Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

Wafanyakazi Wizara ya Fedha waaswa kufanya kazi kwa bidii na kujituma.

$
0
0
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO.

Wafanyakazi Wizara ya Fedha wameaswa kufanyakazi kwa bidii na kujituma kwa moyo ili kukuza uchumi wa nchi na taifa liweze kusonga mbele na kufikia malengo yake. 

Kauli hiyo imetolewa na Mgeni Rasmi ambaye pia ni Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum wakati wa kufungua mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo hivi karibuni jijini Dar es salaam.

“Mnapokuwa kwenye mkutano wenu mjadili bajeti bila kuwa na woga kwa kutumia weledi wenu mlionao na kutoa ushauri na maoni amabayo yatasaidia kujenga na kuimarisha Wizara katika kutekeleza majukumu yake iliyojipangiakwa kuzingatia uhalisia wa uchumi wa nchi” alisema Waziri Saada. 

Katika mkutano huo, Waziri Saada aliwapongeza wafanyakazi hao kwa kufuata maelekezo ya kuwa na vikao vya baraza la wafanyakazi mara mbili kwa mwaka kulingana na mkataba ambapo lengo lamkutano huo ni kupata taafirifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2013/14 pamoja na kupitia na kujadili bajeti ya mwaka 2014/2015.

Aidha, mkutano wa baraza hilo unafanyika kwa kuzingatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete na katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue kuitisha vikao kulingana na utaratibu uliowekwa.

Naye Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Servacius Likwelile akimkaribisha Mgeni Rasmi alisema kuwa mkutano huo ndio una wajibu wa  kupitia na kujadili bajeti ya mwaka uliopita na mwaka ujao wa fedha ambapo bajeti ya Taifa itasomwa Juni 12, 2014.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima alisema kuwa moyo na kiini cha hatima nchi ipo mikononi mwa watumishi wa Wizara ya Fedha, hivyo ameahidi kuwa ofisi yake kwa kushrikiana na Naibu Waziri mwenzake Mwigulu Nchemba ipo wazi wakati wote ili kuweza kusukuma maendeleo ya nchi.

Akimshukuru Mgeni Rasmi kwa niaba ya wajumbe wa mkutano huo, Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Elizabeth Nyambibo alisema kuwa wajumbe wamemsikia na watafanya kazi kwa bidii na kuwa wabunifu ikiwa ni pamoja na kuwapa ushirikiano viongozi wao walioteuliwa na Rais ili waendelee kuwa “Majembe” katika Wizara hiyo.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wajumbe kutoka nchi nzima ambao watahakikisha  nchi imefika hatua ya kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 kulinganana na malengo iliyojiwekea katika mpango mkakati wake.

MAMA SHUJAA WA CHAKULA WAINGIA RASMI KIJIJI CHA MAISHA PLUS, PROFESA ANNA TIBAIJUKA MGENI RASMI KATIKA SHEREHE HIZO.

$
0
0
Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi wa pili kutoka kulia pamoja na Babu wa Kijiji cha Maisha Plus akiwasalimia akina mama Shujaa wa Chakula ambao wameingia Rasmi Kijiji cha Maisha Plus Jana usiku.
Akina Mama Shujaa wa Chakula Wakiwa wanamuimbia wimbo maalum Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi mara baada ya kuwasili Kijijini hapo.
Hawa ndio Mama Shujaa wa Chakula ambao jana usiku wameingia Rasmi katika Kijiji Cha Maisha Plus
Baadhi ya wageni waalikwa waliofika kushuhudia Kukaribishwa Rasmi kwa Mama shujaa wa Chakula katika Kijiji cha Maisha Plus.


Mshindi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2012 Sister Anna Mwasu wa tatu kutoka kulia akiwa katika sherehe za kuwakaribisha mama Shujaa wa Chakula ambao  wameingia rasmi katika Kijiji cha Maisha Plus Jana.
Mwakilishi kutoka Forum CC Faidhari akizungumza jambo wakati wa kuwakaribisha Mama Shujaa wa Chakula katika Kijiji cha Maisha Plus.
Teresa Yates Mwakilishi kutoka OXFAM akitoa salama za Shukurani kwa wadau wote
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mh. Ahmed Kipozi akiwakaribisha Rasmi wageni wote katika Kijiji cha Maisha plus pia kumkaribisha Mgeni Rasmi Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi  ili aweze kutoa hotuba yake
Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi wa katikati akitoa hotuba yake fupi wakati wa Sherehe za kuwakaribisha Mama Shujaa wa Chakula katika Kijiji cha Maisha Plus, katika Hotuba hiyo aliwapongeza waandaaji na wabunifu wa Shindano hilo, pia Grow kupitia OXFAM kwa kuungana na Maisha Plus kuwaleta Mama Shujaa wa Chakula, Mwisho aliahidi kuongeza Milioni 5 kwa Mama Shujaa wa Chakula atakaye nyakua ushindi, Kutoa Milioni mbili na nusu kwa Mama Shujaa wa Chakula aliyepita ili zikamsaidie katika kilimo na Mwisho Kutoa Milioni Mbili kwa Washiriki wa Shindano la Maisha Plus ambao sasa wamebakia 16 mpaka mwisho wa Shindano Tarehe 18.05.2014
Mmoja wa washiriki wa Maisha Plus akisoma Jina la Mama yake ambaye atakuwa naye katika Kipindi hiki kilicho bakia cha Shindano la Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula.
Vijana na Washiriki wa Maisha Plus wakiwa na Mama zao walezi ambao ndio wameingia Rasmi kijijini Jana
Huyu Ndiye Mama Shujaa wa Kwanza kupata nafasi ya Kuwa Markia wa Kijiji cha Maisha Plus Mary J. Mwanga, na wa kwanza kulia ni Rais wa Kijiji cha Maisha Plus Abisai Caron kutoka kenya hapa akiwa anavishwa kofia ya utambulisho na Epheta Msiga Meneja Miradi kutoka DMB
Picha ya Pamoja Mgeni Rasmi  Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi, Wakina Mama Shujaa wa Chakula, Vijana wa Maisha Plus pamoja na wadau mbalimbali waliofika katika sherehe za kuwakaribisha Mama Shujaa wa Chakula  Kijiji cha maisha Plus
Mkurugenzi Mtendaji wa DMB ambao ndio waendeshaji wa Shindano la Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula Ally Masoud(Masoud Kipanya) Akitoa utaratibu wa jinsi Akina mama Shujaa wa Chakula watakavyo ishi na vijana hao katika kijiji hicho
Mama  Shujaa wa Chakula wakipata maelekezo Mbalimbali juu ya Kijiji Hicho
Moja ya Bendi Matata kutoka Bagamoyo wakiwa wanatumbuiza nyimbo Nzuri wakati wa kuwakaribisha Mama Shujaa wa Chakula katika Kijiji Cha maisha Plus


