Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI NA ZINAZOISHI MAZINGIRA HATARISHI UNAORATIBIWA NA TASAF WAHAMASISHA AKINA MAMA WAJAWAZITO KUHUDHURIA KLINIKI

$
0
0
 Baadhi ya akinamama na watoto ambao kaya zao ziko kwenye Mpango wa kunusuru kaya masikini unaoratibiwa na TASAF wakisubiri huduma ya kliniki katika hospitali ya Manyamanyama wilayani Bunda mkoani Mara.
 Baadhi ya wanawake wajawazito ambao kaya zao ziko katika mpango wa knusuru kaya masikini unaoratibiwa na TASAF wakiwa katika msitari wa kusubiri kuonana na Daktari katika hospitali ya Manyamanyama wilayani Bunda mkoani Mara.
 Mratibu wa TASAF wilayani Bunda Nyasegwa Piloty akizungumza na akinamama walioko kwenye Mpango wa kunusuru kaya masikini kwenye zahanati ya Mcharo katika wilaya ya Bunda mkoani Mara.

Muuguzi wa hospitali ya Manyamanyama wilayani Bunda akitoa mafunzo kwa akinamama walioko kwenye Mpango wa kunusuru kaya masikini unaoratibiwa na TASAF waliohudhuria kliniki 
Baadhi ya wanawake wajawazito ambao kaya zao ziko katika Mpango wa kunusuru kaya masikini unaoratbiwa na TASAF wakiwa katika hospitali ya Manyamanyama wilayani Bunda kuhudhuria kliniki ambalo ni moja ya masharti ya Mpango huo

=====  =====  ======
Mpango wa kunusuru Kaya Masikini na zinazoishi kwenye mazingira hatarishi unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF umewahamasisha akinamama wajawazito na wale wenye watoto wa chini ya miaka MITANO kuhudhuria kiliniki ili kulinda afya ya mama na mtoto.

Mratibu wa TASAF katika wilaya ya BUNDA  bwana Nyasegwa Piloty amwaambia Waandishi wa habari waliotembelea zahanati ya Mcharo na Hospitali ya Manyamanyama kuwa mahudhurio ya akinamama wajawazito na watoto katika huduma za kliniki yameongezeka tangu kuanza kwa mpango wa kunusuru kaya masikini wilayani humo.

Naye Muuguzi katika hospitali ya Manyamanyama Beatrice Ludala amesema kuwa mwitikio wa akinamama wajawazito na watoto walioko kwenye kaya zilizoko kwenye mpango wa kunuru kaya masikini chini ya TASAF ni wa kuridhisha ikilinganishwa na hali ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Mahudhurio ya mama mojamzito na watoto wenye umri wa chini ya miaka Mitano ni moja ya masharti muhimu ya kaya zilizoingizwa kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini ili ziweze kuhudumiwa na mpango huo ulioanzishwa na serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini TASAF ambao unatakelezwa kwa awamu nchini kote.

Picha zifuatazo zinaonyesha akinamama na watoto wao wakiwa katika zahanati ya Mcharo na hosipitali ya Manyamanyama katika wilaya ya Bunda mkoani Mara.
End.

UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE JIMBO LA CHALINZE,RIDHIWANI AITEKA KIWANGWA

$
0
0
 Ridhiwani afanya mikutano mitano ya hadhara na miwili zaidi maalum kwa Wazee na Vijana wa Kiwangwa,maeneo ambayo mgombea wa ubunge kupitia CCM alifanya mikutano ya hadhara ni Kijiji cha Msuguru,Mwetemo,Msinune,Bago na Kiwangwa.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambaye pia ndio mratibu wa shughuli za kampeni za ubunge wa jimbo la Chalinze akihutubia umati wa watu waliofurika kwenye uwanja wa kata ya Kiwangwa.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimnadi mgombea wa Ubunge kupitia CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete kwa wananchi wa Kijiji cha Kiwangwa katika jimbo la Chalinze.
Mratibu wa Kampeni za CCM Jimbo la Chalinze Nape Nnauye wakicheza muziki kidogo pamoja na Mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia CCM wakati wa kumtambulisha na kumnadi mgombea huyo kwa wapiga kura wa Kiwangwa.
 Mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia CCM Ridhiwani Kikwete akihutubia mamia ya watu waliofurika kwenye mkutano wa kampeni za CCM na kusisitiza tashirikiana nao bega kwa bega katika kuleta maendeleo.
 Umati wa wakazi wa Kiwangwa wakimsikiliza mgombea wa ubunge jimbo la Chalinze kupitia CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa amedhamiria kuinua wananchi wa jimbo hilo kielimu,afya,maji na namna ya kutatua tatizo la wakulima na wafugaji kuwasaidia vijana na kusisitiza kuna umuhimu wa kudumisha michezo kwa jimbo la Chalinze.
 Meneja wa Kampeni za Ubunge jimbo la Chalinze kupitia CCM Ndugu Steven Kazidi akihutubia wakazi wa mji wa Kiwangwa wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni za kumnadi mgombea ubunge kupitia CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete.
 Katibu wa CCM mkoa wa Mtwara Ndugu Shaibu Akwilombe akihutubia wakazi wa Kiwangwa wakati wa mkutano wa kampeni za ubunge kupitia CCM.
 Mtela Mwampamba akihutupia wakazi wa Kiwangwa na kuwaambia mahusiano mazuri kati ya nchi ya Tanzania na CCM ni makubwa mno.
 Msanii Maarufu 'Dokii' akicheza na madansa wake wakati wa mkutano wa kampeni za ubunge  za CCM jimbo la Chalinze .
 Vijana wa Boda Boda wakiongoza msafara wa mgombea wa ubunge CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete kuelekea kwenye mkutano wa hadhara.
 Mgombea wa Ubunge CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete akizungumza na Bibi Tanazina Mrisho Mfaume wa kijiji cha Msinune ambapo pamoja na mengi waliyoongea pia Bibi alielezea furaha yake na kuzungumzia CCM inavyoleta maendeleo kwa wananchi wake.

MKUU WA WILAYA YA NKASI KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA RUKWA INJINIA STELLA MANYANYA AFUNGUA RASMI KAMPENI YA TOHARA KWA WANAUME MKOANI RUKWA LEO

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akihutubia katika hafla fupi ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya Tohara kwa wanaume Mkoani Rukwa iliyofanyika kimkoa katika Tarafa ya Challa Wilayani Nkasi. Akihutubia katika hafla hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya Mkuu huyo wa Wilaya amesema hadi kufikia mwezi wa tisa mwaka huu 2014 Mkoa wa Rukwa unatakiwa uwe umeshafanya tohara za wanaume 22, 000 ikiwa ni agizo la kitaifa ambapo hadi sasa jumla ya wanaume 7,000 wameshafanyiwa tohara.  

