Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 258 | 259 | (Page 260) | 261 | 262 | .... | 1898 | newer

  0 0
 • 03/27/14--14:11: MWANZA ARE YOU READY?

 • 0 0


  0 0

  Meneja Mkuu wa kampuni ya Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho, akielezea mchakato wa kumpata 'Mwanamke wa Mwaka' utakavyokuwa. Kushoto ni Mratibu wa Matukio wa Global Publishers, Luqman Maloto.
  Abdallah Mrisho akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu tukio hilo.Wanahabari wakiwa kazini.
  Luqman Maloto akisistiza jambo kwenye mkutano huo.
  KAMPUNI ya Global Publishers Ltd ambao ni waandaaji wa shindano la kumtafuta mwanamke bora wa mwaka ambaye mchango wake wa maendeleo kwa jamii umewazidi wenzake, imethibitisha fainali hizo kufanyika keshokutwa Jumamosi.

  Akizungumza na wanahabari kwenye Hoteli ya Atriums, Jijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Abdallah Mrisho, amesema fainali hiyo itafanyika mjini Dodoma ambapo mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambaye atawakabidhi tuzo washiriki wanne walioingia fainali na kumkabidhi tuzo maalum mmoja kati yao aliyewazidi wenzake alioingia nao fainali.

  Washiriki walioingia fainali ni Prof. Anna Tibaijuka, Dk. Asha-Rose Migiro, Anna Kilango Malecela na Dk. Maria Kamm.
  (PICHA : RICHARD BUKOS / GPL )

  0 0

   Mhandisi wa Ujenzi kutoka Shirika la Mafuta Tanzania (TPDC), Mhandisi Mwita Yagela (Kulia) akiwaonesha michoro ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata gesi Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipotembelea eneo la ujenzi huo, Madimba, mkoani Mtwara. Wanaotazama ni wakaguzi hao, kutoka kushoto ni Prof. Longinus Rutasitara, Bibi Salome Kingdom, Bibi Florence Mwanri na Bw. Jordan Matonya.
   Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais ikijionea maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata gesi kilichopo Madimba, mkoani Mtwara.


    Vongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Prof. Longinus Rutasitara (Kushoto) na Bibi Florence Mwanri (Kulia) wakiangalia moja ya bomba la kusafirishia gesi. Bomba moja lina uzito wa tani tano na urefu wa mita 11. Mpaka sasa jumla ya kilomita 350 kati ya kilomita 492 zimeshatandazwa.
  Mhandisi wa Ujenzi kutoka Shirika la Mafuta Tanzania (TPDC), Mhandisi Mwita Yagela (Kulia) akiwaonesha mabomba ya kusafirishia gesi Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipotembelea baadhi ya maeneo yanakopita mabomba hayo. Mpaka sasa jumla ya kilomita 350 kati ya kilomita 492 zimeshatandazwa.  

  Mafundi wakiendelea na ujenzi wa makazi ya wafanyakazi katika kiwanda cha kuchakata gesi kilichopo Madimba, mkoani Mtwara. 


  ============   ==========
   Na Saidi Mkabakuli 
  Maendeleo ya ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu kufuatia kuendelea vyema kasi ya kundaza bomba hilo. 

  Wakizungumza na wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Wahandisi wa Ujenzi kutoka Shirika la Mafuta Tanzania (TPDC), Mhandisi Mwita Yagela na Mhandisi Omary Kitiku wamesema kuwa kasi ya sasa ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata gesi kilichopo kijiji cha Madimba, mkoani Mtwara inatia moyo na hivyo kuashiria kukamilika kwa mchakato huo kwa wakati. 

