Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 266 | 267 | (Page 268) | 269 | 270 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe akiongea na katika ubalozi wa Tanzania nchini Marekani  mjini Washington DC, Marekani, ambako atapokea tuzo ya Africa’s Most Impactful Leader of the Year kwa niaba ya Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania mjini humo leo. PICHA NA IKULU.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amechaguliwa kuwa Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi katika Maendeleo Barani Afrika kwa mwaka 2013 .  Heshima hiyo kwa Rais Kikwete imetolewa na jarida maarufu la kimataifa la African Leadership Magazine Group na Tuzo la heshima hiyo itatolewa jioni ya kesho, Jumatano, Aprili 9, 2014, katika sherehe iliyopangwa kufanyika Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C ikiwa ni pamoja na chakula cha jioni.  Tuzo hiyo itapokelewa kwa niaba ya Rais Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe, ambaye tayari amewasili mjini Washington kwa sherehe hiyo kubwa.  Tuzo hiyo ya heshima kubwa hutolewa kwa viongozi wa Afrika ambao hutoa mchango mkubwa zaidi wa kiuchumi na kijamii kila mwaka kwa watu wao na limetolewa kwa Rais Kikwete kwa mwelekeo wake usiokuwa wa kawaida na wenye mafanikio makubwa kwa masuala ya utawala bora.  Jarida hilo linasema kuwa ukweli wa hali hiyo bora ya utawala bora chini ya  uongozi wa Rais Kikwete umeendelea kumiminiwa sifa kimataifa na leo umeifanya Tanzania kuwa nchi ya kuigwa mfano kama kituo cha uhakika cha uwezeshaji kutokana na mageuzi makubwa yaliyofanywa katika sera na mifumo ya uchumi.            Jarida hilo linasema kuwa Rais Kikwete alikuwa chaguo kubwa na la kwanza la wasomaji wa Jarida hilo ambao walipiga kura kupitia njia mbali mbali za mawasiliano za jarida hilo.  Linasema Jarida hilo, “Kuhusu maoni ya wasomaji wetu juu ya kiongozi yupi wa Afrika ambaye ni hodari zaidi kwa maendeleo ya kiuchumi na maendeleo, matokeo ya majibu ya swali hilo yamedhihirisha bila shaka yoyote kuhusu nafasi ya Rais Kikwete katika uongozi wa nchi yake. Na ushahidi uko kila mahali – ameweza kusimamia uchumi ambao umekuwa kwa wastani wa asili mia saba kwa miaka yote ya uongozi wake.”   Sherehe za kesho, miongoni mwa mambo mengine, zitaliwezesha Jarida hilo kutangaza mafanikio ya Tanzania chini ya uongozi wa Rais Kikwete kwa Jumuia ya Kimataifa, ikiwa ni pamoja na Jumuia ya Kimataifa ya Kibiashara, wanadiplomasia na taasisi nyingine zenye ushawishi mkubwa katika medani za kimataifa na zenye makao yake katika Jiji la Washington na maeneo ya jirani.

           

  Imetolewa na:

                                              Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu,


  DAR ES SALAAM.  0 0


  VURUGU na kampeni chafu zinazofanywa na baadhi ya makada wa CCM wanaojipanga kuwania ubunge katika jimbo la Tarime, zimechukua sura mpya.


  Hatua hiyo imetokana na mbunge wa jimbo hilo Nyambari Nyangwine (pichani), kuweka bayana kuwa atawasilisha malalamiko kwa uongozi wa CCM ngazi ya wilaya, mkoa na taifa.

  Juzi, baadhi ya wanachama wa CCM wilayani Tarime, walilalamikia kampeni chafu  zinazofanywa na baadhi makada na kusababisha makundi ambayo ni hatari kwa Chama.

  Hata hivyo, baadhi ya makada hao ambao baadhi wametajwa kuungwa mkono na baadhi ya viongozi wa CCM wilayani humo, wamekuwa wakieneza siasa chafu za ukabila, jambo ambalo limeelezwa kuwa ni hatari.

  Makada hao ambao baadhi walishindwa kwenye kura za maoni, ambapo sasa wameanza kujipanga upya lakini wakitumia njia ambazo ni kinyume na taratibu za CCM.

  Taarifa ya Nyangwine kwa vyombo vya habari jana, imesema kuwa atawasilisha malalamiko yake ikiwa ni pamoja na kuwataja kwa majina makada hao.  Imesema kuwa makada hao wamekuwa wakieneza siasa za chuki zenye lengo la kukwamisha utekelezaji wa Ilani ya CCM.  Hata hivyo, alisema kamwe hatishwi na makada hao kwa kuwa baadhi waligombea mara kadhaa na kushindwa hivyo jimbo hilo kutawaliwa na wapinzani kwa miaka 10.

  Alisema CCM ni chama chenye demokrasia na kinajali haki za kila mwanachama katika kuwania uongozi, lakini kina taratibu zake ambazo ni lazima zifuatwe ikiwa ni pamoja na kusbiri muda mwafaka wa kufanya kampeni na si kuwahujumu waliopo madarakani.

  “Nitawasilisha malalamiko yangu rasmi kwa uongozi wa chama ngazi zote hadi kwa Katibu Mkuu wetu (Abdulrahaman Kinana), sasa hivi ni wakati wa kutekeleza Ilani za Chama kwa wananchi si kufanya kampeni ili kukwamisha kazi.

  “Waniache nitumikie wananchi walionichagua na muda ukifika waje tupambane kwa hoja ndani ya Chama, haya wanayoyafanya sasa hivi ni uhuni na kutaka kurejesha makundi ambayo mwisho wa siku yatakigharimu chama chetu.

  “Baadhi ya wanaoendesha siasa hizi chafu ni wanasiasa ambao wameishiwa sera na goigoi na ndio sababu wameshindwa mara kadhaa kwenye uchaguzi,” alisema Nyangwine kwenye taarifa yake.

  0 0
  0 0

  WAKATI mpinzani wa Bondia Francis Cheka, Gavad Zohrevand, anawasili nchini kesho, mpinzani wa Francis Miyeyusho, Agelito Merin, atawasili leo kwa ajili ya pambano lao litalaofanyika Jumamosi kwenye Ukumbi wa PTA, Dar es Salaam. Mratibu wa pambano hilo, Mussa Kova, alisema kuwa bondia huyo atawasili majira ya saa 9, alasiri, kwa kutumia ndege ya Emirates, akitokea nchini Iran.

  Kova alisema Merin, ambaye ni mpinzani wa Miyeyusho atawasili saa moja
  asubuhi kwa ndege ya Qatar. Alisema kila kitu kipo vizuri ambapo mabondia hao tayari wameshatumia tiketi zao za kuja nchini, kwa ajili ya pambano hayo. "Kila kitu kinaendelea vizuri ambapo wapinzani wao wote wapo njia, ambapo mpinzani wa Cheka atawasili Jumatano na wa Miyeyusho atawasili siku ya
  Alhamis"alisema Kova.

  Pia Kova alisema licha ya kuwepo na mapambano hayo kuwakuwa na
  mapambano mengine mawili ya utangulizi. Kova alisema moja ya pambano litakuwa kati ya Cosmas Cheka na Ibrahim Clasic, ambapo pambano hilo litakuwa la ubingwa wa Taifa, litakuwa la raundi 10. Pambano la Miyeyusho ambalo litakuwa na ubingwa wa Dunia wa WBU lintakuwa la raundi 12, wakati la Cheka litakuwa na Kirafiki la Kimataifa litakuwa
  la raundi 8.

