Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

MCHEPUKO WA POSHO WA BUNGE LA KATIBA


Milioni 50 za Airtel ‘Mimi ni Bingwa’ kutolewa Ijumaa

$
0
0
 KAMPUNI ya mawasiliano ya Airtel Tanzania Ijumaa hii itachezesha droo kubwa ya promosheni yake ya 'Mimi Ni Bingwa' ambayo itamfanya mmoja wa wateja wake kujishindia zawadi ya kitita cha shilingi milioni 50.

 Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde alisema droo hiyo itakayobadilisha maisha ya mtu, imepangwa kuchezeshwa katika ofisi za makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.

 "Baada ya miezi kadhaa iliyojaa zawadi kwa wateja wetu waaminifu, Ijumaa hii itakuwa ndiyo kilele cha promosheni yetu ya Mimi Ni Bingwa ambapo tutamtafuta na kumtangaza mshindi wa zawadi yetu kubwa," alisema.

 Jane alisema kuwa mshindi atakayebahatika atapatikana kwa kuchezesha droo ya bahati na sibu utakaokuwa chini ya uangalizi na usimamizi wa afisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania na kushuhudiwa na  wafanyakazi wa Airtel na vyombo vya habari.

 "Ningependa kuwashukuru wateje wetu kwa kushiriki promosheni hii na kuwakumbusha wateja wote wa Airtel ambao bado hawajajiunga na mchezo huu kwamba bado wanaweza kujiunga na wanaweza wakawa na bahati ya kushinda zawadi kubwa ya shilingi milioni 50 kwa sababu wote waliojisajili katika promosheni wataingizwa katika droo hii kubwa na ni namba moja tu itakayobahatika,Hii ina maana kuwa kadri uchezavyo ndipo unapata nafasi kubwa ya kuibuka mshindi,” alisema.

 Alisema kuwa wakati wa promosheni, wateja wa Airtel walijishindia pesa taslim ya zaidi ya shilingi milioni 324 na zaidi ya tiketi 36 kwa ajili ya safari iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda kuangalia  mechi ya klabu ya Manchester United katika uwanja wa Old Trafford zilitolewa.

"Promosheni ya Airtel ‘Mimi Ni Bingwa' imeweza kubadilisha maisha ya wateja wake kwa kuwazawadia zaidi ya shilingi milioni 324 pesa taslim na kuwapa watanzania 36 nafasi ya kipekee katika maisha yao ya kuitembelea klabu kubwa ya soka ulimwenguni ya Manchester United pamoja na kuitembelea uwanja wao wa Old Trafford na pia kuwa sehemu ya mashabiki wa soka wanao angalia mechi ya Manchester United moja kwa moja ‘live’ uwanjani," alisema.

 “Kwa mara nyingine tena, hii ni nafasi kwa wateja wengine wa Airtel ambao hawakujisajili kwenye promosheni kuingia kwa kutuma ujumbe mfupi (SMS) wenye neno “BINGWA” kwenda namba 15656, na kujibu maswali mengi iwezekanavyo, unaweza jishindia zawadi kubwa ya pesa taslim ya shilingi milioni 50,” alisema.

 Promosheni ya Airtel ‘Mimi ni Bingwa’ iliyoanza mwezi Novemba mwaka jana, ni matokeo ya ushirika baina ya klabu ya Manchester United na kampuni hii ya mawasiliano, ambayo hailengi tu kuwazawadia wateja wake pekee lakini pia kuwaunganisha washiriki wa promosheni hii na soka la kimataifa ambapo itasaidia kuamsha ari ya michezi miongoni mwa watanzania, hasa katika soka.

 Wakati wa promosheni hiyo, washindi wawili wa Mimi Ni Bingwa walijishindia zawadi ya shilingi milioni moja kila moja kwa kila siku, washindi wawili walijishindia zawadi ya shilingi milioni 5 kila mmoja kila wiki na mshiriki mmoja alikuwa anajishindia tiketi mbili kila wiki kwa ajili ya safari iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda Old Trafford.

 Kundi la awamu ya kwanza la washindi wa tiketi tayari walifurahia safari yao na imebainisha kuwa kundi la pili na la tatu watasafiri kwenda Manchester ifikapo mwezi Machi wakati Manchester United ikitarajiwa kucheza tena katika uwanja wake wa Old Trafford.

WANAFUNZI WA CHUO CHA TAIFA CHA UTALII WATEMBELEA TBL DAR

$
0
0
Msimamizi wa Gharama za Malighafi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emmanuel Sawe (wa pili kushoto), akitoa maelezo kuhusu mitambo ya kutengeneza bia wakati wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Utalii walipotembelea Kiwanda cha TBL, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ikiwa ni sehemu ya mafunzo yao.
SAWE AKIWAONESHA WANAFUNZI AINA YA MALIGHAFI YA HOPS INAYOTUMIKA KUTENGENEZEA BIA
Wanafunzi wakipata maelezo kutoka kwa Sawe kuhusu upikaji wa bia kwa njia ya kisasa
Msimamizi wa Gharama za Malighafi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emmanuel Sawe (kulia), akitoa maelezo jinsi bia inavyopikwa  kwa kutumia njia ya kisasa ya kompyuta wakati wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Utalii walipotembelea Kiwanda cha TBL, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ikiwa ni sehemu ya mafunzo yao.
Wanafunzi wakiwa maabara ya kiwanda hicho

Msimamizi wa Gharama za Malighafi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emmanuel Sawe (kulia), akitoa maelezo kuhusu mitambo ya kuchachua bia wakati wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Utalii walipotembelea Kiwanda cha TBL, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ikiwa ni sehemu ya mafunzo yao.
Msimamizi wa Gharama za Malighafi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emmanuel Sawe (kulia), akitoa maelezo jinsi mitambo ya kuchuja bia inavyofanyakazi wakati wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Utalii walipotembelea Kiwanda cha TBL, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ikiwa ni sehemu ya mafunzo yao.
Mtambo wa kufunga bia za kopo kwenye makasha.


                                                                        Bia zikiwa tayari
Makret ya bia yakiwa tayari kiiwandani hapo
Msimamizi wa Gharama za Malighafi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emmanuel Sawe (wa pili kulia) akiwa na Mkufunzi wa Chuo cha Taifa cha Utalii, Nassoro Sekiuye (kulia kwake) pamoja na  wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Utalii walipotembelea Kiwanda cha TBL, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ikiwa ni sehemu ya mafunzo yao.

