Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46194 articles
Browse latest View live

kumbukumbu.

0
0
Ilikuwa usiku wa kuamkia Alhamisi, Februari 2, 2012, wakati ulipomaliza kwa amani siku yako ya mwisho ya kuishi hapa duniani na kuanza siku yako ya kwanza ya kuishi makazi ya kudumu akhera. Ilikuwa ni siku iliyojaa simanzi kwa mume wako kipenzi Abdallah, watoto wako Hashim na Lulu, mama yako mzazi Mama Babay, Baba yako mzazi Mzee Abdul, kaka yako Yusuf, wadogo zako, shangazi na baba zako wadogo, ambao bado wanakukumbuka.

Kiungo katika familia yetu kimevunjika, maisha yetu hayako sawa tena. Lakini kadri Mungu atakavyotuita mmoja mmoja, viungo vitaungana tena. Mungu ametimiza ahadi na mapenzi yake ya kukuita kwenye makazi yake ya kudumu ukapumzike kwa amani, baada ya kuishi nasi duniani kwa furaha, ukarimu, amani na upendo kwa miaka 42. Kimwili haupo nasi nyumbani, lakini ki roho bado uko nasi popote.

Ni mwaka mmoja kamili umetimia leo, lakini kumbukumbu za upole, ukarimu na tabasamu lako, zinatufanya tuone kama umeondoka jana. Dua njema tunakuombea, Mwenyezi Mungu alijalie kaburi lako liwe miongoni mwa bustani za peponi.

Daima unakumbukwa pia na shemeji zako Dawood, Shigongo, Nasibu, Hassan, Kitenge, wafanyakazi wote wa Global Publishers, wifi zako, majirani na marafiki zako wote. Kifo chako kinaendelea kutukumbusha kwamba kila nafsi itaonja mauti na ulipoiaga dunia tulisema:
HAKIKA WEWE NA SISI NI WA MWENYEZI MUNGU NA KWAKE SOTE TUTAREJEA! UWEZO NA UTUKUFU WAKE UTUKUZWE DAIMA - AMIIN!

MASHINDANO YA KLABU BINGWA YA NGUMI KATIKA PICHA

0
0
Mabondia wa timu ya JKT Makao Makuu kutoka kushoto ni Ismail Gaitano,Hmidu Alfani,Khamis Husein na Wambura Amiri klabla awajaingia kwenye mipambano yao
Bondia Selemani Kidunda akikimbilia kona Nyeupe baada ya kumkalisha chini Mohamed Chibumbui kwa konde zito wakati wa mchuano wa Klabu Bingwa TAIFA iliyofanyika uwanja wa ndani wa Taifa Kidunda alishinda  K,O raundi ya kwanza Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Selemani Kidunda wa Ngome kulia  akimuazibu Mohamedi Chibumbui wa Magereza wakati wa mashindano ya Klabu bingwa yaliyofanyika uwanja wa ndani wa taifa Kidunda alishinda kwa K,O rauni ya kwanza na kuzima ngebe za Chibumbui na kusababisha kumpoteza fahamu kwa takribani dakika 4 ambazo alikuwa akipewa uduma ya kwanza uringoni alipodondoka baada ya kupata makonde yenye kilo nzito 

MEYA WA ILALA JERRY SILAA AWATAKA WATANZANIA KUONA KWAMBA SUALA LA USAFI LINATUHUSU WOTE

0
0
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akizungumzia mwamko wa watanzania katika kujitolea kufanya usafi ambapo amesema, bado ni mdogo ndio maana tulisema wakati ule tunaanza mwezi wa saba tutumie karibu miezi mitatu tutoe elimu, lakini tumeongeza miezi mitatu mpaka Desemba na tukaongeza miezi mingine mitatu mpaka Machi, tutoe elimu ili ifike wakati watu wote waone ni majukumu yao kuhakikisha mji uko safi.

Amesema kuwa wamefanya kampeni hii Usafi kuanzia Kata ya Kivukoni na leo Kata ya Kisutu na wiki ijayo wanatarajia kuwa Kata ya Mchafukoge.

Ameongeza kuwa sasa tumeona iko haja ya kuanza kutekeleza sheria, hivyo tunafanya kampeni hizi tukiwa na askari wetu wa jiji na pale tutakapoona mtu au sehemu inatuchafulia mazingira kwa makusudi basi askari watatumika. Mstahiki Meya amesema anaamini kama kila mtu anaweza kuoga mwili wake, kusafisha nyumba yake basi anaweza kuyaweka safi mazingira yanayo mzunguka.

