Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46366 articles
Browse latest View live

WANAMUZIKI WATAKAOSHIRIKI TAMASHA LA PASAKA KUPIGIWA KURA NA MASHABIKI

$
0
0
1
Bw. Alex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka akizungumzia maandalizi ya tamasha hilo ambapo amesema utaratibu wa kuwapata waimbaji katika tamasha hilo mwaka huu ni kwamba waimbaji wote watakaoshiriki watapigiwa kura na mashabiki wa muziki wa injili ili kuleta ushindani kati ya waimbaji lakini pia kuwaachia mashabiki wenyewe wachague ni mwimbaji gani wanamuhitaji katika tamasha hilo badala ya kutumia utaratibu wa mwanzo.



=======  ======    =======

Na Edina Kahurananga (DSJ)

KAMPUNI ya msama promotions hivi karibuni ilitangaza zoezi la upigaji kura kuchagua  taratibu za ufanyikaji wa Tamasha la Pasaka la mwaka huu linalotarajia kuanza Aprili 20 mwaka huu.


Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Abihudi Mang’era zoezi la upigaji kura litahusika kuchagua mikoa, mgeni rasmi na waimbaji watakaoimba katika tamasha hilo.


Mang’era alisema mwaka huu wametoa nafasi hiyo ili kuwapa nafasi mashabiki wa muziki wa Injili kuchagua mikoa, mgeni rasmi na waimbaji watakaoshiriki katika tamasha hilo.  Aidha Mang’era alifafanua kuwa ili kumchagua mgeni rasmi unaanza na neno Mgeni rasmi Pasaka  unaacha nafasi kisha jina la mgeni rasmi kwenda 15327.


Mang’era alisema kumchagua mwimbaji katika tamasha hilo ni kuandika neno Mwimbaji Pasaka  unaacha nafasi jina la mwimbaji kwenda namba 15327 sambamba na kuchagua mkoa, unaandika neno Mkoa Pasaka  unaacha nafasi kwenda namba 15327.


Makamu huyo Mwenyekiti  alitoa wito kwa Watanzania kupiga kura kuchagua nafasi hizo tatu ili kufanikisha tamasha hilo.

LORI LA MAFUTA LADONDOKA MDA HUU MLIMA SEKENKE NA KULIPUKA NA KUUA WATU WANNE

$
0
0

Lori la mafuta limeanguka jioni hii katika eneo la milima ya sekenke mkoani singida na kuua watu wanne hapohapo.Chanz cha ajali hiyo ni breki kufeli kukamata wakati lori hilo lilipokuwa linashuka mlima huo.Shuhda wa ajali hiyo bwana Julius chacha alipoongea na mtandao wetu wa Dj sek blog amesema kwamba Lori hilo lilipoacha njia lilipinduka na kuingia bondeni na kushika moto.Akiendelea kuongea shuhda huyo alisema walishindwa kutoa msaada wowote kwa kwa moto uliposhika ulikuwa mkubwa na hawakuwa na vifaa vya kuokolea.Watu wanne wamekuufa papo hapo kutokana na ajali hiyo.Polisi walikuwa bado hawajafika eneoo la tukio mpaka tunaondoka eneo la tukio.PICHA NA HABARI NA DJ SEK BLOG
 Wanainchi wakiangalia Lori baada ya kuungua
 Mabaki ya Lori hilo bada ya kuteketea kabisa na moto jioni hii
 Baadhi ya wasafiri wakitazama lori lililongua jioni hii

 Bonde la mlima sekenke linavyoonekana na baadhi ya miti imeunguaa
 Hii ni njia ya mlima sekenke


THE LADIES WAKALI WA VITAFUNWA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 
Ujasiriamali ni jambo lililojema miongoni mwa jamii. Watu wengi wamekuwa wakilalamika kukosa vitu vya kufanya ili kuweza kujipatia kipato na kuacha kuwa tegemezi kwa wazazi au waume na hata wakati mwingine wake zao. Wana dada wawili marafiki ambao kwa bahati majina ya ubini ya wazazi wao yanafanana na wao kuamua kujiita ndugu,  Joan Joseph Massawe (pichani kulia)  na Angel Fabian Massawe wao kwa kuliona hilo waliamua kuanzisha bishara ambayo itawapatia kipato cha ziada mbali na ajira zao nma kuwasaidia katika masomo yao.

Wakiuambia mtandao huu wa Father Kidevu Blog kuwa wao ni wasomi na wameamua kuopika vitafunwa vya aina mbalimbali na kuviuza na pia wamekuwa wakifanya hivyo katika tafrija mbalimbali kwa kupika bite. 
Muiongoni mwa vitu ambavyo leo viilivuta FK Blog hadi katika meza ya wana dada hao 'The Ladies' iliyopo katika maonesho ya Tamasha la Mwanamke na Akiba ndani ya Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam ni vitumbua. Yes Vitumbua hivi hivi, maana ni vikubwa na vinamvuto. Lakini pia katika meza yao kulikuwa na vitu vingi kama chapati za maji na kusukuma, sambusa, kababu, kalimati, na kalimati.

Wanadada hawa ni mfano wa kuigwa kwa namna ambavyo waliamua kubuni biashara hiyo. Na niwazi kuwa hata hapo baade wakiwa na kampuni kubwa ya biashara hii sitaweza jkushangaa.
 Pichani ni Angel na Joan wakiwahudumia wake wa viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mke wa Makamu wa Rais mama Asha Bilali aliyekuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa tamasha la Mwanamke na Akiba.
 Angela na Joan wakimhudumia mama Asha Bilali vitumbua hivi ambavyo leo navizungumzia.
 Hakika kila mama aliyepita katika banda hilo hakuacha kununua kitafunwa.
 Vitumbua hivyoooo kazi kwenu wana dada hawa wanapatikana Oysterbay barabara ya Bongoyo.  