AFTER PARTY YA LADY IN RED YAFANA

$
0
0
DSC_0549
Mama wa Mitindo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fabak Fashions na wandaaji wa onyesho la Lady in Red, Bi. Asia Idarous Khamsin akizungumza na wadau tasnia ya mitindo waliojumuika kwenye After Party ya kuwashukuru wadau waliotoa michango mbalimbali tangu kuanza kwa onyesho la Lady in Red nchini Tanzania.
...Ally Rehmtulla, Martin Kadinda watunukiwa vyeti vya mafanikio

Na Andrew Chale
HALFA maalumu ya kilele cha Miaka 10 ya onesho la mavazi la ‘Lady in Red Super Brand’ usiku wa Jumamosi Februari 22, lilikuwa la aina yake kwa kuvutia watu mbali mbali ndani ya Ukumbi na mgahawa wa kisasa wa Nyumbani Lounge, ambapo pia wadau walikabidhiwa vyeti.
Tukio hilo la aina yake ambalo lilivuta umati mkubwa wakiwemo wadau wa ubunifu na mitindo nchini pamoja na watu maalufu, Pia walipata kupita kwenye zuria jekundu (red carpet) na kupata picha za ukumbusho wa tukio hilo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Fabak Fashions na wandaaji wa onyesho hilo kila mwaka, Asia Idarous Khamsin, aliwashukuru wadau waliojitokeza kwenye halfa hiyo maalumu na kutoa vyeti kwa watu na taasisi zilizoweza kuliunga mkono onyesho hilo pamoja.
DSC_0572
Mama wa Mitindo Bi. Asia Idarous Khamsin akipozi wakati wa zoezi la kugawa vyeti na models waliovaa mavazi yaliyoonyeshwa kwenye onyesho la kutimiza miaka 10 la Lady in Red lililofanyika hivi karibuni.

“Tunamshukuru Mungu kwa kufikisha Miaka 10 ya Lady in red, hadi kufikia hapa, tumeweza kufanya mambo makubwa katika tasnia hii ya ubunifu wa mavazi na jukwaa hili litaendelea kuwa chachu ya mafanikio zaidi na zaidi” alisema Asia Idarous.

Na kuongeza kuwa, jukwaa hilo ndilo pekee lililoweza kuibua wabunifu wakubwa hapa nchini huku wengine wakipeperusha vyema bendera ya Tanzania nje ya nchi, wabunifu hao ni pamoja na Ally Rehmtullah, Martin Kadinda, Ahmed Abdul, Faustin Simon.
DSC_0577
Mwanamitindo wa siku nyingi Fiderine Iranga akipokea cheti kutoka kwa Mama wa mitindo Asia Idarous Khamsin kwa kutambua mchango wake katika tasnia ya mitindo nchini.
Wengine ambao nao wanachipukia kwa sasa akiwemo Salim Ally, Salim Ally, Abdul Mwene,Baby Julieth, Baby Masai na wengine wengi.

Asia Idarous alibainisha kuwa, wapo mbioni kuliboresha jukwaa hilo na kuwa la Kimataifa ikiwemo kushirikisha wabunifu wa kimataifa na kufungua milango kwa wabunifu wa ndani kujiuza kimataifa.
DSC_0581
Mwanamitindo mkongwe Fiderine Iranga akimkabidhi zawadi Mama wa Mitindo Bi. Asia Idarous kwenye After party ya kuwashukuru wadau waliofanikisha sherehe za kutumiza miaka 10 ya onyesho la Lady in Red iliyofanyika mwishoni mwa juma kwenye kiota cha Nyumbani Lounge jijini Dar.

Aidha, katika halfa hiyo pia wageni na wadau waliofika walipata kushuhudia shoo fupi ya mavazi yaliyobuniwa na Lucy Warere wa Tifu tifu fashions, Beda Masai na Asia Idarous Khamsini. Asia Idarous aliwataja wadhamini waliodhamini halfa hiyo ni pamoja na Times fm, Michuzi media group, MOblog, DTV, Nyumbani Lounge, Darling air, G one Media, Channel Ten, CTN na wengine wengi.
DSC_0587
Mbunifu wa Mavazi nchini Ally Rehmtullah akipokea cheti cha shukrani ya ushiriki wa onesho la Lady in Red kutoka kwa Mama yake Mlezi Asia Idarous Khamsin.


DSC_0601
Cake ya After Party ya Onesho la Lady in Red iliyoandaliwa maalum kwa kuwashukuru wadau mbalimbali waliofanikisha sherehe za miaka 10 ya Lady in Red nchini.
DSC_0602
Honest Arroy wa 360 Degrees akikata cake kwa niaba ya wadau kwenye After Party ya Lady in Red iliyofanyika mwishoni mwa juma kwenye kiota cha Nyumbani Lounge.
DSC_0617
Model Richard akililishwa kipande cha cake na Mama wa Mitindo Asia Idarous Khamsin kama shukrani ya kushiriki maonyesho mbalimbali ya Lady in Red.
DSC_0619
DSC_0621
Wadau mbalimbali waliojitokeza kwenye After Party ya kusheherekea miaka 10 ya Lady in Red wakitazama matukio mbalimbali kwenye luninga ndani ya kiota cha Nyumbani Lounge.
DSC_0645
Mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima, Andrew Chale akilishwa kipande cha cake na mmoja wa Models kwenye After Party ya kuwashukuru wadau waliofanikisha tangu kuanzishwa onesho la Lady in Red mpaka leo hii kutimiza miaka 10 kwenye tasnia ya mitindo nchini.
DSC_0631
Wadau wakiwa wamepozi kwenye kiota cha Nyumbani Lounge wakati wa After Party ya Lady in Red iliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar.
DSC_0662
Mdau akipata Ukodak na Models.
DSC_0683
Mama wa Mitindo nchini Asia Idarous Khamsin akipata ukodak na mwanamitindo Mustafa Hassanali kwenye After Party ya kuwashukuru wadau walioshiriki kwenye onesho la Lady in Red lililotimiza miaka 10 hivi karibuni.

WAMILIKI WA MAENEO YA BIASHARA WAOMBWA KUTOA KIPAUMBELE KWA WANAWAKE WAJASIRIMALI

$
0
0
DSC_0935
Mwenyekiti wa Tancraft, Elihaika Mrema akizungumza na waandishi wa habari umuhimu wa jumuiya kubwa za wafanyabiashara na pamoja na serikali kuwaunga mkono wajasirimali wanawake nchini, Kushoto ni Esther Kasenga Msaidizi wa Katibu, Kulia Mweka hazina wa Chama cha Tancraft, Bi.Louise Judicate na Wapili kulia ni Katibu wa Tancraft, Bi. Vicky Shayo.
=========  =======  ======
Na Damas Makangale, MOblog Tanzania.
WAMILIKI Wote wa maeneo ya biashara nchini wameombwa kutoa nafasi ya maeneo ya biashara kwa wajasirimali wanawake ili kumkomboa mwanamke kutoka katika dimbwi la umaskini na utegemezi. MOblog inaripoti.

Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wajasirimali wanawake jijini Dar es Salaam leo mchana, Mwenyekiti wa Tanzania Handcraft Association (Tancraft), Elihaika Mrema amesema kuwa wanawake wafanyabiashara wadogo wana matatizo na changamoto kadhaa mojawapo ni maeneo ya kuuzia bidhaa zao.
DSC_0939
Pichani juu na chini ni Baadhi ya Wajasiriamali Wanawake wakifuatilia hotuba ya mwenyekiti wa TANCRAFT Bi. Elihaika Mrema alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika jengo la Biashara la DAR FREE MARKET lililopo barabara ya Ali Hassan Mwinyi karibu na Ubalozi wa Kenya nchini.

“hata kama mjasirimali mwanamke ukimpa mtaji wa biashara na mafunzo changamoto kubwa ni kupata eneo la kuweza kuuza hiyo bidhaa yake aliyotengeneza kwa mikono yake mwenyewe,” amesema Mrema.

Mwenyekiti, Mrema amesema kuwa chama cha Tancraft kilianzishwa mwaka 2006 chini ya usimamizi wa Board of External Trade (BET) na Small industrial Development Organization (SIDO) na kina wanachama zaidi ya 300 kutoka mikoa yote Tanzania.




DSC_0937DSC_0967
Hii ni moja ya zawadi ya kikombe kwa Chama cha Wajasiriamali Wanawake Tanzania (TANCFRAFT) walichowahi kupata kwa kuonyesha bidhaa zenye ubora wa kimataifa.
Amesema kuwa Tancraft ni chama cha wajasirimali wanaotengeneza bidhaa kwa kutumia mali ghafi za kutoka nchini kama vile nguo za batik, vikapu, minyaa, vitu vya ufinyanzi,vinyago, shanga, bidhaa za ngozi, chakula na usindikaji wa aiana zote zikiwemo asali.
“malengo makuu ya chama yalikuwa ni pamoja na kuwatafutia wanachama wake soko la pamoja kwa ajili ya kuuzia bidhaa zao,” alilisisitiza Mrema
Amesema kwamba chama cha wanawake wa wajasirimali kimepata sehemu ya Dar es Salaam Free Market ambapo wajasirimali wakinamama watapata fursa ya kufanya biashara zao bila kulipa ushuru kama walivyokuwa katika maeneo ya Chang’ombe mikono.
DSC_0849
Mkurugenzi Mtendaji wa J & L Enterprises, Bi. Louise Judicate Mushi, akitoa maelezo ya bidhaa zake za mchai chai za aina mbili black na green tea na mishumaa, amesema kwamba Green Tea ni mchai chai wa kijani kabisa ambao umesagwa kwa matumizi bora kwa afya ya binadamu
Amesema uzuri wa kinywaji hicho unaweza kunywa kikiwa cha moto au baridi, mchai chai ni dawa ya kushusha sukari, homa, presha, misuli na sumu za mwilini.
DSC_0859
Mkurugenzi Mtendaji wa J & L Enterprises, Bi. Louise Judicate Mushi akimuonjesha aina ya chai mmoja wa waandishi wa habari kutoka kituo cha Channel Ten Bw. Salum Mkambala.
DSC_0874
Mjasiriamali Fatuma Amour kutoka kampuni ya Famour Designer, akizungumzia ubunifu wake wa mavazi na ujasirimali utengenezaji wa nguo za wakinamama na wakinababa na Carpet za ngozi, viatu vya ngozi, vikapu na Batiki. Fatuma amesema alianza biashara miaka karibu 12 iliyopita katika biashara yake ya vitu vya asili vya kiafrika na changamoto kubwa kwake ni kujitangaza. Kushoto ni mwandishi wa habari kutoka Mwananchi Communications, Bi. Maimuna Kubegeya.
DSC_0871
Maimuna Kubegeya akiangalia moja ya bidhaa zinazotengenezwa na Mjasiriamali Fatuma Amour kwenye jengo la Biashara la DAR FREE MARKET lililopo barabara ya Ali Hassan Mwinyi karibu na Ubalozi wa Kenya nchini ambapo watakuwa hapo kwa muda wa mwaka mmoja.
DSC_0886
Mwandishi wa kituo cha Televisheni cha ITV, Fatma Almasi, akiangalia moja ya bidhaa zinazotengenezwa na Batiki. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Tancraft, Elihaika Mrema na wa tatu kulia ni Mwandishi wa habari kutoka kituo cha Televisheni cha Channel Ten Bw. Salum Mkambala.
DSC_0902
Baadhi ya Wajasiriamali wa DAR FREE MARKET wakionyesha bidhaa zao. Watanzania tuwaunge mkono wenzetu!
DSC_0878
DSC_0844
DSC_0978
Baadhi ya Wajasiamali Wanawake Tanzania wakionyesha moja ya kazi za Uchoraji za Ujasiriamali kwa wageni waalikwa baada ya Chama cha Wanawake Wajasiriamali Tanzania (TANCRATF) kuandaa mkutano na waandishi wa habari. Kulia ni Glory Matafu na kushoto ni Jacqueline Polycarp.
DSC_0973
Picha hii inauzwa Shilingi Milioni 1.2 inapatikana kwenye Jengo la Biashara la DAR FREE MARKET lililopo barabara ya Ali Hassan Mwinyi karibu na Ubalozi wa Kenya nchini ambapo wajasiriamali hao wanafanya biashara zao hapo kwa muda wa mwaka mmoja.
DSC_0981
Fatuma Amour kutoka kampuni ya Famour Designer akionyesha moja ya kazi za mikono yake.

Mkutano wa Wataalamu wa Nchi Zinazoendelea

$
0
0
 Mgeni Rasmi Bi. Angelina Madete (Wa tatu kutoka kushoto - waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu kutoka nchi mbalimbali, mara baada ya kufungua mkutano wa siku tatu wa kujadili changamoto za mabadiliko ya tabianchi kwa nchi zinazoendea
Bi. Pepetua Latasi (kulia) Mwenyekiti wa Kamati ya wataalamu washauri kwa nchi zinazoendelea akiongoza kikao cha siku tatu katika Hotel ya Cotyard jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Bw. Motsomi Maletjane kutoka sekretariet ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya tabianchi (UNFCCC).

=========  =======   ======= 
Katika jitihada za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, Tanzania kwa mara ya kwanza imekuwa mwenyeji wa mkutano wa wataalamu wa Nchi zinazoendelea dunia (Least Developed Countries Expert Group – LEG).

Akifungua Mkutano huo, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Angelina Madete amesema kuwa ni fursa nzuri kwa Nchi ya Tanzania kuratibu Mkutano huu na kutoa wito kwa Nchi zinazoendelea kupunguza uzalishaji wa gesi joto ambazo kwa kiasi kikubwa zinachangia athari za mabadiliko hayo.


