Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live

RIDHIWANI KIKWETE AKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI,AZUNGUMZIA MWENENDO WA KAMPENI ZAKE.

$
0
0
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wake na waandishi hao wakati akizungumzia mwenendo mzima wa Kampeni zake,leo April 4,2014,Nyumbani kwake Msoga.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete.

MGOMBEA ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete, amesema akipata ridhaa ya wananchi, atahakikisha anajenga stendi ya mabasi na soko ili kutoa fursa kwa vijana kupata eneo la kuuzia bidhaa zao.

Ridhiwani amesema nia ni kuhakikisha vijana wanaouza bidhaa za vinywaji na zingine waweze kuwauzia abiria wa mabasi yatakayowekewa masharti ya kuingia stendi.

Akizungumza katika mkutano wake na Waandishi wa habari alipokuwa akielezea mwenendo mzima wa Kampeni zake, Ridhiwani amesema kiu yake ni kuona vijana wanapata masoko ya uhakika ya bidhaa zao.

Amesema atashirikiana na  madiwani wa halmashauri kutafuta eneo nzuri la kujenga stendi na soko hilo litasaidia kuinua jimbo la Chalinze kiuchumi.

“Nimesikia watu wanasema kuhamishwa kwa mizani ya Chalinze , vijana watakosa mahali pa kufanyia biashara zao.Kimsingi mizani si eneo la kufanyia biashara kwanza mabasi yanasimama muda mfupi lakini suluhisho ni stendi,”alisema


Alisema lengo ni kuhakikisha wanatumia fursa ya kuwa njia panda ya mikoa ya Kaskazini na Nyanda za juu Kusini na mikoa ya Kati , kuhakikisha kunakuwa na soko la uhakika.

Sera ya Taifa ya Idadi ya Watu Kufanyiwa Mapitio

$
0
0
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango), Bi Joyce Mkinga (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati alipokuwa akitoa taarifa ya kupitiwa upya kwa Sera ya Taifa ya Idadi ya Watu. Pamoja nae ni Mchambuzi Mkuu wa Sera (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango), Bw. Edwin Ninde (Kushoto) na Afisa Habari wa Idara ya Habari, Bibi Georgina Misana (Kulia).

 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango), Bi Joyce Mkinga (katikati) na Mchambuzi Mkuu wa Sera (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango), Bw. Edwin Ninde (Kushoto) wakiandika maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wanahabari (hawapo pichani).

ufafanuzi juu ya umuhimu wa kufanyiwa mapitio kwa Sera ya Taifa ya Idadi ya Watu. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoks Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bi Joyce Mkinga na Afisa Habari wa Idara ya Habari, Bibi Georgina Misana (Kulia).

========  ======= =======
Sera ya Taifa ya Idadi ya Watu  Kufanyiwa Mapitio

1.  Utangulizi:

Sera ya Taifa ya Idadi ya Watu kwanza ya iliandaliwa mwaka 1992 ambapo ilifanyiwa na kuandaliwa upya  mwaka 2006 kwa azma ya kuratibu na kushawishi sera za sekta nyingine, mikakati na program za maendeleo kuhakikisha zinajumuisha masuala ya maendeleo endelevu ya watu, kukuza usawa wa kijinsia, uwezeshaji wa wanawake, haki za watoto, na makundi mengine yenye uwezekano wa kuathiriwa kwa urahisi.


Tangu mwaka 2006 hadi sasa, maendeleo mapya yametokea kitaifa na kimataifa yenye uhusiano wa moja kwa moja na masuala ya idadi ya watu na maendeleo, mfano masuala ya mabadiliko ya tabia nchi, Magonjwa yasiyo ya kuambukiza, nk.  Kimataifa kumekuwepo na msukumo mpya wa kuimarisha maendeleo endelevu ya masuala ya idadi ya watu mfano masuala ya diaspora, mabadiliko ya tabia nchi, uhaba wa chakula duniani, nk.


2.  Malengo ya Sera ya Taifa ya Idadi ya Watu:

Lengo kuu la Sera ya Taifa ya Idadi ya Watu ya mwaka 2006 ni kuiwezesha Tanzania kufikia kiwango cha maisha bora ya watu wake. Vipengele muhimu vya ubora wa maisha ni pamoja na afya na elimu bora, chakula cha kutosha na makazi bora, mazingira bora, usawa wa kijinsia na usalama wa watu binafsi. Sera ina malengo ya kuelekeza ubunifu wa sera za kisekta, mikakati na mipango mingine inayohakikisha maendeleo ya watu. Malengo mahususi ya sera ya mwaka 2006 ni pamoja na:

    i.        Maendeleo endelevu na kuondoa umaskini;

  ii.        Kuongeza na kuboresha upatikanaji na ufikiaji wa huduma bora za kijamii;

iii.        Kuwa na mgao sawa, usawa wa kijinsia, uwezeshaji wa wanawake na maendeleo kwa wote; na

 iv.        Mpangilio mzuri baina ya idadi ya watu, matumizi ya rasilimali na mazingira.


