Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 270 | 271 | (Page 272) | 273 | 274 | .... | 1898 | newer

  0 0


   Waziri Mbene akipokelewa Ubungo Plaza na Mkurugenzi Mkuu wa FCC Dk.
  Frederick Ringo.
  Naibu Waziri, Mhe. Janeth Mbene (MB) akitia saini katika kitabu cha
  wageni, Tume ya Ushindani leo.
  =======  =======  ========
  Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Nchini, Mhe. Janeth Mbene (MB) leo
  alitembelea Tume ya Ushindani ambapo aliitaka Tume hiyo kufungua ofisi za
  Kanda ili kuweza kuongeza juhudi za kutoa elimu ya mlaji kwa wananchi walio  wengi sehemu mbalimbali nchini.  Mhe. Mbene alitoa wito huo baada ya Kupata fursa ya kujifunza kwa vitendo
  jinsi ya kutofautisha bidhaa bandia na halisi ambapo sampuli zake zilikuwepo   katikaukumbi wa mikutano wa Tume hiyo, Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam.  Alisema ³Wananchi wengi wa Tanzania tuna tatizo la kupenda kuamini kila
  tunaloambiwa na wafanyabiashara, hivyo ni vema Tume ikafungua ofisi walau za    kanda ili iweze kuongeza kupeleka elimu hii kwa wananchi waweze kuelewa kuwa   zipo bidhaa bandia na kuna mienendo potofu katika soko ili waweze kuwa  makini zaidi.  Alidha, Mhe. Mbene aliitaka Menejimenti ya Tume kuwasilisha maelezo kuhusu    kuongezewa bajeti ili kuwezesha utendaji wenye ufanisi wa chombo hicho  ambacho kina wajibu wa kusimamia utendaji wa uchumi wa soko.  Waziri Mbene pia alipokea maoni ya Tume ya Ushindani kuhusu umuhimu wa      Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuanzisha Sheria za kusimamia na kudhibiti  kusambaa kwa bidhaa bandia ambapo ilibainika kuwa kuna kiasi kikubwa cha  bidhaa zinazoshukiwa kuwa ama ni bandia au zipo chini ya kiwango  zinazoingizwa Tanzania bara kutoka Tanzania Vsiwani kwa njia za magendo.  Aliitaka Tume ya Ushindani kuwasilisha mapendekezo yake kwake ili aweze
  kuona namna bora ya kuwasilisha ushauri huo Seikalini.

  Katika ziara hiyo Waziri Mbene aliambatana na Mkurugenzi Msaidizi wa Sera na    Mipango-Bajeti, Bibi Elizabeth Msengi, Afisa Habari, Edward Nkomola na  Katibu wake, Athumani Nkhungu.  Akimaribisha Waziri Mbene katika Tume Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo, Dk.  Frederick Ringo alielezea kuwa shughuli za Tume hiyo zinashindwa kukamilika    kwa ufanisi kutokana na ufinyu wa bajeti na kuelezea umuhimu wa Serikali  kuipatia Tume hiyo fungu la kutosha la bajeti ya utendaji wa shughuli zake.

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo mafupi kutoka kwa Afisa Zana za Kilimo wa Wilaya ya Mlele,kuhusiana na Mradi wa Mashine ya Kusindika Mpunga mapema leo jioni,katika kijiji cha Mwampuli,Wilaya mpya ya Mlele mkoani Katavi,Mashine hiyo ina uwezo wa kusindika mpunga tani 30 kwa siku.Kushoto ni Mjumbe wa NEC Taifa,Balozi Ali Karume nae akisikiliza kwa makini.Kinana yupo Mkoani Katavi kwa ziara ya siku nne ya kuimarisha uhai wa chama,kukagua na kuhimiza ilani ya Uchaguzi ya 2010.
  Mradi wa Mashine ya Kusindika Mpunga kama uonekavyo pichani uliopo katika kijiji cha Mwampuli,Wilaya mpya ya Mlele mkoani Katavi,Mashine hiyo ina uwezo wa kusindika mpunga tani 30 kwa siku.
  Katibu Mkuu wa CCM,akikagua Ujenzi wa Mradi wa Maji safi,katika kijiji cha Kibaoni,Wilaya ya Mlele,mkoani Katavi.Tanki hilo la maji safi linatarajia kuhudumia wakazi wa kijiji cha Kibaoni na vijiji vingine tisa.

