Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 273 | 274 | (Page 275) | 276 | 277 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Balozi wa Urusi anayefanyakazi hapa nchini  Alexander Rannikh  akiwa  na waumini wenzake wakipewa Baraka na Askofu  wa Dhehebu ya Orthodox  Askofu Dimitrios  wakati wa   Ibada ya Kusherehekea Sikukuu ya Pasaka iliyowashirikisha  Waumini mbalimbali  wakiwemo Watanzania,Wagiriki na Warusi.Ibada hiyo iliafanyika jijini Dar es Salaam.

  Balozi wa Urusi anayefanyakazi hapa nchini  Alexander Rannikh akipewa Baraka na Askofu  wa Dhehebu ya Orthodox  Askofu Dimitrios  wakati wa   Ibada ya Kusherehekea Sikukuu ya Pasaka  iliyowashirikisha  Waumini mbalimbali wakiwemo Watanzania,Wagiriki na Warusi.Ibada hiyo iliafanyika jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa Urusi anayefanyakazi hapa nchini  Alexander Rannikh, akiteta jambo na Askofu Mkuu wa Dhehebu ya Orthodox  Askofu Dimitrios baada ya kumalizika kwa Ibada ya Kusherehekea Sikukuu ya Pasaka  iliyowashirikisha  Waumini mbalimbali  wakiwemo Watanzania,Wagiriki na Warusi.Ibada hiyo iliafanyika jijini Dar es Salaam
  Balozi wa Urusi anayefanyakazi hapa nchini  Alexander Rannikh  akiwa  na waumini wenzake wakipewa Baraka na Askofu  wa Dhehebu ya Orthodox  Askofu Dimitrios  wakati wa   Ibada ya Kusherehekea Sikukuu ya Pasaka iliyowashirikisha  Waumini mbalimbali  wakiwemo Watanzania,Wagiriki na Warusi.Ibada hiyo iliafanyika jijini Dar es Salaam.


  Baadhi ya Waumimi wa Dhehebu ya Orthodox  wakiwa katika Ibada ya kusherehekea  ufufuko wa Yesu Kristu (Pasaka) iliyofanyika katika Kanisa hilo lililpo eneo la Red Cross jijini Dar es Salaam. Picha na Albart Jackson 


  0 0

   Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Dokta Sira Ubwa Mamboya akimkaribisha Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi katika uzinduzi wa kampeni za kutoa huduma za kisukari na shinikizo la damu zitakazofanyika Mikoa yote ya Zanzibar.

   Mratibu wa mtadi wa kutoa huduma za kisukari na shinikizo la damu Mr. Siraji M. Mtulia akitoa maelezo mafupi ya mradi huo utakaoanza kutekelezwa leo na Chama cha wanafunzi Madaktari Tanzania wakishikiana na Wizara ya Afya Zanzibar.
    Mkuu wa CHUO cha (IMTU) Prof. Flora Fabian akitoa maelezo kuhusu madaktari hao walivyojipanga kufanya kazi katika Mikoa yote ya Unguja na Pemba.
   Makamu wa Pili wa Rais Balozi. Seif Ali Iddi akiwahutubia Madaktari na wananchi waliofika katika uzinduzi wa kampeni za kutoa huduma za kisukari na shindikizo la damu huko ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Suza Mjini Zanzibar.
   Balozi Seif na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Sira wakikagua utoaji huduma mara baada ya kuzindua.
   Makamu wa Pili wa Rais Balozi. Seif Ali Iddi (wakatikati waliokaa) katika picha ya pamoja na wanafunzi madaktari kutoka vyuo mbalimbali Tanzania.
  Balozi Seif akiagana na wanafunzi madaktari mara baada ya kuzindua huduma za upimaji afya katika sherehe zilizofanyika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Suza Mjini Zanzibar. PICHA ZOTE NA MAKAME 
  MSHENGA WA MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0

  Bondia Francis  Cheka (kushoto) akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Gavad Zohrehvand wa Iran wakati wa mpambano wao wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba Jumamosi jijini Dar es salaam. Mpambano huo uliamuliwa kwa droo ya kufungana point
  Bondia Francis  Cheka kushoto akipambana na Gavad Zohrehvand wa Iran wakati wa mpambano wao wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es salaam mpambano huo uliamuliwa kwa droo ya kufungana point 
  Bondia Francis  Cheka kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Gavad Zohrehvand wa Iran wakati wa mpambano wao wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es salaam mpambano huo uliamliwa kwa droo ya kufungana point 

   Bondia Sukkasem Kietyongyuth  kutoka Thailand kulia akiwa amemkalisha bondia Francis  Miyeyusho katika raundi ya kwanza ya mpambano wa raundi kumi na kushinda kwa K.O. 

