Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 271 | 272 | (Page 273) | 274 | 275 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Jengo la maabara linalojengwa katika Shule ya Sekondari ya Mtapenda, katika Halmashauri ya Nsimbo, mkoani Katavi
   Katibu Mkuu wa CCM,Kinana akishiriki ujenzi wa mradi wa usambazaji wa maji kwa wananchi alipokagua mradi wa maji uliojengwa kwa sh. mil. 400 katika Kijiji cha Mwenge mkoani Katavi.
   Katbu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisaidia kujenga jengo la maabara ya Shule ya Sekondari ya Mtapenda, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM.
   Kinana akipanda mti katika Shule ya Sekondari ya Mtapenda, Halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi
   Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akisaidia kufyatua matofali ya kujengea Ofisi ya CCM ya Wilaya ya Mlele, mjini Inyonga-
   Kinana akimwagilia maji matofali ya kujengea ofisi hiyo
   Kinana akiangalia maendeleo ya ujenzi wa tanki la maji katika Kijiji cha Mwenge, Halmashauri ya Nsimbo, mkoani Katavi-
   Nape akizungumza na baadhi ya wanachama wa Shina namba 4 katika Kijiji cha Songambele, Nsimbo
   Kinana akisalimiana na watumishi wa Kituo cha Afya cha Inyonga, wakati wa ziara yake wilayani Mlele.
   Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Inyonga, Dk. Adis Koni akimpatia maelezo Kinana na viongozi wengine wa chama na serikali kuhusu kucheleweshwa kwa makusudi kituo hicho kukipa hadhi ya kuwa hospitali ya wilaya. Ucheleweshwaji huo unafanywa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
  Kinana akioneshwa baadhi ya vifaa tiba vya kisasa vilivyotolewa msaada na Mbunge wa Jimbo la Katavi, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda 
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Inyonga,wilayani Mlele mkoani Katavi mapema jioni ya leo. 

  0 0

  Berlin,Ujerumani,
  Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU) unatarajia kufanya mkutano wake mkuu  wa uchaguzi siku ya kilele cha sherehe za muunganno wa Tanzania mjini Berlin, Ujerumani. siku ya tarehe 26.April.2014 kuanzia saa 7 mchana katika ukumbi wa Deutsche Bank, Unter den Linden 13-15, 10117 Berlin, Ujerumani.

  Agenda za Mkutano  

  1 Uchaguzi wa Viongozi
  2 Kuipitisha Katiba Mpya

  Kwenye Attachments nimeweka Katiba ya zamani, na katiba mpya  Satzung  na satzungentwürf tafadhali pitia  katiba hizi ili tuone mabadiliko hayo ili kuepuka kutumia muda mwingi katika kujadili.

  Watanzania wote wanaoishi Ujerumani wanaombwa kuhudhuria kwa wingi katika mkutano huu muhimu wa chombo chao UTU ambao kinawaunganisha watanzania wote waishio ujerumani bila kujali itikadi zao za kidini, jinsia, wala kabila.

  Umoja wa watanzania ujerumani unafuraha kubwa ya kuwafungilia milango wale wote ambao wanataka kujiunga na umoja huo.

  KUFIKA KWENU KATIKA MKUTANO HUU NDIO MAFANIKIO YA WATANZANIA WOTE

  UMOJA NI NGUVU , UTENGANO NI UDHAIFU

  UMOJA WA KITAIFA NDIO MSINGI IMARA KWA WATANZANIA
  MUNGU IBARIKI TANZANI


  Kwa maelezo zaidi wasiliana simu :    +491737363422
  Email. kamati.utu@googlemail.com

  0 0


  0 0


  0 0

  Exim Bank Chief Executive Officer Mr. Dinesh Arora (left) in a group photo together with the bank's long serving staff during an internal strategic meeting held in Dar es Salaam at the weekend.
  ==========  ========  ==========
  EXIM Bank has embarked on implementing its Vision 2016 that seeks to double the balance sheet and increase its market share in deposits by 2016.

  Being the sixth largest bank in Tanzania in terms of total deposits and assets, Exim bank has set its eyes on an ambitious target for the year 2016. The management team has worked upon the Vision 2016 for the bank and it has started to cascade this Vision 2016 to all its employees.