Wakipokea maelekezo kadha wa kadha
MAISHA PLUS/ MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2014

UNDP TRAINS NEC AND ZEC SENIOR OFFICIALS ON ELECTION MANAGEMENT

$
0
0
Twenty (20) senior staff from the National Electoral Commission (NEC) and the Zanzibar Electoral Commission (ZEC) will undergo a two-week train-the-facilitator programme based on the internationally renowned BRIDGE at the Oceanic Bay hotel in Bagamoyo. 

The training is expected to usher the two electoral management bodies (EMBs) in a new era of improved professional conduct of elections through the use of own staff to conduct BRIDGE or any other electronic training for both short term and long term professional development. 
BRIDGE stands for “Building Resources for Democracy, Governance and Elections” and is comprehensive professional electoral curriculum based on adult-learning and participatory methodology. The two-week training will be a Train-the-Trainer (TtF) programme which will introduce the 20 EMB participants to the BRIDGE methodology and tools which they can use to undertake own EMB electoral training using the BRIDGE curriculum, methodology and related resources.  

Speaking at the official opening session of the training today, UNDP Country Director Mr Philippe Poinsot, said the training which is sponsored by UNDP through its Democratic Empowerment Project (DEP) will seek to improve the capacity of the EMBs to undertake long term professional development for their own staff thereby fostering credible, transparent and peaceful elections in the country. It will specifically help the two electoral management bodies (EMBs) to prepare for the referendum and the 2015 general elections.

 “Training of this nature is best conducted during the pre-election phases of the electoral cycle so as to ensure that EMBs capacity is enhanced long before the commencement of the hustle and bustle of the election campaign period”, he said.

In his keynote address, the NEC’s Chairperson, Judge Damian Lubuva, welcomed the training opportunity saying it will go a long way to enhance the democratic process in the country through well run elections which inspire public confidence and stakeholder trust in the EMBs, especially in 2015. “Credible elections can guarantee peace and stability in our country, therefore this training is a great step in our collective effort to conduct elections in a professional and credible way. This will help Tanzania become an example of best practices in election management, not only for our region but for other parts of the world”, he said.  Justice Lubuva requested participants to work hard and ensure they acquire new skills which they can plough back in their respective institutions.

Participants in the BRIDGE programme will undergo a certification process that will qualify them as semi-accredited trainers. After two weeks of both theoretical and practical training, participants will be assessed for certification as BRIDGE semi-accredited trainers. After such certification, the candidates will participate in further assessment and training based on BRIDGE modular.
The training is supported by DEP which is a three-year electoral cycle support project (2013-2016) funded by various development partners through a basket. This includes Canada, Denmark, the European Commission, Finland, Ireland, Norway, Sweden, Switzerland, the United Kingdom and UNDP. The 22 million-dollar project seeks to give capacity to democratic institutions, such as the EMBs, the police, judiciary, political parties to support credible, transparent and peaceful 2015 elections in Tanzania. The project also supports greater inclusion of women, youth and people with disability and giving them a voice in decision making processes including elections.

The two EMBs are expected to conduct more BRIDGE training programmes especially after the 20 trainees in this TtF have acquired full BRIDGE accreditation.  The goal of the DEP is to ensure that between our EMBs, Tanzania has adequate capacity to conduct BRIDGE training by using Tanzanians who are fully-accredited BRIDGE facilitators. Notably, once accredited, BRIDGE facilitators will be in a position to train election officials in other parts of the world.

BENKI YA CRDB YASHIRIKI MAONESHO YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU

$
0
0
 Baadhi ya wanafunzi wakipata maelezo katika banda la Benki ya CRDB wakati wa  wakati wa maonesho kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo vikuu na kuandaliwa na Chama cha Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania (AIESEC), kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzia kujifunza na kujitambua uwezo wao binafsi na mchango wao katika jamii.
 Ofisa Rasilimali Watu wa Benki ya CRDB, Petro Kashindye (kushoto), akifafanua jambo wakati wa maonesho kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo vikuu na kuandaliwa na Chama cha Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania (AIESEC), kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzia kujifunza na kujitambua uwezo wao binafsi na mchango wao katika jamii.
 Baadhi ya wanafunzi wakipokea zawadi kutoka kwa Ofisa Masoko wa Benki ya CRDB, Ninael Munuo waliotembelea banda la benki hiyo  wakati wa kongamano la wanafunzi lililoandaliwa na Chama cha Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania (AIESEC), kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wa vyuo vikuu kujifunza na kujitambua uwezo wao binafsi na mchango wao katika jamii. Kongamano hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
 Ofisa Rasilimali Watu wa Benki ya CRDB,Adam Geni (wa pili kushoto), akifafanua jambo kuhusu huduma zinazotolewa na Benki ya CRDB wakati wa kongamano la wanafunzi lililoandaliwa na Chama cha Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania (AIESEC), kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wa vyuo vikuu kujifunza na kujitambua uwezo wao binafsi na mchango wao katika jamii. Kongamano hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Ofisa wa benki hiyo, Casmir Fissoo.
 Masoko wa Benki ya CRDB, Ninael Munuo (kushoto), akitoa maelezo ya huduma mbalimbali zinazotolewa na benki ya CRDB kwa wanafunzi wa wanafunzi wa vyuo vikuu waliotembelea banda la benki hiyo  wakati wa kongamano la wanafunzi lililoandaliwa na Chama cha Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania (AIESEC), kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wa vyuo vikuu kujifunza na kujitambua uwezo wao binafsi na mchango wao katika jamii. Kongamano hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.

