Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 265 | 266 | (Page 267) | 268 | 269 | .... | 1897 | newer

  0 0

    Baadhi ya abiria kutoka sehemu mbalimbali wakipanda Ngalawa kwenye ufukwe wa ziwa Tanganyika,sehemu ijulikanayo kwa jina la Kibirizi kuelekea upande wa pili wa fukwe ya ziwa hilo pajulikanapo kwa jiina la Kagunga,ambapo abiria hulipa nauli ya shilingi Elfu tano kwa kila kichwa,na huchukua masaa mane kufika kwenye ufukwe huo,ambako ni mpakani mwa jirani na nchi ya Burundi.
  Abiria wakifunikwa turubai wasilowane na mvua,wakati ilipoanza kunyesha mjin hapa.
   Baadhi ya abiria kutoka sehemu mbalimbali wakipanda Ngalawa kwenye ufukwe wa ziwa Tanganyika,sehemu ijulikanayo kwa jina la Kibirizi kuelekea upande wa pili wa fukwe ya ziwa hilo pajulikanapo kwa jiina la Mwagongo mapema leo mchana mkoani Kigoma.
   Sehemu ya Ziwa Tanganyika kama inavyoonekana kwa mbaali mapema leo jioni mkoani Kigoma.

  0 0

   Mkuu wa wilaya ya Makete mh Josephine Matiro (kulia) akizindua albamu ya video ya msanii wa nyimbo za Injili Aldo Sanga wilayani Makete, kushoto ni MC wa shughuli hiyo Bi. Happy Ngogo.Picha na Edwin Moshi, Makete.
   Mwimbaji mahiri wa nyimbo za injili Happy Kamili akitumbuisha mashabiki waliofika kwenye uzinduzi huo.
  Happy Kamili akiwajibika na wimbo wake mahiri wa Mpango wa Mungu.

   Msanii Aldo sanga ambaye albamu yake imezinduliwa akitoa burudani kwa mashabiki wake waliofika kushuhudia uzinduzi wake.
   Aldo Sanga akiimba wimbo wa Nding'ung'uta ambao umebeba jina la albamu hiyo.
   Mwimbaji Madosa akiimba nyimbo zake za injili kwenye uzinduzi huo.
  Bi. Suma akiimba mbele ya mashabiki wake katika uzinduzi huo.
   Mwimbaji Kyando naye hakuwa nyuma.
   Kazi mtindo mmoja, Baraka Swallo naye akiimba kwa hisia kwenye uzinduzi huo.

  Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro akiangalia wimbo wa Nding'ung'uta kupitia televisheni kuashiria kuwa albamu hiyo imezinduliwa rasmi.

  0 0

  kimbari Mgeni Rasmi Mh. Profesa Mark J. Mwandosya Waziri Ofisi ya Rais akipokea Mwenge Maalum wa Kumbukumbu ya Miaka 20 ya Mauaji ya Rwanda kutoka kwa Mustapha Issa wa kwanza kutoka upande wa kushoto pamoja na Amina Mtegeti.
  Akiwasha Mshumaa kwa ajili ya kumbukumbu ya Miaka 20 ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda.
  Aliyekuwa katibu Mkuu wa Saba wa Umoja wa Afrika Dk. Salim Ahmed Salim akiwasha Mshumaa kwa ajili ya Kumbukumbu ya Miaka 20 ya mauaji Kimbari ya Rwanda.

  Baadhi ya mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania, wadau mbalimbali wa mashirika ya Kimataifa na Sekta binafsi waliohudhuria maadhimisho hayo.
  Baadhi ya wanafunzi wakiwa katika Kumbukumbu maalum ya Miaka 20 ya Mauaji ya Rwanda.
  Baadhi ya waliofika katika Kumbukumbu za Miaka 20 ya mauaji.


