More Channels
Showcase
Articles on this Page
(showing articles 4941 to 4960 of 37937)
- 03/13/14--11:49: _ RIDHIWANI ARUDISHA...
- 03/13/14--13:30: _Taarifa kwa Umma: V...
- 03/13/14--20:35: _THE AFROMUN YOUTH C...
- 03/13/14--20:39: _MIYEYUSHO KUZIPIGA ...
- 03/13/14--20:46: _KATIBU WA CCM IRING...
- 03/13/14--20:59: _ASKARI MOSES ALPHAG...
- 03/13/14--21:00: _NIKOPESHENI IMANI Y...
- 03/13/14--21:04: _KUTANA NA DOREEN PE...
- 03/14/14--00:11: _JESHI LA POLISI LAW...
- 03/14/14--02:38: _TUME YA TAIFA YA UC...
- 03/14/14--02:52: _Rais Dkt. Jakaya Ki...
- 03/14/14--08:33: _Kapteni Chiligati: ...
- 03/14/14--08:35: _Tujivunie Uimara wa...
- 03/14/14--08:39: _:MADEREVA WA BODA B...
- 03/14/14--08:59: _Airtel yakabidhi mi...
- 03/14/14--09:18: _Wafanyabiashara na ...
- 03/14/14--10:10: _MAKAMU WA RAIS DKT....
- 03/14/14--10:12: _KISHAKILENA REALITY...
- 03/14/14--10:14: _Wajumbe Bunge Maalu...
- 03/14/14--10:21: _TAASISI YA VIWANGO ...
(showing articles 4941 to 4960 of 37937)
Channel Description:
Karibuni Jamvini Wanajamii
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Ridhiwani Kikwete leo amerudisha fomu ya kugombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi, akisindikizwa na washindani wake katika kura za maoni, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ramadhan Maneno pamoja na Imani Madega.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Ridhiwani Kikwete akiwa ameambatana na washindani wake katika kura za maoni, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ramadhan Maneno pamoja na Imani Madega wakifurahia jambo.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Ridhiwani Kikwete akiwa ameambatana na washindani wake katika kura za maoni, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ramadhan Maneno pamoja na Imani Madega na wadau wengine akielekea kurejesha fomu.
Baadhi ya Wanahabari wakishuhudia tukio la Urudishwaji fomu wa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi mapema leo.
=========== ======== ======
Ridhiwani arudisha fomu za Ubunge Chalinze.
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Ridhiwani Kikwete leo amerudisha fomu ya kugombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi.
Akisindikizwa na washindani wake katika kura za maoni, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ramadhan Maneno pamoja na Imani Madega, Ridhiwani aliwashukuru wana CCM na wakazi wa Chalinze kwa ujumla kwa kumuunga mkono.
Ridhiwani pia ameahidi kushirikiana na wanachalinze katika kutekeleza yote yaliyofanywa na wabunge waliotangulia lakini pia amewataka wakazi wa Chalinze kupuuza hoja inayotolewa na mgombe wa Chadema inayodhihaki kuwa yeye sio mkazi wa Chalinze. Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chadema Matayo Torongey alinukuliwa akisema kuwa Ridhwani hawezi kugombea Ubunge Chalinze kwa kuwa sio mkazi wa Jimbo hilo.
Aliongeza kuwa ili kuwahakikishia wakazi wa Chalinze maendeleo inatakiwa kwa wagombea kutangaza sera zinazotekelezeka na kuacha kutoa kauli zenye nia ya kuwapumbaza wakazi wa Chalinze.
Alisema kuwa hatotaka kutumia muda wake kufanya kampeni za kiubabaishaji kuanza kurumbana na kukejeli kwa kuwa amekuwa katika misingi mizuri ya kisiasa. Alisema hajatokea chumbani kugombania Ubunge badala yake amekuwa katika misingi ya kisiasa tangia mdogo na amechukua uamuzi wa kuingia katika siasa kwa lengo la kusaidia wananchi.
Alisema kuwa kero kubwa inayowakabili wakazi wa Chalinze ni kukosekana kwa maji ya uhakika, kero ambayo kwa sasa inatatuliwa kwa kuanzishwa kwa mradi wa maji ya uhakika. Aliongeza kuwa pia kuna tatizo kubwa la ukosefu wa huduma bora za afya uhakika za afya kwa wakazi wa eneo la Chalinze. "Najua awali wakazi wa eneo la Chalinze walikuwa wachache sana na kwa sasa kuna ongezeko kubwa la wakazi wa Chalinze hivyo hata mahitaji nayo yanaongezeka"alisema Ridhwani.
Aliongeza kuwa ongezeko hilo limepelekea kuongezeka kwa uhitaji wa huduma mbalimbali kama hizo za za kijamii na kuongeza kuwa akiwa Mbunge atatatua kero hizo."Watu wanadhania kuwa mimi nimetokea chumbani kuja kwenye siasa hapana yani tena hata sio kwa sababu ya kuwa mimi ni mtoto wa Rais ndio nimeona ngoja nije kuuza sura huku sio, ila ni kwa sababu nimekulia katika mazingira haya na ninaona kuwa ni wakati wa kutatua kero za wakazi wenzangu wa huku"alisema Ridhiwani.
Kuhusiana na tatizo la migogoro katika jimbo hilo alisema kuwa anaona kuwa analo jukumu kubwa la kuendelea kushiriki katika kutatua kero zao ambazo CCM kwa muda mrefu imekuwa ikifanya hivyo. Alisema kuwa atakuwa na haki ya kupata mikosi iwapo akipuuzia kutatua kero ya muda mrefu ya wafugaji na wakulima.
Ridhwani anatarajia kuzindua rasmi kampeni yake Jumamosi ijayo katika jimbo la Chalinze. Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Chalinze unafanyika kufuatia kifo cha aliekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Said Bwamdogo.
