Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 252 | 253 | (Page 254) | 255 | 256 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Ujenzi Bw. Mrtin Ntemo akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu maendeleo yaliyofikwa katika ujenzi wa barabara hapa nchini tangu Serikali ya  awamu ya nne ilipoingia madarakani . Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Frank Mvungi.

  0 0

   Meneja wa Bia ya Serengeti Rodney Rugambo akiongea kwa njia na mmoja wa washindi wa droo ya sita ya promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti inayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti huku akishuhudiwa na Afisa Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bakari Maggid wakati wa  kuchezesha droo hiyo mapema leo katika ofisi za Kiwanda cha Bia cha Serengeti jijini Dar es Salaam.
   Meneja wa Bia ya Serengeti Rodney Rugambo aeleza jambo kwa wana habari(hawapo pichani)  wakati wa droo ya sita ya promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti inayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti huku akishuhudiwa na Afisa Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bakari Maggid(kushoto), Maafisa waandamizi kutoka PWC(wa pili kulia) na push mobile(wa kwanza kulia) mapema leo katika ofisi za Kiwanda cha Bia cha Serengeti jijini Dar es Salaam.
  Meneja wa Bia ya Serengeti Rodney Rugambo akitangaza washindi wa droo ya sita ya promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti inayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti mara baada ya kuchezesha droo hiyo mapema leo katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.

  0 0


  Mstahiki Meya wa kinondoni Yusuph Mwenda akizungumza wakati wa usainishwaji mkataba baina ya shule ya sekondari mabibo na ubalozi wa Japan
   Mstahiki meya akiendelea kuzungumza wakati wa usainishwaji mkataba baina ya shule ya sekondari mabibo na ubalozi wa Japan
   Baadhi ya walimu na wanafunzi wa mabibo sekondari
   Balozi wa Japani Nchini Tanzania Ndugu Masaki Okada akitia sahihi mikataba hiyo
   Mkurugenzi wa Manispaa Eng Mussa Natty wa kwanza kulia akishuhudia utiaji sahihi wa mikataba hiyo
   Mstahiki meya wa Manispaa ya Kinondoni Yussuph Mwenda akiwa na  Balozi wa Japani Nchini Tanzania Ndugu Masaki Okada
   Muonekano wa shule ya sekondari Mabibo
   Majengo ya shule ya sekondari mabibo
  Mwalimu alipokuwa anakaribisha Ugeni Kutoka kushoto Mstahiki meya, Balozi wa Japan, Mkurugenz wa manispaa na Mkuu wa Shule ya  mabibo sekondari
  mkurugenzi wa manispaa Eng mussa Natty akisalimiana na Mwalimu alipotembele moja ya madarasa kuona ufundishaji unavyoendelea.
  Wanafunzi wakifurahia ugeni uliowatembelea  katika shule yao.
   Picha ya pamoja na  Balozi wa Japan na Viongozi wa Manispaa ya kinondoni na Walimu wa mabibo sekondari.
   Balozi akiwa anaondoka eneo la shule ya sekondari Mabibo  Shule ya Sekondary Mabibo iliyopo katika Manispaa ya Kinondoni leo imesaini Mkataba wa Mradi wa ujenzi wa Maabara ya Kisasa mradi huo unaojulika kwa jina la "Grassroot Human Security" ambao utagharimu kiasi cha USD 118,873 ambazo ni takribani mil 193 za kitanzania umesainiwa leo na Balozi wa Japani Nchini Tanzania Ndugu Masaki Okada mbele ya Mstahiki meya wa Manispaa ya Kinondoni ndugu Yusuph Mwenda na Mkurugenzi wa Manispaa Eng Mussa Natty. 


  Kwa pamoja Wameshukuru sana Serikali ya Japani kwa Msaada huo na kuahidi kutoa ushirikiano mkubwa kwa Nchi hiyo na Kuhimiza watoto wapende masomo ya sayansi na kuifanya Kinondoni iwe juu kwa upande Mwingine Balozi Masaki amewataka watanzania kuwekeza Kwenye sayansi na teknolojia kuliko kutegemea kununua kwa ajili ya kukuza uchumi na kupunguza umaskini vile vile amewashukuru Bi Bernadetha Thomas na Omath Sanga Afisa elimu wa Manispaa kwa kuibua mradi huo.