  0 0

  Exim Bank Tanzania Chief Finance Officer Mr. Selemani Ponda addresses a press conference to announce the bank’s financial performance for the year ended December 2013 in Dar es Salaam yesterday. The bank’s net profit increased by 21 per cent, giving them 20 Billion mark. Looking on is Assistant Marketing Manager Violet Bikoche (left), Head  of Risk and Compliance Mr. David Lusala (Second Left), Head of Treasury George Shumbusho (Second right) and Senior Finance Manager Issa Hamisi (Right). (Photo by our correspondent).

  Exim Bank Tanzania Chief Finance Officer Mr. Selemani Ponda addresses a press conference to announce the bank’s financial performance for the year ended December 2013 in Dar es Salaam yesterday. The bank’s net profit increased by 21 per cent, giving them 20 Billion mark. Looking on is Head  of Risk and Compliance Mr. David Lusala (Left), Head of Treasury George Shumbusho (Third left) and Senior Finance Manager Issa Hamisi (Right).
  Exim Bank Tanzania Head of Risk and Compliance Mr. David Lusala (Left) addresses a press conference to announce the bank’s financial performance for the year ended December 2013 in Dar es Salaam yesterday. The bank’s net profit increased by 21 per cent, giving them 20 Billion mark. Looking on is the bank’s Chief Finance Officer Mr. Selemani Ponda (Photo by our correspondent).
  ============   ============ 
  EXIM Bank Group, with operations in Tanzania and subsidiaries-Comoros and Djibouti has hit profit mark of TZS 20 billion as per recently signed audited results for 2013. This reflects 21% increase from TZS 16.5 billion reported last year.

  The Bank’s balance sheet grew by 18% from TZS 967 billion to cross a 1Trillion mark of TZS 1.14 Trillion, the fifth largest in Tanzania. Customer deposits grew modestly by 11% from TZS 723 billion to TZS 804 billion following a strategic decision to focus on low cost deposits. 

  Loan and advances portfolio recorded a growth of 23% from TZS 455 billion to TZS 559 billion, with disbursements well diversified to all sectors of the economy. Further, increase in value of investments available for sale and business profit resulted to a significant growth of the shareholders’ fund by 43% from TZS 109.4 billion to TZS 157 billion.

  The Exim Bank CFO, Mr. Selemani Ponda said that the impressive results and the on-going performance improvement demonstrated further potential growth of the Bank. “Last year we aggressively implemented growth strategies through mobilization of low cost deposits and operational efficiency that ensured customer satisfaction”, said the CFO.

  He added, “As a result of these strategies, fee-based income recorded a significant growth of 33% from TZS 22.8 billion last year to TZS 30.4 billion.”.The International Business demonstrated marked improvement with a strong performance of 26% pre-tax profit growth year on year of Exim Bank Comoros to TZS 3 billion, thus contributing 15% to the Group profit. The other subsidiary, Exim Bank Djibouti which was opened late 2011 showed improved business performance,  and expects to breakeven in 2014.

  “It's further heartening to mention that post a very healthy performance by Exim Bank Comoros during the year 2013, the Subsidiary declared a dividend equivalent of TZS 2 billion to be received by the parent Exim Bank Tanzania during the current year 2014,” stated Mr. Selemani. 

  During the year, net interest income grew by 1% from TZS45 billion to TZS 45.4 billion. Foreign exchange income posted a significant growth at 73% from TZS 4 billion to TZS 6.9 billion while other fees and commission recorded an increase of 24% from TZS 17.7 billion to TZS 22 billion. “We are excited with this trend in our performance reflecting growth in all our business segments. Our total operating income increased by 12% from TZS 67.7 billion to TZS 75.8 billion,” said the CFO, Mr. Selemani Ponda.

  “Total Operating expenses also went up by 17.8% from TZS 45.5 billion to TZS 53.6 billion attributed to new branches establishment costs and staff benefits in the efforts to widen geographical coverage and strengthen the Bank’s foundation. However, the cost to income ratio maintained at same level @ 73%” he added.

  As the result of recovery efforts and continued monitoring, the quality of the loan book significant improved during the year, where gross Non-performing assets to total gross loan ratio dropped from 14% to 9%. With a good profit posted during the year, the Return on equity (ROI) improved by 120 basis points from 15.21% to 16.41%.

  As it aspires to offer international standards banking services, the Bank scooped overall winner of top customer focused banks in Tanzania out of about 52 banks operating in Tanzania. Further, the training centre-“Exim Academy” got ISO certification in an endeavor to manage talents as well as part of staff retention strategy.   

  With opportunities in the economy, the Bank envisages great growth potentials in the future. In the recent 3-year strategic revalidation process carried out, the Bank will focus on continuous customer service improvements through pre-eminent payments and transactions banking in order to remain a preferred Bank for businesses.

  In conclusion the CFO said “The plan for 2014 is to continue streamlining operations efficiency by centralization of back office and automation solutions through alternative channels”.

  0 0

  SAM_0523
  Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wasioona (TLB) Mwalimu Greyson Mlanga(aliyesimama) akitoa somo juu ya Warsha ya Siku mbili ya Mkatabawa Umoja wa Mataifa Kwa Watu Wenye Ulemavu Mjini Ifakara hivi karibuni. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Hicho Wilaya ya Kilombero Maria Faya na Kulia ni Mwalimu Janet Kalalu, Mratibu wa Chama Wilaya.

  Henry Bernard Mwakifuna, Ifakara-Kilombero
  Watu wenye Ulemavu nchini Tanzania wametakiwa kushiriki katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo kwa muuujibu wa Uwezo wao.

  Akizungumza katika Warsha ya Siku mbili iliyofanyika Mjini Ifakara Wilayani Kilombero hivi karibuni Mwenyekiti wa Chama cha Wasioona (TLB) Taifa Mwalimu Greyson Mlanga amesema kuwa ni vyema watu wenye Ulemavu wakashiriki katika shughuli hizo ili kusaidia Jamiii kuondokana na Dhana ya kuwa Walemavu ni watu omba omba.

  Mwenyekiti huyo amesema kuwa ushirikiano wa Vyama vya Watu wenye Ulemavu ndiyo njia pekee ya kujikwamua katika maisha huku akisisitiza upatikananji wa Takwimu sahihi za Watu wenye Ulemavu ili ziweze kusaidia maendeleo ya Watu wenye Ulemavu.

  Katika Mafunzo hayo yaliyoshirikisha wadau mbalimbali wakiwemo Madiwani, Watendaji na Wawakilishi wa Vyama vya Watu wenye Ulemavu, Mwenyekiti huyo alielezea umuhimu wa kupata Elimu na kujua Haki za Watu wenye Ulemavu. Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Chama cha Wasioona (TLB) Wilaya ya Kilombero yameshirikisha Wadau kutoka Kata za Ifakara, Kibaoni, Kiberege na Kisawasawa yalifadhiliwa na Taasisi ya Foundation for Civil Society.
  SAM_0515
  Viongozi wa TLB Taifa Wakiungana na Viongozi wa TLB Wilaya ya Kilombero katika kuimba Wimbo wa Haki za Binadamu katika Mafunzo ya Siku Mbili yaliyowakutanisha Wadau mbalimbali, Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Wilaya ya Kilombero, uliofanyika hivi karibuni Mjini Ifakara. Kutoka Kushoto ni Maria Faya, Mwenyekiti wa TLB Wilaya ya Kilombero Maria Faya, Mwalimu Robert Bundala,Makamu Mwenyekiti Wasioona Taifa, Mwenyekiti wasiona Taifa Mwalimu Greyson Mlanga na Mratibu wa Wasioona Wilaya ya Kilombero Mwalimu Janet Kalalu.
  SAM_0541
  Washiriki wa Mafunzo ya Siku Mbili ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa Juu ya Watu Wenye Ulemavu wakiwa kwenye Picha ya pamoja na Viongozi wa Taifa wa Chama cha Wasiona (TLB) Mjini Ifakara Hivi karibuni.(PICHA ZOTE KWA HISANI YA HENRY BERNARD MWAKIFUNA WA IFAKARA).