  0 0


  Msanii maarufu nchini Tanzania  Kutoka kundi la Orijino Komedi al maarufu kama Mpoki a k a Muarabu wa Dubai anatarajiwa kuondoka nchini mapema mwanzo wa wiki hii kwenda nchini Ujerumani kuhudhuria  Mkutano mkuu wa Umoja wa Watanzania Ujerumani (U T U), utakaoambatana na Kongamano la kibiashara pamoja na Sherehe za Muungano wa Tanzania , zitakazoanza  siku ya ijumaa tarehe 25.04.14 na kumalizika siku ya Jumamosi Tarehe 26.04.14.

  Mpoki amesema kuwa  umuhimu mkubwa wa safari yake ni  kuwakilisha wasanii wa Tanzania katika Tamasha hili kubwa  la aina yake, na  kufafanua  kuwa wakati umefika kwa wasanii wa Tanzania kushirikiana kikamilifu na Watanzania wanaoishi nje ya nchi ili kuweza kupata fursa mbali mbali  zilizopo huko. 

  Amesema  amevutiwa sana na Umoja Wa Watanzania Ujerumani (U T U) kwa shughuli zake   mbali mbali ambazo umekwishazifanya nchini humo  na ameamua kutoa mchango wake wa hali na mali kuhakikisha     (U T U) inafanya vizuri zaidi  na kwamba yeye binafsi amekuwa ni mfuatiliaji wa karibu sana  wa shughuli za umoja huo.

   Mwenyekiti  wa Umoja Wa Watanzania Ujerumani Bw. Mfundo Peter Mfundo alithibitisha  safari ya msanii huyo Maarufu nchini Tanzania, na kusema U T U Ilipendelea sana wasanii zaidi kuhudhuria sherehe hizi lakini kwa bahati mbaya  haikuwezekana  kutokana na mambo yalio nje ya uwezo wao ingawa UTU  ni chombo kinachokubali sana na kuzifagilia kazi za wasanii wa Tanzania.

  U T U inamtakia Bw Mpoki Safari njema.


  0 0

  Chama  Cha Mapinduzi- London – Uingereza  kinaridhia Salaam za CCM Makao Makuu kuungana na Wakristo- Watanzania na Ulimwenguni kote  kuwatakia kila la kheri na fanaka katika kusherehekea Sikuu Kuu ya PASAKA 2014.

  Aidha CCM UK  inayo imani kubwa kuwa Sherehe hii ya Pasaka itakuwa kigezo cha kuwakaribisha Watanzania wa Imani zote kujitazama kwa wongufu na kuridhia misingi mikuu ya Uhuru, Muungano wetu na Umoja wa Taifa letu.

  CCM UK inaungana na Watanzania wote kukememea dhidi ya vichocheo vya aina zote vinavyohatarisha umoja wa TAIFA LETU, usalama wa raia na mali zao, uhuru wao wa kuabudu na kusujudu ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

  Kwa kuwa Dhamira kuu ya Pasaka ni kujenga Upendo, Mshikamano, Umoja na Uhuru, hasa katika kipindi hiki cha kutafakari mchakato wa Kupata KATIBA MPYA yenye kukidhi kiu ya maendeleo kwa Wananchi Kiuchumi na kimaendeleo kama Taifa moja, CCM UK inawatakia kila la kheri katika kusheherekea sikukuu hii muhimu kwa Wakristo wote Duniani kwa Amani na Utulivu.

  MUNGU IBARIKI TANZANIA.

  Imetolewa na Abraham Sangiwa -  Idara ya Siasa na Uenezi.
  CCM –  TAWI LA UINGEREZA - UNITED KINGDOM.
  20th April -2014

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kalambo enzi za uhai wake Mhe. Moshi Mussa Chang'a ambae amefariki dunia jioni ya leo katika Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu ya ugojwa wa shinikizo la damu na Kisukari. 

  Taratibu za mazishi zitatangazwa mapema mara baada ya kikao cha wanandugu. Tunatoa pole kwa wale wote walioguswa na msiba huu. Sisi tulimpenda lakini Mungu kampenda zaidi. Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe.
  (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

  0 0

   Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa Mh. Bernald Membe aliyemuakilisha Rais Jakaya Kikwete katika Tamasha la Pasaka lililofanyika jana kwenye uwanja wa Taifa akizungumza na mashabiki mbalimbali waliojitokeza katika tamasha hilo na kuwaomba kuwa watulivu wakati huu wa mchakato wa katiba mpya akisema uamuzi mtautoa ninyi, ni serikali gani mnaiihitaji iwe moja, Tatu au Mbili nyinyi ndiyo mtaamua na sisi tutakipitisha kile mlichokiamua, Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama na katikati ni Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Mh. Angela Kairuki.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
   Mwanamuiki wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini Keke Letse Phoofolo akicheza na mashabiki wake wakati alipokuwa akifanya vitu vyake  kwenye uwanja wa Taifa jana.
   Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Zambia Ephraim Sekereti akiimba jukwaani jana.
   Mwanamuiki wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini Keke Letse Phoofolo akicheza na kwa mbwembwe wakati alipokuwa akifanya vitu vyake  kwenye uwanja wa Taifa jana.
    Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa Mh. Bernald Membe aliyemuakilisha Rais Jakaya Kikwete akiongozwa kuelekea jukwaani na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama
   Mwimbaji wa ijini kutoka nchini Uingereza Dayo Bello akiimba na mkewe Ruth Tobi wakati wa tamasha la pakasa kwenye uwanja wa Taifa jana.