  0 0

  Kweli Urais hauna ubia wala muda ama sehemu ya kuchapa kazi. Wakati wowote na mahali popote ni sehemu ya kazi, kama inavyoonekana hapa  ambako Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametulia ndani ya ndege akisafiri kutoka Dar es salaam kuelekea Dodoma  huku  akiifanyia kazi hotuba yake ambayo ataitoa katika Kikao cha Bunge Maalum la Katiba, Ijumaa, Machi 21, 2014.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amealikwa kuwa mgeni rasmi na kuhutubia Bunge Maalum la Katiba kwa mujibu wa Kanuni 7(1)g na Kanuni 75(1) la  ya Kanuni za Bunge Maalum.PICHA NA IKULU.

  =======  =======  =======


  UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS  Telephone:255-22-2114512, 2116898

                press@ikulu.go.tz             

  Fax: 255-22-2113425


  PRESIDENT’S OFFICE,

        THE STATE HOUSE,

                P.O. BOX 9120,  

  DAR ES SALAAM.

  Tanzania.

   
  TAARIFA KWA UMMA.


  Rais Kikwete awasili Dodoma kuhutubia Bunge Maalum la Katiba

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, leo, Alhamisi, Machi 20, 2014, amewasili mjini Dodoma kwa ziara ya kikazi ya siku tatu ambako miongoni mwa mambo mengine atakuwa Mgeni Rasmi na atahutubia Bunge Maalum la Katiba kesho, Ijumaa, Machi 21, 2014.


  Muda mfupi baada ya kuwa amewasili na kulakiwa na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda kwenye Uwanja wa Ndege wa Mjini Dodoma, Rais Kikwete ameendesha Kikao cha Baraza la Mawaziri lake kwenye Ukumbi wa TAMISEMI ikiwa ni shughuli yake ya kwanza katika ziara hiyo fupi ya Mkoa wa Dodoma.


  Kesho, Ijumaa, Rais Kikwete atakuwa mgeni rasmi na atahutubia Bunge Maalum la Katiba kutokana na mwaliko wa Mwenyekiti wa Bunge hilo, Mheshimiwa Samuel  J. Sitta ambaye alimwalika Rais Kikwete kwa barua yake ya Machi 15, mwaka huu, ambayo ilijibiwa Machi 18, mwaka huu, kwa Rais Kikwete kukubali mwaliko huo.


  Mwaliko huo wa Mheshimiwa Sitta kwa Rais Kikwete umetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 7(1) (g) na Kanuni 75 (1) ya Kanuni za Bunge Maalum ambazo zinampa Mwenyekiti wa Bunge Maalum madaraka ya kumwalika Mgeni Rasmi aweze kuhutubia Bunge Maalum.

  Mwisho.


  Imetolewa na;

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu,

  DAR ES SALAAM.

  20 Machi, 2013

  0 0


  0 0

   Afisa Habari wa TASAF (mwenye T-SHIRT NYEUPE) Estom Sanga akizungumza na mmoja wa wanafunzi ambao kaya yake inanufaika na mpango wa kunusuru kaya masikini. 
   Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Mcharo ambao kaya zao zimo kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini wilayani Bunda mkoani Mara. 
   Samweli George na Anna George ambao wanatoka katika kaya inayonufaika na mpango wa kunusuru kaya masikini wakiwa makini kuelekea shuleni. 
    Wanafunzi wa shule ya msingi Mcharo
  Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Mcharo ambao kaya zao zimo kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini wilayani Bunda mkoani Mara.

  Habari kutoka Bunda mkoani Mara kutoka kwa Estom Sanga wa TASAF.
  Michuzi tafadhali nisaidie tutawasiliana baadaye kidogo..

  Mpango wa kunusuru kaya masikini na zinazoishi katika mazingira hatarishi unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini TASAF umewezesha mahudhurio ya wanafunzi katika shule za msingi kuimarisha kwa kati ya asilimi 80 hadi 100.

  Wakizungumza na waandishi wa habari waliotembelea baadhi ya shule ambako wanafunzi wanaotoka katika kaya masikini ambazo ziko katika mpango huo ,wamesema mahudhurio ya wanafunzi kwa sasa ni mazuri hali iliyochangiwa kwa kiwango kikubwa na uboreshwaji wa huduma wanazopata baada ya kaya zao kuingizwa katika mpango wa kunusuru kaya masikini.