  Mshehereshaji wa maadhimisho ya kumbukumbu za Miaka 20 ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda Usia Nkhoma Ledama kutoka UNIC Dar es Salaam, akizungumza jambo kwenye sherehe hizo.
  Baadhi ya wageni waliofika katika kumbukumbu hizo wakiwa wanaimba nyimbo mbili za Taifa kutoka Rwanda na Tanzania.
  Mchungaji Safari Paul akiendesha Maombi Maalum kwa ajili ya Kumbukumbu ya Miaka 20 ya Mauaji ya Rwanda ambapo zaidi ya watu Milioni Moja waliuawa.
  Sheigh Othman akiomba dua Maalum kwa ajili ya Miaka 20 ya kumbukumbu ya Mauaji ya Rwanda.
  Mgeni Rasmi Mh. Profesa Mark J. Mwandosya Waziri Ofisi ya Rais akipokea Mwenge Maalum wa Kumbukumbu za Miaka 20 ya Mauaji ya Rwanda kwa ajili ya kuwasha Mishumaa ili kuwakumbuka wale wote waliopoteza Maisha.
  Mmoja wa wahimizaji wa Amani na Upendo Amina Mtengeti akiwa anazungumza Jambo wakati wa Maadhimisho ya Miaka 20 ya kumbukumbu ya Mauaji ya Rwanda.
  International Criminal Tribunal for Rwanda (ICTR) Registrar, Ndugu Bongani Majola akizungumzia kwa kifupi juu ya Mauaji ya Rwanda ambapo sasa ni Miaka 20 tangu yalipo tokea
  Wanafunzi wakiimba wimbo maalum kwa ajili ya kumbukumbu ya Mauaji ya Rwanda
  Mwakilishi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon , Mh. Dk Jamal Gulaid akisoma Ujumbe wa Katibu mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa.
  Mh. Benjamin Rugangazi akitoa Neno kutoka Ubalozi wa Rwanda Nchini Tanzania
  Zainab Abdallah kutoka Youth of United Nations akisoma Shairi maalum wakati wa kumbukumbu za Miaka 20 ya mauaji ya Rwanda.
  Mgeni Rasmi Mh. Profesa Mark J. Mwandosya Waziri Ofisi ya Rais akitoa hotuba yake kwa wananchi waliofika katika Maadhimisho hayo ya Miaka 20 ya Mauaji ya Rwanda.
  Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Swaumu Vuzzo akitoa neno la Shukurani kwa wageni waalikwa waliohudhuria maadhimisho hayo.
  Maandamano yakiwa yameanza kuelekea ukumbi wa Mlimani City
  Mmoja ya Waandamaji wa siku ya kumbukumbu ya mauaji ya Rwanda ikiwa imetimia Miaka 20 akiwa amebeba Mwenge Maalum kwa ajili ya Maadhimisho.
  Maandamano ya Kumbukumbu ya miaka 20 ya Mauaji ya Kimbari yaliyotokea mwaka 1994 yakiendelea kuelekea Ukumbi wa Mlimani City kwa ajili ya Maadhimisho hayo.
  Baadhi ya Wanafunzi pamoja na watu wengine mbalimbali wakiwa wameshika mabango mbalimbali yanayo elezea siku ya kumbukumbu ya Mauaji ya Rwanda yaliyotokea Mwaka 1994
  Maandamano yakiwa yamewasili nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City kwa ajili ya kukabidhi Mwenge huo kwa Mgeni rasmi Mh. Profesa Mark J. Mwandosya Waziri Ofisi ya Rais.
   Un Leo Press by Tone Radio-Tz

  0 0

   Paul Mashauri wa EASB akitoa mada katika kongamano hilo.

  Kongamano la wanawake Wajasiriamali Tanzania lilofanyika katika ukumbi wa Mbezi Garden Hotel lilifana , mada mbalimbali ziliwasilishwa katika kongamano hilo liliandaliwa na Tanzania Business Entreprenuers for Women(TBEW) wakiongozwa na Haika Lawere Mkurugenzi Mtendaji wa Mbezi Garden Hotel.
   
  Kampuni na vikundi vya wajasiriamali zaidi ya 30 vilishiriki maonyesho ya bidhaa na wajasiriamali zaidi ya 100 walishiriki katika semina zilizokuwa zinafanyika sambamba na maonyesho hayo

   Washiriki wa kongamanno ambao walikuwa wakionyesha bidhaa zao
   Ashura Katunzi Kilewela(Mrs) waTBS akiongelea umuhimu wa viwango katika bidaa za kitanzania
   Benedict Mwambela, Mkufunzi toka ILO akitoa mada
  washiriki wakionyesha baadhi ya bidhaa zao

  0 0

   Mkuu wa Idara ya Bima wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Bi. Kemibaro Omuteku (wa tatu kushoto) akiwa na baadhi ya maofisa wa benki hiyo wakionyesha vipeperushi ikiwa ni ishara ya kuzindua huduma ya Bima ya Bure ya Mkopo  jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni; Mkuu wa Idara ya Mikopo, Andrew Lyimo, Meneja Bima ya Maisha, William Mapela na Mkuu wa Idara ya Mauzo, Mongateko Makongoro.
  Mkuu wa Idara ya Mikopo wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Andrew Lyimo, (kulia) akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya Bima ya Bure ya Mkopo  jijini Dar es Salaam.  Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Bima wa NBC, Bi. Kemibaro Omuteku.


  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, akiwa na mwenyeji wake Katibu Mkuu wa Chama Cha RPF-INKOTANYI, Francois Ngarambe baada ya kuwasili mjini Kigali, Rwanda kwenye tafrija ya viongozi wa vyama tawala barani Afrka. Kulia ni Mjumbe wa NEC, Balozi Ali Karume.
   Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, akiwa na mwenyeji wake Katibu Mkuu wa Chama Cha RPF-INKOTANYI, Francois Ngarambe baada ya kuwasili mjini Kigali, Rwanda kwenye tafrija ya viongozi wa vyama tawala barani Afrka.
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akitoa salaam za shukrani kwa niaba ya vyama Vilivyoalikwa kwa Katibu Mkuu wa RPF wakati wa hafla hiyo.
  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, akiagana na Rais wa Uganda Yoweri Museven baada ya maadhimisho ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbali kwenye uwanja wa Amahoro, mjini Kigali, Rwanda.
   