3.  Viashiria vya idadi ya watu:

Sensa ya Taifa ya Watu na Makazi ya 2012 inaonesha maendeleo na mabadiliko ya viashiria vya idadi ya watu ambavyo ni vizazi, vifo na uhamiaji, hivyo kuwepo haja ya kufanya mapitio katika Sera ya Taifa ya Idadi ya Watu 2006 ili kuendana na mabadiliko hayo.


Uchambuzi wa takwimu za awali za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 unaonesha viashiria vingi vya idadi ya watu na maendeleo vimebadilika hivyo kuhitajika sera na mikakati mipya ya kutekeleza mipango mbalimbali ya idadi ya watu na maendeleo.


Sera ya Idadi ya Taifa ya Idadi ya Watu ya mwaka 2006 iliandaliwa wakati Watanzania walikuwa wanakisiwa kuwa takiribani milioni 38. Hata hivyo, idadi ya Watanzania kulingana na Sensa ya Idadi ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 inaonesha kuwa Tanzania ina jumla ya watu milioni 44,928,923 ambapo Tanzania bara ni 43,625,354 na Tanzania Visiwani ni watu 1,303,569.


Taarifa hizo zinaonesha kuwa idadi ya vifo vya akina mama na watoto vimepungua kutoka 529 mwaka 1990 hadi kufikia 454 mwaka 2010, kwa kila vizazi hai 100,000 (Tanzania Demographics and Health Survey 2010 (TDHS 2010), kasi ya ongezeko la watu imepungua kutoka asilimia 2.9 (kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2002) hadi kufikia 2.7 kwa mwaka 2012.


Vile vile, kasi ya uhamiaji imeongezeka maradufu ambapo kumekuwepo na wimbi kubwa la watu kuhama kutoka vijijini kwenda mijini au kijiji kimoja kwenda kijiji kingine (rural –rural migration). Aidha, kumekuwepo na suala la uhamiaji kutoka nchi moja na kwenda nchi nyingine kutokana na sababu mbalimbali za kiuchumi, kijamii na hata kiusalama, hii inajitokeza sana katika maeneo yanayozunguka maziwa makuu.


Kutokana na mabadiliko haya Serikali inaona kuna haja ya kufanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Idadi ya Watu ya mwaka 2006 na Mkakati wake wa utekelezaji ili kuendana na mabadiliko hayo.


4.  Mapitio ya sera:

Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango kwa kushirikiana na wadau mbalimbali itafanya mapitio ya Sera hiyo ili kuendana na taarifa mpya ambazo zimepatikana baada ya kukamilika kwa sensa, mapitio yanatarajia kufanyika katika kipindi cha mwaka 2014/15.


Sera ya Taifa ya Idadi ya Watu inalenga kuratibu na kuhusisha sera, mikakati na programu nyingine ili kuhakikisha maendeleo endelevu ya watu na kukuza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake.

Vile vile Sera ya Idadi ya Watu inatoa fursa na maelekezo kwa sera zingine za kisekta kuweka kipaumbele masuala ya idadi ya watu na maendeleo katika kupanga mipango ya kisekta.


Katika mapitio hayo, tunatarajia Sera ya Taifa ya Idadi ya Watu iweke msisitizo katika kupanga na kutekeleza masuala yafuatayo;

i)            Ukosefu wa ajira kwa vijana, wanawake na makundi maalum;

ii)          Elimu kwa kuzingatia ngazi zote (awali, msingi, sekondari, hadi elimu ya juu) kwa makundi yote ya jamii;

iii)        Uwezeshaji kiuchumi kwa kuzingatia makundi yote katika jamii;

iv)         Umiliki wa rasilimali ardhi – nini kifanyike katika kuhakikisha kuwa jamii inashiriki katika kumiliki ardhi/mgawanyiko wa rasilimali za nchi kwa kuzingatia idadi ya watu na makundi mbalimbali katika jamii;

v)           Miundombinu kwa kuweka kipaumbele mahitaji ya watu wenye mahitaji maalum, kuweka miundombinu rafiki katika kutunza mazingira na maendeleo ya binadam kwa ujumla;

vi)         Maendeleo ya miji na vijiji;

vii)       Afya ya uzazi kwa kuzingatia mila, desturi, taratibu, sheria na kanuni zilizopo – kuweka msisitizo wa elimu kwa wote kama moja ya mikakati ya kuboresha afya ya uzazi; na

viii)     Kuimarisha haki za binadamu.



5.  Hitimisho:

Kwa ujumla unapozungumzia maendeleo unazungumzia watu na hivyo, katika kupanga tunapanga kwa ajili ya watu; kujua wako wangapi, wako wapi, na wanafanya nini.


Imetolewa na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango

Tarehe 04/04/2014

   

TUME YAANZA UTAFITI KATIKA MAPITIO YA MFUMO WA SHERIA UNAOSIMAMIA HAKI ZA WALAJI

$
0
0
 Katibu Msaidizi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bw. Adam Mambi akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu Mpango wa kuanza utafiti katika mapitio ya mfumo wa sheria unaosimamia haki za walaji ikiwa ni hatua mojawapo katika mchakato wa kuundaa  sheria inayowalinda watumiaji wa huduma mbalimbali hapa nchini. Kulia ni Afisa Sheria wa Tume hiyo ni Fred Kandonga.