  Hivi sasa wanafunzi ambao walikuwa wakikosa masomo kwa kukosa vifaa vikiwemo sare,madaftari,kalamu na hata viatu kwa sasa wanahudhuria masomo yao bila matatizo na hata uelewa wao umeelezwa kuongezeka tofauti na kabla ya mpango huo kuanza.

  Miongoni mwa masharti ambayo kaya masikini zilizoingizwa kwenye mpango wa kuzinusuru ambao unaratibiwa na TASAF ni kuhakikisha kuwa watoto wa kaya husika wanahudhuria shuleni na hata kupata huduma za lishe na matibabu pale wanapoyahitaji.

  0 0
  0 0

  MKurugenzi wa Msama Promotions Ltd,ambao ndio waandaji wa tamasha la krismass na Pasaka,Bwa.Alex Msama amesema kuwa maandalizi ya tamasha la Pasaka linalotarajiwa kuanza kufanyika jijini Dar mnamo April,20 mwaka huu yamekamilika.


  Aakizungumza na Waandishi wa habari jijini dar leo katika viwanja vya Karimjee,Msama amebainisha kuwa kila kitu kimekwishakamilika,wakiwemo wasanii mbalimbali watakaotumbuiza siku hiyo,aidha amesema kuwa pamoja na wanamuziki wa nyumbani kushiriki tamasha hilo,pia kutakuwepo na wanamuziki wengine kutoka nje ya nchi.


  Msama amesema kuwa katika kuhakikisha washabiki na watazamaji wanalifurahia tamasha hilo lenye kujaa nyimbo za kumsifu na kumuabudu Mungu,kutakuwepo na wanamuziki nyota kutoka nchini Afrika kusini,ambao watalipamba vyema tamasha hilo.


  "Katika tamasha hilo kutakuwepo na wanamuziki kutoka Afrika kusini,akiwemo Rebecca Malope  mbaye atatumbuiza kwenye hitimisho la tamasha hilo jijini Mwanza,pamoja na Mwanamuziki Kekeletso Phoofolo ambaye atatumbuiza hapa jijini Dar,wakiwemo na wanamuziki wengine wengi wa hapa nyumbani kama vile Rose Muhando,Upendo Nkone,Bon Mwaitege,John Lisssu,Upendo Kilahilo na wengineo wengi" alisema Msama.

  Msama amesema kuwa Tamasha hilo litazunguka mikoa isiyopungua tisa,ameongeza kuwa pia katika kuisadia jamii,Kamati ya maandalizi ya tamasha la pasaka itaandaa fungu Maalum kwa ajili ya kuwapa Mayatima na watoto waishio katika mazingira magumu.

  Sisi kama Msama Promotions tutaandaa fungu rasmi kwa ajili ya kusaidia watoto Yatima,lengo likiwa ni kuwapa fungu maalum kwa ajili ya kujitegemea,mfano kuwaanzishia biashara ambayo itakuwa endelevu na yenye kuwasaidia badala ya kupewa vitu vya kupita tu kila wakati"alisema Msama.


  Amesema kuwa watatoa fungu maalum kwa kila kituo kwa kuwapa kiasi cha shilingi Milioni tano kwa kila kituo ili kujiendeleza zaidi,na tunalitoa kutokana na mapato ya Pasaka,na mapato mengine yatatumika kuendeleza ujenzi wa kituo cha watoto waishio katika mazingira magumu ,Kituo cha Watoto kiitwacho Jakaya Mrisho Kikwete rafiki wa wasiojiweza.

  0 0

  Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Bw. Harbinder Signh Sethi (kushoto) na Katibu na Mwanasheria Mkuu wa kampuni hiyo Bw. Joseph Makandege (wapili kushoto) wakikabidhi hundi ya shilingi milioni 11 kwa mwakilishi wa Kanisa la Mt. Rita Wakashia lililopo Kimara jijini Dar es Salaam, George Kashushura. Fedha hizo zitatumika kuanzisha SACCOS ya kanisa hilo, lenye lengo la kuwainua vijana kiuchumi. Makabidhiano hayo yalifanyika jijini Dar es Salaam jana
  ======  =======  =======
  IPTL kusaidia miradi ya kuwawezesha vijana kiuchumi  

  Na Mwandishi Wetu

  KAMPUNI ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) imeanza utekelezaji wa mpango wake wa kuiwezesha miradi mbali mbali inayowawezesha vijana wakitanzania kuimarika kiuchumi, ikiwa na lengo la kukuza maendeleo ya uchumi nchini.

