Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 245 | 246 | (Page 247) | 248 | 249 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba,ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Urambo Mashariki,Mh Samwel Sitta ameibuka kinara kwenye nafasi aliyowania ya kuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba mara baada kumbwaga mpinzani wake,Wakili wa Kujitengemea Ndugu Hashim Rungwe,Sitta anaibuka kinara na kuichukua nafasi hiyo ya kuwa Mwenyekiti wa Kudumu wa Bunge hilo Maalum la Katiba kufuatia Mwenyekiti wake wa Muda,Mh Ameir Pandu Kificho,ambaye mda wake wa kuliendesha bunge hilo unakoma leo. 

  Jumla ya Kura zilizopigwa ni 563 na zilizoharibika ni 7,kufuatia idadi hiyo ya Kura Ndugu Hashim Rungwe amepata kura 69 na Mh.Samwel Sitta ameibuka na kura 487,kwa Matokeo hayo imetangazwa kuwa Mh.Samwel Sitta ndiyo mshindi.

  0 0

  )


  0 0

   Timu ya mafundi ya ukarabati na upanuzi wa mitambo ya Ruvu Juu wakiwa kazini katika Ofisi ya Mitambo hiyo, mkoani Pwani.

   Kaimu Meneja wa Mtambo wa Ruvu Juu, Mhandisi Deusdedit Rwegasira (Aliyevaa fulana la mistari) akiwaonesha Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango video ya namna miundombinu ya maji inavohujumiwa na baadhi wananchi wasiofuata taratibu zilizowekwa za kwa kujiunganishia maji kiholela.

   Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikikagua maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa mitambo ya Ruvu Juu ilipofanya ziara ya ukaguzi katika Mtambo huo uliopo mkoa wa Pwani.

   Meneja wa Mtambo wa Ruvu Chini, Mhandisi Emmanuel Makusa (Kushoto) akiwaonesha Wataalamu wa Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango mashine nne mpya zilifungwa na Serikali hivi karibuni walipofanya ziara ya ukaguzi katika Mtambo huo uliopo mkoa wa Pwani.

   Viongozi wa msafara wa wataalam wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Bibi Florence Mwanri (Wapili Kushoto) na Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla), Prof. Longinus Rutasitara (Watatu Kulia) wakionesha eneo la kusafishia maji katika Mtambo wa Ruvu Chini walipokuwa katika ukaguzi wa mtambo huo. Kushoto ni Mratibu wa ziara hiyo, Bibi Salome Kingdom.

   Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikikagua bomba lenye uwezo wa kusafirisha lita milioni 360 za maji kwa siku wakati walipokuwa kwenye ukaguzi wa  mitambo ya Ruvu Chini. Anayewaonesha ni Meneja wa Mtambo wa Ruvu Chini, Mhandisi Emmanuel Makusa (Wapili Kulia).

   Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Mtambo wa Ruvu Chini, Mhandisi Emmanuel Makusa (Watatu kushoto) kwenye lenye uwezo wa kusafirisha lita milioni 360 za maji kwa siku wakati walipokuwa kwenye ukaguzi wa  mitambo ya Ruvu Chini.

  Mafundi wakiendelea kulaza mabomba yatakayotumika kusafirishia maji kutoka Mitambo ya Maji ya Ruvu Chini mpaka kwenye Tanki la kuhifadhia maji lililopo Chuo Kikuu cha Ardhi jijini Dar es Salaam. Mpaka sasa mafundi hao wameshasambaza mabomba kwa umbali wa kilomita takribani 29 kati ya kilomita 55. Kazi hii inatarajiwa kukamilika mwezi Juni, mwaka huu.


  Picha na Saidi Mkabakuli


  0 0

    Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu (kulia) akibonyeza kitufe cha kampyuta kama ishara ya kuzindua rasmi  bidhaa  mpya kwa wateja wao ya NBC Direct,  jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni maofisa wa beni hiyo wa pili kushoto ni, Sarah Laiser-Sumaye, Mary Kapeja, Andrew Massawe na, Mussa Jallow.
   Mkuu wa Hduma Rejareja za Kibenki, Mussa Jallow akizungumza na wateja na waalikwa wengine katika uzinduzi huo akieleza faida mbalimbali zinazopatikana katika bidhaa ya NBC Direct.
   Baadhi ya maofisa wa NBC na wageni wengine waliohudhuria hafla ya uzinduzi hnuo jijini Dar es Salaam jana.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu (kulia) akisamiliama na baadhi ya wagewnzi walihudhuria hafla ya uzinduzi wa NBC Direct  jijini jana. 