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipokelewa kwenye wa uwanja shule ya Msingi Nyenge,Wilayani Kasulu mkoani Kigoma jioni ya leo
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia umati wa  watu katika Kijiji cha Nyenge, wakati wa ziara yake wilayani Kasulu leo ya kuimarisha  uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa  kufuata Ilani ya CCM. Kinana ambaye tayari ameshafanya ziara  mkoani Rukwa, hivi sasa ameanza ziara mkoani Kigoma. 
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia umati wa  watu katika Kijiji cha Nyenge, wakati wa ziara yake wilayani Kasulu leo ya kuimarisha  uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa  kufuata Ilani ya CCM. Kinana ambaye tayari ameshafanya ziara  mkoani Rukwa, hivi sasa ameanza ziara mkoani Kigoma
   Mbunge wa Viti Maalum CCM,Mh.Josephine Gezabuke akizungumza mbele ya umati mkubwa wa wanakijiji cha Nyenge wilayani Kasulu mkoani Kigoma jioni ya leo.
   Karanga zikitafunwa na mama nae kujipatia fedha 
   Mjumbe wa NEC,Balozi Ali Karume akiwa katikati ya akina mama wakiserebuka kwa pamoja,kwenye uwanja wa Tax Kasulu mjini mapema leo jioni mkoani Kigoma.
   Mambo ya Kasulu mjini hayo
   Haya zawadi ya mama kwa mgeni.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia umati wawatu mjini Kasulu, wakati wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayote kelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM. Kinana ambaye tayari ameshafanya ziara mkoani  Rukwa, hivi sasa ameanza ziara mkoani Kigoma.
   Baadhi ya maelfu ya Wananchi  wakiwa wamekusanyika kwenye uwanja wa Tax Kasulu mjini jioni ya leo wakati Katibu Mkuu wa CCM;ndugu Kinana alipowahutubbia kwenye mkutano wa hadhara
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia umati wa watu mjini Kasulu, wakati wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM. Kinana ambaye tayari ameshafanya ziara mkoani  Rukwa, hivi sasa ameanza ziara ya siku tano mkoani Kigoma.
   Mkuu wa Wilaya ya Kasulu,Mh Dan Makanga akijibu baadhi ya maswali kutoka kwa wananchi,kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo kwenye stendi ya Tax,Kasulu mjini mkoani Kigoma.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa na Baadhi ya Wanachama wapya waliojunga na CCM na kukabidhiwa kati.Kutoka kulia ni Katibu wa CHADEMA-SUA Wilayani Kasulu,Adolf Yanda pamoja na Mweyekiti wa Kijiji-CUF katika kata ya Rungwe Mpya,Nahoson Kigamba.CCM imekabidhi kazidi 500 za wananchama wapya walioamua kujinga na chama hicho cha CCM
   Baada ya kukabidhiwa kadi,wanakukula kiapo. 
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Ujumbe wake wakipata taarifa fupi za mradi wa maji katika kijiji cha Nyumbigwa. 
   Kinana akipta taarifa ya mradi huo mkubwa wa maji katika kijiji cha Nyumbigwa,wilayani Kasulu mkoani Kigoma
   Wanakijiji  wa Nymbingwa wakipita kando kando ya tanki la Maji lenye uwezo wa kubebe lita za maji  290,975 na kuwahudumia wananchi zaidi ya elfu 11.
   Katibu Mkuu wa CCM akipokelewa kwa shangwe na wanakijiji wa Nyumbigwa,alipokwenda kukagua mradi mkubwa wa maji kijijini hapo.
   Ndugu Kinana akishiriki Ujenzi wa Ofisi ya CCM pamoja na wananchi wa kijiji cha Magunga,wilayani Kasulu mkoani Kigoma jioni ya leo.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizindua ofisi ya  CCM,Tawi la Migunga kata ya Kurugongo Wilayani Kasulu jioni ya leo .
   Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana ukielekea kwenye kijji cha Nyenga kukagua miradi mbalimbali ikiwemo na kuwahutubia wanakijiji,jioni ya leo Wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
   Ndugu Kinana akikaribishwa na wanakijiji cha Nyumbigwa 


   Karibu Mgeni wetu Ndugu Kinana.

  0 0

  Warembo watakaoshiriki kwenye kinyang’anyiro cha kusaka malkia wa Tabata, Redds Miss Tabata 2014, watatambulishwa siku ya sikukuu Pasaka katika ukumbi wa Da West Park, Tabata. 

  Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga amesema jana kuwa utambulisho huo utaenda sambamba na uzinduzi wa Miss Tabata 2014. Kapinga alisema kuwa wapenzi wa urembo watapata fursa ya kuwaona warembo hao siku hiyo kabla ya kushiriki kwenye shindano la Redds Miss Tabata ambalo limepangwa kufanyika mwishoni wa mwezi ujao.  Katika uzinduzi huo warembo hao watasindikizwa na washiriki wenzao wa Miss Mzizima na Miss Ukonga.
  Pia watakuwepo viongozi waandamizi kutoka kamati ya Miss Tanzania ikiongozwa na Hashim Lundenga na Redds Miss Tanzania Happiness Watimanywa. 

  Kapinga alisema washiriki 21 wanaendelea na mazoezi ya Miss Tabata kila siku katika ukumbi wa Da West Park chini ya wakufunzi watatu - Neema Chaki, Pasilida Bandari na Bokilo.
  Warembo hao ni Esther Frank Kiwambo (20), Jemima Huruma Mawole (22), Badra S. Karuta (20), Mercy Mathias Kazula (19), Lydia Charles (22), Agnes Tarimo (18), Agnes Alex (20), Catrina Lawrence Idfonsi (20), Nuru Omary Athumani (19) na Happyclarrice Wilson Mbahi (19). 

  Wengine ni Annatolia Raphael (21), Mary Henry (21), Evodia Peter (22), Fatma Hussein Ismail (20), Ester Wilson Mbayi (20), Ambasia Lucy Mally (22), Faudhia Hamisi (21), Najma Charles Mareges (19), Lightnes Olomi (18), Husna Ibrahim (19) na Ramta Mkadara (20). 

  Warembo watano kutoka Tabata watashiriki kwenye shindano la kanda ya Ilala, Miss Ilala baadaye mwaka huu.  Mrembo anayeshikilia taji la Miss Tabata ni Noela Dorice Mollel ni Redds Miss Ilala. Miss Tabata inaandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts.

  0 0


  Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuingia makubaliano na kampuni ya Proin Promotions Ltd ya kutengeneza kazi zao kwa ubora zaidi. Kampuni hiyo tayari imetengeneza DVD ambazo huwezi kunakili kwa lengo la kupambana na wezi wa kazi za wasanii. kulia ni Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Evans Steven na Afisa Mauzo, Kaisi Masoud.
  =========  ========  =========
  BENDI ya muziki wa dansi nchini ya African Stars 'Twanga Pepeta', wameingia mkataba maalumu na kampuni ya Proin Promotions Limited kwa ajili ya utengenezaji wa kazi zao. 

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Twanga Pepeta, Asha Baraka, alisema mkataba huo una manufaa kwa bendi hiyo kutokana na kutaka kuwanufaisha wanamuziki na wasanii wa nchini kwa ujumla. 

  Baraka alisema kampuni hiyo ambayo awali ilikuwa ikijishughulisha na usambazaji wa kazi za filamu, imeamua kuingia mkataba na bendi yake kutokana na ubora wao. 

  Alisema wasanii nchini wanatakiwa kunufaika na kazi wanayoifanya, na Prain wameihakikishia Twanga kuwa kazi zao sasa zimetengenezwa kwa ubora wa hali ya juu kiasi cha kumshinda mtu yeyote kuirudufu. 
  "Tunataka maendeleo ya wasanii, tumekuwa tukiwakumbatia zaidi wasanii wa nje, lakini muunganiko wetu sasa utasaidia kuinua hali ya kipato sahihi kwa wanamuziki tulionao," alisema Baraka. 