  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana wa tatu kulia akishiriki kukusanya mawe pamoja na viongozi mbalimbali wa Taifa,Mkoa na Wilaya (CCM),kukusanya mawe kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa shule ya msingi Maji Moto iliyopo katika kijiji cha Maji Moto,Wilaya mpya ya Mlele mkoani Katavi.
  Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Maji Moto jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara,Nape amewataka wana CCM na wananchi kwa ujumla kuishi kwa amani na upendo katika suala zima la kudumisha amani tulionayo na kuwapuuza wanaotaka kuleta mgawanyiko katika nchi yetu kwa namna moja ama nyingine.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Maji Moto jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara,Kinana ameeleza kuwa kumekuwepo tatizo kubwa kila mahali aendapo kufanya ziara kuhusiana na migogoro ya ardhi kati ya Wakulima na Wafugaji,Wafugaji na Hifadhi,jambo ambalo linapaswa kufanyiwa kazi kwa umakini mkubwa sana,aliongeza kuwa migogoro hiyo imekuwa janga la Taifa,kutokana na idadi ya watu kuongezeka katika maeneo mengi,huku mipaka yake kubaki kama iliyo kwa muda mrefu.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mama Mzazi wa Waziri Mkuu,Mh Pinda, mapema mchana huu nyumbani kwake,Katika kijiji cha Kibaoni Wilaya Mlela mkoani Katavi,alipokwenda kumtembelea na kumjulia hali.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza jambo na Mama Mzazi wa Waziri Mkuu,Mh Pinda, mapema mchana huu nyumbani kwake,Katika kijiji cha Kibaoni Wilaya Mlele mkoani Katavi,alipokwenda kumtembelea na kumjulia hali.Kinana yuko Mkoani Katavi kwa ziara ya siku nne ya kuimarisha uhai wa chama,kukagua na kuhimiza ilani ya Uchaguzi ya 2010.
  Kinana akijaribu kuelewesha jambo katika shamba la Ufugaji nyuki la Waziri  Mkuu Pinda,katika kijiji cha Kibaoni Wilaya ya Mlele mkoani Katavi mapema leo mchana.
  Kinana akikatiza kwenye Shamba la Ufuta na Nyuki mara baada ya kujionea ufugaji wa nyuki unavyofanyika.
  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mbunge wa Ilala, Azzan Zungu, na baadhi ya waombolezaji wakati alipowasili nyumbani kwa marehemu Maalim Muhidin Gurumo, Mabibo jijini Dar es Salaam, kwa ajili kuaga mwili wa marehemu kabla ya kusafirishwa kuelekea Kijijini kwao Masaki Wilaya ya Kisarawe kwa maziko, leo, Aprili 15, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mwanamuziki mkongwe, Kassim Mapili, na baadhi ya waombolezaji wakati alipowasili nyumbani kwa marehemu Maalim Muhidin Gurumo, Mabibo jijini Dar es Salaam, kwa ajili kuaga mwili wa marehemu kabla ya kusafirishwa kuelekea Kijijini kwao Masaki Wilaya ya Kisarawe kwa maziko, leo, Aprili 15, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia wa marehemu Maalim Muhidin Gurumo, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu, Mabibo jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuaga mwili wa marehemu kabla ya kusafirishwa kuelekea kijijini kwao Masaki Wilaya ya Kisarawe kwa maziko, leo Aprili 15, 2014. Kulia ni Mjane wa marehemu, Pili Binti Saidi Kitwana.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wanafamilia wa marehemu Maalim Muhidin Gurumo, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu, Mabibo jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuaga mwili wa marehemu kabla ya kusafirishwa kuelekea kijijini kwao Masaki Wilaya ya Kisarawe kwa maziko, leo Aprili 15, 2014. Kulia ni Mjane wa marehemu, Pili Binti Saidi Kitwana.
  Sehemu ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehu wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waombolezaji katika msiba wa Maalim Muhidin Gurumo, wakati alipofika nyumbani kwake Mabibo jijini Dar es Salaam, leo Aprili 15, 2014 kwa ajili ya kuaga kabla ya kusafirishwa kuelekea kijijini kwao Masaki Wilaya ya Kisarawe kwa maziko.
  Baadhi ya wasanii wakijumuika na waombolezaji nyumbani kwa marehemu Gurumo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na waombolezaji wakati akiondoka nyumbani kwa marehemu Maalim Muhidin Gurumo, baada ya kuaga mwili wa marehemu. Picha na OMR.


  0 0

  The National Bank of Commerce, on Monday announced it’s financial results for the year 2013 whereby its Net Interest margin on average Interest bearing assets increased from 8.98% in 2012 to 9.06% in 2013 due to improvement on the quality of loans and advances to customers and higher yield and increased volume on the market securities. Interest income expressed as a percentage of total income increased to 67% (2012: 60 %) mainly due to the increased booking of earning assets.

  The NBC Managing Director Mizinga Melu said that the total assets from TZS 1,518 billion in 2012 to TZS 1,587 billion as at 31 December 2013. Growth is mainly coming from investment of the recapitalised funds. Loans and advances increased by 4.5% to Tzs 684 billion in 2013 from TZS 654 billion in 2012 ( an increase of 3.5% in 2012). This has been attributed by new bookings as well as conversion of customers’ asset pipeline.

  “Customer deposits increased from Tzs 1,291 billion in 2012 to Tzs 1,305 billion in 2013. The increase is mainly attributed to liability campaign carried out in quarter four of the year.” Added Mrs. Melu 
  The liability campaign was launched in October 2013 and it required a customer to open and deposit into their Malengo Savings Account or to open and deposit into a one year Fixed Deposits Account. At the end of the promotion 13 customers won different prizes.

  Apart from the promotions, NBC has launched different products to suit customers’ needs like the recently launched NBC Direct which is a collection of various products packaged together and offered as a bundle at a favourable fee. The product is offered in three different packages, Gold, Silver and Bronze with the lowest package being charged a monthly fee of TZS 1000 per month.

  NBC Direct is a revolutionary product which packages several products and offers them as a bundle to provide a comprehensive solution to all customers’ banking needs at a very affordable fee. The products which are offered in three different packages includes Zero minimum opening balance on all accounts with the lowest package including a free initial debit card as well as free funeral insurance cover.

   Other packages include Free ATM Transactions on all NBC ATMs, Free Internet Banking and Mobile Banking, Free Standing Order to NBC Accounts, Free Balance Inquiry & Mini-Statements as well as Accident Insurance Cover.

  Being a bank which is conveniently everywhere, NBC is living its purpose to help people achieve their ambitions the right way as it has also launched the Free Credit Life insurance which is an insurance cover arranged to pay the outstanding balance of the Personal loan in the event of death or total permanent disability of the borrower provided that loan repayments are up to date as contracted with NBC Limited. It is a free product because NBC Limited will pay the Borrower’s Insurance premiums (charges).

  Furthermore, NBC Management has taken steps to make sure their customers are served by highly knowledgeable and experienced employees by ensuring that they build strong talent pipelines through secondments and Pan African Graduate trainee program which has been designed to build leadership capability and create young and upcoming leaders for Africa and beyond.

  This is in line with their purpose of helping their customers achieve their ambitions – the right way.