  0 0

   Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Bw. Steve Kilindo (wa tatu kushoto), akiwaelekeza jambo wadau kutoka  Shirikisho la wenye viwanda Tanzania (CTI), waliofanya ziara maalumu kiwandani hapo juzi, kuangalia jinsi kampuni hiyo ilivyofanikiwa na kuzalisha na kulinda mazingira (wa nne kushoto) ni Mkurugenzi wa Sera na Ushawishi, Bw. Hussein Kamote mkuu wa msafara na Meneja Uendelezaji Biashara, Bw Hassan Chamshama (wa sita). (Na Mpigapicha Wetu)

   Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bi. Doris Malulu (aliyesimama), akikabidhi zawadi kwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Shirikisho la wenye viwanda Tanzania (CTI), Bi Lilian Manga, baada ya wadau kutoka shirikisho hilo kufanya ziara kiwandani hapo kuangalia jinsi TBL ilivyofanikiwa kuzalisha vinywaji bora bila kuharibu mazingira.
   Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Bw. Steve Kilindo (kulia), akizungumza na wadau kutoka  Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI), waliofanya ziara maalumu juzi kiwandani hapo kuangalia jinsi kampuni hiyo ilivyofanikiwa kuzalisha vinywaji na kulinda mazingira. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Bi. Lilian Manga, Mkurugenzi wa Machapisho na Habari, Bw. Thomas Kimbunga, Bw. Jesper Friis na Meneja Uendelezaji Biashara, Bw Hassan Chamshama. (Na Mpigapicha Wetu)
   Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Bw. Steve Kilindo (kulia), akizungumza na wadau kutoka  Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI), waliofanya ziara maalumu juzi kiwandani hapo kuangalia jinsi kampuni hiyo ilivyofanikiwa kuzalisha vinywaji na kulinda mazingira. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Bi. Lilian Manga, Mkurugenzi wa Machapisho na Habari, Bw. Thomas Kimbunga, Bw. Jesper Friis na Meneja Uendelezaji Biashara, Bw Hassan Chamshama. (Na Mpigapicha Wetu)


  0 0

  Balozi in VOA 027Mkuu wa idhaa ya Kiswahili ya VOA Mwamoyo Hamza akiwa na Mh.balozi wa Tanzania Washington Dc na Mexico Liberata Mula mula alipotembelea idhaa hiyo Jumatano Machi 12, 2014. Balozi in VOA 001Kushoto Mkamiti Kibayasi, akiwa na Mh.balozi Liberata Mula mula na Khadija Riyami katika ofisi za idhaa ya Kiswahili ya VOA. Balozi in VOA 007Mh.balozi Liberata Mula mula akijibu maswali katika mahojiano maalum na Idhaa ya Kiswahili ya VOA. Balozi in VOA 008Khadija Riyami akimhoji balozi Mula mula. Balozi in VOA 003Sunday Shomari na Mh.balozi Mula mula na Khadija Riyami. Balozi in VOA 021Mh.balozi Mula mula na Prodyuza wa VOA Duane Collins. Balozi in VOA 032Mtangazaji maarufu wa "Straight Talk Afrika" VOA-TV Shaka Ssali akiagana na Mh.balozi baada ya mahojiano yake aliyofanya kwa upande wa radio na TV huku akisindikizwa na Khadija Riyami,Mwamoyo Hamza na Mkamiti Kibayasi.

  0 0

  Kina Mama wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakimsindikiza Mjumbe wa Bunge Hilo na Mgombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Bi. Samia Suluhu Hassan(Aliyenyanyua fomu)kurudisha fomu kwa Katibu wa Bunge Mapema Leo asubuhi Mjini Dodoma.
  Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Thomas Kashilila akitoa maelekezo kwa wapambe wa mgombea Nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba kabla ya kupokea Fomu hizo Mapema Leo asubuhi Mjini Dodoma.
  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Bi. Samia Suluhu akizipitia Fomu kabla ya Kuzikabidhi kwa Katibu wa Bunge tayari kwa uchaguzi utakaofanyika joini ya leo Mjini Dodoma.
  Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Thomas Kashilila akisaini fomu za mgombea Nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mapema Leo asubuhi Mjini Dodoma.
  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Bi. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi fomu Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Thomas Kashilila (Kulia) Mapema Leo asubuhi Mjini Dodoma.
  Kina Mama wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakiimba kwa furaha baada ya fomu za Mgombea wa Nafasi ya Makamu Mwenyekiti Samia Suluhu Hassan Mapema Leo asubuhi Mjini Dodoma.
  (PICHA NA HASSAN SILAYO- MAELEZO, DODOMA)

  0 0

  Mr. Enoch Osei-Safo Managing Director Ecobank Tanzania adressing invited guests at the China Direct initiative launch
  Mr. Bertrand Jandoh,Regional Account Manager & Acting Head of Corporate Banking at Ecobank Tanzania adressing guests at the China Direct initiative launch.
  Deputy Managing Director Bank of China-Zambia giving a speech at the China Direct initiative launch by Ecobank-Tanzania.
  Mr.Enoch Osei-Safo introducing Ms.Wenzai Dai the Chinese liaison officer at the Ecobank Tanzania China Desk.
  Deputy Managing Director Bank of China-Zambia (right),Assistant Manager of Banking BOC-Zambia,Ms.Wang Hao interacting with members of the Chinese business community in Tanzania.


