Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

DTBi-COSTECH launch Creative & Innovative Computer Coding programs for the youth

$
0
0
Giving his closing remarks, Permanent Secretary of Ministry for Communication, Science & Technology Prof Patrick Makungu congratulates DTBi and COSTECH for this initiative copy
Giving his closing remarks, Permanent Secretary of Ministry for Communication, Science & Technology Prof Patrick Makungu commends DTBi, COSTECH, the Global Partnership of the US Department of State and CoderDojo of Ireland for their efforts.
DTBi-COSTECH together with the Global Partnership of the US Department of State and CoderDojo of Ireland launched the afriCoderDojo programme, the first of its kind in Africa. 

Based on the global open-source CoderDojo movement founded in Dublin, afriCoderDojo’s curriculum aims provide young people aged 10-20 years old with the basics of coding while having fun. Guest lecturers, local technology entrepreneurs and educators will be invited to participate in the learning program to highlight and showcase the opportunities in the field of internet technology & the first private sector partner joining the team is Technobrain Ltd.
Eng. George Mulamula, CEO of DTBi explains that so far 17 schools from Mbeya, Arusha, Mwanza, Moshi & Dar Es Salaam have asked to be part of this program.
Eng. George Mulamula, CEO of DTBi explains that so far 17 schools from Mbeya, Arusha, Mwanza, Moshi & Dar Es Salaam have asked to be part of this program.
The purpose is to build a community of youth who will develop creative applications and programmes with and a slant towards entrepreneurship and in the future be job creators. The objective is for these youth to be future coders who develop websites, games, computer and mobile applications, and more.

The Minister of Communication Science & Technology, Prof. Mbarawa Makame sent his remarks prior to the launch and expressed his enthusiasm for the program. He expressed that he is, “ proud to be part of an initiative that [he] believes will go a long way towards ensuring young people have the necessary computer & innovative skills, education, and drive to compete in tomorrow’s integrated marketplace.”
H.E Ambassador Fionnuala Gilsenan of Ireland congratulates the students who have joined the AfriCoderGojo program on a job well done
H.E Ambassador Fionnuala Gilsenan of Ireland congratulates the students who have joined the AfriCoderGojo program on a job well done and applauds the team on being the first CoderDojo in Africa.
Students from local primary schools gathered at COSTECH and had their first session on how to program games and cartoons
Students from local primary schools gathered at COSTECH and had their first session on how to program games and cartoons.
Ambassador Fionnuala Gilsenan of Ireland, Permanent Secretary of Ministry for Communication, Science & Technology Prof Patrick Makungu and Director General of COSTECH Dr. Hassan Mshinda pose with one of the students  cop
Ambassador Fionnuala Gilsenan of Ireland, Permanent Secretary of Ministry for Communication, Science & Technology Prof Patrick Makungu and Director General of COSTECH Dr. Hassan Mshinda pose with one of the students.

KAMPENI YA KUPAMBANA NA HOMA YA INI YAZINDULIWA LEO JIJINI DAR

$
0
0
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Dk. Meshack Shimwela, akielezea madhara ya ugonjwa wa Homa ya Ini.
Shigongo akiwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kupambana dhidi ya ugonjwa wa Homa ya Ini.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick akiandika huku akitafakari jambo wakati wa uzinduzi huo.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Magembe akielezea umuhimu wa wananchi kupima virusi vya ugonjwa wa Homa ya Ini (Hepatitis B).
Meza kuu wakibadilishana mawazo.
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakifuatilia uzinduzi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick akizindua rasmi kampeni ya kupambana na ugonjwa hatari wa Homa ya Ini.


Ini likiwa salama kabla ya kushambuliwa na virusi vya Hepatitis B.
...Ini baada ya kushambuliwa na virusi vya Hepatitis B.
...Ini lenye kansa.
Shigongo akimpongeza mgeni rasmi, Said Mecky Sadick baada ya uzinduzi.
Mmoja wa mapaparazi akijiandaa kuchukua matukio katika uzinduzi huo.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wadau waliofanikisha kampeni hiyo.
Mgeni rasmi akiagana na Eric Shigongo baada ya zoezi la uzinduzi kukamilika.
Wananchi wakipima virusi vya Hepatitis B vinavyosababisha ugonjwa wa Homa ya Ini.
Shigongo akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari (DSJ) baada ya uzinduzi.

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick amezindua rasmi kampeni ya kupambana na Ugonjwa wa Homa ya Ini katika Hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar es Salaam.
Kampeni hiyo imeandaliwa na Kampuni ya Global Pulishers Ltd wakishirikiana na Wizara ya Afya, SD Africa, Sanofi, Megra Clinic, Damu Salama na Tamsa.

Katika uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa ambaye alikuwa mgeni rasmi, amewataka wadau mbalimbali kuonyesha ushirikiano katika kupambana na ugonjwa huo hatari kuliko HIV huku akiwaasa wananchi kuacha vitendo vinavyoweza kuleta maambukizi ya ugonjwa huo unaombukizwa kwa njia sawa na za HIV.
(PICHA ZOTE NA GPL)

Wanafunzi wa Sekondari Tanzania Sasa Wanaweza Kujadiliana Mtandaoni Popote Walipo

$
0
0

Kwa siku za hivi karibuni matokeo ya mitihani yamekuwa sio mazuri sana na kuna baadhi ya watu wengi wanalaumu mitandao ya kijamii na internet kwa hili, kwamba inawafanya wanafunzi wawe busy kufanya mambo yasiyo ya msingi na kusahau kusoma. 