  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, William Hague wakibadilishana mawazo kwenye Maadhimisho ya Kumbukumbu ya mauaji ya kimbari, katika Uwanja wa Amahoro leo.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Rais Mstaafu wa  Afrika Kusini Thabo Mbeki wakibadilishana mawazo kwenye Uwanja wakati wa maadhimisho hayo.
  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahma Kinana, akiwa na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, Mama Anna Mkapa na Rais Mstaafu wa Botswana Sir. Ketumile Masire wakati wa maadhimisho hayo.
  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwa na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta
  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akibadilishana mawazo na Rais wa Mstaafu wa Burundi Pierre Buyoya na mke wa Buyoya wakati wa maadhimisho hayo. Picha zote na Edward Mpogolo wa Ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akipokea msafara wa pikipiki wa vijana wa CCM (UVCCM) ambao wanaendesha mbio za Uzalendo Tanzania zikiwa na lengo la kuadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar jana tarehe 07-04-2014. Mbio hizo za kitaifa zinahusisha msafara wa pikipiki tano zinazoongozwa na viongozi watatu wa UVCCM ambao wanakuwa kwenye gari, aidha zinashirikisha wadau mbalimbali wa UVCCM katika kuzifanikisha. Mbio hizo  zinahimiza vijana kudumisha muungano, kuweka utaifa mbele na kutumia fursa zilizopo kwa maendeleo yao. Mbio hizo zitakuwa Mkoani Rukwa tarehe 07 na 08 April 2014 na kuelekea Mkoani Mbeya. 
  Ujumbe wa mbio hizo za Uzalendo Tanzania ambazo zinaendeshwa na UVCCM.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (kati) akiendesha duwa rasmi ya kuwaombea viongozi waasisi wa Muungano ambao wametangulia mbele za haki kama wanavyonekana kwenye picha Hayati Mwalim Julius K. Nyerere na Hayati Abeid Amani Karume muda mfupi baada ya kupokea msafara wa mbio hizi ofisini kwake jana tarehe 07-04-2014.
  Msafara wa Mbio za Uzalendo Tanzania ukiondoka katika Ofisi ya Mkuu ya Mkoa wa Rukwa mara baada ya kupata baraka za kiongozi huyo na kusaini kitabu tayari kwa zoezi la mbio hizo katika Manispaa ya Sumbawanga na baadae kuelekea katika Mji Mdogo wa Laela.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiondoka na pikipiki iliyokuwa ikiendeshwa na Katibu wa UVCCM Mkoa wa Rukwa Ndugu Philipo Elieza ambapo alishiriki mbio hizo hadi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika nje ya uwanja wa Nelson Mandela katikati ya Manispaa ya Sumbawanga.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiongoza mbio hizo na vijana wa UVCCM kuelekea kwenye mkutano wa hadhara.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (Mb) akizungumza katika Mkutano wa hadhara ambapo alisema tunu ya muungano ni lazma ilindwe na kila moja wetu na kuwa sio jambo la hiari. Aliongeza kuwa madai ya uwepo wa Serikali tatu ni hatua za kuhatarisha Muungano uliopo wa Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar hivyo hakuna budi kuimarisha Muungano wa Serikali mbili kwa maslahi watanzania wote. Aliuotelea mfano muungano wa Serikali tatu kuwa hauna tofauti na kuchukua kisu na kugawana mtoto ambapo kila mzazi atachukua kipande ambacho sio mtoto kamili.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkabidhi Katibu wa UVCCM Mkoa wa Rukwa Ndugu Philipo Elieza cheti cha pongezi kwa ushiriki wa Mbio za Uzalendo Tanzania na kingine kwa UVCCM Mkoa na Taifa kwa kuandaa na kufanikisha mbio hizo. Mkuu huyo wa Mkoa aliandaa vyeti vya pongezi kwa washiriki wote wa mbio hizo.
  Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Rukwa Ndugu Agustino Mzurikwao akitoa salam za vijana wa CCM katika mkutano huo wa hadhara ambapo alisisitiza juu ya vijana kutumia fursa zilizopo katika kujiendeleza kiuchumi na kudumisha Muungano wa Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar. Kulia ni Katibu Muenezi wa CCM Mkoa wa Rukwa Ndugu Clemence Bakuli.
  (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

  0 0
  Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Morogoro  Mh Abdalah Shaweji aliyevaa Miwani Akipatiwa maelezo kuhusu kilimo cha Mpunga kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Mkindo kata ya Hembeti Wilaya ya Mvomero ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Jumuiya ya wazazi .
  Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Morogoro  Mh Abdalah Shaweji  Akiwahutubia wananchi wa kata ya Hembeti waliojitokeza kwa wingi katika Sherehe za Umoja wa wazazi Mkoa wa Morogoro Ambapo katika Hotuba yake Aliwataka wana CCM Kushirikiana kwa Pamoja Katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa vitongoji na Vijiji.Pia Alisisitiza Msimamo wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Morogoro ni kwamba Katika Katiba Mpya wanaunga Mkono Msimamo wa Chama cha Mapinduzi wa Serikali Mbili na Kuwaomba wananchi Mara baada ya Rasimu ya Mwisho Kuja waichague serikali Mbili katika Kura ya Maoni ya Kupitisha Katiba Mpya,.
  Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Morogoro  Mh Abdalah Shaweji   Akipanda Miti katika Maazimisho ya Sherehe za Jumuiya ya Wazazi
  Wapenzi wa Chama cha Mapinduzi CCM Kutoka Wilaya ya Mvomero wakiwa wamejitokeza kwa Wingi kwenye Maadhimisho ya Siku ya umoja wa Wazazi Kimkoa ambayo Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Morogoro Mh Abdalah Shaweji Alikuwa Mgeni Rasmi kwa niaba ya Mwenyekiti wa Umoja huo.