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akifurahia jambo wakati akitoa hotuba yake katika mkutano wa Wadau wa Ukanda wa kati(alignment meeting on central corridor), alioufungua leo mchana katika ukumbi wa Mwl. Julius Nyerere. Mkutano huo wa wadau ni sehemu ya utekelezaji wa maamuzi ya Mkutano wa Jukwaa la Kiuchumi Duniani (World Economic Forum) iliofanyika Davos Uswiss Mwezi Januari 2014.
  Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe, akitoa hotuba kabla ya kumkaribisha kufungua mkutano wadau wa Ukanda wa kati (alignment meeting on central corridor), uliofanyika leo mchana katika ukumbi wa Mwl. Julius Nyerere. Kulia kwa Waziri Mwakyembe ni Mkurugenzi wa Jukwa la Kiuchumi Duniani kwa upande wa Afrika, Bi. Elsie Kanza.
  Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka wakati akiwasilisha mada katika mkutano wa wadau wa Ukanda wa kati (alignment meeting on central corridor), uliofanyika leo mchana katika ukumbi wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akimwambia jambo Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bw. Richard Sezibera, wakati wa mkutano wa Wadau wa Ukanda wa kati (ALIGNMENT MEETING ON CENTRAL CORRIDOR), uliofanyika leo mchana katika ukumbi wa Mwl. Julius Nyerere. Mkutano huo wa wadau ni sehemu ya utekelezaji wa maamuzi ya Mkutano wa Jukwaa la Kiuchumi Duniani(World Economic Forum) iliofanyika Davos Uswis Mwezi Januari 2014.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka akiwasilisha mada ya fursa ya uwekezaji katika Ukanda wa kati, katika mkutano uliowakutanisha Wadau wa Ukanda wa kati(alignment meeting on central corridor), uliofanyika leo mchana katika ukumbi wa Mwl. Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete (wa sita kutoka kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Wahisani wa maendeleo, na waadau wa mkutano wa Wadau wa Ukanda wa kati wa(alignment meeting on central corridor), uliofanyika leo mchana katika ukumbi wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Mkutano huo wa wadau ni sehemu ya utekelezaji wa maamuzi ya Mkutano wa Jukwaa la Kiuchumi Duniani (World Economic Forum) iliofanyika Davos Uswiss Mwezi Januari 2014, ambao ulichagua Ukanda wa kati kuwa mradi wa majaribio ya kuwezesha uwekezaji kwa njia ya ubia(PPP).(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)

  0 0

   Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa marehemu Muhidin Maalim Gurumo (mwenye shuka nyeupe) na wanafamilia alipokwenda kuhani msimba huo Ubungo Makuburi jioni ya leo April 15, 2014, siku ambayo marehemu alizikwa kijijini kwao Masaki, Kisarawe, Mkoa wa Pwani.

  Marehemu Gurumo, aliyefariki dunia juzi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matatizo ya moyo, atakumbukwa kama Baba wa Muziki wa dansi nchini akianzia miaka ya 1960 na bendi mbalimbali ikiwemo NUTA Jazz na kumalizia na Msondo Ngoma kabla ya kustaafu muziki mwaka jana.
   Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete pole Bw. Abdallah Muhidin Gurumo, mtoto wa marehemu Muhidin Maalim Gurumo na wanafamilia alipokwenda kuhani msimba huo Ubungo Makuburi jioni ya leo April 15, 2014,
   Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Bw. Omar Muhidin Maalim Gurumo na wanafamilia alipokwenda kuhani msimba huo Ubungo Makuburi jioni ya leo April 15, 2014,
   Sehemu ya waombolezaji
   Mmoja wa wana familia Bw. Salim Zagar akitoa taarifa fupi ya msiba pamoja na mazishi kwa Mhe Rais
  Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Muziki wa dansi Bwana Brighton akimshukuru Rais Kikwete kwa kwenda kutoa pole ya msiba huo

  0 0

   Bendi ya African Stars “Twanga Pepeta” itasindikiza uzinduzi wa Redds Miss Tabata itakayofanyika Jumapili ya Pasaka katika ukumbi wa Da’ West Park, Tabata.

  Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga amesema bendi hiyo itatambulisha nyimbo zao mpya kama zawadi yao ya Pasaka kwa wapenzi wao.
  Pia bendi hiyo ijulikanayo kama Wakali wa Kisigino pia watapiga nyimbo zao zote kali hadi majogoo.

  Mratibu huyo wa Bob Entertainment na Keen Arts alisema kuwa wapenzi wa urembo watapata fursa ya kuwaona warembo hao siku hiyo kabla hawajashiriki kwenye shindano la Miss Tabata ambalo limepangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi ujao.

  Katika uzinduzi huo warembo wa Tabata watasindikizwa na washiriki wenzao wa Miss Mzizima na Miss Ukonga.
  Pia watakuwepo viongozi waandamizi kutoka kamati ya Miss Tanzania ikiongozwa na Hashim Lundenga na Redds Miss Tanzania Happiness Watimanywa.

  Warembo 21 wanaendelea na mazoezi ya Miss Tabata katika ukumbi wa Da West Park chini ya wakufunzi wawili -  Neema Chaki na Pasilida Bandari.
  Warembo hao ni Esther Frank Kiwambo (20), Jemima Huruma Mawole (22), Badra S. Karuta (20), Mercy Mathias Kazula (19), Lydia Charles (22), Agnes Tarimo (18), Agnes Alex (20), Catrina Lawrence Idfonsi (20), Nuru Omary Athumani (19) na Happyclarrice Wilson Mbahi (19).

