Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 228 | 229 | (Page 230) | 231 | 232 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Watoto mapacha kutoka wilayani Kyela mkoani Mbeya waliokuwa wamepelekwa na serikali chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kufanyiwa upasuaji mkubwa wa kuwatenganisha wakiwasili nchini Tanzania kutokea nchini India walipokuwa wakipatiwa matibabu katika hospitali ya watoto ya Appolo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Nje wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Edward Sawe, mama mzazi wa watoto hao Bi. Grace Joel na Daktari aliyekuwa akiwaangalia nchini India Dkt.Glory Joseph.
   Watoto hao wakiwa wamebebwa na Daktari aliyekuwa akiwaangalia nchini India Dkt.Glory Joseph (kushoto) na mama mzazi wa watoto hao Bi. Grace Joel.
  Mama  mzazi wa watoto hao Bi. Grace Joel akiwa amewabeba watoto wake Elikana Erick (kushoto) ns Eliud Erick (kulia) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

   Habari na picha na 
  Aron Msigwa – MAELEZO.
  Hatimaye watoto mapacha kutoka wilayani Kyela mkoani Mbeya waliokuwa wamepelekwa na serikali chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kufanyiwa upasuaji mkubwa wa kuwatenganisha jana jioni wamerejea nchini wakitokea nchini India katika hospitali ya watoto ya Appolo walikokuwa wanapatiwa matibabu.

  Mara baada ya kuwasili katika  Uwanja ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakiwa wameambatana  na mama yao mzazi Grace Joel na Daktari aliyekuwa akiwaangalia nchini India ambaye pia alikuwa masomoni akisomea magonjwa ya Moyo kwa watoto Dkt. Glory Joseph wamepokewa na Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Nje wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Edward Sawe  na baadhi ya wauguzi kutoka Taasisi ya Mifupa (MOI) .

  Mapacha hao wa kiume wakiwa wenye  furaha na afya njema walichukuliwa katika gari maalum na kupelekwa katika Taasisi ya Mifupa (MOI) ambako watakaa kwa muda mfupi na kisha kuruhusiwa kuelekea wilayani Kyela jijini Mbeya ambako ndiko walikozaliwa.

   Kwa upande wake mama mzazi wa watoto hao akizungumza kwa furaha mara baada ya watoto wake kupatiwa matibabu ya kuwatenganisha kwa mafanikio makubwa amesema kuwa sasa maisha yake yamebadilika na ataishi kwa furaha na watoto wake.

  “Najisikia furaha sana kwa hatua niliyofikia mpaka hapa watoto wangu Eliudi na Elikana sasa ni wazima naishukuru sana Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa msaada ilionipatia” amesema.

  Kwa uipande wake Daktari aliyekuwa akiwaangalia nchini India ambaye pia alikuwa masomoni akisomea magonjwa ya Moyo kwa watoto Dkt. Glory Joseph akizungumzia matibabu ya watoto hao nchini India amesema kuwa hatua ya kuwatenganisha imekamilika na mwezi wa 8 mwaka huu watarudi tena nchini India kwa  ajili ya uchunguzi na matibabu zaidi ya afya zao.
  “Ni kwamba watoto hao wametenganishwa, kwa wakati huu wanaelekea MOI ambako watakaa kwa muda na baadaye wataruhusiwa kwenda kwao Mbeya kujumuika na jamaa zao” amesema.

  Kwa upande wake msemaji wa wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bw. Nsachris Mwamwaja amesema kuwa watoto hao waliwasili jana jioni na ndege ya shirika la ndege la Oman baada ya kumaliza matibabu ya awamu ya kwanza.

  Amesema upasuaji huo mkubwa wa kuwatenganisha watoto hao ulichukua saa 18 na kufafanua  kuwa kati ya hizo  saa 13 zilitumika kutenganisha viungo vilivyoungana sehemu ya chini ya uti wa mgongo,sehemu ya utumbo mpana,njia ya mkojo,kibofu cha mkojo na sehemu za uume huku saa 5 zikitumika kuunganisha sehemu zilizotenganishwa.

  “Kumbukumbu zinaonyesha kuwa mpaka sasa duniani upasuaji wa aina hii umefanikiwa mara tano  kutenganisha mapacha watoto wa kiume walioungana” amesisitiza.

  Ameongeza kuwa matibabu hayo ni juhudi za serikali katika kuhakikisha kuwa huduma za afya zinatolewa  kwa kila mwananchi kila inapowezekana na kutoa wito kwa jamii kujenga utaratibu wa kuwafikisha mapema kwenye vituo vya afya wale wote wenye matatizo ya kiafya badala ya kuwafikisha pindi hali zao zinapokuwa mbaya.


  0 0

  Taasisi  ya  RAFIKIELIMU  FOUNDATION  kupitia  mradi  wa   ELIMU  YA  UJASIRIAMALI  MIJINI  NA  VIJIJINI,  inatangaza  nafasi  za  MAFUNZO YA  UALIMU  WA  UJASIRIAMALI .

  Wahitimu  wa mafunzo  haya  watapata  nafasi  ya  kufanya  kazi  kwa  kujitolea   kama  waalimu  wa  ujasiriamali  katika   MRADI  WA  ELIMU  YA  UJASIRIAMALI  MIJINI &  VIJIJINI.


               IDADI   YA   NAFASI  :

  Nafasi  5  katika  kila  kata  ya  jiji  la  Dar  Es  salaam.

     SIFA  ZA  MWOMBAJI :


  1.    Awe  raia  wa  Tanzania  mwenye  elimu  ya  kuanzia  kidato  cha   nne  na  kuendelea.

  2.   Awe  mkaazi  wa  Dar  Es  salaam.
  4.  Awe  na  wito  wa  kufanya  kazi  ya  ufundishaji.
  5.  Awe  tayari  kufanya  kazi kwa  kujitolea   kama  mwalimu  wa  ujasiriamali  katika  kata  yoyote ya  jiji  la  Dar  Es  salaam.


  MAFUNZO   yatatolewa  kwa  mwezi  mmoja   kuanzia  tarehe     10  MACHI  2014 katika  Chuo  Chetu  kilichopo  katika  eneo  la  CHANGANYIKENI.

  ADA   YA  MAFUNZO :  MAFUNZO  HAYA  YANATOLEWA  BURE.