Meneja Msaidizi wa Kampuni ya Usafi ya Green Waste Pro ltd Bw. Abdallah Mbena akizungumzia kampeni hizo za usafi amesema zilianza tangu tarehe 19 Januari katika Kata ya Kivukoni ambapo watu wamejitokeza kwa wingi sana na kufanikiwa kutoa taka nyingi sana katika maeneo ya ufukweni.

Amesema ni kitendo cha kushukuru kuwa watu sasa hivi wanaelewa na kuanza kushiriki katika suala zima la mazingira na pia kuna viongozi wengi wameacha shughuli zao wakaja kushiriki katika kampeni hii ya usafi hivyo zoezi hili likitoka hapa litahamia Kata ya Mchafukoge.

Baada ya kuhitimisha zoezi hilo katika kata hizo tunataka liwe  zoezi endelevu, hatutaki liwe la nguvu za soda kama wengine wengi wameanzisha mikakati kama hii baadae wameishia kwenye makapu, sisi tutaanzisha vipindi katika Television lakini pia katika tarehe za katikati hapa tumeanzisha program ya elimu mashuleni.

Amesema wameanza na shule ya Bunge ambapo amesema katika hatua inayofuata watafanya program na wanafunzi kwa lengo la kusambaza elimu miongoni mwa wanafunzi.

Afisa Usafishaji wa Manispaa ya Ilala Samuel Bubegwa (kushoto) akiwa na viongozi wa kata ya Kisutu kabla ya kuanza zoezi la kusafisha mazingira katika kata hiyo.



Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa (wa kwanza kushoto) akiongoza umati wa wafanyakazi wa kampuni ya Green Waste Pro ltd, wadau wa mazingira, maafisa wa manispaa ya Ilala na wakazi wa kata ya Kisutu wakati wa zoezi la kufanya usafi wa mazingira lilioendeshwa na kampuni ya Green Waste Pro ltd katika maeneo ya kata hiyo ikiwemo mitaro, barabara na maeneo ya wazi na kwingineko.

Afisa Habari wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro ltd Vidah Fammie (wa kwanza kushoto) akishiriki zoezi hilo.

Umoja ni Nguvu Utengano ni Dhaifu.........zoezi la kufagia barabara zinazoizunguka kata ya Kisutu likiendelea.

Moja ya magari ya kisasa ya kampuni ya Green Waste Pro ltd likifagia barabara kwa kutumia Teknolojia inayoenda na wakati.

Barabara ya mzunguko wa DTV ikifagiliwa.

Vijana wakichapa kazi.

Mstahiki Meya Jerry Silaa akimkemea mmoja wa wafanyabiashara ya Chai pembezoni mwa barabara karibu na maeneo ya DTV anayeosha vyombo na kumwaga maji yenye uchafu barabarani.

Mstahiki Meya Jerry Silaa akimuonya kuacha tabia hiyo na kumtaka kufuata utaratibu wa kutunza mazingira kama unavyoelekezwa na manispaa ya Ilala na Kampuni ya usafi ya Green Waste Pro ltd.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo akiunga mkono zoezi la usafi katika maeneo ya Kata ya Kisutu Uhindini jijini Dar leo.

Mstahiki Meya wa manispaa ya Ilala Jerry Silaa (kushoto), Mwanasheria wa Manispaa ya Ilala Paul Wanga na Afisa Usafishaji wa Manispaa ya Ilala Samuel Bubegwa wakivuta pumzi baada ya kupigika na kazi ya kusafisha maeneo ya Kisutu.

Mstahiki Meya Jerry Silaa na viongozi wa manispaa ya Ilala wakifagia korido za majengo ya maeneo mbalimbali ya Kisutu.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiwashukuru wafanyakazi wa kampuni ya usafi katika manispaa ya Ilala ya Green Waste Pro ltd pamoja na wakazi wa kata ya Kisutu waliojitokeza kufanikisha zoezi la usafi katika mazingira yanayowazunguka na kuwataka kujenga utamaduni wa kutunza mazingira.

Rais Kikwete awasili mkoani KIGOMA leo KUONGOZA MAADHIMISHO YA MIAKA 36 YA CCM

0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Mainduzi (CCM),Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,Mh. Issa Machibwa wakati alipo wasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma,Jioni ya leo tayari kwa kuhudhulia Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi (CCM),yatakayofanyika kitaifa kesho kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,Mkoani Kigoma.

