Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

Rais Kikwete aongoza Sherehe za miaka 50 ya Muungano

$
0
0
 -Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia wananchi wakati alipokuwa anaingi uwanja wa Uhuru leo katika maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar..Pembeni ni Mkuu wa majeshi Jenerali Davis Mwamunyange.
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua vikosi vya ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Joyce Banda wa Malawi katika sherehe za miaka 50 ya Muungano.Rais Banda kwa sasa ndiye mwenyekiti wa jumuiya ya uchumi kusini mwa Afrika SADC. 
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dkt.Mohamed Ali Shein wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya muungano.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Mfalme Mswati katika sherehe za miaka 50 ya Muungano zilizofanyika katika viwanja vya uhuru leo.
 Rais dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Yoweri Kaguta Museveni katika sherehe za miaka 50 ya Muungano.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi katika maadhimisho ya hsrehe za miaka 50 ya Muungano
-Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Uhuru Kenyatta katika hsrehe za miaka 50 ya Muungano.(picha na Freddy Maro)

HAFLA YA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA YAFANA VIWANJA VYA IKULU

$
0
0
1Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein wakikata keki katika sherehe ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioasisiwa na Mwalimu J.K.Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume Aprili 26 mwaka 1964 hafla hiyo iilifanyika jana kwenye viwanja vya Ikulu na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Dr. Gharib Bilal, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Seif Ali Idd, Waziri Mkuu Tanzania Mh. Mizengo Pinda na viongozi mbalimbali wa serikali taasisi za dini na vyma vya siasa, Kushoto ni Mke wa Rais mama Salma Kikwete na kushoto ni Mkewa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein3Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein wakiwalisha keki wake zao katika hafla hiyo.4Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akibonyeza kifaa maalum cha kufyatua mafataki wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanzania. (PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)


6Mafataki yakilipuka katika viwanja vya ikulu ikiwa ni moja ya burudani katika sherehe hizo.7Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mh. Januari Makamba akiwa katika picha ya pamoja na Msanii MwanaFA aka Binamu.8Wazee wa Politiko Lifo Chipaka na Fahmi Dovutwa kulia wakifurahia Muungano.9Wasanii mbalimbali walikuwepo katika hafla hiyo.9aWadau kutoka Lugumi Enterprises walihudhuria katika hafla hiyo.10Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jembe Jesca Msambatavangu kushoto na Katibu wa CCM Wilaya ya Mufindi Miraji Mtaturu wakiwa katika hafla hiyo.11Mama Arafa Ridhiwani akiwa na ndugu zake katika hafla hiyo.12Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda katikati akiwa katika picha ya pamoja na Mama Arafa Ridhiwani Kikwete kulia pamoja na ndugu zake.14Wadau wa Fullshangwe wakakaa mble ya Kamera.15gRais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein kulia, Dr. Gharib Bilal Makamu wa Rais wa pili kutoka kulia ni Balozi Seif Ali Idd Makamu wa pili wa Rais Zanzibar wakiongoza watanzannia katika hafla hiyo.16Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi cheti Kijana Calvin Nyoni Mshindi wa Musiki wa kizazi kipya kwa ajili ya sherehe za Muungano wa Tanzania18Kikundi cha muziki kikiburudisha katika hafla hiyo kwenye viwanja vya Ikulu.19Babu Tale Meneja wa Diamond kushoto nia Mkubwa Fella kiongozi wa kundi la TMK Family walikuwepo pia.20Kulia ni Mzee Nyantori kutoka Idara ya Habari Maelezo Mdau Cliford Tandali katikati na Nyakia kutoka CCM Makao makuu. 22Waziri wa Habari, Maendeleo ya Vijana Utamaduni na Michezo Dr. Fennela Mukangara akizungumza na Mhariri Mtendaji wa TSN Bw, Gabriel Nderumaki na mdau Mabhare Matinyi katikati.23Wadau wa Fullshangwe kutoka Zanzibar.24Wake wa viongozi katika picha ya pamoja.25Wadau wa Fullshangwe Mamaa Farida kushoto na Matrina wakipozi mbele ya Keki.26Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia wakati kundi la muziki wa Taarabu kutoka Zanzibar lilipokuwa likitumbuiza jukwaani.27Wadau Esther Zelamula na mume wake kulia ni Frola Wingia wa Nipashe walikuwepo pia.28Mdau David Robert na mke wake Alice pia walikuwepo katika hafla hiyo.29Kikundi cha ngoma kikitumuiza jukwaani30Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Bw. Joseph Msukuma wa kwanza kulia na Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Simiyu Bw. Njalu Silanga wa pili kutoka kulia pamoja na wadau wengine wamehudhuria pia katika hafla hiyo.

Federations urged to develop Airtel Risings Stars soccer talents

$
0
0
 A cross section of the Airtel Rising Stars International soccer clinic attends a class session during the ongoing clinic at the Azam Complex, Dar es Salaam. 
 Former Taifa Stars Zamoyoni Mogella and Abeid Mziba greets the participants of the Airtel Rising Stars International soccer clinic. The duo attended the clinic yesterday to offer support and confidence among the youngsters. 
Former Taifa Stars player Zamoyoni Mogella speaks to the participants of the Airtel Rising Stars International soccer clinic when he visited their camp yesterday at the Azam Complex. He is flanked by another Taifa Stars Abeid Mziba.


=======  ======  ======
Federations urged to develop Airte Risings Stars soccer talents

Dar es Salaam, Tanzania 26thApril 26, 2014 …Football Federations have been urged to place more emphasizes on the youth football programs with the aim to lay down a strong foundation for the development of soccer develop in African countries, citing the Airtel Rising Stars initiative as key drive towards success.

