Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

MKUTANO WA 28 WA MWAKA WA NIMR NA KONGAMANO LA PAMOJA LA WANASAYANSI LAANZA LEO DAR ES SALAAM

$
0
0
Mkutano wa 28 wa Taasisi ya Taifa ya utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Tanzania (NIMR) umeanza leo jijini Dar es Salaam na kufanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) unafanyika sambamba na na Kongamano la Wanasayansi watafiti barani Afrika.
 Mtafiti Mkuu na Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano  kutoka Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu,  Leonard Mboera  akiwasilisha moja ya tafiti walizofanya kuhusiana na ugonjwa wa malaria kwa nchi za Ukanda wa jangwa la Sahara.
 Baadhi ya wa tafiti wanasayansi kutoka nchi mbalimbali wakifuatilia uwasilishaji wa trafiti mbalimbali
 Mtafiti Mkuu na Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano  kutoka Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Dr. Leonard Mboera akiendelea kuwasilisha.
 Watafiti wakifuatilia mada hizo.
 Mkurugenzi wa Vector Control Operations, Dr.Steven Magesa akichangia mada.
Mkurugenzi Mkuu wa Zamani wa NIMR, Dr. Andrew Kitua akichangia mada.

semina ya mpango wa kukarabati reli ya kati itakayowasaidia wajisila mali wa Tanzania, Kongo, Burundi na Rwanda

$
0
0
 Meneja mahusiano wa Shirika la Reli  Tanzania Midladjy Maez akiongea na washiriki wa semina ya mpango wa kukarabati reli ya kati itakayowasaidia wajisiria mali wa Tanzania, Kongo, Burundi na Rwanda leo jijini Dar es Salaam, mpango huo ni muendelezo wa jitihada ya kuboresha miundo mbinu ya reli ya kati.

 Baadhi ya waandishi wa habari na washiriki wa mkutano wa Shirika la Reli Tanzania wakisikiliza kwa makini  hotuba ya mgeni rasmi ( hayupo pichani),wakati wa semina ya mpango wa kukarabati na kuboresha reli ya kati ili kuimarisha uchumi wa nchi leo jijini Dare s salaam.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, ambaye alikuwa mgeni rasmi Shaabani Mwinjaka, akiongea na washiriki wa semina ya mpango wa kuimarisha usafiri wa reli ya kati kwa ajili ya kusaidia usafiri kwa wajasiria mali,leo jijini Dar es salaam.

 Baadhi ya washiriki wa semina ya mpango wa kuimarisha usafiri wa reli ya kati kwa ajili ya kusaidia usafiri kwa wajasiria mali wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi (hayumo pichani) leo jijini Dar es salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, ambaye alikuwa mgeni rasmi Shaabani Mwinjaka, (mstari wa mbele wa nne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa semina ya mpango wa kuimarisha usafiri wa reli ya kati,leo jijini Dar es salaam. (Picha na lorietha Laurence-maelezo)

Article 2

$
0
0
WAZIRI MKUU AONGOZA WAKAZI DAR KUAGA MWILI WA
MAREHEMU CHANG’A
 
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameongoza viongozi kadhaa na baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuuaga mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Bw. Moshi Chang’a ambaye alifariki dunia Aprili 20, 2014 kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alikuwa akipatiwa matibabu.
 
Shughuli ya kuuaga rasmi mwili wa marehemu Chang’a kwa wakazi wa mji wa Dar es Salaam ilifanyika leo mchana (Jumanne, Aprili 22, 2014) nyumbani kwake Mbagala, Kibonde Maji, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Mwili wake utasafirishwa leo jioni kwenda Kihesa, mkoani Iringa kwa mazishi.
 
Akizungumza na waombolezaji hao kabla ya kutoa heshima za mwisho, Waziri Mkuu Pinda alisema amemfahamu Bw. Chang’a kwa muda mrefu kwa sababu sehemu kubwa ya utumishi wake ameifanya akiwa Serikalini.
 
“Ninyi mlimfahamu Bw. Chang’a kivingine lakini mimi nilimfahamu kwa namna ya tofauti kutokana na jinsi alivyokuwa msaada mkubwa kwa Serikali kila tulipokuwa tukipata shida ama migogoro ya kiuongozi.”
 
“Kama TAMISEMI, tumemtumia sana kusawazisha mambo kwa sababu Mungu alimjalia kipaji cha pekee ambacho ni ucheshi... hata jambo lingekuwa gumu vipi, huyu Bwana alijua kufikisha ujumbe bila kumuudhi mhusika kutokana na maneno yake,” alisema Waziri Mkuu.
 
Alitumia fursa hiyo kufikisha salamu za rambirambi kwa wafiwa kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete ambaye yuko safarini kikazi.
 
Vilevile, aliwataka wanafamilia ambao wamebaki bila mama wala baba, wawe na umoja na mshikamano na kuahidi kuwa Serikali itawasaidia watoto wa marehemu wakamilishe malengo ya elimu yao kama ambavyo baba yao alikuwa amepanga.
 