   Mwimbaji Jesca BM naye alipagawisha mashabiki
   Mchungaji mtarajiwa Masanja Mkandamizaji akifanya vitu vyake jukwaani
   Umati uliojitokeza  katika tamasha hilo.
    Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa Mh. Bernald Membe aliyemuakilisha Rais Jakaya Kikwete katika Tamasha la Pasaka akirejea kuketi huku akizungumza na Richard Kasesela na Alex Msama katikati.
   Upendo Kilahiro akiimba jukwaani na kundi la Victoria Singers.
   Mashabiki mbalimbali wakimshuhudia mwanamuziki Kekeletse Phoofolo hayupo ichani wakati alipokuwa akifanya vitu vyake jukwaani.
  Ikafika zamu ya Upendo Nkone
  Mwanamuiki wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini Keke Letse Phoofolo kazi moja tu burudani .
  Rose Muhando na kundi lake wakipagawisha kwenye tamasha la Pasaka jana katika uwanja wa Taifa.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa,Injinia Stella Manyanya akiwa ni mwenye majonzi wakati akisaini kitabu cha Maombolezo ya Kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Mhe. Moshi Mussa Chang'a ambae alifariki dunia jana jioni katika Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu ya ugojwa wa shinikizo la damu na Kisukari.  

  Msiba upo nyumbani kwa Marehemu,eneo la Mbagala jijini Dar es Salaam ambapo taratibu zote zinafanyika hapo.

  Taarifa za awali zinaeleza kwamba Shughuli ya kuaga mwili wa Marehemu,Mhe. Moshi Mussa Chang'a itafanyika kesho Aprili 22,2014 nyumbani kwake Mbagala na baadae mwili utasafirishwa kwenda kijijini kwao Mkoani Iringa kwa Mazishi.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick (katikati) akijadiliana jambo na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa,Injinia Stella Manyanya (kulia) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bahi,Mh. Betty Mkwassa wakati wakiwa kwenye Msiba wa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Mhe. Moshi Mussa Chang'a,nyumbani kwa Marehemu Mbagala,jijini Dar es Salaam leo.
   Baadhi ya Waheshimiwa wakuu wa Wilaya mbali mbali hapa nchini wakiwa kwenye msiba wa Mkuu mwenzao wa Wilaya ya Kalambo, Mhe. Moshi Mussa Chang'a ambae alifariki dunia jana jioni katika Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu ya ugojwa wa shinikizo la damu na Kisukari,nyumbani kwa Marehemu Mbagala jijini Dar es salaam.

  0 0

   Mchezaji wa timu ya Ofisi ya Rais (Utumishi) Fatuma Machenga (GS) akigombea mpira hewani na mchezaji wa timu wa Alliance One (GK) katika mechi ya mashindano ya Mei Mosi 2014 yanayoendelea katika  Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

   Wachezaji wa timu ya Ofisi ya Rais (Utumishi) na Alliance One wakiwa kwenye harakati za kugombea mpira katika mechi ya mashindano ya Mei Mosi 2014 yanayofanyika katika Uwanja wa Jamhuri mjini mjini Morogoro.

   Mchezaji  wa  timu ya Ofisi ya Rais (Utumishi) Fatuma Machenga (GS)  akifunga goli  dhidi ya timu ya  Alliance One katika mechi ya mashindano ya Mei Mosi mwaka huu iliyofanyika jana Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
   Mchezaji wa timu ya Alliance One (GK) akitoa upinzani kwa Fatuma Machenga (GS) wa Ofisi ya Rais (Utumishi) katika mechi ya mashindano ya Mei Mosi mwaka huu iliyofanyika jana Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

  Mchezaji wa timu ya Ofisi ya Rais (Utumishi) Mwadawa Twalibu (GA) akitoa pasi kwa Fatuma Machenga (GS) katika mechi ya mashindano ya Mei Mosi mwaka huu iliyofanyika jana Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.