  Speaking during the bank’s internal strategic meeting for cascading Vision 2016 held in Dar es Salaam recently, Exim Bank Chief Executive Officer, Mr. Dinesh Arora said that EXIM bank sees immense opportunities in the country and hence have put in lot of enablers, strengthened its team to achieve our ambitious goal of Vision 2016.

  “We will continue with our quest into becoming the most preferred and innovative bank in the country. This achievement can only be realized if we continue being the most customer-focused bank in Tanzania by offering the best quality services and products that will go beyond and above our customers’ expectations.

  “Based on our motto ‘Innovation is Life’, we will keep on investing in new banking technologies to better our banking services. We as Exim Bank Tanzania are committed to providing our esteemed customers with a great everyday banking service,” he stressed.

  Adding further, Mr Arora mentioned that “‘Faster turnaround’ has been our USP; blended with the best in class technology platform and processes, we wish to surprise our customers with an exceptional experience of banking service.”

  All the 374 employees of the bank’s head office and branches in Dar-es-Salaam participated enthusiastically in the event braving the rains and inclement weather.

  It was a very interactive session with presentations by all head of departments and participation of all the employees. The bank also recognized its employees for their longevity by giving out the Long Service awards on the occasion.

  0 0

  MUSA DRIVER 001
  Kampuni ya MOHAMMED ENTERPRISES (T) LTD inautangazia umma kutoweka Mfanyakazi MUSA SAID (Pichani) aliyekuwa Dereva wa 21st CENTURY TEXTILES MOROGORO kwa kupeleka kusikojulikana mzigo wa Vitenge na kisha kutelekeza gari lenye namba za usajili T 128 CVJ katika bohari kuu (Main Godown) ya Dar es Salaam kampuni ya MOHAMMED ENTERPRISES (T) LTD.

  Tumeshafungua Jalada CB/RB/4869/2014 na CB/IR/1540/2014.
  Zawadi nono itatolewa kwa yeyote atakayefanikisha kupatikana kwake.
  Kwa taarifa za kupatikana kwake piga simu Na. 022 2118930 au 022 2112756; 0755 030 014 au 0784 783 228; au toa taarifa kituo chochote cha polisi kilicho karibu na wewe.

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya Kashaulili, mjini Mpanda leo, baada ya kuhitimisha ziara ya siku 21ya kikazi ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM katika mikoa ya Rukwa, Kigoma na Katavi.


  Baadhi ya Wanachama wa CCM na wananchi wakishangilia jambo wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndug Kinana alipokuwa akiwahutubia wakazi wa mji wa Mpanda jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Kashaulili mjini Mpanda mkoani Katavi.
  Mjumbe wa NEC Taifa,Balozi Ali Karume akiwahutubia wakazi wa Mpanda mjini mapema leo mkoani Katavi,wakati wa kufunga ziara ya Siku nne ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mkoani humo.Balozi Karume aliwasisitizia wananchi hao kuwa na umoja na mshikamano katika suala zima la kuutetea Muungano,Karume akaongeza zaidi kuwa Wananchi wanahitaji Serikali mbili  na si tatu kama amabvyo wengine wamekuwa wakidai.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrhaman Kinana akipanda juu ya tanki alipokwenda kukagua mradi wa maji wa Ikolongo, eneo la Kazima, mjini Mpanda, Katavi leo.

  Mjumbe wa NEC-CCM kutoka Zanzibar, Balozi Ali Abeid Karume (aliyevaa kofia) akipanda juu ya tanki kukagua mradi wa maji wa Ikolongo, mjini Mpanda leo
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrhaman Kinana akishuka juu ya tanki alipokwenda kukagua mradi wa maji wa Ikolongo, eneo la Kazima, mjini Mpanda, Katavi leo. 
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata maelezo mafupi kuhusiana mradi wa eneo la kuweka tanki la maji katika  eneo la Kazima, mjini Mpanda, Katavi leo.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisaidia kutandaza mabomba katika mradi wa maji wa Ikolongo, eneo la Kazima, Kata ya Kawajense, Mpanda Mjini, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM katika Mkoa mpya wa Katavi. Kinana amehitimisha leo ziara ya kikazi ya siku 21 katika mikoa ya Rukwa, Kigoma na Katavi.

  Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa amejumuika na wajumbe wa shina namba 32,tawi la Makanyagio Mpanda Mjini,wakati Kinana alipokwenda kumtembelea Balozi wa shina
  Balozi wa Shina namba 32, tawi la Makanyagiao,Balozi Thobiasi Kazimzuri akitoa taarifa fupi ya mambo mbalimbali ya shina lake kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokwenda kumtembelea jioni ya leo.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wajumbe wa shina na 32,katika tawi la  mtaa wa Makanyagio kwa balozi Thobiasi Kazimzuri,Mpanda mjini.
  Waendesha Boda Boda wakiongoza msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake walipokuwa wakielekea kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa Kashaulili mjini Mpanda mkoani Katavi.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Mabalozi ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi na Mabalozi wastaafu kwa mujibu wa sheria.
  Mabalozi wateule na aliyehamishwa kituo ni kama ifuatavyo:


  1. Balozi Dora Mmari Msechu (kushioto); ameteuliwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Stockholm, Sweden. Hadi uteuzi huu unafanyika Balozi Dora Mmari Msechu ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Anachukua nafasi ya Balozi Mohamed M .H. Mzale ambaye amestaafu.  2. Lt. Gen. Wynjones Matthew Kisamba (kulia), ameteuliwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Moscow, Urusi. Hadi uteuzi huu unafanyika, Lt. Gen. Wynjones Matthew Kisamba alikuwa Mkuu wa Utendaji Kivita na Mafunzo, Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Anachukua nafasi ya Balozi Jaka Mwambi.  3. Kadhalika, Mheshimiwa Rais amemteua Ndugu Joseph Edward Sokoine  (kushoto) kuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Kabla ya uteuzi huu, Bw. Sokoine alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu na Mkuu wa Utawala katika Ubalozi wa Tanzania, Ottawa, Canada.                 Umetolewa na:

  (John M. Haule)
  KATIBU MKUU,
  WIZARA YA MAMBO YA NJE
  NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
  DAR ES SALAAM.


  0 0


  NDUGU ZANGU,

  MJENGWABLOG HAIKO HEWANI TANGU JANA SAA TATU USIKU. NI KUTOKANA NA MATATIZO YA KIUFUNDI KWENYE DATA CENTRE NCHINI MAREKANI ZINAKOHIFADHIWA.

  WAHUSIKA WALIOKO KWENYE DATA CENTRE WANAFANYA KAZI KATIKA KILA DAKIKA KUHAKIKISHA HITILAFU HIYO INAREKEBISHWA HARAKA IWEZEKANAVYO.

  KWA SASA UNAWEZA KUENDELEA KUTUPATA KWENYE URSTREAM KWANZAJAMII RADIO, WEBSITE KWANZAJAMII.COM, FACEBOOK: KWANZAJAMII RADIO FANS

  POLENI SANA KWA USUMBUFU NA TUNAWASHUKURU KWA KUENDELEA KUTUAMINI,

  MAGGID MJENGWA,
  MWENYEKITI MTENDAJI
  IKOLOMEDIA- MJENGWABLOG/KWANZAJAMII.

  0 0

  10173726_10152036323227864_1413106576404088176_n

  Mpiga Gitaa wa Skylight Band maarufu kwa jina la Chiri Challa(pichani) amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia April 17 katika Hospitali ya Muhimbili.
  Taarifa za awali zimethibitishwa na uogonzi wa bendi hiyo kuwa mpiga gitaa huyo machachari amefariki baada ya kuugua kwa siku mbili ugonjwa wa kupooza nusu ya mwili wake na kuepelekea kutofanya kazi ipasavyo.
  Kwa mujibu wa Meneja wa bendi hiyo Aneth Kushaba AK47 Ugonjwa wa kupooza ulipelekea mishipa ya damu kichwani kupasuka hivyo na kumsababishia maumivu makali sehemu kichwani.
  10268531_10152035773597864_7736400417218686840_n
  Kutokana na msiba huo uongozi unapenda kutoa taarifa kuwa Show ya Escape One iliyokuwa ifanyike Alhamis ya April 17 imeahirishwa hata hivyo uongozi unasikitika kumpoteza msanii huyo ambaye alikuwa ni kiungo muhimu wa bendi na inaungana na familia ya marehemu Chiri Challa kuomboleza kifo cha mpendwa wao na inatoa pole kwa familia na mashabiki wa Skylight Band na wapo bega kwa bega katika kipindi hiki kigumu.
  Msiba na shughuli za mazishi zinafanyika maeneo ya Mwanyamala Ujiji mtaa wa Mpunga.
  Kwa mawasiliano zaidi namba ya Meneja wa Bendi +255 715 677 499.