0 |
|
0 |
|






Promota Ally Mwazoa katikati akiwatambulisha mabondia Fransic Miyeyusho kushoto na Mohamed Matumla wakati wa kutangaza mpambano wao utakaofanyika April 26 katika ukumbi wa PTA Sabasaba. |
Bondia Fransic Miyeyusho kushoto na Mohamed Matumla wakikumbatiana baada ya kukubaliana kuzipiga April 26 katika ukumbi wa PTA Sabasaba . |
Bondia Fransic Miyeyusho wakitunishiana misuli na Mohamed Matumla wakati wa utambulisho wa mpambano wao mbele ya waandishi wa habari Picha nawww.superdboxingcoach. |
Na Mwandishi Wetu
MABONDIA Fransic Miyeyusho 'Chichi Mawe' na Mohamed Matumla 'Snake JR' leo wamesaini mkataba wa kupambana april 26 katika ukumbi wa PTA Sabasaba
Akizungumzia mpambano huo promota wa mchezo wa masumbwi nchini Ally Mwazoa amesema ameingia nao mkataba mabondia hawo kwa kuwa anajua wanaweza mchezo wa masumbwi na ni mafundi wa mchezo huo najua kuna watu wengi walitamani kudhamini mchezo huo lakini bahati imeniangukia mie
mpambano uho utakaopigwa april 26 katika ukumbi wa pta sabasaba kutakuwa na mapambano mengine makali ya utangulizi ambapo mwana dada Lulu Kayage atamvaana na Halima Ramadhani siku hiyo kwa ajili ya kuhamasisha wanawake wenzao wajitokeze katika mchezo wa masumbwi
baada ya kusaini mkataba huo bondia Miyeyusho alijitamba kuendeleza ubabe katika familia hiyo ambapo alisema atamchakaza kama alivyo mchakaza baba yake mdogo Mbwana Matumla ambaye amecheza nae mara tatu na kupigwa mara mbili ambapo mpambano wa mwisho ulikuwa na shamu shamu nyingi kila upande miyeyeyusho alibuka mshindi kwa point
nae Matumla alijibu mapigo kwa kusema Miyeyusho anamuheshimu kwa kuwa yeyey ni mkubwa kiumri ata hivyo atampa kichapo kikali kama alivyompatia mdogo wake Doi Miyeyusho ambaye mara ya kwaza alipigwa kwa K,O raundi ya pili DDC Keko na mara ya pili pia K,O ya raundi ya pili katika ukumbi uho uho uho wa PTA Sabasaba hivyo siwezi kushusha rekodi yangu kwa kupigwa na miyeyusho akitaka kujua mimi ni mkali zaidi yao amulize pia Nassibu Ramadhani ambaye nilimpatia kipigo kibaya sana na kunifanya ninyakue pikipiki.
, Mwazoa

aliongeza kuwa ulizi na usalama wa mali zako ni wa huwakika hivyo familia nzima mnaweza kuja kushudia mpambano huo wa masumbwi bila shaka
0 |
|
0 |
|
)
Wananchi wa kijiji cha Ilandutwa,kata ya Mgama,Iringa Vijijini wakinyanyua mikono yao juu kumuunga mkono Mgombea Ubunge jimbo la kalenga,Ndugu. Godfrey Mgimwa.
Wananchi wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni wa CCM,kwa ajili kuzisikiliza sera za mgombea Ubunge wa Jimbo la kalenga,Ndugu Godfrey Mgimwa,uliofanyika kwenye kijiji cha Ilandutwa,kata ya Mgama Iringa Vijijini
Mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia chama cha Mapinduzi CCM Bw. Godfrey Mgimwa akiwahutubia wananchi katika kijiji cha Ilandutwa kata ya Mgama Iringa vijijini akiendelea na mikutano mbalimbali ya kampeni ambapo amewaomba wananchi wa vijiji hivyo kumkopesha imani yao na kumpa kura za ndiyo siku ya machi 16 jumapili ijayo ili aweze kuwalipa maendeleo katika jimbo hilo.
Wananchi wakishangilia jambo
Diwani wa kata ya Mgama Bw. Denis Lupala akipiga magoti kumuombea kura mgombea wa CCM Bw. Godfrey Mgimwa.
Wakazi wa kijiji cha Itwanga,Kata ya Mgama wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo wa kampeni,ambapo siku ya jumapili machi 16 ndio utafanyika uchaguzi mdogo wa kumpata Mbunge wa Jimbo la Kalenga.
Wakazi wa kijiji cha Udumka,kata ya Ifunda Iringa Vijijini wakimsikiliza mgombea Ubunge wa jimbo la kalenga,Godfrey Mgimwa akinadi sera zake na kuomba kupigiwa kura za kutosha na hatimae kuibuka na ushindi wa Ubunge,ili apate ridhaa ya kuwaongoza na kuyaendeleza yale yaliyoachwa na Mbunge aliyepita,Marehemu William Mgimwa.
Mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia chama cha Mapinduzi CCM Bw. Godfrey Mgimwa akiwahutubia wananchi katika kijiji cha Udumka Kata ya Ifunda, Iringa vijijini mapema leo jioni..
Baadhi ya Wanahabari wakiendelea kuchukua matukio mbalimbali yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo
MOblog Tanzania hivi karibuni ilifanya mahojiano na Mjasiriamali na mbunifu wa mavazi nchini Doreen Noni aliyehudhuria mkutano wa Uchumi Duniani uliofanyika huko Davos, Uswisi (World Economic Forum) mwezi uliopita juu ya yote anazungumzia nafasi ya Wanawake, Vijana na Ujasiriamali endelea…….
MOblog: Ulipata nafasi ya kuhudhuria mkutano wa Uchumi duniani (World Economic Forum 2014) hebu tueleze ulipata vipi nafasi ya kuhudhuria?
Doreen: Mimi nilipata nafasi ya kuhudhuria (World Economic Forum) kupitia asasi ya Global Shapers ambayo ni delegation ya vijana kupitia World Economic Forum na vijana kuanzia miaka 20 mpaka 30 ambao kazi yao kuu ni kuangalia vijana ambao wanaleta mabadiliko katika jamii na ushiriki wa vijana katika maeneo mbalimbali, ya ujasiriamali kwa hiyo nilituma maombi kwenye jukwaa la Uchumi Duniani na wao wakaona nafaa kuhudhuria na nikahudhuria kwa hiyo nikawa mjumbe wa World Economic Forum kama kijana na jukwaa la kuwakilisha vijana wa bara la Afrika na nimehudhuria mikutano mitatu ya uchumi duniani mpaka sasa.
MOblog: Je kwenye mkutano huu wa hivi karibuni nini kilijitokeza?
Doreen: Nilikuwa kwenye session tofauti nilikuwa kwenye panelist mbalimbali, kama vile Innovation and Design na panelist nyingine ilikuwa Africa the next billionaire ambayo kulikuwa na marais mbalimbali kama vile Goodluck Ebele Jonathan; Rais wa Nigeria, Aliko Dangote; Afisa Mtendaji Mkuu wa Dangote Group na John Mahama; Rais wa Ghana, hii session ilikuwa inaogelea kuhusu umati wa watu Afrika na vijana tulikuwa kama 50 ambao tulihudhuria mkutano huu na vijana wengi Afrika wanatuma maombi duniani na kila session wanataka vijana wahudhurie kwa hiyo wanataka kujua uwezo wa vijana katika maswala mbalimbali ya kiuchumi, kijamii na kijamii.
Kusoma Mahojiano yote Ingiahapa
0 |
|
0 |
|
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa,Ramadhani Mungi akizungumza na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali,mapema leo asubuhi kwenye Ofisi zake,kuhusiana na mambo mbalimbali yaliyohusu kuelekea Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Kalenga,mkoani Iringa.
======== ====== ===========
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA
“PRESS RELEASE”
Ndugu waandishi wa habari , kwa niaba ya askari Polisi wa Mkoa wa Iringa, nitumie fursa hii kuwakaribisha hapa ofisini kwetu.
Ndugu zangu tumeitana hapa asubuhi hii ili niweze kuwapa taarifa ya usalama katika Mkoa wetu wa Iringa hususani katika Jimbo la Kalenga katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi wa Jimbo la Kalenga na usalama wa siku ya uchaguzi wenyewe.Ili iwe rahisi kueleweka taarifa hii nitaitoa kwa kifupi sana kwa kuigawa katika maeneo matatu.