VETA YAENDESHA SEMINA KWA WABUNGE WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HUDUMA ZA JAMII JUU YA MRADI WA KUONGEZA SIFA ZA KUAJILIWA - EEVTJIJINI DAR

$
0
0
Mh Jenista Mhagama (Kushoto) akiongea na baadhi ya wabunge kutoka Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii na baadhi ya wafanyakazi wa VETA kutoka Makao Makuu na VETA Kanda ya Kusini wakati wa semina iliyoandaliwa na VETA   Kwaajili ya wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii juu ya mradi wa Kuongeza sifa za kuajiliwa - EEVT iliyofanyika katika Ukumbi wa Benki wa Kuu ya Tanzania, Jijini Dar Es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh Magreth Sitta na Kulia ni Steven Ngonyani.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, Mh Magreth Sitta (Katikati) akiongea wakati wa semina iliyoandaliwa na VETA kwaajili ya Kamati hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Benki kuu ya Tanzania leo Jijini Dar Es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa VETA Tanzania, Mh Mhandisi Zebadiah Moshi(kulia) akifungua semina iliyoandaliwa na VETA kwaajili ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Kijamii loe katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Mh Mhandisi Zebadiah Moshi akiongea wakati wa semina iliyoandaliwa na VETA kwaajili ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii leo
Mkurugenzi wa Soko la Ajira, Mipango na Maendeleo Kutoka VETA, Bw Enock Kibendela akitoa mada juu ya mchango mkubwa unaotolewa na VETA Katika kukuza sekta ya ajira kwa vijana wanaopata mafunzo ya ufundi stadi wakati wa semina iliyoandaliwa na VETA kwa wabunge wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii leo katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania.
Baadhi ya wabunge wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii pamoja na wafanyakazi wa VETA waliohudhuria semina iliyoandaliwa na VETA Kwaajili ya wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii juu ya mradi wa Kuongeza sifa za kuajiliwa - EEVT.

MUENDELEZO WA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA MUUNGANO HUKO UGHAIBUNI

$
0
0
Katika kilele cha kusherehekea Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Timu ya  Zanzibar Heroes kupokea Jezi kutoa kwa wadhaminini wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) ambazo jezi hizo zilitolewa na wageni rasmi walihudhuria katika sherehe hizo akiwemo Mh. Mwigulu Nchemba  ambae ni Mbunge na naibu waziri wa fedha na Uchumi Tanzania bara na upande wa Zanzibar pamoja na Mhe. Dr. Mwinyihaji Makame mwakilishi na waziri wa nchi ofisi ya rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Zanzibar. (Picha zote na swahilivilla.blogspot.com)
Naibu Mwakilishi Balozi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa mataifa New York, Ramadhani Muombwa Mwinyi (kulia) akiwa pamoja na Viwe Juma, ambae ni Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara ya BENKI ya Watu wa Zanzibar (PBZ) ambao ni wadhamin wa timu hiyo wakimkabidhi jezi nahodha wa timu ya Zanzibar Heroes Abuu Qullatein Siku ya Jumamosi April 26, ndani ya Ubalozi wa Tanzania jiji Washington DC nchini Marekani, ili kujianda kupambana na timu ya Kilimanjaro Stars kwa mchezo wa kuwania Kombe la Muungano. 
Viongozi: Wageni rasmi wa sherehe za Muungano  Mhe: Mwigulu Nchemba (wapili kulia) akifuatiwa na Balozi Mulamula, pamoja na Balozi wa Waziri wa Nchi Zanzibar, Ofisi ya Rais na MBM Dr. Mwinyihaji Makame, (wakwanza kulia) Viwe Juma,wapili kulia  ambae ni Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara ya Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) wakimkabidhi jezi nahodha wa timu ya Zanzibar Heroes Abuu Qullatein katika Sherehe za Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Jijini Washington DC.
Wasimamizi wa timu ya Zanzibar Heroes Seif Ameir na Dedie Rouba wakionyesha jezi walizodhaminiwa na (PBZ) Benki ya Watu wa Zanzibar.
Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara ya Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Viwe  Juma akipata picha ya pamoja na Miss Tanzania USA
Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara ya Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Viwe  Juma akipata picha ya pamoja na wanamitindo wa Mitindo Night.
Mwenyekiti wa Zanzibar Diaspora Asociation Bwana Omari Ali akipata picha ya pamoja na mgeni ndani ya Ubalozi wa Tanzania uliopo Jijini Washington DC Nchini Marekani
  
Miss Tanzania USA  akipata picha ya pamoja na  wanamitindo wa Mitindo Night

KAMATI YA FEDHA, BIASHARA NA KILIMO YA MARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR YATEMBELEA KIWANDA CHA SUKARI MAHONDA