  Wanachma wapya wa chama cha Mapinduzi wakiapa Mbele ya Mgeni Rasmi mara baada ya kukabidhiwa kadi.
   Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Morogoro  Mh Abdalah Shaweji Akisikiliza kwa Makini Taarifa za Chama cha Mapinduzi alipowasili wilayani Mvomero kweny Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wazazi Mkoani Morogoro. Katibu wa Jumuiya Hiyo alifanya Shuguli Mbalimbali Ikiwemo Kupanda miti Kufungua Mashina ya Chama cha Mapinduzi Pamoja na Kukabishi kadi za Uwanachama ambapo Jumla ya Wanachama 150 walijiunga na umoja wa wazazi.
  Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Morogoro  Mh Abdalah Shaweji Akisaini Kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Ofisi za CCM Wilaya ya Mvomero
  Wajumbe wa Kmatai ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Morogoro Wakisaini kitabu cha wageni kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Mvomero.

  0 0

  Majaji wa Shindano la Kusaka Vipaji vya Uigizaji Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents, Single Mtambalike (kulia), Yvonne Chery (Katikati) na Roy Sarungi (Kushoto) wakipitia alama za washiriki kwaajili ya kuweza kuwatangaza washindi waliofanikiwa kuingia hatua ya tatu ambapo wanachukuliwa washiriki 30 kwaajili ya kupata mchujo wa washindi watatu bora ambao wataibuka na Kitita Cha Shilingi laki 5 kila Mmoja kwa Kanda ya Ziwa na baadae kujiunga na washindi wengine watatu kutoka kila kanda katika fainali ya mwisho itakayofanyika Mkoani Dar Es Salaam na Mshindi Kujinyakulia Zawadi Kubwa kabisa ya Kitita Cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania. (50,000,000/=)
   Baadhi ya washiriki wakionyesha uwezo wao wa kuigiza mara baada ya kupewa muswada (script).
  Baadhi ya washiriki wakiwa mbele ya majaji (hawapo pichani) kwaajili ya kutajwa washiriki waliofanikiwa kuingia hatua ya tatu ambapo washiriki 30 tu ndio watachukuliwa kwaajili ya kupatikana washindi watatu watakaoibuka na kitita cha Shilingi laki 3 kila Mmoja na Baadae kuungana na washindi wengine wa kanda zilizobakia katika Fainali ya mwisho itakayofanyika Mkoani Dar Es Salaam.
   Baadhi ya washiriki wawili (wa kwanza kulia na wapili) wakiwa hawaamini kama wamechaguliwa kuingia hatua ya washiriki 30 kwaajili ya mchujo wa kupata washindi watatu wa Kanda ya Ziwa, Mkoani Mwanza
   Mmoja wa washiriki aliyefanikiwa kuchaguliwa kwa hatua ya tatu (mwenye fulana nyeupe) akipongezwa na mshiriki mwenzie ambae hakupata bahati ya kuchaguliwa kwaajili ya kuendelea na hatua inayofuata.
   Washiriki wakipongezana mara baada ya kuchaguliwa kuendelea na hatua inayofuata.
  Baadhi ya washiriki waliofanikiwa kuchaguliwa kwa hatua ya tatu wakishangilia mara baada ya kuchaguliwa.Picha na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Mwanza

  0 0

  Mshtakiwa namba 3, Kalisti Joseph Kanje ( aliyebeba mafaili),  Mshtakiwa namba moja, Samwel Gitau Saitoti (alifunika uso) na mwenzake  Mshtakiwa namba 2, Michael Kimani wakitoka nje ya mahakama kuu baada  ya mahakama hiyo kuwatia hatiani kwa kosa la kuua Askari polisi katika  tukio la uporaji wa benki ya NMB Mwanga.
  Washtakiwa namba 4 hadi 12, wakisaidiwa kupanda kwenye gari la Polisi baada ya mahakama kuu  kanda ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, kuwaachia huru leo mchana katika kesi ya mauaji ya askari polisi yaliyotokea Julai 11 mwaka 2007.
  Mshtakiwa namba 3, Kalisti Joseph Kanje ( aliyebeba mafaili),  Mshtakiwa namba moja, Samwel Gitau Saitoti (alifunika uso) na mwenzake  Mshtakiwa namba 2, Michael Kimani wakitoka nje ya mahakama kuu baada  ya mahakama hiyo kuwatia hatiani kwa kosa la kuua Askari polisi katika  tukio la uporaji wa benki ya NMB Mwanga.
  Mshtakiwa namba 12, Salome Materu aliyekuwa Mhasibu wa Benki ya NMB  Mwanga akisaidiwa kupanda katika gari la polisi baada ya mahakama kuu  kanda ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, kumuachia huru pamoja na wengine 8 katika kesi ya mauaji ya askari polisi yaliyotokea Julai 11 mwaka 2007.
  Mshtakiwa namba 12, Salome Materu aliyekuwa Mhasibu wa Benki ya NMB  Mwanga akisaidiwa kupanda katika gari la polisi baada ya mahakama kuu  kanda ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, kumuachia huru pamoja na wengine 8 katika kesi ya mauaji ya askari polisi yaliyotokea Julai 11 mwaka 2007..(picha zote  na Fadhili Athumani).
  Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
  MAHAKAMA kuu kanda ya Moshi, imewaachia huru washtakiwa 9 na kuwatia  hatiani wengine 3 wakiwemo Wakenya wawili na Mtanzania mmoja kwa kosa  la kumuua askari Polisi E6829 Michael Milanzi, aliyeuawa katika tukio  la Ujambazi lilitokea Julai 11mwaka 2007 kwenye Benki ya NMB tawi laMwanga.