  0 0


    Meneja wa Bia ya Serengeti Rugambo Rodney (katikati) akiongea
  na waandishi wa habari wakati akitangaza washindi wa droo ya winda safari ya 
  Brazil na Serengeti iliyofanyika kiwandani Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni 
  ofisa kutoka PWC Bi Golder Kamuzora (Kulia) na afisa mkaguzi kutoka bodi ya 
  michezo ya kubahatisha Bw. Humudi Abdulhussein (Kushoto)
  Meneja wa Bia Serengeti Rugambo Rodney (kulia) akiongea na
  mmoja wa washindi wa droo ya 10 ya winda safari ya Brazil kwa njia ya simu 
  huku akishuhudiwa na mkaguzi kutoka Bodi ya michezo ya kubahatisha Bw Humudi 
  Abdulhussein (kuhoto), wakati wa kuchezesha droo ya 10 ya winda safari ya 
  Brazil na Serengeti iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akitoa maelezo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kabla ya kumkabidhi Tuzo ya Heshima ya Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa ziadi katika Maendeleo Barani Afrika kwa mwaka 2013 aliyoipokea kwa niaba ya Mhe. Rais Kikwete tarehe 9 Aprili, 2014 Jijini Washington D.C, Marekani. Heshima hiyo kwa Rais Kikwete ilitolewa na Jarida Maarufu la Kimataifa la African Leadership Magazine Group.
  Mhe. Membe akimkabidhi rasmi Mhe. Rais Kikwete Tuzo yake. 
  Mhe. Rais Kikwete akionesha Tuzo hiyo mara baada ya kuipokea kutoka kwa Mhe. Membe.  Picha na Reginald Phillip.

  0 0
 • 04/17/14--13:28: MBEYA ZAMU YENU SASA IMEFIKA

 • 0 0

  Kutoka kushoto: Wasanii Dk. Cheni, Bi. Mwenda, Profesa Jay na Wema Sepetu wakishiriki kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa GlobaL TV Online jana.
  Wema Sepetu na Profesa Jay wakifunua vitambaa wakati wa uzinduzi wa GlobaL TV Online jana katika ofisi za Global Publishers Ltd.
  GlobaL TV Online baada ya kuzinduliwa rasmi.
  Mkurugenzi wa Global Publishers & General Enterprises Ltd, Eric Shigongo pamoja na staa wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu wakikata keki wakati wa uzinduzi huo.
  Mkongwe wa sanaa ya maigizo Bongo, Fatuma Makongoro 'Bi. Mwenda' akijiandaa kufungua shampeini.


  Shampeini zikiwa tayari kufunguliwa.
  ....
  IT'S CHEERS TIME...
  Waalikwa na wafanyakazi wa Global wakigonga 'Cheers'.
  Prof Jay, Bi. Mwenda na Steve Nyerere  wakigonga 'cheers'.
  Shigongo akigonga 'cheers' na Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Richard Manyota (kulia) na Oscar Ndauka ambaye ni Mhariri Kiongozi Magazeti Pendwa (katikati).
  Mastaa wakigonga cheers.
  ...Cheers.
  Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd, wachapishaji wa Magazeti ya Uwazi, Championi, Amani, Risasi, Ijumaa na Ijumaa Wikienda jana ilizindua Global TV Online ambayo ni televisheni inayoruka mtandaoni kupitia tovuti ya kampuni hiyo ya www.globalpublishers.infondani ya ofisi zake zilizopo Mwenge-Bamaga jijini Dar es Salaam. Katika uzinduzi huo, mastaa kibao walihudhuria na kupata fursa ya kuona baadhi ya vipindi kutoka Global TV Online pamoja na kutoa maoni yao kuhusu uboreshwaji wa TV hiyo. Mbali na tukio hilo, mastaa waliongoza zoezi la kukata utepe, kufungua shampeini na kukata keki kuashiria uzinduzi rasmi wa Global TV Online.

  UZINDUZI WA GLOBAL TV ONLINE WAFUNIKA Kutoka kushoto: Wasanii Dk. Cheni, Bi. Mwenda, Profesa Jay na Wema Sepetu wakishiriki kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa GlobaL TV Online jana.