These remarks were aired today by Tanzania soccer legends Zamonyoni Mogella and Abeid Mziba who visited and observed the ongoing Manchester United soccer training which was launched last Wednesday by the Deputy Minister for Foreign Affairs and International Coorperation Hon Mahadhi Juma Maalim.

Mogella and Mziba who made headline during their reign in the early 1980s commended Airtel and Manchester United for partnership which will help transform the standard of soccer in the continent.

The five-day clinic brings together over 7o participants, girls and boys, from Kenya, Sierra Leone, DRC, Congo Brazaville, Chad, Niger, Gabon, Madagascar, Burkina Faso and the host – Tanzania.

The clinic gives the youngsters a rare opportunity to enjoy the wealth of football experience from Manchester United soccer schools curriculum which seeks to produce well balanced soccer players who can play attractive attacking game. The program is expected to dwell on technical, physical and behavioral aspects of football.  


The Clinic is part of a sponsorship agreement between Manchester United and Airtel Africa. The Manchester United Soccer Schools has been in existence for 12 years and delivers programs such as this to over 120,000 students around the world. Each coach is specially trained to teach youth how to play the Manchester United way. 

Article 6

Mazoezi ya Miss Sinza kuanza Mei 5 kwenye ukumbi wa Meeda, Sinza

$
0
0
Prisca Clement katikati mara baada ya kushinda taji la vipaji katika mashindano ya Miss Tanzania 2013

MAZOEZI ya warembo watakaowania taji la urembo la Sinza, Miss  2014 yataanza  Mei 5 kwenye ukumbi wa Meeda uliopo Sinza Mori na Lufungila jijini. Taji la Miss Sinza linashikiliwa na Miss Tanzania, Prisca Clement alimaliza katika hatua ya 10 bora katika mashindano ya mwaka jana ya Miss Tanzania na pia alishinda taji la mrembo mwenye kipaji katika mashindano hayo.

Mratibu wa mashindano hayo, Majuto Omary alisema kuwa maandalizi ya mazoezi hayo yamekamilika na yatasimiwa na kamati ya maandalizi huku ikitafuta mwalimu kwa ajili ya kuwanoa.

Majuto alisema kuwa warembo waliowahi kushiriki mashindano hayo wanaruhusiwa kuja kutoa sapoti kwa warembo wapya na kamati yao itawapa nafasi ya kuwafundisha warembo wapya ili kuwapa ‘mbinu’ mbali mbali za mashindano hayo. Alisema kuwa fomu za kuomba kushiriki katika mashindano hayo zinapatikana kuanzia leo (Ijumaa) maduka ya Zizzou, Sinza Afrika Sana, Meeda, Ofisi za Miss Tanzania na Ofisi za gazeti la Mwananchi (Tabata reline.

“ Lengo letu kubwa ni kurudisha hadhi ya Miss Sinza, Kinondoni katika mashindano ya mwaka huu, tumejipanga kulinda heshima yetu na tunaamini titafanikiwa kwa heshima ya wakazi wa Sinza, Kinondoni na Tanzania kwa ujumla,” alisema  Majuto.

Alisema kuwa wanawakaribisha warembo wanaotaka ‘kupata taji’ kuchukua fomu zao ambazo zinatolewa bure.  Majuto pia aliwaomba wadhamini wanaotaka kujitangaza kupitia mashindano yao wanaruhusiwa kuja kudhamini mashindano hayo na milango ipo wazi.

Timu 72 kushiriki Ester Cup 2014, mshindi kupata sh 1.5 million

$
0
0
Jumla ya timu 72 zitashiriki katika mashindano ya soka ya Ester Cup ambayo huandaliwa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, kwa tiketi ya vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Ester Bulaya. Mashindano hayo, yanafanyika mwaka huu kwa msimu wa nne katika Jimbo la Bunda, na yatachukua nafasi katika viwanja vya Sabasaba, Shule ya Msingi Bunda, Nyamswa na Mgeta.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini jana (leo), Bulaya alisema kuwa mashindano hayo yamekuwa kulinganisha na miaka ya nyuma. Alisema kuwa mwaka 2011 jumla ya timu 18 zilishiriki, mwaka 2012 timu 26 wakati mwaka jana ziliongezeka mpaka 38. Bulaya alisema, ameamua kuendeleza mashindano hayo ili iwe fursa ya ajira kwa vijana wenye vipaji vya soka.

“Mimi ni mzaliwa wa Bunda na moja ya changamoto za jimbo letu ni kutokuwa na mashindano ya soka, nilipoanzisha mashindano ya Ester Cup nilileta kuhamasisha michezo jimboni kwetu, nafurahi kwa sasa lengo limetimia na hamasa katika jimbo hilo imeongezeka,” alisema Bulaya.

Alisema, tangu kuanza kwa mashindano, wilaya ya Jimbo la Bunda na wilaya nzima ya Bunda, imepata mafanikio makubwa na wachezaji wengi wamepata ajira kwenye klabu mbalimbali kubwa zinazoshiriki michuano mikubwa nchini.

Alifafanua kuwa ili kuleta maendeleo katika michuano hiyo, wamezuia wachezaji nje ya jimbo la Bunda kucheza Ester Cup jambo ambalo halitasaidia malengo yetu ya kuendeleza michezo kwa vijana wa jimbo husika.

Bulaya alisema kuwa jumla ya Sh15.4 zimetumika kugharimia mashindano ya mwaka  ambapo mshindi atapata Sh 1.5 million ambapo mshindi wa pili atazawadiwa Sh700,000 na mshindi wa tatu atazawadiwa Sh 500,000.

Aliongeza kuwa pia amefanikiwa kugawa vifaa mbali mbali kwa wilaya nne na kata 150 za wilaya nne, shule za sekondari na kutumia jumla ya Sh 75 million. Alisema kuwa wilaya ya Rorya na Tarime pekee ndizo hazijapata msaada huo na yupo mbioni kuwakabidhi.