  ======= ====== ========
   Timu ya mpira wa Pete ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma imeanza mashindano ya Mei Mosi 2014 kwa ushindi mnono kwa kuichapa timu ya Alliance One ya Morogoro magoli 46 kwa 7. 
   Mchezo huo ulifanyika katika Uwanja wa Jamhuri Siku ya Pasaka uliwachukua Utumishi takribani dakika 10 za mchezo kuwasoma wapinzani wao na kuanza kufunga ambapo hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Alliance One walishakubali magoli 23 dhidi ya 5. 
  Wachezaji waliofanikisha ushindi huo ni Fatuma Machenga (GS) kwa kushirikiana Mwadawa Twalibu (GA), ambao walifanikiwa kufunga magoli 34 na 12 katika goli la wapinzani wa Utumishi. 
  Mara baada ya mchezo huo nahodha wa timu ya Ofisi ya Rais (Utumishi) Elizabeth Fusi alisema kuwa amefurahishwa na matokeo hayo na kuahidi kuendelea kuzitimulia vumbi timu pinzani katika michezo itakayofuata. “Tumepania kuwa mabingwa mwaka huu hivyo tutacheza kwa bidii ili kuhakikisha tunatimiza ndoto yetu” Fusi alisema. 
  Naye, Mwenyekiti wa timu ya Alliance One Bw. Charles J. Kung’aro alikiri kuwa timu yake ilizidiwa mbinu za kimchezo na Utumishi hivyo kuwaweka wachezaji wake katika wakati mgumu kimchezo hasa wanaposhambuliwa. “Tuliruhusu wautawale mchezo hivyo ikawa rahisi kwao kutufunga hivyo tumejipanga kurekebisha makosa yetu ili tufanye vizuri katika mechi zijazo” Bw. Kung’aro alisema. 

  Mashindano ya Mei Mosi 2014 kitaifa yanafanyika mjini Morogoro kwa kuhusisha michezo ya mpira wa miguu, netiboli, kuvuta kamba, riadha, mbio za baiskeli, karata, bao na drafti.

  0 0


  Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha wilayani Makete mkoani Njombe, baadhi ya barabara zimeharibika vibaya na kusababisha kero kwa watumiaji wa barabara hizo. 

  Pichani ni hali ya barabara ya Tanesco iliyopo Makete mjini inavyoonekana ikiwa imejaa mashimo na tope kwa wingi, huku vifusi vya kuikarabati vikiwa vimelundikwa pembeni na kazi ya kuikarabati kushindwa kufanyika kutokana na mvua nyingi zinazonyesha wilayani hapo.(Picha na Edwin Moshi)

  0 0

  Mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Gulatone Masiga akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari(hawapo pichani), kushoto ni Acbert Sweya kutoka Chuo Kikuu cha Kampala.wakati wa Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) jana jijini Dar es Salaam.

  =======  =======  ======
  VIJANA WAZALENDO WA VYUO VYA ELIMU YA JUU DAR ES SALAAM


  TAMKO LA KULAANI VURUGU ZINAZOJITOKEZA KATIKA BUNGE MAALUM LA KATIBA.


  Sisi wanafunzi  wasomi katika vyuo vikuu mbalimbali vilivyoko Dar es Salaam (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM); Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU); Dar es Salaam University College of Education (DUCE); USTAWI WA JAMII; Chuo Kikuu cha Mtakatifu John (St. John); Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM); Open University of Tanzania (OUT); Kampala International University (KIU); Dar es Salaam Institute of Technology (DIT); Institute of Adult Education (IAE); Tanzania School of Journalism (TSJ); College of Business Education (CBE) na Chuo cha kumbukumbu ya Mwl JK Nyerere. Sisi sote  tunalaani mwenendo uliyojengeka kwa wanasiasa wanaojiita “UKAWA“ kuvuruga Bunge Maalum la Katiba kwa sababu ambazo si za msingi. Kwanza walianzakudhalilisha wanazuoni wanaoonekana kutofautiana nao kimawazo kuhusu msimamo wao wa kutaka serikali tatu. Wanazuoni ambao wamekuwa wakidhalilishwa na kutungiwa uongo ni pamoja na Profesa Issa Shivji, Profesa Teddy Malyamkono, Profesa Nehemia Osoro, Dk. Francis Michael, na Dk. Kitila Mkumbo. Tungependa kuwataarifu  kuwa wanataaluma wana uhuru wa kutoa mawazo yaani academic freedomna kamwe hawawezi kukaa kimya wanapoona kuna jambo linaloweza kuifanya  nchi ikaangamia na kusambaratika. Wanazuoni  huamini katika “no research,  no data, no right to speak” kwani data zao za kiuchumi, kihistoria, kisiasa na kidiplomasia zinakataa muundo wa serikali tatu. Hoja ya kimsingi ni kuwa “UKAWA” imeanza juzi, je tafiti (research) wamezifanya lini za kuzipa nguvu hoja zao za kutaka serikali 3?