  CHUO  CHETU  kinapatikana    katika  eneo  la CHANGANYIKENI  karibu  na  CHUO  CHA  TAKWIMU  mbele  ya  CHUO  KIKUU  CHA  DAR  ES  SALAAM.

  JINSI  YA  KUTUMA  MAOMBI :

  Matumbi  yote  yatumwe  kupitia barua  pepe  yetu  ambayo  ni  : rafikielimutanzania@gmail.com 

  MWISHO   WA   KUCHUKUA   FOMU  ZA  MAOMBI  NI  TAREHE   28  FEBRUARY  2014..

  0 0  Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam

  Tanzania inatarajiwa kuwa, miongoni mwa nchi 150 zitakazoshiriki maonesho ya 53 ya Kimataifa ya madini ya vito na usonara yatakayofanyika Bangkok Thailand, kuanzia tarehe 25 februari hadi tarehe 1 Machi, 2014.

  Kutokana na kuwa na hazina kubwa ya madini ya aina mbalimbali, Tanzania imealikwa kuwa miongoni mwa nchi zitakazo shiriki maonesho hayo yanayojulikana kama ‘Bangkok Gems and Jewelry  Fair’.

  Akizungumzia ushiriki wa Tanzania katika maonesho hayo jana,   Kamishna wa Madini, Mhandisi Paul Masanja alieleza  kuwa, Tanzania inatarajia kuyatumia maonesho hayo kukuza ushirikiano kati ya Tanzania na Thailand katika biashara ya vito na usonara, kutangaza madini ya vito yanayopatikana hapa nchini, kutafuta masoko mapya ya biashara na bei za uhakika katika tasnia ya madini ya vito, kujifunza na kubadilishana uzoefu wa namna ya kusimamia na kukabiliana na changamoto zilizopo katika tasnia ya madini ya vito na usonara hapa nchini ikiwemo pia kukubaliana maeneo ya kushirikiana.


  Aidha, aliongeza kwamba, maonesho hayo yatasaidia Tanzania kujifunza uzoefu wa kuandaa maonesho ya Kimataifa ya vito na usonara ili kuboresha maonesho ya ‘Arusha Internal Gem, Jewelry and Minerals Fair’ (AIGJMF) yanayofanyika nchini kila mwaka.

  Mkurugenzi wa idara inayoshughulikia kuthamini Almas na madini mengine ya Vito, ‘Tanzania Diamonds and Gemstones Valuation Unit’, (TANSORT) Bw. Archard Kalugendo, ameongeza kuwa, ushiriki wa Tanzania vilevile unalenga kuwavutia wanunuzi na wauzaji kununua bidhaa hizo moja kwa moja nchini badala ya manunuzi kufanyika katika nchi na miji mengine mathalan Tanzanite ambayo kwa sasa inanunuliwa kutoka Hongkong, Mumbai na Afrika Kusini, na madini ya Almas  kutoka India, Dubai na Antwerp.


  Aliongeza kuwa, ushiriki huo, utaiwezesha Tanzania kupata nafasi ya kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji hususan katika madini ya vito yanayopatikana hapa nchini, kutoa taarifa za tafiti mbalimbali, ugunduzi mpya na kuelezea mipango endelevu iliyopo katika sekta hiyo.


  Aidha, mbali na ushiriki wa Wizara, Tanzania itawakilishwa na  Shirika la Madini Tanzania (STAMICO), Kampuni sita za wafanyabiashara wa madini za Isle of Gems, Suju Gem Ltd, Tom Gems, H.B Mining Ltd, Swala Gems Traders, Gems and Rock Ventures. Aidha, kutakuwa na uwakilishi wa shirikisho la wachimbaji Tanzania (FEMATA), (TAMIDA) na kampuni nyingine za madini.


  0 0


  Na Happiness Shayo.


  Shirikisho la Michezo Wizarani (SHIMIWI) limeandaa mafunzo ya uongozi,ualimu wa michezo na huduma ya kwanza viwanjani   kwa viongozi wa vilabu vya michezo ya SHIMIWI,yatakayofanyika mjini Morogoro  Februari 24-28 mwaka huu.


  Hayo yalisemwa na Kaimu Katibu Mkuu wa SHIMIWI Bw.Moshi Makuka mapema leo ofisini kwake alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa mikakati ya shirikisho hilo kwa mwaka wa fedha 2013/2014.


  Bw.Makuka alifafanua kuwa lengo la mafunzo hayo kwa viongozi wa vilabu ni kuwajengea uwezo wa kuongoza shughuli za michezo,kuwapa ufahamu zaidi juu ya  katiba,sheria na kanuni za michezo ya SHIMIWI na kuwapa uelewa wa namna ya kutoa huduma ya kwanza katika viwanja vya michezo.


  Akielezea sababu za Shirikisho hilo kuandaa mafunzo hayo Bw.Makuka alisema kuwa mafunzo hayo yanafanyika kutokana na na changamoto zilizojitokeza katika mashindano ya SHIMIWI ya miaka iliyopita  ambapo baadhi ya viongozi huvunja sheria na kanuni za michezo.


  “Baadhi ya viongozi wa SHIMIWI katika Wizara ,Idara Zinazojitegemea,wakala wa Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI) wamekuwa wakilalamikiwa kutumia wachezaji ambao sio watumishi wa umma .”alisema Bw.Makuka.


  Pia,aliongeza kuwa mafunzo hayo yatawahamasisha viongozi wa ofisi za Serikali zilizoshindwa kushiriki katika michezo ya mwaka jana ili iweze kushiriki mwaka huu kwa kuwa michezo kwa watumishi wa umma hujenga afya,mshikamano na pia huongeza ufanisi mahala pa kazi.  Michezo ya SHIMIWI ilianzishwa kwa madhumuni ya kuwakutanisha watumishi wa Serikali kwa lengo la kujenga na kuendeleza tabia ya ushirikiano,upendo na undugu hivyo hufanyika kila mwaka.Mafunzo haya hufanyika kila mwaka kwa mujibu wa kalenda ya SHIMIWI.