MAWASILIANO ZAIDI KWA WENYE UHITAJI: 
+255 713 185065 AU +255 652 035652

MAFUNZO YA BURE YA UIGIZAJI FILAMU NA UIMBAJI

$
0
0

RAFIKI ELIMU   MUSIC   &  FILM  ACADEMY
·        Je  wewe  ni  kijana  wa  kitanzania?
·       Una  umri  wa  kuanzia  miaka 15  na  kuendelea ?
·       Una  ndoto za  kuwa  muigizaji filamu  mkubwa  nchini  Tanzania?
·       Una  ndoto  za  kuwa  mwanamuziki ama  muimbaji  mkubwa hapa  Tanzania ?

RAFIKIELIMU  MUSIC &FILM  ACADEMY   ni  kituo  kinachotoa  mafunzo  ya  UIGIZAJI  na  UIMBAJI  kwa  vijana wa kitanzania  wenye  umri  wa  kuanzia  miaka  kumi  na  tano na  kuendelea.
Wahitimu  wa  mafunzo  haya  hupata  nafasi  ya  kushiriki  katika  filamu , maigizo, tamthiliya  na nyimbo mbalimbali   zinazo  tayarishwa  na Taasisi  ya   RAFIKIELIMU  FOUNDATION.

ADA  YA  MAFUNZO :  Mafunzo  haya  hutolewa BURE!
Mafunzo  yataanza rasmi  tarehe  02 MACHI  2014.
Mwisho  wa  kujiandikisha   ni  tarehe  28 FEBRUARI 2014.
Chuo  chetu  kinapatikana  katika  eneo  la  CHANGANYIKENI karibu  na  CHUO  CHA  TAKWIMU mbele  ya  CHUO  KIKUU  CHA  DAR  ES  SALAAM.

Kufika  Chuoni  kwetu, panda  daladala za  UBUNGO-CHANGANYIKENI  kisha  shuka  katika  kituo  cha  TAKWIMU  halafu  tembea  hatua  ishirini  mbele, utaona  bango  limeandikwa  RAFIKIELIMU  FOUNDATION.

JINSI  YA  KUJIANDIKISHA :Tuandikie  barua  pepe  kwenda : rafikielimutanzania@gmail.com    
Kwa  maelezo zaidi, wasiliana  nasi  kwa  SIMU 0784406508   Au  Tembelea 
                www.rafikielimu.blogspot.com

WAJASILIAMALI KUPATIWA MAFUNZO IRINGA

$
0
0

 Fredrick Mwakalebela mmoja wa wakufunzi watakaotoa mafunzo kwa wajasiliamali wa mkoa wa Iringa Feb 22
Mratibu wa semina ya ujasiliamali Anzawe Chaula akizungumza kuhusu semina hiyo ya februari 22 ofisini kwake. (Picha na Denis Mlowe)
========  =======  =========
WAJASILIAMALI KUPATIWA MAFUNZO IRINGA

Na Denis Mlowe,Iringa

KAMPUNI ya Vannedrick Tanzania limited (VTL) ya jijini Dar salaam kwa kushirikiana na Kituo cha Maendeleo,Haki na Utetezi TCDA cha mjini Iringa wameandaa semina ya ujasiliamali kwa wakazi wa manispaa ya Iringa zaidi 1000 inayotarajiwa kufanyika Februari 22 mwaka huu.

Akizungumza mratibu wa Semina kutoka TCDA  Anzawe Chaula alisema lengo la kuandaa semina hiyo itakayojulikana kwa jina la Jukwaa la Wajasiliamali ni kuwakomboa wakazi wa mkoa wa Iringa kuondokana na umaskini na kuweza kujitambua katika utengenezaji wa malighafi mbalimbali.

Alisema katika semina hiyo itafanyika katika ukumbi wa Hallfare kutakuwa na mafunzo mbalimbali yanayohusu elimu juu ya kutafuta masoko ya bidhaa kwa wajasiriamali, jinsi ya kupata fursa za mikopo kutoka katika benki mbalimbali za ndani nan je ya nchi ya Tanzania.

Chaula alisema jukwaa la wajasiliamali litawafundisha wajasiliamali kutambua haki za kisheria katika biashara wafanyazo pamoja na kuratibu mafunzo ya mara kwa mara ya kuwajengea uwezo katika shughuli zao za kila siku.

“Kuna umuhimu mkubwa sana kwa wajasiliamali kupatiwa mafunzo ya mara kwa mara katika shughuli zao wazifanyazo kutokana na wengi wao kufanya biashara bila kuwa na elimu mtambuka ya kufanya kazi hizo na kuweza kujiongezea vipato hivyo sisi tutawapatia mafunzo hayo na naomba sana wajitokeze kwa wingi kuweza kuelimika juu ya ujasiliamali.” Alisema Chaula.  

Aliongeza kuwa semina hiyo itawajengea uwezo wajasiliamali katika kutafuta na kutambua fursa mbalimbali zilizoko katika mkoa wa Iringa zikiwemo za utalii wa ndani ambao uko chini sana katika kutumia fursa hizo.

Aidha wajasilimali watapatiwa fursa ya kufungua biashara zinazoendana na wakati uliopo ukiwemo ujenzi wa barabara ya Iringa hadi Dodoma inayotarajiwa kukamilika mwakani kuweza kufungua miradi mbalimbali pembezoni mwa barabara hiyo na kuwatumia wanafunzi walioko vyuoni kujiongezea mapato.