Kwa kiasi Fulani ni kweli kwani kumekuwa na ongezeko la idadi ya vijana nchini Tanzania wanaojiunga na mitandao ya kijamii na internet kwa ujumla. Hata hivyo, ongezeko hili sio jambo la kuliangalia kwa jicho baya bali kulikumbatia kwani linaweza kusaidia wanafunzi wa sekondari, hasa sasa hivi ambapo kuna website kwa ajili ya wanafunzi wote Tanzania kukutana na kujadiliana masomo na topic mbali mbali wanazofundishwa darasani, na masuala yote ya kielimu kwa ujumla. Website hiyo inaitwa myElimu.com.

 Given Edward, mwanzilishi wa myElimu Project, amesema website hiyo itawasaidia wanafunzi kujadiliana na wanafunzi wenzao mambo mbali mbali ya darasani, popote pale walipo. MyElimu.com itamuwezesha mwanafunzi wa shule yoyote ile, mfano ya Dar-es-Salaam, kujadiliana na wanafunzi wengine wa mkoa wowote wa Tanzania mfano mwanza, Arusha au Mbeya kuhusu masomo yao ya darasani. 

Hii ina maana kwamba mwanafunzi aliyeko shule ya sekondari Kibasila, anaweza kuanzisha mjadala na wanafunzi wenzake wa Azania, Shaaban Robert, Nyakato au St. Francis wakaweza kujadiliana naye ndani ya mtandao huo wa myElimu.com. Safi!

MyElimu.com inapatikana kwa lugha 32 duniani nah ii itawezesha hata watembeleaji wa mtandao huo kutoka nje ambao hawajui Kiswahili na kiingereza waweze kutoa michango yao ambayo inaweza kutafsiriwa kuja kwa tena kuwa kwa Kiswahili au kiingereza kutegemea na chaguo la mtu.
Kitu kizuri kuhusu myElimu.com ni kwamba kuna sehemu ya games ambapo members wake wanaweza kwenda na kucheza pale ambacho watakuwa wameboreka au kuchoka kwenye discussions au wakiwa wanasubiri kitu kwenye mijadala yao..
 
Given aliitangaza rasmi myElimu siku 3 zilizopita katika post iliyosomeka:-
 
"I've been working on an initiative. Creating a platform where students all over Tanzania can meet and discuss school topics and every academic related issue. Currently it's difficult for students to share information mainly due to geographical distances. Nevertheless, with the increase in books with no single authorized source, it has been hard for students to know what materials are correct and good for use, hence they're stuck with wrong things. 

So I created My Elimu. My Elimu is a project which will make it possible for students in Dar es Salaam to exchange ideas and learn together with students in Arusha, Mwanza, Iringa and all other parts of Tanzania through www.MyELimu.com. It will be a meeting point for all students from Form 1 to Form 6 to meet and help each other out.

When you visit the website, you will be met with an interactive user interface that displays forums of various subjects of which you will select any that interests you and start or join a topic discussion. You need to register to the website in order to participate or start a discussion. Guests can only read the discussions but not participate."

Kwa wanafunzi wote wa sekondari Tanzania kuanzia form 1 mpaka form 6 mnashauriwa mjisajli kwani ni sehemu nzuri ya kuweza kujikuza kielimu na kutumia internet kwa manufaa yako. Unaweza kujisajili moja kwa moja hapa http://goo.gl/2NvPbO au kwa kutembelea http://goo.gl/j1kMzh na kisha kubonyeza “Register”. Ukijisajili ndio utaweza kuanzisha mijadala na kushiriki katika mijadla iliyoanzishwa tayari.

SBL YACHEZESHA DROO YA NNE YA PROMOSHENI YA WINDA SAFARI YA BRAZILI NA SERENGETI YAENDELEA .

$
0
0
Pichani kati ni Meneja wa bia ya Serengeti Bw Rodney Rugambo akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani),mapema leo jijini dar  kuhusiana na mshidi aliyejishindia tiketi ya kwanza ya kwenda nchini Brazili 
Meneja wa bia ya Serengeti Bw Rodney Rugambo akizungumza na mshidi huyo kwa njia ya simu ya kiganjani.

SBL YACHEZESHA DROO YA NNE YA PROMOSHENI YA WINDA SAFARI YA BRAZILI NA SERENGETI YAENDELEA   .


Hatimaye mshindi wa kwanza wa tiketi ya kwenda Brazili kupitia bia ya Serengeti apatikana.


  Baada ya kusubiri kwa kipindi cha wiki 3 hatimaye mshindi wa kwanza wa tiketi ya kwenda Brazili kupitia promosheni ya 3 Winda Safari ya Brazili na Serengeti amepatikana katika droo ya nne ya promosheni hiyo. Katika droo hiyo pia wamepatikana washindi wawili wa simu aina ya Samsung galaxy tab, pamoja na washindi hao wa droo pia kuna washindi waliojipatia zawadi za papo hapo kama bia za bure, fedha taslimu pamoja na ving’amuzi. 

Droo hiyo imechezeshwa leo asubuhi katika ofisi za Kampuni ya Bia ya Serengeti huku ikishuhudiwa na waandishi wa habari, maofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, PWC na push mobile media. Promosheni hiyo bado ina wiki 8 mbele hadi kumalizika na ndani yake bado droo kubwa 2 za kujishindia tiketi za kwenda Brazili.


Akiongea kwa furaha iliyopita kifani kwa njia ya simu mshindi wa kwanza wa tiketi ya kwenda Brazil Deusdedit Kahwa kutoka Mbezi, Dares Salaam alisema alipata mshangao mkubwa sana kwa kuwa hakutarajia kupata bahati hii ya kuwa mshindi wa tiketi na alishiriki promosheni hii baada ya kuona matangazo yake kwenye televisheni. Aliishukuru Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa  kumpa fursa hiyo kubwa katika maisha yake na kuipongeza kwa kuwajali wateja wake kwa kuwapa zawadi mbalimali zinogusa maisha yao.