  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu akiaga baada ya kumalizika kwa semina aliyowaandalia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusu utendaji wa mfuko huo pamoja na kuwahamasisha kujiunga nao. Waliohudhuria semina hiyo ni wachora katuni, wamiliki wa mitandao ya kijamii na wahabari kutoka vituo vya televisheni, redio na magazeti.
   Ofisa wa PSPF akiwaelekeza baadhi ya wanahabari kujza fomu za kujiunga na mfuko huo katika mfumo wa hiari ambapo kiingilio ni sh. 10,000. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG.   Wanahabari wakiwa katika semina hiyo

   Wanahabari wakiwemo wamiliki wa mitandao ya kijamii wakishiriki katika semina hiyo

    Wanahabari wakiwemo wachora katuni wakihudhuria semina hiyo
   Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa PSPF, Masha Mshomba akifafanua jambo wakati wa semina hiyo.
   Meneja Mawasiliano na Masoko wa PSPF, Costantina Martin akielezea utaratibu wa kujiunga na mfuko huo
   Wamiliki wa mitandandao ya kijamii (Bloggers) wakiwa katika semina hiyo
   Meneja Uchangiaji wa Hiari wa PSPF, Mwanjaa Sembe akielezea umuhimu wa wanahabari kujiunga na mpango huo.
   Mkurugenzi wa  Mipango na Uwekezaji akitaja baadhi ya miradi waliyowekeza
   Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu akijibu baadhi ya maswali ya wanahabari

   Mwandishi wa Habari mkongwe wa magazeti ya Serikali Daily News na Habari Leo, akitoa neno la shukurani kwa PSPF baada ya kumalizika kwa semina hiyo.
   Mtunza Kumbukumbu wa PSPF, Lonick Nkinda akielezea mpangilio wa kuhifadhi kumbukumbu  za wateja kwa njia ya kisasa.
   Nkinda akionesha moja ya faili la mteja
   Meneja wa Huduma kwa Wateja wa mfuko huo, Laila Maghimbi akitoa maelezo kwa wanahabari kuhusu mashine zinazotoa namba kwa mteja inayomwelekeza dirisha la kwenda kuhudumia katika Makao Makuu ya PSPF, Dar es Salaam.
   Wanahabari wakipata maelezo kuhusu kitengo cha kuhudumia wateja kwa simu (Call Centre) kinachotarajiwa kuanza  kutoa huduma hivi karibuni.
  Wateja wakihudumiwa katika kitengo cha Huduma kwa Wateja Makao Makuu ya PSPF, Dar es Salaam.

  0 0

   . Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. John Mngodo akiogea na wadau wa Tehama wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau hao leo jijini Dar es salaam. 

   Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Dkt. Jabir Bakari akitoa mada kuhusu matumizi ya “Broadband” katika shughuli za Serikali wakati wa mkutanao wa wadau wa Tehama nchini katika ukumbi wa NSSF Waterfront leo jijini Dar es salaam.

   Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. John Mngodo akiongea na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa mkutano na wadau wa Tehama nchini leo jijini Da es salaam.

   Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. John Mngodo akiongea na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa mkutano na wadau wa Tehama nchini leo jijini Da es salaam.

   Kaimu Mkurugenzi wa ICT Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dkt. Ally Simba (kulia) akifafanua jambo kwa washiriki wa mkutanao wa wadau wa Tehama nchini katika ukumbi wa NSSF Waterfront leo jijini Dar es salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa Smile Communication Tanzania Ltd Mark Redman, na wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Operesheni Mfuko wa Huduma za Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Albert Richard.

   Mkuu wa kitengo cha cha ICT Broadband cha Taifa-TTCL Adin Mgendi  akitoa mada juu ya Wakati ujao tunaotaka kuuona wakati wa mkutanao wa wadau wa Tehama nchini leo katika ukumbi wa NSSF Waterfront jijini Dar es salaam na kubainisha kuwa TTCL imepanua wigo wa kutoa huduma ya mtandao wa mawsiliano(internet) ndani na nje ya nchi, katika nchi jirani zinazonufaika na huduma hiyo ni Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Malawi na Zambia. 
  . Baadhi  ya wadau wa Tehama  nchini wakifuatilia na kumsikiliza Mgeni rasmi  Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. John Mngodo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau hao leo jijini Dar es salaam. (Picha zote na Eleuteri Mangi – MAELEZO)

  0 0

  Hamis K Omary  from 361 Degrees organiser of Lake gas Indian Food Festival (Right) addressing the Conference about the Festival.
  Vinay Saxena from Lake Gas talking at the press Conference.
  Food is an integral part of the Indian culture and Indian subcontinent. Thanks to the multitude of its flavors and aroma, its popularity is quickly increasing, and with it the number of new Indian restaurants. And so a new project is born – the Indian Food Festival.

  The Lake Gas Indian Food Festival gives you the unique opportunity to try delicious Indian dishes from various Indian Restaurant and Caterers, enjoy a special menu, compare dishes and discover new flavors!

  Thus for the first time ever, The Lake Gas Indian Food Festival is aimed at promoting the tantalizing taste to the general Tanzanian Population. The variety range from array of kebabs, Tikkas, dossa, street food to various types of Biriani. Apart from the savory dishes, there shall be farsans, mithais, jalebi and all the sweet Indian delicacies.

  "Lake gas is proud to associate as a title sponsor for the Indian Food festival. Being one of the market leaders in the LPG in Tanzania, This event provides an ideal platform for our title sponsor 'Lake Gas' to address all LPG consumers on their channel networking and services" states Lake Gas Business Development Manager Numeir Khalid

  The Indian Food festival will be held three times a year. There will not only be culinary delights but also various Kinds Games such as under 12 Chapati rolling competition. There will be a minimal entrance of TZs 5,000 but children below ten years enter for free.

  "The way to the heart is through the stomach,” Hamis K Omary, business development Manager for 361 Degrees stated that the festival is aimed to spur more friendship amongst Tanzanian admirers of India.

  India’s unrivaled myriad cuisine reflects its rich and diverse culinary heritage. “It’s an expertise of striking the balance between form and function, between taste and nutritional value,” concluded Omary, guaranteeing that the dishes prepared for the Festival will tantalize local palate.