Marehemu Chang’a anatarajiwa kuzikwa kesho (Jumatato, Aprili 23, 2014) huko Kihesa, Manispaa ya Iringa ambapo Serikali itawasilishwa na Waziri wa Nchi (OWM-TAMISEMI), Bibi Hawa Ghasia. Marehemu ameacha watoto watano, wa kike watatu na wa kiume wawili.
 
 
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM
JUMANNE, APRILI 22, 2014
 

MAMBO YA NATHAN MPANGALA HAYOO NA MAFURIKO NDANI YA JIJI LA DAR

MNEC Magesa ahutubia mkutano wa hadhara Kigamboni

$
0
0

 Ndg. Magesa akishindikizwa na wanachama na wapenzi wa CCM wakati
anawasili katika viwanja Kigamboni kuhutubia mkutano wa hadhara..
Mjumbe wa Halimashauri Kuu ya Taifa (NEC) Ndg. Phares Magesa
akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Tua Moyo Kigamboni 

======  ======  =========
Chama cha Mapinduzi CCM jana tarehe 21/4/2014 kilifanya mkutano mkubwa wa
hadhara katika viwanja vya tuo moyo Kigamboni, mgeni rasmi katika mkutano
huo alikuwa ni Mjumbe wa Halimashauri Kuu ya Taifa (NEC) Ndg. Phares Magesa
. Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi wengine wa chama na serikali pamoja
kutoka bara na visiwani.

Katika mkutano huo Ndg. Magesa aligawa kadi za CCM kwa wanachama wapya zaidi
ya 350 pamoja na kugawa hundi kwa vikundi vya vikoba zaidi ya 30, yote haya
ni katika kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM. Pia MNEC Magesa alisikiliza
kero za wananchi na kuahidi kuzifikisha katika vikao vya juu kwa hatua za
utekelezaji na amehidi kurudi tena na kutoa majibu ya kero zilizowashilihwa
kwake. Wakati akihutubia mkutano huo Ndg. Magesa aliwaasa wananchi kuendelea
kufanya kazi kwa bidii, na kila mmoja ashiriki kikmilifu katika shuguli zote
za kuichumi na kijamii ili kujihakikishia maisha bora.

Ndg. Magesa pia aliwaomba wananchi wote waunge mkono mapendekezo ya wengi
katika mchakato wa katiba ya kuendelea na muundo uliopo wa serikali 2 na
kupitia mchakato huu wa katiba basi kero zilizojitokeza zipatiwe ufumbuzi na
wananchi watapata nafasi ya kutoa uamuzi kupitia kura ya maoni.

KAMATI ZA BUNGE KUANZA KAZI JUMATATU TAREHE 28 APRILI 2014 JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Afisa Habari wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Owen Mwandumbya akielezea kuhusu kufanyika kwa vikao vya Kamati za Bunge vinavyotarajia kuanza tarehe 28 Aprili hadi 4 Mei, 2014,  Jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza Mkutano wa Bunge wa Bajeti tarehe 6 Mei, 2014.  Picha na Tiganya Vincent-BMK-Dodoma

Waziri Mkuu Pinda kuzindua filamu ya Chini ya Kivuli cha Jua

$
0
0
 Afisa Mahusiano na Habari wa Chama cha Albino Tanzania Bw. Josephat Torner akiongea na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam kuhusu na uzinduzi wa filamu ya “Chini ya Kivuli cha Jua” utakaofanyika mwezi Mei 2, mwaka huu ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda. 
Afisa Mahusiano na Habari wa Chama cha Albino Tanzania Bw. Josephat Torner akiongea na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam kuhusu na uzinduzi wa filamu ya “Chini ya Kivuli cha Jua” utakaofanyika mwezi Mei 2, mwaka huu ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda.


=======  ======  =======
Na Frank Mvungi-Maelezo
Filamu ya Chini ya Kivuli cha Jua kuzinduliwa Jijini Dar es salaam wiki ijayo ikiwa ni moja ya hatua za kuelekea maadhimisho ya Mkutano wa Kimataifa kuhusu ualbino unaotarajiwa kufanyika hapa nchini mapema mwezi Mei mwaka huu.
 
Hayo yamesemwa na Afisa Mahusiano na Habari wa Chama cha Albino Tanzania Bw. Josephat Torner wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam kuhusu uzinduzi wa filamu hiyo.
 
Bw. Josephat alisema kuwa katika uzinduzi wa Filamu hiyo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda na uzinduzi unatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Alliance De Francaise   uliopo Upanga Jijini Dar es salaam.
 
Akifafanua Bw. Josephat amesema kuwa lengo kuu la filamu hiyo ni kuwaelimisha watanzania kuhusu matatizo yanayowapata watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) hapa nchini ili jamii iweze kushiriki kikamilifu katika kuondoa  matatizo yanayowakabili.
 