Bi. Madete amesema kuwa athari za mabadiliko ya tabianchi ni kubwa katika nchi zinazoendelea hususan kiuchumi na kijamii na kupelekea ongezeko la umaskini. Maeneo yanayoathirika zaidi kwa sasa ni katika Nyanja za kilimo, uvuvi, ufugaji na maisha ya kila siku kwa jamii za mijini na vijijini katika nchi zinazoendelea.


Aidha, Bi Madete amesisitiza kuwa jitihada za pamoja zinahitajika katika kuhakikisha masuala ya mabadiliko ya tabianchi yanajadiliwa na kupatiwa ufumbuzi hususan katika nchi zinazoendelea.


Mkutano huo wa siku tatu unalenga kujadili Mipango ya Kitaifa ya Kuhimili Mabadiliko ya tabianchi (National Action Plans – NAP), changamoto na athari za mabadiliko ya tabianchi katika nchi zinazoendelea.


Kwa upande mwingine Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais  - Mazingira Bw. Richard Muyungi amesema kuwa Nchi zinazoendelea zinaathirika zaidi na Mabadiliko ya tabianchi kutokana na uzalishaji unaofanywa na nchi zinaoendea na pia uwezo mdogo wa nchi hizo katika kuyakabili na kuyahimili mabadiliko hayo. Katika Mkutano huu wa siku tatu, nchi wanachama watabadilishana uzoefu wa jinsi ya kukabiliana na changamoto hizo na kuainisha vyanzo vya mapato.


Mikutano hii ya LEG inaendeshwa ikiwa ni moja ya makubaliano katika mikutano ya kila mwaka ya mabadiliko ya tabianchi ambayo hujulikana kama Conference of Parties – COP. Nchi wanachama wa UNFCCC wanapaswa kuandaa Mpango kazi wa Kitaifa wa Kuhimili mabadiliko ya tabianchi (NAPA) na Tanzania ilikwisha andaa mpango kazi huu tangu mwaka 2007.


Ili kurahisisha utekelezaji wa mpango kazi huu nchi wanachama pia wanatakiwa kuandaa mipango kazi katika wizara za kisekta . Mkutano huu umekutanisha wataalamu kwa lengo la kutoa muongozo na maelekezo katika kuandaa mipango kazi hii. Mkutano huu umeandaliwa na Sekretarieti ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya tabianchi (UNFCCC) kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais. Mkutano huu umewakutanisha wajumbe zaidi ya hamsini kutoka nchi mbalimbali Duniani.

Na Lulu Mussa

Afisa Habari

Ofisi ya Makamu wa Rais

Dar es Salaam

Kumekucha Tamasha la Kimataifa la 33 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo

$
0
0
 Kikundi cha Sanaa cha TaSUBa wakifanya vitu jukwaani kwenye moja ya tamasha hilo 2013. jukwaani
 Moja ya kikundi cha Sanaa cha acrobat kikionyesha uwezo wao wa sanaaa hiyo 2013
 Moja ya mchezo wa igizo la hisia kali, lililofanywa na walimu wa chu cha sanaa Bagamoyo 2013
moja ya vikundi vya kigeni kutokka Norway kikiwajibika jukwaani 2012
========   =======  ========
Kumekucha Tamasha la Kimataifa la 33 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo
 
 ...Kufanyika Septemba 22 hadi 28
…Vikundi zaidi ya 40 vinatarajiwa kutoa burudani
….wadau na wadhamini milango ipo wazi sasa

 Na Andrew Chale, Bagamoyo
TAMASHA la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo ambalo kwa mwaka huu (2014) litakuwa la 33, ambapo linatarajia kulindima kwa siku saba, kuanzia Septemba 22 hadi 28, kwenye viunga vya  Chuo cha Sanaa Bagamoyo.
 
Tamasha hilo la 33, mwaka huu, lenye kauli mbiu, “Sanaa na Utamaduni katika kukuza Utalii”,  limekuwa msaada mkubwa  kwa wasanii na vikundi mbali mbali kujitangaza kitaifa na kimataifa pamoja na kutoa fursa za kibishara katika kipindi chote cha tamasha.
 
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tamasha hilo, Abraham Bafadhil ‘Bura’, alieleza kuwa, tayari mipango  na maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea katika kufikia malengo  huku akiwaomba wadau kujitoakeza na kudhamini tamasha hilo.
 
 “Milango ipo wazi hivyo, kwa wadhamini kujitokeza na kuchangamkia fursa hii hadimu, kwani tamasha hili ni kongwe katika ukanda huu wa Afrika ya Mashariki na Afrika kwa ujumla” alisema Bura.
 
Na kuongeza kuwa,  tamasha hilo lenye mvuto wa kipekee ndani na nje ya Tanzania, limekuwa likipata umaarufu mkubwa kila mwaka kutokana na idadi kubwa ya watazamji wa ndani na wale wa kutoka Mataifa mbali mbali duniani.
 
Kwa upande wake, Katibu wa tamasha hilo, Benjamini Mahimbali alieleza kuwa, tamasha hilo limekuwa na mafanikio ikiwemo ongezeko kubwa la watazamaji na vikundi vinavyoomba kufanya maonyesho.
 
“Idadi ya watazamaji na imekuwa ikiongezeka kila mwaka, huku kwa mwaka jana tulikuwa na wastani wa watazamaji elfu nne mia saba kwa siku (4,700), ikiwemo wa rika zote.” Alisema Ben.
 Na kuongeza kuwa, wanatarajia ongezeko hilo kuwa kubwa zaidi kutokana na maboresho na mipango mbali mbali inayotarajiwa kufanyika mwaka huu.
 
Katika tamasha hilo maonyesho mbali mbali yanatarajiwa kuonyeshwa ikiwemo; Muziki wa aina tofauti, ngoma, maigizo, sarakasi, mazingaombwe na maonyesho kemkem ya sanaa na utamaduni wa Mtanzania na ya Mataifa mengine duniani.
 
Kwa upande wa fomu za kushiriki tamasha hilo ambalo kwa mwaka huu wanatarajia kupokea vikundi zaidi ya 40,  zinatarajiwa kutolewa kwenye ofisi za Chuo hicho pamoja na tovuti ya chuo (www.tasuba.ac.tz)
 
Au Kwa mawasiliano na maulizo juu ya ushiriki na udhamini waweza kufika Chuo cha Sanaa Bagamoyo (TaSUBa)  au kupitia  namba;

MTEMVU ACHANGIA SH.IL. MOJA VICOBAYA MASHINE YA MAJI TEMEKE

$
0
0
 Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (aliyevaa miwani) akilakiwa na wanachama wa Masdhine ya Maji Vicoba alipowasili kwa ajili ya sherehe ya kuitunisha mfuko wa Vicoba hiyo iliyopo Temeke, Dar es Salaam. Mtemvu alichangia sh. mil. 1. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
 Mtemvu akimkabidhi Agnes Mangula cheti cha kuhitimu mafunzo ya uwezeshaji wa mpango wa VICOBA wakati wa hafla hiyo
 Mwanachama Novatus Sambi akikabidhiwa cheti baada ya kuhitimu mafunzo hayo
 Mtemvu akihutubia wakati wa hafla hiyo ambapo aliwaasa viongozi kutofuja fedha za VICOBA na kwamba atakayethubutu atatiwa ndani na kutakiwa kurejesha fedha.
 Mtemvu akihesabu fedha tayari kuichangia VICOBA hiyo ya Mashine ya Maji
 Mtemvu akikabidhi mchangio wake
Mmoja wa wageni waalikwa kwenye hafla hiyo akitoa ahadi ya mchango

UZINDUZI WA ALBAMU YA EXTRA BONGO: RED CARPET YA DAR LIVE!

