Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 272 | 273 | (Page 274) | 275 | 276 | .... | 1897 | newer

  0 0  0 0


  0 0

   Wawakilishi wa Taasisi ya I,H,H,kutoka Uturuki wakigawa sadaka ya Unga,Mchele,Mafuta ya kupikia pamoja na Nyama kwa Watoto Yatima katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar.
   Wachinjaji mbuzi kwa ajili ya Sadaka kwa Watoto mayatima wakichinjaji mbuzi huko Kisauni nje ya Mji wa Zanzibar.
   Wawakilishi wa Taasisi ya I,H,H,kutoka Uturuki wakiendelea kugawa sadaka ya Vitu mbalimbali ikiwa pamoja na Unga wa Ngano,Mchele,Mafuta ya kupikia na Nyama kwa Watoto mayatima walio katika maeneo mbalimbali Zanzibar.
   Wawakilishi kutoka Taasisi ya I,H,H, ya Uturuki wakisalimiana na wanafunzi chekechea wa Skuli ya Muzdalifat mara baada ya kushuka kwenye gari huko Kisauni nje ya Mji wa Zanzibar.
  Jumuiya ya Kiislamu ya Muzdalifat(Muzdalifat Islamic Charitable)wakishirikiana na Taasisi ya I,H,H,kutoka uturuki,wakichuna mbuzi waliokwisha kuchinjwa kwa ajili ya sadaka kwa Watoto yatima hafla iliofanyika huko Kisauni nje ya Mji wa Zanzibar. 
  PICHA NA YUSSUF SIMAI - MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0
 • 04/18/14--08:26: Article 0

 • 0 0
 • 04/18/14--11:48: KAZI KWELI KWELI


 • 0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya maafisa na viongozi wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mjini Zanzibar leo jioni kwa ajili ya kufungua rasmi Kongamano la Muungano, linaloanza kesho katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort. Wa pili (kulia) ni mkewe Mama Zakia Bilal. Picha na OMR


  0 0

  Muumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Usharika wa Azania Front, Moses Kombe, (katikati) na wenzake wakiigiza igizo la kumbukumbu ya Kuwambwa Yesu Kristo miaka 2000 iliyopita wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika kanisa hilo Dar es Salaam leo.
  Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowasa akiwa katika ibada ya Ijumaa Kuu katika Kanisa la KKKT la Azania Front Dar es Salaam.
  Waumini wa Kanisa la Kiinjili Tanzania KKT, la Azania Front la Dar es Salaam wakiwa katika Ibada ya Ijumaa Kuu.
  Waumini wa Kanisa la Mtakatifu Joseph wakiwa kwenye ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika leo kanisani hapo.
  Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoriki, Mwadhama Polycap Kadinali Pengo akiubusu Msaraba wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam leo.
  Waumuni wa Kanisa la Mtakatif Joseph Jimbo Kuu la Dar es Salaam wakiwa wanaubusu Msaraba wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
  Mtoto, Vanes Mpupua akiubusu Msaraba wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu katika Kanisa la Mtakatif Josef Dar es Salaam.
  Mmoja wa Watoto waliofika katika Kanisa la Mtakatif Josef akiubusu Msaraba wakati wa Ibada ya Ijumaa Kuu iliofanyika Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON  

  0 0

  Rais Msaafu wa awamu ya pili Ali Hassani Mwinyi akikabidhiwa nyaraka na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chach,zenye ujumbe wa shughuli zinazofanywa na Mamlaka hiyo wakati alipotembelea katika banda la Mamlaka hiyo kujionea shughuli zinazofanywa na Mamlaka katika Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
  Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassani Mwinyi akimsikiliza kwa makini Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chacha wakati alipotembelea katika banda la Mamlaka hiyo katika Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano yanayoendelea katika Viwanja vya  Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. 

  0 0


  Na Andrew Chale
   
  MPIGA gitaa wa bendi ya Skylight, aliyefariki April 17i katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, Chiri Challa, amezikwa katika makaburi ya Mwananyamala kwa Kopa, Kinondoni April 18. Akizungumza  kwa simu , mdau wa bendi hiyo, Zainul Mzige ‘Bigzee’, alisema marehemu Chiri alizikwa majira ya saa tisa alasiri na mazishi yake kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.