  “Mpaka sasa jumla ya kilomita 350 kati ya kilomita 492 za bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam zimeshatandazwa hali inayokwenda sambamba na mpangokazi wa ujenzi wa kiwanda hiki,” alisema Mhandisi Yagela. Kwa mujibu wa Mpangokazi wa ujenzi wa kiwanda hiko hadi kufikia mwisho wa Julai kiwanda kinatakiwa kukamilika, na mpaka sasa, makazi ya wafanyakazi imekamilika. 

  Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Mmoja wa viongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri alisema kwamba kukamilika kwa bomba hilo kunatoa mwanya wa kukamilika kwa wakati uzalishaji wa umeme katika vituo vya Kinyerezi, jijini Dar es Salaam. 

  “Kukamilika kwa bomba hili kunatoa fursa ya kwa Mradi wa kuzalisha umeme kiasi cha Megawati 150 na Megawati 240 kwa kutumia gesi asilia vilivyopo Kinyerezi, jijini Dar es Salaam,” alisema Bibi Mwanri. 

  Kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2011/12 - 2015/16), Miundombinu ni kipaumbele cha kwanza, hasa uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya nishati ambapo nguvu kubwa imewekwa katika uwekezaji wa miundombinu ya nishati ambapo utekelezaji wa ujenzi wa bomba la gesi Mtwara hadi Dar es Salaam unafanywa sambamba na ujenzi wa mitambo miwili ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi katika eneo la Kinyerezi Dar es Salaam. Serikali imeandaa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12 -2015/16) wa kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. 

  Lengo kuu la Mpango huu ni kufungulia fursa za ukuaji uchumi wa nchi ili kuweka misingi ya ukuaji mpana wa uchumi na unaolenga watu walio masikini zaidi.  Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano unawianisha katika mfumo mmoja wa mipango mbalimbali ya maendeleo ya kitaifa ili kutoa mwongozo wa utekelezaji na kuipa Serikali fursa na mfumo rasmi wa ufuatiliaji na tathmini wa miradi ya maendeleo kitaifa. Lengo la Dira ni kuibadili Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

  0 0

  Meneja biashara wa Airtel kanda ya kaskazini Brighton Majwala akimkabidhi vitabu vya sayansi kwa mkuu wa wilaya Arusha John Mongela kwa ajili ya shule ya sekondari Naura ya jijini Arusha vilivyotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya airtel chini ya mpango wake wa Shule Yetu.
  Mkuu wa wilaya ya Arusha John Mongela akimkabidhi vitabu mbalimbali mkuu wa shule ya sekondari Naura Sunday Mushobozi vilivyotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania katika hafla iliyofanyika shuleni hapo.
  Wanafunzi wa shule ya sekondari naura ya jijini Arusha wakiangalia vitabu mara baada ya kukabidhiwa vitabu hivyo na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania.

  Mkuu wa wilaya ya Arusha John Mongela aliwashukuru Airtel kwa msaada wa vitabu kwa shule ya sekondari ya Naura na kusema kuwa licha ya kuwa ni jukumu la Serikali kutoa vitabu kwa shule lakini imekuwa ikizidiwa na majukumu mengi hivyo kwa msaada huo Airtel wanapaswa kupongezwa kwa  kutimiza wajibu wao kwa jamii.

  Kauli hiyo imetolewa wakati Airtel ilipotoa msaada wa vitabu kwa Shule ya sekondari ya Naura mkoani Arusha chini ya mpango wake maalumu wa “shule yetu” ambapo Mkuu wa wilaya ya Arusha Bwana John Mongela alikuwa mgeni rasmi.

  Bwana Mongela alisema “Vitabu ndio nyenzo ya msingi ya kupata maarifa hivyo kwa Airtel kujikita katika kusaidia jamii kupitia vitabu kwa shule za sekondari kutawawezesha wanafunzi na jamii kupata hazina kubwa ya maarifa na mbinu za kujikwamua kiuchumi kupitia vitabu hivi. Napongeza sana jitihada hizi na mpango huu ambao ni endelevu na yenye kugusa shule nyingi na jamii kubwa ya watanzania kwa ujumla”.