MAKAMU ASKOFU JIMBO LA MASHARIKI KASKAZINI ASISITIZA KATIBA BORA

$
0
0
MAKAMU wa Askofu Jimbo la Mashariki Kaskazini, Mch. Spear Mwaipopo amesema Kanisa litaendelea kuliombea Taifa na viongozi wake lakini akawataka viongozi wa nchi hii nao watimize wajibu wao kwa kutenda haki. 

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumapili, Aprili 27, 2014) wakati akizungumza na waumini wa Kanisa la Tanzania Assemblies of Mwenge (TAG) katika ibada ya kuadhimisha miaka 75 ya Kanisa la TAG hapa nchini. 

Mchungaji Mwaipopo ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo alisema: "Kama kanisa tutaendelea kuliombea Taifa lakini na Viongozi wa nchi hawana budi kutimiza wajibu wao wa kulitendea haki Taifa letu kwa kudumisha Muungano, amani na mshikamano na kutupatia  Katiba bora inayotokana na maoni ya wananchi." 

"Sasa hivi kuna mabishano ya kiitikadi yanayoendelea, na sisi tusingependa kuwa na Katiba ya Chama bali ya Watanzania wote... hakuna chama chenye watu zaidi ya milioni 45. Tukiruhusu hali hii tutakuwa hatuwatendei haki Watanzania walio wengi." 

Alisema kila jambo jema husuhuka kutoka kwa Baba wa mianga na kwamba kama Kanisa wamekuwa wakiliombea jambo hilo hivyo anaamini kwamba Mungu atalisimamia hadi mwisho. 

Aliwataka waumini wa Kanisa hilo kuendelea kuomba bila kuchoka. "Kwa hiyo wapendwa msiangalie malumbano tu ndani ya TV, bali endeleeni kuomba ili jambo hili aliloliazimia Bwana liweze kutimia," alisema. 

Alisema anafurahishwa na ukweli kwamba kanisa la TAG linaadhimisha miaka 75 wakati Taifa la Tanzania limetimiza miaka 50 hapo jana tu (Aprili 26, 2014). 

"Nawapongeza Marais wetu wastaafu hayati Mwl. Nyerere na hayati Abeid Amani Karume kwa kudumisha Muungano wetu na kuruhusu kikatiba uhuru wa wananchi kuabudu. Kudumu kwa Muungano kumetusaidia kuweza kuhubiri Injili hadi Zanzibar," alisema. 

Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG - Taifa) lilianzishwa mwaka 1939 na kanisa la kwanza hapa nchini lilijengwa katika kijiji cha Igale, mkoani Mbeya. 

RAIS KIKWETE AONANA NA RAIS MSTAAFU WA NAMIBIA MHE. SAM NUJOMA,IKULU JIJINI DAR LEO

$
0
0
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimtembezea sehemu mbali mbali za Ikulu na Rais Mstaafu wa Namibia Mhe. Sam Nujoma aliyemtembelea leo April 27, 2014. Mhe Nujoma alikuwa ni mmoja wa watu mashuhuri waliohudhuria sherehe za miaka 50 ya Uhuru jana.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Mstaafu wa Namibia Mhe. Sam Nujoma Ikulu jijini Dar es salaam aliyemtembelea leo April 27, 2014. Mhe Nujoma alikuwa ni mmoja wa watu mashuhuri waliohudhuria sherehe za miaka 50 ya Uhuru jana.

RAIS KIKWETE AZINDUA RASMI KITUO CHA MAGONJWA YA MOYO KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Rais Dkt Jakaya Mrisho kikwete akiongea na mmoja wa wagonjwa watoto waliofanyiwa upasuaji kwenye kituo kipya na cha kisasa cha Moyo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kukifungua rasmi leo April 27, 2014
  Rais Dkt Jakaya Mrisho kikwete na Makamu Mwenyekiti wa chama tawala cha China cha National People's Congress Mhe. Chen Changzhi (kushoto) wakioneshwa moja ya vifaa vya kisasa vya kuchunguzia maradhi kwenye kituo kipya na cha kisasa cha Moyo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kukifungua rasmi leo April 27, 2014
 Rais Dkt Jakaya Mrisho kikwete na Makamu Mwenyekiti wa chama tawala cha China cha National People's Congress Mhe. Chen Changzhi (kushoto) wakiangalia baadhi ya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji  kwenye kituo kipya na cha kisasa cha Moyo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kukifungua rasmi leo April 27, 2014
 Rais Dkt Jakaya Mrisho kikwete na Makamu Mwenyekiti wa chama tawala cha China cha National People's Congress Mhe. Chen Changzhi wakipata maelezo ya utendaji wa mashine katika chumba cha wagonjwa mahututi  kwenye kituo kipya na cha kisasa cha Moyo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kukifungua rasmi leo April 27, 2014. 
Rais Dkt Jakaya Mrisho kikwete akimsindikiza  Makamu Mwenyekiti wa chama tawala cha China cha National People's Congress Mhe. Chen Changzhi (kushoto) baada ya uzinduzi rasmi wa  kituo kipya na cha kisasa cha Moyo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili rasmi leo April 27, 2014. PICHA NA IKULU

Mrembo Eveline Baasa atwaa taji la Ulimbwende wilaya ya Karatu kwa mwaka 2014

$
0
0
 Mrembo Eveline katika picha ya pamoja  na wenzake waliotwaa tatu bora, ambapo kwa upande wa kushoto ni Happy Tarmo na kulia ni Merry Joel.
 Mrembo Evelini Baasa ( aliyekaa) akiwa na washiriki wenzake Hapy Tarimo kushoto na Merry Joel Kulia, Na wa kwanza kushoto ni aliyekuwa mwakilishi wa  mgeni rasmi Adam Akyoo, na wa mwisho kulia ni diwani wa Karatu mjini Jublet Mnyenye
Mlimbwende Eveline Baasa akiwa katika picha ya pamoja na majaji wa shindano hilo wakiongozwa na jaji mkuu Faustine Mwandago ( watatu kutoka kulia aliyvalia shati la mistari).
  warembo, wakionyesha vazi la usiku kwa pamoja ambapo wa kwanza kulia ni Eveline Baasa, anaefuata ni merry joel, Asha Bonivenrute,  Upendo Mtweve, Veronika Joel, Scolastika Fransis, Janeth Jackson, Glorry Aloyce, Happy Tarimo.
========  =======  =======
Na Bertha Ismail - Arusha.