  Akizungumza mara baada ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 11 kwa kikundi cha kwaya cha kanisa la Mtakatifu Rita Wakashia lililopo Kimara jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti Mtendaji wa IPTL, Bw. Harbinder Singh Sethi alisema kampuni yake imejidhatiti katika kuhakikisa inatekeleza mipango yake ya kupiga jeki miradi ambayo itasaidia kuondoa umasikini na ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana nchini Tanzania.

  “Hizi milioni 11 tulizotoa kwa Kanisa la Mt. Rita Wakashia, ambazo zitatumika katika uanzishwaji wa SACCOS kwa wanakwaya wa kanisa, ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wetu wa kuchangia katika kusaidia miradi ya kijamii na ya kiuchumi unaolenga kusaidia vijana wa kitanzania kuwa wachangiaji wakubwa katika ukuaji wa uchumi nchini,” alisema Singh.

  Bw. Harbinder alisema mpango huo pia unalenga kusaidia mashule, makanisa, misikiti na makampuni mengine yasiyotengeneza faida yanayofanyakazi ili kuwawezesha vijana kuwa mstari wa mbele katika kuchangia maendeleo ya kiuchumi Tanzania.

  “Tunaamini kuwa SACCOS hii itakayoanzishwa itatoa fursa nzuri ya kujiwekea akiba nakutumika kama  chanzo cha mikopo kwa vijana na wanakwaya wengine wa kanisa. Hii ni hatua kubwa katika kujikwamua kiuchumi katika jumuiya hii ya kanisa, ambayo ni taasisi isiyotengeneza faida,” alisema.

  Naye Katibu na Mwanasheria Mkuu wa IPTL, Bw. Joseph Makandege alisema ili kuwapa sauti vijana na kuwaongezea fursa za kujiimarisha kiuchumi, IPTL kwa kushirikiana na kampuni ya Pan African Power (PAP) imetenga sehemu ya pato lake kwa ajili ya kupiga jeki miradi ya maendeleo ya kijamii, kwa dhamira ya kusaidia miradi ya kimaendeleo inayowalenga vijana.  

  “Sisi kama IPTL na PAP, tumeona kuwa ni jukumu letu kuisaidia jamii inayotuzunguka. Kwa kuanzisha SACCOS, ninaimani vijana wa kanisa la Mt. Rita Wakashia wataweza kuanzisha mradi madhubuti utakaowaletea mabadiliko chanya ya kiuchumi. Hii ndiyo sababu tulishawishika kutoa mtaji huu wa kuanzia ili kuwawezesha kuanzisha SACCOS,” alisema Bw. Makandege.   

  Akizungumza kwa niaba ya wanakwaya na waumini wengine wa kanisa hilo, Bw. George Kashushura alizishukuru IPTL na PAP kwa msaada wao na kubainisha kuwa fedha iliyotolewa itaelekezwa katika malengo mazuri yatakayobadilisha maisha ya vijana walio wengi.

  “Fedha tulizopokea leo hii zitatumika kama mtaji wa kuanzisha SACCOS yetu ya kanisa ambayo itakuwa ni chachu ya mabadiliko ya maisha ya vijana walio wengi katika kanisa letu,” alisema Kashushura.

  0 0

   Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo wakati wa kikao baina ya Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na makampuni washirika ya StatOil, BG Tanzania, Exxon Mobil na Orphir Energy. Katikati ni Rais na Meneja Mkuu wa Kampuni ya BG Kanda ya Afrika Mashariki Bw. Derek Hudson. 

   Rais  na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Exxon Mobil Bw. Rolf Michael de Jong   kwa niaba ya washirika  wa  makampuni  yanayofanya maandalizi ya utekelezaji wa Mradi huo wa gesi iliyosindikwa (LNG)  akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wakati wa kikao hicho.

   Mkuu wa Mashauriano wa Kampuni ya StatOil Tanzania Bw. Ole- Johan Lydersen wa kwanza mwishoni akiongea jambo wakati wa kikao hicho.