Eneo la kwanza ni juu ya wapi tunataka tupafikie ( Where we want to go ), eneo la pili ni lile la wapi tulipo ( Where are we? ) na eneo la tatu ni jinsi gani tutafika huko ( How do we get there ). Tuanze na wapi tunataka tupafikie. Sisi Polisi Mkoa wa Iringa tunataka wananchi wa Kalenga wapinge kura kwa amani na utulivu mkubwa siku ya jumapili tarehe 16/3/2014. Hii ndio dila yetu na tutahakikisha tunafika hapo.
Kuhusu wapi tulipo sasa, naomba niwaelezeni kwa ufupi sana matukio ya kijinai kuanzia tarehe 19/02/14 mpaka leo. Ndugu zangu, kuanzia tarehe hiyo mpaka tarehe 2/03/2014 takribani wiki mbili hakukuwa na tukio lolote la uvunjifu wa amani lililokuwa limepokelewa katika vituo vyetu vya Polisi.
Hali ilianza kubadilika tarehe 3/3/2014 ambapo baadhi ya waandishi walifika ofisi kwangu na kunieleza kuwa kumetoka kwenye mkutano wa CHADEMA ambapo wameelezwa na chama hicho kuwa usiku wa siku hiyo walimkamata mtu mmoja kwa kosa la kujaribu kuchoma moto nyumba waliokuwa wakiishi wafuasi wao katika kijiji cha WASA.
Waandishi hao walinitaka nithibitishe kutendeka kwa kosa hilo na walieleza kuwa wameelezwa kuwa bado halijaripotiwa kituoni. Mimi nilikataa kusema lolote kuhusu hilo kwani lilikuwa bado halijaripotiwa Polisi.
Tarehe 4/03/2014 nilifuatwa tena na baadhi ya waandishi na kunieleza kuwa siku hiyo waliitwa na CCM na kuelezwa kuwa siku ya tarehe 27/2/2014 walitegewa misumari katika kijiji cha WASA ili mabasi yaliyokuwa yamebeba wafuasi wao yaweze kutobolewa magurudumu yake, pia nao walisema tukio hilo halijaripotiwa Polisi. Mimi nilikataa kulizungumzia swala hilo.
Ndugu wanahabari, vitendo vilivyofanywa na vyama hivyo vililenga kuanzisha propaganda za kisiasa kwa kutumia uhalifu kwa kupitia vyombo vya habari. Sisi Polisi tulibaini hali hiyo na ndiyo sababu tuliamua kuwa kimya na nyinyi wenzetu kwa kuzingatia maadili ya kazi zenu pia mlikaa kimya. Kuanzia hapo vyama vilianzisha mashindano ya kuripoti kesi zao Polisi. Leo hii vyama hivyo vimeripoti kesi ishirini na moja ambazo zilisababisha kukamatwa kwa wafuasi (19) wa vyama hivyo viwili.
Ndugu waandishi, kati ya kesi hizo ishirini na moja, kesi kumi na tisa (19) zile ambazo hazina madhara ya moja kwa moja kwa binadamu ama mali, kesi hizo ni zile ndogondogo sana, kama vile kuchana mabango, kuteremsha bendera, kuchana vipeperushi, kutukanana n.k. kesi tatu zilikuwa zile zenye madhara kwa binadamu na mali ambazo ni kupigana hadharani, kujeruhi na kuharibu mali. Kati ya kesi ishirini na moja (21), kesi kumi upelelezi wake umekamilika na majalada yake yamefikishwa kwa mwanasheria wa serikali.
Ndugu waandishi, katika kesi hizo Polisi tumeibaini mengi mfano CHADEMA kilikuwa kikitoa malamiko kuwa tumeacha kumkamata ndugu hassan mtenga mtuhumiwa wa kesi moja iliyokuwa imefunguliwa dhidi yake. Shutuma hizo hazina msingi kwani kesi iliyofunguliwa dhidi ya mtu huyo haikuwa ya jinai bali ya madai na tuliwajulisha hivyo. Nia ya kufanya hivyo ilikuwa kuifanya jamii iamini kuwa Polisi ni dhaifu na wenye kuonyesha upendeleo katika kushughulikia kesi za uchaguzi. Nashukuru Polisi tulikuwa watulivu, hatukujibu na jamii imetuelewa sana.
Ndugu waandishi, sijui mlijulishwa na nani kwamba Padri mmoja alifungwa kamba na alipingwa na kuburuzwa. Nanyi bila ya kuthibitisha kwetu mkaandika habari hiyo. Tuwaeleze kuwa mtu huyo ni miongoni mwa watuhumiwa tuliowakamata katika moja ya makosa yaliyotendeka, tulimhoji, aliandikwa maelezo yake na alipewa dhamana. Hata siku moja hajawahi kutoa taarifa Polisi juu ya matukio aliyotendewa. Nia ya kutangaza taarifa hiyo ni kuzua hofu kwa wananchi na kutaka kuchochea chuki kwa wafuasi wa dhehebu lake na wale wa dini yake.
Ndugu waandishi, pamoja na matukio hayo polisi tumekuwa tukipokea taarifa za vitisho vya kuwepo kwa watu mbalimbali kutoka kwa vyama vyote walioingizwa mkoani humu kwa nia ya kutenda vitendo vya uvunjifu wa amani. Aidha, tumewasikia viongozi wa vyama wakitamba kuingiza maelfu ya watu mkoani mwetu. Kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Arusha, Mbeya kwa visingizio vya kulinda kura.
Sasa nataka niwaeleze kuwa sheria iko wazi kabisa, kila kituo cha kupigia kura kitakuwa na wakala wa chama kinachoshiriki katika uchaguzi huo na hao ndio wawakilishi wa chama hicho na walinzi halali wa uchaguzi ni askari wa Jeshi la Polisi.
Kufuatia hali hiyo mambo yafuatayo yanasisistizwa sana.
1. Hatutaki kuona walinzi wa chama chochote katika Jimbo la Kalenga. Jukumu la kulinda uchaguzi, maisha na mali ya wana Kalenga ni la JESHI LA POLISI.
2. Hatutaki kuona watu wasiokuwa na shughuli maalumu wanapitapita katika maeneo ya kupigia kura.
3. Siku ya uchaguzi si siku ya kampeni. Hatutaki kuona helikopita za vyama vyote zenye kuashiria kufanya kampeni.
Nawaasa watu wote hasa wale waliotoka nje ya Iringa, sisi huku Iringa tunapenda sana amani kuliko kitu chochote kile hivyo ikiwa wameletwa kama MAJESHI YA KUKODIWA ili kuharibu amani ya Kalenga kama walivyozoea kufanya huko walikotoka, Sisi Polisi na wana Kalenga tupo imara, tumejipanga vizuri kukabiliana nao.
Aidha, napenda kuwatoa hofu wana kalenga, wasiwe na wasiwasi kabisa, sisi Polisi Iringa tupo imara na tumejipanga vizuri katika kuwalinda kikamilifu. Nawaomba wajitokeze kwa wingi sana siku ya kupiga kura na wapige kura zao kwa uhuru kabisa.