Afisa Sheria wa wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Fred Kandonga akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu sababu zilizopelekea Serikali kuamua kufanya utafiti utakaopelekea kutungwa kwa sheria itakayosaidia kuwepo kwa mfumo nwa biashara wenye uwiano katika ushindani. Katikati ni Katibu Msaidizi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bw. Adam Mambi, anayemfuatia ni Afisa Habari Idara ya Habari Maelezo Frank Mvungi na Mwisho kushoto ni Afisa habari wa Tume hiyo Munir Shemweta.




JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA KUREKEBISHA SHERIA TANZANIA




 
Anuani ya simu: "TUMESHERIA”.                                                                                P.O.Box 3580      

Simu ya mdomo; 2111387/2123533/4                                                                      DAR ES SALAAM

Namba ya fax: 2123534                                                                                                                                              

Barua pepe: lrct@lrct.go.tz


                                                                                                                  

TAARIFA KWA UMMA 

TUME YAANZA UTAFITI KATIKA MAPITIO YA MFUMO WA SHERIA UNAOSIMAMIA HAKI ZA WALAJI


Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania imeanza kufanya utafiti wa  mfumo wa sheria unaosimamia Haki  za Walaji ili kubaini kasoro mbalimbali zilizoko kwenye  mfumo husika na kupendekeza njia sahihi ya kuboresha mfumo huo nchini Tanzania.


Hatua ya Tume kufanya utafiti huo inatokana na mendeleo ya sayansi, teknolojia pamoja na utandawazi ambayo kwa ujumla yamemfanya mlaji kujikuta akiwa kwenye hatari ya kuathirika kiafya, kiuchumi na kijamii.


Tume katika utafiti wa awali, imebaini kuwa Mfumo uliopo hauendani na  na wakati huu wa mabadiliko ya kiuchumi, kijsamii, kitekenologia yanayotokea, kwani sheria nyingi zilizopo zilitungwa muda mrefu na hivyo hazikuzingatia mahitaji ya wakati wa sasa.


Pia sheria nyingi  hazijajumuishwa kwenye sheria moja  zinasimamiwa na watu au Taasisi tofauti tofauti. Hivyo, Tume imeona haja ya kupitia sheria hizo ili kupendekeza  mfumo wa sheria utakaomlinda mlaji kwa kuzingatia maendeleo yaliyopo sasa.


Na ni matarajio yetu baada ya kukamilika kwa utafiti huu Tume tutakuja na mapendekezo ambayo yataleta tija kwa walaji wetu pamoja na taifa kwa ujumla.

Tume ya Kurekebisha Sheria (Tume) ilianzishwa chini ya kifungu cha 3 cha Sheria ya Kurekebisha Sheria Namba 11 ya mwaka 1980. Sheria hii kwa sasa ni Sura ya 171 ya Sheria za Tanzania Toleo la Mwaka 2002. Tume ya Kurekebisha Sheria ni Idara ya Serikali inayojitegemea chini ya Wizara ya Katiba  na Sheria. 


Imetolewa na;

Tume ya Kurekebisha Sheria (T)

Dar es Salaam


04 Aprili, 2014

TANGAZO LA TAMASHA LA PASAKA

KINANA AAHIDI KUZITAFUTIA UFUMBUZI KERO ZA WAFANYABIASHARA SUMBAWANGA

$
0
0


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wafanyabiashara wa Mji wa Sumbawanga, kuhusu matatizo mbalimbali ikiwemo utitiri wa kodi na jinsi wanavyosumbuliwa  na maofisa biashara pamoja na malalamiko yao kuhusu mashine za TRA.Mazungumzo hayo yalifanyika leo katika Jengo la Chama cha Walimu, mjini Sumbawanga.

MfanyabiasharaWillington Kiziba  akilalamika mbele ya Kinana kuhusu kodi nyingi za biasshara na mazao ya kilimo.

 Mfanyabiashara Nobert Mbala akielezea mbele ya Kinana jinsi wanfanyabiashara wanavyonyaswa


 Honory Daud naye akielezea jinsi wanyabishara wanavyonyanyaswa kiasi cha kuichukia Serikali  




Mfanyabiashara Martine Tulo akilalamikia kitendo cha Manispaa kuweka kodi ya Fire wakati wa ununuzi wa viwanja





Meya wa Manispaa ya Sumbawanga, Sabas Katepa akikiri mbele ya Kinana na wafanyabiashara kuhusu mpangilio mbovu wa kodi na malipo ya leseni na kuahidi kuyafanyia maboresho haraka

 Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, naye akikiri mbele ya Kinana kutowashirikisha wafanyabiashara kupanga kodi mbalimbali

Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini, Aeshi akikubali kuwepo matatizo hayo na kuahidi kusaidiana na Kinana kupata ufumbuzi wa kero hizo ikiwemo ya mashine za TRA

 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Sumbawanga Mjini, Emmanuel Kilindu  akitembelea magongo alipokuwa akitoka kwenye mkutano  na wafanyabiashara