  Akisoma uamuzi mdogo wa mahakama hiyo, Jaji mfawidhi Kasusulo Sambo alisema kwa mujibu wa sheria wa sheria 293 ya muendelezo wa ushahidi  wa makosa ya jinai, kifungu kidogo cha 1, sura ya 20 kamailivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, mahakama imeridhia kuwa Jamhuri  ilishindwa kabisa kujenga kesi dhidi ya watuhumiwa 9, Raia wa Tanzania, na hivyo inawaachia huru.   Jaji Sambo alisema katika uamuzi huo Mahakama vilevile ikiongozwa na sheria hiyo kifungu kidogo cha 2, sura ya 20 kama ilivyorekebishwa mwaka 2002, imeona kwamba upande wa Jamhuri ilifanikiwa kujenga Kesi dhidi ya mshtakiwa namba 1, Samwel Gitau, Mshtakiwa namba mbili Michael Kimani, wote raia wa Kenya na mshtakiwa namba 3, Kalisti Joseph Kanje, Raia wa Tanzania.    "Mahakama ilitafakari ushahidi wote wa Jamhuri, na kufikia maamuzi kwamba mashahidi wote 18 waliofika mbele ya mahakama hii, walionesha ni jinsi gani Jamhuri ilivyoshindwa kujenga kesi dhidi ya washtakiwanamba 4,5,6,7,8,9,10,11, na 12,   "Aidha Mahakama hii tukufu imeridhishwa kwamba Jamhuri kwa kuzingatia sheria ya muendelezo wa makosa ya jinai, kifungu kidogo cha pili, sura ya 20 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, ilifanikiwa kujenga kesi kwa kiwango kisicho mashaka dhidi ya washtakiwa namba 1,2 na 3,"alisema Jaji Sambo.   Katika uamuzi huo, Jaji Sambo aliongeza kuwa Mahakama inaamuru washtakiwa wote 4 hadi 12 walionekana kutokuwa na kesi ya kujibu dhidi ya tuhuma hiyo ya mauaji waachiwe huru maramoja isipokuwa kama wana kesi nyingine inayowakabili ambapo mtuhumiwa namba 10, ElizabethMsanze "Bella" ambaye anatuhuma za ujambazi alilazimika kuendelea kutumikia kifungo chake. 


  Washtakiwa walioachiwa huru ni mshtakiwa namba 4, Deodat Temu, mshtakiwa namba 5, Afande Nathaniel Wanyama, mshtakiwa namba 6, Emmanuel Mziray, mshtakiwa namba 7, Florian Kimati "Babylon", mshtakiwa namba 8 Devotha Msanze. 


  Wengine ni mshtakiwa namba 9, Juliana Msanze, Mshtakiwa namba 10 Elizabeth Msanze, mshtakiwa namba 11, Ntibasalila Msanze na mshtakiwa namba 12, Salome Materu ambaye alikuwa ni Mhasibu wa Benki hiyo wakati wa uvamizi.   Wakati huo huo upande wa utetezi unaomtetea mshtakiwa namba 3, Kalisti Joseph, unaowakilishwa na wakili wa kujitegemea, Prof. Jonas Itemba, umetoa ombi la kuwasilisha mashahidi wawili mahakamani hapo kwa ajili ya kutoa ushahidi wa utetezi kwa mteja wake.   Mashahidi hao ni Josephine Kalisti, ambaye ni mke wa Mshtakiwa huyo, raia wa Tanzania anayetuhumiwa kushiriki na kufadhili tukio la ujambazi lililopelekea mauaji, na mwengine ni Dafrosa Joseph.   Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa tena Aprili 10 mwaka huu, baada ya Mahakama kuridhia ombi la Washtakiwa namba 1 na 2 ambao hawana mashahidi, ya kutaka kuruhusiwa kuwasilisha mahakamani, maelezo ya Shahidi namba moja aliyoandika kwa mkono wake ambaye ni meneja wa Benki hiyo wakati huo, Robert Marandu.

  0 0

   Mwenyekiti wa Bunge la Katiba Samuel Sitta (kulia) akiongea na waandishi wa habari leo mjini Dar es salaam kuhusu mazungumzo yake na Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo(hayupo katika picha) . Kushoto ni Katibu wa Jimbo Kuu la Dar e salaam Padre Denis  Wigira. Picha na Bunge Maalum la Katiba.
  Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo(kushoto) akimkaribisha Mwenyekiti wa Bunge la Katiba Samuel Sitta (kulia) ofisini kwake leo mjini Dar es salaam kuhusu maendeleo ya Bunge Maalum.