Ndugu waandishi, nawashukuru sana kwa jinsi mlivyofanya kazi zenu kwa ueledi mkubwa. Hata siku moja hatujawahi kusikia ama kusoma habari za uchochezi kwa kushabikia chama chochote kile.
AHSANTENI SANA.
0 |
|
0 |
|
Pichani Kati ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Mh.Jaji Mstaafu Damian Lubuva akizungumza mbele ya Waandishi wa habari mapema leo mchana,kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ya Hill Top Hotel,mjini Iringa kuhusiana na ufafanuzi wa Daftari la Kududumu la Wapiga Kura litakalotumika katika Uchaguzi wa Ubunge jimbo la Kalenga,unaotarajiwa kufanyika machi 16 mwaka huu.Jaji Lubuva amebainisha kuwa Tume haijafanya Uboreshaji kwa maana ya kuandikisha Wapiga kura wapya ambao hawakuwa wamejiandikisha kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010.
"Kilichofanyika Mwaka 2014 ni Uhakiki wa Daftari hilo ili kuwa sahihi zaidi na kuhakikisha kila aliyeandikishwa hapo awali na kupewa kadi ya kupigia kura anatumia haki yake ya kupiga kura,hii ni kuondoa malalamiko ya kushindwa kupiga kura kwa sababu ya kukosekana jina lake kwenye Daftari",amesema Jaji Lubuva.Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Mh.Julius Mallaba na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid.
Amesema kuwa kutokana na Uhakiki uliofanyika,ukweli ni kwamba taarifa za wapiga kura zilizohakikiwa zilikuwa 149 tu.Wapiga kura walioongezeka katika Daftari lililotumika katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010 ni saba (7) tu na sio 600 kama ilivyotolewa taarifa kwenye vyombo mbalimbali vya habari
Baadhi ya Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Mh.Jaji Mstaafu Damian Lubuva akitoa ufafanuzi wa Daftari la Kududumu la Wapiga Kura litakalotumika katika Uchaguzi wa Ubunge jimbo la Kalenga,unaotarajiwa kufanyika machi 16 mwaka huu.Jaji Lubuvu amebainisha kuwa Tume haijafanya Uboreshaji kwa maana ya kuandikisha Wapiga kura wapya ambao hawakuwa wamejiandikisha kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010.
0 |
|
0 |
|
![]() |
Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Bw, Yahya Khamis Hamad akiapa mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete Leo Mjini Dodoma. |
![]() |
Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Yahya Khamis Hamad akisaini Kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete Leo Mjini Dodoma. |
![]() |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akisaini kiapo baada ya kumuapisha Katibu bunge Bw. Yahya Khamis Hamad (mbele aliyesimama) |
![]() |
Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Yahya Khamis Hamad akipokea vitabu vya muongozo kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete Leo Mjini Dodoma. |
![]() |
Naibu Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Thomas Kashilila akiapa mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete Leo Mjini Dodoma. |
![]() |
Naibu Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Bw, Thomas Kashilila akisaini Kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete Leo Mjini Dodoma. |
![]() |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akisaini kiapo baada ya kumuapisha Naibu Katibu bunge Maalum la Katiba Bw. Thomas Kashilila (aliyesimama) |
![]() |
Naibu Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Bw, Thomas Kashilila akipokea vitabu ya muongozo kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete Leo Mjini Dodoma. |
![]() |
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akimweleza jambo Naibu Waziri Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Juma Nkamia wakati wa Hafla ya Kuapishwa kwa Katibu na Naibu Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Leo Mjini Dodoma. (PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO)
|
Muungano wa Tanzania kwa miaka 50 umekuwa ni undugu hivyo kuufuta ni sawa na kufuta utaifa wetu na kukaribisha ukabila.
Hayo yamesemwa leo mjini Dodoma, na Kapteni John Chiligati ambaye ni mjumbe aw Bunge Maalum la Katiba wakati wa mahojiano na kipindi cha Jambo kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha TBC One.
Aliendelea kusema kwamba muundo wa kimaisha wa Muungano wetu ni wa serikali mbili, hivyo tusivunje kabisa Muungano huo.
"Kuvunja Muungano ni kukaribisha ukabila na kuchanganya wananchi maana watajitenga kwamba wengine ni Wazanzibar, wengine ni Watanganyika, hivyo ni kurudi nyuma badala ya kusonga mbele" aliongeza Mhesh Chiligati.
Akizungumzia madhara ya serikali tatu Mhesh Chiligati alisema kwamba Serikali tatu italeta utata maana kutakuwa na Serikali ya Tanganyika, Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Muungano. Kwa muundo huo Serikali tatu, serikali ya Muungano haitakuwa na watu, madaraka,utaifa na hata pesa zake.
Akichangia ya kuwa na serikali mbili, Mzee maarufu Mjini Dodoma Jumanne Gombashi alisema kwamba suala la zaidi ya Serikali mbili si tatizo la Watanzania, hivyo tusiwasingizie kwamba wanahitaji serikali tatu , kwani badala ya kutatua matatizo tutaongeza matatizona tutakuwa tunaicha chana nchi yetu.
" Tumekuwa na Serikali mbili kwa miaka 50, kama kuna makosa hatuna budi kujitathmini, na kujisahihisha na kujikosoa ili tutatue matatizo hayo na tuendelee na Serikali mbili.." alisema mzee Gombashi.
Aidha aliendelea kusema kwamba tunapozungumzia serikali tatu tuangalie pia upande wa gharama za uendeshaji wa Serikali hizi. Kila upande yaani Zanzibar na Tanzania Bara utatakiwa kuchangangia uendeshaji wa serikali ya Muungano, na pia tutalazimika kuwa na viongozi watatu, mabaraza ya mawaziri matatu na mabunge matatu.
"Kwa kuwa na serikali tatu hawa watu wote wanahitaji huduma kwa hiyo kwa kufanya hivyo tutapanua matumizi kwa nchi changa kiuchumi kama hii yetu" alisema mzee Gombashi.
Mhesh. Chiligati alitoa ushauri wa kudumisha Muungano,na kuepuka muundo utakaodhoofisha Muungano bali tuhakikishe Muungano unaimarishwa na pande sote mbili.
Naye mzee Gombashi alimalizia kwa kuwahimiza Watanzania kutotetereka na kuburuzwa na watu wasiopenda Muungano, na kwamba iko siku tutafika kwenye serikali moja na tuwe wamoja zaidi.
Hayo yamesemwa leo mjini Dodoma, na Kapteni John Chiligati ambaye ni mjumbe aw Bunge Maalum la Katiba wakati wa mahojiano na kipindi cha Jambo kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha TBC One.
Aliendelea kusema kwamba muundo wa kimaisha wa Muungano wetu ni wa serikali mbili, hivyo tusivunje kabisa Muungano huo.
"Kuvunja Muungano ni kukaribisha ukabila na kuchanganya wananchi maana watajitenga kwamba wengine ni Wazanzibar, wengine ni Watanganyika, hivyo ni kurudi nyuma badala ya kusonga mbele" aliongeza Mhesh Chiligati.