  Wengine ni Annatolia Raphael (21), Mary Henry (21),  Evodia Peter (22), Fatma Hussein Ismail (20),  Ester Wilson Mbayi (20), Ambasia Lucy Mally (22), Faudhia Hamisi (21), Najma Charles Mareges (19), Lightnes Olomi (18), Husna Ibrahim (19) na Ramta Mkadara (20).
  Warembo watano kutoka Tabata watashiriki kwenye shindano la kanda ya Ilala, Miss Ilala baadaye mwaka huu.
  Mrembo anayeshikilia taji la Miss Tabata ni  Dorice Mollel ambaye pia ni Redds Miss Ilala.


  0 0

  Kutokana na kukithiri kwa mfumo dume unaoambatana na ukandamizaji wa mwanamke na kusababisha ongezeko la watoto yatima na wajane katika jamii ya wafuagaji wa kimasai, wanawake wa jamii  hiyo wanaoishi ndani  ya eneo la mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro wameunda baraza  la wanawake  litakalosimamia masuala mbalimbali kwa mtoto wa kike husani elimu,afya,na haki ya mwanamke.

  Wanawake hao wa jamii ya kimasai wanabainisha kuwa hamasa ndogo ya jamii ya kuwasomesha watotot wa kilke na kutopewa kipaumbele ,afya duni ya jamii hasa mama na motto endapo vitazingatiwa katika jamii hiyo vitasaidia kuondokana na changamoto hizo na hatimae kuongeza idadi ya wasomi hasa watoto wa kike ambao wataikomboa jamii hiyo kwa ujumla .

  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa baraza hilo  uliofanyika katika makao makuu ya mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro ukienda sambamba na harambee ya kuchangia mfuko wa elimu kwa watoto wa kike  makamu mwenyekiti wa baraza hilo bibi mereyo muresi anasema   litakua chombo muhimu cha kuwasemea wanawake katika vyombo vya maamuzi ndani na nje.

  Mhifadhi mkuu wa mamlaka ya ngorongoro  dakta  fredy manongi ndiye aliyezindua baraza hilo na kuendesha harambee iliyofanikisha kupatikana kwa zaidi ya shilingi milioni sabini fedha taslimu na ahadi.

  Baraza la wanawake  hao wafugaji linaanzishwa huku tayari kukiwa na baraza la wafugaji ngorongoro ambalo mwenyekiti wa baraza hilo metui ole shaudo anawaasa  kuwa lengo walilokusudia  la kumkomboa mwanamke litafikiwa kwa  wao kushirikiana na wadau wengine

  0 0

  Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa akifungua mafunzo ya Ukimwi mahali pa kazi kwa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa mwishoni mwa juma, Semina hiyo iliyoandaliwa na idara ya maendeleo ya jamii na mratibu wa TACAIDS Mkoa wa Rukwa kwa watumishi hao ilikua na lengo la kuelimishana na kukumbushana juu ya mambo mbalimbali yanayohusu janga la Ukimwi na umuhimu wa Tohara kwa wanaume katika kujikinga na janga hilo. Katika hotuba yake Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa hakusita kuonyesha hisia zake kali kwa watumishi watakaohusika katika rushwa za ngono na kusema kuwa watachukuliwa hatua kali bila ya utetezi wowote kutoka kwake.
  Mratibu wa TACAIDS Mkoa wa Rukwa Ndugu Daniel Mwaiteleke akitoa mada juu ya uelewa wa jumla kuhusu gonjwa la UKIMWI kwa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa katika mafunzo ya siku moja yaliyofanyika katika ukumbi wa RDC Mjini Sumbawanga.
  Muwezeshaji wa mada ya magonjwa ya zinaa STD na STI Dkt. Lunyelele akiwasilisha mada yake kwa umahiri mkubwa bila ya kutafunatafuna maneno
  Dkt. Lunyelele akiwa anatoa mafunzo hayo.
  Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mafunzo hayo.
  Mjumbe katika Semina hiyo Ndugu Frank Mateny akichangia moja ya mada katika mafunzo hayo. 
  Mdau Mussa Mwangoka na Paul Ngany'anyuka ndani ya Semina hiyo.
  Dena na Richard Ndambala nao walikuwepo.
  (Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

  0 0

    
  Na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Dodoma
  Watanzania wa Mikoa ya Mwanza na Dodoma wameipongeza kampuni ya Proin Promotions Limited kupitia shindano lao la Kusaka vipaji vya Kuigiza Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents kwa kuamua kuanzisha shindano hilo ambalo limeanza kuonyesha matumaini kwa vijana wenye vipaji vya kuigiza ambao walisahaulika katika tasnia hiyo ya filamu nchini.

  Shindano hili la Tanzania Movie Talents linawawezesha watanzania wote wenye vipaji vya kuigiza kuweza kujitokeza ili kuweza kuonyesha vipaji vyao na kuvikuza kwa kutumia fursa hii iliyoanzishwa na kampuni ya Proin Promotions Limited.


  Wakiongelea kuhusu shindano hili la Tanzania Movie Talents, wakazi wa Mkoa wa Dodoma walisema" tunafurahishwa sana na shindano hili kuweza kuanzishwa Tanzania na Afrika Mashariki na Kati kwani sasa tunaweza kupata nafasi katika tasnia ya filamu baada ya kuanza kuonyesha vipaji vyetu vya kuigiza".

  "Tanzania Movie Talents inamgusa kila mtanzania mwenye vipaji vya kuigiza kwani ni nafasi kwa vijana na watanzania wote wenye vipaji vya kuigiza kuweza kujitokeza kwaajili ya kuonyesha uwezo na vipaji vyao vya kuigiza, Shindano la Tanzania Movie Talents ni mkombozi wa Vijana na watanzania ambao wana vipaji vya kuigiza ambapo kupitia shindano hili vijana wanaweza kupata nafasi za ajira kupitia tasnia ya filamu nchini ambapo washiriki watakuwa wameweza kuonekana na hatimaye kuitwa kwaajili ya kufanya kazi.  Kwa upande wake baadhi ya wafanyakazi wa timu ya Tanzania Movie Talents walithibitisha kuwa 'Tanzania Movie Talents imepokelewa vizuri na watanzania wa Mikoa ya Mwanza na Dodoma  kwani tumeona ongezeko la washiriki waliojitokeza kwaajili ya usaili wa kushiriki katika Shindano hili kubwa na la kwanza Afrika Mashariki na Kati. 