$
0
0
 Muonekano wa Kiwanda cha Sukari Mahonda kilivyo hivi sasa.
  Mshauri muelekezi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda Dk. Hamza Hussein Sabri (alie simama) akitoa maelezo na changamoto wanazozipata Kiwandani hapo, kwa Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ya Baraza la wawakilishi walipoenda kutembelea Kiwanda hapo.
 Makamo Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ya Baraza la wawakilishi Hija Hassan Hija akizunguza na uongozi wa Kiwanda cha Sukari na viongozi wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko katika kuangalia hatua ya uzalishaji Sukari Kiwandani hapo na changamoto wanazokabiliana nazo.
 Afisa utumishi wa Kiwanda hicho Bw. Bashir Mohammed akionyesha kiroba cha kilo 50 za Sukari. 
 Mkurugenzi wa maendeleo ya viwanda Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Bw. Saleh Suleiman Hamad akiwaonyesha wajumbe wa Baraza la wawakilishi Sukari iliozalishwa kiwandani hapo ambayo bado haijaingia sokoni hadi sasa. (Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

Wastaafu watakiwa kuhakiki taarifa za mafao yao ya uzeeni

$
0
0
Meneja Uhusiano na Masoko kutoka Mfuko wa Pensheni wa PPF Bi. Lulu Mengele akiongea na waandishi wa Habari( Hawapo Pichani) kuhusu wastaafu kwenda kuhakiki taarifa za mafao katika Ofisi za Mfuko huo, wakati wa Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Frank Mvungi.
Baadhi ya waandishi wa Habari waliohudhuria Mkutano huo wakimsikiliza Meneja Uhusiano na Masoko kutoka Mfuko wa Pensheni wa PPF Bi. Lulu Mengele wakati wa Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam.Picha na Georgina Misama

Serikali imetumia zaidi ya Shilingi Bilioni 111 kununua mazao kwa wakulima.

$
0
0

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula Bw. Charles akiongea na waandishi wa Habari( Hawapo Pichani) kuhusu mafanikio yaliyopatikana na wakala hao ikiwamo kutumia Zaidi ya Bilioni 111 kununua mazao kwa wakulima katika kipindi cha Mwaka 2013/2014. wakati wa Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mipango na Uendeshaji wa wakala huo Bi. Anna Mapunda.

Baadhi ya waandishi wa Habari waliohudhuria Mkutano huo wakimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula Bw. Charles wakati wa Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam. Picha na Georgina Misama

Frank Mvungi
SERIKALI imetumia zaidi ya Shilingi Bilioni 111 kununua mazao kwa wakulima katika kipindi cha mwaka 2013/2014 ikiwa ni malipo  kwa wakulima  baada ya kuiuzia  nafaka Serikali.

Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Charles Walwa wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akieleza mafanikio yaliyofikiwa na  wakala huo.

Walwa alisema kuwa wakala huo umeweza kuongeza kiasi cha nafaka zilizonunuliwa kutoka kwa wakulima kutoka  tani 61,587.784 mwaka 2008/2009 hadi tani 219,377.282 mwaka 2013/2014 ikiwa ni matokeo ya kuboreshwa kwa mifumo ya utendaji wa wakala huo.

“Hadi kufikia Desemba 31 mwaka 2013 wakala ulinunua tani 219,377.282 za nafaka sawa na asilimia 110 ambapo tani 218,878.600 ni mahindi na tani 498.682 ni mtama” alisema Walwa.

Aliongeza kuwa wakala umeingia makubaliano ya mashirikiano ( Memorandum  of Understanding(MOU)  na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) ili kuwahakikiishia wakulima soko la uhakika.

Katika kutekeleza makubaliano  na WFP  Walwa alisema kuwa wakala umeuza tani 80,000 mwaka 2011/2012 ambapo kwa sasa wakala unaendelea kutekeleza mkataba mwingine wa kuuza tani 23,000 kwa mwaka 2013/2014.

Katika hatua nyingineWalwa alisema kutokana na mfumo mzuri wa manunuzi ya nafaka kutoka kwa wananchi,  ajira za muda kwa wananchi takribani 3000 zizizalishwa na makundi mbalimbali ya wananchi wakati wa kukusanya nafaka tatika maeneo mbalimbali hapa nchini.


Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula umepanga kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka kutoka tani 241,000 za Sasa hadi tani  laki 400,000 ifikapo mwaka 2016 na Tani 700,000 ifikapo mwaka 2024.

HAFLA MAALUM YA SHEREHE ZA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA HOTELI YA MARRIOTT

$
0
0
IMG-20140427-WA0002Mfanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Washington Dc Bi.Mariam Mkama akijiandaa na mpango mzima wa kukaribisha wageni katika hafla maalum iliyofanyika katika hoteli ya Marriot Washington Dc Jumamosi Aprili 26,2014. IMG-20140427-WA0003Jopo la wafanyakazi wa ubalozi wa Tanzania katika mapokezi na mpangilio mzima wa shamra shamra za sherehe rasmi ya miaka 50 ya muungano wa Tanzania kutoka kushoto Bi.Nyamiti Lusinde,Bi. Mariam Mkama na Bi.Rose Commodore katika hoteli ya Marriot iliyopo Washington Dc ambapo ilifanyika hafla maalum ya sherehe za muungano ambapo serikali ya Marekani iliwasilishwa na naibu waziri mdogo wa mambo ya nje Donald Teitelbaum. Kwa picha zaidi ungana na Sundayshomari.com

EXIM BANK TAKES PART AT CARRIER DAY FAIR AT UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM

$
0
0
 Exim Bank Sales Executive Isaac Mwita (second right) speaks to University of Dar es Salaam (UDSM) students when they visited the bank’s pavilion during the Carrier Day Fair held at University of Dar es Salaam at the weekend. First right is the Exim Bank, Banking Officer Berry Chapaulinge. 
 Exim Bank Sales Executive Isaac Mwita (left) speaks to University of Dar es Salaam (UDSM) students when they visited the bank’s pavilion during the Carrier Day Fair held at University of Dar es Salaam at the weekend.   
Exim Bank Sales Executive Paschal Mosha (first left) takes students through Exim Bank brochures which have details about services provided by the bank during the Carrier Day Fair held at University of Dar es Salaam at the weekend. 