  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akitoa hotuba ya ufunguzi wa kikao cha wadau wa filamu kuhusu mstakabali wa soko la filamu nchini leo jijini Dar es salaam.
  Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini Bi Joyce Fisoo akieleza lengo la kikao cha wadau wa filamu ni pamoja na kujadili masuala ya maendeleo ya tasnia ya filamu nchini na mapendekezo ya wadau kuhusu bodi ya filamu kuitisha mjadala wa wazi wa wadau wa filamu hususani wasambazaji, waandishi wa miswada na watayarishaji ili kujadili masuala mbalimbali yanayohusu tasnia hiyo leo jijini Dar es salaam.
  Baadhi ya wadau wa filamu walioshiriki kikao cha kujadili masuala mbalimbali ya husuyo tasnia hiyo leo jijini Dar es salaam. Pichani ni wasanii wa “Bongo Movie” (wa kwanza kushoto ni Steven Mengele “Manyerere”, Emmanuel Muyamba (katikati) na Jacob Steven “JB”(wa kwanza kulia).
  Picha ya pamoja ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga (wa sita kutoka kushoto mstari wa mbele) baada ya ufunguzi wa kikao cha wadau wa filamu kuhusu mstakabali wa soko la filamu nchini leo jijini Dar es salaam. (Picha zote na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

  0 0

  MTN Group and Bharti Airtel today announced a cross-border remittance partnership that seeks to remove the hassles of transferring money between Ivory Coast and Burkina Faso for the operators’ Mobile Money customers on either side of the border.

  The landmark partnership will enable Mobile Money customers of MTN Ivory Coast and Airtel in Burkina Faso to easily transfer money between the neighbouring countries. Until now, moving money between the two countries was mired by high fees, high usage of informal channels and a lack of proximity to withdraw money.

  MTN and Airtel already enjoy great adoption of Mobile Money services in their respective footprints, and connecting their operations through remittance services appears a logical next step.

  “MTN has reached a great level of adoption of Mobile Money in Ivory Coast, and Airtel has done the same in Burkina Faso. With a sizeable community of Burkinabe working in Ivory Coast and sending money back to their home country, the partnership will greatly enhance the Mobile Money service for customers in both countries. MTN brings the same added value to international transfers that we offer in local transfers; reliable, instant, affordable and proximity with customer through our distribution network,” says Pieter Verkade, MTN Group Chief Commercial Officer.

  “This partnership between Airtel and MTN is quite symbolic; it is the first time that two leading providers of mobile money services are cooperating to offer a service. Secondly, this is the first cross border mobile to mobile remittance service in West Africa and it has been designed to eliminate current pains associated with remitting funds between both countries whilst offering best in class security that protects the “sweat” of hard working Burkinabes that want to remit funds back home to their loved ones” says Chidi Okpala, Airtel Africa Group Director for Airtel Money.

  MTN Mobile Money enables users to perform local and international money transfers, make utility and other service payments, purchase airtime and access range of mobile financial products. As of 31 December 2013, MTN Mobile Money had 14,8 million registered users, and was available in 14 countries. MTN continues to pursue opportunities to develop unique offerings to add to its growing financial services portfolio.

  Verkade paid tribute to the Central Bank of West African States (BCEAO) for their support in enabling this service to the customers.

  0 0

  Wataalam wa afya DMV (HCP Metro DC) wanatuleta huduma ya afya kwa walewasiokuwa na bima ya afya. Huduma hii itatolewa kwa usawa bila kujali dini,rangi,umri,uraia au uchumi.


  Kama una rafiki, ndugu au  mzazi asiyekuwa na bima ya afya tunaomba mshiriki ili tuwe na jamii inayoshamiri na yenye afya njema. Zoezi hili litachukuwa hatua ya kuwaona wale watakaokuwa na hali pungufu ya afya njema mara moja kwa mwezi.


  Tarehe: 04/12/2014   (Jumamosi)
  Saa3:00 asubuhi hadi mchana 7:00 (waweza kuja hata kwa saa moja)  
  MAHALA
  3621 Campus Drive, 
  College Park, MD 20740

  Leo hii wadau wetu tunaomba tujitolee kufanikisha huduma hii ya maangalizi ya afya ya bure kwa wadau wa DMV. 
  Unaweza kujitolea kwa namna mbalimbali
  • Iwe ni kumsadia mtu usafiri,
  • kuandikisha majina ya wanaokuja
  • kubeba na kupanga meza kabla na baada ya maangalizi
  • au kushiriki katika timu ya kitaalam
  Tafadhali wasiliana nasi kupitia barua pepe nesiwangublog@gmail.com ili tuweze kupata idadi na uhakika wa msaada wako.

  0 0

  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Dk. Walid Kaborou akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma. Pichani nyuma ni Mjumbe wa NEC,Balozi Ali Karume walipowasili jioni ya leo kwa ziara ya siku tano mkoani Kigoma.

   Viongozi mbalimbali wa ngazi za juu za chama cha CCM Taifa na Mkoa wakiwa uwanja wa ndege mapema leo jioni ,mjini Kigoma wakimsubiri kumpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisindikizwa na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa Dk. Kaborou wakati akipita katika paredi la UVCCM alipopokelewa Uwanja wa Ndege wa Kigoma jioni ya leo.


  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisalimiana na Katibu wa NEC Siasa,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye,Mkuu wa mkoa wa Kigoma,Kanali Mstaafu Issa Machibya na Kamanda wa Vijana na Mchumi wa CCM mkoa wa Kigoma,Ndugu AbdulKadir Mushi mara alipowasili jioni ya leo kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma.

  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Kigoma,Kanali Mstaafu Issa Machibya jioni ya leo mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma.


  Sehemi ya Waendesha boda boda wakiupokea msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mapema leo jioni,mara baada ya kuwasili mjini Kigoma.