“nimefurahi sana na ninajiona mwenye bahati sana kwa kushinda zawadi hii kubwa, hii ni mara ya kwanza kushinda zawadi katika promosheni hii na nimepata zawadi kubwa sana na itakuwa ni mara yangu ya kwanza kutoka nje ya nchi, nawashukuru sana Serengeti kwa kutujali wateja wao” alimalizia Deusdedit.


Meneja wa bia ya Serengeti Bw Rodney Rugambo alisema kuwa promosheni hiyo ipo wazi kwa wanywaji wote wa bia ya Serengeti, na mpaka sasa kumekuwa na washindi Zaidi ya 50000 waliojishindia bia za bure na pia zaidi ya washindi 2000 wa fedha taslimu kiasi cha shilingi 5000 na 10,000. Washindi waliojishindia simu za Samsung tab katika droo ya leo ni Deo Msofe kutoka Kiboroloni, Moshi na Jeremiah Ndelekwa kutoka Arusha. Pia wamepatikana washindi watano (5) wa ving’amuzi ambao wote kwa pamoja watakabidhwa zawadi zao katika sherehe maalum.


Nae Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Bw Allan Chonjo alisema “promosheni ya Winda Safari ya Brazil na Serengeti bado inaendelea na tunapenda kuwakumbusha wateja wetu kuwa hii ndio tiketi ya kwanza bado kuna tiketi nyingine na zawadi nyingine nyingi zaidi, unaweza kufuatilia kupitia ukurasa wetu wa facebook www.facebook.com/serengetipremiumlagerkwa taarifa zaidi. Napenda kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kutumia bidhaa zetu na sisi tunawaahidi kuendelea kuwapa bidhaa zilizo bora na zenye viwango na ubora wa hali ya juu”



Kunywa kistaarabu. Washiriki wanatakiwa kuwa na umri unaozidi miaka 18. Vigezo na masharti kuzingatiwa.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AOMBOLEZA KIFO CHA MTOTO WA WAZIRI SOPHIA SIMBA, DAR

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maombolezo ya msiba wa Lefoord Simba, mtoto wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, wakati alipofika nyumbani kwa Waziri Masaki jijini Dar es Salaam, leo kutoa pole.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, wakati alipofika nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam, leo kutoa pole kwa kufiwa na mtoto wake, Lefoord Simba. Mazishi yatafanyika kesho kwenye Makaburi ya Kinondoni.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, wakati alipofika nyumbani kwa Waziri Masaki jijini Dar es Salaam, leo kutoa pole kwa kufiwa na mtoto wake, Lefoord Simba. Mazishi yatafanyika kesho kwenye Makaburi ya Kinondoni.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamini Mkapa, Waziri mstaafu (wa pili kulia) Mjumbe wa Nec Wilaya ya Busega, Chegeni (kulia) na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, wakizungumza jambo wakati wakijumuika kwa pamoja katika maombolezo ya msiba wa Lefoord Simba, mtoto wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, Masaki jijini Dar es Salaam, leo.
Baadhi ya waombolezaji.Picha na OMR 

KUMBUKUMBU.

$
0
0

JUDICA STEPHANO TERI

22.06.1946  to  08.03.2012

Passed away peacefully after a short illness.

Deeply missing you daily! You were a very loving husband to Jane (Mwl Teri); a loving, caring dad to Joan, Linda, Davis & Hillary and a dedicated brother to Monyiaichi. All of us including your other brothers Eliona, Tumaini and sister Elingienengasia, the in-laws (Aliko, Leonard & Tina), grand-children (Tumpe-Janice, Lusako-Luke, Evan-Tumaini Alex & Jeannete-Elsa), the entire TERI family, relatives and friends deeply miss you!


It is just like it happened yesterday, yet days have turned into months and it is two years today (08.03.2014) since you departed from this life and promoted to glory.

Each day we are filled with fresh memories of your love, wisdom and care. However,

WE THANK GOD FOR HIS PROTECTION AND BLESSINGS TO ALL OF US.

"John 11:25.. whoever believes in me (Jesus), though he die,

yet shall he live!"



ATCL yapata ndege mpya

$
0
0
 Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la ATCL, Kapteni Milton Lazaro akishuka kwenye ndege mpya ya shirika hilo aina ya CRJ-200, baada ya ndege hiyo kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Alhamis usiku
 Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la ATCL, Kapteni Milton Lazaro (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo mara baada ya kuwasili kwa ndege mpya ya shirika hilo aina ya CRJ-200, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Alhamis usiku.
 Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la ATCL, Kapteni Milton Lazaro (Kulia) akiwatambulisha baadhi ya watendaji wa shirika hilo mara baada ya kuwasili kwa ndege mpya ya shirika hilo aina ya CRJ-200, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Alhamis usiku.
 Wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Taifa Air Tanzania (ATCL) wakisheherekea mara baada ya kuwasili kwa ndege mpya ya shirika hilo aina ya CRJ-200, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Alhamis usiku.
 Picha ya ndege mpya ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL), aina ya CRJ-200 ya nchini Canada, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Alhamis usiku.