$
0
0
Baadhi ya safu ya wanenguaji mahiri wa kiume wa Extra Bongo.
Amini akishoo Love na Linah (kushsoto) pamoja na mwimbaji wake.
Baadhi ya safu ya wanenguaji wa kike mahiri wa Extra Bongo.


Wanenguaji katika pozi poa.
Khadija Kopa na Abdul Misambano wa TOT.
Khadija Kopa, Misambano na 'Okwi' shabiki wa Yanga.
Lina na 'back-up singer' wake.
Mamaa Winnie Masanja, mama watoto wa mwanamuziki Banza Stone.
Mke wa 'Mkubwa' Said Fela (kulia).
Mmoja wa wanamuziki wa Mashujaa Band, Gado.
TX Moshi Jnr wa Msondo Music Band.
Wadau wa Dar Live.
Wasanii Linah na Amini.

(Picha: Abdallah Mrisho/GPL)

Serikali kubadili mfumo wa uzalishaji ili kuleta tija katika sekta ya kilimo

$
0
0
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Chiza akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu mikakati mbalimbali ya wizara yake katika kuendeleza sekta ya kilimo nchini. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Raphael Daluti na kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Assah Mwambene.

                                                        
Na Georgina Misama- MAELEZO.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imelenga kubadili mfumo wa uzalishaji ili kuleta tija katika sekta ya kilimo. Hayo yamesemwa na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Chiza, wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar Es Salaam.

Waziri Chiza alisema kuwa katika mfumo huo maeneo makuu matatu ya kipaumbele, ambayo ni kuwepo kwa mashamba makubwa ya uwekezaji yapatayo 25 kwa ajili ya kilimo cha mpunga na Miwa, kuwa na skimu za umwagiliaji 78 kwa ajili ya kilimo cha mpunga na maghala 275 ya mahindi kwa kutumia mfumo wa pamoja.

“Ili kuendana na kasi ya mfumo wa matokeo makubwa sasa, Serikali imeajapanga kuondokana na kilimo cha mazoea na kujikita kwenye kilio cha kisasa hasa kwenye mazao ya kipaumbele ambayo ni mpunga, miwa na mahindi” alisema Waziri Chiza.

Waziri Chiza alifanunua kuwa Serikali imejikita kwenye uzalishaji wa mazao hayo ili kukabiliana na changamoto zilizo kwenye sekta hiyo ikiwemo  mfumuko wa bei.

Ili kukabiliana na upungufu wa chakula katika baadhi ya maeneo nchini Waziri Chiza alisema kuwa Serikali imeidhinisha tani 23,312 za chakula cha msaada ili kisambazwe kwa waathirika 828,063 ambao walionekana kuwa na upungufu wa chakula katika wilaya 54 za mikoa 16.

Hifadhi ya Taifa ya Chakula hivi sasa ina tani 226,769.544 ambapo tani 226,270.862 ni za mahindi na tani 498.682 ni za mtama, ambapo kiasi hicho kinajumuisha tani 25,452.644 za mahindi kutoka msimu uliopita

WAZIRI NYALANDU AKUNJUA MAKUCHA ,AWANG'OA VIGOGO IDARA YA WANYAMAPORI

$
0
0


 Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu leo ametangaza kuwang'oa vigogo wa ngazi ya juu katika Idara ya wanyamapori akieleza kuwa ni kutokana na kutoridhishwa na utendaji wao. 


Ifuatayo ni Taarifa rasmi ya tamko la Waziri Nyalndu,  kama alivyolisoma leo:
Leo, TAREHE 24 Februari, 2014 Natangaza kuubadili uongozi wa Idara ya Wanyamapori ya Wizara ya maliasili na Utalii kama ifuatavyo: 

Ninamuondoa Profesa Alexander Songorwa katika nafasi ya Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori ya Wizara ya Maliasili na Utalii.  

Nachukua hatua hii kutokana na kutokuridhishwa kwangu na utendaji wa kazi wa idara hiyo katika mapambano dhidi ya ujangili yanayoendelea nchini.
Aidha, hatua hii ni utekelezaji wa Azimio la Bunge lililotolewa tarehe 22 Disemba, 2013, lililotaka Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori kuwajibishwa kutokana na tuhuma za uzembe na ukiukwaji wa haki za binadamu katika Operesheni Tokomeza.  Utekelezaji wa agizo hili unaanza mara moja, nami namteua Bwana Paul Sarakilya kukaimu nafasi hiyo ya Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori ya Wziara ya Maliasili na Utalii kuanzia sasa. 

Aidha, ninamuondoka Profesa Jafari Kidegesho katika nafasi ya Mkurugenzi Msaidizi wa Matumizi Endelevu ya Wanyamapori na kumteua Dr. Charles Mulokozi kuchukua nafasi hiyo.  Hali kadhalika, ninamteua Bwana Julius Kibebe kuwa Mkurugenzi Msaidizi Uzuiaji – Ujangili na anachukua nafasi ya anayeenda kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Wanyamapori. 

Vilevile, Bibi Nebbo Mwina anaendelea kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo, Utafiti na Takwimu, na Bwana Herman Keiraryo anaendelea kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Uendelezaji wa Wanyamapori. Pamoja na Kitengo cha Uzuiaji – Ujangili nilichokitaja awali, hivi ni vitengo vya Idara ya Wanyamapori katika Wizara ya Maliasili na Utafiti. 

Nawaagiza kwamba Wakurugenzi na Wakuu wote wa kila Idara, kila Shirika, na Taasisi zote ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii kutengeneza viashiria muhimu vya utendaji kazi (Key Performance Indicators) na kukabidhi kwangu ndani ya siku 30 zijazo.  

Viashiria hivi ni hatua ya kufanikisha yafuatavyo, 1)  Malengo ya wizara, 2)  Uwajibikaji, 3) Uwazina 4) Ufanisi katika utendaji wa kazi za kila siku.  Ni sharti tutekeleze mikakati ya wizara katika mifumo inayopimika, tuweze kujipima natuweze kupimwa, natutumikie Taifa kwa uadilifu. 