Chaula alisema katika semina hiyo wakufunzi watakaoelimisha wajasiliamali ni Mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF), Dk Didas Lunyungu kutoka Dar salaam na Fredrick Mwakalebela na  mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi.

mama asha bilali afungua Tamasha la mwanamke na akiba leo Dar Live, Mbagala

$
0
0
  Mke wa makamu wa Rais Mama Asha Bilali ambaye alikuwa mgeni rasmi wa Tamasha la   Mwanawake weka akiba, akisoma hotuba  ya ufungunzi wa tamasha hilo,leo jijini Dar es salaam katika viwanja vya Dar live Mbagala.
 Mke wa Waziri Mkuu mstaafu Mama Esther Sumaye akiwasalimia wajumbe waliofika katika ufumbuzi wa Tamasha la Mwanawake weka akiba,Anayepiga makofi mbele ni mke wa Waziri Mkuu mstaafu Mama Regina Lowassa na Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilali.
 Mke wa Waziri mkuu Mama Tunu Pinda akitoa maelekezo ya jinsi ya kutumia asali kwa Mgeni rasmi mke wa Makamu wa Rais Mama Asha bilali katika Tamasha la Mwanawake weka akiba,leo jijin Dar es salaam.
 Mke wa makamu wa Rais Mama Asha Bilali ambaye alikuwa mgeni rasmi wa Tamasha la Mwanawake weka akiba, akikata utepe ikiwa  ishara ya kufungua rasmi  tamasha hilo ,leo jijini Dar es salaam katika viwanja vya Dar live Mbagala.
 Mkurugenzi  Mkuu wa Angles Moments  Naima Malima  akisoma risala ya kumkaribisha mgeni rasmi Mke wa Makamo wa Rais, Mama Asha Bilali katika ufunguzi wa  tamasha la Mwanawake weka akiba litakalofanyika kwa siku tatu katika viwanja vya Dar live Mbagala.
 Washiriki wa tamasha la Mwanamke weka akiba  wakifuatilia kwa makini mambo mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea katika viwanja vya Dar live Mbaggala. 
Meneja Uhusiano  na Masoko wa  Mfuko wa Pesheni PPF,Lulu Mengele akipokea tuzo ya udhamini  kutoka kwa  Mke wa makamo wa Rais Mama Asha Bilali katika tamasha la Mwanawake weka akiba,leo jijini Dar es salaam. Picha zote na Lorietha Laurence-Maelezo.

SEMINIA YA WASANII WA BONGOMOVIE KUFANYIKA IJUMAA VIJANA HALL KINONDONI

$
0
0
Mwenyekiti wa Bongo Movie Steve Nyerere(kati) akifafanua jambo kuhusiana na Semina ya Wasanii Bongo Movie itakayofanyika Siku ya Ijumaa kwenye Ukumbi wa Vijana uliopo Kinondoni Dar es Salaam, kulia ni mkurugenzi wa Kampuni ya Chief Promotion, Amon Mkoga na Meneja Msaidizi wa PSPF, Matrida Nyallo. katika hafla iliyo fanyika kwenye Ukumbi wa Idara Habari Maelezo.

TAARIFA YA IKULU YA UFAFANUZI KUHUSU BARAZA LA MAASKOFU WA KIPENTEKOSTE TANZANIA (PENTECOSTAL COUNCIL OF TANZANIA) KUTOKUWA NA UWALIKILISHI KATIKA BUNGE MAALUM LA KATIBA


MSAADA TOKA UINGEREZA KWA MAMA WA MAPACHA WANNE WA MBEYA

$
0
0
Misaada ya hali na mali imeanza kumiminika kwa ajili ya Aida Nakawala (25) mkaazi wa kijiji cha Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya, ambaye alijifungua watoto wanne mapacha kwa mkupuo (Quadruplets) usiku wa kuamkia Mwaka mpya wa 2014 katika Hospitali ya Wazazi ya META jijini Mbeya. 

 Msamaria mwema wa Uingereza, Bi Gladness Sariah, ametuma maboksi mawili yenye nguo na vitu kadhaa vya watoto, ambavyo vimewasili salama katika ofisi za Michuzi Media Group (MMG) inayoendesha Globu ya Jamii jijini Dar es salaam baada ya kusafirishwa bure na Wazee wa Kazi, Serengeti Freight Forwarders ya huko Uingereza. 

 Hivi sasa MMG ikishirikiana na waratibu wa misaada kwa mama huyo, Mbeya Yetu Blog, wanaandaa utaratibu wa kumfikishia Mama Aida mizigo yake haraka iwezekanavyo.
 Kwa niaba ya mzazi wa mapacha hao, Michuzi Blog na Mbeya Blog zinatoa shukrani za dhati kwa msamaria mwema Gladness Sariah kwa wema na upendo aliouelekeza kwa mzazi huyo. Huo ni mfano wa kuigwa, na tunatarajia misaada zaidi itatolewa na wasamaria wema ambao tunajua mko wengi kila kona ya dunia. 
 Kama umeguswa na hili na unataka kutoa msaada tafadhali wasiliana na: issamichuzi@gmail.com ama jmwaisango@yahoo.com 
nasi tutafikisha ubani wako. 
Serengeti Freight wametoa ofa ya 
kusafirisha bure misaada ya aina hii 
ASANTENI SANA
Michuzi Blog/Mbeya Yetu Blog

Aida Nakawala 25 mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, hivi karibuni alijifungua watoto wanne  mapacha kwa mkupuo(Quadliplets) katika usiku wa kuamkia Mwaka mpya anaendelea vizuri.

Mwanamke huyo ambaye kwa hivi sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wazazi ya Meta akiwa na watoto wake wote wanne alijifungua majira ya saa 10 alfajiri usiku wa kuamkia Januari Mosi Mwaka huu katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi na watoto wakiwa na uzito wa kawaida tofauti na matarajio ya Wengi.



 Misaada kwaajili ya Aida Nakawala (25) mkaazi wa kijiji cha Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya mara baada ya kufikishwa katika makao makuu ya Globu ya Jamii jijini Dar es salaam baada ya kusafirishwa bure toka Uingereza na Wazee wa Kazi Serengeti Freight.