  Lake Gas Indian food festival has been proudly sponsored by Lake Gas Ltd, Indian Culture centre, The Peoples Bank of Zanzibar, Queens Jewellers, The quick print shop, ultimate security, century cinemax, prime advertising, Eventlites, Michuzi blog, missiepopular and 361 degrees

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Angels Moment, Bi Naima Malima akizungumza na wanasemina (hawapo pichani) juu ya lengo la semina hiyo. Bi Naima aliwasihi wanasemina hao kuzingatia wanayofundishwa ili kutimiza malengo yao ya uwekaji akiba. Picha na Salum Sasamalo.
  Baadhi ya wanawake na vijana walioshiriki Semina ya Wanawake na Akiba.

  Katika kuitikia wito uliotolewa jana na Mke wa Makamu wa Rais, Mama Asha Bilali wakati akifungua Tamasha la kwanza la kipekee kwa ajili ya wanawake na vijana lililopewa jina la Mwanamke na Akiba, mamia wa kinamama na vijana kutoka maeneo mbalimbali ya jijini Dar es Salaam na mkoa wa Pwani, leo walijitokeza kuhudhuria Semina ya Mwanamke na Akiba inayoendelea kufanyika katika Ukumbi wa Dar Live.

  Akizungumza katika Semina hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Angels Moment, Bi Naima Malima alisema kuwa Semina ya Mwanawake na Akiba, ni muendelezo wa siku tatu za Tamasha la Mwanamke na Akiba linalotarajiwa kuzunguka nchi nzima lenye lengo la kutoa elimu kwa akina mama hususani walio katika sekta isiyo rasmi kwani linatoa fursa ya kuwatoa wanawake katika utegemezi na umaskini kwa kuongeza kipato chao.

  Aliongeza kuwa muitiko wa wanawake na vijana hao katika semina hiyo, inaonyesha namna wanawake na vijana wa Kitanzania walivyo na nia na dhamira ya kujiongezea ujuzi na kujielimisha kuhusu kuweka akiba na kujitengenezea fursa mbalimbali. “Washiriki wanatumia fursa hii kwa kujipata elimu juu ya kukabiliana na hatari katika uhifadhi wa fedha na masuala mbalimbali yahusikanayo na usimamizi wa fedha,” alisema.

  Tamasha la Mwanamke na Akiba linakusudia kuwaelimisha wanawake na vijana juu umuhimu wa kuweka akiba, mbinu tofauti za kuweka akiba na jinsi ya kukabiliana na changamoto mbalimbali katika kujiwekea akiba.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa kwa Umma kuhusu utaratibu wa manunuzi ndani ya bohari ya dawa. Kulia ni Mkurugenzi wa Manunuzi wa MSD, Heri Mchunga na Mwanasheria, Domonica Meena.

  0 0

  Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt Pindi Chana leo ametembelea Dawati la Jinsia na Watoto la Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Dodoma Mjini kwa lengo la kukagua utendaji kazi wa madawati haya yaliyoanzishwa kwa lengo kushughulikia kesi zote zinazohusiana na unyanyasaji wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto nchini, kama njia moja wapo ya kuboresha utoaji wa huduma bora za ulinzi na usalama kwa watoto na watu wa jinsi zote.
   Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt Pindi Chana ( mwenye suti nyeusi) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Dawati la jinsia na watoto la Polisi wilaya ya Dodoma, Kulia kwake ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya Dodoma, Thadeus Malingumu na Kushoto kwake ni Mkuu wa dawati la jinsia na watoto mkoa wa Dodoma, ASP Hamida Hiki.
  Kamanda wa Polisi Mkoa Wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David Misime akitoa Maelezo mafupi kwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt.Pindi Chana (Mb.) (mwenye suti nyeusi) Wakati alipotembelea Dawati la Jinsia na Watoto katika Mkoa wa Dodoma.
  Katika taarifa yake, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma alieleza kuwa Mkoa wa Dodoma una jumla ya Madawati 9 yaliyopo katika Wilaya saba za mkoa huo.

   Aliainisha moja ya changamoto za uendeshaji wa Madawati hayo kuwa ni baadhi ya wananchi kutokuwa tayari kutoa ushahidi wakati kesi hizo zinapofikishwa Mahakamani. Hivyo, Mkoa umejipanga kuendelea kuimarisha utoaji huduma kupitia madawati haya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Maendeleo ya Jinsia na Watoto.

  Wakati wa Ziara hiyo, Mheshimiwa Naibu Waziri Dkt. Pindi Chana alilisisitiza Wananchi kutumia madawati ya Polisi ya jinsia na watoto kutoa ripoti za matukio yeyote ya unyanyasaji  wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto yanayotokea katika jamii zetu. Aidha, alisisitiza kuwa huduma katika vituo hivi hupatikana pasipo malipo yeyote, na hutolewa kwa usiri stahiki.

  0 0

  Mkurugenzi wa ANSAF, Audax Rukonge alipokuwa akieleza maudhui ya siku ya Mwaka wa Kilimo wa Afrika.
  Ukaguzi wa shamba la mfano katika kijiji cha Kaning'ombe ulifanywa
  Wasanii, Mrisho Mpoto na Profesa J ambao ni mabalozi wa kampeni ya "Kilimo Kinalipa, Jikite" walikuwepo

  Naye Mwakilishi wa shirika la Afrika One kutoka Afrika Kusini alikuwepo kuelezea kilimo kinavyoweza kuwatoa watanzania.

  Msanii Dokii naye alisema mambo na jinsi kilimo kinavyomtoa

  Wazee wa kampeni, Mrisho Mpoto, Profesa J na Masoud Kipanya walisema maneno yao kwa kupokezana wakieleza jinsi kilimo kinavyoweza kuwa mkombozi kama dhamira itakuwepo


  Mkulima wa mfano, Bw. Eusebio Mbagile, alizungumzia changamoto wanazopata wakulima wadogo katika shughuli hiyo ya kilimo.

  Baada ya kueleza changamoto zinazowakabili, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk Christine Ishengoma aliishia kwa kupata ka KUKU ka zawadi ili akale yeye na familia yake

  JUKWAA la Wadau wa Kilimo (ANSAF) limekumbushia ahadi  ya kutenga asilimia 10 ya bajeti ya nchi kwa ajili ya Kilimo, iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete mwaka 2012.

  Mkurugenzi wa ANSAF, Audax Rukonge aliyasema hayo leo wakati Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal aliyewakilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dk Christine Ishengoma akizindua Mwaka wa Kilimo wa Afrika.