Kinana (wa pili kuliai)akiwa na maofisa wengine wa CCM wakitoka kwenye mkutano na wafanyabiashara wa Mji wa Sumbawanga

Rais Kikwete arejea nyumbani baada ya ziara ya Uingereza na Ubelgiji

$
0
0
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadiki baada ya kuwasili leo April 4, 2014 katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea Brussels, Ubelgiji, alikofanya ziara ya kikazi ya siku mbili na kuhudhuria mkutano wa mataifa ya Afrika na nchi za Jumuiya ya Ulaya. Kabla ya hapo Rais Kikwete alifanya zaiara ya kiserikali ya siku tatu nchini Uingereza kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Mhe David Camaron. PICHA NA IKULU

KINANA AINGILIA KATI MGOGORO SUGU WA ARDHI KATI YA WANANCHI NA MWENKEZAJI WILAYANI SUMBAWANGA MKOANI RUKWA

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana ameingilia kati Mgogoro wa ardhi uliokuwa ukifukuta kwa muda mrefu katika kijiji cha Mawenzusi,wilaya ya Sumbawanga mjini.Mgogoro huo uliohusu Wananchi na anayedaiwa kuwa Mwekezaji inaelezwa kuwa maamuzi yalikwishatolewa na Mh.Rais Jakaya Kikwete,kuwa Wananchi wapewe kipao mbele na Mwekezaji apewe kiasi,lakini mpaka sasa hakuna lililotekelezwa kufuatia Watendaji waliokuwa wamepewa dhamana ya kulisimamia jambo hilo kusua sua na hatimaye kutopatiwa ufumbuzi wa haraka.

Kinana yuko mkoani humo kwa ziara ya siku sita ya kuangalia uhai chama,miradi na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi

SHINDANO LA KUSAKA VIPAJI VYA KUIGIZA TANZANIA LAENDELEA VIZURI, WENGI WAHAMASIKA NA KUJITOKEZA KWA WINGI

$
0
0
Vijana waliojitokeza kwa ajili ya kushiriki shindano la kusaka vipaji vya Kuigiza wakiingia katika eneo la Ukumbi wa Isamilo lodge tayari kwa kuanza kuonyesha Vipaji vyao
Baadhi ya vijana wakijaza fomu kwaajili ya kuja kuonyesha vipaji vyao katika shindano la kusaka vipaji Tanzania ambalo linaendelea kufanyika katika Ukumbi wa Isamilo Lodge
Mmoja wa Majaji wa Shindano la Kusaka Vipaji vya Kuigiza Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents, Ivon Chery akitabasamu mwara baada ya kufurahishwa na Mmoja wa Washiriki wa shindano la kusaka vipaji (hayupo pichani) wakati alipofika mbele kuonyesha kipaji chake.
Majaji wakiwa Kazini Kutoka Kulia Ni Single Mtambalike, Ivon Chery na Roy Sarungi.
Cresenciah Helman akiwa mbele ya Majaji wa Shindano la Kusaka vipaji vya Uigizaji Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents akisikiliza kwa makini maelezo ya Majaji wakati alipofika kwaajili ya kuonyesha Kipaji chake leo kwenye ukumbi wa Isamilo lodge.
Kijana akionyesha Kipaji mbele ya Majaji.
Akiwa mbele Ya Meza ya Majaji.
Mmoja wa washiriki, Cresenciah Helman akishukuru timu ya Majaji baada ya kufurahishwa na uwezo wake wakati alipofika kuonyesha kipaji chake cha kuigiza leo katika Ukumbi wa Isamilo lodge.
Vijana wakiwa katika harakati za kujaza fomu kwaajili ya kuonyesha vipaji vya kuigiza katika shindano la kusaka vipaji vya uigizaji Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents linaloendelea Katika Ukumbi wa Isamilo Lodge.Picha na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

TPA yakabidhi msaada wa madawati 110 kwa Mkoa wa Lindi.

$
0
0
 Mkuu wa Bandari ya Mtwara, Absalom Bohela (kushoto) akikabidhi msaada wa madawati 110 yenye thamani ya shilingi milioni 20 kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh. Ludovick Mwananzila (kulia) wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika hivi karibuni katika kijiji cha Mahumbika kilichopo Lindi vijijini. 
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh. Ludovick Mwananzila (kulia) na Mkuu wa Bandari ya Mtwara, Absalom Bohela (kushoto) wakiwa na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Mahumbika wakati wa kukabidhi msaada wa madawati 110 yenye thamani ya shilingi milioni 20 kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kwa shule za mkoa wa Lindi hivi karibuni.
 Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Mahumbika wakifurahia jambo wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa madawati 110 yenye thamani ya shilingi milioni 20 kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), iliyofanyika hivi karibuni katika kijiji cha Mahumbika kilichopo Lindi vijijini.
 Wasanii wa kikundi cha ngoma na maigizo cha kijiji cha Mahumbika, Lindi wakitoa burudani wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa madawati 110 yenye thamani ya shilingi milioni 20 kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), iliyofanyika hivi karibuni katika kijiji cha Mahumbika kilichopo Lindi vijijini.
 Msanii wa kikundi cha ngoma na maigizo cha kijiji cha Mahumbika, Lindi akitoa burudani wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa madawati 110 yenye thamani ya shilingi milioni 20 kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), iliyofanyika hivi karibuni katika kijiji cha Mahumbika kilichopo Lindi vijijini.
 Mkuu wa Bandari ya Mtwara, Absalom Bohela akisoma hotuba kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kabla ya kukabidhi msaada wa madawati 110 yenye thamani ya shilingi milioni 20 kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh. Ludovick Mwananzila hivi karibuni. 

