Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

RADIO 5 YAKULETEA BACK COLLEGE BASH NDANI YA NEW LANDMARK RESORT JUMAMOSI HII


WANAKIBINDU WASEMA :CHONDE CHONDE MH.RIDHIWANI UKIPATA UBUNGE ANZA NA MIUNDOMBINU YA BARABARA KIBINDU

$
0
0
1
Katibu wa CCM Mkoa wa Mtwara Ndugu Shaibu Akwilombe akizungumza na wananchi wa kijiji cha kwa Msanja kata ya Kibindu katika jimbo la Chalinze wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji hicho, ambapo viongozi kadhaa wa Chama cha Mapinduzi wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Ndugu Joseph Msukuma wamewataka wananchi hao wa kata ya Kibindu kumchagua mgombea ubunge wa CCM Bw. Ridhiwani Kikwete kwa kuwa anaweza kuwatatulia matatizo yao mbalimbali yanayowakabili katika kata yao kwani Ridhiwani Kikwete ni msomi, mwanasheria na mtu aliyepewa dhamana na chama cha Mapinduzi chenye uongozi kuanzia shina mpaka ngazi ya kitaifa hivyo wanao uwezo wa kumpata mahali popote kwani anao udhamini wa kuaminika. hata hivyo tatizo kubwa la kata ya Kibindu ni miundo mbinu ya barabara na maji jambo ambalo wananchi hao wanaeleza kwamba ni muhimu mbunge wao anayekuja aanze nalo, Mbunge aliyepita Marehemu Said Ramadhan Bwanamdogo aliugua muda mrefu jambo lililopelekea wananchi hao kukosa mwakilishi wao katika mambo mbalimbali ya maendeleo jimboni humo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KIBINDU-CHALINZE)2Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Ndugu Joseph Msukuma akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kwamsanja Kibindu leo.3
Safari kuelekea kwenye magari

Katibu Mkuu Kiongozi ahitimisha Ziara ya kikazi ya siku mbili kukagua mradi wa bomba la gesi aasilia

$
0
0

 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (katikati) akiwasili kituo cha kufua umeme kwa kutumia gesi asilia kinachojengwa Kinyerezi wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili ya kukagua mradi wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi jijini Dar es salaam. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Mradi huo kutoka kampuni ya Jacobsen Elektro Shaun Moore na wa kwanza ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (katikati) akiteta jambo na Mkurugenzi Mkazi wa Mradi huo kutoka kampuni ya Jacobsen Elektro Shaun Moore (wa kwanza kushoto) na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi.
 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo akiwa na Mkurugenzi Mkazi wa Mradi kutoka kampuni ya Jacobsen Elektro Shaun Moore (wa kwanza kushoto) na wa pili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi na kulia ni Mkurugenzi Mkuu TANESCO Felchesmi Mramba
 Mkurugenzi Mkuu TANESCO Felchesmi Mramba akimweleza Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na msafara wake hatua zilizofikiwa kwenye ujenzi wa kituo cha kufua umeme kwa kutumia gesi asilia kinachojengwa Kinyerezi wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili ya kukagua mradi wa ujenzi wa bomba la gesi jijini Dar es salaam.
Moja ya eneo la kituo cha Kenyerezi I ambapo inajengwa mitambo ya kufua umeme kwa kutumia gesi asilia.  Picha zote na Eleuteri Mangi- MAELEZO.
=======  ========  ========
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO 
Serikali imesema utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirishia gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es salaam unaenda vizuri kulingana na  ratiba yake na utakamilika kwa wakati. 
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue alipotembelea kituo cha kufua umeme kwa kutumia gesi asilia kinachojengwa Kinyerezi wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili ya kukagua mradi wa ujenzi wa bomba la gesi jijini Dar es salaam. 
Balozi Sefue alisema kuwa ni vema kufanyakazi kwa uadilifu na hakuna mchezo, kazi ikitolewa ikamilike kwa wakati. 
"Tujenge uchumi wa nchi yetu kwa kutumia umeme wa uhakika, uhakika huo unatokana na gesi asilia tuliyonayo" alisisitiza Balozi Sefue.
 Akifafanua zaidi Balozi Sefue alisema kuwa kugunduliwa kwa gesi nchini kumeanza kuleta manufaa mengi ikiwamo wanafunzi kupata udhamini katika masomo yao katika ngazi mbalimbali za elimu, shule zimejengwa, wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara wanapata maji safi na kupata ajira mbalimbali. 
 Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi alisema kuwa fedha za ujenzi wa kituo cha kinyerezi I na ujenzi wa vituo vingine vya kinyerezi II, III na IV, zinatolewa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wahisani. 

Fedha za ujenzi wa kituo cha Kinyerezi I zimetolewa na Serikali kupitia TANESCO na ujenzi wa kituo cha kinyerezi II fedha itatokana na ubia kati ya Serikali ya Tanzania na Japani , wakati ujenzi wa kinyerezi III na IV fedha zitatokana na kuingia ubia kati ya Serikali na kampuni ya Kichina. Alimhakikishia Balozi Sefue kuwa Wizara yake ipo tayari kupokea maelekezo na ushsuri kutoka ngazi za juu za Serikali katika kutekeleza mradi huo wa ujenzi wa bomba la gesi asilia na hatimaye kuongeza uzalishaji wa umeme ili kujenga uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka  2025. 

 Mkurugenzi Mkazi wa Mradi huo Bw. Shaun Moore, alimweleza Katibu Mkuu Kiongozi na msafara wake kuwa maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho yanaendelea vizuri kutokana na kampuni hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano mzuri na kampuni za kitanzania zilizochukua kandarasi tofauti za ujenzi wa kituo hicho ambapo takribani asilimia 98 ya kandarasi na wafanyakazi ni kutoka kampuni za kitanzania. 
Ziara hiyo ilianzia mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani na kuhitimishwa Dar es salaam ambapo Katibu Mkuu Kiongozi aliambatana na Makatibu Wakuu 12 wa Wizara zinzotekeleza Mpango wa Mataokeo Makubwa Sasa (BRN).