Aliongeza kuwa filamu hiyo imeandaliwa hapa nchini  na baada ya uzinduzi wake itaonyeshwa katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa muda wa miezi 9 ikiwa na lengo la  kuwafikishia ujumbe wananchi kuhusu hali halisi ya maisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
 
Katika ziara ya kuonesha filamu hiyo Bw. Josephat amesema kuwa wataambatana na Madaktari wataalam wa ngozi watakaosaidia kutoa elimu kwa wananchi kuhusu matatizo ya watu wenye ulemavu wa ngozi na hatua za kuchukua ili kuwakinga na athari zinazotokana na mazingira.
 
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Standing Voice lililofadhili mradi wa uandaaji wa Filamu hiyo Bw.Jon Beale alisema filamu hiyo inaujumbe wa kutaka kuonyesha ulimwengu hali halisi ya maisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) na hatua ambazo jamii inapaswa kuchukua katika kuwalinda wale wenye tatizo hilo.
 
Watanzania wamepewa wito wa kushiriki vyema katika kuelimisha jamii kuhusu matatizo ya watu wenye ualbino hapa nchini ili kujenga jamii yenye kuzingatia misingi ya haki na usawa.
 
Filamu hiyo imeshaonyeshwa katika nchi zisizopungua 50 tangu mwaka 2012 ambapo baadhi ya nchi hizo ni Mexico, Brazil, Marekani, Australia, Norway, Sweeden, Dernmark pamoja na nchi nyingine za Ulaya na mabara mengine.
 

SALAM ZA HERI YA MIAKA 50 YA MUUNGANO KUTOKA NGOMA AFRICA BAND

$
0
0
Bend maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "NGOMA AFRICA BAND" aka FFU Ughaibuni,yenye makao yake kule nchini Ujerumani,inaungana na watanzania wote nyumbani na ughaibuni katika kusherehekea "MIAKA 50 YA MUUNGANO WA TANZANIA",Ngoma Africa band inatoa salam za heri na shangwe kwa watanzania wote popote duniani.

ZIDUMU FIKRA ZA WAASISI WA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR = TANZANIA

                                UDUMU UMOJA WA KITAIFA

                                UDUMU MUUNGANO WETU

                                  MUNGU IBARIKI TANZANIA

Tafadhali pata burudani ya muziki at www.ngoma-africa.com

BADO TIKETI MOJA YA KWENDA BRAZILI KUPITIA KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI

$
0
0
 Meneja wa Bia ya Serengeti Rodney Rugambo(kulia) akizungumza na wana habari wakati wa droo ya Kumi na moja ya promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti inayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti mara baada ya kuchezesha droo hiyo mapema leo katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam na anayemshuhudia ni Afisa Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha  Tanzania Bakari Maggid(kushoto). 
  Meneja wa Bia ya Serengeti Rodney Rugambo akizungumza kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa droo ya kumi na moja ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti katika droo iliyofanyika mapema leo jijini Dar es Salaam
Meneja wa Bia ya Serengeti Rodney Rugambo(kulia) akihakiki jina na namba la mshindi huku akishuhudiwa na Afisa Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha  Tanzania Bakari Maggid(kushoto) wakati wa droo ya kumi na moja ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam.

Mahafali ya Pili Chuo cha Mafunzo ya Jinsia Tanzania Yafanyika

$
0
0

Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Asseny Muro (kushoto) akiwahutubia wahitimu wa mahafali ya pili ya chuo hicho leo katika viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Asseny Muro (kushoto) akiwahutubia wahitimu wa mahafali ya pili ya chuo hicho leo katika viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es SalaamMkuu wa Chuo cha GTI, Zuki Mihyo (wa pili kushoto) akitoa hotuba yake kwa wanamahafali wa mafunzo ya jinsia katika chuo cha GTI leo. Mkuu wa Chuo cha GTI, Zuki Mihyo (wa pili kushoto) akitoa hotuba yake kwa wanamahafali wa mafunzo ya jinsia katika chuo cha GTI leoMwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Asseny Muro pamoja na Mkuu wa Chuo cha GTI, Zuki Mihyo (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi (kulia) wakiongoza maandamano ya wanamahafali ya pili ya Chuo cha GTI kuelekea ukumbuni kabla ya kuanza kwa hafla hiyo. Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Asseny Muro pamoja na Mkuu wa Chuo cha GTI, Zuki Mihyo (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi (kulia) wakiongoza maandamano ya wanamahafali ya pili ya Chuo cha GTI kuelekea ukumbuni kabla ya kuanza kwa hafla
 .