  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Novatus Makunga (watatu kushoto) akipokea msaada wa mabati yenye thamani ya shilingi Milioni 5 kutoka kwa Mkurugenzi wa Kiwanda cha Mega Trade Investiment ya jijini Arusha, Gudluck Kway
    Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Novatus Makunga (watatu kushoto) akipokea msaada wa mabati yenye thamani ya shilingi Milioni 5 kutoka kwa Meneja Mauzo wa Kanda ya Kaskazini  wa Kampuni ya  Mega Trade Investiment ya jijini Arusha, Edmund Rrutaraka, kwaajili ya kusaidia waathirika wa kipunga katika Kijiji cha Kwatito. Katikati yao ni Mkurugenzi wa Masoko wa Mega Trade, Gudluck Kway na wafanyakazi wengine.


  0 0

  Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Gaudensia Simwanza akizungumza na wanahaabari (hawapo pichani) kuhusu vipodozi vilivyopigwa marufuku na mamlaka hiyo.Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari(MAELEZO) Frank Mvungi.
  Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Gaudensia Simwanza, akionesha moja ya vipodozi vilivyopigwa marufuku na mamalaka hiyo kinachotumiwa na wanawake kukuza makalio.
  Baadhi ya vipodozi vilivyopigwa marufuku na Mamalaka ya Chakula na Dawa (TFDA).
  Baadhi ya wanahabari wakimsikiliza Afisa Uhusiano wa Mamalaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Gaudensia Simwanza (hawapo pichani). Picha na Hussein Makame-MAELEZO.

  Frank Mvungi-Maelezo

  MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) imeteketeza vipodozi visivyofaa kwa matumizi ya binadamu vyenye thamani ya takribani Shilingi Milioni 188 katika kipindi cha mwaka 2012/2013.

  Hayo yamesemwa na Afisa Uhusiano wa mamlaka hiyo, Gaudensia Simwanza wakati akizunguza na wanahabari kwenye mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

  Alisema TFDA imeweka mfumo thabiti wa udhibiti wa vipodozi ambao unatumia njia mbalimbali ambazo ni pamoja na usajili wa vipodozi, utoaji wa vibali vya biashara ya bidhaa husika na ukaguzi wa majengo ya vipodozi.

  Simwanza aliongeza kuwa hatua nyingine ni ufuatiliaji wa vipodozi katika soko ili kujiridhisha kuwa vina ubora na usalama unaotakiwa kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa.

  Alibainisha kuwa vipodozi ambavyo havifai kwa matumizi ya binadamu vina madhara kama vile kusababisha kupata mzio wa ngozi, kusababisha ugonjwa wa ngozi kwa mtumiaji.

  “Matumizi ya vipodozi vyenye viambata vya zebaki (mercury) kwa mama wajawazito huathiri mtoto tumboni hali inayoweza kusababisha madhara makubwa kwa mtoto atakayezaliwa.

  Alifafanua zaidi kuwa viambato kama Zirconium na Vinyl Chloride husababisha kansa ya ngozi na mapafu kwa mtumiaji wa vipodozi vyenye kemikali.

  Simwanza alitoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari kwa kuacha matumizi ya vipodozi vyenye viambata vyenye sumu na kemikali.

  TFDA imekuwa ikifanya operesheni na ukaguzi wa vipodizi katika maduka mbalimbali yanayouza bidhaa hizo na kukamata bidhaa zisizofaa kwa matumizi ya binadamu na kuziteketeza kwa mujibu wa sheria.

