Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 259 | 260 | (Page 261) | 262 | 263 | .... | 1897 | newer

  0 0

  1
  Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia chama cha Mapinduzi Ndugu Ridhiwani Kikwete akiwahutubia wananchi katika viwanja vya kwa Mwarabu kata ya Pera Chalinze leo wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, Unaotarajiwa kufanyika Aprili 6 mwaka huu jimboni humo, Ridhiwani amewaomba wananchi hao kumpa kura za ndiyo ifikapo Aprili 6 ili aweze kuwatumikia na kuleta maendeleo ya jimbo hilo akishirikiana na wananchi kwa ujumla wake uchaguzi huo unafanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo marehemu Said Ramadhan Bwanamdogo. (PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-CHALINZE)2Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia chama cha Mapinduzi Ndugu Ridhiwani Kikwete akipunga mkono juu huku Mzee Kazidi ambaye ni Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro na Meneja wa Kampeni wa mgombea huyo akicheza wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo kwenye kata ya 


  10
  Ridhiwani Kikwete akisalimiana na Baadhi ya wazee wa Kimasai wakati alipowasili katika kijiji cha Chamakwera Kata ya Pera na kufanya mkutano wa kampeni katika kijiji hicho.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa akifungua mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi. Kikao hicho kimefanyika leo Machi 28, 2014 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Pembeni ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mheshimiwa Mrisho Gambo (kushoto) na Mwenyekiti wa Hamashauri ya Mji Korogwe ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilole, Mheshimiwa Angello Bendera (kulia).
  Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mheshimiwa Mrisho Gambo akitoa ufafanuzi wa jambo mbele ya mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa (kushoto). Pembeni ni Diwani wa Kata ya Mgombezi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya, Maji na Uchumi, Mheshimiwa Omari Chafesi na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu (kushoto).
  Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu akieleza umuhimu wa matumizi ya Tiba kwa Kadi (TIKA) mbele ya mkuu wa mkoa wa Tanga.
  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Korogwe ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilole, Mheshimiwa Angello Bendera (kushoto) akiendesha mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi. Pembeni ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Bw. Lewis Kalinjuna na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji Korogwe, Dokta Jerry Mwakanyamale.
  Afisa Matekelezo na Uratibu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) – Singida, Bw. Issaya Shekifu akitoa uzoefu wake katika moja ya Wilaya ya Ilamba, Singida jinsi wananchi wanavyofaidika na TIKA.
  Viongozi wa Dini wakifuatilia mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi.
  Wananchi wa Mji wa Korogwe wakifuatilia mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi.


  Wananchi wa Mji wa Korogwe wakifuatilia mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi.
  Wananchi wa Mji wa Korogwe wakifuatilia mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi.
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa akisalimiana na Mjumbe wa Kamati ya Msikiti Mkuu Manundu, Korogwe Mzee Daffa Daffa.
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa akisalimia na viongozi wa dini wa Halmashauri ya Mji Korogwe mara baada ya kumaliza kufungua mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi.
  Waheshimiwa Madiwani wa Kata mbalimbali za Halmshauri ya Mji Korogwe wakiwa katika mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi.
  NHIF 11: Afisa Matekelezo na Uratibu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)- Dar es Salaam, Genoveva Vicent akitoa majumuisho jinsi Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) unavyoweza kuwasaidia wananchi.

   Mchungaji Joseph Mhina wa Kanisa la Anglikana Manundu, Korogwe akitoa shukrani kwa wananchi waliofika katika mkutano huo wa wadau. 
  Timu ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dar es Salaam na Tanga waliokuwa wakiratibu mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa na Wilaya. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
  ---
  MAAZIMIO YA KIKAO CHA WADAU WA TIKA KATIKA HALMASHAURI YA MJI KOROGWE:-
  1. Washiriki wote wa kikao wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga wamekubaliana kwa kauli moja kukatwa Tshs.10,000 za posho zao kama mchango wa TIKA ili kusaidia wazee na wenye mahitaji maalumu.
  2. Kila mshiriki awe mwalimu na mhamasishaji kwa wale wote ambao hawakupata fursa ya kuhudhuria kikao hiki cha wadau wa TIKA
  3. Mfuko wa TIKA ni mali ya wana Korogwe hivyo kila mwananchi mwenye uwezo na mfanyakazi achangie kiwango cha Tshs.10,000 kama mchango wa TIKA kwa mwaka kwa mtu mmoja.
  4. Watendaji wa Mitaa,Kata na halmashauri wawe karibu na wenyeviti wa mitaa katika kuhamasisha jamii kujiunga na TIKA.
  5. Kuhamasisha wanakorogwe walio nje ya Korogwe kuchangia Mfuko wa TIKA kwa kiwango kilichowekwa ili kuuboresha mfuko na kusaidiwa wenye mahitaji muhimu na wazee.
  6. Wana Korogwe wenye uwezo zaidi kiuchumi waliopo Korogwe waombwe kuchangia mfuko huu ili kuuboresha.
  7. Kuhamasisha makundi maalumu kujiunga na TIKA mfano walemavu,na wawakilishi wao waliohudhuria semina hii wakawe mfano kwa kujiunga na TIKA na kuhamasisha wenzao.
  8. Watendaji wa Kata na Mitaa/Vijiji waitishe mikutano ya hadhara kwa ajili ya uhamasishaji na washarikiane na washiriki waliopata mafunzo/semina hii.
  9. Viongozi wa dini watatumia vikao vya kidini kwa ngazi zote kitaka kuhamasisha jamii na waumini (misikitini na makanisani)