Kwa mujibu wa mratibu wa zoezi hilo Mkoani Rukwa tangu kampeni hiyo ianze tarehe 17 Machi 2014 hadi jana tarehe 20 Machi 2014 jumla ya wanaume 583 wameshafanyiwa tohara ndani ya siku 4 katika kituo kilichopo tarafa ya Challa. Kampeni hiyo inaenda sambamba na zoezi la upimaji wa VVU ambapo kati ya wananchi 699 waliopimwa ni mmoja tu amekutwa na maambukizo ya virusi hivyo katika tarafa hiyo ya Challa.

Akizungumzia faida za tohara kwa wanaume amesema husaidia kupunguza uwezekano wa akinamama kupata kansa ya kizazi  pamoja na kusaidia  kuepusha uwezekano wa maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa wanaume kwa zaidi ya asilimia 50%.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa akiwasalimia wananchi wa tarafa ya Challa waliojitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa Kampeni hiyo.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Daktari John Gurisha akizungumza katika hafla hiyo. Akizungumzia juu ya zoezi hilo la tohara amesema tohara kwa wanaume husaidia  kuepusha uwezekano wa maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa wanaume kwa zaidi ya asilimia 50%. 
Zoezi la Tohara likiwa linaendelea katika zahanati ya Challa.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta akimkaribisha Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa awasalimu wananchi wa Challa.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha (watatu kulia), Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa Albinus Mugonya (wa tano kulia) na watumishi wa Idara ya Afya katika Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa (kulia) mara baada ya uzinduzi wa kampeni hiyo. (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com)

Rais Dkt. Jakaya Kikwete azindua rasmi Bunge Maalum la Katiba.

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea salama ya heshima kutoka Jeshi la Polisi kabla ya hotuba ya uzinduzi wa Bunge maalum la Katiba leo mjini Dodoma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride liliandaliwa na Jeshi la Polisi kabla ya hotuba ya uzinduzi wa Bunge maalum la Katiba leo mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta (kulia) na Makamu Mwenyekiti Samia Suluhu wakijadiliana jamba nje ya ukumbi wa Bunge kabla hotuba ya uzinduzi wa Bunge Maalum la Katiba leo mjini Dodoma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutuba Bunge Maalum la Katiba wakati wa sherehe za uzinduzi wa Bunge hilo leo mjini Dodoma.
Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maalim Mh. Seif Sharif Hamad (kushoto) Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh. Omar Othman Makungu(Katikati) na Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Amaan Abeid Karume Wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa Hotuba ya Uzinduzi wa Bunge Maalum la Katiba Mjini Dodoma Leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya Pamoja na Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Leo Mjini Dodoma. 
(Picha na Idara ya Habari-MAELEZO)

DAKIKA 155:46 ZA HOTUBA YA RAIS JAKAYA KIKWETE KWA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA, AMEMALIZA KAZI KWENU WAJUMBE

$
0
0
 Rais Jakaya Kikwete, akiwahutubia Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba leo katika ukumbi wa Bunge mjini Dodom, ambapo katika hotuba yake ametumia dakika 155:46, kwa kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yahusuyo muundo wa Katiba mpya ikiwa ni pamoja na kufafanua kuhusu shinikizo la muundo wa Serikali tatu na mambo kadhaa ya Muungano.
 Wajumbe wakinyanyuka kwa pamoja na kupiga makofi kumshangilia Rais Jakaya, baada ya kukonga kwa Speech yake.
 Sehemu ya Wajumbe waliohudhuria .....
 Sehemu ya Mabalozi waliohudhuria ufunguzi huo wa Bunge la Katiba katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo jioni.
 Mama Maria Nyerere (katikati) Mama Siti Mwinyi (kushoto) na Mama Salma Kikwete, wakiwa ukumbi  humo wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete.
 Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal (kushoto) Mama Tunu Pinda na Mama Asha Seif Balozi, pia wakifuatilia hotuba hiyo kwa makini.
 Rais Jakaya Kikwete, akikagua gwaride maalum kabla ya ufunguzi rasmi wa Bunge hilo.
Badhi ya waandishi wa habari wapiga picha wakiwa bize.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta na Makamu wake, Samiah Suluhu, wakijadiliana jambo wakati wakisubiri kuwapokea viongozi.
Waandishi na watu mbalimbali wakiwa nje ya ukumbi huo wakati wa maopokezi ya viongozi mbalimbali.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu, akiwasili kwenye viwanja vya bunge.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye viwanja vya Bunge.
Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta, akiwasili kwenye viwanja vya Bunge.
Baadhi ya waandishi.....
James Mbatia akiwasili na mjumbe mwenzake....Picha zote na Ofisi ya Makamu wa Rais.

JK ALIPOHUTUBIA BUNGE MAALUM LA KATIBA MJINI DODOMA LEO

$
0
0
 Rais Kikwete akihutubia wajumbe wa Bunge Maalum
 Rais Kikwete akisisitiza jambo katika hotuba yake
Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda akifurahia jambo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Pandu Ameir Kificho, na Mhe Mohamed Seif Khatib na wajumbe wengine. PICHA NA IKULU

=======  =======  =======
SOMA HAPA CHINI HOTUBA YAKE
  
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma leo
 Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman na Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassa Mwinyi na wajumbe wakifuatilia hotuba ya Rais Kikwete leo
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Makungu na Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe Amani Abeid Karume na wajumbe wakisikiliza hotuba ya Rais Kikwete leo 
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mhe Tundu Lissu akigonga meza kuashiria kukunwa na hotuba ya Rais Kikwete
 Mjumbe wa Bunge Maalum Mhe Freeman Mbowe akishangilia hotunba ya Rais Kikwete.