NSSF MEDIA CUP KUANZA KUTIMUA VUMBI MACHI 29

$
0
0
Meneja Kiongozi Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume akizungumza wakati swa hafla ya kukabidhi vifaa kwa timu zinazoshiriki mashindano ya NSSF Media Cup yanayotarajiwa kuanza rasmi Machi 29. 
 Meneja Kiongozi Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume akizungumza wakati swa hafla ya kukabidhi vifaa kwa timu zinazoshiriki mashindano ya NSSF Media Cup yanayotarajiwa kuanza rasmi Machi 29.
 Meneja Kiongozi Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume akimkabidhi vifaa vya michezo, mwakilishi wa timu ya Star Tv, Tom chilala kwa ajili ya mashindano ya NSSF CUP yanayotarajiwa kuanza Machi 29.
Baadhi ya vifaa vilivyotolewa kwa timu shiriki katika michuano ya NSSF Media Cup.
 Meneja Kiongozi Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume (kushoto), akimkabidhi vifaa vya michezo, mwakilishi wa Kampuni ya Free Media Ltd, wachapishaji wa magazeti ya Tanzania Daima na Sayari, Francis Dande kwa ajili ya mashindano ya NSSF MEDIA CUP yanayotarajiwa kuanza Machi 29. 


 Meneja Kiongozi Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume (kushoto), akimkabidhi vifaa vya michezo mwikilishi wa Jambo Leo, Julius Kihampa.
 Antony Siame, mwakilishi wa gazeti la Raia Mwema akipokea vifaa vya michezo kutoka kwa  Meneja Kiongozi Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume (kushoto).

Na Mwandishi Wetu

JUMLA ya sh. millioni 19 zimetolewa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), ikiwa ni fedha taslimu zitakazotolewa kwa washindi mbalimbali wa michezo ya NSSF MEDIA CUP 2014 itakayoanza Machi 29.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Meneja Kiongozi wa Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika hilo, Eunice Chiume, alisema kuwa maandalizi ya michuano hiyo imekamilika na kwa upande wa mpira wa miguu mshindi wa kwanza atapata Tshs. 4,500,000, mshindi wa pili atapata Tshs.3,500,000 na watatu atapata Tshs. 2,000,000.

Aidha alisema, kwa upande wa mpira wa Pete mshindi wa kwanza atazawadiwaTshs. 4,000,000, mshindi wa pili  Tshs.3,500,000 na mshindi wa tatu atazawadiwa Tshs. 2,000,000 taslimu.

“Wachezaji bora wa mashindano haya  kwa upande wa mpira wa miguu na pete wote wata zawadiwa kila mmoja Tshs 350,000 ili kuongeza hamasa  katika michezo hiyo” alisema Chiumea.

Alisema kuwa, mashindano hayo yatashindaniwa kwa njia ya mtoano kwa mechi za mpira wa miguu na pete, yatashirikisha  timu 20 za mpira wa miguu na 18 za mpira wa  pete kutoka vyombo vya habari  vya jiji la Dar es Salaam na Zanzibar.

“Timu zitakazoshiriki kwenye mashindano  hayo ni IPP, Free Media , BTL, New Habari, Mwananchi, Uhuru, Habari  Zanzibar, Tumaini Media, Star TV na TBC ambapo kilele cha michuano hiyo iatkuwa tarehe 12 April mwaka huu ambapo mwenyeji wake ni NSSF” alisema.

Alieleza kuwa, mbali ya timu alizozitaja pia kuna timu nyingine ambazo zipo katika michuano hiyo ikiwa ni TSN, Mlimani, Radio Maria, Wizara ya Habari, Global Publishers, Jambo Leo,  Raia Mwema na Azam  TV ambapo mechi zote zitafanyika uwanja wa DUCE-Chang’ombe na TCC–Club na fainali kufanyika hapo.

Michuano ya NSSF Media Cup 2014, imetimiza miaka 11 tangu kuanzishwa na inakwenda sambamba na sherehe za miaka 50 ya NSSF na pia mika 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Michuano ya mwaka huu ikifanyika katika sherehe hizo kubwa mbili ndio yenye idadi ya timu zinazoshiriki kuliko mwaka mwingine tangu michuano hiyo ianze mwaka 2004.

Michuano hii ilianzishwa mwaka 2004 kwa kuzishirikisha timu 8 mpaka sasa timu zinazoshiriki zimefikia timu 20 wakati mpira wa Pete timu zimeongezeka kutoka 7, miaka mitano iliyopita tangu  mchezo huu ulipozinduliwa kwenye mashindano ya NSSF Media Cup. 

NIMR YAENDELELEA KUWA KINARA TAFITI ZA MAGONJWA YA BINADAMU

$
0
0
 Mtafiti toka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu  NIMR kituo cha Muhimbili Dkt. Godfather Kimaro akitoa wito kwa wanchi kujitokeza kwa aajili ya kupima afya zao mara tu wanapoona dalili za ugonjwa wa Kifua Kikuu ili kupunguza maambukizi mapya. Katikati ni Mkurugenzi wa NIMR kituo cha Muhimbili Dkt Godfrey Mfinanga na wa mwisho kulia ni Afisa habari Idara ya Habari MAELEZO Frank Mvungi.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu NIMR kituo cha Muhimbili Dkt Godfrey Mfinanga akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu hali ya maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu , wa mwisho kulia ni Afisa habari Idara ya Habari MAELEZO Frank Mvungi. Picha zote na Georgina Misama-MAELEZO

Frank Mvungi-Maelezo


Serikali yaendelea kuimarisha Tafiti za kifua kikuu hapa nchini  kwa kushirikiana na Taasisi za Kimataifa. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa  ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kituo cha Muhimbili Dkt.Godfrey Mfinanga wakati wa mkutano na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam.

Akieleza Dkt.Mfinanga alisema kuwa NIMR kituo cha Muhimbili imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika tafiti kwa kushirikiana na Taasisi za kimataifa kama African Research Consortium for Ecosystem and Population Health (AFRIQUE ONE CONSORTIUM) na East African Consortium for Clinical Research ( EACCR).