  0 0

  Kufuatia mpango kabambe wa kuelimisha jamii dhidi ya makosa mtandao tayari kumekua na video za katuni, Mchezo wa komputa “Computer gane”, majarida ya katuni pamoja na machapisho mengine yote yakiwa na lengo la kutoa elimu kwa jamii juu ya jinsi ya kujilinda dhidi ya makosa mtandao kuanzia ngazi ya mtu binafsi hadi kufikia ngazi ya kitaifa.
  Picha:Mfano wa Vijarida vinavyo toa elimu dhidi ya usalama mtandao.
  Aidha, Bwana. Yusuph Kileo ametoa wito kwa vyombo vya habari nchini kuangalia kwa karibu namna itakavyo unganisha nguvu kuhakiki jamii ya watanzania inatambua kwa kina maswala ya husuyo uhalifu mtandao pamoja ulinzi mtandao. Kileo aeleza ni vyema maswala yaha ya uhalifu mtandao yanayoshika kasi sana kwa sasa yanatazamwa kwa karibu ili kuhakiki jamii ya watanzania inabaki salama kimtandao.

  Link:Mfano wa Video za Katuni zinazotoa elimu ya usalama mtandao.

  Athari za makosa ya kimtandao ni kubwa sana endapo hatua za msingi za kudhibiti uhalifu mtandao hazitochukuliwa kuanzia katika ngazi ya mtu binafsi hadi taifa kwa ujumla. Mataifa makubwa tayari wamesha yaona haya na sasa kumekua na jitihada mbali mbali zenye malengo ya kukabiliana na uhalifu mtandao.  Kwa upande mwingine bwana Yusuph kileo ameasa vijana kuwa na juhudi ya kusomea maswala ya ulinzi mtandao kutokana na uhaba mkubwa ulioko wa wataalamu wa maswala ya ulinzi mtandao katika ngazi za dunia huku akitolea mfano mataifa makubwa kuanza kutengeneza majeshi mahususi yatakayokuwa yakikabiliana na vita mtandao “Cyber war”


  0 0

  Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo yenye jukumu la kusimamia sekta ya Vijana nchini imeandaa Kongamano la Vijana kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu kuhusu Wajibu wa Vijana katika Kuimarisha Muungano Wetu Miaka 50 tangu kuzaliwa kwake. 


  Kongamano hili la Vijana kuhusu Muungano linafanyika Jumapili Machi 30, 2014  kuanzia Saa  5:00 Asubuhi katika ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam na litarushwa moja kwa moja na Televisheni ya Taifa, TBC One na TBC Taifa.


  Kongamano hili ni sehemu ya sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tangu kuasisiwa kwake na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mzee Abeid Aman Karume aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Aprili 26, 1964.


  Kauli mbiu ya sherehe za Miaka 50 ya Muungano ni “UTANZANIA WETU NI MUUNGANO WETU, TUULINDE, TUUIMARISHE NA KUUDUMISHA”.


  Lengo la Kongamano hili ni kuzungumzia Wajibu wa Vijana katika kuimarisha Muungano ambao mwezi  ujao unafikisha miaka 50.


  Washiriki wa Kongamano hili  ni vijana  300 kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu vilivyopo Tanzania Bara na Zanzibar.


  Washiriki wa Kongamano hili watapata fursa ya kuwasikia watoa mada ambao ni Wahadhiri wa Vyuo Vikuu Prof. Gaudens Mpangala atakayewasilisha mada kuhusu Wajibu wa Vijana katika Kuimarisha Muungano, Miaka 50 tangu kuzaliwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Aidha mada kuhusu Mapendekezo ya Katiba Mpya kwa Mustakabali wa Muungano wetu itawasilishwa na Prof. Issa Shivji.


  Waandishi wa Habari kutoka Vyombo mbali mbali vya Habari nchini wanakaribishwa kushiriki kwa lengo la kuhabarisha umma kuhusu kongamano hili.


  Imetolewa na Idara ya Habari -  MAELEZO

  29 Machi 2014


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiaga mwili wa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mara Marehemu John Gabriel Tupa, baada ya mazishi yake yaliyofanyika leo Machi 29-2014 Wilayani Kilosa  Mkoani Morogoro.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mara Marehemu John Gabriel Tupa, baada ya mazishi leo Machi 29-2014 Wilayani Kilosa  Mkoani yake yaliyofanyika Morogoro.
   Makamu wa Rais akiweka udongo kwenye kaburi.
  (Picha na OMR)
   
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimpa pole mjane wa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mara Marehemu John Gabriel Tupa Mama Katherine Msamati baada ya mazishi yake yaliyofanyika leo Machi 29-2014 Wilayani Kilosa  Mkoani Morogoro.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimpa pole Baba mzazi wa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mara Marehemu John Gabriel Tupa Mzee Gabriel Tupa, baada ya mazishi yake yaliyofanyika leo Machi 29-2014 Wilayani Kilosa  Mkoani Morogoro.

  0 0
 • 03/29/14--10:52: IN LOVING MEMORY'


 • Dada Grace Simtaji Ngowi.


  Our  beautiful Sister, our beautiful Mother, it is hard to believe that  today 29.03.2014 it is exactly two years since you passed away and left us with sorrows, tears and confusion. We praise God’s name for the time we spent together the joy, laughter and words of encouragement from our sister and mother.  


  Our sister our mother will always be in our hearts, and will be remembered by son Emmanuel and his family, your husband Joseph, your sister Anna, your brothers Bahati, Kotto & Baraka, other members of the family and friends.