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwalile (kulia) kwa niaba ya serikali ya Tanzania akikabidhiana hati walizosainiana na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Maendeleo na Ushirikiano Peter Moors (kushoto) kwa niaba ya serikali ya Ubelgiji hivi karibuni jijini Dar es salaam.
  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwalile (kulia) akisaini mkataba wa msaada ambao serikali ya Ubelgiji imetoa Euro milioni 20 sawa na sh.bilioni 40 za Kitanzania kuisaidia Tanzania. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Maendeleo na Ushirikiano Peter Moors akimwakilisha Waziri wa Ushirikiano kwa niaba ya Serikali ya Ubelgiji hivi karibuni jijini Dar es salaam.
  Baadhi ya wageni na waandishi wa habari waliohudhuria hafla ya kusaini mkataba wa serikali ya Ubelgiji kuisadia Tanzania Euro milioni 20 sawa na sh.bilioni 40 hivi karibuni jijini Dar es salaam.
  Miongoni mwa wageni waliohudhuria hafla ya kusaini mkataba wa serikali ya Ubelgiji kuisadia Tanzania Euro milioni 20 sawa na sh.bilioni 40 hivi karibuni jijini Dar es salaam. (Picha zote na Eleuteri Mangi - MAELEZO) 

  0 0

  Mkurugenzi wa Masoko Na Mahusiano Kutoka  Dhamana ya Uwekezaji  Tanzania Bwana Daudi Mbaga Akitoa Mada Kuhusu Kuwekeza kwenye Mifuko Iliyo chini ya Dhamana ya Uwekezaji Tanzania Kwajili ya Maisha Mara Baada ya Kustaafu kwenye Semina ya Wafanyakazi wanaokaribia Kustaafu Iliyoandaliwa na TAGLA Mkoani Morogoro.

  Washiriki wa Semina ya Wanaokaribia Kustaafu Wakifuatilia Kwa Makini Mada Iliyokuwa Ikitolewa Kuhusu Uwekezaji katika Mfuko wa Jikimu Iliyokuwa Inatolewa Na Mkurugenzi wa Masoko  Ndugu Daudi mBAGA (hayupo Pichani)Kutoka Dhamana ya Uwekezaji Tanzania Inayoendelea Mkoani Morogoro

  Mmoja wa Washiriki wa Semina Hiyo aAkiuliza Swali kuhusu Uwekezaji katika Mfuko wa Jikumu.

  Watanzania Wameshauriwa Kuwekeza kwenye Mifuko Iliyo Chini ya Dhamana ya Uwekezaji Tanzania Kwa Lengo la Kuwekeza kwajili ya Maisha mara Baada ya Kusataafu.Wito Huo Umetolewa  na Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano Kutoka Dhamana ya uwekezaji Tanzania Bwana Daudi Mbaga Wakati Akitoa Mada Kwenye Semina ya wafanyakazi Wanaokaribia Kustafu Inayoendelea Mkoani Morogoro.

  Alisema Kwamba Watanzania Wengi huwa hawajui Nini Cha Kufanya Pindi Wanapostaafu Hali Inayosababisha Watanzania Wanapostaafu wakishapokea Mafao Yao wanajaribu Kufanya Kila Shuguli Mbalimbali Lakini Kutokana na kutokuwa na Uzoefu wa Shuguli Hizo shuguli  nyingi hazidumu.

  Bw Mbaga Amewashauri Watanzania  hasa Wale wafanyakazi wanaokaribia Kustaafu Kuwekeza  Mifuko iliyopo Chini ya Dhamana ya Uwekezaji Tanzania Kama MFUKO WA JIKIMU Wenye "Kauli Mbiu Ishi Vizuri Unastahili". Kwa Lengo la Kuwasaidia Wastaafu Ili Kuondokana na Kupata Hasara na Kufurahia Maisha Zaidi Mara Baada ya Kustaafu.

  Ameongeza Ni vizuri kwa watanzania kuwekeza katika Mfuko Huo kwa kuwa Upo Chini ya taasisi ya Serikali  na uwekezaji wao ni wa Uhakika.Pia Kuwekeza Katika Mfuko Huu watanzania watapata Faida Nyingi kwani Mfuko Huu Unaendeshwa Kitaalamu na Wataalamu Waliobobea Katika Msawala ya Uwekezaji ,Urahisi wa  wawekezaji wanaweza kufuatilia Maendeleo ya Masoko ya FedhaKwa Kufuatilia Mandeleo ya Mifuko.

  Mkurugenzi alisema Uwekezaji katika Mfuko Huo ni wa Uhakika kwasababu Unampa Mwekezaji Unafu wa Gharama za Uwekezaji, Uwazi ,Faida Nzuri,Urahisi wa Kujiunga katika Mfuko Huu.
  Mkurugenzi Mwandamizi wa Masoko na Mahusiano Kutoka Dhamana ya Uwekezaji Tanzania Bi Martha Mashiku Akieleza Faida za Kuwekeza Katika Mifuko iliyo chini ya Dhamana ya Uwekezaji Tanzania.Bi Martha Liwashauri Watanzania Kjiunga katiaka Mifuko Umoja Fund,Wekeza Maisha,Mfuko wa Watoto,Mfuko wa Jikimu,Na Ukwasi.
  Mkurugenzi wa Masoko  Mahusiano Kutoka Dhamana ya Uwekezaji Tanzania Bwana Daudi Mbaga.  0 0

   The IPTL company secretary and the chief counsel, Joseph Makandege
  (right) displays document at a press conference in Dar es salaam, with him
  is the Executive chairman, Harbinder Singh Sethi - who owns IPTL via a
  holding company known as Pan African Power Solutions Tanzania Limited (PAP).