  Meneja biashara wa Airtel kanda ya kaskazini Brightone Majwala akizungumzia msaada huo amesema mpango huo unaolenga kutoa vifaa vya kufundishia mashuleni yaani vitabu vya hisabati, physikia, chemia na biologia una lengo la kupunguza changamoto za uhaba wa vitabu mashuleni, tunayofuraha kutoa msaada wa vitabu kwa shule ya sekondari Naura kwani tunaamini wanafunzi wengi zaidi watanufaika na kuhamasika kujiunga na kusoma masomo ya sayansi

  Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo Gasper Mushobozi aliwashukuru Airtel kwa msaada huu wa vitabu vya sayansi shuleni hapa , lakini alibainisha kuwa msaada huu pia uendelezwe kwa kutuboreshea maabara ya shuleni hapo ili kuweza kupata tecknologia ya sayansi kikamilifu.

  0 0


  WALE MABINGWA WA COSMETICS ORIGINAL KABISA KUTOKA MAREKANI, @AK CLASSIC COSMETICS  WAMEWASHUSHIA TENA MZIGO MPYAA KABISA!! KAMA KAWAIDA BIDHAA ZOOOTE  KUANZIA PRODUCTs ZA KUPUNGUA, MAKE UPS,PRODUCTs ZA KUNG'ARISHA NGOZI ,DAWA ZA KUONDOA STRETCH MARKS, BODY SHAPERs,..NA BIDHAAA ZINGINE LUKUKI MUPYAAAAAA!!EM TUONGOZANE HAPA..

   KWA MAELEZO YA KINA NA PICHA ZAIDI WATEMBELEE BLOGUNI www.akclassic.blogspot.com
   KUWEKA ODA NA KUFIKISHIWA BIDHAA MPAKA ULIPO PIGA  0753-482909/0713-468393. WAPO KINONDONI KWA MANYANYA NA SINZA KUMEKUCHA.


  KARIBUNI SANA.


  0 0

  Gari ya Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam,Meck Sadicky likinasuliwa kwenye tope baada ya kukwama katika kijiji cha Mataya-Ruvu Chini,yote hiyo ikiwa ni sehemu ya changamoto ya Miundo mbinu hasa barabara,Wakati wakiongoza msafara wa Katibu MKuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa anakwenda kukagua chanzo cha Maji Ruvu chini na kujionea upanuzi wa chanzo hicho mapema jana jioni;wakati Ndugu Kinana alipokuwa akihimitimisha ziara yake ya siku tatu ndani ya wilaya ya Kinondoni,ziara hiyo ikiwa na lengo la Kuimarisha uhai wa chama cha CCM na kukagua miradi mbalimbali ikiwa ni sehemu utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi 2010.
  Utaratibu wa kulinasua ukiendelea.
  OOppss..haya twendeeeee....!
  Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam,Mh.Mecky Sadicky akimfafanulia jambo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,mara baada ya kukumbana na changamoto ya miundombinu,wakati wakielekea  kukagua chanzo cha Maji Ruvu chini na kujionea hali halisi na kazi kubwa inayofanyika ya upanuzi wa chanzo hicho mapema jana jioni,wakati Ndugu Kinana alipokuwa akihimitimisha ziara yake ya siku tatu ndani ya wilaya ya Kinondoni,ziara hiyo ikiwa na lengo la Kuimarisha uhai wa chama cha CCM na kukagua miradi mbalimbali ikiwa ni sehemu utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi 2010.
   Wakitafakari namna ya kupita mara baada ya kukutana na changamoto ya miundombinu,hasa barabara kama uonavyo pichani Lori likiwa limeziba njia kutokana na hali ya mvua kunyesha eneo hilo.  
   Gari ya Msafara ikinasuliwa kwenye tope . 
   Wadau kutoka Shirika la Utangazaji,TBC,Mtangazaji Elisha Elia  na Camera Man wake wakirekodi changamoto za miundombinu zilizoikubwa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa anakwenda kukagua upanuzi wa chanzo cha maji Ruvu chini mapema jana jioni.