    ‘’...the Lord gave and the Lord has taken away may the name of the Lord be praised’’


  Job 1:21


  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinuzi Dk.Ali Mohamed Shein na Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Bibi Virginia Blaser,wakikata utepe  kuzindua barabara  5 za mradi zikiwa ni Kipangani-Kangani,Chwale –Likoni,Mzambrauni Takao-Pandani,Finya-Mzambarauni,Karimu-Finya-Mapofu na Bahanasa –Daya Mtambwe,Mkoa wa Kaskazini Pemba,ambazo zimejengwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Changamoto za Millenia MCC.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinuzi Dk.Ali Mohamed Shein na Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Bibi Virginia Blaser,kwa pamoja wakibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa Bara bara 5 za Mradi katika Mkoa wa Kaskazini Pemba ambazo zimejengwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Changamoto za Millenia wa Watu wa Marekani (MCC) hafla iliyofanyika leo katika uwanja wa Gombani wilaya ya Chake chake Pemba.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinuzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na   Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Changamoto za Milenia Tanzania Bw.Bernard S.Mchomvu,katika uzinduzi wa Mradi wa  Barabara 5 zilizojengwa na Mfuko huo wa Mcc Mkoa wa Kaskazini Pemba
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinuzi Dk.Ali Mohamed Shein na Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Bibi Virginia Blaser,(kushoto) wakipata maelezo ya ramani ya michoro  ya ujenzi kutoka kwa Mkurugenzi wa miradi ya Usafirishaji (MCA-T) Eng Salum I.H.Sasillo,alipofika kuzindua Barabara 5 za Mradi Mkoa wa Kaskazini Pemba zilizojengwa kwa udhamini wa Mfuko wa Mcc. 

   Barabara ya Chwale-Likoni ni moja ya barabara zilizozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinuzi Dk.Ali Mohamed Shein, ikiwa tayari kwa matumizi ya wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba ambayo imetengenezwa na Kampuni ya h.yang ltd ya nchini  Kenya kwa udhamini wa Mfuko wa MCC. [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinuzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na  Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Virginia Blaser alipowasili katika uzinduzi wa Barabara  5 za Mradi katika Mkoa wa Kaskazini Pemba leo,barabara zilizozinduliwa Kipangani-Kangani,Chwale –Likoni,Mzambrauni Takao-Pandani,Finya-Mzambarauni,Karimu-Finya-Mapofu na Bahanasa –Daya Mtambwe.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinuzi Dk.Ali Mohamed Shein na Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Bibi Virginia Blaser,wakifuatana baada ya kufanya uzinduzi wa barabara  5 za mradi katika Mkoa wa Kaskazini Pemba,ikiwa ni Kipangani-Kangani,Chwale –Likoni,Mzambrauni Takao-Pandani,Finya-Mzambarauni,Karimu-Finya-Mapofu na Bahanasa –Daya Mtambwe,Mkoa wa Kaskazini Pemba,ambazo zimejengwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Changamoto za Millenia MCC.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinuzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na wananchi katika shrerehe za Uzinduzi rasmi wa barabara  5 za mradi katika Mkoa  wa Kaskazini Pemba,ambazo zimejengwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Changamoto za Millenia MCC.
   Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba waliohudhuria katika sherehe maalum za Uzinduzi wa Barabara 5 za Mradi,zilizojengwa kwa ufadhili wa Mfuko wa MCC,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,wakati alipowahutubia leo katika uwanja wa Gombani Wilaya ya Chake Chake Pemba.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinuzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na wananchi katika shererehe za Uzinduzi rasmi wa barabara  5 za mradi katika Mkoa  wa Kaskazini Pemba,ambazo zimejengwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Changamoto za Millenia MCC.(kulia) Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Bibi Virginia Blaser,na Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Rashid Suleiman.


  0 0
  0 0

   Mchungaji Boniface Frank Mwenegoha akizungumza kuhusiana na sakata la ujenzi wa mji mpya Kigamboni

  Mwenyekiti wa Kamati ya Wananchi inayowakilisha malalamiko yao kuhusiana na ujenzi mpya wa mji wa Kigamboni,Bwa.Kassim Abdallah.

  0 0

  Mabondia Japhert Kaseba na Thomas Mashali wakipambana wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba kugombania ubingwa wa UBO Africa Mashali alishinda kwa Pointi.
  Mtoto Zainabi 'Ikota' Mhamila katikati akiwa na mkata wa Ubingwa wa UBO Africa katika kona ya bondia Japhert Kaseba kabla ya kuanza kwa mpambano wao mkanda uho aliubeba kwa ajili ya kuwaonesha mashabiki pamoja na mabondia waliokuwa wakiwania mkanda huo

  Mtoto Zainabu 'Ikota' Mhamila akiwa na mkata wa Ubingwa wa UBO Africa kabla ya mpambano kuanza katika kona ya Thomas Mashali ambaye alishinda na kuunyakuwa mkanda huo kwa kushinda kwa point.

  Mtoto Zainabu 'Ikota' Mhamila katikati akiwa na mkanda wa ubingwa wa UBO kabla ya kuanza mpambano huo uku Rais wa ngumi za kulipwa nchini Emanuel Mlundwa akiwakumbusha mabondia Thomas Mashali kushoto na Japhert Kaseba sheria zitakazotumika katika mpambano huo.
  Bondia Kalage Suba kushoto akipambana na Alan Kamote wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa Universal Boxing Organisation UBO katika ukumbi wa PTA Sabasaba Kamote alishinda kwa TKO ya raundi ya saba.