.hiyo.Mkuu wa taaluma na mipango wa GTI, Bi Doroth akitamka kuanza kwa sherehe za Mahafali ya Pili ya Chuo cha Mafunzo ya Jinsia Tanzania (GTI) kwenye hafla ya mahafali hayo leo. Mkuu wa taaluma na mipango wa GTI, Bi Doroth akitamka kuanza kwa sherehe za Mahafali ya Pili ya Chuo cha Mafunzo ya Jinsia Tanzania (GTI) kwenye hafla ya mahafali hayo leo.[/caption] [caption id="attachment_45861" align="aligncenter" width="640"]Sehemu ya wanamahafali wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI) wakiwa kwenye sherehe za mahafali yao yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) leo Mabibo jijini Dar es Salaam. Sehemu ya wanamahafali wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI) wakiwa kwenye sherehe za mahafali yao yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) leo Mabibo jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_45859" align="aligncenter" width="480"]Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Jinsia, Asseny Muro (kushoto) akimtunuku cheti cha jinsia mmoja wa wahitimu wa mahafali ya pili ya chuo hicho leo katika viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Jinsia, Asseny Muro (kushoto) akimtunuku cheti cha jinsia mmoja wa wahitimu wa mahafali ya pili ya chuo hicho leo katika viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_45858" align="aligncenter" width="480"]Mmoja wa wanamahafali wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI) (kulia) akionesha cheti chake mara baada ya kutunukiwa. Mmoja wa wanamahafali wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI) (kulia) akionesha cheti chake mara baada ya kutunukiwa.[/caption] [caption id="attachment_45857" align="aligncenter" width="480"]Mmoja wa wanamahafali wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI) (kulia) akikabidhiwa cheti chake mara baada ya kutunukiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Jinsia, Asseny Muro (kushoto). Mmoja wa wanamahafali wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI) (kulia) akikabidhiwa cheti chake mara baada ya kutunukiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Jinsia, Asseny Muro (kushoto).[/caption] [caption id="attachment_45856" align="aligncenter" width="480"]Mmoja wa wanamahafali wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI) (kulia) akionesha cheti chake mara baada ya kutunukiwa. Mmoja wa wanamahafali wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI) (kulia) akionesha cheti chake mara baada ya kutunukiwa.[/caption] [caption id="attachment_45855" align="aligncenter" width="625"]Kaimu Mkurugenzi wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi (kulia) akinong'ona jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Jinsia, Asseny Muro kwenye sherehe za mahafali ya pili ya Chuo cha GTI leo. Kaimu Mkurugenzi wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi (kulia) akinong'ona jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Jinsia, Asseny Muro kwenye sherehe za mahafali ya pili ya Chuo cha GTI leo.[/caption] [caption id="attachment_45854" align="aligncenter" width="640"]Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Jinsia, Asseny Muro, Mkuu wa Chuo cha GTI, Zuki Mihyo, Kaimu Mkurugenzi wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi na meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na wanamahafali baada ya kutunukiwa vyeti vyao. Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Jinsia, Asseny Muro, Mkuu wa Chuo cha GTI, Zuki Mihyo, Kaimu Mkurugenzi wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi na meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na wanamahafali baada ya kutunukiwa vyeti vyao.[/caption][caption id="attachment_45868" align="aligncenter" width="640"]Wanamahafali wakiimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza kwa sherehe za mahafali yao leo. Wanamahafali wakiimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza kwa sherehe za mahafali yao leo.[/caption] Na Thehabari.com, Dar es Salaam

BONDIA THOMAS MASHALI APATA AJALI

$
0
0
Bondia Thomasi Mashali akionesha majeraha aliyoyapata baada ya kupata ajali hivi karibuni picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com


=====  =====  ======
BONDIA Thomasi Mashali amepata ajali ya gari mara baada ya kuangukia mtaloni akiwa anaendesha gari aina ya vitz lenye namba za usajili T 777 BMW ajari hiyo iliyotokea maeneo ya kimara baruti siku ya april 20

wakati akitokea manzese kwenda nyumbani kwake kimara mwisho, akielezea tukio zima la ajali hiyo Mashali 'Alisema nilikuwa naendesha mwenyewe nikakutana na tuta nikaruka tuta nilivyomaliza tu tuta kumbe mbele yangu kulikuwa kumefungwa kutokana na matengenezo ya barabara ya morogoro  ile nataka kukwepa uzio ambapo nilipo kwepea nika ingia mtaloni moja kwa moja

katika gari hiyo tulikuwa wawili na mdogo wangu George Maluma ambaye ajaumia chochote katika ajari hiyo

akizungumzia mchezo wake unao mkabili ambao ulikuwa ufanyike siku ya mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba kwa ajili ya kumkabili Kalama Nyilawila, mashali alisema kuwa kwa sasa sifanyi mazoezi kwa kuwa nauguza majeraha yangu ya kuchubuka na kutoka kwa ngozi katika mkono wangu wa kulia na ubavuni mwangu

namwambia Kalama kuwa kafala laker limegonga mwamba hivyo akae tayali kwa kipigo cha mbwa mwizi kama nilivyo mfanya mwenzie Mada Maugo

kwani na yeye alikuwa anachonga sana lakini mwisho wa siku nikachukuwa ubingwa kupitia kwake yeye mana mpambano huu nilikuwa nausubili kwa hamu kubwa sana leo kesho

mbali na majeraha haya napenda kuwashukuru baadha ya watu walionisaidia  katika tukio zima la mimi kupata ajari na kunisaidia kutoa gari bondeni mpaka sasa ipo katika mikono salama ingawa imearibikwa kwa sababu ya kubondeka

mbali na hivyo nashukuru  promota Ally Mwazoa kwa kuwa na moyo wa huruma na kuhamua kusogeza mbele mpambano huo mpaka siku utakapotangazwa tena pia naomba watanzania waniombee duwa kwani naenderea vizuri kutibu majeraha yangu 