Kwa mtumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii ikiwemo mimi mwenyewe, Lazaro Nyalandu, atapaswa kuzingatia na kutekeleza majukumu ya kazi kwa kuzingatia Kanuni za Mwenendo (Code of Conduct) ambazo zitapendekezwa na kupitishwa na Baraza la Wafanyakazi wa Wizara. 

 Baraza hili liwe limeitishwa na Katibu Mkuu wa Wizara kabla ya mwisho ya mwezi ujao.  Azma ya kanuni hizi ni kuwa na misingi bora ya utumishi, uwajibikaji, utu, usawa na haki katika utekelezaji wa majukumu yetu ya kila siku.

 Mungu ibariki Tanzania.
Asante.
 Lazaro S. Nyalandu (MB)
Wizara ya Maliasili na Utalii
24/02/2014

MISAADA KWA YATIMA NA MAPACHA WANNE YAFIKA SALAMA MBEYA

$
0
0

Aida Nakawala (25) mkazi wa kijiji cha Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya, ambaye alijifungua watoto wanne kwa mkupuo (Quadruplets) usiku wa kuamkia Mwaka mpya wa 2014 katika Hospitali ya Wazazi ya META jijini Mbeya.

Misaada  toka kwa  Bi Gladness Sariah wa Uingereza,  Dar es salaam kwa Norah SilverBoutique 
Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu akiwakilisha msaada toka kwa familia ya mama Masawe wa DSM kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha NURU kilichopo Uyole, mkoani Mbeya.
-----------------------
Kituo cha Mtandao wa kijamii cha Mbeya Yetu (www.mbeyayetu.blogspot.com) kimepokea Misaada mbalimbali kutoka kwa wasamaria wema kwa ajili ya Kituo cha kulelea watoto wa mitaani cha Nuru kilichopo Uyole Jijini Mbeya na  Aida Nakawala (25) mkazi wa kijiji cha Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya, ambaye alijifungua watoto wanne kwa mkupuo (Quadruplets) usiku wa kuamkia Mwaka mpya wa 2014 katika Hospitali ya Wazazi ya META jijini Mbeya.
Msaada wa kwanza ulipokelewa hivi karibuni wenye thamani ya shilingi Laki Moja kutoka Familia ya Masawe wa Dar es salaam kwa ajili ya kituo cha Nuru ambapo Mbeya yetu iliuwasilisha kama ulivyo.

Mbali na msaada huo pia Mtandao huu ukishirikiana na mtandao wa kijamii wenye makao yake makuu Jijini Dar es salaam wa www.issamichuzi.blogspot.com ulipokea kutoka kwa Msamaria mwema wa Uingereza, Bi Gladness Sariah, ambaye alitoa maboksi mawili yenye nguo na vitu kadhaa vya watoto.

Aidha katika kuonesha wengi wameguswa na tukio la Mwanamke huyo kujifungua watoto wanne  ambao wanaendelea vizuri, pia Msamaria  mwema mwingine aliyejulikana kwa jina la  Dada Norah SilverBoutique toka Dar es salaam naye  ametoa Maziwa Lactogen makopo 24 pamoja na nguo ambavyo vimewasili salama katika ofisi ya Mbeya Yetu.

 Shukrani kwa Wazee wa Kazi, Serengeti Freight Forwarders ya huko Uingereza na ofisi za Michuzi Media Group (MMG) kuwezesha kufika kwa mizigo hii Mbeya.

Kutokana na kupokelewa kwa mizigo hiyo ambapo kituo cha Nuru kilikabidhiwa Katoni Mbili za Sukari, Sabuni na Biskuti pia Tunatarajia kuanza  safari ya kwenda huko Chiwanda Wilaya ya Momba Kilomita zaidi ya 260 toka Mbeya mjini kufikisha misaada ya Mama wa mapacha wanne. 

Hivyo ni wito wetu kwenu kuendelea kutuombea na kutuunga mkono katika safari hiyo ili tuweze kuifikisha salama mizigo hiyo ikiwa ni pamoja na kuangalia maendeleo ya Watoto hao ambapo watakuwa wameshatimiza mwezi mmoja na siku 24.

Tunawashukuru sana tena sana wote mliojitolea na Mungu awabariki sana. 
Kama umeguswa na hili na unataka kutoa msaada tafadhali wasiliana na: issamichuzi@gmail.com ama jmwaisango@yahoo.com 
Nasi tutafikisha ubani wako. 
Wazee wa Kazi Serengeti Freight wametoa ofa ya 
kusafirisha bure misaada ya aina hii toka Uingereza.
Mbarikiwe sana Wazee wa Kazi.

SALMA MSANGI: KULIKO UNAVYOMJUA NA ULIVYOWAHI KUMSIKIA [INTERVIEW]

$
0
0
Maisha ni safari ya aina yake. Ndani ya safari moja, zipo nyingine nyingi. Pengine ukweli huo ndio chanzo cha ule usemi kwamba safari moja huanzisha nyingine. Kilicho muhimu ni kwanza kuianza safari yenyewe[moja].

Ninachokiongelea hapo juu kina ukweli zaidi katika maisha ya Salma Msangi ambaye leo kwa wengi ni mtangazaji wa luninga na radio mwenye tabasamu zito, wepesi wa kuelewa mazingira na mwenye kuipenda kazi yake na kuwapenda mashabiki,watazamaji wa vipindi vyake vya kwenye luninga na wasikilizaji wa vipindi vyake radioni.

Mara ya kwanza nilimuona Salma akiwa binti mdogo tu aliposhiriki shindano la kumtafuta mrembo wa Wilaya ya Ilala[ Miss Ilala]. Ilikuwa mwaka 2003. Ukumbi ulikuwa ni Diamond Jubilee. Endapo kungekuwa na mizani ya kupima nani angefika mbali sio tu katika shindano lile bali maishani kwa ujumla, bila shaka Salma angekuwemo. Kilichomtofautisha yeye na wengine si urembo. Ni kujiamini. Bado ninakumbuka jinsi alivyojibu swali. Jibu lake halikuwa jibu sahihi kupita yote. Lakini jinsi alivyolijibu, ilitosha kumuweka katika ukurasa mwingine.

Ndivyo safari yake ilivyoanza. Safari ile ikaanzisha safari nyingine na nyingine mpaka kufikia hapa alipo. Leo hii Salma Msangi ni mtangazaji anayefahamika na mwenye wafuasi wake lukuki ilhali akiendelea kujifunza mambo mengi zaidi na hivyo kuongeza maarifa kila kukicha.

Hivi karibuni nilipata bahati ya kufanya naye mahojiano ambayo utayasoma hivi punde. Endapo uliwahi kutamani kujua amefikaje hapo alipo,fursa ndio hii. Endapo unataka kujua Salma ana mtizamo gani kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii kama vile wanawake, mitandao ya kijamii, wasanii nk, fursa ndio hii. Kikubwa zaidi, Salma ana ushauri ambao naamini kila mtu anapaswa kuusoma hususani vijana.Uuze “sembe” au ufanyeje? Ungana nami….