  Tatizo lingine tunaloliona kwa“UKAWA” ni kujaribu kuwadhalilisha waasisi wa taifa letu hasa Mwl JK Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume. Je tusipomuamini Mwl Nyerere na Sheikh Karume tumuamini nani kati ya hawa ambao hatuna ushahidi wa uzalendo wao? kwani wapo wanasiasa ya aina yao ambao wametumika na mataifa ya kibeberu kuvuruga nchi zao na mpaka leo wananchi wao wanataabikamfano hai ni Misri, Tunisia, Morocco, Sudan Kusini, Somalia, Libya, Mali Na Afrika ya Kati. Heshima walionayo  waasisi wetu Mwl Nyerere na Sheikh Karume ndani na nje ya Tanzania, sio ya kupuuzwa wala kufananishwa hata kidogo na yeyote yule miongoni mwa waliounda “UKAWA”zaidi ya kutumika kama mfano na kielelezo. Tunawashangaa baadhi ya wanasiasa wa“UKAWA” kuwakejeli waasisi wa taifa letu. Wanasiasa hawa ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, Profesa Ibrahim Haruna Lipumba, Mh. Tundu Lissu na Halima Mdee kwani wamesoma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kilichoasisiwa na waasisi wakuu wa taifa letu, Mwl JK Nyerere na Sheikh Karume. Hata wale wanasiasa wengine ambao hawakupata bahati ya kusoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wamesoma kwenye shule za awali na vyuo vya elimu ya juu ambavyo vina msingi wa utawala bora wa waasisi hawa wakuu wa taifa letu. Hivyo tunaona sio busara hata kidogo kukejeli mchango wao katika harakati za kuliendeleza taifa letu. Tunapenda kuwathibitishia watanzaia kuwa mawazo ya waasisi wa taifa letu hajachakaa na wala hayapitwa na wakati hata mara moja.

  Sisi kwa mtazamo wetu kama vijana wasomi wazalendo wa vyuo vya elimu ya juu tunashauri yafuatayo;

  • Katiba bora haiwezi kupatikana kwa kususia vikao halali vya bunge maalum la katiba na maandamano, hivyo tunawasihi warejee bungeni ili waendelee na mchakato kutengeneza katiba. Hatua hii ya kurejea bungeni ikishindikana, warejeshe posho za vikao ambavyo hawajahudhuria.

  • Kutofautiana kimawazo kwa njia ya kujenga hoja ndio demokrasia pevu yenye dhana ya “wachache wasikilizwe na wengi wapewe” ambayo ni moja ya misingi mikuu ya demokrasia itakayotupatia “Katiba Bora” ya sasa na vizazi vijavyo.

  •  Lazima wafahamu kuwa maridhiano ndio njia pekee ya kupata “Katiba Bora” yenye kuleta “Elimu Bora”; “Kilimo Bora”; “Afya Bora”; “Uchumi Bora” na “Utawala Bora” kwa maisha bora ya mtanzania na pia kuifanya Tanzania kuendelea kuwa kisiwa cha amani na utulivu ili kupigiwa mfano na kuwa kimbilio la waafrika wenzetu wengi wanaotaabika kwa kuzikimbia nchi zao kwa machafuko yanachochewa na mabeberu wa siasa na uchumi duniani. 

  • Tunawasihi wenzetu wazingatie umuhimu wa kulinda, kudumisha, kustawisha na kuiendeleza amani katika kipindi cha kutengeneza katiba na baada ya mchakato. Tusipojiangalia tutakuwa kama wenzetu Misri, Tunisia, Morocco, Sudan Kusini, Somalia, Libya, Mali na Afrika ya Kati. Tunaamini kwa kuangalia hali za kisiasa za nchi nyingi za Afrika tunaamini kuwa siasa ya Tanzania ni safi na hakuna haja ya kuhamasisha chuki, uzandiki, uzushi, uongo maandamano na uasi ambao ni sumu kali ya umoja (muungano), amani na uhai wa taifa letu tukufu la Tanzania.

  • Watanzania na wanasiasa wafahamu kwamba mataifa kama Marekani na Uingereza yametawala dunia kwa sababu ya umoja wao. Tunaomba tujifunze kwa yaliyotokea Urusi, leo hii imeona umuhimu wa kuzirudisha nchi ambazo zilisambaratika kutoka kwenye serikali ya umoja wa nchi za kijamaa za kisovieti (USSR). Sisi vijana wa kizazi kipya tunawashauri wenzetu waulinde muungano kwa gharama yeyote na muungano huwa haupitwi na wakati. Tunajiuliza kwa wenzetu wa Ulaya na Marekani ambayo miungano yao imedumu kwa karne zaidi ya tano na sita. Je huko hakuna vijana wa vizazi vipya? Sisi tunaona kuwa wanaodai Utanganyika na Uzanzibari ni wakabila na wabaguzi wanaotaka kuturudisha enzi za ukoloni.