  Bondia Alan Kamote akiwa na ubingwa wa Universal Boxing Organisation UBO
  Mtoto Zainabu 'Ikota' Mhamila katikati akiwa na mkanda wa ubingwa wa UBO kabla ya kuanza mpambano huo
  Baadhi ya watoto ambao wanafanya mazoezi katika GYM mbalimbali walijitokeza kuamasisha ujumbe wa World Boxing Ordanization 'WBO'  kushoto nio Rashidi Matumla na kulia ni Promota kutoka tanga Ally Mwazoa ambaye anakuja kwa kasi uku akiwa na mapasmbano matatu mfululizo yatakayofanyika PTA Sabasaba

  Mabondia wakongwe Jock Hamisi kushoto akipambana na Said Chaku wakati wa mpambano wao waliotoa droo

  Katika kuhakikisha ujumbe wa WBO unazingatia mtoto Zainabu 'Ikota' Mhamila akipiga padi huku akisimamiwa na Emanuel Mlundwa

  Baadhi ya watoto waliojitokeza katika kampeni ya kufanya mazoezi watoto wasipewe madawa wakiwa katika picha ya pamoja na wageni mbalimbali uku wakiwa na zawadi zao walizopewa mabegi flana na glove zenye ubora wa ali ya juu

  Zainabu 'Ikota' Mhamila

  0 0

  Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, akitoa mada kuhusiana na huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo kwenye semina iliyoandaliwa na Mfuko huo kwa wanafunzi wa mwaka wa mwisho Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), ambapo zaidi ya wanafunzi 500 walihudhuria semina hiyo Jumamosi Machi 29, 2014.
  Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), wakifuatilia mada kutoka kwa Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele.
  Meneja wa Kanda ya Mashariki na Kati wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, John Mwalisu, akitoa mada kwenye semina ya siku mbili, iliyoandaliwa na Mfuko huo kwa wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).
   Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), wakifuatilia mada.


  WANAFUNZI wa mwaka wa mwisho wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), wameridhishwa na mada mbalimbali zilizotolewa na Mfuko wa Pensheni wa PPF, na wameahidi kujiunga kwa wingi na Mfuko huo, kwani wengi wao wanatarajia kujiajiri, hivyo itakuwa fursa nzuri kwao kuandaa maisha yao ya baadaye watakapostafu.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti chuoni hapo jana mara baada ya semina iliyoandaliwa na PPF kwa wahitimu wa elimu ya juu, walisema awali walidhani kwamba Mfuko wa Pensheni wa PPF ni kwa ajili ya wafanyakazi walioajiriwa tu, lakini sasa wamefahamu kuwa milango iko wazi hata kwa wale ambao wamejiari ili mradi tu wawe na umri wa kuanzia 18.

  Mmoja wa wanafunzi hao, Oneck Mwalongo, alisema kwa muda wote ambao amekuwa chuoni alikuwa  hajawahi kuona maofisa wa mifuko inayojihusisha na masuala ya hifadhi ya jamii wakifika kwa ajili ya kuwapa semina kuhusiana na fursa zinazotolewa, lakini PPF imekuwa ya kwanza kuwapa elimu hiyo.

  "Lakini leo hii tunashukuru PPF wametufumbua macho kwani tulikuwa tunajua ili uwe mwanachama ni lazima uwe umeajiriwa, kwangu mimi nitajiunga na PPF kwa sababu kozi yangu ya sayansi ya kompyuta si lazima niajiriwe nitajiajiri mwenyewe," alisema Mwalongo.

  Alisema mfumo wa uwekaji amana wa hiari ulioanzishwa na PPF utasaidia vijana wengi watakaokuwa wamejiajiri kujiwekea akiba.
  Pia alisema amefurahishwa na mpango wa baadaye wa PPF wa kuanza kukopesha wanachama wake viwanja, kwani nyumba ndiyo jambo muhimu kwa maisha ya binadamu. 

  Mwalongo, alisema wakati akiingia kwenye semina hiyo alikuwa hafahamu kama  maisha ya kesho huanza kuandaliwa leo, hivyo atakapoondoka chuoni hapo ataanza kujiwekea akiba ili asikumbane na msemo wa fainali uzeeni.

  "Nilikuwa sifahamu kama maisha ya kesho yanaandaliwa leo wamenionesha njia sasa naanza kuandaa maisha ya uzeeni," alisema.
  Kwa upande wake, Elizaberth Elibarick, alisema PPF ni mfuko wa kujiunga nao hasa kwa kuzingatia mfuko huo una mfumo wa uwekaji amana wa hiari na unatoa fao la elimu kwa watoto wa mwanachama anapofariki akiwa bado kazini.

  Alisema si jambo la mchezo Mfuko kumsomesha mtoto au watoto wa wanachama ambao wamefariki kuanzia darasa la awali hadi kidato cha sita  na kizuri zaidi wanalipa mafao kwa wakati.
  Naye Leonard Mgeja, alisema kupitia semina hiyo yeye na wanafunzi wenzake wameweza kufahamu vitu vya msingi ambavyo walikuwa hawafahamu kuhusiana na Mfuko wa PPF.

  "Leo tumefahamu umuhimu wa maandalizi ya maisha ya baadaye tukiwa na umri mdogo ili kufanya mambo sahihi kabla ya kufikia uzeeni," alisema na kuongeza kwamba; 

  "Hivi sasa ambapo tunakaribia kwenda makazini tunaenda na mwanzo mzuri kwani hatutegemei kuajiriwa tu, bali na kujiajiri hivyo tutajiunga na uchangiaji wa hiari kama hatutakuwa kwenye mfumo rasmi wa ajira."
  Awali  Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko huo, Lulu Mengele, aliwaasa wanafunzi hao wa mwaka wa mwisho zaidi ya 500 waliohudhuria semina hiyo, kujiunga na PPF kupitia Mfumo wa asili wa Pensheni au ule wa uwekezaji amana pale ambapo wataamua kujiajiri wenyewe.

  “Mfumo wa uwekezaji amana, unaandikisha watu kutoka sekta isiyo rasmi, kama wakulima, wafugaji, machinga na mama lishe”. Alifafanua.
  Katika mada ya uwekezaji amana, Lulu alisisitiza umuhimu wa kuweka akiba kwani matayarisho ya maisha ya kesho yanaanza sasa.