Mrembo Eveline Baasa (19) amefanikiwa kutwaa taji ya Ulimbwende wa wilaya ya Karatu kwa mwaka 2014 na kuwabwaga wenzake wanane katika kinyanganyiro kilichofanyika katika ukumbi wa Ngorongoro Camp uliopo mjini hapa.

Eveline amekua mrembo wa kwanza kwa wilaya hiyo tangu kuanzishwa kwa wilaya ya karatu ambapo alibahatika kujinyakulia kitita cha shilingi laki tano na pia kuingia katika shindano la miss Arusha linalotarajiwa kufanyika mwezi june sambamba na hilo amepata udhamini wa maandalizi yote kwa ajili ya kushiriki shindano lililoko mbele yake.

Mshindi wa pili alikuwa Happy Tarmo (19) ambaye alijinyakulia fedha taslim shilingi laki tatu na kufuatiwa na Merry Joel (21) aliyezawadiwa shilingi laki mbili na mshindi wa nne ikienda kwa  Veronica John (21) na washiriki wenzake watano ambapo alipata kifuta jasho cha shilingi elfu themanini  kila mmoja.

Hili lilikuwa shindano la kwanza kwa wilaya ya Karatu ambalo lilikuwa kivutio kikubwa kwa wakazi wa wilaya hiyo kufuatia ushindani mkubwa uliojitokeza kwa washiriki wote kuwa na sifa zote hali iliyowapa kazi ya ziada majaji waliokuwa wakiongozwa na mratibu wa miss kanda ya kaskazini Faustine Mwandago.

Mashabiki wa tasnia ya urembo mjini Karatu waliokuwa wakiongozwa na diwani wa Karatu mjini Jubilate Mnyenye walilipuka kwa shangwe baada ya jaji mkuu Mwandago kumtangaza mlimbwende Evaline kuwa ndiye  mshindi wa miss Karatu 2014 matokeo yaliyoungwa mkono na wadau wote wa tasnia ya urembo waliohudhuria onyesho hilo.

Hili linakuwa shindano la kwanza kwa ngazi ya kitongoji cha wilaya ya Karatu kwa mkoa wa Arusha wenye vitongoji vitatu ambavyo ni Karatu, Monduli na kituo cha Arusha mjini         ( Arusha city center).

Aidha baada ya kitongoji cha Karatu kumpata mrembo wake, wiki ijayo kinyang’anyiro cha pili  kitafanyika kitongoji cha monduli na kitongoji cha mwisho kitakua cha arusha city  kitakachofanya baadae mwaka huu ikiwa ni mchakato wa kumpata miss Arusha.
  
Aidha kila kitongoji kitatoa warembo wane kila kitongoji ambapo kutakuwa na jumla ya warembo 12 ambapo watashiriki katika kinyanganyiro cha kumsaka mrembo wa mkoa wa Arusha

Mgeni rasmi katika shindano hilo la miss Karatu alikua ni mhifadhi mkuu wa mamlaka ya Ngorongoro Fredy Manongi ambaye aliwakilishwa na afisa uhusiano wa mamlaka ya hifadhi ya ngorongo Adam Akyoo ambaye aliwataka warembo kutumia fursa walionayo kupambana na ujangili kwa kutoa taarifa za watu wanajishughulisha na ujangili.

Akyoo alisema kuwa kupambana na ujangili siyo lazima kushika mitutu ya bunduki kumzuia mwindaji bali utoaji wa elimu pia unaweza kusaidia kupunguza kama si kumaliza kabisa tatizo la ujangili nchini.

Kwa upande wake diwani wa karatu mjini, Jublet Mnyenye alisema kuwa amefurahishwa na waandaji wa kinyang’anyiro hicho cha kumsaka mlimbwende wa Karatu pia karatu mjini kuwa wenyeji wa mashindano hayo kwa mara ya kwanza wilayani humo ambapo ameahidi kusapoti mashindano hayo mara nyingine yatakapofanyika kwa kujitolea ukumbi, zawadi za washindi pamoja na maandalizi yote kwa ujumla.

Kinyanganyiro hicho cha aina yake kilidhaminiwa na Makampuni mbalimbali na wadau wa urembo wilayani humo wakiwemo  kinywaji cha Redd’s, ZARA tour, hifadhi ya mamlaka ya Ngorongoro, Beauty point Cosmetics pamoja na mdau wa ulimbwende Mh, Steven Siay.

Hotuba Ya Mhe. Mwigulu Nchemba katika sherehe za Muungano Washington DC

$
0
0
Mhe. Mwigulu Nchemba akizungumza katika moja ya hafla hapa Washington DC.Picha kwa hisani ya Vijimambo Blog
Ifuatayo ni hotuba ya Mhe Mwigulu Nchemba.
Naibu Waziri wa Fedha na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (Tanzania Bara) aliyoitoa katika maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano hapa Washington DC.
Audio hii ni kwa hisani ya Vijimambo Blog

closing ceremony of a five-day Airtel Rising Stars International soccer clinic at the Azam Complex

$
0
0
 Airtel Tanzania Marketing Director Levi Nyakundi speaks during the closing ceremony of a five-day Airtel Rising Stars International soccer clinic at the Azam Complex. The clinic had brought together over 70 participants from 12 African countries.