Dkt Mfinanga alibainisha kuwa wastani  wa wagonjwa 295 kati ya watu 100,000  hugundulika kuwa na TB ,ambapo Tanzania bara ilionekana kuwa na wagonjwa wengi zaidi kuliko Tanzania Visiwani,Vijijini kuliko mijini,watu wazima kuliko vijana,ambapo utafiti huo uko hatua za mwisho.


Akifafanua zaidi amesema tafiti zimeonyesha kuwa kwa wastani wa asilimia 35 ya wagonjwa wa TB huchelewa kugundulika  kutokana na uelewa mdogo na tabia ya wananchi walio wengi kuchelewa kwenda Hosipitali. Dkt Mfinanga  alitaja maeneo yanayoathiriwa na Ugonjwa wa kifua kikuu kuwa ni mapafu ,tezi,tumbo,figo, na hata ubongo ikiwa mgonjwa hatapata matibabu kwa wakati muafaka.

Katika hatua nyingine Dkt Mfinanga amesema kuwa  NIMR kituo cha Muhimbili imefanya utafiti ambao umethibitisha kuwa kuna umuhimu  wa kushirikisha jamii katika kusimamia matibabu ya wagonjwa wa TB (Community DOT-PCT).

Kufuatia utafiti huo Serikali ilianzisha mfumo huo ambao umeonyesha mafanikio makubwa kwa kuwa mgonjwa anachagua mahali pa kumezea dawa za TB kati ya nyumbani akisimamiwa na ndugu au kwenye kituo cha tiba akisimamiwa na mtoa huduma wa afya.


Naye mtafiti toka NIMR kituo cha Muhimbili Dkt. Godfather  Kimaro alitoa wito kwa wananchi kuwahi hosipitali pale wanapoona dalili za ugonjwa wa Tb ambazo baadhi yake ni kikohozi kwa muda wa wiki mbili,homa za mara kwa mara na kukonda.


Kituo cha Utafiti cha Muhimbili (NIMR  Muhimbili Centre) ni moja ya vituo nane vya Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya Binadamu (NIMR) Kituo cha Muhimbili kilirithiwa kutoka lililokuwa Baraza la Afrika ya Mashariki mwaka 1980 wakati Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa magonjwa ya Binadamu ilipoanzaishwa kwa sheria ya Bunge Namba 23 ya mwaka 1979.

Mkuu Chuo cha GTI, Bi. Zuki Mihyo Afungua Mafunzo ya Jinsia, Demokrasia na Katiba

$
0
0
Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Bi. Zuki Njalai Mihyo (kulia, aliyesimama) akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya yalioandaliwa na GTI. Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Bi. Zuki Njalai Mihyo (kulia, aliyesimama) akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya yalioandaliwa na GTI.Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Bi. Zuki Njalai Mihyo (aliyesimama) akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya yalioandaliwa na GTI. Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Bi. Zuki Njalai Mihyo (aliyesimama) akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya yalioandaliwa na GTI.Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya. Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya.Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Bi. Zuki Njalai Mihyo (aliyesimama) akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya yalioandaliwa na GTI. Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Bi. Zuki Njalai Mihyo (aliyesimama) akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya yalioandaliwa na GTI.Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya. Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya.

MKUU wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Bi. Zuki Njalai Mihyo leo jijini Dar es Salaam amefungua mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya yaliyowashirikishwa washiriki kutoka katika mikoa ya Dar es Salaam, Lindi, Pwani na Morogoro.

 Akizungumza katika hotuba yake ya ufunguzi wa mafunzo hayo yanayofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Jinsia kilichopo eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam, Bi. Zuki Mihyo alisema kutokuwepo na misingi imara ya kutetea, kulinda na kudumisha demokrasia iliyojengwa kwenye misingi ya usawa wa kijinsia inayo tambulika Kikatiba kumechangia uwepo wa tatizo la unyanyasaji wa kijinsia nchini. 

 Alisema tatizo la unyanyasaji wa kijinsia licha ya kuwapata watu wa jinsia zote, limekuwa likiwaathiri zaidi wanawake na watoto wa kike tofauti na ilivyo kwa wanaume na watoto wa kiume katika jamii, hivyo kushauri kuna kila sababu ya kupambana na mifumo kandamizi inayochangia hali hiyo. "...Wanawake na watoto wa kike mara nyingi wamekuwa wakifanyiwa ukatili huu na wanaume au wavulana ambao wanaweza kuwa ndugu zao wa karibu, marafiki na hata wenzi wao," alisema Mkuu huyo wa chuo cha GTI kilichopo chini ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP).Mmoja wa watoa mada wa mafunzo hayo, Geoffrey Chambua (aliyesimama katikati) akizungumza na washiriki wa mafunzo. Mmoja wa watoa mada wa mafunzo hayo, Geoffrey Chambua (aliyesimama katikati) akizungumza na washiriki wa mafunzo.

Alisema suala la ukekelezaji wa mila na desturi kama vile ukeketaji, kurithi wajane na mila nyingine nyingi zinazowagandamiza wanawake na makundi ya pembezoni na kuwafanya kutokuwa na sauti wala kushiriki katika kutoa uamuzi kuanzia ngazi ya familia hadi taifa vimekuwa vikichangia ukatili wa jinsia kwa wasichana, wanawake na makundi mengine ya pembezoni. 

 "...Tunaelewa kuwa wakati wa zamani mila nyingi zilikuwa na maana lakini kwa wakati huu mila hizo zimepitwa na wakati hivyo ziachwe ili kukomesha dhuluma, manyanyaso, ukandamizaji n.k, ili kuwa na usawa kwa watu wote," alisema. Aidha alifafanua kuwa lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa washiriki kuweza kushiriki katika kuchambua masuala ya jinsia, demokrasia na katiba mpya ili waweze kuyasimamia na kuyatetea katika mikakati mbalimbali ya maendeleo. 