  Afisa Mipango Miji Bw. Daniel Nguno kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akiongea jambo wakati wa kikao hicho cha majadiliano ya utekelezaji wa mradi wa LNG.


   ========  ======  =======

  Tufanyekazi, Watanzania wana matarajio makubwa na gesi –Muhongo


  Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam.


  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ameeleza kuwa, Watanzania wana matarajio makubwa kutokana na kugunduliwa kwa hazina kubwa ya gesi katika maeneo ya kina kirefu cha bahari.


  Profesa Muhongo ameyasema hayo wakati wa kikao kati ya Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na makampuni washirika ya Statoil, BG Tanzania, Exxon mobil na Orphir Energy yanayofanya maandalizi ya utekelezaji wa mradi wa   gesi  iliyosindikwa (LNG).


  Ameongeza kuwa, Serikali inayo nia ya dhati katika kutekeleza mradi huo ili kuhakikisha kwamba uchumi wa gesi unakuwa wa manufaa kwa Watanzania wote. Hivyo, wenye jukumu la utekelezaji wametakiwa kutekeleza mipango mikakati yao kwa kuzingatia muda husika, wakati huo huo wakifanyakazi kwa ushirikiano na mamlaka husika na kwa uwazi.


  “Wananchi wana matarajio makubwa na gesi, msiiangushe Tanzania katika hili, hatutaki kuonekana waongo, mkichelewa mnatupa wakati mgumu. Sisi sote tunatakiwa kuongea lugha moja kwa wananchi. Tumejipanga vizuri tunachotaka ni kutekeleza mipango yetu”. Amesema Profesa Muhongo.


  Katika hatua nyingine, Waziri Muhongo na Katibu Mkuu wa Wizara Bw. Eliakim Maswi, wamesisitiza kuwa makampuni hayo,  yanapaswa kuhakikisha kwamba mipango yao  ya utekelezaji wa mradi huo  inapaswa kwenda sambamba na matakwa   ya Sera ya  Gesi Asilia.


  Katika kikao hicho, makampuni hayo washirika yamewasilisha  taarifa ya hatua waliyofikia katika  maandalizi ya utekelezaji wa mpango kazi wa mradi huo  na kueleza hatua mbalimbali ambazo zimefikiwa na zinazotakiwa kuchukuliwa ili utekelezaji wa mradi  ufanyike kama ulivyopangwa.


  Aidha, katika taarifa hiyo wameainisha hatua mbalimbali ambazo watatekeleza katika maeneo ambayo gesi imegunduliwa vikiwemo vyanzo vya Zafarani, Lavani na Tangawizi katika kitalu namba 2 kilichopo mashariki mwa Mkoa wa Lindi.  0 0

   Mkurugenzi wa Wanafunzi wanaochukua Mafunzo ya Shahada ya kwanza katika Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Dk. Esther Mbise akimkaribisha mgeni rasmi, Meneja Kiongozi Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii ( NSSF), Eunice Chiume (katikati),wakati wa Semina kwa wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), iliyofanyika katika chuoni hapo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Masoko chuoni hapo, Felix Chale. Jumla ya wanachuo 180 walihudhuria semina hiyo.
  Meneja Kiongozi Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume akitoa mada wakati wa semina ya kuwawezesha wanafunzi wa vyuo vya Elimu ya Juu kuwa na uelewa kuhusu Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii  (NSSF), pindi watakapomaliza elimu yao.
  Baadhi ya wanafunzi wakimsdikiliza kwa makini, Meneja Kiongozi Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume wakati akitoa mada katika semina hiyo.
   Meneja Kiongozi Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume akitoa mada kuhusu faida za kuwa mwanachama wa NSSF.
  Tunasikiliza kwa makini.
   Baadhi ya maofisa wa NSSF wakigawa vipeperushi vyenye maelezo ya muhimu kuhusu NSSF.
  Ofisa Uhusiano wa NSSF, Maife Kapinga akigawa vibeberushi kwa wanafunzi wa CBE wakati wa kongamano hilo.
   Tunajifunza hifadhi ya jamii.
   Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha CBE wakisikiliza kwa makini kazi za mfuko wa hifadhi ya jamii na faida zake
   Meneja Kiongozi Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume akijibu maswali ya wanadunzi wa CBE kuhusiana na mfuko wa Taifa Hifadhi ya Jamii wa NSSF.
   Jonas Pera akiuliza swali.
   Mwanachuo wa CBE, Hadson Mwakilima akiuliza swali kuhusu mafao ya NSSF.
  Mwanafunzi aliyejitambulisha kwa jina la Mohamed akiuliza swali.
  Wanafunzi wakipewa zawadi za fulana za NSSF.
  Ofisa Uhusiano wa NSSF, Maife Kapiga akigawa zawadi ya Kalenda za NSSF kwa wanafunzi wa CBE.
  Ofisa Uhusiano wa NSSF, Said Mohamed akifafanua jambo wakati wa semina hiyo.