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), imekabidhi msaada wa madawati 110 yenye thamani ya shilingi milioni 20 kwa shule za Mkoa wa Lindi katika hafla iliyofanyika hivi karibuni katika kijiji cha Mahumbika kilichopo Lindi vijijini. Msaada huo wa madawati umekabidhiwa kwa shule hizo hivi karibuni na mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bw. Absolom Bohella mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh. Ludovick Mwananzila.

KATIBU MKUU WA CCM,KINANA AKAGUA MIRADI YA MAJI TAKA NA MAJISAFI WILAYANI SUMBAWANGA MKOANI RUKWA LEO.

$
0
0

Mkurugenzi wa Majisafi na Majitaka Sumbawanga (SUWASA), mkoani Rukwa, Antipas Shirima akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana kuhusu ujenzi wa tanki la lita milioni moja za majisafi linalojengwa katika mradi wa SUWASA unaotarajiwa kumalizika Machi 7, mwakani (2015). Mradi huo mpaka unakamilika utagharimu kiasi cha fedha shilingi Bilioni 30.Pamooja na kutembelea mradii wa maji safi,Kinana pia alitembelea mradi wa maji taka wilayani humo mapema leo.Ndugu Kinana anamaliza zaira yake leo ya siku sita mkoani Rukwa.
Sehemu ya eneo hilo ambapo litajengwa tanki la lita milioni moja za maji safi na kusambazwa Wilaya ya sumbawanga na vijiji mbalimbali mkoani Rukwa.
Mkurugenzi wa Majisafi na Majitaka Sumbawanga (SUWASA), mkoani Rukwa, Antipas Shirima akimuelekea jambo Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuhusu ujenzi wa eneo la kisima cha kuchujia maji safi na hatimaye kuyapeleka kwenye matanki na baadaye kusambazwa sehemu mbalimbali  za wananchi mkoani Rukwa.

Viingilio Tamasha la Pasaka hadharani,kufanyika uwanja wa Taifa

$
0
0
 Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Alex Msama akizungumza na baadhi ya Wanahabari kwenye moja ya mikutano yake kuhusiana na tamasha la pasaka.
KAMATI ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, mwishoni mwa wiki ilitangaza viingilio vya tamasha hilo jijini Dar es Salaam, viti vya kawaida ni shilingi 5000 na watoto 2000. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Alex Msama viti maalum ni shilingi 20,000 wakati VIP  ni shilingi 10,000.
 Msama alisema hivi sasa wanaendelea na mchakato wa kufanikisha zoezi la mgeni rasmi katika tamasha hilo kwani hivi karibuni watakamilisha zoezi la upigaji kura kumchagua.
Msama alisema mchakato wa kuelekea katika tamasha hilo litakalofanyika jijini Dar es Salaam Aprili 20 na baadaye mikoa mingine saba hapa nchini.
 Aidha Msama alitoa wito kwa wakazi wa Dar es Salaam kujiandaa na tamasha hilo ipasavyo kwani lina mlengo wa kurudisha mapato yanayopatikana na kuyapeleka katika maeneo matatu ambayo yanawahusu, yatima, walemavu na wajane.

 Msama alisema mipangilio yake ya kuwawezesha wenye uhitaji maalum ni kuwajengea kituo kitakachokuwa katika eneo la Pugu nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam ambacho kitajulikana kama Jakaya Mrisho Kikwete, rafiki wa wasiojiweza.
 

DKT. SHEIN AFUNGA KAMPENI ZA CCM JIMBO LA CHALINZE LEO

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Dkt. Ali Mohamed Shein akimnadi Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete wakati wa Mkutano wa kufunga Kampeni za CCM,zilizofanyika jioni ya leo kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Kikaro,Miono ndani ya Jimbo la Chalinze.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Dkt. Ali Mohamed Shein akiwasili kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Kikaro,Miono ndani ya Jimbo la Chalinze,tayari kwa kufunga Kampeni za CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze.
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete na Mkewe Bi. Arafa Kikwete wakiwapungia mikono wananchi wa Jimbo la Chalinze waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Kikaro,Miono ndani ya Jimbo la Chalinze wakiwasili  kwa ajili ya  kufunga Kampeni za CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Dkt. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Kikaro,Miono ndani ya Jimbo la Chalinze,leo April 5,2014 tayari kwa kufunga kampeni za CCM.Kulia ni Mke wa Ridhiwani Kikwete,Bi. Arafa Kikwete.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Dkt. Ali Mohamed Shein akibadilishana mawazo na Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete wakati wa kufunga Kampeni za CCM,zilizofanyika jioni ya leo kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Kikaro,Miono ndani ya Jimbo la Chalinze.
Umati mkubwa wa wananchi wa Kijiji cha Kikaro,Kata ya Miono ndani ya Jimbo la Chalinze wakiwa wamefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Kikaro,Miono ndani ya Jimbo la Chalinze,leo tayari kwa kufunga kampeni za CCM.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi yasisitiza wapiga kura wajitokeze kwa wingi na kwenda kupiga kura.