Aliongeza kuwa malengo mahususi ni pamoja na kukuza uelewa na utambuzi wa uhusiano baina ya dhana za jinsia, demokrasia na katiba, kuchochea ushiriki na uwajibikaji wa asasi za kiraia na makundi maalumu yaliopo pembezoni na mchakato wa kidemokrasia na kutambua changamoto na fursa zilozopo katika kuingiza masuala ya jinsia na demekrasia kwenye katiba mpya. 

 Akifafanua zaidi juu ya mafunzo hayo, mmoja wa watoa mada, Geoffrey Chambua alisema washiriki wanatoka katika ngazi ya jamii; yaani katika asasi za kiraia, vikundi vya kijamii, asasi za kidini, wajasiliamali na makundi maalumu wote kutoka katika mikoa ya Morogoro, Lindi, Pwani pamoja na Dar es Salaam yenyewe. Chambua alisema mafunzo kama hayo pia yanaendelea katika kanda anuai.

UONGOZI WA DAMPO WAAGIZWA KUREKEBISHA MIUNDOMBINU YA BARABARA

$
0
0
DSC_0458
Gari la Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick likiwasili Dampo kuu la taka la Pugu Kinyamwezi, lililopo maeneo ya Gongo la Mboto jijini Dar alipofanya ziara ya ghafla kwenye dampo hilo.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog).

Na. Damas Makangale, MOblog.

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick ametoa agizo mara moja kwa uongozi wa Dampo nje kidogo la jiji la Dar, Pugu Kinyamwezi, kurekebisha miundombinu ya barabara pamoja na taa ili kurahisisha umwagaji wa taka katika dampo hilo. MOblog inaripoti.

Akizungumza na baadhi ya viongozi wa wilaya na jiji hivi karibuni baada ya kufanya ziara ya ghafla katika maeneo kadhaa ya jiji la Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa amesema tatizo la miundombinu ya barabara kuelekea katika Dampo la Pugu Kinyamwezi linasababisha foleni kwa malori ya kusomba taka katika jiji la Dar.

“mara ya mwisho wakati nakuja hapa kukagua hili dampo kulikuwa na taa na kazi ilikuwa inafanyika usiku na mchana sasa kumetokea nini,” alihoji Mkuu huyo wa Mkoa
Sadick aliagiza kwa viongozi wa jiji kushughulikia haraka tatizo la miundombinu ya barabara kuelekea Dampo ili kuongeza tija katika kazi ya kumwaga na kusomba taka katika jiji la Dar es Salaam.
DSC_0468
Kaimu Mkuu wa Idara ya Udhibiti taka kutoka halmashauri ya jiji, Bi. Enezael Ayo (kushoto) akifafanua jinsi magari ya taka yanavyomwaga taka katika dampo kuu taka la Pugu Kinyamwezi jijini Dar wakati wa ziara ya Mkuu wa mkoa wa Dar.

Alisisitiza kwamba utaratibu mbovu wa umwagaji taka na miundombinu mibovu katika Dampo la Pugu Kinyamwezi vinasababisha mrundikano wa taka katika manispaa zote za Temeke, Ilala na Kinondoni.

Amesema kwamba ni muhimu kwa viongozi wa jiji kupata nguvu kazi ya kutosha ili kuwe na watu watakaosimamia umwagaji wa taka wakati wa usiku ili kudhibiti madereva wakorofi wanaomwaga taka ovyo bila kuzingatia taratibu.Sadick aliongeza kuwa watendaji wa jiji ni lazima wawe na utaratibu wa kutoa mafuta kwa wakati kwenye magari ya kusomba (Bull Dozer) na vitendea kazi vingine.
DSC_0485
Mkuu wa mkoa wa Dar, Said Meck Sadick akitoa agizo mara moja kwa uongozi wa Dampo nje kidogo la jiji la Dar, Pugu Kinyamwezi, kurekebisha miundombinu ya barabara pamoja na taa ili kurahisisha umwagaji wa taka katika dampo hilo. Mkuu wa Mkoa aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ndg. Raymond Mushi(mwenye suti nyeusi).

Wakati akitembelea maeneo kadhaa kati kati ya jiji kuanzia soko la Kisutu na mitaa ya Libya, Mkuu wa Mkoa aliagiza mamlaka zinazohusika kushughulikia haraka tatizo la maji machafu kupunguza harufu na kuzuia magonjwa ya mlipuko. “nawaagiza mkae pamoja na mje na mpango mkakati utakaowezesha kumaliza tatizo la maji machafu yanayotoka katika mitaro na mifereji ya maji machafu katika ya jiji,” aliongeza.

Wakati huo huo, wadau kadhaa wa usombaji taka katika jiji la Dar es Salaam wameomba serikali kutoa kipaumbele kwa Dampo la Pugu Kinyamwezi na kulitengea bajeti ya kutosha ili liweze kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
DSC_0479
Mkurugenzi Mtendaji wa Tirima Enterprises, Bw. Robert Ngeleshi akizungumzia changamoto na matatizo ya mawakala wa kusomba taka katika jiji la Dar ambao waliongozana na Mkuu wa mkoa kwenye ziara hiyo.
DSC_0557
Mkuu wa mkoa wa Dar, Said Meck Sadick aliyeambata na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ndg, Raymond Mushi wakiondoka eneo la tukio mara baada ya kuhitimisha zoezi la kukagua miundo mbinu ya Dampo la taka la Pugu Kinyamwezi. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Minael Mshanga.

Article 17

$
0
0
Zanzibarlicious potrait
ZANZIBAR NI ZAMU YENU SASA KUUNGANA NA WANAWAKE WENZENU WA KUNDI LA ZANZIBALICOUS WOMEN GROUP NA KUSHEHEREKA NAO KATIKA UZINDUZI WA KUNDI LAO KATIKA KUUMALIZIA HUU MWEZI WA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI
LITAKALOFANYIKA ::OCEAN VIEW BEACH RESORT
TAREHE ::28 MARCH
BURUDANI ::COCONUT BAND
KWA KIINGIILIO ::100,000 VIP & 50,000 VITI VYA KAWAIDA
KUBOOK /KUNUNUA TIKETI PIGA ::0713 868766,0773 662 662 ,0777 777441 , 0777 418324

PROMOSHENI YA WINDA SAFARI YA BRAZIL NA SERENGETI INAENDELEA.