  0 0

   Pichani ni Postamasta Mkuu na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania,Bwa.Deos Mndeme akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye Makao makuu ya Ofisi hizo jijini Dar mapema leo kuhusiana na taarifa juu ya utekelezaji wa Mpango Kabambe wa miaka kumi (2014-2023) wa shirika la Posta Tanzania,wakati Tanzania ikielekea kuadhimisha miaka 50 ya Muungano
  Pichani Kulia ni Meneja Mkuu Uendeshaji wa Biashara,Bwa.Fortunatus Kapinga akifafanua jambo kuhusiana na taarifa juu ya utekelezaji wa Mpango Kabambe wa miaka kumi (2014-2023) wa shirika la Posta Tanzania,wakati Tanzania ikielekea kuadhimisha miaka 50 ya Muungano.Amesema kuwa Shirika la Posta limeanza utekelezaji mpango kabambe wa miaka kumi (2014-2023) ikiwa ni dira na mwelekeo wa kuliongoza shirika hilo liweze kujiendesha kibiashara,kubuni na kutoa huduma mbadala,kutumia teknolojia maridhawa na kukidhi mahitaji ya soko la huduma za mawasiliano jumuishi.Kushoto kwake ni Postamasta Mkuu na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania,Bwa.Deos Mndeme.
   Pichani kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Masuala ya Kimataifa wa Shirika la Posta Tanzania,Bwa.Elias Madule akifuatilia mkutano huo akiwa sambamba na mdau mwingine wa shirika hilo la Posta.
   Waandishi wa Habari wakisikiliza taarifa juu ya utekelezaji wa Mpango Kabambe wa miaka kumi (2014-2023) wa shirika la Posta Tanzania kutoka kwa Viongozi wakuu wa Shirika hilo,katika mkutano uliofanyika mapema leo,ndani ya Makao makuu ya Ofisi hizo jijini Dar.

  0 0

   Mkurugenzi mtendaji wa Fortis Insurance Brokers Ltd , Bi Maryam Shamo.( wa pili Kulia) akimkabidhi Mshindi wa mwanamakuka 2014‎, nyaraka zake za Bima. Wengine ni wafanyakazi wa kampuni hio.
  Mshindi wa Mwanamakuka 2014, Bi Leyla Mwambungu, baada ya kujinyakulia Tuzo ya Million Tatu, kweye Tuzo za Mwanamakuka Awards, ambazo zinaandaliwa na Unity Of Women Friends. Fortis Insurance Brokers Ltd, Imeamua kulinda Biashara yake Kuwa kwa kumkatia Bima ya Moto Na Wizi, Ili Biashara yake isije ikatetereka atakapopata majanga hayo.

  0 0

  Bw. Sultan A. Sultan akitoa mada wakati wa kongamano la viongozi lililojadili mada kuu isemayo ‘Rasilimali za Taifa kwa amani na Maendeleo, Bagamoyo , Pwani  tarehe 20 Machi,2014.

  =====  ====== =====
  Zipo fursa nyingi kwenye uchumi wa gesi- Sultan

  Na Malik Munisi, Bagamoyo.


  Watanzania wameaswa kutambua fursa zitokanazo na rasilimali zinazogunduliwa nchini ili waweze kunufaika kutokana na uwepo wa rasilimali hizo.


  Hayo yamebainishwa na Bwana Sultan Sultani mkazi wa kilwa alipokuwa akitoa mada juu ya ‘‘Ushiriki wa wenyeji katika shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi asilia’’, katika Kongamano la Viongozi lililojadili mada kuhusu  “Rasilimali zetu za gesi asilia, mafuta na madini kwa amani na maendeleo ya Tanzania” lililofanyika Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.