  Hii nikutokana na ukweli kwamba washiriki wote wanaofika kwaajili ya Usaili hawatozwi kiasi chochote cha pesa kutoka timu ya Tanzania Movie Talents na pia kufurahishwa na uamuzi wa Majaji wa Timu ya Tanzania Movie Talents,  niwazi kabisa kuwa kutotozwa kwa kiasi chochote cha pesa kwa washiriki kumekuwa ni kivutio kikubwa kabisa hivyo kuongeza idadi ya washiriki katika kila Kanda tunayoenda"alisema Stephen Mapunda Mkazi wa Mkoa wa Dodoma

  0 0
 • 04/15/14--14:55: MASIKINI TWIGA WETU.!
 • Pichani ni Maofisa wa TANAPA ndani ya Hifadhi ya Wanyama ya Katavi,Wakiwa wamenaswa na Camera ya Globu ya Jamii,ilipokuwa imetoka kwenye kazi maalum Wilayani Mlele mkoani humo na kukumbana na tukio hilo la Maofisa hao wakimtazama Twiga aliyegongwa na gari na kufa papo hapo,katika tukio hilo la huzuni kubwa,gari iliyohusika na ajali hiyo halikujulikana mara moja.
  Maofisa wa TANAPA waliokuwa doria hifadhini,wakitafakari jambo mara baada ya kumkuta Twiga akiwa amegongwa na kufa papo hapo jioni ya leo ndani ya Hifadhi ya Wanyama Katavi.

  0 0

   Mkurugenzi wa shughuli za Kanda na Huduma kwa wateja  toka Bohari ya Dawa (MSD) Bw. Edward Terry Kulia akizungumza na waandishi wa habari  leo katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo  juu ya mpango wa bohari hiyo kupanua maghala  ya kuhifadhi Dawa na Vifaa  tiba kama moja ya hatua za kuboresha huduma zinazotolewa na Bohari hiyo . Kushoto ni Mkurugenzi  wa Manunuzi wa Bohari hiyo  Bw. Heri Mchunga.
  Mkurugenzi  wa Manunuzi  Bohari ya Dawa (MSD) Bw. Heri Mchunga akielezea kwa waandishi wa habari  jinsi Serikali inavyodhibiti wizi wa Dawa kwa kuweka nembo maalumu ambapo hadi sasa tayari dawa 20 zimewekewa nembo hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa shughuli za Kanda na Huduma kwa wateja  Bohari ya Dawa Bw. Edward Terry.


  =======  ======
  Na Frank Mvungi-Maelezo

  Serikali yajipanga kuhakikisha upatikanaji wa dawa unakuwa wa uhakikika katika hosipitali zote za umma hapa nchini.

  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa shughuli za Kanda na Huduma kwa wateja wa Bohari ya dawa (MSD) Bw.Edward Terry  wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

  Akieleza Terry amesema kwa hivi sasa Bohari ya Dawa imejipanga vizuri kuhakikisha kuwa dawa zinafika kwa wakati katika  maeneo yote zinakohitajika  kwa kuweka mfumo mzuri unahakikisha kuwa  dawa zikifika  zinatumika kwa wananchi waliokusudiwa .

  Akieleza Zaidi Terry alisema kuwa mnamo mwaka 2010 walifanya majaribio ya utaratibu wa kupeleka dawa moja kwa moja kwenye vituo vya afya ambapo utaratibu huu umeonyesha mafanikio makubwa hivyo ni imani ya Bohari ya Dawa kuwa utaratibu huo utasaidia sana kuondoa tatizo la upatikanaji wa dawa hasa maeneo ya vijijini.

   Kwa upande wa Kudhibiti upotevu wa dawa katika vituo vya Afya na Hosipitali Terry amesema dawa zinazotolewa na Serikali zitakuwa na alama maalum ya kuzitofautisha na zile zinazouzwa katika maduka binafsi ili kuondoa tatizo la wizi wa dawa zinazosambazwa na Bohari ya Dawa hapa nchini.

   Kuhusu Faida za  kuweka alama maalum katika dawa za Serikali Terry amesema utasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa  malalamiko ya wananchi kuhusu upatikanaji wa dawa mara wanapahitaji huduma hiyo katika hosipitali au vituo vya afya kwa kuwa tatizo la wizi  litakoma.

  Kwa wale watakaobainika kujihusisha na wizi wa dawa za Serikali  ,Terry amesema hatua kali zitachukuliwa  bila kuwaonea haya na kutoa wito kwa wananchi kuwafichua wale wote wanaojihusisha na wizo huo ili mkondo wa sheria uchukue nafasi yake.

  Bohari kuu ya Dawa imefungua kituo cha Kusambaza Dawa cha Muleba ,Mkoani  Kagera kitakachosaidia kuwahudumia wananchi wa Mkoa wa Geita na Kagera kwa kuwasogezea huduma hiyo karibu.

  0 0

  Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Maji Moto kwenye uwanja wa kijiji hicho mapema jana jioni,Wilayani Mlele mkoani Katavi.