  Uzinduzi wa mwaka huo unaokwenda na kampeni iliyopewa jina la ‘Kilimo Kinalipa, Jikite’ ilifanyika katika kijiji cha Kaning;ombe, wilayani Iringa mkoani Iringa.

  Mbali na ANSAF, wengine wanaoratibu kampeni hiyo ni mashirika ya Cloud Media na Afrika ONE inayowataka viongozi wa Afrika kutimiza Azimio la Maputo linalohimiza uwekezaji katika kilimo

  Mabalozi wa kampeni hiyo, wasanii maarufu, Mrisho Mpoto, Profesa J na Masoud Kipanya walizungumzia namna kilimo kinavyoweza kuwakwamua vijana na lindi la umasikini huku msanii wa filamu nchini Dokii akieleza mafanikio yake ya kilimo katika shamba lake lililoko wilayani Kilosa mkoani Morogoro.

  Mkurugenzi wa ANSAF, alisema kwa kupitia azimio hilo la Maputo wakuu wa nchi walikubalina watenge bajeti ya asilimia 10 ya bajeti zao kwa ajili ya kilimo.

  Alisema kiwango hicho kilitarajiwa kutosha kuchangia kuongeza uzalishaji na tija, kukuza sekta ya kilimo kwa asilimia 6 kwa mwaka na kuondoa tatizo la njaa na umasikini.

  “Leo hii ni miaka 10 tangu makubaliano ya Maputo. Ni nchi nane tu za Afrika zimetimiza ahadi hiyo; Tanzania haimo katika nchi hizo,” alisema bila kuzitaja.

  Alisema tafiti zinathibitisha kuwa kilimo huchangia mara 11 zaidi katika kuondoa umasikini ikilinganishwa na uwekezaji mwingine.

  Alisema kama taifa limedhamiria kuondoa umasikini ni lazima kukipatia kilimo mtazamo mpya wa kiuchumi, usiokuwa na chembe za kisiasa huku uwekezaji ukifanywa kwenye maeneo ya kimkakati.

  Katika hotuba yake kwa wadau wa Kilimo, Makamu wa Rais alisema kilimo ni lazima kiendelezwe kwa usalama wa chakula na maisha.

  Alisema program ya kuendeleza kilimo ilizinduliwa mwaka 2005/2006 ikilenga kilimo kikue kwa asilimia sita kutoka asilimia nne ya hivisasa.

  Alisema kwa kushirikisha sekta binafsi program hiyo inalenga pia kuwatoa wakulima katika kilimo cha kujikimu ili kiwe cha kibiashara.

  “Tunatakiwa kuwa na muda maalumu wa kushughulikia ahadi ya Maputo ya kutenga asilimia 10 ya bajeti ya serikali, kufanya mabiliko ya sera na kuongeza uwajibikaji katika sekta hiyo,” alisema.

  Mmoja wa wakulima wa mfano katika kijiji hicho, Eusebio Mbangile alisema shughuli ya kilimo ni kero kubwa kwa wakulima wadogo kutokana na ukubwa wa bei za pembejeo, upatikanaji wake na masoko.

  Alisema “ninazo heka 45; ninazolima ni 19, wakati wa masika 15 na wakati wa kiangazi heka nne, kwa wastani natumia karibu Sh Milioni 4 kwa shughuli nzima ya kilimo kila mwaka;” alisema huku akionesha mashamba yake hayo ya mahindi.

  Alisema kwa wastani hupata gunia 25 za mahindi kwa kila heka ambayo hata hivyo huwa hauzi kwa vipimo vinavyokubalika kisheria.


  Alisema walanguzi wamekuwa wakinunua gunia la mahindi lenye ujazo wa kilo 150 hadi 160 kwa Sh 38,000 tu hali inayowapa hasara kubwa na kuwafanya waendelee kuwa masikini.

  0 0

  Mkutano wa chama cha walimu manispaa ya iringa (CWT) umefanyika katika ukumbi wa chama hicho huku mgeni rasmi katika mkutano huo  akiwa  mkurugenzi wa manispaa ya iringa TERESIA MAHONGO.

  Akizungumza katika mkutano huo katibu wa chama cha walimu manispaa Fortunata Nalale amesema CWT kwa manispaa inahudumia walimu 1443.  Amesema kuwa waajiri wanatakiwa kuwatumia  walimu hao katika kuboresha elimu ili kutatua migogoro iliyopo katika shule mbalimbali.

   Akizungumza katika Mkutano huo mgeni rasmi amejibia matatizo ambayo yameelezwa na walimu hao na kusema kuwa yote yanawezekana kutatuliwa kwani yaliyo juu ya uwezo wake atayafikisha mahali Husika. Aidha wakiainisha matatizo walimu hao wametaka matatizo yao kutatuliwa kwa wakati.

  Mkutano wa chama cha walimu manispaa ya iringa (CWT) umefanyika katika ukumbi wa chama hicho huku mgeni rasmi katika mkutano huo  akiwa  mkurugenzi wa manispaa ya iringa TERESIA MAHONGO.

  Akizungumza katika mkutano huo katibu wa chama cha walimu manispaa Fortunata Nalale amesema CWT kwa manispaa inahudumia walimu 1443. Amesema kuwa waajiri wanatakiwa kuwatumia  walimu hao katika kuboresha elimu ili kutatua migogoro iliyopo katika shule mbalimbali.

   Akizungumza katika Mkutano huo mgeni rasmi amejibia matatizo ambayo yameelezwa na walimu hao na kusema kuwa yote yanawezekana kutatuliwa kwani yaliyo juu ya uwezo wake atayafikisha mahali Husika. Aidha wakiainisha matatizo walimu hao wametaka matatizo yao kutatuliwa kwa wakati.
  ==========   ========  ======

  WATU WANNE WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI.

  Watu wanne wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani hapa baaya ya kuingia nchini kinyume cha sheria.

  Akithibitisha kutokea  kwa tukio hilo kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa iringa Charles kakamba  amesema  kuwa watu hao  ambao ni raia wa ETHIOPIA  ni pamoja na TEMESON DASELALI [24], BARAKA  SELAFU [28], na SHABANI  HUSSEN [20].

  Kakamba ameongeza kuwa watu hao wamekatwa wakati askari polisi wakiwa  doria katika kijiji cha MTUA - ILULA kata NYABULA.