   Nyenzo ya kuongeza nguvu ikiwakwa sawa.
  Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Mh.Idd Azan akizungumza jambo na mkulima wa Mpunga katika kijiji cha Mataya mapema jana jioni,wakati Ndugu Kinana alipokuwa akihimitimisha ziara yake ya siku tatu ndani ya wilaya ya Kinondoni,ziara hiyo ikiwa na lengo la Kuimarisha uhai wa chama cha CCM na kukagua miradi mbalimbali ikiwa ni sehemu utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi 2010.

  0 0

   
  KaTtibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Maji wa MCAT (Millenium Challenge Acount Tanzania,Bwana William Christian kuhusianana namna maji yanavyokusanywa na kusambazwa maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Pwani na Jiji la Dar,kati ni Mkuu wa Mkoa wa Dar,Mh.Mecky Sadicky akisikiliza.
   KaTtibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwaongoza viongozi wa CCM Wilaya ya Kinondoni kutembelea mitambo mipya baada ya upanuzi wa mitambo ya maji ya Ruvu Chini, wilayani Bagamoyo, kufanyika. Ujenzi wa mitambo hiyo umegharimu sh. Trilioni 1.6. Mradi huo unaotarajia kukamilika mwaka huu utapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la maji katika Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam. Kinana amemaliza ziara yake jijini Dar,wilayani Kinondoni pia kwa kutembelea kituo cha mabasi ya mjini kilichopo sinza na kufungua tawi jipya la vijana wakereketwa Kawe.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiendelea kupata Maelezo kutoka kwa kutoka kwa Mkurugenzi wa Maji wa MCAT (Millenium Challenge Acount Tanzania,Bwana William Christian,juu ya mitambo hiyo mipya ya kuchujia maji.Ndugu Kinana alieleza kuwa ameridhishwa na namna ya kazi ya upanuzi wa mitambo mipya ya maji Ruvu chini inavyoendelea,ameeleza kuwa kazi hiyo ya upanuzi ikikamilika basi jiji la Dar na maeneo mengine mbalimbali tatizo la maji litapungua kwa asilimia kubwa. 
  Ndugu Kinana na Ujumbe wake wa CCM kutoka Wilaya ya Kinondoni wakiangalia sehemu ya kuchanganyia dawa za maji kabla ya kusambazwa kwa matumizi mbalimbali.

   upanuzi wa mitambo ya maji ya Ruvu Chini, wilayani Bagamoyo, ukiendelea.

    KaTtibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana pamoja na  viongozi wa CCM Wilaya ya Kinondoni wakipata maelezo mafupi kuhusiana na usambazaji wa maji maeneo mbalimbali sambamba na namna ya upanuzi wa mitambo mipya ya maji ya Ruvu Chini, wilayani Bagamoyo, a Ujenzi wa mitambo hiyo umegharimu sh. Trilioni 1.6. Mradi huo unaotarajia kukamilika mwaka huu utapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la maji katika Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam.


  0 0


  0 0

   Magari yakipita kwa shida kwenye eneo hilo la barabara  baada ya mti kuanguka kwenye na kupelekea foleni kubwa eneo hilo la Mwenge.
   Foleni kubwa ya magari iliyosababishwa na kuanguka kwa mti huo katika barabara ya TRA eneo la Mwenge jijini Dar leo
   Magari yakipishana kwa shida baada ya mti huo kudondoka barabarani kutokana na mvua zilizokuwa zinanyesha pamoja na upepo.
  Magari yalilazimika kutumia njia moja kwani eneo hili lilikuwa limezibwa na mti huo uliodondoka kwenye eneo la barabara.PICHA NA PAMOJA BLOG