Akizungumzia madhara ya serikali tatu Mhesh Chiligati alisema kwamba Serikali tatu italeta utata maana kutakuwa na Serikali ya Tanganyika, Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Muungano. Kwa muundo huo Serikali tatu, serikali ya Muungano haitakuwa na watu, madaraka,utaifa na hata pesa zake.
Akichangia ya kuwa na serikali mbili, Mzee maarufu Mjini Dodoma Jumanne Gombashi alisema kwamba suala la zaidi ya Serikali mbili si tatizo la Watanzania, hivyo tusiwasingizie kwamba wanahitaji serikali tatu , kwani badala ya kutatua matatizo tutaongeza matatizona tutakuwa tunaicha chana nchi yetu.
" Tumekuwa na Serikali mbili kwa miaka 50, kama kuna makosa hatuna budi kujitathmini, na kujisahihisha na kujikosoa ili tutatue matatizo hayo na tuendelee na Serikali mbili.." alisema mzee Gombashi.
Aidha aliendelea kusema kwamba tunapozungumzia serikali tatu tuangalie pia upande wa gharama za uendeshaji wa Serikali hizi. Kila upande yaani Zanzibar na Tanzania Bara utatakiwa kuchangangia uendeshaji wa serikali ya Muungano, na pia tutalazimika kuwa na viongozi watatu, mabaraza ya mawaziri matatu na mabunge matatu.
"Kwa kuwa na serikali tatu hawa watu wote wanahitaji huduma kwa hiyo kwa kufanya hivyo tutapanua matumizi kwa nchi changa kiuchumi kama hii yetu" alisema mzee Gombashi.
Mhesh. Chiligati alitoa ushauri wa kudumisha Muungano,na kuepuka muundo utakaodhoofisha Muungano bali tuhakikishe Muungano unaimarishwa na pande sote mbili.
Naye mzee Gombashi alimalizia kwa kuwahimiza Watanzania kutotetereka na kuburuzwa na watu wasiopenda Muungano, na kwamba iko siku tutafika kwenye serikali moja na tuwe wamoja zaidi.
Wananchi wa Tanzania wamepongezwa kwa kufikia miaka 50 ya Muungano huku wakiulinda na kuuimarisha mpaka Leo.
Hayo yamesemwa na Balozi Job Lusinde ambaye alikuwa mjumbe wa kamati ya kutayarisha katiba ya Muungano Hivi karibuni Mjini Dodoma.
Balozi Lusinde ambaye pia alikuwa Waziri wa serikali za Mitaa katika Baraza la kwanza la Tanganyika mwaka 1961, baada ya kupata Uhuru amesema kwamba madhumuni ya kuanzisha Muungano huo ilikuwa ni kuonyesha mfano ili siku moja uwepo Umoja wa nchi za Afrika.
"Wakati tunaugana na Zanzibar kulikuwepo upepo wa kuwa na Shirikisho la Afika Mashariki, hivyo ilikuwa rahisi kuanza na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Kama mfano mkubwa wa kimatendo " alisema Balozi Lusinde.
Aliendelea kusema kwamba madhumuni mengine yalikuwa ni kuuimarisha uchumi wa nchi hizi mbili kwani kabla ya Muungano Zanzibar ilikuwa na watu 300 na Tanganyika ilikuwa na watu 8,000,000, hivyo baada ya kufunga na uchumi ukiwa unategemeana na wakaunganisha nguvu kiuchumi , jambo ambalo lilikuwa faida kwa nchi hiyo mbili.
Aidha, Balozi Lusinde alisema kwamba wakati wa kuungana walifikiria suala la usalama wa nchi hizi mbili, kwamba ni muhimu hivyo kwa kuungana kutaweza kuimarisha usalama.
Suala la mwingiliano wa kijamii pia lilichochea kuungana kwa nchi hizi mbili. "kulikuwa na mwingiliano mkubwa awa kijamii kama vile kuoleana, kutembelea a na biashara, hivyo kutokana na Wazanzibar kuishiTanganyika na halikadhalika Watanganyika kuishi Zanzibar, suala la kuungana lilikuwa Kama liko tayari" alisema Balozi Lusinde.
Aliongeza kusema kwamba baada ya Muungano, umoja, usalama na uchumi uliimarika. Balozi Lusinde alisisistiza suala la kuulinda na kuuimarisha Muungano wetu na kushauri changamoto zilizopo zizungumzwe na kutafutiwa ufumbuzi.
Akizungumzia uwepo wa Serikali tatu, Balozi LUsinde alisema Hanoi haja ya kuwepo maana miaka 50, ya Muungano tunaona matunda yake."serikali tatu hazina haja ya kuwepo, kwani zitaleta katika uendeshaji wake, pili serikali hizi zitakuwa na gharama ya uendeshaji wake, na tatu zitawachanganya wananchi" aliongeza Balozi Lusinde.
Balozi Lusinde aliendelea kusema kwamba serikali tatu ni sawa sawa na kuweka gia ya kumrudi nyumbani kwenye gari na kwamba serikali tatu zitatupeleka kwenye uharibifu na kutusambaratisha.
Balozi Lusinde alimalizia kwa kushauri kwamba Muungano wetu usiwekewe kitu chochote cha kuwavuruga Watanzania ili wasivurugike, wasitengane na wasigombane.
0 |
|
0 |
|
Madereva Bajaj wakiwa nje ya ofisi za chadema makao makuu kinondoni wakipinga tamko la kuzuiwa kuingia kati kati ya mji na maeneo ya mjini.
Mmoja wa Madereva Bajaj Akiongea na vyombo vya habari mda huu makao makuu ya chadema kinondoni.
Polisi wakiwa wamefika eneo la tukio mda huu ili kuweza kuweka hali ya usalama na kuzuia vurugu
Waendesha bodaboda na bajaj jijini dar mda huu wameandamana mpaka Ofisi za chadema makao makuu kinondoni,Nia ya maandamano yao hayo ni kupinga tamko linalowataka kutopeleka abiria maeneo yote ya kati kati ya jiji la dar.Mmoja wa madereva hao akiongea na mtandao wetu anasema kwamba wameamua kuandamana mpaka ofisi za chadema kwa kuwa wanaamini ndio watapata msaada.Taarifa kamili na picha zaidi zitakujia inakujia hivi punde.HABARI NA DJ SEK BLOG.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa makabidhiano ya hundi kwa Mshindi wa Promosheni ya Mimi ni Bingwa, aliyejishindia Shilingi Milioni 50, Bw. Kagombo Rashind Jacob (kushoto). Pembeni ni Meneja Masoko wa Airtel , Upendo Nkini.
Meneja Masoko wa Airtel, Upendo Nkini (kushoto) akikabidhi hundi kwa Mshindi wa Promosheni ya Mimi ni Bingwa, aliyejishindia Shilingi Milioni 50, Bw. Kagombo Rashind Jacob (kushoto). Pembeni ni kushoto ni rafiki wa mshindi huyo Antidius Diocresi.
Mshindi wa Promosheni ya Mimi ni Bingwa, aliyejishindia Shilingi Milioni 50, Bw. Kagombo Rashind Jacob (kushoto) akiongea kushukuru kampuni ya Airtel Tanzania kwa kuweza kuanzisha promosheni hiyo ambayo imeweza kumfanya akawa bingwa. Pembeni ni Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando.