Bondia Thomasi Mashali akionesha majeraha aliyoyapata baada ya kupata ajali hivi karibuni picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
JERAHA LINALO ONEKANA MKONONI
Bondia Thomasi Mashali akionesha majeraha aliyoyapata baada ya kupata ajali hivi karibuni picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
THOMAS MASHALI
Bondia Thomas Mashali wa tatu kushoto akiwa na baadhi tya ndugu na jamaa akiuguza majeraha ya vidonda baada ya kupatas ajari hivi karibuni picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Thomasi Mashali akionesha majeraha aliyoyapata baada ya kupata ajali hivi karibuni picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

JUKWAA LA KATIBA WATANGAZA KUSULUHISHA MGOGORO WA BUNGE MAALUM LA KATIBA

$
0
0
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika ofisi za Jukwaa la Katiba jijini Dar es Salaam katika kutoa tamko rasmi za tathimini ya Jukwaa la Katiba Tanzania kuhusu Katiba Mpya, Tulipotoka, Tulipo na Tuendako. Pembeni ni Msimamizi wa Mradi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya (NGO Network for Dodoma) Bw. Edward Mbogo (kushoto) na Mjumbe wa Jukwaa la Katiba toka Pemba Bw. Omari Omari.

Waandishi wa Habari wakifuatilia.
---
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA) limejitolea kuratibu maridhiano miongoni mwa makundi ya kisiasa asasi za kiraia, asasi za wananchi na taasisi zote za muhimu zilizoguswa na migogoro inayoendelea katika Bunge maalum la katiba Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Jukwaa la Katiba jijini Dar es Salam, Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Bw. Deus Kibamba juu ya tathimini walizozifanya katika bunge hilo wameamua kujitolea kufanya maridhiano hayo kwa kuwashirikisha viongozi maarufu Afrika Mashariki akiwemo mheshimiwa jaji mkuu mstaafu wa Tanzania, Barnabas Samatta ambaye atakuwa mkuu wa jopo hilo la usuluhisho na ndugu Patrice Lumumba kutoka nchini Kenya ambaye atakuwa msaidizi.

Aidha jukwaa hilo limeonyesha masikitiko yake kwa kile alichookiita ni uvunjifu wa kanuni mara baada ya wabunge zaidi ya mia mbili kutoka nje lakini wabunge waliobakia kuendelea kurekebisha kanuni za bunge hilo jambo ambalo wamesema kuwa haikustaili kwani wana uwezo wa kujitungia sheria.

Kibamba amesema kuwa kutokana na mwenendo wa bunge hilo hadi hapa lilipofikia wabunge hao hawana nia ya dhati ya kulipatia taifa katiba mpya huku akitolea mfano kuwa katiba mpya ilipangwa kuwekwa saini na Rais siku ya tarehe 26 mwezi huu yani leo lakini hadi sasa hata majadiliano ya sura mbili hayajamalizika, na kuwahakikishia watanzania kuwa hakuna katiba mpya itakayopatikana kwa mwaka huu.

Hata hivyo mwenyekiti huyo amewataka wajumbe wote na asasi zote zilizopo nje ya muendelezo wa bunge hilo maalumu la katiba kuwa tayari kwa maridhiano kwa mtu au taasisi yoyote atakayekuwa tayari kutatua migogoro yao ili kuwezesha upatikanaji wa katiba kwa taifa letu.

ARS Players happy with training

$
0
0
Participants of the five-day Airtel Rising Stars international soccer clinic take part In training at the Azam complex, Dar es Salaam.
Andrew Stokes, a Manchester United Soccer school coach gives instructions to the participants of the Airtel Rising Stars International soccer clinic which is taking place at the Azam Complex, Dar es Salaam. The clinic comes to end on Sunday.

Participants of the five-day Airtel Rising Stars International soccer clinic have praised showers to the Manchester United Soccer school coaches who are guiding the clinic. The young players said they have learned a lot for the last three days and they are confident that they will have improved their soccer skills come the end of the clinic.

“We have learned how to dribble a ball well, and I am more confident in my dribbling skills than I was before I came here,” said Tiago Gova from Malawi. 

Watching the young students at the soccer clinic play, it is evident that in just a few days, they have picked up several professional footballers’ skills, vastly improving their method of playing the sport. This has instilled both pride and confidence among the players. “We feel like we are approaching professional heights, we are getting good!" Thomas Chindeka, a student player from Tanzania. 