  Bw. Sultani alieleza kuwa, wananchi wanatakiwa kuelewa fursa mbadala zipatikanazo kutokana na uwepo wa rasilimali za gesi na mafuta nchini zikiwemo ununuzi wa hisa  kwa makampuni makubwa ili kuwawezesha kuongeza  mtaji yao  ambapo faida yake itapatikana mara tu baada ya gesi kuanza kuuzwa.


  Aidha, alitaja fursa nyingine kuwa ni uwezekano wa uhitaji mkubwa wa majengo na maghala yatakayohitajika kwa ajili ya kutunza vifaa na pembejeo muhimu kwa ajili ya utafutaji na uzalishaji wa gesi katika maeneo yaliyoko baharini.


  Alizitaja fursa nyingine kuwa ni pamoja na makampuni ya ulinzi, kampuni za usafirishaji, maabara, vyuo maalumu vya kuelimisha umma katika tasnia ya petroli na nyanja zake, makampuni ya kutunza mazingira, usalama na afya, na kuongeza kuwa  hizo ni baadhi tu ya fursa zitokanazo na uwepo wa rasilimali gesi na mafuta nchini.

    
  Pamoja na hayo, alieleza uwekezaji katika mafuta na gesi si bahati nasibu ya kutoa moja ukapata milioni moja bali ni ile ya kutoa mamilioni kama sio mabilioni na kisha ukaambulia patupu. Hivyo, alisisitiza kuwa, mifano ipo ya watu walionunua leseni za utafiti kwa kuwekeza mabilioni wakaishaia kukosa na matokeo yake wakapoteza maisha kwa maradhi ya moyo au msongo wa mawazo.


  “Pamoja na kuwa sayansi ya hali ya juu kutumika katika utafiti wa mafuta na gesi, bado kwa kiasi kikubwa ugunduzi wa rasilimali hizi ni wa pata potea huku uwekezaji wake ukiwa ni wa ghali sana” aliongeza Sultan.


  Alisisitiza kuwa, yapo makampuni mbalimbali yaliyofika nchini ili kuwekeza katika maeneo ya Songosongo (Lindi) na Msimbati (Mtwara) ambapo mengi yaliingia kwa kifua mbele lakini yakatokea kwa mlango wa nyuma kutokana na ugumu wa kazi hiyo na kufanya utafiti bila ya mafanikio.


  Mwisho Sultan alihimiza umuhimu wa wananchi kuelezwa mapema ugumu na pata potea iliyopo katika sekta ya mafuta na gesi  ili wananchi waweze kuzitambua fursa na  kujihusisha katika kuanzisha biashara katika maeneo mbalimbali ili waweze kutoa huduma kwa wawekezaji wanaofanya utafiti na wale wanaoendelea na shughuli za uchimbaji wa gesi asilia, ikiwemo  elimu ya soko la hisa ili iweze kuwasaidia wananchi kuwekeza katika makampuni ya mafuta katika namna ambayo itawanufaisha.

  0 0
  Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bi. Joyce Fisoo akionyesha moja ya picha zinazotolewa na wadau wa filamu kama matangazo ya kutambulisha filamu zao sokoni, kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Consilia Niyibitanga. Picha na Genofeva Matemu – Afisa Mawasiliano Serikalilini, WHVUM.

  Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bi. Joyce Fisoo akizungumza na waandishi wa habari, hawapo pichani wakati wa mkutano wa waandishi wa habari kuhusu mafanikio yaliyopatikana Bodi ya Filamu kuanzia miaka ya 1930 hadi sasa, kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Consilia Niyibitanga.