  0 0
 • 03/28/14--12:14: MWANAMKE BORA WA MWAKA 2014
 • WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda kesho atakuwa mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi Tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013-14, itakayowakutanisha wanawake wanne itakayofanyika kesho katika Ukumbi wa The African Dream mjini Dodoma.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ndiye atakuwa mgeni rasmi katika utoaji tuzo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, ambayo ndiyo iliyoratibu zoezi hilo, Eric Shigongo, alisema jana kwamba shughuli hiyo itakuwa ni hitimisho la kazi kubwa ya kupokea na kuchuja kura zilizotumwa na wasomaji kumtafuta mwanamke bora ambaye ni nembo kwa taifa.
  Prof. Anna Tibaijuka.
  “Zoezi hili lilifanyika kwa muda wa miezi tisa, kuanzia Juni mwaka jana hadi Machi mwaka huu. Awali kabisa watu walitakiwa kutuma majina ya wanawake wanaowaona ni bora ili wapigiwe kura, watu waliitikia vizuri sana, kwani jumla ya majina 150 yalitumwa katika kipindi cha miezi miwili.
  Dk. Asha Rose Migiro.
  “Baada ya hapo majina hayo yakaandikwa katika magazeti na watu wakatakiwa kupiga kura ili kuwatoa wanawake ambao wanadhani hawakustahili tuzo hizo,” alisema Shigongo, ambaye kampuni yake inatoa magazeti ya Uwazi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Amani, Risasi na Championi.
  Alisema katika awamu ya kwanza ya miezi hiyo miwili, majina ya wanawake 20 yaling’ara na hivyo kuingia katika awamu nyingine ya kupigiwa kura, ambapo baada ya muda kama huo pia, wanawake kumi walipata alama nyingi na hivyo kuingia katika awamu ya tatu na ya mwisho.
  Mh. Anne Kilango Malechela.
  Alisema kwenye hatua hiyo ya mwisho, wanawake watano walipita ambao ni Ananilea Nkya, Anna Tibaijuka, Anna Kilango Malecela, Asha Rose Migiro na mama Maria Kham. Katika zoezi hilo, wanawake hao wenye mvuto katika jamii walichuana na mmoja wao, Nkya, kuondolewa baada ya kura zake kutotosha kwa ajili ya fainali,” alisema Shigongo.
  Dk. Maria Kamm.
  Kwa upande wake, mratibu wa Tuzo hizo, Luqman Maloto, alisema tukio hilo la kihistoria ambalo pia litashuhudiwa na wabunge wa Bunge la Katiba walio mjini Dodoma, litaambatana na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali, akiwemo Linah,” alisema Maloto.

  0 0  0 0

  Na Kambi Mbwana, Aliyekuwa Handeni
  WANANCHI wa Kijiji cha Komsala, wilayani Handeni, mkoani Tanga, wamemlalamikia mwekezaji anayejulikana kwa jina la Amina Singa, kuwa anapora ardhi zao, huku serikali ya Kata Kwamatuku, ikishindwa kuwatetea wakulima wadogo na kuelemea upande wa mwekezaji.
  Katibu wa Baraza la Kata ya Kwamatuku, Nassib Bakari, pichani.
  Mwandishi wa habari hizi alitembelea katika kijiji hicho na kufanya mazungumzo na wananchi sambamba na Baraza la Kata juu ya mgogoro huo unaosababisha malalamiko mengi kutoka kwa wakulima hao.
  Mjumbe wa Baraza la Kata ya Kwamatuku, Mwanahamisi Nyata, pichani.
  Akizungumza kwa huzuni kubwa, mkulima aliyejitambulisha kwa jina la Hausi Zuberi, alisema kuwa mwekezaji huyo amechota eneo lake, kama alivyofanya hivyo kwa wananchi wengine waliopakana na shamba lake.
   Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu pichani.
  Alisema hali hiyo imewafanya waishi kwa mashaka wakiamini kuwa ataendelea na tabia yake hiyo, licha ya kumiliki eneo zaidi ya heka 120 hali ya kuwa anashindwa kulilima.
  Hausi Zuberi, mmoja wa walalamikaji wa migogoro ya ardhi katika Kata ya Kwamatuku, wilayani Handeni, mkoani Tanga.
  “Mwekezaji huyu ni kero kubwa kwetu kwasababu amechota maeneo yetu wakulima tusiopungua 6 baada ya kuvuka mbele ya mpaka wake, hali inayotufanya tuishi kwa hofu tukiamini kuwa ataendelea kutupora,” alisema.