========   ========  ==========
ATCL yapata ndege mpya
  •  Yaanza utekelezaji wa mkakati wa kuimarisha huduma zake
  • Kupata ndege mbili mpya zenye uwezo wa kubeba abiria 78 ifikapo mwezi Mei
  • Yaondoa adhabu na masharti magumu kwa abiria wanaobadilisha tarehe za safari na wanaochelewa kufika uwanjani siku ya safari 

SHIRIKA la Ndege la Taifa (Air Tanzania) limepata ndege nyingine aina ya CRJ-200 ya nchini Canada yenye uwezo wa kubeba abiria 50, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wake madhubuti wa kuimarisha huduma zake.

Shirika hilo la Air Tanzania (ATCL) linaona ujio wa ndege hii kama chachu ya kutimiza azma yake ya kuimarisha huduma zake ikiwa ni pamoja na kuongeza safari zake katika njia wanazoruka kwa sasa, kuanzisha njia nyingine mpya, na kuwahakikishia wateja wake uhakika wa huduma zake.  

Mara tu baada ya ndege hiyo kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Alhamis usiku, Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa ATCL, Captain Milton Lazaro alisema kuwa kuna matumaini makubwa ya Shirika la Ndege la Taifa kufanya vizuri zaidi katika utoaji wa huduma za usafiri wa anga, ikizingatiwa kuwa shirika lina mkakati madhubuti wa upanuzi wa huduma zake ambao utekelezaji wake umeanza.

“Ndege tuliyoipokea leo hii, ni sehemu ya ndege tatu tulizopanga kuleta mwaka huu. Ndege nyingine mbili zinatarajiwa kufika kati ya mwezi Aprili na Mei mwaka huu. Kuongezeka kwa idadi ya ndege zetu kutatuwezesha sisi kufungua mipaka kwa kuanzisha njia mpya na kuongeza safari nyingi zaidi katika maeneo tunayoenda kwa sasa,” alisema Kapteni Lazaro.  

Alisema kuwa ndege mbili zitakazoletwa nchini ifikapo Mei, zinauwezo wa kubeba abiria 78 na ni toleo jipya katika sekta ya usafiri wa anga, na zitatumika katika kusafirisha abiria ndani na nje ya nchi.

Kapteni Lazaro alisema kuwa shirika lake linampango wa kuanzisha safari mpya ikiwa ni pamoja na ya Tabora – Mpanda, Mbeya- Dar es Salaam na kuongeza idadi ya safari za Mwanza- Dar es Salaam, Dar es Salaam-Comoros na Mtwara pamoja na Kigoma.

“Kwa ongezeko hili la safari zetu, abiria wetu watafurahia safari za kila siku za kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza, ikiwa muda wa kuondoka Dar kuwa 1600hrs na kutoka Mwanza kuwa 1800hrs. Tutakuwa tukienda mkoani Mbeya mara nne kwa wiki; kwa siku za Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumapili. Wakati Moroni katika visiwa vya Comoro tutakwenda katika siku za Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumamosi. Na pia tunategemea kuzindua safari ya Tabora – Mpanda hivi karibuni,” alisema.  

Aliongeza kuwa shirika hilo pia limeondoa baadhi ya adhabu watozwazo abiria endapo wanashindwa kusafiri siku na muda waliyoomba, na kusema kuwa hii itawasaidia abiria wao kutoingia gharama za ziada endapo watakumbana na dharura mbali mbali kabla ya safari.

“Katika jitihada za kuwasaidia abiria wetu na kuwaonyesha kuwa tunayatambua mazingira tunayoishi na yakibiashara vizuri, shirika limeamua kuondoa adhabu kwa abiria ambao watashindwa kufika uwanja wa ndege kabla ya muda wa ndege kuondoka na adhabu ya kubadilisha safari,” alisema Kapteni Lazaro.

Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji huyo, upatikanaji wa ndege hiyo utaongeza idadi ya abiria kwa kati ya asilimia 30 mpaka 40, kutokana na kuwa huduma za shirika hilo bado ni nzuri na viwango vya nauli ni vya kiushindani zaidi na vyenye unafuu ukilinganisha na mashirika mengine.

Kwa kutumia ndege yake aina ya Bombardier Dash-8, ATCL kwa sasa inasafiri katika zaidi ya maeneo nane (8) nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na Mtwara, Mwanza, Tabora, Kigoma, Dar es Salaam, Mbeya, Bujumbura na Moroni nchini Comoro.

Semina ya wajumbe wa Bunge maalum imeahirishwa mpaka saa tisa mchana leo.

$
0
0

Kikao cha semina ya wajumbe wa Bunge maalum la Katiba kilichokuwa kiendelee leo saa nne asubuhi baada ya Mwenyekiti wake wa Muda Mhe. Pandu Amir Kificho Kuaarisha jana mchana sasa kitaendelea leo tarehe 8 machi 2014 saa tisa alasiri. Hii ni kutokana a kamati ya maridhiano inayopitia vifungu ilivyokuwa inafanyia kazi kuomba mda zaidi.Hivyo wajumbe wote wa Bunge maalum wanaombwa kufika Bungeni kuendelea na semina hiyo saa tisa alasiri badala ya saa nnne asubuhi.

Imetolewa na Katibu wa Baraza la wawakiliashi na Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NEWS ALERT: : MAMA MKUBWA WA MTOTO ADOLOTEA NYAVIKE , SALOME KIEGU (35) MTOTO ALIYE UNGUA NA MOTO ATOWEKA NA MTOTO HUYO KUSIKO JULIKANA.

$
0
0
Katika hali ya Kutatanisha na kushangaza mama mkubwa wa Mtoto aliye ungua kwa Moto na kusababisha Shingo yake kuungana na mwili ametoweka na mtoto huyo huku wasamalia wema waliokuwa wakiendelea kutoa michango yao kwa ajili ya kumsaidia akatibiwe wanaendelea kufanya hivyo.