BC: Salma, karibu sana ndani ya BC na shukrani nyingi kwa kukubali kufanya nami mahojiano haya. Mambo yanakwendaje?

Salma: Mambo sio mabaya tunashukuru tunasonga. Ahsante sana Jeff, Kaka hahaa.. kwetu kumoja weweee  au sio? Nashukuru kwa kunipa nafasi hii ya kutaka kufahamu kidogo kuhusu mimi. Mara nyingi huwa sipendi interview na nimekuwa nazikwepa kweli. Huwa naogopa maswali lakini nitajaribu.

BC: Naam, kweli kabisa mimi na wewe njia moja.Salma Msangi ni nani? Alianzia wapi mpaka kufikia hapa alipo?

Salma: Salma Msangi ni msichana aliyezaliwa miaka 29 iliyopita katika wilaya ya Same Mjini mkoa wa Kilimanjaro. Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Msingi Masandare hapo hapo Same kabla ya kuhamia jijini Dar Es Salaam kuungana na mama yake mzazi kwa ajili ya kuendelea na masomo ya sekondari.

Kabla  ya hapo Salma alilelewa na Mama yake mkubwa ambaye alikua ameolewa na Mjerumani. Hii ni baada ya mama yake mkubwa kuamua kumchukua kwasababu wakati anazaliwa mama yake alikua na umri mdogo kama wa miaka 18 hivi kwa hiyo ndugu na jamaa wakashauriana na kukubaliana kwamba kutokana na umri huo mdogo asingeweza kumpa mtoto matunzo mazuri au yanayostahili. Alikuwa bado mdogo na kwa ujumla angehitaji kuendelea zaidi na jitihada zake katika maisha.

VIJANA KUANDALIWA KUWA CHACHU YA MAENDELEO YA JAMII

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo        Pro. Elisante Ole Gabriel akifafanua jambo wakati alipokutana na Mkuu wa Kampuni ya TATA Africa Holdings (Tanzania) Ltd kujadili jinsi watakavyoweza kushirikiana kuanzisha program ya kuwaendeleza vijana kwa maendeleo ya jamii. Kushoto ni Bw. Prashant Shukla Mkuu ya kampuni hiyo na katikati ni Mkuu wa kitengo cha kozi fupi na ushauri chuo cha Mzumbe Pro. Shiv K. Tripathi ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo        Pro. Elisante Ole Gabriel akifafanua jambo wakati alipokutana na Mkuu wa Kampuni ya TATA Africa Holdings (Tanzania) Ltd kujadili jinsi watakavyoweza kushirikiana kuanzisha program ya kuwaendeleza vijana kwa maendeleo ya jamii. Kushoto ni Bw. Prashant Shukla Mkuu ya kampuni hiyo na katikati ni Mkuu wa kitengo cha kozi fupi na ushauri chuo cha Mzumbe Pro. Shiv K. Tripathi ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo        Pro. Elisante Ole Gabriel akifafanua jambo wakati alipokutana na Mkuu wa Kampuni ya TATA Africa Holdings (Tanzania) Ltd kujadili jinsi watakavyoweza kushirikiana kuanzisha program ya kuwaendeleza vijana kwa maendeleo ya jamii. Kushoto ni Bw. Prashant Shukla Mkuu ya kampuni hiyo na katikati ni Mkuu wa kitengo cha kozi fupi na ushauri chuo cha Mzumbe Pro. Shiv K. Tripathi ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Kampuni ya TATA Africa Holdings (Tanzania) Ltd Bw. Prashant Shukla akielezea jinsi watakavyoweza kushirikiana na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuwawezesha vijana kuleta maendeleo katika jamii, kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Pro. Elisante Ole Gabriel na katikati ni Mkuu wa kitengo cha kozi fupi na ushauri chuo cha Mzumbe Pro. Shiv K. Tripathi. (Picha zote na Genofeva Matemu - MAELEZO).

=======  ======  =====

Na Genofeva Matemu (MAELEZO)


VIJANA KUANDALIWA KUWA CHACHU YA MAENDELEO YA JAMII.


Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa kushirikiana na kampuni ya TATA Africa Holdings (Tanzania) Ltd imeadhimia kuanzisha programu ya kuendeleza maendeleo ya jamii kwa kutumia vijana waliopo katika ajira mbalimbali kwa kuwajengea uwezo utakaowawezesha kuleta maendeleo katika jamii yao.


Hayo yameafikiwa wakati Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Pro. Elisante Ole Gabriel alipokutana kwa ajili ya majadiliano ya awali na Mkuu wa Kampuni ya TATA Africa Holdings (Tanzania) Ltd Bw. Prashant Shukla pamoja na Mkuu wa kitengo cha kozi fupi na ushauri chuo cha Mzumbe Pro. Shiv K. Tripathi ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.


Lengo kuu la majadiliano hayo ni kupata ufafanuzi wa awali na kutambua maeneo ambayo Wizara itaweza kushirikiana na kampuni hiyo ili kuongeza ajira kwa vijana haswa ajira ya kujitegemea, pamoja na kuwajengea uwezo vijana katika masuala ya ujasiriamali, uongozi na ufundi makanika.


“Programu itakayoanzishwa italenga vijana hususani wale wanaojihusisha na ufundi makanika, madereva wa daladala, pamoja na waendesha pikipiki kwa maana ya usalama wao, usalama wa pikipiki na ujasiriamali utakaowawezesha kujipatia kipato na kuleta maendeleo katika jamii” amesema Pro. Gabriel.


Kwa upande wake Mkuu wa Kampuni ya TATA Africa Holdings (Tanzania) Ltd Bw. Prashant Shukla ameiahidi Wizara kushirikiana nayo bega kwa bega muda wote ili kuhakikisha kuwa tatizo la vijana mitahani linaisha na kuwa na vijana ambao wanauelewa na uwezo wa kuleta maendeleo katika jamii yao.


Naye Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi ameitaka kampuni hiyo kushirikiana na Wizara kwa kuchukua fursa ya kuboresha karakana ya Ufundi makanika iliyopo katika kituo cha vijana Ilonga Morogoro kama njia mojawapo ya kuwakomboa vijana na kuleta maendeleo.


TANGAZO LA MKUTANO MKUU WA WADAU WA PSPF

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MFUKO WA PENSHENI WA

PSPF



TANGAZO LA MKUTANO MKUU WA WADAU.


Mfuko wa Pensheni wa  PSPF unatangaza kwamba kutakuwa na Mkutano Mkuu wa tatu wa wadau utakaofanyika tarehe 26 na 27  Februari 2014 kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa kumi jioni katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere uliopo barabara ya Shaban Robert  jijini Dar es salaam.