  0 0
 • 04/17/14--13:36: Article 9


 • 0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Green Stars Industry inayomiliki eneo la FAN CITY Bw. Hasan Rizvi akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) mashine za michezo mbali mbali itakayotolewa kipindi cha sikukuu ya Pasaka wakati wa mkutano alioufanya katika eneo la Fun City Kigamboni jijini Dar es Salaam. Pia aliongeza kuwa kwa sasa kampuni yake imeeongeza mitambo yenye uwezo wa kutengeneza mawimbi ya aina sita tofauti kwenye bwawa kubwa la kuogelea.
  Mitambo ya kisasa iliyofungwa katika eneo la Fun City ambayo itawawezesha wananchi kupata burudani kabambe zenye ubora wa kimataifa kwani hakuna mahali popote Afrika Mashariki mitambo hiyo.


  Mawimbi yanayotengenezwa kwa mitambo ya kisasa katika bwawa kubwa la kuogelea lililopo hapa Fun City,
  Moja ya Bwawa la kuongelea.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Fan City, Bw. Hasan Rizvi  akionyesha vigari vya mchezo.
  Bembea za kutosha.
  Bembea za watoto.
  Mapokezi ya Fun City.
  Eneo la Fun City linasehemu ya Ibada. 
   Sehemu ya huduma ya kwanza nayo inapatikana hapa.
   Sehemu ya moja ya sehemu ya bembea za magari ikiongesha madhari nzuri za kiota cha burudani cha Fun City.
  Vigari vya umeme vinavyopita ndani ya maji.
  *YAFUNGA MITAMBO YA KISASA KWA AJILI YA MICHEZO YA KWENYE MAJI
  Na Mwandishi Wetu, Dares salaam
  Wakati Watanzania wakiwa kwenye maandalizi ya sikukuu ya Pasaka kampuni ya Green Stars Industry inayomiliki eneo la FAN CITY limeongeza mitambo yenye uwezo wa kutengeneza mawimbi ya aina sita tofauti kwenye bwawa kubwa la kuogelea.
  Mtambo huo wa aina yake utaongeza hamasa kwa waogeleaji kuhisi kama wapo baharini.
  Akizungumzia mtambo huo Mkurugenzi Mtendaji wa Fan City, Bw. Hasan Rizvi amesema, lengo la kuoberesha michezo hiyo ni kuwawezesha watanzania kufurahia michezo hiyo pamoja na familia zao wakati huu wa Pasaka.
  Ameongeza kuwa mitambo ya kisasa iliyofungwa katika eneo lake itawawezesha wananchi kupata burudani kabambe yenye ubora wa kimataifa kwani hakuna mahali popote Afrika Mashariki mitambo hiyo inapatikana.

  “Tumefunga mtambo huu ambao utakua ukitengeneza mawimbi ya aina sita tofauti kwenye bwawa kubwa la kuogelea lililopo hapa Fan City, lengo letu nikutoa burudani zaidi kwa watu wanaotembelea hapa”.Alisema Rizvi.

  “Tumefanya uwekezaji wa mashine za kisasa za michezo mbalimbali kwenye eneo letu ili kutoa burudani nzuri na za kipekee kwa wananchi wanaotembelea eneo hili na hasa wakati huu wa Pasaka”. Alisisitiza Rizvi. Fan City iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

  Fun City imekuwa ikitoa burudani safi ya michezo mbalimbali kwa familia na katika kipindi hiki cha Pasaka imeandaa michezo kama Sarakasi, Mazingaombwe na zawadi kemkem kwa watakaotembelea eneo hilo. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog

  0 0


  NDUGU ZANGU,

  MJENGWABLOG SASA IKO HEWANI . 
  UNAWEZA KUITEMBELEA KUPITIA http://mjengwablog.com/

  POLENI SANA KWA USUMBUFU NA TUNAWASHUKURU KWA KUENDELEA KUTUAMINI.

  0 0

  Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mkutano wao wa siku mbili uliofanyika jijini Dar es Salaam. Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii wakiwa katika
  picha ya pamoja baada ya mkutano wao wa siku mbili uliofanyika jijini Dar es Salaam.[/caption] BARAZA Kuu la Wafanyakazi la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii limekutana kwa siku mbili jijini Dar es Salaam tangu juzi kufanya vikao vyake vya kazi ikiwa ni pamoja na kuangalia utendaji kazi, kupitia mikakati na malengo mbalimbali iliyojiwekea.