  Naye Paulina Athon Simbaulanga, alisema kuwa uporaji huo umebarikiwa na Baraza la Kata, baada ya kutembelea eneo hilo, jambo linalowafanya waamini kuwa kuna njia ya mkato iliyopitwa katika kufanikisha uporaji huo.

  “Amina alikuja kijijini kwetu na kuomba heka 60, lakini sasa ana heka 120 na bado anapora sisi tusiokuwa na hata heka 5, licha ya yeye kumiliki eneo kubwa.

  “Hatujui hizo heka nyingine amezipata vipi na sheria za ardhi zinasemaje katika hilo, ingawa serikali ya kijiji inajua na mgogoro huu umebarikiwa na viongozi wetu,” alisema.

  Alipotafutwa Amina, alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwakuwa wananchi hao ndio waliovamia shamba lake, licha ya kushindwa kusema ni kiasi gani cha shamba analomiliki kijijini hapo kutoka heka 50 zinazotakiwa kisheria.

  “Kwanza mtakuwa umefanya makosa kama mmeamua kufanya mazungumzo na wananchi hao kabla yangu, hivyo siwezi kusema lolote,” alisema Amina.

  Katibu wa Baraza la Kata ya Kwamatuku, wilayani Handeni, mkoani Tanga, Nassibu Bakari Bigo, alikiri kuupokea mgogoro huo wa Amina na wakulima wa kijiji cha Komsala, huku akisema kesi za aina hiyo zimeendelea kushamiri katika maeneo mengi katika Kata hiyo.

  “Tuliupokea mgogoro huo, lakini kwa kiasi kikubwa umechangiwa na serikali ya kijiji husika kwa kushindwa kutatua kesi hizo na watu kusaka haki yao Baraza la Kata,” alisema Bakari.

  Kwa mujibu wa Bakari, kesi za migogoro ya ardhi zimeshamiri katika eneo lao, hivyo viongozi wa vijiji wanapaswa kusimamia vyema sheria za ardhi, huku wakitoa elimu kwa wakulima na wananchi wao, wakiwamo walalamikaji wa kesi inayomhusisha Amina, kutokana na mashahidi wao kushindwa kufika walipoitwa na Baraza la Kata.  0 0
 • 03/28/14--12:21: Article 4


 • 0 0

  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Ripoti ya Mwaka kutoka kwa Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Ludovick Utouh Ikulu jijini Dar es salaam leo.
  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisikiliza muhtasari toka kwa Mthibiti na Mkaguzi Mkuuwa Hesabu za Serikali Bw. Ludovick Utouh kabla ya kupokea Ripoti ya mwaka Ikulu jijini Dar es salaam leo. 
  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Mthibiti na Mkaguzi Mkuuwa Hesabu za Serikali Bw. Ludovick Utouh baada ya kupokea Ripoti ya mwaka Ikulu jijini Dar es salaam leo. PICHA NA IKULU 

  0 0

  Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu Bwana Juma Chagonja akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma itakayowawezesha wahitimu wa vyuo mbalimbali nchini kurejesha mikopo yao kupitia huduma ya Airtel Money, kushoto ni Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde.
  Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma itakayowawezesha wahitimu wa vyuo mbalimbali nchini kurejesha mikopo yao kupitia huduma ya Airtel Money kulia pichani ni Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu Bwana Juma Chagonja.