  Kwa upande wake Meneja wa Mfuko wa Pesnheni wa PPF, Kanda ya Mashariki na Kati,  inayojumuisha Mikoa ya Morogoro, Dodoma na Singida, John Mwalisu, alisema PPF imeandaa semina hiyo kwa wanafunzi wa mwaka wa mwisho  wa chuo hicho kwa kuwa wao ndiyo wanaingia kwenye soko la ajira.
  Alisema kutokana na wao kuwa na nguvu ya kuajiriwa au kujiajiri wameona ni vema kuwaelimisha namna nzuri ya kutunza akiba ili iwasaidie watakapokuwa fikia hatua ya kustaafu.

  0 0


   Ndege iliyombeba Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana ikiwasili katika uwanja wa ndege mjini Sumbawanga,mkoani Rukwa mchana huu. 
   Ndugu Kinana akishuka kwenye ndege mara baada ya kuwasili mchana huu Sumbawanga mkoani Rukwa,tayari kwa kuanza ziara yake rasmi mkoni humu,ambapo ziara yake rasmi inaanzia Wilaya ya Nkasi,mkoani Rukwa.
   Ndugu Kinana akipokelewa na viongozi mbalimbali wa CCM mkoa Rukwa mara baada ya kuwasilia mapema leo mchana.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akivalishwa skafu na vijana wa chipukizi mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege mjini Sumbawanga,mkoani Rukwa mapema mchana huu.
  Katikubu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na Kada maarufu wa CCM,Ndugu Chrisant Mzindakaya,mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege mjini Sumbawanga,mkoani Rukwa mapema mchana huu.Kinana amewasili mkaoni humu mapema leo mchana ambapo anatarajia kuanza ziara yake rasmi ya siku 21 wilayani Nkasi,mkoani humo.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwasalimia wananchi na wanachama mbalimbali wa CCM waliofika uwanja ndege mjini Sumbawanga kumpokea mapema leo mchana.Kinana amewasili mkoani humu mapema leo mchana ambapo anatarajia kuanza ziara yake rasmi ya siku 21 wilayani Nkasi leo,mkoani humo ikiwemo mkoa wa Katavi na Kigoma..
   Baadhi ya Wananchi na wanachama mbalimbali wakisubiri kumpokea katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana kabla ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege mjini Sumbawanga mkoani Rukwa mapema leo asubuhi.
   Ni Chungu lakini kinatumika kama ngoma kikiwa kimebebwa baada ya kazi yake kuisha wakati wa kumpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kina mapema leo mchana mjini Sumbawanga.
  Msafara wa Katibu Mkuu,Ndugu Kinana ukiondoka uwnaja wa ndege mjini Sumbawanga mapema leo ukielekea wilayani Nkasi kuanza rasmi ziara yake ya siku 21,ambayo itaambata na mikoa mitatau ikiwemo Katavi na Kigoma.
  PICHA NA MICHUZIJR-MICHUZI MEDIA GROUP-RUKWA.


  0 0

  MKE WA WAZIRI MKUU Mama Tunu Pinda amewaeleza wanandoa kuwa ndoa ndiyo taasisi ya kwanza kuwafundisha watu maadili na kumjua Mungu pasipo Mungu haiwezekani.

  Amesema hayo wakati akifungua rasmi semina ya wanandoa wa kuanzia siku moja hadi miaka 25 iliyoandaliwa na watoa huduma wa New Life in Christ (Maisha Mapya Ndani ya Kristo) jana mchana tarehe 29 Machi, 2014 katika Ukumbi wa Msimbazi Centre jijini Dar es salaam. 

  “Ndoa ndiyo Taasisi ya msingi na ya kwanza kabisa kati ya Taasisi zote katika jamii ya mwanadamu ambayo ilianzishwa na mwenyezi Mungu”, alisema Mama Pinda.

  Taasisi hii ni muhimu sana kwani ndiyo chanzo cha Familia na ndio chanzo cha jamii ya watu na mataifa mbalimbali hivyo wanandoa wote inawapasa kuwa wa kwanza katika kukuza maadili kwa kufuata maandiko ya mwenyezi mungu.

  Mama Tunu Pinda alisema, katika Kitabu cha Mwanzo, sura ya kwanza aya ya 27-28 inasema kwamba mungu aliwaumba mtu mume na mtu mke kisha akawabariki akisema: “Zaeni na mkaongezeke, mkaijaze Dunia na kuitiisha. Mkatawale samaki wa baharini, ndege wa angani na kila kiumbe hai kiendacho juu ya ardhi”
  “Wanandoa  hamnabudi kujenga maadili mazuri,masikilizano na uvumilivu katika ndoa ili muweze kuepusha uvunjifu wa maadili katika ndoa”. Inaaminiwa kwamba matatizo mengi ya kuporomoka kwa maadili katika ndoa chanzo chake kikubwa ni kukosekana kwa uvumilivu, alifafanua Mama Pinda.

  “Ndoa zisipokuwa imara watoto wanakosa malezi, ndoa zinapovunjika, si wanadoa tu wanaoharibikiwa, bali watoto pia hupata majeraha makubwa ya kisaikolojia katika maisha yao,hivyo nawaomba wanandoa kuisha katika imani na masikilizano ili kuweza kudumisha ndoa zenu”, alisisitiza.

  Semina hii ni chachu na sehemu muhimu sana ya kujifunza na kukumbushana masuala muhimu ya kujenga ndoa zenu, hivyo mtumie nafasi hii kutafakari hali halisi ya ndoa zenu kwa kuwa wasikivu na wachangiaji wa mawazo na pia kwenda kuwaeleza na wengine kile mlichojifunza: “Naamini semina hii italeta uponyaji na nuru mpya katika ndoa zenu na familia na kuwa kichocheo katika kuimarisha ndoa zenu”, alisema.