Mkuu wa wilaya ya Makete afunga warsha ya maafisa kilimo wilaya ya Makete

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro (katikati) akisisitiza jambo wakati akifunga mafunzo ya siku 3 kwa maafisa ugani wilaya hapo yaliyotolewa na TAHA hii leo, kushoto ni mwakilishi wa shirika la TAHA Bw. Manfred Bitala na kulia ni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Makete Bw. Iddi Nganya.
 Miongoni mwa bwana shamba akizungumzia atakayoyafanya pindi akirudi kwenye eneo lake la kazi mara baada ya mafunzo hayo kumalizika.
 Afisa Mifugo wilaya ya Makete Dr. Nuru Issae akizungumza watakavyopambana na magonjwa ya matunda ya apples.
 Bibi Shamba akichangia hoja.
Habari/picha na Edwin Moshi, Makete

Mabwana na mabibi shamba wa kata na vijiji wilayani Makete mkoani Njombe walioshiriki warsha ya siku 3 ya namna ya kuboresha kilimo cha matofaa maarufu kama apples iliyotolewa na shirika la TAHA, wametakiwa kutekeleza kwa vitendo mikakati waliyojiwekea ya namna ya kuboresha zao hilo

Akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku 3 kwa wagani kazi hao, Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro, amerudia kauli yake kuwa suala hilo ni mkakati wa kitaifa ambao umeagizwa na rais Dk. Jakaya Kikwete, hivyo mafunzo hayo waliyopatiwa yanatakiwa kutendeka kwa kuwa yana manufaa kwa wakulima na wananchi wa Makete kwa ujumla

Mh. Matiro amesema ndani ya muda mfupi anatarajia sifa ya Makete kuwa inaongoza kwa maambukizi ya virusi vya Ukimwi sasa itabadilika mara moja na kuonekana kuwa inaongoza kwa kuzalisha matunda ya apples

"Nadhani mtu ukienda pale Dar es Salaam ama sehemu nyingine ukasema unatoka Makete tayari wanaelewa kuwa kuna Ukimwi, sasa hilo tunaweza kulibadilisha, kwa kwenda kuwasaidia wakulima huko mnakotoka, wazalishe apples kwa wingi kwa kufuata utaalam mliopatiwa na TAHA ili tuone mabadililo" Alisema Mh. Matiro

Amesema mikakati waliyojiwekea baada ya mafunzo hayo ni njia nzuri ya kuifikisha wilaya kule inakotaka kuhusu kilimo cha apples, ambacho kinatarajiwa kuwa kilimo cha biashara kwa lengo la kuinua uchumi wa wakulima na wilaya kwa ujumla

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Makete Bw. Iddi Nganya amesema wagani kazi hao ndio watekelezaji wakubwa wa mikakati hiyo na ndiyo maana wakapatiwa mafunzo hayo, hivyo kila mmoja ana jukumu la kwenda kuitumia ipasavyo kwa wakulima wake

Amesema tathmini itaonekana hivi karibuni, kwani kipimo cha hayo yote ni kuona wamebadilishaje kilimo cha wakulima wao huko wanakotoka, kama ikionekana kuna utofauti itaonekana kuwa mafunzo hayo yameweza kuwasaidia, hivyo waone jitihada zinazofanywa kuhakikisha mkakati huo unafanikiwa

Naye Mwakilishi kutoka shirika la TAHA ambaye alikuwa miongoni mwa mwezeshaji wa mafunzo hayo Bw. Manfred Bitala amesema ili kufanikisha malengo hayo kila mmoja kwa nafasi yake anatakiwa kukubali kubadilika na kuwajibika ipasavyo kwa nafasi yake

Amesema wao kama TAHA wanawajibu wao ikiwemo kutoa elimu ambayo tayari wameshaitoa, na maafisa kilimo hao nao wana nafasi yao na hali kadhalika na wakulima, hivyo jitihada za vitendo zikifanywa anaimani lengo la kilimo cha apples kuzaliwa kwa wingi na kwa ubora wa hali ya juu litafanikiwa

Dk. Nuru Issae ni Afisa mifugo wilaya ya Makete ni miongoni mwa washiriki wa mafunzo hayo ambapo amesema jambo watakaloanza kulifanyia kazi mara moja ni kutambua magonjwa yanayoshambulia apples na kuyatokomeza kwa kuwa wameelezwa aina mbalimbali za magonjwa yanayoshambulia matunda hayo

Dk. Issae amesema kabla ya mafunzo haya hawakuwa na wazo kuwa magonjwa yanaweza kuzorotesha jitihada za mkakati wa kuboresha kilimo cha apple wilayani hapo, na kwa kuwa wametambua kuwa magonjwa ni kikwazo kimojawapo, watapambana nayo mara moja

Miongoni mwa mikakati iliyopangwa baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo ni pamoja na ufuatiliaji wa magonjwa na kampeni ya pamoja ya kuyatokomeza magonjwa yanayoshambulia apples, kushirikiana na taasisi mbalimbali na wadau binafsi wanaolima matunda hayo, kukaa na wakulima na kupanga nao namna nzuri ya kulima apples kwa manufaa kama walivyoelekezwa na mengine mengi

WANAFUNZI WANAWAKE CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA DAR WAWEKA HISTORIA, WAANZISHA MFUKO WA KUWAKOMBOA KIELIMU.

$
0
0
Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Mary Mwangisa (kulia) akizungumza  na wanafunzi wa Kike wa chuo cha CBE kampasi ya Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa mchakato wa kuanzisha mfuko wa Jumuiya ya Wanafunzi wa kike chuoni hapo wenye lengo la kuwakomboa kielimu.
 Baadhi ya wanafunzi wa kike wa chuo hicho wakifurahia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea wakati wa hafla ya uzinduzi wa  mchakato wa kuanzisha mfuko wa Jumuiya ya Wanafunzi wa kike chuoni hapo wenye lengo la kuwakomboa kielimu, kisiasa na kiutamaduni leo jijini Dar es salaam.
Wanafunzi wa Kike wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Mary Mwangisa (katikati). Picha na Aron Msigwa - MAELEZO

========  ========  =========
WANAFUNZI WANAWAKE CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA DAR WAWEKA HISTORIA, WAANZISHA MFUKO WA KUWAKOMBOA KIELIMU.

Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
22/3/2014. Dar es salaam.

Wanafunzi wanawake wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) wamezindua mchakato wa kuanzisha mfuko wa Jumuiya ya wanafunzi wa kike wenye lengo la  kumkomboa na kumwezesha mwanafunzi wa kike kujitambua, kielimu, kisiasa na kiutamaduni.

Akizungumza na jumuiya ya wanafunzi wa kike wa chuo hicho wakati wa uzinduzi  wa mfuko huo  leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Mery Mwangisa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo amesema kuwa kuanzishwa kwa jumuiya hiyo  ni ishara ya umoja na mshikamano wa wanafunzi wa kike chuoni hapo.

Amesema kuanzishwa kwa mfuko huo kunatokana na kuongezeka kwa changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake pia  kukosekana kwa mifuko ya aina hiyo katika taasisi nyingi za elimu ya juu hapa nchini.