  0 0


   Katibu Mkuu wa CC,Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe na kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa nyumba 60 za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),katika kijiji cha Inyonga ndani ya Wilaya Mpya ya Mlele mkoani Katavi mapema leo jioni.
    Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),mkoa wa Katavi,Bwa.Nehemia Msigwa akifafanua zaidi kuhusiana na mradi huo kwa katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mara baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa nyumba 60 za Shirika hilo,katika kijiji cha Inyonga ndani ya Wilaya Mpya ya Mlele mkoani Katavi leo.
   Meneja Huduma kwa jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),makao Makuu jijini Dar,Bwa.Muungano Sagaya akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Ujumbe wake  kwenye uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa nyumba 60 za Shirika hilo,katika kijiji cha Inyonga ndani ya Wilaya Mpya ya Mlele mkoani Katavi mapema leo jioni.
   Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),mkoa wa Katavi,Bwa.Nehemia Msigwa akizungumza mbele ya mgeni rasmi,katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kabla ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa nyumba 60 za Shirika hilo,katika kijiji cha Inyonga ndani ya Wilaya Mpya ya Mlele mkoani Katavi mapema leo jioni.
   Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mh.Rajab Rutengwe akizungumza jambo kabla ya katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa nyumba 60 za Shirika hilo,katika kijiji cha Inyonga ndani ya Wilaya Mpya ya Mlele mkoani Katavi mapema leo jioni.
   Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),mkoa wa Katavi,Bwa.Nehemia Msigwa akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mh.Rajab Rutengwe kabla ya katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa nyumba 60 za Shirika hilo,katika kijiji cha Inyonga ndani ya Wilaya Mpya ya Mlele mkoani Katavi mapema leo jioni.   Katibu Mkuu wa CC,Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),mkoa wa Katavi,Bwa.Nehemia Msigwa kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa nyumba 60 za Shirika hilo,katika kijiji cha Inyonga ndani ya Wilaya Mpya ya Mlele mkoani Katavi mapema leo jioni.
  ========  ======  =====

  KATIBU Mkuu wa CCM amelipongeza Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), kwa kasi ya ujenzi miradi ya nyumba za makazi na biashara kwenye miji mbalimbali hasa makao makuu ya wilaya mpya.

  Kinana aliyasema hayo katika mji wa Inyonga wilayani Mlele mkoa wa Katavi wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba 60 za shirika hilo.

  Alisema uongozi mpya wa NHC umerudisha heshima na hadhi ya shirika hilo kwa kufanya kazi ambazo inapaswa kuzitekeleza.Kwa mujibu wa Kinana, katika kipindi cha karibuni NHC, imekuwa ikitekeleza kwa kazi miradi ya ujenzi wa nyumba za viwango mbalimbali ambazo ni muhimu na kimbilio la watu wa kipato cha chini.

  "Hii ndio kazi inayopaswa kufanywa na shirika la nyumba ambalo ni tegemeo la wananchi. CCM inatambua kazi mnayoifanya inakupongezeni na kuungeni mkono katika kutekeleza majukumu yenu," alisema.

  Akizungumza kuhusu kilio cha kutaka kupunguziwa kodi kwenye vifaa vya ujenzi vya shirika hilo, Kinana alisema hoja hiyo ni muhimu na inayopaswa kusikilizwa na kupewa kipaumbele kwa lengo la kuwasaidia watu wa kipato cha chini.

  "Naona hapa kuna hoja ya msingi kwa kuwa hakuna sababu ya kutoza kiwango kibwa cha kodi kama nyumba zinazojengwa zinawasaidia watu wa kipato cha chini wakiwemo watumishi wa umma wenye mishahara midogo," alisema.

  Kwa upande wake, Meneja wa NHC mkoa wa Katavi, Nehemia Msigwa, alisema nyumba hizo 60 zitajengwa kwa kipindi cha miezi minane.

  Alisema zitakapokamilika, nyumba hizo zitauzwa kwa bei tofauti huku ya juu ikiwa ni sh milioni 54 na ya chini sh milioni 38.

  Msigwa alisema nyumba hizo ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa NHC kujenga nyumba 15,000 kwa kipindi hadi mwaka 2015.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Ghalib Mohamed Bilal akipata maelezo ya Historia, Muundo, Kazi na Utendaji wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Afisa Habari wa Bunge Bw. Prosper Minja wakati kiongozi huyo alipotembelea banda la Bunge lililopo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja leo lijini Dar es Salaam. Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni miongoni mwa washiriki wa maonesho ya maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano. Taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi zinashiriki katika kuonesha mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika kipindi cha Miaka 50 Muungano.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Maalim Seif Shariff Hamad (kulia) akisaini Kitabu cha Wageni Mashuhuri alipotembelea banda la Ofisi ya Bunge lililoko katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam wakati wa maonesho ya maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano. Picha na Prosper Minja - Minja

  0 0

  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Wasioona Malangali Mwl. Orthor M. Mkangara akitoa maelezo mafupi ya shule hiyo iliyoanzishwa rasmi mwaka 1998 ambapo mpaka hivi sasa ina jumla ya wanafunzi 71 wengi wao wakiwa wasioona na baadhi wakiwa ni walemavu wa ngozi "Albinism". Alisema kwa sasa shule hiyo inahitajio kubwa na vifaa vya kufundishia pamoja na usafiri kwa ajili ya kurahisisha shughuli mbalimbali shuleni hapo. 