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na wananchi wa Mkoa wa Kigoma waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Ndege wa Kigoma kumlaki.
Mwenyekiti wa Chama cha Mainduzi (CCM),Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea salamu kutoka kwa vijana wa Chipukizi wa CCM mkoani Kigoma,wakati alipo wasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma,Jioni ya leo tayari kwa kuhudhulia Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi (CCM),yatakayofanyika kitaifa kesho kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,Mkoani Kigoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mainduzi (CCM),Rais Jakaya Mrisho Kikwete akivishwa skafu na Chipukizi wa CCM mkoani Kigoma wakati alipo wasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma,Jioni ya leo,tayari kwa kuhudhulia Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi (CCM),yatakayofanyika kitaifa kesho kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,Mkoani Kigoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mainduzi (CCM),Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM - Bara,Mh. Mwigulu Nchemba,kulia kwake ni Katibu Mkuu wa CCM-Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana.
Mwenyekiti wa Chama cha Mainduzi (CCM),Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya viongozi wa CCM mkoani Kigoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi CCM CCM,Nape Nnauye. 
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza jambo na Kada wa CCM,Mh.Rajab Mwilima.

Rais Kikwete akisikiliza swali lililokuwa likulizwa na Mwandishi wa Habari wa Radio Uhuru.

cuf yawataka wanzanzibar kuongeza mshikamano na kujiiepusha na itikadi za vyama vyao.!

0
0

Mjumbe wa Baraza kuu la Uongozi la Chama cha C.U.F Juma Duni Haji akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na Wanacha wa C.U.F katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika kiwanja cha Komba wapya Mjini Unguja.(Picha zote na Makame Mshenga).
Baadhi ya Wanacha wa Chama cha wananchi C.U.F wakimsikiliza Mjumbe wa Baraza kuu la Uongozi la Chama hicho Juma Duni Haji katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha Komba wapya Mjini Unguja
=============  =======  =========
NA Maelezo Zanzíbar   .                                

Mjumbe wa Baraza kuu la Ungozi la Chama cha Wananchi CUF Juma Duni Haji amewataka Wazanzibari kuongeza mshikamano na kujiepusha na itikadi za vyama vyao katika kutetea maslahi ya Zanzíbar kwenye Muungano.

Juma Duni ameyasema hayo alipokuwa akihutubia wafuasi wa CUF katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kiwanja cha Komba wapya Mjini Zanzíbar.

Amesema njia pekee ambayo itawasaidia kupata maslahi wanayoyataka katika Muungano ni kuwepo kwa umoja na mshikamano miongoni mwa Wazanzibari jambo ambalo ni chachu ya mafanikio.

Ameongeza kuwa kwa muda mrefu Zanzíbar imekuwa ikibanwa na mambo mengi yanayohusu uchumi wake katika Muungano na kwamba sasa ni muda muafaka wa kupigania Muungano ambao utakuwa wa haki na usawa baina ya Zanzíbar na Tanganyika.

Juma Duni ambaye pia ni Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzíbar amewataka Wazanzibari kuendeleza kudumisha amani iliyopo Zanzíbar sambamba na kutii sheria zilizopo kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Mjumbe wa Baraza Kuu CUF Ismail Jusa Ladu amedai kuwa Wazanzibari wanachotaka katika Katiba mpya ni Muungano ambao utatoa haki sawa baina ya Zanzíbar na Tanganyika.

Amedai kuwa Mshikamano ambao waliuonesha Wazanzibari katika kutoa maoni umewajengea uwezo watu wengine kutoka Bara kuwaunga mkono katika kutetea Muungano ambao unaipa hadhi Zanzíbar.

Mkutano huo umekuja ikiwa ni mwendelezo wa kuhamasisha uhai wa Chama na kutoa elimu ya Muungano kwa wanachama wa chama hicho.

Wadau wa Handeni kukutana Ijumaa Leaders Club

0
0
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

WAKAZI wa Dar es Salaam wenye asili ya wilayani Handeni, mkoani Tanga, pamoja na maswahiba zao, wamepanga kukutana Ijumaa, kuanzia saa kumi za jioni  katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, ili kutafuta namna ya kusaidia watu wasiojiweza wilayani humo.
 
Kikao hicho ni cha kwanza kufanywa na watu wa asili ya Handeni, katika jiji hili ambalo wananchi wengine kutoka mikoa na wilaya mbalimbali wamekuwa wakikutana na kujadili hali ya maisha inayowakabili.
 