$
0
0
 Meneja wa Bia ya Serengeti Rodney Rugambo akibonyeza kitufe cha kuchezesha droo ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti mapema leo katika ofisi za Kiwanda cha Bia chaa Serengeti jijini Dar es Salaam, huku akishuhudiwa na Afisa Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha  Tanzania Bakari Maggid(kushoto) na Afisa Mwandamizi kutoka PWC Golder Kamuzora(kulia). 
Meneja wa Bia ya Serengeti Rodney Rugambo akizungumza na wana habari wakati wa droo ya saba ya promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti inayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti mara baada ya kuchezesha droo hiyo mapema leo katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam na kulia kwake ni Afisa Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bakari Maggid.


PROMOSHENI YA WINDA SAFARI YA BRAZIL NA SERENGETI INAENDELEA.

Washindi Zaidi kupatikana, zawadi za ving’amuzi na simu za kisasa zazidi kutolewa!


26 Machi, 2014: katika hafla fupi mapema leo kampuni ya bia ya Serengeti imeendelea kuchezesha droo zake za winda safari ya Brazil na Serengeti na leo washindi wawili wa simu za kisasa aina ya Samsung galaxy tablet wamepatikana. 

Kwa mtu kujishindia zawadi zetu unahitaji kununua chupa ya bia ya Serengeti na kuangalia chini ya kizibo ambapo utakuta bia ya bure au tarakimu 6 ambazo utazituma kwa ujumbe mfupi kwenda namba 15317 ambapo utapata ujumbe ukikujulisha kama umejishindia fedha taslimu kati ya shilingi 5000 na shilingi 10000 na pia namba yako itaingizwa katika droo ambapo utaweza kujishiandia king’amuzi, simu ya mkononi au tiketi ya kwenda Brazil.


Mji wa moshi katika maeneo ya majengo umepata bahati ya kutoa washindi wawili wa simu aina ya Samsung tablet. Juma lililopita katika droo ya 6 ya winda safari ya Brazil washindi wawili waliopatikana wote wanatokea katika maeneo ya Majengo Moshi. Droo hiyo ilishuhudiwa na waandishi wa habari, ofisa kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha, PWC pamoja na Push mobile media. Droo kubwa itatoa tiketi ya kwenda Brazil ambaponmshindi atalipiwa gharama zote kwa siku atakazokaa huko.


Meneja wa bia ya Serengeti Bw Rodney Rugambo aliongea na mshindi wa kwanza Bw Matei Kleti Mofulu kutoka Nyakato, Mwanza. Akiwa na furaha muda wote wa maongezi alisema hajaamini kama ameshinda na amekuwa akiamini michezo hii siyo ya ukweli ila Serengeti wamemfumbua macho kuwa ni za kweli. 

Mshindi wa pili pia alipokea habari hizi kwa furaha na kusema kuwa ni muda kuwa wa kisasa kwa kutumia simu ya kisasa. Pia mshindi wa pili wa simu ya kisasa Bw Godwin Paul ambaye ni mwanajeshi wa JWTZ aliishukuru kampuni ya bia ya Serengeti kwa zawadi hiyo na kuwashauri watumiaji wa Serengeti kushiriki katika promosheni hii.


Tafrija fupi za kugawa zawadi kwa washindi zimeendelea katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania ambapo katika juma lililopita mshindi wa simu ya kisasa wa Dar es Salaam alikabidhia zawadi yake katika maenao ya kimara. Mshindi huyo Bw Erick Mazigo alishukuru kampuni ya bia ya Serengeti kwa kuwa waaminifu kwa wateja wao na kuwapa zawadi zao. Promosheni ya winda safari ya Brazil ambayo imekuwa gumzo nchi nzima imeshapata washindi Zaidi ya 100000 wa bia za bure, Zaidi ya washindi 13000 waliojipatia fedha taslimu shilingi 5000 na 10000.

Kunywa kistaarabu; washiriki wanatakiwa kuwa na umri wa Zaidi ya miaka 18; vigezo na masharti kuzingatiwa.


RIDHIWANI AZIDI KUCHANJA MBUGA CHALINZE

$
0
0
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimnadi mgombea wa nafasi ya ubunge jimbo la Chalinze  kupitia CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye kijiji cha Mazizi ambapo alisema moja ya sifa za mgombea ni kuwafahamu wananchi wake, na wananchi wake kumfahamu, kufahamu changamoto za wananchi na kufahamu namna ya kuzitatua changamoto hizo.
 Ridhiwani Kikwete akijinadi kwa wananchi wa kijiji cha Mazizi kata ya Msata ambapo aliahidi kujenga shule,kusaidia wakina mama na vijana,kushirikiana na wana Chalinze katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya afya,kuinua kilimo,kufanya juhudi za dhati kuboresha kilimo.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Ridhiwani Kikwete  akifungua shina la Tonga Road wakati  wa ziara za mikutano ya  kampeni za ubunge.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha Tonga wakati wa kumnadi mgombea wa CCM jimbo la Chalinze Ndugu Ridhiwani Kikwete.
 Wazee wa kijiji cha Diozile wakisoma vipeperushi vyenye wasifu wa Ridhiwani Kikwete wakati wa mkutano wa kampeni za ubunge jimbo la Chalinze zilizofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Lubaya.
 Kila aina ya furaha kwa vijana wa Msoga ambapo mgombea wa Ubunge jimbo la Chalinze Ndugu Ridhiwani Kikwete alifanya mkutano wa hadhara kwa wananchi wa kijiji hicho.
 Karibu wa NEC Itikadi na Uenezi akihutubia wapiga kura wa Ridhiwani Kikwete wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Msoga ambapo wananchi hao wamesema kijijini kwao hakutokuwa na kura kwa wapinzani.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Ridhiwani Kikwete akikata utepe kufungua shina la UVCCM Msoga baada ya kumaliza mkutano wa hadhara wa kampeni za ubunge.