  Awali uongozi wa bendi hiyo kupitia kwa Meneja wake, Aneth Kushaba ‘AK47’, ulieleza kuwa mwanamuziki huyo alifariki kutokana na ugonjwa wa kupooza nusu ya mwili wake, hali iliyosababisha kutofanya kazi ipasavyo.
  Kushaba alibainisha kuwa kupooza huko kulisababisha mishipa ya damu kichwani kupasuka na kumsababishia maumivu makali sehemu za kichwani. “Tunatoa pole kwa familia ya marehemu na mashabiki wetu wote katika kipindi hiki kigumu cha msiba wa mpendwa wetu,” alisema Kushaba.

  0 0

   Airtel Public Relations Manager Jackson Mbando speaks to the media at a press conference to announce the forthcoming Manchester United International Soccer Clinic to be held in Dar es Salaam from 23rd-27thApril under the tutelage of coaches from Manchester United Soccer Schools.  He is flanked by the Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi .The event was held at the Airtel Tanzania Headquarters, 18th April 2014. 
   Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi speaks to the media at a press conference to announce the forthcoming Manchester United International Soccer Clinic to be held in Dar es Salaam from 23rd-27th April under the tutelage of coaches from Manchester United Soccer Schools.  He is flanked by Airtel Public Relations Manager Jackson Mbando.The event was held at the Airtel Tanzania Headquarters, 18th April 2014.

  ========  =======  ========
  Washiriki wa kliniki ya Airtel Rising Stars kutua Dar Jumatatu

  ·      Ni kutoka nchi 12 Afrika

  ·      Waziri Bernard Membe mgeni rasmi siku ya ufunguzi

  ·      Kliniki kuendeshwa na makocha kutoka Manchester United


  Dar es Salaam, Ijumaa 18Aprili, 2014.  Wachezaji wa soka chini ya umri wa miaka 17 kutoka nchi 12 barani Afrika wanatarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam Jumatatu Aprili 21 kushiriki kliniki ya soka ya kimataifa.  Hii ni mara ya pili Tanzania imepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa kliniki ya kimataifa baada ya ile iliyofanyika kwenye uwanja wa wa kisasa wa Taifa mwaka 2011.


  Kliniki ya mwaka huu itakayofanyika kwenye uwanja wa Azam, Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam inakutanisha wachezaji chipukizi, wasichana na wavulana, kutoka nchi za Kenya, Uganda, Malawi, Sierra Leone, Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville, DRC, Niger, Madagascar, Gabon, Seychelles na mwenyeji – Tanzania. Mafunzo hayo ya siku tano mfululizo chini ya makocha wazoefu kutoka klabu maarufu duniani ya Manchester United yana lengo la kuwapa vijana mbinu mbalimbali za kisoka hasa katika eneo la ushambuliaji.

  Kliniki hii ya kimataifa inashirikisha vijana waliofanya vizuri mwaka jana katika mashindano ya Airtel Rising Stars kwenye nchi zao pamoja na washindi wa mashindano ya kimataifa yaliyofanyika nchini Nigeria ambapo timu ya wasichana ya Tanzania ilitwaa uchampioni wa fainali hizo hizo.


  Hafla ya uzinduzi wa kliniki hiyo imepangwa kufanyika siku ya Jumatano kwenye uwanja wa Azam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe atakuwa mgeni rasmi.  Membe anatarajiwa kuwahamasisha vijana kujituma ili kuweza kuendeleza ipasavyo vipaji vyao vya soka.


  Hafla hiyo ya uzinduzi pia inatarajiwa kuhudhuriwa na mabalozi kutoka nchi zinazoshiriki kwenye kliniki hiyo itakayojumuisha mafunzo ya uwanjani na ya darasani. Vipindi vyote hivyo vitafanyika pale pale Azam Complex.