============ ========= =========
Airtel yakabidhi milioni 50 kwa mshindi wa promosheni ya MIMI ni Bingwa leo
· Washindi wengine 14 kwenda OLD-TRAFFPORD Uingereza kesho -Ijumaa
Kampuni ya simu za mkononi ya kupitia promosheni yake ya mimi ni bingwa iliyomalizika hivi karibuni imemkabidhi mshindi wake BW, Rashidi Kagombora mkazi wa Bukoba hundi ya shilingi milioni 50 leo katika hafla iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel Dar es salaam
Akiongea wakati wa makabidhiano hayo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema “Airtel tunawashukuru wateja wote walioshiriki kikamilifu katika promosheni yetu ya MIMI NI BINGWA, leo tunamkabidhi bw, Kagombola kitita chake kupitia hundi hii ya mfano na baada ya siku chache pesa zake zitaingia katika akaunti yake ya benki moja kwa moja”
Vilevile tunafuraha kuwatangazia kuwa jumla ya wateja 14 wa Airtel walioshiriki katika promosheni ya MIMI BINGWA wataondoka kesho kwenda nchini Uingereza jiji la Manchester CITY na watapata nafasi ya kushuhudia soka LIVE kati ya Manchester United na Liverpool siku ya jumapili tarehe 16/03/2014 soka litakalochezwa saa 9 na nusu alasiri.
Washindi wa MIMI NI BINGWA wanaotarajiwa kuondoka kesho siku ya ijumaa ni GEOFREY DAVID MSITU, JOSEPH STEVEN MAMBO,SEVERA MORIS MATHIAS, HARRSON WILSON, RAFAEL WAIRES KABENGA, EDMUND HENRY KAGIMBO, AMINIYEU NLILIE NATAI, MAULID BARAKA KITENGE, JOSEPH MOSES NDOSSI, CHARLES JOSEPH BUCHWA, GOODLUCK RICHARD KIMARO, RAHABA EUSEBIUS MVUONI, RAJAB SAID MANGARA, na watasindikizwa na Meneja Masoko wa Airtel Bi UPENDO GILLIARD NKINITunatoa pongezi kwa washindi wote walioibuka na zawadi mbalimbali kupitia promosheni hii iliyodumu kwa muda wa miezi mitatu. Pia tunawapongeza wateja wengine wote walioshiriki katika promosheni lakini hawakushinda ikumbukwe kuwa hii ni bahati nasibu hivyo kila mtu anajishindia kwa bahati yake
Nae mshindi wa Promosheni hiyo Bw, Rashidi Kagombola alisema “ninafurahi sana kuwa mshindi wa mamilioni haya, kwa kweli namshukuru sana mungu kwa kuniwezesha kubadili maisha kwa haraka hivi, leo hii natoa ahadi kwa Airtel na watanzania wenzangu kuwa nitahakikisha nazitumia kwa uangalifu pesa hizi ili kukuza biashara yamgu ya samaki”
Promosheni MIMI BINGWA imekwisha huku jumla ya pesa taslim milioni mia tatu ishirini na nne 324 zikiwa zimekwenda kwa wateja toka mikoa na sehemu mbalimbali, vile vile jumla ya washindi wengine 35 wamepata zawadi ya nafasi yakusafiri na kwenda Uingereza katika jiji la Manchester na watalipiwa kila kitu ikiwa ni pamoja na gharama za malazi, usafiri, pamoja na gharama zote za kuandaa safari hadi kupatikana kwa hati ya kusafiria na VISA ya kwenda Uingereza na kushuhudia SOKA katika kiwanja cha OLD Traford cha Mabingwa watetezi wa ligi ya Uingereza.
· Washindi wengine 14 kwenda OLD-TRAFFPORD Uingereza kesho -Ijumaa
Kampuni ya simu za mkononi ya kupitia promosheni yake ya mimi ni bingwa iliyomalizika hivi karibuni imemkabidhi mshindi wake BW, Rashidi Kagombora mkazi wa Bukoba hundi ya shilingi milioni 50 leo katika hafla iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel Dar es salaam
Akiongea wakati wa makabidhiano hayo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema “Airtel tunawashukuru wateja wote walioshiriki kikamilifu katika promosheni yetu ya MIMI NI BINGWA, leo tunamkabidhi bw, Kagombola kitita chake kupitia hundi hii ya mfano na baada ya siku chache pesa zake zitaingia katika akaunti yake ya benki moja kwa moja”
Vilevile tunafuraha kuwatangazia kuwa jumla ya wateja 14 wa Airtel walioshiriki katika promosheni ya MIMI BINGWA wataondoka kesho kwenda nchini Uingereza jiji la Manchester CITY na watapata nafasi ya kushuhudia soka LIVE kati ya Manchester United na Liverpool siku ya jumapili tarehe 16/03/2014 soka litakalochezwa saa 9 na nusu alasiri.
Washindi wa MIMI NI BINGWA wanaotarajiwa kuondoka kesho siku ya ijumaa ni GEOFREY DAVID MSITU, JOSEPH STEVEN MAMBO,SEVERA MORIS MATHIAS, HARRSON WILSON, RAFAEL WAIRES KABENGA, EDMUND HENRY KAGIMBO, AMINIYEU NLILIE NATAI, MAULID BARAKA KITENGE, JOSEPH MOSES NDOSSI, CHARLES JOSEPH BUCHWA, GOODLUCK RICHARD KIMARO, RAHABA EUSEBIUS MVUONI, RAJAB SAID MANGARA, na watasindikizwa na Meneja Masoko wa Airtel Bi UPENDO GILLIARD NKINITunatoa pongezi kwa washindi wote walioibuka na zawadi mbalimbali kupitia promosheni hii iliyodumu kwa muda wa miezi mitatu. Pia tunawapongeza wateja wengine wote walioshiriki katika promosheni lakini hawakushinda ikumbukwe kuwa hii ni bahati nasibu hivyo kila mtu anajishindia kwa bahati yake
Nae mshindi wa Promosheni hiyo Bw, Rashidi Kagombola alisema “ninafurahi sana kuwa mshindi wa mamilioni haya, kwa kweli namshukuru sana mungu kwa kuniwezesha kubadili maisha kwa haraka hivi, leo hii natoa ahadi kwa Airtel na watanzania wenzangu kuwa nitahakikisha nazitumia kwa uangalifu pesa hizi ili kukuza biashara yamgu ya samaki”
Promosheni MIMI BINGWA imekwisha huku jumla ya pesa taslim milioni mia tatu ishirini na nne 324 zikiwa zimekwenda kwa wateja toka mikoa na sehemu mbalimbali, vile vile jumla ya washindi wengine 35 wamepata zawadi ya nafasi yakusafiri na kwenda Uingereza katika jiji la Manchester na watalipiwa kila kitu ikiwa ni pamoja na gharama za malazi, usafiri, pamoja na gharama zote za kuandaa safari hadi kupatikana kwa hati ya kusafiria na VISA ya kwenda Uingereza na kushuhudia SOKA katika kiwanja cha OLD Traford cha Mabingwa watetezi wa ligi ya Uingereza.