WINDHOEK BEER YADHAMINI SHEREHE YA KUTIMIZA MIAKA 3 YA KLABU YA BONGO MOVIE ITAKAYOFANYIKA KESHO NDANI YA UKUMBI WA EAST 24

$
0
0
 Mwenyekiti wa Bongo Movie, Bw Steve Nyerere akiongea na waandishi wa habari wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa East 24 uliopo Arcade house Mikocheni.
 Steve Nyerere akinadi kinywaji cha Windhoek ambao ndio wadhamini wakuu wa sherehe ya Kutimiza Miaka 3 ya kuzaliwa kwa Bongo Movies, Sherehe itakayofanyika katika Ukumbi wa East 24 uliopo Arcade House Mikocheni jijini Dar Es Salaam Ijumaa ya tarehe 28.
Rais wa FM Academia Nyoshi Ali Sadat akiongea na wadau waliofika katika ukumbi wa East 24 wakati wa utambulisho wa wasanii na bendi zitakazotoa Burudani siku ya Sherehe ya Kuzaliwa kwa klabu ya Bongo Movie itakayofanyika katika ukumbi wa East 24 uliopo Arcade House ijumaa ya tarehe 28 Mwezi huu
 Meneja Masoko wa Kampuni ya Mabibo Beer, Bw Jerome Rugemalila akiongea na Waandishi wa habari wakati wa utambulisho wa Bendi na wasanii watakaotoa burudani ya nguvu siku ya sherehe ya Kuzaliwa kwa Bongo Movie itakayofanyika tarehe 28 katika Ukumbi wa East 24 uliopo Arcade House Mikocheni Jijini Dar.
 Baadhi ya wasaniii wa Bongo Movies wakifuatilia kwa makini 
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mabibo Beer, Benadetha Rugemalira (aliyeshika kinywaji cha Climax) akifuatilia kwa makini matukio wakati wa utambulisho wa Wasanii na bendi zitakazotoa burudani siku ya ijumaa kwenye sherehe ya Kuazimisha miaka 3 ya kuzaliwa kwa Bongo Movie
 Baadhi ya wadau waliohudhuria utambulisho huo uliofanyika katika ukumbi  wa East 24
 Mkurugenzi Mkuu wa Mabibo Beer, Mama Benadetha Rugemalira (kulia) akijadiliana jambo na Meneja masoko wa Mabibo Beer, Jerome Rugemalira (pili kulia) na Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie, Bwa Steve Nyerere na Msanii wa bongo movie Adam Kuambiana
Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve Nyerere akijadiliana jambo na Katibu wa Bongo Movie Mtitu wakati wa utambulisho wa Wasanii na bendi zitakazotoa burudani wakati wa sherehe za kutimiza miaka mitatu ya kuzaliwa kwa klabu ya Bongo Movie.

Semina ya mawakala wa shindano la Redd's miss Tz yafungwa Rasmi

$
0
0
 Meneja wa kinywaji cha Redd’s Origina Victoria kimaro katikati akiwa katika picha ya pamoja na baadhi wa viongozi wa kamati ya Miss Tanzania katika siku ya kufunga semina ya mawakala wa shindano la Redd’s miss Tanzania kwa mwaka huu, kushoto kwake ni mkurugenzi wa kampuni ya LINO Intenational Agency Hashim Lundenga, Redd’s Miss Tz 2013 Happines Watimanya na Meneja masoko wa TBL Vimal Vaghmaria kulia mwenye miwani.
 Redd’s Miss Tz 2013 Happines Watimanya  akiwa katika picha ya pamoja na mawakala wa shindano la Redd’s miss Tanzania 2013 kwenye semina ya mawakala hao kulia waliokaa ni meneja wa Redd’s Original Victoria kimaro na kushoto ni Meneja masoko wa TBL Vimal Vaghmaria mwenye miwani na wa mwisho ni mkuu wa itifaki wa kamati ya Miss Tanzania Albert makoye
 ========  =======  ======
MAWAKALA wanaoandaa mashindano ya urembo hapa nchini ‘Redd’s Miss Tanzania 2014” kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini wametakiwa kutotangaza zawadi kwa washindi ambazo hawana kwa sababu wakifanya hivyo wanashusha heshima ya mashindano hayo imeelezwa jana jijini Dar es Salaam.
Akizungmza jana katika semina ya mawakala hao, Meneja wa bia ya Redd’s Original, Victoria Kimaro, alisema kuwa hali hiyo inawafanya washiriki, wazazi, walezi na wadau wa sanaa hiyo kuzungumzia vibaya sanaa hiyo.
Kimaro aliwataka mawakala hao kuhakikisha wanatangaza zawadi walizokuwa nazo na kuwakumbusha pia kutafuta warembo wenye vigezo vya juu ili baadaye mmoja wao aweze kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi katika fainali za dunia.
“Usiahidi kitu usichokuwa nacho, watu wameahidi vitu vikubwa ambavyo hawajafanikiwa kuvipata mpaka siku ya shindano…sio vizuri na ninawashauri msifanye tena hivyo ili kujenga shindano letu,” alisema meneja huyo wa Redd’s.
Aliwataka mawakala hao pia kufanya mazungumzo na makampuni na taasisi nyingine kwa ajili ya kuomba udhamini wa kusaidia mashindano hayo na si kutegemea wadhamini wakuu peke yao ambao wanhitaji kusimamia fainali za taifa kikamilifu.
“Tujipange kufanya maandalii yaliyo bora…kama Redd’s tutajaribu kufika kila mahali kwa uwezo wetu ila nawasisitiza na kuwakumbusha tafuteni mbinu za kuuza mashindano yenu,” aliongeza Kimaro.
Naye Mshauri wa Ufundi wa Kamati ya Redd’s Miss Tanzania, Ramesh Shah, aliwataka mawakala hao kuwaandaa vizuri washiriki kwa sababu wengi wao wanakuwa ni wahitimu wa elimu ya Sekondari hivyo wanahitaji mwongozo.
Aliwataka mawakala hao kuthamini sanaa hiyo ya urembo kwa sababu ni moja ya michezo inayosaidia kukuza uchumi na kutangaza jina la nchi katika ngazi mbalimbali.
Redd’s Original ndiyo wadhamini wakuu wa shindano hilo kwa mwaka watatu mfululizo na mwaka huu wanatarajiwa kutumia zaidi ya Sh. Milioni 500….