   Executive chairman, Harbinder Singh Sethi - who owns IPTL via a
  holding company known as Pan African Power Solutions Tanzania Limited (PAP)
  speaking to journalists..

  ========  ========  ==========

  IPTL TAKE OVER WAS A CLEAN DEAL

  Executive chairman, Harbinder Singh Sethi - who owns IPTL via a holding
  company known as Pan African Power Solutions Tanzania Limited (PAP) ­ denied
  any wrongdoing in the deal on Tuesday, saying he followed all the legal and
  regulatory procedures in the process.

  ³I followed all the procedures....I did not come to Tanzania to make
  money....I want to help Tanzania to get enough electricity that is vital in
  economic development,² he told a section of journalists in Dar es Salaam.

  Mr Sethi puts the amount that was/is in the escrow account at about Sh150
  billion, noting however that there was nothing wrong with his company
  transferring the assets for IPTL ­ including money - to PAP since the latter
  is the legally-accredited holding company for IPTL.

  Before being acquired by PAP, IPTL was owned jointly by a Malaysian firm,
  Mechmar Corporation and Tanzania¹s VIP Engineering and Marketing Company
  Limited, with the former controlling a 70 per cent stake.

  The company, according to its secretary and chief counsel, Joseph Makandege
  operated peacefully for just about five years before unending wrangles
  erupted between the two shareholders ­ prompting money to be sent to the
  escrow account.

  ³With squabbles between shareholders, VIP became suspicious that the money
  would be defrauded so he sought a court order ­ demanding that money, paid
  by Tanesco [the Tanzania Electric Company Limited] to IPTL, should be
  deposited in the escrow account at the BoT,² he explained.

  In 2010, Mr Sethi brought all the documents, confirming that he has been
  duly chosen as the custodian for all of Mechmar assets in Tanzania.

  The court cases notwithstanding, Mr Sethi went ahead to buy all the shares
  that Mechmar had earlier sold to Piperlink and transferred them to PAP.
  This, in essence, meant that Mr Sethi ­ through PAP - now owned 70 per cent
  of shares in IPTL, with VIP owning the remaining 30 per cent.

  He later engaged VIP so he could buy the latter¹s 30 per cent stake. ³VIP
  agreed and was paid $7.51 million as down payment for a deal totalling $75
  million,² explained Makandege, noting that the remainder was covered later.
  Having settled the deal, VIP went to court requesting the judge to drop all
  the cases involving VIP and Mechmar.

  The court ruled ­ on September 5, 2013 - in favour of VIP and all the cases
  were dropped. PAP was thus granted the ownership of all of IPTL assets ­
  including money in the escrow account. PAP also agreed to pay all IPTL
  creditors. The duty of the provisional liquidator ended there

  The new company, according to Mr Makandege, then embarked on a duty of
  searching for wherever IPTL assets were. It arranged a meeting with Tanesco
  where they arrived at the right amount that the state-owned utility firm
  owed IPTL. ³In fact, Tanesco board directed the management to inform key
  stakeholders that there were no more disputes between the state power
  company and IPTL ­ resulting into an official end of depositing IPTL money
  into the escrow account,² he said.

  The duty ahead of PAP remained that of making sure that money from the
  escrow account was transferred into the PAP account.
  ³With that, an agreement had to be signed between IPTL and the government
  through the Ministry of Energy and Minerals....it should be noted that money
  in the escrow account belonged to two of IPTL shareholders.....it was
  neither taxpayers¹ money nor money for Standard Chartered Bank Hong Kong,²
  said Mr Makandege.

  The government also required PAP to sign an Indemnity Agreement to the
  effect that whenever a new creditor comes, then PAP would be responsible.
  The government then wrote to BoT demanding that the money be released to the
  rightful and legally-accredited owner. ³That was how the money was
  released,² he explained.