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, mmoja wa wajumbe wanaoandaa kikao hicho, kilichopewa jina la ‘Handeni Kwetu’, Kambi Mbwana, alisema kwamba kukutana kwa wadau hao ni sehemu maalum ya kutafuta namna pia ya kusaidiana na viongozi wao kwa ajili ya maendeleo yao.
 
Alisema kwamba Wilaya ya Handeni imekuwa ikikabiliwa na matatizo ya kila aina, ikiwamo njaa na shida ya maji, hivyo kwa wananchi hao kukutana pamoja, wanaweza kupata ufumbuzi katika baadhi ya mambo.
 
“Wakati Handeni ikiendelea kutajwa kama wilaya zisizokuwa na maendeleo kwa miaka 51 ya Uhuru, sisi tunakutana na kutoa kauli moja yenye tija kwa watu wote.
 
“Bila kuangalia nafasi zetu, vipato vyetu au heshima katika jamii, naamini moyo tu wa kukaa na kuzungumza au kuimba wimbo mmoja wa maendeleo, naamini mambo yatakuwa mazuri, hasa pale kitakapofanyika kilichojadiliwa na wote,” alisema.
 
Handeni, inayoongozwa na Muhingo Rweyemamu kama Mkuu wa Wilaya na Mbunge wake Abdallah Kigoda, imetajwa kukumbwa na baa la njaa na kulazimika baadhi ya wakazi wake kulalia mboga mboga pamoja na shida ya maji, jambo linalohitaji kujitolea kwa kila mmoja kwa nafasi yake.

rais kikwete aongoza matembezi ya mshikamano kuadhimisha miaka 36 ya ccm mkaoni kigoma leo.

0
0
 
Mwenyekiti wa Chama cha CCM,Rais Kikwete akisalimiana na Mama Koku pima ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha kusaidia wazee wilaya ya  Kasulu mkoani Kigoma na aliwahi kuwa Katibu wa Wilaya ya Kasulu wa chama cha CCM mkoani Kigoma,walipokutana mapema leo wakati Rais Kikwete alipoongoza Matembezi ya Mshikamano kwa ajili ya kuadhimisha miaka 36 ya CCM,yanayofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa Lake Tanganyika.
  Rais Kikwete akizungumza na baadhi ya Wananchi mbalimbali (hawapo pichani) waliojitokeza katika maandamano hayo  yaliyofana kwa kiasi kikubwa.
 Rais Kikwete akizungumza na baadhi ya Wananchi mbalimbali waliojitokeza katika maandamano hayo  yaliyofana kwa kiasi kikubwa.
 Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akiwasalimia baadhi ya wananchi (hawapo pichani),waliojitokeza kwa wingi kuunga mkono matembezi ya mshikamano ya maadhimisho ya miaka 36 ya chama hicho.
Rais Kikwete akiwapungia mkono baadhi ya wanachi (hawapo pichani) waliojitokeza kushuhudia matambezi hayo yalioanzania kwenye Mnara wa Saa na kukomea kwenye ofisi za mkoa wa Kigoma mapema leo asubuhi.
  Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Siasa na Uhusiano wa Kamataifa Dk. Asha-Rose Migiro akiteta jambo na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete,mara baada ya kumaliza matembezi ya mshikamano
 Matembezi ya mshikamano  ya maadhimisho ya miaka 36 ya CCM,mapema  leo asubuhi ndani ya Mkoa wa Kigoma. 
 Baadhi ya wananchi wakisubiri kushuhudia matembezi ya mshikamano yaliyoongozwa na Rais Kikwete,ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha CCM.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula pichani kulia akifafanua jambo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM-Taifa  Ndugu Abdulrahman Kinana, kulia ni Naibu Katibu Mkuu Bara Ndugu Mwigulu Nchemba apia akisikiliza kwa makini.
Pichani kushoto ni  Naibu Katibu Mkuu Bara Ndugu Mwigulu Nchemba akizungumza jambo na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Siasa na Uhusiano wa Kamataifa Dk. Asha-Rose Migiro  kabla ya kuanza matembezi ya mshikamano mapema leo asubuhi.
 Rais Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu-Taifa wa CCM,Abdulrahman Kinana mara alipowasilia mapema leo kwa ajili ya kuanza matembezi ya mshikamano ya kuadhimisha miaka 36 ya chama hicho.