Wafanybiashara na Wachimbaji waliowakilisha wenzao katika Maonesho ya 53 ya Bangkok Gems and Jewelry Fair’ wakiwasikiliza wageni waliotembelea banda la Tanzania kuona aina mbali mbali za madini ya Vito na Usonara yaliyowasilishwa katika maonesho hayo.
Mthamini wa madini kutoka idara ya Uthamini wa madini ya Almas (TANSORT) Bw. Edward Rweymamu (katikati), akiwaeleza jambo wageni waliotembelea banda la Tanzania katika maonesho hayo. Wanaoshuhudia wa kwanza kushoto ni Mratibu kutoka Kituo cha ‘Tanzania Geomological Center’ (TGC), Bw. Musa Shanyangi na wa kwanza kulia ni Mthamini wa Madini kutoka Idara ya uthamini madini ya almsi (TANSORT), Wizara ya Nishati na Madini Bibi. Teddy Goliama.
Mwandishi wa habari hii (Kushoto) Asteria Muhozya, akifanya mahojiano na wafanyabiashara wa madini walioshiriki maonesho ya Vito na Usonara ili kutaka kujua namna walivyofaidika na ushiriki wao katika maonesho hayo. Anayeongea ni Bw. Jeremiah Simioni Mfanyabiashara kutoka Kampuni ya Tom Gems na katikati ni Mfanyabiashara Mhe. Dorah Mushi kutoka Kampuni ya H.B Mining Company.
========== ======== ======
========= ======== ======
Wafanyabiashara na wachimbaji Tanzania walifikia soko la madini Kimataifa.
Na Asteria Muhozya, Bangkok
Wafanyabiashara na wachimbaji wa madini Tanzania wameelezea kufurahishwa na ushiriki wao katika maonesho ya 53 ya madini ya vito na usonara, Bangkok, kutokana na kupata fursa ya kulifikia soko la madini kimataifa.
“Wachimbaji wa madini ya vito na usonara, watarajie kupata masoko ya madini yao nje. Wananunuzi wa bidhaa zetu wapo na wana imani kubwa na madini yetu. Jambo kubwa tulilolihitaji ilikuwa kujua masoko na namna ya kupata taarifa mbalimbali. Tunafurahi kwa hilo, tumefanikiwa. Amesema Mwenyekiti wa Kamati ya Madini ya Vito Tanzania, Bw. Gregory Kibusi.
Aidha, Aliongeza kuwa, ushiriki wake katika maonesho hayo, umewawezesha kupata sehemu ambazo zitawasaidia wachimbaji kupata taarifa mbalimbali, ikiwemo taarifa za bei za madini hali ambayo itawawezesha kupata taarifa sahihi tofauti na awali, ambapo walikuwa wakizipata kutoka vyanzo visivyo rasmi. Hivyo, amewataka wachimbaji kufanya maandalizi mazuri kwa ajili ya maonesho ya madini ya vito na usonara yanayofanyika kila mwaka jijini Arusha.
Akizungumzia namna alivyonufaika na maonesho hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya madini ya H.B Bw. Harry Mushi, alieleza kuwa, maonesho hayo, yamewasaidia kujua nafasi zao kibiashara. Vilevile, ameongeza kuwa, maonesho hayo yamewasaidia kujua aina za madini zinazotakiwa kuwasilishwa kwenye maonesho ya kimataifa, na umuhimu wa kuzingatia ubora wa madini.
“Tumegundua wafanyabiashara wa madini Tanzania tunahitaji kujipanga ili kuliteka soko la kimataifa. Tumejifunza umuhimu wa kukata madini. Madini tunayo na ni bora sana. Wachimbaji wanatakiwa kuyaongezea thamani madini yao. Jambo hili ni muhimu sana, tunahitaji kujipanga.” Ameongeza Mushi.
Kwa upande wake mfanyabiashara wa madini kutoka kampuni ya H.B Mining, Mhe. Dorah Mushi, alieleza kuwa, ipo haja kwa Watanzania kuinuka kutokana na ukweli kwamba, Tanzania inayo hazina kubwa ya madini ya aina mbalimbali takriban katika kila Mkoa kutokana na kwamba, maonesho ni njia mojawapo ya kusaidia kujenga mtandao wa kibiashara.
Aidha, ameiomba Serikali kuwasaidia wananawake walioko katika sekta ya uzalishaji wa madini ili waweze kufahamu fursa zilizopo na kujua namna ya kuzitumia. Ameongeza kuwa, wapo wanawake wengi katika sekta hiyo ambao wameshindwa kufaidika na sekta hiyo kutokana na ukosefu wa elimu.
“Madini ni maisha, ni biashara, ni ajira. Kina mama litambueni hili, jiingizeni katika sekta hii soko la kimataifa lipo. Nimeshiriki hapa Bangkok kwa mara ya kwanza Sitaki kukosa tena maonesho kama haya. Nimejifunza mengi ikiwemo namna ya kuuza madini. Serikali wasaidieni wadau wa madini , hasa kina mama , wafumbueni macho”. Amesema Mhe. Dora Mushi.
Wakati huo huo, mfanyabiashara wa madini na Afisa Masoko wa kampuni ya Tom Gems, Bw. Jeremiah Simioni, aliishukuru Serikali ya Tanzania kutokana na kuwa na uhusiano mzuri na nchi ya Thailand kutokana na kwamba, ushiriki wao katika maonesho hayo, umewafungulia mipaka ya ufahamu kuhusiana na biashara ya madini ya vito na usonara katika ngazi za kimataifa.
“Nataka kuwa balozi kwa wenzangu baada ya kushiriki maonesho haya. Nataka kuwaambia wenzangu fursa zilizopo kimataifa na namna wanavyopaswa kuzitumia. Naishukuru sana Wizara na idara ya uthamini wa madini ya almas TANSORT kwa kufanikisha ushiriki wetu lakini bado naiomba Serikali iendelee kutoa mafunzo mbalimbali kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini”. Aliongeza Jeremiah.
Akizungumzia ushiriki wa Tanzania katika maonesho hayo, Kamishna Msaidizi wa Madini, Mhandisi Hamis Komba, alieleza kuwa, Serikali ina mengi iliyojifunza kutokana na ushiriki wake katika maonesho hayo ikiwemo matumizi ya teknolojia zinazotumika katika sekta hiyo.
Aliongeza kuwa, watanzania wakiwemo wafanyabiashara na wachimbaji wanatakiwa kuwa na uthubutu ili waweze kuleta mapinduzi na mabadiliko katika sekta hiyo, hali ambayo itawasaidia kuendana na biashara za nje ikiwemo pia ushindani wa kimataifa.
Aidha, alieleza kuwa, uwezo wa kuibadilisha Tanzania kupitia sekta ya madini upo hivyo, amewataka wadau wote kila mmoja atekeleze wajibu wake kikamilifu.