  Alisema kuwa zipo changamoto nyingi shuleni hapo ambapo wadau mbalimbali wanakaribishwa katika kusaidia kuzitatua. Aliwashukuru kikundi cha kinamama kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa (pichani kushoto) kwa msaada waliotoa na kuomba wadau wengine kuwa na moyo kama huo katika kusaidia watoto wenye ulemavu hapa nchini. 
  Katibu wa Kikundi cha Kinamama Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa Bi. Joyce Mwanandenje akizungumza kwa niaba ya umoja huo ambapo alisema lengo la ujio wao Shuleni hapo ni kutimiza desturi yao ya kila mwaka ambapo hutembelea makundi ya wahitaji mbalimbali katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani. Katika salam zao shuleni hapo walitoa msaada wa magodoro 20, Sukari, sabubi na zawadi mbalimbali kwa aijili ya wanafunzi. Kikundi hicho cha Kinamama Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa kinaundwa na watumishi wanawake kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Hazina Ndogo, Ukaguzi wa Ndani, Chuo Kikuu Huria na Baraza la Nyumba na Ardhi Mkoa.
  Baadhi ya wanafunzi shuleni hapo wakiimba wimbo mwanana wa kuwakaribisha kikundi cha kinamama Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa walipofika shuleni hapo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilali leo Aprili 16, 2014 ametembelea viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kujionea maonesho ya Miaka 50 ya Muungano yanayoendelea katika vuiwanja hivyo. Miongoni mwa mabanda aliyotembelea ni banda la Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) na pichani ni Makamu wa Rais akikaribishwa bandano hapo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Asangye Bangu.
   Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilali akisalimiana na watumishi wa HESLB mara baada ya kufika bandani haopo na kupokea maelezo ya shughuli za HESLB ikiwa ni mafanikio, matarajio na changamoto mbalimbali zinazowakabili na jinsi wanavyo jitahidi kukabiliana nazo.
   Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Asangye Bangu akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais, Dk. Mohamed  Gharib Bilali juu ya shughuli za bodi wakati alipotembelea banda la Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu  (HESLB) lililopo katika viwanja vya Mnazi mmoja yanapofanyika maonesho ya Miaka 50 ya Muuungano Dar es Salaam leo.
   Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilali akitoa neno wakati alipotembelea banda hilo.
  Baadhi ya watumishi wa Bodi ya Mikopo wakiwa bandani hapo kusubiri wananchi wawape maelezo ya shughuli zao na nini mtu akifanye apate mkopo.

  0 0

   Mgeni rasmi Sarah Shibelea akifungua kongamano
   Kaimu Mkurugenzi wa VETA mkoa wa Dar es Salam Mrs.Bernadeta Ndunguru akisisitiza jambo baada ya mgeni rasmi kumaliza kufungua kongamano
   Msherehehaji wa Kongamano hili Bwana Mongele
  Wakuu na wamiliki wa vyuo vya ufundi stadi  kanda ya Dar es Salaam
   Mgeni rasmi Sarah Shibelea akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu na wamiliki wa vyuo vya ufundi stadi  kanda ya Dar es Salaam
  Mgeni rasmi Sarah Shibelea akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu na wamiliki wa vyuo vya ufundi stadi  kanda ya Dar es Salaam.Kongamano la Wakuu na wamiliki wa vyuo vya ufundi stadi  kanda ya Dar es Salaam inayolenga kupata maoni ya wadau juu ya utekelezaji wa mafunzo ya ufundi stadi lililoendeshwa na ofisi ya VETA Kanda ya Dar es Salaam.

  0 0

  KAMATI ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka imetangaza vituo vitakavyouzwa tiketi kwa ajili ya tamasha hilo kwa mkoa wa Dar es Salaam.

  Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama tiketi hizo zitauzwa katika vituo vitano kwa lengo la kupunguza usumbufu kwa mashabiki wenye nia ya kushiriki tamasha hilo.

  Msama alitaja vituo vitakavyouzwa tiketi hizo ni pamoja na Puma Mwenge na Uwanja wa Ndege, Best Bite Namanga, BM Kinondoni  na ofisi za Msama Promotions Kinondoni.
  Aidha Msama alitoa wito kwa waumini na wadau mbalimbali wa tamasha hilo kujitokeza kwa wingi kujipatia tiketi ambazo zitafanikisha kuhudhuria.

  Msama aliweka bayana viingilio ni shilingi 20,000 kwa viti maalum, VIP ni shilingi 10,000, kawaida ni shilingi 5000 na watoto ni shilingi 2000.

  0 0

  Na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Dodoma
  Hii ni baada ya washindi watatu kutoka Kanda ya Kati kupatikana katika shindano la kusaka vipaji vya kuigiza lililoendeshwa na Kampuni ya Proin Promotion Limited (PPL). Fainali ya kuvisaka vipaji kwa kanda ya Kati  ilifanyika jana Mnamo tarehe 15 April 2014 Mkoani Dodoma na washindi kutangazwa na Jaji Mkuu wa shindano hilo, Roy Sarungi aliyesaidiwa na Yvonne Chery ‘Monalisa’ na Single Mtambalike ‘Richie Richie.’

  Roy kwa kusaidiana na Yvonne Chery ‘Monalisa’ na Single Mtambalike ‘Richie Richie.’ aliwatangaza Joyce Rebeca, Moses Obunde na Mwinshehe Mohamed kuwa washindi wa shindano la kusaka vipaji vya kuigiza Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents ambapo kila mmoja alipewa zawadi nono ya Sh 500,000. Shindano hilo liliwashirikisha washiriki 500, lakini ni washiriki watano wenye vipaji waliofanikiwa kuingia tano bora na baadaye majaji walifanya kazi kubwa ya kuwachagua na kuwatangaza washindi watatu.

  Mshiriki mkubwa kuliko wote , Idrisa Ally  (40), alionesha kipaji cha hali ya juu cha kuigiza na alizawadiwa na majaji Sh 100,000. Idrisa hatakwenda kushiriki fainali za mashindano hayo zinazotarajiwa kufanyika Agosti mwaka huu jijini Dar es Salaam kutokana na umri wake kuwa mkubwa kuliko kigezo cha umri kilichowekwa cha kuanzia miaka 14 hadi 35, ingawa majaji waliahidi kuwasiliana naye kwa lengo la kuendeleza kipaji chake umri wake utakaporuhusu.