 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dk. Rais Jakaya Kikwete akijiandaa pamoja na viongozi wengine wa chama tayari kwa kuanza matembezi ya mshikamano mjini Kigoma leo asubuhi.
  Baadhi ya Wananchi wakiwa wamejitokeza kando kando ya barabara kushuhudia maandamano hayo ambayo yamefana kwa kiasi kikubwa.
 Baadhi ya Wananchi wakiwa wamejitokeza kando kando ya barabara kushuhudia maandamano hayo ambayo yamefana kwa kiasi kikubwa.

kumbukumbu ya mzee

0
0


Gration H Matovu
YOU LIVE ON:
IN THE HEARTS YOU TREASURED.
REST IS THINE AND
SWEET REMEMBRANCE OURS.
       YOU ARE GREATLY MISSED
BY YOUR LOVED ONES.
UNAISHI KATIKA MIOYO YA ULIOWAHIFADHI.
PUMZIKO NI LAKO KATIKA BWANA NA
KUMBUKUMBU NZURI NI YETU.
      TUNAKUKOSA SANA TUKUPENDAO.


VODACOM YAFANYA PROMOSHEni YA KUWAJUZA WANANCHI NA WATEJA WAKE KWA KUBORESHA MTANDAO NCHI NZIMA..

0
0
Mfanyabaishara wa kuku katika kituo cha daladala eneo la Banana Ugonga jijini Dar es Slaam, Mussa Nangwali akiangalia simu aina ya GT-E 2232 Sumsung yenye line mbili inayouzwa kwa shilingi elfu 80 wakati Vodacom Tanzania walipokuwa wakifanya promosheni ya kuwajuza wananchi pamoja na wateja wake kuwa imeboresha mtandao kwa ajili ya kuwafikia wananchi mahali popote Tanzania,Kulia ni Mwangalizi wa promosheni hiyo Said Akungoni.

rais kikwete aongoza maelfu ya watu kushiriki maadhimisho ya miaka 36 ya ccm mkoani kigoma

0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dk. Jakaya Kikwete akihutubia wananchi katika sherehe za miaka 36 ya CCM zilizofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa Lake Tanganyika Mkoani Kigoma na kuhudhuriwa  na wananchi mbalimbali waliojitokeza kushiriki katika sherehe hizo. Wawakilishi wa vyama rafiki vya CCM kutoka nchini Burundi CNDD kinachotawala nchini humo, na PPRD kinachotawala nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Naibu Katibu Mkuu CCM-Taifa,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza jambo mbele ya maelfu ya wakazi wa mkoa wa Kigoma mapema leo jioni,waliojitokeza kwa wingi kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya chama hicho.zilizofanyika katika uwanja wa Lake Tanfanyika,jioni ya leo.
Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe akizungumzia mikakati ya Serikali katika maadhimisho hayo juu ya urejeshaji wa huduma za treni katika kituo cha Reli ya Kati cha Kigoma.
 Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza jambao mbele ya maelfu ya wakazi wa mkoa wa Kigoma,waliojitokeza kushiriki maadhimisho ya miaka 36 ya CCM,mkoani humo yaliyofanyika kwenye uwanja wa Lake Tanganyika.

Pichani juu ni Vijana wa Chipukizi wa CCM wakipita kwa Gwaride la heshima na Utii mbele ya Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani).
Sehemu ya umati wa watu walioanza kuleta fujo pale walipoambiwa msanii Diamond atatumbuiza jjukwaani
Msanii wa muziki wa kizazi kipya atambulikanae kwa jina la Diiamond akiwaburudisha maelfu ta wakazi wa mji wa Kigoma waaliojitokeza kwa wingi jioni ua leo kwenye  kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma katika maadhimisho ya miaka 36 ya CCM mjini Kigoma leo.
Pichani kulia ni Nape akimpa maelekezo mafupi  msanii Diamond.
Sehemu ya umati wa watu uliohudhuria maadhimisho hayo.
Bango likioneshwa
Rais Jakaya Kikwete akiwa sambamba na Mkewe Mama Salma Kikwete,wa akiangalia baadhi ya madini yanayopatikana ndani ya mkoa wa Kigoma.
Rais Jakaya Kikwete akiangalia ndizi zinazozalishwa mkoani Kigoma katika banda la wakulima wa ndizi kutoka mkoani huo.

wasanii wa kikundi cha ngoma kutoka nchini Burundi kilichoshiriki katika maadhimisho ya miaka 36 ya CCM,kikitumbuiza mbele ya maelfu ya watu (hawapo pichani).
Rais Jakaya Kikwete akiwapungia mkono wananchi wa mkoa wa Kigoma waliojitokeza kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika mapema leo jioni.