 Neil Scott, a Manchester United Soccer School coach speaks during the closing ceremony of a five-day Airtel Rising Stars International Soccer clinic at the Azam Complex. The clinic brought together over 70 participants from 12 African countries. He is flanked by Andrew Stoke, another coach and the Airtel Tanzania Marketing Director Levi Nyakundi. 
 A Tanzanian Airtel Rising Stars player Joseph Prosper, receives a certificate of participation from the Airtel Tanzania Marketing Director Levi Nyakundi during the closing ceremony of a five-day Airtel Rising Stars International soccer clinic at the Azam Complex. Left is Airtel Tanzania Public Relations Manager Jackson Mmbando.

 A Sierra Leone Airtel Rising Stars player Fatmata Mansaroly, receives a certificate of participation from the Airtel Tanzania Marketing Director Levi Nyakundi during the closing ceremony of a five-day Airtel Rising Stars International soccer clinic at the Azam Complex. Left is Airtel Tanzania Public Relations Manager Jackson Mmbando. 
 A Sierra Leone Airtel Rising Stars player Fatmata Mansaroly, receives a certificate of participation from the Airtel Tanzania Marketing Director Levi Nyakundi during the closing ceremony of a five-day Airtel Rising Stars International soccer clinic at the Azam Complex. Left is Airtel Tanzania Public Relations Manager Jackson Mmbando.

Airtel Rising Stars Tanzania team in a group photo after a completion of five-day Airtel Rising Stars International soccer clinic at the Azam Compex.  Seated are from left – Tanzania Women team coach Rogasian Kaijage, Airtel Tanzania Marketing Director Levi Nyakundi, MUSS coaches Neil Scott and Andrew Stokes.

Maaskofu Mwanza, Kamati kujadili Pasaka

$
0
0
 Pichani Kulia ni Mkurugenzi wa Msama Promotions Ltd,Alex Msama alipokuwa akizungumza na Wanahabari hivi karibuni kuhusiana na muendelezo wa tamasha la Pasaka 2014.

MAASKOFU wa Makanisa mbalimbali jijini Mwanza asubuhi hiii wanakutana na Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka kabla ya tamasha hilo linalotarajia kufanyika Mei 4 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo.

Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi hayo, Abihudi Mang’era mkutano huo utajadili mipangilio mbalimbali itakayofanikisha tamasha hilo kufanyika kwa ufanisi.

“Tumeonelea tupate mwongozo zaidi kutoka kwa Maaskofu wa Mwanza ili tufanikishe Tamasha la Pasaka linalotarajia kufanyika Mei 4 kwenye uwanja wa CCM Kirumba,” alisema Mang’era.

Mang’era alisema tamasha hilo lengo la Tamasha la Pasaka ni kusaka fedha kwa ajili ya kuwasaidia wenye uhitaji maalum kama yatima, walemavu na wajane sambamba na kujipanga kwa ujenzi wa kituo cha Kimataifa kitachojengwa Pugu nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, kitakachojulikana kama Jakaya Kikwete, Rafiki wa wasiojiweza.

Aidha Mang’era alitaja viingilio katika tamasha hilo jijini Mwanza ni Sh. 10,000 kwa viti maalum, viti vya kawaida Sh. 5,000 na watoto Sh. 2,000.

Kauli mbiu ya Tamasha la Pasaka mwaka huu ni Tanzania Kwanza, Haki huinua Taifa ambayo ina lengo la kuwakumbusha wananchi kuijali na kuipenda nchi yao.

BENKI YA POSTA TANZANIA YATOA MSAADA VITU MBALIMBALI KWA WODI YA WATOTO WENYE MAGONJWA YA SARATANI MUHIMBILI

$
0
0

 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Mystica Ngongi akimkabidhi hundi ya sh. milioni 2 Mkuu wa Idara ya Ustawi ya Jamii Hospitali ya Taifa Muhimbili, Beatrice Mugula kwa ajili ya wagonjwa wa saratani watoto waliolazwa katika hospitali hiyo. Kushoto ni Meneja Mahusiano Mwandamizi TPB, Noves Moses. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Mystica Ngongi (wa pili kushoto) akimkabidhi sehemu ya msaada wa nguo, madaftari, sabuni, vitabu vya watoto, Meneja wa jengo la watoto katika hospitali ya Muhimbili, Praxeda Chenya kwa ajili ya kusoma vikiwa na thamani ya sh. milioni moja, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sikukuu ya Muungano. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja Mahusiano Mwandamizi TPB, Noves Moses na wa pili kulia ni Mkuu wa Idara ya Ustawi ya Jamii Hospitali ya Taifa Muhimbili, Beatrice Mugula. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
 
Wafanyakazi wa TPB wakiweka sawa zwadi kabla ya kuzikabidhi.

 Wafanyakazi wa Benki ya Posta na watoto waliolazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili katika picha ya Pamoja.

Tanzania na Ujerumani kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi

$
0
0
Tanzania imetakiwa kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na Ujerumani  ikiwa ni pamoja na kujipanua kiuchumi badala ya kutegemea misaada kutoka kwa wahisani mbalimbali.

Wito huo umetolewa jana na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo alipokuwa akihutubia kwenye  maadhimisho ya jubilee ya miaka 50 ya Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.


Profesa Muhongo alisema kuwa umefika wakati wa Tanzania kutumia  rasilimali zake  hususani gesi  iliyogunduliwa hivi karibuni ikiwa ni pamoja na madini kujiimarisha kiuchumi  ili kuweza kujitegemea badala ya kutegemea misaada tu kutoka kwa wahisani.