WATAALAMU CHUO KIKUU WATOA RIPOTI YA UZIMAJI WA MITAMBO YA ANALOJIA AWAMU YA KWANZA

muziki wa Tanzania kwa kishindo ndani ya New York Time

$
0
0
The concrete lot next to the Hotel Travertine in downtown Dar es Salaam was full of swaying women in elaborate floor-length gowns trimmed with sequins. Spotlights reflected off bottles of Kilimanjaro beer, and the scent of shisha smoke hung in the air.
It was 11 on a Sunday night in Tanzania’s largest city, and members ofJahazi Modern Taarab, a popular local group, were performing a spirited song about love gone wrong, featuring a male-female call-and-response. Young men, chewing khat leaves and tapping their feet to the music, sat in white plastic chairs next to older women in neon-colored headscarves. For certain songs, the crowd rushed to the dance floor en masse.
Stop by the hotel on any Sunday and you’ll find the band in full swing. Indeed, many bands in this laid-back city on the Indian Ocean have regular gigs at the same venues every weekend, and as many as four concerts at other clubs during the week — all part of a boisterous and exciting music scene that rivals that of any in Eastern Africa.
Launch media viewer
Jagwa Music performs. Nichole Sobecki for The New York Times
“Tanzanians, they love music. I think they want music to play every day so they can come,” said Jackie Kazimoto, lead singer of Jagwa Music, one of the city’s most thrilling live acts.
Dar’s soundscape is a riot of genres, from the music on offer that evening, called modern taarab, which mixes a traditional Swahili sung-poetry style with electronic and Arab-influenced rhythms, to mchiriku, the raw, urban sound that Jagwa Music plays, which is generally found at neighborhood block parties. You can also dance to classic rumba or bongo flava, the local brand of hip-hop, on soft white sand at any number of palm-laden beach clubs, while a pink sun sets over the ocean.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF yaanza kukagua miradi Mkoani Ruvuma

$
0
0
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Hassan Bendeyeko akitoa ufafanuzi juu ya utekelezaji wa miradi ya TASAF katika halmashauri za wilaya na Manispaa Mkoani Ruvuma kwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF Abbas Kandoro, ambaye ameongoza wajumbe wa kamati hiyo kukagua miradi iliyotekelezwa na TASAF kwa kushirikiana na wananchi katika Mkoa wa Ruvuma.
  Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF Abbas Kandoro akisisitiza jambo kwa viongozi (hawapo pichani) wa halmashauri ya wilaya ya Songea na Manispaa ya Songea baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa miradi ya TASAF katika awamu ya pili.

 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF Abbas Kandoro akielekea kukagua mradi wa maabara katika shule ya sekondari ya Mfaranyaki katika Manispaa Songea. Katika shule hii imetekelezwa miradi mitatu ambayo ni Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, maabara mbili na jengo la utawala vilivyogharimu shilingi milioni 197
  Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF ikikagua maabara ya kemia katika shule ya sekondari ya Mfaranyaki Mjini Songea ambako imepokea maelezo kuwa kwa hivi sasa ufaulu wa wanafunzi wanaosomea sayansi ni mzuri kuliko wanafunzi wanaosomea masomo ya sanaa baada ya kuanza kutumika kwa maabara hizo
Baadhi ya wa wajumbe wa kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF wakiwa katika kikao na kamati ya ujenzi ya shule ya sekondari Mfaranyaki. Kutoka Kushoto Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu anayeshughulikia TAMISEMI Bw Zuberi Samataba, Makamu Mwenyekiti wa Kamati Tendaji TASAF Abbas Kandoro na Nyanchege Nanaghi
 Wajumbe wa kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukagua miradi ya TASAF katika shule ya sekondari ya Mfaranyaki Mjini SONGEA.

droo ya pili ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti washindi wawili wapatikana

$
0
0
  Meneja wa bia ya Serengeti Rodney Rugambo  (kushoto) akionyesha zawadi ya simu aina ya Samsung Tab ambayo washindi 2 wa droo ya winda safari ya Brazili  na Serengeti  wamejishindia katika droo iliyochezeshwa leo asubuhi. Anayeshuhudia ni afisa mwandamizi wa PWC Bw Tumaini aliyeko kulia. 
 Meneja wa bia ya Serengeti Bw Rodney Rugambo (katikati) akitangaza mshindi wa promosheni ya winda safari ya  Brazilin a Serengeti aliyejishindia simu aina ya Samsung Tab. Wanaoshuhudia ni msimamizi wa michezo ya bahati nasibu Bw Abdala aliyeko kushoto na afisa mwandamizi wa PWC Bw Tumaini aliyepo kulia.
 Meneja wa bia ya Serengeti Rodney Rugambo (katikati) akiongea na mshindi wa droo ya winda safari ya Brazil na Serengeti aliyejishindia simu aina ya Samsung Tab. Wanaoshuhudia ni msimamizi wa michezo ya bahati nasibu Bw Abdala aliyeko kushoto na afisa mwandamizi wa PWC Bw Tumaini aliyepo kulia.
============   ==========   =========

WINDA SAFARI YA BRAZILI NA BIA YA SERENGETI

BIA YA SERENGETI YAENDESHA DROO YAKE YA PILI YA KAMPENI YA ‘WINDA SAFARI YA BRAZILI NA SERENGETI’!


Februari 19, 2014:  Wiki iliyopita tulishuhudia washindi wakijinyakulia zawadi zao kwa furaha baada ya kushinda katika droo inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti ya “Winda safari ya Brazili na Serengeti”. Asubui ya leo Kampuni ya Bia ya Serengeti imeendesha droo yake ya pili katika Kiwanda cha Bia cha Serengeti.


Droo iliyochezeshwa kiwandani hapo mapema leo, ilishuhudiwa na wana habari, maafisa waandamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha, PWC, na Push Mobile. Promosheni hii ya kurudisha fadhila kwa wateja itaendeshwa kwa wiki 10 zijazo. Katika droo ya pili ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti wamepatikana washindi wawili wa Samsung tab Mwl. Jacob Nnko, 36, wa Nansio, Ukerewe na Vedastus Kalinga kutoka Tunduma, Mbeya .

Akizungumza kupitia simu ya kiganja mshindi wa Samsung tab Vedastus Kalinga kutoka Tunduma mkoani Mbeya, alishikwa na butwaa na kujiona mwenye bahati mara baada ya kutamkiwa kuwa ni moja ya mshindi wa simu aina ya Samsung tab kupitia kampeni hii. 

Washindi hao hawakutegemea kuwa miongoni wa washindi wa droo ya promosheni hiyo.  Mshindi wa pili wa alielezea furaha yake na kuonekana kutoamini alichosikia. Washindi wote wawili waliishukuru Kampuni Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa kuwajali wateja wake siku zote na kuwatimizia mahitaji yao kwa kufanya vitu vya kustaajabisha kila kukicha alisema. Mwalimu Jacob alisema “kwakweli siamini, inanipa furaha na kujivunia kuwa mteja wa bia Serengeti. Kwa mimi kuwa mwenye bahati ya kupata Samsung tablet inanipa ari kubwa hasa katika ulimwengu wa sasa wa dijitali.