“Tunatakiwa kujipanga, kwa mfano kwenye usonara kuna mengi, tunahitaji kuufikisha usonara katika ngazi za kimataifa kuanzia teknolojia. Kila mdau analo jukumu, wafanyabiashara na wachimbaji kuweni na uthubutu, wataalamu nyanyukeni muisaidie Serikali”. Amesema Komba.
Akizungumzia kuhusu uthamini wa madini ya vito na almas katika maonesho hayo, mthamini wa madini kutoka idara ya uthamini wa madini ya almas TANSORT Bw. Edward Rweymamu alieleza kuwa, idara ya uthamini imeyatumia maonesho hayo kutafiti mwenendo wa bei za madini jambo ambalo litawasaidia kuifanyia marekebisho kanzidata ya bei ili kuhakikisha wanapata mrahaba stahiki.
Ameongeza kuwa, si kwa wafanyabiashara na wachimbaji pekee ambao wamenufaika na maonesho hayo bali hata nchi ya Tanzania kutokana na idadi kubwa ya wageni waliotembelea banda la Tanzania kutafuta madini mbalimbali yakiwemo madini ya Tanzanite, Ruby, Saphire na Almas, yakiwemo pia madini ya viwandani hali ambayo inaashiria kukubalika kwa madini ya Tanzania katika soko la Kimataifa.
Katika hatua nyingine, wafanyabiashara na wachimbaji waliipongeza Serikali na Wizara ya Nishati na Madini kupitia Kitengo cha Uthamini wa madini ya Almas (TANSORT) kwa kuratibu na kufanikisha ushiriki wa Tanzania kwa mara ya kwanza katika maonesho hayo ambayo yamewasaidia kufungua mipaka ya kibiashara.
0 |
|
0 |
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, Julian Ilunga, wa Shule ya Sekondari Kitangili Mwanza, aliyeibuka mshindi wa kwanza katika shindano la ‘Junior Mathematics Contest 2013’ wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Pai Tanzania, zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Machi 14, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadiHaji Hassan, wa Shule ya Sekondari Feza Boys ya Jijini Dar es Salaam, aliyeibuka mshindi wa pili katika shindano la ‘Junior Mathematics Contest 2013’ wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Pai Tanzania, zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Machi 14, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, Pelucy John, wa Shule ya Sekondari Nganza Mwanza, aliyeibuka mshindi wa kwanza kwa wasichana katika shindano la ‘Senior Mathematics Contest 2013’ wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Pai Tanzania, zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Machi 14, 2014
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Uhuru Wasichana wakitoa burudani ya kwaya wakati wa sherehe hizo Mnazi Mmoja leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia moja ya vitabu wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya Pai Tanzania, leo kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Umoja ya Kiwalani, jijini Dar es Salaam, wakitoa burudani ya ngoma w Makhirikhiri, wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya Pai Tanzania, zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja leo Machi 14, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kuagana na baadhi ya wanafunzi , wakati akiondoka kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, baada ya kuhitimisha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Pai Tanzania.
Sehemu ya Wanafunzi na Waalimu, wakipita mbele ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiwa na mabango yenye ujumbe kuhusiana na Sherehe za maadhimisho ya Siku ya Pai Tanzania, zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Machi 14, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia moja ya vitabu wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya Pai Tanzania, leo kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya uchapishaji Vitabu ya GDY Publications Co. Ltd, Gabriel Kitua.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wanafunzi waliofanya vizuri katika shindano la ‘Senior & Junior Mathematics Contest 2013’, baada ya kuwakabidhi zawadi zao, wkati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Pai Tanzania. Picha na OMR
KISHAKILENA Reality TV Show
LikeBrothaz Production
KISHAKILENA Reality TV Show is geared towards exploring the complexity of life particularly when beautiful girls referred to as ‘Kishakilena’ come under one roof. Though they share cultural heritage they have different personalities that set out serious life dramas.
Episode‐#1 establishes the show’s characters by zeroing in on; Jestina, CoCo Diva, Kim, Nusrat and Linda the four complex personalities.
JESTINA, an educated and iron lady, cannot stand crazy ideas of her mates particularly on men of their dreams. She gets wild when CoCo DIVA, the crazy party girl, tries to insinuate evil minds to the youngest girl LINDA.
CoCo Diva is highly threatened by the natural beauty of sexy KIM. She Cannot also stand NUSRAT, the eldest among them all who has brilliant ideas but fails to execute them. The serious back rash between CoCo Diva and Nusrat steers up the mood of the house.
Can the youngest, funny, sexy, music lover and model‐dreamer Linda stand the peer pressure?
Enjoy first episode below:
![]() |
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Samwel Sitta akila kiapo mbele ya Katibu wa Bunge hilo Bw. Yahya Khamis Hamad, wakati wa hafla ya kuwaapisha wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba leo Mjini Dodoma.Kulia ni Naibu Katibu wa Bunge Hilo Thomas Kashilila. |
![]() |
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samia Suluhu Hassan akila kiapo mbele ya Naibu Katibu wa Bunge Hilo Thomas Kashilila, wakati wa hafla ya kuwaapisha wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba leo Mjini Dodoma.Kulia ni Katibu wa Bunge Hilo Yahya Khamis Hamad. |
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye ni Mwanasheria Mkuu FrederickWerema akitoa hoja wakati wa hafla ya kuwaapisha wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba leo Mjini Dodoma. |
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na aliyekuwa Mwenyekiti wa Muda wa Bunge hilo Pandu Ameir Kificho akila kiapo cha kuwa Mjumbe wa Bunge Hilo Mbele ya Mwenyekiti wa Bunge Hilo Samwel Sitta |
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda akila kiapo cha kuwa Mjumbe wa Bunge Hilo Mbele ya Mwenyekiti wa Bunge Hilo Samwel Sitta |
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Edward Lowassa akila kiapo cha kuwa Mjumbe wa Bunge Hilo Mbele ya Mwenyekiti wa Bunge Hilo Samwel Sitta |
0 |
|
0 |
|
Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) Prof. Ali Seif Mshimba akitoa nasaha kwa wajumbe wa Kamati za kitalaamu na Divishen za undaji wa Viwango vya Taasisi ya Viwango Zanzibar pamoja na kumkaribisha mgeni rasmin.
Katibu Mkuu Wizara Biashara, Viwanda na Masoko Julian B. Raphael akizindua kamati za kitalaamu na Divishen za undaji wa Viwango vya Taasisi ya Viwango Zanzibar katika hafla iliyofanyika Grand Palace Hotel Mjini Zanzibar (kulia) Prof. Ali Seif Mshimba na (kushoto) ni Naibu Katibu Mkuu Wizara Biashara, Viwanda na Masoko Rashid Ali Salu.
Mkufunzi kutoka (TBS) Bw. Nickonia Mwabuka aliesimama akitoa elimu juu muundo upatikanaji wa viwango kwa tasisi kusika katika hafla iliyofanyika Grand Palace Hotel Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati za kitalaamu na Divishen za undaji wa Viwango vya Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) wakimskiliza Mkufunzi kutoka (TBS) Bw. Nickonia Mwabuka hayupo pichani alipokua akitoa maelezo kuhusu muundo upatikanaji wa viwango kwa tasisi kusika.