  0 0
 • 03/13/14--09:52: TAARIFA MAALUM KUTOKA BUNGE • 0 0

  Na Frank Mvungi-MAELEZO


  SERIKALI imetoa ufafanuzi juu ya vitambulisho vya waandishi wa habari ( Press card) wakati wa Bunge Maalum la katiba na kusema kuwa ndicho kigezo pekee  kitakachowezesha  waandishi wa habari kutimiza majukumu yao vyema katika kipindi  chote cha bunge hilo.


  Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam  na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Assah Mwambene wakati akitoa tamko la Serikali kufuatia  taarifa potofu zilizoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari hapa  nchini.


  Mwambene alibainisha kuwa  utaratibu wa kutoa vitambulisho hivyo si  mgeni kama ilivyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari na kwamba unaweza kukipata ndani ya saa 24 ikiwa tu mwandishi anakidhi vigezo. Alisema vitambulisho vinatolewa tu kwa mwandishi mwenye taaluma ya uandishi wa habari kutoka chuo kinachotambulika naSerikali kwa kuzingatia sheria na kanuani zilizowekwa.

  Alisisitiza  kuwa utaratibu wa kutoa  vitambulisho kwa waandishi  habari upo  na ni wa kisheria  hivyo ni lazima ufuatwe. Pia  alisema kuwa ni vyema kila mwandishi akafuata taratibu zote za kupata kitambulisho kinachotolewa na MAELEZO kwa kuwa bila kitambulisho hicho hataweza kufanya kazi  katika kazi rasmi kama vile Bunge maalum la katiba.

  Alitoa wito kwa waandishi wa habari kujiendeleza katika taaluma ya uandishi wa habari kwa wale wasio na sifa za kupewa vitambulisho hivyo ili kuiniua Sekta ya Habari hapa nchini

  0 0

  FABIAN LEONARD SKAUKI – MGOMBEA CHAMA CHA WANANCHI –CUF
  DHIDI YA MATHAYO MANG’UNDA TORONGEY – MGOMBEA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO -CHADEMA

  13.03.2014

                                                                                                                                                                                                     

  Mimi  FABIAN L. SKAUKI, mgombea ubunge wa uchaguzi mdogo jimbo la CHALINZE kwa Ticket ya THE CIVIC UNITED FRONT (CUF) ninamwekea Pingamizi mgombea wa chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)  kwamba amepoteza sifa za kuwa mgombea kwa sababu zifuatazo.


  1.       Ndugu MATHAYO. M. TORONGEY amejaza Taarifa za uongo kwenye Fomu yake kwamba kazi anayoifanya ni BIASHARA. Sio kweli, kwa sababu hajaweka vielelezo vya yeye kufanya hiyo kazi. Hajulikani anafanya kazi gani.


  2.       Ndugu MATHAYO .M. TORONGEY amejaza  katika fomu kwamba anajua kusoma na kuandika Kiswahili na kiingereza. Taarifa hizi ni za uongo, mgombea huyu hajui kusoma wala kuandika Kiswahili wala kiingereza, na kwamba amedanganya na amepoteza sifa za kuwa mgombea.


  3.       Ndugu MATHAYO .M.TORONGEY  amedanganya kwa kughushi/kufoji sahihi za wadhamini,ambao amewaorodhesha kwenye fomu ya kuomba kuthibitishwa kuwa mgombea. Ambapo katika fomu hizo wadhamini wote sahihi zao zimefojiwa na hazifanani na zile zilizokuwepo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na kwamba sahihi zote hizi zimesainiwa na mtu mmoja ambaye sio muhusika. Hivyo anapoteza sifa ya kuendelea kuwa mgombea.


  4.       Ndugu MATHAYO.M.TORONGEY ameshindwa kutimiza mahitaji ya kisheria ya kuwa na wadhamini wasiopungua 25, badala yake amedhaminiwa na wadhamini 28 ambao kati yao wadhamini 7 sio wapiga kura halali wa jimbo la CHALINZE, na kwamba Taarifa zao na namba zilizojazwa hazifanani.


  Hivyo anabakiwa na wadhamini halali 21 ambao kisheria hawatoshi kutimiza matakwa ya kisheria.  Majina ya wadhamini hao ambao hawakidhi matakwa ya kisheria na namba zao ni


  JINA LA MDHAMINI                                                            NAMBA YA KADI KURA


  1.       HABIBU ALLY SAIDI                                                     * 16886275*

  2.       MOHAMMED RAMADHANI                                             *30376567*

  3.       ABDULKADIR ALLY                                                       *49264905*

  4.       SHABANI SULEYMAN                                                                                      *16984045*

  5.       JUMA MRISHO                                                             *48759563*

  6.       RAJABU ALLY                                                                                                      *16872368*

  7.       MANENO MIRAJI                                                                                                                           *16872059*  Wananchi wenye namba na majina hayo hapo juu waliojazwa kama wadhamini kuanzia namba 1 hadi 7 kwenye fomu yake hawana sifa za kupiga kura kwenye maeneo ambayo wamejazwa wanatokea.