Madhumuni ya Mkutano huu ni kutoa taarifa ya hesabu ya mwaka na utendaji wa Mfuko na kutathmini mafanikio na changamoto zinazokabili Mfuko na sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa ujumla.

“PSPF - TULIZO LA WASTAAFU”


Mkurugenzi Mkuu

Mfuko wa Pensheni wa PSPF,

Makao Makuu,Golden Jubilee Towers,  S.L.P 4843. Dar-es-Salaam.

Simu: +255222120912/52 au +255222127375 /6

 Nukushi: +255222120930


 Barua pepe:pspf@pspf.tz.org


MAKONDA: RASIMU YA KATIBA IMEWASAHAU VIJANA.

$
0
0
Mimi ni Kijana, ninayoyazungumza,ninayoyafanya yana reflect uhalisia huo. Hivyo kwa wito wa Ujana najikuta nashawishika sana kuongeza umakini katika masuala yahusuyo vijana hasa kwenye Katiba.

Ni ajabu lakini kweli kuwa sehemu inayotaja juu ya Haki na Wajibu wa Vijana katika Rasimu yote ni Ibara ya 44 tu, tena inataja kwa ujumla wake bila hata kuweka ibara ndogo ama vipengele vya ufafanuzi.


Ibara hiyo inasema;


"..kila kijana ana haki na wajibu wa kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya Jamhuri ya Muungano pamoja na jamii kwa ujumla, na kwa mantiki hiyo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano, serikali za nchi washirika na jamii zitahakikisha kuwa vijana wanawekewa mazingira mazuri ya kuwa "Raia Wema" na kupatiwa fursa za kushiriki kikamilifu katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni..."


Sikuwa nategemea huu unaweza ukawa ndio mwisho wa maelezo ya Rasimu kuhusu Vijana. Nilitegemea nitakuta vipengele vinavyobainisha namna vijana watakavyonufaika na rasilimali, namna ambavyo sheria ndogo na taratibu baguzi ktk upatikanaji wa ajira na fursa zitakavyobainishwa kikatiba ili kumaliza kabisa matatizo ya Vijana.



Nilidhani Rasimu itaweka bayana Uanzishwaji wa Baraza La Vijana la Taifa ili kiwe chombo cha kikatiba cha Vijana.



Nikitumia fursa na nafasi yangu kama mbunge wa bunge maalum la Katiba zipo hoja hizo kuu (3) tatu ambazo nitazisimamia ziingie kwenye Katiba kwa manufaa na mustakabal mwema wa Vijana bila kujali tofauti ya itikadi, dini ama kabila.



Na nakaribisha mawazo na michango ya fikra ktk hoja zihusuzo Vijana.


IMETOLEWA NA:
PAUL MAKONDA.
MBUNGE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA.

RAY C AANZISHA ASASI YA KUELIMISHA VIJANA NA JAMII JUU YA MADHARA YA UTUMIAJI WA MADAWA YA KULEVYA

WANANCHI MSIWE NA HOFU,HAKUTAKUWA NA VURUGU UCHAGUZI MDOGO WA JIMBO LA KALENGA-MKUU WA MKOA IRINGA

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa iringa DK CHRISTIN ISHENGOMA amewataka wananchi mkoani  Iringa,kutokuwa na hofu katika kipindi hiki cha kuelekea kampeni za uchaguzi wa jimbo la kalenga.

Akizungumza leo  kwenye moja ya kituo cha redio mjini humo,Nuru FM ,kupitia kipindi cha sunrisepower, amesema kuwa tayari ameshakaa na kamati yake ya Ulinzi na Usalama akiwemo Kamanda wa Jeshi la Polisi,aidha ameongeza kuwa wamejiandaa kikamilifu katika ulinzi, hivyo wananchi wanapaswa kutokuwa na hofu.


Amesema kuwa katika kipindi hiki cha uchaguzi wa jimbo hilo wageni wengi watakuwa wanaingia hivyo wananchi wanatakiwa kuwa makini na vishawishi vya makundi mabalimbali katika kipindi hiki cha uchaguzi.


Hata hivyo amesema kuwa pamoja na kuwa yeye yupo katika vikao vya bunge maalum la katiba atakuwa anakuja kushiriki na wananchi katika mkoa wake katika shughuli mbalimbali zikiwemo za kampeni zinazoendelea.


Aidha ameongeza kwa kusema kuwa kuhusu suala la posho kwa upande wake yupo tayari kupokea kiwango chochote atakachopewa ambacho kitakuwa kinatolewa katika kikao cha bunge maalum la katiba.

ZANZIBAR YAANZA MATAYARISHO YA UZINDUZI WA JUMUIYA YA MARADHI YASIYOAMBUKIZA

$
0
0
 Mratibu wa Jumuiya ya Maradhi Yasiyoambukiza Zanzibar (Z-NCDA) Omar Abdallah Ali akitoa muhtasari wa majukumu ya Jumuiya yao kwa Wandishi wa habari hawapo pichani katika Ofisi yao Mpendae Mjini Zanzibar.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maradhi Yasiyoambukiza Zanzibar (Z-NCDA) Ali Mansour Vuai akielezea matayarisho ya Uzinduzi wa Jumuiya yao utakaofanyika Machi 1 katika Viwanja vya Kibandamaiti mjini Zanzibar
 Baadhi ya Waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maradhi Yasiyoambukiza Zanzibar (Z-NCDA)  Ali Mansour Vuai (hayupo pichani) alipokuwa akizungumzia matayarisho ya Uzinduzi wa Jumuiya yao utakaofanyika Machi 1 katika Viwanja vya Kibandamaiti mjini Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar .

Article 2

$
0
0
Institute of Management and

Entrepreneurship Development




RETIREMENT PLANNING COURSE


A unique opportunity for employeesto develop Entrepreneurship, Financial Literacy and Retirement Planning Skills. The longer prior to retirement you take this course, the more you will benefit.


Approach and Contents

The course is delivered by highly experienced facilitators using experiential methods. Participants are guided to recognize opportunities and challenges of retirement; their talents and other tangible and intangible assets and liabilities; alternative  post-retirement “careers”;  to choose when to retire; and to continuously build their asset base, streams of income and fulfilling lives after retirement. 

They are exposed to good practices in starting and running a business, personal finance and health management; expected pension benefits and investment schemes tailored to retirees. They leave with self awareness, a Retirement Vision and look forward to their exit from employment.


Dates, Fee and Registration

24th- 27th March, 2014, Morogoro. Tuition is Tshs 500,000/= per person. Apply: info@imedtz.orgor 0718-942314 (Ulrich) and

0754-548248 (Hellen) or visit us at Mwalimu House, 7th Floor, Uhuru Road, Ilala, Dar es Salaam or www.imedtz.orgto pick the Registration Form.



We also offer Certificate and Diploma courses in Entrepreneurship and Business Management registered by NACTE 

Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images