  Napenda kusisitiza kwamba, hatuwezi kuwa na Taifa la watu wenye maadili mema kama ndoa zenu ambazo ni kiini cha familia, jamii na Taifa hazitaimarishwa, ni dhahiri kwamba hatutaweza kupata viongozi bora ikiwa ndoa zilizo imara ambazo ni kiini cha uhai wa familia zitaachwa ziyumbe:” Viongozi bora hutoka kwenye ndoa bora ni vizuri kujenga utamaduni katika jamii kwa kuwa na ndoa zisizotetereka”alisema Mama Tunu.

  Mama Pinda aliwaomba watoa huduma wa "New Life in Christ" pamoja na makanisa na watu wengine wanaotoa huduma za mafundisho ya uimarishaji wa ndoa kufanye jambo hili kuwa endelevu na kuhusisha ndoa nyingi kadri iwezekanavyo. “Serikalini  wanasema Matokeo ya Haraka sasa au Big Results Now nami nashauri iwe hivo katika ndoa zenu yawe malengo yenu na yaelekezwe katika kuleta Matokeo Makubwa Zaidi”, aliongezea Mama Tunu Pinda.

  Mama Pinda aliwashauri watoa huduma wa "New Life in Christ", kuangalia namna ya kuandaa Semina kwa ajili ya vijana ambao sasa wameingia katika ulimwengu wa utandawazi kwa kuwaaandaa na kuwasaidia waingie kwenye taasisi ya ndoa kwa kumshirikisha Mungu kupata wenza wao kuliko kutafuta wachumba kupitia mitandao ya kijamii kama vile facebook, viber, Instagram na mingineyo. “Semina hizi zitawasaidia kuwajenga kimaadili huku wakitambua majukumu yao kama mume  ama mke, kama baba au mama na hatimaye kuishi katika maadili mema”.

  Mapema, Mwenyekiti wa "New Life in Christ" Dkt. Alyson Mmanyi alisema huduma kama hizi za semina zinatolewa kwa watu wote wakristo wa madhehebu mbalimbali ili kuweza kunusuru ndoa na uvunjifu wa maadili kwani Taasisi ya ndoa imevamiwa na ndoa bila Mungu haiwezekani. 

  ”Tumekuwa tunatoa huduma za kuhubiri Injili kwa watu mbalimbali ambapo tayari tumeshatoa huduma hizi Mkoani Tarime, Rorya na tunatarajia kwenda Butiama mwaka huu”,alisema Dkt. Alyson.
    (mwisho)
   
  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 3021,
  DAR ES SALAAM.
  JUMAMOSI, MACHI,28 2014.


  0 0

  Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni tano Dk. Maria Kamm aliyetwaa Tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013/2014 ndani ya Ukumbi wa African Dreams uliopo Area D, Dodoma jana usiku.
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kushoto) akimvisha medali ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013/2014, Dk. Maria Kamm.
  Waziri Mkuu akimkabidhi tuzo, Anna Margareth Abdallah, kwa niaba ya mshindi wa pili ambaye ni Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro.
  Waziri Mkuu akimkabidhi tuzo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka aliyeibuka mshindi wa tatu katika tuzo hizo.
  Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela, akipokea tuzo kutoka kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda baada ya kushika nafasi ya nne.
  Dk. Maria Kamm akipokea tuzo kutoka kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda baada ya kuibuka kinara wa Tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013/14.
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda (katikati) katika picha ya pamoja na washindi walioingia Nne Bora. Kutoka kushoto; Anna Abdallah aliyechukuwa tuzo kwa niaba ya Dk. Asha-Rose Migiro, Anne Kilango Malecela, Dk. Maria Kamm na Profesa Anna Tibaijuka.
  Waziri Mkuu akiwa katika picha ya pamoja na washindi, waandaaji wa tuzo hizo kutoka Global Publishers Ltd.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers & General Enterprises Ltd, Eric Shigongo, akitoa hotuba fupi wakati wa utoaji tuzo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ambaye alikuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
  Mgeni rasmi, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akihutubia kabla ya kukabidhi tuzo.
  Dk. Maria Kamm na mumewe wakifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu Pinda.
  Anne Kilango Malecela na mumewe Mzee John Samuel Malecela wakiwa katika hafla hiyo.


  Wageni waalikwa wakiimba Wimbo wa Taifa.
  Mama Magreth Sitta (katikati) na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, EsterBulaya (kulia) wakifuatilia zoezi la utoaji tuzo.
  Dk. Kamm na mumewe wakiangalia Tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013/14.
  Shigongo na Waziri Mkuu wakiteta jambo.
  Profesa Tibaijuka akisalimiana na Mama Anne Kilango.
  Dk. Kamm akisakata rhumba naProfesa Tibaijuka.
  Waziri Mkuu akiongea jambo na mume wa Dk. Kamm. Kushoto ni Dk. Maria Kamm.
  Dk. Maria Kamm akitoa hotuba iliyovuta hisia za watu.
  Shigongo akimkaribisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

  0 0

   Hii ndiyo hali halisi, baada ya mvua kunyesha hii leo mkoani Njombe, kituo hicho kimegeuka matope matupu, na kusababisha watumiaji wa kituo hicho kupata tabu ya kutembea kwa shida na kutafuta eneo la kukanyaga ili wapite.