WATU 14 WAFARIKI KATIKA AJALI MKOANI SINGIDA USIKU WA KUAMKIA LEO

$
0
0
WATU 13 akiwemo askari wa kikosi cha usalama barabarani wamepoteza maisha baada ya kugongwa na basi la kampuni ya Sumry lililokuwa likitoka Kigoma kwenda Dar katika kijiji cha Ikungi mkoani Singida usiku huu. 

Ajali hiyo ilitokea baada ya ajali ya kwanza iliyolihusisha lori lililomgonga mwendesha baiskeli aliyepoteza maisha papo hapo na wakati wananchi wakiwa wamekusanyika eneo hilo la ajali huku trafiki akiendelea kupima ajali hiyo, lilitokea basi la kampuni ya Sumry na kuwagonga watu hao pamoja na trafiki na kupelekea jumla ya watu 14 kupoteza maisha eneo hilo. 

Basi hilo lililokuwa likitokea Kigoma kwenda Dar halikuweza kusimama eneo hilo mpaka dereva wake alipokwenda kujisalimisha kituo cha polisi Ikungi, Singida. Miili 14 ya waliopoteza maisha katika ajali hiyo imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Singida pamoja na majeruhi wawili waliopelekwa hospitalini hapo. 

MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!

Community Health Workers boosts maternal health services in Tanzania

$
0
0
 Prof Japhet Killewo, a medical doctor and Epidemiologist from Muhimbili University, speaks to experts who convened in Dar es Salaam to share research findings and discuss meaningful policies to address maternal and newborn health in Tanzania. The third year dissemination workshop was sponsored by the United States Agency for International Development (USAID) and organized by partners within the Ministry of Health and Social Welfare, Muhimbili University, Johns Hopkins University and Tunajali.
 Assistant director, Reproductive and Child Division in the ministry of Health and Social Welfare, Dr Neema Rusibamayila specks during a two days workshop on evaluation of the integrated maternal and newborn healthcare programme in Morogoro (year three) by the Muhimbili University of Health and Allied Sciences and the Johns Hopkins University in partnership with the Ministry of Health and Social Welfare and Junajali, whose target is to reduce maternal and infant mortality.
 Mainen Moshi, Director of research and publications at Muhimbili University of Health and Allied Sciences specks during a two days workshop on evaluation of the integrated maternal and newborn healthcare programme in Morogoro (year three) by the Muhimbili University of Health and Allied Sciences, the Johns Hopkins University and Tunajali in partnership with the Ministry of Health and Social Welfare, whose target is to reduce maternal and infant mortality.
A section of experts who convened in Dar es Salaam for a two days seminar to share research findings and to discuss meaningful policies to address maternal and newborn health in Tanzania, shares a light moment as they follow the proceedings. The meeting was sponsored by the United States Agency for International Development (USAID) and organized by partners within the Ministry of Health and Social Welfare, Muhimbili University, Johns Hopkins University and Tunajali.
Assistant director, Reproductive and Child Division in the ministry of Health and Social Welfare, Dr Neema Rusibamayila (seated center) in a group photo with experts who convened in Dar es Salaam for a two days seminar to share research findings and to discuss meaningful policies to address maternal and newborn health in Tanzania. The meeting was sponsored by the United States Agency for International Development (USAID) and organized by partners within the Ministry of Health and Social Welfare, Muhimbili University, Johns Hopkins University and Tunajali.
======  =====  ======
Community Health Workers boosts maternal health services in Tanzania 


Evidence is showing that Maternal and Newborn Child Health Community Health Workers (MNCH CHWs) in the country are playing key roles in bridging the gaping gaps of improving maternal services.



During a presentation yesterday at the evaluation of integrated maternal and newborn health care programme in Morogoro region, the Tunajali Technical Director, Mr Protas Ndayanga said that in the five regions they operate, between July last year and March this year, they helped track 20,000 HIV/AIDS patients.



"Of these that they tracked, there were 5,500 for three days didn't show up for their appointments and the community health worker tracked them down and recorded the results. The biggest challenge they face is when the patients don't provide the correct address," he explained.



Results from the third year of the Morogoro Evaluation Project indicate that 99 per cent of all CHWs are happy working and that 90 per cent felt their work to be valued by both the health facility workers and the community.



High levels of satisfaction was reported for the availability of job aids (90 per cent) and registers (91 per cent); level and quality of training received (90 per cent) and quality of their own work (88 per cent).



"Almost all (93 per cent) were unsatsified with the availability of transport used for care provision and for travel to the health facility and 80 per cent of CHWs were dissatisfied with financial incentives provided," the interim report read in part.



During the opening of the two day dissemination workshop of the report, the Ministry of Health and Social Welfare Director of Preventive Services, Dr Neema Rusibamayila said that the findings of the evaluation would allow key adjustments for optimal performance of the project and inform the policy.



Dr Rusibamayila said that the workshop was a follow up of two workshops held in January 2012 and March 2013 which also aimed at sharing findings from the first and second year of the activities implemented by the project.



"The reports of these dissemination workshops showed that, there was critical information provided which was used to adjust programme strategies. In addition, the workshops fostered closer collaboration among stakeholders," she said.