Profesa Muhongo aliongeza kuwa uhusiano kati ya Tanzania na Ujerumani ni wa muda mrefu na wenye historia nzuri na kusisitiza kuwa sasa imefikia  wakati ushirikiano huo unatakiwa ulenge kwenye masuala ya uchumi zaidi ili Tanzania iweze kupaa kiuchumi.


Profesa Muhongo alisema kuwa imefikia wakati  uchumi wa Tanzania unatakiwa ukue kulingana na idadi ya watu na kuongeza kuwa sekta ya nishati na madini ni mhimili mkubwa wa ukuaji wa uchumi wa nchi.  “Ili nchi yoyote iweze kuendelea kiuchumi duniani inahitaji  nishati ya umeme ambayo inaweza kuvutia uwekezaji mkubwa.” Alisisitiza Profesa Muhongo.

Aidha, Profesa Muhongo aliongeza kuwa nchi ya Tanzania inahitaji  elimu bora kwa wanafunzi wake ili kupiga hatua kiuchumi na kueleza kuwa katika kutambua hilo, Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imeweka mkakati  wa kuhakikisha shule zote hususani za  msingi na sekondari zinapatiwa umeme ili  kuweka mazingira bora ya wanafunzi kujifunza.


Profesa Muhongo aliongeza kuwa elimu bora inatakiwa  iwe inaendana na teknolojia na kusisitiza kuwa siri ya nchi zilizoendelea duniani kama China ni uwekezaji katika elimu ya sayansi na teknolojia.


Profesa Muhongo aliwataka wawekezaji walioko nchini Ujerumani kujitokeza kwa wingi na kuwekeza Tanzania kwani ni nchi yenye fursa nyingi za kiuchumi hususani katika sekta ya nishati na madini. Aliongeza kuwa  Tanzania ni nchi yenye amani , uongozi bora  tofauti na nchi nyingine za Afrika na kuwahakikishia kuwa zipo sheria bora katika usimamizi wa sekta hizo.

Akizungumzia manufaa ya kugundulika kwa gesi nchini Profesa Muhongo aliongeza kuwa gesi asilia iliyogunduliwa Mtwara na Lindi imekuwa kivutio kikubwa katika mikoa hiyo.


Profesa Muhongo alisisitiza kuwa kugundulika kwa gesi asilia kumepelekea uwekezaji mkubwa katika mikoa huo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kiwanda kikubwa cha sementi cha Dangotte unaoendelea mkoani Mtwara na kiwanda kingine cha sementi kitakachojengwa Lindi.


Alisisitiza kuwa mara baada ya kukamilika kwa mradi huo gesi itakayozalishwa itatumika majumbani, kwenye magari, ikiwa ni pamoja na kuzalisha umeme  wa kutosha ambapo wa ziada utauzwa kwa nchi za jirani. “ Kwa mfano  tunaamini kuwa  gesi itakayotumika majumbani  itaepusha matumizi ya mkaa ambapo inakadiriwa kuwa matumizi katika  jiji la Dar es Salaam ni magunia 50,000 kwa siku.

Naye mhadhiri kutoka chuo  kikuu cha Dar es salaam Profesa Palamagamba Kabudi akizungumza katika sherehe hizo alisema kuwa ni wakati wa Tanzania kuwa makini  sana katika usimamizi wa rasilimali zake ili kuepuka migogoro inayoweza kujitokeza kama katika nchi za Kongo na Nigeria.


Alisema  rasilimali hizi zisiposimamiwa ipasavyo  zinaweza kusababisha uchumi kuyumba ikiwa ni pamoja na kusababisha machafuko. Aidha Profesa Kabudi aliitaka serikali  kushirikiana na nchi washirika katika kusimamia rasilimali hizo ili ziweze kuleta maendeleo.
Na Greyson Mwase, Ujerumani

Rais Kikwete akabidhi vitabu kwa maktaba Jeshini

$
0
0
-Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhi vitabu 2069  kwa uongozi  wa Jeshi(JWTZ) kwa matumizi katika maktaba mablimbali za jeshi nchini.Wapili kushoto ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na Watatu kushoto ni Mnadhimu Mkuu Jeshini Luteni Jenerali Samuel Ndomba.

-Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na viongozi na makamanda waandamizi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakati wa hafla ya kukabidhi vitabu 2069 kwa ajili ya matumizi katika maktaba za jeshi.Vitabu hivyo ni mchango binafsi wa Rais Katika kuboresha mafunzo ya kisasa jeshini(picha na Freddy Maro).
======   ==== ======
Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo katika Ikulu ya Dar es Salaam amekabidhi vitabu 2,181 kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa ajili ya vyuo vya Jeshi ili kuongeza taaluma. 

 Rais amekabidhi vitabu hivyo kwa Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na kuahidi kuendelea kutafuta vitabu zaidi kwa ajili ya kuboresha Maktaba ya Jeshi iliyopo katika Chuo Cha Kijeshi kilichopo Monduli, Mkoani Arusha. 

 Maktaba hiyo ilianzishwa na Mheshimiwa Rais wakati alipokuwa mkufunzi katika chuo hicho miaka iliyopita. 

 "Lazima mtenge bajeti kwa ajili ya vitabu lakini na mimi nitaendelea kutafuta vitabu niwaletee ili kuijengea uwezo Library yetu ya Monduli”. 
 Akipokea vitabu hivyo kwa niaba ya Jeshi, Jenerali Davis Mwamunyange amemshukuru Rais kwa juhudi zake za kuboresha Jeshi la Wananchi Tanzania kwa ujumla na kulifanya kuwa la kisasa zaidi. 