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB) imeanzisha mapinduzi ya malipo ya kielectoniki kwa kuwawezesha watumiaji wa huduma ya Airtel Money kulipia mikopo ya elimu ya juu  kupitia huduma ya Airtel money

  Ushirikiano huo kati ya Airtel na HESLB unawawezesha wahitimu wa masomo ya juu katika vyuo mbalimbali nchini kuweza kulipia mikopo yao kwa urahisi kupitia huduma ya Airtel Money na hivyo kuongeza ufanisi katika  ukusanyaji wa mikopo hiyo

  Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde alisema” tumewawezesha kupitia huduma yetu ya Airtel money wateja wetu kuweza kulipia mikopo yao ya elimu ya juu inayotolewa na bodi ya mikopo ya elimu ya juu kirahisi wakiwa majumbani mwao. Tunawahakikishia wateja wetu huduma bora, salama, ya uhakika yenye viwango vya gharama nafuu  na inayopatikana mahali pote nchini kupitia mawakala zaidi ya elfu 35,000 walionea nchini.

   Huduma hii ni ya haraka na nirahisi kutumia, sasa wateja hawana haja ya kusubiri kwenye mistari muda mrefu kufanya malipo, wanachotakiwa ni kufanya muamala rahisi kwa kupitia simu zao  kulipa na kupata uthibithisho wa malipo ndani ya sekunde chache

  Ili kupata huduma hii mteja anatakiwa kupiga *150*60#  na kuunganishwa na orodha ya Airtel Money kasha kuchagua namba 5 kufanya malipo, alafu chagua namba 8  kupata huduma zinginezo kisha kuandika neno HESLB , ingiza kiasi cha pesa, kumbukumbu namba na namba ya siri kufanya malipo  aliongeza mmbando

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu Bwana Juma Chagonja alisema”hii imekuja wakati muafaka ambapo baadhi ya waliofaidika na mikopo hii muda wao wa kurejesha malipo ya mikopo yao umekwisha,  kwa kupitia huduma hii ya kulipia kwa Airtel Money hakutakuwa na haja ya watu kutembea umbali mrefu na kupanga foleni katika mabenki ili kulipia, tunaleta kwa wateja wetu urahisi wa malipo na njia mbadala ya kurejesha mikopo yao kwa wakati na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mikopo hiyo.

  Chagonja aliongeza kwa kusema kwa kupitia huduma hii ya Airtel Money sasa wateja wetu wataweza kulipa mikopo yao kirahisi wakati wowote mahali popote masaa  24 siku 7 kwa wiki.

  0 0

   Picha ikionyesha mkuu wa wilaya ya Arusha Jonh Mongela akiwa anafungua mkutano wa TACINE  
  picha ikionyesha  washiriki ambao ni mameya na wakurugenzi wakiwa wanafatilia hutoba ya uzinduzi ya mgeni rasmi.Picha zote na woinde shizza
  =========    =======    ========
  Na Woinde Shizza,Arusha

  Wito umetolewa kwa Halimashauri zote nchini kutafuta njia mbadala za kuongezea Mapato yake ya ndani  tofauti na ilivyizoeleka kutegemea mapato yatokanayo na ushuru mbalimbali wanaokusanya katika halimashauri zao.

  Wito huo umetolewa jana  na mkuu wa ya wilaya ya Arusha John Mongela wakati  akifungua mkutano mkuu wa    asasi ya umoja wa majiji Tanzania TACINE   inaowakutanisha  wakurugenzi pamoja na mameya wa majiji tanzania uliofanyika mkoani hapa.

  Alibainisha kuwa  watendaji wa halimashauri  zote hapa nchini wanatakiwa kuangalia namna ya kuleta maendeleo katika halimshauri zao kwa kuunda miradi mikubwa  yenye tija  ambayo inaweza kukuza mapato ya halmashauri zao.