KATIBU MKUU WA CCM,KINANA AJITWISHA SAKATA ZITO LA UJENZI WA MJI MPYA KIGAMBONI

MWILI WA MAREHEMU MKUU WA MKOA WA MARA WAWASILI DODOMA LEO

$
0
0

Askari wakiwa wamebeba mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tupa baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege Dodoma leo Machi 27, 2014. Marehemu ataagwa kwenye viwanja vya Nyerere Dodoma Machi 28, 2014 kabla ya kusafirishwa  kwenda kilosa kwa mazishi. 
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

RIDHIWANI KIKWETE AENDELEA NA KAMPENI KATIKA KATA YA BWILINGU LEO

$
0
0
 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete akilakiwa na Wananchi wakazi wa Kijiji cha Chahua,Kata ya Bwilingu leo Machi 27, 2014 wakati wa Muendelezo wa Kampeni zake za kuomba ridhaa kwa Wananchi hao ya kuwa kiongozi wao kwa Maendeleo ya Jimbo la Chalinze.Picha zote na Othman Michuzi.
 Meneja wa Kampeni za CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Steven Kazidi akiwasisitiza Wananchi wa Kijiji cha Chahua kuzitunza vyema Shahada zao za kupigia kura,ili siku ikifika ya kupiga kura wasipate shida na waweze kupiga kura Mtu anaefaa kuwa Kiongoizi wa Jimbo la Chalinze. 
 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwahutubia na kutoa Sera zake kwa wananchi wa Kijiji cha Chahua,Kata ya Bwilingu leo Machi 27, 2014 .
 Mwenyekiti wa Kijiji cha Chahua,Christina Kejeli (kulia) akitoa maelezo ya Maendeleo ya Kijiji kwa Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kushoto) wakati wa muendelezo wa Mikutano ya Kampeni iliyofanyika leo Machi 27, 2014 katika vijiji vya Chahua na Matuli,Kata ya Bwilingu.
 Diwani wa Kata ya Bwilingu,Ahmed Kalama akisisitiza jambo wakati wa kuzungumzia mafanikio ya Kata yake pamoja na Changamoto ambazo bado hazijafanyiwa kazi ndani ya Kata hiyo,mbele ya Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze.
 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwasalimia wakina Mama wa jamii ya watu Wafugaji (Wamasai) wakati alipowasili kwenye Kijiji cha Matuli kwa ajili ya kuendelea na Mikutano ya Kampeni zake za kuomba ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze.



Baraza la vyama vya siasa lataka wajumbe wa Bunge la Katiba kuweka mbele utaifa.

$
0
0

Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini Peter Kuga Mziray(katikati) akitoa tamko la Kamati ya Uongozi wa Baraza hilo leo mjini Dodoma juu ya mwenendo wa Bunge Maalum la Katiba ambapo aliwataka kuzingatia kanuni za Bunge hilo zinazokataza vitendo vyovyote vya utovu wa nidhamu ndani ya Bunge. Wengine ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili wa Baraza hilo Nancy Mrikaria(kushoto) na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge na Siasa wa Baraza hilo Rashid Mtuta(kulia).

 (Picha na Maelezo-Dodoma) 

(Na Magreth Kinabo ,MAELEZO Dodoma)
KAMATI  ya Uongozi wa Baraza la Vyama vya Siasa inawaomba wajumbe wote wa Bunge Maalum la Katiba kuzingatia kanuni  kwani zinakataza vitendo vya utovu wa nidhamu wakati wa vikao vya Bunge hilo .

 Kauli hiyo imetolewa leo mjini  na  Mwenyekiti wa Baraza hilo, Peter Mziray  katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma kufutia baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo kuonesha vitendo visivyo na nidhamu  ikiwemo kuzomea.    
           
“ Kamati ya  Uongozi wa Baraza la Vyama vya Siasa inawaasa wajumbe wote wa Bunge Maalum la Katiba kubadilika na kuonesha nidamu ambayo Watanzania wote wanategemea kutoka kwao,” alisema Mziray.

 Alisema  Kamati hiyo inaamini kuwa mjumbe anaweza kutoa hoja yake nzito ya kukubali na kupinga jambo ikakubalika au kukataliwa na wajumbe wengine  wengine au Mwenyekiti bila ya kuzomewa.

Aidha Mwenyekiti  huyo Mziray amemtaka Mwenyekiti wa Bunge Maalum kutoyatambua makundi ya Tanzania Kwanza na UKAWA kwa kuwa sio makundi rasimu ndani ya Bunge hilo na ndio yanasababisha vurugu kwa kuweka maslahi ya vya siasa mbele badala ya Taifa.

Amewataka wajumbe  wa Bunge Maalum la Katiba kuacha kujihusisha na makundi  hayo  badala yake wachambue na kuunga mkono hoja kwa uzito wa hoja na kuzingatia masilahi ya taifa badala ya kuzingatia mtazamo wa kundi fulani. 

Mziray ameongeza kuwa wajumbe wanatakiwa kuepuka vitendo ambavyo vinakwamisha mchakato wa kupata Katiba mpya kwa mustakabali wa taifa hili na Wananchi kwa ujumla.


Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo amesema kuwa Kamati ya Uongozi  imeona ni vema wajumbe wa baraza hilo, wakuu wa vyama vya siasa, ambao si wajumbe wa baraza hilo wakutane ili kujadiliana, kushauriana na kuridhiana ili kuweza kufanikisha  azma ya kupatikana kwa Katiba Mpya  kwa mwafaka.