 “Juhudi zako za kuliendeleza Jeshi letu imetuongezea uwezo na kujiamini zaidi. Bila juhudi zako tusingefika hapa tulipo na tunajivunia sana mafanikio haya” amesema Jenerali Mwamunyange .

Olam Tanzania Celebrates World Malaria Day with Partners and Community

$
0
0
Dr. Seif Rashid, Minister of Health and Social Welfare presenting a certificate of recognition to OLAM Tanzania Internal Communications Manager, Elizabeth Nnoko for their commitment to the fight against malaria through the Malaria Safe Initiative.
    A section of workers and villagers who attended a World Malaria Day function in Kyela organized by OLAM Tanzania
 One of the staff of OLAM in Kyela receiving a treated mosquito net

 A section of villagers who attended an event in Mtwara

========  =======  =======
Olam Tanzania Celebrates World Malaria Day with Partners and Community


In commemoration of World Malaria Day, OLAM Tanzania has ran a country wide awareness and prevention campaigns across 4 of its origin locations; Mtwara, Songea, Bunda and Kyela aimed to support efforts of eradicating malaria cases within the communities.


“Unite with Olam in the prevention of Malaria Deaths – Malaria kills” was the theme to Olam Tanzania’s World Malaria Day Campaign that went along with providing treated mosquito nets to its workers.


Olam organized for events in its locations, and 1000 nets were distributed in Songea, 1000 for Mtwara, 100 Bunda and 100 for Kyela, where banners carrying the Malaria Day message in both English and Swahili were strategically placed for visibility, pamphlets were distributed, and awareness speeches were conducted in front of the workers by Johns Hopkins staff.


Trained medical staff conducted fast malaria detection campaigns to sensitize workers on early detection and prevention in the events, which were also attended by local officials and dignitaries.

Speaking of Olam’s effort in ending Malaria related deaths in Tazania, Elizabeth Nnoko Internal Communications Manager for Southern and Eastern Africa, said wellbeing of their workers is its company’s number one priority.


“We are proud to be a part of this important campaign to help end Malaria related deaths in all our operations by using our core capacity as a company, first by educating our employees about Malaria and providing protection’ said Nnoko.

Malaria is a major public health problem in Tanzania with annual deaths estimated at 60,000, with 80 percent of these deaths among children under five years of age. Approximately 14 to 18 million clinical malaria cases are reported annually by public health services and more than 40 percent of all outpatient visits are attributed to malaria.

Olam Tanzania entered a joint partnership with Johns Hopkins Malaria Safe Initiative, committing Olam Tanzania to the 4 pillars of Malaria Safe which is educate employees about malaria, provide protection against malaria, create visibility to the partnership and inspire action through advocacy.


In Dar es Salaam, Johns Hopkins organized an inaugural event for its Malaria Safe Initiative partners at the Hyatt Regency. In attendance was honored guests Dr. Seif Rashid, Minister of Health and Social Welfare, Said Meck Said, Regional Commissioner of Dar es Salaam, Sharon L. Cromer, Mission Director, USAID/Tazania where Malaria Safe partners were commended for “Investing in the Future to defeat malaria.


Olam Tanzania along with other partners was presented with a certificate of recognition from the Tanzania Ministry of Health and Social Welfare presented by Dr. Seif Rashid himself for their commitment to the fight against malaria through the Malaria Safe Initiative.


“TUNALAANI UKATILI MAOVU WANAYOFANYIWA WAANDISHI WA HABARI.” - TIBANYENDERA (MISA-TAN)

$
0
0
DSC_0085
Picha juu na chini ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Bw. Mohamed Tibanyendera (wa pili kushoto) akizungumza jijini Dar es Salaam jana kuhusiana maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari yatakayofanyika wiki hii duniani kote. Kushoto ni Meneja wa Maadili na Usuluhishi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Allan Lawa, Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama (wa pili kulia) na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC), Jane Mihanja (kulia).(Picha na Zainul Mzige).

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Zaidi ya washiriki 200 kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kuhudhuria kwenye matukio ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, inayotarajiawa kuadhimishwa nchini hapa mnamo Mei 3, jijini Arusha, imeelezwa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Bw. Mohamed Tibanyendera, amesema kwamba maadhimisho hayo yenye lengo kuu la kulaani maovu wanayofanyiwa waandishi wa habari barani Afrika na duniani kote, yatafunguliwa na Jaji Mstaafu Mark Bomani.

Tibanyendera amesema kwamba, pamoja na mambo mengine maalum ambayo yatakuwa yameandaliwa, matukio ya mwaka huu yataambatana pia na uzinduzi wa kitabu kiitwacho “Hii Ndiyo Demokrasia, Toleo la 20”, kitachokuwa na taarifa muhimu kuhusu waandishi wa habari walionyanyaswa na kufanyiwa vitendo vilivyokiuka haki za binadamu, barani Afrika.
DSC_0053
DSC_0108
Meneja wa Maadili na Usuluhishi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Allan Lawa (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar kuhusu siku ya maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari itakayofanyika jijini Arusha.

“Tunategemea kuwa na wageni zaidi ya 200, kwa siku hiyo pia tuazindua kitabu kitachozungumzia waandishi walionyanyaswa na kufungwa katika maeneo mbalimbali ya Kusini mwa Afrika pamoja na hali ya vyombo vya habari na uhuru wa habari katika nchi hizo ikiwemo Tanzania,” amesema Tibanyendera.

Tibanyendera ameongeza na kusema kwamba maadhimisho hayo ya siku mbili, yatakayofanyika kuanzia Mei 2 hadi 3, yataambatana pia na utolewaji wa semina za kuwaelimisha washiriki kuhusu mambo mbalimbali ya habari na uhuru wake, kutoka kwa wataalam wakiwemo wahadhiri watakaotoka vyuo mbali mbali hapa nchini na kwingineko, ambao wameandaliwa rasmi kwa ajili ya shughuli hiyo.