  Hii ni kutokana na ukweli kwamba idadi halali ya wadhamini wanaobaki ukiwaondoa hao saba watabaki 21, hawakizi vigezo vya kuwa wadhamini.


  5.       Ndugu MATHAYO.M.TORONGEY  amedanganya Uraia wake, na  kwamba yeye si Mtanzania wa kuzaliwa ndio maana hana vielelezo halali vinavyohusu uraia wake. Hivyo anakosa sifa ya kuwa mgombea.


  Hivyo ninaomba Tume ya Uchaguzi kutengua uteuzi wa mgombea wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA)  ndugu MATHAYO.M.TORONGEY  kwa kuwa anakosa sifa za yeye kuendelea kuwa mgombea.


  Wako katika ujenzi wa Taifa


  FABIAN LEONARD SKAUKI


  ……………………………………………………..


  MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA CHALINZE.  THE CIVIC UNITED FRONT


  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na  Kamishna wa Sensa Hajjat Amina Mrisho (kushoto) na  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa  baada ya kupokea Ripoti ya Mgawanyo wa Watu kwa Umri na Jinsia kwa data za sensa ya watu na makazi mwaka 2012 leo Machi 13, 2014   Ikulu jijini Dar es salaam
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea toka kwa   Kamishna wa Sensa Hajjat Amina Mrisho Ripoti ya Mgawanyo wa Watu kwa Umri na Jinsia kwa data za sensa ya watu na makazi mwaka 2012 leo Machi 13, 2014   Ikulu jijini Dar es salaam.
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa ambaye pamoja na Kamishna wa Sensa Hajjat Amina Mrisho baada ya kupokea Ripoti ya Mgawanyo wa Watu kwa Umri na Jinsia kwa data za sensa ya watu na makazi mwaka 2012 leo Machi 13, 2014   Ikulu jijini Dar es salaam.PICHA NA IKULU

  0 0

   Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Nsachris Mwamwaja akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi(MMAM).Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari(MAELEZO) Frank Mvungi.

  Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Nsachris Mwamwaja (katikati) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi(MMAM).Kushoto ni Afisa Ustawi Mwandamizi Mkuu kutoka kutoka Wizara hiyo, Josephine Lyengi na Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari(MAELEZO) Frank Mvungi. Picha zote na Georgina Misama-MAELEZO
  ===========   ==========  ========
  Na Frank Mvungi

  WIZARA ya Afya na Ustawi wa jamii imefanikiwa kuajiri watumishi 27,795 katika kipindi cha mwaka 2005/2013.


  Hayo yamesemwa na Msemaji wa Wizara hiyo Bw. Nsachris wakati  wa mkutano na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam wakati akizungumzia mafanilkio ya mpango wa maendeleo ya Afya ya msingi (MMAM).


  Mwamaja amebainisha kuwa lengo kuu la mpango huo ni kusogeza huduma za afya ya msingi kwa wananchi wote kwa ubora unaokubalika karibu zaidi na wanakoishi. Alisema aidha malengo mahususi ya mpango wa MMAM  ni kuongeza, kurekebisha, kuimarisha vituo vya kutolea huduma  za afya na ustawi wa jamii na kuhakikisha huduma zinatolewa kwa usawa na kuwafikia wananchi wote.

  Aliongeza kuwa mpango huo unalenga kuhakikisha upatikanaji wa rasilimali watu, vifaa tiba na dawa zenye ubora katika vituo vya afya ili kuhakikisha utendaji ulio bora. Mwamwaja aliongeza kuwa ni vyema wananchi  wakashiriki katika kuhakikisha kuwa mfumo huo unafanya kazi ili kuleta tija na kufikiwa kwa malengo ya mpango huo.

  Katika mpango huo wa MMAM, Serikali imeongeza udahili kwa wanafunzi wa wanaosoma kada za Afya nchini kwa mwaka 2012/2013  hadi kufikia 7,956. Mwamaja aliongeza kuwa  Wizara ya Afya imepewa kibali cha kuwapangia vituo vya kazi watumishi 11,221 wa kada za afya  ambapo zoezi hilo linaendelea.


  Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii inaendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia miongozo ya Kitaifa na Kimataifa ikiwemo Dira ya Taifa 2015, MKUKUTA II, malengo ya millennia,Ilani ya uchaguzi na sera ya Taifa ya Afya.