  Program ya Airtel Rising Stars ni mpango wa maendeleo ya soka kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 barani Afrika ukidhaminiwa na kampuni ya simu za kiganjaji ya Airtel na kuungwa mkono na Manchester United. Lengo lake ni kusaidia kuibua vipaji vya soka kutoka ngazi ya chini (grassroots) hadi Taifa. 


  0 0

  Misa ya Sima na Gavana Joho in Voa 078Kutoka kushoto Seneta wa County ya Monmbasa Hassan Omar , Mtangazaji wa VOA Abdushakur Aboud , Gavana wa Mombasa County Ali Joho na waziri wa Vijana , Jinsia na Michezo wa County hiyo Hazel Koitabawalipotembelea kipindi maarufu cha "LIVE TALK " idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika-VOA Ijumaa Aprili 18,2014.Misa ya Sima na Gavana Joho in Voa 105Kutoka kushoto Waziri wa Vijana , Jinsia na Michezo katika County ya Mombasa, Katibu wa County Hamisi Mwaguya,Barbara Aron, Chanzera, mtangazaji wa VOA Aida Issa na Tuni Mwalukumbi msimamizi mwa utawala County. Misa ya Sima na Gavana Joho in Voa 097Kutoka kushoto Abdushakur Aboud, Mkuu wa idhaa ya Kiswahili Mwamoyo Hamza , Gavana wa Mombasa Ali Joho , Sunday Shomari,Seneta wa Mombasa County Hassan Omar, waziri wa County wa Vijana , Jinsia na Michezo Hazel Koitaba na katibu wa County Hassan Mwaguya. Kusikiliza kipindi hiki fuata link hii .

  http://www.voaswahili.com/archive/jioni/latest/2948/2948.html na kwa picha zaidi ungana na Sunday Shomari.com

  0 0

  Bondia Sukkasem Kietyongyuth  kutoka Thailand kulia akitunishiana misuli na Fransic Miyeyusho baada ya kupima uzito leo kwa ajili ya mpambano wao wa Jumamosi ya leo April 19 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam.
  Bondia Sukkasem Kietyongyuth  kutoka Thailand kulia akitunishiana misuli kwa mkono na Fransic Miyeyusho baada ya kupima uzito leo kwa ajili ya mpambano wao wa Jumamosi ya leo April 19 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam 
  Bondia Sukkasem Kietyongyuth  kutoka Thailand kulia wakipeana salamu ya heshima na Fransic Miyeyusho baada ya kupima uzito leo kwa ajili ya mpambano wao wa Jumamosi ya leo April 19 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Mkufunzi wa mazoezi ya viungo, Taifa Liwewa (Kushoto), akiwaongoza wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakati wa mazoezi ya viungo, kwenye bonanza la michezo lililoandaliwa na Mfuko huo na kufanyika viwanja vya Ustawi wa Jamii, Kijitonyama jijini Dar es Salaam Jumamosi Aprili 19, 2014. Mgeni rasmi kqwenye tamasha hilo lililoshirikisha michezo mbalimbali ikiwemo, kuvuta kamba na soka, alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, akikagua timu za soka za Mfuko huo, wakati wa Bonanza hilo.
  Timu ya wanawake ya kuvuta kamba ya Mfuko wa Pesnheni wa PPF, ikizidiwa nguvu na wenzao wanaume kwenye mchezo wa kuvuta kamba. Hata hivyo timu hiyo ilijitutumua kwani katika raundi ntatu, ilishinda kwa taaabu raundi moja.
  Mchezaji wa soka wa timu ya PPF, kutoka idara ya Utawala, Johnson Aloyce (Kushoto), akichanja mbuga, wakati wa pambano la soka dhidi ya Idara ya kuzuia Majanga.
  Meneja Uhusiano nna Masoko ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele (Katikati), akiwa sambamba na wafganyakazi wenzake, wakati wa mazoezi ya viungo.