$
0
0
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (wa kwanza kushoto) akitoa risala siku moja kabla ya ya kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Chalinze kwa waadishi wa habari leo katika ukumbi halmashauri ya mji wa Bagamoyo. Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Hamid Mahmuod na wa kwanza kulia ni Mjumbe wa Tume hiyo Prof. Amon Chaligha.

 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (wa kwanza kulia) akisisitiza jambo wakati kisoma risala siku moja kabla ya siku ya kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Chalinze kwa waadishi wa habari leo katika ukumbi halmashauri ya mji wa Bagamoyo. Na wa kwanza kushoto ni Mjumbe wa Tume hiyo ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Afrika Mashariki John Joseph Mkwawa.

 Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi akimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (hayupo pichani) wakati kisoma risala siku moja kabla ya siku ya kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Chalinze kwa waadishi wa habari leo katika ukumbi halmashauri ya mji wa Bagamoyo.  
Baadhi ya waandishi wa habari na wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva wakati akisoma risala siku moja kabla ya siku ya kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Chalinze ikiwa ni utaratibu uliwekwa na tume hiyo kabla ya uchaguzi. 


(Picha zote na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AONGOZA MAZISHI YA ALIYEKUWA ASKOFU WA KANISA LA ANGLICAN CENTRAL TANGANYIKA

$
0
0
  Waziri mkuu Mizengo Pinda na mkewe wakitoa heshima za mwisho walipokuwa wakiuaga mwili wa aliyekuwa Askofu wa kanisa la Anglican Central Tanganika Godfrey Mdimi Mhogolo kabla ya ibada ya mazishi iliyofanyika katika kanisa la roho mtakatifu Dodoma.
  Mjane wa Marehemu aliyekuwa Askofu wa Kanisa la Anglican Central Tanganika Godfey Mhogolo, Iren Mhogolo akiwa mwenye huzuni pembeni ya jeneza kabla ya kuingizwa kaburini.
 Maaskofu mbalimbali wa kanisa la Aglican wakilishusha jeneza lenye mwili wa aliyekuwa  Askofu wa kanisa hilo Central Tanganika Godfrey Mdimi Mhogolo kaburini, katika mazishi yaliyofanyika nje ya kanisa la Roho Mtakatifu maarufu  la Mtungi Mjini Dodoma.
 Maaskofu mbalimbali wa kanisa la Aglican wakiweka mchanga kwenye kaburi la aliyekuwa Askofu wa kanisa la Anglican Central Tanganika aliyefariki Mwishoni mwa mwezi uliopita alipokuwa kwenye matibabunchini Africa ya kusini.
 Waziri mkuu Mizengo Pinda akiweka mchanga kwenye kaburi la aliyekuwa Askofu wa kanisa la Anglican Central Tanganika Godfrey Mdimi Mhogolo
 
   Waziri mkuu Mizengo Pinda na mkewe wakiweka shada ya maua juu ya kaburi la aliyekuwa Askofu wa kanisa la Anglican Central Tanganika aliyefariki Mwishoni mwa mwezi uliopita alipokuwa kwenye matibabunchini Africa ya kusini.
Waziri mkuu wa zamani Edwald Lowasa akiweka shada ya maua juu ya kaburi la aliyekuwa Askofu wa kanisa la Anglican Central Tanganika aliyefariki Mwishoni mwa mwezi uliopita alipokuwa kwenye matibabunchini Africa ya kusini.
 Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akiweka shada la maua kwenye kaburi hilo.
 Familia ya Marehemu Godfrey Mdimi Mhogolo aliyekuwa Askofu mkuu wa kanisa la Anglicani Central Tanganika wakiwa katika eneo la makaburi ambapo amezikwa nje ya kanisa la Roho Mtakatifu Dodoma.PICHA NA JOHN BANDA WA PAMOJA BLOG

CIDA NA PLAN INTERNATIONAL KUPITIA MRADI WA WAZAZI NA MWANA (THE MnW PROJECT) LATOA MSAADA WA VIFAA TIBA KUSAIDIA HUDUMA YA DHARURA KWA MAMA WAJAWAZITO NA WATOTO WACHANGA MKOANI RUKWA

$
0
0
Afisa Tawala wa Mradi wa Wazazi na Mwana (MnW) Bwana Mashauri Ndebile akimuonyesha Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mhe. Iddi Kimanta shehena ya vifaa vya msingi kwa ajili ya kutoa huduma za dharura kwa kina mama wajawazito na watoto wachanga Mkoani Rukwa. Vifaa hivyo mbalimbali vyenye thamani ya Tsh. Milioni 912 vimetolewa kwa Mikoa miwili ya Rukwa na Mwanza, ambapo kwa Mkoa wa Rukwa Mhe.

