya mabondia walioleta medali ni kama wafuatao:


  MICHAEL YOMBAYOMBA   :  (Dhahabu)

  HAJI  MATUMLA                     :   (Fedha)

  MAKOYE ISANGURA             :   (Shaba)

  MWAMBEYA   BAKARI        :   (Shaba)

  WILLY  ISSANGURA              :   (Shaba)

  LUCAS MSOMBA                   :   (Shaba)


  Bado BFT tunamuomba azidi kutusaidia  vifaa zaidi hasa ulingo wa kisasa na Computer inayotumika  kuhesabia point za ushindi wakati wa mashindano kwani Nchi zote duniani ndizo wanazozitumia na niagizo kutoka chama cha ngumi cha dunia kwa wanachama wote lazima waitumie katika mashindano..


  Taarifa hii imeletwa kwenu na

                                       

  Makore Mashaga


  KATIBU MKUU.


  0 0

   Nguzo hii ina zaidi ya Mwezi mmoja ikiwa ndani ya nyumba ya mtu na hatari zaidi kwa sababu imelalia katika miti mibichi
   Hivi ndivyo nguzo hiyo inavyo onekana kwa Jirani ikiwa imelalia miti
  Hizi  ni waya zilizopita chini kabisa katika Geti la mtu na ndani ya miti.

   Nguzo ya umeme ya TANESCO ikiwa imekatika katika eneo la Jirani na Daraja la Mlalakuwa ambapo ipo mpaka sasa ikiwa ni zaidi ya mwezi ipo eneo hilo.
   Hii ndio Njia Mbadala waliyo iona TANESCO kutumia kwa kufunga nyaya hizo juu ya Miti baada ya kubadirisha nguzo iliyo haribika
  Hizi ni nyaya za umeme ambazo zimepita Chini ,pia ni hatari kwa watembea kwa miguu
  *****
  Kutokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni   jijini Dar es salaam ambapo mvua hizo zimesababisha uharibifu mkubwa wa mali na  miundo mbinu mbalimbali .

  Uharibifu mkubwa na wahatari  ni katika nguzo za umeme zilizo vunjika  na baadhi ya nyaya zinazo pitisha umeme kushuka chini ambazo ni hatari kwa wananchi.

  Katika eneo la Mlalakuwa  mbele kidogo baada ya kulivuka daraja ukiwa unaelekea kawe  pana nguzo tatu ambapo nguzo moja imevunjika  kabisa na nyingine mbili zimelegea  katika nguzo iliyo vunjika ni mali ya Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) liliweza kufika katika eneo hilo wakachukua hatua ya kufungua nyaya za ile nguzo iliyo katika na kuzifunga juu ya mti ulio pandwa pembeni  mti huo si mkavu ni mbichi.

  Je shirika la umeme la Tanzania madhara ya umeme wananchi watayafahamu vipi wakati ninyi wenyewe wataalamu wa kazi hiyo mnatupotosha, pili sehemu mulipo fungia na nyaya zilipo legea ni sehemu watu wanapo ishi ,hivi huku nikuwajali wateja wenu ?

  Tunaomba  muchukue hatua harakaiwezekanavyo ili kuepusha madhara yanayo weza kujitokeza hapo baadae  kwani ni hatari sana

  Picha na Dar es salaam yetu Blog

  0 0

    Meneja wa Bia ya Serengeti Rodney Rugambo(kulia) akizungumza na wana habari wakati wa droo ya Kumi na mbili  ya promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti inayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti mara baada ya kuchezesha droo hiyo mapema leo katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam na anayemshuhudia ni Afisa Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha  Tanzania  Hummud Abdulhussen(kushoto).
   Meneja wa Bia ya Seregeti kutoka Kampuni ya Bia ya Serengeti Rodney Rugambo pamoja na Afisa Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania Hummud Abdulhussen wakihakiki namba ya mshindi wa tatu wa tiketi ya kwenda Brazili wakati wa droo ya kumi na mbili ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti. 
  Meneja wa Bia ya Seregeti kutoka Kampuni ya Bia ya Serengeti Rodney Rugambo, akiongea na mshindi wa tatu wa tiketi ya Brazili kwa njia ya simu wakati wa droo ya mwisho ya promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti jijini Dar es Salaam huku akishuhudiwa na afisa Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania Hummud Abdulhussen.