  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea zawadi ya kinyago cha umoja kutoka kwa Naibu Waziri , Ofisi ya Makau wa Rais, Umy Mwalimu baada ya kufunga monyesho ya Taasisi za Muungano kwenye viwanja vya Mnazi Moja jijini dar es salaam Aprili 19, 2014. Kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha, Mwiguli Nchemba na kulia kwake Ni Kati Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Florens Turuka. (Picha na Ofisi ya Wairi Mkuu) 

  0 0

   Mshiriki wa Tanzania Movie Talents akihojiwa mara baada ya kumaliza usaili katika Shindano la Tanzania Movie Talents linaloendelea muda huu katika Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo Soko Matola Mkoani Mbeya
   
  Baadhi ya washiriki waliojitokeza kwaajili ya kuhudhuria usaili wa Shindano la Tanzania Movie Talents wakijadiliana jambo kabla ya kuanza kwa usaili.
   
   Washiriki waliojitokeza kwaajili ya kushiriki mashindano yya Tanzania Movie Talents wakijaza fomu kwaajili ya usaili wa shindano la Tanzania Movie Talents linaloendelea Mkoani Mbeya ikiwa unawakilisha Kanda ya Nyanda za Juu Kusini
   Baadhi ya washiriki kutoka Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mkoani Mbeya wakisubiri shindano la Tanzania Movie Talents kuanza.
  Kundi la Kwanza La vijana waliojitokeza kwaajili ya usaili wa Shindano la Tanzania Movie Talents linaloendelea mkoani Mbeya muda huu.Picha na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Mbeya
  Hatimaye Shindano la Tanzania Movie Talents limeanza rasmi leo katika Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ambapo usaili huo unafanyika Mkoani Mbeya Katika Ukumbi wa Benjamini Mkapa uliopo Soko Matola Mkoani Mbeya.

  Mpaka sasa Washiriki wapatao 150 wamejitokeza kwaajili ya kushiriki shindano hili la Tanzania Movie Talents ambapo washindi watatu kutoka kanda ya Nyanda za Juu Kusini watazawadiwa kitita cha Shilingi laki tano za Kitanzania na Baadae kupewa Tiketi ya Kuelekea Mkoani Dar Es Salaam kwaajili ya kushiriki fainali itakayowakutanisha Washindi waliopatikana katika Kanda ya Ziwa, Kati na kanda zilizobakia za Pwani na Kaskazini na mshindi katika fainali hiyo atajinyakulia Kitita Cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania pamoja na Mikataba minono kutoka Kampuni ya Proin Promotions Limited na washindi kumi katika fainali hizo watakuwa chini ya kampuni ya Proin Promotions Limited na kuweza kutengeneza filamu ya Pamoja ambapo watanufaika na Mauzo ya filamu yao.
  Mashindano ya Tanzania Movie Talents yataendelea Mkoani Mbeya kwa Siku nne ambapo siku ya jumanne washindi wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini watapatikana na kupewa Zawadi zao.

  0 0
 • 04/19/14--09:30: Article 9
 •  Mshiriki wa Tanzania Movie Talents akihojiwa mara baada ya kumaliza usaili katika Shindano la Tanzania Movie Talents linaloendelea muda huu katika Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo Soko Matola Mkoani Mbeya
   
  Baadhi ya washiriki waliojitokeza kwaajili ya kuhudhuria usaili wa Shindano la Tanzania Movie Talents wakijadiliana jambo kabla ya kuanza kwa usaili.
   