MKURUGENZI MKUU WA UNESCO IRINA BOKOVA'S AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MBILI

0
0

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa akimlaki Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova's aliyewasili nchini usiku wa kuamkia leo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili nchini. Waliobaki nyuma ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Dkt. Alberic Kacou, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mh. Begum Taj na Msaidizi wa Mkurugenzi wa UNESCO.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa (kulia) akimwongoza Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova's sehemu ya mapumziko kwa viongozi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (VIP Terminal) usiku wa kuamkia leo . Bi. Irina Bokova's atakuwa nchini kwa ziara ya Kikazi ya siku mbili itakayoanza leo.

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova's akisalimiana na Katibu Mkuu wa Natcom Prof. Elizabeth Kiondo. Wanaoshuhudia tukio hilo Mkurugenzi Msaidizi wa UNESCO Africa Bi. Lalla Aicha Ben Barka (wa pili kushoto) na Mwakilishi wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen (kulia).

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova's ( wa pili kulia) akizungumza jambo na mwenyeji wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe. Begum Taj na kulia ni Mwakilishi wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen.
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova's akibadilishana mawazo na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawamba kwenye chumba cha mapumziko katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (VIP Terminal) usiku wa kuamkia leo jijini Dar.
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova's (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wenyeji wake Waziri wa Elimu na Maufnzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa (kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe. Begum Taj.
Dk. Shukuru Kawambwa akimsindikiza mgeni wake Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova's.
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova's akiondoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (VIP Terminal) mara baada ya kuwasili nchini Tanzania usiku wa kuamkia leo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

gazeti lako la dira liko sokoni sasa kwa sh 500/= tu

0
0



Exim Bank supports squash development at Gymkhana Club

0
0
Exim Bank Staff and Gymkhana club members pose for a photo during the event.


 

The Exim Bank Tanzania Managing Director Anthony Grant (centre) and the Gymkhana Club Vice Chairman William Chiume (second right) left cut a ribbon to officially open one of the two squash courts refurbished by Exim Bank. Second left is the Dar es Salaam Gymkhana Club squash captain Akil Hirji. 
 The Exim Bank Tanzania Managing Director Anthony Grant (second right) gives a speech during the opening of two squash courts at Gymkhana Club that have been given a face-lift courtesy of Exim Bank. Left is the Dar es Salaam Gymkhana Club squash captain Akil Hirji. 
 The Dar es Salaam Gymkhana Club squash captain Akil Hirji (centre) hands over an award to the Exim Bank Tanzania Managing Director Anthony Grant (second left) in appreciation of the bank’s efforts of giving a face-lift to two squash courts at the club.
An aerial view of one of the Squash courts at the Dar es Salaam Gymkhana club that has been given a face - lift courtesy of Exim Bank

BEN POL, LINNAH, TID na CASSIM MGANGA kwenye STAGE MOJA VaLentine DAY nDani ya NYUMBANI LOUNGE.

0
0

camera ya jiachie ndani ya wilaya ya kasulu mkoani kigoma.

0
0
















AIRTEL YATOA MSAADA WA VITABU VYA SHILINGI MILIONI 9 KWA SHULE ZA SEKONDARI KAGERA

0
0
 Toka kulia ni Afisa Mauzo wa Airtel Kagera bw Leonard maige na Menejamauzo wa kampuni ya Airtel wa mikoa ya Kagera na kigoma bw. PeterKimaro katikati wakikabidhi sehemu ya vitabu vya sekondari vya masomoya sayansi kwa afisa elimu wa shule za sekondari Kagera bw. FlorianKimolo ikiwa ni msaada uliotolewa na Airtel kwaajili ya shule zasekondari kanyeranyere, Kirushya na Nyamigogo za Kagera, Hafla yaMakabidhioano imefanyima katika shule ya sekondari  kanyeranyere yawilaya ya Muleba -Kagera.Mwishoni mwa wiki. Airtel imekabidhi Vitabuvyenye thamani ya shilingi milioni 9
Toka kulia ni Afisa Mauzo wa Airtel Kagera bw Leona Maige na Menejamauzo wa kampuni ya Airtel wa mikoa ya kagera na kigoma bw. PeterKimaro wakiwa na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondarikanyeranyere ya wilayani muleba mkoani kagera wakiwa wameshikiriavitabu vya sayansi na hisabati walivyokabidhiwa na kampuni ya Airtelmwishoni mwa wiki.Vitabu vilivyokabidhiwa vinathamani ya shilingimilioni 9.