Meneja wa bia ya Serengeti, Bwana Rodney Rugambo alieleza kuwa promosheni iliyofunguliwa kwa wateja wote nchi nzima ambao wameshaanza kunufaika na kampeni hii. Zaidi ya wateja 500 wamejishindia bia za bure na wengine zaidi ya 200 wamejishindia fedha taslimu za kitanzania Shilingi 5000 na shilingi 10,000 ndani ya wiki hii ya pili ya promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti. 

Wote hao wamepata zawadi zao kupitaia simu ya kiganjani kwa kutuma maneno na tarakimu zilizopo chini yz kizibo kwenda namba 15317. Aliendelea kuelezea kuwa wateja wengi wameweza kufaidika zaidi kwani pia wameweza kupata washindi watano (5) waliojishindia ving’amuzi vya Azam, washindi hao ni  Godbles Sehaba(31), Karushe Mathias (34)  kutoka Dar es Salaam, Rose Joseph Swai  (32) kutoka Moshi, Denis Kigoi Mbaga (45) kutoka Arusha and Julius Chao (26) kutoka Mbeya.

.

“Tunataka kuwakumbusha wateja wetu kuwa bado tuna zawadi za kutosha za kushindaniwa katika promosheni hii kubwa zaidi ni ile ya safari ya Brazili itakayolipiwa gharama zote. Pia tunatoa ving’amuzi vya Azam na Samsung tab kwa wateja wetu chakufanya ni wewe kufungua bia yako ya Serengeti kokote nchini na fuatilia maelezo ya promosheni na uweza kuwa mshindi wetu wa wiki inayokuja. Pia unaweza kufuatilia kupitia ukurasa wetu wa facebook www.facebook.com/serengetipremiumlager. Tumeanza vizuri hivyo hatuna budi kuwashukuru wateja wetu.” aliongeza Rugambo. 

MSANII KING MAJUTO,LUFINGO,MUHOGO MCHUNGU WATOKA NA XDENT

$
0
0

MKURUGENZI Mkuu wa Kampuni ya usambazaji wa filamu za kiswahili Lufingo Exaud amesema kuwa wameingiza mtaani filamu yao mpya ijulikanayo kwa jina la xdent ambayo imeshilikisha wasanii mbalimbali wenye majina katika filamu hiyo

utakutana na King Majuto, Muhogo Mchungu, Lufingo, Mzee Pembe na wasanii mbalimbali walio bobea katika sanaa hii ya filamu nchini

filamu hiyo iliyorekodiwa kwa ubora wa hali ya juu na umakini mkubwa yenye mafundisho ndani yake itakuwa chachu kwa jamii kujirekerbisha katika maisha yao ya kila siku

kwa sasa filamu hiyo inapatikana maduka yote yanayouza kanda za kiswahili nchini tanzania na mikoa yote kiujumla

hivyo wapenzi wa filamu waende kununua dvd halali ili waendelee kukuza kipato cha wasanii nchini filamu hiyo ambayo imewashilikisha wasanii wengi wakubwa imekuwa ikigombaniwa sokoni kutokana na ubora wake pamoja na wasanii wenyewe jinsi walivyo onesha uwezo mkubwa wa kuitendea haki filamu hiyo

Kituo cha mafunzo chazinduliwa kuiongezea thamani soko la ajira la uhandisi na usimamizi wa miradi

$
0
0
 Debra Backlund, one of the founders of Desktop Publishing Institute (DPI) speaks during the launch of Computer Aided Drafting and Design (CADD) Center Dar es Salaam, which is a franchise of CADD Center India. The Center plans to train more than 1,200 Tanzanians in professional architectural, engineering and project management job sector annually. Right is Tanzania Commissioner for Education Prof. Eustella Bhalalusesa and center is Director at CADD Center Dar es Salaam Shafiq Abdulrasul.
 Tanzania Commissioner for Education Prof. Eustella Bhalalusesa speaks during the launch of Computer Aided Drafting and Design (CADD) Center Dar es Salaam, which is a franchise of CADD Center India. The Center plans to train more than 1,200 Tanzanians in professional architectural, engineering and project management job sector annually. Seated are Hanif Abdulrasul (second left) followed by Shafiq Abdulrasul, Directors at CADD Center Dar es Salaam, and Managing Director CADD Center Mr Saravanan Karaiadiselvan India.
 Tanzania Commissioner for Education Prof. Eustella Bhalalusesa hands over a certificate to Aci Muzaffer Ismail- one of the graduates from Computer Aided Drafting and Design (CADD) Center Dar es Salaam- during a ceremony to officially launch the center, which is a franchise of CADD Center India. Left is Hanif Abdulrasul, (second right) Shafiq Abdulrasul, Directors at CADD Center Dar es Salaam and right is Managing Director CADD Center India Mr Saravanan Karaiadiselvan. The Center plans to train more than 1,200 Tanzanians in professional architectural, engineering and project management job sector annually.