   Washiriki waliojitokeza kwaajili ya kushiriki mashindano yya Tanzania Movie Talents wakijaza fomu kwaajili ya usaili wa shindano la Tanzania Movie Talents linaloendelea Mkoani Mbeya ikiwa unawakilisha Kanda ya Nyanda za Juu Kusini
   Baadhi ya washiriki kutoka Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mkoani Mbeya wakisubiri shindano la Tanzania Movie Talents kuanza.
  Kundi la Kwanza La vijana waliojitokeza kwaajili ya usaili wa Shindano la Tanzania Movie Talents linaloendelea mkoani Mbeya muda huu.Picha na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Mbeya
  Hatimaye Shindano la Tanzania Movie Talents limeanza rasmi leo katika Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ambapo usaili huo unafanyika Mkoani Mbeya Katika Ukumbi wa Benjamini Mkapa uliopo Soko Matola Mkoani Mbeya.
  Mpaka sasa Washiriki wapatao 150 wamejitokeza kwaajili ya kushiriki shindano hili la Tanzania Movie Talents ambapo washindi watatu kutoka kanda ya Nyanda za Juu Kusini watazawadiwa kitita cha Shilingi laki tano za Kitanzania na Baadae kupewa Tiketi ya Kuelekea Mkoani Dar Es Salaam kwaajili ya kushiriki fainali itakayowakutanisha Washindi waliopatikana katika Kanda ya Ziwa, Kati na kanda zilizobakia za Pwani na Kaskazini na mshindi katika fainali hiyo atajinyakulia Kitita Cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania pamoja na Mikataba minono kutoka Kampuni ya Proin Promotions Limited na washindi kumi katika fainali hizo watakuwa chini ya kampuni ya Proin Promotions Limited na kuweza kutengeneza filamu ya Pamoja ambapo watanufaika na Mauzo ya filamu yao.
  Mashindano ya Tanzania Movie Talents yataendelea Mkoani Mbeya kwa Siku nne ambapo siku ya jumanne washindi wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini watapatikana na kupewa Zawadi zao.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Muungano katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar leo Aprili 19, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanoa, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, (Muungano) Samia Suluhu, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Muungano lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar leo Aprili 19, 2014.
  Viongozi waliohudhuria Kongamano hilo, wakiwa meza kuu. Wa pili (kulia) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa kwanza kushoto) Makamu wa pili wa Rais wa Zanznibar, Balozi Seif Iddi, (wa pili kushoto) ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) na (kulia) ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais, Mohamed Aboud.


  0 0

  Na Andrew Chale
   
  WAPENZI wa nyimbo za zamani za taarabu asilia nchini, jumapili hii ya Aprili 20, ya Pasaka.. wanatarajiwa kupata burudani safi na zawadi nyingi zitakazotolewa na Fabak Fashion ndani ya ukumbi wa  Regency Hotel, Mikocheni, jijini Dar es Salaam.

  Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin, miongoni mwa wadhamini wa onesho hilo, amewaomba wadau kujitokeza kwa wingi kufurahia usiku huo kwa kukumbushiana enzi sambamba na zawadi lukuki zitakazotolewa kwa njia ya bahati nasibu.

  Asia Idarous alisema onesho hilo la kila Jumapili,  usiku huo wa ‘Old is Gold na Spice Modern Taarab,’  pia watafurahia pamoja na wadau katika kusherehekea Pasaka, ambapo  wasanii nguli waalikwa watakuwamo.

  “Jumapili hii ndani ya Old is Gold, pia wasanii Mwanahawa Ally na Rukia Ramadhan, watakuwapo kuwasindikiza  Spice Modern taarab, hivyo shamrashamra kuwa kubwa zaidi,” alisema Asia Idarous.

  Kuhusu kiingilio, alisema kitakuwa sh 5,000 tu,  watafurahia burudani hiyo ya aina yake zikiwemo nyimbo za mwambao hasa zile zilizokuwa zikipendwa, kuanzia saa 12 jioni hadi saa sita usiku sambamba na kuchezesha bahati nasibu na kugawa zawadi kutoka Fabak Fashion.

  Asia Idarous alizitaja baadhi ya nyimbo wanazotamba nazo wasanii  hao waalikwa ni ‘Nikumbatie’ wa Rukia Ramadhan  na ‘Usiku wa Awali’ wa Mwanahawa  Ally.

  Wadhamini wengine katika usiku huo wa taarabu asilia ni Times FM, Regency Park Hotel na Fabak Fashions.