In her keynote speech, the USAID Country Representative, Dr Raz Stevenson said that in this evaluation, the project activities aimed at assess the role of CHWs and the CHW support systems in delivering an integrated package of interventions.





Dr Stevenson said the research aimed to both assess the functionality of the recurrent integrated CHW programme, as well as to generate information to feed into planning for a national scale-up of the facility and community based intervention package.

Airtel yazindua whatsapp, Facebook na Twitter bure kupitia Vifurushi vya yatosha

$
0
0
·       Yatangaza facebook, whatsapp and twitter BURE
·       Sasa wateja kupata whatsapp, Facebook na Twitter bure kupitia yatosha bando
  kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa kutoa huduma bora imezindua huduma ya kibunifu itakayowawezesha wateja wake kupata na kuunganishwa kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook, Whatsapp na twitter BURE kupitia huduma ya Airtel yatosha.

Akiongelea kuhusu huduma hiyo Mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya alisema” sasa ni bure kabisa kwa wateja wetu wote wa Airtel kuunganishwa na mitandao ya kijamii ya Whatsapp, Facebook na Twitter. Airtel tunayofuraha kutoa nafasi kwa wateja wetu kuwasiliana na marafiki na familia kupitia mitandao hii ya kijamii bure bila makato yoyote, huku tukiendelea kuthibitisha kuwa Airtel Yatosha ni BABA LAO!”
Aliongeza kwa kusema mteja yoyote atakayenunua kifurushi cha data cha yatosha kuanzia sasa iwe ni cha siku, Wiki au Mwezi vifurushi vyao vya internet vya MB au GB  hazitakatwa katika matumizi ya Facebook, Whatsapp na Twitter na badala yake wataweza kutumia vifurushi vyao vya data kwenye kuperuzi katika mitandao mingine kama vile YouTube na mingine mingi kadri ya mahitaji yao”
Akiongea kuhusu namna ya kujiunga Meneja Masoko wa Airtel Bi Upendo Nkini alisema” ili kupata Whatsapp, Facebook na Twitter BURE wateja watatakiwa kupiga *149*99# kisha kuchagua kifurushi kinachowafaa na kuanza kufurahia BURE Whatsapp, Facebook na Twitter”
“Sambamba na hilo katika kuendeleza ubunifu na kurahisiaha upatikanaji wa vifurushi vya Yatosha,  tumewawezesha wateja wetu  kutumia simu za kununua vifurushi vya yatosha kwa ajili ya marafiki zao familia na kubaki wakiwa wameunganishwa na kufurahia mitandao hii ya kijamii ya Whatsapp, Facebook na  Twitter BURE, furahia kuunganishwa katika mawasiliano kupitia mtandao wa Airtel” aliongeza Nkini

ZIARA YA SADIFA YATIKISA KATA YA KAWE

$
0
0
 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM, Taifa, Sadifa Juma (wapili kushoto) akiwasili kwenye Uwanja wa Mkutano eneo la Tanganyika Packers, Kawe Dar es Salaam, Jumapili, Aprili 27, 2014 ambako mbali na kuhutubia mkutano wa hadhara, alikabidhi vifaa vya michezo kwa timu mbalimbali za soka katika kata ya Kawe. Kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Kawe, Lilian Rwebangila na Katibu wa UVCCM wa kata hiyo, Aisha Katundu na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Kata hiyo Said Herry.
 Vijana wa CCM na wananchi kwa jumla wakimsindikiza Sadifa, kwa hamasa kuingia uwanjani
 Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM (Bara) Mfaume Ali Kizigo akihutubia kwenye mkutano wa hadhara wa UVCCM uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe Dar es Salaam, Jumapili ya Aprili 27, 2014, kumkaribisha Sadifa kuhutubia.
 Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Kawe Lilian Rwebangila akimkaribisha Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Hamis Juma, kuhutubia mkutano huo wa hadhara kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe.
 Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Hamis Juma, akihutubia mkutano wa hadhara huku shamrashamra zikitawala, kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, Dar es Salaam, Jumapili Aprili 27, 2014.
 Sadifa akigawa vifaa vya michezo kwa kiongozi wa timu ya soka ya Ukwamani Shooting, wakati wa mkutano huo
 Mlezi wa UVCCM Kata ya Kawe, Coolman Massawe, akikabidhi vifaa vya michezo kwa kiongozi wa timu ya Ukwamani, Ali Kidogodogo, wakati wa mkutano huo.


 Sadifa (kushoto) akishuhudia wakati Katibu wa CCM wilaya ya Kinondoni, Athuman Shemsha, akimtawaza Kada wa CCM, Vincet Massawe, wakati wa mkutano wa hadhara wa UVCCM  uliofanyika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, Dar es Salaam, Jumapili, Aprili 27, 2014

 Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma Hamis akimwelekeza jambo, Kamanda wa UVCCM Kata ya Kawe, Vincent Masawe wakati wa mkutano huo
 Kamanda wa UVCCM Kata ya Kawe, Masawe akishukuru kwa kupewa ukamanda huo. Kushoto ni Sadifa akimsikiliza 
 Katibu wa UVCCM Kata ya Kawe, Dar es Salaam, Aisha Kitundu (katikati) akiwa na Wasanii wa Kikundi cha TOT, Malkia wa Mipasho Nchini, Khadija Kopana na Jane Komba wakati wa mkutano huo
 Viajana wa Kikosi kazi cha UVCCM Kata ya Kawe wakipozi kwa picha maalum ya kumbukumbu wakati wa mkutano huo.
 Baadhi ya viongozi wa CCM na UVCCM Kawe waliohudhuria kwenye mkutano huo. Kushoto ni Kamanda wa UVCCM Kawe,Aisha Voniatis na Mlezi wa Wazazi Muta Rwakatare
 Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM (Bara) Mfaume Ali Kizigo akiwa na viongozi wa Chipukizi, Nimka Lameck (Mwenyekiti wa Chipukizi Taifa) na Maleo Motelo (Mwenyekiti wa UVCCM Kinondoni) baada ya uzinduzi wa Tawi UVCCM la Kawe, Mnarani, Dar es Salaam, Jumapili, Aprili 27, 2014.
 Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Hamis Juma akizindua Tawi la UVCCM, Kawe Mnarani, DSar es Salaam, Jumapili, Aprili 27, 2014. 
Kamanda wa UVCCM Kawe, akitoa mchango wa sh.  200,000 kwa Ktb wa tawi la UVCCM Mnarani, Mlangala Zacharia kwa ajili mradi wa maendeleo ya tawi hilo. Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog

Ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria waadhimisha miaka 50 ya Muungano.

$
0
0
 Balozi wa Tanzania chini Nigeria Mh. Daniel Ole Njoolay akifungua kongamano la Biashara na uwekezaji katika Hoteli ya Sheraton jijini Abuja Nigeria ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizoandaliwa na ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria. 

 Mjumbe wa  Bodi ya Wakurugenzi wa TTB Bibi Teddy Mapunda akizungumza wakatio Alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu vivutio vya utalii vta Tanzania katika kongamano la biashara na uwekezaji jijini Abija nchini Nigeria. 

 Mh. Daniel Ole Njoolay, Balozi wa Tanzania nchini Nigeria akikata keki huku akishuhudiwa na mwakilishi wa wa rais wa Nigeria Goodluck Jonathan (wa pili kulia) na baadhi mabalozi wanaowakilisha nchi zao Nigeria katika tafrija iliyotayarishwa na ubalozi wa Tanzania kusherehekea miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyikakatika hotel ya Sheraton jijini Abuja Nigeria.

Kikundi cha  ngoma za asili cha Abuja Nigeria  kikitoa burudani ya ngoma katika tafrija kusheherekea miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika hoteli ya Sheraton jijini Abuja.




Na: Geofrey Tengeneza – Abuja Nigeria


Jumuiya ya wafanyabiashara, wawekezaji na wananchi wa Nigeria kwa ujumla, wameombwa kuja kuwekeza kwa ujumla na kutembelea vivutio vya utalii mbalimbali vinavyopatikana nchini Tanzania.


Hayo yamesemwa na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mheshimiwa Daniel Ole Njoolay katika maadhimisho ya miaka hamsini 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania) yalioandaliwa na ofisi ya ubalozi  waTanzania nchini Nigeria na kufanyika katika Hoteli ya Sheraton jijini Abuja.


Akiongea wakati wa ufunguzi wa kongamano hili la Biashara na Uwekezaji, Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mheshimiwa Daniel Ole Njoolay amesema Tanzania inajivunia muungano wake ulioasisiwa na Hayati Baba wa Taifa la Tanzania Mwl Julius Nyerere na Hayati Abeid Aman Karume muasisi wa Zanzibar mnamo tarehe 26 April, 1964 ambao sasa umetimia miaka 50.


“Watanzania tunajivunia sana muungano wetu kwani ni wa kipekee sana hapa barani Afrika, na ni muungano uliodumu kwa muda mrefu zaidi kuliko muungano wowote ule Barani Afrika”…alisema  Balozi Njoolay.


Akizungumzia kuhusu fursa za biashara Mkurugenzi wa maendeleo ya biashara wa TANTRADE Bwana Edwin Rutageruka amesema kwamba mahusiano ya kibiashara kati ya nchi hizi mbili yameendelea kuimarika mwaka hadi mwaka na kwamba Tanzania imedhamiria kuendelea kukuza biashara kati yake na Nigeria. 


Naye Mkurugenzi wa mipango na maendeleo wa mamlaka ya EPZ Bwana Lamau Mpolo ameelezea uwepo wa fursa nyingi za uwekezaji katika sekta mbalimbali ikiwemo ya gesi na madini.  Ameelezea pia namna serikali ya Tanzania ilivyoweka mazingira mazuri kwa ajili ya kuvutia wawekezaji kutoka duniani kote katika sekta mbalimbali za uchumi nchini Tanzania.


Akiwasilisha mada kuhusu vivutio vya utalii vya Tanzania vilivyomo katika orodha ya maajabu ya 7 ya asili barani Africa, Mkurugenzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTB Bibi Teddy Mapunda amesema pamoja na vivutio vitatu (3) vya utalii ambavyo ni Mlima Kilimanjaro, Crater ya Ngorongoro na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Tanzania imejaliwa kuwa na vivutio vingi zaidi na vya kipekee na akabainisha kuwa imekuwa nchi ya kwanza barani Afrika kutangaza vivutio vyake saba vya asili ambavyo pamoja na vile vilivyomo katika maajabu Saba ya sili barani Afrika, vivutio vingine ni hifadhi ya taifa ya Ruaha, Hifadhi ya Taifa ya Kituro, hifadhi ya Taifa ya Gombe na Pori la akiba la Selous.


Amewakaribisha wananchi wa Nigeria kutembelea Tanzania na kujionea uzuri na upekee wa vivutio vya Tanzania sambamba na kuwekeza katika sekta ya utalii.


Kongamano hilo lililohudhuriwa na takribani wawekezaji na wafanyabiasha kutoka Nigeria mia moja  lilifuatiwa na tafrija iliyofanyika usiku katika hoteli hiyo na kuhuidhuriwa na waalikwa takribani 350 wakiwemo Mabalozi wa mataifa  mbalimbali nchi Nigeria, wageni kadhaa mashuhuri na baadhi ya watanzania waishio nchini Nigeria.