  Kwa upande wake, Ofisa Masoko wa Prain Promotions, Evance Steven, alisema kampuni yao imeamua kuingia kwenye muziki na kuichagua Twanga Pepeta kuwa bendi ya kwanza kutokana na kazi yao wanayofanya katika burudani. 

  Steven alisema kazi kubwa waliyoanza nayo katika albamu ya Twanga Pepeta ya Dunia Daraja ni kuhakikisha kuwa haiwezi kunakiliwa (kurudufiwa) upya na maharamia wa kazi za kisanii nchini kama ilivyozoeleka. 

  "Tumewahakikishia wenzetu wa Twanga Pepeta kuwa kazi zao sasa ziko salama kuuzwa kihalali kutokana na kuziwekea programu maalumu ya kushindwa kunakilika, hivyo kila mtu atanunua kihalali kazi za bendi hii za Dunia Daraja," alisema ofisa huyo. 

  Twanga itaanza kuuza kazi hizo katika kila maonesho yao huku zikionekana kufungwa katika ubora wa hali ya juu alipokuwa akiwaonesha waandishi wa habari utofauti mkubwa uliofanywa na Proin, ambapo pia zina stika maalumu za TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania).

  0 0


  Kaimu Mkurugenzi Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Julius Mjanga akiwaeleza waandishi wa Habari(Hawapo Pichani) kuhusu Taaarifa za Upotoshaji kuwa matumizi ya mashine za kielektroniki(EFD’s) yamesitishwa ila mashine hizo zinaendelea kutumika kwa mujibu wa Sheria na wafanyabiashara wanapaswa kuendelea kuzitumia il kuisaidia serikali katika ukusanyaji wa Kodi. Kushoto ni Afisa Uhusiano Mkuu wa Mamlaka hiyo Bi Oliver Njunwa.
  Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria Mkutano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) leo Jijini Dar es Salaam.
  (Picha Hassan Silayo)
  ======  ========
  Na Frank Mvungi

  Serikali imekanusha taarifa za upotoshaji kuwa imesititisha matumizi  ya mashine za Kielektroniki ( EFD's) hapa nchini.

  Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Julius Mjanga wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

  Akieleza Bw. Julius amesema taarifa kuwa matumizi ya mashine za kielektroniki yamesitishwa ni upotoshaji na hayana ukweli wowote.

  Akifafanua zaidi Bw. Julius amesema kwa kuthibitisha kuwa taarifa hizo si za kweli kwani mnamo tarehe 26Februari 2014,Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda aliitisha kikao kati ya TRA,Wizara ya Fedha,Wizara ya Viwanda na biashara pamoja na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) .

  Bw. Julius alibainisha kuwa katika kikao hicho Mh. Waziri Mkuu alielekeza kuwa orodha ya wafanyabiashara walioainishwa na kupewa barua iwekwe wazi kwa kubandikwa katika ofisi zote za TRA za Mikoa na Wilaya.

  Pia Bw. Julius alisema kufuatia maelekezo hayo Mamlaka yaMapato Tanzania imeendelea kusimamia utekelezaji na usimamizi wa matumizi ya EFds unaoendelea na orodha ya wafanyabiashara husika ipo katika mbao za matangazo ya ofisi za TRA za Mikoa na Wilaya zote pamoja na kwenye tovuti.

  Aliongeza kuwa TRA inatoa wito kwa wafanyabiashara wote nchini wenye sifa za kutumia mashine za kielektroniki ambao ni wa lengwa katika awamu ya pili kuzitumia kama sheria inavyotaka.


  Bw. Julius aliwataka wananchi kutoa taarifa katika mamlka hiyo pale ambapo watatakiwa kutoa rushwa au kubugudhiwa wanapohitaji huduma katika ofisi za mamlaka hiyo kutoa taarifa katika vyombo vya dola au katika ofisi za TRA kupitia simu namba 0689122515 au ujumbe mfupi kwenye namba 0689122516.

  0 0
  0 0
  Mdau wa Mchezo wa ngumi nchini Jay Msangi kulia akiwa na bondia Sajjad Mehrabi wa Iran wa pili kushoto mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa jumatano wengine kulia ni rais wa PST Emanuel Mlundwa na promota Mussa Kova anae promoti mpambano wa cheka na bondia huyo wa Iran .

  Mdau wa mchezo wa masumbwi nchi Jay Msang kulia na Promota Mussa Kova wakibadilishana namba za simu na bondia Sajjad Mehrab mara baada ya kuwasili katika uwanja wa kumataifa ya Julius Nyerere kwa ajili ya mpambano wake na Fransic Cheka utakaofanyika April 12 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam
  Mdau wa mchezo wa masumbwi nchi Jay Msangi wa pili kulia na Promota Mussa Kova wakiongea na bondia Sajjad Mehrab mara baada ya kuwasili katika uwanja wa kumataifa ya Julius Nyerere kwa ajili ya mpambano wake na Fransic Cheka utakaofanyika April 12 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam kulia ni kocha wa bondia huyo wa Iran Lolal Shamlo Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

  0 0

   Mtaalamu kutoka TASAF Makao makuu Bi. Mercy Mandawa mwenye miwani na kompyuta mpakato akiandika baadhi ya mambo yaliyojitokeza kwenye mafunzo ya wawezeshaji ngazi ya wilaya mjini Dodoma.

   Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya namna ya kuendesha kazi yautambuzi wa kaya masikini ngazi ya halmashauri ya wilaya wakimsikiliza mtoa mada hayupo pichani katika ukumbi wa shule ya sekondari ya Dodoma.

   Mtoa mada katika mafunzo ya wawezeshaji ngazi ya Wilaya, Bw. Andrew Kibona akitoa mada kwenye mafunmzo hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa shule ya sekondari ya Dodoma.

  Washiriki wa mafunzo ya uwezeshaji wa mpango wa kunusuru kaya masikini katika manispaa ya Dodoma wakimsikiliza mtoa mada hayupo pichani juu ya namna ya kuzitambua kaya masikini .


  Mfuko wa Maendeleo ya Jamii,TASAF uimeanza  utekelezaji wa Mpango wa  kunusuru kaya masikini katika mikoa ya Dodoma, Singida ,Kigoma na Katavi ambako mafunzo kwa wawezeshaji wa Mpango huo ngazi ya halmashauri za wilaya yameanza kutolewa.


  Mpango huo utakaotekelezwa nchini kote kwa awamu, tayari umekamilika katika mikoa ya Lindi na Mtwara ambako kaya masikini zitaanza kupatiwa ruzuku kwa ajili ya kuboresha afya kwa mama wajawazito na watoto wenyer umnri wa  chini ya miaka 5, na kuziwezesha kaya husika kumudu gharama za elimu na matibabu kwa familia husika ili kuboresha maisha yao.


  Ruzuku hiyo ya fedha pia  inakusudiwa kuzijengea uwezo kaya masikini ziweze kuinua kipato  kwa kuanzisha shughuli za kiuchumi kulingana na mazingira ya eneo husika ili hatiomaye ziweze kuondokana na umasikini wa kipato.


  Akizungumza katika mkutano wa wawezeshaji ngazi ya taifa  mjini Dodoma, Bi Mercy Mandao amehimiza umuhimu wa kuendesha zoezi zima la utanmbuzi wa kaya masikini kwa uangalifu mkubwa ili hatimaye walengwa waweze kupatikana na kuondoa uwezekano wa kuwaacha walengwa kutokana na kutozingatia vigezo maalumu ambavyo huwekwa na wananchi wenyewe kwenye maeneo yao.  Zifiatazo ni picha za baadhi ya washiriki wa mafunzo ya wawezeshaji  katika manispaa  ya Dodoma yaliyoanza leo Jumanne . Mafunzo kaya hao yatolewa pia katika halmashauri zote za mikoa ya Singida, Kigoma, Katavi, Rukwa ,na Dodoma.