  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha la Pasaka, Alex Msama akipeana mkono na mwimbaji wa kimataifa wa nyimbo za injili kutoka Afrika ya Kusini, Kekeletso Phoofolo mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo, kwa ajili ya tamasha la Pasaka litakaloanza kutimua vumbi kwenye Uwanja wa taifa leo. 
  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama (kulia), akiwa na mwimbaji wa Kimataifa wa nyimbo za injili kutoka Afrika ya Kusini, Kekeletso Phoofolo mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam leo, kwa ajili ya tamasha la Pasaka litakaloanza kutimua vumbi kwenye Uwanja wa taifa Jumapili. 
  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha la Pasaka, Alex Msama akipeana mkono na mwimbaji wa kimataifa wa nyimbo za injili kutoka Afrika ya Kusini, Kekeletso Phoofolo mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimatifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya tamasha la Pasaka litakaloanza kutimua vumbi Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa.  
  Mwimbaji wa kimataifa wa nyimbo za injili kutoka Afrika Kusini, Kekeletso Phoofolo (kushoto), akiimba kwa hisia moja ya nyimbo zake mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya tamasha la Pasaka.
   Kekeletso Phoofolo akisalimiana na mke wa Msama.
   Kekeletso Phoofolo akisalimiana na mke wa Msama.
   Mwimbaji wa Kimataifa kutoka Afrika Kusini, Keke Letso Phoofolo (wa pili kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promosheni, Alex Msama (kulia).
    Mwimbaji wa Kimataifa kutoka Afrika Kusini, Keke Letso Phoofolo akiwa katika picha ya pamoja na waimbaji wake pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msam,a Promosheni, Alex Msama (kulia).
  Waimbaji wa nyimbo za injili wakiwa katika picha ya pamoja pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promosheni, Alex Msama. (wa nne kulia).
   Mwimbaji wa kimataifa wa nyimbo za injili kutoka Afrika Kusini, Kekeletso Phoofolo (kushoto), akiimba kwa hisia moja ya nyimbo zake mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya tamasha la Pasaka.
  Baadhi ya waimbaji wakiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kiamataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

  0 0

  Balozi wa Urusi anayefanyakazi hapa nchini  Alexander Rannikh  akiwa  na waumini wenzake wakipewa Baraka na Askofu  wa Dhehebu ya Orthodox  Askofu Dimitrios  wakati wa   Ibada ya Kusherehekea Sikukuu ya Pasaka iliyowashirikisha  Waumini mbalimbali  wakiwemo Watanzania,Wagiriki na Warusi.Ibada hiyo iliafanyika jijini Dar es Salaam.

  Balozi wa Urusi anayefanyakazi hapa nchini  Alexander Rannikh akipewa Baraka na Askofu  wa Dhehebu ya Orthodox  Askofu Dimitrios  wakati wa   Ibada ya Kusherehekea Sikukuu ya Pasaka  iliyowashirikisha  Waumini mbalimbali wakiwemo Watanzania,Wagiriki na Warusi.Ibada hiyo iliafanyika jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa Urusi anayefanyakazi hapa nchini  Alexander Rannikh, akiteta jambo na Askofu Mkuu wa Dhehebu ya Orthodox  Askofu Dimitrios baada ya kumalizika kwa Ibada ya Kusherehekea Sikukuu ya Pasaka  iliyowashirikisha  Waumini mbalimbali  wakiwemo Watanzania,Wagiriki na Warusi.Ibada hiyo iliafanyika jijini Dar es Salaam
  Balozi wa Urusi anayefanyakazi hapa nchini  Alexander Rannikh  akiwa  na waumini wenzake wakipewa Baraka na Askofu  wa Dhehebu ya Orthodox  Askofu Dimitrios  wakati wa   Ibada ya Kusherehekea Sikukuu ya Pasaka iliyowashirikisha  Waumini mbalimbali  wakiwemo Watanzania,Wagiriki na Warusi.Ibada hiyo iliafanyika jijini Dar es Salaam.


  Baadhi ya Waumimi wa Dhehebu ya Orthodox  wakiwa katika Ibada ya kusherehekea  ufufuko wa Yesu Kristu (Pasaka) iliyofanyika katika Kanisa hilo lililpo eneo la Red Cross jijini Dar es Salaam. Picha na Albart Jackson 


older | 1 | .... | 272 | 273 | (Page 274) | 275 | 276 | .... | 1897 | newer