  Aidha kaimu kamanda amebainisha kuwa watu hao walikuwa njiani kuelekea mkoani mbeya. 

  =======  ======  =======
  DIWANI KATA YA MGAMA AANZA KUFANYA JITIHADA ZA KUTATUA MALALAMIKO YA WANANCHI.

  Diwani wa kata ya mgama wilaya ya iringa vijijini DENNISI LUPALA ameanza kufanya jitihada mbalimbali za kutatua malamamiko ya baadhi ya wananchi juu ya kuto somewa mapato na matumizi ya fedha katika vijiji hivyo.

  LUPALA  amekiri kupata malalamiko hayo kutoka kwa wananchi katika kata yake na kusema kuwa amekua akitoa maagizo kwa viongozi wa vijiji akiwemo mtendaji na mwenyekiti kuhakikisha viongozi hao wanatekeleza maagizo yanatolewa na serikali.

  Amesema kuwa tayari wameshapatikana viongozi ambao wanashika nafasi ya watendaji ambao wameshindwa kutekeleza  magagizo ya usomaji wa mapato na matumizi katika maeneo yao , huku kijiji cha itagutwa kikiwa ni moja ya vijiji ambavyo vimebadilishiwa viongozi kutokana na tatizo hilo.


  Ametoa wito kwa wananchi wa kata hiyo kuwa na uvumilivu na ktoa ushirikiano ili kuendelea kutatua changamoto zinazowakabiri katika vijiji vyao kwani mpaka sasa tayari ametatua baadhi yha changamoto kwa asilimia kubwa ikiwa ni pamoja na kuboresha miundo mbinu katika vijiji hivyo


  0 0

   Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kulia) akiangalia takwimu zinazohusiana na masuala ya idadi ya watu nchini Tanzania. Anayemuonesha ni Kaimu Mwakilishi Mkazi wa UNFPA, Bibi Mariam Khan (Wa pili kulia) aliyembelea Ofisi za Tume ya Mipango leo. Wengine pichani ni Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Bibi Florence Mwanri (Kushoto), Mchambuzi Mkuu wa Sera, Bw. Edwin Ninde (Wa pili kushoto) na Mtaalam wa Masuala ya Idadi ya Watu toka UNFPA, Bibi Christine Mwanukuzi-Kwayu.
   Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akifuatilia kwa makini takwimu zinazohusiana na masuala ya idadi ya watu nchini Tanzania zilizokuwa zikiwasilishwa na Bibi Mariam Khan (hayupo pichani) alipotembelea Ofisi za Tume ya Mipango. Kulia ni Mchambuzi Mkuu wa Sera (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango), Bw. Edwin Ninde.

   Kwa umakini zaidi! Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kulia) akiangalia kwa umakini sana takwimu zinazohusiana na masuala ya idadi ya watu nchini Tanzania. Anayemuonesha ni Kaimu Mwakilishi Mkazi wa UNFPA, Bibi Mariam Khan (Kushoto).
   Mtaalam wa Masuala ya Idadi ya Watu toka UNFPA, Bibi Christine Mwanukuzi-Kwayu (Kushoto) akizungumza wakati alipofuatana na Kaimu Mwakilishi Mkazi wa UNFPA, Bibi Mariam Khan (Kulia) kutembelea Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. 

  Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kushoto) akizungumza na Kaimu Mwakilishi Mkazi wa UNFPA, Bibi Mariam Khan (hayupo pichani) aliyembelea Ofisi za Tume ya Mipango leo. Pamoja na masuala mengine, walizungumzia changamoto za idadi ya watu na ukuaji wa miji nchini Tanzania. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Bi Joyce Mkinga. 
  ========  =======  ========
  Tumieni ongezeko la Idadi kama fursa za ukuaji wa uchumi
  Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Masuala ya Idadi ya Watu (UNFPA), Bibi Mariam Khan leo alitembelea Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na kutoa wito kwa serikali kufanya hima katika kukabiliana na changamoto za ongezeko la idadi ya watu na ukuaji wa mijini nchini Tanzania.

  Hata hivyo, Bibi Khan alisema kuwa licha ya kuwa ongezeko la idadi ya watu linaathari mbalimbali kama lisipothibiwa, Tanzania inaweza kutuma fursa hiyo kwa kuwekeza kwa vijana kama nguvu kazi kwa shughuli za kimaendeleo ili kuongeza pato na uchumi wa taifa.

  Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango alisema kuwa serikali inatambua changamoto hizo, na kuwa kwa sasa inajipanga kuipitia Sera ya Idadi ya Watu ya Mwaka 2006 ili iendane na changamoto hizo.

  Na Saidi A. Mkabakuli
  Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango  0 0

   Makamu Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya TASAF Taifa Abbas Kandoro akikagua mradi wa Mashine ya kukoboa na kusaga nafaka wa Wazee katika Mtaa wa Mbulani kata ya Ruvuma Mjini Songea ambao wamewezeshwa kiasi cha shilingi Milioni 8 na TASAF ikiwa ni juhudi za kukabiliana na umasikini kwa wazee.
   Makamu mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya TASAF Taifa Abbas Kandoro akizungumza na Wazee wa Mtaa wa Mbulani katika kata ya Ruvuma Mjini Songea mara baada ya kukagua mradi wa Mashine ya kusaga na kukoboa nafasi wa wazee hao
  Wazee waliopatiwa mradi wa kukoboa na kusaga nafaka katika kata ya Ruvuma Mjini Songea wakifuatilia hotuba ya Makamu Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya TASAF Taifa Abbas Kandoro kuhusu nia ya TASAF kuwezesha jamii.
   Wazee wa Kata ya Ruvuma wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati Tendaji ya Kitaifa ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF
   Wajumbe wa kamati Tendaji ya TASAF Kitaifa wakikagua mradi wa ufugaji wa Ngombe wa Vijana wa Mtaa wa Muungano Mjini Songea. Katika mradi huu TASAF imewawezesha vijana kupata shilingi milioni 5 za kununulia mitamba kwa ajili ya mradi huo
   Meneja rasilimali watu wa TASAF Tekla Makundi akichangia ushauri kuhusu uendeshaji wa mradi wa ng'ombe wa Maziwa hasa baada ya wanakikundi cha vijana cha Muungano Mjini Songea kudai wanakabiliwa na uhaba wa dume la kupandishia mitamba yao
   Vyumba viwili vya madarasa vilivyojengwa katika Shule ya sekondari ya Ndongosi Songea Vijijini vikiwa vimekamilika. Ujenzi wa vyumba hivi umechangiwa na TASAF kwa shilingi milioni 45 na wananchi shilingi milioni 4 wakati wa utekelezaji wa awamu ya pili ya TASAF
   Makamu Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya TASAF Taifa Abbas Kandoro akisoma nembo ya TASAF katika jengo la vyumba viwili vya madarasa lililojengwa katika shule ya Sekondari Ndongosi Songea Vijijini. vyumba hivyo pia vimekewa meza na viti kwa ajili ya wanafunzi 70 pamoja na meza na makabati
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu anayeshughulikia TAMISEMI Zuberi Tamasaba akizungumza na wanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari ya Ndongosi Songea Vijijini