Mama huyo alitoweka mapema alfajili jana huku asiseme ni sehemu gani alikuwa amekwenda bila hata kuaga kwa mtu yeyote yule, Kutokana na swala hili Tulikuwa tunaomba wale watu wote wanao endelea kumchangia mtoto huyo na wanaopanga kumchangia kupitia namba hii ya mama huyo  0752 986879 wasitishe kufanya hivyo, na mpaka sasa namba yake haipatikani na taratibu za kumsaka zinaendelea.
Tutaendelea kuwafahamisha..
Huyu ndiye Mama Mkubwa wa Mtoto Adolotea Nyavike bi. Salome Kiegu(35) ambaye ametoweka na mtoto huyo kusiko julikana huku wasamalia wema wakitaka kutoa misaada.

MTOTO Adolotea Njavike(1.4) ambae Kichwa na Kiwiliwili vimeungana baada ya kupata na ajali ya Moto akiwa na mama yake Mzazi.
Na mbeya yetu.

Matukio Katika Maadhimisho Siku ya Wanawake Duniani na TGNP

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP-Mtandao), Bi. Lilian Liundi akitoa hotuba ya kuwakaribisha wageni mbalimbali na kuzungumza na washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam. 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP-Mtandao), Bi. Lilian Liundi akitoa hotuba ya kuwakaribisha wageni mbalimbali na kuzungumza na washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam.Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Bi. Zuki Njalai Mihyo (aliyesimama) akizungumza na washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na TGNP-Mtandao katika viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Bi. Zuki Njalai Mihyo (aliyesimama) akizungumza na washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na TGNP-Mtandao katika viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa TGNP-Mtandao, Bi. Usu Mallya (aliyesimama) akitoa mada kwa washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania. Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa TGNP-Mtandao, Bi. Usu Mallya (aliyesimama) akitoa mada kwa washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania.Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP-Mtandao), Bi. Lilian Liundi (kulia) akichukua dondoo muhimu wakati wa uwasilishwaji mada anuai katika maadhimisho hayo. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP-Mtandao), Bi. Lilian Liundi (kulia) akichukua dondoo muhimu wakati wa uwasilishwaji mada anuai katika maadhimisho hayo.Washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani wakijumuika katika burudani huku wakionesha majarida anuai ya kupinga ukatili, unyanyasaji wowote wa kijinsia kwa wanawake nchini Tanzania. Washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani wakijumuika katika burudani huku wakionesha majarida anuai ya kupinga ukatili, unyanyasaji wowote wa kijinsia kwa wanawake nchini Tanzania.Baadhi ya washiriki anuai wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na TGNP-Mtandao wakifuatilia mada zilizowasilishwa katika maadhimisho hayo. Baadhi ya washiriki anuai wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na TGNP-Mtandao wakifuatilia mada zilizowasilishwa katika maadhimisho hayoBaadhi ya washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani wakijisajili kabla ya kujumuika na wenzao katika maadhimisho. Baadhi ya washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani wakijisajili kabla ya kujumuika na wenzao katika maadhimisho.Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP-Mtandao), Bi. Lilian Liundi (wa kwanza kulia) akitoa hotuba ya kuwakaribisha wageni mbalimbali na kuzungumza na washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Bi. Zuki Njalai Mihyo akichukua dondoo muhimu. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP-Mtandao), Bi. Lilian Liundi (wa kwanza kulia) akitoa hotuba ya kuwakaribisha wageni mbalimbali na kuzungumza na washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Bi. Zuki Njalai Mihyo akichukua dondoo muhimu.Baadhi ya washiriki wenye ulemavu wakifuatilia maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani. Baadhi ya washiriki wenye ulemavu wakifuatilia maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.Katika maadhimisho hayo baadhi ya wajasiriamali walijitokeza kuonesha bidhaa zao kwa washiriki. Katika maadhimisho hayo baadhi ya wajasiriamali walijitokeza kuonesha bidhaa zao kwa washirikiBaadhi ya viongozi wa vyama anuai vya wanawake wenye ulemavu wakifuatilia maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani. Baadhi ya viongozi wa vyama anuai vya wanawake wenye ulemavu wakifuatilia maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

KAMPUNI YA TANZANIA DISTILLERIES LTD. KONYAGI WASHEREKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

WANAWAKE WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII WAUNGANA NA WANAWAKE WENGINE DUNIANI KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.

$
0
0
 Wanawake wanaowakilisha Wizara ya Maliasili na Utalii wakipita mbele ya mgeni rasmi katika uwanja wa Mwembe-yanga.
 Bibi aliyefurahia maandamano ya wanawake wenzake na kujiunga nao kusheherekea siku ya wanawake duniani.
 Baadhi wa wanawake wa wizara ya maliasili na utalii wakijiandaa kujiunga kwenye maandamano nje ya uwanja wa Mwembe - yanga 
  Wanawake wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakiserebuka wakati wa maandamano kuelekea uwanja wa Mwembe-yanga

TAWOPHA wanawake day

$
0
0
 
Chama cha Wanawake katika Fani ya Wafamasia (TAWOPHA) kinapenda kuwatakia wanawake wote Tanzania na Duniani kote sikukuu njema ya wanawake. Wanawake tunaweza kama tukifanya kazi kwa bidii na kupeana  mawazo chanya  ili kujiletea maendeleo.


“Chochea Mabadiliko Kuleta Usawa wa Kijinsia”.