  “Tumebaini kuwa Kanda ya Kati hususani Mkoa wa Dodoma kuna vipaji vingi vya sanaa ya uigizaji na katika hili Idrisa Ally ametuthibitishia yeye ni mzee mwenye kipaji, lakini amedhihirisha kuwa ana kipaji cha kuigiza,” anasema Jaji Mkuu wa shindano hilo, Sarungi anasema sanaa ya uigizaji ni muhimu kwa vijana, kwa vile sasa hutoa fursa ya ajira ambapo imewawezesha vijana wengi nchini kujiajiri wenyewe na kuimarika kiuchumi.

  “Ni matumaini yangu kuwa kwa washindi hawa wa Kanda ya kati hawataishia hapa watajiendeleza zaidi kwani uigizaji sasa ni ajira,” anasema. Mshiriki Moses Obunde  alishindwa kuzuia furaha yake baada ya kutangazwa mshindi, aliangua kilio kuashiria furaha aliyokuwa nayo na kuufanya ukumbi mzima kutaharuki.


  Ofisa Uhusiano wa Proin Promotion Limited (PPL), Josephat Lukaza, ambao ndio waratibu na waandaaji wa shindano hilo la kusaka vipaji vya uigizaji, anasema mashindano hayo yanaendeshwa kikanda, ambapo kwa kuanzia walianza kusaka vipaji kwa Kanda ya Ziwa na Kumalizika Jana katika Kanda ya kati Mkoa wa Dodoma na hatimaye zoezi hili kuamia Kanda ya Juu Kusini ambapo usaili utafanyika Mkoani Mbeya kuanzia tarehe 19 April.

  “Baadaye tutaelekea Kanda ya Njanda za Juu Kusini lakini tunashukuru kwa ushirikiano tulioupata kwa wakazi wa Kanda ya Kati, tumepata washiriki 600, ambao tuliwachuja hadi kuwapata washindi watatu waliokidhi vigezo tulivyovihitaji,” anasema Lukaza. 

  Baadhi ya vigezo kwa mujibu wa Lukaza, vilikuwa ni mshiriki kuwa na umri kuanzia miaka 14 hadi 35, anayejiamini, mbunifu, anayemiliki jukwaa na igizo lake libebe ujumbe wa kuelimisha. Anasema lengo la PPL kuzungukia kanda hizo sita nchini ni kuhakikisha kuwa inavisaka vipaji vya vijana kupitia sanaa ya maigizo, ambavyo vimejificha ili viendelezwe na kampuni yake. 

  “Tumeamua kuwekeza katika sanaa maana sanaa ni fursa kama zilivyo fursa zingine nchini na ni matumaini yetu kuwa jamii itatuunga mkono katika safari ndefu tuliyo nayo ya kuvisaka na kuviendeleza vipaji,” anaeleza ofisa huyo uhusiano. Anasema PPL inaendesha shindano hilo kwa kanda sita nchini ambazo ni Kanda ya Ziwa, Magharibi, Pwani, Kati, Kaskazini na Kusini.

  “Kwa sasa tumeanza na mikoa sita, lakini matarajio yetu ya baadaye ni kuifikia mikoa yote nchini ambapo tunaamini kuna vipaji vingi vya wasanii vimejificha ili waweze kupata ajira kupitia vipaji vyao,” anasema na kuongeza kuwa mshindi wa jumla baada ya mashindano ya kikanda kumalizika atapatikana Agosti mwaka huu jijini Dar es Salaam, ambako ataondoka na zawadi nono ya Sh milioni 50.

  Anasema usakaji vipaji hivyo huendeshwa kwa umakini na umahiri mkubwa kupitia kwa majaji na watu wenye utalaamu wa tasnia ya filamu na teknolojia ya habari (IT) walio chini ya kampuni yake, ambao pia huzingatia miiko na maadili ya kazi hiyo kwa kila mshiriki. Anasema PPL imesajiliwa rasmi mwaka 2013 kupitia Sheria ya Usajili wa Makampuni ambayo hushughulika na ukuzaji wa sanaa ya filamu nchini.

  “Pia tunashughulika na usimamizi wa uzalishaji wa filamu nchini, uzalishaji na usambazaji wa DVD na filamu zilizokamilika kuingia sokoni na matarajio yetu ya baadaye ni kuwa kampuni bora katika Bara la Afrika,” anaeleza. Wakizungumza na gazeti hili, washindi waliobuka kidedea waliwashukuru waandaaji wa shindano hilo kwa kuibua vipaji vyao ambavyo wanasema visingeweza kutambulika.

  Crecensiah anasema anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumwibua katika shindano hilo na kumwezesha kuwa mshindi, ambapo sasa anaamini kuwa ndoto yake ya kuwa msanii wa kimataifa imetimia. “Namshukuru Mungu kwa yote, lakini zaidi niwashukuru waandaaji wa shindano hili kwa kutumia muda wao na fedha kuvisaka vipaji, binafsi naona kiu yangu ya kuwa muigizaji wa kimataifa imetimia, nitaongeza juhudi kubwa katika tasnia ya filamu,” anasema msanii huyo. Naye Janeth anasema penye nia pana njia, kwa madai kuwa alikuwa na kiu ya kuwa msanii wa kuigiza kwa muda mrefu hasa baada ya kuwaona wasanii mbalimbali kupitia luninga nchini.

  “Kwa kweli naweza kusema nimepata maji ya kunywa dhidi ya kiu yangu ya kuwa msanii, ni kazi ambayo nilikuwa naipenda tangu nikiwa mtoto namshukuru sana Mungu na waandaaji wa shindano hili la kusaka vipaji vya kuigiza,” anaeleza mshindi huyo. Kwa upande wake, Joshua Wambura anasema ushindi wake ni mwanzo wa safari yake ndefu katika kuingia katika tasnia ya filamu ndani na nje ya nchi.

older | 1 | .... | 270 | 271 | (Page 272) | 273 | 274 | .... | 1898 | newer