  Mkutano huo ambao pia umejadili na kupitisha bajeti ya shirika kwa mwaka 2014/15 umeongozwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo, ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani K. Dau na kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa NSSF uliopo Katika Jengo la shirika hilo 'WeterFront House' la jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umejumuisha Watendaji Wakuu toka Makao Makuu, Mameneja wa Mikoa, Watendaji wa kuu wa mikoa na wajumbe wengine wanaounda baraza la wafanyakazi la NSSF. 

  Jumla ya wajumbe 142 wameshiriki katika mkutano huo uliofanyika kwa siku mbili. Shirika la NSSF ni miongoni mwa mwashirika makubwa ya hifadhi ya jamii nchini yenye vitega uchumi lukuki na vya thamani kubwa vinaochangia kukua kwa uchumi wa taifa. *Imeandaliwa na www.thehabari.com
  Baadhi ya Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF wakiwa katika mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na mkutano wao. Baadhi ya Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF wakiwa katika mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na mkutano wao.Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori (kushoto) akikaimu uenyekiti wa moja ya vikao vya Baraza Kuu la Wafanyakazi la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii. Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori (kushoto) akikaimu uenyekiti wa moja ya vikao vya Baraza Kuu la Wafanyakazi la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii. Kulia ni Katibu wake.Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani K. Dau (kushoto) akizungumza na mmoja wa wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika hilo katika mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na mkutano wao. Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani K. Dau (kushoto) akizungumza na mmoja wa wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika hilo katika mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na mkutano wao.Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani K. Dau akizungumza na baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF baada ya kumalizika kwa kikao cha baraza hilo. Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani K. Dau (wa kwanza kushoto) akizungumza na baadhi ya  viongozi waandamizi wa shirika hilo, ambao pia ni wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF baada ya kumalizika kwa kikao cha baraza hilo.  Baadhi ya Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF wakibadilishana mawazo kwenye mapumziko kabla ya kuendelea na majadiliano. Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori (katikati) akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi waandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambao pia ni wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika hilo. Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori (katikati) akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi waandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambao pia ni wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika hilo.Baadhi ya Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF wakibadilishana mawazo kwenye mapumziko kabla ya kuendelea na majadiliano.  Baadhi ya Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF wakibadilishana mawazo kwenye mapumziko kabla ya kuendelea na majadiliano.Baadhi ya Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF wakiwa katika mkutano wa baraza uliofanyika juzi na jana jijini Dar es Salaam. Baadhi ya Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF wakiwa katika mkutano wa baraza uliofanyika juzi na jana jijini Dar es Salaam.Baadhi ya Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF wakibadilishana mawazo kwenye mapumziko kabla ya kuendelea na majadiliano.  Baadhi ya Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF wakibadilishana mawazo kwenye mapumziko kabla ya kuendelea na majadiliano.

  0 0

   498 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA toka  Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Emmanuel Mahinga akitoa maelezo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam (hawapo pichani) kuhusu jinsi Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za Umma (EPICOR 9.05) unavyofanya kazi  na  malengo ya kuanzishwa kwa mfumo huo ikiwemo kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo hapa nchini. Picha zote na Frank Mvungi -Maelezo. 
   Afisa Msimamizi wa Fedha (TEHAMA) toka Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw.  Elisa Rwamiago (katikati)akifafanua kwa waaandishi wa habari jinsi  Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za Umma (EPICOR 9.) utakavyoongeza tija katika utendaji wa Serikali za Mitaa na kuondoa malalamiko ya kuwepo mianya ya  vitendo vya ubadhilifu wa fedha za umma.kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini toka Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bi Rebecca Kwandu.kulia,  ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bi Georgina Misama.

  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini toka Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bi Rebecca Kwandu (kushoto) akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es salaam kuhusu faida za matumizi ya Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za Umma (EPICOR 9.05) Katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ambapo Halmashauri 133 na Mkoa 21 ya Tanzania Bara imeunganishawa katika mfumo huo, katikatika ni Afisa Msimamizi wa Fedha (TEHAMA)  toka TAMISEMI  Bw. Elisa Rwamiago na kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bi Georgina Misama.

  0 0

   Katibu wa vijana wa CCM mkoa wa Iringa Halawi Haidaria akizungumza 
   baadhi ya viongozi wa ccm wakiwa katika picha ya pamoja sambambana picha za waasisi wa muungano katika ngome ya mkwawa iliyoko kalenga.
   baadhi ya washiriki wa mbio za pikipiki wakijiandaa kuanza mbio hizo.