  0 0

  Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samia Suluhu Hassan akimkumbatia Mwenyekiti wa Bunge Hilo Samwel Sitta Leo Mjini Dodoma.Picha na Hassan Silayo MAELEZO.
   Mgombea wa Nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la katiba Bi. Amina Abdallah akimpongeza Bi. Samia Suluhu Hassan baada ya Kutangazwa kuwa Makamu mweyekiti wa Bunge Maalum la Katiba.
   Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Samia Suluhu Hassan akitoa shukrani zake kwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba baada ya Kuteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo.
   Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Mwenyekiti Mteule wa Bunge hilo Bw. Samwel Sitta akibadilishana Mawazo na Mjumbe wa Bunge Hilo Mohamed Seif Khatib ndani ya Ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma.
   Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Thomas Kashilila akieleza wajumbe juu ya utaratibu wa upigaji kura kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti leo Mjini Dodoma.
   Mgombea wa Nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la katiba Bi. Amina Abdallah akinadi Sera zake  kwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba.
   Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la katiba wakibadilishana Mawazo na Mwenyekiti wa Bunge Hilo Samwel Sitta(Aliyekaa).Leo mjini Dodoma  0 0

   Wakazi wa maeneo ya Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) wakiwa wamejazana katika kituo cha Daladala cha Jamatini mjini hapa wasijue cha kufanya baada ya Madereva wa Magari hayo kugoma kwenda njia hiyo wakishinikiza kusimamisha abiria wanapopakia.
   Wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) wakiwaza jinsi ya kusafiri mpaka maeneo ya Makulu, Chimwaga na Ng'ong'onha baada ya wenye Daladala kugoma kutokana na kile walichodai ni kukamatwa mara kwa mara na polisi wa usalama barabarani wakitakiwa kutojaza kupita kiasi.

    Magari yanayosafirisha abiria yakiwa yameegeshwa pembezoni ya Bohari ya mkoa baada  ya madereva wa magari hayo kugoma kutoa huduma ya usafiri kwa njia ya UDOM kwa madai ya kuonewa na Askari wa barabarani mara kwa mara katika njia hiyo japo Kamanda wa Polisi Usalma Barabarani Boniventura Nsokolo kudai polisi hawatashindwa kuwakamata kama watawaona wakivunja sheria.

   Wanafunzi hao wakaamua kutumia usafiri wa pikipiki baada ya kuona mambo ni magumu huku wakishikiza kuwavaa wahusika.

   Na John Banda, Dodoma

  MADEREVA wa Daladala zinazoenda Chuo Kikuu cha Dodoma [UDOM] manispaa ya Dodoma leo wamegoma kutoa huduma hiyo kwa zaidi ya saa 4 hali iliyosababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi wa maeneo hayo.

  Mgomo huo ulioanza majira ya saa 7 mchana ulianza kama mdhaha tu mara baada ya abiria waliokuwa katika kituo hicho kujiuliza maswali yasiyo na majibu baada ya kuona makonda wa Daladala hizo wakikufunga milango na kuwakataza wasiingie na kama haitoshiwakaamuru madereva wao wayaondoe kituoni hapo.

  Madereva hao ambao walipoyaondoa magari waliyapeleka kuyaegesha maaneo ya Bohari walisema waliamua kufanya hivyo kutokana na kusumbuliwa mara kwa mara na polisi wa usarama barabarani kutokana na kusimamisha abiria.

  Walisema wanashangazwa na kitendo hicho kinachofanyika na polisi wa Dodoma pekee kinyume na mikoa kama ya Mwanza, Arusha, Mbeya na hata Dar es laam ambako wanapakia watakavyo na hakuna wa kuwauliza.

  Waliongeza kuwa vitendo hivyo wanavyofanyiwa vya kuzuiliwa kusimamisha abiria ni kuwatia hasara kutokana na kukosa abiria pindi wanapokuwa wakitokea UDOM ilihali sehemu yenyewe ni mbali huku mafuta yakiwa juu.

  Kwa upande wake Mkuu wa polisi wa usalama Barabarani Wilaya Boniventura Nsokolo alisema kila Dereva aangalie leseni yake inamruhusu kupakikia kiasi gani, na wao kama polisi hawawezikuona Dereva akivunja sheria harafu wakamuacha bila kumchukulia hatua.

  ''Lazima tuwakamate kama wakivunja sheria za Barabarani kwani kila mtu ana leseni na inamuongoza apakie abiria wanagapi na kwenye kila mkoa kuna utaratibu kutokana na kitengo husika kinachosimamia na kutoa leseni hivyo ni vizuri kufuata utaratibu'', alisema Nsokolo

older | 1 | .... | 245 | 246 | (Page 247) | 248 | 249 | .... | 1897 | newer