Article 1

$
0
0
MAMA PINDA ATAKA WAZAZI WAJALI ELIMU YA WATOTO WAO BILA KUWABAGUA


MKE WA WAZIRI MKUU, Mama Tunu Pinda amewataka wazazi hapa nchini watoe kipaumbele kwenye suala la elimu kwa vijana bila ubaguzi wa kijinsia.

Ametoa wito huo leo mchana (Jumamosi, Machi 8, 2014) wakati akifungua Kongamano la Wanawake wa Afrika ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani lililofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam.

Kongamano hilo liliandaliwa na Chama cha Walimu Wanawake Tanzania (Tanzania Women Teachers’ Association - TAWOTEA) kwa kushirikiana na taasisi ya African Women Charity Organisation ya Oakland, California, Marekani.

Akizungumza na washiriki wa kongamano hilo, Mama Tunu Pinda alisema: ”Ninawaomba wazazi wenzangu, wake kwa waume tuungane kwa pamoja kwa kutoa kipaumbele kwenye suala zima la elimu kwa vijana wetu bila ubaguzi wa kijinsia. Kwa kufanya hivyo tutawajenga wavulana na wasichana ili wawe na uwezo wa kiuchumi na uthubutu katika masuala ya uongozi na maisha yao ya baadaye.”

Akizindua mfuko wa elimu ulioanzishwa na chama hicho, Mama Pinda  alisema ana imani utakuwa endelevu na utakidhi malengo ya kuazishwa kwake ambayo ni kuwasaidia watoto wenye uhitaji na waishio kwenye mazingira ili wapate elimu ya msingi na ya sekondari.

”Mkiwa ni waalimu wanawake na tena ni walezi wa watoto wetu, mmefanya jambo kubwa na la kihistoria kwa kuanzisha mfuko wa elimu mlioamua kuuita Tanzania Education Fund (TEF). Nimedokezwa kwamba malengo ya mfuko huu ni kusaidia gharama za elimu ya msingi na sekondari kwa watoto wa kike na wa kiume na hasa kwa watoto walio kwenye mazingira magumu na wenye uhitaji. Ni matumaini yangu kwamba utakuwa endelevu.”

”Ni imani yangu kwamba kupitia mfuko huu unaozinduliwa rasmi leo hii, utaowaongezea vijana wetu wa kike na wa kiume wigo wa kupata elimu ambapo kama mfuko huu usingekuwepo, isingekuwa rahisi kwao kumudu gharama za masomo,” aliongeza.

Aliwaomba wadau wote wa elimu na wananchi kwa ujumla, waunge mkono juhudi za walimu hao katika kuikomboa nchi hii, hasa katika sekta ya elimu huku wakiamini elimu ni ufunguo wa maisha.

Mapema, akisoma risala yao, Mkurugenzi Mtendaji wa TAWOTEA, Mwl. Neema Kabale alisema asasi hiyo ambayo imesajiliwa tangu mwaka 2008, inajihusisha na utetezi wa haki za msingi za wanawake, wasichana, vijana na watoto katika masuala ya elimu, afya, na upatikanaji wa chakula.

Katika kongamano hilo la siku moja, asasi hiyo iliandaa mada sita zikiwemo za “Ushiriki wa wanaume katika ukombozi wa mwanamke” na “Majukumu ya Vijana katika Muungano wa Afrika”.

Akitoa hitoria fupi ya Kongamano la Wanawake Afrika, Rais wa taasisi ya African Women Charity Organisation ya Oakland, Marekani, Bi. Rwanda Saleem, alisema Tanzania ni nchi ya nane kupata fursa ya kuratibu wa kongamano kama hili.

”Barani Afrika tayari nchi saba zimekuwa  waratibu wa kongamano hili ambazo ni Ghana, Guinea, Gambia, Senegal, Kenya, Rwanda, na Msumbiji ambayo ilikuwa mwenyeji mwaka jana. Tanzania imepewa fursa ya kuandaa kongamano hili mwaka huu,” aliongeza.

Kaulimbiu ya kongamano hilo ni “Kujenga Muungano wa Afrika kwa Kushirikisha Wanawake kwenye Uongozi” (The Unification of Africa Through the Emancipation of Leadership of Women).


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.
JUMAMOSI, MACHI 8, 2014

LEO NI SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.

$
0
0
WANAWAKE WANAWEZA,WAKIWEZESHWA,TUWAPE NAFASI.!

Rais Kikwete awaongoza viongozi mbali mbali na mamia ya waombolezaji kumfariji Mh. Sophia Simba kwa kufiwa na Mwanae Leeford Simba