  • Tunamuomba Mwenyekiti wa Bunge Maalum azingatie kwamba Bunge Maalum la Katiba si la “UKAWA” ni la watanzania. Hivyo basi liendelee kwa kasi na ufanisi zaidi na lisiyumbishwe na hasira za wachache wanaojiita “UKAWA” kutokana na ukweli kwamba gharama, muda na nguvu  kubwa vimetumika mpaka sasa. Tunaomba bunge liendelee ili kuwapatia watanzania katiba iliyo bora.

  Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika

  Imetolewa na Gulatone Masiga, Mwanafunzi UDSM

  Kwa niaba vijana wazalendo wa Vyuo vya elimu ya juu Dar es Salaam


  0 0

   Wachezaji wa Timu ya Kokni Jamat ya Zanzibar wakiteremka kwenye boti wakitokea Dar es laam kwenye Bonanza la Pasaka ambapo wamefanikiwa kuchukuwa makombe  matatu ya mshindi wa kwanza katika michezo ya Play Station,  mpira wa meza na mpira wa miguu dhidi ya wenyeji wao. Aliebeba kombe kubwa ni Rais wa Jumuia ya Kokn Jamat ya Zanzibar Jeff Babu.
   Wachezaji wa Timu ya Kokni Jamat ya Zanzibar katika picha ya pamoja.
  Nahodha wa Timu ya Kokni Jamat Ibrahim Dalvi (kulia) na msaidizi wake Nabil Shamshuddin wakiwa wameshikilia kombe mara baada ya kuwasili Zanzibar.
  PICHA NA MAKAME MSHENGA-MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0


  0 0

  Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando akiongea kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius mara ya kupokea timu ya Airtel Rising Stars kutoka Sierra Leone ambao watahudhuria kliniki ya soka ya kimataifa ya Manchester United itayoanza Jumatano, 23-27 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
  Mchezaji Fatmata Mansaray wa timu ya Airtel Rising Stars chini ya miaka 17 kutoka Sierra Leone, akiongea na waandishi wa habari baada ya kufika Dar es Salaam kuhudhuria kliniki ya soka ya kimataifa ya Manchester United itayoanza Jumatano, 23-27 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
  Wachezaji wa Airel Rising Stars kutoka Sierra Leone wakiwasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuhudhuria kliniki ya soka ya kimataifa ya Manchester United itayoanza Jumatano, 23-27 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

  Wachezaji sita na kiongozi mmoja kutoka Sierra Leone waliwasili jijini Dar es Salaam jana asubuhi tayari kushiriki kliniki ya soka ya kimataifa ya siku tano itakayofanyika kwenye uwanja wa Azam Complex kuanzia kesho, Jumatano 23 Aprili, 2014. Washiriki kutoka Madagascar walitajiwa kutua jijini jana usiku.

  Kwa mujibu wa kuwasili kwa wachezaji, wengi wao wanatarajia kufika leo mchana na baadaye usiku kuhudhuria mafunzo hayo yanayoshirikisha zaidi ya wachezaji 72 kutoka nchi za Kenya, Uganda, Malawi, Sierra Leone, Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville, DRC, Niger, Madagascar, Gabon, Seychelles na mwenyeji – Tanzania.

  Wachezaji hao chipukizi, wasichana na wavulana, walijipatia tiketi ya kushiriki kliniki baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya Airtel Rising Stars kwenye nchi zao pamoja na timu zilizotwaa uchampioni wa mashindano ya kimataifa yaliyofanyika nchini Nigeria mwaka jana.

  Kliniki hii itaendeshwa na wakufunzi kutoka klabu maarufu duniani ya Manchester United ikiwa na lengo la kutoa mafunzo ya kuwawezesha wachezaji na kuwajengea uwezo wa kutandaza kabumbu ya kusisimua hasa katika idara ya ushambuliaji.

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe atakuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi inayotarajiwa kuhudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka wizara inayohusika na michezo, shirikisho la mpira wa miguu nchini, Airtel Tanzania na wadau wengine wa soka.

  Hii ni fursa nyingine muhimu kwa wachezaji hao chipukizi chini ya umri wa miaka 17 kuonyesha vipaji vyao na kujiendeleza kisoka. 

  Program ya Airtel Rising Stars ni mpango wa maendeleo ya soka kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 barani Afrika ukidhaminiwa na kampuni ya simu za kiganjaji ya Airtel na kuungwa mkono na Manchester United. Lengo lake ni kusaidia kuibua vipaji vya soka kutoka ngazi ya chini (grassroots) hadi Taifa.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  OFISI YA WAZIRI MKUU

  TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA


  MKOA WA RUKWA

  Anuani ya simu:”REGCOM”                          Simu Na:(025)-2802138/2802144

  Fax Na. (025) 2802217               OFISI YA MKUU WA MKOA,

       S.L.P. 128,

       SUMBAWANGA.

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella M. Manyanya (Mb) kwa masikitiko makubwa anapenda kuwajulisha juu msiba mkubwa ulioukumba Mkoa wetu wa Rukwa wa kuondokewa na Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mhe. Moshi Mussa Chang’a (62) aliyefariki jana jioni terehe 20 April, 2014 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa Shinikizo la Damu na Kisukari.