 Kimanta amevipokea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa huo Injinia Stella Manyanya. Jumla ya Zahanati 172 zitapatiwa vifaa hivyo ambapo kwa Mkoa wa Rukwa ni zahanati 114 kwa Halmashauri za Nkasi na Sumabwawanga Vijijini na Mwanza ni zahanati 64. Vifaa hivyo vimetolewa kwa ushirikiano wa mashirika ya Plan International, Jhpiego na Africare.
Dokta Neema Mamboleo mshauri wa Mradi wa Wazazi na Mwana akimuonyesha Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta kitanda maalum kwa ajili ya kusaidia watoto wachanga waliozaliwa kabla ya muda kutimia na kuwa na matatizo ikiwa ni sehemu ya vifaa hivyo vilivyotolewa na mradi huo. Msaada huo ni sehemu ya misaada mbalimbali ya mashirikia hayo Mkoani Rukwa ambapo hivi karibuni walitoa msaada wa "Ambulance" mbili na kujenga vyumba vya upasuaji kwa Halmashauri za Nkasi na Sumbawanga Vijijini.
Dokta Neema Mamboleo mshauri wa Mradi wa Wazazi na Mwana akimuonyesha Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta kitanda maalum kwa ajili ya kusaidia kinamama wajawazito wakati wa kujifungua.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mhe. Iddi Hassan Kimanta kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Ndugu Kimulika Galikunga orodha ya mgao wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya Halmashauri hiyo. 
Wadau na wafanyakazi wa Africare Mkoani Rukwa wakiwa katika hafla hiyo fupi ya makabidhiano. Kulia ni Ndugu Gasper Materu Mratibu wa Africare Mkoa wa Rukwa.
Baadhi ya washiriki wa hafla hiyo.
Picha ya pamoja.
(Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa @rukwareview.blogspot.com)

MBUNGE WA KIGAMBONI ATEMBELEA KITUO CHA AFYA KIGAMBONI KUANGALIA MAENDELEO YA TIBA YA KANSA YA KIZAZI KWA KINAMAMA

$
0
0
 Mbunge wa Jimbo la Kigamboni,Mh. Dkt. Faustine Ndugulile (mwenye fulana ya mistari mbele) akizungumza na baadhi ya kinamama wakazi wa Mji wa Kigamboni waliojitokeza kwa wingi kwenye Kituo cha Afya Kigamboni kwa ajili ya kupatiwa Huduma ya Uchunguzi na Tiba ya Kansa ya Mlango wa Kizazi kwa kina mama inayoendelea kutolewa leo kituoni hapo.
  Mbunge wa Jimbo la Kigamboni,Mh. Dkt. Faustine Ndugulile akimuuliza Muuguzi wa zamu namna zoezi hilo la Utoaji wa Huduma ya Uchunguzi na Tiba ya Kansa ya Mlango wa Kizazi inavyoendelea kwenye Kituo cha Afya Kigamboni.
 Kaimu Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Kigamboni,Dkt. Ansilla Lasway (kushoto) akimueleza Mbunge wa Jimbo la Kigamboni,Mh. Dkt. Faustine Ndugulile namna wanavyoendelea kutoa huduma za matibabu mbali mbali kwa wananchi wa Kigamboni.Mh. Ndugulile alitembelea kituo hicho leo ili kuona namna huduma zinavyotolewa kwa wagonjwa na changamoto zinazokikabili kituo hicho na kuahidi kuzifanyia kazi haraka iwezekanavyo.
 Mbunge wa Jimbo la Kigamboni,Mh. Dkt. Faustine Ndugulile akiwapongeza kinamama wa Kigamboni kwa kujitokeza kwa wingi kwenye Kituo cha Afya Kigamboni na kwa ajili ya kupatiwa Huduma ya Uchunguzi na Tiba ya Kansa ya Mlango wa Kizazi inavyoendelea kwenye kituo hicho.

shindano la kusaka vipaji vya uigizaji laendelea jijini mwanza.

$
0
0
 Majaji wa Shindano la Kusaka la Vipaji vya Uigizaji Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents wakijadiliana jambo wakati wa Zoezi la kusaka vipaji vya uigizaji kuingia Hatua ya pili kwa washiriki waliofanikiwa kupita kwenye mchujo.Kulia ni Single Mtambalike (Rich Rich), Ivon Chery (Monalisa) na Roy Sarungi.
Washiriki waliofanikiwa kuingia kwenye hatua ya pili wakifanyiwa usaili kwaajili ya hatua ya pili sasa
Muongozaji wa Mradi wa Shindano la Kusaka Vipaji vya Kuigiza Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents, Bw Stanford Kihole (kulia) akitoa maelekezo kwa washiriki waliofanikiwa kuingia hatua ya pili katika mashindano ya kusaka vipaji vya uigizaji Tanzania likiwa limeaingia hatua ya pili Mkoani Mwanza
Baadhi ya Washiriki waliofanikiwa Kuingia katika Hatua ya Pili ya Shindano la Kusaka Vipaji vya Kuigiza Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents wakiwa makini kusikiliza maelekezo juu ya hatua ya pili waliofanikiwa kuingia.