Sixteen year old Lily Awour from Kenya who started playing football  at the age of nine says she was inspired by her sports master to play football.  The form two student says that from the skills she has gained at the clinic she is inspired to explore soccer as a profession. “I am excited about soccer now more than ever before. I want to take it higher and play for my team back home,” she added. 

Another  soccer star at the clinic is fifteen year old Ibrahim Shambi Mombasa, Kenya . He says he, too, is motivated to take up soccer as a professional career. “Since I came to the clinic, I have developed great passing and scoring skills. I am now able to pass a ball, with focus and score for my team,” he remarked. “Our coaches have emphasized on teamwork as well as keeping focus on the game and the ball to score a goal,” he added.

Besides football skills the coaches have paid special attention to encouraging the students to stay focused on education. “Not everyone will be a professional footballer," explains Neil Scott, who is the Head coach of the clinic. "I would like you to work hard in school just like you work here in the field.”

In addition, students have also learnt about discipline, respect, and tolerance, to ensure they are groomed as all-round players. 

The clinic runs until Sunday and has seen 72 girls and boys of age 13-17 from 12 African countries come together for the clinic under the guidance of Manchester United Soccer schools. This is the third international soccer clinic for the Airtel, in partnership with Manchester United FC to host.

Tanzania kufikia kipato cha kati ifikapo mwaka 2025

$
0
0
Na Greyson Mwase, Ujerumani

Tanzania inatarajiwa kuondoka kwenye kundi la nchi masikini na  kuhamia kwenye kundi la nchi zenye kipato cha kati ifikapo mwaka 2025. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo alipokuwa akifungua  kongamano linaloendelea huko Berlin nchini Ujerumani  kama njia mojawapo ya kuadhimisha jubilee ya miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Kongamano hilo  linakutanisha wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na mabalozi, wataalamu na wafanyabiashara mbalimbali ambapo  Profesa Muhongo alipata nafasi ya kuwasilisha mada kuhusiana na  fursa zilizopo katika  sekta ya  gesi, mafuta ikiwa ni pamoja na madini.

Profesa Muhongo alisema ili nchi ya Tanzania iweze kupiga hatua kimaendeleo inahitaji uwekezaji mkubwa kwenye nishati ambayo ndiyo yenye mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi.

Akielezea juhudi za serikali katika kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa na maisha  bora, Profesa Muhongo alisema kuwa serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeanza juhudi  za kupeleka umeme kwenye vijiji vyote kwa awamu tofauti tofauti.

“ Hatuwezi kusema kuwa nchi imeendelea wakati wananchi wa vijijini hawana umeme, na katika kutambua hilo serikali imeweka nguvu nyingi  kuhakikisha kuwa nishati ya umeme inapatikana vijijini na kuchochea maendeleo.” Alisisisitiza Profesa Muhongo.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Rais Kikwete atunuku Nishani na Tuzo Za miaka 50 Ya Muungano

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete usiku wa kuamkia leo ametunuku nishani na Tuzo kwa viongozi mbalimbali wa kitaifa na watumishi wa umma wapatao 86 waliotoa mchango wao katika kuulinda na kuudumisha muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliodumu kwa miaka Hamsini 50.
Mama Maria Nyerere akipokea nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano(Order) kwa niaba ya Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Mama Maria Nyerere Nishani ya Kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungnao Daraja nne.

Mama Fatma Karume akipokea Nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano(Order) kwa niaba ya Marehemu Abeid Aman Karume Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Mama Fatma Karume nishani ya kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano Daraja Nne wakati wa hafla ya kutunuku nishani na tuzo za miaka 50 Muungano zilizofanyika katika ukumbi wa mikutano ikulu jijini Dar es Salaam jana usiku.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Rais mstaafu wa Awamu ya tatu Mh.Benjamin William Mkapa Nishani ya Kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano(Order) wakati wa sherehe ya kutunuku nishani na tuzo iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano ikulu jijini Dar es Salaam jana usiku.(picha na Freddy Maro)
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Nishani ya Kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Kwanza Waziri Mkuu mstaafu ambaye pia alikuwa Mwenyekiti Tume ya kurekebisha Katiba  Mhe. JajiJoseph Sinde Warioba wakati wa Sherehe hizo zilizofanyika katika ukumbi wa mikutano ikulu jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia jana Picha zote na Freddy Maro




WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AONGOZA WANANCHI KWENYE MKESHA WA MUUNGANO

$
0
0
 Waziri Mkuu na Mgeni Rasmi wa Mkesha wa Muungano Mizengo Pinda akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kuongoza mamia ya wananchi waliohudhuria kwenye mkesha huo.Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Abdulrahman Kinana na kulia kwake ni Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Iddi na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhandisi Raymond Mushi. 
 Wageni waaliwa ikiwemo Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika za Kimataifa.
 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Mwansoko (katikati) akiwa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Joyce Fisoo (wa pili kushoto) na watumishi wengine wa Wizara hiyo.