 Tanzania Commissioner for Education Prof. Eustella Bhalalusesa hands over a certificate to Rajabu Saidi Mofi- one of the graduates from Computer Aided Drafting and Design (CADD) Center Dar es Salaam- during a ceremony to officially launch the center, which is a franchise of CADD Center India. Left is Hanif Abdulrasul, (second right) Shafiq Abdulrasul, Directors at CADD Center Dar es Salaam and right is Managing Director CADD Center India Mr Saravanan Karaiadiselvan. The Center plans to train more than 1,200 Tanzanians in professional architectural, engineering and project management job sector annually. 
 Tanzania Commissioner for Education Prof. Eustella Bhalalusesa receives a gift from Abdulkarim Bashir, an instructor at Desktop Publishing Institute (DPI), during a ceremony to officially launch Computer Aided Drafting and Design (CADD) Center Dar es Salaam which is a franchise of CADD Center India. Left is Hanif Abdulrasul, (second right) Shafiq Abdulrasul, Directors at CADD Center Dar es Salaam and right is Managing Director CADD Center India Mr Saravanan Karaiadiselvan. The Center plans to train more than 1,200 Tanzanians in professional architectural, engineering and project management job sector annually.
 Managing Director Computer Aided Drafting and Design (CADD) Center India Mr Saravanan Karaiadiselvan receives a gift from Rehema Mtutura, Desktop Publishing Institute (DPI) sales officer, during a ceremony to officially launch CADD Center Dar es Salaam which is a franchise of CADD Center India. Second left is Director at CADD Center Dar es Salaam Hanif Abdulrasul, followed by Tanzania Commissioner for Education Prof. Eustella Bhalalusesa and Shafiq Abdulrasul Director at CADD Center Dar es. The Center plans to train more than 1,200 Tanzanians in professional architectural, engineering and project management job sector annually.
 Director at Computer Aided Drafting and Design (CADD) Center Dar es Salaam Hanif Abdulrasul speaks during the launch of the center in Dar es Salaam yesterday, which is a franchise of CADD Center India. The Center plans to train more than 1,200 Tanzanians in professional architectural, engineering and project management job sector annually. Second left is Tanzania Commissioner for Education Prof. Eustella Bhalalusesa, followed by Director at CADD Center Shafiq Abdulrasul and Managing Director CADD Center India Mr Saravanan Karaiadiselvan.  
 Tanzania Commissioner for Education Prof. Eustella Bhalalusesa speaks to journalists during a ceremony to officially launch Computer Aided Drafting and Design (CADD) Center Dar es Salaam yesterday, which is a franchise of CADD Center India. Left is Hanif Abdulrasul, (second right) Shafiq Abdulrasul, Directors at CADD Center Dar es Salaam and right is Managing Director CADD Center India Mr Saravanan Karaiadiselvan. The Center plans to train more than 1,200 Tanzanians in professional architectural, engineering and project management job sector annually.
=========   =======  ==========
Kituo cha mafunzo chazinduliwa kuiongezea thamani soko la ajira la uhandisi na usimamizi wa miradi

Wataalam zaidi ya 1,200 katika fani ya uhandisi, usanifu majengo na usimamizi wa miradi, wanatarajiwa kuingizwa katika soko la ajira hapa nchini kila mwaka kutokana na uanzishwaji wa kituo cha mafunzo cha Computer Aided Drafting & Design (CADD) cha jijini Dar es Salaam.

Kituo hicho kilichozinduliwa jana, kwa kushirikiana na moja ya taasisi ya uchapishaji ijulikanayo kama Desktop Publishing Institute (DPI) la Dar es Salaam, kitasaidia katika kuongeza thamani katika fani tajwa na hivyo kubadilisha na kuboresha ufanisi wa kazi katika sekta hizo.

Hii ilibainishwa na mmoja wa waanzilishi wa DPI, Bi. Debra Backlund, wakati wa uzinduzi wa kituo hicho ambacho ni wabia katika biashara na kituo cha mafunzo chaComputer Aided Drafting & Design (CADD) cha nchini India.

Bi. Debra alisema kituo hicho kinampango wa kushirikiana na taasisi mbali mbali za elimu ya juu na makampuni ya kibiashara ili kubaini mapungufu yaliyopo katika wataalam wenye ujuzi na kutoa mafunzo ya kipekee kwa wanafunzi na wataalamu katika sekta hiyo.

"Katika jitihada za kupata mafunzo bora yanayotambuliwa kimataifa na kuongeza utaalam katika vitengo vya maendeleo, kituo cha CADD cha Dar es salaam kina nia ya kuongeza ushindani katika soko la Tanzania kwa kutoa mafunzo ya kitaalam kwa kuwawezesha wataalam hao kutumia compyuta katika kazi zao. Tumejipanga kuzalisha wataalam watakaotosheleza mahitaji ya viwanda na sekta za huduma nchini," Debra alisema. 


Aliongeza kuwa kituo hicho kitatoa vyeti vitavyotambuliwa kimataifa kwa watainiwa watakaofanya vizuri baada ya kupata mafunzo katika masomo zaidi ya 15 yakijulikana kama global CAD/ Computer Aided Engineering (CAE)/ Computer Aided Manufacturing (CAM) na Project Management products kutoka Autodesk, PTC, Bentley, Ansys na Siemens. 

Naye, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk Shukuru Kawambwa, katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Kamishna wa Elimu Prof Eustella Bhalalusesa, alisema kuanzishwa kwa kituo cha mafunzo cha CADD jijini Dar es Salaam chenye ubora wa daraja la kwanza ni hatua kubwa ya mafanikio kwa Tanzania, hususani mafunzo hayo yakiwa sasa yanatolewa karibu na wahitaji.

"Hapo awali, Watanzania wengi walikuwa na hamu ya  kupata  mafunzo kama haya, ambayo yalikuwa yakipatikana nchi za nje pekee. Nina hakika kwamba wataalamu wataitumia fursa hii ya mafunzo haya yatakayotolewa kikamilifu ili kuongeza ufanisi katika kazi zao na kupata wataalamu wengi watakao tosheleza soko la Tanzania, " Waziri alisema.

Dk Kawambwa alisisitiza kuwa wakati kituo hichokikitoa mafunzo hayo, kinapaswa kuzingatia taratibu zote zinazotakiwa ili kukubalika kikamilifu na mamlaka zote husika. Hata hivyo, alibainisha kuwa Bodi ya Usajili wa Wahandisi tayari ilishapitisha mitaala itakayotumika katika utolewaji wa mafunzo hayo.

"Kituo hichi hakina budi kutoa mafunzo yakipekee yatakayotosheleza mahitaji ya viwanda na sekta ya huduma nchini kwa kushirikiana na taasisi za elimu ya juu. Hii itawezesha kuziba pengo lililopo la ujuzi huo baina  ya wataalamu na mafundi mbalimbali," alisema.