  0 0

  DSC_0070
  Meneja wa kituo cha Kahama FM Redio, Marco Mipawa, akiwakaribisha washiriki na kufungua warsha ya mafunzo ya siku nne ya waandishi wa habari na watangazaji wa Redio Jamii kuhusu kuandika taarifa za Maafa na Misaada ya Kibinadamu yanayofanyika mjini Kahama. Kushoto ni Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO Mama Rose Haji Mwalimu na kulia ni Hellen Msemo kutoka Mamamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA).

  Na Mwandishi Wetu.
  Ukosefu wa taarifa na lugha sahihi halikadhalika kukosa uelewa katika jamii ni miongoni mwa mambo yanayosababisha kutokea kwa maafa. Katika mada inayohusu Misaada ya Kibinadamu na Taarifa za Maafa katika mafunzo ya siku nne ya wanahabari na watangazaji wa redio jamii mjini Kahama Mratibu wa idara ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bwana Harrison Christopher Chinyuka alisema jamii lazima ifahamu historia ya maeneo yanapotokea maafa na wapate elimu ya kutosha ili waweze kuepusha maafa asili.

  Bwana Chinyuka alisema kwamba hilo litafanikiwa iwapo waandishi wa habari watawajibika kikamilifu kwa kuandika taarifa za majanga na maafa ambazo ni sahihi na kwa wakati kwa sababu wakati mwingine wamekuwa wakishindwa kutumia lugha sahihi ya kusheheneza taarifa husika.
  DSC_0137
  Mratibu wa Idara ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bwana Harrison Christopher Chinyuka Chinyuka, akiendesha mafunzo kwa waandishi na watangazaji wa Redio za Jamii nchini.

  “Wanahabari wana mchango mkubwa katika kuhakikisha kuwa madhara ya maafa yanapunguzwa kwa kuipa uelewa jamii husika kwa kutoa taarifa na lugha sahihi zinazohusu maafa ili kutoa nafasi kwa wahanga kujihami ipasavyo”, alisema Bwana Chinyuka.

  Wajibu wa mwandishi wa habari katika kupunguza maafa ni kukuza uelewa wa jamii kuhusu hatua za hatari, kuzuia na kukabiliana na maafa, kukubaliana juu ya viwango vya taratibu za uendeshaji katika sehemu ya maafa.

  Wajibu mwingine ni kusambaza ujumbe wa onyo kwa kuaminika na haraka iwezekanavyo na kuiweka jamii vizuri kitaarifa wakati huo huo kuepuka uvumi na hofu katika hali ya hadhari.
  DSC_0112
  DSC_0041
  Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO Mama Rose Haji Mwalimu, akihamaisha washiriki katika vikundi kazi.


  “Wajibu wenu waandishi wa habari kabla, wakati na baada ya maafa ni kutimiza jukumu la kulinda na kusaidia kuunganisha familia na kujenga kujiamini, sio kuachia mchakato njiani”, alisema Bwana Chinyuka.

  Madhumuni ya mafunzo hayo ni kutoa uwezo kwa waandishi wa habari na watangazaji wa redio jamii kuandika taarifa zinazohusu kutoa msaada wa kibinadamu na kupunguza madhara yatokanayo na majanga na maafa nchini katika mradi unofadhiliwa na shirika la maendeleo ya Sweden (SIDA) kwa kushirikiana na UNESCO.

  Mafunzo hayo yanatekeleza malengo ya UNESCO linalohusisha kuimarisha uwezo wa kukuza mazingira ya uhuru wa kujieleza kwa ajili ya maendeleo, kuendeleza demokrasia na utamaduni wa mazungumzo ya amani bila migogoro.
  DSC_0163
  Hellen Msemo kutoka Mamamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo.
  DSC_0125
  Mwandishi na mtangazaji kutoka kituo cha Redio O.R.S FM ya Simanjiro, Julius Laizer, akichangia maoni wakati wa mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa kushirikiana na UNESCO.
  DSC_0146
  Picha juu na chini ni sehemu ya washiriki wakifuatilia mafunzo hayo kwa umakini yaliyofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa kushirikiana na UNESCO.
  DSC_0189
  DSC_0019
  DSC_0132
  Mafunzo yakiendelea.

  0 0
 • 04/09/14--22:25: KINANA ANA KWA ANA NA KAGAME

 • Rais Paul Kagame wa Rwanda akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana katika mazungumzo yaliyofanyika katika Hoteli ya Serena, Mjini Kigali Rwanda, juzi. Picha na Edward J. Mpogolo ( Ofisi ya Katibu Mkuu).

  0 0

  Waziri Mkuu Pinda akisisiti jambo
  =======  ======== =======
  Serikali yaendelea kuhimiza matumizi ya mashine za EFDs nchini.


  Na Eleuteri Mangi -MAELEZO


  Nashawishika, natambua na nimejiridhisha kuwa elimu kwa mwanadamu ni mwanga na nuru ya maisha, mwanga huo ni silaha imara ya kuimarisha uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.


  Ujio wa mashine za kielekroniki za kutolea risiti za kodi (EFDs) nchini ni ukombozi wa ukusanyaji wa mapato ya nchi ambayo yalikuwa yakipotea na kulinyima taifa mapato kwa maendeleo yake, tofauti na mfumo wa zamani wa kukusanya mapato kwa risiti za vitabu vya mauzo.


  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliwahakikishia Wafanyabiashara na Watanzania kwa ujumla kuwa utaratibu wa kutumia Mashine za EFD ulianzishwa kwa lengo la kumrahisishia mfanyabiashara utunzaji wa kumbukumbu za biashara za kila siku pamoja na kuondoa usumbufu wakati wa ukadiriaji wa kodi. Kwa mantiki hiyo ni wajibu wa Serikali na taasisi inayosimamia mapato ambayo ni TRA kutoa elimu kwa wateja ambao ni wafanyabiashara wakubwa na wadogo juu ya mfumo mpya wa ukusanyaji kodi.

  Dhamira ya TRA katika Mpango mkakati wake wa Nne wa kukusanya mapato nchini ni “Kurahisisha ulipaji wa kodi na kuyafanya maisha yawe bora”. Kwa dhamira hiyo, TRA imekuwa ikiendesha kampeni za kuwahamasisha walipa kodi na jamii kwa ujumla umuhimu wa kutoa na kudai risiti sahihi za mashine za kielekroniki za kutolea risiti za kodi (EFDs).

  Kabla ya kuanza utekelezaji wa mfumo huu, elimu ilitolewa kwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kupitia vyombo mbalimbali vya habari pamoja na semina ambazo zilitolewa kwa makundi mbalimbali ya wafanyabiashara.


  Ni dhahiri kuwa elimu hiyo bado inaendelea kutolewa kwa njia mbalimbali ambapo kuhusu ununuzi wa mashine hizo kwa awamu ya pili, muda wa maandalizi ulisogezwa hadi Desemba 31, 2013 na taarifa ilitolewa na bado zinaendelea kutolewa kupitia vyombo vya habari.


  Aidha, Serikali kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali wa Sekta Binafsi inaendelea kutoa elimu kuhusu matumizi endelevu na faida za Mashine za EFD kwa wafanyabiashara na wanunuzi wa bidhaa na huduma mbalimbali za kijamii.  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda alipokuwa akihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Desemba 21, 2013 wakati wa kuhitimisha mkutano wa 14 wa Bunge hilo, alisema kuwa Serikali ililiarifu Bunge kuhusu mikakati mbalimbali itakayotekelezwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa lengo la kuimarisha ukusanyaji wa Mapato ya Ndani.