  0 0

   Picha hii na zingine zilizopo chini yake ni za picha ya pamoja ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe (wa tatu kwa waliokaa) na makundi mbalimbali ya washiriki wa warsha  ya kujenga uelewa wa wadau kuhusu mpango wa kunusuru Kaya maskini – TASAF awamu ya tatu Mkoani Katavi, wengine waliokaa kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda Bw. Seleman Lukanga, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bw. Paza Mwamlima na Meneja uratibu TASAF Tunu Alice Munthali. Wengine ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpanda Enock Gwambasa na Makamu M/Kiti Yusuf Msengi Ngassa.
   Meneja Uratibu kutoka TASAF Makao Makuu Tunu Munthali (aliyesimama) akiwasilisha kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe (wa kwanza kulia) salaam za Mkurugenzi mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga. 


  Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dkt. Rajabu Rutengwe akihutubia washiriki wa Warsha ya kujenga uelewa wa wadau kuhusu mpango wa kunusuru Kaya maskini – TASAF awamu ya tatu Mkoani Katavi .
  Hawa nao ni sehemu ya washiriki wa warsha hiyo inayoshirikisha watendaji mbalimbali wa ngazi ya Mkoa, Wilaya, Tarafa na Kata wakifuatilia kwa makini maelezo ya ufunguzi toka kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe (hayupo pichani)
  Baadhi ya washiriki wa Warsha hiyo wakimsikiliza hotuba ya ufunguzi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe  (hayupo pichani)

  0 0


  0 0


   Mkuu wa Chuo Kikuu cha Maunt Meru, mkoani Arusha Mchungaji Profesa Harrison Olang' (kulia), akishikana mikono na Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL), Bw. Devis Deogratius, baada ya kampuni hiyo kutoa miti 1300 kwa ajili ya mkoa wa Arusha, ambapo miti 1250 ilipandwa Chuoni hapo na miti 50 ilipandwa kwenye kiwanda cha TBL.
   Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), mkoani Arusha Bw. Devis Deogratius (aliyepiga magoti), akishiriki kupanda moja ya miti 1250 iliyotolewa na kampuni hiyo kwa ajili ya mkoa wa Arusha, baada ya kampuni hiyo kutoa miti 1300 kwa Manispaa ya Arusha, ambapo miti 1250 ilipandwa Chuoni hapo na miti 50 ilipabswa kwenye kiwanda cha TBL Arusha.
   Mkuu wa Chuo Kikuu cha Maunt Meru, mkoani Arusha Mchungaji Profesa Harrison Olang' (aliyepiga magoti kushoto), akishiki kupanda miti 1250 chuoni hapo, iliyotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kwa ajili ya Manispaa ya Arusha. Wanaoshuhudia katika picha ni baadhi ya wafakazi wa TBL na wafanyakazi wa Chuo hicho.
   Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Bi. Stella Kaaya akishiriki kupanda moja ya miti 1300 iliyopandwa katika Chuo Kikuu cha Maunt Meru, mkoani Arusha, iliyotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). 
  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Bi. Stella Kaaya (kulia) akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Maunt Meru mkoani Arusha Mchungaji Profesa Harrison Olang' (kushoto), baada ya kushiriki zoezi la kupanda miti 1300 kwenye eneo la Chuo hicho, iliyotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

  0 0

   Kaimu Meneja Sehemu ya Habari toka Wakala wa Vipimo Bi. Irene John akiwaeleza jambo waandishi wa Habari (hawapo pichani) na kuwatahadharisha wananchi kuhusu matumizi ya vipimo batili unaofanywa kwa kusutumia visado na ndoo za Plastiki. Wanaofuata Kushoto kwake ni Afisa Habari Idara ya Habari (MAELEZO) Frank Mvungi,Mkurugenzi wa Idara ya Ufundi Bw. Peter Masinga na Mwisho ni Meneja wa Upimaji Bw. Richard Kadeghe.
   Baadhi ya waandishi wa Habari waliohudhuria mkutano wa Wakala wa Vipimo leo Jijini Dar es Salaam.PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO.
   Mkuu wa Kitengo cha Sheria Toka Wakala wa Vipimo Bw. Moses Mbunda akiwaeleza waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mchakato wa Kunazisha Sheria Mpya itakayosaidia kuimarisha Sekta ya Upimaji Nchini, Kulia ni Kaimu Meneja Sehemu ya Habari toka Wakala wa Vipimo Bi. Irene John. 
  Meneje wa Upimaji toka Wakala wa Vipimo Bw. Richard Kadeghe akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi ambavyo vipimo batili vinayotumika.

  =========  =======  ========
  Na Frank Mvungi MAELEZO.

  Serikali yawatahadharisha wananchi kuhusu matumizi ya vipimo batili hususani visado na ndoo za Plastiki.

  Hayo yamesema na Kaimu Meneja wa  Habari,Elimu na Mawasiliano  wa EWakala wa Vipimo Tanzania Bi Irene John wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

  Akieleza Bi Irene amesema ufungashaji na upimaji batili ni kinyume cha sheria ya Vipimo sura 340 (iliyopitiwa mwaka 2002) pamoja na Kanuni zake.

  Akifafanua zaidi  alisema ufungashaji na matumizi ya vipimo batili hudhoofisha uchumi wa Taifa kwa kuwa humpunja mkulima,mlaji,mfanyabiashara na mtumiaji.