MAFUNZO YA KUPIGA ALA ZA MUZIKI KUANZA TENA MWEZI MEI

$
0
0
 Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye mazoezi

Action Music Tanzania (AMTz) inatangaza fursa kwa watu wote kujiunga na mafunzo ya kupiga ala za muziki yanayoanza tarehe 3/5/2014, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wanamuziki wa kupiga ala na kufanya maonesho kwa weledi na utaalamu zaidi.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa darasani

Mafunzo yanayotolewa ni pamoja na upigaji wa ala za muziki zikiwemo gita, kinanda, tarumbeta, saxophone, konga, drum set, na upigaji wa ngoma za asili. Pia yatatolewa mafunzo ya ‘body percussion’ yaani matumizi ya mwili katika kutengeneza midundo ya muziki.

Mafunzo hayo yanafanyika kwenye ofisi za AMTZ zilizopo maeneo ya Mwenge mtaa wa Umoja, nyuma ya magorofa ya jeshi na kwenye Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonesho Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo ili kujiunga na mafunzo haya wasiliana nao kwa simu namba 0686928828/0653075791 ili kupata fomu za kujiunga na mafunzo.

Wananchi waaswa kuzingatia usafi wa mazingira

$
0
0
Afisa Afya wa Manispaa ya Temeke Bw.Willium Muhemu akifafanua kwa waandishi wa habari mafanikio yaliyofikiwa na Manispaa hiyo katika kuwaondoa wafanyabiashara wanaofanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi pamoja na watu wote wanaochafua mazingira,Kulia ni Afisa Uhusiano wa Manispa hiyo Bi. Joyce Nsumba. (Picha zote na FRANK MVUNGI-maelezo).
 Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Bw.Ernest Mamuya akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani),kuhusu hatua zinazochukuliwa na Manispaa hiyo katika kuhakikisha  kuwa kanuni na taratibu za usafi wa mazingira zinazingatiwa na wananchi wote kwa kuyaweka mazingira yao katika hali  ya usafi ili kujikinga na magonjwa ya milipuko.

=======  ====== ======
Na Hassan Silayo-MAELEZO.


Wananchi wameaswa kuzingatia usafi wa mazingira kwa kuwa jukumu la kila mwananchi kulinda na kutunza na kuzingatia kanuni za usafi wa mazingira.


Hayo yamesemwa na Afisa Afya wa Manispaa ya Temeke Bw. Willium Muhemu wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.


Bw. Muhemu alisema manispaa hiyo imeweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha kuwa kanuni za usafi, taratibu na sheria za usafi wa mazingira zinazingatiwa na wadau wote wa mazingira ili kuepusha mlipuko wa magonjwa.


“Moja ya mikakati iliyowekwa na manispaa ya Temeke ni kuhakikisha kwamba hakuna mtu anayefanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi ili kuzuia uchafuzi wa mazingira na yeyote atakaye kiuka utaratibu huo atachukuliwa uchafuzi wa mazingira” Alisema  Bw. Muhemu.


Naye Afisa Mazingira wa Manispaa hiyo Bw. Ernest Mamuya alisema kuwa ili kuhakikisha kuwa manispaa hiyo inakuwa katika hali ya usafi wakati wote wanao mpango mpango wa kuongeza magari ya kubeba taka , kuwa na dampo la kudumu la kuhifadhia taka na kuhakikisha taka zinazolewa kwa wakati. Akitoa wito kwa wananchi Bw. Mamuya alisema kuwa wananchi wanapaswa kuzingatia kanuni za usafi katika ngazi za familia ili kuunga mkono mpango wa manispaa katika utunzani wa mazingira.

Maafisa afya wa kata wanaendesha zoezi la ukaguzi wa nyumba kwa nyumba kwa kushirikiana na wajumbe wa kamati za afya za mitaa husika ili kuhakikisha kuwa wananchi wanazingatia kanuni za usafi.

TBC NA CRI YAZINDUA TAMTHILIYA YA KICHINA ILIYOTAFSIRIWA KWA LUGHA YA KISWAHILI.

$
0
0
 Mkurugenzi Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Clement Mshana akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kwajili ya kuzindua rasmi Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.

 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Elisante Ole Gabriel akitoa hotuba yake mbele ya viongozi mbalimbali wakati wa Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam. 
 Mtendaji Mkuu Kampuni ya Star Media (T) Ltd Bw. Jack Czhou akieleza jambo wakati wa Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya wafanyakazi toka Kampuni ya Star Media (T0 Ltd na wasanii waliotumika kuweka lugha ya Kiswahili katika Tamthiliya ya Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) wakisikiliza kwa makini hotuba toka kwa mgeni rasmi leo wakati wa Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.

 Naibu Kati u Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Elisante Ole Gabriel akifurahi mara baada ya kukata utepe ikiwa ishara ya kukamilika kwa Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.

 Mkurugenzi Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Clement Mshana (kushoto) pamoja na Mshauri wa mambo ya Utamaduni Bw. Lzu Dong (kulia) wakipeana zawadi mara baada ya Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.  
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi, Watendaji na Viongozi mbalimbali mara baada ya Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA.

Ufunguzi wa baraza la wafanyakazi jijini Dar

$
0
0

Katibu Mkuu,Ofisi ya Makamu wa Rais Bw.Sazi Salula (katikati) akifungua rasmi kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais kilichofanyika Karimjee jijini Dar es Salaam leo hii kulia ni Naibu katibu Mkuu  Eng. Angerina Madete, na wa kwanza kushoto Katibu wa Baraza Bw. Isaya Kisiri.
 Sehemu ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi toka Ofisi ya Makamu wa Rais wakimsikiliza Katibu Mkuu Bw. Sazi Salula wakati wa ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images