  Kamera yetu imeshuhudia abiria wakikanyaga matope na madimbwi ya maji machafu yaliyoshamiri kituoni hapo huku pia wakirushiwa maji machafu na magari kituoni humo
  Hali halisi ndiyo hii.
   Abiria ambaye jina lake halijajulikana mara moja akipita kwenye matope yaliyosheheni kwenye kituo hicha cha mabasi Njombe.
  Ni mwendo wa kuchagua eneo la kukanyaga, wengine wanapandisha suruali zao juu zisipate matope.

   Huwenda upande huu unaafadhali kwa abiria hawa lakini wapi, tope tuu.
  Tope lenyewe.

  Licha ya tabu hii inayowakumba watumiaji wa kituo hiki cha mabasi Njombe, ushuru umekuwa ukikusanywa kama kawaida, lakini miezi michache iliyopita halmashauri ya Njombe ilitangaza kuwa haina mpango wa kukikarabati kituo hicho na badala yake imetenga eneo lingine kwa ajili ya kujenga kituo kipya cha mabasi.

  Eddy Blog inaamini kuwa hii adha itaendelea kuwakumba wananchi na watumiaji wa kituo hiki kwa pamoja hivyo kwa kauli ya halmashauri inabidi abiria hao wazidi kuwa wapole na kuvumilia hali hii mpaka kijengwe kituo kipya!


  0 0


  Katika gazeti la Jamhuri Toleo Namba 129 Machi 25-31, 2014 kulikuwa na habari iliyoandikwa chini ya kichwa cha habari “Nyalandu ‘auza’ Hifadhi” ambapo maelezo ya habari hiyo yaliitaja Hifadhi ya Taifa ya Katavi kuwa inatarajiwa kukabidhiwa kwa wawekezaji kutoka nchini Afrika Kusini ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu.

  Shirika la Hifadhi za Taifa linalosimamia Hifadhi ya Taifa ya Katavi pamoja na Hifadhi nyingine 15 nchi nzima linapenda kukanusha habari hiyo iliyoandikwa kwa lengo la kupotosha umma kama ifuatavyo.

  Mosi, hakuna mpango wala uamuzi wowote uliopo au uliokwisha kufanywa wa kuingia Mkataba wa Uendeshaji wa aina yoyote ile baina ya Shirika la Hifadhi za Taifa na Mwekezaji yeyote kutoka nchini Afrika ya Kusini ikiwa ni pamoja na African Parks Network waliotajwa katika habari
  husika.

  Pili, Sheria inayosimamia uanzishwaji wa maeneo ya Hifadhi za Taifa ikiwemo Katavi imelipa dhamana hii pekee shirika kusimamia maeneo haya kwa niaba ya Watanzania na ni kinyume cha sheria kukabidhi kwa wawekezaji kwa ajili ya usimamizi kama ilivyobainishwa katika habari hiyo.

  Tatu, Shirika la Hifadhi za Taifa bado linao uwezo thabiti wa kusimamia uendeshaji wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi ili kuhakikisha rasilimali za wanyama na mimea zinaendelea kutunzwa kwa miaka mingi ijayo kama ambavyo imekuwa ikifanya tangu kuanzishwa kwa hifadhi hiyo mwaka 1974.

  Aidha, kama ambavyo shirika limekuwa likipanga katika mipango yake ya maendeleo mwaka hadi mwaka, katika mwaka mpya wa fedha ujao shirika limepanga kuongeza idadi ya watalii katika Hifadhi za Kusini ikiwemo Katavi Saadani, Mikumi na Ruaha. Mkakati huu utahusisha kuongeza ubora wa utoaji huduma ikiwa ni pamoja na malazi ili kukuza utalii wa ndani. 

  Shirika litafungua ofisi Jijini Dar es Salaam na kuimarisha ofisi za Mwanza na Iringa ili watalii wapate taarifa za Hifadhi na kuweza kufanya
  ‘bookings’ kwa urahisi. Aidha, kama ambavyo imekuwa ikifanyika kwa masoko ya nje, Shirika sasa litaanzisha ‘Road shows’ mbalimbali kwa soko la ndani na nchi za jirani. Vilevile, Shirika litaongeza kujitangaza kupitia Mitandao ya Jamii, TV, majarida na tovuti ya Shirika itaboreshwa katika kuarifu wadau masuala mbalimbali yanayojiri kwenye Hifadhi zetu.

  Tayari Shirika limeanzisha Kurugenzi mpya ya Utalii na Masoko kwa ajili ya kutekeleza mkakati huu wa kuzifanya hifadhi za ukanda wa kusini kuvutia watalii wengi zaidi.

  Imetolewa  na Idara ya Mawasiliano
  Hifadhi za Taifa Tanzania
  30.03.2014

  0 0

   Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana toka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo James Kajugusi akiongea na Vijana (Hawapo pichani) Waliohudhuria katika kongamano la vijana wa vyuo vya elimu ya juu kuhusu wajibu wa vijana katika kuimarisha muungano miaka 50 tangu kuzaliwa kwake. Leo jijini Dar es Salaam.

   Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ruaha Prof. Gaudens Mpangala akiongea na vijana( Hawapo pichani) kuhusu wajibu wao katika kuimarisha  na kuendeleza  muungano wa tanzania  baada ya miaka 50 na kuwataka vijana wa Tanzania kufanya utafiti na uchambuzi wa kina zaidi kuhusu utaifa katika majukumu yao ya kuimarisha na kuendeleza Muungano wa Tanzania.
   4944 Prof. Issa Shivji akiwaeleza vijana( Hawapo pichani) na kuwataka vijana kutambua kuwa wote wamezaliwa wakiwa Watanzania, utaifa wao ni Utanzania, Utambulisho wao ni Utanzania, wanajitambue kama Watanzania na wanatambuliwa na wengine kama Watanzania.Wakati wa Kongamano la Vijana Lililofanyika leo Jijini Dar Es Salaam.