  Mwili wa Marehemu Mhe. Chang’a unategemewa kusafirishwa kesho jioni kutoka Jijini Dar es Saam hadi nyumbani kwao Mkoani Iringa ambapo mazishi yake yatafanyika keshokutwa siku ya Jumatano tarehe 23 April, 2014.


  Marehemu Mhe. Chang’a alizaliwa Mkoani Iringa Januari Mwaka 1952 na amewahi kushika nafasi mbalimbali Serikalini na katika Chama cha Mapinduzi (CCM). Katika nafasi ya Ukuu wa Wilaya amewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Mbeya, Tabora, Mkalama na Kalambo Mkoani Rukwa ambapo mauti yake yamemfika.


  Katika Ngazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) amewahi kuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Njombe na Iringa Vijijini na Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Iringa.


  Marehemu Mhe. Chang’a ameacha watoto watano (5) na Mjukuu Mmoja (1).Watoto wa kiume 3 na Wakike 2.

  Kwa niaba ya Wananchi wa Mkoa wa Rukwa tunatoa pole kwa ndugu, jamaa, marafiki, na wote walioguswa na msiba huu mkubwa. Tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.


  Sisi tulimpenda lakini Mungu kampenda zaidi.


  Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala pema peponi “AAAMIN”  Imetolewa na:


  OFISI YA MKUU WA MKOA

  RUKWA

  Tarehe 21 April, 2014.
  0 0
 • 04/22/14--01:30: Article 9


 • 0 0


  Karibu katika mazungumzo na Dr Patrick Nhigula kuhusu mwenendo wa Bunge Maalum la Katiba na mwenendo mzima wa nchi ya Tanzania.Huu ni mfululizo wa mazungumzo na watu mbalimbali kuhusu suala hili muhimu kwa mustakabali wa nchi ya Tanzania.
  Karibu
  Kwa maoni, tafadhali wasiliana nasi kwa barua pepe kwanzaproduction at gmail dot com

  0 0

  Ofisa utumishi Mkuu  Wilaya ya kinondoni  Bwana Godfrey Mugomi akikata utepe  kuashiaria  uzinduzi  wa Hoteli ya kisasa STAR CITY HOTEL iliyopo Afrikana sinza wanaoshudia ni Mkurugezi mkuu na mmiliki wa Hoteli hiyo Bwana Obadia Mtewele na Mkewe Joyce Msigwa hoteli hiyo ya kisasa inayo uwezo wa kupokea wageni  kutoka nnje ya nchi na ndani ya nchi.
    
   Muhudumu aliye fuzu katika kazi za Hoteli akiandaa vyombo kwa ajili ya wageni

  0 0

  Aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CHADEMA wilaya ya Mbeya,Bwa.Lucas Mwampiki.
  =======  ======  =======
  SIKU mbili baada ya aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CHADEMA Jiji la Mbeya Lucas Mwampiki kutangaza kujiuzulu wadhifa wake, chama hicho kimedai kuwa kilishamvua nafasi hiyo kabla hajatangaza kujiuzulu kutokana na kuvujisha siri za chama kwa upinzani.

  Mwampiki ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mwakibete alitangaza kujiuzulu nafasi ya Katibu Mwenezi kwa madai kuwa amekuwa akitengwa na baadhi ya viongozi wa chama katika shughuli mbalimbali za chama kwa nafasi yake kama mjumbe.

  Akitangaza uamuzi wa chama hicho dhidi ya Mwampiki, Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Mbeya mjini John Mwambigija alisema kuwa kikao cha kumvua uongozi Katibu Mwenezi huyo kiliketi April 14 baada ya kujiridhisha mwenendo wa utendaji wake na  yeye alitangaza kujiuzulu nafasi hiyo April 16.

  Alisema kuwa kufuatia hali hiyo uongozi wa chama wilaya kwa kuhusisha vikao halali vya chama umeridhia kumuengua katika nafasi yake ikiwa ni pamoja na kumzuia kutojihusisha na shughuli zozote za chama.

  Mwambigija alisema kuwa kiongozi  huyo wa juu wa chama alikiuka vifungu vya katiba ya chama kwa kusambaza taarifa za majungu na kutokuwa mkweli na muwazi ikiwa ni pamoja na kujihusisha na upotoshaji juu ya maamuzi halali ya chama.

  ‘’Tumeamua kwa kauli moja kumsimamisha shughuli zote za chama kwa mwaka mmoja,ataendelea na Udiwani wake, hatakiwi kufanya chochote kinachohusiana na chama chetu,akiendelea tutachukua uamuzi wa kumnyang’anya kadi na kumvua uanachama,’’alisema Mwambigija.