=====  =======  ======= ======

AIRTEL YATOA MSAADA WA VITABU VYA SHILINGI MILIONI 9 KWA SHULE ZA SEKONDARI KAGERA

*         Shule za sekondari za kanyeranyere, Kirushya na Nyamigogo
Kagera zakabithiwa vitabu hivyo  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mradi wake wa shule yetu  imeendelea kutoa mchango wake katika sekta ya elimu ili kuboresha  elimu, kuongeza idadi  na ufaulu wa wanafunzi wa sayansi na kupunguza  uhaba wa vifaa vya kusomea mashuleni.  Airtel imefanya hivyo kwa kutoa  msaada wa vitabu vya kufundishia katika shule 3 za sekondari zilizoko Mkoani Kagera mwishoni mwa wiki hii.

Shule zilizofaidika na msaada wa vitabu hivi ni pamoja na shule za
sekondari za  Kanyeranyere iliyoko muleba, Kirushya wilayani Ngara
pamoja na Nyamigogo iliyoko Biharamuro  kagera

Akiongea wakati wa halfa fupi ya kukabidhi vitabu vya masomo ya
sayansi na hisabati  Afisa elimu wa shule za sekondari mkoani Kagera
Florian Kimolo alisema" shule nyingi za sekondari katika mkoa wa
Kagera zimekuwa na upungufu mkubwa wa vifaa vya kujifunzia na
kufundishia sanjari na uhaba wa vifaa vya maabara na walimu.Kutokana
na upungufu wa vitendea kazi katika shule mbalimbali za sekondari hapa
nchini  tunaomba wadau  wa elimu kujitokeza katika kusaidia kulitatua
tatizo hilo ili shule hizo ziweze kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Tunashukuru sana Airtel kwa mchango wao katika elimu na katika
kuhakikisha tunapata wanafunzi wengi wa masomo ya sayansi na walimu
wanapata vitabu vya kutosha katika kufundishia masomo haya na mwisho
kupata ufaulu wa kiwango cha juu.

Naye Meneja  mauzo wa Airtel katika mikoa ya Kagera na Kigoma Peter
Kimaro alisema " Airtel imejipanga kuendeleza ushirikiano na serikali
ili kuisaidia wizara ya elimu kufikia malengo waliojiwekea ikiwemo
upatikanaji wa vitabu mashule na kuongeza kiwango cha  ufaulu. Hadi
sasa kwa kupitia mradi wa " shule yetu tumeweza kufikia shule nyingi
za sekondari nchini. Na nimatumaini yetu vitabu tunavyowakabidhi leo
vitaleta mabadiliko ya elimu kwa shule hizi na mkoa wa Kagera kwa
ujumla.

Naye mkuu wa shule ya sekondari Kanyeranyere iliyoko wilyani Muleba
mkoani Kagera alitoa shukurani kwa niaba ya walimu wakuu wa shule za
sekondari za kanyeranyere, Kirushya na Nyamigogo na kusema,
tunashukuru Airtel kwa kuzikumbuka shule za mkoani Kagera, tunaahidi
kuvitumia vizuri vitabu hivi ili kuleta ufanisi zaidi na maendeleo ya
kitaaluma katika shule zetu.

Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia vitabu mashuleni,
zaidi ya shule 900 za sekondari hapa nchini zimenufaika kupitia
kampeni ya mradi wa kampuni ya simu za mkononi Airtel ujulikanao
"Airtel  shule yetu".

MKURUGENZI UNESCO AWASILI ZANZiBAR

0
0


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO Bi. Irina Bokova amewasili leo Zanzíbar kwa ziara rasmi ya siku mbili.

Mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Amani Karume Bi.Bokova amepokelewa na Mwenyeji wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzíbar Ali Juma Shamuhuna.

Kwa mujibu wa Ratiba ya ziara yake Bi.Bokova atafanya atatembelea maeneo mbali mbali ya Mji Mkongwe ikiwa ni pamoja na kukagua Jengo la Makumbusho kuu ya Taifa ambalo lilianguka katika siku za karibuni.