  0 0

   Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Simambwe, Salome Mwaipopo (kulia) akizungumza na mwandishi wa habari hizi. Kushoto ni mmoja wa manesi wa kituo.
   Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Simambwe, Salome Mwaipopo (kulia) akizungumza na mwandishi wa habari hizi.
  Sehemu ya jengo la Kituo cha Afya Simambwe, likitoa huduma.
  ======  ======  ======
  Wajawazito walalamikia ‘Rushwa’ Kituo cha Afya Simambwe

  Mbeya Vijijini

  BAADHI ya akinamama na wanakijiji wa baadhi ya vijiji vya Kata ya Tembela Wilaya ya Mbeya Vijijini wamewalalamikia wauguzi na wahudumu wa afya katika Kituo cha Afya Simambwe kwa kile baadhi yao kuwaomba kitu kidogo (rushwa) hasa kwa wajawazito wanapofika katika kituo hicho kupata huduma.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wanawake kutoka vijiji vinavyohudumiwa na kituo hicho vya Usoha Njiapanda, Shibolya, Simambwe, Garijembe, Ilembo Usafwa, Ngoha na Zunya walisema mjamzito amekuwa akiombwa kutoa shilingi 2000 kila anapojifungulia nyumbani kwa dharura baada ya kushindwa kufika katika kituo hicho.

  Mmoja wa akinamama aliyezungumza na mwandishi wa habari hizi ambaye aliomba kutotajwa kwa kuwa huenda akapata taabu kihuduma za afya kituoni hapo, alisema kwa sasa ni jambo la kawaida wahudumu kuwaomba chochote wajawazito kituoni hapo.

  “…Unajua vijiji vingi vinavyohudumiwa na kituo hiki vipo mbali na miundombinu ya barabara si mizuri, yaani hakuna usafiri zaidi ya bodaboda ambazo lazima zitoke Simambwe…sasa kutokana na hali hii inatokea mjamzito anajifungulia nyumbani kwa msaada wa wakunga wa jadi, akipeleka mtoto huyo kituo cha afya basi wanamuomba shilingi 2000 haijulikani ya nini, sasa hili si tunaamini sio haki,” alisema mama huyo.

  Aidha baadhi ya wanakijiji walikilalamikia kituo hicho kwa kitendo cha kulalamika muda wote hakina dawa huku wahudumu wakiwaelekezwa kwenda kununua dawa jambo ambalo wanahisi kuna mchezo mbaya unafanywa na wahudumu hao.

  “Muda wote ukienda kutibiwa utasikia kauli za hakuna dawa tunakuandikia nenda kanunue, tena wengine wanaelekeza hadi maduka ya kununua dawa hizo ndio maana baadhi yetu tunahisi kuna mchezo mbaya (kuhujumu dawa) unaofanywa na baadhi ya wahudumu.,” alisema Mzee aliyejitambulisha kwa jina la Kalamwa.

  Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Simambwe, Salome Mwaipopo  alipinga vikali uwepo wa vitendo vya kuomba rushwa kwa watumishi wa kituo hicho na kudai malalamiko kwa wanachi wanaohudumiwa na kituo hicho imekuwa kitu cha kawaida hasa wanapotembelewa na mgeni.

  “..Hakuna kitu kama hicho unajua wakazi wengi wa vijiji hivi wamezoea kulalamika hasa wanapotembelewa na mgeni…hakuna wanaoombwa fedha, mjamzito akijifungua nyumbani tunampokea bila masharti na kumpatia huduma anazostahili, si kweli wanachokilalamikia,” alisema Mwaipopo.

  Hata hivyo alisema kituo hicho kinahudumia idadi kubwa ya watu zaidi ya uwezo wake jambo ambalo hukifanya kuelemewa kwa idadi ya dawa wanazoletewa, wahudumu na vifaa vingine tiba hivyo kuiomba Serikali kukiongezea mgao wa dawa.

  Kituo kinahudumia idadi kubwa ya watu kupita uwezo wake hivyo unakuta hata baadhi ya changamoto kama ufinyu wa dawa na wahudumu vinatokana na hali kama hiyo…,” alisema Mganga huyo Mkuu wa Kituo cha Afya Simambwe. *Imeandaliwa na www.thehabari.com kwa ushirikiano na TGNP

older | 1 | .... | 277 | 278 | (Page 279) | 280 | 281 | .... | 1897 | newer