  Alifafanua kuwa miongoni mwa sababu zilizosababisha avuliwe wadhifa wake ni pamoja na kuvujisha siri za chama kwa wapinzani ikiwa ni pamoja na kutotoa ushirikiano katika harakati za chama za sasa za ‘Chadema ni Msingi’ na kwamba uamuzi waliouchukua uko katika sheria zinazolindwa na Katiba ya chama.

  Alisema kuwa kabla ya kuchukua uamuzi huo chama kilimuita kiongozi huyo katika vikao mara nne ambapo alishindwa kuhudhuria hivyo uamuzi waliouchukua una baraka za vikao halali vya chama na kuwa hata hivyo anayo nafasi ya kukata rufaa kwa ngazi za juu iwapo ataona kuwa hajatendewa haki dhidi ya uamuzi huo.

  Kwa upande wake Katibu Mwenezi aliyejiuzulu Mwampiki alisema kuwa aliamua kujiuzulu baada ya kuona hapewi ushirikiano na viongozi wenzake na kuwa mara nyingi alipokuwa akihoji mambo ya msingi ya kukiendeleza chama amekuwa akinyooshewa kidole kama msaliti.

  ‘’Nimeamua kujiuzulu mwenyewe bila kushinikizwa na mtu, kutokana na afya ya chama, kwa mujibu wa Katiba ya chama ya mwaka 2006 kifungu 6.3.4(a) hiki kinaainisha ukomo wa uongozi, nimetumikia chama kwa kila hali hadi rasilimali fedha, nitaendelea kuwa mwanachama mwaminifu,’’alisema Mwampiki.

  Aidha alisema kuwa hajawahi kuitwa na viongozi  wala kuandikiwa barua yoyote inayomtaka kufika ofisini ambayo kulingana na taratibu ilipaswa kumfikia ndani ya siku 14 na yeye kuweka saini yake hivyo uamuzi wowote uliochukuliwa dhidi yake ulipaswa kuzingatia taratibu hizo.

  ‘’Siwezi kuchukuliwa hatua bila maandishi ambayo yanapaswa kunifikia ndani ya siku 14, vinginevyo uamuzi wowote dhidi yangu mbali na kutamka kujiuzulu kwangu, haujafuata taratibu za kisheria,’’alisema Mwampiki.

  0 0

  Afisa Uhusiano Manispaa ya Ilala Bi. Tabu Shaibu akiwaeleza waandishi wa Habari (hawapo pichani)kuhusu mpango wa serikali wa kuendelea kuimarisha Masoko katika Jiji la Dar es Salaam, Wakati wa Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Masoko wa Manispaa hiyo Bw. Athuman Mbelwa.

  ======  ==== ======
  Na Frank  Mvungi- Maelezo

  Serikali yaimarisha masoko 18 katika jiji la Dar es salaam katika kukabiliana na Ongezeko la Mahitaji ya Wananchi. Hayo yamesemwa na Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala Bi Tabu Shaibu wakati wa mkutano nawaandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

  Akifafanua Bi Shaibu amesema masoko makubwa ni 5  ambayo ni Buguruni,Ilala,Ferry,Kisutu na Mchikichini ambapo jumla ya wafanyabiashara  wanaotumia masoko hayo ni 8,432. 
   

  Akieleza  zaidi Bi Shaibu alimesema kutokana na Utafiti uliofanywa na Ofisi ya Biashara ya Manispaa ya Ilala mwaka 2009,ilibainika kuwa jumla ya wafanyabishara 21,500 hawana maeneo ya kufanyia biashara na wanatumia hifadhi ya barabara na maeneo yasiyoruhusiwa kufanya biashara.


  Kutokana na hali hiyo Bi Shaibu alibainisha kuwa katika bajeti  ya 2013/2014 jumla ya sh.Milioni 240 zilitengwa kwa ajili ya ujenzi wa mabanda ya masoko ya Pugu ,Kigogo fresh,Kiwalani na Kinyerezi ambapo wakandarasi wameshaonyeshwa maeneo ya ujenzi  kwa njia ya zabuni.


  Katika hatua nyingine Bi shaibu alisema sh. Milioni 170 zimetumika kuboresha soko la Samaki feri kwa ajili ya ujenzi wa  zoni ya kukaangia samaki baada ya kuungua. Pia sh. Milioni 75 zilitumika. kuboresha mifereji ya maji taka,ukarabati wa meza 23 za kunadia samaki,kuzibua mitaro ya maji taka na maji ya mvua.

  Ni jukumu la wafanyabiashara wote kuzingatia usafi kwa kuhakikisha kuwa taka zinazozalishwa katika masoko yote zinahifadhiwa katika maeneo husika na kutunza mazingira ya maeneo ya masoko ili kuwalinda watumiaji wa huduma zinazotolewa katika maeneo hayo.

older | 1 | .... | 273 | 274 | (Page 275) | 276 | 277 | .... | 1897 | newer