Kesho Bi.Bokova atakuwa na Mazungumzo na Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzíbar wanaohusiana na Ofisi yake ikiwemo Waziri wa Wazira ya Elimu, Waziri wa habari Utamaduni Utalii na Michezo, Waziri wa Ustawi wa Jamii maendeleo ya Wanawake na Watoto na Waziri wa Ardhi Makaazi Maji na Nishati katika Hoteli ya Serena mjini Zanzibar.

Aidha Bi. Bokova baada ya Mazungumzo hayo anatarajiwa kufanya Mkutano na Waandishi wa habarí kuhusiana na ziara yake.

Mkurugenzi huyo wa UNESCO atahitimisha ziara yake kwa kumtembelea Rais wa Zanzíbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein Ofisini kwake. 

IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR

TPBC INAWATAKA MABINGWA WAKE WOTE WAWE WAMETETEA MIKANDA YAKE IFIKAPO MARCH, 2013

0
0

 Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini TPBC inewataka mabingwa wake wote wawe wametetea mikanda yao ya ubingwa ifikapo tarehe 30 Marchi kwaka huu ili kuepuka kunyanganywa.

Kwa kipindi kirefu mabingwa kadhaa wamekuwa wanakaa na mikanda bila kuitetea. Tunataka ieleweke kuwa muda wa kukaa na ubingwa wa TPBC ni miezi sita (6) tu na sio mwaka mmoja.

Bingwa wa kweli anatakiwa awe anafuata sheria, kanuni na taraibu za ubingwa alionao na sio kujiita bingwa wakati hufuati masharti yaliyowekwa.

Katika kipindi hiki cha mwaka 2013 tunawataka mabondia waheshimu sheria za mikataba wanayotiliana sahihi na mapromota. Tunataka ngumi ziboreshwe kakini pamoja na changamoto nyingi zilizoko, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa wadhamini, mabondia wakiheshimu mikataba yao mchezo wa ngumi utakua na kuwavutia wadhamini.

Tunapenda pia kuwaomba wenye mapenzi mema na nchi hii wajitolekeze kwa wingi ili kushirikiana na sisi tuiweke Tanzania kwenye chati ya dunia kama zilivyo nchi nyingine.

Imetolewa na:
  
Onesmo A.M. Ngowi
Rais,
TPBC
Dar-Es-Salaam, Tanzania

NYIMBO ZA JAY MO ZAWAENDESHA PUTA WASHIRIKI THE MIC KING

0
0
Ally Kawina akichana mistari ya moja ya nyimbo zilizowahi kuimbwa na Jay Mo.
Martin Fundi akishiriki mchuano huo.
Ally Zuberi akionyesha umahiri katika mistari ya Jay Mo.
Jay Mo akiwaangalia kwa umakini washiriki walioimba nyimbo zake.
…Akiwachana washiriki waliboronga.
Jay Mo akiwa amepozi na majaji (kutoka kushoto) Abdallah Mrisho, DJ John Dilinga na Baucha.
Majaji Mrisho, JD na Baucha baada ya kumaliza shughuli hiyo.
MWANAMUZIKI mkongwe wa muziki wa kizazi kipya, Juma Mohamed Mchopanga ‘Jay Mo’, jana usiku alikuwa mwiba mchungu kwa washiriki wa The Mic King shindano linalofanyika kila Jumapili katika ukumbi wa burudani wa Taifa wa Dar Live uliuopo Mbagala jijini Dar es Salaam.
Washiriki hao waliambiwa waimbe nyimbo yoyote ile ambayo imeimbwa na mwanamuziki huyo na majaji kuendelea na maamuzi yao huku Jay Mo akikosoa, kusifia na kupongeza kwa wale ambao walimudu kuimba vyema mistari yake.
(PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY, GPL)

GHANA TO REASUME ITS ROLE AS THE BOXING POWER HOUSE IN WEST AFRICA

0
0

DAR-ES-SALAAM, TANZANIA.

Discussions are at a final stage for the Ghanaian Middleweight champion Issah Samir to meet his countryman Philip Kotey for the “IBF Continental Africa Middleweight Crown” in March 30th.

Another card on the offing in the same day March 30th will see the world class boxer Albert Mensah meeting Ben Odamettey also from Ghana for the “IBF Continental Africa Welterweight Title” respectively.

The tournament will be promoted by both Golden Concept and Gold Mike Boxing Promotions Syndicate as undercards in Helen Joseph vs. Mariana Gulyas for their IBF Vacant Intercontinental Female Crown.

ISSUED BY:

INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)

DAR-ES-SALAAM, TANZANIA.
Viewing all 46194 articles
Browse latest View live




Latest Images