  Alisema kuwa  inabidi halimashauri za majiji ziunde miradi   ambayo itasiaidia kuongeza ushuru mkubwa wa masoko wakati miradi hiyo kama ilivyo kuwa   awali  kwa halmashauri ya jiji la Arusha ilikuwa ikikusanya kiasi cha shilingi milioni  kumi ambapo kiasi hicho  kitasiaidia kwani kitaongezaka adi kufikia milioni ishirini.
  Mongela alisema kuwa Halmashauri zina nafasi kubwa ya kufanya miradi mikubwa yenye tija na ambayo inaweza kuleta faida kubwa  na aendeleo makubwa.

  Aidha aliwasihi wakurugenzi pamoja na mameya wote kujitaidi kutumia ipasavyo nafasi zao za ungozi haswa katika swala la kuwaletea wananchi maendeleo ili wakifikia  katika kipindi cha kustaafu au kupunzika katika nafasi zao za uongozi waache kitu hususa ni mradi ambao utakuwa  wa kihistoria. “iwapo meya au mkurugenzi utafanya kitu  ambacho kitakuwa kizuri kama mradi ukifikia kipindi cha kustaafu au utakapo maliza kipindi chako  mradi ambao uliufungua kipindi cha   uongozi wako basi utanufaisha watu na utapata sifa kubwa ambayo aita saulika”alisema Mongela

  Kwa upande wa  mwenyekiti wa   TACINE ambaye ni meya wa jiji la mbeya Atanasi Kapunga alisema kuwa dhamira kubwa ya umoja wao  kukutana katika jiji hili ni kuwaakikisha majiji yote yana kuwa na hadhi ya  inayo fanana . Aliongeza kuwa pia  umoja huu unawezesha  majiji haya kuwa katika hali ya madhari nzuri pamoja na mpangilio uliomzuri ambao unahadhi ya jiji jambo ambalo litapelekea kuongezeka kwa vipato na maendeleo kwa wananchi.

  Kwa upande wa meya wa shinyanga Gulamhafeez Mukadam alisema kuwa umoja  huu umesaidia mambo mengi ikiwa ni pamoja   na  kuleta maendeleo mbalimbali katika halimashauri mbalimbali. Alitolea mfano bara bara za mijini ambazo zimejengwa katika halimashauri   mbalimbali alibainisha kuwa bila umoja huu wa majiji zisingewezwa kujengwa.

  Alibainisha kuwa changamoto moja wapo wanaopata katika umoja huu ni pamoja na kukosa ushirikiano wa kutosha kutoka katika wizara zetu    jambo ambalo alibainisha kuwa ni changamoto kubwa inayowakabili hivyo aliiomba wizara husika ijitaidi kuwapa ushirikiano.

  0 0
 • 03/28/14--12:42: Article 0


 • 0 0

   Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mkutano na Mabalozi wa nchi za Jumuiya ya Ulaya (EU) Ikulu jijini Dar es salaam leo.PICHA NA IKULU.
  0 0

  Bondia Japhert Kaseba akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake wa ubingwa na Thomasi mashali kushoto mpambano utakaofanyika PTA Sabasaba siku ya jumamosi march 29.
  Mabondia Thomasi Mashali kushoto na Japhert Kaseba wakiwa na mkanda ambao wataugombania katika ukumbi wa PTA sabasaba siku ya jumamosi .

  Promota wa mpambano huo Ally Mwazoa akizungumza mbele ya waandishi wa habari
  Mabondia Alani Kamote wa Tanga kushoto pamoja na Karage Suba wakiwa na mkanda watakaougombania kesho kwenye ukumbi wa PTA Sabasaba picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
  Ally Mwazoa akisisitita jambo.

older | 1 | .... | 258 | 259 | (Page 260) | 261 | 262 | .... | 1898 | newer