 Baadhi ya washiriki waliofanikiwa kuingia hatua ya pili wakiwa mbele ya majaji kwaajili ya kupewa maelekezo ambapo washiriki watapewa muswada (script) kwaajili ya hatua ya pili ambapo wataingia wawili wawili na kuanza kuonyesha vipaji vyao.
Kikosi Kazi kikiendelea kurekodi matukio yanayoendelea katika Shindano la Kusaka Vipaji Vya Kuigiza Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents linaloendelea kufanyika Kanda ya Ziwa, Mkoani Mwanza.
 Baadhi ya washiriki waliofanikiwa kuingia hatua ya pili katika Mashindano ya Kusaka Vipaji vya Uigizaji Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents wakiwa makini katika kupitia muswada (script) waliopewa na majaji ili waweze kusoma na baadae kuingia mbele ya majaji na kuonyesha vipaji vyao kutokana na muswada (script) waliopewa.
Baadhi ya washiriki waliofanikiwa kuingia hatua ya pili wakifanya mazoezi mara baada ya kupewa muswada (script) na majaji kabla ya kwenda kuonyesha vipaji vyao mbele ya majaji.Picha na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

WATANZANIA WASOMAO BEIJING CHINA WACHAGUANA, WAWEKA MIKAKATI YA KUDUMISHA MUUNGANO

$
0
0
 Mwenyekiti mpya Suleiman Serera akishikana mkono na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Bw. Daninga Philip. Wengine katika picha ni uongozi mzima wa Watanzania wasomao Beijing.
  Mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa Umoja wa wanafunzi wanaosoma Beijing, China (TzBeijing ) Bw.Philip Daninga akiongea na wanachama wa umoja huo muda mfupi kabla ya zoezi la kupiga kura lililofanyika mwishoni mwa wiki hii kwenye Ukumbi wa Ubalozi wa Tanzania, China. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Bw. Eusebia John (Makamu Mwenyekiti) na Suleiman Serera (Kaimu Mhasibu). Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA.

CCM YASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE JIMBO LA CHALINZE

$
0
0
Ridhiwani Kikwete akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupiga kura mjini Chalinze jana.
.........................................................................................
NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-CHALINZE
  
Ridhiwani Kikwete aliyekuwa mgombea ubunge uchaguzi mdogo jimbo la chalinze bagamoyo mkoani pwani kupitia chama cha mapinduzi CCM ,ameibuka kidedea kwa asilimia 86.61 katika uchaguzi huo na kuwamwaga wagombea wengine kutoka vyama vinne vya upinzani.


Matokeo ya uchaguzi huo yanaonyesha Ridhiwani ameongoza akifuatiwa na CHADEMA ,CUF,NRA na ASP.


Matokeo hayo yametangazwa usiku wa kuamkia leo April 7 majira ya saa nane usiku katika shule ya sekondari Chalinze na  Msimamizi wa uchaguzi huo  Bw.Samwel Salianga ambapo amesema CCM –Ridhiwani Kikwete amepata kura  20,828 sawa na  86.61%,Chadema-Mathayo Torongei amepata kura 2,544 sawa na asilimia 10.58,CUF- Fabian Skauki  476 sawa na asilimia 1.98,NRA-Hussein Ramadhani kura 60 asilimia 0.25 huku AFP Ramadhani Mgaya amepata kura 186 sawa na asilimia 0.59.

 Salianga amesema kati ya watu waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ni watu elfu 92,waliojitokeza katika zoezi hilo ni watu 24,422 ambapo kura halali zilikuwa 24,047 na  kura 375 zikiharibika.

Wagombea waliokuwepo wakati wa kutangaza  matokeo katika uchaguzi huo na kusaini fomu ya kukubalina na matokea alikuwepo mgombea wa NRA na CCM pekee.


Aidha Wakizungumza baada ya kupokea matokeo hayo aliyekuwa mgombea wa chama cha NRA pamoja na Ridhiwani Kikwete kupitia CCM,kila Mmoja ameshukuru wananchi na kuahidi kushirikina na wananchalinze kuleta maendeleo.

MOblog INAOMBA RADHI KWA WASOMAJI WAKE

$
0
0
Print
Mtandao wako wa habari www.modewjiblog.com unaomba radhi wa wasomaji wake kwa kutokuwa hewani kutokana na matatizo ya kiufundi yaliyojitokeza siku ya Jumamosi ambayo yameshughulikiwa na wataalamu wetu.

Kwa hivyo tunapenda kuwapa taarifa kuwa mtandao wetu umerudi hewani katika hali yake ya kawaida.Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza husani kwa wasomaji wetu pamoja na wadhamini wetu BancABC, East Coast Oils and Fats Ltd, MeTL AGRO, Dar Insights, Wanawake Live pamoja MeTL Group.

Endelea kuperuzi www.modewjiblog.com kwa updates za kila siku.
Usikose kutembelea Page yetu ya facebook na ku-like https://www.facebook.com/dewjiblog
Asanteni kwa uvumilivu wenu.
Operations Manager
MOblog.
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live




Latest Images