Ameeleza kuwa  malengo ya mfuko huo ni kumwezesha mwanafunzi wa kike wa CBE kujitambua kielimu, kisiasa na kiutamaduni na kuongeza kuwa yamekuja  wakati muafaka kufuatia  mabadiliko yaliyopo sasa ya kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiutamaduni.

 Amefafanua kuwa mfuko huo ulioanzishwa katika chuo hicho ni fursa pekee ya kuwawezesha wanafunzi wa kike kunufaika kwa kupata elimu bora bila vikwazo.

“Napenda kutumia fursa hii kuushukuru uongozi wa chuo hiki kwa kuonyesha njia ya kuwajali wanawake na pia katika kuweka taratibu nzuri za kulinda maadili, katika maisha yangu sijawahi kusikia chuo kikuu chochote kimezindua jukwaa la wanawake lenye malengo mazuri kama yenu” Amesema Dkt. Mwangisa.


Ameeleza kuwa kwa muda mrefu wanawake kote nchini wamekuwa na juhudi  mbalimbali za kujikomboa kiuchumi pamoja na kulitumikia taifa kwa kushika nyadhifa mbalimbali serikalini kwa ufanisi mkubwa na kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii pindi wanapokabidhiwa madaraka.

“Ninapowaangalia ninyi nafarijika maana naona viongozi wakuu wa serikali, naona marais na pia wakurugenzi wa biashara”

Akizungumza kuhusu kuanzishwa kwa mfuko huo na mafanikio yake Dkt. Mwangisa amesema kuwa atatoa ushirikiano kwa wanafunzi hao ili kuhakikisha kuwa mfuko huo unajengewa uwezo wa  kusimama na kuwanufaisha wanawake wanaokumbwa na changamoto zinazokwamisha maendeleo yao ikiwemo ukosefu wa fedha.

Amesema kuwa kukamilika kwa taratibu za jumuiya hiyo ikiwemo maandalizi ya katiba ya jukwaa hilo kutaliwezesha jukwaa hilo kupanga, kuandaa na kutekeleza mikakati mbalimbali ya kujiendesha ili kuwawezesha wanafunzi hao kutatua changamoto zinazowakabili kwa kulinda heshima yao katika jamii.

Kwa upande wake mjumbe wa Bodi ya Taaluma ya Chuo hicho Dkt. Ellen Oturu Okoedion amesema kuwa wanafunzi wa kike wa chuo hicho wanahitaji msaada kupitia mfuko huo utakaowawezesha kupambana na wimbi la wanafunzi wa kike kushindwa kumaliza masomo yao kwa kushindwa kumudu gharama za masomo.

Amewataka wanafunzi wa kike wa chuo hicho kutumia ipasavyo taaluma wanayoipata  kusaidia mfuko huo kupata fedha  ili uwe endelevu kwa maendeleo ya wanawake na chuo hicho.

“Ninyi mnasoma elimu ya biashara na ndio watalaam wenyewe sitarajii mfuko wenu ukose uwezo, naamini mtatumia taaluma yenu mnayoipata hapa chuoni kutafuta fedha kwa kuwa mnao uwezo huo” Amesisitiza Dkt. Ellen.

Naye Waziri wa Wanawake wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Bi. Mwajuma Sangali ameeleza kuwa wanawake kote nchini wana jukumu la kuandaa kizazi cha watu wenye upendo, uzalendo, kupenda kazi na maendeleo.

Amesema kuanzishwa kwa chombo hicho kunalenga kuboresha maisha ya wanawake hasa katika masuala ya elimu,jamii,uchumi na siasa.

Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Mary Mwangisa (kulia) akizungumza jambo kabla ya kuanza kwa maandamano ya wanafunzi wa Kike wa chuo cha CBE kampasi ya Dar es salaam kuzindua  mchakato wa kuanzisha mfuko wa Jumuiya ya Wanafunzi wa kike chuoni hapo wenye lengo la kuwakomboa kielimu.Kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya Taaluma ya Chuo hicho Dkt. Ellen Oturu Okoedion.
 Waziri wa Wanawake wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) Bi. Mwajuma Sangali akiwaongoza wananfunzi wa Kike wa chuo hicho wakati wa uzinduzi  wa mchakato wa kuanzisha mfuko wa Jumuiya ya Wanafunzi wa kike wenye lengo la kuwakomboa kielimu.

Baadhi ya wanafunzi wa Kike wa Chuo cha CBE wakiwa wamebeba bango lenye ujumbe mahususi kutetea haki za wanawake na usawa wa kijinsia wakati wa uzinduzi wa mfuko maalum wa Jumuiya ya Wanafunzi wa kike wa chuo hicho.

Wanafunzi wa Kike wa chuo cha CBE wakiwa kwenye maandamano kuelekea eneo la tukio.
Moja ya kundi la Burudani la Waswahili Classic Group la chuo hicho likitoa buruduni wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfuko huo.
Kikundi cha maagizo cha chuo hicho kikionyesha namna vitendo vya ukiukwaji wa maadili unavyodhibitiwa chuoni hapo na namna uongozi wa chuo hicho unavyowachukulia hatua za kinidhamu wanaokiuka maadili ya chuo hicho.


Igizo la wanafunzi wakiwa kwenye majadiliano chuoni hapo bila kujali tofauti za jinsia .

DAKIKA 90: Kupotea kwa Air Malaysia na takwimu za usalama wa anga duniani

$
0
0
Ndege aina ya Boeing 777 ya Malaysia Airlines ikiruka kutoka Roissy-Charles de Gaulle Airport nchini Ufaransa mwaka 2011. Photo Credits: PressTv
Wakati harakati za kutafuta ndege ya Shirika la ndege la Malaysia iliyopotea zikizidi kushika kasi na kuvunja rekodi ya kushirikisha mataifa mengi duniani, baadhi ya takwimu kuhusu hali ya usalama wa safari za anga duniani zimezidi kuibuka na kufungua macho ya wengi waliokuwa wakiamini kuwa tukio hili ni la kwanza na / ama miongoni mwa machache kupata kutokea duniani.

Mtandao wa Usalama wa safari za Anga ama Aviation Safety Network ilitoa orodha ya ndege zilizopotea tangu kumalizika kwa vita kuu ya pili ya dunia. Kwa mujibu wa takwimu hizo, ndege 88 zimepotea tangu mwaka 1948, hivyo kufanya wastani wa ndege zinazopotea na kutopatikana wala miili ya abiria kuwa 1.33 kwa mwaka.

Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM). Hii ilikuwa ripoti ya Machi 22, 2014
JamiiProduction . jamiiproduction@gmail.com 11:40 AM (10 hours ago) to bcc: me
Ndege aina ya Boeing 777 ya Malaysia Airlines ikiruka kutoka Roissy-Charles de Gaulle Airport nchini Ufaransa mwaka 2011. Photo Credits: PressTv
Wakati harakati za kutafuta ndege ya Shirika la ndege la Malaysia iliyopotea zikizidi kushika kasi na kuvunja rekodi ya kushirikisha mataifa mengi duniani, baadhi ya takwimu kuhusu hali ya usalama wa safari za anga duniani zimezidi kuibuka na kufungua macho ya wengi waliokuwa wakiamini kuwa tukio hili ni la kwanza na / ama miongoni mwa machache kupata kutokea duniani.
Mtandao wa Usalama wa safari za Anga ama Aviation Safety Network ilitoa orodha ya ndege zilizopotea tangu kumalizika kwa vita kuu ya pili ya dunia.

Tasnia ya Filamu ikiendelezwa vizuri ni chanzo kikubwa cha ajira kwa vijana nchini.

$
0
0
Na Georgina Misama-MAELEZO.


Serikali imesema inatambua Tasnia ya Filamu ikiendelezwa vizuri ni chanzo kikubwa cha ajira kwa vijana na ni njia madhubuti ya kukuza uchumi kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.


Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa kitenngo cha mawasilianao serikalini Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Concilia Niyibitanga wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyikia ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO. Concilia alisema kuwa mwamko unaongezeka kwa wasanii na watengenezaji wa filamu kutoka ndani na nje ya nchi.

Hii inajidhihirisha kwa idadi ya vibali vya utengenezaji filamu imeongezeka kutoka 100 mwaka 2000 hadi 472 Januari 2014.    Aidha, kampuni zinazojishughulisha na uendeshaji wa shughuli za filamu nchini zimeongezeka kutoka Kampuni moja ya Filamu Tanzania (TFC) na kufikia 129 mwaka 2013.

Kwa upande wa watengenezaji wa filamu za ndani, uwasilishaji wa ukaguzi umeongezeka kutoka filamu 96 mwaka 2000 hadi kufikia 1059 Februari 2014. Naye Katibu Mtendaji wa Bodi ya filamu nchini Joyce Fisoo alitoa rai kwa wasanii wa filamu kutumia lugha ya Kiswahili hasa katika uandaaji wa jina ili kulinda na kuikuza lugha yetu ya Kiswahi.


Tasnia ya Filamu nchini ilianza tangu mwaka 1920 wakati wa ukoloni, baada ya Uhuru, Serikali ya Tanzania kupitia bunge iliamua kutunga sheria namba 4 ya mwaka 1976 ya Filamu na Michezo ya kuigiza ili kuweka usimamizi mzuri wa tasnia hiyo.

INTRODYUZING NEW VIDEO : Kitenge By Team Racerz

Tuboreshe Rasimu iliyopo-ZITTO KABWE.

$
0
0
Na Zitto Kabwe, MB
 
Wiki ya Machi 18 - 22, 2014 ilianza kwa siku ya Jumanne Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba aliwaslisha rasmi Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Bunge Maalumu la Katiba. Wiki hiyo imeishia kwa siku ya Ijumaa Rais wa Jamhuri ya Muungano ndugu Jakaya Mrisho Kikwete kutoa hotuba kwa Bunge Maalumu. 

Hotuba zote zimepokelewa kwa hisia tofauti kulingana na msimamo wa kila mtu kuhusu hoja inayoonekana ni kubwa kuliko zote katika mchakato wa kuandika Katiba Mpya - Muundo wa Muungano. Wale wanashabikia muundo wa Serikali Tatu, walifurahishwa mno na hotuba ya Jaji Warioba. Wale wanaoshabikia muundo wa Serikali mbili walifurahishwa mno na hotuba ya Rais Kikwete. Sikufurahishwa na hotuba zote mbili.
 
Nitaeleza.
 
Moja, hotuba zote mbili zilichukua muda mrefu zaidi kuelezea sura moja tu ya Rasimu ya Katiba nayo ni sura ya Sita inayohusu muundo wa Jamhuri ya Muungano kana kwamba Katiba hii inahusu suala hilo tu. Ni dhahiri suala hili ni kubwa na muhimu kwani linahusu uhai wa Dola yenyewe na siwezi kubeza. Hata hivyo masuala kama Haki za Raia ni muhimu zaidi kwani hata uwe na muundo wa namna gani wa muungano au hata muungano wenyewe kuvunjika, bila ya kuwa na haki za msingi za raia kwenye katiba katiba hizo zitakataliwa tu na wananchi. 

Huu mtindo unaozuka wa kudhani muundo wa muungano ndio mwarobaini wa matatizo ya ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka, ubadhirifu, umasikini, elimu ya hovyo, afya dhaifu, utatufikisha pabaya na hata kurudi tena kuandika katiba kudai haki hizo. Jaji Warioba na Rais Kikwete wameshindwa kuruka kiunzi cha kwamba Katiba ni zaidi ya Muungano.
 
Pili, wote wawili Rais Kikwete na Jaji Warioba wamejenga hoja zao kuhusu miundo ya Muungano wanayopendekeza au kuunga mkono kutokana na misingi ama ya 'malalamiko' au 'hofu'. Jaji Warioba aliorodhesha malalamiko 11 ya upande wa Zanzibar dhidi ya Muungano na malalamiko 10 ya upande wa bara. Kimsingi malalamiko yote ya upande wa bara yanazaliwa na vitendo vya upande wa Zanzibar isipokuwa lalamiko namba vii linalohusu kupotea kwa utambulisho wa Tanganyika katika muundo wa Muungano.
 
Jaji Warioba anajenga msingi wa pendekezo la Tume yake kutokana na kujibu malalamiko au maarufu kero za Muungano na anasema
"....muundo wa Serikali mbili hauwezi kubaki kwa hali ya sasa. Muungano wa Serikali mbili waliotuchia waasisi siyo uliopo sasa...... waasisi walituachia Muungano wa Nchi Moja yenye Serikali mbili, na siyo Nchi Mbili zenye Serikali Mbili". Nukuu hii niliipenda kuliko zote katika Hotuba ya Mzee wangu Warioba.
 