Mafunzo ya TEHAMA kwa Simu yasisitizwa kukuza Demokrasia Vijijini

$
0
0
IMAG0271
Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya Kilombero, Hassan Masala, akifungua mafunzo ya matumizi ya simu kwa habari katika ukumbi wa Mazingira Kibaoni, Ifakara 03 Februari 2014 yanayolenga kukuza taaluma ya upashaji habari kwa kutumia simu. Kushoto ni Afisa Tawala wa Wilaya ya Kilombero Bi. Christa Njovu na Kulia ni Mkufunzi kutoka UNESCO Mama Rose Haji Mwalimu.

Na. Mwandishi wetu.

Demokrasia vijijini itapatikana iwapo vyombo vya habari jamii vitatumika kikamilifu na kutekeleza wajibu wake wa kupasha habari kwa kutumia teknolojia mpya.

Akifungua mafunzo ya wiki moja katika Ukumbi wa Mazingira, Kibaoni Ifakara yanayowashirikisha wanahabari jamii kutoka Pemba, Unguja, Pangani, Ifakara na Kyela, Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Hassan Masala amesema mbinu za kisasa zinahitajika kuelimisha jamii na mambo gani yafanyike ili kupata uongozi bora vijijini na taifa kwa ujumla.
20140204_111348
Mkufunzi wa Teknolojia ya simu kwa habari kutoka Chuo Kikuu Bibi Faith Shayo akifafanua jinsi simu za “SMART” zinavyoweza kutumika kwa habari mbalimbali, picha na maoni kutoka na kwenda katika jamii kupitia maelekezo husika yaliyomo katika simu.

Bwana Masala amesema pamoja na changamoto zilizoko vijijini, Redio Jamii Pambazuko iliyoko Ifakara, ina mchango mkubwa katika kuelimisha na kukuza demokrasia katika wilaya ya Kilombero kwa kuwa inafika sehemu kubwa ambako serikali haifiki kwa urahisi.
Amesema kutokana na miundo mbinu mibovu ya usafiri, mafunzo ya matumizi ya simu kwa kiasi kikubwa yataongeza ujuzi katika taaluma ya upashaji habari.

Mafunzo hayo yaliyofanyika kuanzia tarehe 3 hadi 7 mwezi Februari 2014 yanalenga kutambua uwezo wa simu katika kutafuta na kutoa habari, kujifunza jinsi Tehama inavyorahisisha mawasiliao kwa njia ya simu aina ya “SMART” na kuboresha mbinu za upatikanaji na utoaji wa habari.

Mafunzo ya Tehama kwa redio jamii ni mwendelezo wa mradi wa kuzipatia uwezo redio hizo kwa kutumia teknolojia mpya unaofadhiliwa na UNESCO kwa ushirikiano na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA).
DSC_0397
Mkufunzi na Mtaalamu wa Masuala ya Redio Jamii Mama Rose Haji Mwalimu kutoka UNESCO, akieleza madhumuni ya mafunzo kwa washiriki, katika Ukumbi wa Mazingira Kibaoni, Ifakara.
20140204_155711
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya TEHAMA kutumia simu kwa mawasiliano wakifanya kazi za vikundi.
20140204_155841
Washiriki katika vikundi kazi wakitumia simu zao kufanya mazoezi kutokana na mafunzo waliyopata kwa mawasiliano rahisi vijijini.
IMAG0275
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wakufunzi pamoja na washiriki wa Redio Jamii kutoka Pangani, Pambazuko, Kyela, Pemba na Unguja.

KATIBU MKUU WIZARA YA ULINZI AWASILI MKOANI RUKWA KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU TATU

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wiazara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Ndugu Job Masima akishuka kwenye ndege aina ya Auric Air katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga mapema jana kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Rukwa kufuatia mwaliko wa Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kulia akimtambulisha Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Symthies Pangisa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ndugu Job Masima mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga jana.
Katibu Mkuu wa Wiazara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Ndugu Job Masima kulia akisalimiana na mwanasiasa Mkongwe nchini Ndugu Chrissant Mzindakaya katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga, Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na msafara wa Katibu Mkuu wa Wiazara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Ndugu Job Masima ofisini kwake jana. Mkuu huyo wa Mkoa alimshukuru Katibu Mkuu huyo kwa kukubali mwaliko wake. Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ameahidi kuboresha miundombinu ya viteule vya jeshi vilivyopo Mkoani Rukwa ukiwepo usafiri, majengo na nishati ya umeme wa jua.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta akisalimiana na rafiki yake wa siku nyingi Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Luten Kanali Sipe mara baada baada ya kuonana na msafara wa Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ofisini kwake jana.  (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

HONEY KAUR MAIR AIBUKA MSHINDI WA SHINDANO LA VALENTINES DAY SPECIAL LILILOANDALIWA NA MeTL KWENYE UKURASA WAKE WA FACEBOOK

$
0
0
1 (5)
Honey akiwa amepozi pembeni ya kikapu maalum cha wapendanao, kilichosheheni zawadi mbali mbali.

Na.Mwandishi wetu.

Honey Kaur Mair, ni msichana mwenye bahati. Bila shaka sikukuu yake ya wapendanao ilimalizika kwa furaha baada ya yeye na mumewe kuibuka kidedea wa shindano lililoandaliwa na kudhaminiwa na METL la Valentines Day Special Competition kupitia ukurasa wao wa Facebook. Pamoja na kuzawadia kikapu maalum cha wapendanao kilichosheheni zawadi kem kem, pia wapenzi hawa walipatiwa vocha maalum iliyowawezesha kupata dinner matata usiku wa siku ya Wapendanao katika mgahawa maarufu wa AK's Cafe.
1511482_472007099595581_152425816_n
Shindano hilo lililoshika kasi kuanzia tarehe 5 February na kumalizika tarehe 12 February, lilishuhudia washiriki wengi wakijitosa kuwania zawadi maalum iliyoandaliwa kwa kutuma picha za couple zao na wapenzi au watu wao wawapendao ambao wangesherehekea pamoja sikukuu ya wapendanao na picha zao kuwekwa kwenye ukurasa wa Facebook wa METL kisha kupigiwa kura.