  Seki Kasuga akizungumza kuhusu umuhimu wa serikali mbili
   =======
  UVCCM YAHAMASISHA SERIKALI MBILI MIKOANI

  Na Denis Mlowe,Iringa
   
  KATIKA kuhakikisha Chama cha Mapinduzi kimedhamiria kupitisha serikali mbili katika bunge maalum la katiba, Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wako katika harakati za kuhamasisha wananchi kukubaliana serikali mbili ambazo wamekuwa wakitumia mbio za pikipiki kueneza ujumbe huo kwa kutumia  jumuiya ya vijana wa chama hicho.
   
  Akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Stand ya Mlandege juzi,Kiongozi wa mbio za pikipiki kitaifa, Hassan Bamboko alisema lengo za mbio hizo ni kufikisha ujumbe wa chama hicho kwa wananchi kuwa serikali mbili ndizo zitakazopitishwa na chama hicho na kuwataka wananchi kuuwanga mkono katika harakati hizo.

  Alisema licha ya kuhamasisha ujumbe wa serikali mbili ambao wananchi wengi wamekuwa wakiukataa mbio hizo zinatumika kuadhimisha miaka 50 ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar ambao nao uko mashakani kutokana na chama cha mapinduzi kuendelea kung’ang’ania serikali 2 badala ya tatu ambazo ni chaguo la wengi.

  "Mbio hizi za pikipiki tunaenda nazo nchi nzima lengo nikuwaeleza wananchi kuwa serikali mbili zinatosha wanaotaka tatu wanauchu wa madaraka na ni mzigo kwa kweli na nawaomba muelewe hili kutokana na ni ya chama cha mapinduzi kwa wananchi wake kuwa ni nzuri katika kulinda usalama wa nchi" alisema Bamboko na kuongeza kuwa tuna miaka 50 tukiwa na Muungano wa serikali mbili licha ya kuwa na kasoro zilikuwa chache na kuongezeka zinaweza kurekebishwa na hakika serikali mbili zinatosha" alisisitiza.

  Kwa upande wake kiongozi mwingine wa mbio za pikipiki,Seki Kasuga alisisitiza kuwa serikali mbili ndio mustakabali wa Watanzania katika maisha ya mbele  na wanaotaka kuugawa Muungano watafute kwanza udongo uliochanganywa ili ugawanywe.

  Naye Katibu wa ccm wilaya ya Mufindi Miraji Mtaturu akizungumzia kuhusu muundo wa Serikali Tatu alisema Chadema wanatumiwa na magaidi wa nchi za nje kutaka serikali tatu ili kuwavuruga wananchi.
   
  Aliwataka wananchi kumfikishia ujumbe Mwenyekiti wa Ukawa, Freeman Mbowe kuwa serikali tatu haikubaliki kwa Watanzania hivyo wanajidanganya kwa kuwa mwarubaini wa maendeleo ya Watanzania ni serikali mbili na sio tatu kama zinazoshinikizwa na wapinzani.

  Na Katibu wa vijana wa CCM mkoa wa Iringa Halawi Haidari mwenyeji wa Zanzibar, alisema Wazanzibar wanautambua Muungano wa Serikali mbili hivyo hawawezi kutoka katika Muungano kwa sababu Wazanzibar wapo huru kuishi popote  katika ardhi ya Tanzania
   
  Alisema kuwa muungano ukivunjika na  kufikia hatua ya mgawanyiko watambue kuwa hata  Unguja na Pemba navyo vitagawanyika kwa sababu leo wamedai hati ya Muungano wa Watanzania mwisho watataka hati ya Unguja na Pemba lakini Wazazibar hawakubali msimamo wa serikali tatu.
   
  Katika mbio hizo vijana hao walikabidhi kwa kaimu mkuu wa wilaya ya Iringa, Gerald Guninita picha ya Rais wa kwanza wa Tanzania mwalimu Julius Kambarage Nyerere na picha ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Shekhe Abeid Amani Karume pamoja na mabango mawili moja likiwa na ramani ya Tanzania na lingine likiwa na ujumbe maaulum wa mbio hizo unaosema, miaka 50 ya Muungano, “Dumisha Muungano vijana tutumie fursa zilizopo kwa maendeleo yetu, Tanzania kwanza mengine baadae.

older | 1 | .... | 271 | 272 | (Page 273) | 274 | 275 | .... | 1898 | newer