Rais Kikwete alijenga msingi wa maoni yake kwenye hofu za kuwa na Serikali tatu. Hofu hizo ni pamoja na gharama za kuendesha Muungano, kuzuka kwa hisia za Utaifa wa Utanganyika na Uzanzibari, uwezekano wa Muungano kuvunjika kwa kushindwa kuhudumia majeshi na hata Jeshi kuchukua Nchi ikipidi na kutupilia mbali katiba na Serikali ya Muungano kutokuwa na Rasilimali zake. Rais alisema 'Serikali ya Muungano ni egemezi na tegemezi' nukuu ambayo niliipenda kuliko zote katika Hotuba ya Mzee wangu Jakaya Kikwete.
 
Rais Kikwete hakuniridhisha kabisa namna ya kumaliza kero za Muungano kwa muundo uliopo sasa kwani muundo huo umeshindwa kuzimaliza kwa takribani miaka 50 tangu Muungano uundwe. Haiwezekani muundo uliozalisha kero lukuki ndio utarajiwe kuzimaliza kero hizo. Kwa vyovyote vile ni lazima kuwa na muundo mpya lakini kiukweli ni lazima muundo huo mpya ujibu hofu alizoeleza ndugu Rais maana ni hofu za kweli.

Jaji Warioba hakuniridhisha na namna suala la Uraia litakavyotatuliwa kwani kutoa jibu la kubakia na 'kukubali' Nchi mbili halafu uraia mmoja kunaleta mashaka makubwa. Kama tunataka kuwa na Uraia mmoja ni lazima tuwe Nchi moja, hatuwezi kuwa na Nchi mbili uraia mmoja.
 
Vilevile vyanzo vya mapato ya Muungano ni vidogo mno kuendesha dola. Hivyo basi rasimu iliyopo mbele ya Bunge Maalumu ina mapungufu makubwa japo imetoa mapendekezo yatakayomaliza malalamiko ya Muungano.
 
Sasa kazi ya Bunge ni moja tu nayo ni kuboresha rasimu iliyopo mbeleyake ili kumaliza kero za muungano zilizopo na kujibu hoja za hofu za muundo mpya. Hakuna sababu ya kubishana kwenye takwimu za Tume, tume imefanya wajibu wake na sasa Bunge Maalumu nalo litimize wajibu wake.
 
Iwapo kama kweli tunataka kusikia Watanzania wanataka nini kwenye muundo wa Muungano, tusimamishe Bunge na twende tukawaulize kwa kura (referendum). Vingivenyo tuboreshe rasimu iliyopo na iliyotokana na maoni ya wananchi wote kwa kujibu hizo hofu muhimu alizoainisha ndugu Rais na hayo malalamiko muhimu yaliyoainishwa na Tume. 

Sio kazi ya Bunge Maalumu kutafuta ubora wa hotuba zilizotolewa mbele yetu bali kuona mazuri ndani ya hotuba hizo yasaidie kazi yetu Tuzingatie kuwa tusijenge Nchi kwa kujibu malalamiko na hofu tu maana hofu na malalamiko hayaishi katika dunia inayobadilika kwa kasi sana.
 
Tuamue tunataka kuwa Jamhuri ya Muungano ya namna gani. Nini sababu ya Jamhuri yetu na aina gani ya Tanzania tunataka kujenga. Tuanze kwa kutafsiri sababu ya Tanzania kuwepo na Tanzania gani tunataka kujenga kisha tutunge Katiba itakayowezesha kutufikisha huko tutakapo kufika.

BAADHI YA WIZARA, IDARA NA TAASISI ZA SERIKALI ZAPEWA VIFAA VYA TEKNOLOJIA, HABARI NA MAWASILIANO (TEHAMA)

$
0
0
PICHA ZA KUKABIDHI VIFAA 2Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum akimkabidhi laptop Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa baadhi ya Wizara, Idara na Taasisi za Serikali iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Fedha.PICHA ZA KUKABIDHI VIFAA 3 - 1Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum akihutubia wageni waalikwa (hawapo pichani)  wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa baadhi ya Wizara, Idara na Taasisi za Serikali iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Fedha.

PICHA ZA KUKABIDHI VIFAA 1Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akitoa maelezo mafupi juu ya Mpango wa Kuboresha na Kuimarisha Takwimu nchini wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa baadhi ya Wizara, Idara na Taasisi za Serikali iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Fedha.
PICHA ZA KUKABIDHI VIFAA 3Mwakilishi wa Wadau wa Maendeleo nchini Bw. Richard Martin akitoa maelezo mafupi kwa Wageni waalikwa (hawapo pichani)wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa baadhi ya Wizara, Idara na Taasisi za Serikali iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Fedha.PICHA ZA KUKABIDHI VIFAA 6Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum (Mb) akikata utepe kuonesha baadhi ya vifaa vya TEHAMA vilivyokabidhiwa kwa baadhi Wizara, Idara na Taasisi za Serikali leo katika Ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Fedha.PICHA ZA KUKABIDHI VIFAA 5Baadhi ya vifaa vya TEHAMA vilivyokabidhiwa kwa baadhi Wizara, Idara na Taasisi za Serikali leo katika Ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Fedha.PICHA ZA KUKABIDHI VIFAA 4
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum (Mb) (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongonzi mbalimbali wa Serikali pamoja na mwakilishi wa Wadau wa Maendeleo nchini Bw. Richard Martini (kulia kwake) baada ya kumaliza hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa baadhi ya  Wizara, Idara na Taasisi za Serikali iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Fedha.

RIDHIWANI KIKWETE AHANI MSIBA WA WATOTO WAWILI WALIOPOTEZA MAISHA BAADA YA KUTUMBUKIA KWENYE KISIMA CHA MAJI,KIWANGWA

$
0
0
 Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kushoto) akiwa na Bw. Geofrey Nestory pamoja na Mkewe,Renata Pascal ambao ni Wazazi wa Watoto wawili,Jesca Geofrey (5) na Redempta Geofrey (2) waliopoteza maisha hivi karibuni kwa kutumbukia kwenye kisima cha maji,wakati alipofika Nyumbani kwa wazazi hao ambao ni Wakazi wa Kijiji cha Msinune,Kata ya Kiwangwa leo Machi 22,2014 kuhani msiba wa Watoto hao.Wazazi hao walimueleza Ndg. Ridhiwani Kikwete kuwa walibaini kupotea kwa watoto hao mnamo tarehe 18 Machi wakati wa jioni baada ya kuona hawajarudi nyumbani,hivyo walianza kuwatafuta na kubaini kuwa walipoteza maisha baada kutumbukia kwenye kisima hicho cha maji.Watoto hao walizikwa siku ya pili yake tarehe 19 Machi,Shambani kwao.
 Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwa amesimama kutoa pole kwa Wazazi wa Watoto hao pamoja na Waombolezaji Wengine waliokuwepo msibani hapo,kwenye Kijiji cha Msinune,Kata ya Kiwangwa leo Machi 22,2014.
Meneja wa Kampeni za CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ndg. Steven Kazidi akitoa pole kwa niaba ya CCM kwa Watoto wawili,Jesca Geofrey (5) na Redempta Geofrey (2) waliopoteza maisha hivi karibuni kwa kutumbukia kwenye kisima cha maji,wakati walipofika Nyumbani kwa Wazazi hao kuhani msiba huo leo Machi 22,2014.