Wakati huo huo, Meneja wa Maadili na Usuluhishi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) ambao pia ni moja ya taasisi zitakazoshiriki kwenye maadhimisho hayo, Bw. Allan Lawa, amesema kwamba MCT itazindua katika maadhimisho hayo machapisho matatu yatakayohusu masuala ya habari ikiwepo ripoti ya uvunjifu wa uhuru wa habari nchini ambayo yatapatikana katika ofisi zao.
DSC_0126
Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa ambao ni mmoja wa wadhamini wa siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani, Bi. Usia Nkhoma Ledama (wa pili kulia), ambaye alisisitiza kwamba uhuru wa vyombo vya habari nchini ni muhimu kusaidia nchi zinazoendela kufika malengo ya milenia.

“Sisi kama MCT tumeandaa machapisho matatu ambayo yatazinduliwa siku hiyo yanayogusia hali ya uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania 2013, ripoti ya utafiti wa uvunjifu wa uhuru wa habari katika mwaka 2013, na ripoti ya ukiukwaji wa uhuru wa vyombo vya habari nchini.

“Tuna furaha kuwaambia kwamba machapisho yote haya yatapatikana siku hiyo na wote mnakaribishwa kujipatia nakala zenu,” amesema Lawa.Akimalizia, Bw. Lawa alisema waandishi wa habari wanapaswa kufika katika ofisi za Makao Makuu ya MCT zilizopo jijini Dar es Salaam kuchukua machapisho hayo ili waweze kuyasoma kwa kina na kuweza kutambua haki zao za msingi. Alisema pia kwamba muda si mrefu, nakala za machapisho hayo zitasambazwa na kupatikana kwenye vilabu vya vyombo vya habari (Press Club) vya mikoani ili waandishi ambao wako nje ya Dar es Salaam nao waweze kunufaika na machapisho hayo. Maadhimisho hayo yamembeba kauli mbiu ya “Uhuru wa vyombo kwa Maendeleo ya Utawala Bora”.
DSC_0144
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC), Jane Mihanja ambaye amesema mwandishi wa habari yoyote akizuiwa kuingia kwenye mkutano ambao ni wawazi anatakiwa kutoa taarifa katika juhudi za kuhamasisha uhuru wa vyombo vya habari nchini.
DSC_0033
Pichani juu ni chini ni baadhi ya waandishi wa habari na wadau wa tasnia hiyo waliohudhuriwa mkutano huo.
DSC_0031

Mhe Mwigulu Nchemba akizungumzia suala la uraia pacha Washington DC

$
0
0
Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba akihojiana na Mubelwa Bandio wa Kwanza Production Washington DC.
Photo Credits: Habari Kwanza blog
Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba, amesema kuwa anajivunia kiasi cha UZALENDO walichonacho waTanzania hapa nchini, jambo linalompa moyo kuendeleza harakati zake za kusaidia kupatikana kwa uraia pacha, ombi lililo kuu kwa waTanzania waishio nje ya nchi katika mabadiliko ya katiba mpya.

Mhe Nchemba, ambaye alikuwa mmoja wa wageni waalikwa kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanzania yaliyofanyika jijini Washington DC nchini Marekani, amesema kuwa ushiriki wa waTanzania na rafiki zao katika maadhimisho haya, umemdhihirishia nia na mapenzi yao kwa nchi yao, na hilo limemsukuma zaidi kusaidia kupitishwa kwa suala la uraia pacha kwenye katiba mpya.

Hii ni ripoti katika kipindi cha Morning Jam, asubuhi ya Aprili 28, 2014

TBL YAPATA TUZO YA MAPAMBANO DHIDI YA MALARIA NCHINI

$
0
0
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa taasisi mbalimbali zinazoshirikiana na serikali katika mapambano dhidi ya Malaria nchini.Mstari wa mbele kutoka kulia ni Athuman Mfutakamba, Waziri Dk. Rashid  Balozi wa Malaria nchini, Leodgar Tenga.
 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid (kulia) akimkabidhi Meneja Vipaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Lillian Makau cheti cha shukurani cha kutambua ushiriki wa kampuni hiyo katika mapambano dhidi ya Malaria nchini, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katikati ni Balozi wa Malaria Tanzania, Leodegar Tenga.


 Katibu wa Afya wa TBL (katikati), akitoa maelezo jinsi kampuni yake ilivyojidhatiti kutoa elimu na tiba ya malaria kwa wafanyakazi pamoja na wananchi.
 Katibu wa Afya wa TBL (katikati), akitoa maelezo jinsi kampuni yake ilivyojidhatiti kutoa elimu na tiba ya malaria kwa wafanyakazi pamoja na wananchi.
 Wananchi wakiwa katikasherehe za maadhimisho ya hayo kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, Dar es Salaam.
Makau akielezea mikakati ya TBL ya kuisaidia jamii na wafanyakazi katika mapambano  dhidi ya Malaria.
 Wageni waalikwa wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani
 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid , akimkabidhi Meneja Vipaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Lillian Makau (kulia) jinsi kampuni hiyo inavyoshiriki katika mapambano dhidi ya malaria kwa kuisaidia jamii na wafanyakazi wake, alipotembelea banda la TBL wakati wa maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani, Dar es Salaam jana. Katikati ni Katibu wa Afya wa TBL, James Lyimo. Wa pili kulia ni Meneja Uhusiano wa TBL, Editha Mushi.

 Katibu wa Afya wa TBL, James (kushoto akijadiliana jambo na Meneja Uhusiano wa TBL, Editha Mushi wakati wa maadhimisho hayo.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG.
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images