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Waziri wa Maendeleo ya jamii jinsia na Watoto Mhe.Sophia Simba kufuatia kifo cha mwanaye Marehemu Leeford Simba huko Mikocheni jijini Dar es Salaam leo.Marehemu Leeford Simba anatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.Marehemu Leeford Simba amezikwa jioni ya leo kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa mkono wa pole na kumfariji Waziri Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mhe.Sophia Simba kufuatia kifo cha Mwanaye Leeford Simba wakati wa ibada ya kumuombea marehemu iliyofanyika nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam leo.Marehemu Leedford anatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.Marehemu Leeford Simba amezikwa jioni ya leo kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Neema Mathew(kulia) na waombolezaji wengine kufuatia kifo cha Mumewe Leeford Simba kilichotokea juzi. Marehemu Leeford Simba ni mtoto wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii jinsia na Watoto Mhe.Sophia Simba.Marehemu Leeford Simba amezikwa jioni ya leo kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu,Mh. Benjamin Mkapa akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Leeford Simba ambaye ni Mtoto wa Waziri Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mhe. Sophia Simba wakati wa ibada ya kumuombea marehemu iliyofanyika nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam leo.Marehemu Leeford Simba amezikwa jioni ya leo kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu,Mh. Benjamin Mkapa akimfariji mtoto wa Marehemu Leeford Simba ambaye ni Mtoto wa Waziri Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mhe. Sophia Simba wakati wa ibada ya kumuombea marehemu iliyofanyika nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam leo.Marehemu Leeford Simba amezikwa jioni ya leo kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mke wa Makamu wa Rais,Mama Zakhia Bilal akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Leeford Simba ambaye ni Mtoto wa Waziri Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mhe. Sophia Simba wakati wa ibada ya kumuombea marehemu iliyofanyika nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam leo.Marehemu Leeford Simba amezikwa jioni ya leo kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akitoa heshima za mwisho kwa Marehemu Leeford Simba ambaye ni Mtoto wa Waziri Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mhe. Sophia Simba wakati wa ibada ya kumuombea marehemu iliyofanyika nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam leo.Marehemu Leeford Simba amezikwa jioni ya leo kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Mhe. Sophia Simba kufuatia kifo cha mwanaye,Marehemu Leeford Simba,Masaki jijini Dar es Salaam leo.Marehemu Leeford Simba amezikwa jioni ya leo kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

PPF YAMWAGA MISADA TEMEKE HOSPITAL SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

$
0
0
 Wafanyakazi Wanawake wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakiungana na wanawake wenzao kusherehekea siku ya Wanawake Duniani kwenye viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es Salaam, Jumamosi Machi 8, 2014.
 Lucy Raphael (Kulia), akifurahia jambo na wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, baada ya kumtembelea na kumpatia zawadi kwenye hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam jana. Lucy ambaye amejifungua watoto mapacha ni miongoni mwa watu waliofaidika na zawadi mbalimbali zilizotolewa na Mfuko huo kwa hospitali hiyo.
 Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Kanda ya Temeke, Erica Sendegeya (Kushoto), akimvisha karatasi maalum (Pampers), mtoto huyu aliyelazwa kwenye hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam, Jumamosi Machi 8, 2014. Wafanyakazi Wanawake wa Mfuko huo, walitembelea hospitali hiyo jana Jumamosi ili kuwafariji na kuwapatia misada wagonjwa baada ya kushiriki sherehe za siku ya wanawake Duniani.
 Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakigawa misada kwa wagonjwa kwenye hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam, Jumamosi Machi 8, 2014. 
 Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Kanda ya Temeke jijini Dar es Salaam, Erica Sendegeya (Kushoto) na Mama wa Mapacha, Lucy Raphael (Kulia), wakifurahi, huku Erica akiwa amewabeba watoto hao, wakati Wafanyakazi Wanawake wa Mfuko huo, walipotembelea hospitali ya Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, Jumamosi Machi 8, 2014, ili kuwafariji na kuwapatia misada, baada ya wafanyakazi hao kushiriki matembezi ya kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani kwenye viwanja vya Mwembeyanga.
 Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele (Kushoto), akiwa amempakata kichanga, saa chache baada ya kuzaliwa na kubahatika kukutana na wafanyakazi wanawake wa Mfuko huo waliotembelea hospitali ya Temeke kwa nia ya kuwafariji na kuwapatia misada mbalimbali Juammosi Machi 8, 2014. Ziara hiyo ni baada ya kushiriki matembezi ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani kwenye viwanja vya Mwembeyanga.
 
Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Kanda ya Temeke jijini Dar es Salaam, Erica Sendegeye(Wapili kulia), akimpatia mama huyu mzazi, karatasi maalum za kujivunga watoto(Pampers), wakati wafanyakazi wanawake wa Mfuko huo, walipotembelea wagonjwa kwenye hospitali ya Temeke jana, ambako walitoa misaada mbalimbali ya vyakula na vifaa kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani. Wakwanza kushoto ni Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko huo, Lulu Mengele.
Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, akiwa amebeba boksi lenye maji ya Kilimanjaro akiingia nalo kwenye wodi, tayari kugawia wagonjwa

MUUNGANO WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI YANAYOTETEA HAKI ZA WANAWAKE WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

$
0
0
Kutoka kushoto ni Miss Tanzania 2013 Happy Watimanywa , Dk. Agnes Nyomola kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam ambaye ni Mtaalam wa mambo ya Sayansi, na Specioza Rweyemamu ambaye ni Ispecta katika mambo ya anga katika Mamlaka wa usafiri wa Anga Tanzania, ambao ndio walikuwa wasemaji katika sherehe hizo
Dk. Agnes Nyomola kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam ambaye ni Mtaalam wa mambo ya Sayansi akizungumza na wanafunzi kutoka shule mbalimbali jijini Dar es salaam waliofika katika sherehe hizo za siku ya wanawake Duniani na kuwasihi kupenda masomo ya Sayansi kutokana na kwamba kwa sasa Dunia imebadilika na tunapo elekea ni Karne ya Sayansi na Teknolojia, amewasihi pia wasichana kupenda masomo hayo akiamini kuwa wanaweza na kwamba ni Fursa muhimu sana kwao.
 Specioza Rweyemamu ambaye ni Ispecta katika mambo ya anga katika Mamlaka wa usafiri wa Anga Tanzania akizungumza na wanafunzi pamoja na wageni waalikwa mbalimbali hasa wanafunzi na kuwaasa kuwa wanatakiwa kuwa mfano wa kuigwa katika jamii na kusoma kwa bidii kwani hakuna kisicho wezekana kila mtu anaweza, pia amewasihi wasichana hasa wadogo kupenda kusoma zaidi ili waje kuwa viongozi wa baadae.
 Wakili wa Mahakama Kuu Modesta Mahiga akizungumza na wanafunzi waliofika katika Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Chuo Kikuu Dar es salaam na kuwahimiza wanafunzi hasa wakike wanaokuwa wasikimbilie katika mambo makubwa lakini wakazane na masomo ili kupata kufanikiwa zaidi.
 Miss Tanzania 2013 Happy Watimanywa akiongea na wanafunzi, alisisitiza sana wanafunzi wenzake wa kike kuwa wanatakiwa kusoma kwa Bidii ili kuweza kuja kufanikiwa katika mambo yao ya mbeleni, aliongeza kuwa mtoto wa kike ndio taifa la kesho na kiongozi wa kesho hivyo  ni lazima wakazane sana katika masomo yao na kuichukulia siku ya leo kama changamoto na chachu kwao ya kujibidisha zaidi.
 Mwenyekiti wa Muunganiko wa mashirika yasiyo ya Kiserikali yanayotetea haki za Wanawake Tanzania Bi. Juliana Bwire akitoa neno la Shukurani kwa wasemaji wote waliokuwa wakizungumza kila mmoja kwa wakati wake , pia kuwashukuru wote waliofika katika Sikukuu hiyo ya Mwanamke Duniani.