TASWIRA ZA RAIS KIKWETE BAADA YA KUHUTUBIA BUNGE MAALUM LA KATIBA MJINI DODOM MACHI 21, 2014

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongozwa na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe Samuel Sitta mara baada ya kulihutibia Bunge hilo Ijumaa  mjini Dodoma Machi 21, 2104 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe Samuel Sitta mara baada ya kulihutibia Bunge hilo Ijumaa  mjini Dodoma Machi 21, 2104. 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipewa pongezi kwa hotuba nzuti na Makamu  Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samia  Suluhu Hassan mara baada ya kulihutibia Bunge hilo Ijumaa  mjini Dodoma Machi 21, 2104. 
  Rais Kikwete katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba.
PICHA NA IKULU


Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Zanzibar Dkt Mohamed Ali Shein,  Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe Samuel Sitta na Makamu  Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Suluhu Samia Hassan wakifurahia jambo mara baada ya Rais  kulihutibia Bunge hilo Ijumaa  mjini Dodoma Machi 21, 2104


UVCCM WAZINDUA MBIO MAALUM ZA PIKIPIKI KUHAMIASISHA UZALENDO MIONGONI MWA VIJANA LEO MKOANI DODOMA

$
0
0

Leo Tarehe 22/03/2014 katika Manispaa ya Dodoma, Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), tumezindua mbio maalum za pikipiki zenye lengo la kuhamasisha uzalendo miongoni mwa vijana na kuibua fursa zinazopatikana maeneo mbalimbali ya Tanzania.

Mbio hizi maalum zimezinduliwa na Rais wa Zanzibar, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mheshimiwa Dr. Ali Mohamed Shein, katika hafla fupi ya kufana iliyofanyika katika makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa Dodoma.

Mbio maalum za pikipiki zitazunguka nchi nzima na zitahitimishwa rasmi kwa matembezi ya miguu kuanzia Kibaha Mkoani Pwani hadi Dar es Salaam tarehe 25/04/2014 yatakayopokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Mrisho kikwete katika ukumbi wa Nyerere Convention. 
Kauli Mbiu Yetu

"MIAKA 50 YA MUUNGANO; VIJANA TUDUMISHE MUUNGANO WETU NA TUTUMIE FURSA ZILIZOPO KULETA MAENDELEO YETU"
TANZANIA KWANZA, MENGINE BAADAYE

Imetolewa na;
Paul C. Makonda 
Katibu wa Hamasa uhamasishaji UVCCM

VYUO mbalimbali nchini Vyashauriwa kujenga mahusiano ya kirafiki ili kubadilishana uzoefu katika kufanya kazi zao.

$
0
0
 Mtembeza wageni wa Kidishi Multi Spices Farm Bwana. Mur- tala Rashid akiwaonyesha mmoja wa mmea wa Spice na kuwafahamisha matumizi yake, mmea huo unaotambuliwa kwa jina la mchaichai katika chamba hilo.
 Wanafunzi wakifurahiya maelezo kutoka kwa Mtembeza wageni wa Kidishi Multi Spices Farm Bwana. Mur- tala Rashid (hayupo pichani). 
Baadhi ya wanafunzi wakionyeshana Spices walipokuwa wamepumzika katika shamba la Kidishi Multi Spices Farm lililopo Kidichi nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. (Picha zote na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar).

========  =======  ========
Na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar.

VYUO mbalimbali nchini, vimeshauriwa kujenga mahusiano ya kirafiki kati yao ili kubadilishana uzoefu katika kufanya kazi zao.

Ushauri huo umetolewa na mkuu wa msafara wa wanafunzi 70 kutoka Chuo cha Taifa cha Utalii Dar es Salaam, Dawson Kyungai, wakati wakiwa katika ziara kuwatembelea viongozi wenzao wa Chuo cha Elimu Zanzibar (Zanzibar Education College).

Kyungai ameupongeza uongozi wa chuo hicho kwa ujasiri wao wa kutafuta njia za kujenga mahusiano na vyuo mbalimbali nchini. Naye Mkuu wa Zanzibar Education College Ussi Said Suleiman, akizungumza na waandishi wa habari katika Kanisa la Mkunazini walikotembelea, alisema suala la urafiki wa vyuo linawasaidia walimu na wanafunzi kubadilishana mawazo na kujifunza kwa ufanisi zaidi.

Wanafunzi hao 70 wako katika ziara ya siku tatu kuwatembelea wenzao wa Zanzibar kwa lengo la kubadilishana uzoefu pamoja na kuzuru sehemu mbalimbali za kihistoria za Zanzibar.

Kwa upande wao, wanafunzi na walimu wa Zanzibar Education College, wanatarajia kufanya ziara kama hiyo Mkoani Dodoma mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu.


  Mtembeza wageni wa Kanisa la Mkunazini akiwafahamisha kitu wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Utalii kutoka Dar es salam walipokuwa wakitembelea Kanisa hilo.
 Wanafunzi wakipata maelezo kwa Mtembeza wageni juu sehemu walipokuwa wakihifadhiwa watumwa Kanisani hapo.
 Wanafunzi wakitoka nje kwa furaha mara baada ya kutembelea Kanisa la Mkunazini liliopo Mjini Unguja. 
 Hapa wanafunzi wakijichagulia katika moja ya maduka ya vinyago na nguo za Kiswahili yaliopo Ngome kongwe Mjini Unguja. 
 Wanafunzi wakionyeshana Spices. 