  0 0

   Waziri wa Maji Maji Profesa.Jumanne Maghembe, akiweka jiwe la msingi kuashiria kuzindua rasmi kisma cha bomba la maji katika kijiji cha Kwadelo Halmashauri Wilaya ya Kondoa Machi 20, 2014 sambamba na maadhimisho ya kilele cha wiki ya maji dunia ambapo kitaifa yana fanyikia Mkoani Dodoma (kulia kwake), Mbunge wa Jimbo la Kaskazini Kondoa Mhe: Zabeini Mhita. kauli mbiu ni uhakika wa maji na nishati.
   Profesa.Jumanne Maghembe akipanda mti baada ya kuzindua mradi wa maji.
   Waziri wa Maji Maji Profesa.Jumanne Maghembe akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa kijiji cha Kwadelo Bi.Hawa Athuman baada ya kuzindua rasmi kisima cha bomba la maji.
   Waziri wa Maji Maji Profesa.Jumanne Maghembe pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara  hiyo, Enjinia Bashir Mrindoko wakihutubia wakazi wa kijiji cha Kwadelo Halmashauri Wilaya ya Kondoa sambamba na maadhimisho ya kilele cha wiki ya maji dunia ambapo kitaifa yana fanyikia Mkoani Dodoma
   wakazi wa kijiji cha Kwadelo Halmashauri Wilaya ya Kondoa wakishuhudia uzinduzi wa mradi wa mji.
   wakazi wa kijiji cha Kwadelo Halmashauri Wilaya ya Kondoa wakishuhudia uzinduzi wa mradi wa mji.

  0 0

  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid wakati akitoa tamko kuhusu ugonjwa  wa kifua kikuu   kwenye ukumbi wa wizara hiyo mjini Dodoma leo.
   Baadhi ya waandishi wa habari wakimsilikiza Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid wakati akitoa tamko kuhusu ugonjwa wa kifua kikuu   kwenye ukumbi wa wizara hiyo mjini Dodoma leo 
    Meneja Mpango  wa kudhibiti kifua kikuu na ukoma, Dk. Beatrice Mutayoba wa kwanza kulia , katikati ni Naibu Meneja wa  mpango  huo, kushoto ni Afisa wa mpango huo Dk.Deus Kamara wote  kutoka Dodoma.Picha na Magreth Kinabo -Maelezo
  ========  ======  =======
  Na Magreth Kinabo-
   
  Imeelezwa kuwa ugonjwa wa kifua kikuu  ni ugonjwa wa tatu ambao unasababisha vifo vya watu wengi hapa nchini  baada ya Malaria na Ukimwi.

   Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid wakati akitoa tamko kuhusu ugonjwa huo kwenye ukumbi wa wizara hiyo mjini Dodoma, ambayo itaandhimishwa Machi 24, mwaka 2014 hapa nchini na nchi nyingine  duniani .

  Aidha  kwa mujibu wa takwimu za Wizara hiyo zinaonesha kuwa  idadi ya wagonjwa wa ugonjwa huo imeongezeka kutoka 11,000 mwaka 1980  hadi kufikia 63,892 mwaka 2012. “ Utafiti unaonesha kuwa zaidi ya asilimia 30 ya vifo vya watu vya watu walioathirika na ukimwi vinatokana na kiifua kikuu.

  “Tangu kuzuka kwa ukimwi hapa nchini ,inakadriwa kuwa  asilimia10 ya waathirika wa ukimwi wana ugonjwa wa kifua kikuu na takribani asilimia 40 ya wagonjwa wa kifua kikuu wana maambukizo ya VVU. Hali hii inafanya kifua kikuu kuwa miongoni mwa changamoto kubwa katika mapambano dhidi ya ukimwi na katika vita vya kutokomeza umasikini hapa nchini,” alisema Dk. Rashid.

   Dk. Rashid   aliongeza kuwa  miongoni mwa sababu nyingine zinazochangia kuongezeka kwa idadi ni msongamano wa watu mijini, makazi duni  ya watu na wagonjwa kuchelewa kupata matibabu.Aliitaja kauli mbiu ya mwaka huu “ Fikia  kila mtu Gundua .Tibu na Ponya mgonjwa wa TB” .

   Aliongeza kuwa sasa  takribani zaidi ya watu milioni mbili  hufariki kwa ugonjwa huo kila mwaka na asilimia kubwa ya vifo hivyo hutokwa Barani Afrika hususa Kusini mwa Jangwa la Sahara. Hivyo Tanzania ni nchi ya 14 kati ya nchi 22 zenye idadi kubwa  ya wagonjwa wa  ugonjwa huo duniani.

   Alisema  miongoni mwa mikoa inayoongoza kuwa na  wagonjwa wapya  wengi  kwa takwimu za mwaka 2012  kati ya mikoa iliyoathirika kwa tatizo hilo ni Dares Salaam 13,983,Mwanza 5,946 na Shinyanga 4,074.
   

  0 0


  0 0
  0 0

older | 1 | .... | 252 | 253 | (Page 254) | 255 | 256 | .... | 1897 | newer