  Aliongeza kuwa Serikali imekuwa ikipoteza mapato yake ambapo Halmashauri hukusanya mapato pungufu wanapotoza ada kwa gunia badala ya uzito au ujazo.

  Irene  alitaja athari nyingine kuwa ni kuathiriwa kwa biashara ya kimataifa kutokana na wananchi kutokuzingatia vipimo hasa kwa kutumia mizani wakati wanapofanya biashara ya kununua na kuuza.

  Naye Mkurugenzi wa Idara ya ufundi wa wakala huo bw.Peter Masinga alisema ni vyema wananchi wakaacha kutumia vipimo batili kwani vimekuwa vikidhoofisha ukuaji wa uchumi kwa muda mrefu na hivyo kwenda kinyume na jitihada za Serikali za kuwaletea maendeleo wananchi.

  Bw. Peter aliongeza kuwa kuanzishwa kwa vituo vya kununulia mazao vijijini ni moja ya hatua zitakazosaidia kuondoa tatizo la vipimo batili kwa kuwa Serikali itaweza kusimamia kwa ukaribu matumizi ya vipimo sahihi kama vile mizani.

  Wakala wa vipimo ni Wakala wa Serikali ambayo ilianzishwa Mei,2002 kwa Tangazo la Serikali namba 194 kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma bora kwa wananchi, jukumu kuu likiwa kumlinda mtumiaji kupitia matumizi ya vipimo sahihi.

  0 0

  Janneth Emmanuel (kushoto),  Cresenciah Herman (katikati) na Joshua Wambura Stanslaus ambao ndio washindi wa Shindano la kusaka vipaji vya kuigiza Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents wakiwa wanaonyesha zawadi zao za pesa taslimu shilingi laki 5 kila mmoja mara baada ya kutangazwa washindi wa Kanda ya Ziwa.

  Shindano la Kusaka VIpaji vya Kuigiza Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents limemalizika leo kanda ya ziwa, Mkoani Mwanza kwa washindi watatu kupatikana na kupewa zawadi zao. Washindi hao ni Janneth Emmanuel , Cresenciah Herman  na Joshua Wambura Stanslaus huku binti mwenye umro mdogo kuliko washiriki wote Emiliana Fidelis mwenye umri wa Miaka 11 aliweza kung'ara kwa kuonyesha kipaji cha hali ya juu tokea mwanzo hadi Mwisho wa mashindano haya na kuweza kuvuta hisia za majaji na kupelekea majaji kumtangaza mshindi wa shindano hili lakini kutokana na Umri wake kuwa ni chini ya kigezo cha umri uliohitajika hatoweza kwenda Dar Es Salaam Kwaajili ya fainali lakini majaji hawakumuacha bure walimpatia zawadi za Shilingi laki Moja kama ishara ya yeye kuwa Mshindi pia.

  Baada ya Mashindano haya kumalizika Kanda ya Ziwa Mkoani Mwanza sasa Zoezi linahamia Kanda ya Kati Mkoani Dodoma wiki hii ambapo Zoezi zima la usajili litafanyika kuanzi jumamosi ya tarehe 12 hadi 15 aprili  ambapo pia watatafutwa washindi watatu pia wa kanda ya kati.
  Washindi hawa watatu wataungana na washindi wengine watakaopatikana katika kanda zingine katika fainali itakauofanyika Mkoani Dar Es Salaam Na mshindi kupata Zawadi kubwa ya Shilingi Milioni 50 za Kitanzania.
  Washiriki waliofanikiwa kuingia hatua ya 15 bora wakiwa mbele ya majaji tayari kwa kuchaguliwa washiriki watano bora.
  Hawa ndio washiriki walioingia tano bora
  Emiliana Fidelis akiwa amesimama mbele ya meza ya majaji mara baada ya majaji kufurahishwa na kuvutiwa na Kipaji chake, Emiliana ni mmoja kati ya waliotakiwa kuwa mshindi wa Kanda ya ziwa ila kwa bahati mbaya Umri wake ndio ulikuwa kikwazo.
  Jaji Yvonne Cherry akimkabidhi zawadi ya shilingi laki Moja Mshiriki Emiliana Fidelis mara baada ya kuvutiwa na Kipaji chake huku akiwa mshiriki pekee mwenye umri mdogo kuliko wote kwenye mashindano ya Kusaka Vipaji vya Kuigiza Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents.
  Jaji Mkuu wa Mashindano ya Kusaka vipaji vya kuigiza Tanzania yajulikanayo kama Tanzania Movie Talents, Roy Sarungi akimkabidhi zawadi mmoja wa Washindi watatu wa mashindano hayo mara baada ya kutangazwa washindi.
  Jaji Single Mtambalike akimpongeza mmoja wa washiriki aliyefanikiwa kuibuka kidedea katika Mashindano ya Tanzania Movie Talents.
  Mshiriki Crensenciah Herman akilia kwa furaha mara baada ya Kutajwa kuwa mmoja kati ya washindi katika shindano la kusaka vipaji vya uigizaji Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents lilomalizika Leo Mkoani Mwanza
  Majaji wakiwa katika picha ya Pamoja na washindi watatu wa Kanda ya Ziwa Mkoani Mwanza mara baada ya Kuwatangaza na kuwakabidhi washindi zawadi zao.Picha na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Mwanza

older | 1 | .... | 265 | 266 | (Page 267) | 268 | 269 | .... | 1897 | newer