  Moja ya hatua hizo muhimu ni kuendelea kuimarisha matumizi ya Mashine za Kielektroniki za kutoa Risiti za EFDs. Mashine hizi zimeunganishwa kwa Mtandao wa Kompyuta moja kwa moja na Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa lengo la kuwezesha Serikali kupata mapato stahiki bila udanganyifu.

  Aidha, Mashine hizi zinasimamiwa kupitia Mtandao wa Kielektroniki ambapo hupeleka taarifa moja kwa moja kwenye hifadhi kuu ya kumbukumbu TRA kila siku. Kwa kuzingatia kuwa Wabunge ni wadau muhimu, Waziri Mkuu Pinda alitoa wito kwao na Viongozi wa ngazi zote kushirikiana na Serikali kuwaelimisha Wananchi na Wafanyabiashara kuhusu manufaa ya Mfumo huo wa Mashine za Kielektroniki ili kwa pamoja washirikiane kujenga uchumi wa nchi na kuleta maendeleo endelevu kwa kulipa kodi stahiki.

  Siku za hivi karibuni kumekuwa na upotoshwaji na uvumi kuwa matumizi ya mashine za EFDs yamesitihwa, Serikali tayari Aprili 9 mwaka huu ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari jijini Dare s salaam kuwa uvumi huo hauna ukweli wowote.


  Kwa dhihirisha kuwa mashine za EFDs bado utaratibu wake unaendelea, Februari 26, mwaka huu Waziri Mkuu Pinda alikaa na TRA, Wizara ya Fedha, Wizara ya Viwanda na Biasha pamoja na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na kutoa maelekezo ya Serikali kwa ajili ya utekelezaji.


  Maelekezo hayo yaliyotolewa ni pamoja na kutolewa orodha ya wafanyabiashara walioainishwa na kupewa barua iwe wazi kwa kubandikwa ofisi zote za TRA za mikoa na wilaya.


  Aidha TRA itoe tamko kupitia vyombo vya habari na kutangaza namba za simu zitakazotumika kutoa taarifa kwa vitendo vya rushwa na unyanyasaji wakati zoezi linaendelea.


  Jambo hilo la utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu Pinda limetekelezwa na TRA kama ilivyoelekezwa ambapo mpaka sasa tayari orodha ya wafanyabiashara zimekabidhiwa kwa wakuu wa mikoa na wilaya zote nchini.


  Kuhusu taarifa za vitendo vya rushwa na unyanyasaji, utaratibu huo umekamilika ambapo namba za simu 0689 122515 itatumika kwa kupiga simu endapo mteja atakutana na moja ya vitendo vilivyoainishwa na 0689 122516 imetolewa mahususi kwa kutuma ujumbe mfupi.


  Nia ya Serikali kwa kushirikiana na TRA ni kuendelea kuhamasisha na kuimarisha  matumizi na udhibiti wa Mashine za Elektroniki za kutoa stakabadhi za kodi (EFDs) na kutoa elimu kwa walipakodi na wafanyabiashara kuhusu matumizi ya mashine hizi.


  Walengwa katika mfumo huu wa kutumia mashine za kodi za kielektroniki ulianza kutekelezwa kwa awamu ambapo awamu ya kwanza ilianza mwaka 2010 ni wafanyabiashara waliosajiliwa kwenye kodi ya ongezeko la thamani, yaani VAT.


  Awamu ya pili ilianza kutekelezwa mwaka 2013 kwa kuzingatia Sheria ya kusimamia Kanuni ya Kodi ya Mapato ya mwaka 2012 (Income Tax Electronic Fiscal Devices Regulations) ambayo inawahusu wafanyabiashara ambao hawajasajiliwa kwenye VAT ambao mauzo ghafi kwa mwaka ni shilingi milioni 14 na zaidi kwa mwaka.

  Wafanyabiashara wasio rasmi aina ya Mama Ntilie na wale wanaotembeza bidhaa barabarani hawahusiki katika mpango wa kutumia mashine za EFD kwa sababu hawana sehemu maalum ya kufanyia biashara.

  Serikali imewataka wafanyabiashara hawa waendelee na shughuli zao na wala hawatabughudhiwa. Walioko kwenye mpango huu ni wale wenye biashara wenye mauzo ya milioni 14 na zaidi.

  Katika kunyambulisha, wafanyabiashara wanaotambuliwa katika mfumo huu wa ukusanyaji kodi, mfumo na sheria ziliainisha kuwa ni wenye biashara zifuatazo; wenye maduka ya vipuri, mawakili na maduka ya jumla (Sub wholesale shops).

  Wengine ni wafanyabiashara wakubwa wa Mbao, migahawa mikubwa, maduka ya simu na vipuri vyake, baa na vinywaji baridi, studio za picha, watoa huduma ya chakula (Catering Services), wauzaji wa pikipiki, wauza magari, maduka makubwa ya nguo na biashara zinginezo.

  Kwa Nchi nzima mfumo umewalenga wafanyabiashara 200,000 tu kwa awamu ya pili kati ya wafanyabiashara zaidi ya 1,500,000 ambao wamesajiliwa kulipa kodi.

  Uzuri wa mashine hizi zimemlenga mtumiaji moja kwa moja, wanunuzi na serikali ikizingatiwa mfanyabiashara ana faida anapotumia kwa kazi zake za kibiashara.

  Kitu chochote kinapoanzishwa huwa na faida na changamoto zake, miongoni mwa faida za Mashine za Kodi za Kielekitroniki ni kutoa risiti na ankara za kodi.

  Kwa kuwa sheria inamtaka kila mfanyabiashara anayeuza au kutoa huduma ya Tsh. 5,000 na zaidi atoe risiti, mfanyabiashara huyu mwanzoni alilazimika kuchapisha vitabu vya risiti mara zote, kwa kutumia mashine hizi anaondokana na uchapishaji wa vitabu ambavyo ni vingi na utunzaji wa nakala zake unaleta usumbufu.

  Mashine hizi zina uwezo mkubwa wa kutunza kumbukumbu za mauzo, manunuzi na mali ya biashara (Stock) bila kufutika kwa muda usiopungua miaka mitano na hivyo kuondokana na usumbufu wa kuchapisha vitabu vya risiti kwa kipindi hicho.

  Zaidi ya hapo mashine hizi zintumia lugha ya Kingereza na Kiswahili ambazo zinamrahisishia mtumiaji kuchagua lugha anayoitaka.

  Vile vile mtumiaji ana uwezo wa kutoa taarifa za mauzo kwa siku, wiki, mwezi na mwaka, kwa kipindi kisichopungua miaka mitano muda ambao mtumiaji hatahangaika ni namna gani atatunza kumbukumbu za biashara yake kwa uhakika bila kuhofia kuharibika kwa njia mbalimbali ikiwemo kuungua moto au kulowana kwa maji.

  Mfanyabiashara pia ana faida inayomuwezesha kupokea maelekezo moja kwa moja kutoka kwenye mfumo wa Mamlaka ya Mapato (TRA Server) kuruhusu kuziongezea uwezo wa hizi mashine wakati wowote bila kuathiri ufanyaji kazi wake.

  Faida nyingine kwa mtumiaji ni kutuma na kupokea ujumbe (SMS) kutoka kwenye mfumo wa Mamlaka ya Mapato. Hii huwezesha TRA kumtaarifu mtumiaji taarifa yoyote ya kodi inayomuhusu bila kuonana ana kwa ana njia ambayo imeondoa usumbufu kwa wateja kwa kupanga foleni ofisi za TRA kusubiri huduma.