Watumiaji ardhi umewataka wajumbe wa Bunge la Katiba kufanya kazi walizotumwa na wananchi.

$
0
0

Mwenyekiti wa Umoja wa Watumiaji Ardhi ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Dkt. Maselle Nzingula Maziku (katikati) akitoa tamko la Umoja huo leo mjini Dodoma la kuwataka wanasiasa waliomo katika Bunge hilo kuacha mabishano na badala yake wafanye waliotumwa na wananchi ya kuichambua rasimu ya Katiba ili kufikia malengo yaliyokusudiwa. Wengine katika picha ni Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo ambye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Issa Suleman (kulia) na Kushoto ni Katibu wa Umoja huo na Mjumbe wa Bunge hilo Doreen Maro.



(Picha na Maelezo-Dodoma) 

(Na Magreth Kinabo- MAELEZO,Dodoma)
Umoja wa Watumiaji wa Ardhi umewataka wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kuanza kuifanya kuichambua Rasimu ya Katiba Mpya kama walivyotumwa na wananchi  ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na kuacha  kufanya kampeni za  kufatuta madaraka  kuliko kusimamia maslahi ya wananchi. 

Kauli hiyo imetolewa leo na  Mwenyekiti wa umoja huo , Dk. Maselle  Maziku  katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma .
Amesema  umoja huo utafanya kazi ya ya kuhakikisha unatetea haki za wakulima ,wafugaji na wavuvi katika mchakato wa kujadili Rasimu ya Katiba Mpya. 

 “ Tunawataka  wanasiasa watambue kwamba katikaBunge hili,  hatukuja kufanya mabishano yasiyokuwa na mwisho na badala yake tunataka tuanze kuifanya ile kazi ambayo wananchi wametutuma ya kupitia  na kuichambua Rasimu ya Katiba,” alisema Dk. Maselle .


 Aliongeza kuwa umoja huo , umegundua kwamba makundi ya wanasiasa yanavuruga mchakato wa Bunge hilo  kwa kuendekeza misimamo yao ya kiitikadi na kusahau azma iliyowaleta  ya kuhakikisha Watanzania wanapata  Katiba Mpya isiyokuwa na upendeleo wa chama chochote  cha siasa.Hivyo umeshoshwa na hali ya Bunge hilo kuonekana kuwa ni sehemu ya makundi ya wanasiasa.

SINDA ISLAND TOUR

RAIS KIKWETE AONGEA NA WANANCHI WILAYANI MUHEZA, AHITIMISHA ZIARA YA KIKAZI MKOA WA TANGA

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia Mkutano wa hadhara mjini Muheza jana jioni. Rais Kikwete anatarajia kuhitimisha ziara yake ya kikazi mkoani Tanga leo. Picha na Freddy Maro.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mtoto Hassan Mustafa(13) mwenye tatizo la kudumaa muda mfupi baada ya Rais Kikwete kukagua na kuzindua maabara katika shule ya sekondari ya Potwe, wilayani Muheza 

KAMATI YA UCHUMI NA FEDHA YA HALMASHAURI YA MJI KOROGWE, TANGA YAPITISHA MPANGO WA TIBA KWA KADI (TIKA)

$
0
0
Mwenyekiti wa Hamashauri ya Mji Korogwe ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilole, Mheshimiwa Angello Bendera akiendesha kikao cha Kamati ya Uchumi na Fedha cha Halmashauri ya Mji kujadili mchakato wa kubadilisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda katika Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA). Kikao hicho cha tatu kimefanyika leo Machi 27, 2014 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. 

Pembeni ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji ambaye ni Diwani wa Kata ya Mtonga, Mheshimiwa Francis Komba (kushoto), anayefuatia ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji Korogwe, Dokta Jerry Mwakanyamale (kulia) na Meneja wa Bima ya Afya – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu (kushoto).
Meneja wa Bima ya Afya – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu (kushoto) akieleza umuhimu wa matumizi ya Tiba kwa Kadi (TIKA) kikao cha Kamati ya Uchumi na Fedha cha Halmashauri ya Mji kujadili mchakato wa kubadilisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda katika Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA). Kikao hicho cha tatu kimefanyika leo Machi 27, 2014 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Pembeni ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji Korogwe, Dokata Jerry Mwakanyamale (kulia), Mwenyekiti wa Hamashauri ya Mji Korogwe ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilole, Mheshimiwa Angello Bendera na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji ambaye ni Diwani wa Kata ya Mtonga, Mheshimiwa Francis Komba.
Wajumbe wa Kamati ya Uchumi na Fedha ya Halmashauri ya Mji Korogwe, Tanga wajadiliana jambo wakati wa kikao.
Diwani wa Kata ya Kwamdolwa, Mheshimiwa Hillary Ngonyani akijadili jambo.
Mchumi wa Halmashauri ya Mji Korogwe, Bw. Kikonge Jeremiah akitoa tathimini zake juu ya matumizi ya Tiba Kwa Kadi (TIKA) kwa wananchi wa halmashauri yao.
Diwani wa Kata ya Ngombezi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya, Maji na Uchumi, Mheshimiwa Omari Chafesi akitoa mwongozo na mtazamo wake katika mchakato wa kubadilisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda katika Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA).
Mwanasheria wa Halmashauri ya Mji Korogwe, Rabeca Balisidya (wa kwanza kulia) kitoa ufafanuzi wa vifungo vya sheria katika mchakato wa kubadilisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda katika Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA). Pembeni yake ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji Korogwe, Dokta Jerry Mwakanyamale na Mwenyekiti wa Hamashauri ya Mji Korogwe ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilole, Mheshimiwa Angello Bendera.
Afisa Muuguzi Kitengo Cha Afya ya Akili, Ayubu Mwakalila nae hakuwa nyuma kutoa mtazamo wake juu ya mada iliyokuwa ikijadiliwa. Picha zoe na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live


Latest Images