 Jane Mrema Mshauri wa Jinsia  kutoka Shirika la Plan International akielezea nia yao kubwa ya kushiriki katika Sherehe hizo Leo.
<![endif]-->Gloria Chambo mwanachama  wa chama cha Muunganiko wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ambaye ndiye alikuwa mshereheshaji wa Siku hiyo ya wanawake akizungumza Jambo wakati wa Sherehe hizo na kuongoza ratiba hiyo.


 Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali kutoka Jijini Dar es salaam wakiwa wanafuatilia mambo mbalimbali yanayo endelea wakati wa sherehe hizo
 Hawa ni wanafunzi wa Chuo cha ufundi kwa watu wenye ulemavu walemavu wa jumla, wakiwa wanafuatilia kwa umakini kinacho endelea uwanjani hapo
 Msichana mfupi Mbele ni Mwanafunzi wa  Chuo cha ufundi kwa watu wenye ulemavu Jovina Vedastus  ambaye ni Fundi wa Ushonaji na utengenezaji wa Batiki akicheza muziki ambapo alikonga nyoyo za watu wengi kwa umahili wake huo katika kucheza
 Wasemaji wakifurahia Burudani mbalimbali zinazo endelea
 wanafunzi wa Chuo cha ufundi kwa watu wenye ulemavu walemavu wa jumla, hapa wakiwa viziwi, wasio ona, wenye ulemavu wa Miguu , mikono mapoja na Matatizo mengine wakiwa wanatumbuiza na burudani ya aina yake ambapo watu wengi walivutiwa sana na kufurahishwa.
 Banana Zoro akitoa Burudani ya uhakika pamoja na Bendi yake wakati wa maadhimisho hayo.
 Mwakilishi kutoka OXFAM ambao pia ni wanachama wa  chama cha Muunganiko wa mashirika yasiyo ya Kiserikali  Afisa utetezi wa haki  za kiuchumi OXFAM Bi.Mkamiti Mgawe  akifunga Rasmi sherehe hizo na kuwashukuru wote waliofika katika katika sherehe hizo zilizofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu jijini Dar es salaam leo.
 Hili lilikuwa ni Tukio la Aina yake ambapo Miss Tanzania 2013 Happy Watimanywa alipo vamiwa na wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Sekondari Jijini Dar es salaam wakiomba awasainie katika Madaftari yao kama kumbukumbu ya kwamba na wao walisha wahi kumuona Mrembo huyo, Hapa akiwa anasaini katika Baadhi ya Madaftari hayo.


MEYA WA ILALA JERRY SILAA AVAMIA KALENGA,AMPIGIA DEBE LA NGUVU MGOMBEA UBUNGE WA CCM

MAMA ALIYETOROKA NA MTOTO ALIYEUNGUA NA MOTO APATIKANA NJOMBE, NI BAADA YA TAARIFA HIZI KUSAMBAA.

$
0
0
Hatimaye Mama aliyetoroka na mtoto aliyeungua moto apatikana kupiga  simu katika Chombo cha Mbeya yetu Blog  kuwa yupo Njombe kwa baba mzazi wa mtoto huyo nakuomba radhi kuwa aliondoka bila kuaga kesho saa nane mchana atakuwa amerudi na mtoto huyo 


Mama huyo amejitokeza baada ya mtandao wa Mbeya yetu kuandika mapema leo kwamba alikuwa ametoweka bila Taarifa zozote, Akiongea na Mbeya yetu amedai kwamba yeye aliondoka ili akashauriane na wazazi wa Mtoto huyo ili waone ni jinsi gani watamsaidia lakini alipo hojiwa amejikanyaga kanyaga na kuongea bila kuwa na uhakika na kile anacho zungumza.


Hata hivyo hapo kesho atafanyiwa mahojiano ya kina na kuona ukweli ukowapi kwa kuwa anatia mashaka na maelezo yake, Tunaendelea kusisitiza kuwa Kama kuna Mtu anahitaji kumchangia mtoto huyo asifanye hivyo kwa kuwa mama huyo kasha onesha wasiwasi na kuondoa imani watu.

Habari zaidi zitakuja.
Huyu ndiye Mama Mkubwa wa Mtoto Adolotea Nyavike bi. Salome Kiegu(35) ambaye alitoweka  na mtoto huyo kusiko julikana huku wasamalia wema wakitaka kutoa misaada.
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images