  Kwa kuwa tupo kwenye ulimwengu wa sayansi na teknolojia mashine hiyo hiyo inaweza kutumika kutuma na kupokea fedha “mobile money” na kwa hiyo kumruhusu mtumiaji kuitumia kuongeza kipato zaidi au kulipa kodi na huduma zingine kama vile umeme, maji na huduma nyinginezo bila kupoteza muda kwenda kwenye ofisi husika.

  Kwa kuzingatia umuhimu wa kutunza kumbukumbu kwa wafanyabiashara nchini, TRA pamoja na watengenezaji na wasambazaji wa mashine za kielektroniki walijadiliana na kuafikiana kwamba bei za mashine ziuzwe kuanzia Sh. 600,000/= na ukomo uwe Sh. 778, 377 kwa kulinganisha na mauzo dola za Kimarekani  ambazo bei ya chini ya mashine za EFD nchini ni dola za Kimarekani 375 na   bei ya juu ni Dola za Kimarekani 487.

  Bei za mashine hizi hapa nchini zipo chini ukilinganisha na bei ya mashine katika nchi zinazotumia mfumo unaofanana na wa Tanzania.

  Nchi hizo ni pamoja na Italia, zinauzwa kwa bei ya chini kwa Dola za Kimarekani 870 na bei ya juu ni Dola 1,000, Rwanda, bei ya chini kwa dola za Kimarekani 800 bei ya juu ni dola za Kimarekani 830, Ethiopia, bei ya chini kwa Dola za Kimarekani 446 na bei ya juu ni Dola za Kimarekani 1,026.

  Nchi nyingine ni Serbia, bei ya chini ni Dola za Kimarekani 360 na bei ya juu ni dola za kimarekani 1,750 na Bulgaria bei ya chini ni Dola za Kimarekani 230 na bei ya juu ni Dola za Kimarekani 400.

  Ili kumrahisishia mfanyabiashara nchini anunue mashine hizi, TRA imeongea na wasambazaji ambao wamekubali kuuza mashine hizi kwa kupokea malipo kwa awamu iwapo wafanyabiashara watajiunga katika vikundi vitakavyopewa dhamana ya kuhakikisha wauzaji wanapata malipo yao.

  Kuhusu gharama za matengenezo kuwa kubwa, watengenezaji wametoa “warranty” ya miaka mitatu kwa mashine inayoharibika pasipo makusudi.

  Hivyo pale mashine inapoharibika mfanyabiashara anatakiwa kuwasiliana na mtengenezaji kwa ajili ya matengenezo. Wasambazaji wanawajibika kufunga mashine, na kutoa elimu bora ya matumizi ya mashine hizo. 

  Ni vyema wafanyabiashara wakaelewa kuwa sheria inamtaka kila msambazaji pamoja na kuuza mashine anawajibika kuzifanyia matengenezo mashine hizo. Hii itasaidia kudhibiti taarifa ambazo zimo ndani ya mashine.

  Ikumbukwe kuwa gharama zote za ununuzi wa mashine hizi zinarudishwa kwa wafanyabiashara pale watakapowasilisha mahesabu yao ya kodi. Hivyo kuifanya Serikali kulipia gharama za mashine kwa kupitia kodi ambayo itasamehewa pindi mfanyabiashara atakapowasilisha mahesabu.

   Kwa wajenga nchi wote ni vema tuitikie wito wa kujenga tabia ya kiungwana ya kila mwananchi kudai risiti kila anaponunua bidhaa au kupata huduma.

  Kwa kufanya hivyo, kama asipopewa risiti kodi hiyo inaingia mfukoni mwa mfanyabiashara maana haitowasilishwa TRA na hivyo kuikosesha serikali mapato ambayo yangesaidia miradi ya maendeleo ya taifa na kuboresha huduma za jamii kwa wananchi.

  Kwa kuwa mawasiliano ni njia pekee ya kupata taarifa, TRA kwa kutambua hilo imeanzisha mawasiliano ya simu yasiyo na malipo katika kituo cha huduma kwa wateja wake.

  Simu hizo ni 0786 800 000 kwa watumiaji wa Airtel, 0713 800 333 kwa watumiaji wa Tigo, 0800110016 kwa watumiaji wa Vodacom na TTC ikiongozwa na kauli mbiu “Pamoja tunajenga taifa letu”.

  Ili kuhakikisha kumbukumbu zipo sahihi karatasi zinatumika zinazojulikana kama “Thermal Paper” ni za kisasa na hazifutiki kwa urahisi na zina Alama za Siri ndani yake kwa ajili ya kuongeza usalama.

  Kwa kuzingatia ubora wa karatasi, zina uwezo wa kutoa wastani wa risiti kati ya risiti 200 hadi 1,000 kulingana na urefu wa “Paper Roll”! au bunda ambazo zinafaa kwa matumizi ya kila siku.

  Kwa kuzingatia umuhimu wa ukusanyaji wa mapato nchini, Manaibu Waziri wa Fedha Adam Malima na Mwigulu Nchemba kupitia ziara walizofanya walisema kuwa Serikali itaendelea kuwasisitiza wafanyabiashara kununua na kuzitumia mshine za EFD kwa maendeleo yao endelevu na ya taifa.

  Manaibu Waziri hao kwa nyakati tofauti walipoongea na wafanyabiashara wa mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza, Njombe, Ruvuma na Mbeya walisema kuwa mashine ya EFD zinawarahisishia wafanyabiashara kulipa kodi na kufanya biashara yenye tija na bora nchini.

  Kwa upande wao wafanyabiashara hao wamesema hawapingi kutumia mashine hizo za EFD lakini wakanung’unikia changamoto ya bei za mashine hizo na  wakidai zinawaumiza kwa kuwa ni kubwa zisizolingana na mitaji yao.

  Changamoto ambayo Kamishna wa Kodi za Ndani wa TRA Patrick Kasera alibainisha kuwa hiyo ni hofu waliyopandikizwa wafanyabiashara ambayo sio sahihi.

  Mchakato wa ununuzi wa mashine za EFD ulifanyika kwa uwazi kupitia tenda ya kimataifa na kila mtu alikuwa na uhuru kushiriki. Kati ya walioomba walipatikana wasambazaji 11 na sio mmoja au wachache kama inavyopotoshwa.

  Mchakato wa kuwapata wazabuni ulifuata Sheria ya Manunuzi ya Umma ya Mwaka 2004 inayotumika, na uligawanyika katika sehemu mbili kama ifuatavyo;

  Sehemu ya kwanza ilikuwa kuwapata watengenezaji wa Mashine; Tenda ya wazi ya Kimataifa (International bidding) ilitangazwa kupitia magazeti ya Daily News ya Agosti 10, 2012 na The East African ya Agosti 11-17, 2012.  Watengenezaji waliokidhi vigezo vilivyoainishwa ndio waliopata tenda.

  Sehemu ya pili ilikuwa kuwapata wasambazaji; Tenda ya wazi vile vile ilitangazwa kwenye gazeti la Daily News la Agosti 10, 2012 kwa wasambazaji wenye vigezo vinavyojumuisha; wajibu wa kufungua ofisi kila mkoa, mtaji usiopungua Shilingi za Kitanzania milioni 500, uzoefu wa kusambaza na kufanyia matengenezo mashine za kielektroniki kwa zaidi ya miaka miwili. Wasambazaji waliokidhi vigezo vilivyoainishwa ndio waliopata tenda. Ukweli ni kwamba bei za mashine hizo nchini ni ndogo ikilinganishwa na nchi nyingine duniani.

  Ili kuendelea kuwaelimisha wafanyabiashara nchi nzima, Serikali kupitia Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na TRA inatarajia kuendelea na ziara ya kutembelea vituo vikuu vya ukusanyaji mapato vilivyopo mipakani ikiwemo kanda ya kaskazini katika mikoa ya Arusha, Tanga na Kimanjaro kupitia mipaka ya Namanga, Horohoro na Holili.