MKUU WA MKOA WA NJOMBE AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA TENKI LA MAJI MWONGOLO MAKETE MJINI

$
0
0
 Mkuu wa mkoa wa Njombe Kapeteni Mstaafu Aseri Msangi akiweka jiwe la msingi ujenzi wa tanki la maji lililopo Mwongolo Makete Mjini.
 Ujenzi wa tanki la maji Mwongolo Makete mjini ambao umewekwa jiwe la msingi na mkuu wa mkoa wa Njombe.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni mstaafu Aseri Msangi (katikati) akielekea kwenye ujenzi wa mradi wa maji Mwongolo Makete mjini kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi, kulia ni mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro na kushoto ni katibu tawala msaidizi upande wa maji mkoa wa Njombe Bw. Christopha Nyandiga.
 Meneja Mamlaka ya maji Makete mjini Bw. Yonas Ndomba akisoma taarifa ya ujenzi wa tanki la maji Mwongolo, Makete mjini mbele ya mkuu wa Mkoa.
 Mkuu wa mkoa wa Njombe kapt. Mstaafu Aseri Msangi akimsikiliza meneja wa maji Makete mjini akisoma taarifa, kushoto kwake ni mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro.
Meneja wa mamlaka ya maji makete mjini, Bw. Yonas Ndomba akimkabidhi taarifa ya ujenzi wa tanki la maji la Mwongolo Makete mjini Mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni mstaafu Aseri Msangi.
Tanki la Maji lililopo Mwongolo ambalo linatumika sasa kama linavyoonekana.Picha zote na Edwin Moshi, Makete.

MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI MKOA WA NJOMBE YAFANA KATIKA VIWANJA VYA MABEHEWANI

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni mstaafu Aseri Msangi akipata maelekezo kwenye banda la idara ya maji kuhusu bili za maji, katika wiki ya maji kimkoa katika viwanja vya mabehewani Makete mjini.
Mkuu wa mkoa Kapt. Msangi akisikiliza maelekezo toka kwa mtaalamu wa maji, katikati ni mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro.
Mkuu wa mkoa akipata maelekezo kuhusu mfumo mzima wa maji Makete mjini unavyofanya kazi.
 Kikundi cha sanaa cha SUMASESU kikitumbuiza kwenye maadhimisho hayo ya wiki ya maji.
 Kikundi cha sanaa kijulikanachoa kama Mchana Hasarani kikikonga nyoyo za washiriki wa maadhimisho hayo.
 Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro akizungumza kwenye maadhimisho ya wiki ya maji kimkoa katika viwanja vya mabehewani Makete mjini.
 Mkuu wa mkoa wa Njombe kapteni Mstaafu Aseri Msangi akihutubia wananchi waliofika kumsikiliza katika maadhimisho ya wiki ya maji kimkoa katika viwanja vya mabehewani makete mjini.
Mkuu wa mkoa akihutubia wananchi.Picha zote na Edwin Moshi, Makete.

PUNGUZENI GHARAMA YA KUCHIMBA VISIMA - WAZIRI MKUU

$
0
0

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameitaka Wizara ya Maji itafute njia mbadala zitazosaidia kupunguza gharama za kuchimba visima ili wananchi waweze kupata maji safi na salama.
 
“Wizara ya Maji angalieni uwezekano wa kupunguza gharama za uchimbaji wa visima ili wananchi waweze kumudu kuchimba visima na wapate uhakika wa maji safi na salama,” alisema.
 
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana (Jumamosi, Machi 23, 2014), wakati akifunga Maadhimisho ya Wiki ya Maji Kitaifa yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
 
“Hivi sasa nimeambiwa gharama ya kuchimba kisima mita moja ni sh. 150,000/. Je kama mtu anataka kuchimba kisima chenye urefu wa mita 180 au 200 itakuwaje? Ni dhahiri kuwa watu hawataweza kumudu hizo gharama. Angalieni namna ya kuzipunguza,” alisisitiza.
 
Waziri Mkuu ambaye alikuwa akifunga maadhimisho hayo kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete aliwataka wakazi wa mkoa wa Dodoma waendelee kuthamini dhana ya uchangiaji ili waweze kumudu kuendeleza miradi hiyo.
 
Aliwataka pia watunze vyanzo vya maji na kutunza miundombinu pamoja na mitambo iliyonunuliwa kuendesha visima mbalimbali kwani maji yana gharama. “Ninawasihi sana muitunze mitambo iliyowekwa kuendeshea visima hivi kwani ni vifaa vya gharama sana,” aliongeza.
 
Mapema, Waziri Mkuu alizindua kisima cha maji kwenye kijiji cha Mkonze nje kidogo ya mji wa Dodoma ambacho ujenzi wake umegharimu sh. milioni 519.6/-. Kisima hicho chenye vichoteo 15, kitawanufaisha wakazi 5,887 kati ya 6,869 sawa na asilimia 85.7 ya wakazi wa kijiji hicho.
 
“Kabla ya kujengwa kisima hiki, ndoo ya maji ya lita 20 ilikuwa ikiuzwa sh. 500/- lakini sasa ndoo moja inauzwa kwa sh. 100/- tu,” alisema Mhandisi Mohammed Kali wakati akitoa taarifa ya mradi huo kwa Waziri Mkuu.
 
Waziri Mkuu pia aliweka jiwe la msingi kwenye tenki la maji katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) lenye uwezo wa kuhifadhi mita za ujazo 4,500. Ujenzi wake unatarajiwa kukamilika Novemba, 2014.
 
Akizungumza na wanajumuiya ya UDOM walioshiriki uzinduzi huo, Waziri Mkuu alisema mradi huo mkubwa unaenda sambamba na ujenzi wa mradi mwingine mkubwa wa maji taka (recycling plant). “Ninawasihi muangalie uwezekano wa kutumia maji machafu yatakayosafishwa ili yatumike kumwagilia miti na maua muweze kutunza mandhari ya UDOM,” alisema.
 
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa tenki hilo, Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe alisema hadi kukamilika kwake, mradi huo utagharimu sh. bilioni 28. Alisema mradi huo unaojumuisha ujenzi wa miundombinu ya maji safi na maji taka katika Chuo hicho, umefanyika chini ya Mpango wa Kuendeleza Sekta ya Maji nchini (WSDP).
 
Naye Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za Tanzania, Burundi na Uganda, Bw. Phillippe Dongier alisema wao kama wadau wa maendeleo, wanaona fahari kushirikiana na Wizara ya Maji katika kuleta maendeleo ya sekta hiyo kwa Watanzania.
 
Uzinduzi wa miradi hiyo ya maji ni sehemu ya miradi 13 iliyopangwa kuzinduliwa mkoani Dodoma kwenye maadhimisho ya maji ya mwaka huu. Hata hivyo, mkoa huo una miradi 69 ya maji ambayo ujenzi wake unaendelea kwa awamu tofauti.
 

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
JUMAPILI, MACHI 23, 2014
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images