  Baadhi ya Vijana waliohudhuria kongamano la vijana kuhusu wajibu wa vijana katika kuimarisha muungano miaka 50 baada ya muungano wa tanganyika na Zanzibar.
   Mwanafunzi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Peter Magoti akiongea na Vijana waliohudhuria kongamano hilo na Kuwataka kuwa wamoja na kuhakikisha wanaulinda na kuuenzi muungano wa Tanzania kwa Miaka mingi zaidi.Picha na Hassan Silayo -MAELEZO
  Katibu hamasa Taifa wa Umoja wa vijana CCM Paul Makonda akiwaeleza Jambo Vijana wakati wa Kongamano la Vijana Lililofanyika leo Jijini Dar Es Salaam.


  0 0

   Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Pro. Elisante Ole Gabriel akifungua Tamasha la Muungano la Fainali la Muziki wa Dansi, Taharabu, Kizazi Kipya na Utenzi siku ya Jumamosi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

   : Mgeni rasmi katika Tamasha la Muungano la Fainali la Muziki wa Dansi, Taharabu, Kizazi Kipya na Utenzi Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Regina Kikuli akitoa hotuba fupi wakati wa tamasha hilo, kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Pro. Elisante Ole Gabriel.

   }:Mshereheshaji kutoka kikundi cha Temeke akionyesha umahiri wake kwa kula moto wakati wa Tamasha la Muungano la Fainali la Muziki wa Dansi, Taharabu, Kizazi Kipya na Utenzi lililofanyika siku ya Jumamosi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

  Viongozi wa makundi ya muziki wa Dansi, Taharabu, Kizazi kipya na Utenzi waliooshiriki katika Tamasha la Muungano la Fainali la Muziki wa Dansi, Taharabu, Kizazi Kipya na Utenzi wakiwa katika picha ya pamoja ambapo katika mziki wa dansi kundi la Msondo ngoma liliibuka kidedea huku upande wa taharabu Jahazi Modern Taharabu walishika nafasi ya kwanza huku muziki wa kizazi kipya msanii Kelvini Nyoni kuwabwaga wenzake na katika fani ya Utenzi Bi. Mariam Mponda kushika nafasi ya kwanza.

   Kundi la muziki wa dansi lijulikanalo kwa jina la Mashujaa wakitumbuiza wakati wa Tamasha la Muungano la Fainali la Muziki wa Dansi, Taharabu, Kizazi Kipya na Utenzi siku ya Jumamosi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Picha na Genofeva Matemu – Afisa Mawasiliano Serikalini WHVUM

  0 0  Bondia Juma Fundi kushoto akitinishiana misuli na Baina Mazola baada ya kusaini mkataba wa kupigana Mei 11 katika ukumbi wa DID HALL Mabibo Mwisho
  Promota wa mchezo wa masumbwi Mahiyo Mkumbi kulia akiwaonesha mkataba mabondia pamioja na viongozi wa masumbwi kabla ya kutia saini mkataba huo kwa ajili ya mpambano wa mei 11


  Bondia Juma Fundi akitia saini mkataba wa kupambana na Baina Mazola mei 11 katika ukumbi wa DID Mabibo mwisho


  Promota wa mchezo wa masumbwi Mahiyo Mkumbi katikati akiwainua juu mabondia kutambulisha mpambano wao utakaofanyika mei 11 mabibo mwisho picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

  0 0

   Pichani juu na chini ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wakazi wa Halamshauri ya mji mdogo wa Namanyere Wialayani Nkasi jioni ya leo,kwenye mkutano wake wa hadhara uliofanyika nje ya uwanja wa Ofisi za chama hicho.Kinana alieleza kuwa kufuatia na taarifa mbalimbali alizokabidhiwa na Viongozi wa chama wilayani humo,alieleza kuwa wilaya ya Nkasi ina kero kadhaaa ikiwemo suala la Maji,Umeme,Uhaba wa walimu,Barabara pamoja na tatizo la soko la kuuza mazao ya wakulima,Kinana ameahidi yote hayao kuyafannyia kazi kwa kuhakikisha utekelezaji unafanyika kwa namna moja ama nyingine.
  Baadhi ya Wananchi waliofika kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana wakisikiliza kwa makini huku na wao wakiandika mambo kadhaa yaliyokuwa yakizungumza na Kinana kwa ajli ya kuweka kumbukumbu.
   Mwenyekiti wa CCM,Mkoa wa Rukwa,Ndugu Hypolitus Matete akimtambulisha Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa,kutoka Zanzibar,Balozi Ali Abeid karume kwa wananchi halmashauri ya mji mdogo Namanyere,wilayani Nkasi mkoani Rukwa,kwenye mkutano wa hadhara.
   Moja ya Kikundi cha ngoma za asili cha halmashauri ya mji mdogo,Namanyere Wilayani Nkasi wakitumbuiza kwenye mkutano wa hadhara uliondaliwa na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana aliyewasili leo wilayani humo mkoani Rukwa kwa ziara ya kichama mkoani Rukwa.
   Baadhi akina mama wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo wa hadhara uliofanyika nje ya uwanja wa ofisi za sisi,wilayani Nkasi mapema leo jioni
   Wanachama mbalimbali wa CCM na wananchi waliofika kwenye mkutano huo wa hadhara,wakishangilia jambo.Ambapo katika mkutano huo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana aliwahutubia wananchi wa halmashauri ya mji mdogo wa Namanyere wilayani Nkasi  mkoani Rukwa jioni ya leo.
   Baadhi ya wananchi wakishangilia jambo


older | 1 | .... | 259 | 260 | (Page 261) | 262 | 263 | .... | 1897 | newer