  0 0

  f4702a40d1bf22563232e0028aa968db-e1391201911777
  Don’t miss an Exclusive Interview of BBC World TV with Hon; Mohammed Dewji (MP) on Friday this week, the Interview will be part of African Business Report a new weekly business TV show on BBC World News.
  Watch it on BBC World TV at 1940 GMT on Friday, 1810 GMT on Saturday and 0010 GMT on Sunday.

  0 0

  Media For Development International (MFDI) – Tanzania usiku wa jana wamefanya uzinduzi wa aina yake katika sekta ya filamu Tanzania kwa kuzindua filamu tatu kupitia mradi wake wa Swahiliwood katika Ukumbi wa Century Cinemax uliopo Oysterbay, jijini Dar es salaam.

  Uzinduzi huo ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya filamu hapa nchini pamoja na mashirika ya ya ndani na nje ya nchi ikiwa ni hatua ya kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya filamu hapa nchini.

  Filamu zilizozinduliwa jana zikiwa na lengo la kuelimisha jamii ni Mdundiko iliyotengenezwa na Timothy Conrad, Sunshine iliyotengenezwa na Karabani na Network iliyotengenezwa na John Kallage.

  Mradi wa Swahiliwood umewezeshwa kwa msaada wa Watu wa Marekani kupitia USAID kwa kushirikiana na Johns Hopkins University Center for Communication Programs pamoja na kampuni ya Proin Promotion inayokuwa kwa kasi katika usambazaji wa kazi za filamu nchini Tanzania.

  Lengo la Swahiliwood ni kuongeza nguvu ya ubunifu kwa vijana watengeneza filamu wa Kitanzania, ili kupeleka maudhui kwa walengwa kwa njia ya burudani kwa kushirikiana na sekta binafsi kuhakikisha filamu zinawafikia walengwa mbalimbali kupitia mitandao ya wasambazaji. Mradi huu unafanya kazi pamoja kwa kushirikiana na wadau muhimu kutoka sekta ya umma pamoja na COSOTA (Chama cha haki miliki), Mamlaka ya mapato Tanzania, bodi ya filamu na BASATA, kama idara inayosimamia maendeleo ya Tasnia vya filamu.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi John Riber, mkurugenzi MFDI Tanzania alisema kwamba “Tulizindua mradi wa Swahiliwood kwa sababu tuliona kwamba vijana wana uwezo mkubwa wa kutengeneza filamu. Muundo wa Swahiliwood unazingatia nguvu ya vijana katika kuhakikisha tasnia ya filamu inasambaa ikielimisha jamii juu ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi. Na hiyo imetambuliwa na Serikali ya Tanzania kama ni changamoto kuu ambayo inalikabili Taifa”.

  Muundo wa Swahiliwood unatoa mafunzo na ushauri kwenye uzalishaji wa filamu. Pia ni sekta ambayo inaongoza kwa kutoa ajira kwa vijana wa Tanzania. Serikali ya Tanzania na sekta binafsi pamoja na Watanzania wabunifu wenye vipaji vya utengenezaji wa filamu wameshirikiana, kwa msaada wa Serikali ya Marekani. Wamekuwa nyenzo katika kukuza biashara na uchumi unaokuwa haraka, na kuhakikisha kwamba filamu zinawafikia watazamaji wa Afrika ya Mashariki kwa ujumla.

  MDUNDIKO: Ni hadithi ambayo inazungumzia mfarakano wa imani za kimila, maadili, na hoja za maisha katika jamii. NETWORK: Ni hadithi inayohusu kuwindwa kwa mhalifu anae tuhumiwa kufanya mauaji ya mwendelezo ambayo yanawahusisha wapelelezi, askari mzee na kijana mwenye mvuto.

  SUNSHINE: Ni hadithi ya uraiani yenye mguso kuhusu majaribu ya uhalifu na mapenzi yasiyokuwa na mashariti kati ya mama na mtoto.

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ndugu Job Masima kulia akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kukagua gari aina ya Ashok Leyland iliyotolewa na Wizara yake kwa ajili kuimarisha viteule vya kijeshi vya Kasanga na Kirando Mkoani Rukwa. Katika kukabiliana na changamoto zilizokuwa zinavikabili vitua hivyo Wizara ya ulinzi kupitia kwa Katibu Mkuu huyo imetoa gari mbili, boti mbili na fedha Tsh. Milioni 150 kwa ajili ya kuboresha makazi na miundombinu katika viteule hivyo. Kwa upande mwingine amesema kuwa baadhi ya vifaa vingine vitatoka makao makuu ya jeshi katika kuboresha viteule hivyo. 
  Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ndugu Job Masima kulia akimkabidhi funguo ya gari Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kama ishara ya makabidhiano ya gari mbili pamoja na michango mingine itakayotumika katika viteule vya jeshi vya Kasanga na Kirando Mkoani Rukwa.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiwasha gari hilo kama ishara ya kupokea misaada hiyo kwa viteule viwili vya Kirando na Kasanga vilivyopo Mkoani Rukwa.
  Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ndugu Job Masima wa pili kushoto akitoa majumuisho ya ziara yake kwa uongozi wa Mkoa wa Rukwa leo. Katika majumuisho yake pamoja na mambo mengine aliongeza kuwa mchakato wa kupanua kiteule cha Kasanga utawekwa kwenye bajeti ya mwaka ujao wa fedha ili kukiongezea ufanisi zaidi. Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya ambae ndiye chachu kubwa ya mafanikio haya kwa kumualika Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi kuja kujionea changamoto zilizopo amemshukuru kwa kuitikia wito wake na mchango wa ujumla uliotolewa na Wizara yake katika kuimarisha ulinzi katika ukanda wa ziwa Tanganyika unaopakana na nchi za Burundi, Zambia na DRC. 
  Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu  Symthies Pangisa kushoto  akizungumza katika kikao hicho cha majumuisho ambapo amemshukuru Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na msafara wake kwa kazi nzuri waliyoifanya Mkoani Rukwa katika kipindi chote cha ziara yake ya siku tatu.
  Baadhi ya wajumbe walioshiriki kikao hicho cha majumuisho wakifuatilia kwa makini. (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