Hatimaye baada ya mchuano mkali, Honey na mpenzi wake Davinder waliibuka kidedea kwa kushinda baada ya picha yao kupata LIKES nyingi kushinda wengine hivyo kumaanisha kwamba wao ndio wamechaguliwa na wengi kama 'best couple' kushinda shindano hilo.
1661983_472006856262272_804463697_n
METL inapenda kuwapongeza Honey na Davinder kwa ushindi huo na pia inawashukuru wateja wake wote ambao walishiriki kwa moyo katika shindano hilo. Kwetu sisi, nyote ni washindi, na hawa ni wawakilishi wenu tu katika kuchukua zawadi!
ASANTENI, ENDELEENI KUPENDANA KILA SIKU!
Like Ukurasa wetu wa Facebook hapa www.facebook.com/MeTLGroup

Serikali yasema itaendelea kusimamia masuala ya amani katika bara la Afrika.

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu masulala mbalimbali ya uhusiano wa kimataifa ikiwamo hatua zinazochukuliwa na Tanzania katika kusuluhisha Migogoro inayotokea ndani na nje ya mataifa mbalimbali na kusisitiza kuwa Tanzania haiwezi kuingia katika mgogoro na majirani zake, Wakati wa Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe akifanya mahojiano na Mwandishi wa shirika la utangazaji la Uingereza (BBC) Erick David Nampesya leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa Habari waliohudhuria mkutano wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam. 

(Picha na Hassan Silayo)

Frank Mvungi
Serikali ya Tanzania imesema  haina ugomvi na nchi jirani kwa kuwa ni wadau  wa maendeleo katika  kujenga uchumi imara kwa kutumia fursa  zilizopo.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe wakati akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam kuhusu taarifa mbalimbali zinazoripotiwa na vyombo vya habari kuhusu uhusiano wa Tanzania na Rwanda.

Akieleza zaidi Mh.Membe alisema vyombo vya habari  vinalojukumu kubwa la kuielimisha jamii na kuimarisha uhusiano kati Tanzania na nchi jirani na si kufanya jambo lolote linaloweza kuleta tofauti kati ya Taifa moja na jingine.

Mh. Membe amesema kuwa Tanzania ni nchi inayotumia njia za Kidiplomasia kuondoa tofauti zozote zitakazojitokeza kati yake na nchi yoyote na haina mpango wa kuingia kwenye mgogoro na nchi yoyote ile.

Aliongeza kuwa Tanzania kwa miaka mingi imekuwa kisiwa cha amani na mfano bora katika bara la Afrika ndio maana imekuwa mstari wa mbele katika kutatua migogoro ndani ya bara la Afrika. Akifafanua zaidi Mh. Membe amesema Tanzania imepeleka vikosi vyake  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,Lebanon,Sudan ya Kusini, katika kutimiza jukumu la kulinda amani Duniani.

“Tunafikri ni vyema Jukumu la ulinzi  wa Bara la Afrika likawa mikononi mwa Afrika yenyewe” alisisitiza Mh.Membe alipokuwa akifafanua kuhusu nafasi ya Tanzania katika kuleta amani katika mataifa mbalimbali ndani na nje ya Bara la Afrika.

Pia alieleza kuwa tangu harakati za ukombozi wa bara la Afrika Tanzania imekuwa  makao makuu ya vyama vyote vya ukombozi barani Afrika na kusaidia katika harakati za kuleta ukombozi .


Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mwaka huu imepanga kufanya maandalizi mazuri yatakayoiwezesha timu ya Taifa kushiriki na kupata medani katika michezo ya jumuiya ya madola.

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YATOA SEMINA KWA WAHARIRI WA HABARI JUU YA KANZA INAYOONESHA VIASHIRIA VYA KIUCHUMI NA KIJAMII

$
0
0
Meneja wa Teknojia ya habari na Masoko Bi. Mwanaidi Mahiza akifafanua jambo kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari (hawapo pichani) wakati wa washa ya siku moja iliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu,katika hoteli ya JB Belmont jijini Dar es salaam leo.
Mchambuzi wa Mifumo ya Kiteknolojia kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu,Martin Kimario akitoa maelezo ya mtandao wa TSED kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari (hawapo pichani) wakati wa washa ya siku moja iliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu,katika hoteli ya JB Belmont jijini Dar es salaam leo.
Mmoja wa wahariri wa vyombo vya habari akichangia mada kwenye warsha hiyo.
Sehemu ya Wahariri wa vyombo vya habari wakiwa kwenye warsha hiyo.Picha na Othman Michuzi.

Na Veronica Kazimoto – MAELEZO

Watanzania wameshauriwa kutumia kanza inayoonesha viashiria vya kiuchumi na kijamii (Tanzania Social Economic Database -TSED) ili kurahisisha upataji wa taarifa pindi wanapokuwa katika kazi zao za kila siku.

Akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari katika washa ya siku moja iliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu leo jijini Dar es salaam, Meneja wa Teknojia ya habari na Masoko Bi. Mwanaidi Mahiza amesema kuwa TSED inasaidia kupata taarifa kwa haraka kwa njia ya mtandao bila kuzifuata katika ofisi mbalimbali za Serikali.

“TSED inasaidia kuondoa mlolongo wa upatikanaji wa taarifa uliopo kwenye  baadhi ya ofisi nyingi ambapo wakati mwingine mteja utaambiwa uandike barua au urudi baada ya siku kadhaa,” amesema Mahiza.

Bi. Mahiza amesisita kuwa ni muhimu kutumia kanza hiyo kwa kuwa ndani yake kuna takwimu rasmi ambazo zinatoka katika vyanzo sahihi vyenye mamlaka ya kutoa takwimu hizo hapa nchini.

Kanza inayoonesha viashiria vya kiuchumi na kijamii ilizinduliwa rasmi mwaka 2001 ikiwa na viashiria 75 ambapo hivi sasa ina viashiria 940 na inapatikana katika mfumo wa DVD, CD ROMs na tovuti ya www.tsed.org.
Viewing all 46366 articles
Browse latest View live




Latest Images