  Zoezi hili la kutembelea maeneo mbalimbali nchini ni endelevu ambapo lengo lake ni kuhakikisha elimu inayotolewa inawafikia watanzania wote katika maeneo yao mahalia na watambue wajibu wao kwa nchi katika kukusanya mapato.


  Ni matumaini mema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazotumia mashine za EFD katika kukusanya mapato yake ya ndani kwa maendeleo endelevu ya uchumi wake.

  Miongoni mwa nchi ambazo zinatumia mahine za EFD duniani ni pamoja na Malawi, Rwanda, Ethiopia, Serbia, Italia na Bulgaria.


  Watanzania wote tuunge mkono juhudi za Serikali katika kukusanya mapato kwa kuzingatia kauli mbiu ambayo ndio dira, “Unapouza toa risiti, unaponunua dai risiti” na “Pamoja tunajenga taifa letu” iwe ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku yanayozingatia kujali maendeleo endelevu na ustawi wa watu wote nchini.

  0 0

  Na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Mwanza
  Hatimaye Kikosi Kazi cha Kampuni ya Proin Promotions Limited ambao ndio waratibu na waandaaji wa Mashindano ya Kusaka vipaji vya uigizaji Tanzania yajulikanayo kama Tanzania Movie Talents (TMT) kinaondoka leo asubuhi Mkoani Mwanza Kuelekea Mkoani Dodoma kwaajili ya kuendelea na shindano la kusaka vipaji vya kuigiza katika Kanda ya Kati.

  Ambapo mashindano yatafanyika Mkoani Dodoma katika Ukumbi wa African Dream kuanzia Jumamosi ya tarehe 12 April 2014 kuanzia Saa moja asubuhi hadi tarehe 15 April 2014, kabla ya mashindano hayo kufanyika Mkoani Dodoma mnamo Siku ya Ijumaa tarehe 11 April 2014 kutakuwa na Promo pati itakayofanyika katika Ukumbi wa Disco wa 84 Mjini Dodoma na Wasanii Lulu, Joti, Rich Rich, Monalisa na MC Pilipili watakuwepo ndani ya nyumba.

  Mashindano haya yatakuwa ni muendelezo wa mshindano yaliyoanza kufanyika katika Kanda ya ziwa Mkoani Mwanza ambapo Washindi watatu kutoka Mkoani Mwanza wakiwakilisha Kanda ya Ziwa wakiwa wameshapatikana na kila mshindi aliweza kupewa zawadi ya shilingi laki tano kila mmoja na kusubiria kwenda Mkoani Dar Es Salaam kwaajili ya kuungana na washindi wengine Wa kanda zilizobaki kwaajili ya Fainali kubwa itakayofanyika mkoani Dar Es Salaam   na mshindi katika Fainali hizo ataibuka na Kitita cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania pamoja na Mikataba minono kutoka Kampuni ya Proin Promotions Limited na washindi kumi bora watakaopatikana katika Fainali hiyo watacheza filamu ya kwao na hatimaye itauzwa Nchini Nzima.

  Katika Mashindano haya ya Kusaka Vipaji vya Kuigiza Tanzania yajulikanayo kama Tanzania Movie Talents yatajumuisha kanda ya Juu Kusini ambapo yatafanyika Mkoani Mbeya, Kanda ya Kaskazini ambapo usaili utafanyika Mkoani Arusha, Kanda ya Kati zoezi litafanyika Mkoani Dodoma, Kanda ya Kusini ambapoo usaili utafanyika Mkoani Mtwara, Kanda ya Pwani ambapo usaili utafanyika Mkoani Dar Es Salaam na hatimaye mashindano haya yakapewa upendeleo tena kufanyika Kanda ya Ziwa Mkoani Kigoma Kwa kuelewa kuwa Kigoma ni Mkoa ambao una wasanii wengi wa muziki wa bongo fleva na Proin Promotions Limited kutoa nafasi ya Upendelo kwa kuhisi pia wanaweza kupata Vipaji vya uigizaji Tanzania katika Mkoa Huo. Mshindi katika Fainali ya mwisho ataibuka na Shilingi Milioni 50 za kitanzania.

  Katika Mashindano haya Fomu zitapatikana siku ya Usaili na hakuna gharama zozote zile zitakazotozwa kwaajili ya usaili na tunawaomba Wakazi wa Kanda ya kati kujitokeza kwa wingi Mkoani Dodoma siku ya usaili na kuweza kuonyesha vipaji vyao maana hii ndio fursa pekee ambayo watanzania wanaipata kutoka Kampuni ya Proin Promotions Limited na hatimaye kuweza kutimiza ndoto zao za kuwa waigizaji katika tasnia ya filamu nchini .
  Shindano hili la Tanzania Movie Talents lina lengo la kusaka na kuibua Vipaji vya kuigiza na kukuza tasnia ya filamu nchini.

  0 0

  http://www.mjengwablog.com/habari-za-kijamii/item/10551-sikiliza-kipindi-cha-soko-la-habari-kariakoo.html#.U0Yo3VdQ7U4

  0 0

   Meneja wa Bia ya Serengeti Rodney Rugambo(wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa droo ya nane ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao mapema leo katika Kiwanda cha Bia cha Serengeti jijini Dar es Salaam kutoka kushoto Henry Martin, Bruno Thobias na Alex Vicent(wa kwanza kulia) ambao wamejipatia ving’amuzi na simu aina ya Samsung Galaxy Tablet. 
   Meneja wa Bia ya Serengeti Rodney Rugambo(kushoto) akiongea kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa droo ya tisa ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti wakati wa droo ya tisa iliyofanyika mapema leo jijini Dar es Salaam, anayemshuhudia ni Afisa Mwandamizi kutoka PWC Golder Kamuzora. 
  Meneja wa Bia ya Serengeti Rodney Rugambo(wa pili kulia) akitoa ufafanuzi wa jambo kwa wana habari mara baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa droo ya nane ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti mapema leo katika Kiwanda cha Bia cha Serengeti jijini Dar es Salaam kutoka kushoto ni Bruno Thobias,  Henry Martin na Alex Vicent (wa kwanza kulia).

  0 0

   Mwenyekiti wa Timu ya watoto wa mitaani ya jijini Mwanza Alfat Mansoor (Dogo) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya timu hiyo kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana jijini Dar es Salaam.

   Mchezaji aliyesabibisha timu ya watoto wa mitaani kutoka Tanzania kuibuka mabingwa wa Dunia kw kufunga magoli matatu kwa mojadhidi ya Burundi Frank William(mwenye kofia nyekundu) akiwa na baadhi ya wachezaji wenzake mara baada ya juwasili airport,kushoto ni Hassan Jaffar,Emmanuel Amos, na Hassan Seleman.

   Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Bi. Juliana Yassoda akiwa amebeba kombe la ubingwa dunia mara baada ya kupokea timu ya watoto wa mitaani kutoka Tanzania iliyochukua ubingwa huo kwa kuifunga timu kutoka Burundi jumla ya magoli 3-0. Timu hiyo imewasili nchini jana majira ya saa 9:35 mchana na kulakiwa na uongozi wa Serikali na wadau mbalimbali wa soka.

   Wachezaji wa timu ya watoto wa mitaani ya Tanzania ilyo nyakuwa ubingwa wa dunia katika mashindano yaliyofanyika nchini Brazil kwa kushirikisha timu za watoto wa mitaani, wakiwa wamebeba makombe waliyoyapa katika mashindano hayo.

  Afisa Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Frank Shija akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachezaji wa timu ya watoto wa mitaani.Picha zote na Frank Shija, Afisa Mawasiliano Serikalini, WHVUM

older | 1 | .... | 266 | 267 | (Page 268) | 269 | 270 | .... | 1897 | newer