  0 0

  Kiongozi wa Extra Bongo, Ally Choky, akizungumzia uzinduzi huo ndani ya hoteli ya Atriums iliyopo Afrika Sana, Sinza.
  Mratibu wa Burudani Dar Live, Luqman Maloto, akizungumza na waandishi wa habari. Kushoto ni Choky na Hamis Mwinjuma.
  Extra Bongo wakiwa katika picha ya pamoja na Maloto katika hoteli ya Atriums.
  Wanamuziki wa Extra Bongo wakipozi pamoja na Hamis Mwinjuma kwenye ukumbi wa hoteli ya Atriums iliyopo Afrika Sana, Sinza.

  HAYAWI hayawi, sasa yamekuwa! Ule uzinduzi wa albamu ya ‘Mtendwa Akitendewa’ kutoka bendi ya Extra Bongo kesho utafikia kilele ambapo watadondosha bonge la shoo katika ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem.

  Akizungumzia maandalizi ya mwisho kuelekea shoo ya albamu hiyo katika hoteli maarufu ya Atriums iliyoko Afrika Sana, Sinza, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choky, alisema kila kitu kinaenda sawa na hivi sasa kilichobaki ni kudondosha mashambulizi siku ya kesho usiku.


  Burudani hiyo itanoga zaidi kutokana na kusindikizwa na wakali wa Bongo Fleva kina Amin na Linah, Makhirikhiri wa Bongo, Bendi ya Mashujaa, TOT Band chini ya ‘Malkia wa Mipasho’ Khadija Kopa. Kiingilio kitakuwa ni sh. 6,000 tu.


   Wanamuziki wa Extra Bongo (kutoka kulia) Sharapova, Super Nyamwela na Semsekwa wakijiandaa kutoa burudani kidogo.
  ...SemsekwaSuper Nyamwela na Sharapova wakionyesha mbwembwe zao kwa wanahabari (hawapo pichani).
  Mnenguaji wa Extra Bongo, Sharapova akiwa katika pozi.
   Semsekwa katika picha ya pozi.
  Banza Stone mmoja wa vivutio katika uzinduzi huo wa kesho.
  Semsekwa, Nyamwela na Sharapova wakiwa katika pozi.
  (HABARI/PICHA: ANDREW CARLOS, GPL)

  0 0

  Mkurugenzi wa Media For Development International (MFDI) – Tanzania Bw. John Riber akizungumza na wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Filamu tatu chini ya mradi wa Swahiliwood. MFDI inatambua umuhimu wa tasnia ya filamu (ambayo kwa sasa inajulikana kama Bongo movie), na sio tu kwamba ni daraja linaloelezea habari za kijamii, lakini pia kama tasnia am­bayo inaweza kuleta maendeleo na ajira kwa vijana wa Kitanzania.

  Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria katika usiku wa kipekee kushuhudia uzinduzi wa filamu za Swahiliwood wakimsikiliza Mkurugenzi wa Media For Development International (MFDI) – Tanzania Bw. John Riber. Filamu tatu zilizozinduliwa katika usiku wa jana ni Network, Sunshine na Mdundiko.

  Wakongwe katika tasnia ya filamu hapa nchini Tanzania Bw. Jacob Steven (JB) kushoto na Bw.  Muhsin Awadh (Dk. Cheni) wakiwa ukumbini  kushudia uzinduzi wa Filamu za Swahiliwood katika Ukumbi wa Century Cinemax – Oysterbay.
  Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika moja ya kumbi za Century Cinemax – Oysterbay wakitazama filamu ya Mdundiko mara baada ya uzinduzi. Filamu zote zinahusu mapam­bano ya UKIMWI ambapo watazamaji watapata elimu na watengenezaji watapambana na kufanikiwa katika maswala ya kibiashara kwa kuiga muundo wa Swahiliwood.

  Wadau wa Proin Promotion ambao ni wasambazaji wakuu wa Filamu zote tatu nchi nzima wakiwa katika picha ya pamoja kwenye Red Carpet ya uzinduzi wa filamu za Swahiliwood.Picha Na Josephat Lukaza

  0 0

    Makamu wa Rais Dkt Bilal (katikati) akizungumza na Rais wa Uganda Yower Museven (kulia) kabla ya Mkutano huo. 
  Viongozi Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki wakiimba wimbo maalumu wa Afrika Mashariki, kabla ya kuanza rasmi Mkutano wa Nne wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Ushirikiano wa Kanda ya Kaskazini, uliofanyika jana kwenye Hoteli ya Speke Resort Munyonyo jijini Kampala Uganda, ambapo Tanzania imeshiriki Mkutano huo kama Mwalikwa.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto) na Makamu Rais wa Burundi Gervas Rufykiri, wakitia saini kushiriki katika mkutano huo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto) akizungumza katika mkutano huo.
   Rais wa Uganda Yoweri Museven, akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Nne wa wakuu wa Nchi wanachama wa Ushirikiano wa Kanda ya Kaskazini. Umoja huo unaundwa na nchi za Uganda, Kenya, Rwanda na Sudan Kusini,Tanzania na Burundi zimeshiriki mkutano huo kama nchi waalikwa ambao pamoja na mambo megine waliyojadili ni kukamilisha miradi mbalimbali inayofanywa kwa pamoja na ushirikiano huo.

  Baadhi ya washiriki wa mkutano huo na ujumbe wa Tanzania. 
  Picha na OMR

older | 1 | .... | 228 | 229 | (Page 230) | 231 | 232 | .... | 1898 | newer