 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kujumuika katika Mkesha wa Muungano.Kulia kwake ni mwenyeji wake Wilaya ya Ilala Mhandisi Raymond Mushi . 
Kikindi cha Taifa cha Taarabu kikitumbuiza wananchi waliohudhuria kwenye mkesha na wimbo Maalum unaojulikana kama Muungano Wetu.  
 Kikundi cha Burudani kutoka Tanga kikuburudisha hadhira 
 Mzee Yusuf na Kundi lake la Jahaz Morden Taarabu.
 Baadhi ya vijana wakiburudika

 Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda, akiwaaga baadhi ya wageni waalikwa na kuondoka baada ya kuongoza Mkesha wa Muungano.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Iddi, akitoa salamu zake kwa wananchi.
 Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda, akitoa neno kwa wananchi.

 Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda, akijiandaa kubofya kitufe cha kuashiria kuzaliwa upya kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

 Maandishi Maalumu yakihamasishana kuashiria kutimia kwa Miaka 50 ya Muungano.
 Fashfash na fataki zikamiminika kwenye anga ya viwanja vya Mnazi Mmoja. 
 Profesa Mwansoko akizungumza na Televisheni One.
 Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda, akiwaaga baadhi ya wageni waalikwa na kuondoka baada ya kuongoza Mkesha wa Muungano.

Katibu wa Nchi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushelisheli, Barry Faure akutana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Prof. Anna Tibaijuka jijini Dar leo

$
0
0
 Katibu wa Nchi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushelisheli, Barry Faure (Kulia) akitia saini kitabu cha wageni wakati alipowasili kwenye Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Prof. Anna Tibaijuka jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo.Kushoto ni Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania.
 Katibu wa Nchi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushelisheli, Barry Faure (Kulia) akizungumza na Wazirii wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Prof. Anna Tibaijuka (Kushoto) wakati alipotembelea Wizara hiyo jijini Dar es Salaam.Pembeni yao ni Maafisa kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Wizara ya Mambo ya Nje.

 . Wazirii wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Prof. Anna Tibaijuka akifafanua jambo wakati alipokuwa akizungumza na mgeni wake wa Katibu wa Nchi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushelisheli, Barry Faure(hayupo pichani) alipotebela Wizara hiyo jijini Dar es Salaam.

Wazirii wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Prof. Anna Tibaijuka akizungumza (Kushoto) wakati Katibu wa Nchi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushelisheli, Barry Faure (Kulia) wakati alipotembelea Wizara hiyo jijini Dar es Salaam.Pembeni yao ni Maafisa kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Wizara ya Mambo ya Nje.Picha zote na Hussein Makame-MAELEZO

SHEREHE ZA MIAKA 50 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR ZAFANA BERLIN, UJERUMANI. PROFESA MUHONGO AZINDUA SHEREHE HIZO

$
0
0
 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (Mb.) (kushoto) akiingia katika ukumbi wa Deustche Bank uliopo Berlin, Ujerumani kabla ya kuzindua rasmi sherehe za jubilee ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kulia ni balozi wa Tanzania Ujerumani Mhe. Philip Marmo.

 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (Mb) akizungumza na  baadhi ya wajumbe waliohudhuria  sherehe hizo

 Kikundi cha ngoma za sanaa kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania  kikitumbuiza  kabla ya kuanza kwa sherehe hizo
 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (Mb) akibadilishana mawazo  na balozi wa heshima wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Hamburg Petra Hammelmann. Kulia ni mume wa balozi huyo Bw.Bertold Zink.

 Waziri wa Nishati na  Madini Profesa Sospeter Muhongo (Mb) (wa  pili kutoka kulia) akiwa amesimama kwa heshima na wajumbe wengine wakati wimbo wa taifa ukipigwa na kikundi cha ngoma za sanaa cha Jeshi la Wananchi Tanzania (hawapo pichani)

 Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Philip Marmo akimkaribisha Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ili afungue maadhimisho hayo

 Waziri wa Nishati na  Madini Profesa Sospeter Muhongo (Mb) akifungua sherehe hizo

 Mhadhiri kutoka chuo  kikuu cha Dar es salaam Profesa Palamagamba Kabudi (wa tatu kutoka kulia) akichangia mjadala juu ya historia ya ushirikiano baina ya Tanzania na Ujerumani wakati wa maadhimisho ya sherehe hizo

Timu ya wataalamu kutoka Tanzania waliohudhuria sherehe hizo wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania Nchini Ujerumani Mhe. Philip Marmo (wa kwanza kulia)

Katibu wa CHADEMA Jimbo la Mufindi Kusini, Emannuel Ngwalanje , Ahamia CCM

$
0
0

Emmanuel Ngwalanje akitoa yake yaliyokuwa moyoni kwa wananchi kabla ya kujiunga na CCM.
Katibu wa Chadema Jimbo la Mufindi Kusini, Emannuel Ngwalanje akikabidhi vitendea kazi vyake na kadi ya Uanachama wa CHADEMA kwa katibu wa CCM wilaya ya Mufindi Miraji Mtaturu (kushoto ) baada ya kukihama chama hicho na kujiunga na CCM
Aliyekuwa Katibu wa CHADEMA Jimbo la Mufindi Kusini, Emannuel Ngwalanje akipewa vitendea kazi vya CCM na kadi ya Uanachama baada ya kujiunga na chama chenye umoja na mshikamano, CCM.

=======  =====  =======

MZIMU wa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe umeelezwa kumkimbiza hadi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Katibu wa Chadema jimbo la Mufindi Kusini, Emannuel Ngwalanje.


Hatua ya Ngwalanje kujitoa Chadema na kujiunga na CCM imeelezwa na baadhi ya wafuasi wa Chadema kuwa ni pigo kubwa kwa chama hicho.

Akizungumzia kujitoa kwa Ngwalanje, mwanachama wa Chadema Michael Ngimbusi alisema; “Ngwalanje alikuwa nguzo kuu ya Chadema wilayani Mufindi, aliogopwa na wana CCM, hiyo ikiwa ni kutokana na uwezo wake mkubwa wa kushawishi na kujenga hoja.

Katika kipindi cha zaidi ya miaka minne ambacho Ngwalanje amekuwa Katibu wa Chadema jimbo la Mufindi Kusini ameweza kushawishi zaidi ya wakazi 600 katika maeneo mbalimbali jimboni humo kujiunga na chama hicho.

Katika mkutano wa mapokezi yake uliofanyika kijijini kwake Kimilinzowo kata ya Itandula alisema; “Kazi ya kuibomoa Chadema haitaishia katika wilaya ya Mufindi pekee, bali nitaiendeleza hadi Jimbo la Iringa Mjini linaloongozwa na Mchungaji Peter Msigwa kupitia Chadema.” Ngwalanje alisema utawala mbovu na matumizi mabaya ya fedha za ruzuku utaisambaratisha Chadema katika kipindi kifupi kijacho.

Alisema chama hicho kinapata fedha nyingi zinazotokana na ruzuku ya serikali na michango ya wanachama, wafuasi na marafiki zake wa ndani na nje ya nchi lakini zimekuwa zikiwanufaisha wachache.

Alisema wakati kundi kubwa la viongozi wa chama hicho likifanya kazi kwa kujitolea, kundi la wachache walioko makao makuu wamekuwa wakitafuna fedha hizo bila woga huku wakiwatishia wanaohoji.

Alisema demokrasia inayohubiriwa kutafutwa na chama hicho nchini ina walakini kwa kuzingatia kwamba ndani ya chama hicho zipo nafasi za uongozi ambazo kwa wengine ni uhaini kuziwania.
Kwa hisani ya Habarileo.

SHEREHE ZA MUUNGANO KITUO CHA GENEVA, SWITZERLAND ZAFANA

$
0
0
Balozi wa Tanzania katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Geneva,  Mhe.  Modest Mero, akimkaribisha Balozi wa Jamhuri ya watu wa  China-Geneva, Liu Jieyi katika tafrija maalum ya maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa ILO hii leo na kuhudhuriwa na mabalozi wa nchi mbalimbali ikiwemo balozi huyo China UN mjini Geneva, Balozi wa Kenya, Balozi wa Afrika Kusini, Balozi wa Togo, Balozi wa Botswana, Balozi wa Cameroon, Balozi wa Rwanda, wawakilishi wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa na Watanzania waishio Switzerland. Kushoto ni Mke wa balozi huyo Rose  Mero.
 

 Mke wa Balozi Mero, Rose  Mero akisalimiana na ujumbe wa Ubalozi wa Denmark. pamoja nao ni Balozi Modest Mero na Balozi wa Dernmark-UN.
 Balozi Mero akijumuika na mabalozi wa nchi mbalimbali waliohudhuria katika tafrija hiyo.
 Familia ya Balozi Mero katika picha ya Pamoja.
 Wanawake mbalimbali waliohudhuria tafrija hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na mke wa Balozi Mero.
 Balozi Mero alitoa hotuba ambayo ilielezea historia, maendeleo, na maendeleo ya mchakato wa Katiba mpya, Hotuba hiyo pia iliweza kubaiinisha wazi ni vipi Tanzania na Watanzania wameweza kumudu kurumu katika muungano huo kwa miaka 50 sasa.
  Afisa Utawala katika Ubalozi wa Tanzania UN, Hamisa Mkoma akiwa na Mke wa Balozi wa Tanzania UN, Mama Rose Mero
Balozi Modest Mero akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maofisa katika Ubalozi wa Tanzania UN mjini Geneva. 

Wageni mbalimbali waliohudhuria tafrija hiyo.
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images